MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA 60%

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA Mwandishi:
: AMIRALY M.H.DATOO
Kundi: Vitabu mbali mbali

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA
  • Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 17025 / Pakua: 3232
Kiwango Kiwango Kiwango
MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

Mwandishi:
Swahili

12

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 111: QURAN TUKUFU NI YA KILA ZAMA

Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema:

Allah swt hakuifanya Qur'an Tukufu kuwa kwa ajili ya zama fulani tu, wala si kwa ajili ya taifa fulani, hivyo daima huwa ni mpya na kwa ajili ya kila taifa ulimwenguni humu hadi siku ya Qiyama. 116

Maelezo mafupi: Al-Imam 'Ali ar-ridha a.s. alimjibu mtu mmoja ambaye alitaka kujua ni kwa nini Qur'an Tukufu haizeeki kwa kusomwa kila mara au kuchapwa ? Katika kusema huku kwa Al- Imam 'Ali ar-ridha a.s. amezungumzia kwa maana kamilifu kwa uhakika huu kuwa Qur'an Tukufu haikuumbwa na vitu vya dunia hii au haikutengenezwa na mwanadamu ambaye mwenyewe ataangamia na kuisha pamoja na mawazo yake yanayokaa yakibadilika. Hivyo vumbi hilo la kuzeeka haufuniki Qur'an Tukufu kwa kupita muda. Kwa hakika Qur'an Tukufu imetokea kutokana na sayansi na elimu ya Allah swt, ambaye kuwapo kwake kumekuwapo tangia mwanzoni na utakuwepo milele. Kila itakavyosomwa zaidi, ndivyo hivyo itakavyokuwa mpya na yenye kuvutia, na kwa hakika huu ndio mojawapo wa muujiza wa Qur'an Tukufu.

SOMO LA 112: JITAHADHARISHE NA MATAMANIO

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Ole wako kwa matamanio ya nafsi yako kama vile unavyojihadhari na maadui zako kwa sababu hakuna adui wako mkubwa kuliko matamanio yako na yale yanayotokana na ndimi zao. 117

Maelezo mafupi: Bila shaka maadui wa ndani ni hatari zaidi kuliko maadui wa nje. Kwa hivyo, matamanio ambayo humwathiri mwanadamu kwa undani, kwani huchukuliwa ni adui hatari kabisa wa mwanadamu. Upofu wa matamanio humfanya mtu akawa kiziwi na kipofu wa macho. Huondoa nuru ya busara, hugeuza nyuso za ukweli na hatimaye humwongoza katika maovu.

SOMO LA 113: NJIA MOJA TU YA KUWA SHI'A

Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) alimwambia to jaber jofi:

Wafikishie salaam zangu kwa Mashi'a wetu na uwaambie kuwa wao hawatakuwa na uhusiano pamoja nasi na Allah swt ambapo njia moja tu iliyopo ni ya kujisalimisha kwa amri za Allah swt. 118

Maelezo mafupi: Kwa hakika wapo watu wengi ambao wanadai kuwa wao ni Mashi'a na mapenzi yao pamoja na Ahlul Bayt a.s. ndiyo yanayotosheleza kwa ajili ya uokovu wao Siku ya Qiyamah. Ati kwa kudhania kwao hivyo, wao wataingizwa katika ndugu na jamaa za Ahlul Bayt a.s., na kwamba watakuwa na uhusiano maalumu pamja na Allah swt, na hivyo kila kitu chao kitakuwa sawasawa kwa kuomba kwao. Kwa hakika uhusiano wa mwanadamu na Allah swt ni ule tu unaotokana na utiifu na kutimiza wajibu wake mtu. Yeyote yule anayejisalimisha mbele ya amri za Allah swt ndiye mtu wa karibu kabisa, na kwa hakika yeyote yule asiyemtii Allah swt kwa hakika amejiweka mbali mno na Allah swt, yeyote yule awaye.

SOMO LA 114: UHUSIANO WA MALI NA MATUMIZI!

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Yeyote yule anayechuma mali kwa njia ya haraam, ataitumia kwa njia ambayo haina baraka za Allah swt. 119

Maelezo mafupi: Inaaminiwa kwa kawaida kuwa si kila mali au milki inayopaswa kutumiwa kwa ajili ya wema wa jamii au njia nzuri na zilizo bora. Kwa hakika Hadith ya hapo juu ni uthibitisho mzuri kwa imani hii ya kawaida. Ni ukweli ulioonekana kwamba baadhi ya watu wamenuia kushiriki katika jambo jema kwa kutumia mali na milki yao, lakini ama wamesitisha wakiwa wamefikia katikati, au iwapo watakuwa wamekamilisha basi juhudi zao hizo hazitakuwa na ufanisi wa kutosha au itaonekana yenye matokeo yaliyogeuka. Kwa hakika wapo watu wengi mno ambao watoa huduma kubwa mno kwa moyo msafi na kwa mitaji yao midogo.

SOMO LA 115: MKWELI KABISA NA MWENYE BUSARA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Kila Ummah unao mtu aliye mkweli na mbainifu, na hivyo mkweli na mbainifu wa Ummah wangu ni Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib (a.s) 120

Maelezo mafupi: Kwa ajili yakutaka kukamilisha Dini halisi, Dini ya kudumu milele kama Islam, basi kunatakiwa kuwepo na mtu ambaye ni mzoefu na mwenye kujua masuala yote na undani wa Dini hiyo ili aweze kubainisha tofauti iliyopo baina ya ukweli na uwongo ( mstahikiwa jina la mbainishaji) baada ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., sehemu kubwa ya Misheni yake ilipita katika magomvi mbalimbali pamoja na maadui wake. Inabidi yeye awe mkweli, mwaminifu, msemaji bora na msema ukweli ili aweze kuondoa kero zozote zinazowakera watu baada ya kiongozi wa kwanza. Kwa hakika wadhifa huu, kama ilivyo bayana hapo juu, ulikuwa umepewa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) tu.

SOMO LA 116: MAISHA NA KUENDESHA NYUMBA

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa akikusanya na kuzichana kuni (kwa ajili ya nyumbani kwake) kutokea jangwani na kuchota maji na kufanya usafi kwa kufagia, na Bi. Fatimah az-Zahra a.s. alitayarisha unga na alikanda unga na kupika mikate. 121

Maelezo mafupi: Ukuu na utukufu wa ulimwengu mzima wa moyo na daraja kuu umefichika katika Hadith hii fupi kwa kuhusiana na Kiongozi Adhimu wa Islam, Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) na mfano mkubwa wa wanawake, Bi.Fatimah az-Zahra(a.s) kwani maisha yao kwa hakika yalikuwa ya kawaida na yenye kujaa uaminifu, uhalisi, kusaidiana na kushirikiana. Kufanya kazi haikuwa kudhalilika, na ushirikiano na kuelewana yalikuwa yakichukuliwa kuwa ni kipaumbele ya kimsingi, na kisichopendeza kulichukuliwa kama ndicho kipa umbele. Kwa hakika masuala haya hayapatikani tena majumbani mwetu na matokeo yake ni kwamba udugu na amani na mapenzi ndiyo maana yametoweka.

SOMO LA 117: SAA NZIMA YA UADILIFU

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Saa moja ya uadilifu ni bora kuliko ibada ya mwaka mzima. 122

Maelezo mafupi: 'Ibada ni uhusianao sawa wa viumbe pamoja na Muumba wao na 'uwezekano' pamoja na lazima na kuzingatia kwa uhusiano na muungano huu. Kwa hakika 'Ibada hizo ndizo zilizo mafunzo muhimu ambazo kwa hakika yanaathiri mno katika kurekebisha nafsi na akili ya mtu. Hata hivyo, sisi tunasoma katika Hadith hiyo hapo juu kuwa saa moja ya uadilifu ni bora na afadhali kuliko 'Ibada ya Sunnah ya mwaka mzima.

Na mahala pengine tunasoma kuwa saa moja ipitishwayo katika kufikiria na kutafakari, basi ni bora kuliko usiku mmoja ( au mwaka mmoja) upitishwao katika 'Ibada. Kwa hakika maneno haya yanaonyesha muhimu wa uadilifu ulivyo na fikara, kwani yote yana asili sawa. Popote pale ambapo hapatakuwa na uadilifu, basi hakutakuwa na ufikiriaji sahihi na busara.

SOMO LA 118: MGANGA WA KWELI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Kwa hakika mgamnga halisi ni Allah swt, na vitu ambavyo vikufaavyo vinaweza kuwa vyenye kumdhuru mtu mwingine. 123

Maelezo mafupi: Matukio yanayotokea katika maisha ya mwanadamu kwa mara nyingi hutokana na sera zake mbaya, uchaguaji au moyo wake na kwa hakika yapo matukio mengi mno kama haya yanayoumiza. Lakini mara nyingine matukio yasiyo mazuri hutokea si kwa kutokana na sababu hizo za juu, lakini kwa hakika hutokana na amri za Allah swt kama ndizo dawa kwa ajili ya waja wake. Dawa hizo mara nyingi huwa ni chungu, lakini huwa ni kama kengele ya kumwamsha na kumzindua mwanadamu, au kumtanabahisha juu ya udhaifu wake na au kuondoa kiburi na upotofu wake.

SOMO LA 119: MAKHALIFA WA MTUME S.A.W.W.

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Dini hii ya Allah swt daima itaheshimiwa na kuhifadhiwa kutokea maadui hadi hapo Makhalifa kumi na wawili (12) watakapoiongoza, na wote watatokana na Maqureish. 124

Maelezo mafupi: Hadith na Riwaya zilizo wazi na kujieleza zenyewe zimetolewa katika kuzungumzia Makhalifa 12 halisi wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) katika vitabu vinavyoheshimiwa na kuaminiwa katika Ahl as-Sunnah kama vile Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Sahih Tirmidhi, Sahih Abu Dawud, Masud Ahmad na vitabu vingi vinginevyo, na jumla ya Hadith hizi zilizotolewa na Mashi'a na Masunni zinafikia idadi ya Ahadith 271! Ni jambo la kuvutia kuwa Ahadith hizo hazikubaliani na hata mmojawapo wa Waislamu waliongoza au kutawala baada ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) isipokuwa Maimamu 12 wa Mashi'a tu kwani makhalifa 4 wa kwanza, au wa-Bani Umayyah or Bani 'Abbas si wanaozungumziwa katika Hadith hii.

Kwa hivyo Masunni wameingia katika hali ngumu ya kutafsiri Hadith hii iliyo sahihi lakini kwa hakika tafsiri ya Hadith hii ipo wazi kabisa katika Ushi'a wa Ahlul bayt a.s. ya wananyumba wa Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w)

SOMO LA 120: FURAHA YENEY MADHAMBI

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Si haki kwa Waumini kushiriki katika hafla na sherehe ambamo kunatendwa maasi ambayo wao hawawezi kuzibadilisha. 125

Maelezo mafupi: Kushiriki katika karamu au sherehe zenye madhambi ni dhambi lenyewe, ingawaje mtu mwenyewe hatendi dhambi wala kushirikiana na washiriki katika karamu au sherehe hiyo. Kwa sababu kushiriki katika karamu au sherehe kama hizo kunachukuliwa ni kusaini dhambi, isipokuwa tu iwapo hatima ya mtu itakuwa ni kubadilisha hali hiyo na kutekeleza jukumu gumu kabisa la kuhubiri uwema na kukataza ubaya na maovu. Zaidi ya hayo, kujishughulisha na hali za madhambi, wakati kuwa tofauti na wao, kunaitia kiza nafsi ya mtu na kupunguza hali ya kujiepusha na madhambi na kumfanya mtu kuzoea madhambi.

13

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 121: UFANYE KAZI ZINAZOZALISHA

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Lima na panda mti. Kwa kiapo cha Allah swt , watu hawajafanya tendo lolote lililo halisi zaidi ya hili. 126

Maelezo mafupi: Maisha ya mwanadamu yapo juu ya kazi zinazo zalisha, ikiwemo kilimo, na biashara mbalimbali, na hata wingi wa viwanda havitakuwa na maana bila ya kilimo kwani kwayo hujipatia mali ghafi. Kwa kuongezea, uovu na uzushi hauwezekani katika kilimo kama vile ilivyo kawaida katika mambo mengine. Kwani misingi yake ipo ni kawaida na kwa hakika faida yake ni kwa kutokana na jitihada za mtu. Kwa misingi hii, kilimo na upandaji wa miti kumeitwa kuwa ni kazi njema na halisi katika Hadith ya hapo juu.

SOMO LA 122: UREFU NA UFUPI WA MAISHA

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Kifo kinamwijia mtu mapema kuliko kawaida kwa kutokana na madhambi, na urefu wa maisha unatokana na uchamungu wake zaidi ya maisha ya kawaida. 127

Maelezo mafupi: Hakuna shaka kuwa wingi wa madhambi na tabia mbaya zinafupisha maisha moja kwa moja ( kama vile kulewa, kamari, husuda, wivu na shari na kutaka kulipiza kisasi) na nyingi zinafupisha maisha vinginevyo kwa kuathiri mivurugano ya kijamii na kuondoa amani na usalama wa kijamii na kuzuka kwa vita na mapigano ( kama vile riba, dhuluma na ukandamizaji).

Kwa upande wa pili, uchamungu ndio unaweza kuwa ndiyo sababu ya kurefuka kwa umri mrefu kwa kutokana na athari za utulivu wa nafsi na nyoyo na dhamira. Hivyo, madhambi, kutokujali athari zake mbaya, ni kichocheo kikubwa katika kufupisha maisha ya mwanadamu, ambapo kwa hakika uchamungu ni sababu kubwa katika kurefusha maisha pamoja mema yake yote.

SOMO LA 123: URAFIKI NA SHETANI!

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Usimlaani Shetani kidhahiri, wakati wewe ni rafiki yake kwa undani mwako. 128

Maelezo mafupi: Baadhi ya watu wanijiepusha na kuogopa kutokea maneno, maneno ya umasikini, unafiki, sheitani na kama hayo, wakati ambapo kimatendo wao wanakuwa wametumbukia ndani mwao. Sisi tunawajua baadhi ya matajiri ambao huishi maisha ya kimasikini kwa kuhofia umasikini. Sisi vile vile tunawajua wanafiki ambao kwa kurudia huwalaani wanafiki, lakini kwa hakika maisha yao yanakuwa yamejaa kwa unafiki.

Sisi vie vile tunawajua watu waovu ambao kwa udhahiri kabisa wanajiingiza katika kujinusuru kwa Allah swt dhidi ya Shetani, kwa maneno yao ya ulimini, lakini wao ni marafiki wa Shetani kwa undani mwao na hutilia mkazo na usisitizo juu ya mipango ya kishetani. Kwa hakika wao ni maadui kwa maneno na wala si kwa wa kweli kwa hisia au ukweli.

SOMO LA 124: POKEA USHAURI ILI UONGOZWE !

Al-Imam Hasan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Hakuna mataifa yanayoshauriana miongoni mwao hadi pale wanapokuwa wameongozwa kwa mema na faida zao. 129

Maelezo mafupi: Kwa umoja daima imeilipa jamii neema, maendeleo na uboreshaji wao, hususan katika masuala ya kiakili na mipango ya maendeleo na utatuaji wa matatizo yao, kwa hakika kutekelezeka ushauriano na majadiliano kwa kimaajabu. Wale ambao wamezoea kujitolea mawazo yao wenyewe na kujitenga, mara nyingi kudhurika kwa makosa na hasara. Akili yoyote inayo mchocheo ambao haupo katika akili nyingineyo. Wakati vichocheo hivi vinapokutana na nyenzao, basi kutatokea mwanga ambao utang'arisha kiza wowote utakao kuwapo. Inatubidi sisi sote tuamue kuwa tutashauriana pamoja na watu walioelimika na wale walio makini.

SOMO LA 125: SALAAM, KUSALIMIANA KIISLAMU

Al-Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Salaam (kusalimiana) zina thawabu 70, sehemu 69 za Salamu hiyo ni kwa ajili ya yule anayetoa Salaam na sehemu moja ni kwa ajili ya yule anayejibu Salaam hiyo. 130

Maelezo mafupi: Miongoni mwa kusalimiana katika mataifa ya ulimwenguni, Salaam, usalimio wa Kiislamu na kuamkiana, kwa hakika unao nuru ya ajabu, kwa sababu hiyo inamaanisha ukaribisho na amani, furaha na urafiki, na vile vile Dua ya amani na usalama na kheri kutokea Allah swt kwa mtu anayesalimiwa. Kwa sababu hizi, maamkizi ya wakazi wa Jannat ni Salaam, na Malaika wa Rahma huwapokea wachamungu na watendao mema kwa Salaam. Lakini kwa bahati mbaya, baadhi ya Waislamu wanaikataa amri hii ya Dini ya Islam kwa kujifakharisha kuwa kwa kutokusalimiana ndiko kunakoonyesha heshima zao na kwa kusalimiana hivyo kunawadhalilisha wao na kwa hakika wao ndio wenye hasara ya kukosa baraka, amani na Dua iliyopo katika Salaam kwa mujibu wa hadith hiyo ya hapo juu !

SOMO LA 126: KUTOKUKUBALIANA KWA IMANI NA MATENDO

Al-Imam Zainul 'Abidiin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Wale watu wanaochukiwa na Allah swt ni wale ambao wameukubalia uongozi wa Imamu, lakini hawafuati matendo yake. 131

Maelezo mafupi: Mojawapo ya makosa makuu ya mwanadamu ni kutokukubaliana kwa imani yake pamoja na matendo yake. Yeye huamini kitu kingine, lakini hakuna ufuatio wa imani yake hiyo unaopatikana katika matendo yake. Yeye huamini katika Allah swt, lakini hukana katika matendo yake. Yeye huamini katika Mahakama Kuu ya Allah swt, lakini haonyeshi kujitayarisha kwayo. Yeye huamini kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Mtume Mkuu na kwamba Al- Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) kuwa ni kiongozi Mkuu, lakini utaona hawana sifa yoyote katika matendo yake yoyote. Hivyo tunasema kuwa matendo yake yapo upande mmoja na matendo yake yapo upande wa pili

SOMO LA 127: ADHABU ZA ALLAH SWT !

Al-Imam Muhammad al-Baqir(a.s) amesema:

Allah swt ameweka adhabu (kwa ajili ya madhambi na uasi) katika nyoyo na miili: 132 " Umasikini katika kipato " Uvivu katika 'Ibada Lakini Allah swt hajamwadhibu mja wake yeyote yule aliye na kitu kiovu kuliko moyo mgumu."

Maelezo mafupi: Adhabu za Allah swt kwa hakika ni matokeo ya matendo na matokeo ya madhambi ya mwanadamu mwenyewe. Kwa hakika baadhi ya nyakati hatima hizi mbaya huonekana kama nyakati mbaya katika maisha ya kidunia na nyakati zinginezo kama kunyimwa uhalisi katika 'Ibada na Dua pamoja na Muumba wetu. Lakini jambo lililo la muhimu na hatari kabisa ni kule kwa mwanadamu kudhihirisha maasi na makosa na matendo maovu kabisa kwa nyonyo ngumu na ukatili wa mwanadamu, kuondokana kutokea moyo wa mwandamu kwa hisia za kibinadamu na ukarimu, mapenzi na huruma, na kwa hakika moyo wa mwanadamu unaweza kuwa ndio chanzo kikuu cha madhambi na maasi mengi mno.

SOMO LA 128: UHAKIKA ULIO SAHAULIKA

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Allah swt ameumba yakini bila shaka kama mauti, lakini inaonekana kuwa shaka ndimo kamwe hakuna yakini. 133

Maelezo mafupi: Kwa hakika msemo huo ni wa kustaajabisha, na tafsiri bayana ya kutokujua kwa mwanadamu kuhusu hatima ya maisha na mauti. Mtu anaweza kusita katika kitu chochote kile na asiamini katika dini yoyote, lakini hasiti kwa kukiri kuwa maisha yatafikia mwisho wake tu na kuisha. Lakini yeye anaonekana hajui katika suala hili kama kwamba hakutakuwa na kifo ambacho ndicho kitakacho malizia maisha yake ! Hivyo, yeye hajitayarishi kwa kuikaribisha mauti na mwisho wake kwa imani, matendo mema, uhalisi na uchamungu. Hata hivyo, inatubidi sisi kwa lazima tuwe watu wenye uhakika na uhalisi katika kila hali na umri ili tusije tukajuta na kuaibika wakati wowote pale maisha yetu yatakapo malizika.

SOMO LA 129: NAFASI YA ELIMU NA BUSARA

Al-Imam Musa al-Kadhim(a.s) amesema:

Uoteshaji unakuwa katika ardhi laini, na wala si juu ya majiwe ! Na vile vile elimu na busra vinachomoza katika nyoyo za wachamungu, na kamwe si katika nyoyo za wadhalimu. 134

Maelezo mafupi: Hatua ya kwanza katika kutafuta elimu ni unyenyekevu, unyenyekevu kuelekea ukweli, unyenyekevu kuelekea mwalimu, na mtu yeyote anayejua zaidi kuliko sisi, na ambaye anaweza kutufundisha chochote. Kwa sababu hizi, ujahili na kiburi na ufidhuli yanakuwa yameambatana pamoja. Mfedhuli na mjauri kamwe hawezi kukubali kukiri kwa ujinga, na hata kama iwapo ukweli hautakuwa kwa mujibu wa nafsi yake ya kiburi na ufedhuli, si kwamba ati kuwa wao hukanusha hayo, bali hupinga pia. Wao hawakubali ukweli kutokea wale walio chini yao na mara nyingi hubakia kuwa wapumbavu kwa ukamilifu.

SOMO LA 130: MAJUKUMU MAZITO YA IMAM

Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema:

Imam ni Mwakilishi wa Allah swt juu ya ardhi hii na miongoni mwa waja wa Allah swt, na ni ushahidi kwa waja wake na mwenye kuwalingania watu kwake na mwenye mlinzi wa mipaka ya Allah swt dhidi ya yale yaliyoharamishwa. 135

Maelezo mafupi: Katika Hadith hii, ambayo ni sehemu ya Hadith ndefu katika kuzungumzia nafasi ya Uimamu, inazungumzia sehemu tano zilizo nzito za majukumu ya Imam(a.s)

1- Imam(a.s) ni mweka hazina na wakala wa Ufunuo na mhifadhi wa sayanzi zote, maamrisho na elimu za Dini.

2- Imam(a.s) ni sababu iliyohai na udhihirisho na mtambulishaji na mwendelezaji wa Dini ya Islam

3- Imam(a.s) ni mwakilishi mtakatifu wa Allah swt na mamlaka yake miongoni mwa watu

4- Imam(a.s) , hualika katika mema na kuzuia mabaya na ni Mjumbe mkuu wa Dini

5- Imam(a.s) ni mhifadhi wa mipaka ya Dini ya Islam dhidi ya uvamizi wa maadui wake. Na mtu kma huyo ndiye awenayo elimu ya Allah swt na daraja la utoharifu na hakuna mtu yeyote mwingine anayeweza kuwachagua hao Maimamu(a.s) isipokuwa ni Allah swt tu.

14

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 131: MILANGO ILIYOFUNGWA ITAFUNGULIWA

Al-Imam Muhammad at-Taqi(a.s) amesema:

Iwapo milango ya Jannat na ardhini zimefungwa kwa ajili ya mtu, na achaguapo uchamungu, Allah swt atamtoa humo. 136

Maelezo mafupi: Baadhi ya nyakati katika maisha, milango yote huwa inafungwa kwa ajili ya mwanadamu na popote pale anapogeukia, hukumbana na matatizo na magumu. Kwa hakika matukio kama hayo ni majukumu kwa ajili ya kumwamsha mwanadamu na kumfanya arejee kwa Allah swt, urejeo ulio sahihi na kubadilisha maisha na bahati yake. Wakati huu, iwapo yeye atajipatia usisitizo unaostahili kwa moyo wake wote, na kuomba msaada kutokea Allah swt, basi hakuna shaka kuwa msaada huo ataupata kutokea kwa Allah swt na upepo murua za baraka na rehema za Allah swt zitamkumba yeye na kwa hakika utakua ni muujiza mkubwa kwani milango yote iliyokuwa imefungwa itafunguka !

SOMO LA 132: JITAHADHARISHE NA WAOVU!

Al-Imam Muhammad at-Taqi (a.s) amesema:

Jitahadharishe na ugonjwa wa mtu yule ambaye hajistahi mwenyewe! 137

Maelezo mafupi: Kwa hakika, mojawapo ya hoja muhimu katika kuzuia ufisadi na uovu ni heshima au kuwa na hisia za heshima. Watu walioheshimika au wale wanaochukua heshima kwa ajili yao wenyewe, ingawaje wao inawezekana wasihesabike miongoni mwa walioheshimika katika mtazamo wa kijamii, wanajiepusha na mengi ya maovu na matendo mabaya kwa ajili ya kujitunzia nafasi yao. Lakini pale wao wanapohisi kuwa hawana heshima yoyote, jina au , basi wao hawatajali chochote. Hivyo Imam a.s. ametuonya tujitahadharishe na watu kama hao ! Na kwa misingi hiyo, mojawapo ya jambo lililo muhimu ni kuwaelimisha watoto au watu kwa ujumla ni kutengeneza heshima ndani mwao ili wao wawe na hisia ya kuwa na heshima maalum. Ama kwa upande mwingine, kinyume na hayo, kuwapunguzia watu heshima kwa hakika inayo athari mbaya kwa mtazamo wa kielimu na kuelimishana.

SOMO LA 133: VITA VIKUU

Al-Imam Hasan al-Askari(a.s) amesema:

Mtu aliye shupavu kabisa ni yule ambaye anaacha madhambi. 138

Maelezo mafupi: Sisi tunajua kuwa harakati dhidi ya matamanio ya maasi na za nafsi ndizo chanzo kikuu cha madhambi na inaitwa 'vita vikuu' katika Dini ya Islam, ikiwa kwa hakika harakati na vita vikali na vigumu hata kuzidi vita dhidi ya maadui. Kwa sababu vita hivi ni kwa ajili ya kujitakasisha kwa nafsi na hakutakuwa na ushindi wowote kwani kushindwa hutokea mara nyingi kwa sababu ya mipango na mikakati dhaifu. Katika jamii ambazo zilizojaa kwa madhambi, thamani ya vita hivi vinakuwa lazima na umuhimu wake katika kuboresha malengo na matakwa yake ya kijamii huwa yako wazi. Ushindi wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika mji mtukufu wa Madinah kwa hakika ulikuwa ndio uhitimisho wa utakasishaji wa nafsi na nyoyo, na harakati tukufu za Masahaba wake katika mji mtukufu wa Makkah.

SOMO LA 134: GHAIBU IMAM MUHAMMAD MAHDI A.S.

Al-Imam Muhammad Mahdi Sahib az-Zamaan(a.s)

amesema:

Katika matukio mengi yatakakayotokea katika kipindi hiki cha kuwa- ghaibu, rejea kwa wanaohadithia Hadith na Riwaya zetu. 139

Maelezo mafupi: Jamii za kibinadamu hazina mpangilio bila ya kuwa na kiongozi sawasawa. Na kwa sababu hizi, Allah swt kamwe hakuwaachia waja wake bila ya kiongozi na daima kumekuwapo viongozi wa Allah swt miongoni mwao. Hata katika kipindi cha kuwepo Ghaibu kwa Al-Imam Muhammad Mahdi Sahib az-Zamaan(a.s) kumekuwapo na wawakilishi wake mahsusi, na baada ya kusita kwa kipindi chao, aliwachagua wawakilishi wake wa kawaida kwa ajili ya kuwaongoza watu. Watu waliojitolea, waaminifu na watu walio makini ambao kwa hakika wanakuwa wameelimika vya kutosha kuhusu Kitabu Kitakatifu cha Waislamu, yaani Qur'an Tukufu, na vile vile Sunnah za Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) na Ahlul Bayt(a.s) tu ndio wanaopewa jukumu hili na yeyote yule mwingine ambaye anajidhania kuwa anaweza kulibeba jukumu hili, kwa hakika hukataliwa!

SOMO LA 135: CHANZO CHA MAOVU

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Jiepushe na pombe kwani hiyo ndiyo ufunguo (chanzo) cha maovu yote. 140

Maelezo mafupi: Ingawaje kunaandikwa vitabu na makala mbalimbali kuhusu athari na matokeo mabaya ya pombe na vileo, juu ya mishipa yetu ya fahamu, na mpangilio mzima wa kuivisha chakula tumboni na moyo, mishipa ya damu, maini na mafigo na kwa kifupi, sehemu zote za mwili zinatajwa na kwa hakika athari zake mbaya zinazozikumba jamii zimefanyiwa utafiti wa hali ya juu na wanasayansi na matokeo yao yanatisha, lakini sentenso hiyo fupi ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) haiwezi kupatikana popote kwani imeelezea uhakika wote katika sentenso (Hadith) moja tu. Naam, pombe kama maovu yote mengineyo, ni chanzo cha magomvi na balaa na shida za kila aina.

SOMO LA 136: KUTIMIZA WAJIBU NDIYO IBADA KUU

Yeyote yule atimizaye wajibu wake, basi atakuwa miongoni mwa wachamungu. 141

Maelezo mafupi: 'Ibada haijawekwa tu kwa ajili ya kuwahudumia watu, wala kusali na kufunga. Ambapo kwa hakika 'ibada kuu ni kule ambapo kila mmoja atatimiza wajibu wake sehemu yake. Je ni 'ibada ipi iliyo juu na bayana kuliko hiyo? Kwa hakika ni 'ibada ambayo inaweza kubadilisha jamii katika bustani ya maua na ambapo kunawza kupatikana mema na maendeleo. Kutimiza wajibu kuna imani kubwa ikiwemo wajibu wa kuabudu, zaidi ya wajibu wa kibinadamu na kijamii na hata huduma za kiuchumi, na hapo ndipo ubainisho sahihi wa wale walioacha wajibu zao zilizo za lazima na kujivunia na kuchunguza and kujidhania wao kuwa ni wafuasi wa Dini ya Islam, imebainishwa wazi.

SOMO LA 137: MAKAZI KATIKA SAYARI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Nyota hizi angani ni kama miji ilivyo juu ya ardhi, kila mji unakuwa umeunganishwa (na miji mingine) kwa kupitia mihimili ya mwanga. 142

Maelezo mafupi: NI jambo la ubinafsi kwa kuchukulia dunia yetu hii kuwa ni mahala pa kuishi tu na ambapo mamilioni ya sayari hazitumiki, zikiwa ati ni kimya bila ya viumbe vyenye uhai vinavyoishi humo. Leo wanasayansi wamepiga mahisabu yao kuhusiana na kuwapo maisha katika sayari zinginezo na wanao uhakika kuwa mamilioni ya sayari hizi zinazo viumbe vyenye uhai vinavyoishi humo, na kuna uwezekano mkubwa kuwa nyingi za sayari hizo zinamaendeleo makubwa hata kuliko sisi wakaazi wa sayari hii ya dunia kwa sababu maisha ya huko yameanza miaka maelfu ya mamilioni kabla dunia yetu hii. Hadith hiyo ya juu ni mojawapo ya muujiza wa kisayansi wa Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambayo yeye ameizungumzia karne 14 zilizopita.

SOMO LA 138: QUR'AN TUKUFU NA KANUNI YA UZITO

Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amemwambia mmoja wa marafiki zake:

Je Allah swt hasemi kuwa ameumba Jannat juu ya nguzo isiyoonekana ? Mimi nilimjibu : "Naam!" Naye (a.s) alinijibu : "Kwa hakika kuna nguzo ambayo nyinyi hamuioni." 143

Maelezo mafupi: Siku hizi, imethibitishwa kuwa sayari zimewekwa kwatika mizunguko yao, kwa hakika shukrani kwa uwiano sahihi wa uzito wa mvutano na nguvu zinazorudisha. Kwa hakika uvutio huo huvutiana kwa mfano wa mnyororo mkubwa, na nguvu za kurejesha huondoka kutokea nyenzake na uwiano wao upo sawasawa ambao umesababisha kubakia katika mzunguko wao bila ya kutokea badiliko au kulemea upande wowote, na kubakia imara katika nafasini mwao juu ya nguzo zao zisizoonekana. Je kuna maelezo yaliyo na nguvu kama ya hapo juu katika kuelezea ukweli huu katika zama hizo ambapo maajabu haya yalikuwa bado hayajavumbuliwa ? Je huu si muujiza mojawapo wa Viongozi wetu Wakuu?

SOMO LA 139: MAAJABU YA MILIMA!

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Mitikisiko na mienendo ya ardhi inadhibitiwa na milima. 144

Maelezo mafupi: Siku hizi, imethibitishwa kuwa mvuto wa Mwezi unaathari katika mwenendo wa maji ya mabahari na maji kujaa na kupwa kwa mara mbili kwa siku, kwa utofautisho wa mita 1 na hata zaidi ya mita 15 katika baadhi ya sehemu, vile vile inayo athari zake juu ya uso wa dunia (ardhi) na huiinua kwa zaidi ya sentimeta 30 na tena kuirudisha chini. Lakini kwa kutokana na ugumu halisi wa uso wa dunia kwa kutokana na kuwepo kwa milima, mizizi ambayo imeshikamana na nyenzake na kufanya mtandao kuuzunguka dunia ndio unaouponyesha athari zake zaidi. Kwa hakika, iwapo kusingalikuwapo na milima na gamba gumu la dunia lisingekuwa gumu kabisa, na kama kungalikuwapo na daima mwongezeko wa maji na kupwa, je kungalikuwapo na amani na usalama wetu ? Kwa hakika viongozi wetu wa Kiislamu wameyaelezea ukweli na uhakika huu karne 14 zilizopita.

SOMO LA 140: WANYAMA WADOGO KABISA

Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) amesema:

Sisi tunamwita Allah swt kuwa ni Mwerevu na Mwenye ustadi mwingi kwa sababu ameumba viumbe vidogo mno ambavyo sisi hatuwezi kuviona kwa sababu ya udogo wao, na wala mikono yetu haziwahisi hao. 145

Maelezo mafupi: Kile ukionacho hapo juu ni sehemu tu ya Hadith ndefu ambayo Fat'h Ibn yazid Gurgani ameihadithia kutokea Al-Imam 'Ali ar-ridha(a.s) , ambamo imeelezwa kuwa, 'wanyama hawa ni wadogo mno kiasi kwamba hawawezi kuhisiwa, na wapo wametawanyika katika mawimbi ya baharini na magamba ya miti, na majangwani na ardhi tambarare'. Hadith hii ambayo imeandikwa kiasi cha miaka elfu moja iliyopita imebakia kama ndiyo ukumbusho wa Al-Imam 'Ali ar-Ridha(a.s) na imetaja masuala haya miaka elfu zilizopita hata kabla ya kuvumbuliwa vifaa vya kuchunguzia na kukuzia viumbe vidogo kiasi hicho, na kwa hakika huu ni muujiza wa kisayansi.

15

MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA

SOMO LA 14 1: LITABAKIA JINA TU KUTOKEA ISLAM

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Itawafikia watu zama ambapo herufi na maandishi kutokea Qur'an Tukufu na jina kutokea Islam yatakuwa yamebakia miongoni mwao. Misikiti ya Waislamu itakuwa ikiimarishwa kimajengo lakini yatakuwa yameteketea kwa mtazamo wa mwongozo na hidaya. 146

Maelezo mafupi: Sisi hatuwezi kusema kuhusu ubashiri huu wa kiajabu iwapo umekwisha dhihirika siku hizi au itahusika maishani mbele, lakini kwa hakika sisi tunashuhudia baadhi ya mifano yake hapa na pale na inashangaza kuwa Waislamu wanalalamikia kurudi nyuma kama kwamba kwao jina la Islam na mapicha ya Qur'an Tukufu tu vinatosha. Wao kamwe hawakuitumia Qur'an Tukufu kama ni Kitabu kifundishacho kwa ajili ya kumwelimisha mwanadamu na wala hawakuichukulia Islam kama ni shule yenye mpango wa kufundishia kiakili na kimatendo. Je wewe umeshashuhudia jamii halisi ya Kiislamu ambayo imerudi au kubakia nyuma au jamii ambayo haikutukuzwa au kuheshimiwa ulimwenguni ?

SOMO LA 14 2: KUTAMBUA UWEREVU NA UJAHILI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Ulimi ni utambulisho wa kukadiria kiasi cha ujahili na kupima uwerevu na busara. 147

Maelezo mafupi: Kwa hakika ulimi ni dirisha muhimu la nafsi na utu wake na kupima upeo wa fahamu za kila mtu. Ulimi ambao hufunua pazia kwa kupitia mizunguko yake ya kawaida na hivyo hudhihirisha vile ilipo na ilivyo nafsi ya mtu. Kwa misingi hii, mafunzo mengi mno ya Dini ya Islam yanazungumzia na kusisitiza usahihishwaji wa ulimi na maonyo na tahadhari zinakaa zikitolewa na hata viongozi wetu na ingawaje kusahihishwa kwa kikamilifu kwa ulimi hauwezekani bila ya kuirekebisha nafsi na akili na fahamu, lakini sisi tunaweza kudhibiti matokeo yanayoumiza kwa kutokwenda kwa ulimi katika mkondo sahihi kwa kukaa kimya au kujidhibiti na hiyo ndiyo njia ya kujiepusha na maovu yatokanayo na ulimi.

SOMO LA 14 3: ZAIDI YA NEEMA

imam hadi(a.s.) amesema:

"Yeyote yule anayeshukuru msaada, kuneemeka kwake kwa kushukuru kwake ni zaidi ya neema kwa ajili ya msaada, kwa sababu misaada ni mambo ya maisha ya humu duniani na shukurani ni mtaji wa humu duniani na Aakhera." 148

Maelezo mafupi: Tukichukulia ukweli huu kuwa shukrani si shukrani kwa mdomo tu, bali ni shukrani kwa uhakika na vile vile kwa kutumia msaada mahala panapostahiki, basi hapo ndipo inasemwa kuwa shukrani kwa msaada ina matokeo katika neema na mali yake kiasi kwamba msaada wenyewe si jambo kubwa kwa kulinganishwa nayo. Kwa kutumia misaada kwa uridhisho wa Allah swt na mahitaji ya waja Wake kwa hakika ni rasilimali na mtaji mkubwa kwa kuheshimika humu duniani na vile vile kwa neema kubwa huko Aakhera, wakati ambapo msaada unaweza kuwa ni neema cha kitu tu. Hivyo, shukurani ina thamani zaidi na zaidi ya msaada wenyewe.

SOMO LA 14 4: KUHUISHA SIRA ZA MA'ASUMIIN A.S.

Al-Imam 'Ali ar-Ridha (a.s) amesema:

Yeyote yule akaaye katika kikao au mkusanyiko ambapo huisha sira zetu, basi moyo wake hautakufa pale patakapo kufa nyoyo zingine. 149

Maelezo mafupi: Inafahamika wazi wazi kutokana na kauli ya hapo juu kuwa wajibu mkuu wa lazima juu ya wafuasi wa Ahlul Bayt(a.s) ya wananyumba ya Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) ni kuhuisha katika mikutano na mikusanyiko yao, kwa kujua imani na akida zao, kuelewa maana na ujumbe halisi kutokana na kauli na semi zao na kujizoesha na kufuata maamrisho yao na ni kusema kwamba mikutano na mikusanyiko yao iwe daima ni mikutano ya kusahihishana na kuwa tayari kwa maisha vile ipasavyo, na wala isiwe mikutano na mikusanyiko yao kwa ajili ya kuupoteza muda kwa starehe tu, kujiombea maslahi yao ya kibinafsi na kujifikiria mwenyewe na matatizo yake mwenyewe na matakwa yake mwenyewe bila kujali maslahi ya binadamu wengineo, imani na jamii kwa ujumla. Kwa hakika iwapo mikutano na mikusanyiko itakapokuwa vile tulivyofundishwa na Ahlul Bayt(a.s) basi nyoyo zetu zitahuika na vile vile fikara zetu zitakuwa njema zenye kuzaa matunda.

SOMO LA 14 5: SIRI NI AMANA

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Wakati mtu asemapo jambo lolote na kujitazama mwenyewe, basi mazungumzo yake hayo ni amana na siri kwetu (na inatubidi sisi kuitunza). 150

Maelezo mafupi: Kuamini katika Dini ya Islam ina sura nyingi, ikiwemo uaminifu katika kuweka na kutunza siri za watu. Jambo ili lina umuhimu mno katika Dini ya Islam kiasi kwamba kutoa siri za watu kumesemwa kuwa ni mojawapo ya Madhambi Makuu. Kwa ajili ya kutaka kuthibitisha jambo fulani kuwa siri, si lazima kwa msemaji kusema na kuomba na kusisitiza kuwapo kwa siri na kuitunza kwake. Na badala yake, ishara ndogo inatosheleza kuelewa uhakika huu. Iwapo mtu akijitazama mwenyewe na kujichambua mbele ya mtu mwingine basi inatosheleza kwake yeye kuweka mazungumzo ya ndugu yake Mwislamu kama siri yake.

SOMO LA 14 6: ALAMA ZA IMANI YA DINI YA ISLAM

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Wakati matendo yako mema yanapokufurahisha na matendo yako maovu yanapokuhuzunisha, basi wewe ni Mumin. 151

Maelezo mafupi: Dini ya Islam inasema kuwa kila mtu huzaliwa akiwa katika maumbile yaliyo halisi na safi, imani halisi na mapenzi ya mema. Maovu na maasi ndiyo yanayokuja kuathiri nafsi yake na kuibadilisha na kuigeuza kabisa. Hata hivyo, hadi pale mwanadamu anapokuwa akipenda mema na kuchukia mabaya, nafsi yake ya imani na hali ya uhalisi wake bado unakuwapo hai ndani mwake. Watu walio waovu ambao wanakuwa wamekerwa kwa matendo yao maovu, na hujisikia fahari katika hali hiyo na au wanapojitolea mhanga, uwema, usamehevu na uadilifu huwa ni kero kwao, kwa hakika wao ni makafiri.

SOMO LA 14 7: SHARTI LA KWANZA KWA AJILI YA KILA KAZI

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amemwambia Kumail ibn Ziyad:

Hakuna harakati wala kazi hadi pale utakapohitaji maarifa yake, uzoefu na elimu ya kutekeleza hivyo. 152

Maelezo mafupi: Iwapo sisi tutatafakari juu ya 'harakati zozote' zile, ndipo hapo sisi tutakuwa na uzoefu kwa mikakati na mipango ya Kiislamu na tutatambua hapo kuwa Dini ya Islam si mfuatilio wa 'ibada na dua tu na au inakosa mipango ya kimatendo. Badala yake inayo mipango na mikakati ya maisha ya mtu binafsi na vie vile masuala ya kijamii na vile vile hatua za maendeleo ya kibinadamu, jambo la kwanza ni akili na elimu ya uhakika. Islam inachukulia harakati na jitihada zote zisizo na matunda, ambazo zina elimu kidogo au mwongozo mdogo.

SOMO LA 14 8: UMUHIMU WA WAGENI

Mtume Muhammad Mustafa(s.a.w.w) amesema:

Wakati Allah swt anapowatakia watu kheri na ukarimu, basi huwazawadia. Wao waliuliza: "Je ni zawadi ipi hiyo?" Kwa hayo Mtume (s.a.w.w) alijibu: "Mgeni." 153

Maelezo mafupi: Hayo ni ya kweli kabisa. Kwa hakika mgeni ni zawadi kutoka Allah swt , zawadi yenye heshima na thamani kubwa mno. Lakini katika ulimwengu ambamo mapenzi yote yameshapotea, mgeni hathaminiwi. Na badala yake ngeni anachukuliwa kusumbua na kutokupendwa. Hivyo, ni kwa nadra tu hutokea kwa mtu kumwalika mtu mwingine au kutembelewa isipokuwa kwa maada tu, kibiashara na uhusiano wa kisiasa. Wakati ambapo katika nchi za Kiislamu na familia ambazo bado utamaduni wa Kiislam upo hai, basi kwao mgeni huheshimiwa na kutukuzwa kama ni zawadi kutokea Allah swt hata kama hatakuwa na uhusiano wowote wa kijamaa pamoja nao.

SOMO LA 1 4 9: HESHIMA NA MAPENZI

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq(a.s) amesema:

Yeyote asiyewaheshimu wakubwa na wala kuwahurumia na kuwapenda wadogo, basi huyo si miongoni mwetu. 154

Maelezo mafupi: Jamii za binadamu ni kama msafara mkubwa ambao daima upo katika mwendo. Watoto wachanga huzaliwa na mama zao, na watoto hao hukua na wakubwa huwa wazee na wazee hufa na hakuna mtu ambaye asiyepitia msafara huu. Humu ndani, watu wazima ndio kwa kawaida wanakuwa na uzoefu zaidi na kuwa na mtazamo wa undani zaidi na wamekuwa ndio vianzio vya huduma mbalimbali katika maisha yao lau wao wangalikuwa watu wenye kutuonya kuhusu matendo yetu iwapo ni mema au mabaya, na mahisabu yote yanaonyesha kuwa wao waheshimiwe na vijana na mabarobaro waelewe heshima zao.

Na kwa kuwa watoto bado ni wapya na mwazoni mwa maisha yao, lazima wapendwe na misingi ya ukuaji wao lazima ijengwe na wakubwa kwa moyo halisi, na kwa hakika hivyo ndivyo ilivyo njia na utamaduni wa kibinadamu na jamii inayoendelea kimaendeleo.

SOMO LA 150: JICHUKULIE NJIA HII KWA AJILI YAKO

Al-Imam 'Ali ibn Abi Talib(a.s) amesema:

Chochote kile kutokea kheri utakachokituma, kitahifadhiwa kwa ajili yako, na chochote kile utakachokiahirisha wewe, kitawafaidia wengineo ( na uwajibisho huo utakuwa mzigo juu yako). 155

Maelezo mafupi: Mali na utajiri unapatikana katika ulimwengu wetu wa leo kuliko kabla ilivyokuwapo bila ya kujali madhumuni muhimu na falsafa ya mali. Wale ambao hulimibikiza mali kama vichaa, na ambao hawajali ni njia zipi za halali, haraamu, haki au kudhulumu, kamwe hawafikirii kuwa wao kamwe hawataambatana pamoja na mali yao, na wala kuila yote kwa pamoja. Kwa hakika mzigo mzito upo juu ya mabega ya wenye kuimiliki mali hiyo; kulimbikiza, kuiacha na kuondoka na hatimaye kubeba wajibu wote juu yao.

VITABU VILIVYOKUSANYWA NA KUTARJUMIWA NA AMIRALY M. H. DATOO

BUKOBA - TANZANIA

Anwani ya pepe: datooam@hotmail.com

Hazina kubwa ya elimu inapatikana katika mtandao:

"www.alitrah.org

"www.dartabligh.org

"www.al-islam.org/kiswahili

VITABU VILIVYOTAYARI

1. AHADITH 2500 ZA MTUME S.A.W.W. NA MA-IMAMU A.S.

2. BWANA ABU TALIB (a.s) MADHULUMU WA HISTORIA

3. DALILI ZA QIYAMA NA KUDHIHIRI KWA IMAM MAHDI a.s.

4. DHAMBI KUU LA ISRAAF (UFUJAJI)

5. DHAMBI KUU LA KHIANA

6. DHAMBI KUU LA KUFICHA UKWELI

7. DHAMBI KUU LA KULA VIAPO VYA UONGO

8. DHAMBI KUU LA KUTOA USHAHIDI WA UONGO

9. DHAMBI KUU LA KUTOKUTIMIZA AHADI

10. DHAMBI KUU LA UCHAWI

11. DHAMBI KUU LA ULAWITI

12. DHAMBI KUU LA ULEVI

13. DHAMBI KUU LA KUTOKULIPA ZAKA, KHUMS NA SADAQAH

14. ELIMU KWA MADRASSAH : KITABU CHA KWANZA

15. FUNGUO ZA PEPONI - DUA MBALIMBALI

16. HADITHI ZA WATOTO ( PAMOJA NA PICHA )

17. HISTORIA YA ISLAM

18. HUKUMU ZILIZOTOLEWA NA IMAM 'ALI IBN ABI TALIB a.s.

19. IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s. : FADHAIL NA HUKUMU

20. JANNAT NA JAHANNAM

21. JE MAKHARIJI NI NANI ?

22. KANUNI ZA SAUM

23. KESI YA FADAK

24. SADAKA : KUTOA NA KUPOKEA

25. MAANDISHI YA NAWHA 200 ZA 14 MASUMIIN a.s. (KATIKA LUGHA YA URDU )

26. MAELEZO NA KANUNI YA HAJJ

27. MAFUNZO 150 YA MAISHA

28. MAKALA MCHANGANYIKO No. 1

29. MAKALA MCHANGANYIKO No. 2

30. MAKHALIFA 4 BAADA YA MTUME MUHAMMAD MUSTAFA S.A.W.W.

31. MASIMULIZI KUTOKA QUR'AN TUKUFU

32. MKUSANYIKO WA FAHIRISTI YA AYAH ZA QUR'AN

33. MSAFARA WA IMAM HUSAYN IBN Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. MADINA - KARBALA

34. MWONGOZO KATIKA KUTENGENEZA USIA.

35. NAWHA, MARTHIYYAH 3100 ZA 14 MASUMIIN a.s. (SAUTI KATIKA LUGHA YA URDU)

36. TADHWIN AL-HADITH

37. TAJWID ILIYORAHISISHWA

38. TAWBA

39. USAMEHEVU KATIKA ISLAM

40. UWAHHABI - ASILI NA KUENEA KWAKE

41. VITA VILIVYOPIGANWA KATIKA ISLAM

42. WAANDISHI MASHI'A KATIKA SAHIH NA SUNAN ZA AHL SUNNA

43. WANYAMA WALIOTAJWA KATIKA QUR'AN TUKUFU

VITABU VILIVYOCHAPWA 44. DHAMBI KUU LA KAMARI

45. DHAMBI KUU LA RIBA

46. DHAMBI KUU LA UWONGO (juzuu ya kwanza )

47. DHAMBI KUU LA UWONGO (juzuu ya pili )

48. HEKAYA ZA BAHLUL

49. KITABU CHA TAJWID

50. NDOA KATIKA ISLAM

VITABU VINAVYOTAYARISHWA

1. DHAMBI KUU LA KUDHULUMU HAKI ZA WENGINE AU KUTOZITIMIZA

2. DHAMBI KUU LA KUDHULUMU MALI YA MAYATIMA

3. DHAMBI KUU LA KUIBIA UZITO

4. DHAMBI KUU LA KUKWEPA JIHAD

5. DHAMBI KUU LA KURUDIA UKAFIRI BAADA YA KUSILIMU

6. DHAMBI KUU LA KUTOKUJALI ADHABU ZA ALLAH swt

7. DHAMBI KUU LA KUTOKUWATII WAZAZI

8. DHAMBI KUU LA KUVUNJA UHUSIANO NA NDUGU NA JAMAA

9. DHAMBI KUU LA KUWASAIDI MADHALIMU

10. DHAMBI KUU LA KUWATUHUMU WATU KWA ULAWITI

11. DHAMBI KUU LA MAUAJI

12. DHAMBI KUU LA MUZIKI

13. DHAMBI KUU LA SHIRK

14. DHAMBI KUU LA UTUMIAJI WA KILICHO HARAMISHWA

15. DHAMBI KUU LA UWIZI

16. DHAMBI KUU LA ZINAA

17. DHAMBI KUU LA KUTOWASAIDIA WANYONGE

18. HIARI NA SHURUTISHO KATIKA ISLAM

19. MADHAMBI MAKUBWA NA MADHAMBI MADOGO

20. MAJINA YA WATOTO WAISLAMU

21. MASWALI NA MAJIBU MBALIMBALI

22. QUNUT

23. QURBAA-MAPENZI YA WANANYUMBA YA MTUME MUHAMMAD MUSTAFA S.A.W.W.

24. TAFSIRI YA JUZUU' 'AMMA

25. TAFSIRI YA SURAH AL-YA-SIIN

26. TAQWA

27. TUSIUPOTEZE WAKATI

28. USINGIZI NA NDOTO

29. YAAS

10

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA TATU

Sura Ya Arubaini Na Tisa: Surat Al- Hujurat. Imeshuka Madina. Ina Aya 18.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kure-hemu

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١﴾

1. Enyi ambao mmeamini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ ﴿٢﴾

2. Enyi mlioamini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaanguka, na hali hamtambui.

إِنَّ الَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَاتَهُمْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ امْتَحَنَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَىٰ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿٣﴾

3. Kwa hakika ambao wanateremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amezitia mtihani nyoyo zao kwa takua. Hao watakuwa na maghufira na ujira mkubwa.

إِنَّ الَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَاءِ الْحُجُرَاتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٤﴾

4. Hakika ambao wanakuita nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili.

وَلَوْ أَنَّهُمْ صَبَرُوا حَتَّىٰ تَخْرُجَ إِلَيْهِمْ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥﴾

5. Na lau wao wangelingojea mpaka uwatokee ingelikuwa kheri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

MSINYANYUE SAUTI ZENU KULIKO SAUTI YA NABII

Aya 1 – 5

MAANA

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawakumbusha waumini mambo haya yafutayo:-

1.Enyi ambao mmeamini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Msifanye haraka kusema au kufanya tendo lolote linaoamabatana na dini na masilahi ya uma, mpaka alipitishe Mwenyezi Mungu kupitia Mtume wake mtukufu.

Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Katika Nahjul-balagha imeandikwa: “Mche Mwenyezi Mungu kwa baad- hi ya takua hata kama ni kidogo. Na weka sitara baina yako na Mwenyezi Mungu hata kama ni nyembamba.”

Kwa uchache kabisa wa mtu kumcha Muumba wake ni kujizuia kusema: Lau Mwenyezi Mungu angelihalalisha hili ambalo ameliharamisha au angeliharamisha lile alilolilihalalisha. Au kusema afadhali Nabii angeli- fanya hivi au asingelifanya vile alivyofanya na mengineyo ya ujeuri na ujinga.

2.Enyi mlioamini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii.

Si jambo zuri kuinua sauti bila ya dharura. Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Na uinamishe sauti yako. Hakika sauti mbaya zaidi ni ya punda.” Juz. 21 (31:19). Sikwambii tena ikiwa ni kuinua sauti mbele ya wakubwa na kwenye vikao vyao. Na Mtume mtukufu(s.a.w. w ) ni bwana wa manabii na mtukufu wa viumbe wote.

3.Wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyosemezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaanguka, na hali hamtambui.

Mnapozungumza na Nabii msizungumze kama mnavyozungumza nyinyi. Mwenye kufanya hivyo atakuwa amebatilisha imani yake bila ya kutaka wala kujua. Na mwenye kubatilika imani yake ndio vimebatilika vitendo vyake na atakuwa mikononi mwa waliopata hasara.

Kwa hakika ambao wanateremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amezitia mtihani nyoyo zao kwa takua – yaani amezisafisha nyoyo zao kwa matendo mema -Hao watakuwa na maghufira na ujira mkubwa.

Mwenyezi Mungu huwajaribu waja wake kwa aina mbalimbali ya mitihani, ili apate mawaidha mwenye kuwaidhika na ajikanye mwenye kukanyika. Mwenye kuwaidhika na akawa na subira Mwenyezi Mungu humtakasa, humuongoza njia ya usawa na humneemesha kwa maghufira na ujira wa wenye kuwa na subira.

Aya inaashiria kwamba kuzungumza kwa adabu na kwa inavyotakikana ni katika imani. Imam Ali(a . s) anasema:“Imani ya mja hainyooki mpaka unyooke moyo wake na moyo haunyooki mpaka unyooke ulimi wake.

Hakika ambao wanakuita nyuma ya vyumba, wengi wao hawana akili.

Mtume(s.a.w. w ) alikuwa na wake tisa, kila mmoja alikuwa na chumba chake kilichojengwa kwa makuti ya mtende, mlangoni kukiwa na pazia ya manyoya.

Wafasiri wanasema kuwa mabedui walikuja Madina na wakasimama nyuma ya vyumba vya Mtume wakaanza kuita kwa sauti: Ewe Muhammad(s.a.w. w ) tutokee! Mtume akangoja kidogo; kisha akawatokea. Mwenyezi Mungu amewataja kuwa wengi wao hawakujua walichokuwa wakikifanya, kutokana na ubedui na ushamba.

Na lau wao wangelingojea mpaka uwatokee ingelikuwa kheri kwao, kwa sababu kungoja na kutofanya haraka kuna malipo na thawabu, kumwdhimisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na kuchunga adabu.

Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu. Rehema yake inaenea kwa washamba, walalahoi n.k.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ ﴿٦﴾

6. Enyi mlioamini! Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.

AKIWAJIA FASIKI NA HABARI YOYOTE, ICHUNGUZENI

Aya 6

MAANA

Enyi mlioamini! Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda.

Imekuwa mashuhuri kwa wafasiri kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) alimtuma Walid bin Uqba bin Abu Muit kwa Bani Mustaliq kuchukua Zaka, wakampokea kwa shangwe ya kumzunguka, lakini akadhania kuwa wanataka kumzuia.

Akarudi kwa Mtume(s.a.w. w ) na kumwambia: wamenizuia na kunifukuza. Basi Mtume(s.a.w. w ) akakasirika na baadhi ya swahaba zake wakamwambia tuwashambulie? Ndio ikashuka Aya hii kuwaondolea tuhuma Bani Mustaliq. Kuna sababu nyingine ya kushuka Aya hii.

Sisi hatutegemei lolote katika sababu za kushuka Aya ila ikithibiti kwa nukuu ya Qur’an au Hadith mutawatir. Zaidi ya hayo ni kuwa kudhania Walid shari hakuwezi kusababisha ufasiki; isipokuwa ni kukosea na kutatizika. Mwenye kukosea haitwi fasiki.

Vyovyote itakavyokuwa sababu za kushuka, lakini Aya haishilii kwenye sababu hiyo, bali inaenda mbali zaidi, kwa vile sababu haiwezi kuhusisha isipokuwa inaenea. Itakuwa sababu inatajwa kwa ajili ya jambo fulani ambalo halihusishi tamko. Kwa hiyo niwajibu kuichukulia dhahiri ya Aya, ambayo inafahamisha uharamu wa kuyachukulia maneno ya fasiki bila ya kuchunguza na kuthibitisha habari yake, kuhofia kuingia kwenye hatari; kama kuwadhuru wengine na kujuta, na majuto ni mjukuu.

Tunapata tafsiri ya Aya hii katika kauli ya Imam Ali(a . s) :“Mwenye kufuata njia iliyo wazi atakunywa maji, na mwenye kuacha atahangaika.”

Kundi la masheikh wa kisunni na kishia wameitumia Aya hii kuwa ni dalili ya wajibu wa kuchukulia kauli ya mwenye kutegemewa bila ya sharti la kuchunguza ukweli wake. Baadhi yao wameitolea dalili kwa maneno ya undani yaliyojifungafunga.

Iko wazi kuwa Aya imechukua msingi wa kiujumla wa kupima habari ambayo haifai kuitegema ila baada ya uthibitisho na hiyo ni habari ya fasiki. Vile vile habari inayotegemwa bila ya uthibitisho ambayo ni habari ya mwenye kutegemewa.

Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameshartiza kuitegemea habari ya fasiki kwa ubainifu na uthibitisho, lakini hakuitaja habari ya mwenye kutegemewa. Lau ingelikuwa ni wajib kuichunguza habari ya mwenye kuaminika basi angeliitaja. Kwa kuwa haikutajwa basi sharti hiyo haipo.

Tuanavyo sisi ni kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Akiwajia fasiki na habari yoyote, ichunguzeni,” inafahamisha tu wajibu wa kuichunguza na kuithibitisha habari ya fasiki wala haifahimishi wajibu huo kwa habri ya mwenye kuaminika. Sisi tuko na wale wasemao kuwa kuitegemea habari ya mwenye kuaminika bila ya uchunguzi ni njia wanayoitumia wenye akili wa kale na wa sasa.

Hata hivyo kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda,” inafahamisha kuwa habari yoyote ambayo hatuna wasiwasi nayo kuingia katika matatizo na haramu, basi inafaa kuitumia bila ya kumwangalia mtoaji habari.

Kimsingi ni kuwa tusiamini habari ila ikiwa inatoka kwa mwenye kuaminika au tuithibitishe na kuichunguza ikiwa inatoka kwa fasiki.

وَاعْلَمُوا أَنَّ فِيكُمْ رَسُولَ اللَّـهِ لَوْ يُطِيعُكُمْ فِي كَثِيرٍ مِّنَ الْأَمْرِ لَعَنِتُّمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ حَبَّبَ إِلَيْكُمُ الْإِيمَانَ وَزَيَّنَهُ فِي قُلُوبِكُمْ وَكَرَّهَ إِلَيْكُمُ الْكُفْرَ وَالْفُسُوقَ وَالْعِصْيَانَ أُولَـٰئِكَ هُمُ الرَّاشِدُونَ ﴿٧﴾

7. Na jueni kuwa yuko kati yenu Mtume wa Mwenyezi Mungu. Lau angeliwatii katika mambo mengi, bila ya shaka mngelitaabika. Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezea Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na akauchukiza kwenu ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walioongoka.

فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَنِعْمَةً وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٨﴾

8. Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.

MWENYEZI MUNGU AMEWAPENDEKEZEA IMANI

Aya 7 – 8

MAANA

Na jueni kuwa yuko kati yenu Mtume wa Mwenyezi Mungu na mtukufu wa wa mwanzo na wa mwisho. Basi ni juu yenu kumwadhimisha wala msimpe habari isipokuwa ya ukweli.

Lau angeliwatii katika mambo mengi, bila ya shaka mngelitaabika.

Hii ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ikielekezwa kwa wau- mini kuwa wamsikilize Mtume na wamtii, wala wasimshauri lile analolijua kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambalo wao hawalijui. Lau angeliwaitikia kwenye mambo mengi wanayomwambia wangelitaabika na kuingia kwenye tabu na dhambi.

Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezea Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na akauchukiza kwenu ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walioongoka.

Mwenyezi Mungu amewaamrisha waja wake wamwamini Yeye na wamtii, akawabainishia uzuri wa imani na utiifu, akatumia kila njia kuwahimiza hilo na akamwahidi malipo na thawabu kubwa mwenye kuamini na akatenda mema. Vile vile amewakataza ukafiri na uasi, akabainisha hasara zake na akamtishia kwa adhabu mwenye kukufuru na kuasi na akazisifia adhabu hizo kwa namna ambayo haiwezi kufikirika akilini ila baada ya kubainishwa. Ni mtu gani anayeweza kufikiria adhabu ambayo si mauti wala uhai.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewatuma Mitume wake kwa watu ili wafikishe amri, makatazo ahadi na kiaga chake. Kuna wale wanaoitikia kihaki na kiukweli, wengine wakapinga na kufanya inadi na kuna wale waliotikia kuhofia masilahi yao na tamaa ya ngawira.

Wale waliomwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume kihaki na kiukweli ndio aliowakusudia katika kauli yake: “Amewapendezea Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu.” Yaani ameipendekeza na kuipamba kutokana na kueleza uzuri wa imani na kivutio cha thawabu nyingi. Akauchukiza ukafiri kwa kueleza mabaya yake na tishio la adhabu chungu.

Unaweza kuuliza : Mwenyezi Mungu (s.w.t) amelibainisha hilo kwa waumini na makafiri, kwanini amehusisha kuwataja waumini, kinyume na wengineo?

Jibu : Ndio, lakini sio kila mwenye kusikia ubainifu wa Mwenyezi Mungu anauamini na kunufaika nao, wala sio kila mwenye kunasihiwa na Mwenyezi Mungu anakubali nasaha zake. Bali wema wamekubali na waovu wakakataa. Ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamtaja na kumsifu mwenye kusikia maneno akafuata mazuri yake na akampuuza mwenye kupinga na akaachana nayo.

Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.

Hakuna mwenye shaka kwamba mwenye kuchagua uongofu badala ya upotevu ana fadhila na malipo, lakini fadhila kubwa ni ya yule aliyemwandalia njia ya uongofu, akamwongoza na akampa uweza wa kuifuata. Walisema wakale: “Kama si sababu asingelifaulu msababishaji”

وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ فَإِن فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ ﴿٩﴾

9. Na ikiwa makundi mawili katika waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hayo linadhulumu jingine, basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirejea basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki.

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٠﴾

10. Hakika Waumini tu ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemiwe.

NA IKIWA MAKUNDI MAWILI KATIKA WAUMINI YANAPIGANA

Aya 9 – 10

MAANA

Na ikiwa makundi mawili katika waumini yanapigana, basi yapatanisheni.

Uaislamu una mafunzo na miongozo ya kujenga jamii na kuitengeneza; miongoni mwayo ni wajibu wa kumlinda binadamu damu yake, mali yake, hadhi yake na uhuru wake wa kusema na kutenda. Hakuna yeyote mwenye utawala wa hayo isipokuwa haki. Akitoka kwenye haki na akaingilia haki ya wengine, basi hapo atakuwa amejiondolea kinga ya hayo yeye mwenyewe. Mwenyezi Mungu anasema:

وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ ﴿٧٠﴾

“Na hakika tumewatukuza wanadamau.” Juz. 15 (17:70).

Amesema tena kumwambia Mtume wake:

لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ ﴿٢٢﴾

“Wewe si mwenye kuwatawalia” (88:22).

Akasema tena:

إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَظْلِمُونَ النَّاسَ وَيَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ﴿٤٢﴾

“Bali njia ya lawama ipo kwa wale wanaowadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika ardhi bila ya haki.” Juz. 25 (42:42).

Mafunzo mengine ya Uaislamu ni kuhurumiana na kusaidiana katika yale yaliyo na heri na masilahi kwa wote. Ikiwa itatokea uhasama baina ya makundi mawili ya waumini, basi wajibu wa waumini ni kusuluhisha kwenye misingi ya haki na uadilifu na kuchunga umoja usivunjike.

Kuna Hadith tukufu inayosema: “Je, niwaambie jambo lililo na daraja kubwa zaidi kuliko kufunga, kuswali na kutoa sadaka? Wakasema: Naam! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: Ni kuwaunganisha waliotengana”

Na likiwa moja la hayo linadhulumu jingine, basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu.

Ikiwa kundi moja litakataa kurudi kwenye haki na likang’ang’ania uchokozi, basi ni juu ya waumini wengine kulihami na dhulma lile kundi linaloonewa, kwa hekima na mawaidha mazuri. Ikiwa lile kundi ovu halitakoma ila kwa vita, basi lipigeni katika mipaka ya sharia inayohakikisha amani ya wote.

Na likirejea basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki.

Likitubia lile kundi linaloonea na likaacha kabisa, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira mwenye kurehemu, na hakuna atakayeruhusiwa kulifanyia lolote. Lililobaki ni wajibu wa waumini, kwa juhudi zao waondoe, yaliyotokea kwenye nafsi za pande mbili.

Al-Jassas Al-Hanafi, anasema katika Kitabu Ahkamul-Qur’an akiwa anazungumzia Aya hii: “Ali Bin Abi Twalib alipigana na kundi ovu kwa upanga akiwa pamoja na maswahaba wakubwa wa Badr (Ahlu Badr) waliojulikana. Na alikuwa ni mwenye haki. Hakuna aliyehalifu katika kundi kabisa isipokuwa kundi ovu na wafuaisi wake aliokuwa akipigana nao.”

Na akasema Abu Bakr Al-Malik, Maaruf kwa jina la Ibn –Al-Arabi Al- Muafiri, katika Ahkamul - Qur’an: “Imethibiti kwa maulama wa Kiislamu na imethibiti kwa dalili ya dini kwamba Ali Bin Abu Twalib alikuwa Imam na kwamba kila mwenye kupigana naye ni muovu na kupambana na mtu huyo ni wajibu mpaka arudi kwenye haki.”

UDUGU WA KIDINI NA UDUGU WA KIBINADAMU

Hakika Waumini tu ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.

Hii ni kusisitiza kuleta suluhu baina ya pande mbili zilzigombana, pamoja na kuashiria kuwa upatanishi huu ni lazima kwa mfungamano wa udugu. Kuna Hadith isemayo: mwislamu ni ndugu wa mwislamu, hamdhulumu, hamtelekezi wala hamtii aibu.

Unaweza kuuliza: Kwanini Mwenyezi Mungu (s.w.t) amesema: Hakika waumini tu ni ndugu, na asiseme: Hakika watu wote tu ni ndugu. Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) naye akasema:

“Mwislamu ni ndugu wa mwislamu.” Na asiseme: Mtu ni ndugu wa mtu? Tunajua kuwa Mola ni mmoja, asili ni moja, umbile ni moja na usawa baina ya watu ni wajibu. Kwa hiyo upendo unatakikana uwe ni wa jumla sio mahsusi; sawa na rehe- ma ambayo imekienea kila kitu?

Basi mgawanyo huu utakuwa na tofauti gani na ule unaowagawanya binadamu kwa misingi ya kiuchumi; walivyofanya wamarksi, au kuwagawanya kwa misingi ya kijinsia; kama walivyofanya wanazi au kwa misingi ya vita na silaha kama ilivyo siasa ya kimarekani?

Kisha nini kilichosababisha matatizo na maangamizi haya yanayomkabili binadamu leo, hadi kufikia kumalizana, baada ya binadmu kuweza kumiliki nguvu mbaya ya silaha za maangamizi? Je, hii imesabishwa na binadamu kama binadamu au imesabishwa na aina kwa aina za migawanyo?

Hatimaye sasa binadamu wasaidiane kwa misingi ya dini au asasi za kibanadamu?

Jibu : Maswali yote haya ni haki, na jibu lake ni moja tu litakoloweza kutosheleza maswali yote haya; nalo ni: Kusaidiana ni wajibu baina ya binadamu wote bila ya kubagua. Huu ndio mwito wa uaislamu hasa, unaofahamishwa na makumi ya Aya na riwaya. Tutatosheka kutaja Aya moja na riwaya moja.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Aya ya 13 ya sura hii: “Enyi watu! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane. Hakika mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na takua zaidi yenu.

Kwa hiyo mwito wake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Enyi watu!’ pamoja na kusema kwake: ‘Kutokana na mwanmmke na mwanamume’ na ‘aliye na takua zaidi’ ni dalili mkataa na wazi kuwa mwito wa Qur’an ni wa kiutu na wa mataifa, unamzingatia mtu ni ndugu wa mtu kwa namna yoyote itakvyokuwa itikadi yake, utaifa wake na jinsia yake.

Mfano wa Aya hii na ufafanuzi wake ni kauli yake Mtume mtukufu(s.a.w. w ) : “Watu wote wako sawa kama chane za shanuo. Jueni kuwa hakuna ubora wa mwarabu kwa mwajemi wala wa mwajemi kwa mwarabu, wala wa mwekundu kwa mweusi wala wa mweusi kwa mwekundu isipokuwa kwa takua … nyote mnatokana na Adamu na Adam ametokana na mchanga.”

Zaidi ya hayo katika Juz.21 (30:30) kuna Aya inayosema kuwa uislamu ni dini ya maumbile na katika Juz. 9 (8:24) kuna Aya inayofahamisha kuwa dini ya Mwenyezi Mungu ni dini ya maisha.

Kwa hali hiyo basi inatubainikia kuwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake zinazingatia kuamini utu ni sehemu inayokamilisha kumwamini Mwenyezi Mungu, mitume wake na Vitabu vyake.

Kwa hiyo Makusudio ya mumin katika Aya na mwislamu katika Hadith ni yule anayeamwamini Mwenyezi Mungu na mtu kwa kuwa ni mtu.

Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna mzozo wala kupingana baina ya udugu wa kibinadamu na udugu wa kiislamu; huu wa kiislamu unauongeza nguvu ule wa kibinadamu.

11

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿١١﴾

11. Enyi ambao mmeamini! Kaumu isidharau kaumu nyingine, huenda wakawa bora kuliko wao; wala wanawake kwa wanawake wengine, huenda wakawa bora kuliko wao. Wala msitiane kasoro, wala msiitane majina ya kejeli. Na wasiotubu, hao ndio madhalimu.

KAUMU ISIDHARAU KAUMU NYINGINE

Aya 11

MAANA

Enyi ambao mmeamini! Kaumu isidharau kaumu nyingine, huenda wakawa bora kuliko wao; wala wanawake kwa wanawake wengine, huenda wakawa bora kuliko wao.

Imesemekana kuwa neno Qawm, tulililofasiri kwa maana ya kaumu, kwa maana yake ya kiarabu huwa halitajwi ila kwa wanaume tu, kwa dalili ya kuunganishwa wanawake baada ya neno hilo.

Katika Juz. 19 (25:55-62) tulisema kuwa dhalimu kesho atachukuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa ni kafiri ingawaje duniani anachukuliwa kuwa ni mwislamu kama akitamka shahada mbili.

Na mwenye kuwadharau wema atakuwa ni dhalimu na safihi.

Hili Mwenyezi Mungu amelikemea kwa ukali sana; kama aliposema:

فَيَسْخَرُونَ مِنْهُمْ سَخِرَ اللَّـهُ مِنْهُمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٩﴾

“…Wakawafanyia maskhara; Mwenyezi Mungu atawafanyia maskhara na wana wao adhabu iumizayo. “ Juz. 10 (9:79).

Pia kauli yake:

إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ ﴿٢٩﴾ وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ ﴿٣٠﴾ وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ ﴿٣١﴾ وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ ﴿٣٢﴾ وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ ﴿٣٣﴾ فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ ﴿٣٤﴾

“Hakika wale walio na hatia walikuwa wakiwacheka wale ambao wameamini. Wakiwapitia wanakonyezana na wakirudi kwa watu wao walirudi wakishangilia. Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. Basi leo wale ambao wameamini wanawacheka makafiri” (83: 29-34).

Vile vile amesema:

وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾

“Ole wake kila mtia kasoro mwenye kusengenya.” (104:1).

VIPI UTAPATA MARAFIKI?

Nimekumbuka, wakati nikifasiri Aya hii, kwamba kiasi cha mika 16 au zaidi iliyopita nilisoma tarjuma ya kitabu: How to win friends and influence people (vipi utapata marafiki na kuathiri nafsi) cha Dayl Karengi.

Vile vile nimekumbuka hekima ya hali ya juu ya Imam Zainul’abidin, inayohusiana na maudhui hii ambayo ina athari zaidi ya kitabu nilichokitaja pamoja na kuwa kimeenea sana na kufasiriwa kwenye lugha nyingi.

Imam, kwenye hekima yake, alikuwa akikusudia kauli yake Mwenyezi Mungu: “Kaumu isidharau kaumu nyingine, huenda wakawa bora kuliko wao.” Hekima yenyewe ni hii:

“Jihadhari na kuzungumza ambayo moyo unayakanya hata kama una udhuru. Kwani sio kila utakayemwambia shari unaweza kumfafanulia udhuru. Aliye mkubwa kuliko wewe muweke daraja ya mzazi, mdogo daraja ya mtoto, na aliye marika daraja ya kaka. Ni nani katika hawa unapenda kumvunjia heshima yake?

“Ikiwa shetani atakuingilia kujiona kuwa u mbora zaidi ya mwingine, angalia haya yafutayo: Ikiwa ni mkubwa zaidi yako, sema: amenitangulia kwa imani na matendo mema, kwa hiyo ni bora kuliko mimi. Ikiwa ni mdogo kuliko wewe, sema: nimemtangulia kwa maasi, kwa hiyo yeye ni bora kuliko mimi. Akiwa ni marika yako sema: mimi nina uhakika nimefanya dhambi, lakini nina shaka kuwa yeye amefanya dhambi, basi kwanini niache uhakika nichukue shaka?

“Ukiwaona watu wanakutukuza, sema: wamechukulia wema, na ikiwa wanakutenga, sema: kuna makosa nimefanya.”

Imam anaendelea kusema:“Ukiyafanya haya maisha yako yatakuwa mepesi, utakuwa na marafiki wengi na utakuwa na maadui kidogo, na utafurahi kwa wema wao wala hutasikitika kukutenga.”

Vyovyote watavyosema maulama na wenye hekima kuhisiana na maudhui haya, hawatazidisha kitu kwenye hekima hii fasaha ya hali juu.

Hilo si ajabu kwa vile aliyeisema ni mtoto wa wahyi, hazina ya ilimu ya wahyi na aliyekulia kwenye malezi yake.

Wala msitiane kasoro.

Msitiane ila wala msiwambie wengine lile ambalo hampendi kuambiwa.

Wala msiitane majina ya kejeli.

Mtu asimwite mwenzake kwa jina analolichukia. Mafaqihi wamesema kuwa ikiwa jina halikukusudiwa kasoro wala dharau na ni mashuhuri wa hilo, basi halina ubaya; kama vile Hassan Madafu, n.k.

Ni uovu kutumia jina baya baada ya imani.

Hapa kuna tafsiri mbili: Ya kwanza ni msimwite mumin ewe kafiri! Ya pili, ni uovu huko kumwita mwingine kwa jina asilolipenda. Tafsiri hii ina ngvuvu, kwa wafasiri wengi kuliko ile ya kwanza.

Na wasiotubu, hao ndio madhalimu.

Mwenye kutubia ni kama asiye na dhambi na mwenye kung’ang’ania dhambi atakuwa ameidhulumu nafsi yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu atawaadhibu wenye dhambi.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾

12. Enyi ambao mmeamini! Jiepusheni na dhana nyingi. Hakika baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipeleleze, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je, anapenda mmoja wenu kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.

DHANA, UJASUSI NA KUSENGENYA

Aya 12

MAANA

Katika Aya iliyotangulia Mwenyezi Mungu (s.w.t) amekataza dharau, kutia ila, kubeza na kuitana majina ya kuchukiza. Na akamkemea mwenye kufanya moja katika hayo. Katika Aya hii anakataza dhana mbaya, ujasusi na kusengenya. Ufafanuzi ndio huu ufuatao:-

DHANA

Enyi ambao mmeamini! Jiepusheni na dhana nyingi. Hakika baadhi ya dhana ni dhambi.

Sehemu hii ya Aya inawezekana kufanyiwa muhtasari kwa jumla moja tu: “Kila mtu hana hatia mpaka lithibitike kosa lake.”

Inawezekana jumla hii kuifafanua kwa urefu, tuweke mpaka wa linalopelekea asili ya dhana, kuwa je, inafaa kuichulia dhana au kuna wajibu wa kujieupusha wakati wote au wakati wa kuweko udhuru na wa kutokuweko ilimu? Na je, kuna udhuru wa kutojua au hakuna?

Ikiwa inafaa kuichukulia dhana, je, tuichukulie dhana vyovyote ilivyo sababu yake na mfungamano wake? Na ikiwa haifai kuichukulia dhana kwa namna yote ile, je ni nyenzo gani za ilimu kwenye hukumu ya sharia na mengineyo katika ilimu ya usul (misingi ya sharia) ambayo tumeimalizia miaka si kidogo kuisoma?

Ni vizuri tuchuke tafsiri ya wastani si kurefusha wala kufupiliza. Kabla ya lolote ni lazima tufanye maandalizi ya kujua toafauti baina ya shaka, dhana na ilimu. Shaka ni kuwa sawa uthibitisho na ukanusho. Dhana ni kuwa na nguvu upande mmoja baina ya hizo mbili, lakini bado kunakuwa na uwezekano kwa upande ule usio na nguvu. Ilimu ni kubainika upande mmoja unaofunga kabisa njia ya upande mwingine.

Unaweza kumdhania mtu heri au shari, ukawa umepatia au umekosea katika dhana yako. Hakuna ubaya kabisa ikiwa utamdhania mwenzako heri, iwe umepatia au umekosea; au iwe litajitokeza hilo kwenye kauli yako na vitendo vyako au lisijitokeze.

Mtume mtukufu(s.a.w. w ) anasema:“Wadhanieni waumini heri.” Imam Ali(a . s) anasema:“Liweke jambo la nduguyo kwenye heri.” Tazama Juz. 1 (2:83) kifungu cha ‘Kuchukia usahihi.’

Kwa hiyo basi inatubainikia maana ya kuwa kwanini Mwenyezi Mungu (s.w.t) amesema:“Jiepusheni na dhana nyingi,” na wala asisema ‘jiepusheni na kila dhana.’

Neno wingi huwa pia linatumiwa kwa maana ya baadhi; na haya ndiyo Makusudio yake kwenye Aya hii; yaani jiepusheni na dhana mbaya.

Dhana mbaya yenyewe sio haramu ikiwa haitajitokeza kwenye kauli au kitendo, wala mwenye dhana hiyo hana majukumu yoyote. Lakini ni lazima asiitolee maamuzi yoyote na aifanye kama haiko. Akiitolea uamuzi na ikajitokeza athari yake kwenye kauli au kitendo, basi atawajibika na atastahili lawama na adhabu.

Hii ndio dhana aliyoikusudia Mwenyezi Mungu aliposema: “Hakika baadhi ya dhana ni dhambi.”

Mtume mtukufu(s.a.w.w) anasema:“Mambo matatu hasalimiki nayo yeyote: Kisirani, hasadi na dhana: Ukiona kisirani endelea, ukiona husda usiitake, na ukidhania hakikisha. Kwa hiyo basi maana ni kuwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Jiepusheni na dhana nyingi’ nikuwa msizitolee maamuzi wala msizitumie; sawa na kauli yake “Asiwafitini shetani.”

UJASUSI

Wala msipeleleze.

Kupeleleza ni kuchunguza siri na makosa kwa njia ya kujificha. Ni haramu kwa Kitabu, Sunna, Ijmai (kongamano la maulama) na kiakili. Na kauli yake:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتًا غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّىٰ تَسْتَأْنِسُوا ﴿٢٧﴾ فَإِن لَّمْ تَجِدُوا فِيهَا أَحَدًا فَلَا تَدْخُلُوهَا حَتَّىٰ يُؤْذَنَ لَكُمْ... ﴿٢٨﴾

“Enyi ambao mmeamini! Msiingie nyumba zisizo nyumba zenu mpaka muombe ruhusa… na msipomkuta yeyote humo msiingie mpaka mpewe ruhusa.” Juz. 18 (24:27-28).

Katika Sunna ni Hadith ya Mtume mtukufu(s.a.w. w ) :“Mwenye kukuchungulia ukamtupia kijiwe na ukamtoboa macho yake, basi huna lawama.” Mafaqihi wamekubaliana kwa pamoja kuitumia Hadith hii. Ama akili inauona ujajusi ni vita dhidi ya maisha ya watu na kuingilia uhuru wao na mambo yao yanayowahusu katika mila na desturi.

Nimekumbuka, wakati nikiandika maneno haya, makala ndefu kuhusu maudhui haya, iliyotolewa na gazeti Al-Ahram la 27-6-1969, nililisoma wakati huo, kisha nikalihifadhi katika mafaili ya magazeti. Nililihifadhi na kuliweka akiba ya kulitumia nikilihitajia. Basi nikalisoma tena, mara nikaona mambo ambayo hata kuyawaza tu ni muhali; baadhi yake ni haya yafuatayo:

“Wamarekani hivi sasa wanajua kuwa sio kuwa kuta zao zina masikio tu, bali zina macho na mboni vile vile, kama lilivyosema gazeti la Times. USA wametengeneza kifaa kidogo cha ukubwa wa milimita, kinachoweza kusajili mazungumzo; na mtu anaweza kukiweka kwenye jaketi kama kifungo. Kila mtu anaweza kukitumia na kinagharimu kati ya dola 10 na 15.

Huko New York, wafanyabiashara wameweka matangazo ya biashara kwenye magazeti kuuza vifaa vya kurikodi mazungumzo ya watu majumbani mwao na wanaviuza madukani kama michezo ya watoto. Bei yake haizidi dola 18.

Mtu akiweka kifaa hiki kwenye gari kikielekezwa kwenye jengo basi kitarikodi kila neno linalosemwa kwenye jengo lile. Bali kuna kifaa cha kusikilizia maneno kisichozidi ukubwa wa punje ya choroko, kinachoweza kuwekwa kwenye kalamu nk, kinatumia betrii ya masaa 18 hadi 50.

Pia wametengeneza kifaa kidogo cha kutuma, kinachoweza kutangaza yanayopita kwenye majumba kwa umbali wa futi 50 na bei yake ni dola 400.

Ajabu ya yote ni kamera zinazopenya ukutani na kupiga picha mambo yote anayoyafanya mtu chooni na hata kwenye giza. Vile vile inawezekana kuchora chale (tattoo) katika mwili wa mtoto wakati anapozaliwa ambayo itafuatilia harakati zake katika maisha yake yote.

Kuna shirika katika Marekani yote linalokusanya habari na harakati binafsi za watu mashuhuri wa siasa, elimu, uandishi uchumi na wengineo na kurikodi maneno yao, na kupiga picha ya vitendo vyao, hata wanapofanya tendo la ndoa na wake zao na wengineo. Mtu anaweza kupata habari hizi kwa dola moja tu. Shirika hili linaitwa Benki ya habari.

Yote hayo yanatokea ikiwa serikali inajua kila kitu, bila ya kufanya lolote, kwa sababu imekuwa ni jambo la kawaida kama vile kuuza magazeti tu.” Mwisho wa nukuu ya gazeti.

Haya ni machache katika mengi. Watunzi wameandika vitabu maalum kuhusiana na maudhui haya. Lau wamarekani wangeliyafanya haya kwao tu wenyewe kwa wenyewe, tungeliwaambia wao na wanowatawala: “shauri yenu, kila mji una uhuru wa kujichagulia unavyotaka.” Lakini wamarekani wamevuka mipaka, wanafanya ujasusi kwenye nchi nyingine kwa ndege na satalaiti.

Usishangae msomaji. Marekani ni nchi ya maendeleo, demokarasia, bwana mkubwa wa uhuru, na polisi wa ulimwengu.

Tena zaidi ya hayo wanaamini Mwenyezi Mungu… Dalili kubwa kuwa wanamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ni mauaji ya kinyama waliyoyafanya kwenye kijiji kimoja katika Vietnam ya kusini[6] , na kuwasheheneza silaha za kisasa mayahudi ili kuwamaliza wananchi wa Palestina, kuwaua watoto kwa ujumla na kutupa mabomu kwa kutumi ndege za Phantoum kwa watoto wa shule wa Misr! Kweli kabisa USA ni dola kubwa kwenye uwanja huu wa mauaji!

KUSENGENYA

Wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je, anapenda mmoja wenu kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.

Kusengenya ni kumtaja mtu kwa jambo asilolipenda. Mtume mtukufu(s.a.w. w ) anasema:“Kusengenya ni kumtaja ndugu yako kwa jambo analolichukia. Ikiwa jambo hilo analo huko ni kusengenya na ikiwa hana itakuwa ni kumsingizia.” Na kusingizia ni kukubwa zaidi kuliko kusengenya na kumeharamishwa kwa Kitabu Sunna na Ijmai (kongamano la maulama).

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemfananisha mwenye kusengenywa na maiti kwa vile anakuwa hayupo na akaifananisha hishima yake na nyama yake na kumtaja kwa uovu kuwa ndio kula.

Maana ya mnalichukia hilo ni kuwa ikiwa mnaona kinyaa kula nyama ya maiti basi pia muone kinyaa kumsengenya asiyekuwepo, kwa sababu yote mawili hayo yako sawa.

Hakuna jambo linalofahamisha kupungukiwa na udhalili kuliko kusengnya. Imam Ali(a . s) anasema:“Kusengenya ni juhudi ya asiyejiweza.” Na Mwenyezi Mungu hasamehi kusengenya mpaka asamehe aliyesengenywa. Mafaqihi wameuvua uharamu wa kusengenya kwa wafuatao:-

Mpagani, hakimu dhalimu, mwenye kuudhihirisha ufuska wake, kwa sababu mwenye kulitupa joho la haya hana cha kuficha, kumpa ushauri mwenye kutaka ushauri katika kushirikiana na mtu au kumwakilisha kwenye jambo muhimu, kumtengua shahidi kwa kadhi, na mwenye kudhulumiwa kwa yule aliyemdhulumu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا عَلِيمًا ﴿١٤٨﴾

“Hapendi Mwenyezi Mungu maneno ya kutangaza uovu ila kwa aliyedhulumiwa.”

Juz. 6 (4:148).

Katika Kitabu Al-Makasib cha Sheikh Ansari, imesemwa kuwa sehemu zinazoondolewa uharamu wa kusengenya hazina idadi. Kwa sababu kusengenya kunakuwa haramu ikiwa kutangaza huko hakuna masilahi yenye nguvu. Vinginevyo, basi itakuwa wajibu kutangaza na kueneza kwa kuangalia masilahi yenye nguvu zaidi, kama ilivyo katika kila maasi ya haki za Mwenyezi Mungu na haki za binadamu.Tazama mwanzo wa Juz. 6.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿١٣﴾

13. Enyi watu! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane. Hakika mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na takua zaidi yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari.

قَالَتِ الْأَعْرَابُ آمَنَّا قُل لَّمْ تُؤْمِنُوا وَلَـٰكِن قُولُوا أَسْلَمْنَا وَلَمَّا يَدْخُلِ الْإِيمَانُ فِي قُلُوبِكُمْ وَإِن تُطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ لَا يَلِتْكُم مِّنْ أَعْمَالِكُمْ شَيْئًا إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤﴾

14. Mabedui walisema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatawapunguzia chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ ﴿١٥﴾

15. Hakika Waumini ni wale tu waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasiwe na shaka, na wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli.

قُلْ أَتُعَلِّمُونَ اللَّـهَ بِدِينِكُمْ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٦﴾

16. Sema: Je, mnamjulisha Mwenyezi Mungu Dini yenu, na hali Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na katika ardhi, na Mwenyezi Mungu anajua kila kitu?

يَمُنُّونَ عَلَيْكَ أَنْ أَسْلَمُوا قُل لَّا تَمُنُّوا عَلَيَّ إِسْلَامَكُم بَلِ اللَّـهُ يَمُنُّ عَلَيْكُمْ أَنْ هَدَاكُمْ لِلْإِيمَانِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٧﴾

17. Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye anayewasimbulia kwa kuwaongoza kwenye imani, ikiwa nyinyi ni wakweli.

إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٨﴾

18. Hakika Mwenyezi Mungu anajua siri za mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.

MTUKUFU ZAIDI YENU NI MWENYE TAKUA ZAIDI

Aya 13 – 18

MAANA

Enyi watu! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane. Hakika mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na takua zaidi yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari.

Watu wanajua kuwa baba yao ni Adam na mama yao ni Hawa, lakini lengo la kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Tuewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke, ni kuwa watu wote wajue kwamba wao ni ndugu ni udugu wa usawa katika haki na wajibu.

Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu; “Ili mjuane,” ni kuwa Makusudio ya kutofautiana kwenu katika miji, nasaba na rangi, sio kuwa muwe vikundi, mchinjane na mjifaharishe kwa mataifa yenu, baba zenu na jinsi zenu, hapana! Sivyo kabisa.

Lengo ni muhurumiane na msaidiane katika yale yaliyo na heri yenu na masilahi yenu. Na mbora kabisa atakuwa yule anayemuogopa Mwenyezi Mungu zaidi na akawanufaisha waja wake.

Aya hii ni mwito kutoka kwenye Qur’an kuwa watu wawe umma mmoja wa kiutu na ulimwengu mmoja unaokusanywa na uadilifu na upendo. Ulimwengu huu ni tegemeo la wenye fikra safi na ni ndoto ya walio wema.

Tuna uhakika kuwa makubaliano ya haki za binadamu, yatabakia kwenye karatasi na yatakuwa ni nadharia tu, ikiwa hautapatikana umoja wa ubinadamu uliotolewa mwito na Qur’an, zaidi ya mika 1300 liliyopita. Amerika na Israil zilitia saini makubaliano ya haki za binadamu, lakini bado ndio za kwanza kuangamiza watu Vietnam na Palestina.

Leo ninapoandika maneno haya 22 April 1970, kamati ya umoja wa mataifa imehakikisha kuwa Israil imevunja haki za binadamu, ikasema waziwazi kuwa Israil imevunja majumba ya wakazi ikaacha miili ya wanaume, wanawake na watoto kwenye kifusi na ikakataa isizikwe. Pia imevunja sehemu takatifu na mahospitali[7] na kuwaadhibu wenyeji kwa umeme. Watu wazima wanawang’oa viungo, watoto wanawakata mikono na kupasua matumbo yao mbele ya baba zao na mama zao na mengineyo ya kinyama na mauji ya maangamizi.

Mabedui walisema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatawapunguzia chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Makusudio ya uaislamu hapa ni kutamka shahada mbili. Katika Juz. 1 (2:82), tumetaja tofauti baina ya mumin na mwislamu. Hapa tutamnukuu Dkt Twaha Hussein katika kitabu Mir’atul-islama (Kioo cha uaislamu).

Yeye ni mwanafasihi anayefahamika kwa siri za fasihi, ninamnukuu: “Wakati wa Mtume kulikuweko waumini na waislamu. Basi, niipi tofauti baina imani na Uislamu? Imani kwa dhahiri ya Aya hii ni jambo lilio moyoni ambalo mihimili yake ni ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu na kusadikisha, kwa kina ndani ya dhamiri, kila aliloletewa wahyi Mtume.

Natija ya imani hii ni kumwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume katika kila wanalolitolea mwito, bila ya kigugumizi, kugwazagwaza, wala kutaradadi, kwa hali yoyote ile itakavyokuwa; iwe kuna matukio au majanga. Mhimili mwingine wa imani hii ni kumwogopa Mwenyezi Mungu kiundani kabisa likitajwa jina lake na kumtegemea kwa undani zinaposomwa Aya zake.

“Ama Uislamu ni twaa ya dhahiri ya kutekeleza wajibu na kujiepusha na yaliyokatwaza; hata kama haitafikia imani ya kweli. Kuna watu wanaosilimu kuhofia ubaya; kama walivyosilimu makuraishi walioachwa bila ya kutekwa nyara siku ya kutekwa Makka. Wengine walasilimu kwa hofu na tamaa; kama walivyofanya mabedui aliowataja Mwenyezi Mungu katika Aya hii.”

Hakika Waumini ni wale tu waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasiwe na shaka, na wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli.

Waumini wa kwelikweli kabisa ni wale wasiokuwa na shaka yoyote kwenye itikadi zao na wanaojitolea kihali na mali, kuihakikisha haki na kuibatilisha batili. Umetangulia mfano wake mara kadhaa; miongoni mwazo ni Juz. 10 (9:88).

Sema: Je, mnamjulisha Mwenyezi Mungu Dini yenu, na hali Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na katika ardhi, na Mwenyezi Mungu anajua kila kitu?

Mabedui walisema tumeamini, ndio Mwenyezi Mungu anawajibu, kuwa hivi mnamjulisha Mwenyezi Mungu imani yenu na hali Yeye anajua siri na yaliyofichika; kila kitu amekizunguka. Tena je imani inakuwa kwa kudai? Inatosha kuwa mtu ni mjinga kuwa hajui uweza wake Mwenyezi Mungu.

Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye anayewasimbulia kwa kuwaongoza kwenye imani, ikiwa nyinyi ni wakweli.

Makusudio ya kusimbulia kwake Mwenyezi Mungu ni kuwafanyia hisani, kwa sababu Yeye amekataza masimbulizi, na hawezi kukataza jambo kisha alifanye. Makusudio ya kuongoza kwake kwenye imani ni kutoa mwongozo wa haki na kuipendekeza.

Maana ni kuwa mabedui na walio mfano wao wanaona kuwa wamemfanyia hisani Mola wao na mtume wao kwa dini yao na wanataka walipwe; hali yakuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyewafanyia hisani wao, pale alipowaongoza kwenye haki na kuwahimiza kupitia Mtume wake.

Kwa hiyo wao ndio wamshukuru kwa alivyowafanyia hisani na kuwaneemesha; sio wao wasimbulie na kutaka kulipwa; ikiwa kweli wameamini dini yao na wakafanya ikhlasi kwenye imani yao. Vinginevyo watakuwa wanastahili kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale aliyowaandalia waongo na wahaini.

Hakika Mwenyezi Mungu anajua siri za mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anajua imani ya kweli na ya uwongo na kuzipamabanua amali zilizokusudiwa dunia na zile zilizokusudiwa radhi ya Mwenyezi Mungu. Aina zote za amali pamoja na imani au kufuru ndio kipimo cha uadilifu wa hisabu na malipo.

MWISHO WA SURA YA ARUBAINI NA TISA: SURAT AL- HUJURAT

4

5