• Anza
  • Iliyopita
  • 9 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 17312 / Pakua: 3832
Kiwango Kiwango Kiwango
VAZI LA MWANAMKE

VAZI LA MWANAMKE

Mwandishi:
Swahili

VAZI LA MWANAMKE

P.O. Box 79662

Dar es Salaam

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:

AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987- 9022 - 9 - 4

Kimeandikwa na: Sheikh Muhammad Ibrahim El-Qazwini.

Kimetafsiriwa na: Sheikh Msabah S. Mapinda

S. L. P. 79662

Email:info@alitrah.org

Website:www.alitrah.org

Kupangwa katika kompyuta na: Ukhti Pili Rajabu

Toleo la Pili: April, 2005 Nakala: 2000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation

P. O. Box 1017

Dar-es-Salaam, Tanzania

Simu: +255 22 2110640

Fax: +255 22 2113107

Email: info@alitrah.org

Website: www.alitrah.org

NENO LA MCHAPISHAJI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu, kwa jina la: Al-Hijab Saa'datun laa shiqaaun, kili-choandikwa na, Sheikh Muhammad Ibrahim El-Qazwiniy Kitabu hiki kinahusu vazi la Hijabu; vazi ambalo ni rasimi kwa wanawake wa ki-Islamu kwa ajili ya kustiri maungo yao. Maadui wa Uislamu wanalibeza sana vazi hili kiasi cha kutaka kuwakatisha tamaa wavaaji wake - ambao ni wanawake wa ki-Islamu. Mazingira ya sasa tayari yanaonesha kwamba, azma ya maadui hawa wa Uislamu kiasi fulani inafanikiwa. Kwani sasa hivi katika miji yetu asili mia kubwa ya wanawake wanatembea nusu uchi, na hali ni mbaya sana. Hivyo tulipo kiona kitabu hiki, tukaona ni wakati muafaka tukitoe kwa lugha ya kiswahili, kwa kutekeleza amri ile ya Mwenyezi Mungu ya, "kuamrisha mema na kukataza maovu."

Mwandishi wa kitabu hiki ameelezea kwa ufasaha sana falsafa na hekima ya vazi hili, na kuvunja hoja za wale wote wanaolipinga. Katika kufanya hivyo ametumia elimu, akili na hoja zenye manti-ki. Tunamshukuru ndugu yetu, Sheikh Msabah S. Mapinda kwa kukubali kwake kuchukuwa jukumu hili la kutarjum kitabu hiki, kutoka lugha yake ya asili ya Kiarabu kwenda lugha ya Kiswahili. Halikadhalika tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manu-faa kwa wasomaji wetu, hususan wanawake wa ki-Islamu na kuiokoa jamii yetu kutokana na maovu.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 1017 Dar-es-Salaam.

DIBAJI

Kijitabu hiki ni tarjuma ya kijitabu kiitwacho Al-Hijab Saa'datun laa shiqaaun, kilichoandikwa na Sheikh Muhammad Ibrahim El-Qaz-wini mwaka 1979. Ingawaje ni kiasi cha miaka ishirini na minne imepita tangu kilipoandikwa, maelezo na mafunzo yaliyomo yanaafikiana kabisa na hali iliyopo ndani ya jamii yetu leo hii. Mwandishi amejitahidi sana kufafanua maana ya Hijabu, ikiwa ni pamoja na kuleta mifano mbali mbali na matukio ya kweli ili kuonesha umuhimu wa Hijabu katika maana inayokusudiwa na sheria ya Ki-Islamu. Hoja zilizotumika ni madhubuti na zinakuba-lika iwapo tu uadilifu utatumika katika maamuzi, bila kujali zime-semwa na Uislamu au kinyume chake. Kijitabu hiki kimekuwa katika lugha ya Kiarabu kwa kipindi kirefu, na baadaye ikapen-dekezwa kifanyiwe tarjuma ya kiswahili, kwa matarajio ya kuwan-ufaisha watu wengi wa eneo la mashariki ya Afrika na kwingineko inakozungumzwa lugha ya Kiswahili. Kwa mara ya kwanza tarjuma ya kijtabu hiki ilifanywa mnamo mwaka 1991. Ndugu yetu Bwana Qurban Khaki alikuwa ni mtu wa kwanza kupendekeza tarjuma hiyo. Mwenyezi Mungu amlipe kila la kheri katika kuhudumia Uislamu na Waislamu.

Chapa uliyonayo mkononi sasa hivi ni chapa ya pili ya tarjuma ya kijitabu cha Al Hijab Saadatun laa Shiqaaun, ambacho kimechapishwa na Al itra Foundation. Kama ile chapa ya kwanza katika kutarjum kijitabu hiki, tulichokizingatia zaidi ni maana aliy-oikusudia mwandishi. Hivyo basi tarjuma hii siyo neno kwa neno ingawaje safari hii mwandishi wa kijitabu hiki amejitahidi kufanya marekebisho ya kukiboresha kwa kuweka mambo mengi ndani ya chapa mpya iliyoko katika lugha ya Kiarabu. Isitoshe sisi wenyewe tumejaribu kufanya ufafanuzi katika maeneo kadhaa ya kijitabu hiki kutokana na umuhimu tuliouona, hasa kwa kuzingatia hali na mazingira tunayoishi hapa kwetu Tanzania na hata kwa majirani zetu wa eneo hili la mashariki ya Afrika.

Kijitabu hiki kimechapishwa mara kumi katika lugha ya Kiarabu kutokana na umuhimu wa maudhui ya Hijabu kwa umma wa ki-Islamu na wanaadamu wote kwa jumla. Napenda kuitumia nafasi hii kumshukuru Dr Mohamed Kanju kwa msaada wake mkubwa wa kukipitia kijitabu hiki. Si hivyo tu bali namshukuru tena kwa mchango wake wa kututolea tarjuma za Habari moto moto tulizozinasa kutoka kwenye mtandao wa Inter Net wakati wa kumalizia tarjuma ya kitabu hiki. Habari hizo kwa umuhimu wake tumezitia mwishoni kitabuni humu kwa kuwa ni miongoni mwa njama za wapinzani wa Uislamu na Waislamu katika utekelezaji wa Sheria hii tukufu inayomtaka mwanamke wa ki-Islamu avae Hijabu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujalie tuwe ni wenye kunufaika na miongozo iliyomo kitabuni humu, na tuonyeke kwa kila onyo lililomo.

Was-salaam Alaikum, Msabah S. Mapinda. Mtarjumi. 19/10/03. Utangulizi Bismillahi Rahmani Rahimi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya kitabu chake kitukufu: "Na mnapowauliza kitu ( wakeze Mtume) waulizeni nyuma ya pazia".1 Baada ya kauli hii ya Mwenyezi Mungu, ni wajibu wetu kuufa-hamisha ulimwengu mzima ya kwamba, Mwanamke ni kiungo muhimu katika jamii, na anayo haki na heshima kama mtu mwingine yeyote anayeishi katika dunia. Siyo kweli kwamba yeye ni kiumbe tofauti, au ni kiumbe kigeni katika suala zima la maisha ya kila siku, bali yuko katikati ya mazingira na matukio yake daima. Kwa kuwa Uislamu ni dini inayoshughulikia hali ya maisha ya wanadamu kwa kila nyanja, imetoa umuhimu wa pekee katika kulinda na kutetea utu, heshima, pamoja na haki za mwanamke. Kwa sababu hiyo basi, Uislamu umemuwekea mwanamke kanuni za sheria zitakazomfaa kulingana na mazingira yake kimaisha, iwe katika maisha yake peke yake au katika ndoa, na au ndani ya familia na jamii yote kwa ujumla.

Kadhalika Uislamu umempa mwanamke nafasi ya kushughulikia masuala yanayomhusu katika dunia na pia akhera, kama yalivy-oelekezwa kisheria. Nafasi hii inaweza kumfikisha katika safu za Malaika na kumfanya kuwa kiumbe kitakatifu hapa duniani na akhera. Kutokana na umuhimu wa mwanamke katika jamii ya wanadamu, Qur-an inayo sura nzima inayoitwa Sura An-nisaa, ambayo inata-ja baadhi ya masuala yanayowahusu wanawake. 1Qur'an 33:33.

Isitoshe ndani ya Quran zimo Aya nyingi zinazozungumzia mion-gozo mbali mbali juu ya mwanamke, ikiwemo namna ya mienen-do na mavazi yake ndani ya jamii, halikadhalika na haki zake. Yote haya lengo lake ni kuonesha umuhimu wa mwanamke na kumtakia mafanikio na usalama wake. Maumbile ya mwanamke yanapoangaliwa kwa makini sana, hapana shaka yoyote yanaonekana kwamba, yanatofautiana mno na maumbile ya mwanaume, kisaikolojia na katika sehemu fulani ya mazingira ya kijamii. Kutokana na tofauti hii, ilibidi pia kuwe na tofauti kati ya mwanamke na mwanaume katika baadhi ya hukumu za kisheria na kanuni. Tofauti hii imekuja kutokana na hali halisi ya maumbile ya mwanamke. Kwa hiyo basi, kanuni na sheria nazo zikaja katika baadhi ya nyakati kufuatia hali na maumbile ya mwanamke. Siyo kweli kwamba tofauti hii ni kwa ajili eti ya kumdhalilisha na kumfanya mwanamke kuwa ni kiumbe pungufu, kama wanavyodai maadui wa Uislamu.

Katika moja ya kanuni muhimu za sheria ya ki-Islamu iliyotiliwa mkazo, na kumlazimisha mwanamke kutoachana nayo ni Hijabu. Kanuni ya Hijabu haikuja isipokuwa ni kwa ajili ya kuhifadhi na kulinda mafanikio ya mwanamke, bila kusahau heshima yake na utu wake. Kanuni hii inazingatiwa kuwa ni miongoni mwa kanuni muhimu sana ndani ya Uislamu. Kutokana na umuhimu wake, Mwenyezi Mungu ameitaja katika Aya nyingi za Qur'an, na wala hakutosheka kuitaja katika Aya moja au nusu ya Aya, kama ambavyo kuna kanuni ambazo Mwenyezi Mungu amezitaja mara moja katika Aya moja au hata nusu ya Aya.

Tutaonesha umuhimu wa kanuni hii ndani ya kitabu hiki kwa mujibu wa Aya nyingi za Qur'an zilizoitaja kanuni hii. Mwenyezi Mungu amelikariri mara nyingi suala la Hijabu katika Qur'an ili kuonesha umuhimu wake ndani ya jamii na maisha ya wanadamu. Je ni kwa nini basi Waislamu inawapasa kuliangalia suala la Hijabu kwa makini, na pia kutumia muda mwingi kulitafakari na kuzinduana? Jawabu lake ni kwa sababu upinzani na uchochezi wa kutia dosari Hijabu, na kuitolea tafsiri ambazo siyo maana halisi iliyokusudiwa katika vazi hili, umeongezeka na unazidi kuongezeka. Upinzani na uchochezi huu unakuja kutoka kwa maadui wa Uislamu na watu wapenda maovu. Na kwa kutumia kalamu zao na kelele zao, siku zote wamekuwa wakijaribu kuonesha ubaya wa Hijabu, na kwamba eti inarudisha nyuma maendeleo. Pia hupata wakadai, "Ati Hijabu ni kumdhalilisha mwanamke na ni kumtesa."

Hayo ni pamoja na uzushi mwingineo wanaouona kuwa unaweza kuwasaidia katika kampeni yao hii dhidi ya Hijabu. Kwa masikitiko makubwa, ziko baadhi ya serikali zinaonesha msimamo wa wazi kabisa katika kupinga Hijabu, bali zinatumia kila aina ya uwezo walionao kusambaza upinzani huo kwa kuwataka wanawake wa ki-Islamu waache kujisitiri kwa mujibu wa sheria ya dini yao.*2 Mambo haya hayafanyiki kwa siri, kwani mara kwa mara tunaso-ma magazetini na au kusikia kwenye vyombo vya habari vingine kwamba serikali fulani imetoa agizo kuwazuwia mabinti wa ki-Islamu wasiendelee na masomo ya sekondari au chuo kikuu kwa sababu tu ya wao kuvaa Hijabu. Na kuna baaadhi ya serikali zina-toa maagizo kuwa, miongoni mwa masharti ya kujiunga na vyuo vikuu vya nchi hizo, mwanamke anatakiwa asivaae Hijabu!!

Mpenzi msomaji, ukirejea nyuma kidogo tu katika historia ya nchi ya Iran utakuta kwamba, mwanzoni mwa utawala wa mfalme Shah aliyepinduliwa, lilipitishwa azimio rasmi la kuzuia kabisa uvaaji wa Hijabu kwa wanawake wa ki-Islamu nchi nzima. 2 Wakati tunafanya tarjuma ya kitabu hiki, habari kutoka Ufaransa zinasema kuwa: "Serekali ya Ufaransa imepiga marufuku vazi la Hijabu kwa wanawake wa ki-Islamu nchini humo." Kwa bahati mbaya sana Mufti wa Misri Sheikh Tantawi ameonesha udhaifu mkubwa kwa kusema kuwa: "Wanawake wa ki-Islamu nchini Ufaransa wanaweza kuvua hijabu iwapo watalaz-imishwa kufanya hivyo." Habari kamili ya tukio hili tumeichapisha mwishoni mwa kitabu hiki kama tulivyoipata katika mtandao wa Internet. Mtarjumi.

Askari walitawanywa njiani, sokoni mpaka katika njia za majang-wani kwa ajili tu ya kuwazuia kuvaa na kuwavua wanawake wanaoonekana kuwa wamevaa Hijabu. Kutokana na unyama huu, wanawake wengi wa ki-Islamu waliona ni bora wabakie majumbani mwao kwa muda wa miaka mingi kutokana na hofu ya kunyanyaswa na askari wa serikali. Enyi watu nyie! Ni ya nini vita hii munayoineza dhidi ya Hijabu? Ni kwani nini hampambani na umalaya na maovu yaliyokithiri ndani ya jamii yetu na badala yake mnaelekeza mapambano yenu kwa wanawake wanaolinda heshima ya mwanamke, heshima ya jamii bali pia wanalinda utu wetu?3 Ni kwa nini mapambano hayo msiyaelekeze kwenye madanguro ambayo tuna hakika kwamba yanajulikana fika? Kwa nini hampambani na ulevi unaotishia familia zetu? Kwa nini hampambani na madawa ya kulevya yanayoziangamiza nchi zetu na kizazi chetu, bali pia yanaan-gusha uchumi wa nchi zetu?

Kwa nini hampambani na umaskini uliokithiri ndani ya jamii yetu? Mbona hampambani na vibaka 3Kwa hakika ni jambo la kuhuzunisha sana kuwaona wanawake wanaotambua nini maana ya mwanamke wanaishi kwa hofu na mashaka nchini mwao kwa sababu tu wanafuata maagizo ya dini yao. Iko haja tufahamu kwamba, wanawake hawa wanafahamu maana ya kuwa mwanamke na thamani yake katika jamii yoyote ile na si ya ki-Islamu peke yake. Wanawake hawa wanatambua vyema kwamba umbile la mwanamke linastahiki vazi gani ili kuibakisha heshima ya mwanamke ndani ya jamii. Lakini kwa huzuni na masikitiko makubwa wanawake hawa na utamaduni wao ndiyo maadui wakubwa ndani ya jamii yetu na kwa mawazo ya watu wengi wanastahiki kupigwa vita mpaka wazivue hizo Hijabu zao.

Enyi watu nyie; na hasa wanawake! Hamuoni namna utu na heshima ya mwanamke ivy-opoteza thamani yake? Hivi kweli nia yenu ni kuisaidia jamii iondokane na majanga ya ukimwi, watoto wa mitaani na umalaya uliokithiri nchini mwetu? Tazameni mabinti zenu namna wanavyovaa, hivi kweli mnatufunza nini sisi watoto wa kiume? Nashindwa kuizuia kalamu isiandike kwamba, hata watoto wadogo katika zama hizi kwa namna mnavyojidhalilisha wanafahamu maumbile ya wanawake yakoje. Je, huu ndio uhuru? Je, hizi ndizo haki za binaadamu mnazozipigania? Je, haya ndiyo maendeleo ya nchi yetu? Kwa upande wa serikali yetu hivi kweli mmeshindwa kuiongoza jamii kwenye maadili ya kibinaadamu? Hivi kweli wasichana wetu na wanawake wetu wamekushindeni kuwadhibiti kiasi cha kuwa tunaona mambo ambayo hayastahiki konekana hadharani? Mbona hakuna hatua zozote mna-zochukua dhidi ya matendo haya yanayofanyika hadharani? Mtarjumi.

wanaotishia usalama wa raia kila kukicha? Mwenyezi Mungu anasema: "Na anapotawala hujitahidi kufanya uharibifu katika nchi na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hawapendi watu waharibifu."4 Siyo ajabu watu hawa kusema hayo wayase-mayo hasa tunapozingatia kwamba, wao wanaelewa vizuri na kutambua hekima zilizomo ndani ya kanuni hii na falsafa zake, mambo ambayo yanakubalika kiakili na kimaumbile. Kwa upande mwingine wanakuta Hijabu ndiyo kizuizi kikubwa na madhubuti dhidi ya matendo yao machafu ndani ya jamii safi ya Waislamu. Ndiyo maana wakawa wanaipinga kanuni hii ya ki-Islamu kwa njia mbali mbali kupitia maonesho ya Television, Redio, Magazeti, Majarida, Sinema n.k. Nia yao ni kumuondeshea aibu na haya mwanamke wa ki-Islamu, pia kumvua vazi la utamaduni wake kama Mwislamu, na baadaye asiwe na haya wala aibu kisha wamtelekeze na kumsukumiza katika janga la maovu na uchafu mwingineo.

Maadamu mambo yako katika hali hii, yaani vita inaendeshwa dhidi ya mwanamke wa ki-Islamu, basi hana budi mwanamke huyu wa ki-Islamu ashikamane na vazi hili la Hijabu. Inampasa pia asimamie kwa uwezo wake wote kueneza mafunzo na hekima za Hijabu baina ya wanawake, wasichana walioko mashuleni na majumbani, na asisitize uvaaji wa vazi hili la Hijabu. Wajibu huu ni kwa mwanamke kwa upande wake na pia kwa Waislamu wote.

4 Qur'an 2: 205. Makusudio ya Aya hii ni kuonesha kwamba watawala wanapopewa madara-ka, badala ya kushughulikia matatizo na maslaha ya raia zao, wao hufanya kila juhudi kueneza uovu, machafu na uharibifu mwingineo ikiwemo ule wa mazingira ya nchi na hati-maye kuziacha nchi hizo zikiwa ni mateka wa maovu, ujinga na umasikini mkubwa. Mtarjumi.

Halikadhalika Waislamu wasikubali kutoa nafasi kwa maadui hawa kutekeleza malengo yao ya kishetani, ambayo yanaudhuru Uislamu na Waislamu. Nataraji kitabu hiki kitakuwa ni chenye kuongeza hamasa ya kuimarisha kanuni ya Hijabu na kuivaa. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kufanikisha na ndiye msaidizi. Muhammad Ibrahim Muwahidi El-Qaz-wini. 1-5-1400/1979.

QUR-AN INASISITIZA KUVAA HIJABU

Katika utangulizi tumetaja kwamba, Qur'an inahimiza sana sana kuvaa Hijabu, na katika Aya nyingi za Qur-an umetajwa mkazo wa jambo hili, nasi tutataja baadaye baadhi ya Aya nyingi zinazohusu suala hili na kuzifasiri kwa kifupi.

1. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema; "Ewe Nabii, waambie wake zako na binti zako na wake wa waaminio, wateremshe shungi zao. Kufanya hivyo kutapelekea wao kutambulikana ( kwamba ni wanawake waungwana) hawatakerwa ( na watu waovu), na Allah ni Mwingi wa kusamehe (tena) Mwenye huruma". 5

Katika Aya hii tukufu, Mwenyezi Mungu anamuamuru Nabii wake Muhammad(s.a.w.w) , awaamrishe wanawake wa ki-Islamu waki-wemo wakeze, binti zake na wake wa waaminio, wajisitiri kwa kuvaa Hijabu iliyokamilika. Katika zama za mwanzo wa kuja Uislamu wanawake walikuwa wakitoka majumbani mwao bila kujisitiri miili yao kikamilifu, kama vile walivyokuwa wakitoka wanawake wa zama za Jahiliya ( kabla kuja Uislamu). Hali ya kutokujisitiri kikamilifu kwa wanawake, haikuridhiwa na sheria ya ki-Islamu, ndipo Mwenyezi Mungu alipomuamuru Mtume wake Muhammad(s.a.w.w) awaambie wanawake waumini wajisitiri na wavae Hijabu, na awakataze kutoka majumbani mwao bila sitara iliyokamilika kisheria.

Akasema Allah s.w.t kumwambia Mtume(s.a.w.w) , "Ewe Nabii waambie wake zako na binti zako na wake wa waaminio wateremshe shungi zao."

Tamko (Jalabib) ambalo limetumika kwenye Aya ya hamsini na tisa, maana yake kilugha ni ushungi ambao hufunika kichwa cha mwanamke na uso wake na kumkinga asionekane kwa watu kwani kwa mujibu wa sheria haifai kuonesha mbele yao baadhi ya sehemu za mwili wake. Bali ilivyo ndivyo, ni mwanamke asitiri sawa maungo yake kama sheria inavyomtaka kuyasitiri. Ama maana inayopatikana katika kauli ya Mwenyezi Mungu ali-posema; "Kufanya hivyo kutapelekea wao kueleweka ( kwamba ni wanawake waungwana)" Kauli hii inalenga kufahamisha kuwa, Hijabu humfanya mwanamke atajwe kwa utajo wa wema, na katika jamii hupambika kwa sifa ya Uchamungu.

Ni mara chache Wachamungu kukumbwa na mikasa itokanayo na watu waovu, ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaendelea kuse-ma katika Aya hiyo ya hamsini na tisa kuwa; "Hawatakerwa na watu waovu" Hii inamaanisha kwamba, macho ya watu waovu, wajeuri na wenye khiyana, hayamfikii mwanamke ambaye amejisitiri kikamil-ifu tena kisheria, kwa kuwa vazi la Hijabu humlinda dhidi ya aina mbali mbali za uovu, hata kumfanyia maskhara (utani) huwa ni vigumu. Hijabu huwa inasitiri mwili wa mwanamke na kuufanya uzuri wake na mapambo yake kutoonekana, kwani (awapo ndani ya Hijabu) hakuna kinachoonekana katika mwili wake, na mwanamke huyo huwa amesalimika kutokana na shari za aina tofauti. Salama hii hupatikana kwa kuwa, muovu amuonapo na kumtambua kwamba mwanamke huyo ni Mchamungu, tena ni mwenye kujihifadhi barabara hushindwa kumtendea ubaya. Kwa hiyo katika Aya hii tukufu, tuna dalili iliyo wazi inayotujulisha kwamba, kuvaa Hijabu ni lazima, pia inatujulisha kwamba, Hijabu inamhifadhi mwanamke kutokana na ufisadi na aina nyinginezo za uchafu.

2. Mwenyezi Mungu anasema tena kwamba; "Na mnapowauliza (kitu wakeze Mtume), waulizeni nyuma ya pazia, kufanya hivyo kutatakasa nyoyo zenu na nyoyo zao"

Aya hii inawaamuru Waislamu wanapouliza au kuomba kitu kuto-ka kwa wake wa Mtume(s.a.w.w) waulize hali ya kuwa wako nyuma ya pazia. Hapa wametajwa wake wa Mtume, lakini matu-mizi ya amri hii ni kwa wanawake wote ambao sheria ya ki-Islamu hairuhusu kuonana nao bila ya kuwepo kizuizi kwa ujumla.

Maana inayojitokeza katika Aya hii, ni kupatikana wajibu wa kuwepo sitara, yaani Hijabu baina ya wanaume na wanawake. Siyo sawa wanaume na wanawake kukosa mipaka ya mawasil-iano, lazima papatikane muongozo utakaoeleza mipaka hiyo. Ndani ya Aya hii ya hamsini na tatu, Mwenyezi Mungu aliposema; "Kufanya hivyo kutatakasa nyoyo zenu na nyoyo zao" Kilichokusudiwa ni kwamba, suala la Hijabu kwa maana yake halisi ni jambo jema kwa pande zote mbili yaani wanaume na wanawake. Hapana shaka kwamba mwanaume anapomuangalia mwanamke, jambo hilo huamsha hisia za kijinsia, na kumpa shetani nafasi ya kumsukumiza mwanaume huyo katika mambo ya haramu na ufisadi.

Na kwa upande wa mwanamke, pindi anapokosa kuwa ndani ya mazingira ya Hijabu, tayari huwa anai-weka heshima yake na utu wake katika hatari ambapo wakati wowote ule anaweza kuvunjiwa heshima yake. Hivyo basi vazi la Hijabu ni utakaso kwa wanaume na wanawake, na ikiwa kizuizi cha wanawake na wanaume kuchanganyika kitaondolewa, hali hiyo inaweza kusababisha ufisadi na fitna ndani ya jamii, mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyakataza na kuyaharamisha. Hali hii ya uovu ndani ya jamii inajitokeza kwa wingi mno ndani ya maeneo yasiyozingatia kanuni hii ya Hijabu.6

Ni mara nyingi mno tunasikia wanawake wakivunjiwa heshima zao ndani ya misongamano isiyozingatia tofauti zilizoko baina ya wanawake na wanaume, k.m. ndani ya vyombo vya usafiri, sokoni na maeneo mengine mengi. Kumbuka ndugu msomaji, hapa kwetu Tanzania k utokana na hali hii ya kuhuzunisha dhidi ya wanawake ilipata kutokea msamiati unaoitwa mfadhaiko. Yote haya hayakuja kwa bahati mbaya, bali ni kutokana na kupuuzwa kwa mafunzo ya Mwenyezi Mungu na kuyapa mgongo. Basi ni kwa nini tusiadhirike? Mtarjumi.

Wakati huo huo ni lazima tufahamu ya kwamba, Mwenyezi Mungu ameyakemea maovu na ufisadi kwa aina zake na vyanzo vyake vyote. Baada ya maelezo haya yatupasa tujiulize, je ni kwa nini Mwenyezi wakati akilielezea suala la Hijabu tamko lake akalielekeza kwa wakeze Bwana Mtume(s.a.w.w) ? Jawabu lake ni kwamba, wakeze Mtume wanayo daraja maalum ndani ya jamii ya ki-Islamu, kadhalika wao ni Mama wa Waumini wote, na kwa ajili hiyo wanatarajiwa mno kuwa na ziada katika utekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwa sheria muhimu ni hii kanuni ya Hijabu. Kutokana na ukweli huu, mwan-zoni tu mwa Aya hii Mwenyezi Mungu ameanza kwa kusema: "Enyi Wake wa Mtume, ninyi si kama yeyote miongoni mwa wanawake" .7 Maana ya maneno haya ni sawa na kumwambia mtu mwenye elimu, "Wewe Bwana ni mwanachuoni usiseme uongo". Sasa basi, maneno kama haya huwa hayamaanishi kuruhusu kusema uongo kwa asiyekuwa Mwanachuoni, bali maana yake ni kuwa sifa ya kuwa mkweli inamsatahikia mno mtu huyo na uongo kwake ni jambo baya sana. Bali ukweli ulivyo ni kuwa, jambo lolote ambalo huwa ni sababu ya mwanaadamu kuingia ndani ya makosa, huwa ni haramu kwa mujibu wa sheria ya ki-Islamu. Ni wazi kabisa kwamba, wanawake wengi walikuwa wakienda kwa wake wa Mtume(s.a.w.w) na kujifunza mambo mengi waliliyokuwa wakiyaona kwao.

3.Mwenyezi Mungu anatoa maelekezo zaidi anasema: "Na kaeni majumbani mwenu (enyi wanawake) wala msioneshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionesha (mapambo yao) wanawake wa zama za Jahiliyya (kabla kuja Uislamu) .8 7.Qur'an 33:32 8Qur'an 33;33. Ndani ya Aya hii mnapatikana amri ya Mwenyezi Mungu inay-omtaka mwanamke kutulizana nyumbani mwake, ili ashughulikie masuala ya ndani miongoni mwake ni kuhusu ndoa yake na familia, ikiwa ni pamoja na kuwalea wanawe kwa malezi ya kidini na tabia nzuri.

Hii ndiyo maana sahihi ya wanawake kutulizana majumbani mwao. Na iliposemwa katika Aya hii ya 33; "Na wala msioneshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionesha mapambo yao wanawake wa zama za kijahiliya." Maana yake ni kuwataka wanawake wa ki-Islamu wasitoke majumbani mwao kila inapobi-di kutoka, bila ya kujisitiri sawa sawa kama walivyokuwa na tabia hiyo wanawake wa zama zajahiliya. Si sawa mwanamke kuone-sha mapambo yake hadharani. Na inapotajwa mapambo, lazima ieleweke wazi kwamba mapambo ni kama vile hereni, bangili, mikufu n.k. Istoshe kwa vitu hivyo kuwa ni mapambo, bali mwanamke yeye mwenyewe bila kuongeza hereni au mkufu ni pambo. Kwa hiyo basi mwili wake asiuache wazi na kuufanya uonekane kwa kila mtu.

Kitu kingine muhimu kinachojitokeza katika Aya hii ni kwamba, Mwenyezi Mungu anamtaka mwanamke wa ki-Islamu apambike kwa sifa tofauti na wanawake wasio Waislamu katika mavazi na Uchaji Mungu. Hali hii ni kwa sababu wanawake wa ki-Yahudi, ki-Kristo na washirikina huwa hawajilazimishi kufuata hukmu hii ya sheria ambayo ndani yake mna hekima nyingi Wao hutoka bila kujali kulinda heshima zao kama wanawake na mapambo yao huwa wazi mbele ya kila mtu. Suala la kutojiheshimu kwa wanawake wa ki-Islamu, Mwenyezi Mungu hapendezwi nalo, ndiyo maana akawatakia utukufu na heshima kwa kuwachagulia vazi litakalowasitiri na kulinda hadhi yao.

Kutokana na maelezo haya, linapatikana fundisho ambalo linamtaka kila mwanamke alizingatie kuhusu namna ya kuvaa. Na iwapo mwanamke wa ki-Islamu ataacha kuvaa Hijabu na akaamua kuuacha wazi mwili wake, basi atakuwa kajifananan-isha na wanawake wa kiyahudi kikristo na washirikina. Pia huonekana kama mtu anayekataa heshima na utukufu ambao Uislamu unamtaka awe nao. Si hivyo tu bali huwa anajisogeza taratibu hadi kwenye mwelekeo mbaya unaomchukiza Mwenyezi Mungu.

Kuna hadithi isemayo kwamba; Mwenyezi Mungu alimpelekea Wahyi (ufunuo) Mtume fulani miongoni mwa Mitume wake akamwambia, "Waambie Waumini; wasivae mavazi ya maadui zangu, na wala wasile vyakula vinavyoliwa na maadui zangu, na wala wasipite katika njia wanazopita maadui zangu, (ikiwa watayafanya haya niliyoyakataza) basi nao watakuwa miongoni mwa maadui zangu kama walivyo hao ambao ni maadui zangu."9 Aya hizi tatu zimekuja kuzungumzia maana ya Hijabu, na kuna Aya nyingine nyingi kuhusu suala hili ambazo hatujazitaja ili kufupisha maelezo.

1

VAZI LA MWANAMKE

BIBI FATIMA (A.S) KIIGIZO CHEMA KWA WANAWAKE

Bibi Fatimah(a.s) ni mwanamke anayezingatiwa kuwa ni mwanamke wa kutolea mfano katika dini ya ki-Islamu, na pia ni kiigizo chema kwa kila mwanamke anayetafuta mafanikio katika maisha yake. Bibi Fatimah binti Muhammad(s.a.w.w) ndiye mwanamke bora ulimwenguni aliyezaliwa na kupata malezi katika nyumba iliyokuwa ikishuka ndani yake Wahyi kutoka mbingu-ni.

9 Hadithi hii imenukuliwa kutoka ndani ya kitabu kiitwacho Tuhaful- Uquul. Katazo hili linajumuisha mambo mengi na khususan mambo yote ambayo Mwenyezi Mungu hayaridhii na yanatendwa na maadui wa Mwenyezi Mungu. Mwislamu inamuwajibikia kujiepusha nayo vinginevyo hapatakuwa na tofauti kati ya Muumini na adui wa Mwenyezi Mungu. Mtarjumi.

Si hivyo tu bali Bibi Fatimah alihitimu mafunzo ya Uislamu katika madrasa ya Utume, na kutokana na mafunzo hayo aliweza kufikia daraja ya juu na tukufu. Katika kuthibitisha ubora wa Bibi Fatimah, Mtume(s.a.w.w) amepata kusema,"Hakika Mwenyezi Mungu huwa radhi kwa radhi ya Fatimah, na huchukia kutokana na kuchukia kwa Fatimah. " 10 Kwa ajili ya daraja kubwa aliyonayo Bibi Fatimah katika Umma wa Nabii Muhammad(s.a.w.w) imekuwa ni wajibu kwa kila mwanamke duniani kuiga mwenendo wa Bibi huyu katika maisha yake, ajing'arishe kwa nuru yake nzuri na afuate nyayo zake ambazo zitamuelekeza kwenye mafanikio na utukufu. Hakika Bibi Fatimah(a.s) , ni mfano wa kila utukufu na kila jema. Mwanamke yeyote atafanikiwa iwapo ataamua kufuata mwenendo wa Bibi Fatmah (a.s.) , na kinyume chake ni kuwa, kila mwanamke ataangamia iwapo ataamua kujichagulia mwenendo wake au kuiga usiyokuwa mwenendo wa Bibi Fatimah. Pia Fatimah(a.s.) alikuwa Mchaji Mungu na mwenye kutekeleza vilivyo maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Pia ile maana nzima ya Hijabu aliifahamu vema na kuitekeleza kama ilivyoamriwa na Mwenyezi Mungu.

Hivyo utekelezaji wake katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu ulikuwa wa hali ya juu, kwani hakupata kutoka nje ila huwa amevaa vazi la kumsitiri mwili wake wote tangu kichwani hadi miguuni. Isitoshe alikuwa akiichukia mno tabia ya wanawake kutoka majumbani mwao bila kujisitiri kisheria. Bibi Fatimah alichukizwa na tabia hiyo kwa sababu Mwenyezi Mungu pia anaichukia tabia ya kutokujisitiri na hasa kwa kuwa kukosa sitara ya kishera kwa wanawake ni ufunguo wa kuyaendea maovu na ni miongoni mwa vitangulizi vinavyosababisha watu kuteleza, bali wanaaanguka kabisa. 10Mustadrak Alhakim juz 3 uk , Al isabah ya Ibn Hajar Al asqalani juz 4 uk. 10 Sasa hivi tunawaletea baadhi ya mafundisho kuhusu Hijabu na tutaona pia utukufu wa Bibi Fatimah katika mafunzo hayo.

NI KITU GANI KILICHO BORA KWA MWANAMKE?

Inasimuliwa katika historia kwamba, Mtume(s.a.w.w) siku moja aliwauliza Masahaba suali lifuatalo:"Je! ni kitu gani kilicho bora kwa mwanamke?" Masahaba walinyamaza kwa kuwa jibu la mkato na sahihi hawakulifahamu, ikawa kama kwamba akili zao zinahangaika baina ya kuwa kilicho bora kwa mwanamke ni mali, uzuri wake, kuolewa au kitu gani? Kipindi chote hiki Bibi Fatimah alikwisha lisikia swali hilo, na baada ya kimya cha kukosekana jibu, Bibi Fatimah alimtuma mtu aende kwa Mtume(s.a.w.w) aka-toe jibu sahihi la swali hili nalo ilikuwa;"Kilicho bora kwa mwanamke ni yeye mwanamke asimuone mwanaume na mwanaume naye asimuone mwanamke." 11

Baada ya jibu la bibi Fatimah Masahaba walikuwa wakisubiri jibu la Mtume atasema nini kuhusu jawabu alilotoa Binti yake. Mtume(s.a.w.w) akasema "Amesema kweli Fatimah." Na akaongeza kusema,"Fatimah ni sehemu iliyotokana na mwili wangu." Maana ya maneno ya Mtume yalimaanisha kwamba hilo ndilo jawabu sahihi na hiyo ndiyo imani. Kutokana na jawabu hili, Bwana Mtume(s.a.w.w) akawa ameitangazia dunia nzima kwamba; Utu, heshima, utukufu, na wema wa mwanamke unapatikana ndani ya Hijabu, na kinyume chake ni uovu na shari, isitoshe hasara hum-fika mwanamke anapoitupa Hijabu. 11Hapana shaka makusudio yaliyomo ndani ya jawabu la bibi Fatimah(a.s) ni kwamba, waw-ili hawa yaani mwanamke na mwanaume ni wale wasiokuwa na uhsiano wa kisheria. Watu wenye uhusiano kisheria ni kama hawa wafuatao: Mama, dada, shangazi na au Baba, kaka, mjomba na wengine ambao wametajwa katika vitabu vinavyohusika na sheria. Ama mume na mke, wawili hawa uhusiano kati yao hauna haja ya kutolewa maelezo. Mtarjumi.

MAZUNGUMZO YA KUSTAAJABISHA

Historia inaendelea kutufahamisha kwamba Bibi Fatimah(a.s) alikuwa amekaa na baba yake ambaye ndiye Mtume(s.a.w.w) , mara alibisha hodi Sahaba Abdalla ibn Ummi Maktum ambaye alikuwa kipofu. Kabla Sahaba huyu hajaingia Bibi Fatimah(a.s) alisimama akaondoka mahali hapo. Baada ya kwisha mazungumzo baina ya Mtume na Sahaba huyu, Sahaba Abdallah ibn Ummi Maktum aliondoka. Bibi Fatima alirudi na akaendelea kuzungumza na Mtume(s.a.w.w) Bwana Mtume(s.a.w.w) .wakamuuliza Binti yake sababu ya kuondoka wakati alipoingia Sahaba Abdallah ibn Ummi Maktum hali kuwa anafahamu kabisa kwamba yule ni kipofu haoni.12

Bibi Fatimah alijibu kama ifuatavyo."Ikiwa yeye hanioni basi mimi namuona na yeye ananusa harufu ya wanawake. " Mtume(s.a.w.w) alifurahishwa mno na jawabu la Binti yake ambalo linaonyesha kipimo cha Uchamungu na utukufu unaotoka kwa Binti yake Mwenye hekima. Isitoshe kwa jawabu hilo, Bwana Mtume hakumlaumu binti yake kutokana na mkazo huu mkali unaohusu Hijabu, bali furaha ya Mtume iliendelea kwa upeo mkubwa na akaunga mkono kwa dhati kabisa kisha akasema;"Nashuhudia kwamba wewe ni sehemu iliyotokana nami" 13.

12 Ni vyema ikaeleweka wazi kwamba Bwana Mtume(s.a.w.w) alimuuliza Binti yake suali hilo hali ya kuwa yeye mwenyewe anajua wazi kuwa Sahaba yule alikuwa haoni, lakini lengo la Bwana Mtume (s.a.w) kuuliza suali hilo alitaka aone namna Binti yake atakavyo toa jawabu la suali hilo ili historia ipate kusajili mazungumzo haya ya kiimani na ubakie kuwa ni mfano mzuri wa kuigwa siku zote.

13 Mustadrak Al-Wasail Kitabun-Nikah. Biharul-An-Waar juz 104 uk 38.

TUKIO MUHIMU NDANI YA MSIKITI WA MTUME (S.A.W.W.)

Siku moja Bibi Fatimah(a.s.) alitaka kutoa mhadhara ndani ya msikiti wa Mtume(s.a.w.w) Kabla ya kuanza kuhadhiri aliten-genezewa sitara humo Msikitini, akakaa yeye na Waumini wengine wakike upande mmoja na Waumini wanaume wa Kiansari na Muhajirina nao wakakaa upande wa pili. Sitara hii aliyotengenezewa Bibi Fatimah(a.s) ilikuwa ina maana nyingi ndani yake. Kwanza ilikuwa ni kutekeleza sheria inayohusu Hijabu katika sura ya kuweka kizuizi, ambapo pande mbili hizo zilitenganishwa. Pili, hali hiyo ilikuwa ni kuonesha kutokuukubali kwa vitendo mchanganyiko wa wanaume na wanawake, jambo ambalo maadui wa Uislamu wanatumia kila mbinu kulihalalisha kwa kuli-tolea hoja batili.

Sasa nakutazama ewe dada yangu wa ki-Islamu, nikitarajia umeiona mifano hii mitatu inayohusu maisha ya Bibi Fatimah(a.s.) ambaye ni mwanamke bora kuliko wanawake wote duniani, na ni mwanamke anayestahiki kuigwa katika Uislamu. Inafaa uige na ujifunze kwake ili upate kupambika kwa umbile la kike ( yaani kuwa na haya) na utukufu, kadhalika ifanye nafsi yako iwe ya mwanamke Mchamungu mwenye kushika mafunzo ya ki-Islamu na hukmu za Qur'an. Ewe dada wa ki-Islamu hebu shikamana na mafunzo ya ki-Islamu ambayo Mwenyezi Mungu amekupa ili ufanikiwe duniani na akhera. Mafunzo haya yatakupandisha kwenye daraja tukufu la wenye imani na mafanikio. Fahamu kwamba hutafanikiwa isipokuwa uwe umeshikamana na kuyatu-mia mafunzo hayo kwa kuyatekeleza maishani mwako.

KUJIHESHIMU NDIYO PAMBO LA MWANAMKE

Bwana Mtume(s.a.w.w) amesema,"Kujiheshimu ndiyo pambo la Mwanamke." Hapana shaka kwamba pambo limegawanyika sehemu mbili: Pambo lisilo halisi na pambo halisi. Ama pambo lisilo halisi ni lile ambalo linaloonekana wazi, na ni lenye kubakia kwa muda maalum, kisha hutoweka bila hata ya kumuongezea kitu muhusi-ka katika utu wake. Ama lile pambo halisi, ni lile ambalo hubakia muda wote na pia humfanya mwanamke aupate ule utu wake kamili na kumfikisha kwenye daraja ya ukamilifu. Ukweli usiokuwa na shaka ni kuwa, pambo halisi ndilo lenye umuhimu mno kuliko lile jingine, bali ndilo lengo analopaswa kulishughulikia kila mtu. Endapo mtu atakosa kuwa na fungu fulani katika pambo hili halisi, basi pia huwa hana faida yoyote ndani ya lile pambo la dhahiri.

Hapana shaka kwamba kujiheshimu ndilo pambo pekee linalom-faa mwanamke kama alivyosema Bwana Mtume(s.a.w.w) . Pambo hilo humjengea mwanamke utu, heshima na utukufu hapa duniani na kesho akhera. Ama madawa ya kujirembesha, manukato na mengineyo miongoni mwa mapambo, yote hayo ni mapambo ya nje tu na hayana maana yoyote khususan mwanamke mwenyewe atakapokuwa si Mchajimungu; Mwenyezi Mungu apishe mbali.

Hijabu ndiyo alama pekee inayoweza kutambulisha Uchaji Mungu wa mwanamke na pia heshima yake na utu wake. Wakati huo huo tabia ya kutokuwa na Hijabu huchafua heshima ya mwanamke na kuacha maswali chungu nzima kuhusu Uchaji Mungu wake na kujiheshimu kwake kwa jumla. 14Kalimatur-Rasuli uk 110 cha Sayyid Shirazi.

Yote haya yanakuja kwa sababu yeye mwenyewe kauweka mwili wake kuwa maonesho mbele ya maelfu ya watu siku zote. Kutokana na hali kama hiyo, hata huwezi kutambua ni mikono mingapi iliyowahi kuushika mwili wake kwa kuuacha wazi na kutokujisitiri kwa mujibu wa sheria!! Hivi unadhani watu wa kale na hata wa leo hii, nyoyo zao zitasal-imika vipi katika mazingira hayo ya wanawake kuicha wazi miili yao? Kamwe hawatasalimika kabisa, kwani wanawake wanapoiacha wazi miili yao ni jambo linalopelekea tuhuma mbaya kwa wanawake. Imam Ali(a.s.) anasema"Yeyote mwenye kui-weka nafsi yake mahala penye tuhuma mbaya, basi asimlaumu mtu atakaye mdhania vibaya." 15

Hapana shaka kwamba, mwanamke asiyekuwa na Hijabu huwa anaidhuru nafsi yake mwenyewe kwa sababu; Kwanza, huwa anapata hasara mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Pili, heshi-ma yake ndani ya jamii huwa inaporomoka. Hasara anayoipata mwanamke huyo mbele ya Mwenyezi Mungu inakuja kwa sababu mwanamke huyo huwa amekwenda kinyume na kanuni za mbinguni na kukosa utiifu kwa Mwenyezi Mungu. Baadaye tutaeleza adhabu za huko akhera atakazozipa-ta mwanamke asiyejali kujisitiri kwa mujibu wa sheria ya KiIslamu.

Ama hasara atakayoipata mwanamke kutoka na na heshima yake kuporomoka ndani ya jamii, hali hiyo inasababishwa na yeye mwenyewe kutokana na tabia yake ya kuyaacha wazi maungo yake yaonekane kwa kila mtu, hali ambayo humuingiza ndani ya kila aina ya uovu na ufisadi na hatimaye akadhalilika vibaya. 15 Al-kafi juz uk 152. Miongoni mwa dhana mbaya atakayodhaniwa mwanamke asiyejali sitara ya kisheria ni kuwa, wakati wote huonekana yuko tayari kufanya ufisadi. Kama si hivyo, amtazamaye hushawishika kumtendea uovu. Mtarjumi.

Na tukirejea kwa mwanamke mwenye kujisitiri kwa mujibu wa sheria ya ki-Islamu, huyu hupata faida za aina mbili kwa pamoja: Faida aipatayo mbele ya Mwenyezi Mungu ni kwamba, yeye huwa ni mwanamke mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu na Malaika wake pamoja na Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Utukufu huu anaupata kwa kuwa amemtii Mola wake, ametekeleza maamrisho yake na ameyasitri maungo ambayo Mwenyezi Mungu ameamrishsa yasitiriwe. Na kwa ajili hii basi, mwanamke kama huyu kamwe hatonyanyua unyayo wake bali rehma za Mwenyezi Mungu huwa ziko pamoja naye, pia radhi za Mwenyezi Mungu humbatana naye, na wakati huo huo Malaika wa Mwenyezi Mungu wanamuombea msamaha. Mwenyezi Mungu anasema; "Kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na ni chenye kubakia." 16 Ama faida atakayoipata ndani ya jamii, ni pale mwanamke huyo anapokuwa ni mwenye kuheshimiwa na kutukuzwa, yote haya anayapata kwa kuwa yeye amejipamba kwa pambo la kuji-heshimu na kuuhifadhi utu wake, kisha akausitiri uzuri huo aliopewa na Mwenyezi Mungu.

MAJADILIANO NA MSICHANA WA KIKRISTO

Msichana mmoja wa Kikristo alikwenda kwa mwanachuoni wa ki-Islamu na kumwambia. "Mimi nimefahamu mambo mengi kuhusu Uislamu na kwa hakika dini hii imenishangaza sana kwa kanuni zake na miongozo yake, na nimeupenda Uislamu kwa mapenzi ya kweli. Lakini kanuni moja tu kwangu mimi imekuwa ni kikwazo kuingia katika Uislamu. Nimewauliza watu wengi kuhusu kanuni hiyo, mpaka sasa sijapata jawabu la kunitosheleza. 16 Qur'an 42:36.

Iwapo wewe Sheikh utaweza kunibainishia hekima iliyomo ndani ya kanuni hii, basi nakuthibitishia kuwa nitaingia katika Uislamu." Yule Mwanachuoni akasema, "Ni ipi kanuni hiyo?" Msichana aka-jibu. "Kanuni ya kuvaa Hijabu, ni kwa nini Uislamu haumuachi mwanamke akatoka nje apendavyo kama ilivyo kwa wanaume.?" Mwanachuoni yule wa ki-Islamu akasema, "Je umepata kumuona sonara ameweka dhahabu na johari nyinginezo katika sanduku la kioo, kisha akalifunga sanduku hilo kwa kufuli? Msichana akajibu, "Ndiyo." Sheikh huyu akamwambia tena yule msichana, "Je, ni kwanini sonara hakuziacha johari hizo zikawa zinashikwa na kila mtu ajaye kutaka kununua? Kwa nini amezihifadhi ndani ya sanduku la kioo lililofungwa?" Msichana akasema; "Amefanya hivyo ili azilinde johari zake kutokana na wezi na mikono yenye khiyana." Yule Mwanachuoni akamwambia msichana; "Hii ndiyo hekima ya Hijabu, fahamu kwamba mwanamke ni johari ya thamani ambayo ni lazima kuilinda kutokana na waovu na wahaini.

Pia ni wajibu kumhifadhi mwanamke kutokana na macho ya watu waovu ndani ya kitu ambacho kitamsitiri barabara kama inavy-olindwa lulu katika kola lake, ili asije akaangukia mikononi mwa watu hao na kumgeuza kuwa ngawira yao." Hakuna njia bora isipokuwa Hijabu, hicho ndiyo kizuwizi na ni mlinzi wa mwanamke. Kwa hakika mwanamke mwenye Hijabu huwa sala-ma kutokana na shari. kwa kuwa mwili wake umesitirika, na mapambo yake nayo hayaonekani mbele ya kila mtu.

Hali ya kuvaa Hijabu inawafanya watu wasimtamani mwanamke huyo kwa kuwa hakuna wakionacho cha kuwafanya wamtamani. Kutokana na hali hiyo huwa wanamuepuka, wala hakiwageuzi kitu chochote cha kuwafanya wamuangalie mwanamke huyo, bali humuogopa na kumuheshimu. Mwisho wa yote watu humuogopa na kumpa heshima yake kama anavyostahiki. Yote hayo yatap-atikana kwa ajili ya kuvaa Hijabu, na hali hii inamaanisha kwam-ba, Hijabu ndiyo mlinzi wako na ni hifadhi ya heshima, na utuku-fu wako. Ewe msichana huu ndio upande mmoja wa falsafa ya Hijabu."

Baada ya maelezo hayo ya Sheikh, msichana yule wa Kikristo alionesha furaha na akaridhishwa na maelezo ya Sheikh kisha akasema, "Sasa nimetosheka na falsafa iliyomo ndani ya kanuni hii ya ki-Islamu, na pia nimefahamu hekima iliyomo na ninapen-dezwa kuingia katika Uislamu." Baada ya hapo msichana akatoa Shahada mbili na akawa Muislamu. Majadiliano haya mazuri ya kidini yanatubainishia kwamba Uislamu unakusudia kuihifadhi hehsima na utukufu wa mwanamke, pia Uislamu unataka kuilinda jamii. Na kwa sababu hizo basi, Uislamu umewajibisha Hijabu kama sharti la msingi kuweza kutimiza malengo hayo.

TOFAUTI YA MWANAMKE MWENYE HIJABU NA ASIYE NA HIJABU

Mmoja wa marafiki zangu alinisimulia tukio la kufurahisha lililom-tokea Muumini mmoja wa ki-Islamu. Tukio hili lilikuwa kama ifu-atavyo. Siku moja Muumini huyo alikuwa akitembea pamoja na mkewe aliyekuwa kavaa Hijabu. Matembezi hayo yalimfikisha katika moja ya bustani zinazotembelewa na watu wa aina tofauti. Ghafla Muumini huyo alijiwa na mtu fulani ambaye naye alikuwa na mkewe. Mke wa mtu huyu hakuwa amevaa vazi la Hijabu na hivyo basi kwa dharau na kejeli alimwambia yule Muumini. "Kwa nini umemvalisha mkeo Hijabu, kwa nini hukumuacha akatoka bila Hijabu kama jinsi alivyo mke wangu? Hijabu ina faida gani?" Jawabu alilotoa Muumini yule lilikuwa la kushangaza na la kishu-jaa. Alimwambia.

"Je unafahamu tofauti ya mwanamke mwenye Hijabu na asiyekuwa na Hijabu? Bwana yule mwenye kejeli akasema "Nini tofauti yake?" Yule Muumini akajibu kwa njia ya kuuliza, je, kuna tofauti gani baina ya taxi na gari ambalo mtu hulitumia yeye binaf-si? Yaani kwa matumizi yake pekee yake." Bwana yule akajibu akasema, "Taxi hutumiwa na kila mtu, wakati ambapo gari maalum linamuhusu mwenyewe peke yake. Hii ndiyo tofauti iliyopo." Basi yule Muumini akasema, "Hali hiyo ndio iliyopo baina ya mwanamke aliyevaa Hijabu na yule asiye na Hijabu.

Mwanamke asiye na Hijabu ni sawa na taxi ambayo kila mtu anaweza kuikodisha na kuitumia. Mwili wa mwanamke huyo huwa wazi na kuonesha mapambo yake na uzuri wake, na kuwafanya watu wavutike kutokana naye, jambo ambalo linaweza kusababisha kutendewa maovu, kama ambavyo mara kwa mara hali hii inavyowapata wanawake wa aina hii. Ama mwanamke aliyevaa Hijabu yeye ni bibi aliyemtukufu, ni maalum kwa ajili ya mumewe, mapambo yake na uzuri wake havionekani kwa kila mtu. Pia watu wenye nyoyo chafu na dhaifu hawamuangalii, na uso wake na mapambo yake havikutani na macho yenye khiana, kwa kuwa amehifadhiwa ndani ya Hijabu.

Kwa hiyo utukufu wa mwanamke huyu na mwili wake vimo ndani ya hifadhi bora, pia bibi huyu hupendwa na kupendeza mbele ya mumewe na kum-fanya mume kuwa na imani na mkewe, kwa sababu ya hifadhi hiyo inayomkinga kuwa na mahusiano na watu wengine kwa njia mbaya." Baada ya maelezo yaliyotolewa na yule Muumini wa kiIslamu, bwana yule mwenye kejeli aliona haya na akaanza kumwambia yule Muumini, "Najuta kwa kukuudhi, kwani maneno yako ni ukweli mtupu, na mifano uliyonipa ni sawa kabisa naom-ba samahani kwa haya niliyokutamkia na pia natubia kwa Mwenyezi Mungu kwa kitendo nilichokitenda na sasa...Kabla bwana huyu hajamaliza kujieleza mkewe alimkatiza na kusema. "Naam; naapa maneno haya aliyosema bwana huyu ni sawa na mfano aliotoa ni mzuri sana, kwani kabla ya leo nilikuwa sijasikia mawaidha kama haya. Mfano huu umeniingia moyoni nami pia natubia kwa Mwenyezi Mungu."

Baadaye yule mume akarudia kukamilisha usemi wake akasema, "Na mimi sasa naiamini Hijabu na kuanzia leo mke wangu atain-gia katika uwanja mtukufu kwa kuvaa Hijabu. Kamwe sikubali mke wangu atoke bila Hijabu, kwani ndiyo vazi la amani na imani. Nafsi yangu haipendi kabisa kumuona mke wangu akidhihiri mbele za watu kama kwamba yeye ni kwa ajili ya kila mtu."

NI LIPI LENGO LA WANAOPINGA HIJABU?

Baada ya kuusoma Uislamu kwa undani, maadui wa Uislamu wameandaa mikakati ya kuuangamiza Uislamu na Waislamu kidogo kidogo, bila Waislamu kuigundua hali hii isipokuwa wachache. Na miongoni mwa mikakati yao ya kishetani katika kutilia mkazo kuiondoa Hijabu, wametumia na bado wanatumia kila njia za kuvutia na madai batili kutimiza lengo lao hilo. Kuna mambo mengi machafu wanayoyaeneza katika jamii ya Waislamu, chini ya kiza kinene chenye ibara zinazovutia na kam-peni ambazo matokeo yake ni mabaya.

Kwa kutumia mbinu za kimaendeleo na utaalamu, wamefaulu kuwapotosha Waislamu, na wakasambaza uovu mwingi. Kwa madai hayo hayo ya maen-deleo na kupigania uhuru na haki za binadamu., uchafu wao umeenea ndani ya jamii zetu za ki-Islamu. Kwa hakika wamefaulu kuzinyang'anya jamii zetu maumbile ya kuwa na haya na heshi-ma. Ibara hizi zimewahadaa Waislamu wengi, wake kwa waume.

Masikini Waislamu hawa wamekuwa wafuasi wa itikadi hizi zenye sumu kali inayovuja kuelekea kwenye maovu na maangamio. Wanawake wa ki-Islamu na mabinti wa ki-Islamu wanafanya upin-zani hadharani dhidi ya vazi hili la ki-Islamu. Wametoka katika nyumba ya utukufu na imani na kuingia katika nyumba ya kiza na upotovu.

Wanawake wetu na wasichana wetu wameathiriwa na mavazi ya Kiyahudi na Kikristo yatokayo kwa wapinzani wa kimagharibi na makafiri wa mashariki. Maadui na wavamizi hawa wamefanikisha kwa kiasi kikubwa lengo lao, kwa kuwa sasa hivi jamii ya ki-Islamu imekwisha tumbukia na kuzama katika dimbwi la matendo machafu. Jamiii ya ki-Islamu ambayo asili yake ni adil-ifu na yenye muruwa, leo imegeuka na kushika bendera ya maovu ya kila aina.

Matukio ya kubaka,17 kupora, udanganyifu, dhulma, kutoa mimba na mengineyo, yameivamia jamii yetu tukufu. Watu hawa wa Ulaya magharibi na mashariki yake, hawali wakashiba wala hawalali wakapata usingizi, ila mpaka watimize lengo lao la kutu-achisha utamaduni wetu wa ki-Islamu. Ni wazi kabisa kwamba watu hao wanaomtaka mwanamke wa ki-Islamu avue Hijabu lengo lao wanataka wamuone mwanamke huyu anafanya ufisadi kwa kumlazimisha akae uchi. Nia yao ni kumuangamiza na kuipotosha jamii kwa jumla. Kumtaka mwanamke asivae Hijabu ni kumuondolea heshima yake na uchamungu wake.

Ewe msomaji wangu, iwapo utataka kuyafahamu vizuri maneno yangu, muulize mzee yeyote katika wazee wa makamo na mababu ambao bado wanayo kumbukumbu ya hali ya mambo ilivyokuwa hapo zamani. Waulize kwa kusema, "Hivi maovu haya yaliyopo sasa hivi ya kuwavunjia heshima wanawake na kuwaba-ka, na watu kudhulumia, mambo haya yakulikuwepo hapo zamani kabla ya miaka ishirini au thelathini iliyopita?" Watakujibu kwa nguvu zao zote, kwa kusema, Hapana kabisa hayakuwako."

17 Kwa asili mia kubwa wakazi wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba, pwani ya Kenya inay-ojumuisha Mombasa, Lamu n.k, Visiwa vya Ngazija na miji mingi ya Tanganyika (Tanzania bara) kwa kipindi kirefu imekuwa ni miji ya amani na utulivu. Mazingira haya mazuri yali-jengeka kutokana na wakazi hao kuwa ni wafuasi wa dini ya ki-Islamu iliyowajenga katika maadili mema ya ki-Islamu. Ni ukweli usiyopingika kwamba hapo zamani hapakuwa na matukio ya kuwavunjia heshima wanawake kama tunavyoyashuhudia mambo hayo leo hii ndani ya miji yetu. Misamiati ya kufadhaika na kubaka haikuwako hapo zamani. Utoaji mimba na kutupa watoto ni mambo mageni kwetu hayakuwako. Ujambazi, utapeli na kutokuaminiana ni misamiati mipya. Lakini haya yote ni mipango ya maadui wa dini ya ki-Islamu, na kwa bahati mbaya Waislamu wamehadaika na mbinu za kikafiri na kujikuta wanapoteza dini yao na hata hiyo dunia waliyopambiwa imewatupa mkono hawana nayo asilani. Msiba uliyoje kwa Umma wa Ki-Islamu!! Mtarjumi.

Sasa yametoka wapi mambo haya maovu na matukio ya kuhuzu-nisha? Watakuambia, "Hali hii imetokana na mambo mengi, mion-goni mwake ni wanawake wenyewe kutembea mabarabarani bila sitara ya kisheria." Hili ndilo jibu sahihi kwa matatizo kama haya ya ubakaji ambayo takwimu zake zinaongezeka kila siku. Iwapo utataka uhakika zaidi, waulize wakazi wa miji michache ambayo wakazi wake bado wanashikamana na sheria za ki-Islamu na imani zao zingali hai na uwaambie, "Hivi katika miji yenu kuna matukio maovu ya kubaka na unyang'anyi kama inavyotokea katika miji mikubwa?" Bila shaka watakujibu hapana. Sababu kubwa ya kutokuwepo maovu kwa wingi katika sehemu hizo, ni kwa kuwa jamii bado inauheshimu na kuulinda Uislamu na kanuni zake zenye hekima.

Maovu mengi zaidi yanajitokeza katika miji au sehemu ambazo zinadai kuwa zimeendelea. Miji hiyo imehusika kwa kiwango kikubwa na ongezeko la maovu ambayo yanakithiri kwa kasi ya kutisha, licha ya serikali zao kutoa adhabu kali kwa wanaohusika kila wanapobainika na kukamatwa.18

Hali hii inaonyesha wazi kwamba kanuni peke yake hazitoshelezi, wala hazinufaishi katika kuirekebisha jamii, bali kinachotakiwa ni kuing'oa mizizi ya maovu kwanza, ili maovu hayo yapate kunyau-ka yenyewe. Kwa kawaida kila kitu kina asili yake, na asili ya maovu yaliyozikumba jamii zetu sasa hivi, ni hizi picha za video wanazooneshwa vijana wetu, 18 Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimekumbwa kwa kiasi kikubwa na matatizo ya mmomonyoko wa maadili, na zinatungwa sheria kali kila leo ili labda? itawezekana kureke-bisha hali hii, lakini bila mafanikio. Tunachokiona ni ongezeko la maovu ambayo yanatende-ka wazi wazi na kila mtu anayashuhudia wakiwemo hao wanaokaa na kutunga sheria hizo kwa matumaini ya kukomesha maovu. Hakuna njia inayoweza kukomesha hali hiyo isipokuwa ni kushikamana na mafunzo bora ya ki-Islamu. Ni muhimu kwa viongozi wetu wakatambua mambo yanayochangia uharibifu wa mwenendo wa jamii na kuhakikisha kuwa wanaing'oa mizizi yake. Mtarjumi.

picha ambazo huwa zinaonesha hali ya maumbile ya siri, isi-toshe huonesha pia matendo ya jinsiya baina ya mke na mume bila kuona aibu wala huzuni kuuchezea na kuudhalilisha uanadamu ambao ni kitu cha thamani, kutokana na kuwa na uwezo wa kutambua nini cha kufanya na nini si cha kufanya. Kitu kingine kinachochangia ni nchi zetu zinaporuhusu uingizaji wa magazeti na majarida yanayochapisha picha zinazoonesha sehemu za siri na kisha magazeti hayo na majarida yanasam-bazwa katika jamii. Maadam asili ya maovu bado ipo kama mifano ya picha za video na majarida tuliyoyataja hapo kabla, basi maovu na matukio machafu yataendelea kutokea siku hadi siku, na kamwe hayataondoka kwa kutegemea kanuni hizi za kidunia.

2

VAZI LA MWANAMKE

NI YUPI MWANAMKE BORA

Sasa napenda kutoa mifano miwili ya wanawake wawili ambao kila mmoja anao mwelekeo wake na mwenendo tofauti na mwenzake, lakini wote wanaishi katika jamii moja. Wa kwanza ni yule mwanamke mwenye kuvaa Hijabu ambayo ni sitara ya imani na ni vazi la ki-Islamu, tena ni vazi la heshima na humpa utukufu mvaji. Kwa kuvaa Hijabu, mwanamke huyu atakuwa amepata radhi za Mola wake na kupata utukufu wa watu wa peponi. Kwa vazi hili mwanamke huyu huvutia mvuto wa ucha Mungu na heshima.

Pia dalili za utulivu hujitokeza kwa mwanamke huyu na dhana njema kwake hutawala fikra za kila amuonaye. Amtazamapo mwenye kumtazama, huwa ni shida kutambua, je, mwanamke huyu ni msichana au ni mtu mzima? Sura yake ikoje nzuri au la? Hutatizika wanaomuangalia. Matokeo yake watu humuangalia kwa jicho la heshima, hakuna awezaye kumkabili kwa maneno chafu au maudhi, kwani anafahamu wazi kwamba mwanamke huyo ameshikamana na dini yake na anaheshimu utu wake. Isitoshe mwanamke kama huyu huwa amejitenga na matendo ya aibu na kujiepusha na wanawake wasio na sitara, na kwa ajili hiyo hayuko tayari kuidhalilisha nafsi yake.

Huo ndiyo mfano wa mwanamke mmoja na namna alivyojiweka katika jamii yake. Kwa upande wa yule mwanamke wa pili, ni yule asiyejali kujisitiri uso wake amevua vazi la la stara, hana aibu wala haya. Kwa maana hiyo ameing'oa imani yake, kwa sababu Mtume anasema: "Mtu kuwa na haya ni sehemu ya imani, na mtu asiye na haya hana imani." Kwa mwenendo wake mwanamke huyu, huwa ni mpinzani mkubwa wa muongozo wa Qur'an na huwa anajidhalilisha kwa kuonesha mapambo yakem, kama walivyokuwa wakionesha mapambo yao wanawake wa zama za kijahiliya kabla ya kuja Uislamu. Isitoshe kwa mwanamke huyu, hali aliyo nayo huwa amejifananisha na wanawake wa Kiyahudi na Kikristo, na huwa yuko mbali na heshima yake na utu wake. Kutokana na kuudhihirisha mwili wake na uso wke na mikono yake, pia kifua chake na sehemu nyingine katika maumbile ya kike. Watu waovu na wenye tamaa huyaona wazi wazi maumbile yake na hapo tayari anakuwa mfano wa bidhaa zilizotandazwa sokoni, kwani kila mtu ana uhuru wa kuziangalia bila mipaka.

Matokeo ya uovu wa mwanamke huyu, ni kupata usumbufu toka kwa wahuni ambapo hatimaye wanaweza kumtendea matendo machafu yanayoweza kumharibia tohara yake. Na iwapo itafikia hali ya kuharibiwa tohara yake, basi atakuwa amepoteza heshima yake na utu wake katika jamii. Hii ni kwa sababu ameacha kuulin-da mwili wake ndani ya vazi la kisheria. Baada ya kuwa mmefahamu namna za wanawake hawa wawili sasa tuwe pamoja kaitka kulinganisha hali zao kati yao na tujiulize masuali yafuatayo.

1.Je ni yupi mwanamke bora baina yao? 2.Yupi kati yao ni mtulivu na anayevutia, 3.Mwenye kujilinda au yule anayeuacha wazi mwili wake? 4.Ni yupi mwenye kuheshimika kati yao, mwenye Hijabu au yule asiye na Hijabu? Bila shaka, mwanamke mwenye Hijabu na ucha Mungu ni bora na ni mtukufu tena ni mwenye thamani kuliko yule mwingine.

KIPINDUPINDU NDANI YA JAMII

Miongoni mwa maradhi yanayoua haraka ni kipindupindu kwa mujibu wa taarifa ambazo huwa zinatolewa baada ya maradhi hayo kuingia katika kijiji au mji. Kila yanapodhihiri maradhi haya, hutangazwa hali ya hatari katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kuwekwa karantini. Kama ilivyo katika kuzuia kipindupindu kisie-nee katika mji au kijiji, na fisadi nyingine ni hivyo hivyo. Sasa basi mtazamo wa Uislamu katika kuitazama jamii ni mtazamo wenye hekima kubwa, na ni mtazamo ambao lengo lake ni kujenga jamii nzuri na safi isiyokuwa na maovu ndani yake. Miongoni mwa mambo yanayoweza kudhibiti amani na ubora wa jamii ni mavazi. Siyo kweli kwamba kila vazi linaweza kukidhi haja hii, bali Hijabu pekee ndiyo jawabu, kwa sharti ya kuwa mvaaji aivae kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na siyo kinyume chake.19

baadhi ya watu wanajaribu kulitia dosari vazi la Hijabu kuwa eti ni vazi linalovaliwa ili kuficha maovu ya hao wanovaa. Upo ukweli fulani kuhusu madai haya, lakini upotoshaji huu wa vazi la Hijabu usiwe miongoni mwa sababu za kuwakatisha tamaa wanawake wa kiIslamu wanaovaa Hijabu kwa kumtii Mola wao, kwani ni mara ngapi watu wanautumia usiku kwa mambo maovu wakati Mwenyezi Mungu ameuweka kuwa ni kipindi cha mapumziko baada ya kazi za kutwa nzima? Kwa hiyo matumizi mabaya ya kitu kizuri hayawi ni sababu ya kukifanya kitu hicho kuwa kibaya. Mtarjumi.

Hijabu humlinda mwanamke kutokana na ufasiki na inamzuia kukhalifu maumbile yake aliyopangiwa kuishi ndani yake. Kwa kanuni hii ya Hijabu, Uislamu unakuwa umeisalimisha jamii na kuilinda isije ikajikuta imeteleza na kuvamiwa na maovu. Hali hal-isi inayojitokeza katika malengo ya msingi kuhusu kanuni hii ya Hijabu, ni kuitakasa jamii na kuisafisha, pindi wanawake watakapofuata sheria ya kuvaa Hijabu. Kinyume chake haitawezekana kabisa kudai kwamba jamii yetu ni safi, wakati wanawake zetu wanatembea bila kujali ni nguo gani wamevaa, kwa kuwa suala la mavazi kwa wanawake linataka litazamwe kwa mapana na marefu isiwe mradi kuvaa tu. Ni mara ngapi tunashuhudia mambo ya aibu na ya kuhuzunisha wanafanyiwa wanawake? Hivyo uchafu unasambaa haraka na kuleta madhara kwa wingi, kama kipindupindu kilichoingia mjini au kijijini. Na kwa ajili hiyo karantini inahitajika kuwekwa na kufuatwa kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu.

Uislamu kwa upande wake unataka kukata na kung'oa mizizi ya fitina na maovu kwa kutumia njia mbali mbali ikiwemo kusisitiza vazi la Hijabu. Pia Uislamu kwa nafsi yake unapinga kwa nguvu uovu na kila jambo linalokuwa ni sababu ya kueneza uchafu ndani ya jamii, miongoni mwa sababu hizo ni mwanamke kutokuwa na Hijabu ambayo ni vazi la kisheria.

KUKOSEKANA SITARA KUNALETA MAOVU

Miongoni mwa maovu na athari mbaya katika jamii, ni wanawake kuacha kuisitiri miili yao ipasavyo, kitu ambacho kimesababisha vijana wetu wa kiume kuteleza na kujikuta wanafanya mambo machafu bila kukusudia. Imam Ali ibn Musa Ar-ridha anasema,"....Imeharamishwa kuangalia nywele za wanawake, kwani katika kuziangalia nywele hizo kunasababisha kuamsha hisia za wanaume ambazo huwafanya waingie katika maovu na mambo yasiyo halali na yasiyopendeza." 20 Hapana shaka kwamba, mwanamke anayetoka nyumbani mwake na kwenda sokoni bila kujali ni vazi gani alilovaa, hajali kama limemsitiri vizuri au hapana, ni wazi kabisa huko njiani ataonekana kwa watu wa aina mbali mbali wakiwemo vijana ambao ndiyo kwanza wanaingia katika rika la ujana na nafsi zao bado hazijaweza kujimiliki kuhusu suala la kijinsiya.

Hali kama hii ni lazima itaamsha hisia za kimaumbile za vijana hao kutokana na jinsi mwanamke huyo atakavyokuwa amevaa na umbile lake linavyoonekana kwa jumla pindi atakapopita mbele yao. Hisia hizi za kimaumbile ni lazima ziamke kwa kuwa ndivyo ilivyo hali halisi. Kwa hali hii basi nafsi za vijana hawa kwa tabia ya maumbile ya mwanaadamu huanza kuhangaika kutafuta njia za kuyatosheleza maumbile yao.

Suala la kujiuliza hapa ni je, vijana hawa watafanya nini? Ikiwa wao sio watu walioshikamana na mafunzo ya dini wala hawafuati miongozo ya ki-Islamu, basi watajaribu kutosheleza hamu zao kwa njia ya siri ambayo ni kujitoa manii jambo ambalo ni hasara na aibu. Ama wengine hufanya baya zaidi ambalo ni kinyume cha utaratibu aliotuwekea Mwenyezi Mungu, hawa hufanya liwati. Kundi jingine wao huamua kuzini na katika huko kuzini huwa wanatumia kila njia kufanikisha azma yao hiyo, ikiwa ni kwa hila au hata kwa nguvu ambayo ni kubaka wanawake mitaani. Matokeo ya ubakaji ni kuvunja heshima za watu na kuwadhalil-isha wanawake.

20 Biharul Anwaar juz 6 uk 130. Kilichokusudiwa hapa bila shaka ni nywele za mwanamke ambaye si maharim wako wala siyo mkeo. Ikiwa nywele tu zinatosha kumuingiza mwanaume ndani ya madhambi, basi ikoje hali ya watu leo hii kwa namna wanawake wa kileo wanavy-ovaa.? Je! Ni kwa kiasi gani wanatuingiza katika madhambi? Leo hii siyo nywele tu bali vifua vya wanawake vinaonekana kwa kila mtu na maungo mengi yanakashifiwa na kila mtu. Hivi kweli kwa hali kama hii vijana wetu watasalimika na maovu? Pia hao kina dada nao watam-laumu nani watakapovunjiwa heshima? Mtarjumi.

Pamoja na matendo haya kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu, pia yanasababisha maradhi hatari na vifo vya ghafla..21 Inakadiriwa kwamba idadi ya hospitali zinazo shughulikia maradhi ya uasherati peke yake inafikia hospitali mia sita hamsini. Hesabu hii ni kwa nchi ya Marekani peke yake. Chanzo cha balaa lote hili ni kwa wale wanawake wasiojali kutenganisha maumbile yao na ya wanaume mpaka wakawa wanaona miili yao haistahiki kulindwa na kupewa hadhi ya pekee. Lakini kila mwanamke asiyezingatia suala la mavazi kisheria ni lazima atambue kwamba, yeye ni mshiriki mkubwa anayesababisha madhambi na mis-iba hii, na anayo sehemu yake ya adhabu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Yote yaliyotajwa hapa sasa hivi, yanatokana na vijana ambao wao siyo watu wa dini wala hawashikamani na Uislamu. Kwa upande wa pili inawezekana vijana hao wakawa ni watu wa dini na wanaambatana na mafunzo ya ki-Islamu na sheria zake, basi vijana hao huzuia hisia zao zisivuke mipaka ya Mwenyezi Mungu na hupambana na matamanio ya nafsi zao na kumlaani shetani asije akawahadaa. Vijana hawa huvumilia kero ya maumbile na kubeba mzigo mzito ambao hawakutarajia kuubeba. Kwa mara nyingine tena mwanamke au wanawake wasiojali sheria ya mavazi kama Mwenyezi Mungu alivyoamrisha, wanabeba uzito wa taabu na maudhi yanayowapata watu hawa wa dini.

21 Asili ya yote hayo ni mwanamke au wanawake ambao kwa makusudi kabisa wanaamua kuvaa nguo ambazo zitahatarisha usalama wao na usalama wa jamii yote. Kuhatarisha usala-ma wao na wa jamii peke yake haitoshi, bali waelewe kwamba wanasababisha vijana wetu wa kiume kuchuma madhambi makubwa, na wakati mwingine kuwaharibia maisha yao ya baadaye kwa kufungwa jela kutokana na hatia ya kubaka. Madhara mengine yaletwayo na matukio ya zinaa na liwati ni pamoja na kuambukizwa maradhi hatari kama vile kisonono, kaswende, na leo ukimwi. Maradhi haya hatari yameleta huzuni na misiba inayotisha katika ulimwengu. Mtarjumi.

KUTOKUVAA HIJABU NA MADHAMBI YA UBAKAJI

Miongoni mwa athari mbaya zinazosababishwa na tabia ya wanawake ya kutokuvaa Hijabu ni yale makosa ya jinai ya kuwabaka wanawake na kuwaingilia kwa nguvu bila hiyari yao. Ni jambo lisilofichikana pindi mwanamke anapouacha wazi mwili wake na mapambo yake, hali hiyo huamsha hisia za kijinsia kwa wanaume. Kwa hakika ni juu ya mwanamke mwenyewe kuulinda mwili wake, mapambo yake na utu wake kutokana na hatari hiyo inayoweza kumkabili.

Hapana shaka kwamba, macho ya vijana wasiokuwa na msi-mamo wa dini, pindi wanpomuangalia mwanamke ni sawa na macho ya mbwa mwitu anapomuangalia kondoo. Pia tunaweza kuyalinganisha macho hayo na macho ya paka anapomuona panya, au tuseme yanafanana na macho ya mnyama mkali wa porini, anapomuona mnyama mwingine au kitu kimngine amba-cho kinamfaa kwa chakula. Siyo ajabu kabisa kwa mazingira kama haya kumkuta mwanamke amenasa ndani ya mtego alio-jitegea mwenyewe kutokana na tabia ya kujitangaza mbele ya watu waovu.

Tabia hii ya ubakaji mara nyingi inatokea katika sura ya kutisha huko kwenye nchi za magharibi ambazo zimeporomoka mno katika suala zima la maadili. Katika ripoti moja kati ya matoleo ya gazeti la The Gurdian la nchini Uingereza iliandikwa kwamba; "Takwimu za polisi zinaonesha kuwa, makosa ya jinai ya kubaka yanaongezeka mwaka hadi mwaka. Katika mji wa Washington peke yake kila baada ya dakika kumi na tano huwa kuna tukio la kubaka, na katika mji mkuu wa Uingereza (London) yalitokea matukio 2095 ya kubaka wanawake na wasichana mnamo mwaka wa 1970 peke yake."22 Haya ni machache katika mengi ambayo tungeweza kukuorodheshea.

22Majallatud-Dastuur Lebanon.

Na miongoni mwa matukio ya kubaka kutokana na wanawake kutokujali kujisitiri kwa mujibu wa sheria na maumbile yao, mimi nimesikia kwamba, kuna rais fulani anayeongoza nchi moja miongoni mwa nchi za Kiarabu, yeye hufanya ziara za mara kwa mara kuvitembelea vyuo vikuu akitafuta mabinti katika vyuo hivyo na kuwachagua wale wazuri na wanaopendeza. Kisha humtoa nje ya msitari binti anayemuona kuwa atamfaa. Baada ya muda mfupi askari wa usalama wa taifa huwa wanakwenda nyumbani kwa binti huyo na kumweleza baba yake kwamba rais wa jamhuri anamtaka binti yake akakeshe naye katika usiku wa siku hiyo!!

Hali kama hii husababisha msiba mkubwa kwa baba, mama, binti huyu na hata familia nzima huingia ndani ya mtihani huu. Msiba huu huwagubika watu hawa kwa sababu wanafahamu wazi kwamba rais huyu ataishi na binti yao kwa usiku huo mmoja tu!! Sasa je, watu hawa watalikataa ombi la rais? Na je, inawezekana kwa watu hawa kuuepuka unyanyasaji unaowasubiri kutoka kwa rais wao? Basi je, matokeo ya jambo hili yatakuwaje? Hapana jambo jingine litakalotokea hapo isipokuwa msichana itamlazimu kuuendea uovu kwa miguu yake mwenyewe. Ataifuata fedheha na aibu hiyo kubwa bila kupenda, na kisha atarudi nyumbani hali ya kuwa amekwishapata hasara ya kuvunjika kwa heshima yake na utu wake pia kagubikwa na kiza la ulimwengu machoni mwake.

Ewe msomaji mpendwa, hapana shaka kwamba watu wanaoso-ma au kusikia unyanyasaji huu, utawaona wanamlaani na kumsh-tumu rais huyu muovu. Lakini hebu tufikiri kidogo juu ya misingi inayosababisha mateso haya na tujiulize swali lifuatalo: Je! Ni nani mwenye makosa? Hivi kweli mwenye makosa siyo yule baba ambaye toka hapo mwanzo alimruhusu binti yake atoke ndani hali ya kuwa maungo yake yako wazi na uzuri wake unaonekana kwa kila mtu? Lau binti huyo angekuwa ni mwenye kujisitiri, hivi unadhani yule rais mpumbavu angelimtamani na kumfanya kuwa kiwindo chake?

Ni baba ndiyo mwenye kustahili lawama tangu ile siku aliponunua television (ambayo ni adui mkubwa muovu aliye-mo ndani) ili kuistarehesha familia yake kwa kuangalia vipndi viit-wavyo kuwa ni vya watu walioendelea!! Baba huyo huyo ndiyo mwenye lawama siku zile alipokuwa akiichukua familia yake kwa ajili ya kwenda sinema kuangalia filamu za watu walio uchi. Na mama pia anastahili lawama... Je ! Siyo yeye yule ambaye alikuwa akizifumua nywele za binti yake na kumpamba utadhani siku hiyo ndiyo siku ya harusi yake na kisha akamwacha kwenda shuleni akiwa katika mazingira kama hayo?

Ni huyo mama aliyekuwa akimchagulia binti yake asiyejuwa kitu mavazi mafupi yanayobana mwilini ambayo hayamsitiri inavy-opasa? Binti naye anapaswa kulaumiwa kutokana na matokeo hayo yenye kiza kinene cha majonzi kwa kuwa ni yeye mwenyewe ndiye aliyechagua tabia ya kuuweka wazi mwili wake, na pia akachagua kupita njia ngumu iliyojaa miba na mawe. Naam, watu hawa ndiyo tabaka la mwanzo la kulaumiwa, na baada ya hapo ndio mnapaswa kumlaani rais yule!!

KUTOKUVAA HIJABU NA MADHAMBI YA UTOAJI MIMBA

Ni vema pia kutaja mambo mengine ambayo yanaletwa na makosa ya jamii inapokuwa imepuuza na kuacha Hijabu. Yapo mengi, lakini yanayotajwa ndani ya kijitabu hiki ndiyo ya msingi. Suala la kutoa au kuharibu mimba ni miongoni mwa athari mbaya ziletwazo na ukosefu wa sitara bora ya kisheria kwa wanawake. Ni mara nyingi inatokea kwa wanawake wasio na Hijabu kuvunji-wa heshima zao na utu wao.

Mwanamke asiyekuwa na sitara bora pindi anapodhihiri mbele ya vijana wenye dhiki ya kukidhi haja zao za kijinsia, hapana shaka vijana hao hushindwa kuyazuwia matamanio yao na hapo ndipo huamua kumbaka. Hapo mwanamke huwa anajikuta ametum-bukia mikononi mwao bila hiyari, na huenda ikatokea bahati mbaya mwanamke huyo anaweza kubeba mimba haramu ambayo hakuitarajia. Kutokana na uovu huu aliofanyiwa hulaz-imika kuitoa au kuiharibu mimba hiyo. Leo hii katika anga la dunia yetu matukio kama haya ni mengi mno. Yako wazi kila mahali na hasa nchi za Ulaya Magharibi na zile zote zinazojaribu kuiga ustaraabu wa magharibi.

Tarehe 28 Februari mwaka 1972. jarida la An Nahaar la Lebanon lilichapisha katika ukurasa wake wa makala maalum kama ifu-atavyo. "Katika mji wa London idadi ya utoaji mimba imeongezeka kutoka wanawake hamsini elfu mwaka 1969 hadi kufikia wanawake themanini na tatu elfu mwaka 1970 na idadi inayokaribia laki mbili mwaka 1971. Na huko Ufaransa hali hii imeongezeka na kufikia kutolewa mimba arobaini na sita hadi mia moja arobaini na tatu katika kila mimba mia mbili wanazobeba wanawake kwa mwaka. Ama huko Urusi, kuna mimba zipatazo milioni sita zinazotolewa kila mwaka.23 Kwa hakika takwimu na taarifa hizi zinatisha, na yote haya ni matokeo ya tabia ya wanawake kuyaonesha wazi maumbile yao na uzuri wao mbele ya kila mtu. Hakuna njia ya kuzuwia mad-hambi haya isipokuwa vazi la Hijabu iwapo litavaliwa kwa mujibu wa sheria na kutunza mipaka ya dini.


3

4

5