MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.)

MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.) 0%

MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.) Mwandishi:
: S. Muhammad Ridha Shushtary
Kundi: Midahalo na majadiliano kielimu

MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.)

Mwandishi: Sheikh Tabarsiy
: S. Muhammad Ridha Shushtary
Kundi:

Matembeleo: 5461
Pakua: 1613

Maelezo zaidi:

MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.)
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 3 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 5461 / Pakua: 1613
Kiwango Kiwango Kiwango
MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.)

MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.)

Mwandishi:
Swahili

1

MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.)

Safari moja Imamu Ja'far Swadiq(a.s.) aliwahi kuhojiana na Mlahidi mmoja, na mahojiano hayo yalikwenda kama ifuatavyo: -

MLAHIDI

Vipi viumbe wanaweza kumwabudu Mwenyeezi Mungu ambaye hawamwoni?.

IMAMU

Nyoyo ziaminizo humwona Mwenyeezi Mungu kwa kufahamu. Imani Wenye hekima hukujua kuwepo kwa Mwenyeezi Mungu kwa ajili ya hekima zao. Wale wenye maarifa, humwona Yeye kwa sababu ya nidhamu inayolingana ya maumbile na sheria yake. Vile vile, Mwenyeezi Mungu hujulikana kwa sababu ya Mitume, Manabii, Vitabu Vitakatifu na dalili zao. Wanavyuoni wanapotafakari juu ya Utukufu wake, wanajiona kwamba hawawezi kumwona (kuwa ni mwenye umbo).

MLAHIDI

Je, Mwenyeezi Mungu hana uwezo wa kujionyesha binafsi kwa viumbe vyake, ili kwamba kwa kuonekana Kwake, waweze kumfahamu na kumwabudu kwa imani?

IMAMU

Hakuna jibu kwa kitu kisichoyumkinika. Haiyumkiniki, kwa sababu tendo la kuangalia kitu au kinachoangaliwa huwa wakati miali yake inapofika juu ya macho (retina) yetu na kufanya taswira yake. Kwa kufanyika taswira ni lazima kwamba kinachoangaliwa kiwe ni kitu (chenye umbo), ili kwamba kila kijisehemu chake kidogo kiwe kinatoa mwalii wa kufanya taswira. Hivyo, vitu viwili ni lazima. Kwanza, kinachoangaliwa kiwe ni kitu, Pili, miali ya mwanga ifike machoni mwetu. Mwenyeezi Mungu ni Mwangaza (Nuru) wa mbingu na ardhi. Mtu yeyote hawezi kuliangalia jua wakati wa adhuhuri katika Kiangazi, ingawa huwa ni mwangaza mdogo. Macho ya nani yanathubutu kuangalia mwanga wa Mwangaza (yaani Mwenyezi Mungu) Ambaye hana kifani? Hivyo, haiwezekani kumuona Yeye.Isitoshe, kitu kitazamwacho lazima kiwe na "uzito" (dense) kwa ajili ya kuona na kugusa. Chukua mfano wa hewa. Uzito wake ni mdogo.Ingawa haionekani, lakini inahisika.Mwenyeezi Mungu hana uzito.

MLAHIDI

Vipi unathibitisha kuwepo kwa Manabii na Mitume wa Mwenyeezi Mungu?

IMAMU

Inapothibitika kwamba Muumba wetu ni Mwenyeezi Mungu Mtukufu, na ni Muumba Mwenye Hekima, haiwezekani kwa viumbe vyake kumuoa, kumgusa, kumwenza au kuzungumza Naye, hivyo, ni lazima kwamba Manabii na Mitume Wake wawe ni miongoni mwa viumbe Vyake, ili kwamba waweze kuwawaidhi waja Wake yale mambo yenye manufaa kwao, na ambayo ni muhimu kwa kuwepo kwao, na ikiwa hatutawafuata, itatuongoza kwenye mauti. Hivyo, ni lazima Mwenyeezi Mungu kwa ajuaye kuwapelekea viumbe vyake Mitume wake, ambao wanawaamrisha mema na kuwakataza maovu, nao watabaki na kuendelea kuwepo katika dunia hii kutoka Kwake. Wao ni Mitume na Manabii wake miongoni mwa viumbe vyake. Wanawafundisha watu hekima, na wanajishirikisha pamoja nao katika mambo yao. Mwenyeezi Mungu amewapa elimu, hekima, hoja na dalili, kwa mfano, wanawahuisha maiti, wanawaponyesha vilema n.k. Hivyo, dunia haiwezi kuwa tupu bila ya "Hoja"(Imamu) ya Mwenyeezi Mungu, ambaye ana elimu ni shahidi wa maneno na vitendo vya haki vya Mtume, na uadilifu wa Mwenyeezi Mungu. Baada ya haya, Imamu(a.s) alisema: Tunaamini kwamba dunia haiwezi kuwa tupu bila ya "Hoja" (Maiamamu) Zake zinazotoka katika kizazi cha Mitume tu; vile vile Mwenyeezi Mungu humchagua Mtume Wake miongoni mwa kizazi cha Mitume. Ni hivyo, kwa sababu Mwenyeezi Mungu ameweka njia imulikayo kwa wanaadamu. Ameumba kizazi tohara na kisafi, na miongoni mwao amewachagua Mitume na Manabii Wake ambao ni wateule wa Mwenyeezi Mungu na mfano bora kwa wanaadamu.

Walitoharishwa tangu kwenye manii ya wazazi wao na wakawekwa salama katika mifuko ya uzazi ya mama zao. Uchafu wa ujinga haukuwagusa, wala hawakuchanganyika nao baadaye, kwa sababu Mwenyeezi Mungu amewapa daraja tukufu na dhimu kabisa. Hivyo, yeye ambaye ni hazina ya elimu ya Mwenyeezi Mungu, mdhamini Wake wa yasioonekana, mwenye kujua siri Zake Hoja Yake kwa viumbe Vyake, kinywa chake na ulimi Wake, lazima awe nazo sifa Zake. Kwa hivyo, Hoja (yaani Imamu) anatoka miongoni mwa vizazi vya Mitume, ili kwamba kwa kuwa nayo elimu ya Mtume aweze kuwa badala ya Mtume, na amrithi kama wasii wake, ili kwamba ikiwa watu watakataa kumkubali, aweze kuwanyamazisha. Elimu ya Mtume wa mwenyeezi Mungu (s.w.t.) ambayo watu walikuwa nayo, ilidumu (baada ya Mtume Mtukufu) kwa muda mfupi, kwa sababu kwa haraka tofauti kati yao zikatokeza, na wakaanza kutumia maoni na fikara zao wenyewe. Kama wangelimkubali Hoja (Imamu au Khalifa) wakamtii na kumfuata, haki ingesimamiwa na Hoja, tofauti na mabishano yangeondoka, dini ingekuwa imara na salama, na imani ingeshinda shaka. Baada ya kufariki kwa Mtume wa Mwenyeezi Mungu (s.w.t.),watu hawakuungana kumfuata Hoja huyo, wala kumtii. Kwa hakika, hakuna Mtume au Nabii wa Mwenyeezi Mungu, ambaye umati wake hawakutofautiana baada yake. Sababu ya tofauti zao miongoni mwao ni kwa ajili ya kupinga na kujitenga na Hoja, ambaye amechaguliwa baada ya Mtume wa Mwenyeezi Mungu.

MLAHIDI

Vipi watu wamtendee Hoja (Imamu) mwenye sifa hizo ulizozitaja?.

IMAMU

Watu wamfuate.Hoja huyo atawaonyesha hakika ya mambo ambayo yatawafaa watu.Ikiwa wataongeza mambo mapya (bid'a) katika dini, atawaonya.Ikiwa wataongeza chochote ndani yake, atawatahadharisha.Ikiwa watapunguza chochote ndani yake, atawakataza.

MLAHIDI

Kutokana na kitu gani Mwenyeezi Mungu ameumba vitu vyote?

IMAMU

Hakuviumba kutokana na kitu chochote.

MLAHIDI

Ikiwa chochote hakikuwepo, vipi vitu vimeumbwa bila ya chochote?.

IMAMU

Lazima kuwepo mambo mawili.Ama vitu vyote vya ulimwenguni vimumbwa kutokana na "kitu" au katokana na "bure". Ikiwa vimeumbwa kutokana na "kitu," basi "kitu" hicho lazima kiwe cha Mwenyeezi Mungu. Kitu cha azali hakichakai (hakina mwanzo wala mwisho).Hakitoweki wala hakibadiliki.Ni lazima vile vile kwa "kitu" hiki cha azali kiwe nafsi moja na rangi moja. Basi kwa nini panapatikana nafsi tofauti na rangi tofauti? Ikiwa "kitu" hicho cha azali kilikuwa na uhai ambao kwa huo, vitu vyote vimetoka, basi kifo kimetokea wapi? Na ikiwa "kitu" hicho hakina uhai, basi vitu hivi vilipata wapi uhai?.

Aidha, ni upuuzi kusema kwamba kunaweza kuwepo vitu viwili vya azali - kimoja chenye uhai, kwa sababu kitu kisicho na uhai hakiwezi kutokana na kitu chenye uhai. Vile vile ni upuuzi kusema kwamba "kitu" kisichokuwa na uhai ni cha azali, kwa sababu "kitu" kisichokuwa na uhai hakina nguvu wala uthabiti

MLAHIDI

Basi kwa nini wanasema kwamba vitu ni vya azali?

IMAMU

Wanaosema hivyo ni wale watu ambao wanakana kuwepo kwa Msawiki hasa wa vitu. Wameyakana maneno ya Mtume na Manabii wa Mwenyeezi Mungu.Wamekataa kusikiliza wasemayo Mitume Watukufu. Wameviita vitabu vyao "Asatiyrul-Awwaliyn" (Hadithi za watu wa zamani). Wameasi dini yao nyingine kwa ajili ya maoni na fikara zao wenyewe.Kwa kweli, "vitu" vyenyewe vinathibitisha kwamba vitaangamia. Mbingu inazunguka pamoja na vitu vyote hivyo ambavyo ni pamoja na vyote vilivyomo ndani yake, inazunguka pia. Mabadiliko ya maisha na wakati, na matukio yanayotokea, yanasababisha kuzidi na kupungua, mauti na kuharibika dunia. Mambo yote haya yanailazimisha akili ya mtu kukiri kwamba kuna Mwenye Hekima na Nguvu ambaye ni Muumba. Mambo yote haya yanathibitisha kwamba dunia hii ni ya muda tu. Kila kitu kinatuongoza kwenye mabadiliko na kuharibika.

MLAHIDI

Je, Muumba wa dunia hii alijua kabla ya kuumba dunia kwamba mabadiliko yote haya na uharibifu utatokea?

IMAMU

Yeye alijua tokea azali.Hivyo,aliumba dunia ambayo alijua kila kitu chake tangu mwanzo.

MLAHIDI

Je, Mwenyeezi Mungu ni mwenye maumbo tofauti au ni 'murakkab' (mchanganyiko wa vitu)?

IMAMU

Kwa kweli, Yeye si chochote katika hivyo.Kwa sababu "tofauti" maana yake ni sehemu mbali mbali, na 'murakkab' maana yake ni viungo vyake ni tofauti na vimechanganyika.

MLAHIDI

Basi nini maana y a kusema kuwa Mwenyeezi Mungu ni Mmoja?

IMAMU

Yeye ni Mmoja kwa maana ya kuwa Dhati Yake ni Kamili, Yeye si pekee kama "vitu" vingine, kwa sababu kila kitu kimefanywa kwa vijisehemu isipokuwa Mwenyeezi Mungu tu Ambaye ni Mkamilifu na hana sehemu za kuhesabiwa.

MLAHIDI

Kwa nini Ametuumba sisi,ingawa hana haja nasi wala hakulazimishwa kufanya hivyo? Wala haiwi kuwa ametuumba bure?.

IMAMU

Ametuumba ili kwamba Hekima Yake ibainike, Elimu Yake ijulikane, na kuona Kwake mambo yajayo kutambulikane.

MLAHIDI

Kwa nini hakujiwekea Mwenyewe uumbaji wa dunia? Angeweza kuifanya Mahali pa Malipo na Mahali pa Adhabu. Yaani, watu wangeweza kupata malipo na adhabu katika dunia hii?

IMAMU

Sababu ni kwamba dunia hii ni mahali pa majaribio (mtihani), ambayo kwayo malipo yanapatikana na baraka zinanufaika. Ndani yake kuna balaa na matamanio, ili kwamba viumbeVyake viweze kujitakia chochote wakipendacho.Mahali pa majaribio hapawezi kuwa mahali pa Malipo.

MLAHIDI

Kuna umuhimu gani Kwake kumuumba adui Yake, ingawa hakuwa na adui mwanzo.Kama unavyosema, 'Yeye Mwenyeezi Mungu amemuumba Shetani (Ibilisi na kumfanya awatawale viumbe Vyake ili kwamba aweze kuwashawishi watu wasimtii Mwenyeezi Mungu. Shetani huwashawishi watende dhambi, na kama unavyofikiri, Mwenyeezi Mungu vile vile amempa nguvu, ambayo kwayo hufikilia nyoyo zao kwa njia nyingi na kuzitia shaka. Huwafanya kuwa wenye shaka juu ya Mwenyeezi Mungu na dini.Kwa sababu hii, hawawezi kumtambua, Mwenyeezi Mungu. Wale ambao wamekuwa na shaka katika nyoyo zao wanaukana Utukufu wa Mwenyeezi Mungu.Wameanza kuwaabudu wengine badala ya Mwenyeezi Mungu. Kwa nini Mwenyeezi Mungu amemruhusu Shetani awatawale viumbe Vyake na kumpa fursa ya kuwapoteza?

IMAMU

Sababu ni kuwa uadui wa Shetani hauwezi kumdhuru Yeye wala urafiki wake haumnufaishi. Uadui wa Shetani hauwezi kupunguza chochote katika Utukufu Wake, wala mapenzi yake kwa ajili Yake hayawezi kuongeza chochote. Adui anaepukwa wakati nguvu zake zinapoweza kutudhuru, au anapoasi huweza kuhujumu nchi yetu na kutushinda. Shetani ni kiumbe chake tu, ambaye amemuumba ili aweze kumwabudu na kuuamini Umoja Wake. Mwenyeezi Mungu alipomuumba alijua mwanozo wake na mwisho wake utakuwa vipi. Shetani alibaki pamoja na malaika, na alikuwa akimwabudu Yeye, mpaka alipomfanyia mtihani kwa kumwambia amsujudie Adamu. Kwa sababu ya kiburi chake na ubaya wake ambao ulimtawala, Shetani alikataa kusujudu. Kwa hivyo, Mwenyeezi Mungu akamlaani na kumwondoa miongoni mwa daraja za malaika na akamteremsha duniani akiwa amefukuzwa. Kwa sababu hii, alimfanyi uadui Adamu na vizazi vya Adamu. Shetani hana utawala juu ya wana wa Adamu. Yeye anapoteza tu kwa kuwadanganya na kwa kuwatia shaka katika akili zao, ingawa yeye mwenyewe anaamini kuwa Mwenyeezi Mungu Yu Mola.

MLAHIDI

Je, kumsujudia yeyote asiyekuwa Mwenyeezi Mungu kunaruhusiwa?.

IMAMU

La!

MLAHIDI

Basi kwa nini Mwenyeezi Mungu aliwaamuru malaika wamsujudie Adamu?

IMAMU

Ikiwa mtu amesujudu kwa amri ya Mwenyeezi Mungu, ina maana kwamba amemsujudia Mwenyeezi Mungu. Sijda yake itakuwa kwa ajili ya Mwenyeezi Mungu kwa maana amefanya kwa amri Yake.

MLAHIDI

Nini ukweli wa uramli? Vipi tunajua matokeo ya baadae kwa kupiga ramli?

IMAMU

Uramli ulikuwa ukitumika wakati wa ujahili kati ya zama za Mitume. Mpiga ramli alikuwa kama Mola. Katika mambo ambayo watu walikuwa na shaka juu yao, walitaka shauri ya wapiga ramli, ambao waliwatabiria matukio ya baadaye. Waliendelea kupiga ramli kwa njia mbali mbali. Kama vile kutazama sura ya mtu, kutumia akili, madaraka ya shetani na utambuzi wa kiroho. Walikuwa na ushirikiano wa kishetani, kwa sababu Shetani alijua mambo yote yaliyotokea au yatakayotokea katika sehemu yoyote ya dunia, naye aliwapasha habari wapiga ramli. Ama kuhusu mambo ya mbinguni, mashetani waliketi mahali pafaapo ambapo wangesikia mambo hayo. Katika siku hizo, mashetani hawakuzuiliwa kwenda, nao haikuwasibu taabu yoyote kwa ajili ya utabiri (unajimu). Lakini sasa wamezuiliwa kusikiliza mambo hayo, ili watu wasiingiwe na shaka baina ya 'wahyi' (ufunuo wa Mwenyeezi Mungu) na habari za mbinguni, na waweze kujua yale yaliyokuja kutoka kwa Mwenyeezi Mungu. Aliyakamata huko na akayaleta duniani na kumwambia mpiga ramli. Mpiga ramli pia, kwa shauri lake aliyaongezea mambo mengine na kuchanganya kweli na uwongo. Tabiri za mpiga ramli, ambazo mara nyingi zilikuwa kweli, zilikwa maneno ya Mwenyeezi Mungu ambayo Shetani aliyasikia na kumpa mtu. Tabiri ambazo hazikuwa kweli, zilikuwa uwongo kwa sababu ya maongozo ya mpiga ramli mwenyewe.Tangu mashetani walipozuiliwa wasisikie siri za mbinguni, uramli ukakoma. Sasa mashetani wanawaambia wapiga ramli wao yale waliyoyasikia kutoka kwa watu wengine, na vile vile wanawaambia yale ambayo mashetani wamewaambia, mathalan, wanawaambia juu ya mtu aliyetoweka, na juu muuaji nakadhalika. Miongoni mwao, wako pia wanaosema uwongo au wanaosema ukweli kama wanadamu.

MLAHIDI

Vipi mashetani wanaweza kupanda mbinguni,ingawa wana umbo la asili ya kiwili wili? Vipi waliweza kumjengea Nabii Suleiman(a.s) majumba makubwa na ya ajabu ambayo hakuna binaadamu yeyote anayeweza kufanya?

IMAMU

Tangu Nabii Suleiman(a.s.) alipowamiliki, walijifanya umbo lenye kiwiliwili. Wao wana umbo la kiroho, na chakula chao ni hewa. Wanaweza kupanda mbinguni kusikiliza mazungumzo,wakati umbo lenye kiwiliwili haliwezi kupanda mbinguni bila kipandio au kamba.

MLAHIDI

Vema, tuambie nini ukweli wa uchawi (usihir)?Vipi mchawi anafanya uchawi wake?

IMAMU

Uchawu ni wa aina nyingi. Moja katika aina zake ni kama elimu ya tiba. Kama mganga anavyotoa dawa kwa kila maradhi, wachawi vile vile wanatumia uchawi wao kuleta maradhi, shida n.k. kwa mtu. Aina ya pili ya uchawi ni kiinimacho ambacho hugeuza mambo yanayotokea kwa kudanganya macho, kwa mfano, vitu vizito huonekana vyepesi na kadhalika. Aina ya tatu ni ile ambayo mashetani wanawachukulia kwao.

MLAHIDI

Elimu ya mashetani inatoka wapi? Yaani,vipi mashetani wanapata elimu?

IMAMU

Kama mganga anavyopata elimu kwa kutibu watu. Mara nyingine kwa majaribio na mara nyingine kwa matibabu.

MLAHIDI

Unasemaje kuhusu malaika wawili Harut na Marut? Je,wao waliwafundisha watu uchawi?

IMAMU

Hapa ni mahali pa mtihani mkubwa. Wote walikuwa wakisema kwamba ikiwa mtu atafanya kitu fulani na fulani, matokeo yake yatakuwa Fulani na fulani. Watu walijifunza kwao yale waliyokuwa wakisema. Walikuwa wakisema:"Sisi ni chanzo cha mtihani, msijifunze kwetu yaliyo na madhara kwenu,au yasiyokuwa na faida yoyote kwenu."

MLAHIDI

Je,wachawi wanaweza kumgeuza mtu awe mbwa au punda?

IMAMU

Mchawi hawezi kufanya hivyo.Hakupo chini ya uwezo wake kugeuza umbo aliloliumba Mwenyeezi Mungu na kuwa umbo jingine. Ikiwa mtu anaweza kukibadili au kukigeuza kile kilichoumbwa na Mwenyeezi Mungu, ina maana kuwa yeye ni mshirika wa Mwenyeezi Mungu katika kuumba vitu. Kama mchawi angeweza kufanya mambo hayo, basi yeye mwenyewe angeweza kujiondolea huzuni, shida, balaa na maradhi, angeweza kujigeuza kuwa kijana, angeweza kujifanya tajiri. Kwa kweli, uchawi mkubwa ni kusengenya, ambako husababisha uadui miongoni mwa marafiki, na huongeza chuki kati ya maadui. Husababisha umwagikaji wa damu na kuangamia kwa jamii.Huwaletea fedheha. Kwa hakika, msengenyaji ni mtu mwovu kabisa duniani. Jambo barabara linaloweza kusemwa juu ya uchawi ni kuwa ni kama elimu ya tiba. Mchawi anaweza kutumia nguvu yake juu ya watu kwa kadiri ya kuweza kumfanya mtu asiweze kumjamii mwanamke. Lakini mganga anaweza hubatilisha nguvu yake na kumrudisha nguvu yake na kumrudisha katika siha nzuri.

MLAHIDI

Ikoje miongoni mwa kizazi cha Nabii Adamu (a.s.) mmoja ni mtu bora na mwingine ni mtu duni?

IMAMU

Mtu bora ni yule ambaye ni mtiifu kwa Mwenyeezi Mungu na mtu duni na mbaya ni yule ambaye ni muasi na mhalifu.

MLAHIDI

Je, hakuna tofauti yoyote katika daraja zao?.

IMAMU

Tofauti yao ni katika uchamungu.

MLAHIDI

Kwa hivyo, tunaweza kusema kuwa wana wa Adamu(a.s) wote ni sawa. Mmoja ni bora kuliko mwenziwe kwa sababu ya uchamungu wake tu.

IMAMU

Ndivyo ilivyo.Tunavyoona sisi ni kuwa sote tumeumbwa kutokana na udongo, na wazazi wa kila mtu ni Adamu(a.s) , na Hawa(a.s), na Mwenyeezi Mungu ni Mmoja ambaye ndiye aliyewaumba. Wao ni viumbe wa Mwenyeezi Mungu. Bila shaka, Mwenyeezi Mungu amewachagua baadhi ya wana wa Adamu(a.s) na kuwafanya wazaliwe watoharifu (Mwenyeezi Mungu) ameitakasa miili yao, amewahifadhi katika manii ya baba zao, na katika mifuko ya uzazi ya mama zao, na katika wale aliowachagua, amewapeleka Mitume na Manabii wake. Hivyo, wao ni kizazi kitoharifu kabisa cha wana wa Adamu. Kuchaguliwa na kuteuliwa kwao kuwa Mitume na Manabii hakukuwa kwa sababu ya haki yao. Lakini Mwenyeezi Mungu alipoumba roho zao alijua kwamba watamtii, watamwabudu na hawatamshirikisha yeyote pamoja naye. Ni kwa sababu ya ibada yao, Mwenyeezi Mungu amewapa hadhi kubwa na tukufu kama hivyo. Hao ni watu ambao ni bora kuliko wengine. Waliobaki wote ni sawa. Kati yao, Mwenyeezi Mungu atawapa hadhi kubwa kwa wale watu ambao wanamcha, na atawapenda wale ambao wanamtii, na hatawafanya wale watu ambao anawapenda waadhibike na moto wa Jahannamu.

MLAHIDI

Kwa nini Mwenyezi Mungu hakumfanya kila mtu kuwa anamini Mungu Mmoja na kuwa mtiifu Kwake, ingawa alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo?

IMAMU

Kama angeliwafanya wote wawe watiifu Kwake, basi wasingepata malipo yoyote, kwa sababu kwa jambo hilo utii usingekuwa kitendo chao wenyewe. Na kama hakuna kitendo kwa kupande wao, basi kusingekuwepo Pepo wala Moto. Hivyo basi, kwanza aliwaumba, tena akawaamuru wamtii Yeye na wajiepushe wasifanye madhambi. Tena aliwatuma Mitume na Manabii na akathibitisha dalili zake. Akawateremshia Vitabu Vyake ili kwa hivyo wajue kwamba anayemtii Yeye ataingia Peponi, na anayemuasi Yeye ataingia Motoni.

MLAHIDI

Kwa hivyo, ina maana kwamba vitendo vyote viwili - vizuri na vibaya, ni vitendo vya viumbe wa Mwenyeezi Mungu?

IMAMU

Ndiyo! Kitendo kizuri kinatendwa na viumbe kwa agizo la Mwenyeezi Mungu. Kitendo kibaya kinatendwa na viumbe wenyewe, ingawa Mwenyeezi Mungu amewakataza kutenda hicho.

MLAHIDI

Je, vitendo vya viumbe si vinatendwa kwa viungo vya mwili, ambao Mwenyeezi Mungu amempa?

IMAMMU

Ndiyo.Viungo vya mwili ambavyo anavitumia kufanya vitendo vizuri ni vile vile ambavyo anavitumilia kufanya vitendo vibaya, lakini Mwenyeezi Mungu amemkataza asifanye vitendo vibaya.

MLAHIDI

Kwa kadiri gani mtu ana jukumu juu ya masharti aliyoamriwa?.

IMAMU

Ikiwa Allah anamkataza kiumbe Chake asifanye jambo fulani,Yeye anajua kwamba (kiumbe) anaweza kujiepusha nalo, na ikiwa anmwamuru kufanya jmbo fulani, anajua kwamba anweza kulifanya hilo. Kwa hivyo, hakuna dhuluma au upuuzi ndani yake.Na Mwenyeezi Mungu hamuamuru mtu sharti lolote ila tu lipo chini ya uwezo wake.

MLAHIDI

Mwenyeezi Mungu alipomuumba mtu fulani kuwa kafiri,je, (mtu alikuwa nao uwezo wa kufahamu imani (ya kweli), yaani alikuwa na uwezo wa kuikubali imani)? Na kama alikuwa nao, je, kulikuwepo dalili yoyote kwamba alitaka kuikubali imani?

IMAMU

Mwenyeezi Mungu amemuumba kila mtu Mwislamu, na amemuamuria masharti juu yake na amemkataza mambo fulani. Neno la ukafiri linatiwa juu ya kitendo fulani anapokifanya kiumbe wa Mwenyeezi Mungu. Mwenyeezi Mungu hamuumbi mtu yeyote kuwa kafiri. Yeye (mtu) hujifanya kafiri wakati dalili ya Mwenyeezi Mungu inapomjia na anapopewa Haki, yeye hukataa kuzikubali. Hivyo, anapokataa Haki huwa kafiri.

MLAHIDI

Je, inafaa kwamba Mwenyeezi Mungu amjaalie mtu maovu, kisha amuamuru afanye mema na atakaposhindwa kufanya mema, Mwenyeezi Mungu atamwadhibu?

IMAMU

Haistahili kwa uadilifu na rehema ya Mwenyeezi Mungu kumjaalia mtu maovu. Haiyumkiniki kwa Mwenyeezi Mungu amjaalie mtu fulani aabudu sanamu, kisha amuamuru kufanya jambo ambalo Mwenyeezi Mungu anajua kuwa halipo chini ya uwezo wa kiumbe chake, au amkataze mtu fulani kufanya jambo fulani ambalo Yeye anajua kuwa haiyumkiniki kwake kujiepusha nalo, kisha amwadhibu kwa sababu ya kutojiepusha nalo.

MLAHIDI

Ikoje watu ambao Mwenyeezi Mungu amewafanya matajiri na kuwapa riziki kubwa, wastahili neema hiyo, na ikoje maskini na wahitaji wastahili umaskini?

IMAMU

Haya yamefanywa kwa ajili ya mtihani.Mwenyeezi Mungu amewapa wote wawili mtihani. Matajiri wanajaribiwa kwa shukrani zao, na maskini kwa subira yao. Yaani, anataka kuona kama matajiri watamshukuru kwa utajiri aliowapa, na kama maskini watavumlia dhiki ya umaskini. Pili, kwa kuwafanya baadhi ya watu kuwa matajiri kwa haraka, na kwa kuwachelewesha maskini kuneemeka,amefanya kwa ajili ya siku moja ambapo watahitaji. Sababu nyingine ni kuwa Mwenyeezi Mungu alijua uwezo wa kuvumilia wa kila aina ya watu. Kwa hivyo, kila alichompa kila mmoja kilikuwa ni kufuatana na uwezo wake na kama watu wote wangelikuwa matajiri, basi kungekuweko machafuko na matata makubwa kaktika utaratibu wa dunia, na wote wangeelekea kwenye maangamizo. Amewafanya wategemeane, na kufanya riziki zao zitegemee vitendo vyao na kazi zao tofauti. Na kwa namna hiyo ndiyo ilivyokuwa kuishi kwao kwa salama. Matajiri wamepewa mtihani kuonyesha kwa kadiri gani watakuwa wema kwa maskini. Hayo yote ni Rehema na Ukarimu wa Mwenyeezi Mungu Mwenye kujua, ambaye Hekima yake haina shaka.

MLAHIDI

Kwa nini mtoto mchanga hupata maumivu au maradhi bila ya kosa lolote lake,kwa kuwa bado hakufanya dhambi yoyote?

IMAMU

Maradhi yanatokana na sababu nyingi:

(1) Maradhi ni kama mtihani,

(2) Maradhi ni kama adhabu

(3) Maradhi yanayo sababisha mauti. Wewe unafikiri kuwa maradhi yote yanatokana na chakula kibaya, au chanzo chake ni mama wa mtoto. Unafikiri kuwa jambo bora la kuweka mwili na akili katika hali nzuri ni kwa kula chakula fulani ambacho hakitaleta maradhi. Vile vile wewe unaelekea kukubaliana na wale watu wanaosema kwamba maradhi na mauti yanasababishwa na chakula na maji, ingawa Aristotle aliyekuwa mwalimu wa matibabu alikufa pia. Plato, aliyekuwa Bwana wa matabibu hayupo tena. Galen amekuwa mzee, na macho yake yamedhoofika. Yeye pia, akiwa ni mtu mwenye busara, hawezi kuepuka mauti.Wao hawakupuuza kabisa kuweka miili yao katika siha nzuri. Kuna wagonjwa wengi ambao maradhi yao yanawachosha matabibu wanaowatibu. Kuna matabibu wengi walio wataalam, waangalifu na mabingwa, ambao hufa kitandani mwao, na kuna mtu mjinga wa elimu ya tiba ambaye huishi zaidi kuliko wao. Mauti yanapofika, ikiwa mtu ni tabibu au mgonjwa, elimu ya tiba haitomsaidia, na ikiwa saa yake ya kufa haikufika bado, ujinga wake wa tiba hautamdhuru. Matabibu wengi wanasema kuwa Mitume walikuwa hawajui elimu ya tiba, hivyo, hawakufuata mashauri yao kuhusu mambo ya tiba. Ukweli ni kuwa Mitume ni Dalili ya Mwenyeezi Mungu kwa watu, wao ni Agizo lake duniani, wao ni hazina ya Elimu yake, na wao ni warithi wa Hekima yake. Wao wanawaongoza watu kwenye Njia ya Mwenyeezi Mungu na kuwanasihi wamtii Yeye. Nimeona kuwa wanafalsafa hawafuati njia iliyoonyeshwa na Mitume, na hawaamini Vitabu ambavyo Mwenyeezi Mungu amewateremshia. Kwa sababu hii,mimi siwapendi.

MLAHIDI

Vipi unajiweka mbali na kikundi hicho na hali wewe ni Kiongozi wao na mkubwa wao?

IMAMU

Nilimwona mmoja kati yao, ambaye alikuwa mwanchuoni mahiri wa elimu ya tiba. Nilipomuuliza maswali, niligundua kuwa hafahamu maumbile ya akili na mwili wa mwanadamu. Hakujua hata vipi chakula kinafika matumboni, vipi anavuta pumzi, vipi ulimi hufanya kazi, vipi anazungumza, vipi macho yanafanya kazi, nini nguvu za uchu, na tabia ya asili ya maumbile mengine, vipi machozi yanafanyika, vipi masikio yanafanya kazi, wapi mahali pa hekima na mahali pa roho, kwa nini tunapiga chafya, hali gani inaletwa na huzuni: nini chanzo cha furaha, vipi mtu huwa kiziwi na bubu. Kwa ufupi, yeye hakuwa na elimu hasa ya vitu hivi. Yeye aliyakusanya baadhi ya maelezo yanayotoana na dhana tu.

MLAHIDI

Hebu nijulishe chochote kuhusu Mwenyeezi Mungu.Je, yupo yeyote ambaye ni mshirika Wake? Je,yupo yeyote anayeweza kuipangua mipango yake?

IMAMU

Hapana.

MLAHIDI

Basi kwa nini kuna misukosuko mingi dunia nzima?Kuna wanyama wakali, watu wabaya, wadudu, mbu, nyoka, ng'e, wote wanatupa maumivu, nawe unasema kuwa Mwenyeezi Mungu hakuumba chochote ambacho hakina faida au hakifai.

IMAMU

Je,hujui kwamba ng'e anafaa katika maumivu ya mafigo. Vile vile anafaa kwa nayeumwa na jiwe.Pia anampa nafuu yule anayekojoa kitandani. Dawa nzuri kabisa ya kuvunja nguvu ya sumu inatengenezwa kutokana na ngozi ya nyoka.Ikiwa mwenye ukoma atakula ngozi ya nyoka, itamsaidia. Je, hujui kuwa nyungunyungu (red worms) wanaopatikana chini ya ardhi ni dawa ya mapele?

MLAHIDI

Naam. Najua.

IMAMU

Mbu ni chakula cha ndege, na vile vile ni kama wasila wa kuyaangusha majivuno ya anayejiona. Palikuwepo dhalimu mmoja, ambaye Mwenyeezi Mungu alimtia katika fedheha kwa kumtumia mbu. Yeye alikuwa akikana uwezo wa Mwenyeezi Mungu. Mwenyeezi Mungu alimfanya mbu ambaye ni kiumbe dhaifu kabisa amshinde. Mbu aliingia ndani ya pua na akafika mpaka ndani ya ubongo wake.Matokeo yake dhalimu huyo akafa. Ikiwa sisi tutajua kwa nini Mwenyeezi Mungu amemuumba kila kiumbe, basi tutakuwa sawa naye katika elimu, hivyo hatutakuwa wahitaji Wake.

MLAHIDI

Je, kuna makosa yoyote katika uumbaji na mipango ya Mwenyeezi Mungu?

IMAMU

Hakuna.

MLAHIDI

Mwenyeezi Mungu amemuumba mtu bila ya kutahiriwa.Je, ni jambo la hekima au ula upuuzi?

IMAMU

Ni jambola Hekima.

MLAHIDI

Wewe unafanya mabadiliko katika alichokiumba Mwenyeezi Mungu na unamtahiri mtoto.Humpendi yule ambaye hakutahiriwa, ingawa Mwenyeezi Mungu amemuumba bila ya kutahiriwa.Unasifu kutahiri. Ina maana kwamba unasifu kitendo chako na unapinga kitend cha Mwenyeezi Mungu?

IMAMU

Hekima hii yote na ustawi unatoka kwa Mwenyeezi Mungu.Lakini Mwenyeezi Mungu Mwenyewe ametuamrisha tutahiriwe.Amewajibisha kwetu. Mtoto anapotoka kwenye tumbo la uzazi la mama yake, kitovu (umbilical cord) chake ambacho huanza kwenye mfuko wa mimba (foetus) mpaka kwenye kondo la nyuma (placenta) likiwa limeshikana na tabaka la ndani ya tumbo la uzazi (womb) la mama, hilo ndilo lililoamrishwa na Mwenyeezi Mungu likatwe. Hilo linasababisha mtengano baina ya mam na mwana.Vile vile ametuamuru tukate kucha zetu zinapoota, ingawa yeye anaweza kutuumba katika hali ya kutoota kucha zetu. Kwa njia hiyo hiyo, tunakata nywele zetu, na tnatengeneza masharubu yetu. Tazama kuwa Mwenyeezi Mungu amemuumba fahali awe dume, lakini anahasiwa. Mambo haya, hayana maana kwamba kuna makosa katika mipango ya Mwenyeezi Mungu.

MLAHIDI

Je husemi kuwa Mwenyeezi Mungu anasema: "Niombeni nitakupeni"? Lakini tunawaona watu wengi walio na shida, wanamwomba Yeye, lakini hawapati maombi yao, na wale ambao ni watiifu kwa Mwenyeezi Mungu wanamwomba kwa dhati awasaidie, lakini hawasaidii.

IMAMU

Ikiwa mtu anamwomba Mwenyeezi Mungu,Yeye humpa maombi yake, lakini maombi ya muasi yanakataliwa mpaka atubu. Na ikiwa mtu ni mtiifu kwake na yupo kwenye njia ya haki, Mwenyeezi Mungu hukubali maombi yake, na kama kuna hatari yoyote karibu naye, itaondoka kwa njia ambayo hatahisi, au kuna malipo juu yake kwa siku ambayo atahitajia. Kama kitu kinachoombwa na kiumbe hakina manufaa kwake, basi humnyimwa. Muumini ambaye anamtambua Mwenyeezi Mungu huudhika kwa sababu huenda akaomba kitu ambacho hakijui kuwa ni kizuri au kibaya kwake. Kadhalika, maombi ya mtu hayakubaliwi ikiwa anamwombea mtu mwovu kufa, ambaye maisha yake lazima bado yaendelee, au anapoomba mvua wakati inapoleta hasara.Mwenyeezi Mungu anajua vizuri kuhusu mipango yake na usimamizi wake.

MLAHIDI

Ewe Mwenye hekima! Tujulishe kwa nini (kiumbe) yeyote haji duniani kutoka mbinguni, na mtu yeyote haendi mbinguni kutoka duniani?Kwa nini hakuna njia itokayo duniani mpaka mbinguni? Ikiwa mara moja katika kila zama mtu mmoja kutoka duniani angekwenda mbinguni, na mwingine akatoka mbinguni kuja duniani, ingetupa dalili ya utukufu wa Mwenyeezi Mungu, shaka zote zingeondoka, imani ingeimarika, na viumbe wangejua kwamba kuna Mwawadhi Mkuu wa mbingu, kutoka kwake mtu huenda mbinguni na mwingine huja duniani.

IMAMU

Utaratibu wowote unaokwenda hapa duniani kwa nidhamu kamili, ni ule ule ulioletwa kutoka mbinguni. Je, huoni kuwa jua linakucha na kuangaza siku.Kwalo hutegemea kuwepo duniani. Kama jua lingelisimama na lisingelikucha, wale waisihio duniani wangehangaika na kuangamia. Mwezi ni mmoja katika dalili hizo. Unazunguka na unatoa nuru kwa ajili ya usiku. Kwa huo huhesabiwa miaka, miezi, na siku. Kama usingelizunguka, viumbe wangeshtuka na kuangamia, na utaratibu ungeharibika. Nyota za mbinguni huwaongoza wasafiri wa bara na baharini.Mawingu yanaleta mvua ambayo kwayo maisha ya kila kiumbe yanategemea. Miti na ukulima unayategemea. Kama isingelikuweko mvua, hakuna ambaye angeliweza kuishi.Kama hewa ingeondoshwa kwa siku chache, vitu vyote vingebadilika na kuangamia. Hivyo, mawingu ya mbinguni, ngurumo ya radi umeme na mwangaza - vyote vinathibitisha kuwa kuna Mwawadhi ambaye anayasimamia mambo haya yote, na kutoka Kwake mambo hayo yanafanyika.

Mwenyeezi Mungu alizungumza na Nabii Musa(a.s) kwa utukufu. Alimpaaza Nabii Issa(a.s) mbinguni.Malaika walitoka Kwake.Ni jambo jingine, ikiwa huamini yale usiyoyaona kwa macho yako. Lakini ikiwa utafikiri na kuzingatia yale unayoyaona yanatosha kukuongoza.

MLAHIDI

Uzuri ulioje utakuwa, ikiwa mara moja katika karne moja, Mwenyeezi Mungu ataturudishia mmoja katika wafu wetu, ili tuweze kumuuliza kitu gani kimewafika wale waliokufa. Nini hali yao ya sasa, na kitu gani watakabiliana nacho baada ya kifo. Kama watu wangejua jinsi gani wanatendewa wafu wangetekeleza wajibu wao kwa imani, na shaka zote za bughudha zingeondoka mioyoni mwao.

IMAMU

Haya yanasemwa na wale wenye kukataa kuwakubali Mitume wa Mwenyeezi Mungu, na hawaamini dalili walizozileta kutoka kwa Mwenyeezi Mungu. Mwenyeezi Mungu katika Kitabu chake ametuarifu katika kinywa cha Mtume(s.a.w.w) kuhusu wale waliokufa miongoni mwetu. Je, yupo anayeweza kuwa mkweli zaidi kuliko Mwenyeezi Mungu na Mtume Wake(s.a.w.w) ? aidha,wengi katika wafu wamehuishwa. Miongoni mwao ni 'As-habul Kahf (Wenzi wa Pangoni), ambao Mwenyeezi Mungu aliwalaza (kama wamekufa) kwa muda wa miaka 309.kisha Akawarudishia ufahamu wa nafsini wakati ambao watu walikuwa hawaamini ufufuo wa wafu, ili Azibatilishe fikra zao na awaonyeshe Nguvu Zake, waweze kuamini kuwa ufufuo ni Kweli (uko).

Mwenyeezi Mungu amemfisha Nabii Armiya, ambaye aliona Baitul Muqaddas ikibomolewa katika vita vya Bakht Nusr.Alitaka kujua vipi Mwenyeezi Mungu huweza kumhuisha baada ya kufa.Mwenyeezi Mungu akamweka mfu kwa miaka mia moja, kisha akamuhuisha. Akajitazama jinsi miguu na mikono yake inavyojaa nyama. Akatazama jinsi viungo vyake na mishipa vinavyoungana. Kisha akainuka na kusema: "Nilijua Mwenyeezi Mungu Mtukufu ana uwezo juu ya vitu vyote"

Vile vile, Mwenyezi Mungu aliwahuisha watu ambao walikimbia kwao kwa sababu ya hofu ya njaa. Idadi yao haihesabiki. Mwenyezi Mungu aliwaweka watu mpaka miili yao ilipobadilika na kuoza. Viungo vyao vikaachana na wakageuka mchanga. Kisha Mwenyezi Mungu akawahuisha wakati alipotaka kuwaonyesha Uwezo Wake kwa Bani Kharqiil

Nabii Kharqiil aliwaita wafu, na viungo vya miili yao vikakusanyika. Wakarudishiwa uhai wao na wakasimama kama walivyokuwa wamesimama siku waliyofishwa. Idadi yao ilikuwa ile ile. Kasha wakaishi kwa muda mrefu. Vile vile Mwenyezi Mungu akafikisha kikundi cha watu waliokuwa wamefuatana na abii Musa(a.s) na wakamtaka awaonyeshe Mwenyezi Mungu.Mwenyezi Mungu aliwafisha kisha akawahuisha.

2

MAHOJIANO BAINA YA MLAHIDI NA IMAMU JA'FAR SADIQ (A.S.)

MLAHIDI

Sasa nijulishe kuhusu watu wanaoamini kuwa roho ya mtu huingia katika mwili mwingine mtu afapo.Juu ya msingi gani wanaithibitisha imani yao?

IMAMU

Wale wanaoamini kuingia kwa roho ya mtu katika mwili mwingine, wameipuuza misingi yote ya dini, na wamejivika dhana zisizokuwa za kweli. Wanafikiri kuwa mbingu i tupu, na hakimo kitu cho chote ndani yake ambacho chaweza kuelezwa maana yake; na kwamba Mola wa dunia hii yu kama kiumbe. Wanasema kuwa chanzo cha hoja yao inatokana na dai la watu wasemao kwamba Mwenyezi Mungu amemwumba Adamu kwa mfano wa "mwili" wake. Wao hawaamini kuwepo kwa Pepo, Moto, Kiyama n.k. Kufuatana na itikadi yao, "Kiyama" maana yake ni kuingia kwa roho ya mtu aliyekufa katika mwili mwingine. Ikiwa mtu alifanya vitendo vizuri katika mwili wake zamani, basi roho yake itaingia katika mwili mzuri zaidi, na atapata hadhi kubwa katika maisha. Ikiwa amefanya vitendo viovu katika mwili wake wa zamani, au hakujua cho chote, basi roho yake itaingia katika miili ya wanyama, na atabaki katika hali mbaya. Hawaamini kufunga, kusali n.k. Wanapenda kujua yale tu yaliyo muhimu kwao.

Kujitosheleza na tamaa zao za kidunia kunaruhusiwa kwao. Katika jambo hili, hawataona dhara lo lote ikiwa watazini na mwanamke ye yote wanayempenda hata akiwa ni dada, mabinti, mashangazi na wanawake walioolewa. Vile vile, inaruhusiwa kwao kula (au kunywa) mizoga, ulevi, damu n.k. Vitu hivi vinakatazwa na watu wote.Watuw enye dini wanawalaani. Na wanapotakiwa wathibitishe msingi wa msimamo wao wanafadhaika na kubabaika. Torati inakana madai yao, na Qurani inawalaani. Mbali na mambo haya, vile vile wanadhani kuwa Mwenyezi Mungu hutoka katika mwili mmoja na kuingia mwili mwingine, na kwamba roho zote ni za azali (hazina mwanzo wala mwisho). Wanasema kuwa roho hiyo hiyo ya Adamu bado inatoka mwili mmoja na kuingia mwili mwingine. Kwa hivyo, ikiwa Mwumba ni kama kiumbe chake, basi vipi inawezekana kusemwa kuwa mmoja wao ni mwumba wa wingine? Vile vile, wanasema kuwa malaika ni wazao wa Adamu(a.s.) , na yule mwenye kujipatia hadhi kubwa katika dini yake baada ya kuzipita daraja za mitihani, huwa malaika. Kwa baadhi ya mambo wanaelekeana na Wakristo, na kwa mambo mengine wanaelekeana na wenye kumkana Mungu.wanasema kuwa vitu havina uhakika.Hivyo, hawali cho chote chenye nyama. Kwa kufuatana na imani yao, wanyama ni wazao wa Adamu, lakini wameyabadili maumbo yao.Kwa hivyo, hawali nyama zinazohusiana ambazo zimeharamishwa kwao.

MLAHIDI

Kuna kikundi cha watu wasemao kuwa Mwenyezi Mungu ni wa azali, na kitu kinachochakaa pia kilikuwa pamoja Naye tangu azali. Mwenyezi Mungu hana uwezo wa kujiondolea kitu kichakaacho. Kwa sababu hiyo, wanasema kuwa Mwenyezi mungu mwenyewe amejiambatanisha nacho na anaingia kwacho. Mwenyezi Mungu ameumba ulimwengu mzima kutokana na kitu hicho.

IMAMU

Mwenyezi Mungu atukuzwe! Vipi Mwenyezi Mungu ambaye ni Mwenye Uwezo asiwe na uwezo wa kujiondolea kitu? Ikiwa kitu kilikuwa kihai na cha azali, ina maana kuwa palikuwepo vitu viwili vya azali, ambavyo viliungana na vikaupanga ulimwengu.Kama hivyo ndivyo ilivyokuwa, basi kifo kimetoka wapi? Ikiwa kitu hakina uhai, basi kwa huko kutokuwa nao, hakuwezi kuwa pamoja na mwenye kuwa wa azali. Uhai hauwezi kutoka pasipokuwa na uhai. Hii ni imani ya wale makafiri wabaya kabisa. Wao wanaendelea kufuata maandiko ya mababu zao na kuyakariri kwa ujinga na bila ya kufikiri. Hawawezi kuthibitisha yale wanayoyadai. Yote haya yameazimiwa kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuwakana. Wapo watu wasemao kuwa miili ni giza na roho ni nuru; baya halitoki kwenye nuru, na giza haliwezi kufanya zuri lo lote. Hivyo, si barabara kumlaumu mtu ye yote kwa ajili ya dhambi yake. Giza lenyewe halina kosa, kwa sababu ni kitendo chake; wala Mwenyezi Mungu asinyenyekewe, kwa sababu Nuru ni Mola, na Mola hajinyenyekei wala hamtaki mtu amtii. Hakuna mtu ye yote katika kikundi hicho mwenye haki ya kumwambia mwenziwe kwamba fulani amefanya zuri au baya, kwa sababu ubaya ni sifa ya giza. Kadhalika, uzuri ni sifa ya nuru, na nuru haiwezi kusema kuwa ni mtenda zuri na imefanya kitendo kizuri na kwamba hakuna mtendewa. Vile vile, kufuatana na imani yao, giza ni huru katika vitendo vyake, na imara katika mpango wake, na yenye nguvu zaidi kuliko nuru, ilivyokuwa miili ni mizima na madhubuti.

Hivyo, yule aliyeumba juu ya msingi, ingawa katika umbo tofauti, lazima awe Mwenyezi Mungu. Kila kitu ambacho chaweza kuonekana kama miti, matunda, ndege, wanyama n.k., lazima kiwe Mungu, kw sababu kimehusika na nuru.Ni maneno matupu wanapodai kwamba nuru itamiliki mwishowe. Wanasema kuwa nuru haiwezi kufanya kitendo cho chote, imejifunga, haina nguvu na haitaharuki. Kama nuru ingekuwa na nguvu sawa na giza, ingeweza kujifunga. Ingekuwa huru na yenye nguvu. Hivyo, kama haina uhuru na nguvu ila tu imefungika katika giza, basi mazuri na mema yanachanganyika pamoja na mabaya na maovu katika dunia hii. Kwa hivyo, ina maana kuwa giza linazaa mazuri pia, kama linavyozaa mabaya. Kwa maneno mengine, giza ni mwumba wa mazuri na mabaya. Ikiwa wanasema kuwa haimkiniki, basi haithibitiki giza wala nuru. Hivyo, madai yao hayafai.

Kwa hivyo, mwisho wake ni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja tu, wala kitu chochote kingine ghaira Yake hakina uhakika. Maani kafiri mkubwa, pamoja na wafuasi wake waliokuwa na fikira hizo. Wanaposema kwamba zaidi ya nuru na giza, kuna nguvu ya tatu yenye kuamua; basi hapana shaka kuwa nguvu ya tatu ni kubwa kuliko hizo mbili, kwa sababu wenye kudhiliwa, wajinga na wanaoonewa huomba msaada wa mwenye kutawala. Haya ni yale wanayoamini wafuasi wa Maani, na hadithi yao ni ndefu.

MLAHID

Nini habari ya Maani?

IMAMU

Maani alifuata mafundisho ya Majusi, na katika baadhi ya mambo alikubaliana na Wakristo; hivyo, yalikuwa ni mchanganyiko wa makosa, naye hakuweza kufahamu hata dini moja. Aliamini kuwa ulimwengu umeumbwa na miungu miwili - nuru na giza; na kwamba nuru ipo katika kifungo cha giza. Wakristo wanakana itikadi hii, na Mamajusi wanaikubali

MLAHID

Ni nani Mamajusi? Nini dini yao?Je, Mwenyezi Mungu amewatumia Mtume ye yote kwao? Nimeona kwao vitabu vizuri, mawaidha na mafafanuzi ya kitaalam.Wanayo sherria ya dini iliyo kamili, ambayo kwayo wanafanyia vitendo vyao.

IMAMU

Hakuna umati ambao miongoni mwao hakukuwepo mwonyaji.Bila shaka, Mtume pamoja na Kitabu amepelekwa na Mwenyezi Mungu kuwaongoza. Lakini watu walimkataa mtume huyo pamoja na Kitabu chake.

MLAHID

Mtume gani alikuwa huyo? Inasemekana kwamba alikuwa Khalif bin Sinaan.

IMAMU

Khalid bin Sinaan alikuwa Mwarabu wa Kibedui. Hakuwa Mtume. Ni mawazo ya watu tu.

MLAHID

Je, alikuwa Zarasushtra?

IMAMU

Zarasushtra alileta zaburi (wimbo) na akadai utume. Baadhi ya watu walimwamini, na baadhi yao walimkataa.Baadaye akafukuzwa mjini.

MLAHID

Hebu nipe habari kuhusu Mamajusi.Je, walikuwa wema zaidi katika dini yao kuliko Waarabu?

IMAMU

Waarabu katika zama za ujahili (ujinga) walikuwa karibu zaidi na dini ya haki kuliko Mamajusi; kwa sababu Mamajusi hawakumkubali Mtume ye yote. Walikana vitabu vyao na dalili zao.Hawakufuata desturi zao.Katika siku za mwanzo za Mamajusi, mfalme Kai Khusro aliwaua mitume mia tatu. Mamajusi walikuwa hawafanyi 'ghusl' (Mwogo wa Kidini) baada ya kutokwa na manii. Lakini Waarabu katika zama za Ujahili walikuwa wakifanya 'ghusl', na 'ghusl' (kuoga kwa utaratibu maalum baada ya kuwa na janaba n.k.) ni moja katika jambo la lazima katika dini yetu. Mamajusi walikuwa hawatahiri.Kutahiri ni jambo lenye kupendelewa sana ('sunnah') na Mitume.Nabii Ibrahim(a.s) alianzisha jambo hili.Mamajusi walikuwa hawaoshi maiti zao wla hawakafini.Nabii Ibrahimu(a.s) alianzisha jambo hili. Waarabu walikuwa wakifanya haya yote.Mamajusi walikuwa wakiwaacha maiti zao katika majangwa na milima. Lakini Waarabu walikuwa wakizizika makaburini, na hii ni desturi ya Mitume. Mamajusi walikuwa wakiwazini mama zao, na wakiwaoa binti zao na dada zao, lakini Waarabu walikuwa wakiona kuwa mambo hayo ni haramu. Mamajusi walikuwa hawalikubali Nyumba ya Mungu (Kaaba) na wakiliita Nyumba ya Shetani. Waarabu walikuwa wakihiji na kuiheshimu Kaaba, na waliiita Nyumba ya Mwenyezi Mungu. Waarabu waliamini Torati na Injili, na walikuwa wakiwauliza maswali wafuasi wa vitabu hivyo na wakiyafuata maamrisho yake. Kwa hivyo, katika mambo haya yote, Waarabu walikuwa karibu zaidi na dini yetu kuliko Mamajusi.

MLAHID

Kuhusu kuwaoa dada, Mamajusi walitoa hoja kuwa desturi hiyo ilikuwa kawaida tangu zama za Adamu(a.s)

IMAMU

Kuhusu kuwaoa dada na mama, hakufuatani na hoja barabara, kwa sababu Adamu, Nuhu, Ibrahimu, Musa Isa na Manabii wote (Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao), wamesema kuwa ni haramu. Katika Vitabu vya Mwenyezi Mungu, imetajwa kuwa ni haramu.

MLAHID

Kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha ulevi, ingawa hakuna kitu kitamu kama hicho?

IMAMU

Mwenyezi Mungu ameharamisha ulevi kwa sababu ni chanzo cha maovu yote. Ulevi unamwathiri mwenye kunywa kwa jinsi ya kumpotezea fahamu zake zote, kumfanya amsahau Mwenyezi Mungu. hakuna dhambi asiyoifanya mlevi.Hujiingiza katika kila kitendo cha aibu. Huharibika sana hata akapoteza mema yote.Mlevi ana hatamu moja tu, ambayo ipo mikononi mwa Shetani.Ikiwa Shetani atamwamuru ayasujudie masanamu, basi atafanya.Huenda po pote ambapo Shetani humwongoza.

MLAHID

Kwa nini Mweyezi Mungu ameharamisha kunywa damu?

IMAMU

Kwa sababu humfanya mtu kuwa katili na humwondolea huruma, huupa mwili harufu mbaya na huibadili rangi yake.Wale wanywao damu, aghalabu huugua ukoma.

MLAHID

Kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha kula sehemu za mwili wa wanyama na ndege zambazo ni kama vifuko mnamofanyiwa maji yenye dawa yaingiayo damuni na kufanya kazi nyinginezo mwilini? Kama vile korodani)

IMAMU

Kwa sababu zinasababisha ukoma.

MLAHIDI

Kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha kula nyama ya mnyama aliyekufa (mzoga)?

IMAMU

Imeharamishwa ili kuweka mbali na (mnyama) yule aliyechinjwa kwa jina la Mwenyezi Mungu. isitoshe, mnyama anapokufa, damu yake huganda ndani ya nyama. Hivyo, nyama huwa nzito na mbaya inapochanganyika na damu.

MLAHIDI

Lakini samaki vile vile ni mnyama aliyekufa!

IMAMU

Kutoka kwake nje ya maji kuna maana kuwa ni kujitolea kwake.Anapotolewa nje ya maji, huachwa juu mpaka afe mwenyewe. Ni hivyo,kwa sababu hana damu. Vivyo hivyo kwa nzige.

MLAHIDI

Kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha kuzini?

IMAMU

Kwa sababu huleta machafuko.Vizazi havitambulikani.Nasaba haziimariki. Mwanamke hajui yu nani baba wa mtoto wake. Mtoto hajui ni mwana wa nani. Huondoa ujamaa na ukabila.

MLAHIDI

Kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha kulawiti?

IMAMU

Kwa sababu kama kulawiti wanaume kungelihalalishwa, basi watu wasingewakaribia wanawake maana wasingefaa. Kwa sababu hiyo, vizazi visingeendelea.Isitoshe kuhalalishwa kwake kungesababisha mizozano mikubwa na misukosuko ya wenyewe kwa wenyewe.

MLAHIDI

Kwa nini Mwenyezi Mungu ameharamisha kuwajamii wanyama?

IMAMU

Kulionekana kuwa hakufai kuwa mtu apoteze bure manii yake ili kwamba ikiwa mtoto atazaliwa asiwe na namna nyingine. Kama ingelikuwa halali, wanaume wangewajamii wanyama majike na kutosheleza tama zao za kimwili. Hayo yangesababisha machafuko makubwa. Hivyo, Mwenyezi Mungu ameturuhusu kuwapanda juu ya migongo yao wala si juu ya uke zao. Mwenyezi Mungu amewaumba wanawake kwa ajili ya wanaume ili kwamba wanaume wawapende na wajitosheleze nao tama zao za kimwili, na wanawake wawe vikimbilio vya tama za kiume na mama wa watoto wao.

MLAHIDI

Kwa nini tufanye 'ghusl' baada ya kuwa na janaba, wakati kitendo chetu ni cha halali; na katika kitendo cha halali hakuna unajisi? IMAMU: Janaba ni kama hedhi, kwa sababu manii ni damu pia, ingawa haipo katika umbo hilo. Hutoka kwa kujamii, kujichua (uke au uume) au kwa kuzidi tamaa ya mwili. Mtu anapojamii, huvuta pumzi sana na huhisi harufu mbaya inatoka mwilini mwake. Kwa hivyo 'ghusl' ni lazima. Mbali ya mambo haya yote, 'ghusl' ya janaba ni jukumu ambalo Mwenyezi Mungu amemwamulia kiumbe chake ili amjaribie kwayo.

MLAHIDI

Ewe Mwenye hekima! Unasema nini kuhusu wale watu wanaosema kuwa dunia nzima ipo chini ya usimamizi wa Nyota Saba?

IMAMU

Hawana uthibitisho wa kuthibitisha dai hilo. Hii ni dunia kubwa. Dunia yenye sayari ni kama dunia ndogo. Sayari zinazunguka kama dunia (galaxy). Zinafuata sheria za Mwenyezi Mungu na haziwezi kuacha njia zake. Miendo yao imeimarishwa.Hazisimami kabisa. Nyota zote hizi na sayari zimeamriwa kufanya kazi zao kama watumwa.Kama zilikuwepo tangu azali, zisingebadilika.

MLAHIDI

Nijulishe kuhusu wale wanaoamini kuwa Maumbile (Nature) yanasimamia kila kitu.

IMAMU

Hao ni wanamaumbile. Hawana uwezo juu ya maisha yao au balaa, ambayo inawabadilisha usiku na mchana kutoka hali hii na ile. Watu hawa hawawezi kuepukana na uzee, wala hawawezi kujikinga na mauti.

MLAHIDI

Unasema nini kuhusu wale wanaoamini kuwa dunia ilikuwepo na itaendelea kuwepo katika hali hii hii zama baada ya zama. Watu wataendelea kuzaliwa na kufa. Nyakati zitakuja na kuondoka. Ugonjwa na maradhi yatawapata watu.Balaa zitaleta uharibifu.Kila kitu cha mwisho kinaonyesha mwanzo wake. Ukoo mmoja unatuambia kuhusu koo zao zilizowatangulia. Zama ya sasa inadhihirisha zama za kale. Wameona dunia katika hali hii hii kama miti na mimea. Katika kila zama, baadhi ya watu huzaliwa miongoni mwa wanadamu ambao hutambua kilicho kizuri na kibaya kwa watu.Huandika vitabu juu ya fikira zao. Hekima na akili zao ni pazia baina yao na mtu wa kawaida. Ni akili yao na hekima yao ambazo huwaongoza katika njia iliyo sawa na kuwashawishi kuifuata. Inawahifadhi kutokana na vitendo vyote viovu na vibaya.Hawauani.

IMAMU

Ole kwake! Umesema nini? Aliyezaliwa jana atakufa kesho. Hajui lililotukia kabla yake wala litakalotukia baada yake.Lazima pawepo mambo matatu: Ama mtu amejiumba mwenyewe, au ameumbwa na mtu mwingine, au yeye ni kiumbe wa azali; yaani amekuwepo daima. Yule asiyekuwepo kabla, hawezi kujiumba mwenyewe, vivyo hivyo, yule asiyekuwepo kabla na amekuwepo sasa, hawezi kujua asili yake. Na kama mtu alikuwepo tangu azali, hangeweza kubadilika, kwa sabab kilicho cha azali hakiwezi kubalika kwa sababu ya wakati, wala hakiwezi kutoweka au kuangamia. Juu ya haya, hatuoni msingi wowote usiowekwa na mtu. Kila sanaa tunayoona lazima ina msanifu. Ikiwa mtu anasema kuwa mtu ameumbwa na baba yake, basi swali huja, ni ani alimwumba baba yake; na ikiwa baba yake alimwumba yeye, basi lazima alimfanya kwa matakwa yake, na uso wake na sura yake lazima ziwe nzuri sana, pia lazima awe na uwezo juu ya maisha yake, tena aweze kumweka katika hali nzuri kama anavyotaka. Lakini ukweli ni kuwa, mtu akiwa mgonjwa, baba yake hawezi kumpa afya, na akifa hawezi kumhuisha. Kwa hakika, ikiwa mtu ana uwezo wa kumwumba mtu mwingine na kuweza kumpa roho ili aweze kwenda na kuwa na hisia, basi vile vile lazima awe na uwezo wa kumwepusha na mabaya yote.

MLAHIDI

Nini maoni yako kuhusu utabiri?

IMAMU

Utabiri (unajimu) ni sayansi, na faida yake ni kidogo kuliko madhara yake.Hauwezi kubadili kilichojaliwa. Watabiri hawana uwezo wa kuwahifadhi wale wanaowaogopa.Ikiwa mtabiri anatabiri baadhi ya balaa zitakazotukia, basi hataweza kujiepusha nazo. Ikiwa anatabiri jambo zuri kwa mtu fulani, basi hawezi kufanya litokee mapema zaidi kuliko wakati uliojaliwa.Ikiwa anatabiri jambo baya, basi hawezi kuliepuka. Mtabiri anataka kushindana na Mwenyezi Mungu, na anafikiri kuwa anaweza kubadilisha majaliwa yake.

MLAHIDI

Yupi bora zaidi - Mtume wa Mwenyezi Mungu au malaika? IMAMU: Mtume wa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi. MLAHIDI: Nini haja ya kuwachagua malaika, ambao wameaminiwa kazi ya kuandika mema na maovu ya watu, ingawa Mwenyezi Mungu Mwenyewe anajua mambo yote yaliyo siri na dhahiri. IMAMU: Mwenyezi Mungu amewachagua kwa kazi hii. Wao wanashuhudia yale yanayofanywa na viumbe Wake, ili kwamba viumbe wa Mwenyezi Mungu wazidi kumtii na kujikinga na maovu, wanapojua kuwa vitendo vyao vinarekodiwa. Kuna watu wanaokusudia kufanya dhambi, lakini mara wanakumbuka kwamba malaika wapo pamoja nao.Hivyo basi, hujikinga na dhambi wakifikiri kuwa Mwenyezi Mungu anawaona na malaika Wake wanashuhudia vitendo vyao. Ni kwa sbabu ya rehema na upole wa Mwenyezi Mungu kwamba amewachagua malaika ili kwamba mashetani wajiweke mbali na viumbe Vyake. Wao (malaika) wanawakinga wabaya na balaa.Malaika watabaki kuwa hawaonekani mpaka amri ya Mwenyezi Mungu itakapowafika katika namna ya mauti.

MLAHIDI

Je, Mwenyezi Mungu amewaumba viumbe wake kwa ajili ya rehema au adhabu?

IMAMU

Amewaumba kwa ajili ya rehema. Kabla ya kuwaumba, ilikuwa katika Elimu yake kuwa miongoni mwao wataadhibiwa kwa sababu ya vitendo vyao viovu na kukataa kwao Haki.

MLAHIDI

Mshirikina anastahili adhabu kwa sababu amekataa kuamini dini. Lakini kwa nini yule anayeamini Umoja wa Mwenyezi Mungu na anamtambua Yeye aadhibishwe pia?

IMAMU

Mshirikina atapata adhabu ya milele, na yule anayemuamini kuwa ni Mmoja, ataadhibiwa kwa kutojali wajibu wake.Kisha atatolewa kwenye adhabu.Mwenyezi Mungu hamdhulumu mtu ye yote.

MLAHIDI

Je, kuna tabaka la baina ya Ukafiri na Uislamu?

IMAMU

Hakuna.

MLAHIDI

Imani ni nini na kufuru ni nini?

IMAMU

Imani maana yake: Mtu ausadiki Utukufu wa Mwenyezi Mungu ambao ni mbali na kuona Kwake, kama anavyousadiki utukufu anaouona. Kufuru ni kutousadiki Utukufu Wake.

MLAHIDI

Ushirikina ni nini na shaka ni nini?

IMAMU

Ushirikina maana yake: Kumshirikisha mtu ye yote pamoja na Mwenyezi Mungu. Shaka ni kuwa na wasiwasi juu ya unayoyaamini.

MLAHIDI

Je,mwanachuoni anaweza kuwa mjinga?

IMAMU

Mwanachuoni ni mwenye kujua yale yaliyopo katika elimu yake. Mjinga anaitwa mjinga kwa sababu ya kutokujua kwake.

MLAHIDI

Baraka ni nini na balaa ni nini?

IMAMU

Baraka ni chanzo cha mema ambayo mwenye kubarikiwa hushikilia, nayo humpeleka kwenye wokovu. Balaa ni chanzo cha visirani ambavyo mwenye kuzibiwa hushikilia, nayo humpeleka kwenye maangamizo. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mambo yote.

MLAHID

Mwangaza wa taa huenda wapi, inapozimika taa?

IMAMU

Unakwenda mahali ambao haurudi tena.

MLAHIDI

Ndivyo ilivyo kwa binadamu pia.Roho huacha mwili unapokufa. Haimrudii tena, kama ambavyo mwangaza wa taa hauirudii taa baada ya kuzimika.

IMAMU

Umekosea katika dhana yako.Moto unafunikika ndani ya kitu na kuhifadhika. Vitu huwaka moto kwa sababu ya vijisehemu vya moto kuweko ndani yao. Kwa mfano mawe na chuma, ukivigonganisha pamoja, cheche za moto zitatoka. Wewe unayaeleza hayo kwa mfano wa taa. Kuna tofauti baina yao. Moto hukaa katika mawe na chuma, wakati mwangaza wa taa hutoweka. Roho ni laini sana na nyembamba. Huvaa nguo chafu kwa kuingia ndani ya mwili wa mtu. Si kama taa, ambayo wewe umeizungumzia. Mwenyezi Mungu amewaumba viumbe ndani ya mifuko ya uzazi ya wanawake kwa maji safi, atawafufua baada ya mauti na atawahuisha baada ya kuangamia. Kuna kila aina ya vitu pamoja nayo, kama mishipa,vena, meno, nywele na mifupa n.k.

MLAHIDI

Roho hukaa wapi(baada ya kutoka mwilini)?

IMAMU

Hubaki chini ya ardhi,ambapo maiti hubakia mpaka siku ya ufufuo.

MLAHIDI

Roho ya mtu aliyetiwa tanzi (aliyenyongwa) hukaa wapi?

IMAMU

Hubaki pamoja na malaika aliyejitoa maisha yake, mpaka atakapofufuliwa. Malaika huiweka kama anavyoiweka ya maiti wa kaburini.

MLAHIDI

Niambie, nini kinachokuwa pamoja na roho je, ni damu?

IMAMU

Naam, kitu muhimu kinachokuwa pamoja na roho ni damu. Kutokana na damu, hupatikana unyevu wa mwili. Damu inasafisha, inalainisha sauti na hulidhihirisha tendo la kucheka.Roho hutoka mwilini wakati damu inapoganda.

MLAHIDI

Nini asili ya hewa?

IMAMU

Hewa ni upepo unaopepea.Unapokuwa haupepei, unaitwa hewa. Maisha ya dunia hutegemea hewa.Ukisimama,machafuko yataanza katika mambo yote ya dunia. Hewa ni kama kipepeo. Hutoa uchafu wote katika vitu na kuvisafisha. Ni kama roho. Inapopulizwa kutoka mwilini, huchakaa na kubadilika umbo lake. Atukuzwe Mwenyezi Mungu, Muumba bora kabisa.

MLAHIDI

Je,roho hupotea angani baada ya kutoka mwilini au huendelea kuwapo?

IMAMU

Roho huendelea kuwepo mpaka litakapopigwa Baragumu.Vitu vyote vitatanguka na kuangamia.Hakutabaki kitu kihisicho wala anayehisi.Baada ya hayo, vitu vyote vitakuwepo tena katika umbo la kwanza, katika hali ile ile aliyowaumba. Kutakuwepo kipindi kati ya kupigwa Baragumu na Marejeo.Kisha Baragumu la pili litapigwa.

MLAHIDI

Vipi mwili uliofufuliwa wa mwanaume utakuwa mwanaume. Miili haitakuwepo kwa sababu ya kuoza.Viungo vitatanguka. Sehemu nyingine zitakuweko mahali ambako zitaliwa na wanyama. Viungo vingine vitageuka kuwa mchanga na vitachanganyika na mchanga. Kutokana na mchanga huo, utajengwa ukuta. Sehemu zingine zitaliwa na wadudu.

IMAMU

Mwenyezi Mungu ambaye aliwaumba, akawapa umbo na sura, ana uwezo wa kuwaumba upya. Hakuwa na kalibu alipowaumbia kwanza? Roho inashikilia vema pahali pake pa watu wema katika anga ya mwangaza na uwanda; na waovu katika pahali pa giza na pembamba. Miili itageuka kuwa mchanga (udongo) kama ilichoumbiwa kwanza. Wanyama na wadudu wataitapika miili waliyoila.Kila kitu kinahifadhiwa duniani. Hakufichiki cho chote Kwake.Hata kijichembe cha kitu katika giza totoro hakifichiki Kwake. Anajua idadi na uzani wa vitu. Mchanga wa watu watakatifu ni kama dhahabu katika mchanga. Wakati wa ufufuo, dunia itatikisika kama maziwa yanayosukasukwa.

Mchanga wa mtu utakuwa safi kama dhahabu inayokuwa wakati inapooshwa kwa maji utakapopondwa kama mapovu ya maziwa, huo mchanganyiko utamiminwa katika kalibu.Hizo kalibu zitapelekwa mahali penye roho. Kwa amri ya (mwenyezi Mungu) Msanii wa Azali, hizo kalibu zitakuwa na maumbo ya mwanzo.Roho zitaingia ndani mwake. Kisha mtu atakuwa na umbo lake la asili, na hataona cho chote kigeni kwake.

MLAHIDI

Je,watu watafufuliwa miili mitupu?

IMAMU

Watafufuliwa pamoja na sanda zao.

MLAHIDI

Sanda zao zitatoka wapi? Zitakuwa zimeshaoza.

IMAMU

Mwumba atakayefufua miili,vile vile atazifanya sanda mpya.

MLAHIDI

Je, yule aliyekufa bila ya kuwa na sanda?

IMAMU

Mwenyezi Mungu atazifunika sehemu zake ambazo zitatakikana kufunikwa.

MLAHIDI

Je, watakusanywa kwa mistari?

IMAMU

Itakuweko mistari elfu ishirini, urefu wke ni kama upana wa dunia.

MLAHIDI

Je, vitendo vitapimwa kwa mizani?

IMAMU

La! Vitendo si vitu, bali ni sifa. Ikiwa mtu hajui idadi ya vitu au uzito wake (kama ni chepesi au kizito) basi huvihesabu au huvipima. Lakini kwa Mwenyezi Mungu hakufichiki cho chote.

MLAHIDI

Basi nini maana ya Mizani?

IMAMU

Mizani maana yake ni uadilifu.

MLAHIDI

NINI MAANA YA Mizani katika aya 2:9

".. na ye yote mizani yake ikiwa nzito?"

IMAMU

Ina maana,". Na yeyote vitendo vyake vikiwa vizito"

MLAHIDI

Je, moto hautoshi hata mtu aadhibishwe pamoja na ng'e na nyoka?

MLAHIDI

Je, moto hautoshi hata mtu aadhibishwe pamoja na ng'e na nyoka?

IMAMU

Watu watakaoadhibiwa pamoja na hao ni wale tu ambao wanaamini kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu ndiye aliyeviumba viumbe hivi; na kwamba hivi viumbe si vya Mwenyezi Mungu. kwa sababu hiyo, Mwenyezi Mungu ataviwekea viumbe hivyo ili waadhibike kwa sababu ya matokeo mabaya ya itikadi yao ya batili.

MLAHIDI

Vipi watu wanasema kuwa watu wa Peponi watakula matunda kutoka mitini.Kisha matunda hayo yatarudi katika hali yake ya kwanza.Tunda lililoliwa, litarudi pahali pake pale pale kwenye mti.

IMAMU

Ndiyo,itakuwa vivyo hivyo. Mtu huwasha kibatari kutoka kingine, na mwangaza wa kwanza haupungui wakati dunia inaangaza.

MLAHIDI

Huko, watu watakula na kunywa. Je, hawatakuwa na haja ya kunya na kukojoa?

IMAMU

Chakula chao kitakuwa chepechepe sana na kitamu.Mavi hayatafanyika, badala yake yatatoka majasho.

MLAHIDI

Vipi hurulaini (wanamwali wa Peponi) watabaki kuwa bikira baada ya kujamiiwa na waume zao?

IMAMU

Hurulaini wameumbwa kutokana na kitu kilichotakasika na safi. Cho chote hakiwezi kuwabadilisha,wala dhara lolote kuwadhuru.Cho chote hakitoki kwenye sehemu zao za stara, wla hawapati hedhi. Matumbo yao ya uzazi hayatatungika mamba. Hakutakuwa na nafasi zaidi ya kuingia cho chote katika sehemu zao za stara isipokuwa uume.

MLAHIDI

Ingawa hurulaini huvaa nguo, lakini musuli ya miguu yao itaonekana kwa waume zao. Vipi?

IMAMU

Ni kama tunavyoona sarafu inayong'ara chini ya mto wenye maji safi.

MLAHDI

Vipi watu wa Peponi watastarehe neema za Peponi wakati watoto, baba, mama na marafiki zao hawatakuwa pamoja nao. Ikiwa hawatakuwepo huko, lazima watakuwepo Motoni.Vipi watakuwa na furaha juu ya kuwa wapenzi wao wanaadhibiwa Motoni?

IMAMU

Watawasahau.Au watawaona baada ya kutolewa katika A'araf (mahali ambapo watu huwekwa kwa kungoja kutolewa uamuzi juu yao).

TAMATI