MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 0%

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA Mwandishi:
: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi: Vitabu mbali mbali

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

Mwandishi: Kimeandikwa na: 'Ayatullah al-'Udhma Nasir Makarim Shirazi.
: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi:

Matembeleo: 15759
Pakua: 2260

Maelezo zaidi:

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA
Tafuta ndani ya kitabu
  • Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 15759 / Pakua: 2260
Kiwango Kiwango Kiwango
MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

Mwandishi:
Swahili

7

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 6 1: DAIMA UWE TAYARI KWA AJILI YA NDUGU ZAKO

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Yeyote yule atakayejishughulisha katika kutimiza haja na mahitaji ya ndugu yake Mwislamu, Allah swt atamtimizia haja zake. 65

Maelezo mafupi: Watu wengi wanakuwa na dhana potofu kuwa iwapo wao watajishughulisha katika kutatua matatizo ya watu wengineo, basi wao wenyewe watarudi nyuma kimaendeleo katika maisha yao wenyewe, ambapo kwa hakika mantiki ya Kiislamu ipo vinginevyo. Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema :"Iwapo wewe utajishughulisha na kutatua matatizo ya watu na kuwatimizia matakwa yao, basi Allah swt, ambaye uwezo wake upo zaidi kabisa ya uwezo wa mtu yeyote, atakusaidia wewe katika kutatua matatizo na shida zako." Kwa hakika sisi wenyewe tumeshawahi kushuhudia vile matatizo na shida za watu wenye kuwasaidia watu wengine zinavyokwisha kiajabu na kwa hakika haya ndiyo malipo na kudura za Allah swt.

SOMO LA 6 2: MAKOSA MAISHANI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Usiushughulishe moyo wako kwa huzuni na masikitiko kwa yale yaliyopita kwani utaponyokwa na fursa ya kujitayarisha kwa yale yanayokuja. 66

Maelezo mafupi: Ni watu wachahce kabisa ambao wataonekana hawana makosa na wasiopoteza baadhi za fursa wazipatazo maishani mwao. Hawa kuna makundi mawili ya watu. " Baadhi yao hupoteza wakati wao kwa kujutia yale yaliyopita na hivyo hupoteza nguvu iliyobakia kwa njia hii. " Ama wengineo huchukulia yale yaliyopita kama yamepita na kwisha na kuyasahau kwani huchukulia mafunzo tu kutokea hayo kwa ajili ya kuongoza maisha yao na kutumia nguvu na nishati zao zote kwa ajili ya ujenzi wa leo na kesho. Kwa hakika kikundi hili la pili ndilo litakalofuzu kwa mujibu wa kauli tukufu ya Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s)

SOMO LA 63: DINI YA UISLAM ITAKUWA DINI YA ULIMWNEGU MZIMA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Hakutabakia nyumba hata moja juu ya ardhi hii, hata kama nyumba hizo zitakuwa za udongo au za mahema ya sufu, hadi pale Allah swt atakapokuwa ameshaingiza Dini ya Islam ndani mwake. 67

Maelezo mafupi: Kila siku ukweli huu umekuwa dhahiri kuwa ulimwengu huu umekuwa na machaguo mawili : Ama itakubalia Dini ya Islam au haitakubalia dini yoyote ile. Na kwa kutokuwa watu wa dini ni kinyume na maumbile ya dini, basi hatimaye ulimwengu utakuja kukubalia dini ya Islam. Kwa hakika sasa hivi mawimbi ya kuyazingatia Dini ya Islam yametanda ulimwenguni sehemu mbalimbali. Lakini jambo hili litakuja kukamilika wakati atakapodhihiri Al-Imam Muhammad Mahdi Sahib az-Zamaan(a.s) Siku hiyo, kuabudu masanamu na ushirikina wa kila aina utatokomezwa kutokea ulimwengu huu na Dini ya Islam ndiyo itakayokuwa Dini ya ulimwengu mzima. Kwa hakika Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ameshatupatia ubashiri huu katika Hadith hiyo ya juu.

SOMO LA 6 4: USILICHUKULIE DHAMBI LOLOTE KUWA DOGO !

Al-Imam Hasan al-Askari(a.s) amesema:

Moja wapo ya dhambi ambalo haliwezi kusamehewa ni lile ambalo mtu husema 'Natumai kuwa dhambi langu hili liwe ni hili tu (la mwisho).' 68

Maelezo mafupi: Madhambi madogo yanageuka kuwa madhambi makuu kwa sababu mbalimbali, mojawapo ni kwa sababu ya kulichukulia dhambi hilo kuwa ni dogo na lisilo na umuhimu, likiwa ni mojawapo la vutio hatari la Kishetani. Madhambi yaliyo makubwa na ambayo mtu huyaogopa si tishio kwani mtu huwa daima ni mwangalifu kwa kutoyatenda. Lakini hatari ni pale ambapo yeye anapoyaona kuwa ni madogo na anapokosa hofu yake, basi huweza kuyatenda kwa urahisi, na vile vile huwa mwepesi kuyarudia kila mara, na hivyo ndivyo kwa hakika ni sababu mojawapo ya kubadilishwa kwa dhambi dogo kuwa dhambi kuu, na kwa hakika humwepusha mwanadamu raha, furaha na utajiri kwa milele. Zaidi ya hayo, dhambi lolote liwalo, ni kwa hakika dhambi kuu kwani linakuwa limekiuka mipaka iliyowekwa na Allah swt kwani mtu anakuwa ameasi amri za Allah swt.

SOMO LA 6 5: UTUKUFU WA ELIMU

Al-Imam Musa al-Kadhim(a.s) amesema :

Ubora wa Mwanazuoni juu ya Mchamungu ni sawa na ubora wa jua juu ya nyota. 69

Maelezo mafupi: Nyota zinang'ara zenyewe lakini nuru yao haitufikii sisi na wala haitung'arishii njia zetu, lakini mwanga wa jua na miale yake ya kidhahabu na yenye kung'ara, si kwamba yanahuisha bali huweza kuwaongoza wakazi wote duniani kutambua njia zilizo sawa ili wasije wakatumbukia katika njia zilizo mbovu na mashimo. Na kwa hakika hii ndivyo ilivyo tofauti kati ya Wanazuoni na mfuasi. Huyu wa pili si kwamba kuwa hutaabika kwa matatizo yake mwenyewe, ambapo huyo wa kwanza (Mwanazuoni) daima hujaribu kuwaokoa wale wote waliopotoka. Sisi tunaelewa vyema kuwa sayari zote hufaidika kwa mwanga wa Jua, na kama wasingelikuwapo Wanazuoni, basi kusingalikuwapo wafuasi.

SOMO LA 6 6: HAKI ZA WOTE

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:Kama vile watoto wanawajibika kwa kutokuzijali haki za wazazi, vivyo hivyo wazazi pia wanawajibika kwa kutokutekeleza haki za watoto. 70

Maelezo mafupi: Hakuna haki yoyote iliyoambatanika na kazi za dunia. Yaani ni kusema kuwa kuna uwajibikaji pamoja haki yoyote na haki kubwa kunaita kwa ajili ya wajibu mkubwa na uwajibikaji. Kwa misingi hii, wazazi ambao wana haki kubwa juu ya watoto wao, kama vile ilivyoelezwa katika Qur'an Tukufu baada ya haki za Allah swt, itachukua wajibu mkubwa kwa ajili yao. Wao hawatapuuzia kuwalea na kuwafunza hata kiasi kidogo kitakachowezekana na kujaribu kuwainua kiroho na kimwili na papo hapo kumwokoa dhidi ya maovu ya kiakili na kukosa maadili, na misukosuko ya maishani mwao yasiwapotoshe wao katika kutimiza wajibu wao mkubwa.

SOMO LA 6 7: TUMIA FEDHA KWA UTIIFU HAUTATENDA DHAMBI

Al-Imam Musa al-Kadhim(a.s) amesema:Msijiepushe na kutumia mali yenu katika utiifu na njia ya Allah swt, ama sivyo itakubidi wewe kutumia mara dufu katika kumuasi na kwa kutenda dhambi. 71

Maelezo mafupi: Wapo baadhi ya watu walio makini katika kulipia, kwa mfano, gharama zao za afya, na hivyo hulipia mara dufu kwa kutibu maradhi yao. Hili ni jambo la kawaida kwani mtu ambaye anapojiepusha na kulipia kwa ajili ya matumizi ya kawaida, itambidi avumilie gharama zaidi. Wale wanaojizuia na gharama au muda kwa ajili a watoto wao, basi hao watajitwisha gharama kubwa kwa tabia yao hizo, madhambi, upotofu na upuuzaji, dharau zao na wale ambao hujiepusha na kulipia mahitaji ya wanaohitaji katika jamii zao, basi utawaona mara nyingi hulipia zaidi ya hayo, kwa sababu ya kutokujidhibiti kuanzia mwanzoni. Kwani hawajachukua hatua za tahadhari kutokea mwanzoni.

SOMO LA 6 8: SOKO KUBWA LA KIBIASHARA

Al-Imam 'Ali an-Naqi(a.s) :Ulimwengu ni kama soko ambapo wapo wanaopata faida na wengine kupata hasara. 72

Maelezo mafupi: Ulimwengu huu si nyumba halisi ya mwanadamu, wala si makazi yake ya kudumu milele. Na badala yake ni jumba kubwa la kiuchumi ambapo mwanadamu hutumwa duniani humu akiwa na mitaji mikubwa kwa maisha yake yote, ikiwemo nguvu zake, akili na fahamu ili aweze kuwa na upendo kwa ajili ya kujineemesha na maisha ya milele. Wale waliowakakamavu, hodari na makini, wafanyao kazi kwa bidii na makini ndio huwa waangalifu dhidi ya njama katika biashara hii kubwa. Wao hawajuti hata kwa punde ndogo na huwa daima wakiwa katika mikakati ya kutafuta na kuchagua mambo mazuri, mali ya kudumu milele na maisha mema kwa ajili yao wenyewe na vile vile kwa ajili ya jamii kwa kutumia mitaji hii. Wao kamwe hawaipotezi mitaji yao katika maovu, maangamizo na ubadhirifu, ili hatimaye wasije wakatoka humu duniani wakiwa mikono mitupu (wamefilisika).

SOMO LA 6 9: WATU WALIOTUKUZWA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:Siku ya Qiyama watu watakao kuwa wametukuzwa na Allah swt watakuwa ni wale ambao wanakuwa wamejishughulisha zaidi katika kuwanufaisha watu. 73

Maelezo mafupi: Kutoa huduma kwa watu, ni jukumu moja lililo kubwa katika Dini ya islam, na ni njia mojawapo ya kuwahudumia watu wa Allah swt kwa kuheshimu maslahi yao na kwa ajili ya manufaa yao, na kwa kuyashughulikia hayo kama kwamba ni kwa ajili yake menyewe na wala kutokudharau ukarimu wanapokuwa mbele yako au wasipokuwa mbele yako.

SOMO LA 70: KANUNI 3 ZA MISINGI YA JAMII

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Watu wote wako sawa (katika haki za kijamii) kama vile zilivyo meno katika fizi ! Mtu mmoja mmoja ndio jamii kuu kwa pamoja na ndugu zao Waislamu. Na wala haijuzu kuhusiana na yule mtu ambaye hakutakii wewe kile ajitakiacho kwa ajili yake mwenyewe. 74

Maelezo mafupi: Kanuni 3 za kimsingi za kijamii zimetajwa katika Hadith hii : " Kwanza, usawa na haki miongoni ma watu kutokea makabila yote, lugha na daraja katika haki za kijamii. " Uhusiano wa mtu pamoja na jamii na jamii pamoja na mtu ambapo kila mtu anakuwa ndugu kwa mwenzake.

" Umuhimu wa kuheshimu maslahi ya mwenzake kama kwamba ni maslahi yake mwenyewe kwani hivyo ndivyo ilivyo kanuni ya urafiki na udugu. Kwa hakika jamii ambayo haina kanuni hizi tatu basi jamii hiyo si ya Kiislamu wala si jamii ya kibinadamu.

8

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 7 1: HARAKA NA PUPA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Haraka na pupa ni aina mojawapo ya upumbavu kwa sababu wale walio na tabia hii hujuta katika muda mfupi baada ya matendo yao, na ama sivyo huonyesha kuwa upumbavu wao upo umetua na sawa. 75

Maelezo mafupi: Akili na busara kunamfanya mtu ajiepushe na pupa isiyohitajika pale apatapo fursa yoyote kwani katika hali kama hiyo, yeye hushindwa kuchunguza masuala yote kwa usahihi ipasavyo na hushindwa kutoa uamuzi sahihi, na punde si punde hujutia matokeo ya maamuzi yake aliyoyafanya kwa pupa na matendo yake asiyoyafikiria vyema. Baadhi ya nyakati, mtu huharibu kauli yake yote kwa pupa moja tu katika maongezi yake, hupoteza marafiki wake wa zamani na majuto yanakuwa yamepigiwa lakiri moyoni mwake. Lakini iwapo watu hawatafanya Tawbah baada ya kutambua matokeo mabaya ya matendo yao, basi kwa hakika wao hawana akili na fahamu timamu, ni vichaa wasio na akili.

SOMO LA 7 2: ZAHID 76 KWA HAKIKA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Uzahid katka dunia hii unategemea mambo matatu: Udogo wa matamanio Kushukuru kwa kujaaliwa neema Kujiepusha na yale yaliyoharamishwa. 77

Maelezo mafupi: Wingi wa watu wanakosea kuelewa maana halisi ya Ucha-mungu na hudhania kuwa ni kujitenga na maisha ya kidunia na kijamii, huwaita wachamungu wale ambao kwa hakika wamejitenga kabisa na raha za maisha ya kijamii, na hivyo hudhania kuwa maisha haya ni ya mpango wa kikabaila. Ama kwa hakika uchamungu wa uhakika ni ule ambao una imani sahihi za kijamii kama vile ilivyoelezwa katika Hadith hapo juu. Kujiepusha na kudhulumu haki za wengine na vile vile kujiepusha na kujipatia mali na milki kwa njia zisizo halali, na utumiaji sahihi wa mali na milki katika njia sahihi na za manufaa kwa wanaadamu ( ambavyo ndivyo kwa hakika njia ya imani ya kutoa shukurani) na kwa kupunguza matamanio yanayomtumbukiza mtu katika utenganisho baina yake na pesa, wadhifa na tamaa zake.

SOMO LA 7 3: JARIBIO LA HESHIMA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:Kwa mambo matatu watu wenye akili hutahiniwa :

Mali

Cheo au wadhifa

Misiba. 78

Maelezo mafupi: Majaribio ya Allah swt yanamaanisha maendeleo na uboreshaji na huwa hazina ala au vifaa maalum. Mwanadamu anaweza kujaribiwa kwa njia tatu ambazo ni muhimu kuliko zinginezo:

1. Iwapo mtu atapoteza fahamu au busara pale anapopata mali na milki ?

2. Wakati mtu anapopewa wadhifa au cheo, hata kama uwezo wake utakuwa mdogo kiasi gani iwapo atasahau kila kitu ?

3. Pale linapomsibu jambo lisilomfurahisha yeye, jee anaanza kukosa subira na kutoa malamiko yake kwa kuufungua mdomo wake kwa kutoa maneno ya kukufuru na kukosa shukurani ? Kwa hakika haya ndiyo mambo ambayo mwanadamu hujaribiwa zaidi.

SOMO LA 7 4: MPANGO SAHIHI A DUNIA NA AKHERA

Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema:

Fanyia kazi dunia hii kama utaishi daima, na uifanyie kazi akhera kama kwamba utakufa kesho ! 79

Maelezo mafupi: Hadith hiyo ya juu inabainisha wazi mwelekeo wa dini ya Islam katika masuala yanayohusiana na maisha haya ya kimali na kiroho. Inambidi kila Mwislamu awe na nidhamu kamili katika masuala yote yanayohusiana na maisha ya kimali kama kwamba ataishi daima, na hivyo unafiki wa kujitenga na maisha ya duniani yanayofanywa na wale wenye kudai uchamungu, hapa unakanushwa wazi wazi.

Inambidi mtu awe makini na masuala yanayohusu kiroho na utayari wake kwa ajili ya akhera iwapo yeye atakufa kesho, basi hatakuwa na kasoro yoyote ile. Yeye inambidi awe ameshajitakasisha kwa maji ya Tawbah na awe ameshalipa madeni yote na asiwe na sehemu yoyote yenye kiza katika maisha yake.

SOMO LA 7 5: ATHARI ZA DHAMBI

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Wale wanaokufa kwa kutokana na madhambi ni wengi kuliko wale wanaokufa vifo vya kawaida, na wale ambao wana maisha marefu kwa kutokana na mema ni wengi kuliko wale walio na maisha ya kawaida. 80

Maelezo mafupi: Imethibitishwa katika zama hizi kuwa mengi ya magonjwa ya kimwili yanatokana na masuala ya kiroho, na mojawapo ya sababu muhimu kabisa ya ugonjwa wa kiakili ni kule kushinikizwa na kulemewa zaidi nafsi ya mtu kwa dhamira yake. Mtenda dhambi anahukumiwa katika mahakama ya dhamira yake na hutaabika kwa adhabu kali ya kiroho na matokeo yake yanadhihirika katika mwili na nafsi yake na hata katika sura za mauti. Kwa upande mwingine, watu waliobarikiwa wanapewa hima na dhamira zao na hima hizi za kiroho zinawapa nguvu wao na kuwafanya wao wawe wachangamfu na hivyo umri wao ulioongezwa, wao huweza kufikia umri wao kwa ukamilifu. Hivyo, kwa kifupi ni kwamba madhambi hufupisha umri wa mtu na mtu asiye na madhambi. Umri wake huongezeka.

SOMO LA 7 6: SHI'A SAHIHI

Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) alimwambia mmoja wa marafiki zake:Wabainishie Mashi'a wetu kuwa hakuna anayepokea neema za Allah swt isipokuwa ajitumikishe (afanye kazi). 81

Maelezo mafupi: Hotuba hii ya Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) ni jibu kwa wale ambao hudhani kuwa wao wanaweza kufikia daraja la juu mbele ya Allah swt kwa kuketi tu huku wakijiita Mashi'a na wakionyesha mapenzi yao kwa Ahlul Bayt(a.s) , ambapo sisi tunatambua wazi kuwa Dini ya Islam inaamini katika matendo na Mashi'a wa kweli ni wale ambao kwa hakika wanakuwa na mikakati ya kimatendo kwa kumfuata Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) katika matendo na Masahaba wake, ambapo kwa hakika Ushi'a umetokana na neno `mushaieat' yaani 'kumfuata mtu'. Hivyo Mashi'a ni wale ambao huwafuata Wananyumba wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) (Ahlul bayt a.s.) kwa ukamilifu.

SOMO LA 7 7: NI NANI TUMWULIZE ?

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Usiwatake ushauri wale watu walio bakhili kwa sababu wao watakukosesha wewe kuwafanyia watu wa Mungu fadhila, na kukuogopesha wewe kwa umasikini Na wala usiwatake ushauri wale walio woga, kwani wataifanya dhamira yako iwe dhaifu kwa kufanya mambo yaliyo muhimu Na wala usiwatake ushauri walafi, kwani wao wanakurembeshea shari kwa ajili yako. 82

Maelezo mafupi: Ushauriano ni mojawapo ya amri za Kiislamu, lakini kama vile ushauriano pamoja na mtu anayestahiki inavyoweza kuwa na faida na maendeleo, vivyo hivyo ushauriano pamoja na watu walio dhaifu ni hatari na yenye matokeo mabaya. Ndiyo maana Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) anatuzuia tusichukue ushauri wa aina tatu za watu hususan katika masuala muhimu ya kijamii.

Wale walio bahili, woga na walafi kwani wa kwanza humkosesha mtu baraka na rehema za Allah swt , wakati wa pili hudhoofisha hima yake, wakati wa tatu humshawishi mtu kukiuka haki za wengineo kwa misingi ya ulafi na uroho.

SOMO LA 7 8: NEEMA ILIYO BORA KABISA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Neema iliyo bora ni siha (afya) na jambo lililo bora kabisa linalojaa moyoni mwa mtu ni kuwa na yakini juu ya Allah swt. 83

Maelezo mafupi: Kwa hakika Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amelizungumzia jambo kubwa mno na hisani za kiroho. Afya ya kidhahiri si kwamba ni neema kubwa mno ya Allah swt , bali ni chanzo cha shughuli zetu zote, jitihada na baraka na miongoni mwa neema zisizoonekana, hakuna kilicho bora kuliko nuru ya Imani ambayo ni nuru inayomwongoza mwanadamu katika njia ya maisha na kiponyesho cha maradhi ya ujahili, unyenyekevu, kujiona chini na kujivuna na ni dawa bora kabisa ya moyo na nafsi ya mtu!

SOMO LA 7 9: IMAM A.S. ASIYEONEKANA

Al-Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. aliulizwa ni kwa vipi watu wanafaidika kwa Imam anayeonekana na yule asiyeonekana ? Kwa hayo Imam a.s. alijibu: Wanafaidika kama vile wanavyofaidika kwa jua linapokuwa nyuma ya mawingu ! 84

Maelezo mafupi: Mwanga wa jua ni chanzo cha uhai na harakati nyeti juu ya ardhi hii na hakuna kiumbe chochote juu ya ardhi hii inaweza kuendelea na maisha yake bila ya mwanga huu wa jua, na vivyo hivyo ndivyo ilivyo nuru ya Imam aliye hai na Kiongozi katika maisha ya mwanadamu na ya kiroho. Mwanga wa jua nyuma ya mawingu, ni sawa na mwanga nyuma ya kioo kinachopitisha mwanga, hutuma mwanga wake wa kutosha na huondoa kiza nyakati za usiku na hivyo huathiri mimea na viumbe vyote vilivyo hai.

Kwa hakika baraka za Imam a.s. hujaza ulimwengu wa wanaadamu kwa baraka zao hata kama Imam a.s. atakuwa nyuma ya pazia, kwa kuwa kila jengo hutumia mwanga wa jua kwa kiasi kinachojifungua, hivyo hisa za watu kutokea mwanga wa kiongozi ni sawa na uwiano huo na hutegemea kiasi kilichopo cha uhusiano na mfungamano pamoja na Imam a.s.

SOMO LA 80: USIYASIKILIZE YALE YOTE YANAYOTAMKWA !

Al-Imam Muhammad at-Taqi(a.s) amesema :

Mtu amsikilizaye mhutubiaji, kwa hakika amemwabudu yeye. Hivyo iwapo mhutubiaji akiongea kutokea yale ya upande wa Allah swt, basi atakuwa amemwabudu Allah swt, na iwapo atakuwa ameongelea kwa kupitia ulimi wa Ibilisi, kwa hakika atakuwa amemwabudu Ibilisi. 85

Maelezo mafupi: Matamshi, yoyote yale na kutokea mtu yeyote yule, yanaathiri, na kwa hakika kusikiliza matamshi kwa kawaida hupiga chapa moyoni mwa mtu, na kwa kuwa madhumuni ya wazungumzaji hutofautiana, kwani badhi yao huongelea kuhusu ukweli ambapo wengine huzungumzia uwongo, na hivyo kujisalimisha mbele ya mojawapo ya makundi haya mawili ni aina mojawapo ya 'ibada kwani uasili wa 'ibada si kingine ila ni kujisalimisha. Hivyo, wale ambao husikiliza yale yaliyo ya kweli ni waumini wa kweli. Na ambao husikiliza yale yaliyo ya uwongo na mapotoshi, basi ni waumini wa uwongo. Hivyo ni wajibu wa kila mtu kujiepusha na wazungumzaji wote walio waongo na hivyo wasiweze kuathiriwa na mapotoshi yao kufikia nyoyo zao kwa kupitia masikio yao.

S9

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 8 1: WATU MASHETANI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:Wakati utakapomwona mtu yu tofauti kwa kile akisemacho au kisemwacho kuhusu yeye, basi wewe utaelewa kuwa yeye ni mwovu au Shaitani. 86

Maelezo mafupi: Kutumbukia kwa mtu katika madhambi mbalimbali hakumtoi nje ya kila aina ya shutuma. Yeye hajali kile akisemacho kuhusu wengineo na kile kinachosemwa kuhusu yeye. Yeye huwashutumu kila mtu na wala haoni aibu wala kuhangaika kwa kile kinachonasabishwa kwake. Kwa hakika watu hao ni waovu, dhalili, walianguka chini na kishetani.

SOMO LA 8 2: FURAHA YA UHAKIKA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Leo ( Siku ya Idd ) ni Idd ya wale ambao saumu zao zimekubaliwa na kushukuriwa kwa qiyam zao, na siku yoyote ile ambamo wewe hautatenda dhambi, kwa hakika ndiyo siku yako ya Idd. 87

Maelezo mafupi: Sherehe na furaha baada ya saumu za mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa hakika ni sherehe na furaha kwa ajili ya kughalibu matakwa ya mtu, na furaha hizo ni kwa sababu ya kutii amri za Allah swt. Kwa hakika Siku hiyo ni sherehe na furaha kwa ajili ya wale tu ambao wamefuzu katika kutekeleza wajibu huu mkuu wa Allah swt na kuelewa falsafa yake, ama kwa wale watu wasio na aibu ambao hawakuuheshimu mwezi huu adhimu na mpango wake wa kimafunzo, kwa hakika si kitu kingine isipokuwa na siku ya majonzi na udhalilisho kwa ajili yao.

SOMO LA 8 3: MTAJI WENYE THAMANI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Allah swt kwa hakika haangalii sura wala mali zenu, bali kwa hakika anaangalia nyoyo na matendo yenu. 88

Maelezo mafupi: Katika jamii nyingi kigezo cha kumtukuza na kumsifu mtu ni kwa mujibu wa utajiri na vile alivyonavyo, lakini Dini ya Islam kwa wazi kabisa inasema: Uteuzi kwa kutokana na hayo kama ndiyo kigezo cha utukufu, basi ni makosa makuu katika kuchagua. Badala yake, kile kinachochukuliwa na Allah swt na kilicho na uzani mzito katika ukweli ni fikara na matendo, fikara safi ni chanzo cha matendo safi. Na katika mahakama ya Allah swt ni watu hawa tu wenye mitaji hii ndio watakaofuzu.

SOMO LA 8 4: VITU 2 HUSABABISHA MAANGAMIZO YA WATU

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:Vitu viwili vinawaangamiza watu :89 " Hofu ya umasikini na " Kujitakia ufakhari !

Maelezo mafupi: Iwapo sisi tutachunguza sababu za kuongezeka kwa dhuluma, rushwa, uwizi, kuibia mizani katika sura mbalimbali na vile vile ulafi usio wa kawaida na harakati za watu za kupora, basi tutaona kuwa mambo haya mawili ndiyo yenye mizizi na athari katika kutendwa kwa maovu haya na mengine mengi kama hayo katika sura mbalimbali. Baadhi ya watu pamoja na kuwa na kila kitu, hutenda madhambi si kwa hofu ya umasikini na kama vile wanavyodai wao ati kuweka usalamani maisha yao, na wengineo hujitolea mhanga wa amani ya maisha na roho zao kwa ajili ya heshima zisizo za uhakika, ambapo kwa hakika wangeweza kuishi maisha ya utulivu na raha iwapo wangaliacha mienendo hii miwili iliyo miovu.

SOMO LA 8 5: HAKUNA WEMA ULIO MDOGO

Al-Imam Zaynul 'Abidiin(a.s) amesema:Tendo lililotendwa kwa Taqwa si dogo, ingawaje laweza kuonekana kuwa dogo. Je itawezekanaje kwa tendo linalopendwa na Allah swt kuwa dogo ? 90

Maelezo mafupi: Qur'an Tukufu inatuambia kuwa Allah swt hukubalia matendo yale tu yaliyoambatanishwa na taqwa na nia halisi. Hivyo usafi katika nia na uaminifu na taqwa ndiyo mambo yanayotakiwa kuzingatiwa kuliko jambo lingine lolote, na wala si idadi ya matendo ! Kwa hakika tendo kama hilo lina thamani hata kama litakuwa dogo kiasi gani kwani ndilo linalopendelewa na Allah swt. Je tendo linalokubaliwa na Allah swt likaweza kuwa dogo? Kwa kifupi, matendo mengi hewa, yasiyo halisi na ya kinafiki hayana thamani yoyote, lakini matendo yale ambayo ingawaje ni mepesi, lakini huwa ni halisi, kwa moyo na kweli ndiyo matendo hayo yaliyo na thamani na nzito.

SOMO LA 8 6: USITENDE DHAMBI HAUTAOMBA MSAMAHA

Al-Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:Usitende dhambi ili usihitaji kufanya tawba (kutubu), kwani Mumin hatendi dhambi wala kuomba msamaha wake, lakini mnafiki kila siku hetenda dhambi na kuomba msamaha wake. 91

Maelezo mafupi: Kial mtu anaweza kutenda dhambi, lakini Waumini wanayo tofauti mojawapo mbali na wanafiki waliomo. Waumini hujiepusha na kutenda madhambi ili wasitakiwe kufanya tawba, kwani wanatambua wazi kuwa tawba haimwondoi mtu kutokea hukumu. Lakini wanafiki hawajali kutenda madhambi na kila mara utawaona wakiomba tawba, na kwa hakika hii ndiyo dalili mojawapo ya unafiki wa kidhahiri kwa kuonyesha tawba kwa sababu ya kujionyesha tu ambapo kwa hakika undani mwake huwa hawana hofu yoyote ile kwa sababu ya kurejea kwa madhambi kila mara.

SOMO LA 8 7: MAISHA MAOVU KABISA

Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema:

Watu waovu kwa mtazamo wa maisha ni wale ambao hawawasaidii watu wengineo katika maisha yao, na wengine wasioishi katika maisha yao. 92

Maelezo mafupi: Uchumi bora ni ule ambao una imarisha uhusiano na mfunagamano wa kijamii kwa pamoja na kuwaunganisha wanajumuia wote. Pale apalipo na daraja mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya maslahi ya baadhi ya watu fulani tu, basi hiyo kwa hakika ni saratani ya kiuchumi na kamwe si dalili nzuri za uchumi mzuri. Kwa hakika Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema, kwa hakika haya ndiyo maisha maovu kabisa na ya kiuchumi.

SOMO LA 8 8: AHADI ZETU NDIZO MADENI YETU

Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema:

Sisi Ahlul Bayt (a.s) wa Wananyumba ya Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) tunachukulia ahadi zetu kuwa ni madeni yetu kama vile alivyokuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akifanya hivyo. 93

Maelezo mafupi: Deni si kitu tu anachopokea mtu kutokea kwa mtu mwingine na hivyo kuwa mdaiwa. Wale wanaowapa ahadi watu wengine, kwa hakika wanachukua jukumu la kazi na kukubalia wajibu basi kwa hakika huwa na wajibu wa kinidhamu. Kwa kutimiza ahadi kunadalilisha utukufu, imani, ukuu, uaminifu, ukweli na huimarisha misingi ya imani katika jamii na huisha moyo wa ushirikiano na kwa misingi hii, Dini ya Islam imesisitiza mno kutimizwa kwa ahadi.

SOMO LA 8 9: MALI HARAMU

Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

Wakati wowote pale mtu ajipatiapo mali kwa njia za haramu, basi 'Umra au Hajj yake haitakubalika kwa mapato yatokanayo na hayo, wala uwema wake. 94

Maelezo mafupi: Malengo matukufu haitoshelezi katika mantiki ya Kiislamu. Badala yake, njia za kujipatia vile vile huwa muhimu mno. Wale waliotosheka na kutenda matendo mema, lakini hawazingatii njia wanazozipitia katika kutenda mema hayo, wanakuwa wamepuuzia ukweli huu kuwa Allah swt hazikubalii mema yao yote hayo, hadi pale njia zao zitakapokuwa safi na takatifu. Kwani Allah swt daima hukubalia kutokea wachamungu halisi tu.

SOMO LA 90: USIMWOMBE MTU KITU CHOCHOTE

Al-Imam Zaynul 'Abidiin(a.s) amesema:

Ni udhalilisho wa mtu katika maisha yake kuomba kutokea watu na huteketeza heshima na kudhalilisha heshima ya mtu, na kwa hakika ni umasikini ambao mtu mwenyewe hujitafutia. 95

Maelezo mafupi: Baadhi ya watu hujiachia katika umasikini kwa kuchukulia kuwa wao wanaukwepa umasikini. Wao hujifanya wategemevu na wahitaji kwa kupitia mahitaji yasiyo ya lazima kutokea wengineo na hivyo ndivyo kujidhalilishia ubinadamu wao wenyewe. Dini ya Islam inawataka waumini wake wawe ni watu wa kujitosheleza na kujitegemea na hivyo waepukane na maisha ya kuwategemea wengine kwani kufanya hivyo ni udhalilisho mkubwa.

10

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 9 1: AMELAANIWA MTU KAMA HUYU!

Al-Imam Zaynul 'Abidiin(a.s) amesema:

Ole wake ! Yule anayezidiwa kwa mara kumi yake. 96

Maelezo mafupi: Qur'an Tukufu inatuambia kuwa Yeyote yule atendaye mema hulipwa mara kumi yake, lakini yule atendaye maovu ataadhibiwa kwa hayo tu.97 Tukitilia maanani Ayah hiyo ya Qur'an Tukufu basi tunaona kuwa Hadith hiyo ya juu inatuwia wazi kabisa. Mtu asiye na msaada ni yule ambaye anaacha maamrisho ya Allah swt ambayo yamejaa thawabu na hujishughulisha na kutenda madhambi.

SOMO LA 9 2: TUSISULUHISHE MATATIZO KWA DHAMBI!

Al-Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:Yeyote yule aombaye kutenda tendo lolote lile kwa maasi ya Allah swt, atapoteza chochote kile akiombacho, chochote kile akihofiacho, kitamfikia si muda mrefu. 98

Maelezo mafupi: Baadhi ya watu hudhania kuwa iwapo watachukua njia zisizo sahihi, basi matakwa na malengo yao yatakamilika kwa haraka. Hata hivyo, Hadith ya hapo juu inatuambia wazi wazi kuwa watu kama hao watapoteza hamu zao katika kipindi kifupi na punde watatumbukia katika mashimo ya majuto. Kwa mfano, yeye hujitakia raha katika mapato yake yasiyo halali ambapo kwa uhakika hupoteza raha kwa sababu ya hivyo na hatimaye hutumbkia katika shaka na majuto aliyokuwa akihofia.

SOMO LA 9 3: KUTOSHEKA MWENYEWE !

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Yeyote yule ambaye ameridhika kwa nafsi yake mwenyewe, basi wengi hawatakuwa wamefurahishwa nae. 99

Maelezo mafupi: Ingawaje kujipenda na kujijali kiasi fulani ni muhimu kwa ajili ya kuendelea kwa maisha, lakini iwapo itapita mipaka yake, basi itabadilika katika ubinafsi na kujifakharisha. Watu wenye kujifakharisha wenyewe kamwe hawaziangalii makosa yao wenyewe na kujichukulia wenyewe kuwa ni watu walio watukufu, safi, makini, wakakamavu, wema, wasio na hatia na muhimu katika jamii, na kwa sababu hizi, wao huwa na matumaini mengi kupita kiasi kutokea watu, na kwa hakika haya ndiyo yanayowaudhi watu hadi kuwaangusha chini waovu kama hao.

SOMO LA 9 4: NDUGU NA JAMAA WA KARIBU NA MBALI

Al-Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Jamaa wale walio karibu ni wale wanaopendwa zaidi, hata kama wanaweza kuwa wa mbali kijamaa, na jamaa wa mbali ni wale wanaopendwa kidogo, hata kama watakuwa ni jamaa wa karibu. 100

Maelezo mafupi: Uhusiano wa kijamaa ni mojawapo ya uhusiano muhimu kabisa wa kijamii katika Islam na kwa hakika hutengeneza makundi shupavu katika kitovu cha jamii kubwa ya wanaadamu ambao daima huwa na ushirikiano na mfungamano madhubuti miongoni mwao na watasaidiana na kushirikiana miongoni mwao katika kutatua matatizo hata yatakuwa magumu na sugu kiasi gani. Lakini kigezo cha uhusiano katika Dini ya Islam (kwa mujibu wa Hadith ya hapo juu) unaegemea juu ya mapenzi na urafiki, na wala si uhusiano wa kizazi peke yake.

SOMO LA 9 5: KUTUPILIA MBALI TABIA

Al-Imam Hasan al-Askari(a.s) amesema:

Kutupilia mbali tabia mbovu za mtu ni kama miujiza. 101

Maelezo mafupi: Tabia kwa hakika ni neema mojawapo ya baraka za Allah swt kwani husahilisha masuala mengi yaliyo magumu ya mwanadamu na huratibu kazi nyingi zilizo mushkeli na muhimu katika maisha ( kama kuongea, kutembea, n.k.). Lakini pale tabia inapotumika katika kazi mbaya, inabadilika katika tabia ovu kabisa kiasi kwamba kuiachia inakuwa vigumu mno hadi kwamba Al-Imam Hasan al-Askari a.s. ameilinganisha hivyo na muujiza.

SOMO LA 9 6: TUKIO LA KARBALA

Al-Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi kamwe sitaungana mkono pamoja nao kama mnyenyekevu, na wala sitatoroka kama mfungwa. Mimi ninachukulia mauti kama ni furaha, na maisha pasi na haki si kitu kingine isipokuwa ni sababu za lawama na maafa. 102

Maelezo mafupi: Karbala ni tukio kuu na la kudumu milele katika historia ya mwanadamu. 'Ashura ni Siku isiyosahaulika katika historia ya wanaadamu na mataifa ambayo yanataka kubakia kuheshimiwa, kuishi na kufa kwa heshima, na sentenso hizo mbili za hapo juu kutokea kwa Al-Imam Hussain ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. ndizo dalili mbili zilizo wazi na bayana kwa uhakika huu.

SOMO LA 9 7: JE NI NANI ALIYE MWENYE BUSARA ?

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. aliombwa kuelezea mtu mwenye busara. Alijibu:

Mtu mwenye busara ni yule anayeweka mambo yake sawa. 103

Maelezo mafupi Kwa hakika kuna imani na maoni mengi mno kuhusu busara, lakini sentenso fupi hiyo hapo ya juu kwa hakika ndiyo iliyo bora kabisa katika kuitafsiri kuhusiana na hilo. Kwa hakika busara si kitu kingine chochote kile isipokuwa kuweka kila kitu mahala pake palipo sahihi, kumweka kila mtu mahala pake na anapostahiki katika jamii na kuonyesha huzuni na furaha, urafiki na uadui, uwepesi na ukali, huruma na ghadhabu, 'ibada, kazi na kustarehe kiafya na kazi yoyote ile katika nafasi yake sahihi na wakati wake.

SOMO LA 9 8: SABABU ZA UADUI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Watu ni maadui wa mambo yale wasiyoyajua 104

Maelezo mafupi: Sisi tunawaona baadhi ya watu wakikanusha ukweli kwa wingi na kuwa dhidi ya hao wasemao ukweli bila hata ya kuwa na sababu isipokuwa ni ujahili na kutokufahamu. Kwa hakika hotuba hii ni yenye busara katika masuala ya Dini. Kwa hakika, iwapo baadhi ya watu, hata wale waliobobea katika fani mbalimbali za kisayansi, wanapinga na hudiriki nao katika kupinga, na wakati tunapochunguza, tunaona kuwa wao wanakuwa hawakujua kina na falsafa ya Dini na masuala yanayohusiana na Dini. Ama sivyo, wao kamwe wasingeliweza kuwakanusha na ukweli huu umekuwa ukitambuliwa kila mara.

SOMO LA 9 9: UHALISI

Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w) amesema:

Allah swt huwapenda waja wake wale walio halisi 105

Maelezo mafupi: Uhalisi kwa hakika unamaanisha kuinusuru Dini au utukufu au maji na ardhi na nchi ya Kiislamu na au neema za Allah swt. Mtu halisi ni yule ambaye amejitolea na anajichukulia yeye jukumu la kuyalinda na kuyahifadhi mambo haya na huchukizwa na kubughudhiwa kwa hujuma au maovu yoyote yanayofanywa katika masuala haya. Kwa hakika uhalisi ni sifa mojawapo za Mitume(a.s) na watu wa Allah swt. Sisi tumewahi kusoma kuhusu Mtume Ibrahim(a.s) , shupavu wa kuvunja masanamu, 'kwa hakika Ibrahim alikuwa shupavu.' Kwa kifupi, uhalisi ni kizuizi madhubuti dhidi ya hujuma za maadui.

SOMO LA 100 : MWENYE BARAKA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:Mumin ni sawa na mtende, chochote kile utakacho chukua kutokea kwake, ni chenye faida na manufaa. 106

Maelezo mafupi: Mtende kwa hakika ni mojawapo wa mti wenye rutuba. Matunda yake huliwa kama mojawapo ya vyakula bora kabisa. Mara nyingi mbegu zake huchomwa, na vile vile kutengenezwa kwa mikeka, majamvi, kofia na mambo mengi husukwa kwa manyasi na matawi yake. Magogo yake hutumika katika kujengea majumba ya kawaida na vile vile hutumika katika kupitia juu ya mito kama madaraja. Kutokea maua yake kunatengenezwa manukato. Kwa maneno mengine, hakuna sehemu yoyote ya mtende usio na kazi au ukatupwa.

Waumini wako vivyo hivyo. Mawazo yao yana manufaa makubwa, hotuba zao zinafaidisha, mikutano nao hutoa mafunzo, Dini yao huturekebisha nao huwa ni waaminifu katika urafiki wao, washupavu katika kutoa uamuzi na ndiyo maana tunasema kuwa kila kitu chao kinathamani kubwa mno.

11

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 101: MIKONO BORA KABISA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Zipo aina tatu za mikono : " Mikono yenye kuomba " Mikono inayoweka " Mikono yenye kheri (inayotoa) Na mikono iliyo bora kabisa ni ile ambayo yenye kheri (inayotoa). 107

Maelezo mafupi: Islam inawafundisha Wafuasi wake kuwa na ari na moyo mkubwa na jitihada na mapenzi makubwa na hivyo inawasisitizia wafuasi wake kutokuomba kitu chochote kutokea mtu yeyote kwa kujizuia kiasi kiwezekanacho, na kamwe wasimwombe mtu yeyote, na si hayo tu kuwa wasiwaombe watu kitu chochote tu bali wawe wakijitosheleza kwa kile walichonacho. Kwa hakika, inawapasa wao wawe na moyo wa kuwagawia na kuwasaidia wengineo kwa neema waliyonayo kwa kiasi wawezacho, na kwa misingi hii, ndipo sisi unasoma katika Hadith hiyo ya hapo juu, kuwa mikono iliyo bora ni ile inayotoa!.

SOMO LA 102: OVU HATA KULIKO MAUTI

Al-Imam Hasan al-Askari(a.s.) amesema:

" Nini kilicho bora kuliko maisha, ni kile utakachokichukia pale utakapokipoteza ! " Na mbaya kabisa kuliko mauti ni pale wewe uatakapoikaribisha mauti pale itakapokuijia wewe. 108

Maelezo mafupi: Baadhi ya watu wanadhania kuwa kile kilicho bora kabisa ni mambo yaliyo ya humu duniani ambapo kwa hakika kuna mambo mengi mno yaliyo yenye thamani zaidi kuliko hayo. Zipo baadhi ya nyakati ambapo mwanadamu huomba kifo, na yapo ukweli ambapo yeye kwa hakika hujitolea mhanga katika kuridhika kwa kutosheleza. Mashahidi katika njia ya haki ya Allah swt, na kujitolea kwa uadilifu, ni wale ambao kwa hakika wameelewa maana halisi ya kauli hiyo ya Al-Imam Hasan al-Askari a.s., na wao walipoona maisha ya dunia hii kuwa hayana furaha na mauti kama ni dirisha kwa dunia iliyo kubwa na pana, a vile vile ridhaa ya Allah swt , wao waliiaga maisha na kuikubalia mauti.

SOMO LA 103: UTAMBULISHO BAINA YA MUMINI NA MNAFIKI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Utakapomwona Mumin yu mkimya, umwendee kwani utapata kusikia mambo ya hekima. Mumin ni mtu wa maneno machache lakini mwenye matendo mengi ambapo wanafiki ni wazungumzaji wa maneno mengi na wasio na uzoefu (wasiojua). 109

Maelezo mafupi: Uwezo wa mwanadamu haujawekewa mipaka wala vikomo. Hivyo inamaanisha kuwa iwapo nguvu zake zitakapokuwa zimeelekezwa upande mmoja tu basi kutatokea kasoro upande mwingineo. Hivyo ni dhahiri kuwa wapiga gumzo na porojo huwa hawana uzoefu na huwa si watu wenye kutenda matendo. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambaye kwa hakika ni kigezo katika kila jambo na kila mahala, huchukulia jitihada kwa tendo lolote kama ndiyo dalili ya waumini kuliko maneno matupu, ambapo yeye huchukulia kinyume na hayo kwa ajili ya Wanafiki (ambao hupiga midomo tu bila ya matendo).

SOMO LA 104: URITHI BORA KABISA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Urithi ulio bora kabisa ambao mzazi anawaachia watoto wake ni adabu njema. 110

Maelezo mafupi: Tabia na adabu njema ni jambo lililo bora na uhusiano unohusiana na heshima na adabu. Tabia njema mara nyingine huwa ni mbele ya waja wa Allah swt na mara nyingine huwa ni mbele ya Allah swt. Katika sura zote, kwa hakika ni mojawapo ya hazina kubwa ya kibinadamu kama ndiyo ufunguo wa maendeleo katika nyanja zote. Na kwa misingi hii ndiyo maana Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ameitaja adabu njema kuwa ni urithi mkubwa mno ambao mzazi humwachia mtoto wake. Adabu njema ni chanzo cha mapenzi, uaminifu, urafiki, na muungano na jambo lililo muhimu mno kwa ajili ya kuathiri kwa kauli na maendeleo katika mikakati na mipango ya kijamii.

SOMO LA 105: KUHESHIMU UHURU WA FIKARA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Mumin anapaswa kufanya Taqiyyah miongoni mwa watu waovu. 111

Maelezo mafupi: Kufanya Taqiyya na kuficha mawazo na fikara unatokea kwa kawaida wakati wengi wa watu katika jamii wanapokuwa na ubinafsi na hususan pale wanapowazuia watu walio katika haki katika kuelezea mawazo na maoni yao na kushirikisha mawazo yao. Kwa hakika jamii kama hiyo haitaendelea. Katika jamii ya Kiislamu na kibinadamu, watu walio katika haki ni kwa lazima wawe na haki ya kushirikisha maoni na mawazo yao katika maoini ya jamii kwa ujumla, watu wa kawaida wasiwabughudhi wala kuwazuia, na badala yake waheshimu uhuru wa kufikiriwa na kuchangia katika kutengeneza na kuboresha masuala na kutoa nafasi ya kufundishia na kuyafanya mawazo kama hayo yaweze kuzaa matunda.

SOMO LA 106: SIFA 6 ZISIZO NDANI MWA MUMIN

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Yapo mambo sita ambayo hayapatikani ndani mwa Waumini:

" Ushurutisho

" Mwepesi wa Hasira za ghafla

" Husuda

" Ukaidi

" Uwongo

" Asiye mwadilifu

Maelezo mafupi: Wale ambao wanakuwa wametosheka kwa jina la imani, si uhakika na kwa hakika si Waumin wa kweli. Kwa hakika sifa zote hizo za juu zinahusiana na uhusiano na mfungamano na wanadamu miongoni mwao na masuala ya kijamii. Waumini wa kweli ni wale wanaokwenda bila matatizo, wenye tabia njema, wenye huruma, wakijisalimisha mbele ya ukweli, waaminifu, na kwa hakika kulichagua jina hili takatifu bila ya kuwa na sifa hizi kwa hakika ni kosa lililo kubwa na jambo lisilo sahihi !

SOMO LA 107: USIVUNJE UHUSIANO WOTE

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Muwe watu wenye Taqwa hata kama itakuwa ni kwa kiasi kidogo, na muidumishe mipaka baina yako na Allah swt, hata kama utakuwa mwembamba kiasi gani. 112

Maelezo mafupi: Wapo baadhi ya watu ambao huvunja uhusiano wote pamoja na wenzao na Allah swt wakati wanapokuwa wakisonga mbele katika njia ya maasi na makosa, na huteketeza madaraja yote nyuma yao na kujifungia milango yote ya kurejea. Al-Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. katika hotuba yake anasisitiza kuwa mtu asijifungie yeye mwenyewe njia za kufanya Tawba, na hivyo asizichane pazia zote ambapo atahitaji kufanya tawba, asije akakosa.

SOMO LA 108: IBADA SAHIHI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) alimwambia Kumail ibn Ziyad:

Ewe Kumail! Si muhimu kusali, kufunga saumu na kulipa sadaqa. Kile kilicho muhimu ni kuwa Sala yako (na matendo mengineyo) yawe yamefanywa mbele ya Allah swt kwa moyo msafi na ikiambatana pamoja na unyenyekevu kamili. 113

Maelezo mafupi: Hali halisi ya matendo na vile vile njia yake na ubora wake ndio unaoelezea thamani yake ya kweli, na wala si kuonekana kwake au idadi yake. Kama vile Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. anavyomsisitiza Kumail Ibn Ziyad kuwa inambidi mtu azingatie kiini cha tendo badala ya kuonekana kwake au kuangalia idadi yake, kwani malengo ya matendo haya mema ni mafunzo kwa mwanadamu, maendeleo na uimarishaji, na kwa hakika hutegemea uhalisi na wala si kiasi au idadi yake.

SOMO LA 109: USILISAHAU KOSA LAKO

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:Utakapomwona mtu anajishughulisha katika kutafuta madhambi ya watu na kubishana nao bila kisa, akisahau madhambi yake mwenyewe, basi ujue kuwa mtu huyo yupo katika adhabu za Allah swt 114

Maelezo mafupi: Wapo watu wengi walio fedhuli na wajeuri kwa vikali na stadi katika kuwalaumu wengineo ambapo wao hawajui hali zao wenyewe, na kama ulivyo msemo mashuhuri, wao wanauona mwiba miguuni mwa wengineo, ambapo hawalioni tawi machoni mwao wenyewe ! Kwa hakika, pazia za maovu na kutokujua zimefunika macho ya watu kama hao kwa sababu ya kuzama katika madhambi na maasi, kujiona na ubinafsi, nao wapo wanazurura huku na huko katika njia potofu. Kwa hakika amefuzu yule mtu ambaye amekataa kabisa chochote kile kinachomzozanisha pamoja na wengineo.

SOMO LA 110: ADHABU KUBWA

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:Mtu aliye na tabia mbaya basi anajiadhibu mwenyewe. 115

Maelezo mafupi: Kwa kawaida inasemwa kuwa mtu mwenye tabia mbaya ambao ni wepesi kuwakasirikia watu, huwabughudhi na kuwaumiza marafiki na ndugu na jamaa zao, ambako kwa hakika wao wenyewe hujiadhibu zaidi kwa sababu wao huufanya utamu wa maisha kuwa machungu na hujiharibia maji safi kwa ajili yao wenyewe. Watu wenye tabia mbaya huishi maisha mafupi na moyo usiotulia, mwili wao huwa katika maumivu, na kwa hakika huhangaika na kutaabika zaidi ya watu wengine wote. Tabia njema ni jambo mojawapo ambalo Dini ya Islam inawataka Waumini wake kwayo kwa msisitizo mkubwa na imeliita kuwa ni suala mojawapo lililo muhimu katika kujipatia Jannat inayodumu milele.