HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)0%

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S) Mwandishi:
Kundi: Vitabu mbali mbali

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

Mwandishi: ASIYEJULIKANA
Kundi:

Matembeleo: 35392
Pakua: 3089

Maelezo zaidi:

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 12 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 35392 / Pakua: 3089
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

Mwandishi:
Swahili

8

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W) PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

MAADILI YA UISLAM

Nafs aina na sifa zake Masomo ya akhlaq- maadili katika Uislam ni mojawapo ya bora ya sayansi na inamwelekeza asomaye hadi katika elimu ya kujielewa nafsi yake mwenyewe, ambayo Islam inaamini kuwa ni faradhi.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Yeyote yule aliyeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi kwa hakika ametambua Allah."

Hivyo hivyo kuna mapokezi mengi ya habari kuhusu umuhimu wa somo hili hata Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amebainisha kuwa: "Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.

Tuanze kuzichambua aina za nafsi alizonazo mwanadamu vile alivyo: Hapana shaka kuwa mwanadamu hana nafs zaidi ya moja, lakini hii nafsi au inayo masharti fulani fulani. Kwa hiyo, hali ya kuonyesha kama 'nafsi ya kujilaumu' 'au nafsi ya kuamrisha' 'nafsi inayotosheka' (kama vile vielezwavyo katika Qu'rani), na hivyo haidhihirishi idadi ya nafsi. Upande mwingine, yote haya ni miongoni mwa ngazi za sifa ambazo zinaleta kwa ukamilifu na ustawi wa hali ya nafsi, pamoja na yale yanayoozesha nafsi na kuleta maovu.

NAFSI SAFI AU THABITI

QUR'AN TUKUFU

(Thabit.) Katika Qur'an Tukufu, Surah Ash Shua'raa, 26, Ayah 89, aina mbili hizo za masharti za nafsi zinaelezwa:

﴿ إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّـهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴾

"Isipokuwa mwenye kuja kwa Allah swt na moyo safi"

Uhalisi huu ni aina ya moyo, na moyo halisi (safi) ni ule ambao haufungamani na upande wa kuhangaika wala upande ule wa wapotofu.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Imenakiliwa kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) kuwa:

"Moyo ulio msafi- halisi ni ule ambamo hakuna chochote kile isipokuwa Allah swt tu"

Katika hali hii, Nafsi imetunukiwa hatua mojawapo ya umuhimu kuwa kamilifu. Hivyo inamaanisha kuwa hakutakuwa na mapenzi mbali na ile ya Allah swt tu.

MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Kuna habari nyigine iliyonakiliwa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ambamo twaambiwa:

"Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba, mama, watoto wake, mali yake na hata kuliko maisha yake."

Ndivyo hivyo, nafsi safi ni nafsi ambamo hakuna mapendo mengine yoyote yale isipokuwa Allah swt na wale wapendwao kwa ajili ya Allah swt (Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na Ahali yake a.s.)

NAFSI YENYE KUTUBU (AL-NAFS AL- MUNIIB)

QUR'AN TUKUFU

Sharti lingine la moyo au Nafsi ni kutubu na hivyo huitwa moyo wenye kutubu au nafsi yenye kutubu. Hivyo huwa daima inarudi kwa Allah swt, Qur'an Tukufu, Surah Qaaf, 50, Ayah 33:

﴿ مَّنْ خَشِيَ الرَّحْمَـٰنَ بِالْغَيْبِ وَجَاءَ بِقَلْبٍ مُّنِيبٍ﴾

"Anayemuogopa ( Allah swt Mwingi wa kurehemu), na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa moyo ulioelekea ( kwa Allah swt)."

Kuwa na khofu ya Allah swt pale mtu awapo peke yake ni mojawapo ya masharti bora ya nafsi, na hii ina maanisha kuwa nafsi imemtambua Allah swt kiasi kile kuwa hakutakuwa na tofauti yoyote itakapokuwa pekee yake au katika kundi la watu. Hata kama hakutakuwa na mtu yeyote karibu nayo, basi ile khofu ya Allah swt imo ndani yake thabiti.

Hii haipo katika kundi la zile nafsi zilizo ghafilika katika maasi na matendo maovu wakiwa katika kundi la watu au wakati wengine watakapokuja julishwa, na hawatajizuia nayo na hata kama iwapo watakapopewa habari zilizo bainika. Hii ni ile aina ya nafsi ambayo haielewi kuwa Allah swt yupo anaangalia yote na Aliye dhahiri popote pale na kwa hakika aina hii ya nafsi haipo pamoja na Allah swt na wala haitorudi kamwe kwa Allah swt.

NAFSI MWONGOZI (AL- NAFS AL- MUHTADI)

QUR'AN TUKUFU

Sharti lingine la nafsi ni ile iongozwayo. Qur'an Tukufu, Surah Attaghaabun, 64, Ayah 11, inatuambia:

﴿ مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴾

"Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Allah swt. Na anayemuamini Allah swt huuongoza moyo wake. Na Allah swt ni Mjuzi wa kila kitu."

Mtu ambaye moyo wake ukiwa umeongozwa na kujitosa katika habari ya imani na sheria Tukufu za Allah swt, yeye anaielewa njia yake vyema kabisa. Zile imani atakazokubalia na matendo yake yampasa kuyatenda huwa ni dhahiri kwake kuelewa vyote hivyo kwa uadilifu.

NAFSI ILIYO RIDHIKA (AL-NAFS AL- MUTMAI'NA)

QUR'AN TUKUFU

Sharti lingine lijulikanalo vyema la moyo au nafsi ni kuridhika. Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Ar-Raa'd, 13, Ayah 28 " Sikiliza: Kwa kumkumbuka Allah swt nyoyo hutulia." Na vile vile mwishoni mwa Qur'an Tukufu, Surah al-Fajr, 89, Ayah 28 -29, twaambiwa:

﴿ يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾ ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴾

"Ewe nafsi yenye kutua"! "Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika na umemridhisha."

Nafsi iliyo ridhika ni ile iliyokwisha ridhika, ina maanisha kuwa mtu yupo anapigana vita vikali na matakwa yake na kwa kuyatimiza yale yaliyo fardhi kwake katika dini na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa, na anajipa umuhimu kwa kuelimisha na kuikamilisha nafsi yake hadi hapo yeye hapindukii kutii chochote kile isipokuwa Allah swt tu. Ni marufuku kwake kuelekea pale penye madhambi na huwa ni mwenye kupenda amani na utulivu na huwa ni mwenye kujiridhikia mwenyewe hadi hapo yeye huwa thabiti kama jabali madhubuti. Hakuna madhambi, matakwa ya ubinafsi, tamaa, mvutano wa dunia, mapenzi ya mali au cheo yatakayoweza kuja kumpotosha yeye na kumwelekeze pengine na vile vile hakuna sheitani atakayeweza kumghalibu na kumpotosha yeye. Hali ya juu kabisa ya sharti hili kama ilivyokuwa katika Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na ma - Imamu(a.s) waliokuwa halisi kuwa hata mawazo ya kutaka kutenda madhambi hayakutokea kamwe.

NAFSI YA TAHADHARI YA UADILIFU (AL-NAFS AL MUTTAQI )

QUR'AN TUKUFU

Sifa nyigine ya nafsi inajulikana kama uangalifu wa uadilifu wa nafsi, nafsi ambayo imejaa kwa khofu na tahadhari. Hali hiyo inatokana na nyakati fulani kwa kupotoshwa na (kwa akili na ) huzungukwa na uchafu na ubovu ili nafsi iingie sharti sawa sawa na itahadharishwe na madhambi. Nafsi ikiwa katika hali hiyo huitwa nafsi ya tahadhari ya uadilifu. Qur'an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 32 :

﴿ ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴾

"Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Allah swt, anayezihishimu alama za (dini ya ) Allah swt, basi hili ni jambo la katika utawala wa nyoyo."

Kwa mtu yule ambaye imani yake inafikia kiwango hiki cha Taqwa kiwango cha tahadhari ya uadilifu, huheshimu na kumthamini Allah swt na yale yote yaliyotolewa ishara nae kama Dini, Msikiti, shariah, waumini wake, Makkah, Al-Ka'abah Tukufu n.k. Kwa ufupi chochote kile kinachohusika na Allah swt huwa kina kuwa na umuhimu na ta'adhima kubwa kwa mtu kama huyu wa namna hii. Na hii ndiyo kwa hakika matokeo ya taqwa

NAFSI NYENYEKEVU (AL- NAFS AL- MUKHBIT)

QUR'AN TUKUFU

Hali nyingineyo ya Nafsi ni unyenyekevu na uvumilivu, yaani humaanisha kuwa mtu mwenye nafsi hali hii huwa mnyenyekevu mbele ya maamrisho ya Allah swt Kwa mara nyingine tena twaambiwa katika Qur'an Tukufu, Surah al Hajj, 22, Ayah 54:

﴿وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَيُؤْمِنُوا بِهِ فَتُخْبِتَ لَهُ قُلُوبُهُمْ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهَادِ الَّذِينَ آمَنُوا إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴾

"Na ili walio pewa ilimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waamini, na zipate kutua nyoyo zao. Na hakika Allah swt anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia iliyo nyooka."

Kwa sababu nyoyo hizi hujiinamisha chini mbele ya Allah swt na maamrisho yake, na wale wenye kuwa na nyoyo hizo hujiwakilisha kwa Allah swt nao kamwe hawavunji maamrisho ya Allah swt na wala hawazisaliti au kuzipinga.

NAFSI HALISI (AL-NAFS AL-ZAKIYYAH)

QUR'AN TUKUFU

Aina nyigine ya nafsi ni ile nafsi au iliyo mtakatifu. Katika Qur'an Tukufu, Surah Ash-Shams, 91, Ayah 9-10, Allah swt anakula kiapo cha jua, mwezi mbingu, ardhi na vitu vingine na baadaye akiisemea nafsi, anatuambia:

﴿ قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا ﴿٩﴾ وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا ﴾

"Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)"

Ni dhahiri kuwa inambidi mtu afanye jitihada ili kufikia hatua hii. Kabla ya yote yale mengineyo, nafsi lazima iwe huru kutoka sifa zote zile zilizo ovu na hapo ndipo uwanja utakuwa tayari kwa kuzitambulisha sifa zilizo nzuri na bora kabisa na kwa uanzishaji na uendelezaji. Mtu ambaye nafsi yake itatakasika, basi amehakikishiwa msamaha (ukovu) na kufikia kipeo cha furaha ya milele.

NAFSI YA KUKARIPIA - LAUMU (AL-NAFS AL- LAWWAMA)

QUR'AN TUKUFU

Inawezekana wakati mwingine kuwa hivyo kwa vyovyote vile na kiasi chochote kile cha madhambi ayafanyayo, mtu hajisikii chochote cha kutenda kosa, wala hasikitiki, wala hajilaumu mwenyewe. Nafsi kama hiyo ni ile iliyoshindikana. Hata hivyo, ile nafsi baada ya kuanguka na kutenda madhambi na itajikaripia yenyewe na kujishutumu yenyewe, kabla ya yeyote yule kufanya hivyo, basi imeingia katika sharti tukufu mojawapo la nafsi itakiwavyo kuwa. Qur'an Tukufu, Surah Al Qiyamah, 75, Ayah 1-2, inatuelezea:

﴿ لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ ﴿١﴾ وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ ﴾

"Naapa kwa siku ya Qiyamah. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)".

Ni dhahiri kuwa iwapo Allah swt akiapia kwa vitu, basi kuna utukufu wake humo. Nayo pia ni wazi kuwa yeyote yule aifunzae nafsi yake vyema hadi ule wakati wa kutenda madhambi, yenyewe (nafsi) hujaa masikitiko na kujilaumu, basi imefikia mojawapo ya vina vya utakatifu.

NAFSI ILIYOFUNGULIWA HERI (AL-NAFS AL-MULHAM)

QUR'AN TUKUFU

Sharti lingine la nafsi ni kuongozwa na Allah swt. Twaambiwa katika Qur'an Tukufu, Surah Ash-Shams, 91, Ayah 8:

﴿ فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا ﴾

" Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake"

Maongozi haya ni kutia moyo kwa nafsi wakati itapokuwa katika hali ya kutakasika- Nafsi halisi si ambayo tumeishaizumgumzia. Ni lazima iwapo nafsi itaelekezwa kwa mujibu wa madhambi basi muongozo na kufunguliwa kwa heri kutoka kwa Allah swt yatafikia kikomo chake.

Kwa kupingana na sifa na masharti ya nafsi ambazo ni sababu ya furaha ya milele na utakatifu, baadhi ambazo zimekwisha tajwa hapo awali, pia hapo hapo kuna sifa na masharti yanayosababisha maovu ya nafsi, sasa tuziangalie.

NAFSI YENYE MADHAMBI (AL-NAFS AL-AATHIMA)

QUR'AN TUKUFU

Iwapo nafsi ya mtu ikiwa na tabia ya kutenda madhambi, basi huitwa yeye madhambi. Qur'an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 283 inazungumzia kulipa kwa amana:

﴿وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ﴾

"Na mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, yatosha kukabidhiwa rahani. Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe basi aliye aminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Allah swt, Mola wake Mlezi. Wala msifiche ushahidi. Na atakaye ficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allah swt ni Mjuzi wa mnayo yatenda."

Hii inathibitisha kuwa nafsi ya yeyote yule ambaye ameshajizoelesha madhambi ni nzito na ni wazi na tayari kwa kutenda madhambi wakati wowote ule.

NAFSI ILIYO SINZIA (AL-NAFSAL-GHAFIL)

QUR'AN TUKUFU

Sababu mojawapo ya kushidwa na kufifia kwa nafsi ni kulegea au kusinzia au kuwa zembe. Kwa kutenda mambo maovu na kwa kuendelea kutenda madhambi ndiko kunakosababisha nafsi kuelekea palipo paovu na kutomsikia Allah swt. Anaelezea Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Al Kahf, 18, Ayah 28:

﴿وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا﴾

"Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata matamanio yao yakawa yamepita mpaka"

NAFSI ZILIZOTIWA MUHURI (AL-NAFS AL- MATBU')

QUR'AN TUKUFU

Hapa inamaanisha kufungwa muhuri juu yake na hivyo ndivyo hatua ya mwisho,Amesema Allah swt katika Quran:

"Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu."

Popote pale mtu anapokuwa fidhuli au juvi kuelekea Allah swt hadi kudharau na kutokubali ujumbe Wake na maamrisho ya Allah swt ambayo amemwekea mbele yake, au , iwapo yeye atazikubalia, anazipa umuhimu kidogo na kuwa na kosa la upinzani basi hapo nafsi yake inaingia katika hatua ile ambayo ni sawa na kama tahadhari, maamrisho matukufu na yale yaliyo haramishwa hayatakuwa na athari yoyote ile kwake yeye. Na hii ni hatua mojawapo ya kudidimia kwa nafsi na kushindwa kwake.

NAFSI ILIYO POFUKA ( AL-NAFS AL- AMYA)

QUR'AN TUKUFU

Hali nyingine ya Nafsi ni kupofuka. Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 46:

﴿أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَتَكُونَ لَهُمْ قُلُوبٌ يَعْقِلُونَ بِهَا أَوْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ﴾

"Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo zao za kuzingatia, au masikio ya kusikia? Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka."

Nyoyo hizi zinaona vingine mbali na Allah swt na hazimwoni Allah swt. Nyoyo za aina hizi huona yale tu yatakayo yenyewe bila ya kuyazingatia yale maamrisho ya Allah swt na kwa hakika ndizo zilivyo kama vile vimepofuka tu.

NAFSI YENYE MARADHI (AL-NAFS AL-MARIDHA)

QUR'AN TUKUFU

Qur'an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 10:

﴿ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ﴾

"Nyoyoni mwao mna maradhi, na Allah swt amewazidishia maradhi. basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uongo."

Ugonjwa wa aina hii inawezekana kuonekana mioyoni mwetu kwa sababu ya yale madhambi tuyafanyayo sisi siku hadi siku. Kama vile mtu mgojwa huwa hana hamu ya vyakula wala madawa ambavyo ni vyenye manufaa kwake na vile vile vyakula vizuri havitakuwa na ladha yoyote kwake, ndivyo vivyo hivyo kuhusu NAFSI iliyougua, kwani inapatikana kuonywa ( na Allah swt) na kukaribia kwa upole kwa mapendo na matakwa yake ya humu ulimwenguni na Aakhera kuwa yenye adhabu kali sana na yenye kutisha mno.

Kilicho zaidi ni kwamba mtu aliyeugua hivyo ni yule mwenye, kuipendelea kwa ajili ya nafsi yake yale yote yaliyo mabaya na maovu, kwani huwa anavutiwa navyo kama kwamba ndivyo vyenye kumfaa yeye. Kwa hakika hii ndiyo ile nafsi iliyokwisha ugua; kama vile ilivyo kifo kwa mtu hatakayetibiwa magonjwa yake na hivyo ndivyo vinaweza kutokea kwa ajili ya aina hii ya nafsi iwapo haitoweza kutibiwa kabla ya ugonjwa kuenea pote na hatimaye mtu aweza kuangamia.

Popote pale mtu aonapo kuwa yeye hatamani chochote kile atakiwacho kukifanya yaani kumkumbuka Allah swt katika sala na kutii Sharia Tukufu za Dini ambazo hazimfai na ambazo ni chungu kwake, kwa hivyo ni wazi kabisa kuwa atambua kuwa hiyo nafsi wake imeshaanza kuugua maradhi, na bila ya kusita inambidi afanye kila hila awezayo ili ajielekeze kwa mujibu wa aya za Qur'an Tukufu, kwa watawa na walio waumini halisi na wale walio hodari katika elimu na ujuzi huu: waganga wa moyo, wanavyuoni waelewao na wafuatao mienendo ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., ili waweze kuitibu nafsi ya aina hiyo iliyopatwa na maradhi.

NAFSI INAYOKWENDA UPANDE (AL-NAFS AL-ZA'IGHA)

Moyo au Nafsi pia inaweza kusemwa kuwa inakwenda upande au inapotoka. Aina hii ya Nafsi ni ile ichaguayo upotofu wakati ipatiwapo chaguo katika hali mbili ya wema na uovu. Kama mategemeo yote ya maisha, katika sehemu zote za Imani, maadili na matendo, mambo yake yote yaliyo dhahiri na yale yote yaliyo batili mwake, mwanadamu daima anakumbwa na mgawanyiko wa njia mbili mbele yake , mtu ambaye amefaulu na kufurahika ni yule ambaye daima anachagua njia ile aitakayo Allah swt. i.e njia iliyonyooka (Sirat al-Mustaqeem) ya dini katika kila hali. Hata hivyo, mtu ambaye moyo wake unampotosha, huwa daima ndiye achanguaye njia ya upotofu.

QUR'AN TUKUFU

Katika Qur'an Tukufu, kuzungumzia mifano na mafumbo ya aya na kwa kuelezea wazi wazi, Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Surah Al I'mran, 3, Ayah 7:

﴿فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ﴾

"Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. lakini hawakumbuki hayo isipokuwa wenye akili."

Hivi kwa kuchagua mfano (mutashabih) wa aya za Qur'an Tukufu ili kuitumia Qur'an Tukufu kwa kuhakikisha matakwa ya mtu binafsi ni sampuli ya ile nafsi iliyopotoka.

NAFSI YA MOYO MGUMU (AL-NAFS AL-QASIYA)

QUR'AN TUKUFU

Sharti lingine la nafsi kuwa hivyo ni kutokana na moyo mgumu na katili. Katika Qur'an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 13

﴿فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ﴾

"Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Allah swt huwapenda wafanyao wema."

Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu Surah Al H'adiid, 57, Ayah 16:

﴿ أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ﴾

"Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah swt na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, Kwa hivi nyoyo zao zikiwa ngumu na wengine wao wakawa wapotovu."

Hali kama hii inaelezewa katika aya zinginezo pia. Nyoyo kama hizi zina sifa kama zile za jiwe na chuma, kuwa hakuna chochote kile kiwezacho kuathiri au kuacha alama yoyote juu yake ila kwa mshindo mkali tu moto. Hadi kufikia hali ya moyo kuwa mgumu kiasi hiki ni dhahiri ikionekana vile maovu yalivyo mteka huyo mtu hadi akawa mtumwa wa matakwa na maovu yake. Kwa hakika imepotoka!

NAFSI WASIWASI (AL-NAFS AL-MURTABA)

Nafsi ya aina hii imo katika hali hii ya wasiwasi kuhusu vile vitu ipasavyo kuvijua na kuviamini. Shaka kuhusu mizizi ya Dini ya Islam kama vile kushuku kuwapo kwa Allah swt, Aakhera, Utume wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na vile vile Uimamu (wa ma-Imamu a.s.), na kushuku matawi ya Dini kama vile sala, saumu na mema na mengineyo mengi. Katika Qur'an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 45:

﴿ إِنَّمَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَارْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِي رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ﴾

" Wasio muamini Allah swt na Siku ya Mwisho na nyoyo zao zina shaka, hao tu ndio wanao kutaka ruhusa. Basi hao wanataradadi katika shaka zao."

Hii ni mojawapo ya sababu ya upotofu wa Nafsi na ni fardhi kwa watu wale walio katika hali kama hii kujielekeza katika Ayah za Qur'an Tukufu na Ahadith Tufuku za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na Ma-Imamu(a.s) na kwa wanavyuoni wa dini ili kuweza kutokomeza hali hii kabla ya kutanda juu ya Nafsi nzima undani mwake. Ama sivyo, iwapo hali kama hii haitashughulikiwa na badala yake ikapuuzwa na kubakia Nafsini, basi itamwelekeza mtu katika hali ya kukatiza na kukataliwa (kupuuzwa na kudhoofika).

NAFSI ILIYOPATA KUTU (AL-NAFS-AL-RA'INA)

Kutu ni shida nyingineyo ambayo nafsi inaweza kupatwa kwani ni sawa na ule mfano wa kioo cha kujitazamia, iwapo ile poda itabanduka basi hutaweza kujitamazama kiooni. Basi kioo cha nafsi ambavyo ni sehemu umuhimu kwa ajili ya Allah swt utukufu wa ukamilifu wake, fadhila zake zitamorudishwa kwake, hazitoweza kurudishwa iwapo itashika kutu, na hatimaye itaweza kupoteza ile nguvu ya kupeleka ujumbe wako kwa Allah swt.

Ingawaje mwanadamu hawezi kumtazama Allah swt kwa macho yake, lakini anao uwezo wa kumwona Allah swt, Utukufu wake na Ukuu wake kwa kupitia NURU iliyomo katika Nafsi yake. Nafsi ile ambayo imeshakwisha shikwa na kutu ambamo sasa hakuna uwezo wa kurudishia kutokana kwa Allah swt, basi bila shaka itatapatapa huko na huko ikimtafuta sheitani na hasa kwa mujibu wa maana yake.

QUR'AN TUKUFU

Qur'an Tukufu, Surah Al Mut'affifiin, 83, Ayah 14, ikiwa inatukumbusha kuwa:

﴿ كَلَّا بَلْ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴾

"Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma."

Katika aya hii twaelezewa vyema kabisa kuwa chanzo cha kupatwa kwa kutu kwa Nafsi ni kule kutenda madhambi. Kwa hivyo kila dhambi itatupia uzito (itatanda kiza juu ya moyo; na ifikiapo hali kama hii, inambidi mtu afanye Tawba (Kipo kitabu nilichokitarjumu katika lugha ya kiswahili kinachozungumzia swala hili kwa marefu na mapana ) mara moja kwa ajili ya kuyasafisha hayo matendo maovu na atende matendo mema ili kuzuia kupotea kwa nuru iliyotunukiwa Nafsi yake. Vile vile, twaambiwa katika hadith Tukufu kuwa: "Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Qiyama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka 'naomba msamaha wa Allah swt' chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa hivyo inambidi kila Mwislam miongoni wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Allah swt azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

NAFSI AMURU (AL-NAFS AL- 'AMMARA)

QUR'AN TUKUFU

Nafsi isiyofunzwa hasa wakati wa ujana wa mtu, huamuru kutendwa kwa matendo ya madhambi bila kiasi. Katika Qur'an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53 , kuhusu kisa cha Mtume Yussuf(a.s) , inazungumziwa Nafsi:

﴿ وَمَا أُبَرِّئُ نَفْسِي إِنَّ النَّفْسَ لَأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّي إِنَّ رَبِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾

"Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu."

Sentensi hiyo inaonyesha kuwa ilitamkwa na Zuleikha aliyekuwa amependa Mtume Yussuf(a.s) Pale alipotoa ushahidi, alithibitisha kuwa ndiye chanzo cha uovu huo. Kwani Mtume Yussuf(a.s) alikuwa hayupo wakati huo wa ushahid, lakini kwa kuwa Zuleikha alikuwa hana hila yoyote ile dhidi ya Mtume Yussuf(a.s) . Pia kuna uwezekano kuwa hayo yametamkwa na Mtume Yussuf(a.s) au ni wote vyovyote vile. Qur'an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53, inatuambia kuwa:

﴿ وَمَا أُبَرِّئُ نَفْسِي إِنَّ النَّفْسَ لَأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّي إِنَّ رَبِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾

"Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu."

Nafsi yoyote ile isiyokuwa imeongozwa kwa mujibu wa mfano ya Islam, huwa daima inavutwa popote pale penye madhambi na ma'asiyah kwani yote hayo yako yamedhalilishwa kabisa. Mfano wa Nafsi hii ni sawa na mtoto mchanga atakaye kila kitu kuchezea bila kutazama ubora wake, faida au hasara zake, ilimradi yeye apate kuchezea tu, Nafsi ya yule aliye na utamaduni mzuri, aliyekomaa na kubaleghe inavutika pale penye mema na hujiepusha na maana yake; na ile nafsi iliyo ilimishwa na inavutika pale penye maovu ya kila aina na kwa hivyo lazima ifunzwe vyema, itasaidia kutakasisha hiyo Nafsi.

HATIMAYE

Kile kilichoelezwa hapo kinasema kuwa Nafsi inaweza kuwa bora kabisa ama mbovu kabisa au vinazidiana katika vina na ngazi. Kuna nafsi zifikiapo kuitwa Nafsi halisi na Nafsi ridhika n.k. na vile vile kuna zinapofifia hadi kufikia hali mbaya kabisa na matokeo yake ni majanga, majonzi na maovu na kufikia ile sifa ya kupigwa mihuri au zilizopofuka na zenye maradhi zikiwa ni kama mifano. Hali hii inadhihirisha kuwa Nafsi zinapangwa na kila mtu na kila mtu anayo Nafsi moja tu.

QUR'AN TUKUFU

Qur'an inatuambia katika, Sura Ya-Sin, 36; Ayah 79: Sema:

"Ataihuisha yule aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni Mjuzi wa kila (namna ya ) kuumba"

AL-IMAM JA'AFAR AS- SADIQ (A.S)

Amesema Al-Imam Ja'afar as- Sadiq(a.s) katika Al-Kafi:

"Kuwazulia uwongo Allah swt na Mtume Muhammad s.a.w.w. ni Dambi Kuu (dhamb kabirah)."

FADHAIL ZA IMAM ALI (A.S)

MIMI NILIMWULIZA MTUME (S.A.W.W)

Kutokea 'Ala, amesema yeye: "Mimi nilimwuliza 'Aysha kuhusu 'Ali ibn Abi Talib. Mimi nilimwuliza Mtume(s.a.w.w) kuhusu yeye. 'Ayesha alijibu, naye akasema kuwa:

'Ali ni mtu bora kabisa katika Wanadamu, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa ni mpagani tu."

ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Na kutoka 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , kasema:

"Aliniambia Mtume Muhammad(s.a.w.w) 'Wewe ni bora wa viumbe vya Allah swt, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa atakuwa ni kafiri"

MIMI NILIMWULIZA MTUME (S.A.W.W)

Na kutoka kwa Hudhaifa: "Alisema Mtume Muhammad(s.a.w.w) kuwa

''Ali ni bora wa Wanaadamu. Yeyote yule anayekataa haya kwa hakika ni kafiri."

ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Kutokea kwa Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alisema:

"Alisema Mtume Muhammad(s.a.w.w) :

'uadui, chuki na bughudha dhidi ya 'Ali ibn Abi Talib ni ukafiri na uadui dhidi ya Bani Hashim ni unafiki.'"

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

Na kutokea kwake, kutokea Mtume Muhammad(s.a.w.w) akasema:

"Hakuna ampendaye 'Ali ibn Abi Talib(a.s) isipokuwa ni mumiin halisi, na hakuna amchukiaye 'Ali isipokuwa ni kafiri."

. Na kutokea Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. , alisema: "Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. kuwa yeyote yule atakaye msema vibaya 'Ali ibn Abi Talib, basi ajue kuwa amenisema mimi vibaya hivyo, na yeyote yule anisemaye mimi vibaya, basi amemsema hivyo Allah swt (na hilo ni dhambi kuu )."

AL-IMAM ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Amesema Al-Imam Ali ibn Abi Talib(a.s) kuwa; Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema:

"Kwa hakika Allah swt alitazama kuelekea dunia hii na akanichagua mimi kutoka watu wa dunia; na kwa mara nyingine tena aliangalia duniani na kukuchagua wewe kutoka watu wa dunia; na kwa mara ya tatu alipoangalia akawachagua Maimamu(a.s) kutokea vizazi vyako miongoni mwa watu wote wa dunia hii; na kwa mara ya nne alipoangalia akamchagua binti yangu Fatimah kutokea wanawake wote wa dunia hii."

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

Kutokea Ja'abir, anasema kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema:

"Ali ibn Abi Talib(a.s) ni bora miongoni mwa watu wa dunia. Yeyote yule aliye na shaka, basi ni kafiri."

Amesema Ibn 'Abbas kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema:

"Ali ibn Abi Talib(a.s) ni mlango wa Hitta Yeyote yule atakayeingia ndani mwake basi kwa hakika ndiye mumiin wa kweli, na yeyote atakayetoka kutoka humo ni kafiri."

AL-IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) kutokea baba yake amesema kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) aliulizwa kuhusu hali ya watu, naye akajibu

"bora kabisa na Mcha Mungu halisi na ambaye aliye karibu kabisa nao ambay yuko karibu nami ni Ali ibn Abi Talib(a.s) , na hakuna Mcha-Mungu halisi miongoni mwenu, na ambaye yupo karibu nami kuliko Ali ibn Abi Talib(a.s) "

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W

Jami' bin 'Omair, alisema kuwa yeye alimwuliza 'Ayesha kuhusu daraja la 'Ali ibn Abi Talib a.s. mbele ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) ? Yeye alijibu:

"Kwa hakika ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad(s.a.w.w), "Yeye alimwuliza tena kuhusu nafasi ya Ali ibn Abi Talib a.s. katika macho ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) Alijibiwa kuwa "Ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad(s.a.w.w) "

Na kutokea Ibn 'Umar amesema kuwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema :

"Bora wa mtu miongoni mwenu ni 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na bora wa vijana wenu ni Al - Hassan na Al -Husayn"

'Urwah anaripoti kutoka 'Ayesha kuwa: Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w)

"Kwa hakika nimeahidiwa na Allah swt kuwa yeyote yule atakayeinuka dhidi ya 'Ali ibn Abi Talib(a.s) basi kwa hakika ni kafiri na kwa hakika ataingia Jahannam aunguzwe na moto. 'Aisha akasema kuwa "Mimi niliisahau hadith hii siku ya (vita vya) Jamal, hadi hapo nilipoikumbuka au nilipokumbushwa tukiwa Basra (Iraq), nami namwomba Allah swt anisamehe, na sitegemei kuwa miongoni mwao."

Abu Salim bin Abu al-Jaada amesema kuwa yeye alimwomba Ja'abir azungumze chochote kuhusu 'Ali ibn Abi Talib(a.s) Ja'abir akasema:

"'Ali ibn Abi Talib(a.s) alikuwa bora miongoni mwa wanadamu."Mimi nilimwuliza tena "Je unasemaje kuhusu mtu atakayemchukia 'Ali ibn Abi Talib(a.s) " Yeye alinijibu: "Hakuna atakayemchukia 'Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa kafiri."

Hashim bin Barid alisema kuwa'Abdullah ibn Mas'ud alisema:

"Mimi nilijifunza Sura 70 za Qur'an Tukufu kutokea kinywani mwa Mtume Muhammad(s.a.w.w) na Surah za Qur'an zilizobakia nilijifunza kutokea mbora wa Ummah wetu yaani Ali ibn Abi Talib(a.s) "

Muhammad bin Salim al-Bazzar anasema kuwa yeye alikuwa pamoja na Said bin al-Musayyib katika Masjidi-Nabi, siku ya Ijumaa, ndipo alipotokezea mhubiri kutoka kabila la Banu Omayyah (laana za Allah swt ziwafikie juu yao ) na akapanda juu ya mimbar na akaanza kumtusi Ali ibn Abi Talib(a.s) kwa kusema:

"Kwa hakika, Allah swt hakumtukuza Ali ibn Abi Talib(a.s) kwa mapenzi yake ba dala yake amefanya hivyo kwa kuhofu uchochezi wake."

Kwa hayo Said bin Al-Musayyib alimlaani na kumwambia: "Kwa hakika wewe unasema uongo mtupu" Na hapo alimtupia nguo aliyokuwa akijifunika juu ya mdomo wa mhubiri huyo. Hapo watu walipomwambia kuwa itakuwaje iwapo Abu Muhammad wakati Imam huyo anatokana na Banu Omayyah ? Hapo Said alijibu:

"Kwa kiapo cha Allah swt! Mimi sijui nilichokisema, lakini mimi nilimsikia Mtume Muhammad(s.a.w.w) akisema haya kutokea makbara haya nami ndipo nilipoyarudia kuyasema."

Ummi Hani binti Abu Talib(a.s) kasema kuwa; Mtume Muhammad(s.a.w.w) kasema kuwa:

"Bora wa viumbe vya Allah swt katika mtazamo wake Allah swt, ni yule anayelala kaburini mwake na kamwe hakumshuku 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na kizazi chake ni bora wa vizazi katika viumbe vyote."

Ja'abir anasema kuwa "Hakuna anayeshuku fadhail za 'Ali ibn Abi Talib(a.s) isipokuwa ni kafiri na kasema kuwa:

"Kwa kiapo cha Allah swt sisi kamwe tulikuwa hatuwajui wanafiki, katika zama za Mtume Muhammad(s.a.w.w) isipokuwa kwa yule mwenye chuki dhidi ya 'Ali ibn Abi Talib(a.s) "

Said bin Ja'abir alise kuwa yeye alikuwa akimwongoza Ibn 'Abbas baada ya yeye kupoteza nuru ya macho yake, kutokea Msikitini, na aliwapita kundi la watu waliokuwa wakimtukana 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na aliniambia kuwa nimchukue hapo.

Hivyo mimi nilimfikisha kwao. Kufika hapo alisema "Ni nani miongoni mwenu anayemkashifu Allah swt ?! Kwa hakika yeyote yule anayemkashifu Allah swt amekuwa kafiri. Na ni yupi yule anayemkashifu 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ? Na kwa hakika hili limetokea" akasema. Ndipo alipoendelea kusema: "Nashuhudia Allah swt, kwa kiapo cha Allah swt, mimi nilimsikia Mtume Muhammad(s.a.w.w) akisema 'Yeyote yule anayemkashifu 'Ali ibn Abi Talib(a.s) basi amenikashifu mimi na kwa hakika anayenikashifu mimi basi ajue kuwa amemkashifu Allah swt na yule anayemkashifu Allah swt, Mtume wake basi watatakiwa kutoa maelezo yake." Na hapo ndipo Ibn 'Abbas aligeuka.

Amesema Mtume Muhammad(s.a.w.w) :

"Muzirembeshe vikao vyenu kwa mazungumzo na makumbusho ya 'Ali ibn Abi Talib(a.s) kwani dhikr zake ni dhikr zangu na dhikr zangu ndizo dhikr za Allah swt na dhikr za Allah swt ni 'ibadah. Na mwenye kufanya 'ibadah huingia Peponi."

. Amesema:

"Siri ya ufanisi ni hii, kwamba uhusiano wetu na wengine uwe wa mapenzi badala ya uhasama. Ikiwa mtu hawezi kufanya urafiki na watu wenye tabia nzuri, basi hataweza kabisa kuishi bila kuwa na fazaa!"

Mwanachuoni mmoja amesema: "Maisha yetu ni kama eneo la milima ambapo ikiwa patapigwa ukelele mmoja, mtu atasikia mwangwi wake ukirudi kwake; hivyo, wale waliojawa na mapenzi ya wengine katika nyoyo zao, wataona hali kama hiyo kutoka kwao. Ni kweli kwamba maisha yetu ya kidunia yamesimama juu ya mabadilishano na malipano. Hatutaki kusema kwamba maisha yetu ya kiroho pia yamesimama juu ya msingi huohuo, lakini vipi inayumkinika kutaraji kuona uaminifu kutoka kwa wengine bila ya wewe mwenyewe kuwa mwaminifu kwao? Na vipi mtu atake apendwe na wengine bila yeye mwenyewe kwanza kuwapenda wao.?"

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) aliwakunjulia watu wote moyo wa mapenzi. Upendo wake mkubwa juu ya watu, upole na mvutio wake ulikuwa ukidhihirika kwenye uso wake wa kimalaika. Alikuwa akiwatendea vizuri na kuwakirimu Waislam wote sawasawa. Rawdhatu 'l-Kafi, uk. 268. "Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa akiwashughulikia na akigawa wakati wake kati ya masahaba zake sawasawa." Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) alikuwa akikataza tabia mbovu, na alikuwa akisema:

"Tabia mbaya ni kisirani, na mtu mwovu kabisa kati yenu ni yule mwenye tabia mbovu."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 371.

Mahali pengine amesema:

"Enyi wana wa Abdul Muttalib! Ninyi hamtaweza kamwe kuwaridhisha watu kwa mali zenu, hivyo kutaneni nao kwa uso mchangamfu na mwendo mzuri."

Wasa'ilu 'sh-Shi'ah, jz. 2, uk. 222.

Aliyekuwa mtumishi wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , Anas bin Malik, alikuwa daima akikumbuka hulka nzuri ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , na alikuwa akiwaambia watu kwamba katika kipindi cha miaka kumi aliyomtumikia Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , hakuwahi kabisa kumwona ameukunja uso wake unaonawiri, wala hakuwahi hata mara moja kumwona amepandisha nyusi zake au ameonyesha uso wa hasira kwa sababu ya kufanya jambo lisilopendeza. Tabia njema na uchangamfu ni katika sababu zinazozidisha umri wa mtu.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Wema na tabia nzuri hustawisha ardhi na huzidisha umri."

Wasa'ilu 'sh-Shi'ah, jz. 2, uk. 221.

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Tabia njema ni miongoni mwa ufanisi wa mtu."

Mustadriku 'l-Wasa'il, jz. 2, uk. 83.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Tabia nzuri hupanua riziki na huvuta (nyoyo za) urafiki."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 279.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Watu wenye akili kamilifu kabisa ni wale wenye tabia nzuri kabisa."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Vitakavyowaingiza kwa wingi umma wangu katika Jannat ni ucha-Mungu na tabia njema."

Wasa'ilu 'sh-Shi'ah, jz. 2, uk. 221.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Chukulia jambo la ndugu yako (wa imani) kwa maana nzuri kabisa mpaka ulione kinyume chake wala usilidhanie vibaya neno analolitoa ndugu yako wakati kuna uwezekano wa kuwa sahihi na kheri."

Jami'u 's-Sa'adaat, Jz. 2, uk. 28.

Matunda mojawapo ya dhana nzuri ni kupatikana urafiki wa watu wa kuwepo mapenzi na usafi wa moyo. Amirul Muuminin Ali a.s. ametaja matokeo na matunda ya dhana nzuri katika maneno yake mbalimbali, amesema:

"Mwenye kuwadhania vizuri watu hujifaidia mapenzi yao."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 687

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Dhana nzuri humwokoa mwenye kufuata madhambi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 378.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Dhana nzuri ni raha ya moyo na usalama wa dini."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 376.

Dhana nzuri humpunguzia mtu taabu na matukio mabaya.

.Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Dhana nzuri hupunguza majonzi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 377.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye kuwa na matumaini juu yako huwa amekuamini na kukudhania vizuri, hivyo usiharibu dhana yake (ukamvunja moyo)."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 680.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Dhana ya mtu ni mizani ya akili yake, na kitendo chake ni ushahidi wa kweli kabisa wa dhati yake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 74.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye kutojali dhana mbaya juu ya ndugu yake, huwa ana akili timamu na moyo mtulivu."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 676.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Miongoni mwa haki za muumin kwa muumin mwenzake ni kutomkadhibisha (kumsadiki)."

Usulu 'l-Kafi, jz. 1, uk. 394.

QUR'AN TUKUFU

Qur'an Tukufu, Surah Al Hujaraat, 49, Ayah 12. inasema waziwazi kwamba dhana mbaya ni dhambi, na inawatahadharisha Waislamu wajiepushe na kudhaniana dhana mbaya:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ﴾

Enyi mlioamini! Jiepusheni sana na kuwadhania watu dhana mbaya, kwani kuwadhani watu dhana mbaya ni dhambi.

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema:

"Allah swt amewaharamishia Waislamu vitu vitatu: damu zao, mali zao, na kudhaniana vibaya."

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Si uadilifu kutoa hukumu kwa kutegemea dhana."

Nahju 'l-Balaghah, uk. 1174.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Jihadhari na kudhania vibaya, kwani dhana mbaya huharibu ibada na huifanya dhambi kubwa zaidi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 154.

Vile vile amesema kwamba kuwadhania vibaya watu wanyoofu ni aina moja ya udhalimu:

"Kumshuku mtu mwema ni dhambi mbaya kabisa na ni udhalimu unaochukiza sana."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 434.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye kutawaliwa na dhana mbaya hakubakii amani baina yake na rafiki yake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 698.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Dhana mbaya hufisidi mambo na huchochea maovu."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 433.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Jihadhari na ghera (inayotokana na kushuku) mahali si pake, kwani humtia mzima maradhi na humshuku asiyekuwa na hatia."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 152.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Humwoni mwenye kushuku kuwa mzima."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 835.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Yule ambaye dhana yake si nzuri humwogopa kila mtu."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 712.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Nyoyo zina kumbukumbu mbaya ambazo huchukiwa na akili."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 29.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) amesema:

"Mwovu hamdhanii vizuri mtu mwingine kwa kuwa haoni kwake ila tabia yake mwenyewe."

Ghuraru 'l-Hikam, uk.80.

QUR'AN TUKUFU

Qur'an Tukufu, Surah An-Nahl, 16, Ayah 105, inasema wazi kwamba mwongo yuko nje ya jamii ya Waislamu:

﴿إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ﴾

Wanaozua uwongo ni wale wasioziamini ayah za Allah swt, na hao ndio waongo (hasa)!"

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)

Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema:

"Halahala na ukweli, kwani ukweli huongoza kwenye wema, na wema huongoza kwenye Jannat. Mtu haachi kusema ukweli na kutafuta ukweli mpaka aandikwe ni mkweli mbele ya Allah swt. Na jihadharini na uwongo, kwani uwongo huelekeza kwenye ufisadi, na ufisadi huelekeza kwenye Moto. Mtu haachi kusema uwongo na kufuata uwongo mpaka aandikwe ni mwongo mbele ya Allah swt."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 418.

Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema:

"Watu wenye kuwasadiki upesi wengine ni watu wenye kusema kweli kuliko wengine; na watu wenye kuwakadhibisha zaidi wengine ni watu wenye kusema uwongo kuliko wote."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 118.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Lau vitu vingeainishwa (kwa ulingano wao), ukweli ungekuwa pamoja na ushujaa, na uwongo ungekuwa pamoja na uwoga."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 605.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amejata matunda ya kusema kweli katika usemi mfupi huu:

"Msema kweli hujichumia vitu vitatu: kuaminiwa, kupendwa na kuheshimiwa."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 876.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Msidanganywe na sala na saumu zao, kwani huenda mtu akawa amezoea kusali na kufunga na endapo ataziacha ataona taabu. Hivyo, wajaribuni katika kusema ukweli na kuweka amana."

Usulu 'l-Kafi, jz. 1, uk. 460.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Tabia mbaya kabisa ni kusema uwongo."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 170.

AL IMAM HASAN ASKARI (A.S)

Al Imam Hasan Askari(a.s) amesema:

"Maovu yote yamewekwa katika nyumba moja, na ufunguo wake ni uwongo."

Jami'u 's-Sa'adaat, jz. 2, uk. 318.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Jihadharini na wanafiki, kwani wao ni wapotevu na wanapoteza (watu). Nyoyo zao zina maradhi lakini nyuso zao ni safi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 146.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Maneno ya mnafiki ni matamu lakini moyo wake ni maradhi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 60.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ametoa taswira nzuri ya mnafiki kwa kusema:

"Mfano wa mnafiki ni kama kondoo anayebabaika kati ya makundi mawili ya kondoo."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 562.

Mtume Muhammad(s.a.w.w) ametoa alama tatu za kauleni:

"Na mnafiki ana alama tatu: anaposema husema uwongo, anapotoa ahadi huvunja, na anapoaminiwa hufanya hiana."

Biharu 'l-Anwar, jz. 15, uk. 30.

AL IMAM MUHAMMAD BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad Baqir(a.s) amesema:

"Ni uovu mno kwa mja kuwa na nyuso mbili na ndimi mbili. Humsifu nduguye mbele yake lakini humsengenya nyuma yake. Akifanikiwa humwonea wivu, na akipata mashaka humtupa."

Biharu 'l-Anwar, jz. 15, uk.172.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mnafiki hujisifu mwenyewe na huwakejeli watu wengine."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 88.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amemdondoa Luqman akimwusia mwanawe haya:

"Mnafiki ana alama tatu: ulimi wake hukinzana na moyo wake, moyo wake hukinzana na vitendo vyake, na dhahiri yake hukinzana na batini yake."

Biharu 'l-Anwar, jz. 15, uk. 30.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Mtu mmoja alimwuliza Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) :

"Mtu mmoja alikuja kwangu na kuniambia kwamba ananipenda sana. Vipi nitajua kama kweli ananipenda sana?" Imam(a.s) akamjibu; "Tahini moyo wako. Ukimpenda, basi anakupenda. Tazama moyo wako. Ukimkataa mwenzako, basi mmoja wenu ana ila."

Al-Wafi, jz. 3, uk. 106.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Dhamiri safi ni ushahidi bora zaidi wa ukweli kuliko lugha fasihi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 501.

QUR'AN TUKUFU

Qur'an Tukufu, Surah Al Hujaraat, 49, Ayah 12, inatoa picha ya maana halisi ya usengenyaji katika jumla ndogo na fasihi:

﴿أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا ﴾

Je, mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa?"

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Mimi nimetumwa kukukuzieni na kukukumilishieni maadili mema."

Mtume Muhammad(s.a.w.w) amesema:

"Ukiwepo katika baraza ambapo mtu mmoja husengenywa, basi msaidie mtu huyo, au wakataze wasengenyaji, au ondoka hapo."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 48.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Mwenye kumtetea nduguye anayesemwa kwa ubaya wakati hayupo, hustahiki kwa Allah swt kuepushwa na Moto."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 613.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema pia:

"Mwenye kumsengenya Mwislamu, Allah swt hatazikubali funga na sala zake za mchana na usiku arobaini mpaka asemehewe na msengenywa Na mwenye kumsema Mwislamu katika Mwezi wa Ramadhani, hatapewa thawabu ya kufunga."

Biharu 'l-Anwar, jz. 16, uk. 179.

Mtume Muhammad(s.a.w.w) wa Waislamu amewasifu Waislamu kwa sifa hii:

"Mwislamu ni mwenye kuwasalimisha Waislamu kutokana na mikono na ulimi wake."

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Kumsengenya ni juhudi za mtu dhaifu."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 36.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Yatakikana muumin awe ni kiburudisho cha (roho ya) muumin (mwenzake) kama vile maji baridi yanavyokata na kutuliza kiu."

Al-Kafi, jz. 2, uk. 247.

AL IMAM MUHAMMAD BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad Baqir(a.s) amesema:

"Inatosha kuthibitisha aibu ya mtu anayeona aibu za watu wengine bila ya kuona yake mwenyewe, au anayewagombeza watu jambo ambalo yeye mwenyewe anashindwa kuliacha, au anayemwudhi rafiki yake kwa jambo lisilomhusu."

Al-Kafi, jz. 2, uk. 459.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ameonyesha nukta muhimu juu ya maudhui hii pale aliposema:

"Mtu bora kuliko wote mbele yako ni yule mwenye kukuonyesha aibu zako na kuisaidia nafsi yako."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 558.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye (kutaka) kutafuta aibu za watu, aanze na zake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 659.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Inatosha mtu kujifanya mpumbavu mwenyewe kwa kutazama aibu za watu wengine huku akizificha zake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 559.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema maneno matamu na yenye kuvutia kuhusu utambuaji na utibabu wa maradhi ya kinafsi kwa njia ya mtu mwenyewe kujichungua:

"Ni lazima kwa mwenye akili kuichungua nafsi yake na kuziona dosari zake katika dini, maoni, maadili na adabu; kisha azikusanye (azihifadhi) katika kitabu na achukue hatua ya kuziangamiza."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 448.

QUR'AN TUKUFU

Qur'an Tukufu, Surah An-Nisaa, 4, Ayah 32, inasema:

﴿وَلَا تَتَمَنَّوْا مَا فَضَّلَ اللَّـهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ﴾

Wala msitamani vile ambavyo Allah swt amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Asili ya kijicho ni upofu wa moyo na ukanyaji wa fadhila na neema za Allah swt. Sifa hizo ni mabawa mawili ya ukafiri. Kijicho humtia mwanadamu katika uchungu wa daima na humwangamiza kabisa kabisa asiokoke kamwe."

Mustadraku 'l-Wasa'il, jz. 2, uk. 428.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Watendeeni sawasawa watoto wenu mnapowapa zawadi."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 366.