HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)0%

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S) Mwandishi:
Kundi: Vitabu mbali mbali

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

Mwandishi: ASIYEJULIKANA
Kundi:

Matembeleo: 34998
Pakua: 2999

Maelezo zaidi:

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 12 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 34998 / Pakua: 2999
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

Mwandishi:
Swahili

4

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W) PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

USAFI KATIKA ISLAM

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Amesema Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :

"Kuna mema matatu ambayo Allah swt huyapenda katika watu: Ufupi katika uzungumzaji, usingizi mfupi, na ulaji mdogo; Na mambo matatu ambayo hayamfurahishi Allah swt: Kuzungumza kupita kiasi Kulala kupita kiasi, na Kula kupita kiasi"

Al-Ithna- 'Asheriyyah, Uk. 92.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema:

"Jaribuni kuwa wasafi kila muwezavyo Kwa hakika Allah swt ameweka misingi ya Islam juu ya usafi; hivyo kamwe mtu mchafu hawezi kuingia Jannat mpaka awe msafi"

Kanz-ul- 'Ummal, Hadithi no. 26002.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam Amiril Muuminin 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Amesema:

"Kula kupita kiasi kunasababisha wingi wa magonjwa"

Ghurar-ul-Hikam, Uk. 356.

AL IMAM MUSA AL-KADHIM (A.S)

Amesema Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) :

"Zipo Sunnah tano kuhusu kichwa na tano zingine kuhusu mwili. Sunnah tano zinazohusiana na kichwa ni: Kuosha mdomo, kunyoa mashurubu, kuchana nywele, kupitisha maji kupita mdomo na pua.

Sunnah tano zinazohusiana na mwili ni: Kukaa jando, kunyoa nywele za sehemu za siri, kunyoa nywele kwenye mabega, kupunguza na kukata makucha, na kusafisha na kuosha sehemu za siri (kwa maji au kwa karatasi, kwa kitambaa, au chochote kile kinachoweza kukufaa n.k"

Khisal-i-Sadduq, Uk. 125

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB(A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alimwambia Al Imam Hasan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) :

"Je nikufundishe mema manne ambayo hautahitaji dawa ya matibabu ya aina yoyote ? "Naam" alijibu Al Imam Hasan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. Kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimjibu: Usikae kula chakula hadi uwe una njaa; Na usiondoke juu ya meza ya chakula bila ya kubakiza njaa kidogo; Tafuna chakula chako vyema mdomoni mwako; Na unapotaka kwenda kulala, uende ukajisaidie haja. Iwapo utatekeleza haya basi kamwe hautahitaji matibabu ya aina yoyote"

Wasa'il ush-Shi'ah, J. 24, Uk. 245.

BIASHARA NA UHUSIANO WA KIJAMII

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema:

"Iwapo mtu atanunua mali ambayo katika vyakula ambacho ni muhimu katika jamii na akakificha kwa siku arobaini kwa matumaini kuwa bei yake itapanda miongoni mwa Waislam, na kama atafanikiwa kukiuza kwa bei ya juu hicho chakula basi kama fedha zote atazigawa katika sadaka kwa na wenye kuhitaji misaada maskini, basi hiyo haitapunguza adhabu yoyote mbele ya Allah swt kwa kile alicho kitenda (kuhujumu uchumi)"

Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 89.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Yeyote yule anayefanya biashara bila ya kuzingatia sheria na kanuni za Islam, basi kwa hakika ataingia katika riba, (bila ya yeyemwenyewe kujijua"

Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 93.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ananakili kutoka Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) kuwa Amesema:

"Yeyote yule aliye katika biashara na anayenunua na kuuza vitu lazima ajiepushe mambo matano, ama sivyo asinunue wala asiuze kitu chochote: Riba, Kula kiapo, Kuficha ubaya na kasoro za mali, Kusifu kitu kama hakistahili hivyo wakati wa kuuza; na kutafuta kasoro au ubaya wakati wa kununua"

Khisal-i-Sadduq, J. 1, Uk. 286.

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) Amesema:

"Yeyote yule anayetafuta riziki humu duniani ili aondokane na shida za kutegemea watu katika mahitaji yake, na ili kuwalisha na kuwasaidia wananyumba wake, na kueneza mapenzi yake kwa majirani zake basi atakutana na Allah swt siku ya Qiyamah huku uso wake ukiwa uking'ara kama mwezi"

Al-Kafi, J. 5,Uk.78.

KUGHUSHI KATIKA BIASHARA

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Yeyote yule anaye lala huku akiwa amepanga njama dhidi ya Muislam mwenzake moyoni mwake, basi amelala katika adhabu za Allah swt, na atabakia katika hali hiyo hadi pale afanye Tawba"

Safinat-ul- Bihar, J. 2, Uk. 318.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema:

"Na yeyote yule anayemlaghai ndugu yake Mwislam, basi Allah swt humwondoshea riziki kwa wingi na huharibu maisha yake na kumwachia katika hali yake mwenyewe"

Wasa'il ush- Shi'ah, J. 17, Uk. 283.

IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) :

"Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ameharamisha kuchanganywa kwa maji katika maziwa wakati wa kuuza"

At-Tahdhib, J. 7, Uk. 13.

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) Amesema,

"Yeyote yule anayewaghushi Waislam kwa ujumla basi huyo hayupo nasi"

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Mtu yeyote anaye walaghai Waislam wenzake katika kununua au kuuza kitu chochote, hayupo miongoni mwetu, na siku ya Qiyamah atainuliwa akiwa miongoni mwa Wayahudi, kwa sababu wao wamekuwa daima wakiwadanganya na kuwaghushia Waislam"

Bihar al- Anwaar, J. 103, Uk. 80.

MATAMANIO NA TAMAA ZISIZO HALALI

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Baada yangu mimi, ninawahofia umma wangu katika vitu vitatu: Upotofu baada ya kuelimika, matamanio yanayo potosha na Tamaa ya tumbo na sehemu za siri"

Al-Kafi, J. 2, Uk. 79.

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

"Hakuna 'ibada ya Allah swt iliyo na thamani zaidi kuliko usafi, uhalisi wa tumbo la mtu na sehemu zake za siri kutokana na matamanio au tamaa."

Al-Kafi, J. 2, Uk. 80.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Amesema:

"Kwa mtu ambaye anakuwa na matamanio na maovu yanapokuwa daima yako tayari na yeye anayaepukana nayo kwa sababu ya hofu ya Allah swt, basi Allah swt atamharamishia moto wa Jahannam na atamhakikishia kuwa hatakuwa na tishio kubwa"

Makarim-ul- Akhlaq, 429.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Yeyote yule anayejinusuru na maovu ya tumbo, ulimi, na sehemu zake za siri basi kwa hakika amejinusuru kutoka madhambi"

Al-Muhajjat-ul-Baidha.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema: "Kumbuka (wakati wa kutenda dhambi),kuwa raha zinapotea wakati matokeo (yatakayotokea) yake yanabakia."

Nahjul Balagha U. 553.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Yeyote yule anayembusu kijana wa kiume kwa matamanio ya kitamaa, basi Allah swt atamadhidhibisha na kumchapa kwa miale ya moto"

Al-Kafi, J. 5, Uk. 548.

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

"Je kuna jitihada gani iliyo afadhali kuliko usahihi wa tumbo na wa sehemu za siri"

Al-Kafi, J. 2, Uk. 79.

MALI YA DUNIA NA ULIMBIKIZAJI KWA UROHO

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Kwa yeyote yule ambaye siku zake mbili za maisha yakawa sawa (hakuna maendeleo ya kiroho) kwa hakika yupo katika hasara"

Bihar al- Anwaar, J. 71, Uk. 173.

AL IMAM MUSA AL-KADHIM (A.S)

Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) amesema:

"Mfano wa dunia hii ni sawa na maji ya bahari. Kiasi chochote yule anywacho mwenye kiu kutoka bahari, kiu chake kitaendelea kuongezeka hadi kinawez kumuua."

Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 311.

AL IMAM MUHAMMAD AT-TAQI (A.S)

Al Imam Muhammad at-Taqi(a.s) amesema:

"Watu wanaheshimiwa humu duniani kwa kuwa na mali na Akhera watu wataheshimiwa kwa kuwa na matendo mema."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA(S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Makusanyo ya Waram: "Maangamizo ya wanawake wangu yako katika mambo mawili: Dhahabu na mavazi yasiyo ya heshima; Na maangamizo ya wanaume wafuasi wangu yapo katika kuiacha elimu na kukusanya na kulimbikiza mali"

Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 368.

DUNIA INAYO HADAA, MAVUTIO NA SUMU YAKE

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Wakati Jeneza maiti ya mtu inapoinuliwa na kuchukuliwa kwenda kuzikwa, basi Ruh yake inaifuata maiti na katika hali ya masikitiko makubwa inasema: 'Enyi watoto na Jama'a zangu ! Jitahadharisheni sana kuwa ulimwengu huu hauwahadai nyie kama mulivyonifanyia mimi. Mimi nimekusanya mali yote hii bila ya kujali uhalali au uharamu wake na nimeiacha nyuma huku kwa ajili ya wengine. Sasa mimi nimeondoka na mzigo juu yangu (kwa sababu ya kutenda kila aina ya madhambi ya uhalali na uharamu) wakati matunda yake wanafaidi watu wangineo; kwa hivyo, mujiepushe na hayo ambayo sawa na yaliyo nifika mimi"

Bihar al- Anwaar, J. 6, Uk. 161.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Iwapo huyu mtu angeweza kuiona mauti yake na kasi yake inavyo mwelekea yeye basi kwa hakika angechukia na kuiacha dunia na matumaini yake yote"

Bihar al-Anwaar, J. 73, Uk. 166l.

AL IMAM MUSA AL-KADHIM (A.S)

Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) amesema:

"Mfano wa dunia ni kama nyoka ambaye ngozi yake ya nje ni laini na nyororo kwa kugusa wakati kuna sumu kali mno inayoua ndani mwake. Aliye na hekima wanajaribu kujiepusha nayo (lakini watoto wasio na fahamu kamili) wanapendezewa na kuvutiwa nayo na wanatamani kugusa na kucheza kwa mikono yao"

Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 311.

Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) :

"Mapenzi ya dunia hii itakayo angamia ndiyo chanzo cha maovu yote"

Al-Kafi, J. 2,Uk. 315.

WATUMWA WAPUUZAJI WA DUNIA HII INAYO HADAA

IMAM HUSSEIN IBN 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Amesema Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) :

"Kwa hakika, watu ni watumwa wa dunia na imani yao haina misingi yoyote, ipo katika ndimi zao tu. Wao wanaitilia maanani ili mradi wanapata mahitaji yao wanayoyahitaji, lakini pale wanapojaribiwa, basi idadi ya waumini halisi inakwenda ikipungua"

Tuhaful-'Uqul na Bihar al-Anwaar, J. 44, Uk. 374.

Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mimi nastaajabishwa kuhusu yule mtu ambaye yuko mashughuli kwa ajili ya kula tu lakini hafikirii kwa ajili ya chakula cha akili yake. Hivyo yeye anajiepusha na kile kinachomdhuru tumboni mwake na papo hapo anaiachia akili yake ijae kwa yale yanayoangamiza"

Safinat-ul-Bihar, J. 2, Uk. 84.

ULAFI NA MATUMAINI YA KIPUUZI

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Ingawaje uchoyo, uoga na uroho ni vitu vyenye sifa tofauti, lakini vyote viko sawa katika mambo ya kufikiria kwao kuhusu Allah swt"

Nahjul Balagha Barua no. 52.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Iwapo mwanaadamu atakuwa na mabonde mawili ambamo kumejazwa dhahabu na fedha, basi yeye hatatosheka nayo bali atakwenda kuitafuta ya tatu"

Man la Yahdharul Faqih, J. 4, Uk. 418.

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Yeyote yule anaye uendekeza moyo wake kwa dunia hii basi atapatwa na hali tatu: Mateso yasiyoisha, kiu ya matamanio isiyoisha na matumaini yasiyo timika"

Al-Usul-i- Kafi, J. 2, Uk. 320.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Wako kiasi gani cha watu ambao ni waovu na siku zao ziko zinahesabika lakini bado wanaendelea kwa juhudi zao zote za kuitafuta hii dunia"

Ghurar-ul-Hikam, Uk. 240.

MAJIVUNO NA KIBURI

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Msiwe wakaidi (na msing'ang'anie kufuata vile mfikiriavyo nyie wenyewe), kwa sababu watu kama hawa hukumbana na maangamizo"

Tasnif-i-Ghurar-ul- Hikam,Uk. 443.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Yeyote yule ajionaye kuwa yeye ndiye mkubwa kabisa (hana mfano mwingine) basi si kitu chochote kile mbele ya Allah swt."

Tasnif-i-Ghurar-ul- Hikam,Uk. 308 na Bihar al-Anwaar, J. 6, Uk. 91.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mambo mawili yanasababisha watu kuangamia (na kutumbukizwa katika Jahannam): Kuogopa umaskini, na Kutaka ukubwa kwa kupitia majivuno"

Bihar al-Anwaar, J. 72, Uk. 39

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mjiepushe na kujifakharisha wenyewe, kwa kutegemea yale muyaonayo mazuri ndani mwenu na kwa kupenda kuzidishiwa sifa kwa sababu hayo ndiyo majukumu makubwa yakutegemewa na Shaytani"

Ghurar-ul-Hikam, Uk. 298.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Yeyote yule aliye na kiburi hata kidogo moyoni mwake basi hataruhusiwa kuingia Jannat"

Al-Kafi, J. 2, Uk. 310.

KUBANA MATUMIZI

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Yeyote yule anaye panga matumizi yake basi kamwa hatakuwa fakiri"

Bihar al-Anwaar, J. 71 Uk. 346.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Sera bora kabisa ni katika kutekeleza ukarimu"

Ghurar-ul-Hikam,Uk.182.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Matumizi ya kupita kiasi cha kile kinachohitajika, ni ufujaji"

Mustadrak-ul-Wasa'il, J. 15, Uk. 271.

AL IMAM MUSA AL-KADHIM (A.S)

Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) amesema:

"Lau watu wangekuwa na tabia ya kula kwa kiasi, basi miili yao ingekuwa na nguvu"

Bihar al-Anwaar, J. 66, Uk. 334.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Hakuna m tu anayepita makaburini isipokuwa waliokufa wanamwambia: 'Ewe uliye ghafilika! Je unaelewa yale tulivyoeleweshwa sisi, itakufanya wewe damu yako ipoozwe"

Irshad-ul- Qulub.

USHAURIANO

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Hakuna mtu anayepita makaburini isipokuwa waliokufa wanamwambia: 'Ewe uliye ghafilika! Je unaelewa yale tulivyoeleweshwa sisi, itakufanya wewe damu yako ipoozwe'"

Irshad-ul- Qulub.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Iwapo watawala wenu ni watenda wema, na matajiri ni wale wenye kukushukuruni, na mambo yenu yanakwenda kwa ushauriano miongoni mwenu, basi kwenu nyinyi kuishi duniani ni vyema kuliko chini yake. Lakini iwapo watawala wenu ni waovu kwenu nyie, na matajiri ni mabakhili miongoni mwenu, na mambo yenu yanakwenda bila kushauriana, kwa hivyo kwenu nyie kutakuwa afadhali kuwa ndani ya ardhi kuliko kuishi juu yake"

Manhaj-us-Sadiqiin,Tafsiri, J. 2, Uk. 373.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Yeyote yule anayeshauriana pamoja na wenye busara na akili, kwa ajili ya kupata mwangaza ili aweze kupata mwanga katika masuala yake (na ataweza kuona sahihi kile kilicho sawa kutoka na kile kilicho potofu"

Ghurar-ul-Hikam, Uk. 336.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Yeyote yule anayeshauriana pamoja na watu wa maelewano, basi huonyesha maendeleo yake"

Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 105.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema;

"Hakuna muumin atakaye kuwa mwovu kwa ushauriano, na wala hakuna atakayefaidika kwa ukaidi wake"

Nahaj-ul-Falsafa, Uk. 533.

KUFANYA KAZI NA KUKAA BURE

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Ibada imegawanyika katika matawi sabini, na bora ni kule mtu kujitafutia riziki halali"

At-Tahdhib, J. 6, Uk. 324.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Kamwe, Kamwe hakutapatikana raha na starehe za maisha kwa kubakia bila kazi au kuwa mvivu"

Ghurar-ul-Hikam Uk. 197.

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

"Jiepusheni uvivu na kutokuridhika, Na haya mawili ndio ufunguo wa kila aina ya maovu"

Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 175.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliambiwa na Sa'ad Ansari kuwa mikono yake imekufa ganzi au imekuwa ngozi ngumu ni kwa sababu ya kufanya kazi kwa kutumia kamba na koleo kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kutumia yeye, mke na watoto wake. Kwa kusikia hayo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliibusu mikono yake (akionyesha heshima) na akasema:

"Kwa hakika huu ndio mkono ambao moto wa Jahannam kamwe hautaugusa"

Usd-ul-Ghabah, J. 2, Uk. 269.

SHAHIDI NA SHAHADA

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Kuna jema kwa kila jema hadi wakati mtu anapouawa katika njia ya Allah swt na zaidi ya hapo hakuna tena jema lingine juu yake. (Kupigana dhidi ya maadui Waislam ambao wanawaua Waislam"

Bihar al-Anwaar, J. 10, Uk. 100.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Yeyote yule anayeuawa katika njia ya Allah swt kama shahidi, basi yeye kamwe hataulizwa chochote kuhusu madhambi yake. (Madhambi yake yote yatakuwa yamesamehewa kwa ujumla"

Furu'i al-Kafi, J. 5, Uk. 54.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"kwa kiapo cha yule ambaye maisha na roho yangu iko mikononi mwake, iwapo viumbe vyote vya duniani na angani vikijumuika pamoja kumuua muumin ambaye hana kosa hata moja au watakapo shawishiwa kufanya hivyo, basi Allah swt atawatia wote kwa pamoja katika moto wa Jahannam"

Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 149.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Hakuna tone ambalo linalopendwa na Allah swt kuliko tone la damu ya yule, linalomwagika akiwa anakuwa shahidi katika njia ya Allah swt"

Wasa'il ush-Shi'ah, J. 15, Uk. 14

MTARAJIWA AL-MAHDII A.S. NA UTAWALA WAKE WA HAKI

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Al Mahdi anatokana na kizazi changu kutokea kwa wana wa Fatma Bi Zahra(a.s) "

Sunan Abi Daud, J. 4, Uk. 107.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema kuwa:

"Mwenye furaha ni yule ambaye ataweza kumfikia Al-Qaim(a.s) wa Ahlul Bayt(a.s) na kumfuata kabla ya kudhihiri kwake. Mtu huyu atawapenda wapenzi wa Imam Al Mahdi a.s. na atawachukia maadui wake, na atakubalia uongozi wa Maimam a.s. kabla ya kudhihiri kwake. Na hawa ndio marafiki zangu, na kwa hakika hawa ni watu halisi katika umma wangu ambao mimi ninawatukuza sana."

Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 129.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Allah swt atamwinua mtu mmoja kutokana na kizazi changu, kutokea Ahlul Bayt a.s. yangu, kwa kuja kwake ardhi hii itajazwa kwa uadilifu kama vile ilivyojaa sasa hivi kwa dhuluma na kukosekana kwa haki"

Al-Musannif, J. 11 Uk. 371

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w.) amesema:

"Mtu yeyote atakayekufa bila kumjua Imam wa Zama zake (Imam wa zama zetu hizi ni Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s.) Basi atakuwa amekufa kama vile walivyo kuwa wakifa katika zama za Ujahiliyyah"

Musnad Ahmad ibn Hanbal, J. 2, Uk. 83 na J. 3, Uk. 446 na J. 4, Uk. 96; Sahih Bukhari, J. 5, Uk. 13 na Sahih Muslim, J. 6, Uk. 21, na No. 1849 ya Riwaya-25 na Marajeo mengine ambayo yameelezwa na Wanazuoni wa Kisunni.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema kuwa:

"Atakapo dhihiri Al Qaim a.s., basi mbingu itanyesha mvua, ardhi itaotesha miti yake, uadui utakwisha kutoka mioyo ya waja (ili kwamba wote waweze kuishi kwa amani na mapenzi ya kindugu), na wawindaji na wanyama wataendelea kuishi kwa amani kwa pamoja"

Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 316

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Abil Jarudi amesema:

" Mimi nilimwuliza Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) iwapo yeye alikuwa akijua kuhusu mapenzi yangu na utiifu wangu kwake, naye alinijibu kuwa alikuwa akijua. Nami nikamwambia kuwa nilikuwa na swala nililokuwa nikitaka kumwuliza ili aweze kunijibu, kwa sababu mimi nilikuwa kipofu na nilikua nikitembea kwa uchache sana, na hivyo nilikuwa siwezi kumtembelea kila mara. Naye alinitaka mimi nimwulize swala nililokuwa nikitaka kumwuliza. Hivyo mimi nilimwomba anijulishe dini au madhehebu yeye na Ahlul Bayt(a.s) wanayoifuata na ambayo inapendwa na Allah swt, ili nami niweze kufanya 'ibada ya Allah swt kwa mujibu wa madhehebu hayo."

Kwa hayo Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) alinijibu:

"Kwa hakika wewe umeniuliza swala kubwa sana, ingawaje umeniuliza kwa kifupi sana. Kwa kiapo cha Allah swt mimi ninakujibu kuhusu dini yangu na dini ya mababu zangu kupitia huyo tunavyomwabudu Allah swt. Nayo ni: 'Kwa kukiri imani yetu kuwa hakuna Allah swt mwingine isipokuwa ni Allah swt, na kwamba Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni Mtume wa Allah swt, na kusadiki kuwa chochote kile kilichomteremkia yeye (Qur'an Tukufu) ni kutoka kwa Allah swt, na kuwa na mapenzi (yetu) ya wapenzi wetu na watiifu kwetu (Ahlul Bayt a.s.) na kuwachukia maadui wetu, kujisalimisha kwa njia yetu, na kumsuburi Al Qaim(a.s) (Imam wa kumi na mbili ambaye atadhihiri pale itakapotokea amri ya Allah swt), na kutaka (kudumisha yale yaliyofaradhishwa na mambo yaliyo halalishwa) na kwa kuwa mcha Allah swt halisi (kwa kujiepusha na yale yote ambayo ni haramu).

Al-Kafi, J. 1, Uk. 34.

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema,:

"Atakapo dhihiri Al Qaim(a.s) basi mikono yake itakuwa juu ya vichwa vya waumini, naye atawapa maendeleo ya kiakili na kukamilisha subira yao na kile wanacho kiangalia mbele. Baada ya hapo Allah swt ataongezea nuru yao macho na uwezo mkubwa wa kusikiliza ili kwamba kamwe kusitokezee vizuizi baina yao na Al Qaim(a.s) pale atakapo amua kuongea nao, na watakapomsikiliza, wataweza kumwona ilhali atakuwa mahala pake"

Yaumul-Khalas, Uk. 269.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema: "Wakati wa Al Qaim(a.s) muumin atakaye kuwa mashariki ataweza kumwona muumin mwenzake aliye magharibi, na vivyo hivyo muumin aliye magharibi ataweza kumwona muumini aliye mashariki. Tanbih. Ndugu msomaji ! Kwa hakika sasa hivi tunayo ala za mawasiliano mbalimbali kama vile Satellite, Television yafuatayo ambayo yanaweza kuwa yenye manufaa makubwa kwetu ili kuwaza kuangalia vyema na kuelewa hiyo riwaya vitu ambavyo havikuwapo wakati maneno matukufu ya riwaya hiyo yalipokuwa yakisemwa.

Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 391.

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

"Huyu Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) atakuwapo mahala ambapo ni karibu na Al Ka'aba Tukufu baina ya nguzo na nafasi ya kusimamia ya Mtume Ibahim(a.s) na atatoa mwito, atakapo kuwa akisema: 'Enyi watu wangu hasa ambao Allah swt amewawekeni kwa kuwatayarisha nyinyi kwa ya furaha ya kudhihiri kwangu juu ya ardhi hii! Njooni kwangu kwa utiifu. Na kwa hakika kauli hii itawafikia wale wote watakapokuwa nafasi wanaposalia na hata kama watakuwa vitandani wakiwa mashariki ya ardhi au magharibi yake. Na watamsikiliza kwa mwito wake huo mmoja tu ambayo yatafikia kila sikio la kila mtu, nao watajitayarisha kwa ajili ya kuja kwake. Kwa hakika haitawachukua muda wowote isipokuwa pumzi tu kiasi kidogo kukusanyika hapo baina ya mlingoti na nafasi ya kusimama ya Mtume Mtume Ibahim(a.s) wakimwitikia Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan (a.s)"

Bihar al-Anwaar, J. 53, Uk.7.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) alimwambia mfuasi wake aliyekuwa halisi, Mufadhdhal, mambo fulani kutokea kisa cha Al Imam Muhammad al-Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) na kudhihiri kwake,

"Ewe Mufadhdhal! Waambie wafuasi wetu habari za Al-Mahdi ili wasiwe na shaka katika Dini yao"

Bihar-ul-Anwaar, J. 53, Uk. 6.

AL IMAM MAHDI SAHIBUZ-ZAMAAN (A.S)

Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) amesema:

"Mimi ni Al Mahdi na mimi ni yule ambaye bado nipo hai na ambaye nitaijaza ulimwengu kwa haki na uadilifu kama vile ilivyojazwa kwa maovu na dhuluma. Kwa hakika ardhi haitabakia bila ya kuwa na mbashiri, na watu kamwe hawataisha bila ya kuwa na kiongozi. Na hii ni amana na hivyo msiwaambie wote wale Waislam wenzenu isipokuwa wawe ni watu wa Allah swt (wawe katika haki)."

Kamal-ud-Din, Uk. 445.

Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) amesema:

"Kwa mambo yanayotokea kwa Waislam, murejee katika riwaya zetu, (yaani Wanazuoni au Ma'ulamaa), kwa sababu wao ndio wawakilishi wangu kwenu na mimi ni Hujjatullah juu yao"

Kamal-ud-Din,Uk.484.

Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) alimwandikia barua Sheikh Al Mufid:

"Sisi tunaelewa hali yako na mazingara yako na hakuna jambo lolote lako lililojificha kwetu sisi"

Bihar al-Anwaar, J. 53, Uk.175.

Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) alimwandikia barua Sheikh Al Mufid:

"Si kwamba sisi hatukujali wewe au tumekusahau, kwa sababu kama ingekuwa hivyo, matatizo na balaa zingekuwa zimekuondokea wewe na maadui wako wangekuwa wameisha kumaliza. Hivyo, muogope Allah swt na uwe mtiifu kwake, asifiwe Allah Jalli Jalalahu" Dua: Tunamwomba Allah swt aharakishe kudhihiri kwa Imam wetu wa kumi na mbili Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan(a.s) ili aweze kudumisha usawa, ukweli, na haki katika ulimwengu mzima. Amina.

Bihar al-Anwaar, J. 53, Uk. 175.

UMMA WA WAISLAM KATIKA ZAMA ZA MWISHO

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Kutakuja zama kutakuja wakati katika zama miongoni mwa watu kuwa: Wao hawatawaheshimu Wanazuoni wao (yaani Maulamaa) ila kwa mavazi yao mazuri; wao hawatasikiliza Qur'an Tukufu ila kwa sauti ya kuvutia; Na wao hawatamwabudu Allah swt isipokuwa katika mwezi wa Ramadhani tu; wanawake wao hawatakuwa na aibu, maskini miongoni mwao hawatakuwa na subira, na matajiri wao hawatakuwa wakarimu, kwani wao hawataridhirika kwa kidogo na wala hawatakinai kwa wingi

Wao hawatashiba kwa kingi, wao watafanya kila jitihada kwa ajili ya matumbo yao; dini yao itakuwa ni mapesa (mali na utajiri); na wake zao ndio watakuwa Qiblah zao (tunapoelekea kusali huko Al-Ka'abah tukufu); na majumba yao ndio itakuwa Misikiti yao; wao watakimbia kutoka Maulamaa wao kama vile kondoo anavyo kimbia kutoka kwa mbwa mwitu.

Hapo watapokuwa kama hivyo (basi Allah swt atawatumbukiza katika mambo matatu). Atawaondolea baraka katika mali zao. Watatawaliwa na mtawala dhalimu. Watakufa (kutoka humu duniani) wakiwa hawana imani iliyo halisi"

Waqayi-ul-Ayyam, Uk. 439.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Utafika wakati katika umma wangu kwamba: watawala wao watakuwa wakatili na wadhalimu, Maulamaa na Wanazuoni wao watakuwa waroho wa mali na utajiri na watakuwa na imani kidogo, waumini wao watakuwa ni wanafiki, wafanya biashara wao watakuwa wakijishughulisha kwa kutoa na kupokea riba na kuficha maovu na kasoro ya vitu wanavyonunua na kuuza na wanawake wao watakuwa wamejihusisha mno na mambo ya kujirembesha ya dunia.

Hivyo, wakati huo, mwovu kuliko wote miongoni mwao ndio watakaokuwa wakiwaongoza wao, na wema miongoni mwao watakuwa wakiwaita watu lakini hakuna mtu atakaye wajibu"

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Utafika wakati katika Umma wangu ambapo wao watakuwa wakipenda vitu vitano na kuvisahau vitu vitano: Wao watakuwa wakiipenda dunia na kuipuuzia Akhera. Wao watapenda mali na kusahau hesabu ya siku ya Qiyamah Waume zao watawapenda wanawake waovu na kuwasahau Hur al-'Ayn Wao watapenda majumba na watayasahau makaburi yao. Wao watajipenda wenyewe kupita kiasi na kumsahau muumba wao. Kwa hakika watu kama hawa hawanipendi mimi na mimi pia siwapendi wao"

Al-Ithna-'Asheriyyah, Uk. 202.