• Anza
  • Iliyopita
  • 4 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 5461 / Pakua: 1731
Kiwango Kiwango Kiwango
SURATUL-FAATIHA

SURATUL-FAATIHA

Mwandishi:
Swahili

SURATUL-FAATIHA

UTANGULIZI

Naomba kinga kutokana na shetani aliyelaaniwa, kuanza kwa Jina la Mola Ambaye ameumba, bila yeye Mwenyewe kuumbwa. Sifa zote zinamstahiki Allah (s.w.t) Ambaye ameiteremsha Qur'an Tukufu juu ya mja Wake mpenzi mno ili kwamba aweze kuwa mbebaji wa habari njema na muonyaji kwenye ulimwengu. Baraka ziwe juu ya Mtukufu Mtume (s.w.t) na juu ya kizazi chake kitoharifu ambao walitoharishwa kwa utakaso ulio kamili kabisa.

Naomba mwongozo kutoka kwa mola wa ulimwengu ili kuniwezesha kukamilisha jukumu hili kubwa ambalo ninaliingia kabla ya kuondoka kwenda kwenye awamu nyingine ya maisha yangu. Sijifikirii mwenyewe kuwa na uwezo hata wa kuweza kukwaruza uso wa Kitabu kitukufu mno ya vitabu vyote na nitajiona mwenyewe mwenye bahati kama ningekuwa na uwezo wa kufikisha kitu kidogo mno cha mabadiliko ya milele na maana ya Qur'an Tukufu kwa watu wa kawaida katika namna nyepesi ya kutosha kwa kadiri kwamba iwe rahisi kueleweka. Ili kufanikisha hili nitajaribu na kuepusha nyingi ya hoja za kifundi na kifilosofia ambazo huonekana kwa zaidi katika vitabu vikubwa vya tafsir.

Namuomba Allah (s.w.t) Aliye juu, kunipa umri mrefu wa kutosha kukamilisha tafsir hii na kukubali jaribio langu hili la unyenyekevu mno kuanza kulipa ajr-e-risaalat. Kwa mara nyigine tena namuomba Allah (s.w.t) Yeye aliye juu, kuniongoza na kunisaidia kuweka maelezo yangu kwenye lengo. Hakika Yeye ni Msaidizi na Kiongozi bora.

Mtumishi wa Allah (s.w.t) Bashir Haiderali Alidina

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ ﴿١١﴾

Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini na makafiri hawana Mlinzi - 47:11

MAONI ZAIDI

JINA

Sura hii inaitwa 'Ufunguzi Wa Kitabu', na kuna hadithi nyingi ambazo huonyesha kwamba hili ndilo jina ambalo kwamba kwalo ilijulikana wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume(s.a.w. w ) . Hivyo basi inashangaza kukona Waislamu wengi wakishikilia juu ya dhana kwamba Qur'an Tukufu haikuwa katika hali ya kitabu wakati wa uhai wa Mtukufu mtume(s.a.w. w ) , bali kwamba ilikuwa tu umekusanywa ivyo wakati wa Makhalifa wakati wa mwanzo. Naone nu ukosefu wa mantiki kwa mtu kutaja sura hii kama kuwa 'Ufunguzi Wa Kitabu' wakatai kitabu chenyewe kilikuwa hakipo. Hili hutiliwa nguvu zaidi na hadithi ya mwisho inayokubaliwa na wote ya Mtukufu Mtume(s.a.w.w) kuhusu vitu viwili vizito ambavyo kwavyo kimoja kilikuwa ni Qur'an Tukufu, ambavyo ilitajwa na yeye(s.a.w. w ) kama 'kitabu'. Ni kutokana na sura hii kwamba kawaida njia ya kufikia kwenye kitabu hiki hupatikana, kwa vile huchukuliwa kama mukhtasari mfupi wa kitabu chote.

Qur'an Tukufu ni mwonogozo kwa wacha Mungu, na mtu anavyozidi kuwa Mcha Mungu ndivyo anavyozidi kuongozwa na kitabu hiki. Kitabu hiki kinakawaida ya 'kufunguka' kwa ajili ya muongozo kwa wasomaji wake kwa kutegemea kiwango cha uchaji Mungu wao na elimu. Ama kwa wasomaji wengine anbao sio wacha Mungu, kwa kawaida kitabu hiki hufunga mlango wake, na watapita jiji la elimu kwa kweli bila kuingia ndani yake kwa kupitia mlango wake na kunufaika kutokana nayo. Hufuatilia kutokana na maneno hayo hapo juu kwamba kitabu hiki kitafunguka zaidi kwa muongozo kwa 'Imam Al Muttakiin' kwa vile kwa hakika alikuwa mwenye elimu zaidi na Mcha Mugu zaidi kama ambavyo kwa pamoja marafiki zake na halikadhalika maadui zake isipokuwa Allah (s.w.t) na wale ambao wamezama ndani kwa imara katika elimu.

ILITEREMSHIWA WAPI?

Sura hii iliteremshiwa Makka, lakini kuna baadhi ya Wafasir ambao wamechukulia maoni ya kwamba hii ni moja ya Sura ambayo iliteremshwa mara mbili, kwanza ni katika mji wa Makka na mara nyingine tena katika mji wa Madina.

Maoni hayo ambayo vile vile yanatolewa na baadhi ya hadithi, yataifanya kuwa ni sura pekee iliyopata kuteremshwa mara mbili, huenda kwanza kama sehemu ya kitabu na tena kama Sura inayojitegemea.

IDADI YA AYA

Kuna watu wachache walio na maoni ya kwamba Sura hii ina aya sita na kwamba 'Bismillah' ni sehemu na fungu la sura hii na kwamba idadi ya aya ni saba. Maoni haya yanategemea juu aya ifuatayo:

وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعًا مِّنَ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ ﴿٨٧﴾

Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu (15:87).

Hii huleta swali la iwapo kama sura hii yenyewe ni sehemu ya Qur'an Tukufu au la. Kuna hadithi ya Kiutume isemayo kwamba:"Allah (s.w.t) ameweka juu yangu mimi upendeleo kwa kunipa mimi sura hii, na kuifanya sawa sawa na Qur'an na hii ni moja ya Hazina bora za Arish". [1]

Yeye(s.a.w. w ) binafsi amewaamrisha Waislamu kuiweka sura hii mwanzoni mwa Qur'an Tukufu, na kuifanya kama ufunguzi wa Kitabu. Zaidi ya hayo, Qur'an Tukufu ni Kitabu kamili na sio pungufu katika hali yeyote, kama ilivyoeleza kabla, na hivyo vipi ingeliweza kuwa kamili bila kuwa na ufunguzi wake. Allah (s.w.t) Mwenyewe amedai kwamba Yeye (s.w.t) ameikamilisha dini yetu na ametimiza neema Zake.

UTAALAM

Sifa moja ambayo kutofautisha sura hii na nyingine, ni lugha na dhamira yake. Ambapo sura nyingine zimeteremshwa katika maneno ya Allah (s.w.t), hii iliteremshwa katika hali ambayo kwamba iko katika maneno ya watumishi wa Allah (s.w.t).

Hutupa sisi mafunzo muhimu kutuwezesha sisi kuongea na Allah (s.w.t). Hutuweka sisi taktika hali wa akili ya sawa sawa kabla ya kwenda kuomba chochote.

MANUFAA YAKE

Sura hii ni msingi wa Qur'an Tukufa na malipo kwa ajili ya kisomo chake ni saw na yale ya kitabu chote. Vile vile imesimuliwa kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari kwamba nguvu za kuponya za sura hii huweza kuponya magonjwa zote isipokuwa kifo. Kwa kweli ziko hadithi ambazo husema kwamba hata kifo kinaweza kuahirishwa kwa msaada wa sura hii. Mtukufu Mtume(s.a.w. w ) alisema kwamba: "Allah, Ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake, Alisema - 'Nimegawnya Ufunguzi wa Kitabu hiki kati Yangu na mja mtumishi Wangu; hivyo, nusu yake ni kwa ajili Yangu na nusu nyingine ni kwa ajili ya mtumishi Wangu. Na mja Wangu atapata kile anachokiomba kwayo.

Wakaji mja anaposema: 'Kwa Jina la Allah Mwenye kuneemesha na Mwenye Kurehemu', Allah, ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake, Husema; 'Mja Wangu ameanza kwa kulitaja Jina Langu, na ni wajibu juu Yangu Mimi kwamba Yanipasa kukamilisha kazi zake kwa ajili yake na kumbariki katika mambo yake'.

Na wakati akisema:'Shukrani zote zinastahiki Allah, Mola wa ulimwengu wote'. Allah, Ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake, Husema; 'Mja Wangu amenitukuza Mimi, na najua kwamba neema alizonazo zinatoka Kwangu, na kwamba balaa ambazo zimeepushwa kutoka kwake zimeepushwa hivyo kwa Rehemu Yangu; Enyi Malaika Wangu! Nimewateua ninyi kama mashahidi kwamba nitaongeza neema kwa ajili yake za ulimwengu ujao (Akhera) kwa zile za ulimwengu huu, na nitaepusha kutoka kwake misiba ya ulimwengu ujao (akhera) kama nilivyoepusha kutoka kwake misiba ya ulimwengu huu.'

Na wakati akisema: 'Mwenye Rehema na Mwenye Kurehemu', Allah, Ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake Husema :"Mja Wangu anatia ushuhuda kwa ajili Yangu Mimi kwamba Mimi ni Mwenye Rehema na Mwenye Kurehemu; Ninawafanya ninyi mashahidi wangu kwamba hakika kweli kabisa nitazidisha mgao wake katika Rehema Yangu, na kwa hakika kabisa nitaongeza mgao wake katika neema Zangu.'

Na wakati anaposema, 'Mola kwa siku ya malipo', Allah Alye Juu Husema; "Ninakufanyeni ninyi mashahidi kwamba, kwa vile amekubali kwamba Mimi ni Mola wa siku ya malipo, kwa hakika kabisa mtafanya hesabu yake kuwa rahisi mno (kwa ajili yake) katika siky ya hesabu, na kwa hakika kabisa nitakubali matendo yake mema, na sitaangalia madhambi yake".

Na wakati anaposema, 'Yeye Peke Yake tunamuabudu', Allah ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake Husema; "Mja wangu anasema kweli, ananiabudu Mimi tu. Kuweni mashahidi wangu kwamba hakika nitampa kwa ajili ya ibada yake zawadi ambayo atakuwa (ni kitu cha) kuonewa wivu kwa wote ambao walimpinga wakati akiniabudu Mimi".

Na wakati akisema: 'Na Kwake tunataka msaada', Allah, Aliye Juu, Husema; "Mja wangu ametaka msaada kutoka kwangu, na kwangu Mimi amechukuwa hifadhi. Kuweni mashahidi wangu kwamba kwa hakika kabisa nitamsaidia katika mambo yake, na nitamsaidia katika shida zake, na nitampa msaada katika misiba yake".

Na wakati anaposema; 'Tuongeze katika njia iliyoonyooka . ', Allah, Ambaye Nguvu na Uwezo wote ni Wake Husema; "Hii (sehemu) ni kwa ajili ya mja Wangu, atapata kile alichokiomba; na nimejibu du'a ya mja Wangu, na nimempa kwa ajili yake kile anachokitumaini; na nimemlinda kwa kile anachokihofia"[2] .

Kwo wote pamoja imekubaliwa na Waislamu wote kwamba ni wajibu kuisoma sura hii wakati Sala au kwamba vinginevyo Sala hiyo kaitaswihi. Hii peke yake inatosha kwa ajili ya utukufu wake kuhusiana na sura nyingine za Qur'an Tukufu. Imesimuliwa kutoka kwa Imamu Ja'far Al Sadiq(a.s) kwamba: "Mara nne Iblisi alilia; kwanza, wakati alipotumwa nje ya mkusanyiko; pili, alipotupwa nje ya bustani na kuletwa chini kwenye ardhi; tatu, wakati Mtukufu Mtume(s.a.w.w) alipolekezwa kutangaza utume wake; na nne wakati sura hii ilipoteremshwa."[3]