HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)27%

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S) Mwandishi:
Kundi: Vitabu mbali mbali

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)
  • Anza
  • Iliyopita
  • 12 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 39078 / Pakua: 4594
Kiwango Kiwango Kiwango
HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W)PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

6

7

9

HADITHI ZA MTUME (S.A.W.W) PAMOJA NA MAIMAMU (A.S)

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ametaja madhara ya kimwili ya kijicho:

"Naustaajabia mghafala wa mahasidi juu ya uzima wa miili yao."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 494.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Kijicho huuangamiza mwili."

Ghuraru 'l-Hikam, uk.32.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Jihadharini na uhasidi, kwani huitia ila nafsi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 141.

AL IMAM ZAYNUL ABIDIN (A.S)

Al Imam Zaynul Abidin(a.s) alimwomba Allah swt hivi:

"Ewe Allah swt ! Teremsha rehema na baraka kwa Muhammad na Aali za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ; na nipe kifua kilichohifadhika na uhasidi, ili kwamba nisimwonee wivu yoyote kati ya viumbe Vyako juu ya fadhila Zako; wala nisione kijicho juu ya neema Zako ulizompa yeyote kati ya viumbe Vyako - ziwe ni neema za dini au dunia, afya au takwa, nyingi au nyepesi, ila kwamba nitamani bora zaidi kwa ajili yangu lakini kutoka Kwako peke Yako, (Ewe) usiye na mshirika."

Sahifah Kamilah, dua ya 22.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Shindaneni katika maadili yanayovutia, matumaini makubwa na mawazo matukufu ili mpate jazaa kubwa."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 355.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Lau Allah swt angeruhusu kiburi kwa waja wake, basi angewaruhusu Manabii na Mawalii Wake. Lakini Allah swt amewakataza kuwa na kiburi na amewaridhia kuwa na unyenyekevu. Hivyo, huweka videvu vyao juu ya ardhi (kumnyenyekea Allah swt), huzisugua nyuso zao kwenye ardhi, na huwanyenyekea waumini."

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Jiepusheni na kiburi, kwani mja anapotakabari, Allah swt husema: 'Mwandikeni mja huyu miongoni mwa waasi.'"

Nahju 'l-Fusahah, uk. 12.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) ametaja kwa ufupi asili ya kinafsi ya ndweo na majivuno:

"Hakuna mtu anayeugua kiburi ila kwamba amehisi uduni (dhila) nafsini mwake."

Al-Kafi, jz. 3, uk. 461.

Al Imam Musa bin Jaafar(a.s) amesema:

"Maringo na majivuno yana vidato; kimojawapo ni kumpambia mja amali yake mbaya akaiona nzuri na akaipenda na kufikiria kwamba amefanya vizuri."

Wasa'ilu 'sh-Shi'ah, jz.1, uk. 74.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Jihadhari na kujipenda (kujiona) mwenyewe, kwani utazidiwa na wenye kukuchukia."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 147.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Kiburi huharibu akili."

Ghuraru 'l-Hikam, uk 26.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye kudhoofisha fikra zake huimarisha ghururi yake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 651.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Unyenyekevu ni kiini cha akili, na majivuno ni kiini cha ujinga."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 102.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Kibur ni maradhi ya ndani."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 478.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye kuona bora mwendo wake, hushindwa kurekebisha nafsi yake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 677.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye kujipenda nafsi yake haoni aibu zake, na lau angejua mema ya wengine angetengeneza dosari na hasara zake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 95.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Jikingeni kwa Allah swt kutokana na ulevi wa utajiri, kwani una nishai (ulevi) inayochelewa kutoka."

Ghuraru 'l-Hikam, uk.138.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Siku moja tajiri mmoja alikwenda katika baraza la Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) Baadaye akaja maskini mmoja na akakaa karibu na tajiri huyo. Tajiri akakusanya nguo zake alipomwona maskini amekaa ubavuni mwake. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akamwambia tajiri:"Unaogopa umaskini wake ukuguse?" Tajiri akajibu: "Hapana!" Akamwuliza:"Unaogopa sehemu ya mali yako aipate yeye?" Akajibu:"Hapana!" Akamwuliza:"Unaogopa nguo zako ziingie uchafu?" Akajibu: "Hapana!"

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akamwuliza: "Basi kwa nini umezikusanya nguo zako na umekikunja kipaji chako ?" Tajiri akasema:"Ewe mtume wa Allah swt! Utajiri wangu na mali zangu zimenifumba macho yangu nisitambue uhakika, na zimenifanya niyaone mazuri yale mabaya yangu. Kwa kufuta kosa hilo lisilofaa, natoa nusu ya mali zangu kumpa maskini huyu." Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akamwuliza maskini:"Je, unaikubali tuzo hiyo?"

Maskini akakataa, na alipoulizwa sababu yake, akasema:"Naogopa nami pia nisiwe na sifa mbaya kama yake baada ya kuwa na utajiri mwingi."

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Wafanyieni uadilifu watoto wenu katika kutoa zawadi kama vile mtakavyopenda wakufanyieni uadilifu kwa mema na mapenzi."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 66.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Mcheni Allah swt na adiliana na watoto wenu kama vile mpendavyo wakutendeeni wema."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 8.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Wafanyie (Wamisri) uadilifu, endeana nao kwa upole, changamka nao, na fanya insafu katika kuwatazama pia ili kwamba watukufu wasitazamie dhuluma kutoka kwako wala wanyonge wasikate tamaa ya kuona uadilifu kutoka kwako." Mabalozi wa Allah swt ni waasisi wa uadilifu na waratibu wa sera ya ukamilifu wa mwanadamu. Katika zama za ukhalifa wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) , siku moja Aqil alikwenda kwa ndugu yake mtawala (yaani Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ). Baada ya kumwelezea matatizo yake na umaskini wake, akamshika nduguye (Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) .) ampe karibu mani moja (ratili mbili) ya ngano zaidi kuliko sehemu yake kutoka Baitul Maal (Hazina). Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) badala ya kumkubalia akamsogezea kipande cha chuma kilichopashwa moto ili kumwonya. Aqil akapiga kelele. Hapo Imam(a.s) akamwambia:

"Ewe Aqil! Mamako akulilie! Unapiga kelele hivyo kwa kuogopa kipande cha chuma tu kilichopashwa moto na mtu, lakini mimi nitavumilia vipi moto utakaowashwa kwa ghadhabu za Allah swt ? Je, inafaa wewe upige kelele kwa sababu ya kuungua mwili, nami nivumilie adhabu ya roho?"

Baada ya ya kusema hayo, akaongeza: "Wallahi! Hata kama nitapewa dunia nzima pamoja na utajiri wake wote ili kwamba nimnyang'anye siafu ganda la shayiri alilonalo mdomoni mwake, sitafanya hivyo kamwe! Mimi ni duni na haina thamani kuliko ganda hilo hata kutaka kumuudhi siafu."

Nahaj 'l-Balaghah, uk. 877.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Kutosamehe ni aibu mbaya kuliko zote, na kulipiza kisasi ni dhambi kubwa kuliko zote."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 537.

Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amewasifu waungwana wanasamehe makosa ya wengine, kwa kusema:

"Ni murua wa watukufu kusamehe makosa kwa haraka."

Ghuraru 'l-Hikam, uk.768.

Mambo mazuri na mabaya hayawi kamwe sawasawa katika dunia hii. Hivyo, ni afadhali kulipa ubaya kwa amali njema kabisa ili kwamba yule aliyekufanyia ubaya na uadui awe ni rafiki yako wa karibu.

Msamaha huwa na thamani kubwa sana wakati mtu anapokuwa na uwezo na nguvu za kulipiza.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) ameihesabu sifa hii tukufu kuwa ni miongoni mwa sifa njema za Mitume na wachaji:

"Msamaha wakati wa (kuwepo) uwezo (wa kulipiza ubaya) ni miongoni mwa mienendo ya Mitume na wacha-Mungu."

Safinatu 'l-Bihar, jz. 2, uk. 702.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ameutaja msamaha kama ni silaha bora kabisa ya kuwapigia wapinzani:

"Mlaumu nduguyo kwa (kumfanyia) mema, na jiepushe na shari yake kwa kumfadhili."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 1150.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amefichua uhakika wa ndani wa maana ya kinyongo na chuki kwa kutoa usemi mfupi:

"Moyo wa mwenye kinyongo ni mgumu kuliko nyoyo zote."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 178.

Wakati wa adhabu ya roho daima humtesa mwenye chuki.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Kinyongo huadhibu nafsi na huzidisha adhabu yake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 85.

. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Dhamiri zinapotibiwa ndipo siri zinapojitokeza na kuonekana."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 490.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Chuki ni moto wa ndani ndani usiozimika ila kwa ushindi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 106.

Chuki hukoka moto wa hamaki.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Chuki huwasha hasira."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 21.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye kuondoa chuki hutuliza moyo na akili yake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 666.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mja mwenye furaha ni yule ambaye moyo wake hauna chuki wala wivu."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 399.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Hamaki huziba (nuru ya) moyo wa mwenye hekima. Asiyeweza kuidhibiti hamaki yake hawezi kuitawala akili yake."

Usulu 'l-Kafi, jz. 2, uk. 305.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye kuiacha hamaki yake ipande, huharakisha mauti yake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 625.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Jihadhari na hamaki, kwani mwanzo wake ni wendawazimu na mwisho wake ni majuto."

Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Hamaki ni moto uliokokwa, mwenye kuipoza hamaki huuzima (moto wake), na mwenye kuiachilia huwa ni wa kwanza kuungua humo."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 71.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ametuusia tuwe na subira na uvumilivu ili tuweze kukabiliana na hasira na hamaki, kwa sababu tunavihitajia hivyo kuepukana na maumivu yake.

"Jilindeni kutokana na ukali wa hamaki na jiandaeni kupambana nao kwa kuvunja hamaki na kwa kuvumilia."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 133.

Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Kujidhibiti wakati wa kushikwa na hasira humsalimisha mtu wakati wa maangamizo."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 463.

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

"Kitu gani kilicho kiovu zaidi kuliko hamaki wakati mtu aliyepandwa na hamaki hutoa roho iliyoharamishwa na Mungu.?"

Al-Wafi, jz. 3, uk. 148.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ametoa mwongozo mzuri wa kufanya wakati mtu anapopandwa na hamaki:

"Ikiwa mmoja wenu atapandwa na hamaki, kama amesimama akae chini, na kama amekaa alale. Na kama hamaki haikupoa baada ya kufanya hivyo, basi atawadhe kwa maji baridi au aoge-kwani moto hauzimiki ila kwa maji."

Ahyau 'l-Ulumu 'd-Din, jz. 3, uk. 151.

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

"Allah swt hakumruhusu mtu yeyote kwenda kinyume katika mambo matatu: " Kuweka amana ya mwema au mwovu; " kutimiza ahadi ya mwema au mwovu; na " kuwatendea mema wazazi wema au waovu."

Al-Kafi, jz. 2, Uk. 162.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ametaja kuvunja ahadi kama ni alama mojawapo ya unafiki:

"Mwenye kuwa na sifa nne (zifuatazo) ni mnafiki; na hata akiwa nayo mojawapo kati ya hizo pia atasifika kwa unafiki isipokuwa aiache: " Mwenye kusema uwongo anapozungumza; " mwenye kuvunja ahadi anapoahidi; " mwenye kufanya hiana anapoaminiwa; na " mwenye kufisidi anapogombana."

Biharu 'l-Anwar, jz. 15, uk. 234.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ameandika:

"Jihadhari usiwasimange raia zako kwa hisani ulizowafanyia, wala usijione bora kwa ajili ya kazi unazowafanyia, na unapowaahidi usiende kinyume na ahadi zako. Hakika masimango huharibu hisani, na kujiona huondoa nuru ya haki, na kuvunja ahadi husababisha kuchukiwa na Allah swt na watu. Allah swt anasema: katika Qur'an Tukufu, Surah Ass'af, 61, Ayah 3 'Ni chukizo kubwa mbele ya Allah swt kusema msiyoyatenda."

Mustadriku 'l-Wasa'il, jz. 2, uk. 85.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Kutimiza ahadi hufuatana na uaminifu, nami sikijui kinga kinachokinga vizuri zaidi kuliko kutimiza ahadi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 228.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Mtu asimwahidi mwanae asipoweza kutimiza."

Nahju 'l Fasahah, uk. 201.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ameonyesha namna ya mtu kusuhubiana na mwenzake:

"Ukimchagua mtu kuwa rafiki yako, basi kuwa mtumishi wake na mwonyeshe uaminifu wako wa kweli na moyo safi."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 323.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Mwenye furaha kayaya kuliko watu wote ni yule mwenye kuingiliana na watu watukufu na ambaye huendeana na watu bila ya kuwadhulumu, huzungumza nao bila ya kuwadanganya, na huahidiana nao bila ya kuvunja. Hakika mtu kama huyu amekamilisha murua wake, amedhihirisha uadilifu wake, na anastahiki udugu na urafiki wake."

QUR'AN TUKUFU

Allah swt amezitaja sheria alizowatungia waja wake kama ni amana, na amekataza kabisa kufanya khiana ya aina yoyote: katika Qur'an Tukufu, Surah Al-Anfaal, 8, Ayah 27:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ﴾

Enyi mlioamini! Msimfanyie khiana Allah swt na Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) na mkakhini amana zenu na hali mnajua.

Vile vile Allah swt amesema: katika Qur'an Tukufu, Surah An-Nisaa, 4., Ayah 58:

﴿إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا﴾

Hakika Allah swt anakuamrisheni kuzirudisha amana kwa wenyewe.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema: Ghuraru 'l-Hikam, uk. 505. "Ukomo cha khiana ni kumfanyia khiana rafiki mpendwa na kuvunja ahadi." Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: Ghuraru 'l-Hikam, uk. 446. "Mtu mwovu kuliko wote ni yule asiyeamini kuweka amana wala hajizuii kufanya khiana."

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Jihadharini na khiana kwani ni dhambi mbaya kabisa; na kwamba mwenye kukhini ataadhibiwa katika Moto kwa khiana yake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 150.

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Halahala na kusema ukweli na kurejesha amana kwa mwema au mwovu, kwani sifa mbili hizi ni ufunguo wa riziki."

Safinatu 'l-Bihar, jz. 1, Uk. 41.

AL IMAM ZAYNUL ABIDIN (A.S)

Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Halahala na kuweka amana. Naapa kwa yule aliyembaathi Muhammad kwa haki kuwa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , kwamba lau mwuaji wa babangu Husayn bin Ali angenipa upanga ule aliomwulia bababngu, kumwekea amana, nisingemfanyia khiana."

Amali as-Sadaq, uk. 149.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Mwenye kutenda kitendo kiovu atalipwa (hapahapa) duniani."

Nahju 'l-Fasahah, Uk. 592.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Uaminifu katika (kuweka) amana ni alama ya usafi wa mwenye imani."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 453.

Vile vile Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Khiana ni dalili ya upungufu wa uchaji na utovu wa dini."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 53.

AL IMAM SAJJAD (A.S)

Al Imam Sajjad(a.s) amesema:

"Una wajibu wa kumlea (Mwanao) kwa adabu nzuri, kumwongoza kwa Mola wake Mtukufu, na kumsaidia katika kumtii."

Al-Wafi, uk. 127.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Wenye akili huhitajia adabu kama vile shamba linavyohitajia mvua."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 224.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Hakuna jambo linalochukiwa mno katika Uislamu kama uchoyo."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 549.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Mwenye kuwa na raha kidogo kabisa kati ya watu wote ni bakhili."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 81.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Allah swt amrehemu mtu anayebana mengi (ziada) ya maneno yake, na anayetoa ziada ya mali yake."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 81.

Vile vile Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Jihadhari na uchoyo, kwani uchoyo umewaangamiza waliokutangulia, umewafanya wamwage damu zao, na wahalalishe yaliyoharamishwa."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 8.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Nashangaa juu ya bakhili mwovu; huuharakisha umaskini anaokimbia na huupoteza utajiri anaotafuta. Huishi katika dunia maisha ya maskini na atahukumiwa katika Akhera kwa hesabu ya matajiri."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 497.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Ukarimu wa mtu huwafanya maadui zake wampende, na ubakhili wake humfanya achukiwe na watoto wake."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 368.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Uroho na uchoyo umesimama juu ya msingi wa shaka na kutoaminiwa."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 488.

AL IMAM MUSA AL-KADHIM (A.S)

Al Imam Musa al-Kadhim(a.s) ameelezea juu ya thamani ya ukarimu:

"Karimu mwenye murua yuko katika ulinzi wa Allah swt; na Allah swt hamwachi mpaka amtie Peponi. Allah swt hamtumi Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) wala Wasii yeyote ila kwamba huwa ni karimu; wala hakutokea mwema yeyote ila kwamba alikuwa karimu. Babangu hajafariki mpaka aliponiusia ukarimu."

Furu' al-Kafi, jz. 4, uk. 38.

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) ameshabihisha maisha ya mroho na taswira hii:

"Mfano wa mwenye tamaa ya dunia ni kama kiwavi cha nondo, kila akizidi kujizungushia nyuzi (za hariri) ndivyo hujifungia mpaka kufa kwa kujisonga roho."

Usulu 'l-Kafi, Babu ya Huba ya Dunia.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Jihadharini na uchu wa mali, kwani uliwaangamiza waliokutangulieni. Uchu uliwashawishi mabakhili na wakafanya ubakhili; uliwaamrisha kukata ujamaa na wakakata; na uliwaamrisha ufisadi na wakafanya ufisadi."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 199.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Epukaneni na mwenye tamaa, kwani kuingiliana naye huleta udhalili na mashaka."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 135.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Mwenye tamaa ni mfungwa wa udhalili na kifungo chake hakifungiki."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 50.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) ameashiria jambo hili kwa usemi murua:

"Mtukufu kuliko wote ni yula ambaye hukata tamaa (juu ya watu), hushika ukinaifu na uchaji, na huacha uroho na tamaa, kwani tamaa na uroho ni sawa na umaskini, na kukata tamaa (juu ya watu) na ukinaifu ni utajiri wa dhahiri."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 255.

Anayejifanya mtumwa wa tama na uchu, huutia maradhi mwili na roho yake.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) anasema:

"Kila mwenye tamaa ni mgonjwa."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 544.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema;

"Tamaa huchafua nafsi, huharibu dini (imani) na huondoa uungwana."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 77.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ametaja matatizo yanayotokana na tamaa:

"Mwenye tamaa husumbuliwa na matatizo saba mabaya:

1. Fikra inayomdhuru mwili wake na isiyomnufaisha;

2. hamu (hima) isiyokwisha;

3. tamaa isiyompa raha ila baada ya kufa na wakati wa kupumzika huona taabu zaidi;

4. hofu isiyoacha kumhangaisha;

5. huzuni inayofanya maisha yake machungu bila ya kuwa na faida;

6. hesabu isiyomsalimisha na adhabu ya Allah swt ila asemehewe na Allah swt; na

7. adhabu asiyoweza kuikimbia wala kuiepuka."

Mustadriku 'l-Wasa'il, jz. 2, uk. 435.

AL IMAM 'ALI IBN ABI TALIB (A.S)

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

"Tamaa humsukuma mtu kwenye mabaya."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 16.

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) vile vile amesema:

"Matokeo ya tamaa ni kumtia mtu katika aibu."

Ghuraru 'l-Hikam, uk. 360.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

"Miongoni mwa (alama za) uungwana ni mtu kunyamaza kimya na kumsikiliza ndugu yake anaposema."

Nahju 'l-Fasahah, uk. 633.

AL IMAM MUHAMMAD AL-BAQIR (A.S)

Al Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

"Na jifunze kusikiliza vizuri kama vile unavyojifunza kusema vizuri, wala usimkatize mtu yeyote anaposema."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Mja hataipata imani halisi mpaka atakapoacha ubishi hata kama ni haki."

Safinatu 'l-Bahar, jz. 2, uk. 522.

AL IMAM HAD (A.S)

Al Imam Had(a.s) amesema:

"Ubishi huharibu urafiki wa muda mrefu, huvunja uhusiano ulio madhubuti, na sehemu ndogo ya kitu kinachopatikana ni mashindano - na mashindano yenyewe ni chanzo hasa cha kutosikilizana."

AL IMAM JA'AFER AS-SADIQ (A.S)

Al Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

"Epukaneni na mabishano, kwani huunguza moyo, huleta unafiki na husababisha chuki."

Usulu 'l-Kafi, jz. 1, uk. 452.

MTUME MUHAMMAD MUSTAFA (S.A.W.W)

Mtume Mtukufu(s.a.w.w) amesema:

"Hakika,miongoni mwa dalili za saa, ni kuwa

1. watu watapuuza sala

2. watafuata matamanio yao wenyewe

3. wataelekeza kujipendelea wao wenyewe, watawaheshimu matajiri,

4. na watauza Dini yao kwa manufaa ya kidunia

5. wakati huo roho na moyo wa Muumin itayayuka (kwa huzuni) kama chumvi inavyoyayuka katika maji, kwa sababu ataona mambo yaliyoharamishwa na hataweza kuyabadili."

Salman akasema: "Haya yatatokea, ewe Mtume wa Allah swt?" Mtume Mtukufu(s.a.w.w) akasema:"Ndiyo, naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake." "Ewe Salman ,

6. wakati huo watawala watakuwa wadhalimu

7. Mawaziri watakuwa waasi,

8. na wadhamini (wale waliopewa amana kwa kuaminiwa) watafanya hiana,

9. hakika wakati huo maovu yatakuwa mema na mema yatakuwa maovu,

10. wale wafanyao hiana wataaminiwa na waaminifu watafikiriwa kuwa si waaminifu;na mwongo atasadikiwa,na msema kweli atahesabiwa mwongo.

11. Wakati huo kutakuwapo na utawala wa wanawake,

12. Masuria watashauriwa,

13. na watoto watakaa juu ya mimbar,

14. udanganyifu utahesabiwa kuwa ni uerevu

15. na Zaka itakuwa ni kama kutozwa faini;na mateka ya vita (yaani mali ya ummah) yatakuwa kama ni mali ya mtu binafsi;na mtu atakuwa mjeuri kwa wazazi wake na atakuwa mwema kwa marafiki zake,

16. na wakati huo kutatokea na nyota zenye mikia (comets)."

Salman akasema: "Haya yatatokea,ewe Mtume wa Allah swt?" Mtume Mtukufu(s.a.w.w) akasema:"Ndiyo,naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi mwake." "Ewe Salman!

17. wakati huo mwanamke atakuwa mshiriki wa mumewe katika biashara,

18. na mvua itakuwa moto sana

19. na watu wema watabaki katika huzuni;na masikini hawata heshimiwa;na wakati huo masoko yatakaribiana,

20. Tena huyu atasema,"Mimi sikuuza chochote,na yule atasema, "Mimi sikupata faida yoyote." Kwa hivyo hutamkuta mtu yeyote asiyemlalamikia Allah swt.

"Ewe Salman!

21. tena itatokea iwapo watu watawazungumzia watawala wao, watawaua, na ikiwa watanyamaza kimya, watanyang'anywa mali yao, watanyimwa heshima zao,watamwaga damu yao na mioyo ya watu itajaa woga;kisha hutamwona mtu yeyote ila atakuwa mwoga,mwenye khofu,ametishika na ameshstushwa" "Ewe Salman!

22. Bila shaka wakati huo mambo fulani yataletwa kutoka Mashariki

23. na mambo fulani yataletwa kutoka Magharibi,

24. Basi ole kwa watu walio dhaifu (wa imani) katika Ummah wangu kutokana na hayo; Ole ya Allah swt iwe kwa hayo. Wao hawatakuwa na huruma juu ya wadogo

wao,wala hawatamsamehe yeyote aliyefanya kosa.Miili yao itakuwa ya wanadamu,lakini mioyo yao itakuwa ya mashetani."

"Ewe Salman!

25. Wakati huo wanaume watawaashiki wanaume,

26. na wanawake watawaashiki wanawake;

27. na watoto wa kiume watapambwa kama wanawake;

28. na wanaume watajifanya kama wanawake

29. na wanawake wataonekana kama wanaume;

30. na wanawake watapanda mipando

31. Hapo tena patakuwepo laana ya Allah swt juu ya wanawake wa Ummah wangu."

"Ewe Salman!

32. Bila shaka wakati huo Misikiti itapambwa (kwa dhahabu n.k.) kama inavyofanywa katika masinagogi na makanIssa,

33. na Qur'an zitapambwa (kwa nakshi na rangi za kupendeza n.k.)

34. na minara (ya misikiti) itakuwa mirefu;na safu za watu wanaosimama katika sala zitazidi,lakini nyoyo zao zitachukiana na maneno yao yatatofautiana."

"Ewe Salman!

35. Wakati huo wanaume watatumia mapambo ya dhahabu;kisha watavaa hariri,na watatumia ngozi za chui."

"Ewe Salman!

36. Wakati huo riba itakuwako,

37. na watu wata- fanyia biashara kwa kusemana na rushwa

38. na dini itawekwa chini,na dunia itanyanyuliwa juu."

"Ewe Salman!

39. Wakati huo talaqa zitazidi

40. na mipaka ya Allah swt hayatasimamishwa

41. Lakini hayo hayatamdhuru Allah swt."

"Ewe Salman!

42. Wakati huo watatokea wanawake waimbaji,

43. na ala za muziki

44. na wabaya kabisa watawatawala Ummah wangu."

"Ewe Salman!

45. Wakati huo matajiri katika Ummah wangu watakwenda Kuhiji kwa matembezi,na walio wastani kwa biashara,na masikini kwa kujionyesha.

46. Hivyo basi wakati huo watakuwapo watu ambao watajifundisha Qur'an si kwa ajili ya Allah swt na wataifanya Qur'an kama ala ya muziki.

47. Na watakuwapo watu ambao watasoma dini si kwa ajili ya Allah swt

48. na idadi ya wanaharamu itazidi

49. watu wataiimba Qur'an,

50. na watu watavamiana kwa uroho wa kidunia."

"Ewe Salman!

51. Haya yatatokea wakati heshima zitakapo- ondoka,na madhambi yatatendwa

52. na watu waovu watakuwa na uwezo juu ya watu wema,

53. na uongo utaenea na mabishano (matusi) yatatokea

54. na umasikini utaenea,

55. na watu watajiona kwa mavazi yao

56. na itakuwepo mvua wakati si wake

57. na watu watacheza dama, kamari na Ala za muziki,

58. na hawatapenda kuhimizana mema wala kukatazana maovu

59. na kwa ajili hali itakavyokuwa hata itafikia wakati huo kuwa Muumin atakuwa na heshima ndogo kuliko hata mjakazi

60. na wanaosoma na wanaotumia wakati wao katika kumwabudu Allah swt watalaumiana.

61. Hao ndio watu watakaoitwa wachafu na wanajisi katika Ufalme wa mbinguni."

"Ewe Salman!

62. Wakati huo matajiri hawataogopa chochote isipokuwa mtu masikini; hadi kwamba masikini wataendelea kuomba kati ya ijumaa mbili,na hawatamwona mtu yeyote wa kutia chochote mikononi mwao."

"Ewe Salman!

63. Wakati huo itazungumzwa Ruwaibidhah."

Salman akauliza:"Ni nini Ruwaibidhah ? Ewe Mtume wa Allah swt, baba na mama yangu wawe fidia kwako."

Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) akajibu:

64. "Watu fulani watazungumza kuhusu mambo ya watu ambayo hayakuwahi kuzungumzwa namna hii zamani.

65. Tena baada ya muda mchache machafuko yatatokea duniani,na kila nchi itafikiri kuwa machafuko yapo katika nchi yao tu."

66. "Watabaki katika hali hiyo kwa muda ambao Allah swt atapenda wabaki;

67. kisha ardhi itatapika vipande vya moyo wake dhahabu, fedha na madini mengineyo; (Hapo Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w.) alinyosha kidole chake penye nguzo, na akasema:"Kama hizi (kwa ukubwa), lakini siku hiyo dhahabu wala fedha hazitamsaidia mtu yeyote. Na hii ndiyo maana ya maneno ya Allah swt 'Hakika dalili Zake zimekuja. '

UBASHIRI WA IMAM JAAFER AS-SADIQ (A.S)

Mazungumzo yafuatayo yamefanywa na Imam Jaafer as-Sadiq(a.s) ambamo ameripoti ubashiri wa siku za mwisho wa dunia hii. Yametolewa kutoka Darul Islam,Bihar-ul-Anwar na Raudhat-ul-Kafi. Wanaoripoti habari hizo ni Allamah Naraqi na Sheikh Kulaini r.a. kutokea kwa Himran.

Imam(a.s) alisema:

1 "Haki itakuwa imetokomezwa na watu walio katika haki hawatapatikana.

4. Dhulma na uonevu utaenea katika miji yote.

5. Kufuata Qur'an kimatendo itajulikana kama tabia ya kizamani.

6. Zitatolewa maana ya Aya za Qur'an kwa mujibu wa matakwa ya watu,hivyo mafhum ya Qur'an itakuwa imebadilishwa na kupotoshwa.

7. Wadhalimu watakuwa wakiwa kandamiza wale walio katika haki.

8. Uchokozi na uchochezi utatokea kutoka kila pande na pembe.

9. Matendo maovu na kukosa aibu vitaenea na kuzagaa kila mahala.

10. Ulawiti utakuwa ni jambo la kawaida.

11. Muumin atakuwa akionekana kama mtu dhalili ilhali waovu watakuwa wakiheshimiwa

12. Vijana hawatakuwa wakiwaheshimu wakubwa wao.

13. Huruma itakuwa imepotea kabisa.

14. Waovu watakuwa wakitukuzwa kwa udhalimu wao na hakutakuwapo na mtu yeyote wa kuwapinga.

15. Wanaume watafurahishwa mno kwa kuingiliana na wanaume wenzao.

16. Wanawake watawaoa wanawake wenzao.

17. Mapesa yatatumika kwa ajili ya matumizi yale yaliyo haramishwa na Allah swt.

18. Starehe, anasa na zinaa zitashamiri.

19. Zinaa itajulikana kama maadili yaliyopitwa na muda.

20. Muumin atatengwa kwa sababu ya kufanya ibada za Allah swt.

21. Jirani mmoja atafurahi mno kwa kumuudhi na kumbughudhi jirani mwenzake.

22. Wazushi (kama Salman Rushdie wa Uingereza) watatukuzwa na kusifiwa katika kueneza fitina na yale wanayozusha.

23. Ushauri mzuri utakanwa.

24. Milango ya wema yatafungwa wakati milango ya maovu yatafunguliwa.

25. Al-Kaaba haitatumika au haitafikika kwa sababu ya vikwazo na ugumu utakaowekewa mahujaji.

26. Watu watalazimishwa kuacha kwenda Makkah kuhiji.

27. Watu hawatakuwa wakitimiza ahadi zao watakazokuwa wakizitoa.

28. Wanaume watakuwa wakitumia dawa za kuamsha tamaa za kiume kwa ajili kulawiti na wanawake watakuwa wakitumia vyakula vya mafuta ili kujitayarisha kwayo.

29. Baadhi ya wanaume watakuwa wakiishi kwa kujipatia mapesa kwa kuuza mikundu yao.

30. Na wanawake watakuwa wakijipatia mapesa kwa kufanyisha biashara kuma zao.

31. Wanawake wataunda vilabu vyao,mashirika na umoja wao.

32. Wanaume atajigeuza kama wanawake na watavutia na wanawake.

33. Wanaume watajirembesha kama wanawake.

34. Ulawiti utachukuliwa kama ndiyo ustaarabu na starehe ya kweli.

Na Banu Abbas watalipia ulawiti.

35. Wanawake wataona fakhari kwa kuwa na waume nje ya mume mmoja wa ndoa na vivyo hivyo wanaume watakuwa hivyo hivyo.

36. Heshima itakuwa ikitolewa kwa utajiri wa mtu na wala si ucha Mungu.

37. Riba ndiyo itakayokuwa biashara ya kila siku.

38. Ushahidi wa uongo utakuwa ukIssadikiwa mno.

39. Kile alichokiharamisha Allah swt kitachukuliwa ni halali na chochote kile alichokihalalisha Allah swt kitachukuliwa ni haramu.

40. Maamrisho ya Dini yatageuzwa kwa mujibu wa matakwa yao.

41. Wachokozi na waovu watatenda maovu kwa udhahiri bila ya khofu yoyote ile na Muumin hawataweza kuwazuia vyovyote vile.

42. Watawala watawapenda mno Makafiri kuliko Muumiin.

43. Rushwa ndiyo itakuwa njia ya kujitimizia kazi kutoka maofIssa wanaohusika.

44. Wanaume wata walawiti wake zao.

45. Watu watakuwa wakiuawa kwa visingizio vidogo vidogo na magomvi madogo madogo.

46. Wanawake watawafanyia wanaume dhihaka, nao watashawishiwa kufanya uhusiano na wanawake.

47. Wanaume wataishi kwa mapato ya wake zao zitakazopatikana kwa zinaa.

48. Wanawake watakuwa wakiendesha hukumu majumbani huku wanaume wakiwatii wake zao kwa sababu wanawake hao ndio watakuwa wenye mapato.

49. Wanawake watatumiwa katika kupatikana huduma mbalimbali.

50. Kula kiapo kwa jina la Allah swt litakuwa ni jambo lililowekwa ulimini.

51. Pombe na kamari vitapatikana kila mahala na vitakuwa vimezagaa.

52. Wanawake wa Kiislamu wataingiliana na Makafiri,ambapo Waislamu hawataweza kuwazuia na wala hawatakuwa na uwezo kama huo.

53. Maadui wetu watasaidiwa na watawala na marafiki zetu watadhalilishwa kiasi kwamba hata kiapo chao hakitakubaliwa.

54. Udanganyifu na hila ndizo zitakuwa desturi miongoni mwa watu.

55. Usomaji na usikilizaji wa Qur'an utakuwa ni bughudha kwa watu.

56. Kusikiliza mambo fidhuli ndiyo itakuwa ikipendelewa na watu.

57. Jirani hatamstahi jirani mwenzake illa kwa khofu ya ulimi mkali na mchafu.

58. Sheria na kanuni za Allah swt hazitatambuliwa na waovu hawataadhibiwa kwa maamrisho hayo.

59. Ghiba na kulaghaiana ndivyo vitakuwa vitu vya kawaida.

60. Madhumuni ya Hajj na Jihad yatakuwa mbali na yale ya Kiislamu.

61. Misikiti itarembeshwa kwa dhahabu.

62. Watawala watawataka ushauri kwa nia ya Makafiri.

63. Litakuwa ni jambo la kawaida kuibia katika uzani na vipimo vya biashara.

64. Kumwaga damu ya watu wegine litakuwa ni jambo la kawaida.

65. Watu watajigamba kwa ndimi zao chafu zenye matusi mabaya ili kuwatishia watu wengine.

Imam a.s. aliendelea kusema:

66. "Watu watakuwa wakipuuzia sala na kutojali.

67. Watu hawatakuwa wakilipa zaka ingawaje watakuwa na utajiri mkubwa.

68. Sanda za maiti zitakuwa zikiibiwa na kuuzwa tena.

69. Mauaji yatakithiri mno kiasi kwamba hata wanyama pia wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe.

70. Watu watakuwa wakIssali katika mavazi ya kiajabu.

71. Macho na mioyo itapoteza nuru zao za heshima na huruma.

72. Watu watakuwa wamejishughulisha na maswala ya kutafuta mali na mapesa tu.

73. Watu watasali kwa kuonyesha tu.

74. Watu watatafuta ilimu ya Dini kwa ajili ya kujipatia mali ya dunia.

75. Ushirika katika makundi yatakuwa ndiyo mambo ya maisha.

76. Wale watakaojipatia riziki kwa njia ya halali,watasifiwa kwa midomo tu.

77. Matendo maovu na machafu yataenea hata Makkah na Madina.

78. Watu waliokufa watafanyiwa mizaha na vichekesho.

79. Mwaka hadi mwaka hali itakuwa ikiendelea kuharibika kuwa mbaya zaidi.

80. Matajiri wataigwa.

81. Masikini, mafukara watafanyiwa dhihaka na kufedheheshwa.

82. Matukio ya kudura kama yale ya mitetemeko,maporomoko n.k. yatakuwapo lakini watu watakuwa hawaviogopi.

83. Matendo maovu yatakuwa yakitendwa kiwaziwazi.

84. Wazazi watatupa watoto wao na watoto watawatusi wazazi wao na daima watakuwa wakitaka mali na utajiri wa wazazi wao.

85. Wanawake hawatawatii na kuwafuata waume wao.

86. Siku itakayopita bila ya mtu kutenda madhambi,basi itachukuliwa ni siku yenye nuksi.

87. Watu wenye uwezo wataficha mali muhimu na kuviuza kwa bei ya ulanguzi.

88. Waombaji na walaghai watajumuika katika kucheza kamari na kulewa.

89. Pombe itatumika kama ni kitu chenye kuponya i.e.dawa.

90. Makafiri watatukuzwa juu ya watu wengine na Muumin watadhalilishwa na kupuuzwa.

91. Kutafanywa malipo kwa ajili ya kutoa Adhan na sala.

92. Misikiti itajaa kwa watu wasiokuwa na khofu ya Allah swt.

93. Watu wenye fahamu na akili kasoro ndio watakaokuwa wakiongoza sala za jamaa' na watu kama hao kamwe hawatashutumiwa au kusutwa na badili yake wataheshimiwa."

2

MUANDAMO WA MWEZI

SURA YA PILI

JAWABU KWA WANAFUNZI WA BACHOO JAWABU YA UTANGULIZI

Wahusika ndugu zetu wa Masjid Al-Sunna Zanzibar, wameanza kitabu chao hicho kwa utangulizi wenye kumshukuru na kumuhimidi Allah na kumtakia rehema na amani Bwana wetu Muhammad (s.a.w.) kama zilivyo khutuba na vitabu vya kiislamu. Na hayo yote yamefanyika chini ya utangulizi wenye anwani:

UKWELI JUU YA KUANDAMA KWA MWEZI

Na hii ndio sehemu ya kwanza ya kitabu chao. Wakasema katika utangulizi huo: Msisitizo wetu mkubwa katika kitabu hiki ni ile nukta muhimu ya kwamba suala la kufunga na kufungua kwa muandamo mmoja kwa dunia nzima si jambo jipya kama wanavyodhani baadhi ya watu, ni jambo la kale mno ambalo linaweza kutekelezeka na kwamba huo ndio uliokuwa msimamo wa 'Jamhur' ya wanavyuoni.

Jawabu Nakubali kuwa hili ni jambo la zamani, lakini kudai kuwa hii ni kauli ya Jumhuri ni madai hewa: hayana ushahidi. Leo hii duniani hakuna madhehebu yoyote ambayo inaitendea kazi kauli hio kama ni madhehebu nzima, bali kuna baadhi ya watu tu katika kila madhehebu ambao wanafata kauli hio. Hata zile madhehebu ziliotajwa kuwa ni zenye kufata kauli hio kama vile Malik, Hanbal na Hanafi, basi hawaitendei kazi kauli hio ila baadhi yao tu. Libya, Algeria na nchi nyengine za Afrika Kaskazini na Magharibi - kwa mfano - ni nchi za wafuasi wa madhehebu ya Malik, nao wanafata miandamo yao wenyewe. Kwa hivyo, dai kuwa hii ni kauli ya Jumhur ya wanavyuoni, si dai sahihi.

SEHEMU YA PILI

Katika sehemu ya pili, ndugu waandishi wanasema:

2. Si Fikra Za Shaykh Naaswir Bachuu "Ndugu yetu Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui amejitahidi kuandika kitabu alichokiita: "Ushahidi Uliowekwa Wazi Katika Suala La Miandamo Ya Mwezi. Makusudio yake yalikuwa ni kutaka kukijibu kitabu kilichoandikwa na Shaykh Naaswir Abdullah Bachuu kinachojulikana kwa jina la "Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi."

Jawabu Kidogo na mimi naomba niweke wazi kwamba kitabu changu hakikuwa kabisa na lengo la kujibu kitabu cha Sheikh Nassor Bachoo. Hili la kunukuu maneno yake na kuyajadili lilikuwa ni jambo la kutokea tu baada ya mtu Fulani kuniletea kitabu chake. Kwa havyo, kama mulivyosema nyinyi katika kitabu chenu kwamba: Kitabu hiki ni kama nasaha kwa Waislamu wote ili kuweza kudumisha umoja wetu hususan pale ambapo pamejitokeza misimamo tofauti katika mambo ya ibada. Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili.

Basi na mimi nakuombeni munielewe hivyo hivyo, kwamba wakati mimi naikubali fikra Fulani na kuikataa fikra Fulani, hakuna budi ninukuu fikra pinzani na kuonesha kwanini siikubali; na kwa upande wa pili ni lazima nioneshe kwanini naikubali fikra ninayoikubali. Na nitaposema kuwa kuna watu wana fikra hii, basi nadhani haitokuwa jambo la busara kama watu hao sikuwataja na nikiwataja ni lazima nitaje marejeo. Kwa sababu hii ndio maana nimekuwa nikinukuu maelezo ya Sheikh wetu Nassor Bachoo na kumjadili mule nisimokubaliana naye. Naomba musihuzunike kwani kujibizana katika kutafuta ukweli ni suala mashuhuri katika uwanja wa elimu. Wanavyuoni wakubwa wa kale na wa sasa wamekuwa wakijibizana ili kutafuta ukweli na hatimae huwabainikia woa pamoja na wasomaji. Kwa hivyo, hamukuwa na haja ya kutumia lugha: "Wala hapakuwa na lengo la kumkashifu": hii si kashfa hata kidogo: hii ni elimu.

Lakini, hakuna haja ya kufichana; kitabu chenu mumeandika kwa kujibu kitabu changu. Hamuna haja ya kusema: "Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili", kwani kitabuchenu kimeanza kwa kunitaja mimi mwanzo hadi mwisho na kuniaga kwa kunipa nasaha mimi. Ama mimi naandika jawabu hii kukujibuni nyinyi: sikufichini wala sisemi uwongo.

Munasema Kutokana na jambo hilo , sisi kwa upande mmoja tunashukuru kwa juhudi yake hiyo na kwa upande wa pili tunatuma masikitiko yetu kwake kwa kutokuwa makini na muadilifu katika kulifafanua jambo hilo muhimu. Kwani kitabu chake hicho kimeandikwa katika mfumo wa chuki, kibri, kejeli na malumbano huku akisisitiza kwa mara nyingi kauli chafu ambazo muandishi hapaswi kuzitumia katika kitabu au katika mijadala ya Dini. Jawabu Hizi chuki, kibri na kejeli, mimi nimezisoma kwenu, kwa hivyo na iwe kama msemo wa Waswahili: "Papa akipea mafuta huwapa wanawe". Je nyinyi munayakumbuka haya:

1) Munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo ambao alisema kuwa wasionyanyua mikono katika sala wanasali kama mipopoo? Jamani! Hii si kejeli? Je katika nyinyi yuko aliyetoa muhadhara au kuandika kitabu ili kumjibu Sheikh wetu. Sasa uadilifu uko wapi?

2) Je munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo aliozungumzia mas-ala ya udhu kasha akasema: "Wengine wakitia udhu kiungo hiki huomba dua hii na kiungo hiki huoma dua hii; upumbavu mtupu". Je haya si matusi? Je hii si kejeli?

3) Siku moja palikuwa na maziko. Maiti alisaliwa msikiti wa wajiitao "Watu wa Sunna". Kijana mmoja akasimama akasema: "Leo tunataka kukuonesheni vipi Mtume (s.a.w.) kamsalia maiti: si kama wanavyofanya Ibadhi na Shia.

4) La nne ni kuwa ikiwa nyinyi mumethubutu kunita mjeuri, mwenye kibri na kejeli; maneno ambayo mimi sikukwambieni wala kumwambia Sheikh Nassor; mimi nimemtoa makosa tu Sheikh wetu: na hii ni kawaida katika uwanja wa elimu; sasa je na nyinyi pia ni majeuri, wenye kibri na kejeli? Katika uwandishi wenu, pia mumesema: "Hatujui dhana hii potofu ameitoa wapi." Mwenye dhana potufu naye ni mpotufu, kwa hivyo na nyinyi hamukutoa nasaha bali mumetukana. Nakupeni mifano hii mitatu ya Sheikh wetu na mmoja wenu nyinyi wenyewe enyi wenye kuandika Radan mardudan na mifano iko mingi. Inatosha kuwaita kwenu watu wengine kuwa ni watu wa bidaa na nyinyi ndio watu wa Sunna. Kwa hivyo, hii hali mumeiuda nyinyi wenyewe: Zanzibar bali Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla haikuwa hivi. Chuki mumeziunda nyinyi; mukijirekebisha kwa kutumia lugha nzuri nadhani hakuna atayekwambieni jambo kwa lugha nzito.

Mnasema Mfano wa kauli zake mbaya ni kama zifuatazo:

(vuta-nikuvute) [uk. 6]

(hii ni ajabu katika ajabu za dunia!) [uk. 124]

(Kwa hivyo, uwezekano huo alioutoa Sheikh hauwashi wala hauzimi [uk. 124]

(Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja,)

(Utaona kwamba masuala yote haya si yenye kima katika soko la elimu, bali ni masuala ya kuwababaisha watu wasiojua nini cha kujadiliwa katika mas-ala haya ya funga) [uk. 167]

(Hoja nyengine - nayo pia ni hoja ya mitaani - ni kuwa watu wengi wa kawaida wanapouona mwezi mkubwa husema: "E basi ule ndio mwezi wa leo ule?!!!")

(Jawabu hii ya mwisho, inaufanya upinzani mzima wa Sheikh Bachoo kuwa hauna maana yoyote.) [uk. 132]

(Kwa ufupi ni kuwa hicho walichokidai watetezi wa rai pinzan) [uk. 32]

(utaona jinsi gani mwanamume alivyokuwa bingwa wa kubadilika! Na hili si jengine bali ni lile Waswahili wanalolisema: "Mfa maji hukamata maji.") [uk. 128]

(Hakuna hapa kinachoonesha mas-ala ya kufunga kwa muandamo mmoja wala kumi na moja.)) [uk. 125] (haina maana kwamba usiku ukiingia sehemu moja ndio umeingia dunia nzima. Kwa ufupi ni kuwa hii ni hoja ambayo haina faida yoyote ya kielimu, lakini tunaijadili kwa ajili ya watu wa mitaani tu.)

Jawabu Sikubaliani na nyinyi kwamba humu muna maneno mabaya. Lakini hata nikikubali basi nasema kwamba lugha ya namna hii sababu ni nyinyi, na kwa hivyo, utaona kwamba ninapojadiliana na watu wengine basi lugha yangu hubadilika. Kwa hivyo, tujirekebisheni sote na tujadili tafauti zetu kwa lugha ya kiungwana. Ama ukinita mpopoo, basi usinilaumu na wewe nikikwita mnazi: unanilaumu nini na wewe unakifanya kile kile nikifanyacho?! Bali hata katika kitabu hiki munachonijibu, basi nanyi mumetumia lugha hizo hizo. Katika baadhi ya sehemu umesema: "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti..". Na mwishoni mwa kitabu mumesema: "Dhana ya pili ya ndugu Juma imejengeka katika msingi dhaifu wala haina nafasi katika uwanja wa fani (kitaalamu) nao ni kule kusukuma kwake juu ya elimu ya Jiografia". Na yamo mengi katika kitabu chenu. Sasa nyinyi mwasema nini na mwatenda nini?

Munasema "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti: Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi i likuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini? Na ni nani aliyemwambia kwamba jambo lenye khitilafu halizungumzwi? Yeye angezungumza nini katika kitabu chake kama si masuala ya ikhtilafu? Pia anatwambia haya ni katika mambo ya furui (matawi) za Kidini, kwa hivyo zisizungumzwe. Kwani ni nani aliyemwambia kuwa furui za Kidini hazizungumzwi?"

Jawabu Ikiwa lugha hii ndogo hamukuweza kuifahamu, vipi mutaweza kufahamu kitu chenye kuhitaji fani za lugha na usuli na mengineo. Ikiwa mimi niliingia msikitini kwenu Raha Leo nikakuta juu ya ubao wenu munawasomesha vijana na katika darsa hio Mubtadaa mumemwita Fa'il (vipi mutaweza kujadili masuala haya?!!! Mimi nimempongeza Sheikh Bachoo kwa juhudi au moyo wake; na sikumpong eza kwa kulikuza suala ambalo:

1) Ni la furuu'i

2) Lina khilafu. Na hii haina maana kuwa Furu'i zisizungumzwe; suala la Furu'i huwa halishadidiwi; bali unawaacha watu kama walivyo tu. Lakini yeye anapenda kushadidia katika mas-ala kama haya; ndio maana akashadidi hata katika suala la kufunga mikono hata kuwaita watu mipopoo bali na kuwambia kuwa hawana Sala. Kwa hivyo, nieleweni kwamba ninachokipinga ni kushadidia au kuwakoroga watu katika kitu ambacho ni furu'i za dini ilhali yeye kawakuta na msimamo tafauti tangu zamani. Katika mas-ala ya furu'i, wanavyuoni huwa hawashadidi juu ya Mas-ala kama haya. Mimi leo nikisimama nikaanza kufanya kampeni kwamba watu wasiitikie amina wa kisali, nalo ni jambo la furu'i, si nitakuwa natia fitna tu? Jambo kama hili huwachwa wasomi wakalitafiti kaiha kila mmoja akafanya vile ilivyombainikia. Lakini kufanya kampeni maalumu na da'awa kana kwamba waliotangulia wote ni wapotovu, hili ndilo jambo la kulaumiwa.

Ama kauli yenu: "Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi ilikuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini?" Mwisho wa kunukuu. Na mimi nikuulizeni nyinyi mumenishukuru kwa juhudi yangu kisha mwisho wa kitabu mukaniambia: "Mwisho tunachukua fursa hii kumuonya ndugu Juma kuwa amuogope Mwenyezi Mungu hususan katika mas-ala ya kielimu. Akumbuke kuwa Mwenyezi Mungu Ameonya juu ya mtu kusema jambo au kufanya asilolijua. Aelewe kwamba ataulizwa juu ya hilo. Lingekuwa jambo la busara kama ndugu Juma angalikubali kuuliza na kufanya utafiti zaidi juu ya mas-ala haya kama agizo la Mwenyezi Mungu linavyotutaka". Sasa na nyinyi munanishukuru nini?

Munasema "Sisi tunapenda kumfahamisha kuwa suala hili la kwamba mwezi ukiandama sehemu moja unatosheleza kufuatwa kwa kufunga au kufungua ulimwengu mzima, si suala jipya bali ni jambo la kale. Tunasikitika kwamba hakuangalia vizuri maoni ya Wanavyuoni wakubwa walivyoelezea msimamo huo. Angalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 51-58. Hapa tunanukuu baadhi ya kauli hizo:

Imamun-Nawawy aliyekisherehesha Kitabu cha Sahihi Muslim anasema:

"Na jambo lililo sahihi kwa wenzetu (Mashaffi) ni kuwa muandamo mmoja hauwahusu watu wote bali unawahusu wale walio karibu kwa kiasi ambacho hawaruhusiki kupunguza Sala (Sala ya safari). Pia imesemwa kuwa iwapo matlai ni mamoja watalazimika (watu) kufunga pamoja. Pia imesemwa kuwa ikiwa (wanaishi) katika eneo la Iklimu moja (maili 72 au km 89) (watalazimika kufunga pamoja) vyenginevyo kila mmoja atafunga kwa muandamo wake. Na wakasema wenzetu wengine (Mashaffi) kuwa muandamo katika sehemu moja utawahusu wote wa dunia nzima".

Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar katika kitabu chake "Bayaanullinnas" J. 2 uk 203 - 204 ameandika yafuatayo juu ya kauli hiyo ya Imamun-Nawawy:

"Hapa Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasari kauli zilizomo katika madhehebu ya Kishaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu mengine ya Kiislamu. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika maf ungu matatu makuu: "...Hapo Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasar kauli zilizomo katika madhehebu ya Shaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu nyengine za Kiislam. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika mafungu matatu makuu: Kauli ya kwanza: "Kila nchi iwe na matlai yake, wala muandamo wa nchi moja hautalazimu nchi nyengine ya mbali wala karibu". Kauli ya pili: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi zote za dunia hata kama ziko mbali".

Kauli ya tatu: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi iliyo karibu nayo au inayowafikiana kimatlai". Kisha, Shaykh Jaadul-Haq akaendelea kusema kwamba:

"Na (kauli) zote hizo ni maoni yatokanayo na Ijtihaadi ambazo hazikusimama juu ya hoja kat-ii, si sanad wala matni. Kwa hivyo ingefaa ichaguliwe kauli ambayo inakubaliana na maslahi ya (Waislam wote wa) dunia nzima kwa jumla"."

Jawabu Sikubaliani na mtazamo wa Sheikh Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar, kwamba zote hizi ni rai na itihad kwani kanuni ni kuwa "Hakuna ijtihadi mbele ya andiko" Ijtihad mwahala mwake ni musimo andiko. Wakatika katika suala hili, utaona kwamba asemaye kuwa tufunge kwa muandamo mmoja, hoja yake ni Hadithi "Fungeni kwa kuuona"; na anayesema kuwa kila mahala na muandamo wake, anatoa ushahidi wake ni Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib. Kwa hivyo, ijtihad ni katika kuyafahamu maandiko: si ijtihad kwa maana ya rai tupu pasi na andiko kama alivyosema Sheikh. Kilichobaki ni kuzijadili riwaya mbili hizi zina maana gani?

Munasema Tungependa kumueleza ndugu yetu kwamba hata hapa Afrika ya Mashariki jambo hili hakulianzisha Shaykh Naaswir Bachuu kama alivyodai mwenyewe (Nd. Juma) kwamba: (Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro)) Inasikitisha hakuweza kuangalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 161-163 wametajwa walioonyesha kwa vizuri kabisa misimamo hiyo tofauti. Mashaykh wenyewe ni hawa wafuatao: Al-marhuum Shaykh Juma Abdul Waduud (wa Zanzibar), Shaykh Abdillahi Naaswir ( Nairobi Kenya ), na Shaykh Naaswir Khamis Abdul Rahman ( Mombasa Kenya ).

Jawabu Kwani wapi katika kitabu changu nilisema kuwa Sheikh Nassor Bchoo ndiye aliyeanzisha fikra hii hapo Afrika ya Mashariki hata mukaleta dai hili? Mimi nimeeleza kuwa zamani Afrika Mashariki watu wote wakifata muandamo mmoja. Nilisema: Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo. Dr. Ramadhan Al-butti - miongoni mwa wanavyuoni wakubwa wa ulimwengu wa sasa - anaona kwamba harakati hizi hazisifiki kama ni madhehebu: bali ni hatua (phase) katika mapito ya Historia.

Na katika uk. 97, nimesema:

Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya. Kwa hivyo, ni wazi kwamba mimi nazungumzia Afrika Mashariki. Na mfano wa hilo pia kalisema Sheikh Nassor Bachoo, lakini yeye hamukumjibu. Anasema: "Pamoja na kuwa mgogoro wa kuandama kwa mwezi umeanza kuonekana hadharani katika jamii za Waislam wa hapa Afrika ya Mashariki katika miaka ya hivi karibuni". Inasikitisha kwamba hata maneno yangu mumeyakata na kuchukua yale ambayo hayakamilishi maana nilioilenga. Maneno "Karne zimepita" hamukuyataka kwani hayakufikisheni kule mutakako!

Pili narejea tena kusema kwamba hao wanavyuoni aliowataja Sheikh Nassor, hawajathibitisha habari za kuwa watu wafunge au wakifunga kwa muandamo mmoja Africa Masharik, ukimtoa Sheikh Nassir Khamis wa Mombasa ambaye naye pia ni mtu wa sasa. Ama sheikh Juma Abdu-Wadood yeye, kwa mujibu wa nakala hio ya Sheikh Nassor Bachoo, kasema hivi: Kuona huku kwa mwezi kumekusudiwa kuonekana na Waislam, na kuonekana na Waislamu huko, sio lazima kuonekana na Waislamu wote. Bali inatosha shahada ya mtu mmoja muadilifu".

Pia inampasa mtu mmoja pekee kama ameuona mwezi yeye afunge na kila aliyemuamini; hata akiwa haijakubaliwa shahada yake. Haya ndio maneno ya Sheikh Juma Abdu-Wadood kwa mujibu wa alivyomnukuu Sheikh Bachoo. Sasa ikiwa ndugu zetu mumeshindwa kuyafahamu maneno haya ya Sheikh Juma Abdu-Wadood, bado mutaendelea kupoteza watu bila ya elimu?! Sheikh Juma Abdul-Wadood hapa anazungumzia mas-ala ya ushahidi kwamba si lazima - katika suala la kuonekana kwa mwezi - kwamba kila mmoja auone: bali akiona mtu mmoja basi inatosha kwa wengine kufunga. Hii ndio kauli ya Sheikh Juma Abdul-Wadood na hili nimelieleza kwa urefu katika kitabu changu.

Kisha Sheikh Juma Abdul-Wadood akazungumzia suala la kufunga kwa muandamo mmoja akasema: "Rai za Maimamu wengine wameifasiri hadithi isemayo: (Fungeni kwa kuuona Mwezi) kwamba ukionekana popote mashariki au magharibi (watu) wafunge; hapana kutazama masafa fulani au nini. Hii ni rai nayo na wengi wamesema (hivyo) kama Imamu Malik , Ahmad na kundi kubwa la Hanafi. Inakurubia kuwa n dio rai ya Jamhuri - kufata rai hii ni kuhakikisha umoja wa dunia nzima. Wala hatuwezi kusema kwamba rai ya Shaffiy ndio ya Jamhur". Hapa Sheikh Juma anasimulia rai za Maimamu wengine: si rai za Maulamaa wa Afrika Mashariki. Mimi dai langu nililodai ni kuwa jambo hili la kufunga kwa muandamo mmoja, napenda munifahamu: ni jipya kwa Africa Mashariki. Mimi sikusudii jambo la wanazuoni kuzungumzia rai mbali mbali: bali nazungumzia jambo la watu kufata muandamo mmoja kwamba karne zimepita ya sikio la Muafrika Mashariki wa Kawaida halijiapata kusikia. Na nimetumia maneno "Muafrika wa Mashariki wa kawaida" ili kuwatoa wanavyuoni wao hata kama walikuwa hawafati kauli hio, lakini wanaijua. Kwa hali yoyote ile:

1) Sheikh Juma Abdul-Wadoo hajazungumzia kwamba Afrika Mashariki watu walikuwa wakifunga au wafunge kwa muandamo mmoja, bali kazungumzia rai za wanavyuoni wasio wa Afrika Mashariki - Al-Imamu Shafi, Hanbal n.k. Na mimi sijakanusha tafauti hizi.

2) Kauli yake ilikuwa ni kuhusu suala la mashahidi.

Ama Sheikh Abdillahi Nassir, yeye ni mwanachuoni wa sasa. Na mimi sijasema kuwa sasa hakuna rai hizo. Pili ni kuwa nakala alizotupa Sheikh Bachoo za kitabu cha Sheikh Abdillahi utaona kwamba Sheikh Abdillahi hazungumzii kuwa kauli ya kufatwa ni ile ya muandamo mmoja; bali yeye kasema kuwa hili ni suala la khilafu kwa hivyo tusigombane kila mtu afate rai anayoiona kuwa ni sawa. Sheikh Abdillah kayasema haya baada ya kutokea mizozo hii ya sasa. Kwa hivyo tunarudi pale pale kwamba "Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo". Kwa hivyo, nukta hii hamukuuijibu: na wala sioni kuwa kuna haja ya kuijibu kwani haina umuhimu katika maudhui yetu. Bali kitabu chenu chote, munachagua mambo yasio na umuhimu "Juma kantutukana; Juma kanfanya hivi" nyinyi ndio munajibu baada ya kuzungumzia dalili za kielimu.

Ama Sheikh Nassor: yeye pia ni mtu wa sasa na ni mfuasi wa skuli hio hio munayoifuata nyinyi, kwa hivyo kusema kwake alivyosema hakujapindua nilioyasema kuwa - kimatendo - hili ni suala jipya kwa kwetu Afrika ya Mashariki. Wala mimi sikusema kuwa Sheikh Nassor Bachoo ndiye muasisi wa fikra hio huko kwetu. Naomba munifahamu ninachokisema kwanza kisha ndio munijibu. Na sijui munapinga nini kitu ambacho watu wote wanakijua. Bila ya kusahau kwamba mimi sikusudii kusema kuwa kitu sahihi ni kilichofanywa zamani au kilichofanywa leo: laa! Bali kitu sahihi ni chenye ushahidi sahihi uliojengeka juu ya misingi sahihi ya kielimu. Na kielimu, suala la kuzingatia muandamo mmoja - hamutoweza kulithibitisha.

MNASEMA

Pia Shaykh Ahmad Al Khalil, Mufti wa Omani amethibitisha kwamba Ikhtilaf hii ya muandamo wa mwezi katika hukmu ya kufunga au kufungua ipo na kwamba ni jambo la kale. Kama alivyosema maneno yake yaliyotafsiriwa na Shaykh Muniir Sulayman 'Aziz kwamba: "Hakuna madhehebu iliyokuwa imesalimika na kuwa na Khitilafu baina ya Wanavyuoni wake juu ya suala la kutafautiana miandamo ya mwezi." Jee ndugu Juma anataka kusema kwamba Shaykh Naaswir Bachuu ndiye mwalimu aliyeanzisha madhehebu zote? Au ndiye aliyeanzisha mtafaruku huu kama alivyouita mwenyewe ndugu Juma?

JAWABU

Suala hilo jiulizeni wenyewe; mujijibu wenyewe; kwani nyinyi ndio mulioliunda: mimi sikusema hivyo kamwe bali nilichokisema ni hiki: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nami sikusudii kusema kwamba upya huo ni katika kuzungunzwa au kusomwa suala hilo katika vitabu; nakusudia kimatendo sula hili lilikuwa halipo Afrika Mashariki. Sasa ili muwe mumenijibu, twambieni nani alikuwa akifata muandamo mmoja hapa Afrika Mashariki. Jamani! Tafuteni hoja mujadili: musijadili kitu kisichokuwa na umuhimu. Kama hamuna hoja nyamzeni musijitie aibu!

MNASEMA

Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani; Ndugu Juma anasema: (Kama tunavyojua kwamba Sheikh Nassor Bachoo, ni mmoja wa wenye kusisitiza ulazima wa kuwa na muandamo mmoja.) Sisi kwa upande wetu tunasema: Katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu hakuna pahala alipolazimisha watu wafuate huo aliouita ndugu Juma (msimamo wa Shaykh Naaswir). Bali yeye ameonesha mitizamo ya Wanavyuoni kwa kutumia Aya za Qur-aan, Hadiythi na vitabu vinavyokubalika. Lugha aliyotumia Shaykh Naaswir katika huo unaonekana ni msimamo wake ni maneno yaliyozimuliwa kilugha (polite language) kama vile: (inawezekana) ((inaonyesha) .

JAWABU

Na mimi hapa sijasema kuwa Sheikh Nassir Bachoo kalazimisha watu wafunge kwa muandamo mmoja. Nimesema "Anasisitiza ulazima" yaani yeye analingania msimamo huo kwani kwake ndio msimamo sahihi na ndio wajibu kuufata. Naomba tena tuelewane musiseme kitu kinyume na nilivyosema. Wala musitafute kitu kisicho na maana mukajadili eti ndio jawabu! Pili maneno yenu: "Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani". Sasa je na nyinyi pia munaonesha udhaifu huo huo kwa kumuandama mtu fulani katika kitabu chenu?

MNASEMA

Aliyelazimisha rai ni ndugu Juma mwenyewe kama anavyosema: (Lakini kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali) [uk. 112]

JAWABU

Bali hata Sheikh Bachoo pia kalazimisha kwani ukidai kuwa huu ndio msimamo wa haki au ndio msimamo sahihi au ndio wajibu kufatwa, bila kusema kuwa rai zote zinafaa basi na wewe huwa umelazimisha rai yako. Sasa je Sheikh Bachoo anakubali hivyo kuwa rai zote ni sawa? Mimi kweli sisemi kuwa rai zote ni sawa: nasema kuwa nyinyi mumekosea na sahihi ni kinyume na munavyofanya, na kwa hivyo bado nipo katika msimamo wangu huo huo kwamba: "Kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali".

MUNASEMA

"Kisha katika uk 85 ndugu Juma anataja kwamba msimamo huu wa muandamo mmoja kwa dunia nzima ni ((kitu kipya)) na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu baada ya kutaja baadhi ya nchi zinazofuata miandamo yao - yaani kila nchi na muandamo wake kama Al-yaman , Oman , Misri na Saudia. Kisha hapo hapo akataja: ((isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.)) Inafaa ndugu Juma aulizwe masuala yafuatayo:

i) Kama ni jambo lisilotekelezeka vipi tena Imarat wanalitekeleza?

ii) Je hawa wa Imarat nao ni wanafunzi wa Shaykh Naaswir Bachuu?

iii) Kwani hiyo sio kauli ya Jamhuur ambayo ndio msimamo wa maimamu wakubwa wakiwemo Ahmad bin Hanbal, Malik na Abu Hanifa? (Angalia pia sehemu ya 11 na 13 za kitabu hiki)

JAWABU

Kwanza mumemefanya ghushi: maneno yangu hamukuyanukuu yote. Mimi nimesema: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nyinyi maneno "Kwa kwetu Afrika Mashariki" mumeyatoa ili ionekane kuwa mimi nasema kuwa hili ni suala jipya kila pahala. Watu kama nyinyi vipi tutakuamini katika dini yenu na uadilifu wenu, ikiwa munaghushi maandiko hivi? Hii ndio kamati ya Msikiti Sunna na hii ndio suna yenyewe?! Halafu mukaendelea na tadlis (ghushi) yenu mukasema: "Na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu". Mimi sikusema hapa kuwa "Halitekelezeki", bali nimesema:

Lakini ukweli ni kuwa hata katika nchi nyengine zote za dunia taqriban kauli kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ni kauli ilioishia katika vitabu tu, kimatendo (practically) kauli hio haitumiwi isipokuwa na mtu mmoja mmoja. Hadi leo hii: watu Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao, Misr wanafata muandamo wao na nchi zote taqriban ni hivyo, isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.

Haya nionesheni hapa maneno "Halitekelezeki". Mimi nimesema kuwa kimatendo kauli hii, hadi leo haitendewi kazi isipokuwa na baadhi ya watu. Nyinyi mumebadilisha na kuweka ghushi yenu mukasema nimesema halitekelezeki. Kwa hivyo, hilo Sula (a na b) jibuni wenyewe kwani mumesema kinyume na nilivyosema. Suala (d), najibu kuwa sio: hio si kauli ya jumhur bali jumhur kauli yao ni kinyume na hivyo na hili nimelithibitisha katika uk. 189-193 wa chapa ya pili ya kitabu changu au uk. 171 wa kitabu hicho chapa ya kwanza. Na Al-Imamu Malik riwaya zake zimegongana na riwaya kwamba kila watu na muandamo wao ndio ilio bora kwani ni riwaya ya Madina aliko kuweko Al-Imamu Malik, wakati riwaya nyengine ni ya watu wa Irak kulikokuwa na viwanda vya kutunga riwaya!

MNASEMA

Na sisi tunamuongezea habari moja ambayo ni vyema kuielewa, kwamba nchi ya Uganda iliyo katika Afrika ya Mashariki pia inafuata rasmi muandamo mmoja wa duniani. Pia aelewe kwamba huo msimamo wa kila nchi na mwezi wake huku Afrika ya Mashariki haukuwepo tokea zamani. Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja. Yeye anaendelea kushika msimamo wake: (Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka.

JAWABU

1) Kitu rasmi Uganda hakizingatiwi kwani Uganda kimsingi sin chi ya Kiislamu wala ya Waislamu: Waislamu ni wachache ukilinganisha na Wasio Waislamu. Kwa hivyo, hakuna kitu rasmi. Na jambo hilo ni jambo la sasa. Na mimi sijapinga kwamba sasa fikra hio ipo Afrika Mashariki.

2) Ama kauli yenu: "Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja". Ndio maana nikatumia lafdhi "Kwa kwetu Afrika Mashariki" nikijua kuwa wanavyuoni wote wa kwetu Afrika Mashariki wana msimamo huo. Ama kauli yenu: "Yeye anaendelea kushika msimamo wake: ((Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao,)). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka". Mwisho wa kunukuu. Inaonesha kuwa kitabu changu mumekijibu bila ya kukifahamu. Nilichosema ni kuwa, ijtihadi ifanywe katika kubainisha wapi hadi wapi watu wafunge pamoja. Kwa vile, hakuna andiko lililobainisha hivyo. Ama muandamo mmoja kwa dunia nzima hili ni kinyume na andiko. Kwa hivyo, wakiwa wanavyuoni wa zamani wamefanya ijtihad hio, sisi tunafata ijtihad yao kwa vile hapa ni mahala pa ijtihad na haikugongana na andiko. Ama madai yenu nyinyi ni kinyume na andiko lilivyoonesha.

MNASEMA

"Kuna suala moja la nyongeza tunapenda tumuulize ndugu yetu Juma: Hata kama hizo nchi alizozitaja ( Al-Yaman , Oman , Misri na Saudia) hazijakubaliana kufuata muandamo mmoja, je hakuna uwezekano (japo wa sadfa) unaoweza kutokea kufunga siku moja ijapokuwa kila mmoja ameona mwezi katika nchi yake? Sasa tuseme kila nchi katika hizo imeona mwezi usiku wa Alkhamisi kuamkia Ijumaa - Wote si watafunga siku moja ya Ijumaa? Basi huo ndio utekelezaji aliosema hautekelezeki. Ni wazi kuwa unatekelezeka.

JAWABU

Munaendelea kuuliza masula haya kwa sababu masuala yenu mumeyajenga katika kitu nisichokisema kamwe. Wapi nimesema kuwa "Hilo halitekezeki" hata mukauliza masuala haya?

11