MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO0%

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO Mwandishi:
Kundi: Misingi mikuu ya Dini

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

Mwandishi: AYATULLAHI: SAYYID SWAADIQ AL-HUSAINIY SHIRAZIY
Kundi:

Matembeleo: 8984
Pakua: 2359

Maelezo zaidi:

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 11 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 8984 / Pakua: 2359
Kiwango Kiwango Kiwango
MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

Mwandishi:
Swahili

3

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

IMAM WA NNE: IMAMA SAJJAD (a.s)

Yeye ni Imam Ali bin Hussen(a.s) na mama yake ni Shahri banuu binti wa mfalme Yazdjard na Imam huyu(a.s) alikuwa akiitwa Mtoto wa wateule wawili, kutokana na kauli ya Mtume(s.a.w.w) :

Hakika mwenyezi Mungu ana wateule wawili katika waja wake, mteule wake katika waarabu ni Quraishi na katika waajemi (wasio waarabu) ni Mfursi. Na kwa kuyazingatia maana ya maneno haya Abul Aswad akaimba shairi lifuatalo:

Hakika mtoto alie zaliwa kati ya Kisraa na Haashim ni mkarimu zaidi ya watoto wote walio vishwa hirizi shingoni mwao.

Amezaliwa(a.s) katika mji wa Madinanatul-munawwarah siku ya Alikhamisi mwezi mtukufu wa Shaaban[29] mwaka (38) hijiria na kufa shahidi kwa sumu siku ya juma mosi tarehe (25) mwezi wa Muharram[30] mwaka (95) akiwa na umri wa miaka (57), na mwanae Imam Baaqir(a.s) ndie alie simamia suala la mazishi yake na kumzika karibu na kaburi la Ami yake Imam Mujtaba(a.s) katika mji wa madinatul-munawwarah.

Na alikuwa ni wa aina yake (kwa maana ya kuwa hakuwa na mfano) katika zama zake katika suala la elimu, ibada, fadhila, uchamungu, kuwasaidia watu wenye kuomba misaada na wenye kutaka usaidizi na mengineyo, na maulamaa wengi pia mafaqihi wamepokea riwaya nyingi sana na zisizo hesabika kutoka kwake na kuhifadhi kutoka kwake dua na mawaidha mengi na karama mbalimbali na mengine mengi yasiyo hesabika. Na alikuwa akitoka usiku wa kiza na kubeba mfuko mabegani mwake ukiwa na Dinari na Dirham napengine alikuwa akibeba mgongoni mwake mfuko wa vyakula, au kuni na kupita mlango mmoja mmoja akibisha hodi na kumpatia kila atokae kwenye nyumba hizo pesa hizo, na alikuwa akifunika kichwa chake ili mafakiri wasimfahamu, na pindi alipo fariki watu wa madina wakafahamu na kuelewa ya kuwa yeye(a.s) ndie ambae alikuwa akibeba mfuko na kuwapatia vyakula.

Pamoja na hayo akipendezewa sana kula pamoja na mafukara au kuhudhuria kwenye chaku chake mayatima na mafakiri na kula pamoja nae. Na miongoni mwa tabia zake njema(a.s) ni kuwa katika kila mwezi alikuwa akiwaita wahudumu wake na kusema: Mwenye kutaka kuolewa kati yanu nitamuoza, au akitaka kuuzwa nitamuuza, au akitaka kuachiwa huru nitamuachia huru. Na pindi alipokuwa akijiwa na muombaji husema: Karibu wewe ambae huibeba akiba yangu ya akhera.

Na kutokana na uchaji mwingi wa mola ni kuwa alikuwa akisali kwa usiku na mcana wake rakaa elfu mmoja na anapo kuwa kwenye sala ngozi yake husinyaa na kukunjamana na rangi yake kubadilika na kuwa ya njano na kutetemeka kama kuti la mtende, na miongoni mwa laqabu zake ni Dhuthafanaati (mwenye sugu au magamba), kutokana na athari za sajda katika paji lake la uso na vitanga vyake pia magotini mwake. Mtu mmoja alimtusi na kumtolea maneno machafu na mabaya na yeye(a.s) akiwa kimia hazungumzi wala kasema chochote na baada ya muda Imam(a.s) akamwendea, waliokuwa wamehudhuria wakadhania ya kuwa anataka kumfanya kama alivyo fanya yeye, mara akasoma aya ifuatayo:

وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾

Na wenye kuvunja ghadhabu na kuwasamehe watu na Mwenyezi Mungu anawapenda watu wema[31] .

Kisha akamsimamia bwana yule na kusema: Ewe ndugu yangu hakika wewe ulisimama kwangu (ulinisimamia) muda ulio pita na kusema uliyo yasema, ikiwa umeyasema kwangu hayo uliyo yasema, basi mimi nina muomba Mwenyezi Mungu msamaha na ikiwa umesema mambo ambayo siko nayo, Mwenyezi Mungu akusamehe[32] .

IMAM WA TANO: IMAM BAAQIR (a.s)

Yeye ni Imam Mohammad bin Ali Al-baaqir(a.s) na mama yake ni Fatuma binti Hassan(a.s) alizaliwa katika mji wa madina siku ya Ijumaa mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Rajab[33] mwaka (57) hijiria.

Na yeye ndie mtu wa kwanza katika kizazi cha Ali alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi hicho cha Ali, na ni mtu wa kwanza wa kizazi cha Haashim alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi cha Haashim, na ni mtu wa kwanza alie zaliwa na wazazi wawili watokanao na kizazi cha Fatuma, kwani yeye ndie wa mwanzo alie kusanya kati ya kizazi cha maimamu wawili Hassana na Hussen(a.s) na alikufa shahidi kwa sumu siku ya juma tatu tarehe (7) Dhul hajjil haraam mwaka (114) hijiria akiwa na umri wa miaka (57) na mwanae Imam Swaadiq(a.s) ndie alie simamia suala la maandalizi ya mazishi yake na kumzika pembezoni mwa kaburi la baba yake Imam Sajjad(a.s) na Ami wa baba yake na babu yake Imam Mujtaba(a.s) katika makaburi ya Baqii'i kwenye mji wa Madinatuil munawwarah. Na alikuwa ni mwenye fadhila kubwa mkarimu na mwenye kushikamana na dini na alikuwa ni mwenye elimu nyingi na kubwa na mpole sana, pia mwenye tabia njema na mwenye kufanya ibada sana, mwenye unyenyekevu, ukarimu, ukunjufu na alifikia kwenye kilele katika tabia zake njema, mkiristo mmoja alimwambia: Wewe ni mfunguzi na mpasuaji! Imam akasema: Mimi ni Mfuinguzi.

Akasema wewe ni mtoto wa mpishi. Imam akasema:Hiyo ni kazi yake . Akasema: Wewe ni mtoto wa mtu mweusi na mbaya. Imam(a.s) akasema:

Ikiwa umesema kweli Mwenyezi Mungu amsamehe na ikiwa umesema uongo Mwenyezi Mungu akusamehe . Yule Mkiristo akasilimu.

Na katika elimu alikuwa kama Bahari yenye mawimbi mengi, akijibu kila mas'ala na swali lolote analo ulizwa bila kusita.

Na Ibnu Atwaa Al-makiy amesema: Sija wahi kuona kamwe wanazuoni na maulamaa kwa mtu yeyote alie kuwa mdogo zaidi kuliko nilivyo waona kwa Baaqir(a.s) hakika nilimuona Al-hakam bin Utaybah-pamoja na utukufu wake na heshima yake kati ya watu-akiwa mbele yake kama mtoto akiwa mbele ya mwalimu wake, na Mohammad bin Muslim amesema: Sikujiwa na fikra yoyote isipokuwa nilimuuliza Mohammad bin Ali(a.s) mpaka nilimuuliza hadithi elifu thalathini (30).

Na Imam(a.s) alikuwa ni mwenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wakati wote, mpaka Imam Swaadiq(a.s) akasema: Baba yangu alikuwa ni mwenye kumtaja sana Mwenyezi Mungu, nilikuwa nikitembea pamoja nae hali ya kuwa akimtaja Mwenyezi Mungu na alikuwa akizungumza na watu na lisimshughulishe hilo kunako kumtaja Mwenyezi Mungu[34] .

Na Imam alikuwa ni mwingi wa tahajjud (sala za usiku) na ibada, mwenye kulia sana na mwenye mazingatio.

IMAM WA SITA: IMAM SWAADIQ (a.s)

Yeye ni Jaafar bin Mohammad As-swaadiq(a.s) na mama yake ni Fatuma alie kuwa akiitwa kwa kunia ya (Ummu farwah) alizaliwa(a.s) katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarehe (17) mwezi wa Rabiiul Aawwal (mfungo sita) siku ya kuzaliwa Mtume(s.a.w.w) mwaka (83) hijiria na kufa shahidi kwa sumu siku ya juma nne tarehe (25) mwezi wa Shawwal (mfungo mosi) mwaka (148) hijiria akiwa na umri wa miaka (65), na mwanae Imam Kaadhim kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika katika makaburi ya Baqii'i pembezoni mwa kaburi la baba yake Imam Baaqir(a.s) na babu zake wawili: Imam Sajjad na Imam Mujtaba(a.s) .

Na alikuwa na Fadhila nyingi zisizo hesabika kama elimu, fadhila, hekima, fiqhi, zuhdi, uchamungu, ukweli, uadilifu, ubora, furaha na utoaji, ukarimu, ushujaa na fadhila zinginezo.

Na kwa hakika Mufiid alisema (Mwenyezi mungu autukuze utajo wake): Na maulamaa hawakunukuu kwa yeyote kati ya Ahlul bayti wake kama walivyo nukuu kutoka kwake na hakuna yeyote kati ya watu wakusanyao hadithi na wakusanyaji wa habari, mfano wa Jaafar bin Mohammad As-swaadiq(a.s) hakika walikusanya majina ya wapokezi kutoka kwake kati ya watu waaminifu pamoja na kutofautiana kwao kirai na itikadi, na walikuwa ni watu elfu nne (4000)[35] . Hadi mwisho wa maneno yake.

Na Abu hanifa Imamu wa madhehebu ya hanafi alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wake moja kwa moja, kama ambavyo maimam wengine wa madhehebu za Ahli sunna walikuwa ni wa wanafunzi wake pia(a.s) lakini si moja kwa moja bali kwa kupitia wanafunzi wake na kwamba elimu nyingi na mpya kama vile Kemia, Fizikia na elimu ya maumbo na nyota na elimu ya ugunduzi wa madini na kuchimbuaji wa hazina zilizoko ardhini na zinginezo nyingi ambazo Imam ndie alie weka misingi yake na kuwaongoza watu kwenye elimu hizo.

Hakika Imam(a.s) alitumia fursa iliyopatikana ya ugomvi kati ya bani Abbas walio fanya mapinduzi dhidi ya bani Umayyah na kati ya bani umayya walio kuwa mbioni kuanguka na kutoweka dola lao, alitumia fursa hiyo kuanzisha Madrasa kubwa ya kielimu na kujishughulisha na kazi ya ulezi wa wanafunzi na watafutaji wa elimu na kuwabainishia mafunzo ya kiislaam na uzuri wa sheria zake na kuwafafanulia fikra za batili na mbaya zilizo ingia kwenye Uislaam na kubatilisha shubha zitolewazo, mpaka misingi ya sheria ikaimarika na ubainifu wa Uislaam kudhihiri na kubainika wazi na akafahamika(a.s) kama Raisi na kiongozi wa Madhehebu ya Jaafaria, kama ambavyo wafuasi wake(a.s) walifahamika pia kwa jina la Shiatu Jaafar (wafuasi wa Jaafar au mashia wa Jaafar).

Na miongoni mwa uongofu wake(a.s) ni kuwa yeye alikuwa akila siki na mafuta na kuvaa kanzu ngumu na nzito napengine alikuwa akivaa nguo yenye viraka na alikuwa akifanya kazi zake mwenyewe kwenmye mabustani na mashamba yake.

Na miongoni mwa Ibada zake ni kuwa alikuwa akisali sana na pengine alikuwa akizimia katika sala na kuitwa watu wa kumsaidia usiku, Mtumishi wake anasema: Nilikwenda mlangoni kwake na nikamkuta katika chumba chake cha faragha akiwa ameweka shavu lake juu ya udongo hali akiomba kwa kuinua vitanga vyake na huku kukiwa na athari ya mchanga usoni mwake na kwenye shavu lake.

Na Imam(a.s) alikuwa ni mwingi wa kutoa, mwenye tabia njema, mwenye maneno laini, mwenye vikao vizuri na mwenye bashasha kwa kila mwenye kukutana nae na alikuwa na muashara mzuri kwa kila anae kutana nae.

IMAM WA SABA: IMAM KAADHIM (a.s)

Yeye ni Imam Mussa bin Jaafar Al-kaadhim(a.s) na mama yake ni Hamidah Al-muswaffah, alizaliwa(a.s) katika sehemu iitwayo (Ab'waa) nayo ni sehemu iliyoko kati ya Makka na Madina siku ya juma pili tarehe (7) mwezi wa Safar mwaka (128) hijiria na aliiaga Dunia akiwa na umri wa miaka (55) kwa kulishwa Sumu na kufa shahidi katika jela ya Haroun baada ya kumfunga kwa muda mrefu kwa muda wa miaka (14) kwa dhuluma na uadui, na alifariki siku ya Ijumaa tarehe (25) ya mwezi wa Rajab mwaka (183) na mwanae Imam Ridhaa(a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika mahala lilipo kaburi lake tukufu kwa hivi sasa katika mji wa Kaadhimiyyah huko Iraq.

Na Imam alikuwa ndie mwenye elumu zaidi kati ya watu wa zama zake na mbora wao na mkarimu zaidi kati yao na shujaa zaidi na amwenye tabia njema, mwenye umbile bora na mororo, mwenye kudhihiri juu yake fadhila, elimu na mwenye hadhi tukufu, mwenye kufanya sana ibada na mwenye kurefusha sijda zake, na kutokana na kuvunja kwake ghadhabu na kuto kasirika akaitwa Al-kaadhim, na kutokana na wema wake na utukufu wake alikuwa akiitwa Al-abdus swalih (mja mwema). Na kutokana na elimu yake nyingi aliweza kudhihirisha elimu za aina tofauti, elimu ambazo ziliwashangaza watu, na kati ya elimu hizo ni hadithi ya (Burayha)[36] mkuu wa Wakiristo alie mashuhuri alie shindwa na Imam na kukosa la kusema mwishowe kusilimu na kuwa muislaam safi.

Na miongoni mwa ukarimu wake(a.s) ni kuwa: fakiri mmoja alimuomba Dinari mia moja na Imam kwa kutaka kumjaribu akamuuliza mas'ala au swali moja ili kujua kiwango cha maarifa yake, yule fakiri alipo jibu mas'ala yale Imam akampatia Dinari elfu moja. Na Imam(a.s) alikuwa ni mwenye sauti nzuri sana pindi anapo soma Qur'ani na alikuwa ni mfanya ibada sana kati ya watu na kusoma sana Qur'ani, na alikuwa ni mwenye kurefusha sana sijda na rukuu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na mwenye kulia sana na mwenye mazingatio, na alifikiwa na shahada hali ya kuwa yuko kwenye hali ya kusujudu (yaani akiwa ni mmwenye kusujudu).

IMAM WA NANE: IMAM RIDHAA(a.s)

Yeye ni Imam Ali bin Mussa Ridhaa(a.s) na mama yake ni Sayyidah Najmah, alizaliwa(a.s) siku ya Al-khamisi tarehe (11) mwezi wa Dhulqaadatul-haraam, mwaka (148) hijiria katika mji wa Madina na kufa shahidi kwa sumu siku ya Ijumaa mwishoni mwa mwezi wa Safar, mwaka (203) na mwanae Imam Jawaad(a.s) kusimamia suala la maandalizi ya mazishi yake na kumzika katika sehemu ya khorasani sehemu ambayo ndiko liliko kaburi lake tukufu. Na Imam(a.s) alikuwa mashuhuri sana kwa elimu nyingi, fadhila, ukarimu, mwingi wa kutoa, mwenye tabia njema, mnyenyekevu, na mwenye kufanya ibada sana.

Maamun-kutokana na vitimbi na hadaa-alimuita Imam Ridhaa(a.s) kutoka Madinah hadi Khorasani (Iran) na kumtaka achukue ukhalifa wa kiislaam-badala yake-lakini Imam alikuwa amejiweka kando na kuyapa mgongo mambo ya kidunia (yaani alikuwa ni mwenye zuhdi) na hakukubali, kwani alifahamu matokeo ya maombi hayo, kuwa ni vitimbi na hadaa, kama ambavyo babu yake Amirul muuminiin(a.s) alivyo kataa Ukhalifa-katika shura-wakati Ibnu Auf alipo mpatia Ukhalifa huo kwa sharti kwamba afuate sera ya mashekhe wawili walio mtangulia, (Abubakar na Omar), kwani Imam aliona ya kuwa Ukhalifa wakati huo ulikuwa umesimama juu ya jambo moja wapo kati ya mambo mawili, na mambo yote mawili hayo ni ya uongo na si yenye kukubaliwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu: Ama jambo la kwanza ni kuwa Imam(a.s) akubali sharti kisha asilitekeleze -kama alivyo fanya Othumani - na huo ni uongo wa kikauli na wenye kuchukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Ama jambo la pili ni kuwa: Imam akubali sharti na atekeleze, maana yake ni kuwa aridhie sera ya mashekhe wawili pamoja na kuwa hakuwa na ridhaa na hakuridhishwa na matendo yao na huo ni uongo wa kimatendo na ni wenye kukemewa mbele ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo basi Imam hakuona njia yenye kuridhiwa na Mwenyezi Mungu tofauti na kukataa na kupinga na kuto kubali[37] .

Na baada ya Imam Ridhaa(a.s) kuukataa Ukhalifa, Maamun alishikwa na butwaa na kunyongea sana kwani aliona ya kuwa mpango wake ambao kwa ajili yake alimuita Imam umeshindwa na kufeli, hapo alimtaka achukue wilayatul ahad - cheo cha waziri mkuu- na kumlazimisha kukubali(a.s) lakini Imam(a.s) alimuwekea sharti ya kuwa hato ingilia katika jambo lolote kati ya mambo ya dola na kukubali cheo hicho kwa sharti hilo. Imam(a.s) alikuwa ni mrithi wa baba zake watukufu(a.s) katika elimu na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) na elimu yake ilionekana na kudhihiri kiasi kidogo kuhusiana na mambo ya dini na Madhehebu fikra na Itikadi-katika kikao cha majadiliano ambacho kiliandaliwa na Maamuun-na yaliyo jitokeza kwenye hadithi ya Rukbaan.

Vile vile katika ibada alikuwa(a.s) akikesha katika masiku mengi kwa ibada na kuhitimisha Qur'ani kwa muda wa siku tatu na mara nyingi alikuwa akisali usiku na mchana rakaa elfu moja, na mara nyingi alikuwa akisujudu kwa muda mrefu, pengine alichukua masaa kadhaa kwenye sijda na alikuwa ni mwengi wa kufunga. Na Imam(a.s) alikuwa ni mwingi wa kutenda mema, na akitoa sana sadaka na sadaka nyingi alikuwa kizitoa kwa siri na hasa kwenye usiku wa kiza.

Na miongoni mwa tabia zake na adabu zake(a.s) ni kuwa hakumuudhi mtu yeyote kwa maneno kamwe na wala hakumfanyia ukali mtu yeyote katika kauli, na hakuwa akiegemea kukiwa kuna watu wamekaa mbele yake na hakuwahi kucheka kwa sauti kubwa na ya juu kamwe, na hakuwahi kutema mate mbele ya yeyote kamwe, na chakula kilipo kuwa tayari mezani huwaita ahli zake wote na wahudumu wake na kula pamoja nao.

4

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

IMAM WA TISA: IMAM JAWAAD(a.s)

Yeye ni Imam Mohammad bin Ali Al-jawaad(a.s) na mama yake ni Sayyidah Sabiika, alizaliwa(a.s) siku ya Ijumaa tarehe (10) katika mwezi mtukufu wa Rajab, mwaka (195) hijiria, katika mji wa Madinatul munawwarah na kufa shahidi kwa sumu katika mji wa Baghdaad, mwishoni mwa mwezi wa Dhul-qaadah (mfungo pili) mwaka (220) hijiria, na mwanae Imam Al-hadiy(a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika kwenye maburi ya Makuraishi pembezoni mwa kaburi la babu yake Muusa bin Jaafar(a.s) katika mji wa Kaadhimiyyah mahala lilipo kaburi lake kwa hivi sasa.

Na Imam(a.s) alikuwa ni mjuzi zaidi kati ya watu wa zama zake na mbora zaidi kuliko watu wote, mkarimu, pia mwingi wa kutoa na mwenye vikao vizuri, na alikuwa ni mwenye tabia njema, mfasaha na kila alipo kuwa akipanda mnyama wake hubeba Dhahabu na Fedha na hakuna aliekuwa akimuomba isipokuwa humpatia, na alie kuwa akimuomba pamoja na wingi wao alikuwa hampatiii chini ya Dinari Khamsini (50) na alie kuwa akimuomba kati ya shangazi zake alikuwa hampi chini ya Dinari ishirini na tano (25).

Na miongoni mwa elimu yake kubwa ambayo ilidhihiri kwa watu: Ni kuwa wanazuoni thamanini kati ya wanazuoni wa miji mbalimbali walikusanyika kwake baada ya kurudi kwao kutoka kwenye ibada ya hijja na kumuuliza kuhusiana na mas'ala mbali mbali na yeye(a.s) kuwajibu, namiongoni mwa mambo ya ajabu yaliyo simuliwa kutoka kwake(a.s) ni kuwa watu wengi walikusanyika kwake na kumuuliza mas'ala thelethini elfu-katika kikao kimoja nacho ni kikao kiitwacho kwa siku hizi kwa jina la kongamamno, kongamano ambalo hufanyika na kuendelea kwa muda wa siku kadhaa na Imam kuwajibu mas'ala hayo bila kusita kufanya hivyo wala kukosea na wakati huo akiwa na umri wa miaka tisa (9), lakini jambo kama hili si jambo la ajabu na la kushangaza kutokea kwa Ahlul bayti-watu wa nyumba ya Wahyi na mahala alipokuwa Jibril(a.s) akitelemka akiwa na Qur'ani na hasa baada ya Qur'ani kuzungumzia kuhusiana na kupewa kwa Issa bin Maryam kitabu na Utume hali ya kuwa bado yuko kwenye kitanda chake akiwa mtoto mchanga. Kisha ni kuwa khalifa Alimuoza binti yake na hilo lilifanyika baada ya kumtahini kwa maswali (mas'ala) muhimu na kuyajibu yote-katika kisa mashuhuri.

IMAMA WA KUMI: IMAM AL-HADIY(a.s)

Yeye ni Imam Ali bin Mohammad Al-hadiy(a.s) mama yake ni Sayyidah Samanah. Alizaliwa(a.s) katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarehe (2) mwezi mtukufu wa Rajab, mwaka (212) hijiria na kufa shahidi kwa sumu kwenye mji wa Samarraa siku ya juma tatu tarehe (3) mwezi wa Rajab, mwaka (254) hijiria, na mwanae Imam Askariy(a.s) kusimamia maandalizi ya mazishi yake, na kumzika ndani ya nyumba yake kwenye mji wa Samarraa mahala lilipo kaburi lake kwa hivi sasa na mahala kilipo lazwa kiwili wili chake kitukufu. Na Imam(a.s) alikuwa ni mtu bora kati ya watu wa zama zake na alikuwa ni mwenye elimu zaidi na alie kusanya fadhila zote na mkarimu sana na mwingi wa kutoa na alikuwa ni mwenye maneno laini na aliekuwa akimuabudu sana Mwenyezi Mungu na mwenye sera nzuri nasafi na mwenye tabia njema.

Na miongoni mwa ukarimu wake ni kisa kilicho pokelewa na (Ardabiliy) katika kisa chake ya kuwa: Khalifa alimtumia Dirham elfu thalathini, Imam akampatia bedui mmoja wa Al-kufa kama zawadi na akamwambia: Toa kiasi ulipe madeni yako na kiasi kitakacho bakia kitumie kwa ajili ya matumizi na mahitaji ya familia yako na ahali zako na utusamehe. Yule bedui akamwambia Imam: Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika deni nililo kuwa nalo halifikii theluthi ya pesa hii. (Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kufahamu vema mahala pakuuweka ujumbe wake), na akachukua pesa zile na kwenda zake[38] .

IMAM WA KUMI NA MOJA: IMAM ASKARIY(a.s)

Yeye ni Imam Hassan bin Ali Al-askariy(a.s) na mama yake ni Sayyidah Hadiitha. Alizaliwa katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarhe nane (8) mwezi wa Rabiul-aakhir, na inasemekana kuwa amezaliwa tarehe kumi na mbili (12) Rabiul-aakhir[39] mwaka (232) hijiria na kufa shahidi kwa Sumu siku ya Ijumaa tarehe nane (8) mwezi wa Rabiul-awwal mwaka (206) hijiria, na mwanae Imam Hujjatul-muntadhar (mwenye kungojewa) ndie alie simamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika karibu na kaburi la baba yake Imam Al-hadiy(a.s) katika mji wa Samarra, mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake kwa hivi sasa.

Na Imam(a.s) alikuwa ni mfano wa juu kabisa katika ubora, elimu, utoaji, sharafu, furaha na ukarimu, ibada, unyenyekevu na tabia zingine nyingi njema, na alikuwa ni mfano wa kuigwa na kigezo chema kwa wengine, na alikuwa ni mwenye urefu wa wastani na mzuri wa umbile, mwenye uso mzuri na kiwiliwili cha wastani, mwenye heshima na hadhi kubwa kwenye nyoyo na mwenye nafasi ya juu na tukufu katika nafsi za watu, na Imam(a.s) alikuwa akimfanana sana babu yake Mtume(s.a.w.w) katika tabia zake na mwendo wake mwema na uzuri wa kuishi vema na watu.

Na miongoni mwa visa vya ukarimu wake ni kisa kilicho pokelewa na Ismail kisemacho: Nilimkalia na kumsubiri Imam(a.s) katikati ya njia, alipo fika na kupita mahala nilipo kuwa nikamueleza ufukara wangu. Imam akasema(a.s) : Unaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo kwani umefukia Dinari miambili chini ya Ardhi na kusema kwangu maneno haya si kwa sababu ya kuto taka kukupa, ewe ghulam (Mhudumu) mpatie ulicho nacho, akasema: Yule mhudumu akanipatia Dinari mia moja[40] . Na kuna mtu mwingine alimwendea Imam-alipo sikia ukunjufu wake na ukarimu wake-na alikuwa akihitaji Dirhamu mia tano, Imam(a.s) akampatia Dirham mia tano na kumuongezea Dirhamu zingine mia tatu[41] .

Na kwa hakika watu wote walitoa ushahidi na kuthibitisha ubora wake na ukarimu wake, hata wakiristo walimshuhudia(a.s) ya kuwa yeye anafanana na masihi (Yesu) katika ubora, elimu, ukarimu na miujiza yake, na Imam(a.s) alikuwa ni mwenye kufanya sana ibada, akisali sala za usiku (tahajjud) daiama na alikuwa ni mwenye mandhari ya wema, na mwenye heba kubwa.

IMAM WA KUMI NA MBILI: IMAM AL-MUNTADHAR(a.s) (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake)

Yeye ndie Imam na Al-hujjatul-mahdiy(a.s) , Mohammad bin Hassan(a.s) na mama yake ni Sayyidah Narjis. Alizaliwa(a.s) katika mji wa Samarraa usiku wa nusu ya mwezi wa Shaaban, mwaka (255) hijiria. Na yeye(a.s) ndio hoja wa mwisho wa Mwenyezi Mungu juu ya ardhi na Khalifa wa mwisho wa Mtume(s.a.w.w) na Imam wa mwisho wa Waislaam, maimam ambao ni kumi na mbili na Mwenyezi Mungu-kwa utashi wake - ameurefusha umri wake mtukufu katika Dunia hii ili ardhi isibakie bila hujja wa Mwenyezi Mungu, kwani kama kusinge kuwa na hujja basi ardhi inge didimia pamoja na watu wake na yeye Imam haonekani kwa watu na Mwenyezi Mungu atamdhihirisha katika Aakhiriz-zamani (Zama za mwisho) baada ya Dunia kujawa na dhuluma na ujeuri (uovu), ili aijaze dunia hiyo kwa uadilifu na usawa.

Hakika Mtume(s.a.w.w) na maimam watwaharifu walitoa habari ya kuwa yeye atakuwa na ghaibah (Atatoweka na kuto onekana) kwa muda mrefu, na hatakuwa thabiti kwenye juu ya Uimam na wilaya yake na kumuamini isipokuwa yule ambae Mwenyezi Mungu ameujaribu moyo wake kwa Imani, na katika siku za ghaiba yake atakuwa katika hali ya kuwafikishia manufaa watu wa Ardhini kama jua lifikishavyo manufaa na faida zake kwa watu hao hata kama litakuwa limefunikwa na mawingu, na Mwenyezi Mungu atambakiza hai mpaka utakapo fika wakati wa kudhihiri kwake, na hapo kudhihiri kwa idhini yake Mwenyezi Mungu mtukufu na kuimiliki (kuitawala) Dunia yote na kueneza uadilifu na usawa Duniani na kueneza Uislaam na misingi yake yote na kuitekeleza Qur'ani na amri zake kwa watu wote na katika nyanja zake zote za maisha, na hapo Kheri kuenea na saada kutangaa kwenye miji yote na kuwaenea waja wote na kuthibitika kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo:

لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾

Ili auidhihirishe Uislaam juu ya dini zote hata kuma washirikina watachukia [42] .

Ewe Mwenyezi Mungu harakisha faraja yake na kufanye kwepesi kudhihiri kwake na utujaalie tuwe miongoni mwa wasaidizi na answari wake. Baada ya hayo ni jambo lililo wazi ya kuwa Imam Al-mahdiy(a.s) alipokuja kuandaa mazishi ya baba yake Imam As-kariy(a.s) na kumsalia watawala waovu walifahamu kuwepo kwa mrithi na mshika nafasi baada ya Imam Askariy(a.s) na hili lili waogopesha sana juu ya utawala wao na wakafikiria njia ya kumkamata na kumuua kama walivyo waua baba zake(a.s) ili kwa kufanya hivyo waokoke na kujinusuru na habari zilizo wafikia kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuhusiana na habari za Imam wa kumi na mbili na kwamba yeye ndie ambae atakae maliza na kuangamiza utawala wa waovu na kuchukua utawala huo, na Imam Mahdiy(a.s) alikuwa ameamuriwa na Mwenyezi Mungu mtukufu kuwa kwenye ghaiba na kuto onekana kwa watu.

Na pindi majasusi wa Khalifa walipo muona na kuivamia nyumba yake akaghibu na kutoweka na kuto onekana kwa watu na kufichika kunako macho yao, na hilo lilifanyika kwa Imam kutokea kwenye mlango mwingine ulio kuwa wazi wenye kutokea kwenye Sirdab (nyumba ya chini) iliyo kuwa na mlango wa kutokea nje bila yeyote kati yao kumuona, na kutokana na ukweli kwamba sehemu ambayo ilikuwa ndio mahala pa kughibu kwake ni nyumba yake(a.s) Waislaam wakaifanya ile sehemu inasibishwayo kwake-katika mji wa Samarra-iliyo mashuhuri kuwa ni sirdab ya kughibu kwake, wakaifanya kuwa msikiti na mahala pa kufanyia ziara (kutembelea).

5

MISINGI YA DINI NA MENGINEYO

MAREJEO YA KIAMA

Maana yake ni kuwa: Mwenyezi Mungu mtukufu anamuhuisha na kumfanya mwanadamu awe hai katika Akhera baada ya kumfisha duniani, ili amlipe thawabu mtu mwema juu ya wema wake na kumlipa muovu kwa uovu alio ufanya. Kwa hivyo basi mwenye kuamini na kutenda matendo mema na kusali, kufunga, katoa sadaka (zaka) na kumtakasia nia Mwenyezi Mungu (kuwa na ikhals) na kuwahifadhi Mayatima na kuwalisha Masikini na mengineyo mengi, hakika yeye Mwenyezi Mungu humpa thawabu mtu huyo kwa kumuingiza kwenye pepo yenye neema ambayo hutiririka chinio yake mito, na yenye vivuli vyenye kumfunika na yenye rehma nyingi sana na majumba ya kifalme na kifakhari na mahurulaini walio fungiwa kwenye majumba yao na kupata maridhio ya Mwenyezi Mungu ni kukubwa zaidi.

Na mwenye kukufuru na kufanya matendo mabaya na kusema uongo, kufanya khiyana, kuua, kuiba, kuzini, kunywa pombe, na mfano wa hayo, hakika Mwenyezi Mungu humlipa kwa kumuingiza katika jahannama iliyo jawa na moto na adhabu, na chakula chake ni cha miti ya miba na kinywaji chake ni maji ya moto na wakati yuko kwenye matatizo na adhabu yenye kudhalilisha na ya milele isio katika wala kukoma.

Na kuna visimamo vingine viwili kabla ya moto na pepo:

1. Kaburi: Nayo ni sehemu au hatua ya kwanza kati ya hatua za ulimwengu wa barzakh baada ya kuwa mauti ni mlango wa kuingia kwenye ulimwengu huo, kwa hivyo kila mmoja huulizwa aliyo yafanya akiwa kaburini mwake, na kupewa thawabu kwa matendo mema aliyo yatenda na kuadhibiwa juu ya matendo mabaya na kutokana na hayo Mtume(s.a.w.w) akasema:Kaburi ima ni shimo kati ya mashimo ya moto, au ni bustani kati ya mabustani ya peponi [43] na hali ya mwanadamu akiwa kaburini kwa mfano na kwa kutaka kukuletea karibu maana na hali yake ni kuwa: ni kama hali ya mtu alie lala ambae anaota ndoto nzuri na kufurahi kwa ndoto hiyo, au kuota ndoto mbaya na kuteseka na kuadhibika kwa ndoto hiyo, wakati ambapo yule ambae humkaribia yule mtu alie lala na kumuona, hafahamu ya kuwa yuko kwenye raha au kwenye adhabu, vilevile walio hai huwaoni watu walio kufa katika hali ya kuwa ni vilivyo haribika, ama kujua ya kuwa wana adhibiwa au wako kwenye neema, hawalihisi hilo na hilo linatokana na ukweli kuwa vipimo katika ulimwengu wa barzakh ni vipimo vipya tofauti na vipimo vya duniani, na havifanani na vipimo vya maisha ya kidunia ambavyo tunavifahamu na tumevizowea.

2. Kiama: Nayo ni kuwa baada ya kuvifufua viwiwili hivi na kuvitoa kwenye makaburi, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu atavifufua katika siku hiyo vyote katika jangwa kubwa na pana kwa ajili ya hesabu na malipo na huko kuwekwa mahakama kubwa na kuwekwa vipimo na mahakimu kuhudhuria-nao ni mitume wa Mwenyezi Mungu na mawasii wao-na kugawiwa madaftari ya matendo: Nyaraka za matendo ya waja na mashahidi kwa ajili ya kutoa ushahidi, na viungo vya mwanadamu kukiri juu ya matendo yaliyo tendwa na mwanadamu na kuyafanya, na waumini wale ambao walifanya matendo mema duniani kuneemeka kwa kuingia peponi na waovu wale ambao walikuwa wakitenda maovu duniani kuwa katika hali mbaya ya uovu na kuingia motoni. Kwa hivyo ni juu ya mwanadamu kujitahidi kwa kadri ya uwezo wake katika kutekeleza matendo mema na kujiepusha na matendo maovu, ili asije kuwa muovu huko katika Akhera uovu wa milele na milele, uovu usio kuwa na makimbilio wala muokozi, kiasi kwamba waovu watabakia jela wakati wote na wakiwa kwenye adhabu ya milelel.

Mwenyeziu Mungu anasema:

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾

Mwenye kufanya matendo ya kheri hata kama ni kiasi cha tembe moja atayaona. Na mwenye kufanmya matendo ya shari kiasi cha tembe moja atayaona[44] .

SEHEMU YA PILI MATAWI YA DINI

Kabla ya kuanza kubainisha na kufafanua sehemu ya pili katika mafunzo ya juu ya Uislaam, hapana budi kuashiria hapa ya kuwa sehemu ya kwanza ya mafunzo ya kiislaam ya hali ya juu na yaliyo matukufu yaani: Usulud-dini ambazo tumezi zungumzia, ni lazima mwanadamu aziitakidi au awe na itikadi nazo-kwani misingi hiyo ndio inayo husiana na ukafiri na itikadi- kutokana na ijtihadi na kwa kutegemea dalili na wala haitoshi kwenye misingi hiyo kujitegemeza sehemu fulani au kwa mtu fulani na kumfuata mtu huyo.

Wakati ambapo Furuud-dini (matawi ya dini), ambayo hivi sasa tuko mbioni kuyafafanua na kuyazungumzia, hakika matawi hayo yameenea na kuzihusu sehemu na nyanja zote za maisha na yanazihusu harakati zote za mwanadamu na matendo yake yote kabla ya kuzaliwa kwake mpaka baada ya kufariki kwake na maranyingi mwanadam-kwa sababu ni mambo yanayo husiana na matendo kama harakati za mwanadamu na kutulia kwake na utendaji au utekelezaji wa mambo ya aina tofauti na mabadiliko-hawezi kufanya ijtihadi (kujitahihi) katika mambo yote hayo na kufahamu hukumu zake kutokana na dalili zake kwa uchambuzi wake ulio tajwa katika vyanzo vine vya sheria: Qur'ani tukufu, Sunna sharifu- Yaani hadithi za Mtume(s.a.w.w) na riwaya za Ahlul bayti(a.s) - na Ijmaa (Makubaliano ya wanazuoni) na Akili, kwa hivyo Uislaam ukajuzisha (ukamruhusu) kwa mwanadamu kumfuata mujtahidi alie kusanya masharti ya kufuatwa (kufanyiwa taqliid) kwenye mas'ala hayo na kurejea kwake katika mas'ala hayo kwa ajili ya kumfanyia wepesi na kumrahisishia mambo.

Ndio, hakika matawi ya dini ni mengi sana na sisi tuta ashiria yale yaliyo muhimu sana nayo ni kumu yaliyo maarufu, kisha tutabainisha na kufafanua yale ambayo yanahitaji kufafanuliwa kati ya hayo inshaa allah taala ama matawi hayo kumi yaliyo maarufu ni kama yafuatayo:

1. Sala

2. Saumu (Funga)

3. Khumsi

4. Zaka

5. Hajji

6. Jihadi

7. Kuamrisha mema

8. Kukataza maovu

9. Kuwatawalisha mawalii wa Mwenyezi Mungu

10. kujitenga na kujiepusha na maadui wa Mwenyezi Mungu.

Kwa kuyafahamu hayo ni jambo lililo wazi kuwa matawi haya pamoja na kuongezea matawi mengine kama uuzaji (bayii) na ununuzi na Nikah (Ndoa) na Talaka, Kisasi na Diyaa (fidia), hayo yamefafanuliwa na kufanyiwa bahthi kwa upana zaidi katika kitabu hiki-katika kifungu cha masaail-lakini baadhi yaliyo muhimu kati ya hayo yamebakia na ambayo ni katika mambo yaliyo sambamba na yenye kuwiana na zama hizi tunazo ishi, kama jamii ya wanadamu na nidhamu ya kijamii na kisiasa, Uchumi, Jeshi na nguvu zadola, kama Jeshi la ulinzi na polisi, Mahakama na utoaji hukumu, Utamaduni na Vyombo vya habari, Afya na nyenzo za tiba, Uhuru wa kila mtu mmoja mmoja na uhuru wa jamii na mengineyo, haya ndio ambayo tutayazungumzia katika sehemu hii kwa utashi wake Allah.

JAMII NA DOLA (NIDHAM) LA KIISLAAM

Hakuna shaka ya kuwa Uislaam unayo nidhamu maalum ya utawala na uendeshaji wa mambo ya kijamii, kama ambavyo hakuna shaka ya kuwa nidhamu hii maalum ya kiislaam imekuwa ikitekelezwa katika nchi za kiislaam kwa muda wote wa karne kumi na tatu (13) mpaka lilipo anguka dola la kiislaam kabla ya zaidi ya nusu karne - sawa utekelezaji huo ulikuwa ni utekelezaji kamili wa kanuni zote au ulikuwa ni utekelezaji pungufu- Kisha mtu ana weza kusikia ya kuwa utamaduni wa kiislaam (Al-hadharatul- islaamiyyah) ulikuwa ni utamaduni wa aina yake na bora kwa kiwango kikubwa na ulio pituka tamaduni zingine zote, na anaweza kusikia ya kuwa Uislaam - kutokana na hekima za kanuni zake zitokazo mbinguni na zilizo na uadilifu-umebeba jukumu la kutatua matatizo yote ya ulimwengu na kwamba kanuni hizo lau kama zitatumika na kurudishwa kwenye utawala, dunia itabadilika na kuwa pepo yenye neema na watu kuishi kwenye kivuli na neema zake raha mustarehe, na wangeishi maisha mema na yenye raha tele.

Kwa msingi huo: Basi nidhamu hiyo ni ipi? Na je kuna uwezekano wa Nidhamu na Utawala wa kiisalam kurudi tena kwenye uhai katika zama hizi za upanukaji wa dunia na maendeleo ya kianga na maendelo ya atomi na katika zama za maendeleo ya Internet na kupanuka kwa habari na vyanzo vyake? Na ikiwa Uislaam utachukua Utawala vipi utaweza kutatua matatizo yaliyopo ya kiulimwengu? Hakika haya ni maswali yanayo paswa kupatiwa majibu

Na Pengine - majibu ya maswali tutakayo yataja hapa - yakaamsha hali ya mshangao na kustaajabu na msomaji kupigwa na butwaa na kudhania ya kuwa sisi tunazungumzia kuhusu mji ulio bora kabisa, pamoja na kuwa sisi tuna maandalizi kamili na tuko tayari kuondoa mshangao huo na kustaajabu huko kwa kutoa dalili na ushahidi wa kiisalaam juu ya majibu hayo[45] , na kutoa mifano hai na ya wazi kabisa kutoka kwenye historia ya utawala wa kiislaam ulio safi na halisi, jambo linalo thibitisha uwezo wa Utawala na Nidhamu ya kiislaam kurudi tena na kwa mara nyingine kwenye uhai na kushika hatamu ya uongozi na kuendesha mambo kwa ujasiri kamili na kwa umadhubuti bila kuteteleka, kwani Nidhamu ya kiisallam ndio Nidhamu pekee kati ya Nidhamu zote za ulimwengu- kuanzia hizo za zamani na za hivi sasa na zitakazo jitokeza kwa siku za baadae-kutokana na hekima za kanuni na sheria zake zitokazo mbinguni- yenye uwezo wa kuuendesha ulimwengu wenye maendeleo na ulio funguka au ulio wazi, uendeshaji uwezao kuufikisha kwenye matarajio yake na kuyathibitisha matumaini yake na kuutatulia matatizo yake na kuuondolea matatizo unayo kabiliana nayo na kuuondolea mambo yanayo usibu kama Uovu Madhara Ujinga Maradhi na kuufikisha ulimwengu huo kwenye ukingo wa Amani na Matumaini na kuufikisha kwenye ufukwe wa sa'aada na Amani, na Nidham hii imekusanya sababu na nyenzo zote za kuuletea maendeleo na kuufisha kileleni na kuyathibitisha yote ayatakayo mwanadamu katika nyanja hizi: kama Siasa Uchumi Uhuru na mengineyo ambayo tutayaelezea kwa muhtasari:[46]

UISLAAM NA SIASA

Swali : Je katika Dini ya kiislaam kuna siasa?

Jawabu : Ndio, ndani ya Uislaam kuna sehemu au fungu bora kabisa kati ya mafungu ya siasa na kuna aina nzuri kabisa kati ya aina za idara na uendeshaji wa nchi na wananchi (waja wa Mwenyezi Mungu).

Swali : Je utawala katika Uislaam ni utawala wa kijamhuri au ni utawala wa kifalme?

Jawabu : Utawala katika Uislaam si utawala wa kijamhuri wala wa kifalme-kwa maana ya kiistilahi ya maneno hayo yalivyo elezwa kwenye kamusi za ulimwengu wa kimagharibi (yaani kama yanavyo elezwa kwenye makamusi ya nchi za magharibi katika zama hizi-bali ni utawala wa mashauriano ya watu na inasihi kuuita kuwa ni utawala wa kijamhuri, kutokana na kuwa ni utawala unao tegemea mashauriano ya wananchi, kwani katika Uislaam hakuna utawala wa kifalme wa kurithishana.

Swali : Ni zipi sifa za mtawala (kiongozi) wa kiislaam?

Jawabu : Kiongozi wa kiislaam ni mtu muumini, mwenye elimu ya sheria ya dini ya kiislaam kikamilifu na mwenye kufahamu mambo ya kidunia na mwenye kusifika na sifa ya uadilifu kikamilifu, kwa hivyo basi mtu yeyote atakae kamilisha masharti haya na watu wengi kumridhia, basi anakuwa mtawala na akipungukiwa na moja wapo kati ya masharti haya atauzuliwa na kutolewa kwenye cheo chake kwa haraka sana, lakini ikiwa umma (watu) hawakuridhia abakie kwenye cheo chake hicho na kuwa raisi, na wanayo haki ya kumbadilisha na kumuweka mwingine alie kusanya masharti hayo.

Swali : Ni nani anae mteua mtawala wa kiislaam?

Jawabu : Sehemu kubwa ya umma (watu walio wengi) na hii inahusika tu ikiwa mtawala huyo au kiongozi huyo si maasuum alie teuliwa na Mwenyezi Mungu alie takasika na mtukufu kama Mtume(s.a.w.w) na maimamu watwaharifu(a.s) .