MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 0%

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA Mwandishi:
: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi: Vitabu mbali mbali

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

Mwandishi: Kimeandikwa na: 'Ayatullah al-'Udhma Nasir Makarim Shirazi.
: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 15891
Pakua: 2335

Maelezo zaidi:

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 15891 / Pakua: 2335
Kiwango Kiwango Kiwango
MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

Mwandishi:
Swahili

3

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 21 : UKAMILISHO WA KAZI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema :

Kukamilisha na kuendeleza matendo mema ni bora kuliko kuanzisha hivyo. 21

Maelezo mafupi: Mara nyingi sisi tunakumbana na kazi zilizo zenye faida na matendo yetu na majukumu ya maisha ya jamii ambazo zinabakia hazikukamilika. Watendaji wake wameanzisha kwa sababu mbalimbali za kuathiriwa, lakini wakaja kupoteza moyo wa kuendeleza na hivyo kuacha bila ya kukamilika. Islam inapendelea watu walio waaminifu na wenye moyo wa kujitolea ambao hukamilisha kazi yoyote ile wanayoianza.

SOMO LA 22: MIKAKATI YA KUDUMU

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Allah swt amewaamrisha Mitume yote kuwausia watu kuhusu uaminifu na amana. 22

Maelezo mafupi: Jamii bora ni ile ambayo inayo mambo mema mbalimbali, na muhimu mojawapo ni kwa watu kuwa na uaminifu na amana, kuaminiwa kwa kauli na matendo na tutambue wazi kuwa adui mkubwa wa mtaji huu ni uwongo, udanganyifu na hila. Jamii ambamo uwongo na udanganyifu na hila yanakuwa mambo ya kawaida, basi watu wote wataogopana, watajikuta wamekuwa pekee, hivyo kila mmoja itambidi aubebe mzigo mzito wa majukumu ya maisha peke yake na kwa hakika jamii hii itakuwa ni ya kipekee bila ya ushirikiano na wengineo. Na kwa misingi hii hii ndiyo maana Mitume a.s. yote imekuwa na mikakati ya kuhubiri na kuwalingania watu katika ukweli, uaminifu na kutimiza amana.

SOMO LA 23: ADHABU KALI KABISA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Mtu yeyote yule ambaye anajua jambo na wala hakifuati, basi siku ya Qiyamah atakuwa na adhabu kali mno. 23

Maelezo mafupi Katika mantiki ya Dini ya Kiislam, elimu imekuwa daima ni chombo cha kutumika na vile vile kuboresha maisha ya jamii. Ama sivyo elimu hiyo haitakuwa na manufaa wala faida yoyote. Wale watendao madhambi kwa kutokujua, wana wajibika kidogo, lakini wale wanapotenda dhambi huku wakitambua wazi wazi, wao watakuwa na mzigo mzito na mkubwa wa kubeba na wale ambao wanapuuzia kuwahudumia jamii katika nyanja mbalimbali, na yeyote yule aliye na hata kiasi kidogo au kikubwa cha elimu, basi watabebeshwa wajibu huo huo.

SOMO LA 24: MAOVU YA MADENI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Jiepusheni kukopa kwa kiasi muwezacho, kwani huleta majonzi usiku na udhalilisho wakati wa siku. 24

Maelezo mafupi: Urembo na mavutio ya maisha haya ya vitu na mashindano ya anasa katika zama zetu hizi zinawafanya watu wengi watumbukie katika gharama wasizoziweza kwa kuchukua mikopo na madeni yasiyolipika au kwa kufanya malipo kwa awamu. Kwa kuwa mdaiwa si mtu huru, hivyo tunaelekezwa kutokutumbukia katika madeni isipokuwa katika nyakati za shida kubwa tu. Hatari na athari za madeni yanakuwa makubwa na hatari kwa mujibu wa kanuni za nchi mbalimbali, na kwa hakika inaumiza uhuru na uhuru wa kiroho wa mataifa.

SOMO LA 25: MAISHA BORA YA KIJAMII

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Iwapo watu watalipana haki zao miongoni mwao, na kutimiza mahitaji ya wahitaji, wote wataishi maisha yaliyo mema na kutosheleza. 25

Maelezo mafupi: Katika Hadith iliyotajwa hapo juu, ambayo inazungumzia sadaka, kodi juu ya mali na milki na kuwasaidia mahitaji wale waliomuhtaji katika jamii zetu, inawaonya watu kuwa kwa kutimiza haki za watu wengine si jambo la hisani au la kibinadamu tu, bali ni kanuni iliyo muhimu mno ya kijamii ambapo amani na uhai wa jamii unapotegemea. Matokeo ya hatari yanayotokana na kutokuwapo na haki na vile vile ubaguzi wa watu ambayo yanahatarisha jamii za siku hizi na kwa hakika zinahatarisha na kuvuruga amani hivyo tunatambua umuhimu wa amri adhimu hii ya Dini ya Islam. Jamii zote za Wanaadamu zinahatarishwa na watu wa ulimwengu huu ambao wanachukulia haki ya kulazimisha na watu wenye uwezo mkubwa hujiepusha na haki zilizo faradhi juu yao kulipa.

SOMO LA 26: UFUNGUO WA MAAFA

Al-Imam Hasan al-Askari(a.s) amesema:

Allah swt ametuma kufuli za baadhi ya maovu na maradhi, ufunguo wao ni pombe, na uwongo ni mbaya zaidi kuliko pombe. 26

Maelezo mafupi: Jambo kubwa ambalo linaudhi maovu na magonjwa ni busara na akili, na kwa hakika haya ndiyo makufuli madhubuti yaliyowekea haya. Iwapo kufuli la busara litafunguliwa kwa ufunguo wa pombe, basi maovu na machafu yote yatakuwa huru na vile vile mlevi anaweza kutenda kosa, dhambi na ufisadi wowote ule.

Lakini iwapo mlevi atatenda kosa lolote lile akiwa katika hali ya ulevi, na mwongo huku akitambua wazi kwa fahamu zake, iwapo ataidanganya na kuihadaa taasisi ya maisha ya jamii, na akaua moyo wa kujitolea na akawa ndie chanzo cha madhambi na ufisadi wote katika jamii, hivyo uwongo ni hatari na uovu mkubwa hata kuliko pombe.

SOMO LA 27: ALAMA ZA WATU WA JANNAT ( PEPONI )

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Watu wa Jannat ( Peponi) wanakuwa na alama nne:Uso wazi, ndimi zao zinazungumza kwa nguvu na mambo yaliyo wazi, moyo wa huruma na mikono ya kheri .27

Maelezo mafupi: Shule bora kabisa ya wanaadamu ni ile ambayo inamchukulia mtu ndani ya jamii na jamii kama mkufunzi wa watu bora kwa sababu jamii ndiyo chanzo cha baraka zote za maada na kiroho. Hadith ya hapo juu inazungumzia alama za watu walioneemeka na wa Jannat ( Peponi), masuala hayo manne yamejihusisha na ukakamavu wa mfungamano wa kijamii na kupandikiza mbegu ya mapenzi na upendo wa kibinadamu katika jamii. Nyuso zilizo wazi na za kuvutia, na ndimi zilizo nyororo na zilizojaa huruma, mipigo ya moyo kwa ajili ya kuwahurumia watu, na mikono isiyositisha misaada, naam, hizi ndizo alama za watu wa Jannat.

SOMO LA 28: ALAMA ZA MNAFIKI

Al-Imam Ja'afar as-Sadiq(a.s) amesema kuwa: Luqman, mwenye busara alimwambia mwanake:

Zipo alama 3 za wanafiki: Ndimi zao hazioani wala nyoyo zao, Ndivyo zilivyo nyoyo zao ambazo hazioani na matendo yao, Yale yaliyo dhahiri hayaoani na yale yaliyo ndani mwao. 28

Maelezo mafupi: Unafiki ni maumivu makubwa yanayotokana na mtu mwovu na asiye na hima. Wale ambao wanajaribu kujionyesha kile ambacho sivyo walivyo, ndimi na nyoyo zao, udhahiri na undani wao, na vile vile kauli na matendo yao yanatofautiana. Kwa hakika watu kama hao huwa ni dhaifu na wala si mashupavu kwa kuelezea walivyo wao wenyewe kwa uhakika, na wala hawana mori na wla hawana maamuzi sahihi ya kufanya.

Wao wanaonekana katika sura mbalimbali na kwa hakika ni waovu kwa kila mtu hata wao wenyewe. Hata jamii ambazo zinajionyesha wema kwa nje wakati ni waovu kwa ndani. Ndimi zao ambazo ni vyombo vya kupasha habari kwa hakika yanapingana na kile kinachoendelea mioyoni mwa jamii hizi.

SOMO LA 29: USHAURI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Wachukulie ushauri na mawaida vizazi zinavyokuja kutokea waliokutangulia na ushauri na mawaidha hayo yawe ni kwa ajili ya maisha na mustakbal wako. 29

Maelezo mafupi: Tarikh (historia) imejaa kwa ushauri na mawaidha na mafunzo tunayotakiwa kuyapata, na hatima za kukosa haki, udhalimu, utofauti na ubaguzi, vilio na kugeuka jiwe (wagumu), kutokujua na kutokujali hali ya mazingira na nyakati hizo, na kwa hakika yote hayo yapo bayana katika historia. Lakini Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., mtu bora kabisa katika historia ya wanaadamu, anatuonya sisi tuchukue fundisho kwa ajili ya maisha yetu kutokea historia na hatima ya wale waliotutangulia ili isitokee sisi tukawa ndio mfano wa maovu na kasoro zetu zikawa ndizo mifano kwa vizazi vijavyo. Kwa hakika mawimbi haya ya muda yanawakumba watu wote na kuwachukua pamoja nao. Kwa hakika mataifa ambayo yanayamulika yale yaliyopita na kujenga utajiri na maendeleo yao ya mustakbal ndiyo yaliyobahatika na wenye ufanisi.

SOMO LA 30: KUONGEA NA UKIMYA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema :

Hakuna wema wala faida katika ukimya wa mtu mwenye busara, na vile vile hakuna wema wala faida katika mazungumzo ya jahili. 30

Maelezo mafupi Allah swt amefanya ahadi pamoja na wale ambao wamejulishwa na waliosoma kuwa kamwe hawatabakia kimya pale patokeapo upotofu, tabia mbaya, kutokuwapo na haki na usawa na njama za maadui na hueneza kote nuru ya hidaya, haki, usawa na uadilifu katika nyoyo kwa kutokana na maelezo na maneno yao yaliyo ya unyenyekevu na kwa mantiki sahihi (na kila mtu anachukuliwa kuwa amejulishwa na kuwajibika kwa kile ajuacho, hata kama kitakuwa kidogo kiasi gani).

Ama kwa upande wa pili, wale wasio na habari au taarifa za kutosha, wasiwapotoshe watu kwa kutokana na kutokujua kwao vya kutosha. Kwa hakika ukimya ule na mazungumzo haya yanaweza kuleta maafa na upotoshi. Yaani anayejua vya kutosha asikae kimya na yule asiyejua vya kutosha asizungumze kwa sababu ya kutokujua.

4

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 31: FURAHA YA USAMEHEVU

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Wewe utakapomzidi adui wako, basi mjaalie msamaha na kumwachia kama ni kuonyesha shukurani za ushindi wako . 31

Maelezo mafupi: Katika mtizamo wa Kiislamu, aina yoyote ya msaada na hisani, bila ya suala lolote, yanahitaji kushukuriwa, na shukurani ya uwezo ni usamehevu. Ushindi dhidi ya adui utaonekana pale tu ambapo moyo wa adui utakapo takasika dhidi ya maovu, na pale ambapo mizizi ya uadui utakapotokomea. Kwa kutoa sadaqa ya uwezo na nguvu ni usamehevu, kwa hakika ndicho kilicho jambo hilo kwa ajili ya sababu hizi. Kwa njia hii, adui atakuwa ameguswa moyoni mwake na hivyo adui wa jana atakuwa ndiye rafiki wa leo, na ni dhahiri kuwa ushindi utakuwa umepatikana wa undani na nje mwa mtu. Lakini, kinyume na hayo, wale ambao wanakuwa wamejitumbukiza katika kulipiza kisasi baada ya ushindi, si kwamba wanakuwa wamejinyima ubindamu, bali wanakuwa wanahatarisha ushindi wao vile vile.

SOMO LA 32: ZAHID KATIKA MAANA SAHIHI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Kwa hakika, Zahid duniani humu ni yule ambaye haghalibiwi na yale yaliyo haramu, bali hufanya as-Sabr na wala hapotoshwi na yale yaliyo halali latika kumshukuru Allah swt na kutimiza wajibu wake kumkumbuka Allah swt. 33

Maelezo mafupi: Baadhi ya watu wasioelimika vya kutosha wameigeuza u-Zohdi katika sura ya kupotosha. Wao wameichukuliwa u-Zohdi kama ni kuachalia neema za Allah swt na kujinyima mambo yote ya maisha na badala yake kuamua kuishi kama masikini na mafukara. Wakati ambavyo sivyo hivyo ilivyo ukweli. U-Zohdi kwa hakika ni kama vile ilivyoelezwa na Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. hapo juu na inaweza kuelezwa kwa kusema :Subira na kujizuia dhidi ya yale yaliyo haram na kutokuachilia au kusahau wajibu wetu kwa ajili ya yale yaliyo halali.

Iwapo sisi kwa hakika tutaitafsiri hivyo U-Zohdi, basi kwa hakika itakuwa ni kujitengezea kwetu upya, kuboresha na kuwa fundisho kwa jamii nzima kuliko kuchukulia msimamo wa upotofu na kujinyima yaliyo halalishwa.

SOMO LA 33: KULINGANA NA MASHAHIDI 34

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Yeyote yule awaye katika jitihada katika njia ya Allah swt na akiuawa, hatakuwa katika daraja la juu kuliko yule ambaye anajiepusha na kutenda dhambi ingawaje angeliweza kulitenda hilo. 35

Maelezo mafupi: Katika msimamo wa mantiki ya Dini ya Islam, vita vikuu vitakatifu ni kupigana dhidi ya matamanio ya nafsi hususan katika mazingira yaliyochafuka. Kwa hakika vita dhidi ya maadui yatapewa ushindi iwapo yatapiganwa kwa uhalisi na moyo msafi, nia halisi isiyojipendelea na tamaa za kibinafsi. Kwa hakika haya hayatawezekana kupatikana hadi hapo mtu awe amepata elimu ya kutosha ya maadili na mapambano ya nafsi. Hivyo Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa wale ambao wanafanikiwa kushinda katika uwanja wa vita dhidi ya nafsi, na wanabakia watu halisi katika mazingira yaliyo machafu, kwa hakika hawapo katika daraja la chini kuliko mashahidi wanaouawa katika njia ya Allah swt. Kwa kufuata Hadith hii, sisi twasoma katika Nahjul Balagha kuwa watu kama hao wanakuwa katika daraja la Malaika huko Jannat (Peponi).

SOMO LA 34: WATU WALIO BORA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Bora ya watu ni wale ambao hufanya maamuzi kwa haki na uadilifu . 36

Maelezo mafupi: Uamuzi wa haki katika Shariah, jamii na kimaadili itawezekana pale tu ambapo mtu anapochukulia maslahi yake na ya wengine kuwa sawa na mapenzi yake na chuki zake hazimshawishi wala kumzuia yeye asiweze kufanya haki na uadilifu. Na kwa hakika haya yatawezekana pale tu ambapo maisha ya mtu yatakuwa yameingiwa na nuru ya imani, uthamini wa kibinadamu, na mapenzi ya jamii kiasi kwamba mawingu ya ubinafsi, kutaka faida na uasherati hayawezi kupoteza fahamu na dhamira zake. Kwa hakika watu kama hawa inabidi waitwe watu bora kabisa.

SOMO LA 35: IBADA ZA WATU WALIO HURU

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Waumini wapo wa makundi 3 :

Wale wanaomwabudu Allah swt kwa kuiogopa Jahannam; ibada hii ni ya watumwa Wale wanaomwabudu Allah swt kwa kutarajia malipo Yake; hii ni ibada ya mamluki; Wale wanaomwabudu Allah swt kwa mapenzi na huruma zake; kwa hakika hii ndiyo ibada ya mtu aliye huru. 37

Maelezo mafupi: Ingawaje ahadi ya kulipwa mema kwa matendo mema na adhabu kwa kutenda maasi na madhambi, basi tutambue kuwa thawabu za Allah swt huwa bora kabisa papo hapo Adhabu za Allah swt huwa ni kali na zenye kuumiza kabisa, lakini wale waja wake halisi hawaoni chochote isipokuwa Allah swt tu na wala hawamwombi yeyote mwingine isipokuwa Allah swt tu na nyoyo zao zimeja kwa mapenzi ya Allah swt na huruma tu, wao daima huangalia kile kilicho zaidi ya thawabu na adhabu. Na nia yao huwa ni kuzitii amri za Allah swt ambayo huwa imejaa kwa mapenzi yaliyochanganyikana na kumtambua na kumjua Allah swt .

SOMO LA 36: KILE KIVUNJACHO MGONGO WA MTU

Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

Mambo 3 yanamwangamiza mtu : Yule ambaye anayejigamba kwa mema yake Yule ambaye anayasahau madhambi yake Yule ambaye ni mbishi. 38

Maelezo mafupi: Wale ambao hukuza matendo yako, kwa hakika wanaridhika kwayo, na kwa hakika tabia hii huwadhuru kwa kupatikana maendeleo na ufanisi. Na wale ambao huyasahau madhambi yao, basi kila siku hupakwa kwa madhambi mapya badala ya kufidia madhambi yao yaliyopita na hatima yao itakuwa ni kuanguka kwa ghafla.

Ama wale ambao hubakia katika maoni yao tu, wanakuwa wameepukana na msaada wa fikara za kijamii na akili zilizojaa na elimu na maarifa na uzoefu wa wengineo. Kwa hakika watu kama hao hutumbukia katika makosa, na hatimaye migongo yao huvunjika kwa kulemewa na uzito mkubwa wa matatizo na shida za kila aina.

SOMO LA 37: KUWA MSAFI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Mdomo wako ni njia mojawapo ya Allah swt. Mdomo ulio bora kabisa mbele ya Allah swt ni ule wenye harufu nzuri. Hivyo uweke mdomo wako unukie harufu nzuri kiasi uwezacho. 39

Maelezo mafupi: Katika Hadith hii ambayo imetolewa kutokea Al Wasa'il as-Shi'a kwa kuhusiana na kanuni za kupiga mswaki ambayo yanayo maana mbili za kidhahiri na batini. Kidhahiri inamaanisha kwa kuwa mwanadamu hufanya dhikiri ya Allah swt, husoma Ayah za Qur'an Tukufu na kumwabudu Allah swt kwa midomo yenu, basi yeye atazifanya midomo yao kuwa safi na kunukia manukato mazuri.

Na maana yake ya kibatini (kindani) inathibitisha mdomo ule ambao unao uhusiano pamoja na njia takatifu za Allah swt na waja wake, ndiyo iliyopendelewa zaidi mbele ya Allah swt wakati pale inapokuwa na manukato kwa wema, usafi na mazungumzo mema na inapokuwa huru bila ya kuzungumza chochote kibaya, kashfa, uwongo na ukali au ufokaji.

SOMO LA 38: HATIMA YA UJAHILI

Al-Imam Jawad(a.s.) amesema:

Yeyote yule atendaye chochote bila ya kuwa na elimu na maarifa ya kutosha, basi atakuwa mharibifu zaidi kuliko kutengeneza au kurekebisha. 40

Maelezo mafupi: Hasara za ujahili haipo tu kufikia kiasi ambacho mtu kwa hakika hawezi kufikia uthamini wake wa maisha halisi. Bali, ubaya na maangamizi yanayotokana na makosa ni kubwa kwa wale wanaotenda mambo bila ya kuwa na elimu.

Hivyo, ni kwamba mtu jahili anajaribu kufanya jambo jema kwa ajili ya mtoto wake, lakini humtumbukiza katika mabaya na bahati mbaya; anajaribu kuisaidia Islam, lakini anaiaibisha Dini; anajaribu kudumisha amani miongoni mwa watu, lakini yeye ndiye huwa mchochezi wa utenganisho na unafiki; kwa kifupi, maovu yake na maangamizo yake katika nyanja zote yatakuwa makubwa na hatari zaidi kuliko matengenezo yake.

SOMO LA 39: MISINGI YA MUONGOZO

Al-Imam Muhammad at-Taqi(a.s) amesema :

Mumin anahitaji kuwa na sifa 3 : Ufanisi kutokea kwa Allah swt Mhubiri halisi anayehubiri kutokea moyoni mwake Kukubali kutokea yale anayoshauriwa. 41

Maelezo mafupi: Katika njia hii, pamoja na wingi wa mipando na miteremko ambayo mwanadamu hupitia maishani mwake kwa ajili ya kuokolewa kutokana na wingi wa hatari ambazo zinahatarisha ukuaji na yenye manufaa na kuwa mtu wenye manufaa katika jamii, kwanza kabisa yeye anahitaji uhusiano wa kiroho pamoja na Allah swt ikisaidiwa na uasili wake, na baadaye kuwa na dhamira ambayo huwa makini na ile ambayo inamwongoza undani mwake, baadaye masikio yasikiayo kwa kutumia mawazo yake, miongozo, nasiha na mashauriano pamoja na wengineo.

SOMO LA 40: MASIKITIKO NI TABIA ZA UJAHILIYYAH

Al-Imam Muhammad al-Baqir (a.s) amesema kuwa; katika mojawapo ya hotuba fupi ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) , ambayo haijawahi kusemwa na mtu yeyote kabla yake :Masikitiko ni mojawapo na tabia ya zama za ujahiliyyah (haimbidi mtu kulalamikia matatizo na magumu, na badala yake inambidi ajitahidi kuyatatua). 42

Maelezo mafupi: Hadith hii fupi iliyojaa maana inayo maana ya kidhahiri na kibatini. Udhahiri wake unazungumzia matendo yasiyo sahihi ambayo yamekuwapo mashuhuri katika zama za ujahiliyya. Wakati mtu alipokufa, waombolezaji wanawake walikuwa wakiitwa kuimba nyimbo, mashairi mahsusi yasiyokuwa na maadili.

Na maana nyingineyo ambayo Al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. labda atakuwa akimaanisha ni, uombelezaji na masikitiko kwa nyakati ngumu na yenye shida na matatizo ya kibinafsi na kijamii, kwa hakika haya yote ni bure na upuuzi kwa kupoteza nguvu na wakati. Kwa hakika inambidi mtu ayatatue hayo kwa kuyatafutia utatuzi kwa kutumia uwezo wa akili na kufikiria njia endelevu na uvumilivu (subira).

5

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 4 1: KUJIPIMA MWENYEWE KILA SIKU

Al-Imam Musa al-Kadhim(a.s) amesema:

Yeyote yule asiyejipima kila siku, hana uhusiano wowote pamoja nasi. 43

Maelezo mafupi: Kuepukana na hasara na kujaribu kupata faida kubwa, katika taasisi yoyote ile iliyo kubwa au ndogo katika ulimwengu huu, haitawezekana bila ya kuwa na ukaguzi wa kila mara, majaribio na mahisabu kamili. Kwa hakika jambo la kushangaza ni kamba watu wapo waangalifu mno katika kuweka mahisabu yao ya mali na milki zao, na vile vile huwa waangalifu katika kupunguza au kuongeza uzito wao kwa gramu chache, lakini baadhi ya nyakati wao hata hawajali kuchunguza ubinadamu wao, maadili na masuala ya kiroho hata mara moja maishani mwao. Kwa hakika hili ndilo janga kubwa!

Lakini Mwislamu ambaye ni makini na halisi ni yule ambaye, kwa mujibu wa kauli ya Al- Imam Musa al-Kadhim a.s. katika hadith ya hapo juu, anachambua na kupitia mahisabu yake ya siku nzima bila kukosa. Iwapo atakuwa ametenda mema, basi hujaribu kuendeleza, na iwapo ametenda maovu, hujuta na kutubu.

SOMO LA 4 2: NISHANI ZA IMANI NI NGUMU KULIKO CHUMA

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Waumini ni madhubuti kuliko chuma kwa sababu chuma kinapowekwa motoni, hubadilika, lakini Waumini wanapouawa na kuhuishwa tena, basi hakutakuwapo na mabadiliko yoyote katika nyoyo na imani zao. 44

Maelezo mafupi: Maisha ni mlolongo wa matatizo na masuala magumu. Wale walio dhaifu hujisalimisha kwa urahisi, na hujitoa kutoka uwanja wa mapambano, lakini wale walio madhubuti kwa baraka za imani zao, kamwe hawajisalimishi kwa idadi yoyote ya matatizo. Wao wanajua kuwa daima vizuizi huwa vingi katika amri na njia ya Allah swt, kujiepusha na madhambi, na kujipatia heshima na sifa, na kwa ajili ya kutaka kujipatia utukuzo haya, kujidhibiti mtu mwenyewe,moyo wa kujitolea na kujizuia dhidi ya nguvu za matamanio na matatizo mengineyo. Hivyo, wao hawasiti kuendelea na juhudi zao katika njia ya dini, na wala hawaogopi chochote cha matukio haya.

SOMO LA 4 3: UHAKIKA WA UMOJA NA UADILIFU WA ALLAH SWT

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Uhakika wa upweke wa Allah swt unaonyesha kuwa mtu asijaribu kufikia kuhusu uasili wa Allah swt, na imani juu ya uadilifu Wake unamfanya mtu asimtuhumu Allah swt kwa jambo lake lolote lile. 45

Maelezo mafupi: Kwa kiwango ambacho kanuni ya kuwapo kwa Allah swt ilivyo wazi na ushahidi kwa ajili yetu na kitu chochote kile kutokea duniani humu ni sababu za Ukuu Wake, nguvu, maarifa na uwezo, uhakika wa uasili wake upo umejificha mbele yetu. Kwa asababu Yeye si kitu cha kuonekana na yupo nje ya uwezo wetu wa kumjua. Hivyo tunachukulia uhalisi wake upo zaidi ya mtu yeyote yule anavyomdhania na huu ndio uhakika wa umoja. Ama kwa upande wa pili, baadhi ya matukio ya humu duniani hutokea kiasi kwamba sisi hatuelewi maajabu na majibu yao. Kwa kuzingatia uadilifu wa Allah swt unatuambia kuwa matukio haya yote ni wastani, na shaka yoyote ile inayojitokeza si kwa mujibu wa uadilifu na busara Zake.

SOMO LA 4 4: BAADHI Y ALAMA ZA IMANI

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Mumini anao msaada mkubwa kabisa, na kwa gharama ndogo, na yenye busara maishani, na kamwe haipigwi mara dufu kutokea tundu moja ( haipatwi na madhara kwa mara nyingine kutokea mahala moja). 46

Maelezo mafupi: Imani inayo udhihirisho wa kisayansi, kimaadili na kijamii na dalili, ambapo bila ya hayo litakuwa ni jina tupu lisilo na maana. Hivyo Hadith ya hapo juu inazungumzia dalili zake nne :

1- Waumini wanawapatia misaada muhimu ndugu zao Waislamu kwa sababu misaada yao hiyo inakuwa pamoja na mapenzi, uadilifu na kutambua wazi.

2- Wao hawana maisha ya anasa na ghali na wala hawatendi makosa kwa ajili ya kujipatia vitu vyao.

3- Wao wanakuwa makini na kutambua katika maisha hususan katika masuali ya kiuchumi.

4- Wao wanajifunza somo kutokea kila tukio litokeapo na hivyo wao hawapatwi na majanga kwa suala hilo hilo moja.

SOMO LA 4 5: ULIMWENGU SI MWISHO WETU BALI NI NJIA YA KUPITIA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Ulimwengu umeumbwa kwa makusudi mengineyo, na kamwe haikuumbwa kwa ajili yake mwenyewe. 47

Maelezo mafupi: Kwa hakika inakuwa vigumu kwa watu kuelewa tafsiri za Ayah za Qur'an Tukufu na hotuba mbalimbali zinazoisifu dunia, yaliyomo duniani, kwa kuitambulisha dunia kama ni jumba la biashara au ni shamba la Waja wa Allah swt upande mmoja na kwa upande wa pili, kwa Ayah za Qur'an Tukufu na hotuba ambazo zinazoilaumu dunia hii na kwa kuiita kuwa ni hatari, danganyifu na chanzo cha movu.

Lakini, Hadith ya hapo juu inazitafsiri hayo kwa uwema kabisa, kwani inabainisha waziwazi kuwa iwapo dunia na yale yaliyomo yatatumiwa vyema na ipasavyo kwa ajili ya kujipatia maendeleo ya binadamu na upanuzi wa uadilifu na vile vile kama neema kwa ajili ya wanaadamu, basi kwa hakika itakuwa ni jambo la thamani na njema kabisa. Lakini iwapo mtu atadhania kuwa huu ndio mwisho wake tu na kuipendelea kupita kiasi, na kufanya uasi, maovu na madhambi, basi hakuna shaka kuwa itakuwa kuchukiwa na hatari mno.

SOMO LA 4 6: THAMANI YA MTU

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Ole wako ! Hakuna thamani yako isipokuwa ufanisi na Jannat, hivyo usibadilishane nacho kwa thamani ya kitu kingine. 48

Maelezo mafupi: Kwa kawaida iwapo mtu ataulizwa thamani ya maisha yake, basi hawezi kukisia au kukadiria. Hata hivyo, tunaona kuwa siku baada ya siku mtu huyu huyu anabadalisha thamani ya maisha yake kwa vitu ambavyo hatimaye anajikuta kuwa amepata hasara kubwa kwani amejibadilisha kwa vitu ambavyo havina thamani wala havitabakia (ni vitu vyenye kwisha na kuangamia) kama vile nyumba au jengo, au gari.

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anasema kuwa hakuna kitu chochote cha humu duniani kinachoweza kubadilishwa kwa maisha yako matakatifu! Jambo ambalo unaweza kubadilisha nacho ni ridhaa ya Allah swt, uendelevu wa kibinadamu na kiroho na vile vile neema isiyokwisha na yenye kudumu milele. Kwa hakika inastahili kujaribu na kujipatia na vile vile hata kama itabidi kujitolea mhanga kwa ajili ya kujipatia kiasi kiwezekanacho.

SOMO LA 4 7: UKWELI NA UWONGO

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Ukweli ni nzito ipendezayo, na uwongo ni nyepesi na rahisi, lakini ni yenye maumivu na hatari mno. 49

Maelezo mafupi: Tunaona vile Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alivyoweza kuelezea kwa uzuri kabisa kuhusu ukweli na uwongo katika sentenso fupi ya hapo juu! Kwa hakika ukweli unaonekana mkali na mara nyingi huwa chungu lakini hatima yake ni yenye kufurahisha na njema. Inafyonzwa kwa urahisi na jamii na hivyo huimarika kuwa madhubuti.

Lakini uwongo ni kitu kilicho rahisi na mara nyingi huwa tamu ipendezayo, lakini athari zake huwa maangamizi kama ilivyo chakula kitamu ambacho kwa hakika ni chakula chenye sumu ambacho kinadhuru moyo, tumbo, na matumbo ambayo yanatokezea hivyo iwapo vitaliwa na kumezwa. Na vivyo hivyo ndivyo ulivyo uwongo kama chakula hicho chenye sumu, ambapo kwa hakika uwongo huo huangamiza sehemu zote za jamii.

SOMO LA 4 8: URITHI WENYE THAMANI MKUBWA WA WAARABU

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Sentenso iliyo sahihi na yenye nguvu ni ile iliyotolewa na Waarabu katika msemo wa Lubaid (mshairi maarufu) pale asemapo: Ole wenu ! Kitu chochote mbali na Allah swt ni batili na uwongo na hatimaye kupotezwa kwa neema. 50

Maelezo mafupi: Tukitilia maanani kuteketea na kuangamia kwa mali na wadhifa au cheo na kuondolewa kwa baraka, kwa hakika yote yanam tanabahisha mtu kushikilia ukweli na haki katika kujipatia hayo na vile vile awe mtumiaji wa kiasi, yaani asiwe mfujaji 51 Kudumu na umilele ni mfano wa nguo ambayo inafaa kwa ajili ya kimo adhimu, kusimoingia uharibifu wa aina yoyote na kwa hakika heshima na adabu ndiyo yanayonasibishwa na uhalisi Wake. Inambidi mtu atambue uhakika huu katika kila hali ya maisha yake na kamwe asiwe mjeuri au mwenye kiburi.

SOMO LA 4 9: NINAWACHUKIA

Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema:Yule ambaye anaghushi au kumlaghai na kumfikishia hasara Mwislamu mwenzake, basi huyo hayupo pamoja nasi . 52

Maelezo mafupi: Wale ambao huchukulia furaha yao katika hali mbaya ya wengineo na faida zao kwa hasara za wengineo, basi watu kama hao kamwe hawatahesabiwa kuwa ni binadamu kwa hakika wala Wasilamu waaminiwao. Fadhila za mtu juu ya viumbe vinginevyo ni tabia na desturi zake katika jamii na yeyote yule anayejipatia faida kwa hasara za wengineo, kwa hakika anakuwa amekosa hadhi hiyo.

Mara nyingine tunaona kuwa sababu za hasara zinakuwa wazi na kutegemewa ambapo mara nyinginezo sababu hizo zinakuwa zimefichika kwa sababu ya kughushi na kukandamiza ama kwa njama au kukosa uaminifu. Kwa hakika haya yameharamishwa wazi wazi katika dini ya Islam katika sura yoyote ile, na hivyo ndivyo maana Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema:"Mimi huwachukia wale watu wafanyao maovu na madhambi haya."

SOMO LA 50: JITIHADA ZA WALIO WAOVU NA DHAIFU

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Kusengenya ni jitihada za mwisho za wale waliodhaifu 53

Maelezo mafupi: Baadhi ya madhambi yanapatikana kuwa ni miongoni mwa Madhambi Makuu (kabair dhamb) 54 ambayo machache ni Uchoyo au Ubahili, Udhaifu, Udhalilisho, na pasi na ushujaa kama Uwongo na Uzushi. Wale ambao wana tabia za kutafuta aibu na kasoro za wengine na hivyo kuzitoboa huku wakiwavunjia adabu na heshima za watu hao, na kwamba tunaona kuwa wingi wa watu wanakuwa wamejihusisha na moja wapo ya maovu kama hayo na hivyo ndivyo utawaona wanajiridhisha kwa mioto yao ya husuda na maovu na uwongo wao kwa njia hii, kwa hakika watu kama hawa ni dhaifu na ni watu waovu ambao hawaonyeshi uhodari wao kwa kujitokeza mbele bali utaona wao wanalengea kutokea nyuma ya migongo. Imeelezwa katika Hadith kuwa mtu yeyote anayezua uwongo, akatubu, basi atakuwa wa mwisho kuingia Jannat (Peponi). Ama sivyo, atakuwa ndiye mtu wa kwanza kuingia Jahannam (Motoni).

6

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 5 1: ALAMA ZA UKANDAMIZAJI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Dhalimu anazo alama 3 :

Kuwadhulumu wale walio zaidi yake kwa upinzani na kutokutii Kuwadhulumu wale walio chini yake kwa kuwakandamiza na kuwanyanyasa Na kushirikiana pamoja na wadhalimu. 55

Maelezo mafupi: Yeyote yule ambaye hutawaliwa na kasumba ya ukandamizaji akilin mwake, na kuathiriwa na ukosefu na maadili, hujidhihirisha tu vyovyote vile. Yeye hujiepusha na kutekeleza wajibu wake mbele ya wale ambao yeye atakuja kuwatii, na hufikia mwisho wa ukandamizaji, kutumia nguvu, vitisho na kudhulumu mbele ya wale walio dhaifu kwake, na huwachagua marafiki na wenzake miongoni mwa wale walio dhalimu. Yeye huwa daima dhalimu.

SOMO LA 5 2: HAKUNA UGONJWA USIOTIBIKA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Allah swt hakujaalia ugonjwa wowote hadi pale ameumba dawa yake. 56

Maelezo mafupi: Katika ulimwengu huu tunaoishi kuna matukio na athari zake. Zipo nguvu sahihi na zile zilizo pingamizi ambazo zinahitajiwa kutafutwa ili ziweze kutumiwa vile ipasavyo. Si kwamba hakuna magonjwa yoyote yasiyotibika na vile vile hakuna tatizo la kijamii lisiloweza kusuluhishwa. Wale ambao huchukulia msimamo kuwa matatizo hayawezi kutafutiwa ufumbuzi na popote pale wanapokumbana na masuala magumu husema kuwa hayo ni magonjwa sugu yasiyoweza kupatiwa ufumbuzi, kwa hakika wao hukiuka uhakika huu wa kusema kuwa hakuna ugonjwa usiotibika. Hivyo inatubidi sisi tujihusishe katika uwanja wenye matukio magumu maishani kwa subira na ustahimilivu na tujaribu kutafuta ufumbuzi wake.

SOMO LA 5 3: KWA NINI UPENDELEO HUTOKOMEA ?

Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

Allah swt amefanya Sharia ya kudumu kuwa Yeye kamwe hazichukui neema alizowajaalia watu, hadi pale wao watakapotenda dhambi litakalosababisha kuondolewa kwao kwa neema hizo. 57

Maelezo mafupi: Neema za Allah swt zipo chungu nzima bali si bila sababu. Allah swt kamwe hagawi wala kuzichukua neema Zake bila sababu. Wakati wanaadamu wanapozitumia neema zake kwa maovu, madhambi, maangamizo na uharibifu na pasi na haki, basi neema hizo hizo zinabadilishwa katika maangamizo yao wenyewe. Neema hizo walizojaaliwa zinachukuliwa tena na kubadilishwa kwa maafa na misiba. Viwanda na teknolojia yao yanageuka kuwa maangamizo na jamii zao zinakuwa ndizo vianzio vya kutokuwa na amani na usalama, na vie vile vyombo vya upesi vinageukia kuanguka kwao, na yote hayo ni kwa sababu wao wametumia vibaya neema za Allah swt alizowajaalia.

SOMO LA 5 4: SHAHADA NA UHALISI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Ukifa katika hali ya utohara, utakuwa miongoni mwa Mashahidi. 58

Maelezo mafupi: Hadith ya hapo juu ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni sehemu ya maagizo kwa mmoja wa Masahaba wake; "Iwapo itawezekana kwako, fanya wudhuu usiku na mchana, kwani iwapo utafariki ukiwa tohara katika hali ya wudhuu, basi wewe utahesabiwa kuwa Shahidi." Hivyo tunaona kuwa amri ya kwanza ni kufanya wudhuu, na papo hapo ujumbe mkubwa ni kutuambia sisi kuwa ni umuhimu mno kuishi maisha na kufa tukiwa bila madhambi. Wale ambao ni watoharifu wasio na madhambi, nyoyo zao huwa safi na maisha halisi na akili zao, na hufa kutokea humu duniani katika hali hiyo, na hivyo kwa hakika wao watahesabiwa miongoni mwa Mashahidi kwani ushahidi si tu kuuawa vitani tu. Zipo Ahadith sahihi zinginezo za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambazo zinathibitisha ukweli huu.

SOMO LA 5 5: WAJIPENDEAO KUJITOA MHANGA WENYEWE

Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

Babu yangu (Al-Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. ) kwa sababu ya Masahaba wake, hakusikia maumivu ya dharuba za mapanga wala mikuki ya maadui (Jeshi la Muawiyah bin Abi Sufian ). 59

Maelezo mafupi: Wakati uvutio wa mtu unapokuwa katika hatua ya mapenzi, kwa hakika mapenzi mahsusi, basi hisia zake zote zinakuwa zikilenga mahala hapo, hivyo chochote kile kitakachomwia basi kitavumiliwa nae. Si kuvumilia tu, bali hatajisikia vibaya. Wakati ambapo wanawake wa Kimisri, kwa kuuona uso wa Mtume Yusuf a.s., wakiwa wameghalibiwa na mapenzi, walipoteza fahamu zao na wakajikata vidole vyao badala ya matunda, hivyo hatushangai kuwa wale walio na mapenzi halisi katika njia ya Allah swt hawaoni ugumu wala maumivu katika kujitolea mhanga katika njia ya haki na ukweli ya Allah swt. Kwanza kabisa inambidi mtu awe mfanya mapenzi, ndipo hapo kutakapokuja kufikiwa hatua ya kuweza kujitolea mhanga na kuweza kuvumilia.

SOMO LA 5 6: MWENYE BUSARA NA MPUMBAVU

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Mtu mwenye busara hutegemea akili yake, wakati ambao mpumbavu hutegemea matakwa yake tu. 60

Maelezo mafupi: Watu wenye busara huwa ni watu wanyoofu na wenye kutaka ukweli na haki. Hivyo utawaona daima wao wakitafuta malengo yao makuu katika msaada wa Watakatifu ambao kuwafikia wao haiwezekani bila jitihada na matendo, kwani wao hulenga jitihada zao katika malengo, wakati ambapo wapumbavu wasiojua wanakuwa wametumbukia katika bahari la matakwa na fikara, na hujitafutia katika ulimwengu wa kubuni na ndoto, na kwa kuwa kutumbukia katika ndoto hakuhitaji jitihada wala matendo basi fikara potofu zinakuwa zikiwepo katika kila sehemu ya maisha yao. Wao daima hubakia katika ndoto zao kuwa kweli kesho, ambavyo haitakuja na kamwe isije, hivyo wao hawana msaada wowote ule katika maisha yao isipokuwa ndoto na matakwa yao tu.

SOMO LA 5 7: WAPO WACHAMUNGU WACHACHE

Al-Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Wingi wa watu ni watumwa wa ulimwengu wa vitu, na kwa hakika Dini ipo katika ndimi zao tu. Maisha yao ilimradi yapo sawa chini ya dini yao, wao wanaiunga mkono. Lakini pale wanapojaribiwa na matukio magumu, basi hubakia wachamungu wachache. 61

Maelezo mafupi: Dini, hususan Dini ya Islam, inahifadhi haki za watu katika jamii na kusaidia na kuunga mkono matakwa yao yaliyohaki na sawa. Lakini mara nyingine Dini inakuwa kizuizi kwa ajili ya matakwa ya mtu binafsi. Kwa hakika hapa ndipo watu wanapoweza kutambuliwa iwapo kweli ni watu wa Dini kama vile wanavyojiita.

Watu wengi huangalia kila kitu kwa mtazamo wa maslahi yao na kuitangaza Dini pale wanapoona kuwa inalinda maslahi na haki zao, lakini pale Dini inatenganishwa na maslahi yao ya kibinafsi, wao wanaiacha moja kwa moja na wanashuhudia kuwa sisi twaamini katika baadhi na hatuamini katika baadhi. Ama kwa hakika wale walio katika Dini huwa daima waaminifu na waumini halisi katika kila hali, na kwamba Dini ndiyo inayokuwa kila kitu kwao, na kamwe hawajali wala kupotoshwa na maslahi yao ya kibinafsi.

SOMO LA 5 8: UADILIFU MIONGONI MWA WATOTO

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:Fanya uadilifu mingoni ma watoto wako kama vile utakavyopenda wewe utendewe uadilifu miongoni mwenu. 62

Maelezo mafupi: Mojawapo ya makosa makuu ni kufanya upendeleo miongoni mwa watoto. Baadhi ya wazazi huwapendelea watoto wao wakubwa na ambapo wengine huwapendelea watoto wao walio wadogo. Kwa hakika utaona kuwa katika baadhi ya nyakati wazazi hao hupita mipaka na kwamba humpendelea mmoja wao kwa kupita kiasi kwa kumwonea huruma, mali na milki na mapenzi na hivyo kuwanyima kabisa watoto wake wengine haki kama hizo.

Kwa hakika hali hii inaibua moto wa uchoyo na husuda mioyoni mwao, na kwenda mbele, wao watakuwa maadui miongoni mwao na kugombana na kutengana na wazazi wao na hata wataweza kuthubutu kutaka kulipiza visasi katika jamii. Hivyo tujiepushe na tabia hii, kwani inatubidi tuwe waadilifu miongoni mwa watoto wetu.

SOMO LA 5 9: WEWE UPO DAIMA UKIDHIBITIWA

Al-Imam Muhammad at-Taqi(a.s) amesema :

Uelewe wazi wazi kuwa wewe hauwezi kutoka nje ya jicho la Allah swt. Sasa jitazame utakuwaje ? 63

Maelezo mafupi: Chapa ya kwanza ya Imani katika Allah swt ni daima kuwa na hisia na kujidhibiti vyema kwa maarifa ya Allah swt. Utambue wazi kuwa hakuna mwanya wowote ule ambao unakuwapo wewe nje ya elimu Yake, kwani walinzi wake wapo daima wametuzunguka pande zote.

Kiwango cha juu cha Imani kinamfanya mtu awe daima akijihisi akiwa mbele ya Allah swt. Kwa hakika kuwa na hisia kama hizi ni kipeo cha juu kwa ajili ya mwanadamu na jamii kwa ajili ya kujirekebisha na kujiongoza katika ubora kabisa wa Imani, na kwa hakika hutengeneza na kurekebisha kasoro zote za kijamii.

SOMO LA 60: SI KUSIFU KWA KUDANGANYA, WALA SI WIVU

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Kusifu na kutukuza zaidi ya ustahiki na haki ni udanganyifu na kusifu na kutukuza kasoro ya ustahiki ni udhaifu katika kuelezea au wivu. 64

Maelezo mafupi: Hakuna shaka kuwa mtu anayepaswa na mwenye sifa za kusifiwa ni lazima asifiwe na kushukuriwa, kwa njia hii sisi tutampa hima na nguvu katika mwelekeo wanaoelekea mbele. Lakini haya yanatakiwa lazima yawe sawa kabisa na sifa za mtu mwenyewe anavyostahiki. Ama sivyo, kutakuwa na matokeo na madhara mabaya. Iwapo yatakuwa zaidi ya mema, basi hapo tunasema kuwa ni udanganyifu ambayo kwa hakika huumiza sifa za msemaji na kusababisha kujiona na kujipenda kwa mtendaji. Na iwapo kwa hakika itakuwa kasoro ya sifa za mtu, basi itamvunja moyo mteda mema na huonyesha wivu au kuthibitisha udhaifu wa msemaji.