HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)27%

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S) Mwandishi:
Kundi: Vitabu mbali mbali

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)
  • Anza
  • Iliyopita
  • 12 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 39075 / Pakua: 4593
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

Mwandishi:
Swahili

1

1

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W) PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema kuwa: Ayah ya Qur'an Surah Al-Hajj, 22, Ayah ya 28:

﴿لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ ﴾

Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama hoa alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri.

"Allah swt katika ayah hii anamaanisha kuwalisha wale walio na shida na kuwasaidia, ambapo wao kwa heshima zao wenyewe hawajitokezi nje mbele ya watu kuomba."

Isack bin Ammar amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kuwa:

"Utafika wakati mmoja ambapo waombaji wanaorefusha mikono yao kwa watu watakuwa wakiishi kwa starehe na wale watakao kaa kimya kwa kutunza heshima zao watakuwa wakifa kwa shida zitakazo kuwa zikiwakabili.

Kwa hayo mimi nikamwuliza Imam(a.s) , "Ewe Maula ! Je yakitokea hayo katika zama za uhai wangu mimi nifanyeje?"

Imam(a.s) akamjibu:"Kwa hakika kile ulichonacho wewe uwasaidie hao watu kwa hali na mali na kwa hata cheo chako ulicho nacho na kwa wadhifa wako ulio nao uwasaidie ipasavyo."

Abu Basir anasema kuwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) aliitolea maelezo Ayah ya Qur'an Tukufu Surah Al Baqara, 2, ayah ya 267 isemayo:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ﴾

Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

amesema Kuwa:"Zama kabla ya Uislam watu walikuwa wamejilimbikizia mali iliyopatikana kwa njia zisizo halali (kwa njia zilizo haramu) na baada ya wao kusilimu, walikuwa wakidhani kuwa kwa kutoa mali iliyo patikana kwa njia haramu, watakuwa wametakasisha mali yao iliyo halali, kwa hivyo Allah swt alitoa amri kuwa sadaka itolewe kutoka mali iliyo halali tu."

Kwa kuzungumzia ayah hiyo ya juu Shahab amenakili riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kuwa:

"Ambamo amesema kulikuwa na kaumu moja ambayo walikuwa na mali nyingi iliyo chafu (iliyopatikana kwa njia za haramu ). Wakati wao walipoukubalia Islam walianza kuchukizwa na malimbikizo yao hayo machafu na wakataka kutoa kwa njia za sadaka. Allah swt aliwaonya kwa kuwaambia kuwa sadaka hutolewa kutokea mali iliyo halali tu."

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Iwapo watu watachuma au watajipatia mali kwa mujibu wa hukumu za Allah swt na wakaitumia kinyume na hukumu za Allah swt au iwapo watachuma kwa njia zilizo kinyume na hukumu za Allah swt na wakazitumia kwa mujibu wa hukumu za Allah swt; katika hali zote mbili Allah swt hazikubalii.

Katika kutaka kukubaliwa sharti ni kwamba mapato hayo yawe yamepatikana kwa njia zilizo halali na zitumiwe katika njia zilizo halali vile vile."

Halabi anasema kuwa mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kuhusiana na ayah hii katika Qur'an Tukufu Surah Al Baqarah, 2, ayah ya 267:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ﴾

Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

Na hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) akasema:

"Wapo baadhi ya watu ambao baada ya kuingia katika Uislam bado wameendelea kubakia na mali iliyopatikana kwa njia zisizo halali. Na humo kulikuwa na mmoja ambaye kwa makusudi alianza kutoa sadaka kutoa mali hiyo isiyo halali. Na Allah swt alimzuia kufanya hivyo yaani sadaka haiwezi kutolewa isipokuwa kutokea mali iliyotokana kwa njia halali."

AL IMAM HASSAN AL-'ASKARI (A.S)

Katika Ma'anil Akhbar Al Imam Hassan al-'Askari(a.s) kwa kupitia sanad amenakili riwaya moja kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kuwa amesema:

"Wale ambao wanajiona utukufu na wakubwa na ambao wanatenda matendo kwa mujibu wa nafsi zao, mfano wake ni wa yule mtu ambaye mimi nilisikia watu wakimsifu sana na kumheshimu sana, na hivyo mimi nikawa na shauku ya kutaka kuonana na mtu huyo lakini katika hali ambayo yeye hataweza kunitambua. Siku moja mimi nilimwona alikuwa amezingirwa na watu. Baada ya muda mchache kupita mimi nikamwona yeye ametoka humo na akawa anaondoka, basi mimi nilimfuata nyuma yake.

Tulipita katika duka la muuza mikate, huyo mtu kwa kuficha macho yake na kificho ficho akaiba mikate miwili. Kwa hakika mimi nilistaajabishwa mno, na nikadhani kuwa labda wao wana maelewano fulani kabla ya tukio hilo. Tukaendelea mbele yeye akamghafilisha mfanya biashara huyo na akaiba makomamanga mawili humo. Na hapa pia nikafikiria kwa labda wao watakuwa na maelewano kama hayo kabla ya kutokea tukio hili, nikiwa hapo nikaingiwa na wazo kuwa je iwapo watakuwa na maelewano kama hayo basi kwa nini achomoe vitu kimafichoficho? Basi mimi niliendelea kumfuata nyuma yake, tukafika njiani akamwona mtu mmoja mgonjwa basi huyo akasimama kwa mgonjwa huyo na akatoa ile mikate miwili na hayo makomamanga mawili, akampa huyo mgonjwa.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) akamwuliza huyo mtu:kulikuwa na dharura gani kwa kufanya hivyo? Mtu huyo kwa kuniona mimi akasema: je wewe ni Ja'afar bin Muhammad? Nami nikamjibu: naam, basi yeye hapo akaanza kusema: nasikitika sana kwa kutokujitambulisha kwako hapo kuja kukufikishia faida (kwa sababu Imam(a.s) alikuwa hakujionyesha kuwa yeye ni Imam, bali alikuwa amejiweka kama yeye ni mtu wa kawaida) Imam(a.s) akamwambia:kwa hakika matendo yako hayo yana aibisha. Basi yeye akasema kuwa: Allah swt anasema katika Qur'an Tukufu Surah An A'Am, 6, Ayah 160:

﴿مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴾

Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. Na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa.

Ama kwa mujibu wa ayah ya Qur'an Tukufu mimi nimeiba mikate miwili hivyo nimetenda madhambi mawili na nimeiba makomamanga mawili hivyo nimetenda madhambi wawili na kwa ujumla nimetenda madhambi manne. Na pale mimi nilipompa mgonjwa sadaka mimi kwa kila wema nimepata malipo kumi ya thawabu hivyo jumla nimepata malipo ya thawabu arobaini. Na kutoka arobaini ukitoa nne ninayo mema thelathini na sita bado." Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) akamjibu:

"Mama yako akae kwenye kilio chako! Wewe kwa hakika umeitoa maana isivyo ya Ayah za Qur'an Tukufu. Je wewe huelewi ayah ya Qur'an Tukufu isemayo Surah Al Ma'ida, 5, Ayah ya 30:

﴿فَطَوَّعَتْ لَهُ نَفْسُهُ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ فَأَصْبَحَ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴾

Basi nafsi yake ikampelekea kumuuwa nduguye,akamuuwa na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika.

Kwa mujibu wa ayah hiyo wewe umeiba mikate miwili umetenda madhambi mawili na kwa kuiba makomamanga mawili umetenda madhambi mawili mengine na hivyo jumla umetenda madhambi manne, na pale ulipotoa hiyo mali yaani mikate na makomamanga, kama sadaka bila idhini ya mwenye mali basi umetenda madhambi mengine manne. Kwa hivyo umetenda madhambi nane kwa pamoja. Sasa wewe unafikiria mema hayo arobaini yametoka wapi?" Kwa hakika mtu huyo aliduwaa, akimwangalia Imam(a.s) na akajiondokea zake. Baada ya hapo Imam(a.s) akasema:

" kwa kujitolea maana potofu ya ayah za Qur'an Tukufu vile isivyo sahihi ndio matokeo yake haya na vile vile kuwapotosha watu wengine pia."

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Katika tafsiri Ayyashi Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amenakiliwa akitoa tafsiri ya ayah Surah Al Baqara, 2, ayah ya 267:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ﴾

"Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa".

Imam(a.s) akaelezea:"Miongoni mwa watu kulikuwa kumelimbikwa mali iliyopatikana kwa riba na njia zingine zisizo za halali, basi wao walinuia kutoa sadaka humo, na ndipo Allah swt alipowakataza kufanya hivyo (kutoa sadaka kutoka mali iliyopatikana kwa njia za haramu hairuhusiwa)."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) ameripoti riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kuwa amesema: "Katika vitu vya kuleta uokovu mojawapo ni kuwalisha chakula wale wenye kuwa na shida na dhiki, na pili mtu awe ni mwanzilishi awe ni mwanzo wa kutoa salamu na vile vile wakati watu wamelala usingizi mtu anaamka kwa ajili ya kusali na kufanya 'ibada."

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Muhammad Yakub amenakili kutoka 'Ali bin Ibrahim ambaye naye amenakili kutoka Muhammad bin 'Isa bin 'Ubaid ambaye naye amenakili kutoka kwa Ahmad bin Muhammad, naye amenakili kutoka kwa ibn Fazzal Ma'aruf, naye kutokea Tha'alaba bin Maymun, ambaye naye pia amenakili riwaya hiyo kutoka kwa Zurarah, kuwa: Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa:

"Allah swt hupendezewa mno kulishwa chakula wale wenye dhiki na shida na njaa, na vile vile hupendezewa kutolewa kwa dhabihu (qurbani)."

AL IMAM 'ALI AR-RIDHA (A.S)

Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema:

"Yeyote yule ambaye hakubahatika kutufanyia sisi wema basi ni wajibu wake kuwafanyia mema na kuwatimizia mahitaji ya marafiki zetu. Na yeyote yule ambaye hakubahatika kudhuru makaburi yetu basi adhuru makaburi ya wafuasi na marafiki zetu."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Muhammad bin Ali bin Hussein Jamil amenakili riwaya moja kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kuwa:

"Miongoni mwenu mtu aliye bora kabisa ni yule mwenye moyo mkarimu,(mwenye moyo wa kutoa) na mtu mwovu kabisa ni yule ambaye ni bahili. Na usafi wa imani dalili yake ni kwamba huwawia kwa wema muumin mwenzake na kuwatimizia dharura na mahitajio yao. Bila shaka yeyote yule anayewafanyia hisani ndugu zake katika imani basi ndiye mpenzi wa Allah swt, kwa sababu katika kufanya wema huko kuna mambo mengi yanayomzuia mtu asiingie katika mitego ya Sheitani, na vile vile asiingie Jahannam, na kwa matokeo yake ndiye mtu anayeingia Jannat." Baada ya hapo Imam(a.s) alimwambia Jamil:

"Ewe Jamil! Habari hizi uwafikishie wenzako". Kwa hayo mimi nikasema, "Ewe mwana wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ! Niwe fidia juu yako. Je ni watu gani hao?" Imam(a.s) akasema:

"Hao ni wale ambao wanawafanyia wema ndugu zao katika imani wakati wa shida huwa pamoja nao na vile vile wakati wa furaha pia huwa nao."

Sheikh Sadduq (r.a) amenakili riwaya kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) ambaye amesema kuwa:

"Yeyote yule ambaye hakupata fursa kufanya wema nasi, basi awafanyie wema wapenzi na wafuasi wetu basi atapata thawabu za kutufanyia wema sisi. Na vile vile ambaye hakubahatika kutuzuru sisi katika uhai wetu na uhai wake basi awazuru wapenzi na wafuasi wetu, basi atapata thawabu kama za kutuzuru sisi."

Safwan Al-Jammal anasema kuwa: siku moja Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) alimwambia Mu'alla bin Hunais:

"Ewe Mu'alla! Uwe wa Allah swt, ili Allah swt aweze kukutunza na kukuhifadhi.

Kwa hayo Mu'alla alianza kusema: "Je hivyo inawezekanaje?" Basi Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) akamjibu:

"uwe na hofu ya Allah swt, uwe daima ukimwona yeye katika mawazo yako, kwa hiyo yeye atakifanaya kila kitu kiwe kikikuogopa wewe, na vile vile kitakuwa kikikuwazia wewe na kukujali wewe. Ewe Mu'alla ili kujipatia mapenzi ya Allah swt lazima uwatendee watu matendo mema, na utambue wazi wazi kuwa Allah swt anapendezewa sana na moyo wa ukarimu na huchukizwa sana na ubahili na huwa na uadui nao".

Angalia ! Wewe kama utaniomba chochote na mwisho wake wewe ukaaza kufanya mapenzi nami, na badala yake mimi nitafurahishwa sana iwapo wewe hautaniomba chochote na hautapata chochote kutoka kwangu na baada ya hayo wewe bado ukawa na mapenzi nami. Na kwa hakika ukiniuliza mema yote naweza kuyafanya kwa ajili yako basi ukweli ni kwamba sifa zote ni za Allah swt kwa sababu yeye amekupitishia neema yake kwa mikono yangu mimi nimekuwa ni kipitishio tu kwa ajili yako kwa hiyo yeye ndiye anayestahiki sifa zote." "Kwa kusikia hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) alimwambia,

"Nyamaza!" Wale mafukara ambao wanawajali ndugu na jamaa zao na kuwawia wema wenzao, Allah swt huwapa ujira mzuri sana, kwa sababu Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu: Surah Sabaa, 34, ayah 37:

﴿وَمَا أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُم بِالَّتِي تُقَرِّبُكُمْ عِندَنَا زُلْفَىٰ إِلَّا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ جَزَاءُ الضِّعْفِ بِمَا عَمِلُوا وَهُمْ فِي الْغُرُفَاتِ آمِنُونَ﴾

"Na si mali yenu wala watoto wenu watakao kukaribisheni kwetu muwe karibu, isipo kuwa aliye amini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu kwa walio yafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa"

Sheikh uleyni amenakili riwaya kutoka kwa Ahmad bin 'Isa kuwa Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

﴿إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ﴾

"Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea".

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema kuwa:neno 'Innama' inamaanisha kuwa katika kazi zenu au shughuli zenu zote, mwenye kuwa na haki zaidi kuliko yeyote juu ya nafsi zenu na mali zenu ni Allah swt, baada yake ni Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) na baada yake ni, Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) na hadi kufikia Qiyama Maimamu (a.s) kutokea kizazi chake.

Vile vile Allah swt ameelezea fadhila zao kwa kusema katika Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

﴿إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ﴾

"Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea"

Kisa katika ayah hii ni kwamba: Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alikuwa akisali sala ya Dhuhuri, alipomalizia raka'a ya pili tu akatokezea mwombaji. Siku hiyo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alikuwa amevaa Khullah yenye thamani ya Dirham elfu moja ambayo alikuwa amepewa zawadi na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Na Imam(a.s) alipokuwa katika hali ya Ruku'u, kulitokezea maskini mmoja ambaye akasema, "Ewe Walii wa Allah swt na muumin halisi, iwe salamu juu yako, naomba unipe mimi maskini sadaka yoyote. Kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) aliinamisha chini Hulla na kwa ishara akamwambia huyo maskini aichukue."

Kwa tukio hili ndipo Allah swt alipoteremsha ayah hii kwa ajili yake na kwa ajili ya kizazi chake na kuonyesha fadhila na kufuzu kwao. Fadhila zao kuwa wanagawa sadaka hata kama watakuwa katika hali ya Rukuu. Kwa hakika imekuja kujulikana kuwa yule maskini aliyekuja kuomba alikuwa si mtu bali alikuwa ni Malaika ambaye alikuja kuomba, na vile vile katika kizazi kizima cha Maimam a.s. pia tumeona mara nyingi sana Malaika huwa wanakuja kuomba katika sura ya maskini.

Katika kitabu kiitwacho Ihtijaj humo Tabarasi amenakili riwaya kutoka Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ameelezea kuhusu ayah hiyo kuwa:

"Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) katika hali ya sala akiwa katika Ruku'u alitimiza wajibu wake na akatoa Zaka na Allah swt ndipo alipoiteremsha hiyo ayah na makusudio yake yalikuwa ni kupata ridhaa ya Allah swt."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Ali bin Ibrahim katika kitabu chake Tafsir ananakili riwaya kutoka kwa baba yake Ma'arifat Safwan kuwa Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) amesema: "Siku moja Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipokuwa amekaa pamoja na 'Abdullah bin Salam kulikuwa na kikundi cha Mayahudi pia. Na wakati huo ikateremshwa ayah ya Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

﴿إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ﴾

"Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea"

Baada ya hapo mara Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akatoka nje haraka na akaelekea msikitini na huko njiani alikutana na mwombaji mmoja na hivyo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwuliza:

"Je kuna mtu aliyeweza kukusaidia?" Basi huyo mwombaji akasema: "Naam, kuna mtu anayesali msikitini humo ndiye aliyenisaidia." Na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alivyoukaribia msikiti akamwona huyo mtu si mwingine bali ni Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Na riwaya hii vile vile imenakiliwa na Abu Hamza ambaye ameandika katika Tafsir Ayyashi.

2

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Muhammad bin Ali bin Hussein katika kitabu cha Amali amenakili riwaya kutoka Abul Ja'rud Ma'rifat kuwa Al Imam Muhammad al-Baquir(a.s) amenakiliwa riwaya kuwa amezungumzia kuhusu ayah Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

﴿إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ﴾

"Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea"

kama ifuatavyo: "Katika Mayahudi ambaye mnafiki mmoja alipoukubalia Uislam akaanza kuiga: "Ewe Mtume wa Allah swt! Je ni nani Wasii na Khalifa wako? Na nani huyo atakaye kuwa Walii baada yako?"

Ndipo hapo ayah hiyo ilipoteremshwa na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) akawaambia inukeni, basi hao wote wakainuka na wakaanza kuelekea msikitini. Walipofika msikitini wakakutana na maskini mmoja akitoka nje na hivyo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akamwuuliza, "Je kuna mtu yeyote aliyekupa chochote ?" Huyo akasema "Kwa nini isiwe hivyo pete hii je niliyoipata?" Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema,"Je ni nani aliyekupa?" Huyo mwombaji akasema "Huyo mtu ambaye bado anasali." Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akasema:"Je alipokupa hiyo pete alikuwa katika hali gani?"

Huyo mwombaji akasema: alikuwa katika hali ya Ruku'u. Na hapo ndipo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipopaaza sauti ya Takbira, yaani Allahu Akbar na wale wote waliokuwepo pamoja naye nao pia walitoa Takbira kwa nguvu na sauti na hapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ndipo alipowaambia wote:"Mtambue wazi kuwa baada yangu Walii ni huyu Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) na wa si mwingine" Karta anasema kuwa: "Kwa mujibu wa riwaya zilizopatikana kuwa katika sala moja aliitoa Hullah, na katika sala ya pili alitoa pete basi inadhihirika kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) anatoa sadaka katika hali ya sala zaidi ya mara moja ndivyo inavyothibitika kwa mujibu wa riwaya zinazopatikana."

Ayyashi katika Tafsir yake ananakili riwaya moja kutokea kwa mwana wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) kuwa Ammar Yasir amesema: "Siku moja Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alipokuwa akisali sala ya Sunnah aliahirisha tendo moja kiasi kwamba mpaka akavua pete yake kwa ajili ya kumpa aliyekuja kuomba. Na pale Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alipokuja basi alimwelezea hivyo. Na wakati huwo iliteremshwaayah yake hadi kufikia : Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 55:

﴿إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ﴾

"Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea"

Basi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alitusomea ayah hiyo na akasema:

"Yeyote yule ambaye mimi ni Mawla wake basi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ni Mawla wake. Ewe Allah swt! Uwe na mapenzi na yule ambaye anawapenda wao, na uwe na uadui na yule ambaye anafanya uadui pamoja nao."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Halabi anasema kuwa; yeye alipomwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) basi Imam(a.s) akamjibu:

"Naam kabisa! Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib (a.s) aligawa nusu ya mali yake katika njia ya Allah swt - hadi kwamba nguo kwa nguo, Dinar kwa Dinar, alivigawa vyote katika njia ya Allah swt, na alikwenda Hija ishirini kwa kutembea na miguu."

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

Mtume Muhammad(s.a.w.w) Amesema:

"Umma wangu utaendelea kuishi kwa heri pale watapokuwa waaminifu miongoni mwao, watakapokuwa wakirejesha amana watakazokuwa wakiachiana, na watakapokuwa wakitoa sadaka kutoka mali zao; Lakini, Iwapo wao hawatatimiza wajibu hizo, basi watakumbwa na ukame na baa la njaa."

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s), katika Nahjul Balagha, uk.512, Msemo 254 :

"Enyi wana wa Adam ! Muwe wawakilishi wenu wenyewe katika mali yenu na mfanye kile chochote kile mnachotaka kufanyiwa nyie baada ya kifo chenu." Tanbih Iwapo mtu atataka baada ya kifo chake sehemu fulani ya mali utajir wake utumike katika kutoa sadaka au misaada, basi asisubiri mpaka afe bali aitumie popote pale atakapo katika uhai wake kwa sababu inawezekana kuwa baada ya kifo chake warithi wake wasiweze kutekeleza kwa mujibu wa vile alivyotaka au usia wake na labda inawezekana asipate wakati wa kuandika usia hivyo akakosa fursa hiyo."

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema, katika Kanz-ul- 'Ummal, J. 6, Uk. 371:

"Toeni sadaka na muwatibu wagonjwa wenu kwa hayo, kwa sababu sadaka kwa hakika inatoa balaa na magonjwa; na inaongezea umri wenu ukawa mrefu na kuongezeka kwa thawabu zenu."

Imenakiliwa kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Al-Ithna-'Asheriyyah, Uk. 85 akisema:

"Nilipokuwa nimekwenda mbinguni, mimi niliona mistari mitatu imeandikwa juu ya mlango wa Jannat: Mstari wa kwanza ulikuwa umeandikwa Bismillah Rahman Rahim; Mimi ni Allah swt na hakuna Allah swt mwingine isipokuwa mimi na Rehema zangu zinazidi adhabu zangu. Mstari wa pili ulikuwa umeandikwa Bismillah Rahman Rahim; Sadaka inalipwa kwa mara kumi (10) na mkopo unalipwa mara kumi na nane (18), na kuwajali maJama'a na ndugu kunalipwa mara thelathini (30). Mstari wa tatu ulisomwa yeyote yule anayeelewa wadhifa Wangu na Ukuu wangu basi kamwe asinishutumu mimi katika maswala ya maisha."

AL IMAM ZAYNUL 'ABEDIIN (A.S)

Taus-ibn-il-Yamani anasema kuwa; yeye alimsikia Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) akisema:

"sifa za muumin ni tano na pale alipoombwa kuzitaja alijibu, Khisal-i-Sadduq, Uk. 127: "Ucha Allah swt katika hali ya upweke, kutoa sadaka wakati unaohitajika, Subira anapopatwa na matatizo au anapokuwa na shida, uvumilivu wakati wa ghadhabu, ukweli ponapokuwa na hofu."

KUTOA SADAKA NA UBAHILI

Mali ya mchoyo huliwa na warithi wake au hupeperuka bila kujulikana.

Hakuna mtu mwenye upweke vile alivyo bahili.

Mchoyo ni mweka/mtunzi hazina wa warithi wake.

Ubahili na uchoyo huangamiza upendo wa urafiki wa kweli.

Ubahilifu ni kujipatia ubadhirifu.

Kuwa mchoyo kwa kile ulichonacho ni kutomwamini Allah swt.

Sifa ya upole na wema huangamizwa kwa ubahili.

Fedha haimnufaishi mwenye kuwa nayo hadi hapo atenganapo nayo.

Maovu hufichwa kwa ukarimu.

Bora wa watu ni yule afaaye watu

Hakutakuwa kuwafadhili watu kwa mifuko mitupu.

Fadhila huuliwa kwa matumizi fidhuli.

Uachie ngome ya Sadaqa iilinde ufanisi wako.

Kutoa baada ya kughairi ni bora zaidi kuliko kughairi baada ya kutoa.

Uso ulio mcheshi ni mojawapo ya ne'ema mbili.

Usimuudhi mtu yeyote yule pale akutakiapo kila la kheri.

Fadhila na ukarimu hupatiwa sifa.

Fadhila ya kweli (kwa moyo safi) huondoa dhiki zote

Makosa ya mwenye kutoa fadhila ni afadhali kuliko dharau ya mchoyo.

Fadhila isiongozwe kwa uoga wala kuwa na matumainio ya kupata chochote (tamaa).

KUWAJALI NDUGU NA MAJAMA'A

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema

"Yeyote yule anayetaka kuongezewa riziki na baraka na siku yake ya mauti icheleweshwa, basi inambidi awajali ndugu na maJama'a zake."

Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 89

AMESEMA AL IMAM 'ALI AR-RIDHA (A.S)

Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) , kuwa:

"Mali haiwezi kulimbikana kupita kiasi isipokuwa kwa njia tano: Ubahili kupita kiasi, matarajio makubwa sana, uroho kupita kiasi, kuvunja uhusiano pamoja na ndugu na maJama'a za mtu mwenyewe, na kuijali na kuipenda dunia hii kuliko Akhera."

Bihar al-Anwaar, J. 73, Uk. 138

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQUIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) , Amesema:

"Kuwajali Jama'a na ndugu kunaleta faida tano: Kutakasika na kukubalika kwa matendo ya mtu Kuongezeka katika utajiri na mali Kuondoa balaa na shida mbalimbali Kurahisisha maswala yake katika Akhera Umri kuwa mrefu."

Al-Usuli- AlKafi , J. 2, Uk. 150

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , Amesema:"Kuna makundi matatu ya watu ambao hawataruhusiwa kuingia Jannat: Wanywaji wa pombe, Wachawi , na wale wanaokana Jama'a na ndugu zao.

Al-Khisal Uk. 179

KUWAHURUMIA WAZAZI

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , kuwa:

"Furaha ya Allah swt ipo katika furaha ya wazazi wa mtu (kama ndio hivyo ni kweli, basi adhabu na ghadhabu zake pia zipo katika ghadhabu za wazazi wa mtu"

Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 15, Uk. 176

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , kuwa:

"Bora ya matendo ni: Kusali kwa wakati wake, kuwa mwema na mwenye huruma na mwenye mapenzi kwa wazazi wake, na kuchangia katika vita vitakatifu vya Jihad (dhidi ya Mapagani) katika njia ya Allah swt."

Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 85

Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , kuwa:

"Iwapo mtu anataka Allah swt ampunguzie makali ya mauti, basi lazima awajali Jama'a na ndugu zake, na awawie wema wazazi wake. Na pale mtu anapofanya hivyo, basi Allah swt atampunguzia makali ya mauti na kamwe hatapata umaskini katika maisha yake."

Safinat-ul-Bihar, J. 2, Uk. 553.

Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , kuwa:

"Yeyote yule anayewatazama wazazi wake kwa macho ya ghadhabu, hata kama wao hawakuwa waadilifu kwake, basi Allah swt hatazikubalia ibada za mtu huyo (hadi hapo atakapofanya Tawba)."

Al-Usuli- Kafi, J. 2, Uk. 349.

Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , kuwa:

"Watendee wazazi wako kwa huruma ili na watoto wako waje wakutendee vivyo hivyo; na uwe mcha Allah swt kwa wake wa watu wengine ili wake zako wabakie wacha Allah swt."

Al-Kafi J. 5, Uk. 554.

Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) , kuwa:

"Safari moja mtu alimwijia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na kumwuliza namna ya kuwashughulikia wazazi. Hapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimjibu uwe mwenye huruma kwa mama yako: uwe mwenye huruma kwa mama yako na uwe mwenye huruma kwa mama yako; Uwe mwenye huruma kwa baba yako uwe mwenye huruma kwa baba yako; na uwe mwenye huruma kwa baba yako lakini huruma hiyo uianzie kwa mama yako kabla ya baba yako."

Al-Kafi J. 2, Uk. 162.

HAKI ZA WATOTO

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alimwambia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) :

"Ewe Ali ! Allah swt huwalaani wazazi wale wanao wafanya watoto wao wasiwe watiifu kwao kwa sababu ya kuwalaani kwao."

Wasa'il ush-Shi'ah, J. 31, Uk. 290

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alimwambia mmoja ya wafuasi wake: "Usiupitishe wakati wakati wako mwingi pamoja na mke wako na watoto wako waliokuwa wakubwa, kwa sababu kama mke wako na watoto wako ni wampendao Allah swt, basi Allah swt hatawaacha wapenzi wake bila ya kuwajali, iwapo watakuwa ni maadui wa Allah swt, basi kwa nini wewe uwe na wasiwasi na ujiweke mashughuli kwa ajili ya maadui wa Allah swt.

Na mambo mawili yanayoweza kuchukuliwa katika wanaume katika kuhusiana na kuwapatiapo familia zao. Moja ni kutokutimiza wajibu wake kwao, na pili kinachotajwa hapa ni kulimbikiza kupita kiasi kwa mali kwa ajili yao."

Nahjul Balagha Uk. 536, Msemo, No. 352.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) ,:

"Chukueni hatua za kuwafundisha watoto wenu riwaya na ahadith za Ahlul Bayt(a.s) kabla watoto wenu hawajaharibika na hawajachafuliwa akili zao."

Al-Kafi J. 6, Uk. 47.

Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) :"Heri ya mtu kwa mtoto wake ni kule kwa mtoto wake kuwa heri kwa wazazi wake."

Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 483

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) :

"Haki ya mtoto kwa wazazi wake ni kwamba apewe jina zuri kabisa, afundishwe adabu njema na afundishwe Qur'an kwa kanuni zake."

Nahjul Balagha, Msemo 399

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

A. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Wafundisheni watoto wenu kuogelea na kulenga shabaha"

Al-Kafi J. 6, Uk. 47

B. Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) "Watoto wenu wanapokua kufikia umri wa miaka saba, wafundisheni sala, wanapokuwa na umri wa miaka kumi, muwalazimishe kusimamisha sala; na mutenganishe vitanda vyao vya kulalia."

Kanz-ul- 'Ummal, J. 16, No. 45, 330:

AL IMAM ZAYNUL 'ABEDIIN (A.S)

Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin(a.s) :

"Haki ya mtoto wako ni kwamba wewe utambue wazi kuwa yeye amekuja humu duniani kwa kukupitia wewe, kwa hiyo yaliyo sahihi na yaliyo mabaya yanatokana na wewe. Wewe unawajibika kumpa mafunzo na elimu bora, kumwelekeza kwa Allah swt, na kumsaidia katika kumtii Allah swt. Kwa hivyo iwapo utamsaidia utamfanyia hisani mtoto wako, basi utaweza kufikia malengo hayo; na kama wewe utamwia kiovu, basi hayo yatakurejea wewe mwenyewe."

Man la Yahdharul Faqih, J. 2, Uk. 622:

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) Amesema:

"Muwaheshimu watoto wenu na muwafundishe kuwa wema, mtasamehewa na Allah swt."

Bihar al- Anwaar, J. 104, Uk. 95:

KUNYOYESHA MAZIWA

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Amesema Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w)

"Naam malipo ya mwanamke wakati wa mimba yake hadi kuzaa mtoto, na wakati pale anapolea mtoto ni sawa na kuwekwa askari katika kituo cha kulinda mipaka ya Waislam dhidi ya hujuma za makafiri, kwa ajli ya Allah swt. Kwa hivyo iwapo atakufa katika kipindi hiki, basi mwanamke huyo atakuwa katika daraja la mashahidi"

Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 561:

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB ( A.S)

Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) :

"Hakuna maziwa yenye faida zaidi kwa mtoto isipokuwa maziwa anayonyonya kutoka kwa mama yake."

Wasa'il ush-Shi'ah, J. 21, Uk. 452

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Wakati mwanamke anaposhika mimba basi atakuwa ni kama mpiganaji ambaye anafunga saumu wakati wa mchana na anakesha usiku kucha katika 'ibada, na amejitolea mhanga maisha yake na mali yake katika njia ya Allah swt. Hivyo anapozaa anapata malipo makubwa sana ambayo hakuna mtu anayeelewa isipokuwa Allah swt mwenyewe. Na pale anaponyonyesha mtoto maziwa basi atapata thawabu za kumfanya mtoto mmoja kuwa huru kutoka katika kizazi cha Mtume Ismail(a.s) kwa kila mara atakapo nyonyesha. Na wakati ufikapo kipindi cha kumuachisha mtoto kunyonya, basi malaika aliyekaribu naye humwambia kuanza matendo kwa mara nyingine tena kwani kwa hakika yeye sasa hivi alipo ni katika hali ya kusamehewa kikamilifu (yaani ashike mimba na kuzaa na kunyonyesha tena kwa mara nyingine"

Bihar al- Anwaar, J. 104, Uk. 106:

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Hakuna maziwa yaliyo bora kabisa kwa mtoto isipokuwa maziwa ya mama yake."

Mustadrak- ul-Wasa'il, sehemu ya 48

NDOA 'IBADA KUU

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) Amesema:

"Raka'a mbili za sala zinazosaliwa na mtu aliyeoa ni nzito kuliko yule asiyeoa ambaye anakesha usiku kucha katika ibada na kufunga saumu nyakati za mchana."

Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 384

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Usingizi wa mtu aliyeoa ni afadhali mbele ya Allah swt kuliko ibada afanyazo mtu asiyeoa usiku kucha na anayefunga saumu nyakati za mchana."

Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 221

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Wengi wa watendao wema katika 'ummah wangu ni wale waliooa na kuolewa wakati watendao maovu wengi wao ni wale wasio oa au kuolewa."

Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 221

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

. Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) anasema:

"Siku moja mtu mmoja alimwijia baba yangu naye a.s. alimwuliza iwapo alikuwa ana mke naye akajibu alikuwa hana. Hapo baba yangu(a.s) alimjibu kuwa yeye hawezi kulala usiku mmoja bila ya mwanamke hata kama atapewa badala yake dunia nzima na yale yote yaliyomo ndani yake. Na hapo Imam(a.s) alimwambia kuwa Raka'a mbili anazosali mtu aliyeoa ni bora kuliko ibada ya yule asiyeoa kwa kukesha usiku kucha na kufunga saumu katika nyakati za mchana. Na baadaye Imam(a.s) alimpa Dinar za dhahabu saba na akamwambia akaolee kwa hayo"

Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 217

KUWAPA HIMA KWA AJILI YA KUOA

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema:

"Mtu anayeoa hujipatia nusu ya imani yake, na nusu ya imani inayobakia lazima awe na Taqwa."

Al-Kafi J. 5, Uk. 328

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema::

"Wengi wa watu wa Jahannam watakuwa wale wasioolewa (bila kujali mwanamme au mwanamke)."

Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 384

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Wengi wa wapotofu na walio haribika katika wale walio kufa miongoni mwenu ni wale wasioolewa na wasiooa."

At-Tahdhib, J. 7, Uk. 239

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Yeyote yule anayetaka awe msafi na aliye takasika wakati atakapo onana na Allah swt, basi aoe na awe na mke."

Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 385

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Oeni, ama sivyo mtahesabiwa miongoni mwa Rahbani au ndugu wa maShaytani"

Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 221:

NDOA NI UFUNGUO WA REHEMA ZA ALLAH SWT NA BASHARA NJEMA

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Milango ya Jannat kwa rehema itafunguliwa katika nyakati nne: Pale inaponyesha mvua, wakati mtoto anapoangalia kwa huruma nyuso za wazazi wake, pale wakati mlango wa Al Ka'aba tukufu inapofunguliwa, na pale ndoa inapofanyika"

Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 221.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema:

"Waunganisheni watoto wenu wavulana kwa wasichana kwa ndoa kwa sababu, humo Allah swt huwajaalia tabia njema, na huwazidishia katika riziki na heshima zao"

Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 222.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema:

"Muolewe na muwaoze mabinti zenu, kwa sababu ni bahati nzuri kwa Mwislamu mwanamme kumtoa au kuwapa mtoto wake aliyekua au dada yake kwa ajili ya ndoa."

, Al-Kafi J. 5, Uk. 328

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Hakuna kilicho kipenzi mbele ya Allah swt kuliko ile nyumba ambayo kuna maamrisho ya Islam yanatekelezwa kwa ndoa; na hakuna kitu chochote kinacho mghadhabisha Allah swt kuliko nyumba ile ambamo kunatokea talaka na ufarakano na utengano kati ya bibi na bwana."

Al-Kafi J. 5, Uk. 328.

6

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

UCHAMBUZI WA MADA

Madda muhimu katika uchambuzi: Imebakia madda moja muhimu ndani ya uchambuzi wote huu, madda ambayo inataka kuangaliwa kwa makini na kusomwa, na huenda hiyo pekee ndiyo kikwazo ambacho huwachemua wapinzani pale wanaposhinikizwa kwa hoja nzito. Utawaona wanashangaa na kutokuamini ya kuwa Masahaba wapatao laki moja walihudhuria kutawazwa kwa Imam Ali (kuwa Khalifa wa Mtume) na hatimaye hao hao Masahaba wakaafikiana wote kumkhalifu Imam Ali na kumpuuza na miongoni mwao wamo Masahaba wakubwa.

Hali hii (ya kushangazwa kwa wapinzani) imepata kunitokea mimi mwenyewe wakati nilipoingia kikamilifu ndani ya utafiti, sikuamini na haiwezekani kwa mtu yeyote kuamini pindi tukio hili linapoaridhiwa kama lilivyo, lakini wakati tunapolisoma tukio hili kwa pande zote basi kule kushangaa kunaondoka kwani hali halisi haiko kama tunavyoitazamia sisi au kama wanavyoiaridhi Masunni (ya kuwa) haiwezekani Masahaba laki moja wakaenda kinyume na amri ya Mtume, hivyo basi ilikuwaje mambo yakatokea kama yalivyotokea?

Kwanza Siyo kila aliyehuduria Baia ya Ghadir alikuwa akiishi Madina, bali ilikuwa kama ambavyo hali halisi ilivyokuwa kwamba kwa kiasi kikubwa itakuwa ni watu elfu tatu au Nne tu miongoni mwa Masahaba hao ndiyo waliokuwa wakiishi Madina.Na tutakapofahamu ya kwamba wengi wa hawa walikuwa ni watumwa na walioachwa huru na wanyonge ambao walimfikia Mtume (s.a.w.) kutoka sehemu mbali mbali na hapo Madina hawakuwa na uwenyeji wala jamaa (kwa mfano watu wa As-Safah) basi haitabakia isipokuwa nusu yao yaani watu elfu mbili tu, na hata hawa nao ni watiifu kwa viongozi wa makabila na muongozo wa kidugu ambao ndiyo wanaohusika nao na Mtume aliwakubalia (kuwa watiifu kwa viongozi wao) kwani ulipokuwa ukimfikia ujumbe wa kabila fulani, Mtume (s.a.w.) humtawalisha juu yao kiongozi wao, na kwa ajili hiyo ndiyo tumekuta katika Uislamu Istilahi ya kuitwa kwao kuwa ni Ahlul-Hilli wal-Iqdi, watu wanaotumainiwa kutowa maamuzi katika jamii au nchi.

Kadhalika tunapoutazama mkutano wa Saqifah ambao ulikutana mara tu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.), tunawakuta waliohudhuria ambao waliuthibitisha uchaguzi wa Abubakar kuwa ni khalifa, idadi yao haizidi watu mia moja kwa makadirio ya juu, kwani katika Ansari ambao ndiyo wenyeji wa Madina hawakuhudhuria isipokuwa viongozi wao kama ambavyo Muhajirina ambao ni wenyeji wa Maka waliohama pamoja na Mtume (s.a.w.) hawakuhudhuria isipokuwa watu watatu au wanne wakiwakilisha Maquraishi. Hali hii itoshe basi kuwa ni dalili ya kupima ukubwa wa hiyo Saqifah ikoje, Saqifah ambayo ilikuwa haina nafasi ya kutosha, kwani haikuwa inakosa kuwa karibu katika kila nyurnba.

Kwa hiyo haikuwa uwanja wa maadhimisho wala siyo jumba la mikutano, na tunaposema kuwa watu mia moja walihudhuria hapo Saqifah bani Saida basi idadi hiyo sisi ndiyo tunaoizidisha ili tu, mwenye kutafiti aweze kufahamu kwamba wale Masahaba laki moja hawakuwepo wala hata hawakusikia mazungumzo yalivyofanyika ndani ya Saqifah isipokuwa baada ya muda mrefu kupita, .kwani hapo zamani hapakuwa na mawasiliano ya anga wala simu au Satellite.

Na baada ya mabwana wakubwa hawa kuafikiana juu ya Abubakar pamoja na upinzani wa bwana wa Kiansari Saad bin Ubbadah ambaye ni kiongozi wa kabila la Khazraj na mwanawe Qais, lakini wengi mno miongoni mwao (kama isemwavyo hii leo) walipitisha makubaliano hayo na kumpa Abubakar mkono wa Baia, wakati ambapo Waislamu wengi hawakuwepo hapo Saqifah, na baadhi yao walikuwa wameshughulika kumuandaa Mtume (s.a.w.) kwa mazishi au walihamanika kutokana na khabari za kifo chake, ambapo Umar bin Al-Khatab naye alikuwa amewatisha na kuwatia khofu iwapo watasema kuwa Mtume amefariki. Taz: Sahih BukhariJuz. 4 -195.

Zaidi ya hayo wengi wa Masahaba wa Mtume walikuwa amewateua wawemo ndani ya Jeshi la Usamaha na wengi wao walikuwa wameweka kambi mahala paitwapo Jorfi wakiwa tayari kwenda vitani na jeshi la Usamah hawakuwepo Mtume alipofariki wala hawakuhudhuria mkutano wa Saqifah. Basi je, inaingia akilini baada ya haya yaliyotokea kwamba mtu fulani katika kabila au ukoo kumpinga kiongozi wake kwa lile alilolipitisha na hasa inapokuwa hilo alilolipitisha lina ubora na utukufu mkubwa ambao kila kabila linaukimbilia? Ni nani ajuwaye ya kwamba huenda siku moja naye atawatawalia Waislamu wote, maadamu mwenye haki hiyo kisheria amekwisha tupwa mbali na mambo sasa yanakwenda kwa kushauriana wanabadilishana kwa kuachiana, basi ni kwa nini wasilifurahie hilo, na ni kwa nini wasiliunge mkono?

Pili Ikiwa wenye uwezo wa kuamua ni wakaazi wa Madina na wamepitisha jambo fulani, basi watu walio mbali katika sehemu mbali mbali za bara Arabu hawawezi kupinga na hali ya kuwa hawajui yanayopita wakati hawapo kwani vifaa vya mawasiliano kwa zama hizo vilikuwa ni vile vya kizamani kisha wao walikuwa wakifahamu kwamba wakazi wa Madina ndiyo waliokuwa wakiishi na Mtume wa Mwenyezi Mungu hivyo basi hao ndiyo wajuao mno mambo mapya miongoni mwa hukmu, kwani huenda ukashuka Wahyi wakati wowote au siku yoyote. Kisha kama kuna kiongozi wa kabila lolote lililo mbali na makao makuu basi jambo la Ukhalifa kwake si muhimu sana sana iwapo Abubakr atakuwa Khalifa au Ali au mtu mwingine yeyote, kwani watu wa Maka ndiyo wajuao zaidi utaifa wao, na cha muhimu kwao ni kubakia kwenye uongozi wa ukoo wake ambapo hakuna anayemkera katika uongozi huo.

Basi ni nani ajuwaye kwamba huenda baadhi ya watu waliulizia juu ya jambo hilo (la Ukhalifa) na walitaka kufahamu mambo yalivyokwenda lakini vyombo vya mtawala viliwanyamazisha sawa iwe kwa njia ya kuwapa tamaa ya mali au vyeo au vitisho, na huenda kisa cha Malik bin Nuwairah ambaye alikataa kutoa zaka kwa Abubakr ni utokea jambo hilo. Na yeyote mwenye kufuatilia matukio hayo yaliyotokea katika vita ya wanaokataa kutoa zaka katika zama za Abubakr atakuta kuna kupingana (kwa maelezo), wala hawezi kutosheka kwa maelezo yaliyoelezwa na baadhi .ya wanahistoria kwa lengo la kulinda heshima ya Masahaba na hasa wale watawala.

Tatu Kiini cha tatizo hili ni kule kushitukizwa ghafla kupatikana kwa Khalifa, hili ni jambo lililochangia mno kukubalika kwa kile ambacho leo kinaitwa kuwa "Hali halisi iliyopo". Kwani mkutano wa Saqifah ulifanyika ghafla kwa kuwashitukiza baadhi ya Mashaba ambao walikuwa wakimshughulikia Mtume (s.a.w.), na miongoni mwao alikuwa Imam Ali na Abbas na wengine miongoni mwa Bani Hashim, Miq-dad, Salman, Abu Dharri, Ammar, Zubair na wengineo wengi. Ama wale waliokuwa Saqifah walipotoka huko hali ya kuwa wakimshangilia Abubakr walielekea msikitini huku wakitoa mwito kwa watu wafanye baia ya jumla na watu wakaipokea baia hiyo kwa wingi watake wasitake kipindi hicho Imam Ali na wafuasi wake walikuwa hawajamaliza wajibu wao Mtukufu ambao tabia zao (mwenendo wao) mwema uliwalazimisha (wautimize) basi haikuwezekana kwao kumuacha Mtume (s.a.w.) bila ya kumkosha, kumvisha sanda, kumtayarisha na kumzika eti badala yake wakimbilie Saqifah kugombea Ukhalifa.

Walipomaliza wajibu wao huo, mambo yalikuwa yamekwisha kamilika kwa Abubakr na yeyote mwenye kwenda kinyume na baia hiyo akawa anahesabiwa kuwa ni miongoni mwa watu wenye fitna ambaye anabomoa umoja wa Waislamu, hivyo ni wajibu kwa Waislamu kumpinga au hata kumuuwa ikiwa itabidi, na ndiyo maana tunamuona Umar alimuonya Saad bin Ubbadah kuwa atauawa pale alipokataa kumbai Abubakr, Umar akasema, "Muuweni hakika yeye ni mtu wa fitna"[52] na baada ya hapo Umar aliwatishia wote waliobaki ndani ya nyumba ya Ali ya kuwa atachoma moto nyumba hiyo na wote waliomo humo. Tukishakufahamu vyema maoni ya Umar bin Al-Khatab kuhusu baia tutatambua mengi baada ya hapo miongoni mwa mambo yanayotatanisha.

Kwa hakika Umar anaona kuwa baia inatosha kusihi pale mmoja miongoni mwa Waislamu anapowahi, basi hapo inakuwa ni lazima kwa wengine kumfuata na yeyote atakayeasi miongoni mwao huyo atakuwa ametoka nje ya mshikamano ya Waislamu na ni wajibu kumuuwa. Basi hebu na tumsikilize yeye mwenyewe hasa kuhusu baia, kama alivyoeleza Bukhar ndani ya Sahih yake juzuu ya nane ukurasa wa ishirini na nane, Babu Rajmi Al-Hubla Minaz-Zinaa Idha-Ah-Sanat amesema: akisimulia yale yaliyotokea ndani ya Saqifah. "Basi fujo ikazidi na sauti zikapaa mpaka nikatishika kuwa kutatokea kuhitilafiana, nikasema, Ewe Abubakr kunjua mkono wako, Abubakar akakunjua mkono wake nikambai nao muhajirina wakambai[53] Ansari (nao wakambai) na tukamruka Saad bin Ubbadah, akasema msemaji miongoni mwao, "Mmemuuwa Saad bin Ubbadah" Mimi nikasema:

"Mwenyezi Mungu amuuwe Saad bin Ubbadah" Umar akasema: "Wallahi sisi hatujakutana na jambo gumu katika yote tuliyohudhuria kuliko kumbai Abubakar, tulichelea kuwa hawa jamaa tukiwaacha bila kupitisha baia, basi watambai mtu miongoni mwao baada yetu, hivyo imma tuwape madaraka, jambo ambalo hatulikubali, au tuwapinge itokee uharibifu, (naonya) yeyote atakayetoa baia bila ya kushauriana na Waislamu asifuatwe yeye wala yule aliyembai ili asiuawe. Basi jambo lililovyo kwa Umar siyo uchaguzi wala hiyari wala mashauriano, bali inatosha pale Mwislamu mmoja anapoiwahi baia hiyo iwe ni hoja kwa wengine na ndiyo maana alimwambia Abubakr, "Kunjua mkono wako Ewe Abubakar," na Abubakr naye akakunjua mkono wake akambai bila ya mashauriano tena haraka haraka kwa kuchelea kutanguliwa na mwingine na kwa hakika Umar amekwisha ieleza rai hii pale aliposema:

"Tulichelea lau tutawaacha watu hawa bila ya kuipitisha baia, watambai mtu miongoni mwao baia yetu (Umar aliwachelea Maansar wasimtangulie wakambai mtu miongoni mwao), na kinachomuongezea ufafanuzi zaidi ni pale anaposema: "Basi imma tuwape Baia jambo ambalo hatulikubali na au tuwapinge patokee uharibifu."[54]

Na ili tuwe waadilifu katika maamuzi na wenye kuchunguza kwa undani, inatupasa tukiri kwamba Umar bin Al-Khatab alibadilisha mtazamo wake kuhusu baia mwishoni mwa uhai wake na hilo ni pale mtu mmoja alipomjia Umar mbele ya Abdur-Rahman bin 'Auf katika Hijja yake ya mwisho aliyohiji, yule mtu akamwambia: "Ewe Amirul-Muuminina unayo habari kuwa fulani anasema, bila shaka Umar akifa hakika nitambai fulani kwani wallahi baia ya Abubakar haikuwa isipokuwa kwa kushitukiza tu na ilitimia". Umar alikasirika na kwa ajili hii alisimama akawahutubia watu alipokuwa akirudi Madina, miongoni mwa aliyoyasema katika khutba yake ni haya yafuatayo:

"Kwa hakika nimepata habari kwamba kuna asemaye miongoni mwenu kuwa, Wallahi lau Umar atakufa nitambai fulani, basi na asijidanganye mmoja wenu kusema kuwa baia ya Abubakar ilikuwa hivyo lakini Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake.."[55] Kisha Anasema: "Yeyote mwenye kumbai mtu bila mashauriano kutoka kwa Waislamu, basi huyo asipewe baia yeye wala huyo aliyembai kuhofia asije uwawa.[56]

Basi laiti Umar angekuwa na mtazamo huu siku ya Saqifah na asiwalazimishe Waislamu kumbai Abubakr ambako kulikuwa kwa kushitukiza, na Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake kama alivyoshuhudia yeye mwenyewe, lakini imekuwaje Umari awe na rai hii mpya katika mtazamo huu mpya, hakika atakuwa amejihukumia kifo yeye mwenyewe na rafiki yake (Abubakr) kwa kuwa kwenye mtazamo wake mpya anasema: "Yeyote mwenye kumbai mtu bila ya mashauriano toka kwa Waislamu basi asipewe Baia yeye wala huyo aliyembai ili asije uwawa."

Imebakia juu yetu kufahamu ni kwa nini Umar alibadilisha maoni yake mwishoni mwa uhai wake pamoja na kwamba yeye anafahamu mno kuliko mwingine ya kuwa mtazamo wake mpya unatengua baia ya Abubakar iliyotimia bila ya mashauriano toka kwa Waislamu na ilikuwa ni baia ya kushitukiza? Pia mtazamo wake huu mpya unatengua baia yake yeye aliyopewa, kwani aliupata ukhalifa kwa tamko la Abubakar wakati wa kufa bila ya makubaliano kutoka kwa Waislamu, kiasi baadhi ya masahaba walikwenda kwa Abubakar wakamkemea kwa kuwatawalishia mtu msusuavu tena mgumu wa tabia.[57] Na Umar alipotoka ili awasomee watu maandiko ya Abubakr kuna mtu alimuuliza: "Ewe Baba Hafs kuna nini ndani ya waraka huo?" Umar akasema, Sijuwi, lakini mimi nitakuwa wa kwanza kusikiliza na kutii." yule mtu akasema: "Lakini Wallahi mimi najua kilichomo, wewe ulimtawalisha (Abubakar) kipindi cha mwanzo naye amekutawalisha kipindi hiki".

Taz: Al-Imam Was-Siyasah cha Ibnu Qutaibah Juz. 1 uk. 25Mlango unaohusu maradhi ya Abubakri na kumtawalisha kwake Umar. Kauli hii inafanana na kauli ya Imam Ali kumwambia Umar pale alipomuona anawalazimisha watu kwa nguvu wambai Abubakr akasema "Nifanye jambo ambalo wewe utakuwa na hisa (wanitaka) leo nilikazanie jambo lake ili kesho akurudishie"? Taz: Al-Imamah Was-Siyasah cha ibnu Qutaiba Juz. 1 uk. 18. Cha muhimu ni kufahamu ni kwa nini Umar alibadilisha mtazamo wake kuhusu Baia?

Mimi ninakurubia kuamini kwamba, wakati alipowasikia baadhi ya Masahaba wanataka kumbai Ali bin Abi Talib baada ya kufa Umar jambo ambalo yeye Umar kamwe hakubaliani nalo, kwa kuwa yeye ndiye aliyezipinga maagizo ya Mtume yaliyobayana, na akapinga Mtume (s.a.w.) asiwaandikie yale maandiko[58] kwa kuwa yeye alilifahamu lengo lake kiasi kwamba akamtuhumu Mtume kuwa anaweweseka na akawatisha watu wasiseme kuwa Mtume amekufa[59] yote hayo ni kwa sababu wasije wakawahi kumbai Ali. Umar alitilia mkazo baia ya Abubakr na akawalazimisha watu kwa nguvu waikubali baia hiyo na kisha kumuonya kila atayepinga kuwa atamuua[60] ili tu kumtenga mbali Ali na ukhalifa.

Hivi itawezekana Umar aridhie aseme msemaji kwamba fulani atapewa baia lau Umar atakufa? Hasa pale msemaji huyu ambaye jina lake limebakia kuwa halijulikani na hapana shaka kuwa alikuwa miongoni mwa Masahaba wakubwa? Msemaji huyu alitumia hoja ya kitendo alichokitenda Umar mwenyewe alipombai Abubakar pale anaposema: "Wallahi Baia ya Abubakr haikuwa isipokuwa ya kushitukiza na ikatimia", yaani pamoja na kuwa ilitokea kwa kuwashitukiza Waislamu na bila kupata ushauri wao lakini ilitimia na likawa jambo lililothibitika, kwa hiyo ilifaa kwa Umar kulifanya kwa Abubakr kwa nini isifae kwake kulifanya yeye mwenyewe kwa njia ile ile kwa mwingine? Na hapa tunaona kwamba ibn Abbas na Abdur-Rahman bin Auf na Umar bin Khatab wanakwepa kulitaja jina la huyu msemaji kama ambavyo wanakwepa kulitaja jina la mtu anayetaka kupewa baia msemaji huyu. Na ilipokuwa wawili hawa wanao umuhimu mkubwa kwa Waislamu, tunamuona Umar alikasirika kwa usemi huu na haraka katika Ijumaa ya kwanza aliwahutubia watu na akaieleza maudhui ya Ukhalifa itakavyokuwa baada yake na akawaonesha maoni yake mapya kuhusiana na Ukhalifa, ili azuwie njia ya huyu anayetaka kurudisha ile ghafla iliyokwisha tokea kwani njia hiyo itamnufaisha mgomvi wake, kwani kwa kupitia uchunguzi tumefahamu kuwa usemi huo haukuwa ni maoni ya fulani tu peke yake, bali ulikuwa ndiyo mtazamo wa Masahaba wengi, na ndiyo maana Bukhari anasema: "Umar alichukia na kisha akasema bila shaka apendapo Mwenyezi Mungu mimi nitasimama usiku huu miongoni mwa watu niwaonye hawa ambao wanataka kuwapora mambo yao..." [61]

Basi kubadilisha kwa Umar mtazamo wake kuhusu Baia ilikuwa ni kuwapinga hawa ambao wanataka kuwapokonya watu mambo yao na wambai Ali, na hili ni jambo ambalo Umar hakubaliani nalo kwani yeye anaitakidi kuwa Ukhalifa ni miongoni mwa mambo ya watu na siyo haki ya Ali bin abi Talib, na itikadi hii itapokuwa ni sahihi, basi ni kwa nini yeye Umar aliruhusu kuwapokonya watu mambo yao baada ya kufariki Mtume (s.a.w.) na haraka haraka akambai Abubakar bila ya makubaliano na Waislamu. Na msimamo wa Abu Hafs (Umar) dhidi ya Abul-Hasan (Ali) unaeleweka na ni mashuhuri mno, nao ni kumtenga Ali kwenye utawala kwa kutumia njia yoyote inayowezekana.

Na matokeo haya hatukuyafahamu kutokana na hotuba yake (Umar) iliyotangulia hapo kabla peke yake, lakini yeyote mwenye kufuatilia historia atafahamu kuwa Umar bin Al-Khatab alikuwa ndiye mtawala mtendaji hata katika Ukhalifa wa Abubakr na ndiyo maana tunamuona Abubakr anamuomba Usamah bin Zaid amuachie Umar bin Al-Khatab ili amsaidie kuhusu suala la Ukhalifa kama alivyoeleza hilo Ibn Saad ndani ya Tabaqat yake na pia wanahistoria wengi walioelezea jeshi la Usamah - pamoja na hayo tunamuona Ali bin Abi Talib anabakia mbali na majukumu, hawakumpa cheo chochote wala utawala wowote wala kumpa uamiri wa jeshi lolote lile na wala hawakumuamini kuwa mweka hazina na yote haya ni kwa kipindi cha Ukhalifa wa Abubakr, Umar na Uthman, nasi sote twamjua Ali bin Abi Talib ni nani.

Cha kushangaza kuliko yote haya ni kuwa, sisi tunasoma ndani ya vitabu vya historia kwamba kifo kilipomfikia Umar alisikitika kwamba lau Abu Ubaidah bin Al-Jarrah au Salim Huru wa Abu Hudhaifah wangekuwa hai angewatawalisha baada yake. Lakini hapana shaka Umar alikumbuka kuwa hapo kabla alikwisha badilisha mtazamo wake juu ya baia kama hii na akaiona kuwa ni ya kushitukiza na ni kupokonya mambo ya Waislamu, basi hapana budi kwake aweke njia mpya kuhusu baia ili kati kwa kati asije yeyote akafaulu kumbai amuonaye kuwa anafaa na kuwalazimisha watu kumfuata kama alivyofanya yeye kwa Abubakr na kama alivyofanya Abubakar kwake Umar au kama atakavyofanya fulani ambaye anangoja kufa kwa Umar ili ambai jamaa yake.Basi hili haliwezekani baada ya Umar kuwa ameuhukumia Ukhalifa kuwa ni jambo lililofanyika ghafla na kuwa linataka kuwa ni jambo la kupora, na haiwezekani pia kwake kuliacha jambo hili liwe la makubaliano baina ya Waislamu. Na ule mkutano wa Saqifah uliofuatia kufariki kwa Mtume (s.a.w.) yeye Umar alihudhuria na akajionea mwenyewe hitilafu iliyotokea ambayo karibu zitoke roho za watu na damu imwagike.

Basi baadaye alitoa fikra ya watu wa mashauriano au (tuseme) watu sita ambao peke yao ndiyo wenye haki ya kumchagua Khalifa na Muislamu mwingine yeyote hana haki ya kushirikiana nao katika jambo hilo, na Umar alikuwa akitambua kwamba tofauti baina ya watu hawa sita haiwezi kuepukwa, ndiyo maana aliusia ikiwa watatofautiana basi wawe kwenye upande alioko Abdur-Rahman bin Auf hata kama itapelekea kuwauwa watu watatu ambao watamkhalifu Abdur-Rahman bin Auf wakati watakapogawika watu hawa sita makundi mawili, na hilo ni muhali kwani Umar anafahamu kwamba Saad bin Abi Waqas ambaye ni ibn Ammi ya Abdur-Rahman bin Auf na wawili hawa ni ukoo wa Bani Zuhrah, na alifahamu pia kwamba Saad hampendi Ali na moyoni mwake kulikuwa na chuki kwani Ali ndiye aliyewauwa wajomba zake wa ukoo wa Abdis-Shams, kama ambavyo Umar alikuwa akifahamu kwamba Abdur-Rahman bin Auf ni shemeji wa Uthman kwani mkewe aliyekuwa akiitwa Ummu Kul-thum ni dada wa Uthman. Si hivyo tu kadhalika alifahamu kuwa Tal-hah akimpenda Uthman kutokana na mahusiano yaliyokuwepo baina yao kufuatana na maelezo ya baadhi ya wapokezi wa khabari, na hakika ilitosha kwa Tal-hah kumpenda Uthman kutokana na kumpinga kwake Ali kwani yeye Tal-hah ni katika ukoo wa Bani Taym, na kulikuwa na chuki fulani baina ya Bani Hashim na Bani Taym kutokana na Ukhalifa wa Abubakar.

Taz: Shark Najul-Balaghah ya Muhammad Abdoh, Juz. 1 uk. 88.

Umar alikuwa akiyajuwa yote hayo na kwa ajili hii ndiyo maana akawachagua hawa peke yao. Umar aliwachagua hawa watu sita na wote wakiwa ni Maquraish na wote ni kutoka katika Muhajirina na hakuna yeyote kati yao ambaye ni kutoka miongoni mwa Ansar na wote hawa kila mmoja wao akiwakilisha na kuongoza kabila lenye umuhimu wake na athari yake.

1. Ali bin Abi Talib, kiongozi wa Bani Hashim.

2. Uthman bin Affan kiongozi wa Bani Umayyah

3. Abdur-Rahman bin Auf, kiongozi wa Bani Zuhrah

4. Saad bin Abi Waqqas, yeye ni kutoka katika Bani Zuhrah na wajomba zake ni Bani Umayyah.

5. Tal-ha bin Ubaidullah, Bwana wa Bani Taym.

6. Zubair bin Al-Awwan, yeye ni mtoto wa Safiyyah ambaye ni shangazi yake Mtume na ni mume wa As-maa binti Abubakr.

Basi hawa ndiyo wenye kutoa maamuzi, na hukmu yao ikubaliwe na Waislam wote, sawa sawa wakiwa ni wakaazi wa Madina (Makao Makuu ya Ukhalifa) au wengineo katika ulimwengu wote wa Kiislamu na ni wajibu wa Waislamu yeyote atakayetoka miongoni mwao akawa kinyume cha maamuzi yao basi damu yake imwagwe (auawe). Na hili ndilo jambo pekee tulilokuwa tunataka kulisogeza katika akili ya msomaji kuhusiana na kunyamaziwa kwa tamko la Ghadir katika maelezo yaliyotangulia.

Na ikiwa Umar anaufahamu undani, mapenzi na mtazamo wa watu hawa sita, basi bila shaka yeye alikuwa kisha mpendekeza Uthman bin Affan kuwa Khalifah au alikuwa anajua kuwa wengi miongoni mwa hawa sita hawamkubali Ali, vinginevyo ni kwa nini na ni kwa haki gani Umar anatilia nguvu upande wa Abdur-Rahman bin Auf dhidi ya Ali bin Abi Talib wakati ambapo Waislamu tangu hapo zamani na mpaka leo wamekuwa wakishindana juu ya ubora wa Ali na Abubakar na hatujamsikia yeyote akimlinganisha Ali na Abdur-Rahman bin Auf.

Na hapa hapana budi nisimame kidogo ili niwaulize Masunni ambao wanatetea msingi wa mashauriano na pia (niwaulize) watu wenye fikra iliyohuru wote kwa ujumla, nawauliza wote hawa, ni vipi mnaafiki baina ya mashauriano kwa maana yake ya Kiislamu na baina ya fikra hii ambayo kama itajulisha kitu fulani basi haitajulisha isipokuwa ni maoni ya ki-dikteta, kwani yeye Umar ndiye aliyewachagua watu hawa sita na siyo Waislamu, na iwapo kuufikia kwake Ukhalifa lilikuwa ni jambo la ghafla, basi ni kwa haki ipi anawalazimisha Waislamu wakubali mmoja wa hawa sita?

Kinachojitokeza kwetu ni kwamba Umar anauona Ukhalifa kuwa ni haki ya Muhajirina peke yao na mwingine yeyote hana haki ya kuwakorofisha kwenye jambo hili, bali zaidi ya hivi ni kuwa Umar anaitakidi kama anavyoitakidi Abubakar kwamba Ukhalifa ni milki ya Maquraish, bali wamo pia wasiokuwa Waarabu, hivyo basi haistahiki kwa Sal-man Al-Farisi wala Ammar bin Yasir wala Bilal wa Uhabeshi wala Suhayb Mrumi, wala Abu Dharri Al-Ghifari wala maelfu ya Masahaba ambao siyo Maquraish (haistahiki kwao) kujitokeza kwa ajili ya Ukhalifa. Na haya siyo madai ya hivi hivi tu sivyo kabisa, bali hiyo ndiyo itikadi yao ambayo historia na wataalamu wa hadithi wameisajili kutoka vinywani mwao (kina Abubakar na Umar) na hebu tuirudie khutba yenyewe ambayo Bukhari na Muslim wameieleza ndani ya Sahih zao:

Umar bin Al-Khatab anasema:

"Nilitaka kusema, na nilikuwa nimetunga vizuri usemi ambao ulinifurahisha nikitaka niutamke mbele ya Abubakr na nilikuwa nikimzunguka karibu. Basi nilipotaka kusema Abubakr akasema, tulia (ewe Umar), na sikupenda kumkasirisha. Abubakar akazungumza, na alikuwa mpole mno kuliko mimi na mtulivu mno, Wallahi hakuacha neno lolote katika maneno nilioyaandaa isipokuwa aliyasema vizuri zaidi mpaka aliponyamaza kisha akasema, nilichokieleza kwenu katika wema ninyi ndiyo mnaostahiki (akiwaambia Maansari) na wala jambo hili halitatambulika isipokuwa kwa upande huu wa Maquraish. Taz: Sahih Bukhar Babul-Wasiyyah.

Kwa hiyo inatubainikia wazi- kwamba Abubakr na Umar hawaamini mashauriano na hiyari, na baadhi ya wanahistoria wanasema kwamba Abubakar alitoa hoja dhidi ya Maansar kwa hadithi ya Mtume (s.a.w.) isemayo kuwa "Ukhalifa uko kwa Maquraish" Na hadithi hiyo hapana shaka ni sahihi (kama walivyoitaja Bukhar na Muslim na Sahih zote kwa Masunni na Mashia) Mtume (s.a.w.) amesema: "Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili na wote ni kutoka kwa Maquraishi" na hadithi iliyo wazi zaidi kuliko hii ni ile kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema:

"Jambo hili (la Ukhalifa) halitakoma kwa Maquraish muda wote hata wakibakia watu wawili"[62] pia kauli yake isemayo "Watu ni wafuasi wa Maquraishi katika kheri na shari[63].

Basi ikiwa Waislamu wote wanaziamini hadithi hizi, ni vipi mtu aseme kuwa Mtume aliliwacha suala la Ukhalifa liwe la mashauriano baina ya Waislamu wamchague wamtakaye? Na haiwezekani kwetu sisi kukwepa kupingana huku, isipokuwa tutakapoyachukua maneno ya Maimamu wa nyumba ya Mtume na wafuasi wao na baadhi ya wanachuoni wa Kisunni ambao wanasisitiza kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwataja Makhalifa na akawabainisha kwa idadi yao na majina yao, na hapo ndipo utakapoweza pia kuufahamu msimamo wa Umar na kuuthibiti Ukhalifa kwa Maquraish na huyu Umar ni mtu aliyefahamika kwa Ijtihadi yake dhidi ya maagizo ya Mtume hata katika uhai wake mwenyewe Mtume (s.a.w.), kwani matukio ya Sul-hu ya Hudaybiyah[64] kuwasalia wanafiki,[65] msiba wa siku ya Al-Khamis,[66] na kuzuwiya kwake kubashiria watu pepo[67] ni ushahidi mkubwa wa haya tuyasemayo.

Basi haishangazi kwa Umar kufanya Ij-tihad baada ya kufariki Mtume dhidi ya hadithi inayohusu Ukhalifa, haoni ulazima wa kukubali agizo linalomuhusu Ali bin Abi Talib ambaye ni Quraish, mdogo kwa umri. Ni yeye aliyeidhibiti haki ya kumchagua Khalifa kwa Maquraish peke yao, na ni yeye ambaye alilazimisha peke yake kuchagua watu sita miongoni mwa watukufu wa Kiquraishi kabla hajafa ili ikubaliane kati ya hadithi ya Mtume (s.a.w.) na vile aonavyo yeye juu ya haki ya Maquraishi peke yao kuhusika na Ukhalifa. Huenda kumuingiza Ali katika kundi hilo hali yakuwa akifahamu kwamba wao hawatamchagua, ni udhibiti wake kwa Umma ili amlazimishe Ali kuingia pamoja nao ndani ya mchezo wa Kisiasa kama wanavyouita leo hii na ili pasibakie kwa Ali na wafuasi wake na wapenzi wake ambao walikuwa wakidai kuwa yeye ndiye wa mwanzo (pasibakie kwao) hoja yeyote. Lakini Imam Ali aliyazungumza yote hayo katika hotuba yake mbele ya watu wote akasema kuhusu jambo hilo:

"Nilivumilia muda wote wa taabu na majaribu mpaka alivyoondoka akauweka (Ukhalifa) chini ya maamuzi ya kikundi cha watu sita akidhania kuwa mimi nafanana nao oh! hayawi sawa ya Mungu na mashauriano! Toka lini nikatiliwa mashaka na wa kwanza miongoni mwao mpaka imebidi nilinganishwe na watu kama hawa! lakini nilitua walipotua na niliruka waliporuka (yaani, niliishi nao kwa hekima).

Nne: Hakika Imam Ali (a.s.) alitoa hoja dhidi yao kwa kila namna lakini bila mafanikio, na je, Imam Ali aombe baia ya watu ambao walimgeuzia nyuso zao na nyoyo zao zikawaelekea wengine imma kwa husuda dhidi yake kutokana na yale aliyompa Mwenyezi Mungu miongoni mwa fadhila zake, na imma kwa chuki dhidi yake kwani yeye ndiye aliyewaua mabwana zao, akawabomoa mashujaa wao, akawakatisha tamaa, akawadhalilisha na kuvunja ujeuri wao kwa upanga wake na ushujaa wake mpaka wakasilimu na kujisalimisha hali ya kuwa Imam Ali akiwa ni Mtukufu akimtetea mwana wa ammi yake (Mtume s.a.w.) na alipokuwa akifanya hayo haikumzuwia kuyatenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lawama ya mwenye kulaumu na wala hakurudi nyuma kwenye azma yake kutokana na tamaa ya dunia. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) naye alikuwa akiyajua vema hayo na kila tukio alikuwa akitilia mkazo fadhaila za nduguye na mwana wa ammi yake ili kuwafanya wampende. Mtume alikuwa akisema "Kumpenda Ali ni (dalili ya) imani na kumchukia (ni dalili ya) unafiki"[68] Na pia husema "Ali anatokana nami, nami natokana na Ali."[69] Na alikuwa akisema: "Ali ni mtawala wa kila muumini baada yangu"[70] na husema kuwa, "Ali ni mlango wa mji wa elimu yangu na ni baba wa wanangu."[71] Pia Mtume alikuwa akisema, "Ali ni Bwana wa Waislamu na ni Imamu wa wachamungu na ni kiongozi wa waumini wenye kutowa mwanga na nuru."[72]

Lakini inasikitisha kwamba yote hayo hayakuwazidishia isipokuwa chuki na husuda na kwa ajili hiyo Mtume alimuita Ali kabla ya kufariki akamkumbatia kisha akalia na akamwambia: "Ewe Ali bila shaka mimi nafahamu kwamba ndani ya nyoyo za jamaa hawa kuna shinikizo la chuki dhidi yako, na hapo baadaye watakudhihirishia baada yangu mimi, iwapo watakupa baia kubali vinginevyo basi subiri mpaka hapo utapokutana nami hali ya kuwa mwenye kudhulumiwa". Taz: Ar-Riyadun-Naz-Rah Fi Manaqibil-Asharah cha Tabari Babu Fadail Ali ibn Abi Talib. Basi ikiwa Abul-Hasan (a.s.) ilimlazimu kuvumilia baada ya baia ya Abubakr, hilo ni kutokana na usia wa Mtume kwake yeye na ndani ya hilo muna hekima ambayo iko wazi.

Tano: Zaidi ya yote hayo yaliyotangulia ni kwamba, Muislamu ataposoma Qur'an Tukufu na kuzizingatia aya zake, atafahamu kwa kupitia masimulizi yake kuhusu mambo ambayo yaliwafika watu na mataifa yaliyopita kwamba, kwao yalitokea mengi kuliko yale yaliyotokea kwetu sisi. Basi mwangalie huyu Qabil anamuuwa nduguye Habil kwa dhulma na uadui tu, na huyu hapa Nuh ambaye ni babu wa Manabii, baada ya miaka elfu moja ya jihadi hakuna aliyemfuata katika watu wake isipokuwa wachache tu, isitoshe mkewe na mwanawe walikuwa miongoni mwa makafiri.

Mtazame Nabii Lut haikupatikana katika kitongoji chake isipokuwa nyumba moja tu ya Waumini. Nao Mafirauni ambao walikuwa wenye kiburi katika nchi wakawafanya watu kuwa watumwa, hapakuwepo miongoni mwao isipokuwa Muumini mmoja anayeficha imani yake. Hawa hapa nduguze Yusuf watoto wa Yaaqub nao ni kikundi, wanakula njama kumuuwa ndugu yao mdogo asiye na kosa lolote lakini (wanafanya hivyo) kwa kumhusudu kwa kuwa yeye ni kipenzi kwa baba yao. Watazame wana wa Israel ambao Mwenyezi Mungu aliwaokoa kupitia kwa Musa na akawapasulia bahari na kumuangamiza adui yao Firauni na askari wake bila ya kuwakalifisha taabu yoyote ya vita, basi mara walipotoka baharini na nyayo zao hata hazijakauka, wakawafikia watu wanaoabudia sanamu (wana wa Israel) wakasema:

"Ewe Musa tutengenezee Mungu kama wao walivyo na Miungu, Musa akawaambia hakika ninyi ni watu msiojua." Na alipokwenda kwenye ahadi ya Mola wake na kumuacha nduguye Harun, walifanya njama dhidi yake karibu wamuuwe, wakamkufuru Mwenyezi Mungu, na wakamuabudia ndama kisha baadaye waliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema: "Kila walipokufikieni Mitume kwa yale ambayo nafsi zenu haziyapendi mlijivuna, kundi moja mlilipinga na kundi jingine mkaliua".(Qur'an, 2:87)

Huyu hapa naye Bwana wetu Yahya bin Zakariya naye ni Nabii na Mtawa miongoni mwa watu wema anauwawa na kichwa chake anazawadiwa mtu muovu miongoni mwa waovu wa Kibani Israel. Mayahudi na Wakristo nao walikula njama kumuua na kumsulubu bwana wetu Isa. Nao ummati wa Muhammad wanaandaa jeshi la kiasi ya watu elfu thelathini ili kumuuwa kipenzi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu na Bwana wa vijana wa peponi ambaye hawakuwa pamoja naye isipokuwa watu Sabini miongoni mwa wafuasi wake, wakawauwa wote ikiwa ni pamoja na mwanawe mchanga. La ajabu ni lipi baada ya yote haya? Lipi litashangaza baada ya kauli ya Mtume kuwaambia Masahaba wake yakuwa: "Mutafuata nyendo za wale waliokuwa kabla yenu shubiri baada ya shubiri na dhiraa baada ya dhiraa mpaka hata wakiingia kwenye shimo la kenge nanyi mutaingia". wakasema, "Wadhani kuwa hao ni Mayahudi na Wakristo"? Mtume akasema, "Ni kina nani basi (kama si hao)"?

Taz: Sahih BukharJuz. 4 uk. 144 na Juz. 8 uk. 151. Ni kipi cha ajabu basi, nasi twasoma ndani ya Bukhar na Muslim kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo: "Siku ya Kiyama Masahaba wangu watapelekwa upande wa kushoto nami nitasema wanapelekwa wapi? Patasemwa Wallahi Motoni, nitasema, Ewe Mola wangu Masahaba wangu hao, patasemwa, Hakika wewe hujuwi waliyoyazusha baada yako, nitasema atengwe mbali aliyebadilisha baada yangu, na sitamuona anaokoka miongoni mwao isipokuwa kikundi kidogo kama cha ngamia waliotelekezwa".

Tax: Sahih Bukhar Juz. 7 uk. 209 na Sahih Muslim Babul-Haudh. Basi lipi la ajabu baada ya kauli yake Mtume (s.a.w.) aliposema: "Umati wangu utagawanyika makundi sabini na tatu na yote yataingia motoni isipokuwa kundi moja". Taz: Sunan Ibn Majah Kitabul-Fitan Juz. 2 hadith Na. 3993, Ahmad Juz. 3 uk. 120, Sunan Tirmidhi Kitabul-Iman. Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola mwenye nguvu na Utukufu, mjuzi wa undani wa nyoyo pale aliposema: "Na watu wengi hawataamini japo utapupia" (Qur'an, 12:103)

"Bali amewajia na ukweli na wengi wao wanaichukia kweli" (Qur'an,23:70)

"Bila shaka tumekujieni na ukweli lakini wengi wenu hawaupendi ukweli" (Qur'an 43:78)

"Fahamuni ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli lakini wengi wao hawafahamu" (Qur'an, 10:55)

"Wanakuridhisheni kwa vinywa vyao na nyoyo zao zinakataa, na wengi wao ni mafasiki (Qur'an, 9:8)

"Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru" (Qur'an, 10:60)

"Wanaitambua Neema ya Mwenyezi Mungu kisha wanaipinga na wengi wanakataa ila kukufuru tu" (Qur'an, 25:50)

"Na wengi wao hawawezi kumuamini Mwenyezi Mungu ila hali ya kuwa wanamshirikisha" (Qur'an, 12:106)

"Bali wengi wao hawaijuwi haki basi wao wanapinga" (Qur'an, 21:24)

"Hivi mwashangazwa na mazungumzo haya na mnacheka wala hamlii hali ya kuwa ninyi mmeghafilika (mmejisahau)" (Qur'an, 53:61

5

6

7

8

9

10

11