• Anza
  • Iliyopita
  • 9 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 16241 / Pakua: 2457
Kiwango Kiwango Kiwango
VAZI LA MWANAMKE

VAZI LA MWANAMKE

Mwandishi:
Swahili

3

VAZI LA MWANAMKE

KUTOKUVAA HIJABU NA UHARIBIFU WA NDOA

Tangu utamaduni wa kutovaa Hijabu ulipokuwa umeenea baina ya wanawake, yapo matatizo mengi yamezuka katika ndoa, na idadi ya matatizo haya inaongezeka siku hadi siku. 23 Jarida la An Nahar la Lebanon tar 28/2/1972. Tatizo hili la ndoa wakati mwingine huwa mume ndiyo sababu kubwa inayochangia uharibifu wa ndoa yake. Hasa pale mume huyu anapochukua fursa ya kutoka yeye na mkewe kwenda kwenye sherehe au mahafali mbali mbali zilizo na mchanganyiko wa wanaume na wanawake au kumpeleka mkewe katika majum-ba ya starehe na sinema. Wakati mwingine mume huyu hupata akaleta nyumbani kwake wageni wanaume na mkewe akaja kuwapokea kwa tabasamu zuri na kupeana nao mikono na chun-gu nzima ya makaribisho mengine ambayo mke wa bwana huyu huwafanyia wageni wa mumewe, ikiwa ni pamoja nakuwaletea matunda na vyakula vingine mbali mbali. Yote haya yanafanyika bila ya mume huyu kukumbuka kwamba wageni hao ni wanaume na jinsi yao kimaumbile inatofautiana na maumbile ya mkewe, pia pande mbili hizi hazina uhusiano wa kisheria.

Katika kipindi cha kubakia hapo, wageni hawa huendelea kupata kila aina ya makaribisho yasiyokuwa na mipaka ya kisheria. Kutokana na hali kama hii mara ghafla mume huyu humkuta mkewe amekwishaanzisha uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa marafiki zake hao. Hapa ndipo mume huyu huzusha ugomvi na mkewe na kuwasha moto wa volkano dhidi yake, pamoja na ukweli ulio wazi kwamba, yeye ndiyo sababu iliyoleta huzuni hii kubwa na msiba ndani ya nyumba yao. Mume huyu anasahau kwamba, yeye ndiye aliyekuwa kiongozi na muandalizi wa njia ya mkewe kulifikia giza hili na dhambi hii kubwa. Baada ya tatizo kama hili baina ya mke na mume, hapo huji-tokeza moja katika mambo mawili. Ama mume huyu aendelee kubaki na mkewe huyu muovu katika hali ya maisha ya dhiki yatakayokuwa yakiumiza roho yake na kuiadhibu nafsi yake, na kutokuaminiana tena na mkewe. Au pengine aende mahakamani ili akapate kufungua madai dhidi ya mkewe na kudai fursa ya kutoa talaka.

Na mara nyingi talaka ndiyo uamuzi ambao mume huuchagua ili atatue tatizo hili. Lakini uamuzi huu unakuja baada ya kutokea fedheha, aibu na unyonge mkubwa katika familia hii. Na mwisho huu mbaya huleta matokeo ya kusikitisha, kwani familia hii hubomoka na maisha mazuri ya ndoa ya wawili hawa huvunjika. Zaidi ya hapo msiba mkubwa hubaki kwa watoto ambao huwa bado wanahitajia kuwa na mama yao. Kuishi mbali na mama, watoto hawa hukosa huruma na upole wa mama yao, pia hukosa malezi mazuri na mwelekeo mwema. Hapo ndipo mahali ambapo hujitokeza fundo la moyo kwa watoto hawa na kujihisi kuwa na upungufu katika jamii wanayoishi. Watoto hawa hubadilika tarat-ibu katika tabia zao na hatimaye hutokea wakajiunga katika magenge au makundi yenye mielekeo mibaya na kujikuta wamo miongoni mwa wezi na majambazi.24

Mengi ya matukio ya aina hii yamekuwa yakitokea katika nchi zisi-zo za Ki-Islamu. Katika moja ya makala zake, gazeti la Kisovieti liitwalo Pravda liliandika kama ifuatavyo: "Asilimia themanini ya makosa ya uvunjaji sheria yafanywayo na vijana wenye umri wa kukaribia balehe (miaka kumi mpaka kumi na tano) yanatokana na kuvunjika kwa familia." Pia likaendelea kueleza gazeti hilo kwamba: "Katika kila matatizo tisa yanayohusu ndoa, moja katika matatizo hayo, matokeo yake huwa mume na mke kupeana tala-ka." Pravda likaendelea kutoa sababu za matatizo hayo kwa kusema: "Sababu za msingi zinazochangia kuleta hali hii, ni kuharibika kwa mwenendo wa jamii kutokana na ulevi wa kupin-dukia.25

24 Hapa kwetu Tanzania uko msamiati usemao: "Watoto wa mitaani." Lakini ukifanya uchun-guzi utakuta kwamba msamiati huu umeundika kutokana na matatizo ya kuvunjika kwa ndoa bila ya sababu za msingi, pia madhara yatokanayo na? ?kukosekana kwa uaminifu ndani ya ndoa za watu ni sehemu kubwa sana inayozalisha watoto wa mitaani. Pamoja na hali hiyo kuna mambo mengine k.m. umasikini. Kwa hakika kila mtu anapaswa kuwa muaminifu katika ndoa yake si kwa maslahi yake tu bali akiangalie kizazi chake kisije kuishia mitaani na kud-hurika kwa mambo mengi yaliyoko huko. Mtarjumi. ti la Al Ahram linalochapishwa mjini Cairo Misri la Tar 26 April 1966 likinukuu kutoka gazeti la Pravda.

Sasa basi, ukweli uliopo ni kwamba matokeo ya yote haya yanakuja kutokana na uovu unaosababishwa na kutokujisitiri wanawake kama sheria inavyowataka. Uislamu kwa upande wake haukuharamisha bila mantiki mavazi yasiyowafunika wanawake kwa mujibu wa sheria, isipokuwa ni kwa lengo la kuzuwia maovu haya, na pia haukufaradhisha vazi la Hijabu kwa mwanamke isipokuwa ni kwa nia ya kumuepusha mwanamke asi-fikwe na maovu haya na mengine mfano wa haya. Kwa hiyo Uislamu unawalazimisha wanawake kuvaa Hijabu ambalo ndilo vazi rasimi kisheria ili kuzuia kuzuka kwa maovu kama yalivy-otangulia kuelezwa.

Magazeti na vyombo vingine vya khabari kila mara vinatuarifu habari mbali mbali zinazohusu matatizo ya ndoa na khiyana zina-zofanyika baina ya mke na mume, na hali hii husababisha watu kupeana talaka na pengine ikasababisha kutokea mauaji. kila unapofanyika uchunguzi, Sababu za msingi zinarudi kwenye upu-uzaji wa Hijabu kwa ile maana yake halisi iliyokusudiwa na Uislamu. Ni mara nyingi tunasoma magazetini au kusikia redioni kwamba mtu kamuacha mkewe na wanawe kwa ajili ya msichana asiye na Hijabu ambaye kakutana naye ofisini au katika mabus-tani ya mapumziko na au mahali pengine. Au ni mara ngapi tume-sikia na pengine kuona mke anamuacha mume wake ili tu akaolewe na kijana aliyekutana naye sinema au pwani wakati wa kuogelea?

Kuna gazeti moja liliandika kama ifuatavyo: "Mtu mmoja alimuua rafiki yake ili amchukue mkewe ambaye alikuwa akijidhihirisha wazi mbele ya bwana huyo bila Hijabu wala aibu. Gazeti liliende-lea kueleza kwamba, kuna mwanamke mwingine ambaye yeye alimuua mumewe kwa msaada wa huyo mpenzi wake na kisha wakamkatakata viungo vyake na kuvitupa ndani ya mfereji wa maji machafu. Bibi huyu alifanya madhambi haya ili tu aolewe na huyo bwana mpya."

Pia kulitolewa habari na gazeti moja la Kiarabu ambalo liliandika tukio moja miongoni mwa matukio yanayosababisha ndoa za watu kuvunjika, hasa mijini ndiko kwenye matukio mengi ya aina hii. Tukio hilo kwa hakika lilikuwa la kuhuzunisha sana, na cha kuhuzunisha zaidi ni kwa kuwa lili-tokea katika moja ya nchi za Ki-Islamu, lau lingekuwa limetokea katika nchi za magharbi, hali hii ingekuwa ni mahala pake kwa kuwa nchi hizo ndiyo vituo vya kila aina ya maovu, kama vile zinaa na uchafu mwingineo. Lakini ni vipi leo mambo haya yana-tokea hata katika nchi takatifu za Ki-Islamu ambazo hapo kabla zilikuwa zimetakasika kutokana na uchafu huo?

Hapana shaka, hayo ni matokeo ya wanawake kuuwacha uta-maduni wao wa Ki-Islamu katika suala la mavazi, pia mienendo ya Waislamu imebadilika na wameshawishika na utamaduni mbaya wa kimagharibi. Kutokana na kupotea kwa Waislamu na kuacha mwelekeo na utamaduni wao, sasa hivi imekuwa kazi ngumu kuyaepuka maovu na balaa hizi isipokuwa njia pekee ni kurudia utamaduni wetu kama alivyotuamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake(s.a.w.w)

Ewe msomaji mpendwa, hebu kaa tayari nikusimulie hicho kisa ili ujionee mwenyewe umuhimu wa Hijabu kwa maana yake kamili na pia ubaya wa kuacha Hijabu: "Naam, wanamichezo wa nchi fulani walitoa mwaliko wa kimichezo kwa mmoja wa wanamichezo mashuhuri wa nchi fulani. Kwa bahati nzuri mwanamichezo mualikwa aliukubali mualiko huo na kufanya safari kuelekea huko akifuatana na mkewe ambaye hakuwa amevaa Hijabu, na kwa sura binti huyo alikuwa kaumbika.

Walipofika uwanja wa ndege wa nchi aliyoalikwa mwanamichezo huyu na mkewe, kwa pamoja walilakiwa na wenyeji wao ambao nao ni wanamichezo. Mwanamichezo huyu mgeni alisalimiana na wenyeji wake kisha akamtambulisha mkewe kwa wenyeji hao nao wakampa mikono mkewe huyu, kitendo ambacho Uislamu umek-iharamisha. Wanamichezo hawa wenyeji walionyesha furaha kubwa sana na tabasamu kwa mke wa rafiki yao kiasi kwamba mmoja wao alimtamani mke wa mgeni wao na akafikiria lau ange-muoa yeye. Isitoshe alifikiria pia njia za kumuwezesha kutimiza azma yake hiyo. Mwisho wa yote alitumia kila ujanja na mbinu za kishetani za kumhadaa bibi yule na akapata fursa ya kukaa naye faragha. Hapo alimuuliza thamani ya mahari aliyopewa alipoole-wa na mumewe, na bila kusita mwanamke yule alitaja thamani ile, k.m. dinari alfu moja.

Bwana yule aliendelea kusema; 'Mimi nitakupa dinari elfu tatu kwa sababu uzuri wako unastahiki hivyo, siyo thamani aliyokupa mumeo ni ndogo mno na kwa kweli amekudhulumu.' Kisha akamuuliza mumeo ana kazi gani afanyayo zaidi ya michezo? Yule mama akajibu; 'Mume wangu ni karani katika wizara fulani.' Bwana yule aligutuka na kusema 'Aah!!! Hii ni dhuluma kubwa uliyofanyiwa, hivi kweli pamoja na uzuri wote ulionao unakuwa mke wa karani? Haiwezekani kabisa, wewe thamani yako ni kubwa mno. Napenda kukufahamisha kwamba, mimi ni mhandisi na ninayo shahada ya udaktari na nimemaliza Chuo Kikuu, nataka kukuoa lakini kwanza mumeo huyu akuache.' Na mwisho yule bwana alimuhadaa mke wa rafiki yao na wakaafikiana afanye kila hila adai talaka toka kwa mumewe naye atamuowa. Yote haya wakati yanafanyika masiki-ni mume yule hana habari anandelea na michezo.

Ziyara hiyo ilipokwisha bwana yule na mkewe wakarudi nyumbani kwao. Baada ya safari yao bwana huyu akaanza kuona mabadi-liko ya tabia ndani ya nyumba yake. Tabia ya mkewe ikawa si nzuri tena, wakati hapo zamani alikuwa akiliona tabasamu la mkewe ambalo lilikuwa likimsahaulisha taabu ya kutwa nzima kazini, leo ni kinyume chake. Baadaye alimuuliza mkewe sababu ya mabadiliko haya. Mke akajibu, 'Wewe umenidanganya.' Mume akasema, 'Nimekudanganya nini?'

Mke akasema, 'Umenioa kwa mahari ndogo ambayo mimi sikustahiki, yuko mtu ambaye anaweza kunioa kwa mahari inayonistahiki na sasa nipe talaka yangu.' Mume huyu akili zilimruka baada ya kusikia majibu ya mkewe. Alipigwa na butwaa la majonzi ambalo yeye ndiye aliyeliandaa siku aliposafiri na mkewe asiye na sitara na kum-tambulisha kwa watu wasio maharimu wake. Hata hivyo bwana huyu alijaribu kumpa rai mkewe abadili uamuzi wake, lakini jitiha-da zake zilishindikana na baadaye akamwacha mkewe kwa uchungu mkubwa hali akiwa bado anampenda. Na yule bibi baada tu ya kuachwa, alisafiri hadi kwa yule bwana aliyemuhadaa akiwa na ushahidi wa talaka mkononi ili akatimize lengo lake la kuolewa upya."

Fikiria ewe msomaji, hili ni tukio katika matukio mengi yanay-oharibu ndoa za watu. Hebu tafuta sababu yake, hutapata isipokuwa ni kwa sababu bibi yule alikuwa hakusitiriwa Ki-Islamu, na lau angekuwa kavaa Hijabu inayositiri maungo yake na uzuri wake, je bibi huyu angetumbukia katika mtego huu? Je, mume huyu naye angeingia katika machungu ya kumwacha mkewe hali ya kuwa bado anampenda kutokana tu uovu aliouandaa mwenyewe kwa kumwacha mkewe bila ya kuwa na sitara ya Ki-Islamu? Lakini taabu hii na machungu haya aliyataka mwenyewe kwa kutomlea mkewe ndani ya malezi ya Ki-Islamu. Na haya ndiyo malipo ya mtu anayekwenda kinyume na kanuni za Ki-Islamu na hukmu za Qur-an.

Wakati huo huo tunajiuliza, hivi kweli mke huyu baada ya kuachwa na yule mume wa kwanza, je ndoa ile kwa huyu mume wa pili ilidumu? Jawabu la swali hili linasema kuwa: "Mara nyingi ndoa za aina hi huwa hazidumu isipokuwa chache tu miongoni mwa hizo, kwa sababu mume wa aina hii huwa hamuowi mwanamke kwa lengo la kujenga maisha ya ndoa kwa maana ya mke na mume, bali huwa anaowa ili tu atosheleze matamanio yake ya kijinsiya na kuyashibisha matamanio yake ya kinyama. Matokeo yake ni kwamba bibi yule aliachwa na kurudi kwenye mji wao hali ya kuwa ni mwenye huzuni na majonzi tele. Alipata hasara ya kumpoteza mumewe wa kwanza ambaye alikuwa akiishi naye kwa kila aina ya mapenzi na huruma. Ewe msomaji mpendwa, hili ni tukio moja tu kati ya maelfu ya matukio ya hiyana za ndoa za watu.

Lakini hebu fanya uchunguzi juu ya sababu zinazos-ababisha hali hii. Huwezi kupata sababu isipokuwa ni ile tabia ya wanawake kujidhihirisha na kuyaacha wazi maungo yao. Lau mwanamke yule angelikuwa na Hijabu, akausitiri uzuri wake ipasavyo, hivi kweli angenaswa katika mtego huu? Na je, lau yule mume angejikuta ameanguka ndani ya machungu yale ambayo kwa hakika yeye mwenyewe ndiye aliyeyaandaa? Hapana shaka kwamba haya ndiyo malipo ya mtu yeyote anayekwenda kinyume na kanuni za Uislamu na hukmu za Qur'an.

NAFASI YA SINEMA NA PICHA ZA VIDEO KATIKA UHARIBIFU WA JAMII

Sinema na picha za video zinachangia kwa kiwango kikubwa katika kuharibu mwelekeo sahihi na wa kweli kwa vijana kutokana na kuonesha filamu zinazohusu mambo ambayo ni ya siri baina ya mke na mume. Isitoshe sinema hizi huonesha maumbile ya shemu hizi mbili za siri wazi wazi kiasi kwamba, hupanda mbegu mbaya kifikra kati ya wasichana na wavulana. Si hivyo tu bali sinema hizi zinawaondolea vijana wetu aibu machoni mwao na kuwapokonya imani, kisha kuwaingiza kwenye matendo maovu na machafu ambayo yanawafanya wasahau utamaduni wao wa Ki-Islamu na kuwafanya waige wanayoyaona humo. Ni mara nyingi sinema na picha za video zimekuwa zikitumiwa kupotosha jamii zetu, kwa kuonesha miili iliyo uchi ya wanawake.

Wacheza sinema huthubutu kudhihiri mbele ya watazamaji kwa kitendo ambacho kwa kweli ni aibu na ni fedheha kwa mwanadamu kukitenda hadharani, na hiyo ni tabia ya kinyama kabisa. Kwa hali hiyo basi, sinema zinatangaza uchafu huu wazi wazi na kuupigia kampeni huu kama kwamba ni kitendo kizuri. Mwenyezi Mungu anajua sana idadi ya maovu haya na matukio yanayotokea kutokana na jamii zetu kuendelea kuoneshwa filamu hizi chafu. Katika kuonesha madhara ya filamu hizi, kuna kijana mmoja wa kiume alikwenda kuangalia filamu zinazohusu mapen-zi kati ya mume na mke. Baada ya kuangalia onesho hilo amba-lo liliyateka mawazo yake na alirudi nyumbani kwao haraka sana. Alipofika tu alimkamata dada yake aliyekuwa kalala na kumtenda kitendo kichafu huku akiigiza namna ya kitendo hicho kama alivy-oona katika filamu. Kitendo hiki kilisababisha maumivu makali kwa nduguye huyu aliyekuwa mdogo kwa umri, maumivu ambayo baadaye yalisababisha kifo cha msichana huyu.26

Bila shaka ndugu msomaji kwa mfano huu mmoja tu, unaona ni jinsi gani sinema zimekuwa ni nyenzo kubwa ya kueneza uchafu ndani ya jamii zetu. Kwa hiyo basi, sinema hizi ni vituo vikubwa wanavyovitumia wakoloni wa magharibi katika kuwavua Hijabu mabinti zetu na hatimaye kuwasukumiza kwenye shimo la maovu. Vile vile vituo wanavyotumia kugeuza vijana wetu kuwa watumwa wa matamanio yanayohusu mambo ya jinsiya na kuwafanya kuwa wasomi wa maraha na upuuzi huo. Sasa hivi imefikia mahali ambapo vijana wetu hakuna wanachokiwaza isipokuwa starehe tu, hawafikirii tena suala la maendeleo au utalaamu wa aina mbali mbali. 26

Jarida la An nahar la Lebanon toleo la 1311 Hizi ni siasa za mataifa hayo makubwa, na lengo lao ni kuona vijana wetu na mataifa yetu hayajikwamui kiuchumi wala kisiasa, ili maendeleo ya viwanda, uchumi na elimu viendelee kuwa chini ya milki yao. Kamwe hawataridhika mpaka watuone sisi Waislammu tunabakia katika unyonge na udhalili, tukiendelea kuwategemea wao kwa kila mambo makubwa na hata madogo, na wao waendelee kuwa watawala wetu. Kwa hakika wametuny-ooshea panga zao mbele ya nyuso zetu na wametufanya kuwa ni vinyago vyao na wanatuchezea na kututumia namna wapen-davyo.

Mpaka hapa mimi nauona umuhimu wa kuelekeza tena usemi wangu kwa Waislamu wote wanaohisi wajibu na jukumu katika dini. Mimi nawaambia kwamba, "Zipigeni vita sana sana hizi sinema za X 27 na wawakemee watu wasiziangalie. Si hivyo tu bali wanapaswa kuwatahadharisha watu, kwani kujiingiza katika mambo hayo licha ya kuwa ni kumuasi Mwenyezi Mungu, bali hali hii inatumikia maslahi ya maadui wa Uislamu na kuharibu mwe-nendo wa vijana wa Ki-Islamu kwa kutumia kigezo cha utaalamu na maendeleo.

MADHARA YA KUCHANGANYIKA WANAUME NA WANAWAKE

Mchanganyiko unaokusudiwa hapa ni ule wa kukaa pamoja wanaume na wanawake wakawa wanatazamana ana kwa ana bila kuwepo kizuizi baina yao kitakacho tenganisha pande mbili hizi. 27Sinema za X ni zile sinema ambazo mara nyingi zinajihusisha kuonesha matendo ambayo hayapaswi kuonekana hadharani na khususan huwa ni matendo ambayo hufanywa kwa siri baina ya mke na mume, tena kwa mujibu wa sheria yaani wawe ni mke na mume waliy-oowana.

Lakini kutokana na wanaadamu kuzama ndani ya maasi dhidi ya Muumba wao na hasa wazungu, matendo haya sasa yamebadilishwa na kuwa mambo yanayofanyika wazi-wazi, siyo kwenye sinema peke yake bali hata picha za Camera na zinafanywa kuwa ni biashara motomoto. Tuseme nini kwa namna watu wasivyokuwa na aibu sasa hivi, kwani wamekubali kuacha ubinaadamu na kuchagua maumbile ya wanyama wasiyostahi kufanya lolote na popote pale. Mtarjumi.

Kutokana na maumbile ya wanaadamu yalivyo, sheria ya KiIslamu haikubaliani na kitendo hiki cha kuchanganyika wanawake na wanaume, na hapana shaka kwamba Mwenyezi Mungu anachukizwa na jambo hili. Kwa nini basi jambo hili liwe baya?

1.Ni kuvunja moja katika sheria za Ki-Islamu (Hijabu) na ni kukaribisha maovu katika jamii.

2.Jambo hili huandaa na kurahisisha njia za kupatikana mahu-siano ya kijinsiya baina ya pande mbili hizi kinyume na utarati-bu uliowekwa kisheria.

3.Jambo hili huwa ndiyo chanzo na sababu ya kuharibu familia na kuzitenganisha na ni kivutio kikubwa cha maovu ndani ya jamii. 4.Jambo hili linasababisha misiba na majonzi, pia linaleta uharib-ifu mkubwa kati ya pande mbili husika.

Kwa hiyo mchanganyiko kati ya wanaume na wanawake ni kirusi chenye maradhi hatari yanayotishia usalama na mwenendo wa familia, kiasi kwamba tunaweza kuyafananisha na maradhi ya kansa ambayo mgonjwa huwa hapati nafuu isipokuwa kwa kuika-ta shemu iliyopatwa na ugonjwa huo na kukiondoa kiini cha ugonjwa. Katika nchi au jamii zilizoruhusu mchanganyiko huu, hapana shaka kwamba zimechangia sehemu kubwa ya ongezeko la maovu na kufikia idadi inayotisha hasa katika mashule na vyuo vikuu ambako wasichana na wavulana wanachangaywa pamoja utadhani ni viumbe wenye jinsiya moja. Matokeo ya mchanganyiko huu ni kugeuka kwa mashule haya na vyuo hivi kuwa vituo vya mafunzo ya uhuni na mambo machafu ambapo lengo lake lilikuwa ni kupafanya kuwa mahali pa kujifunza elimu. Yote haya yanakuja kwa sababu ya kukosekana kwa sitara au kizuwizi cha kuzitenganisha jinsiya hizi mbili.

Katika ripoti moja iliyotolewa na Jaji mmoja wa Kimarekani anasema: "Asilimia 45% ya wasichana wanaosoma katika shule za mchanganyiko hupoteza bikra zao kabla ya kutoka shuleni, na asilimia hii huzidi kadri wasichana wanavyoendelea katika maso-mo ya juu." Huko Uingereza wasichana wamekuwa wakiandaliwa kutembea na vidonge vya kuzuwiya mimba, na kwamba asilimia 80% ya wasichana hutembea na vidonge hivyo katika mikoba yao. Hii ni dalili ya wazi inayotuonesha kwamba, wasichana hao huwa wako tayari wakati wowote ule kutenda kitendo kichafu kwa kuwa kinga wanayo. Wasichana hawa wanayafanya haya kuk-wepa matokeo mazito yanayoweza kuwakuta ndani ya uchafu huo wanaoutenda.28 Lakini je hivi kweli ni sahihi kumuacha msichana akawa katika mazingira kama haya ndani ya jamii hasa ya Ki-Islamu?

Baada ya maelezo haya bila shaka ina dhihiri wazi hekima kubwa iliyomo katika Uislamu katika kupiga marufuku michanganyiko baina ya wanaume na wanawake. Hapana shaka kabisa kwamba, Uislamu lengo lake ni kutaka kuiepusha jamii kutokana na hatari tulizozitaja hapo kabla. Ndiyo maana umeharamisha mchanganyiko kati ya wanaume na wanawake katika sehemu zote, kama vilemashuleni, vyuoni, katika sehemu za sherehe, na kwa ujumla popote katika jamii mchanganyiko kati ya wanaume na wanawake hauruhusiwi.

Yote haya makusudio ni kuihifadhi jamii kutokana na maovu yanayozaliwa na michanganyiko. Na ama hali ya mikusanyiko ya wanaume na wanawake tunayoiona katika msimu wa Hija na katika maeneo matakatifu na pia ndani ya kumbi za Huseiniyyah, mikusanyiko kama hiyo haikuharamishwa hasa kwa kuwa wanawake wanaohudhuria ndani ya maeneo hayo huwa wako katika hali ya kujisitri kama sheria inavyowataka wajisitri. QadhAya Az ziwaj wal Usrah.

4

VAZI LA MWANAMKE

UISLAMU SIYO DINI YA NADHARIA

Mara nyingi tunasoma katika baadhi ya magazeti kwamba, baad-hi ya watu waliohadaika na wasiojuwa chochote kuhusu Uislamu, eti wanajaribu kutoa fikra zao katika kukosoa baadhi ya kanuni za sheria ya Ki-Islamu. Miongoni mwa kanuni ambazo wamekuwa wakijaribu kuzikosoa kwa kutumia kalamu zao ni hili vazi la Hijabu. Waandikapo husema; "Mimi sioni umuhimu wa Hijabu, kwani Hijabu katika maoni yangu sio lazima kwa kuwa inarudisha nyuma maendeleo." Au hupata wakasema kuwa; "Kuna ubaya gani wanaume na wanawake kuchanganyika pamoja?" Na mengine mengi wanasema lakini kifupi ni hayo. Sisi tunawajibika kuwaambia watu hawa na wengine mfano wa hao kwamba; "Ninyi ni kina nani? Ninyi ni kina nani hasa mpaka mnathubutu kutoa maoni yenu dhidi ya desturi na mila ya Mbinguni?

Na mna utuku-fu gani mbele ya maamuzi ya MwenyeziMungu na sheria nzima ya Ki-Islamu? Na je Uislamu ni dini ya fikra za kinadharia mpaka mumediriki kuusemea kwamba mimi naona kadhaa, au mtazamo wangu katika sheria ya Ki-Islamu naona hivi au vile.? Kisha nawauliza hawa wanaosema maneno haya; "Je, ninyi kweli ni Waislamu? Ikiwa wao ni Waislamu wanawajibika kuwa watiifu katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake, pia washikamane na sheria za Ki-Islamu ambazo miongoni mwake ni Hijabu. Na kama ninyi siyo Waislamu basi, hamna haki ya kuingilia mambo ya Ki-Islamu, wala hamna haki ya kutoa maoni yenu potofu mbele ya Umma wa Ki-Islamu.

Mpaka hapa ndugu msomaji nashangazwa na ujeuri wa watu hawa dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na ni kwa misingi gani viumbe hawa dhaifu wamejasirika na kufikia kiasi cha kukosoa hukmu na kanuni za Mwenyezi Mungu? Je wanasahau kwamba Mwenyezi Mungu anasema katika sura al-maidah katika Aya tatu mfululizo: "Na wale wasiyohukumu ( kwa sheria) aliyoi-teremsha Mwenyezi Mungu basi watu hao ni makafiri, madhal-imu, mafasiki.29 Watu hawa mbele ya Mwenyezi Mungu watabeba mzigo mzito kwa makosa yao ya kuhamasisha watu kuvunja amri za Mwenyezi Mungu na kutenda machafu yaliyo katazwa. Malipo (adhabu) yao pia ni mazito kutokana na maneno yao hayo, kwa adhabu kali watakayoadhibiwa kutokana na wao kuunga mkono maasi na kuyatia nguvu yatendwe.

Mimi naamini kuwa, watu hawa hawasemi kutoka katika nafsi zao, bali wao wanatumwa na maadui wa Uislamu wanaoupiga vita Uislamu kupitia nyuma ya pazia. Lengo lao ni kuiangamiza maana nzima ya Uiislamu, na kisha kuwapotosha wasichana na wavulana wa Ki-Islamu. Jambo la kusikitisha na kuhuzunisha ni kwamba, kauli kama hizi zimekuwa zikirudiwa mara kwa mara na katika nyakati tofauti, ima ndani ya magazeti na majarida na au katika mikutano mbali mbali. Kuna lugha nyingi zinazotumika katika kampeni hii ikiwemo lugha ya Kiarabu ambayo inawaun-ganisha Waislamu wa dunia nzima kama lugha ya dini yao.

Yote haya ndugu Waislamu, ni majaribio ya makusudi kabisa yenye lengo la kuivuruga na kuipoteza jamii takatifu ya Ki-Islamu. Kinachotakiwa kwa Waislamu wenye uchungu na dini yao ni kun-yanyuka na kuyapinga magazeti haya kwa kuwa yenyewe ndiyo sauti ya vita vya kuutokomeza Uislamu na Waislamu. Kwa hakika wajibu wa kisheria unamtaka kila Mwislamu kupambana na majaribio haya hatari kwa uwezo wake wote kinadharia na kivi-tendo, hadi lengo la maadui hawa lisitimizwe katika nchi zetu tukufu za Ki-Islamu na jamii za Ki-Islamu popote zilipo duniani. 29Suratul Maidah Aya No 44, 45 na 47.

Kadhalika kukabiliana na maadui hawa dhidi ya njama zao za kutaka kugeuza nchi zetu kuwa ni mapori ya wanyama kufuatia mila zao wanazokusudia kuturithisha.Watu hawa madhalimu, katika nchi zao wamebadilika kutoka katika mila ya wanaadamu na wamekuwa na tabia za wanyama, kiasi kwamba mwanamke na mwanaume wanakidhi matamanio yao mabarabarani kama wafanyavyo wanyama bila kuwa na hisiya zozote za kuona haya wala kuogopa kwamba wao ni viumbe teule na watakatifu kwa kuumbwa kwao kama wanaadamu.

VIPI WAMEFAULU KUTUPOTOSHA?

Sasa tuangalie namna gani watu hawa wamefanikiwa kutupoto-sha, kwa kuwavua binti zetu na wake zetu mavazi ya Ki-Islamu. Pia ni kwa vipi wamefaulu kututeka kwa kupitia anuani ya kutetea uhuru wa mwanamke. Ili kupata ufumbuzi wa suala hili hatuna budi kufanya ziyara ya uchunguzi katika nchi za magharibi na kuiangalia jamii yao, na ni vema pia kufuatilia magazeti yao na majarida ili tuyaone mazingira mabaya wanayoishi wanawake wasio na Hijabu huko kwao. Kwa watu wa magharibi mambo hayaishii kwenye kukosa Hijabu na kutembea kichwa wazi na miundi nje basi. Bali hali yao inakwenda mbele zaidi kiasi kwamba kifua nacho huwa wazi, na wanawake hao kadhalika huvaa nguo nyepesi inayodhihirisha rangi ya mwili hadi kufikia kufanana na mtu aliye uchi kabisa.

Matokeo ya mavazi haya ni umalaya au kutekwa nyara na baa-daye kubebeshwa mimba za haramu kisha kuingia katika kufanya mauaji pindi wanapotaka kuzitoa mimba hizo. Linalojitokeza hapa ni kudhulumu kiumbe hicho kinachotolewa kwa nguvu au muhusika kukumbwa na kifo wakati wa zoezi hilo.

Hali hii ndiyo iliyoko kwenye nchi zinazoitwa zimeendelea. Nchi zetu za Ki-Islamu na Waislamu kwa jumla kwa sasa wanakabili-wa na tishio la hatari hii inayokuja kwa kasi ya ajabu kutoka kwenye hizo nchi za mashariki na magharibi. Kinachotakiwa kwa Waislamu ni kuwa na tahadhari kubwa na kuikabili kasi hii ya hatari inayokuja kutoka katika nchi hizo za mashariki na magharibi. Kwa hakika wameeneza uovu wao katika jamii yetu chini ya kivuli cha utaalamu na elimu. Idadi kubwa ya makosa ya jinai yanayotokea katika nchi zinazo-daiwa kuwa zimeendelea ni mengi mno, ukilinganisha na matukio kama hayo yanayotokea katika nchi zetu za Ki-Islamu. Tofauti hii ni kwa sababu Uislamu unahimiza na kutilia mkazo watu wawe na maadili mema, tabia nzuri na waepukane na kila tabia chafu.

Pamoja na hali hii ambayo kwa kiasi fulani inaone-sha tofauti baina ya nchi za Ki-Islamu na hizo za magharibi, Ni lazima kwa Waislamu kuchukua tahadhari, wasihadaike na hali waliyonayo, kwani hatari inakuja na shari zinaandaliwa dhidi yao, na ni wajibu wa kila Mwislamu kuwa na tahadhari. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayotendeka katika nchi ambazo ndizo zina-zoongoza katika kupiga vita utamaduni wa Ki-Islamu.

1.Nchini Uingereza peke yake karibu filamu 10 zinazohusu mambo machafu hukamilika kutengenezwa kila wiki na kutumwa nchi za nje. Kwa hali hii basi kila mwaka filamu zisi-zopungua 500 hutengenezwa nchini Uingereza na zote ni za kuonesha mambo ya aibu tupu na uchafu ambao jamii yetu inapotea na kuangamia kutokana na yaliyomo ndani ya filamu hizi. 2.Mwaka 1961 polisi wa Uingereza walijaribu kuwaangamiza wanawake wapatao laki moja, ambao kazi yao ilikuwa umalaya na machafu mengineyo, lakini baadaye walitangaza kushindwa kwa jaribio hilo.30

3.Mjini Rome kuna majumba yapatayo mia tano ya malaya, humo ndani mna maelfu ya wanawake ambao kazi yao ni kusubiri wanaume.31

Gazeti la " The Gurdian" liliandika kwamba takwimu za polisi zinaonesha kuwa, makosa ya jinai ya kubaka yanaongezeka mwaka hadi mwaka. Katika mji wa Washington peke yake kila baada ya dakika kumi na tano huwa kuna tukio la kubaka. Na katika mji mkuu wa Ungereza (London) yalitokea matukio 2095 ya kubaka wanawake na wasichana mwaka 1970 peke yake. Haya ni machache katika mengi ambayo tungeweza kukuorodheshea.

EWE DADA WA KI-ISLAMU

Ewe dada wa ki-Islamu nakuomba uyafanyie mazingatio baadhi ya mafunzo ya Ki-Islamu ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu kwetu Tanzania Serikali imejaribu mara kadhaa kuwaondoa mitaani wasichana na wanawake wanaofanya umalaya hadharani, lakini bila mafanikio. Kuna wakati sisi tunajiuliza hivi kweli serikali imedhamiria kupiga vita tabia hizi chafu au la? Swali hili linakuja pale tunapoyaona na kuyasikia makongamano mbali mbali ambayo yanahusu kuitahadharisha jamii kutokana na ugonjwa hatari wa ukimwi. Hivi ni kweli tutaweza kupambana na janga hili kwa mikutano na semina zisizokwisha wakati mitaa yetu kila inapofika jioni wasichana wetu na wanawake wetu wanatoka barabarani wak-isubiri wanaume? Pamoja na hali hiyo, mavazi wanayovaa wanawake na wasichana hao pindi wanapofuatilia mawindo yao, ni mavazi hatari ambayo bila kuuliza ni kichocheo kikubwa kwa wanaume kunasa katika mtego huo.

Binafsi yangu ninaingiwa na mashaka makubwa juu ya lengo na madhumuni ya semina, mikutano pamoja na mabango yanayoitahadhrisha jamii kuhusu janga la ukimwi. Haiwezekani kabisa kuupiga vita UKIMWI wakati vyanzo vyake viko huru ikiwemo kuwahamasisha Watanzania kuwa wazinifu kwa kuwaambia wavae kondom. Hapana shaka sote tunafahamu kwamba, njia kuu ya maambukizo ya ugonjwa huu ni uzinifu. Hivyo basi, ni wazi kwamba kwa utaratibu huu hatuwezi kushinda vita dhidi ya UKIMWI.

31Majumba hayo kwa hapa kwetu yanajulikana kwa jina la madanguro. Imani yangu ni kwamba madanguro hayo yanajulikana fika, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa na jamii au vyombo husika kuyaondosha majumba hayo ili kuisalimisha jamii yetu kutokana na tabia hizi za kinyama. Je, huku nako sikuupalilia UKIMWI uzidi kushamiri katika jamii yetu? Iko wapi hapa dhamira ya kupiga vita UKIMWI? Mtarjumi.

amekupangia ili uweze kufanikiwa duniani na akhera. Mafunzo hayo ni mafunzo mema yatakayo kupandisha daraja ya ubora, imani, na utukufu. Na sina shaka kwamba utafanikiwa na kupata kheri nyingi mno, lakini sharti uyatumie na kushikamana nayo maishani mwako. Hijabu kabla ya mambo mengine: Hijabu pekee ndiyo kinga yako ya kuaminika ambayo itakulinda kutokana na maovu na waovu, na ni hifadhi madhubuti dhidi ya kila aina ya uchafu na wahusikao na uchafu huo. Vazi la Hijabu ewe dada wa Ki-Islamu, ni ujumbe rasmi wa Mwenyezi Mungu kwako, basi mtii Mola wako na tekeleza amri yake. Hakika Hijabu ni kwa faida yako na umewekewa kwa ajili ya kulinda hadhi yako wewe mwenyewe. Dada mpendwa, Muumba wako ni mpole kwako naye anakwambia katika Qur-an,

"Na wala msioneshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za jahiliya." Q. 33:33 Na anasema tena Muumba wako. "Wanawake wateremshe (vizuri) shungi zao hadi vifuani mwao na wala wasioneshe mapambo yao." 24:31 Maelekezo ya Mola wako ndiyo haya, ole wako ukiyapa mgongo utaangamia duniani na akhera.

Dada mpendwa, ufunguo bora wenye thamani kubwa utakaoweza kufungua milango ya dini yako, dunia yako na heshi-ma yako umo ndani ya Hijabu, hebu jitahidi kufuata amri ya Mola wako ili uupate ufunguo huo. Pia fahamu kwamba uzuri wako, thamani yako na heshima yako vimo ndani ya Hijabu. Ole wako kama utaiacha Hijabu, basi uzuri wako na heshima yako vita-poromoka. Ningependa pia ufahamu kwamba, njia ya wewe kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuingia peponi imo ndani ya Hijabu. Kwa hiyo radhi za Mola wako na pepo utavikosa iwapo utaitupa Hijabu. Kadhalika dada mpendwa fahamu kwamba, njia inayoelekea kwenye ghadhabu za Mwenyezi Mungu na motoni inapitia kwenye kuvua Hijabu na kutoitekeleza. Basi ole wako usi-jeanguka ndani ya kina kirefu cha moto wa Jahanam.

Imamu Ali(a.s.) amesema:"Mwanamke ni kama mmea mzuri wenye harufu nzuri, na wala siyo kama nyenzo." Basi ni juu yako ewe dada ujifahamu thamani yako. Usiruhusu mwili wako na mapambo yako yachezewe na kila mtu, isipokuwa mumeo tu. Katika kumsifu mwanamke mchamungu, Bwana Mtume(s.a.w.w) anasema;"Mwanamke mchamungu ni yule anayejihifadhi na kujisitiri mbele ya wanaume wengine, lakini huuacha wazi mwili wake anapokuwa faragha na mumewe, husikiliza ni kitu gani aki-takacho32 mumewe, ni mtiifu kwa mumewe, na wakikaa faragha humpa akitakacho."

Dada yangu katika Uislamu, angalia sana usije ukawa mfano wa bidhaa zilizotandazwa sokoni, au bidhaa za dukani kila mmoja huangalia na kuzikamata kamata apendavyo.33

32 Al kafii juz 5 uk 324.

33 Makusudio ya usemi huu ni kwamba: "Mwanamke muovu ni yule ambaye mwili wake hauna hifadhi popote pale, ndani au nje, akiwa na mumewe au hata mbele ya wanaume wengine." Kwa hiyo mwanamke huyo ni sawa na bidhaa iliyoko sokoni au dukani inatafuta na au inan-gojea wanunuzi waione. Endapo wataipenda watainunua na wasipoipenda wataiacha. Na kawaida ilivyo ni kwamba, bidhaa inapokuwa sokoni au dukani, basi wanunuzi wana uhuru mkubwa katika kuchagua bidhaa wanayoitaka na hapo ndipo mtu huikamata bidhaa hiyo na kuigeuza kila upande ili tu aone kama itamfaa au la. Bwana Mtume(s.a.w.w) anamtahad-harisha mwanamke asiwe ni kiumbe kinachokamatwa na kila mtu kama bidhaa iliyoko sokoni, ni lazima aulinde uwanamke wake na utu wake. Mtarjum

Usitumie vifaa vya kujirembesha na manukato ila unapokuwa nyumbani mwako na nduguzo wanaokuhusu kisheria. Tahadhari tena tahadhari sana na tabia ya kujirembesha kisha ukatoka barabarani, jambo hili ni hatari unaweza ukafanyiwa maovu, pia litakusababishia ghadhabu na laana za Mwenyezi Mungu. Bwana Mtume(s.a.w.w) amesema:"Usijifananishe na wanaume katika mavazi na mambo mengine, bali bakia katika maisha na maum-bile yako ya kike." Bwana Mtume(s.a.w.w) amesema:"Mwenyezi Mungu awalaani wanawake wanaojifananisha na wanaume (katika mavavi na mengineyo) na awalaani pia wanaume wanaojifananisha na wanawake." 34 Ewe dada mpendwa, usipeane mkono na mwanamume asiye kuhusu, japo kuwa yeye ni mion-goni mwa jamaa zako, kama watoto wa ami zako au watoto wa mjomba. Iwapo mwanaume atanyoosha mkono wake kwako mwambie; "Dini yangu na Mola wangu ananizuia kupeana nawe mkono.

Usimuogope mtu ikiwa atachukia au kukasirika kwani radhi ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko radhi za watu. Na kuogopa kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu ni bora kuliko kukasirikiwa na watu. Imesimuliwa ya kwamba Mwenyezi Mungu alimwambia Mtume Isa(a.s.) ; "Ewe Isa iwapo Mimi nitakukasirikia, basi hapana radhi ya mtu yeyote itakayokunufaisha, na iwapo mimi nitakuridhia hapana ghadhabu ya mtu yeyote itakayokudhuru. "35 Usione haya kuvaa Hijabu, bali shikamana nayo kila inapokuwa. Ni lazima popote pale japo iwe ni katika jamii isiyovaa Hijabu, au hata kama umo ndani ya shule au chuo ambacho wengi wao hawana Hijabu wala hawataki kuvaa. Inakupasa uwe na msi-mamo wa dini yako sawa sawa kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika Qur'an; 34 Al kafi juz 5 uk 552 35 Al kafi juz 8 uk 138 "Uwe imara (na msimamo) kama ulivyoamrishwa. 11:112 Mwenyezi Mungu amesema tena.

"Hakika wale waliosema Mola wetu ni Allah kisha wakawa na msimamo (katika dini yao) huteremkiwa na malaika (wakati wa kutoka roho zao na wakawaambia) msiogope wala msi-huzunike na furahini kwa pepo mliyokuwa mkiahidiwa." 41:30 Usijali kelele za wapinzani, sawa sawa wakiwa ni wanawake au wanaume, bali waambie kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Ikiwa ninyi mnatukejeli basi na sisi tutawakejeli kama mnavyotukejeli." Hud:38 Hapana shaka kwamba tabia ya wapinzani wa sheria za Mwenyezi Mungu siku zote imejaa kejeli na dharau dhidi ya

Waumini na Watu Watakatifu. Yote hayo wanayafanya kwani wao hawana utu, na wala hawana dalili wala hoja ya kutetea upinzani na upotofu wao. Na kwa ajli hiyo basi wao hutegemea zaidi njia za kutukatisha tamaa ili tu wapate kufanikisha maovu na maasi yao. Hapana shaka kwamba njia hizi za upinzani ulioshindwa dhidi2 yetu, ndizo hizo hizo walizokuwa wakizitumia kupambana na Mitume wa Mwenyezi Mungu na watu wema na waumini tangu hapo zamani katika historia ya ulimwengu. Mwenyezi Mungu anasema: "Na hapana Mtume yeyote aliyewafikia isipokuwa wao wal-imfanyia kejeli." Al-Hijr: 15:11 Na anasema tena Mwenyezi Mungu: "Hakika wenye kutenda maovu walikuwa wakiwacheka walioamini. Na wanapopita karibu yao wanakonyezana." 83:29-30 "Na pindi wanapowaona husema kuwa hakika hawa wame-potea.83:32

Ewe dada yangu katika Uislamu, je unafahamu kwamba mwenda wazimu hujiona kuwa yeye pekee ndiye mwenye akili na wengine wote ni wenda wazimu, wakati ukweli hauko hivyo?36 Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Basi leo Walioamini watawacheka wale waliokufuru." 83:34 Hapana shaka kwamba, iko siku Mwenyezi Mungu na waumini watawakejeli wapinzani hawa wanaozicheza shere sheria na kanuni za Mwenyezi Mungu. Mwenyzi Mungu anasema; "Mwenyezi Mungu atawalipa kejeli zao na watapata adhabu kali." 9:79 Anasema Mwenyezi Mungu; "Yakawazunguka wale waliyofanya mzaha miongoni mwao, yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha." 6:10 Huu ni mfano mzuri sana kwa hao wanaopinga sheria na muongozo wa Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema tena: "Moto utababua nyuso zao nao watakuwa humo wenye kukenya (meno yao kwa adhabu). (Waambie) Je hamku-somewawa Aya zangu na ninyi mkazipinga? Watasema; Mola wetu! Uovu wetu ulituzidi na tukawa ni watu wenye kupotea." 23:104-106 Maneno haya ya Mwenezi mungu yanaonesha namna watakavyokiri watu hao wenye kejeli kwamba wao katika ulimwengu huu walikuwa waovu, wenye kupoteana kutangatan-ga. Lakini Mwenyezi Mungu atawajibu kwa jawabu kali;

"Atasema (kuwaambia watu hao): Dhalilikeni humo motoni na wala msinisemeshe. (Kumbukeni kwamba) Bila shaka kulikuwa na kundi katika waja wangu likisema; Mola wetu tumeamini basi utusamehe na utuhurumie kwani wewe ndiwe Mbora wa wanao-hurumia. Lakini ninyi mliwafanyia mzaha hata wakakusahaul-isheni kunikumbuka na mlikuwa mkiwacheka. Hakika leo nime-walipa (wema) kwa sababu ya kusubiri kwao, bila shaka hao ndiyo wenye kufuzu." 23:108-111 Kwa hiyo jione mwenye fahari kwa kuvaa Hijabu, kwani umo katika hali ya kuonesha utiifu wako kwa Allah (s.w.t), na unapata thawabu kila hatua yako moja utembeayo. Kilichoko kwa Allah (s.w.t.) ni bora na ni chenye kudumu Basi Je, Hamfahamu?" 28:60."

"Na radhi za Mwenyezi Mungu ni kubwa." 9:72 Kinyume chake katika thawabu ni, yule mwanamke asiye na Hijabu, kwa kuwa anapata madhambi kwa kila hatua yake moja anayotembea. Wapo wanawake wasemao; "Mimi najiamini nafsi yangu siwezi kufanya maasi na maovu, hivyo sioni sababu ya kunilazimisha kuvaa Hijabu." Jawabu la fikra kama hii ni hili lifu-atalo. Kwanza: ni lazima ifahamike kwamba vazi la Hijabu ni jambo la wajibu juu yako kwa mujibu wa sheria kati hali yoyote ile iwayo, sawa sawa ukiwa unajiamini au la. Pili: Kujiamini peke yake hakutoshi kwa sababu.

"Hapana shaka kwamba nafsi ni yenye kuchochea maovu isipokuwa ambayo Mola wangu ameirehemu. "12:53 Kuna wasichana wengi wameteleza na wakajikuta wameingia ndani ya maovu kwa sabau ya kuacha Hijabu. Tatu: Kuishi bila sitara ya Ki-Islamu kunasababisha kuamsha hisia za kimaumbile kwa wanaume wanaokutazama, pia inaweza kuwa sababu ya kukufanyia uchafu bila wewe kutarajia. Je! hili hali-wezekani? Hali kama hii ikikufika, huko kujiamini kwako kutaku-saidia na au kunaweza kuizuwia hali kama hii isitokee? Ewe msichana na mwanamke wa Ki-Islamu, usihadaike na fikra poto-fu, maadui wa Uislamu ndiyo hao hao maadui wa mwanamke, wanaipiga vita Hijabu kwa njia nyingi. Huna budi kuzinduka na kuepuka kampeni hizo sizizo na hekima. Wala usidanganyike na mitego yao iliyomo ndani ya mtizamo wao. Kwa kukuzindua ni kwamba; maneno wayasemayo huenda yakawa yanavutia hasa yanapokuja kwa lugha ya kutaka eti kukukomboa. Maneno yao haya ni sawa na asali tamu lakini ina sumu ukiila itakudhuru. Angalia iwapo utahadaika utakuwa umeiuza nafsi yako na dini yako kwa maadui wa Mwenyezi Mungu, pia fahamu ya kwamba utakuwa umeshawauzia kwa thamani ya kukuangamiza wewe mwenyewe.

Hebu jitahidi kuwa Mwislamu kwa ulimi wako na vitendo vyako. Wachana na nyendo za kiulaya, kwani miongoni mwa malengo yao ni kumtumia mwanamke kama chombo cha kutangaza biashara hali ya kuwa hana sitara. Jilinde kwa Mwenyezi Mungu akuepushe na nyendo zao ambazo nia yake ni kuichafua jamii ya

Ki-Islamu na kuiangamiza. Fahamu ewe dada mpendwa kwam-ba, maendeleo na uungawana kwa mwanamke ni kuwa na sitara inayokubaliana na mazingira na hali yake kama mwanamke. Dada wa Ki-Islamu, utamaduni na uhuru wa kweli unapatikana ndani ya Uislamu na kanuni zake toka mbinguni.

Elewa pia kwamba, uovu na fedheha vitakupata iwapo utakwen-da kinyume na kanuni za Ki-Islamu. Ni wajibu wako kutangaza na kuelimisha hekima ya Hijabu na falsafa yake kwa nduguzo, jamaa na marafiki. Kazi hii ifanye popote, ikiwa nyumbani, shuleni, chuoni, ofisini na sehemu nyinginezo unazoweza kufanya hivyo katika muda wote wa uhai wako. Kufanya tabligh siyo kazi ya wanaume peke yao, bali na wanawake inawahusu kikamilifu. Mtume(s.a.w.w) anasema;"Kila mmoja wenu ni mchungaji na ataulizwa kuhusu uchungaji wake aliokabidhiwa."

Historia inatuonesha kwamba Bibi Fatma(a.s.) alikuwa akifafan-ua mambo yanayohusu sheria kwa wanawake wa Madina. Bibi Zainab binti Ali bin Abi Twalib alikuwa akifundisha tafsiri ya Qur'an kwa wanawake wa mji wa Al-Kufah huko Iraq. Fahamu ya kwamba Mwenyezi Mungu atakulipa thawabu nyingi kwa kila msichana au mwanake atakayefuata nasaha yako ya kuvaa Hijabu na akaongoka kupitia mkononi mwako.

Imesimuliwa ndani ya hadithi kwamba, Mwenyezi mungu alimpelekea ufunuo Nabii Musa(a.s.) akamwambia; "Ewe Musa ikiwa utamrejesha mlangoni kwangu mtu amabaye ni mwenye kuniasi au ukamrejesha uwanjani kwangu mtu aliyepotea, ni bora mno jambo hilo kwako kuliko ibada ya miaka mia moja ambayo mchana utakuwa umefunga saumu na ukasimama usiku ukisali. "37 37 Biharul Anwar juz 2 uk 4.

Hapana shaka kwamba mwanamke asiyevaaa Hijabu ni muasi anayeziasi kanauni zitokazo mbinguni. Basi mtu kama huyu akirudi kwenye uwanja wa Mwenyezi Mungu kisha akashika-mana na Hijabu kutokana na juhudi zako na maelekezo yako, hapana shaka utapata malipo yaliyomo ndani ya hadithi iliyotajwa hapo juu Kwa hakika hayo ni malipo makubwa mno na ni thawabu nyingi. Hivyo basi ifanye nafsi yako iwe miongoni mwa watu wa tabligh hasa kuhusu Hijabu na elekeza tabligh yako baina ya wasichana wenzio na wanawake wenzio.

Usikatae kuolewa: Dada mpendwa endapo atakuja mtu kuku-posa, tafadhali chunguza vitu muhimu na vya msingi. Vitu hivyo ni kama vile Dini yake na tabia yake. Iwapo mtu huyu kakamilika sawasawa kwa sifa mbili hizi usibabaike baina ya kuolewa au hapana. Kwani Dini na tabia ndiyo msingi wa mafanikio ya maisha yako ya ndoa. Usichunguze shahada yake au jinsi yake (utaifa) wala usiangalie suala la mahari kwamba ni kiasi gani anachotoa. Pia nakusihi acha visingizio vya eti mpaka nikamilishe masomo yangu ili nipate shahada ya juu, na sababu zingine zisizokuwa na maana ambazo huenda zikakusababishia kuharibikiwa na Mwenyezi Mungu hatakuridhia. Mtume(s.a.w.w.) anasema:"Atakapokujieni mtu ambaye mwenendo wake na dini yake vinakuridhisheni, basi muozeni mtu huyo, na iwapo hamtamuoze-sha mtasababisha fitina na uchafu duniani."

Kuolewa ni sawa na kiota cha dhahabu ambacho ukikipata utat-ulia na kustarehe ndani yake, na ukweli ulivyo kitakulinda na kuyadhibiti maumbile yako. Mwenyezi Mungu hakumuumba mwanamke ili aishi maisha ya ujane na upweke, bali amemuum-ba aishi na mume bega kwa bega ili wajenge familia na jamii bora katika kuendeleza kizazi cha wanaadamu. Kwa maelezo haya elewa jambo jingine muhimu nalo ni kuwa: Kuchelewa kuolewa ni makosa na ni hatari, chukua tahadhari ya jambo hili.

"Mtume(s.a.w.w) anasema:"Enyi watu! Jibril ameni-jia kutoka kwa Allah (s.w.t) akaniambia, hakika wasichana bikra ni sawa na matunda yaliyomo mtini, matunda hayo yakishawiva na yakachelewa kuchumwa jua litayaharibu, upepo nao ukivuma utayaangushwa chini, hiyo ndiyo hali ya wasichana bikra wakisha vunja ungo hakuna dawa nyingine kwao isipokuwa ni kupata mume (waolewe) na kama hawakuolewa basi hawatasalimika na dhambi, kwani wao ni wanaadamu."

Baada ya Mtume kumaliza kusema maneno haya, alisimama mtu fulani akasema: 'Tumuoze nani basi?' Mtume akajibu: 'Wanaume wanaostahiki kuwaowa.' Yule mtu akauliza ni kina nani hao? Mtume akajibu;'Waumini baadhi yao ni stahiki kwa baadhi nyingine.' Akakariri mara mbili." 38

Ama ikiwa mchumba atakayekuja ni muasi wa Dini yake au kuna kitu kibaya katika tabia yake, kwa mfano asiyeswali, mlevi na mengineyo, huyu mkatae wala usitishike kwa mali yake au cheo chake. Maisha ya upweke ni bora kuliko kuishi na Mume muasi wa Mungu au mwenye tabia mbaya, japo awe na mali au cheo kikubwa. Ewe dada yangu wa Ki-Islamu, muombe Mwenyezi Mungu akukadirie upate mume mwema ambaye ni muumini aliyekusanya sifa za uzuri wa sura, Dini na tabia njema, kwani Yeye Mwenyezi Mungu anasema: "Niombeni nami nitakujibuni maombi yenu." 40-60 38 Al kafi juz 5 uk 337, Biharul Anwar juz 103 uk 371.