MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 0%

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA Mwandishi:
: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi: Vitabu mbali mbali

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

Mwandishi: Kimeandikwa na: 'Ayatullah al-'Udhma Nasir Makarim Shirazi.
: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 15880
Pakua: 2320

Maelezo zaidi:

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 15880 / Pakua: 2320
Kiwango Kiwango Kiwango
MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

Mwandishi:
Swahili

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

KIMEANDIKWA NA: 'AYATULLAH AL-'UDHMA NASIR MAKARIM SHIRAZI.

KIMETARJUMIWA NA :

AMIRALY M. H. DATOO

( Bukoba - Tanzania)

YALIYOMO

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 1

MANENO MAWILI YA MTARJUM 8

KWA JINA LA ALLAH SWT , AMBAYE NI RAHMAAN NA RAHIIM 8

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 10

SOMO LA 1: KUFIKIRIA, TAAMULI 10

SOMO LA 2: KIPIMO CHA MAJADILIANO 10

SOMO LA 3: WANAJALI VYAKULA VYA MIILI YAO LAKINI 10

SOMO LA 4 : KAZI YA KALAMU 11

SOMO LA 5 : BAINA YA WAJIBU KUBWA MBILI 11

SOMO LA 6 : SABABU ZA MAANGAMIZO YA JAMII 11

SOMO LA 7: UVIVU NA UMASIKINI 12

SOMO LA 8: ATHARI YA MVUA JUU YA MIOYO 12

SOMO LA 9: CHANZO CHA KIBURI NA UJEURI 12

SOMO LA 10: MAMBO 3 YENYE THAMANI MBELE YA ALLAH SWT 12

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 14

SOMO LA 11: KUUAWA SHAHIDI KWA AL-IMAM HUSSEIN IBN 'ALI IBN ABI TALIB A.S 14

SOMO LA 12: ALAMA MBILI ZA MWISLAMU WA KWELI 14

SOMO LA 13: MOTO WA GHADHABU 14

SOMO LA 14: VIANZIO VYA MALI 14

SOMO LA 15 : SHUGHULI MBAYA KABISA 15

SOMO LA 16 : BWANA NA MFUNGWA 15

SOMO LA 17 : UNAFIKI NA KIBURI 15

SOMO LA 18 : HUSUDA 16

SOMO LA 19 : ALIYENYIMWA NEEMA ZA ALLAH SWT 16

SOMO LA 20 : MARAFIKI WAOVU 16

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 17

SOMO LA 21 : UKAMILISHO WA KAZI 17

SOMO LA 22: MIKAKATI YA KUDUMU 17

SOMO LA 23: ADHABU KALI KABISA 17

SOMO LA 24: MAOVU YA MADENI 17

SOMO LA 25: MAISHA BORA YA KIJAMII 18

SOMO LA 26: UFUNGUO WA MAAFA 18

SOMO LA 27: ALAMA ZA WATU WA JANNAT ( PEPONI ) 18

SOMO LA 28: ALAMA ZA MNAFIKI 19

SOMO LA 29: USHAURI 19

SOMO LA 30: KUONGEA NA UKIMYA 19

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 21

SOMO LA 31: FURAHA YA USAMEHEVU 21

SOMO LA 32: ZAHID KATIKA MAANA SAHIHI 21

SOMO LA 33: KULINGANA NA MASHAHIDI 34 21

SOMO LA 34: WATU WALIO BORA 22

SOMO LA 35: IBADA ZA WATU WALIO HURU 22

SOMO LA 36: KILE KIVUNJACHO MGONGO WA MTU 22

SOMO LA 37: KUWA MSAFI 23

SOMO LA 38: HATIMA YA UJAHILI 23

SOMO LA 39: MISINGI YA MUONGOZO 23

SOMO LA 40: MASIKITIKO NI TABIA ZA UJAHILIYYAH 24

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 25

SOMO LA 4 1: KUJIPIMA MWENYEWE KILA SIKU 25

SOMO LA 4 2: NISHANI ZA IMANI NI NGUMU KULIKO CHUMA 25

SOMO LA 4 3: UHAKIKA WA UMOJA NA UADILIFU WA ALLAH SWT 25

SOMO LA 4 4: BAADHI Y ALAMA ZA IMANI 26

SOMO LA 4 5: ULIMWENGU SI MWISHO WETU BALI NI NJIA YA KUPITIA 26

SOMO LA 4 6: THAMANI YA MTU 27

SOMO LA 4 7: UKWELI NA UWONGO 27

SOMO LA 4 8: URITHI WENYE THAMANI MKUBWA WA WAARABU 27

SOMO LA 4 9: NINAWACHUKIA 28

SOMO LA 50: JITIHADA ZA WALIO WAOVU NA DHAIFU 28

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 29

SOMO LA 5 1: ALAMA ZA UKANDAMIZAJI 29

SOMO LA 5 2: HAKUNA UGONJWA USIOTIBIKA 29

SOMO LA 5 3: KWA NINI UPENDELEO HUTOKOMEA ? 29

SOMO LA 5 4: SHAHADA NA UHALISI 30

SOMO LA 5 5: WAJIPENDEAO KUJITOA MHANGA WENYEWE 30

SOMO LA 5 6: MWENYE BUSARA NA MPUMBAVU 30

SOMO LA 5 7: WAPO WACHAMUNGU WACHACHE 31

SOMO LA 5 8: UADILIFU MIONGONI MWA WATOTO 31

SOMO LA 5 9: WEWE UPO DAIMA UKIDHIBITIWA 31

SOMO LA 60: SI KUSIFU KWA KUDANGANYA, WALA SI WIVU 32

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 33

SOMO LA 6 1: DAIMA UWE TAYARI KWA AJILI YA NDUGU ZAKO 33

SOMO LA 6 2: MAKOSA MAISHANI 33

SOMO LA 63: DINI YA UISLAM ITAKUWA DINI YA ULIMWNEGU MZIMA 33

SOMO LA 6 4: USILICHUKULIE DHAMBI LOLOTE KUWA DOGO ! 34

SOMO LA 6 5: UTUKUFU WA ELIMU 34

SOMO LA 6 6: HAKI ZA WOTE 34

SOMO LA 6 7: TUMIA FEDHA KWA UTIIFU HAUTATENDA DHAMBI 35

SOMO LA 6 8: SOKO KUBWA LA KIBIASHARA 35

SOMO LA 6 9: WATU WALIOTUKUZWA 35

SOMO LA 70: KANUNI 3 ZA MISINGI YA JAMII 36

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 37

SOMO LA 7 1: HARAKA NA PUPA 37

SOMO LA 7 2: ZAHID 76 KWA HAKIKA 37

SOMO LA 7 4: MPANGO SAHIHI A DUNIA NA AKHERA 38

SOMO LA 7 5: ATHARI ZA DHAMBI 38

SOMO LA 7 6: SHI'A SAHIHI 38

SOMO LA 7 7: NI NANI TUMWULIZE ? 39

SOMO LA 7 8: NEEMA ILIYO BORA KABISA 39

SOMO LA 7 9: IMAM A.S. ASIYEONEKANA 39

SOMO LA 80: USIYASIKILIZE YALE YOTE YANAYOTAMKWA ! 40

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 41

SOMO LA 8 1: WATU MASHETANI 41

SOMO LA 8 2: FURAHA YA UHAKIKA 41

SOMO LA 8 3: MTAJI WENYE THAMANI 41

SOMO LA 8 4: VITU 2 HUSABABISHA MAANGAMIZO YA WATU 41

SOMO LA 8 5: HAKUNA WEMA ULIO MDOGO 42

SOMO LA 8 6: USITENDE DHAMBI HAUTAOMBA MSAMAHA 42

SOMO LA 8 7: MAISHA MAOVU KABISA 42

SOMO LA 8 8: AHADI ZETU NDIZO MADENI YETU 43

SOMO LA 8 9: MALI HARAMU 43

SOMO LA 90: USIMWOMBE MTU KITU CHOCHOTE 43

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 44

SOMO LA 9 1: AMELAANIWA MTU KAMA HUYU! 44

SOMO LA 9 2: TUSISULUHISHE MATATIZO KWA DHAMBI! 44

SOMO LA 9 3: KUTOSHEKA MWENYEWE ! 44

SOMO LA 9 4: NDUGU NA JAMAA WA KARIBU NA MBALI 44

SOMO LA 9 5: KUTUPILIA MBALI TABIA 45

SOMO LA 9 6: TUKIO LA KARBALA 45

SOMO LA 9 7: JE NI NANI ALIYE MWENYE BUSARA ? 45

SOMO LA 9 8: SABABU ZA UADUI 45

SOMO LA 9 9: UHALISI 46

SOMO LA 100 : MWENYE BARAKA 46

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 47

SOMO LA 101: MIKONO BORA KABISA 47

SOMO LA 102: OVU HATA KULIKO MAUTI 47

SOMO LA 103: UTAMBULISHO BAINA YA MUMINI NA MNAFIKI 47

SOMO LA 104: URITHI BORA KABISA 48

SOMO LA 105: KUHESHIMU UHURU WA FIKARA 48

SOMO LA 106: SIFA 6 ZISIZO NDANI MWA MUMIN 48

SOMO LA 107: USIVUNJE UHUSIANO WOTE 49

SOMO LA 108: IBADA SAHIHI 49

SOMO LA 109: USILISAHAU KOSA LAKO 49

SOMO LA 110: ADHABU KUBWA 50

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 51

SOMO LA 111: QURAN TUKUFU NI YA KILA ZAMA 51

SOMO LA 112: JITAHADHARISHE NA MATAMANIO 51

SOMO LA 113: NJIA MOJA TU YA KUWA SHI'A 51

SOMO LA 114: UHUSIANO WA MALI NA MATUMIZI! 52

SOMO LA 116: MAISHA NA KUENDESHA NYUMBA 52

SOMO LA 117: SAA NZIMA YA UADILIFU 53

SOMO LA 118: MGANGA WA KWELI 53

SOMO LA 119: MAKHALIFA WA MTUME S.A.W.W 53

SOMO LA 120: FURAHA YENEY MADHAMBI 54

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 55

SOMO LA 121: UFANYE KAZI ZINAZOZALISHA 55

SOMO LA 122: UREFU NA UFUPI WA MAISHA 55

SOMO LA 123: URAFIKI NA SHETANI! 55

SOMO LA 124: POKEA USHAURI ILI UONGOZWE ! 56

SOMO LA 125: SALAAM, KUSALIMIANA KIISLAMU 56

SOMO LA 126: KUTOKUKUBALIANA KWA IMANI NA MATENDO 56

SOMO LA 127: ADHABU ZA ALLAH SWT ! 57

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 59

SOMO LA 131: MILANGO ILIYOFUNGWA ITAFUNGULIWA 59

SOMO LA 132: JITAHADHARISHE NA WAOVU! 59

SOMO LA 133: VITA VIKUU 59

SOMO LA 134: GHAIBU IMAM MUHAMMAD MAHDI A.S 60

SOMO LA 135: CHANZO CHA MAOVU 60

SOMO LA 136: KUTIMIZA WAJIBU NDIYO IBADA KUU 60

SOMO LA 137: MAKAZI KATIKA SAYARI 61

SOMO LA 138: QUR'AN TUKUFU NA KANUNI YA UZITO 61

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 63

SOMO LA 14 1: LITABAKIA JINA TU KUTOKEA ISLAM 63

SOMO LA 14 2: KUTAMBUA UWEREVU NA UJAHILI 63

SOMO LA 14 3: ZAIDI YA NEEMA 63

SOMO LA 14 4: KUHUISHA SIRA ZA MA'ASUMIIN A.S 64

SOMO LA 14 5: SIRI NI AMANA 64

SOMO LA 14 6: ALAMA ZA IMANI YA DINI YA ISLAM 64

SOMO LA 14 7: SHARTI LA KWANZA KWA AJILI YA KILA KAZI 65

SOMO LA 14 8: UMUHIMU WA WAGENI 65

SOMO LA 1 4 9: HESHIMA NA MAPENZI 65

VITABU VILIVYOKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA AMIRALY M. H. DATOO 67

VITABU VILIVYOTAYARI 67

VITABU VINAVYOTAYARISHWA 68

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 70

MAREJEO (REFERENCES) 70

MANENO MAWILI YA MTARJUM

KWA JINA LA ALLAH SWT , AMBAYE NI RAHMAAN NA RAHIIM

Katika historia ya Dini ya Kislam na hususan Madhehebu ya Shi'a Ithna-Ashariyyah wamekuwapo na bado wapo Maulamaa ambao kwa hakika wametoa michango yao mikubwa katika kuuelemisha Ummah juu ya masuala mbalimbali yakiwemo ya kidunia, kijamii na kiroho vile vile.

Ni matumaini yangu kuwa kitabu hiki kitakuwa ni mwongozo katika mwelekeo na mwenendo wa Kiislamu katika masuala mbalimbali ya humu duniani na kutufaidisha Aakhera. Kazi ya awali ilikuwa katika lugha ya Kiajemi ambayo ilitarjumiwa katika Kiingereza na Ndg. Munir Shafe'i na ndipo nilipotarjumia katika Kiswahili.

Wabillahi tawfiq,

Amiraly M.H.Datoo

P. O. Box 838

Bukoba- Tanzania (E.Africa)

13 Ramadhaan al-Mubarak 1424 H (8 Novemba 2003 )

Barua Pepe : datooam@hotmail.com

Utapata hazina kubwa ya 'ilimu katika : www.dartabligh.org na

www.Alitrah.org na www.al-islam.org/kiswahili

UTANGULIZI

Mtaji wetu mkubwa baada ya Kitabu Kitakatifu, Qur'an Tukufu, ni Sunnah na Sirah za bwana wetu mtukufu Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na Ahlul Bayt(a.s) ya wanayumba wake, kwa hakika vitu hivi viwili ni vizito mno baada ya kifo chake na kwa hakika kwa kushikamana navyo kutawaokoa wanaadamu wasipotoke wala kukosea.

Kwa bahati mbaya, Ahadith hizi ambazo ni bahari ya sayansi na elimu, hazijajulikana vile ipasavyo. Kwa hakika zipo Ahadith nyingi mno katika kipimo kidogo ambamo kitabu cha maisha kipo kimejificha na kwa hakika kinaweza kutatua matatizo yote ambayo yanamkabili mwanadamu wa leo katika masuala mbalimbali.

Kitabu hiki ambacho ni mkusanyiko wa Ahadith na riwaya hizo zilizotarjumiwa pamoja na maelezo machache kwa mukhtasari. Kwa hakika Hadith hizi zilikuwa zikitolewa kila Siku ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Hussein(a.s) ( Teheran, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) wakati wa mazungumzo na majadiliano ya Kidini na kisayansi, kwa hakika kila mmoja aliweza kuizingatia kwa muda wa juma zima kama ndilo somo lao, na wengi wa vijana, wavulana kwa wasichana, waliziihifdhi (walizikariri) mioyoni mwao.

Kwa hakika upokeo wake ulivyokuwa ukionekana na kuvutia, ilisababisha kuchapwa na kutolewa kila mahala. Hivyo kitabu hiki kidogo kitakuwa ni mwongozo kwa wale wote ambao wanataka kuuelewa Uislamu vyema kwa njia ya mafundisho madogo. Lakini jambo lililo la muhimu na maana ni kule kufuata na kutekeleza maamrisho na maongozo hayo.

Hivyo sote kwa pamoja tumwombe Allah swt atujaalie tawfiq ya kuelewa na kuweza kutekeleza kwa mujibu wa Ahadith hizi na hatimaye kuzingatia na kujipima. Qum, Nasir Makarim Shirazi, 1976

1

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 1: KUFIKIRIA, TAAMULI

Uwe tahadhari ! Elimu isiyo ambatana na ufikiriaji, haina faida. Uwe tahadhari ! Usomaji wa Qur'an Tukufu iwapo hautakuwa na ufikiriaji, basi hautakuwa na maana ! Uwe tahadhari ! 'Ibada isiyo na fikara ndani mwake, haina athari yake.1

Maelezo mafupi: Kuujaza ubongo wa mtu kwa kanuni za kisayansi, mantiki na kifalsafa, au na elimu yoyote itakuwa na athari ndogo sana hadi hapo itakapokuwa kwa misingi ya fikara sahihi, mtazamo wazi wa ulimwengu na kuzitambua misingi ya maisha ya mwanadamu. Ama usomaji wa Qur'an Tukufu utakuwa na athari ndogo iwapo haitaambatana na uchambuzi na kuzizingatia na kuzifikiria hizo Ayah zake, 'Ibada ambayo haina nuru ya ufikiriaji na busara ni sawa na mwili usio na roho, na kukosa athari za elimu ya hali ya juu.

SOMO LA 2: KIPIMO CHA MAJADILIANO

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema :

"Kuboresha hali ya maisha na uhusiano inawezekana kwa kutumia kipimo, sehemu mbili ya tatu ni kuwa makini na theluthi moja ni upuuziaji."

Maelezo mafupi: Hakuna kazi inayoanzishwa bila ya kufanyiwa utafiti, mpango au umakini, na vile vile hakuna kazi ambayo haimaliziki bila ya upuuzaji. Itakuwa wazi kusema vyema kuwa iwapo sisi tutataka kufanya kazi pasi na uchunguzi au utafiti na umakini, basi sisi kamwe hatutafanikiwa. Lakini iwapo sisi tutataka kung'ang'ania kila jambo linaloweza kutokea bila ya kutabiriwa wakati tufanyapo kazi, basi kamwe hatutaweza kufanya kazi zetu kwa uwepesi, na itatubidi tuishie miaka mingi katika kusomea tu kwa ajili ya kufanya jambo au kumchagua rafiki, mke na mambo kama hayo. Ndiyo maana inasemwa kuwa sehemu mbili ni za umakini na theluthi moja ni ya kutokuwa makini.

SOMO LA 3: WANAJALI VYAKULA VYA MIILI YAO LAKINI

Al-Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) anasema :"Ninastaajabishwa na wale ambao hufikiria vyakula kwa ajili ya miili yao tu, lakini hawafikirii vyakula kwa ajili ya Roho zao. Wao huondoa vyakula vinavyowasumbua kutokea matumbo yao, na papo hapo wa wanazijaza nyoyo zao kwa mambo yanayoangamiza nyoyo zao." 3

Maelezo mafupi : Kama vile Al-Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alivyosema, watu huwa wanajali mno vyakula vya kula, na hawali hadi wapo katika mwanga, na hawafungui vinywa vyao hadi pale macho yao yawapo wazi. Wao hujiepusha na vyakula vyote vyenye mashaka na wengi wao huzingatia maelfu ya hatua za afya na siha zao kwa ajili ya kuzilisha miili yao. Lakini, ama kuhusiana na vyakula vya Roho, wao, huku wakiwa wamefumba macho yao katika kiza kikali, wanajilisha vyakula vya nyoyo zao zenye kushukiwa, katika nyoyo zao. Wao kwa urahisi hukubalia maneno ya marafiki wasio wema, habari zisizo kweli na sahihi na usambazaji wenye sumu na mashaka, na kwa hakika haya ni yenye kushangaza mno.

SOMO LA 4 : KAZI YA KALAMU

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema :"Mimi sijamwona mfagiaji akiwa na tabasamu njema kabisa kama kalamu." 4

Maelezo mafupi: Kalamu inadhihirisha hisia za mwanadamu na kutarjumu busara ya mwanadamu. Kalamu ni mvumbuzi wa utamaduni na kuzungusha magurudumu ya jumuiya. Kalamu huelezea maumivu ya fikara za mwanadamu kwa kuendela kulia kwake, na vile vile husisimua mapenzi, kutamani maisha, maajabu ya maisha na maelfu kwa maelfu ya mema ambayo yamefichika katika kutabasamu ambayo huwapo baina ya midomo miwili. Lakini jambo la kusikitisha ni pale ambapo kalamu inapokuwa katika mikono ya watu ambao si mustahiki wake, machozi yake hubadilika kuwa matone ya damu, na ubashasha wake huwa ni aibisho kwa mema yote ya mwanadamu.

SOMO LA 5 : BAINA YA WAJIBU KUBWA MBILI

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema :Muumini mwaminifu daima huwa na shauku ya mambo mawili : Madhambi yake yaliyopita ambapo hajui vile Allah swt atakavyomshughulikia kwayo, Maisha yake yaliyobakia hajui kile atakachokifanya ! 5

Maelezo mafupi: Dalili kuu ya udhihirisho wa imani ni kuhisi na kutambua wajibu wa mtu, kwa yale aliyoyatenda na wajibu na ufaradhisho wake kwa yale yanayotakiwa kutendwa. Ama kwa hakika wale wenye hisia hizi mbili, daima huwa wanafikiria vile watakavyoweza kufidia upuuzaji wao uliopita, na vile vile kutumia mustakbal kwa njia njema kabisa. Kwa hakika fikara hizi ndizo chachu za maendeleo na usongaji mbele wa mtu au taifa. Ama wale amabo hawafikirii matendo yao ya nyuma, wala wasiojali kujenga maisha yao ya mbeleni, huwa ni masikini na wenye shida wasio bahatika.

SOMO LA 6 : SABABU ZA MAANGAMIZO YA JAMII

Yapo mambo manne iwapo mojawapo likiingia katika nyumba yoyote, basi itaangamiza nyumba hiyo na kwayo baraka za Allah swt zitatokomea : udanganyifu, wizi, ulevi na zinaa. 6

Maelezo mafupi: Kwa hakika si majumbani mwetu tu bali hata kama maovu haya yataingia katika jumuiya au jamii, basi jumuiya au jamii hiyo itaangamia na kuteketea. Wakati udanganyifu, uhaini unapopenya katika jamii, ule moyo wa kujiamini unapotea kimoja.

Na wakati wizi unapoingia, katika sura zake mbalimbali, basi amani haitapatikana kamwe. Na wakati pombe na vinywaji haramu vitakapokuwa mashuhuri na kawaida miongoni mwa watu, basiwatadhoofisha fikara zao, watakuwa na vizazi vya vijana na watoto wasiofaa katika jamii. Na wakati watakapokuwa wamejitumbukiza katika zinaa, basi misingi ya kifamilia zitadhoofika na vizazi vyao vijavyo vitakuwa vya waasherati na waovu.

SOMO LA 7: UVIVU NA UMASIKINI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) amesema :

Siku ambapo kila kitu kiliozeshwa na mwenzake, basi uvivu na umasikini zilifungamana kwa pamoja, na mtoto wao aliyezaliwa aliitwa ufukara. 7

Maelezo mafupi Kila kitu kinapatikana au kuvunwa kwa kutokana na jitihada na bidii. Na kwa hakika haya ndiyo yaliyo mafunzo makuu ya Dini ya Islam. Uvivu, kutokufanya kazi, udhaifu na kukwepa majukumu magumu na matatizo ndiyo mambo ambayo kamwe hayawezi kupatana na moyo huu wa imani. Kwani hakutakuwapo na matokeo yoyote isipokuwa umasikini katika kila jambo, ikiwemo kiuchumi, kimaadili na umasikini wa kiimani. Wakati huo huo Waumini halisi watakuwa wanajitosheleza kwa kila jambo na watakuwa ni watu wenye kutosheka katika kila jambo.

SOMO LA 8: ATHARI YA MVUA JUU YA MIOYO

Luqman mwenye hekim alisema :

Ewe mwanangu ! Allah swt huuisha nyoyo za watu kwa nuru ya elimu kama vile anavyohuisha ardhi iliyokufa kwa baraka za mvua kutokea mbinguni ! 8

Maelezo mafupi Moyo wa mtu kama ardhi sawa na bustani ambapo kila ya aina ya mimea, mbegu za maua, miche na miti imara huwa imeenea kila mahala, na lau itapatiwa maji kwa wakati wake, basi bustani hiyo itashamiri na kupendeza mno. Kwa hakika umwagiliaji wa bustani hiyo ya mioyo yetu huhitaji matone ya mvua ya sayansi na elimu. Hivyo nyoyo ambazo hazina elimu huwa zimekufa, zisizo na nuru wala mazao yoyote. Inatubidi sisi daima tuhuishe nyoyo zetu kwa nuru ya elimu.

SOMO LA 9: CHANZO CHA KIBURI NA UJEURI

Imeripotiwa kutokea Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) kuwa :

Hakuna mtu anayeweza kujivuna au kuwa na kiburi kwa wengine hadi pale yeye mwenyewe anapokuwa na hisia za kuwa chini undani mwake! 9

Maelezo mafupi: Siku hizi, utafiti wa kiakili na kifahamu umethibitisha kuwa ujeuri na kiburi si kitu kingine bali hali ya kujiona kwa mtu mwenyewe kuwa yu chini kuliko wengineo. Wale ambao wanakuwa wameambukizwa hayo, basi hujitwisha ubandia huu kwa kuficha kasoro zao hizo, na hivyo huongezea uchini wao kijamii na kujifanya wao wakachukia zaidi. Kwa mtazamo huu wa kiakili imetambulikana vyema kabisa kutokana na msemo wa Al- Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. lakini kwa hakika Waumini halisi daima huwa ni watu ambao wanafanya kazi zao kwa heshima kubwa undani mwao.

SOMO LA 10: MAMBO 3 YENYE THAMANI MBELE YA ALLAH SWT

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema :

Yapo mambo matatu ambayo yanaondoa pazia na kukaribia Utukufu wa Allah swt : Sauti ya harakati za kalamu ya mwandishi wa kisayansi ! Sauti za mwendo wa wapiganaji wanapokuwa katika Vita vya Jihad ! Na sauti ya gurudumu la kusuka nyuzi la mwanamke mtoharifu ! 10

Maelezo mafupi: Kwa hakika maana na maelezo yenye nasiha kubwa! Kwa hakika zipo sauti tatu ambazo zinapenya kina cha uhai na kuendelea mbele katika maumbile yasiyoangamia wala kuteketea na kuelekea katika Ukuu na Utukufu wa Allah swt : sauti ya elimu na kalamu, ingawaje inaweza kuwa dhaifu na polepole, sauti ya Vita vitakatifu na kujitolea mhanga, na sauti ya jitihada, kuendelea na kufanya kazi hata kama itaonekana ndogo kiasi gani. Na kwa hakika, mambo haya matatu, elimu,Vita Vitakatifu, na kazi vinatengeneza msingi na jumuiya ya kibinadamu iliyoheshimika.

2

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 11: KUUAWA SHAHIDI KWA AL-IMAM HUSSEIN IBN 'ALI IBN ABI TALIB A.S.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :Kuuawa Shahidi kwa Al-Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib (a.s) imeanza vuguvugu la joto katika nyoyo za Waumini ambavyo kamwe haitapoa. 11

Maelezo mafupi: Kwa hakika tumeviona vita vingi mno ulimwenguni ambavyo vinasahaulika kwa kupita kwa muda wa miezi na miaka. Hata vivyo, ukumbusho wa harakati na vuguvugu za wale waliojitolea mhanga katika njia ya Allah swt na kwa ajili ya uhuru wa wanaadamu na vile vile kwa ajili ya heshima na mema, kamwe havitasahaulika kwa sababu Allah swt, uhuru, heshima na mema kamwe hayatazeeka. Kwa hakika Al-Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. pamoja na wafuasi wake walikuwa ndio kitovu cha hayo kama wapiganaji kwa ajili ya imani.

SOMO LA 12: ALAMA MBILI ZA MWISLAMU WA KWELI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) :Usiheshimu tu wingi wa Sala, Saumu, Hijja, uchamungu na ukeshwaji wao katika ibada ( ingawaje hayo ni muhimu upande wao wenyewe ). Badala yake angalieni ukweli, uadilifu na uaminifu wao ! " 12

Maelezo mafupi Tukisoma nyaraka za Kiislamu, tunapambanuliwa bayana ukweli huu wa alama za Mwislamu halisi awe ni mkweli, mwadilifu na mwaminifu, na ingawaje katika Islam Sala, Saumu, Hajj ni ibada za hali ya juu, lakini hizo si dalili za Uislamu na badala yake zinatakiwa zitekelezwe pamoja na ukweli, uadilifu na uaminifu.

SOMO LA 13: MOTO WA GHADHABU

Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) anasema :

Kwa hakika ghadhabu ni miale ya mioto ambayo huwashwa na Sheitani katika nyoyo za Wanaadamu . 13

Maelezo mafupi: Wakati mtu aliye katika hali ya ghadhabu (hasira) anapotenda kitu au kufanya uamuzi, mara nyingi imeonekana kuwa huja kujuta majuto na kusikitika kwa sababu mito ya ghadhabu imemsababisha yeye kutokuwa mwangalifu na makini kutokea fahamu na busara zake, na kwa ujumla, msisimko na hisia zake humwelekeza mahala ambapo hakutawezekana kufidia hasara hizo maishani mwake ! Inatubidi sisi tuweze kuuzima moto huu wa Kishetani kwa haraka iwezekanavyo na kwa uangalifu mkubwa. Ama sivyo, inawezekana ikateketeza maisha yetu na ya wengine.

SOMO LA 14: VIANZIO VYA MALI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema :

Tafuteni riziki yenu ndani mwa ardhi . 14 Maelezo mafupi Maagizo haya yalikuwa yametolewa na Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) wakati ambapo kulipokuja kujulikana kuhusu machimbo ya vito vya thamani na mengineyo mengi ndani ya ardhi, ikimaanisha kuwa Waislamu inawabidi wapeleleze chini ya ardhi kwa ajili ya kujipatia riziki zao na kwa ajili ya mahitajio yao ya maishani. Kwa hakika maamrisho kama haya ni dalili za uzito wa maamrisho ya Kiislamu na vile vile ni somo la jitihada na juhudi na ni kwa ajili ya Waislamu kuishi maisha mema na yenye heshima!

SOMO LA 15 : SHUGHULI MBAYA KABISA

Na Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) vile vile amesema :

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:shughuli iliyo ovu kabisa ni ile ambayo imechangnyikana na riba . Vile vile Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) amesema :"Wakati Allah swt anapotaka kuuangmiza ummah, basi humo kutakuwa kumetokezea riba . 15

Maelezo mafupi Pamoja na kuwa na soko rahisi la riba kushamiri katika ulimwengu wa kisasa, na kutegemea mno kwa dunia ya kisasa juu ya riba katika sura mbalimbali, ni dhahiri kuwa riba inaangamiza taratibu zote za kifedha na kiuchumi za jamii na hatimaye kusababisha kulimbikizana kwa utajiri uliokithiri mikononi mwa matajiri wachache na taasisi, kwa hakika kuwapo kwa mgawanyo wa aina hii ndicho chanzo cha matatizo na maangamizo ya kijamii na ufisadi wa kimaadili.

SOMO LA 16 : BWANA NA MFUNGWA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema :

Mfanyie fadhila mtu yeyote, nawe utakua bwana wake ! Usimwombe mtu yeyote, ama sivyo utakuwa kama yeye ! Kuwa na haja ya mtu yeyote, itakufanya wewe uwe mfungwa wake ! 16

Maelezo mafupi: Kanuni hii inaongoza kwa nguvu juu ya uhusiano wa kijamii wa mtu binafsi na mataifa, kuwa daima mikono yenye kutoa huwa daima ni mabwana na mikono inayopokea huwa ni duni. Mataifa au watu muhtaji kwa hakika ni watumwa ambao wametia saini zao za utumwa wao kwa kupitia msaada kutokea wengineo. Kwa hakika Mwislamu wa kweli hujaribu kuufanya uhusiano wake juu ya misingi ya maelewano, na wala si kuegemea msaada upande mmoja. Kwa hakika kutolewa kwa misaada ya shukuruani iwe imelengwa kwa wale walio mustahiki na dhaifu.

SOMO LA 17 : UNAFIKI NA KIBURI

Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) amesema :

Usitende matendo yako kwa kujionyesha au kiburi kwa watu ambao hawana uwezo juu ya maisha wala vifo yao, na ambao hawawezi kukutatulia matatizo yako. 17

Maelezo mafupi: Udhihirisho wote wa maisha ya wale ambao wamezoea kiburi na unafiki yanakuwa tupu. Wao wanakuwa na udhihirisho usio na moyo kutokea maendeleo, ufikirio na mazua zua kutokea uhai, hakuna umashuhuri kutokea furaha na utajiri, na maendeleo isipokuwa ni kutokana na Dini tu, na kwa hakika watu wenye kiburi hawajipatii chochote isipokuwa kujionyesha tu ! Kwa hakika ndiyo maana Dini ya Islam imekanusha kwa nguvu sifa hii mbaya na imesema kuwa hatima yako haipo chini ya watu hawa, sasa je kwa nini unajidai na kufanya kiburi ?

SOMO LA 18 : HUSUDA

Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) amesema:

Mtu mwenye husuda hujifikishia hasara yeye mwenyewe kabla hajawafanyia wale anaowahusudu . 18

Maelezo mafupi: Moyo wa husuda ni ule ambao hauvumilii wengine wawapo na neema, na hujaribu kuwakosesha wao kutokana na neema hiyo, au kujaribu kuwapatia hasara kwa njia zinginezo. Kwa hakika, hasidi (mtu mwenye husuda) huwa ni mtu mwenye kurudi nyuma na kamwe si mwenye maendeleo.

Husuda kwa hakika ni ugonjwa mwovu kabisa wa kimaadili katika jamii na kwa mtizamo wa kiakili, mtu mwenye husuda huwa katika hasara zaidi na hufifia, hurudi nyuma na kudhalilika zaidi kuliko wengineo. Hivyo ni vyema kwa ajili yake kujaribu kujiendeleza kuliko kujishughulisha kuwarudisha nyuma wengineo.

SOMO LA 19 : ALIYENYIMWA NEEMA ZA ALLAH SWT

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) amesema :

Yeyote yule aliye na maji na ardhi, na bado akabakia kuwa masikini na mwenye shida, basi huyo atakuwa amenyimwa neema za Allah swt ! 19

Maelezo mafupi: Kwa mujibu wa Ahadith na Riwaya za Dini ya Kiislamu, imesisitizwa mno kwa Waislamu ulimwenguni kote, kutumia vianzio mbalimbali kama ufugaji wa wanyama, kilimo, uchimbaji wa madini, vito na mali ghafi nyinginezo, ustadi, viwanda na biashara kwa ajili ya kupigana vita dhidi ya umasikini. Iwapo nchi yoyote itakuwa nacho chochote kati ya hizo, basi watumie kwa ajili ya kutimiza mahitaji yao ya kiuchumi. Sasa hebu fikiria kwa wale ambao wanavyo yote hayo. Ama sivyo watalaaniwa na kunyimwa neema za Allah swt na moyo wa Uislam. Kwa hakika tabia ya kuomba omba imelaaniwa vikali katika mtazamo wa Dini ya Islam.

SOMO LA 20 : MARAFIKI WAOVU

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema :

Marafiki zako waovu kabisa ni wale wanaokusifu na kuongea nawe maneno mengi kama maji na wanazificha aibu zako. 20

Maelezo mafupi: Kwa kukwepa uhakika wa maisha na kuficha ukweli, haya kamwe hayawezi kutatua matatizo yoyote, na wala haiwezekani kusemwa kuwa itaweza kumsaidia mtu yeyote. Kwa hivyo wale marafiki ambao hujaribu kuficha ukweli badala ya kukushutumu wewe kwa ajili ya kujirekebisha, na huficha makosa na kasoro za marafiki zao kwa kufurahika na udanganyifu, au wanaonyesha hivyo kama wema, si kwamba wao wameshindwa kuwa waaminifu katika urafiki wao, bali wametenda dhambi kubwa mno la udanganyifu na usaliti. Usaliti wao huo utaweza kuja kumharibia heshima, hadhi na mafanikio ya rafiki yao huyo.