• Anza
  • Iliyopita
  • 9 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 4392 / Pakua: 2138
Kiwango Kiwango Kiwango
QURANI MUUJIZA WA MILELE

QURANI MUUJIZA WA MILELE

Mwandishi:
Swahili

QURANI MUUJIZA WA MILELE

QUR ANI: MUUJIZA WA MILELE WA MTUME (S.A.W)

Qur'ani ni muujiza wa Mtume(s.a.w.w) ulio hai na wa milele, kwani Qur'ani ndio kitabu pekee kutoka mbinguni ambacho utashi wa Mwenyezi Mungu ulitaka kibakie ni chenye kuhifadhiwa kutokana na mabadiliko, nyongeza, pia upungufu na kugeuzwa- pamoja na kukithiri kwa watu wenye nia na malengo ya kukibadilisha na wafanyao mipango ya kukizua na kukigeuza- ili kitabu hiki kiwe cha milele na katiba ya milele ya maisha hadi siku ya kiama, maadamu kuna mwanadamu anae ishi juu ya ardhi hii na hilo ni kutokana na hukumu za hali ya juu zilizomo kwenye majalada yake mawili na mafunzo ya kiwango cha juu ambayo kuyatekeleza kwake yana mhakikishia mwanadamu saada na kumpatia maendeleo, kupea na kufikia kwenye daraja za juu mwanadamu huyo.

Hakika Qur'ani pamoja na kuwa ni kitabu cha kielimu, utamaduni hukumu, haki, maadili, adabu, siasa na uchumi, ni muujiza wa mbinguni na wa milele wenye athari kubwa ya kiroho na kimaaanawia ya hali ya juu, hakika kitibu hiki kiliwapituka na kuwashinda wanafasaha wakubwa wa kiarabu waliokuwa na nyaraka au waandishi wa nyaraka saba zilizo kuwa zimetundikwa na kuwekwa kwenye kaaba tukufu, na hawakuweza kuleta mfano wa sura moja tu ya Qur'ani, bali kutokana na kushikwa na aibu walikuwa wakizitoa nyaraka walizo zitundika juu ya kaaba kati ya zile nyaraka zao, na walifanya hivyo kutokana na kushindwa kwao na kudhalilika kwao, pia kutokana na aibu iliyo washika mbele ya Qur'ani ambayo ni muujiza katika fasaha na balagha yake na katika mfumo wake na utaratibu wake, na lau kama wangeliweza kuleta sura moja tu mfano wa Qur'ani kusinge kuwa na haja ya kutumia mapigano na vile vita vibaya na vyenye kuangamiza ambavyo viliwafikia waheshimiwa wao na watu wao na kuvunja utukufu na heshima zao na hadhi zao, pia utawala wao, na kuwavisha vazi la njaa, khofu, udhalili na taabu.

Hii ndio Qur'ani ambayo ni muujiza, na hiki ndio kitabu cha mbinguni cha milele, kitabu ambacho ndani yake kuna mambo yamfikishayo mwanadam kwenye saada na maisha ya neema na raha, kitabu ambacho hueneza kheri na baraka kwa watu wote, na hutawanya amani na salama katika ardhi hii na katika nchii zote, kumepokelewa riwaya mbali mbali kuhusiana na ubora wa kujifunza kitabu hiki na kukisoma pia kukihifadhi na kutekeleza maamrisho yake, na kufanya matendo kwa mujibu wa maamrisho ya kitabu hicho na zingine nyingi ambazo zinazo muhimiza mwanadamu kukitilia umuhimu, na sisi katika sehemu hii tuta ashiria juu ya baadhi ya riwaya hizo kwa uwezo wake Allah na nguvu zake inshaa allah.

1

QURANI MUUJIZA WA MILELE

UBORA WA KUJIFUNZA QUR'ANI NA KUWAFUNZA WENGINE

Kuna riwaya nyingi zilizo pokelewa katika kitabul wassail: sehemu izungumziayo Qur'ani, tutazitaja hapa kwa ajili ya kutabarruk na kwa ajili ya faida ya watu wote.[1] Imepokeleswa kutoka kwa Saad Al-khaffaf, kutoka kwa Abii Jaafar(a.s) amesema:

Ewe Saad jifunzeni Qur'ani hakika Qur'ani itakuja siku ya kiama ikiwa katika hali nzuri na ikiwa ni yenye sura nzuri yenye kupendeza na ambayo haija wahi kuonwa na viumbe (hadi akafikia kusema) mpaka itafika mbele ya mola mwenye utukufu na kukoma au kusimama kwa mola mwenye utukufu, na Menyezi Mungu alie tukuka ataiita kwa kusema: Ewe hojja wangu katika ardhi na maneno yangu ya kweli na mwenye kutamka, inua kichwa chako na omba ukitakacho utapewa na fanya uombezi utakubaliwa uombezi wako, waja wangu umewaonaje ?

Itasema: Ewe mola wangu miongoni mwao wapo walio nilinda na kunihifadhi na hawakupoteza chochote, na kuna miongoni mwao walio nipoteza na kuniacha na kunidharau au kutoniheshimu wala kunitukuza na kusema uongo kupitia kwangu hali ya kuwa mimi ni hoja wako kwa viumbe wako wote, Mwenyezi Mungu alie takasika atasema: Nina apa kwa izza yangu na utukufu wangu na ukubwa wangu au kwa utukufu wa mahala pangu hakika hivi leo nitawapa watu malipo mema kabisa kwa ajili yako, na kwa ajili yako nitawaadhibu watu siku ya leo kwa adhabu yenye kuumiza (hadi akafikia kusema) atakuja mtu mmoja kati ya wafuasi wetu (mashia wetu) na kusema: je hunifahamu, mimi ni Qur'ani ambayo ulikesha usiku kucha na kuyataabisha na kuyaacha maisha yako kwa jili yangu, na itaondoka pamoja nae hadi kwa mola mwenye utukufu na izza na kusema:

Ewe mola wangu mja wako huyu alikuwa ni mwenye hima na mimi, mwenye kunijali, akiwafanyia watu uadui kwa sababu yangu na kuwapinga wengine kwa sababu yangu na kuwachukia wengine, na hapo Mwenyezi Mungu atasema: Muingizeni mja wangu katika pepo yangu na mvisheni pambo kati ya mapambo ya peponi (vazi) na mvisheni kofia ya kifalme na kifakhari iliyo nzuri na akisha mfanyi hivyo ataigeukia Qur'ani na kusema je umeridhia nilivyo mfanyia walii wako (rafiki)? Qur'ani itasema:

Ewe mola hakika mimi nayaona haya kuwa ni machache basi muongezee nyongeza yote ya kheri na nzuri, Mwenyezi Mungu atasema: Nina apa kwa izza na utukufu wangu na ukubwa pia utukufu wa mahali pangu hakika nitampatia siku ya leo vitu vitano pamoja na nyongeza na wale walio kuwa na nafasi au cheo chake na walio kuwa mfano wake: Nayo ni kuwa watakuwa vijana wasio zeeka na wenye afya njema wasio patwa na magonjwa, matajiri wasio patwa na ufukara, wenye furaha wasio huzunika, wenye uhai na wasio kufa. (Hadithi) [2]

Na imepokelewa kutoka kwa Yuunus bin Ammar amesema: Amesema Abu Abdillah(a.s) katika hadithi:

Ataitwa muumini kwa ajili ya hesabu, mara Qur'ani itamtangulia mbele yake ikiwa kwenye sura nzuri yenye kupendeza na itasema: Ewe mola wangu mimi ni Qur'ani na huyu ni mja wako muumini hakika alikuwa akiitaabisha nafsi yake kwa kunisoma na kukaa muda mrefu wa usiku akinisoma na macho yake yakitokwa na machozi na kulia akisali sala za usikku (Tahajjud), basi mridhishe kama alivyo niridhisha, Mwenyezi Mungu alie mtakasifu na jabbar ( mwenye nguvu na shupavu) atasema: Ewe mja wangu nyoosha mkono wako wa kuume na kuujaza kwa ridhaa za Mwenyezi Mungu na kuujaza mkono wake wa kushoto kwa rehma zake kisha akasema: Hii hapa pepo ni halali kwako (ni ruhusa kwako) kuingia soma na kukwea juu na kila akisoma aya moja hukwea juu daraja moja. [3]

MUUMINI NA QUR'ANI

Imepokelewa riwaya kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema:Inampasa kila muumini asife mpaka amejifunza Qur'ani, au awe katika hali ya kuwafundisha watu Qur'ani. [4] Na imepokelewa kutoka kwa Waliid bin Muslim, kutoka kwa Abdaalah bin Lahiiah, kutoka kwa Al-musrij, kutoka kwa Uqbah bin Ammar amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) Mwenyezi Mungu hata uadhibu moyo wa mja alie hifadhi Qur'ani. [5]

Na pia imepokelewa kutoka kwa Nuumaan bin Said kutoka kwa Ali(a.s) ya kwamba Mtume(s.a.w.w) amesema:

Mbora wenu ni yule alie jifunza Qur'ni na kuwafundisha wengine Qur'ani hiyo.[ 6] Na imepokelewa katika Nahjul-balagha kutoka kwa Amirul muuminiin(a.s) ya kuwa amesema katika hotuba yake:Jifunzeni Qur'ani kwani Qur'ani ndio shamirisho la moyo (Rabiil) na jitibuni kwa nuru yake kwani Qur'ani ni tiba ya vifua na nyoyo, na isomeni vizuri kwani ni yenye manufaa (ni nzuri) na ni masimulizi (visa) mazuri, hakika mwanazuoni mwenye kufanya amali zake kinyume na elimu yake ni kama mjinga mwenye kutahayari ambae hazindukani kutoka kwenye ujinga wake, bali hoja juu yake ni kubwa zaidi na majuto kwake ni kitu cha lazima na mbele nae mbele ya Mwenyezi Mungu ni mwenye kulaumiwa zaidi. [7] Na imepokelewa kutoka kwa Muaadh amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) akisema:Hakuna yeyote amfunzae mwanae Qur'ani isipokuwa Mwenyezi Mungu atawavisha wazazi wake kofia ya kifalme na kifakhari siku ya kiama na kuvalishwa mavazi mawili ambayo watu hawaja wahi kuona mfano wake. [8]

Na imepokelewa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) ya kuwa amesema: Watu wa Qur'ani wao ndio watu maalum (yaani watu makhsuusi na wateule) wa Mwenyezi Mungu.[9] Na imepokelewa kutoka kwake(a.s) amesema:

Ibada iliyo bora kabisa ni kusoma Qur'ani. [10] Pia imepokelewa kutoka kwake(a.s) amesema: Qur'ani ni utajiri hakuna utajiri ulio mkubwa na bora baada yake, na hakuna ufukara baada yake.[11] Pia imepokelewa kutoka kwake(a.s) amesema:Watu bora kabisa katika umma wangu ni wabebaji wa Qur'ani na wasimamao usiku kwa ibada.[ 12] Pia imepokelewa kutoka kwake(a.s) amesema:Hakika Qur'ani hii ni mahala pa kupatia adabu za Mwenyezi Mungu, basi jifunzeni adabu za Mwenyezi Mungu kwa kadri muwezavyo, hakika Qur'ani hii ni kamba ya Mwenyezi Mungu, nayo ni nuru iliyo bayana na shifaa (tiba) yenye manufaa, na kinga kwa mwenye kushikamana nayo, na njia ya uokovu kwa mwenye kuifuata. [13] Hadi mwisho wa hadithi.

Na imepokelewa kutoka kwake(a.s) amesema:Mwenye kuisoma Qur'ani mpaka akaihifadhi na kuielewa Mwenyezi Mungu atamuingiza peponi na kumpa uombezi wa watu kumi (10) kati ya watu wa nyumbani mwake ambao wote walikuwa wamewajibikiwa kuingia motoni.[14] Pia imepokelewa kutoka kwake(a.s) amesema:Wabebaji wa Qur'ani (yaani wenye kuhifadhi Qur'ani) katika dunia watakuwa ni watu wenye wenye maarifa zaidi kati ya watu wa peponi. [15] Na imepokelewa kutoka kwake(a.s) amesema:Pindi mwalim akisema kumwambia mtoto: Sema: Bismilaahir-rahmaanir-rahiim, na mtoto yule kusema: Bismillahir-rahmaanir-rahiim, Mwenyezi Mungu humuandikia mtoto yule na wazazi wake na pia mwalim kuepukika na kuwa mbali (Baraa) na moto wa jahannama. [16]

QUR'ANI NI MUOMBEZI MWENYE KUKUBALIWA UOMBEZI WAKE

Imepokelewa kutoka kwa Is'haaq bin Ghaalib [17] amesema: Amesema Abu Abdilaah(a.s) :Mwenyezi Mungu pindi atakapo wakusanya wa mwanzo na wa mwisho ghafla watamuona mtu akiwajia, mtu ambae hawaja wahi kuona mfano wake na haja wahi kuonekana mtu mzuri zaidi yake kamwe, waumini watakapo muangalia nae akiwa ni Qur'ani watasema: huyu ni miongoni mwetu, huyu ni mtu au kitu kizuri sana ambacho tumewahi kukiona, na atakapo wafikia atawapita (mpaka akasema) hadi atasimama kuliani kwa Arshi (kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu) na hapo Mwenyezi Mungu alie jabber na alie takasika atasema: Nina apa kwa utukufu wangu na izza yangu na utukufu wa mahala pangu, hakika hivi leo nitamkirimu alie kukirimu na nita mtweza na kumuhini alie kuhini wewe na kukutweza .[18]

Imepokelewa kutoka kwa Abil jaaruud amesema: Abuu jaafar (a.s) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w): Mimi ndie wa mwanzo nitakae ingia na kwenda kwa Mwenyezi Mungu mwenye izza na utukufu na alie jabber siku ya kiama na kitabu chake na Ahlul bayti wangu kisha umma wangu, kisha nitawauliza mlikifanyia nini kitabu cha Mwenyezi Mungu na Aahlul bayti wangu. [19]

Na imepokelewa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) ya kuwa amesema:Mwenye kuisoma Qur'ani na kudhania ya kuwa kuna yeyote aliepewa kitu bora kabisa kuliko alicho pewa yeye hakika atakuwa amekipa daraja ya chini na kukidharau kitu ambacho kimetukuzwa na Mwenyezi Mungu na kukitukuza kitu ambacho kimepewa daja ya chini na kudharauliwa na Mwenyezi Mungu. [20] Na imepokelewa kutoka kwa Twalha bin Zaid, kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema:Hakika Qur'ani hii ndani yake kuna taa za uongofu na taa zenye kumeremeta, basi mwenye kuangalia na ayatoe macho yake na kuangalia na ayafungue macho kwa ajili ya kupata mwanga, hakika kufikiri ndio uhai wa moyo wenye busara kama atembeavyo mwenye nuru au mwenye kimuli katika kiza akiwa na nuru.[ 21]

Na imepokelewa kutoka kwa Sammaa'ah amesema: Amesema Aba Abdillah(a.s) : Inampasa alie soma Qur'ani anapo soma aya ya Qur'ani ambayo ndani yake kuna maombi au vitisho aombe kheri yenye kutarajiwa kwenye aya hiyo na amuombe ampe afya na amsalimishe pia amuepushae na adhabu.[22]

Na imepokelewa kutoka kwa Sukuniy, kutoka kwa Abi Abdillah, kutoka kwa baba zake(a.s) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) (katika hadithi):Pindi mtakapo fikwa na fitna na kukuchanganyeni kama usiku wenye kiza basi ni juu yenu kushikamana na Qur'ani, hakika Qur'ani ni muombezi mwenye kukubaliwa uombezi wake na ni yenye kumuombe mtu dua au maombi ya adhabu na yenye kuswadikishwa maombi yake (yaani mkweli), na mwenye kuitanguliza mbele yake itamuongoza hadi kwenye pepo na mwenye kuiweka nyuma yake itamswaga hadi motoni nayo ni dalili njema ijulishayo na kuongozea kwenye njia ya kheri, nacho ni kitabu ambacho ndani yake kuna ufafanuzi na ubainifu, nayo ni kauli ya kweli na yenye kukata shauri na wala sii upuuzi, na ina dhahiri na batini, dhahiri yake ni hukumu na batini yake ni elimu, dhahiri yake ni yenye kustaajabisha na nzuri na baatini yake inakina, inazo maana za ndani na katika kila maana ndani yake kuna maana nyingine, maajabu yake si yenye kuhesabika na maajabu yake si yenye kumalizika na kuzeeka wala kuchoka, ndani yake kuna taa za uongofu na miali ya hekima na dalili za maarifa kwa mwenye kufahamu sifa zake, basi mwenye kuangalia na aangalie na aziangalie sifa hizo, na azifikishie mboni ya macho yake, ataokoka kutokana na maangamio na kuepukana na mabalaa, hakika kufikiri ndio uhai wa moyo wenye busara kama atembeavyo mtu mwenye kimuli katika kiza akiwa na nuru, basi ni juu yenu kushikamana na njia bora ya kuwaokoa na kuwa na matarajio (Amal) au mategemeo machache. [23]

2

QURANI MUUJIZA WA MILELE

MTUME (S.A.W) NA QUR'ANI

Imepokelewa kutoka kwa Maymuun Al-qaddah [24] kutoka kwa Abi jaafar(a.s) (katika hadithi) amesema:Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): Hakika mimi ninastaajabu sana kwanini sichoki pindi ninapo soma Qur'ani. Na imepokelewa kutoka kwa Jaafar bin Mohammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Amiirul muuminiin (a.s) katika maneno yake marefu akiwasifu wachamungu amesema: (Ama usiku niwenye kunyoosha miguu nyayo na miguu yao huku wakisoma juzuu za Qur'ani na wakiisoma kwa utaratibu (kwa kisomo cha tartiil), wakizihuzunisha nyoyo zao kwa Qur'ani hiyo na wakizitia bishara na furaha nyoyo zao kwa Qur'ani hiyo wakiziamsha huzuni zao, wakiyalilia madhambi na makosa yao na kutokana na maumivu ya majeraha yao, wanapo fika kwenye aya ambayo ndani yake kuna vitisho huyafungua masikio ya nyoyo zao na kuisikiliza vema na kufungua macho yao, na kutokana na aya hizo miili yao husisimuka na nyoyo zao kuingiwa na khofu na kudhania ya kuwa kelele za moto wa jahannam na milindimo yake (miungurumo) yake imo ndani ya masiko yao, na pindi wanapo ifikia na kuisoma aya yenye kutia shauku na kuhamasisha husimama kwenye aya hiyo kwa huku wakiwa wameshikwa na tama ya mambo hayo, na nyoyo zao kuiangali kwa shauku kubwa na hudhania kuwa ndio lengo na kilele cha macho yake.[ 25]

Na imepokelewa kutoka kwa Abi Hamzah At-thamaliy, kutoka kwa Abi jaafar(a.s) amesema: Amesema Amiirul muuminiin(a.s) je nikufahamisheni mwanazuoni wa kweli wa fiqhi? Ni yule ambae hawakatishi tamaa watu kutokana na rehma za Mwenyezi Mungu na hawaaminishi na adhabu ya mwenyezi Mungu na hawakatishi tamaa kutokana na roho ya Mwenyezi Mungu na hawaruhusu watu na kuwarahisishia kumuasi Mwenyezi Mungu na haiachi na kuitelekeza Qur'ani kwa kuichukia na kushikamana na kitu kingine, fahamuni ya kuwa hakuna kheri katika elimu yoyote ambayo haina ufahamu, fahamuni ya kuwa hakuna kheri yoyote katika kisomo ambacho hakina mazingatio ndani yake, fahamu ya kuwa hakuna kheri katika ibada ambayo hakuna ufahamu wa ndani (wa sheria ya ibada) katika ibada hiyo.[26]

WATU WA QUR'ANI NA FADHILA ZAO

Imepokelewa kutoka kwa Sukuniy [27] kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :Hakika watu wa Qur'ani wako kwenye daraja ya juu kabisa kati ya wanadamu isipokuwa manabii na Mitume mursal, kwa hiyo basi msizidharau haki za watu wa Qur'ani, hakika wanayo nafasi tukufu mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na alie jabber. Na imepokelewa na Abdallah bin Abbas kutoka kwa Mtume (a.s.w) amesema: Watu bora katika umma wangu ni wabebaji wa Qur'ani na watu wa usiku ( wasimamao usiku kwa ibada). [28] Pia imepokelewa kutoka kwa Abi Said Al-khudriy amesema: Amesema Mtume(s.a.w.w) :Wabebaji wa Qur'ani ni watu wenye maarifa (Urafaau) zaidi kati ya watu wa peponi .[29]

Na imepokelewa kutoka kwa Imam Hassan Al-askariy(a.s) katika tafsiri yake, kutoka kwa baba zake kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) ya kuwa amesema:Wabebaji wa Qur'ani ni wenye kuhusishwa na rehema za Mwenyezi Mungu, na ni wenye kuvishwa nuru ya Mwenyezi Mungu, wenye kufundishwa maneno ya Mwenyezi Mungu, wenye kukurubishwa kwa Mwnyezi Mungu, mwenye kuwapenda hakika amempenda Mwenyezi Mungu, na mwenye kuwafanyia uadui hakika amemfanyia uadui Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humuepushia mwenye kusikiliza Qur'ani mitihani na mabalaa ya dunia, na mwenye kuisoma humuepushia mitihana na mabalaa ya Akhera na nina apa kwa haki ya yule ambae nafsi ya Mohammad iko mikononi mwake, mwenye kusikiliza aya moja ya kitabu cha Mwenyezi Mungu hali ya kuwa ni mwenye kuitakidi (hadi akasema) ni mwenye malipo makubwa kuliko mlima wa Dhahabu wa Habiir autoa sadaka, na mwenye kusoma aya moja ya kitabu cha Mwenyezi Mungu hali ya kuwa ni mwenye kumuitakidi Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko vitu vyote vilivyo chini ya Ardhi hadi chini ya Ardhi .[30]

Na imepokelewa kutoka kwa Fudhailiy bin Yasaar, kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema: Mwenye kuhifadhin Qur'ani na kutekeleza amri zake yuko pamoja na wasuluhishaji (mitume) watukufu na wema. Na imepokelewa kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema:Nimemsikia akisema: Hakika mtu yule ambae anajifunza Qur'ani na kuihifadhi kwa matatizo na mashaka makubwa na akiwa ni mchache wa kuhifadhi, ana malipo ya aina mbili. [31]

VIJANA NA USOMAJI WA QUR'ANI

Imepokelewa kutoka kwa Minhaal Al-qaswaab[32] kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema: Mwenye kusoma Qur'ani hali ya kuwa ni kijana mwenye imani, Qur'ani huchanganyika na nyama yake na damu yake na Mwenyezi Mungu humuweka pamoja na wajumbe watukufu na walio wema na Qur'ani huwa ni kizuizi kati yake na mabalaa ya siku ya kiama itasema: Ewe mola hakika kila mwenye kutenda amali amepata malipo ya amali zake isipokuwa mtumishi wangu, basi mpatie yatokanayo na utoaji wako na ukarimu wako, akasema: basi Mwenyezi Mungu alie tukuka na jabber atamvisha mavazi mawili kati ya mavazi ya peponi na kichwani mwake atavishwa taji la utukufu kisha ataambiwa je tumekuridhisha kwa haya tuliyo kupa? Qur'ani itasema: Ewe mola nilikuwa nikimtakia yaliyo bora zaidi kuliko haya, akasema: basi akapewa amani kuliani kwake na kukaa milele peponi kushotoni mwake, kisha kuingizwa peponi na kuambiwa: Soma aya moja na upande daraja moja, kisha ataambiwa: Je tumemfikisha mahala pake na tumekuridhisha? Atasema: Ndio, pia atasema: Na mwenye kuisoma sana na kuisoma mara kwa mara bila kuiacha tena kuisoma kwa taabu kutokana na ugumu wa kuhifadhi Mwenyezi Mungu alie takasika atampa malipo ya usomaji huo wa taabu mara mbili.[33]

Na imepokelewa kutoka kwa Abaan bin Taghlib kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema (katika hadithi):Mwenye kupewa Qur'ani na imani, mfano wake ni kama mfano wa tunda harufu yake ni yenye kupendeza na ladha yake ni nzuri, ama yule ambae hakupewa Qur'ani wala imani mfano wake ni sawa na mti wa Handhaala ladha ya tunda lake ni chungu na wala halina harufu yeyote. [34]

Na imepokelewa kutoka kwa Fudhaili bin Yassar, kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) Jifunzeni Qur'ani kwani siku ya kiama itamjia mwenye kuisoma ikiwa katika sura ya kijana mzuri sana, mwenye rangi yenye kubadilika na itamwambia: Mimi ni Qur'ani ambayo ulikuwa ukikesha usiku wako kwa kunisoma na kulitia kiu koo lako na kuya kausha mate yako na kutiririsha machozi yako kwa kunisoma (hadi akasema) basi pokea bishara ya furahia mara litaletwa taji na kuwekwa kichani mwake, na kupewa amani kuliani mwake na kukaa milele peponi kushotoni mwake na kuvishwa mavazi mawili kisha kuambiwa: Soma na ukwee juu, kila atakapo soma aya moja atakwea juu daraja moja na wazazi wake watavishwa mavazi mawili wakiwa wote wawili ni waumini, kisha wata ambiwa haya ni malipo ya kumfundisha mwanenu Qur'ani.[35] Na imepokelewa kutoka kwa Al-asbagh bin Nabaatah amesema: Amesema Amirul muuminiin(a.s) :Hakika Mwenyezi Mungu atawaadhibu watu wote wa Ardhini na hata muacha na kumbakisha yeyote kati yao ikiwa watamuasi (wataasi na kufanya makosa) na pindi akiwaangalia wazee wakitoka na kutembea kuelekea kwenye sala na watoto wakijifunza Qur'ani atawahurumia na kuichelewesha adhabu hiyo. [36]

WABEBAJI WA QUR'ANI NA SIFA ZAO

Imepokelewa kutoka kwa Amru bin Jami'i [37] kutoka kwa Abi Abdillah amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w): hakika watu wanao stahili kunyenyekea zaidi au kuwa wanyenyekevu zaidi kisiri na kidhahiri ni wabebaji wa Qur'ani, na watu wenye haki zaidi ya kusali na kufanya matendo kisiri na kidhahiri ni wabebeji wa Qur'ani, kisha akaita kwa sauti kubwa: Enyi wabebaji wa Qur'ani! Kuweni wanyenyekevu kwa Qur'ani hiyo Mwenyezi Mungu atakuinua na kukutukuza na wala usijitukuze na kujiiinua kwa Qur'ani hiyo Mwenyezi Mungu atakutweza na kukushusha daraja au kukudhalilisha, ewe mbebaji wa Qur'ani! jipambe kwa Qur'ani hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu atakupamba kwa Qur'ani hiyo, wala usijipambe kwa watu kwa Qur'ani hiyo Mwenyezi Mungu akakutia aibu na kasoro kwa Qur'ani hiyo, mwenye kusoma Qur'ani nzima na kuihitimisha malipo yake au hadhi yake ni kuwa hasiwe jahili kwa yule asie mjua na asighadhabike kwa yule mwenye kughadhabikiwa na asihuzunike kwa kitu chenye kuhuzunisha lakini yeye asamehe na kufuta yaliyo pita na atoe msamaha na afanye upole kwa ajili ya kuitukuza Qur'ani na mwenye kupewa Qur'ani kisha akadhania ya kuwa kuna yeyote kati ya watu alie pewa kitu bora kabisa kuliko alicho pewa yeye hakika atakuwa amekitukuza kitu kilicho twezwa na Mwenyezi Mungu na amekitweza kitu kilicho tukuzwa na Mwenyezi Mungu.[38]

Na imepokelewa kutoka kwa Abi Jaafar(a.s) amesema:Kuna aina tatu za wasomaji wa Qur'ani: Wa kwanza ni yule mtu ambae ameisoma Qur'ani na kuifanya kuwa ni bidhaa ya biashara na kuitumia kuwavutia wafalme na watawala, na kuitumia kujifanya bora kwa watu, na mtu wa pili ni yule ambae ameisoma Qur'ani akaihifadhi herufi zake na kuipoteza mipaka na hududi zake na akaiweka kama kikombe kitupu kisicho na kitu, Mwenyezi Mungu asijaalie kuwepo watu wengi wa aina hii (awaangamize) wabebaji wa Qur'ani mfano wa mtu huyu, na mtu wa tatu ni yule ambae ameisoma Qur'ani na kuifanya dawa au tiba ya moyo wake na akakesha usiku kucha akiisoma na kujitia kiu mchana akiisoma kwenye sehemu zake za kusujudia, na kukihama kitanda chake akijishughulisha na usomaji wa Qur'ani hiyo, kutokana na watu mfano wa huyu Mwenyezi Mungu huyaondoa na kuyaepusha mabalaa, na kutokana na watu hao Mwenyezi Mungu huwanusu watu kutokana na maadui na kwa watu hao Mwenyezi Mungu hutelemsha mvua kutka mawinguni, nina apa kwa jina la Mwenyezi Mungu wasomaji wa Qur'ani mfano wa hawa ni watukufu zaidi kuliko Baruti (Kibriitil-ahmar). [39]

Na imepokelewa kutoka kwa Hussein bin Yaziid kutoka kwa Swaadiq(a.s) kutoka kwa baba zake(a.s) kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) katika (hadithi ya makatazo) amesema: Mwenye kusoma Qur'ani kisha akanywa vitu vya haram au akaathirika na kupenda dunia na mapambo yake, basi atawajibikiwa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa ikiwa atatubia, fahamuni ya kuwa hakika mtu huyo ikiwa atakufa bila kutubia itamtolea hoja siku ya kiama na haita muacha wala kufarakiana nae isipokuwa baada ya kumuangusha na kubatilisha hoja zake.[40]

Na imepokelewa kutoka kwa Ismail bin Abi Ziyaad kutoka kwa Swaadiq(a.s) kutoka kwa baba zake(a.s) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a) watu wa aina mbili katika Umma wangu wakiwa wema Umawangu nau utakuwa mwema na ikiwa wataharibika Umma wangu nao utaharibika: Nao ni watawala na wasomaji wa Qur'ani).[41] Na imepokelewa kutoka kwa Sukuniy, kutoka kwa Aba Abdillahi kutoka kwa baba zake(a.s) amesema: Mwenye kusoma Qur'ani hali ya kuwa ni mwenye kula mali za watu au kuwatawala kwa kupitia Qur'ani hiyo atakuja siku ya kiama uso wake ukiwa ni mifupa mitupu, usiokuwa na nyama.[42]

3

QURANI MUUJIZA WA MILELE

MWENYE KUIJUA QUR'ANI NA ASIFUATE AMRI ZAKE

Imepokelewa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) katika Hadithi[43] ya kuwa amesema: Mwenye kujifunza Qur'ani na hakufuata wala kutekeleza Amri zake na kuathirika na mapenzi ya dunia na mapambo yake, atawajibikiwa na ghadhabu ya Mwnyezi Mungu na atakuwa katika daraja moja pamoja na Mayahudi na Wakiristo ambao walikiweka kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa kutaka umashuhuri na kwa kuitaka dunia, siku ya kiama atakutana na Mwenyezi Mungu uso wake ukiwa ni mifupa mitupu usio kuwa na nyama na Qur'ani kumrusha kinyumenyume hadi kwenye motoni na kuangukia kwenye moto huo pamoja na walio ingia humo, na mwenye kusoma Qur'ani na hakutekeleza amri zake Mwenyezi Mungu atamfufua siku ya kiama akiwa kipofu na atasema:

Ewe mola kwanini umenifufua kipofu ilihali nilikuwa ni mwenye kuona. [44] Atasema:

Vile vile zilikujia aya zetu ukazisahau na hivyo hivyo leo unasahaulika. [45]

Na hapo itatolewa amri ya kumtupia motoni, na mwenye kusoma Qur'ani kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kuzama katika kuifahamu dini, atakuwa na thawabu mfano wa walizo pewa malaika, Manabii na Mitume, na mwenye kujifunza Qur'ani akitaka kujionyesha na kuwa mashuhuri na ili ajigambe kwa Qur'ani hiyo mbele ya wajinga na kujifakharisha kwa maulamaa na kuitafuta dunia kwa Qur'ani hiyo, Mwenyezi Mungu ataitenganisha mifupa yake siku ya kiama na hakutakuwa ndani ya moto mtu mwenye adhabu kali zaidi kuliko mtu huyo na hakuna aina yoyote ya adhabu isipokuwa ataadhibiwa nayo kutokana na ukubwa wa ghadhabu hiyo na chuki yake, na mwenye kujifunza Qur'ani na kuwa mnyenyekevu kwenye elimu na kuwafunza waja wa Mwenyezi Mungu huku akiyataka malipo ya Mwenyezi Mungu hakuta kuwa ndani ya pepo mwenye thawabu nyingi zaidi kuliko yeye na hakutakuwa na kitu kizuri isipokuwa atakuwa na hisa yake kubwa kwenye kitu hicho na atakuwa na mahala au nyumba tukufu zaidi.[46] Na imepokelewa kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) amesema:Hakika katika moto wa jahannam kuna bonde ambalo watu wa motoni kila siku wanaomba msaada waokolewe na bonde hilo (hadi akasema) akaulizwa: Adhabu hiyo ni ya mnywa pombe kati ya watu wa Qur'ani na taarikus- salaa (wenye kuacha kusali)? .[47]

Na imepokelewa kutoka kwa Abil-ashhab An-nakh'iy amesema: Amesema Ali bin Abi Twalib(a.s) :Mwenye kuingia katika Uislaam kwa utiifu na kusoma Qur'ani kidhahiri, basi kila mwaka anayo dinari mia mbili katika baytul-maali ya Waislaam (Hazina ya Waislaam) na ikiwa atazuiliwa pesa hiyo duniani ataipata siku ya kiama ikiwa kamili na mahala ambapo atakuwa akiiihitajia zaidi. [48] Na imepokelewa kutoka kwa Mohammad bin Ali bin Hussein amesema: Amesema Abu Abdillah(a.s) : Wanawake msiwaweke vyumbani na wala msiwafundishe kuandika na wala msiwafundishe surat Yuusuf bali wafundisheni kusokota sufi na surat Nuur- Hadithi.[49] Anasema muandishi : Makusudio ya kukataza ni yale matendo ambayo ndani yake kulikuwa na fitina.

KUWA NA QUR'ANI WAKATI WOTE

Imepokelewa kutoka kwa Muawia bin Ammar[50] kutoka kwa Aba Abdillah(a.s) katika usia wa Mtume(s.a.w.w) kwa Ali(a.s) amesema: Ni juu yako kusoma Qur'ani wakati wote. Na imepokelewa kutoka kwa Zuhriy amesema: Nilimuuliza Ali bin Hussein(a.s) :Ni matendo gani au ni amali zipi zilizo bora? Akasema: Hali yenye kuhama au kuondoka, nikasema ni ipi hali hiyo yenye kuhama? Akasema: Ni kuifungua Qur'ani kwa kuisoma na kuihitimisha yote, kila unapo soma mwanzo mwake huendelea na kufikia mwishoni mwake (yaani huendelea hadi mwishoni mwake) [51] Na imepokelewa kutoka kwa Hafs amesema: Nilimsikia Mussa bin Jaafar(a.s) akisema: katika Hadithi: Hakika daraja za pepo ziko sawa na kiwango cha aya za Qur'ani huambiwa msomaji, soma na upanda daraja moja, hapo basi atasoma kisha atapanda juu daraja moja.[52]

Na imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Sulaiman, kutoka kwa Abi Jaafar(a.s) amesema:Mwenye kusoma Qur'ani hali ya kuwa amesimama kwenye sala yake, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi aisomayo mema mia moja na mwenye kuisoma katika sala yake hali ya kuwa ni mwenye kukaa, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi moja mema khamsini (50) na mwenye kuisoma sehemu nyingine tofauti na sala, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi mema kumi (10). [53]

Na imepokelewa kutoka kwa Bashiir bin Ghaalib Al-asadiy kutoka kwa Hussen bin Ali(a.s) amesema: Mwenye kusoma aya moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu alie takasika katika sala yake hali ya kuwa ni mwenye kusimama, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi mema mia moja, na ikiwa ataisoma sehemu nyingine tofauti na kwenye sala, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi mema kumi na ikiwa ataisikiliza Qur'ani humuandikia kwa kila herufi jema moja, na ikiwa ataihitimisha Qur'ani usiku, malaika humtakia rehma hadi asubuhi na ikiwa ataihitimisha mchana husaliwa na kutakiwa rehma na malaika walinzi mpaka imfikie jioni, na maombi yao kwake hujibiwa na hilo ni bora kwake kuliko yote yaliyomo mbinguni na ardhini, nikauliza:Haya ni malipo ya alie soma Qur'ani, je yule ambae hakuisoma? Akasema: Ewe ndugu wa bani Asad hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kutoa mtukufu na mkarimu akisoma alicho nacho humpa kwa kadri ya hicho alicho nacho. [54]

4

QURANI MUUJIZA WA MILELE

MWENYE KUSIKILIZA QUR'ANI

Imepokelewa kutoka kwa Mohammad bin bashiir [55] kutoka kwa Ali bin Hussen(a.s) na ameipokea hadithi hii kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema: Mwenye kusikiliza herufi moja ya kitabu cha Mwenyezi Mungu bila ya kusoma, Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja na kumfutia kosa moja na kuinuliwa daraja moja, na mwenye kusoma kwa kuangalia bila ya kusali Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi jema moja na kumfutia kosa moja na huinuliwa daraja moja, na mwenye kujifunza herufi moja ya dhahiri ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humuandikia mema kumi na kumfutia makosa kumi na kuinuliwa daraja kumi, akasema: Si semi kwa kila aya lakini kwa kila herufi sawa iwe baa au faa au mfano wa hizo, akasema: Na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amekaa kwenye sala, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi hiyo mema khamsini, na kumfutia makosa khamsini, na kumuinua daraja khamsini, na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amesimama kwenye sala yake, Mwenyezi Mungu humuandikia mema mia moja na kumfutia makosa mia moja na kumuinua daraja mia moja, na mwenye kuihitimisha, maombi yake ni yenye kukubaliwa, sawa yachelewe au yawahi akasema: Nikasema: Niwe fidia yako mwenye kuihitimisha yote? Akasema: Mwenye kuihitimisha yote. [56]

Na imepokelewa kutoka kwa Is'haq bin Ammar, kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema:Mwenye kusoma aya mia moja akisali kwa kisomo hicho kwa usiku mmoja Mwenyezi Mungu humuandikia kwa aya hizo kunuti za usiku na mwenye kusoma aya mia mbili tofauti na kwenye sala ya usiku Mwenyezi Mungu humuandikia kwenye lauhul mahfuudh mema yaliyo sawa na mali nyingi (qintwaar ) na qintwar ni kinaya ya mali nyingi, aukia miamoja, na awqiyah ni kubwa zaidi ya mlima wa Uhudi .[57] Na imepokelewa kutoka kwa Anas amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :Mwenye kusoma aya mia moja, hataandikwa miongoni mwa wenye kughafilika, na mwenye kusoma aya mia mbili huandikwa miongoni mwa wenye kunyenyekea na watiifu, na mwenye kusoma aya mia tatu Qur'ani haitamtolea hoja, yaani mwenye kuhifadhi kiwango hicho cha aya za Qur'ani, husemwa: Hakika mtoto amesoma Qur'ani: Kwa maana amehifadhi. [58]

SURATUL FAATIHA NA FADHILA ZAKE

Imepokelewa kutoka kwa Hassan bin Ali Al-akariy kutoka kwa baba zake(a.s) (katika hadithi) amesema: Hakika Faatihatul kitaab (yaani Al-hamdu) ni bora zaidi kuliko vilivyomo kwenye arshi (hadi akasema) fahamuni ya kuwa mwenye kuisoma kwa makusudi kabisa kwa ajili ya kumtawalisha Mohammad na Aali zake Mwenyezi Mungu atampa kwa kila herufi aisomayo ya sura hiyo jema moja na kila jema moja ni bora kwake kuliko dunia na yaliyomo ndani ya dunia hiyo kati ya mali za aina tofauti na kheri zake, na mwenye kumsikiliza msomaji akiisoma atakuwa na thawabu mfano wa msomaji, basi ni vema kila mmoja wenu kujilimbikizia kheri hizi zilizo nyingi.[59]

Na mepokelewa kutoka kwa Fudhaili bin Hassan At-twabrasiy (katika majmaul bayan) kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) amesema: Ibada bora kabisa ni kusoma Qur'ani.[60] Na imepokelewa kutoka kwake (a.s) ya kuwa amesema (katika hadithi):Hakika Qur'ani hii ni kamba ya Mwenyezi Mungu, nayo ni Nuru iliyo wazi na dawa yenye manufaa (hadi akasema): Basi isomeni, hakika Mwenyezi Mungu atakulipeni kwa kuisoma kwa kila herufi mema kumi, ama mimi sisemi ya kuwa Alif laam ni mema kumi lakini Alif ni mema kumi na laam ni kumi na miim ni mema kumi. [61]

Na imepokelewa kutoka kwake(a.s) ya kuwa amesema: Ataambiwa mwenye Qur'ani: Soma na upande juu na soma kwa tartiil kama ulivyo kuwa ukisoma duniani, hakika daraja yako ni mwisho wa aya uisomayo.[8] Na imepokelewa kutoka kwake(a.s) amesema:Mwenye kusoma Qur'ani ni kama vile ameuweka utume pembezoni mwake ispokuwa ni kwamba yeye si mwenye kutelemshiwa wahyi .[62] Na imepokelewa kutoka kwa Ahmad bin Fahdi (katika kitabu Uddatud-daaiy) kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) amesema: Amesema Mwenyezi Mungu alie takasika: Mwenye kuacha kuniomba na kujishughulisha na kusoma Qur'ani nitampa thawabu bora zaidi za watu wenye kushukuru.[63]

MWENYE KUSOMA QUR'ANI KISHA AKAISAHAU

Imepokelewa kutoka kwa Abi Baswiir [64] amesema: Amesema Abu Abdillah(a.s) mwenye kusahau sura moja ya Qur'ani itamtokea ikiwa katika sura nzuri yenye kupendeza na itamjia ikiwa na sura ya daraja la juu kabisa peponi, pindi atakapo iona atasema: wewe ni nani? Uzuri ulioje ulio nao? Laiti unge kuwa wangu mimi, nayo itasema je hunifahamu? Mimi ni sura fulani na fulani na lau kama usinge nisahau ninge kuinua hadi mahala hapa. Na imepokelewa kutoka kwa Yaakuub Al-ahmar, amesema: Nilimuuliza Aba Abdillahi(a.s) : hakika mimi nina madeni mengi na hakika nimeingiwa na mambo ambayo huenda Qur'ani ikanikimbia na kunitoka, Abu Abdillah(a.s) akasema:Qur'ani Qur'ani hakika aya moja ya Qur'ani na sura ya Qur'ami itakuja siku ya kiama na zita panda hadi kwenye daraja elfu moja yaani peponi na zitasema lau kama unge tuhifadhi basi tunge kufikisha hapa kwenye daraja hii .[65]

Na imepokelewa kutoka kwa yaakub Al-ahman amesema: Nilimwambia Aba Abdillah(a.s) Niwe fidia yako hakika nimepatwa na mambo na hima, hakukubakia kheri yoyote isipokuwa sehemu fulani imeniponyoka na kunikimbia hata Qur'ani hakika sehemu yake fulani imeniponyoka na kunikimbia, akasema: basi akahuzunika na kufazaiaka kwa wakati huo pindi alipo taja Qur'ani kisha akasema: Hakika mwenye kusoma sura moja ya Qur'ani itamjia siku ya kiama na kumuangalia ikiwa kwenye daraja mojawapo kati ya daraja za peponi na itasema:Amani iwe juu yako, nae atasema: Amani iwe juu yako pia, (yaani Assalaam alykum) wewe ni nani? Itasema: Mimi ni sura fulani na fulani ulinipoteza na kuniacha, ama lau kama unge shikamana na mimi ninge kufikisha kwenye daraja hili, kisha akaashiria kwa vidole vyake, kisha akasema: Basi ni juu yenu kushikamana na Qur'ani jifunzeni Qur'ani hiyo hakika kati ya watu kuna wanao jifunza Qur'ani ili watu waseme fulani ni msomaji wa Qur'ani na kuna wanao jifunza Qur'ani hiyo na kuisoma kwa sauti au kuitafutia sauti ili watu waseme: Fulani anasauti nzuri, na katika hayo hakuna kheri yoyote, na kuna wanao jifunza Qur'ani na kuitumia kusimama usiku na mchana na hamjali mwenye kuifahamu na asie ifahamu. [66]

Na imepokelewa kutoka kwa Said bin Abdallah Al-aaraj amesema: Nilimuuliza Aba Abdillahi kuhusiana na mtu mwenye kusoma Qur'amni kisha akaisahau, kisha akaisoma na kuisahau, je kuna tatizo juu yake kwa kufanya hivyo? Akasema hapana.[67] Na riwaya iliyo pokelewa kutoka kwa Hussein bin Zaidi kutoka kwa Swaadiq(a.s) katika (hadithi ya makatazo) ya kuwa Mtume(s.a.w.w) alisema:Fahamuni ya kuwa mwenye kujifunza Qur'ani kisha akaisahau atakutana na Mwenyezi Mungu siku ya kiama akiwa amefungwa minyororo na Mwenyezi Mungu kumuwekea juu yake nyoka kwa kila aya aliyo isahau na kuwa ndie mwenza hadi motoni isipokuwa ikiwa atamsamehe. Makusudio yake ni kuwa ikiwa ataacha kutekeleza hukumu zake. [68]

5

QURANI MUUJIZA WA MILELE

MIONGONI MWA ADABU ZA KUSOMA QUR'ANI

Imepokelewa riwaya kutoka kwa Mohammad bin Fudhail kutoka kwa Abil Hassan(a.s) amesema: Nilimuuliza: Ninasoma msahafu (qur'ani) kisha ninabanwa na mkojo nikasimama nikakojoa na kustanji na kuosha mikono yangu na kurudi kusoma msahafu huo? Akasema: Hapana mpaka utawadhe kwa ajili ya sala. Na katika kitabu Al-khiswaal imepokelewa kwa sanadi na upokezi wake kutoka kwa Ali(a.s) -katika hadithi ya mia nne- amesema: Asisome mmoja wenu Qur'ani ikiwa hayuko kwenye twahara mpaka ajitwaharishe. Na imepkelewa kutoka kwa Ahmad bin Fahd katika kitabu (Uddatud-daiy) amesema: Amesema(a.s) : Mwenye kusoma Qur'ani hali ya kuwa amesimama kwenye sala, anayo mema mia moja kwa kila herufi aisomayo, na akiisoma kwa kukaa anayo mema khamsini, na akiisoma hali ya kuwa ni mwenye twahara na akiwa kwenye sala, anayo mema ishirini na tano (25), na ikiwa kama hakuwa ni mwenye twahara atapata mema kumi (10), ama mimi sisemi ya kuwa (Alif laam miim) ni kumi, bali ninasema Alif ni kumi, na laam ni kumi, na miim ni kumi, na Ree ni kumi).

Na imepokelewa kutoka kwa Hassan bin Ali Al-askariy(a.s) katika tafsir yake amesema:Ama kauli yake ambayo alikuitia na kukuhimiza kuitekeleza na akakuamuru kuitekeleza wakati wa kusoma Qur'ani ni, Audhu billahis samiul aliim minash-shaitwanir rajiim, hakika Amirul muuminiin (a.s) amesema ya kwamba: Kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo (Audhu billahi, yaani ninajizuilia na kujikinga kwa Mwenyezi Mungu-hadi akasema- na istiiadha ni kule kuamuru Mwenyezi Mungu waja wake wakati au pindi wanapo taka kusoka Qur'ani pale aliposema: Na pindi utakapo taka kusoma Qur'ani basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani alie laaniwa), na mwenye kufuata adabu ya Mwenyezi Mungu atampeleka na kumfikisha kwenye mafanikio ya milele na milele, kisha akataja hadithi ndefu kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema kwenye hadithi hiyo: Ukitaka usipatwe na sharri yao (mashetani) na usipatwe au kufikwa na vitimbi vyao, basi sema unapo amka asubuhi: Audhu billahi minash-shaytwanir rajiim, hakika Mwenyezi Mungu atakulinda na kukukinga na sharri zao.

QUR'ANI NI AHADI YA MWENYEZI MUNGU BASI KUWENI NAYO WAKATI WOTE

Na imepokelewa kutoka kwa Harizi kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema: Qur'ani ni ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake kwa hiyo basi inampasa kila Muislaam aangalie kwenye ahadi yake na asome ahadi hiyo kwa kila siku aya khamsini. Na imepokelewa kutoka kwa Zuhriy amesema: nilimsikia Ali binil Hussen(a.s) akisema: Aya za Qur'ani ni hazina, kwa hivyo basi kila inapofunguliwa hazima inakupasa uangalie yaliyomo kwenye hazina hiyo. Na imepokelewa kutoka kwa Muammar bin Khali, kutoka kwa Ridhaa(a.s) amesema: Nilimsikia akisema:Mtu anapo amka asubuhi inampasa baada ya kusoma nyuradi na dua baada ya sala asome aya khamsini (50). Na imepokelewa kutoka kwa Abdul-aalaa Aali Saam, kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema ya kuwa:Nyumba ambayo huishi Muislaam na kusoma Qur'ani ndani yake huonekana kwa watu wa mbinguni kama nyota yenye kung'ara mbinguni ionekanavyo kwa watu wa Ardhini.

Na imepokelewa kutoka kwa ibnul-qaddah, kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) amesema: Amesema Amirul muuminiin(a.s) : Nyumba ambayo husomwa Qur'ani ndani yake na Mwenyezi Mungu alie takasika kutajwa ndani ya nyumba hiyo baraka zake hukithiri na malaika huja kwenye nyumba hiyo na mashetani kuiacha na kuikimbia, na huwaangazia watu wa mbinguni kama nyota ziwaangaziavyo watu wa ardhini, kwa hakika nyumba ambayo haisomwi ndani yake Qur'ani na wala hatajwi Mwenyezi Mungu alie takasika ndani yake basi baraka zake hupungua na malaika huikimbia na kuihama nyumba hiyo na huhudhuriwa na mashetani. Na imepokelewa kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) , kutoka kwa baba yake (katika hadithi) amesema: Alikuwa akitukusanya na kutuamuru kumtaja Mwenyezi Mungu mpaka linapo chomoza jua na humuamrisha kusoma Qur'ani kila yule ambae alikuwa ni msomaji wa Qur'ani kati yetu, na yule ambae hakuwa msomaji kati yetu akimuamuru kuvuta au kusoma nyuradi, na nyumba ambayo husomwa Qurani ndani yake na hutajwa Mwenyezi Mungu ndani yake baraka zake huongezeka.

Na imepokelewa kutoka kwa Laythi bin Abi Saliim ameiinua kwa kusema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) :Yatieni nuru majumba yenu kwa kusoma Qur'ani na wala msiyafanye kama makaburi kama walivyo fanya Mayahudi na Wakiristo, wali salia kwenye Makanisa na Masinagogi na kuziacha nyumba zao, hakika nyumba inapo somewa sana ndani yake Qur'ani basi kheri zake huongezeka na kukithiri na watu wake kuongezeka na kupanuka, na huwaangazia watu wa mbinguni kama nyota ziwaangaziavyo watu wa duniani.

Na imepokelewa katika (Uddatud-daiy) kutoka kwa Ridhaa(a.s) akiinua hadi kwa Mtume(s.a.w.w) amesema:Ziwekeeni nyumba zenu sehemu fulani ya Qur'ani, hakika nyumba inaposomewa ndani yake Qur'ani basi huwa njema, nyepesi na pana kwa watu wake na kheri zake hukithiri na wakazi wake huongezeka wakati wote na kama haikusomwa Qur'ani ndani yake basi huwa finyu na mbaya kwa watu wake na kheri zake kuwachache (kupungua) na watu wake au wakazi wake huwa ni wenye kupungua.