HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU23%

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU Mwandishi:
: AZIZI NJOZI
Kundi: Wanawake

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU
  • Anza
  • Iliyopita
  • 33 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 47722 / Pakua: 5538
Kiwango Kiwango Kiwango
HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

Mwandishi:
Swahili

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

Kimeandikwa na: Allamah Murtaza Mutahhari

Kimetarjumiwa na: Aziz Njozi

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 9987 - 427 - 37 - 5

Kimeandikwa na: Allamah Murtaza Mutahhari

Kimetarjumiwa na: Aziz Njozi

Kimehaririwa na: Dr. M. S. Kanju

Email: mokanju2000@yahoo.com

P.O. Box 19701, Dar es Salaam/Tanzania.

Kupangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab.

Toleo la kwanza: Mei, 2007 Nakala:1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation P.O. Box 19701 Dar es Salaam, Tanzania

Simu:+255 22 2110640 Fax: +255 22 2131036

Email: info@alitrah.org Website: www.alitrah.org

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

NENO LA MCHAPISHAJI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la: "Woman and her rights." Sisi tumekiita: "." Kitabu hiki, "" ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Allamah Murtaza Mutahhari. Allamah Murtaza Mutahhari, mwandishi wa kitabu hiki ameichambua historia ya maisha ya mwanamke katika nchi za Magharibi na Mashariki (Asia) na mifumo yao ya ndoa. Mwandishi amerejea vyanzo vya wanasaikolojia na wanasosholojia wa Magharibi ili kuthibitisha hoja zake. Madhumuni yake ni kutaka kuthibitisha kwamba Uislamu una mfumo mzuri wa ndoa na haki za wanawake, kinyume na wanavyoamini watu wa Magharibi na wengine waliokuwa na kasumba ya umagharibi.

Inakubaliwa na kila rafiki na adui kuwa Qur'ani Tukufu ilifufua haki za wanawake. Hata maadui wanakiri angalau kwamba Qur'ani wakati wa kuteremshwa kwake ilichukuwa hatua kubwa katika kuboresha hali ya mwanamke na kurejesha haki zake za binadamu. Qur'ani ilifufua haki za mwanamke kama mwanadamu na kama mwenzi wa mwanaume katika utu na haki za binadamu lakini haikupuuza jinsia yake wala jinsia ya mwanaume. Kwa maneno mengine Qur'ani haikupuuza maumbile ya mwanamke. Ndio maana kuna kuwafikiana kikamilifu kati ya kanuni za maumbile na kanuni za Qur'ani. Mwanamke katika Qur'ani ni sawa na mwanaume katika maumbile. Vitabu hivi viwili vikubwa vya kimungu (Qur'ani na maumbile), kimoja kikiwa kimeumbwa na kingine kikiwa kimekusanywa, vinakubaliana na kuafikiana kabisa. Nia ya kitabu hiki ni kuangazia na kuelezea kuafikiana huku. Kutokana na umuhimu wa maudhui hii tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ili kutoa mwanga kwa Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Aziz Njozi kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

Kwa Fatima Zahra Binti anayeheshimika wa Mtukufu Mtume wa Uislamu, na kiigizo cha wanawake wa Ulimwengu.

MWANDISHI

Ayatullah Murtaza Mutahhari, alizaliwa mwaka wa 1920, na alikuwa ni miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu hodari sana na waandishi mashuhuri wa zama hizi. Alikuwa amezama sana katika kujifunza kimapokeo (traditional learning) na alivutiwa na watetezi wa masomo haya ya kimapokeo. Alikuwa ni mwanafalsafa na alikuwa amesoma falsafa kwa undani sana. Kazi yake ina sifa ya uwazi wa kifalsafa ambao ulimfanya awe na sifa ya kushughulikia tatizo la msingi la fikra ya kidini ambalo ndio kiini cha kitabu hiki. Ayatullah Mutahhari alipata elimu yake ya msingi ya theolojia kutoka kwa baba yake, Sheikh Muhammad Husain, huko kwao, katika mji wa Fariman, Ayatulah alipofikisha umri wa miaka kumi na mbili alijunga na kituo cha elimu cha Mashhad, na hapo alisoma kwa miaka mitano. Kisha alienda Qum kituo kikuu cha elimu ya Kiislamu.

Alikaa na kusoma hapo kwa miaka kumi na tano. Alihitimu masomo yake katika Imani za Kiislamu na Maarifa ya Sheria chini ya usimamizi wa mwanafalsafa mashuhuri Allamah Muhammad Husain Tabatabai, Imam Khomeini na wanazuoni wengine wakubwa. Kisha akahamia Tehran. Katika kipindi cha elimu yake Ayatulah alihisi kuwa wakomunisti walitaka kuibadilisha dini takatifu ya Uislamu na kuharibu roho yake kwa kuchanganya mitazamo yao ya kumkana Mwenyezi Mungu na Falsafa ya Uislamu na kwa njia ya kuzitafsiri Aya za Qur'ani kiyakinifu.

Kwa kusema kweli, sio ukomunisti tu uliomshughulisha Ayatullah. Pia aliandika tafsiri ya Qur'ani, na falsafa, maadili, sosholojia, historia na masomo mengine mengi. Katika kazi zake zote, lengo lake lilikuwa ni kujibu hoja potofu zilizotolewa na watu mbali mbali dhidi ya Uislamu, kuonyesha udhaifu wa itikadi nyingine na kuonyesha utukufu wa Uislamu. Aliamini kuwa ili kuonyesha uongo wa Ukomunisti na itikadi nyinginezo ilikuwa muhimu sana kutoa maana juu ya ukomunisti na kuielezea taswira halisi ya Uislamu. Ayatullah Mutahhar aliandika kwa uangalifu na bila kuacha wala kuchoka toka enzi za uwanafunzi hadi mwaka 1979, mwaka aliouawa shahidi. Kazi zake nyingi zimechapishwa ndani na nje ya Iran. Ameandika vitabu vingi na si juu ya mada anazozipendelea bali juu ya mada zinazohitajika.

Kila ilipotokea kuwa kitabu fulani juu ya mada muhimu za Kiislamu kinahitajika na hakipo basi alikiandika. Kazi za Mutahhari hazikuvumiliwa na wale wanaomkana Mwenyezi Mungu na hivyo waliamua kumuondoa mnamo tarehe 1 Mei mwaka 1979. Kifo chake cha kishahidi kilikuwa ni msiba mzito. Habari za msiba huu zilipomfikia Imam Khomeini hakuweza kuyazuia machozi yake. Katika salamu zake za rambirambi alisema; "Nimenyang'anywa mwanangu kipenzi. Ninaomboleza kifo cha yule ambaye alikuwa ni matunda ya uhai wangu". Maelfu wa Waislamu walihudhuira mazishi yake. Alizikwa Qum jirani na kaburi la Bibi Fatima Ma'sumah. Ayatullah Mutahhari alikuwa ni mtu mashuhuri katika nyanja za kidini na kielimu nchini Iran. Alifanya kazi katika Chuo Kikuu cha Tehran kama Mkuu wa Idara ya Theolojia na Mafunzo ya Kiislamu. Wakati alipouawa shahidi alikuwa ni Rais wa Baraza la Kikatiba la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na alikuwa akitekeleza majukumu yake kwa namna inayofaa kabisa. Kazi zake zimetafsiriwa na kuchapishwa katika lugha za Kifaransa, Kiarabu, Kituruki, Kikurdi na Kiingereza. 'The Islamic Seminary' ilipata heshima ya kuchapisha baadhi ya vitabu hivi.

NENO LA AWALI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu Mahitaji ya zama zetu hizi yanalazimisha kutathmini maswali mengi yenye umuhimu na sio kuridhika na tathmini zake za awali. Mfumo wa haki za ndoa na majukumu ya kifamilia ni miongoni mwa masuala haya. Kwa sababu mbali mbali, ambazo tutazieleza baadaye, imedhaniwa kuwa katika zama hizi, suala la msingi ni uhuru wa mwanamke na haki zake ziwe sawa na za mwanamume, na kwamba maswala mengine yote yapo chini ya suala hili kuu. Hata hivyo kwa mtazamo wetu, suala la msingi kabisa, au angalau tuseme moja ya masuala ya msingi kabisa, juu ya haki za kifamilia, ni iwapo mfumo wa ndoa unajitegemea na hautangamani na mifumo mingine yote ya kijamii na una vigezo na mantiki yake maalum, au ni moja tu ya mifumo mingi ya kijamii na kuwa vigezo na falsafa zile zile ndizo zinazotumika kulishughulikia suala hili kama ilivyo kwa mifumo mingine ya kijamii.

Kiini cha shaka yetu ni kuwa, kwa upande mmoja, katika mfumo huu makundi makuu yanayohusika yapo katika jinsia mbili tofauti, na kwa upande wa pili, inahusisha ongezeko na muendelezo wa vizazi. Maumbile yamefanya tabia za kimaumbile na viungo vya uzazi vya makundi haya mawili kuwa tofauti. Jamii ya wanandoa ni nusu-asili na nusu -mkataba. Ni njia ya kati na kati baina ya jamii ya silika kama ile ya nyuki na siafu ambayo haki na majukumu yake yameshaamuliwa na maumbile na hakuna uwezekano wa kuvunja sheria, na pia baina ya jamii ya kimkataba kama jamii ya wanaadamu, ambayo ina umbile la asili au silika. Kama tunavyojua, wanafalsafa wa kale walilichukulia suala la maisha ya familia kama tawi linalojitegemea la busara za kivitendo, na waliamini kuwa sehemu hii (maisha ya familia) ya maisha ya mwanadamu ina vigezo vyake tofauti.

Plato katika kitabu chake 'The Republic', Aristole katika kitabu chake, 'The politics,' na Abu Ali bin Sina (Avicenna), katika kitabu cha al-Shifaa, wamelizungumzia suala hili katika mtazamo huu pia. Ni suala lenye utata iwapo haki za asili za mwanaume na mwanamke zinafanana au hazifanani; kwa maneno mengine, iwapo haki kwa mujibu wa maumbile ya mwanadamu, ni ya jinsia moja au jinsia mbili, na iwapo kuwa na jinsia ya kike au ya kiume kunaathiri haki na majukumu ya mwanadamu. Katika ulimwengu wa Magharibi, harakati za haki za binadamu zilianza katika karne ya 17, kipindi cha mwamko wa harakati za kisayansi na kifalsafa. Waandishi wanafalsafa wa karne ya 17 na 18 walifanya jitihada zinazostahili sifa kwa kueneza mawazo yao juu ya haki za msingi za asili na zisizoondosheka za binadamu.

Jeans Jacques Rousseau, Voltaire na Montesquieu, ambao ni miongoni mwa wanakundi hili la waandishi na wanafalsafa, ni wafadhili wakubwa wa jamii ya mwanadamu, na inafaa kusema kuwa mchango wao kwa maisha ya wanaadamu haukuwa mdogo kuliko wa wagunduzi na wavumbuzi wakubwa, vilikuwa na thamani sawa. Wazo lao kuu lilikuwa kwamba wanaadamu wana mfululizo wa haki za asili walizozaliwa nazo pamoja na uhuru - vyote ambavyo haviwezi kuondosheka wala kuhamishwa na yeyote kwa visingizio vyovyote. Watu wote, ikiwa ni pamoja na watawala na watawaliwa, weupe na weusi, matajiri na maskini, wote ni sawa. Matokeo ya harakati hizi za kijamii na kisomi zilionekana kwanza Uingereza na kisha Marekani na baadaye Ufaransa. Yakaja yakatokea mapinduzi hapa na pale, mifumo ikabadilishwa na mikataba ikasainiwa. Polepole, harakati zilienea katika nchi nyingine.

Katika karne ya 19, mawazo mapya ya kiuchumi, kijamii na kisiasa juu ya haki za binadamu yaliibuka. Maendeleo mapya yalipelekea kutokea kwa ujamaa, ushiriki wa wafanyakazi katika faida za viwanda, na kuhamishwa kwa serikali kutoka kwa jamii ya mabepari kwenda kwa watetezi wa wafanyakazi (wavuja jasho). Mpaka kufikia mwishoni mwa karne ya 19, mazungumzo yote na hatua zozote za kivitendo zilizochukuliwa katika anga ya haki za binadamu, zilikuwa zimejikita tu katika haki za mataifa juu ya serikali na haki za waajiriwa dhidi ya waajiri. Katika karne ya 20, suala la haki za wanawake liliibuka kwa mara ya kwanza mwaka wa 1948, Umoja wa mataifa ulitangaza Azimio la Dunia la Haki za Binadamu ambapo ulitoa mbiu ya usawa wa haki kati ya mwanamke na mwanaume kwa wazi kabisa.

Harakati zote za kijamii huko Magharibi toka karne ya 17 zimekuwa zikizunguka kwenye uhuru na usawa, kwa vile harakati za haki za wanawake zilikuja mwisho kabisa, na historia ya masaibu ya wanawake Ulaya, kutokana na mtazamo huu, ilikuwa mbaya sana, Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu halikuzungumzia chochote zaidi ya uhuru na usawa.

Wanaounga mkono harakati hizi wanashikilia kuwa harakati hizi zinakwenda pamoja na harakati za haki za binadamu. Wanasema kuwa bila kuhakikisha uhuru na haki za wanawake hakuna maana yoyote kuzungumzia uhuru na haki za mwanadamu. Pia walidai kuwa sababu kubwa ya migogoro ya kifamilia ilitokana na mwanamke kunyimwa uhuru na usawa wake dhidi ya mwanaume, na kwamba matatizo yote haya ya kifamilia yatatatuliwa mara tu tatizo hili litakapoondolewa Kilichosahauliwa katika hili kilikuwa ni kile tulichokieleza kama suala la msingi kuhusiana na mfumo wa haki za familia, hii ni kuwa, iwapo mfumo huu unajitegemea au unategemea mifumo mingine ya kijamii, na ikiwa una vigezo na mantiki tofauti au la.

Msisitizo uliwekwa tu kwenye kanuni za jumla za uhuru na usawa na nukta pekee iliyozingatiwa ilikuwa ni ile ya haki za asili na zisizoondosheka za binadamu. Ilidaiwa kuwa mwanamke, kama binadamu, alikuwa na stahili ya kupata haki zote anazozifurahia na anazozipata mwanaume. Katika sura fulani za kitabu hiki, tumejadili vya kutosha juu ya suala la vyanzo ambavyo kutokana navyo haki za asili zimechukuliwa au zimetengenezwa. Huko, tumeonyesha kuwa misingi ya haki zote ni maumbile yenyewe.

Ikiwa mwanadamu ana haki maalum, ambazo farasi, kondoo, ndege na samaki hawana, hii inatokana na maumbile yake na jinsi alivyoumbwa. Ikiwa wanaadamu wote ni sawa katika haki za asili na wote lazima waishi maisha huru, hii ni kwa sababu mfumo huo ndio walioumbwa nao. Wasomi wanaounga mkono wazo kuwa uhuru na usawa ni haki aliyozaliwa nayo mwanadamu, hawana hoja nyingine zaidi ya hii. Hivyo katika suala la haki za familia pia, tunapaswa pia kuongozwa na maumbile. Sasa hebu tuangalie kwa nini mazingatio ya kutosha hayakuwekwa kwenye suala tulilolielezea kama la msingi.

Je imeshathibitika kisayansi kwamba tofauti kati ya mwanaume na mwanamke ni ya kioganiki tu (kimaumbile) na haiwaathiri kiumbo na kiroho au haki na majukumu yao, na ndio maana imepuuzwa katika falsafa ya kisasa ya jamii? Kusema kweli, ilivyo ni kinyume kabisa na swali hili. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi na ugunduzi wa kibaiolojia na kisaikolojia imethibitika kuwa kuna tofauti muhimu kati ya hizi jinsia mbili. Katika kitabu hiki, tumejadili suala hili na tumenukuu maoni ya wanabaiolojia na wanasaikolojia juu ya hili. Inashangaza kwamba licha ya yote haya, suala hili la msingi lilipuuzwa.

Labda kutolijali suala hili la msingi kumetokana na maendeleo ya haraka mno ya harakati za ukombozi wa mwanamke. Ndio maana, wakati harakati zikirekebisha hali ya mambo kuondoa taabu za wanawake, katika baadhi ya maeneo zimewasababishia maafa wao na jamii nzima kwa ujumla. Tutaangalia baadaye katika kitabu hiki, kwamba mwanamke wa Kimagharibi, hadi mwishoni mwa karne ya 19, alinyimwa haki zake za msingi za binadamu. Ilikuwa ni juzi tu hapa katika karne ya 20 ambapo watu wa Magharibi walifikiria kurekebisha hali ya mambo.

Hii harakati ilipoanza, katika kipindi cha mwamko wa harakati nyingine, kudai usawa na uhuru, walitegemea miujiza kwa maneno haya mawili tu. Walisahau kuwa usawa na uhuru ulihusiana na uhusiano baina ya watu, kama wanadamu tu. Hakuna shaka yoyote kuwa mwanamke ni mwanadamu na amezaliwa huru kama mwanadamu mwingine yeyote na kwa sababu hiyo anastahili haki sawa. Lakini mwanamke ni mwanadamu mwenye sifa fulani za kipekee. Mwenendo wa tabia zao ni tofauti (na wanaume) na mfumo wa akili zao ni wa kipekee.

Tofauti hii sio matokeo ya sababu za kijiografia, kihistoria au kijamii, bali ni ndio maumbile yao. Maumbile kwa makusudi kabisa yamewafanya wawe tofauti (na wanaume) na jitihada zozote zitakazochukuliwa dhidi ya malengo ya maumbile zitakuwa na matokeo mabaya. Kama tulivyochukuwa hamasa zetu kutoka kwenye maumbile juu ya usawa na uhuru wa mwanadamu, basi vivyo hivyo ndivyo tunavyopaswa kupata mwongozo kutoka kwenye maumbile ili tuweze kuamua iwapo haki za mwanamke zinafanana na za mwanaume au hazifanani na iwapo jamii ya kifamilia ni angalau nusu-asili (semi-natural society).

Ni jambo linalofaa kutafakari iwapo kuwepo kwa jinsia mbili katika wanyama, ikiwa ni pamoja na binadamu kumetokea kama ajali au ndio muundo wa maumbile uliokusudiwa; yaani iwapo tofauti za jinsia ni za juu juu tu, au ni kama Alexis Carell alivyoonyesha kuwa kila seli ya mwili ya mwanadamu ina jinsia, iwapo mwanaume na mwanamke wanayo, au hawana, kazi tofauti za kufanya, na kama haki ni za jinsia moja au za jinsia mbili. Swali kama hilo pia linaweza kuulizwa juu ya maadili, elimu adhabu, majukumu na ujumbe. Wakati wa harakati za ukombozi wa mwanamke, haikuzingatiwa iwapo, mbali na usawa na uhuru, kuna maswali mengine pia. Hapana shaka kuwa uhuru na usawa ni mambo muhimu. Lakini mambo sio haya tu. Usawa wa haki ni jambo moja, lakini kufanana kwa haki ni jambo jingine tofauti kabisa. Usawa wa haki za mwanaume na mwanamke kwa mtazamo wa thamani ya kimaada na maadili ni tofauti na kufanana kwa haki zao.

Wakati wa harakati hizi, kwa makusudi au kwa bahati mbaya, usawa umetumika kumaanisha kufanana, na hivyo ubora umefunika uwingi. Ilisisitizwa kuwa mwanamke ni binadamu, lakini ilisahauliwa kuwa ni mwanamke pia. Kwa kusema kweli, kutokujali huku hakukutokana na haraka peke yake, kulikuwa na sababu nyingine pia, ambazo zilimfanya mwanamke anyonywe kwa jina la uhuru. Moja ya sababu hizo ni tamaa iliyopindukia ya wamiliki wa viwanda waliotaka kumuondoa kutoka nyumbani kwenda kiwandani ili kuvuna uwezo wake kwa maslahi yao ya kiuchumi.

Wakiwa na malengo haya, walitetea haki za mwanamke, uhuru wake wa kiuchumi na uhuru wa usawa wa haki kama zile za mwanaume. Ni wao waliokazia utambulukaji rasmi wa madai haya. Will Durant katika sura ya tisa ya kitabu chake 'The pleasure of philosophy,' baada ya kutaja baadhi ya nadharia zenye kumdhalilisha mwanamke zilizokuwa zimebuniwa na Aristole, Neitzsche, Schopenhauere na baadhi ya maandiko (matakatifu) ya kiyahudi na kuonyesha ukweli kuwa wakati wa mapinduzi ya Ufaransa japo kulikuwa mazungumzo ya uhuru wa mwanamke, kivitendo hakukuwa na mabadiliko yoyote, anasema kuwa hadi mwishoni mwa karne ya 19 mwanamke hakuwa na haki yoyote iliyopaswa kuheshimiwa, na ambayo mwanaume angepaswa kuizingatia au ingemfanya abanwe na sheria.

Kisha anajadili mambo yaliyoleta mabadiliko katika karne ya 20. Anasema kuwa uhuru wa mwanamke ni matokeo ya ziada ya mapinduzi ya viwanda. Anaongeza kuwa wafanyakazi wa kike walikuwa ni wa gharama nafuu na waajiri walipenda kuwatumia hawa zaidi kuliko wanaume waliuokuwa jeuri (wabishi) na walikuwa ghali zaidi. Katika karne moja iliyopita ilikuwa vigumu sana kwa wanaume kupata kazi, lakini kulikuwa matangazo yaliyokuwa yanawaomba wanaume wawapeleke wanawake wao na watoto viwandani.

Hatua ya kwanza ya kumkomboa mwanamke ilichukuliwa mwaka wa 1882, ambapo sheria ilipitishwa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, wanawake wa Uingereza walipata fursa na haki ambayo haikuwahi kutokea kabla, haki ya kujiwekea fedha zozote walizopata.1 Sheria hii iliyoelezewa huafikiana na maadili matukufu ya kikristo, ilipitishwa na wamiliki wa viwanda na Bunge, ili kuwashawishi wanawake wa Uingereza kwenda kufanya kazi viwandani. Tokea mwaka huo, hamu isiyozuilika ya kujichumia fedha imewalazimisha kuhenyeka katika maduka na viwanda, na imewaondolea mzigo wa kufanya kazi za nyumbani (The pleasure of philosophy, uk. 155-159). Kutokana na maendeleo ya mitambo na ongezeko la uzalishaji ilionekana ni muhimu kwa mabepari, ili kulazimisha bidhaa zao za ziada juu ya walaji wanapaswa kutumia mbinu zote za kusikia na kuona (TV), kiakili, kihisia, kisanii na hata ngono.

Katika kuwabadilisha walaji (wanunuzi) kuwa vipengele vya utumiaji na kuwafanya wawe kama zana zisizo na nguvu katika soko la walaji, waliamua kuwatumia wanawake, lakini hawakuwatumia kama wafanyakazi tu katika mchakato wa uzalishaji pamoja na wanaume. Wao, kwa upande mwingine walitumia urembo wao, uchangamfu na mvuto wa kingono na kuwashawishi kujitolea muhanga heshima na kujistahi kwao ili kuweza kuwapotosha hao wateja na kuwalazimisha hiari zao wenyewe juu yao.

Ni dhahiri kwamba yote haya yalifanyika katika jina la uhuru kwa ajili ya wanawake na usawa wao na wanaume. Kisiasa vile vile haikurudi nyuma katika kutekeleza kipengele hiki. mara kwa mara utakuwa unasoma taarifa kama hizo katika magazeti na majarida. Mwanamke ananyonywa na huduma zake hutumiwa kutekeleza malen1. Dr. Ali Shayagan, katika kusherehesha sheria ya Iran ya kiraia, anaandika kuwa uhuru wa kumiliki mali, ambayo mwanamke anayo sasa na ambayo imetambuliwa na sheria ya Shia'h toka awali kabisa, haikupata kuwepo siku za kale huko Ugiriki, Urumi, Ujerumani na mpaka hivi karibuni hali imekuwa hivyo katika nchi nyingine nyingi. Alionekana kama mtu mdogo tu na kama kichaa, hivyo alizuiwa kumiliki mali. Huko Uingereza, ambapo mwanamke alihesabiwa kuwa sehemu ya mume wake hivyo si mtu anayejitegemea, sheria mbili zilipitishwa, moja mwaka 1870 na nyingine mwaka 1882, ambazo ziliondoa kizuizi cha mwanamke aliyeolewa kumiliki mali.

go ya wanaume chini ya joho la uhuru na usawa. kwa dhahiri kijana (wa kiume) wa karne ya 20 hawezi kukosa fursa hii ya thamani. Ili kumzuzua (mwanamke), bila kumbebesha dhamana za kawaida, na kucheza na akili yake kwa uhuru yeye (mwanaume) zaidi kuliko mtu yeyote yule, hutoa machozi ya mamba kwa ajili ya kutojiweza kwa wanawake na uonevu usio na maana dhidi yake (huyo mwanamke). ili kuwa na uwezo wa kutoa mchango mkubwa kwenye 'mwenendo huu mtakatifu' huenda mpaka kiasi cha kuchelewesha ndoa yake mwenyewe mpaka kufikia umri wa miaka 40 au hata kubakia kapera maisha yake. Hapana shaka, karne ya sasa imerekebisha malalamiko mengi ya mwanamke, lakini imeleta shida nyingi kwake. Kwa nini? Je, ameangamia daima milele na hana njia ya kufanya katika mzunguko huu?

Je, haiwezikani yeye kuondokana na shida zake zote hizi za zamani na za sasa kwa mara moja na wakati huo huo? Je, wanawake wamewekwa (kutaabika) kwenye shida hizi mbili na kwamba lazima alazimike kuchagua moja ya njia hizi mbili? Kwa kweli sio muhimu kiasi hicho kwamba apaswe kuendelea kuteseka. Alitaabika huko nyuma, zaidi hasa kwa sababu ilisasahauliwa kuwa yeye ni binadamu. Anataabika sasa hivi kwa sababu ya uwanamke wake, mahitaji yake aliyozaliwa nayo, haki zake na madai ya kawaida na vipawa vyake maalum vimepuuzwa kwa makusudi au vinginevyo.

Kinachoshangaza zaidi ni kuwa kila zinapozungumziwa tofauti za mwanamke na mwanaume, baadhi ya makundi yana tabia ya kuzichukulia tofati hizo kama kutokuwa mkamilifu kwa mwanamke na ukamilifu wa mwanaume. Fikra kama hizi zimewafanya waamini kuwa wana upendeleo fulani wa kipekee, ambao wanawake wamenyimwa. Hawaelekei kuelewa kuwa hakuna suala la ukamilifu na kutokuwa kamilifu.

Haikuwa nia ya Muumba kumfanya mmoja mkamilifu na aliyependelewa, na mwingine kuwa mbovu na aliyenyimwa. Watu wa aina hii wakiegemeza hoja zao hizi juu ya dhana zao za kushangaza za kimantiki na za busara, wanadai kwamba kwa vile maumbile yamekuwa katili kwa mwanamke, tusiongeze tusi kwenye jeraha na kwa hiyo itakuwa ni wema zaidi kuupuuza uwanauke wake! Lakini, kwa kweli ni kupuuzia nafasi ya asili ya mwanamke ambayo inasababisha yeye kunyimwa haki zake. Ikiwa wanaume wataungana dhidi ya wanawake na kusema, "Kwa vile sisi wote ni sawa, kazi zetu, majukumu yetu malipo na adhabu ziwe sawa.

Lazima mshiriki pamoja nasi katika kazi ngumu na nzito, mlipwe kutokana na kiasi cha kazi mliyofanya na msitarajie kuhurumiwa, kuheshimiwa wala kulindwa. Bebeni gharama zenu wenyewe na tutachangia gharama za matunzo ya watoto sawa kwa sawa na muweke utaratibu wa kujilinda dhidi ya hatari zote.

Mnapaswa mtugharamie kama tunavyowagharamia." Hali kama hii ikitokea, wanawake ndio watakaoumia, kwa sababu kimaumbile hawana nguvu za kuzalisha kama wanaume, wakati wao wanatumia fedha zaidi kuliko wanaume. Hedhi zao, taabu za mimba, uchungu wa kuzaa na malezi ya watoto vinawaweka katika nafasi ya kuhitaji ulinzi wa wanaume. Wanahitaji haki zaidi na hawawezi kumudu gharama kidogo. Hali hii sio kwa binadamu tu. Hata kwa wanyama wote, madume kwa silika huyalinda majike yao.

Mazingatio sahihi ya nafasi ya asili ya mwanamke na mwanaume na usawa wao na haki zao zinazofanana kama wanaadamu yanamuweka mwanamke katika nafasi hii ya raha ambapo utu wake haudharauliwi wala haiba yake haiathiriki. Ili kupata picha ya matokeo ya kupuuza nafasi asili ya mwanaume na mwanamke, hebu tuangalie wanachosema na kuandika wale ambao wamepitia njia hii kwa ukamilifu. Siku za nyuma kuna makala moja iliandikwa katika gazeti la Marekani liitwalo 'Coronet'. Linafaa kusoma. Linaelezea kisa cha mwanamke ambaye, kwa ajili ya haki sawa kati ya mwanaume na mwanamke alipoteza tahafifu aliyokuwa anapewa hapo awali. Mwanzo wanawake hawakutakiwa kunyanyua zaidi ya ratili 25, wakati kikomo hiki hakikuwepo kwa ajili ya wanaume.

Anasema sasa mazingira ya kazi katika kiwanda cha General Motors, katika jimbo la Ohio, ambapo takriban wanawake 2500 wanamenyeka, yamebadilika. Sasa anajikuta akihudumia injini yenye nguvu sana au kusafisha oven yenye uzito wa ratili 250, iliyowekwa hapo na mwanaume wa miraba minne. Anahisi kuchoka kabisa na anaona amepigika. Anasema pia kuwa kila dakika analazimika kutumia kulabu yenye kishikio cha inchi 25 mpaka 50 chenye uzito wa ratili 35. Mikono yake mara zote imevimba na inauma.

Makala baadaye inasimulia mashaka na masaibu ya mwanamke mwingine ambaye mume wake ni baharia katika jeshi la wanamaji. Hivi karibuni, Afisa wa jeshi (Admiral) aliamua kuwaingiza wanawake 40 na wanaume 480 na akawatuma kazini. Meli iliporudi baada ya safari ya kwanza, wasiwasi wa wake wa wanamaji ulithibitika. Muda si mrefu ikajulikana kwamba sio tu kwamba walifanya mapenzi ndani ya meli, lakini wanawake walio wengi walifanya mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja.

Makala inasema kuwa katika jimbo la Florida, wajane wana wasiwasi sana tangu ukombozi wa mwanamke ulipoanza kwa vile Jaji wa jimbo hili ameitangaza sheria inayoruhusu ruzuku ya dola 500 kwa wajane kuwa inakwenda kinyume na katiba kwa vile inawabagua wanaume. Makala inaongeza kuwa wanawake ni wa kwanza kuumia. Wengine pia, wakati wa zamu yao, wataonja ladha ya ukombozi.

Kwa walio wengi swali ni iwapo wanawake wamepoteza zaidi kuliko walivyopata. Haina maana kulilia maziwa yaliyomwagika. Onyesho limeanza na watazamaji wameshachukua viti vyao. Mwaka huu marekebisho ya 27 ya katiba yanakusudiwa kupitishwa na kwa mujibu ya marekebisho hayo, marupurupu yote yanayohusiana na ngono yatafutwa. Hivyo, hofu iliyoelezwa na Profesa Ruscobound, wa chuo cha sheria cha Harvad, kwamba ukombozi wa mwanamke ni chanzo cha machungu yasiyoelezeka katika medani ya sheria ya mwanamke wa Marekani yatadhihirika.

G. Irvin, Seneta wa North Carolina, baada ya kuisoma jamii ya Marekani, ambapo wanawake na wanaume wana haki sawa, anapendekeza zirekebishwe na wanaume wasiwajibike tena kutunza familia. Kwa mujibu wa makala hii, Mrs. Macdaniel anasema kuwa, kutokana na kunyanyua vitu vizito baadhi ya wafanyakazi wa kike katika kiwanda chake walipatwa na tatizo la kuvuja damu ndani kwa ndani (hemoreji).

Wanawake hawa wanataka kurudi katika nafasi zao za awali. Wanataka watendewe kama wanawake na sio kama wafanyakazi tu. Kwa wapiga kampeni wa usawa linaweza kuwa jambo rahisi. Wanakaa katika nyumba zao za fahari na kuzungumzia usawa, lakini hawajawahi kufanya kazi viwandani, ambako wanawake wengi walioajiriwa katika viwanda katika nchi hii wanafanya kazi. Mrs.

Macdeniel anasema hataki usawa huu, kwa sababu hawezi kufanya kazi za kiume. Wanaume wana nguvu zaidi kuliko wanawake. Ni bora aache kazi kuliko kushindana na wanaume. Faida ambazo wanawake wa Ohio wamezipoteza ni nyingi sana kuliko faida wanazopata chini ya sheria ya wafanyakazi.

Wanawake wamepoteza haiba yao. Haifahamiki ni nini wamekipata baada ya kukombolewa. Hali ya wanawake wachache inaweza kuwa imeboreka, lakini si wanawake wote. Hiki ndio kilikuwa kiini cha makala. Ni dhahiri kutokana na yaliyomo ndani yake kuwa wanawake hawa wamechoshwa mno na matatizo waliyosukumiwa kwa jina la uhuru na usawa kiasi kwamba wamepatwa na mzio (allergy) wa maneno haya mawili. Wanasahau kuwa maneno haya hayapaswi kulaumiwa.

Mwanaume na mwanamke ni nyota mbili kila moja ikiwa na obiti yake. "Jua halipiti njia ya mwezi wala usiku hauuzidi mchana Kila kimoja kinaelea katika Obiti (njia) yake." (36:40). Furaha yao, na pia furaha ya jamii nzima ya wanaadamu inategemea sharti kuwa kila mmoja anatembea katika obiti yake. Uhuru na usawa unaweza kuwa n a maana tu ikiwa jinsia zote mbili zitafuata njia zake za asili.

Tunaposema kwamba suala la haki za wanawake nyumbani na katika jamii litathminiwe upya na lisibakie katika uzito wa tathmini ya awali, tunamaanisha kuwa tuongozwe na maumbile na tuzingatie uzoefu uchungu na utamu tulioupata huko nyuma, hasa wa karne hii. Hapo tu ndipo harakati za wanawake zitakapokuwa na maana. Inakubaliwa na kila rafiki na adui kuwa Qur'ani Tukufu ilifufua haki za wanawake. Hata maadui wanakiri angalau kwamba Qur'ani wakati wa kuteremshwa kwake ilichukuwa hatua kubwa katika kuboresha hali ya wanamke na kurejesha haki zao za binadamu.

Qur'ani ilifufua haki za mwanamke kama mwanadamu na kama mwenzi wa mwanaume katika utu na haki za binadamu lakini haikupuuza uwanauke wake wala uwanaume wa mwanaume. Kwa maneno mengine Qur'ani haikupuuza maumbile ya mwanamke. Ndio maana kuna kuwafikiana kikamili kati ya kanuni za maumbile na kanuni za Qur'ani. Mwanamke katika Qur'ani ni sawa na mwanamke katika maumbile. Vitabu hivi viwili vitakatifu, kimoja kikiwa kimeumbwa na kingine kikiwa kimekusanywa, vinakubaliana na kuafikiana kabisa. Nia ya kitabu chetu ni kuangazia na kuelezea kuafikiana huku.

1

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

DIBAJI

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

MATATIZO YA MAHUSIANO YA KIFAMILIA.

Tatizo la mahusiano ya kifamilia katika zama zetu sio rahisi sana kiasi kwamba mtu anaweza kulitatua kwa kuandaaa kura za maoni ya vijana wa kike na wa kiume, au kwa kuendesha semina. Sio tatizo la nchi wala hakuna nchi iliyodai kulitatua kabisa. Will Durant, mwanafalsafa anayejulikana vyema, na mwandishi wa kitabu kiitwacho 'History of Civilization' anasema, "Tukijaalia kuwa tunaishi katika mwaka wa 2000 A.D na tunataka kujua tukio lililokuwa muhimu kabisa katika robo ya kwanza ya karne ya 20, tutaona kuwa haikuwa vita ya kwanza ya Dunia wala Mapinduzi ya Urusi. Lilikuwa ni badiliko la nafasi ya mwanamke. Historia haikuwahi kushuhudia badiliko la kusisimua kiasi hicho ndani ya muda mfupi kiasi hicho.

Nyumbani, ambapo ndio ulikuwa msingi wa kiuendeshaji wetu wa kijamii, mfumo wa unyumba (ndoa), ambao ulizuia ufisadi na zinaa na kuleta utengamano wa maisha ya familia, na sheria madhubuti ya maadili iliyotusaidia kuondoka katika ushenzi kwenda katika utamaduni na tabia inayokubalika ya kijamii, yote haya yalisukumiziwa mbali na badiliko hili la kimapinduzi."

Hata sasa tunapoishi katika karne ya 21, tunasikia malalamiko mengi kuliko kipindi kingine chochote kuwa mfumo wa familia unaporomka, msingi wa ndoa unadhoofika, wavulana wanakwepa kuoa, wasichana wanachukia kuzaa (kuwa mama), mahusiano baina ya wazazi hasa akina mama na watoto yanazidi kuwa mabaya, mwanamke wa dunia ya leo hana adabu, ngono ya bei nafuu inachukua nafasi ya mapenzi ya dhati, talaka zimeongezeka, idadi ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa inaongezeka, mapenzi ya dhati, heshima na uchangamfu kati ya mume na mke vinazidi kupungua.

JE TUIGE WAZUNGU AU TUJITEGEMEE?

Inasikitisha kuona kuwa baadhi ya watu wasioelewa mambo wanafikiria kuwa suala la mahusiano ya kifamilia ni sawa na matatizo ya kuongoza watalii, kuendesha taksi, kuendesha basi na kuunganisha mtandao wa mabomba ya maji na umeme, mambo yaliyotatuliwa na wazungu miaka mingi iliyopita na hivyo tukipatwa na tatizo lolote tuwaige wao mara moja. Hizi ni njozi tu. Wazungu wana matatizo makubwa sana ya kifamilia kuliko sisi. Wanataabika sana na wasomi wao ni waropokaji. Ukiacha elimu kwa wasichana, wana matatizo makubwa katika masuala mengine. Familia zao zina huzuni kubwa kuliko zetu.

KULAZIMISHWA NA HISTORIA

Baadhi ya watu wanafikiri kuwa kuporomoka na kuchafuka kwa mfumo wa familia kunatokana na ukombozi wa wanawake, ambao kwa upande mwingine ulikuwa ni matokeo yasiyoepukika ya mapinduzi ya viwanda na maendeleo ya sayansi na ustaarabu. Ni suala la kulazimishwa na historia. Hatuna njia ya kufanya isipokuwa kukubaliana na ufisadi na vurugu hizi, na kusahau furaha ya maisha ya familia tuliyokuwa tukiyafurahia huko nyuma. Kufikiri kwa staili hii ni kwa juu juu na kwa kitoto. Tunakubali kwamba maisha ya viwanda yameathiri mahusiano ya kifamilia na bado yanaathiri, lakini mambo makuu yaliyoathiri mfumo wa maisha ya familia huko Ulaya, ni mawili:

La kwanza ni mila katili na za kipumbavu, mazoea na sheria zilizokuwepo Ulaya hadi karne iliyopita. Ilikuwa ni mwishoni tu mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20 ambapo wanawake wa Ulaya walipata haki ya kumiliki mali. Jambo jingine lililochangia ni kuwa, wale waliojitolea kurekebisha hali za wanawake walichagua njia potofu. Walikusudia kuziremba nyusi zake za macho lakini walimnyima uwezo wa kuona. Mbali na maisha ya viwanda, sheria za zamani za Ulaya na mageuzi ya watu wa kisasa (modernists) yamechangia katika vurugu na mkanganyiko uliopo. Hivyo hakuna sababu inayotulazimisha sisi Waislamu kupita njia waliyopita na kuangukia katika utata na ugumu huu ambao wenzetu wameangukia.

Tunapaswa kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari na maisha ya kimagharibi. Tunapaswa kuyatazama maisha ya Magharibi kwa tahadhari. Huku tukitumia na kupata maarifa yao, viwanda vyao, mbinu zao na baadhi ya kanuni za kijamii zinazofaa kuigwa. Tunapaswa kujiepusha kuiga mila zao, mazoea (desturi) na sheria ambazo zimewaletea masaibu makubwa. Kwa mfano kurekebisha sheria za kiraia na mahusianao ya kifamilia ili ziafikiane na sheria za kimagharibi.

UHURU WA KIJAMII WA MWANAMKE

Uhuru wa kujichagulia majaliwa yake. Siku moja msichana aliyeonekana kuwa na wasi wasi na kutatizika alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kusema: "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Baba yangu amenifanyia dhulma kubwa." "Amekufanyia nini?" "Ana mpwa wake na amenioza kwake bila idhini yangu." "Kama ni hivyo, kubaliana na alichofanya na kuwa mke wa binamu yako." "Simpendi binamu yangu. Vipi naweza kuwa mke wa mtu nisiyempenda?"

"Basi hakuna kilichoharibika. Kama humpendi chagua mtu mwingine unayempenda." "Lakini pia, ninampenda sana. Sipendi mtu mwingine. Sitakuwa mke wa mtu mwingine. Lakini kwa sababu baba yangu aliniozesha bila idhini yangu, nilikuja kwa makusudi kuzungumza na wewe. Nilitaka useme hayo uliyoyasema. Nilitaka wanawake wote wajue kuwa akina baba hawana haki tena ya kuamua watakavyo na kuwaozesha binti zao kwa yeyote ambaye wao akina baba wanayempenda." Kisa hiki kimesimuliwa na fakihi mashuhuri katika vitabu: Masalik (cha Shahid Thani), na Jawahirul Kalam.

Katika kipindi cha kabla ya Uislamu, Waarabu, kama watu wengine wote wa zama hizo, walifikiri kuwa walikuwa na mamlaka kamili juu ya binti zao, dada zao na wakati fulani hata mama zao. Hawakuitambua haki ya wanawake ya kujichagulia waume zao, mtu pekee aliyekuwa na haki ya kuchagua mume wa muolewaji alikuwa ni baba au kaka, na kama hawa hawapo basi baba wadogo na baba wakubwa. Ilikuwa inafikia hatua kuwa akina baba walichagua mume wa binti yao ambaye bado hata hajazaliwa.

Mwanaume aliingia mkataba na mwanaume mwingine kuwa akizaa mtoto wa kike, basi akikua atakuwa mke wa huyu mwanaume wa pili. Ndoa kabla ya kuzaliwa. Siku moja Mtume alipokuwa katika Hija yake ya mwisho, akiwa juu ya farasi na akiwa na bakora mkononi mwake alifuatwa na mtu mmoja, mtu huyo akasema: "Nina malalamiko" "Ndiyo, sema kuna nini?" "Miaka kadhaa huko nyuma, katika kipindi cha kabla ya Uislamu Tariq bin Murqa'a na mimi tulishiriki katika vita. Wakati wa mapigano alikuja kutaka mkuki na akapiga kelele; "Je, kuna yeyote ambaye atanipa mkuki na achukue zawadi?" Nilimwendea na kumuuliza ni zawadi gani angetoa.

Akasema: angenipa binti yake wa kwanza atakayemzaa. Toka kipindi hicho miaka mingi imepita. Hivi karibuni, baada ya kuulizia, niligundua kuwa ana binti aliyekua katika nyumba yake. Nilimwendea na kumkumbusha juu ya ahadi. Lakini alirudi nyuma na kutaka mahari mapya. Sasa nimekuja kuulizia ili kuona kama mimi ni mwenye haki au yeye ndiye mwenye haki.?" "Huyo msichana ana umri gani?" "Msichana ameshakua. Mvi zinaonekana kichwani mwake." Kama ukiniuliza mimi, nyinyi wote hamko na haki. Endeleeni na shughuli zenu na mwacheni huyu msichana kivyake."

Mwanaume huyu alishangazwa na jibu hili na alimtazama Mtume mara kadhaa. Alishangaa hii ni aina gani ya fatwa. Hata kama angelipa mahari mpya na baba wa binti angemuozesha kwake kwa hiari, bado ndoa hiyo isingekuwa halali. Mtume alitazama kushangaa kwa mwanaume huyo na akasema: "Usiwe na wasi wasi. Ukifanya mambo kama nilivyokwambia, basi wewe na rafiki yako Tariq, hamtakuwa mnafanya makosa." Kubadilishana mabinti. Katika kipindi cha kabla ya Uislamu, Uarabuni kulikuwa na aina ya ndoa iliyokuwa ikipendwa ikijulikana kama ndoa ya Shighar (kubadilishana mabinti) ambayo ilikuwa ni dhihirisho la mamlaka yasiyo na kikomo ya akina baba juu ya binti zao. Mwanaume alikuwa akimuoza binti yake kwa mwanaume mwingine kwa matarajio ya yeye pia kupewa binti wa huyo mwanaume kama mke. Katika ndoa za aina hii, hakuna mke yeyote katika hawa wawili aliyepata mahari. Uislamu ulipiga marufuku ndoa za aina hii. Inafaa kuzingatiwa kuwa Mtume(s.a.w.w.) alimpa uhuru kamili binti yake Fatimah Zahra(a.s) katika kuchagua mume.

Aliwaoza pia binti zake wengine wengi, lakini hakuwanyima uhuru wao. Imam Ali bin Abi Talib(a.s) alimwendea Mtume(s.a.w.w) na kueleza nia yake ya kumposa Fatima(a.s) , Mtume alisema:wanaume wengi walimwendea Mtume, na yeye akafikisha ujumbe kwa Fatimah, lakini aligeuza uso wake pembeni, kama ishara ya kukataa. Mtume alimhakikishia Ali kuwa angefikisha ujumbe wake pia. Mtume alikwenda kwa Fatimah na kumweleza binti yake mpendwa alichotaka Ali. Safari hii hakugeuza uso wake, lakini alinyamaza kimya na hivyo alielezea ridhaa yake.

Mtume alipotoka nje, alikuwa na furaha, akasema:"Mungu ni Mkubwa!" Harakati za Kiislamu juu ya haki za wanawake. Uislamu umewafanyia wanawake mambo makubwa. Sio tu kwamba ulikomesha udhibiti usio na mipaka wa akina baba, lakini pia uliwapa wanawake uhuru, haiba na uhuru wa kufikiri na kutoa maoni. Uislamu kirasmi kabisa ulizitambua haki zake za asili. Hata hivyo, kuna tofauti mbili za msingi kati ya hatua zilizochukuliwa na Uislamu na kile kinachotokea katika nchi za Magharibi na zinazofuatwa na wengine. Tofauti ya kwanza inahusiana na saikolojia ya mwanaume na mwanamke. Uislamu umefanya na kufunua maajabu katika hili. Tutalijadili hili baadaye katika sura zinazofuatia. Tofauti ya pili ni kuwa, japo Uislamu uliwafanya wanawake wazijue haki zao na ukawapa utambulisho, haiba na uhuru, haukuwachochea kuasi na kuwafanyia uovu wanaume zao. Harakati za Kiislamu, za ukombozi wa wanawake zilikuwa nyeupe.

Hazikuwa nyeusi wala nyekundu, hazikuwa bluu wala urujuani. Hazikukomesha heshima ya mabinti waliyokuwa nayo kwa baba zao wala ya wake kwa waume zao. Hazikuvuruga msingi wa maisha ya familia na hazikuwafanya wanawake wayatilie mashaka majukumu yao kwa baba zao na waume zao. Hazikutoa mwanga kwa wanaume ambao hawajaoa ambao mara zote huwa wanatafuta mwanya wa kuwalaghai wanawake. Haukuwapokonya wanawake kutoka kwa waume zao na mabinti kutoka kwa wazazi wao na kuwakabidhi fisi wa ngono na wenye mivuto ya kilaghai ya pesa. Harakati za Kiislamu hazikufanya yale yaliyosababisha makelele na vilio katika mabahari kiasi cha mfumo wa familia kuvunjika vipande vipande.

Huko ulinzi wa akina baba umetoweka. Hakuna anayejua cha kufanya juu ya ufisadi na uchafu wa maadili uliokomaa na kuenea, juu ya uuaji wa watoto wachanga na utoaji wa mimba, juu ya asilimia 40 ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa na juu ya wale watoto wachanga ambao baba zao hawajulikani na ambao mama zao hawataki kuhusishwa na lolote juu ya watoto hao, kwa sababu hawakuzaliwa ndani ya ndoa. Akina mama wa watoto hao wanachokifanya ni kuwakabidhi watoto hao katika taasisi au mashirika ya kijamii na kamwe hawarudi tena kuwaulizia watoto wao.

Hapana shaka kwamba katika nchi yetu tunahitaji harakati za ukombozi wa wanawake, lakini tunazozihitaji ni harakati safi za Kiislamu na sio harakati za muundo wa Ulaya wenye madoa meusi. Tunataka harakati ambazo wavulana wenye ashiki watakuwa na nafasi ndogo na ambazo zinatakiwa zitokane na mafundisho bora ya Uislamu na yawe yamejengwa juu ya uelewa wa ndani na wa kimantiki wa jamii ya Kiislamu. Ruhusa ya baba Suala linalotakiwa kuchunguzwa kutokana na mamlaka waliyonayo akina baba juu ya binti zao, ni iwapo idhini ya baba ni ya lazima kwa ndoa ya kwanza ya binti yake.

Kwa mtazamo wa Uislamu baadhi ya mambo hayana ubishi. Mvulana na msichana wote wana uhuru wa kiuchumi. Kila mtu mzima mwenye akili timamu anapaswa kuwa na mamlaka ya mali zake ikiwa anao uwezo wa kuzidhibiti. Baba, mama, mume au kaka hawana mamlaka ya usimamizi au uingiliaji kati katika hili. Nukta nyingine ambayo haina ubishi ni juu ya ndoa. Watu wazima na wavulana waliokwishakua wana uhuru kamili juu ya jambo hili na hakuna mtu mwingine mwenye haki ya kuingilia. Hali hiyo iko hivi hivi pia kwa mwanamke ambaye amewahi kuolewa lakini sasa hana mume. Lakini kuna tofauti kidogo juu ya mwali ambaye anataka kuolewa kwa mara ya kwanza.

Hapana shaka kuwa baba hawezi kumlazimisha binti yake kuolewa na mtu ambaye yeye binti hajamridhia. Tayari tunajua Mtume alichomwambia yule binti ambaye baba yake alikuwa amemwozehsa bila idhini ya huyo binti. Mtume alisema ikiwa hakuridhika, anaweza kuolewa na mtu mwingine. Lakini kuna tofauti ya maoni ya wanazuoni juu ya iwapo binti anaweza kufunga ndoa bila idhini ya baba yake au iwapo idhini ya baba ni ya lazima. Kuna nukta moja ambayo haina ubishi kabisa.

Ikiwa baba atakataa kutoa idhini bila sababu ya maana, anapoteza haki yake. Mafakihi wamekubaliana kuwa katika hali hiyo binti ana uhuru wa kuolewa na yeyote anayempenda. Lakini vinginevyo, ni kama tulivyosema, kuwa mafakihi wanatofautiana juu ya nukta hii, iwapo uthabiti wa ndoa ya binti inategemea idhini ya baba au la. Wanavyuoni wengi, hasa wa siku hizi wana maoni kuwa idhini sio lazima. Lakini kuna baadhi ambao wana maoni kuwa idhini ni ya lazima.

Kwa sababu nukta hii inabishaniwa haiwezi kujadiliwa kwa mtazamo wa Kiislamu lakini inaweza kujadiliwa kwa mtazamo wa kijamii. Mwanaume anahitaji ngono, mwanamke anahitaji upendo. Msingi wa kanuni kwamba mabinti wadogo wanalazimika kutoolewa au angalau hawapaswi kuolewa bila idhini ya baba zao hautokani na kuonekana kuwa hawajakomaa ikilinganishwa na wavulana. Ingekuwa hivyo kusingekuwa na tofauti kati ya msichana wa miaka 17 ambaye hajawahi kuolewa ambaye anahitaji idhini ya wazazi wake kwa mujibu wa baadhi ya mafakihi. Na zaidi ya hayo, kama Uislamu ungekuwa unawachukulia wasichana kuwa hawajakomaa, usingetambua uhalali wa malipo wanayoyafanya (baina yao na hao wachumba kama mahari).

Mbali na hoja za kisheria, nukta hii ina falsafa maalum ambayo haiwezi kupuuzwa. Sio suala la kutokomaa au mwanamke kutokuwa na akili za kutosha. Hili linahusiana na sura maalum ya saikolojia za jinsia hizi mbili; yaani silika za mwanaume za kushawishi na silika za mwanamke za kuamini kiwepesi uaminifu na ukweli wa mwanaume. Mwanaume anahitaji ngono na mwanamke anahitaji upendo (wa dhati).

Mwanaume huelemewa na hamu na uchu wa kufanya mapenzi, wakati mwanamke kwa mujibu wa wanasaikolojia, ana uwezo mkubwa zaidi wa kudhibiti na kuficha matamanio yake. Ni sauti tamu ya mapenzi, udhati na uaminifu ambao humzidi nguvu mwanamke na kumfanya apige magoti. Hiki ndicho tunachomaanisha tunaposema tabia ya mwanamke ya kumwamini mwanaume kiwepesi. Hivyo pindi mwanamke anapokuwa kigoli na hana uzoefu na wanaume, anaweza kushawishika kirahisi na nyimbo (za mwanaume) za kimapenzi kirahisi.

Profesa Reek, mwanasaikolojia wa kimarekani, anasema kwamba sentensi tamu na nzuri kabisa ambayo mwanaume anaweza kumwambia mwanamke ni 'Mpenzi ninakupenda' Anasema bahati kwa mwanamke ina maana kuwa na uwezo wa kuuteka moyo wa mwanaume kwa maisha yake yote. Mtukufu Mtume, mwanasaikolojia aliyefundishwa na Mwenyezi Mungu, alieleza wazi wazi ukweli huu miaka 1425 iliyopita. Amesema kwamba mwanaume akielezea upendo wake kwa mwanamke, mwanamke huwa hasahau sentenzi hiyo.

Wanaume wenye nia ya kuwarubuni wanawake, hutumia hisia ya wanawake (ya kupenda kuambiwa wanapendwa) kwa maslahi yao. "Nitakufa kwa ajili yako' ndio maneno yao ya kuwashawishi wasichana ambao hawana uzoefu na wanaume. Hii ni sababu muhimu kwamba msichana ambaye hana uzoefu na wanaume apate idhini ya baba yake kabla ya kuoelwa. Akina baba wanazijua akili za wanaume vizuri zaidi na mara nyingi huwatakia binti zao mema. Katika hali hii, sheria haijamdharau mwanamke, lakini imechukua hatua kuyalinda maslahi yake (mwanamke).

Kuibua pingamizi dhidi ya ulazima wa kupata idhini ya baba ni kwa ovyo zaidi kuliko kuuliza kwanini idhini ya baba au mama haijafanywa lazima kwa upande wa wavulana. Ninashangaa kwanini watu ambao kila siku wanashuhudia uovu wa mapenzi holela kati ya wavulana na wasichana, bado wanashauri wasichana wawaasi na wasiujali ushauri wa walezi wao. Kwa mtazamo wetu hii inatokana na hila na njama zinazofanywa kati ya wale wanaodai kumhurumia mwanamke na wale wanaowarubuni. Wa kwanza anamtengenezea mazingira mazuri huyu wa pili na kazi yao inakuwa nyepesi. Wasichana wana mamlaka kamili juu ya ndoa zao. Ila uthabiti wake tu ndio unaegemea idhini ya baba, maadamu baba mwenyewe hatazuia idhini kwa nia mbaya au kwa sababu hana uwezo wa kutoa hukumu sahihi bila sababu yoyote ya maana. Je kuna tatizo lolote juu ya kanuni hii, au inaweza kuonekana kwenda kinyume cha dhana ya uhuru wa binadamu? Ni tahadhari tu kwa ajili ya kulinda maslahi ya wasichana wasio na uzoefu na imejengwa juu ya dhana ya asili ya kutoaminika sana ya wanaume. Kwa mtazamo huu hakuna pingamizi linaloweza kutolewa dhidi ya sheria ya Kiislamu.

Kinachoweza kupingwa ni mila iliyoenea miongoni mwa Waislamu. Akina baba walio wengi bado wanafikiri kuwa wana mamlaka kamili na wanaona kuwa ni kinyume na stahili yake, ikiwa msichana atatoa maoni yake juu ya uchaguzi wa mwenzi wake katika maisha, ambaye atakuwa baba wa watoto wake atakaowazaa baadaye. Hawazingatii ukomavu wa kiakili wa msichana, ambao kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, ni wa umuhimu mkubwa na usioweza kuepukwa.

Ndoa nyinyi zinazofungwa kabla wasichana hawajakomaa, kisheria ni batili. Mara nyingi hawazingatii ukomavu wa msichana, kuvunja ungo tu kunaonekana kutosheleza. Lakini tunajua walichoandika mafakihi wakubwa juu ya kupima ukomavu wa kiakili wa wasichana. Baadhi ya mafakihi wanazingatia kuwa ukomavu wa kidini ni sharti muhimu la ndoa. Wanashikilia kuwa ni wale wasichana tu wanaojua kanuni za dini kwa mantiki na ushahidi ndio wanaofaa kuolewa. Kwa bahati mbaya, wengi wa walezi na wale wanaosimamia sherehe za ndoa, hawazingatii masharti haya. Tunaweza kuona kuwa katika hati za zamani za ndoa maneno 'mtu mzima, mwenye akili timamu na aliyekomaa yalikuwepo pamoja na majina ya bwana harusi na bibi harusi. Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria ya Shia, mwanamke mtu mzima na aliyekomaa na ambaye amewahi kuolewa huko nyuma, hahitaji idhini ya baba.

2

MUANDAMO WA MWEZI

SURA YA PILI

JAWABU KWA WANAFUNZI WA BACHOO JAWABU YA UTANGULIZI

Wahusika ndugu zetu wa Masjid Al-Sunna Zanzibar, wameanza kitabu chao hicho kwa utangulizi wenye kumshukuru na kumuhimidi Allah na kumtakia rehema na amani Bwana wetu Muhammad (s.a.w.) kama zilivyo khutuba na vitabu vya kiislamu. Na hayo yote yamefanyika chini ya utangulizi wenye anwani:

UKWELI JUU YA KUANDAMA KWA MWEZI

Na hii ndio sehemu ya kwanza ya kitabu chao. Wakasema katika utangulizi huo: Msisitizo wetu mkubwa katika kitabu hiki ni ile nukta muhimu ya kwamba suala la kufunga na kufungua kwa muandamo mmoja kwa dunia nzima si jambo jipya kama wanavyodhani baadhi ya watu, ni jambo la kale mno ambalo linaweza kutekelezeka na kwamba huo ndio uliokuwa msimamo wa 'Jamhur' ya wanavyuoni.

Jawabu Nakubali kuwa hili ni jambo la zamani, lakini kudai kuwa hii ni kauli ya Jumhuri ni madai hewa: hayana ushahidi. Leo hii duniani hakuna madhehebu yoyote ambayo inaitendea kazi kauli hio kama ni madhehebu nzima, bali kuna baadhi ya watu tu katika kila madhehebu ambao wanafata kauli hio. Hata zile madhehebu ziliotajwa kuwa ni zenye kufata kauli hio kama vile Malik, Hanbal na Hanafi, basi hawaitendei kazi kauli hio ila baadhi yao tu. Libya, Algeria na nchi nyengine za Afrika Kaskazini na Magharibi - kwa mfano - ni nchi za wafuasi wa madhehebu ya Malik, nao wanafata miandamo yao wenyewe. Kwa hivyo, dai kuwa hii ni kauli ya Jumhur ya wanavyuoni, si dai sahihi.

SEHEMU YA PILI

Katika sehemu ya pili, ndugu waandishi wanasema:

2. Si Fikra Za Shaykh Naaswir Bachuu "Ndugu yetu Juma Muhammad Rashid Al-Mazrui amejitahidi kuandika kitabu alichokiita: "Ushahidi Uliowekwa Wazi Katika Suala La Miandamo Ya Mwezi. Makusudio yake yalikuwa ni kutaka kukijibu kitabu kilichoandikwa na Shaykh Naaswir Abdullah Bachuu kinachojulikana kwa jina la "Ufafanuzi Wa Mgogoro Wa Kuandama Kwa Mwezi."

Jawabu Kidogo na mimi naomba niweke wazi kwamba kitabu changu hakikuwa kabisa na lengo la kujibu kitabu cha Sheikh Nassor Bachoo. Hili la kunukuu maneno yake na kuyajadili lilikuwa ni jambo la kutokea tu baada ya mtu Fulani kuniletea kitabu chake. Kwa havyo, kama mulivyosema nyinyi katika kitabu chenu kwamba: Kitabu hiki ni kama nasaha kwa Waislamu wote ili kuweza kudumisha umoja wetu hususan pale ambapo pamejitokeza misimamo tofauti katika mambo ya ibada. Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili.

Basi na mimi nakuombeni munielewe hivyo hivyo, kwamba wakati mimi naikubali fikra Fulani na kuikataa fikra Fulani, hakuna budi ninukuu fikra pinzani na kuonesha kwanini siikubali; na kwa upande wa pili ni lazima nioneshe kwanini naikubali fikra ninayoikubali. Na nitaposema kuwa kuna watu wana fikra hii, basi nadhani haitokuwa jambo la busara kama watu hao sikuwataja na nikiwataja ni lazima nitaje marejeo. Kwa sababu hii ndio maana nimekuwa nikinukuu maelezo ya Sheikh wetu Nassor Bachoo na kumjadili mule nisimokubaliana naye. Naomba musihuzunike kwani kujibizana katika kutafuta ukweli ni suala mashuhuri katika uwanja wa elimu. Wanavyuoni wakubwa wa kale na wa sasa wamekuwa wakijibizana ili kutafuta ukweli na hatimae huwabainikia woa pamoja na wasomaji. Kwa hivyo, hamukuwa na haja ya kutumia lugha: "Wala hapakuwa na lengo la kumkashifu": hii si kashfa hata kidogo: hii ni elimu.

Lakini, hakuna haja ya kufichana; kitabu chenu mumeandika kwa kujibu kitabu changu. Hamuna haja ya kusema: "Wala lengo la kitabu hiki sio kuendeleza malumbano baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe hata kwa wale wenye misimamo tofauti. Kutajwa ndugu yetu Juma Muhammad Rashid lilikuwa ni jambo lisilobudi wala hapakuwa na lengo la kumkashifu au kumuumbua bali ni kutokana na kuwa hapakuweza kupatikana njia mbadala kwa vile ameshaandika kitabu ambacho ameshakichapisha chapa ya kwanza na ya pili", kwani kitabuchenu kimeanza kwa kunitaja mimi mwanzo hadi mwisho na kuniaga kwa kunipa nasaha mimi. Ama mimi naandika jawabu hii kukujibuni nyinyi: sikufichini wala sisemi uwongo.

Munasema Kutokana na jambo hilo , sisi kwa upande mmoja tunashukuru kwa juhudi yake hiyo na kwa upande wa pili tunatuma masikitiko yetu kwake kwa kutokuwa makini na muadilifu katika kulifafanua jambo hilo muhimu. Kwani kitabu chake hicho kimeandikwa katika mfumo wa chuki, kibri, kejeli na malumbano huku akisisitiza kwa mara nyingi kauli chafu ambazo muandishi hapaswi kuzitumia katika kitabu au katika mijadala ya Dini. Jawabu Hizi chuki, kibri na kejeli, mimi nimezisoma kwenu, kwa hivyo na iwe kama msemo wa Waswahili: "Papa akipea mafuta huwapa wanawe". Je nyinyi munayakumbuka haya:

1) Munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo ambao alisema kuwa wasionyanyua mikono katika sala wanasali kama mipopoo? Jamani! Hii si kejeli? Je katika nyinyi yuko aliyetoa muhadhara au kuandika kitabu ili kumjibu Sheikh wetu. Sasa uadilifu uko wapi?

2) Je munaukumbuka muhadhara wa Sheikh Bachoo aliozungumzia mas-ala ya udhu kasha akasema: "Wengine wakitia udhu kiungo hiki huomba dua hii na kiungo hiki huoma dua hii; upumbavu mtupu". Je haya si matusi? Je hii si kejeli?

3) Siku moja palikuwa na maziko. Maiti alisaliwa msikiti wa wajiitao "Watu wa Sunna". Kijana mmoja akasimama akasema: "Leo tunataka kukuonesheni vipi Mtume (s.a.w.) kamsalia maiti: si kama wanavyofanya Ibadhi na Shia.

4) La nne ni kuwa ikiwa nyinyi mumethubutu kunita mjeuri, mwenye kibri na kejeli; maneno ambayo mimi sikukwambieni wala kumwambia Sheikh Nassor; mimi nimemtoa makosa tu Sheikh wetu: na hii ni kawaida katika uwanja wa elimu; sasa je na nyinyi pia ni majeuri, wenye kibri na kejeli? Katika uwandishi wenu, pia mumesema: "Hatujui dhana hii potofu ameitoa wapi." Mwenye dhana potufu naye ni mpotufu, kwa hivyo na nyinyi hamukutoa nasaha bali mumetukana. Nakupeni mifano hii mitatu ya Sheikh wetu na mmoja wenu nyinyi wenyewe enyi wenye kuandika Radan mardudan na mifano iko mingi. Inatosha kuwaita kwenu watu wengine kuwa ni watu wa bidaa na nyinyi ndio watu wa Sunna. Kwa hivyo, hii hali mumeiuda nyinyi wenyewe: Zanzibar bali Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla haikuwa hivi. Chuki mumeziunda nyinyi; mukijirekebisha kwa kutumia lugha nzuri nadhani hakuna atayekwambieni jambo kwa lugha nzito.

Mnasema Mfano wa kauli zake mbaya ni kama zifuatazo:

(vuta-nikuvute) [uk. 6]

(hii ni ajabu katika ajabu za dunia!) [uk. 124]

(Kwa hivyo, uwezekano huo alioutoa Sheikh hauwashi wala hauzimi [uk. 124]

(Ninasema: Enyi walimwengu wenzangu tazameni hoja za kielimu hizo!!!!!!! Kwani nyinyi Wazanzibari kabla ya kuja fikra hio ya Sheikh Nassor Bachoo ya kufunga kwa muandamo mmoja,)

(Utaona kwamba masuala yote haya si yenye kima katika soko la elimu, bali ni masuala ya kuwababaisha watu wasiojua nini cha kujadiliwa katika mas-ala haya ya funga) [uk. 167]

(Hoja nyengine - nayo pia ni hoja ya mitaani - ni kuwa watu wengi wa kawaida wanapouona mwezi mkubwa husema: "E basi ule ndio mwezi wa leo ule?!!!")

(Jawabu hii ya mwisho, inaufanya upinzani mzima wa Sheikh Bachoo kuwa hauna maana yoyote.) [uk. 132]

(Kwa ufupi ni kuwa hicho walichokidai watetezi wa rai pinzan) [uk. 32]

(utaona jinsi gani mwanamume alivyokuwa bingwa wa kubadilika! Na hili si jengine bali ni lile Waswahili wanalolisema: "Mfa maji hukamata maji.") [uk. 128]

(Hakuna hapa kinachoonesha mas-ala ya kufunga kwa muandamo mmoja wala kumi na moja.)) [uk. 125] (haina maana kwamba usiku ukiingia sehemu moja ndio umeingia dunia nzima. Kwa ufupi ni kuwa hii ni hoja ambayo haina faida yoyote ya kielimu, lakini tunaijadili kwa ajili ya watu wa mitaani tu.)

Jawabu Sikubaliani na nyinyi kwamba humu muna maneno mabaya. Lakini hata nikikubali basi nasema kwamba lugha ya namna hii sababu ni nyinyi, na kwa hivyo, utaona kwamba ninapojadiliana na watu wengine basi lugha yangu hubadilika. Kwa hivyo, tujirekebisheni sote na tujadili tafauti zetu kwa lugha ya kiungwana. Ama ukinita mpopoo, basi usinilaumu na wewe nikikwita mnazi: unanilaumu nini na wewe unakifanya kile kile nikifanyacho?! Bali hata katika kitabu hiki munachonijibu, basi nanyi mumetumia lugha hizo hizo. Katika baadhi ya sehemu umesema: "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti..". Na mwishoni mwa kitabu mumesema: "Dhana ya pili ya ndugu Juma imejengeka katika msingi dhaifu wala haina nafasi katika uwanja wa fani (kitaalamu) nao ni kule kusukuma kwake juu ya elimu ya Jiografia". Na yamo mengi katika kitabu chenu. Sasa nyinyi mwasema nini na mwatenda nini?

Munasema "Kwa hakika katika kitabu chake hicho kwenye uk 6, anajionyesha alivyo na kauli mbili tofauti: Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi i likuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini? Na ni nani aliyemwambia kwamba jambo lenye khitilafu halizungumzwi? Yeye angezungumza nini katika kitabu chake kama si masuala ya ikhtilafu? Pia anatwambia haya ni katika mambo ya furui (matawi) za Kidini, kwa hivyo zisizungumzwe. Kwani ni nani aliyemwambia kuwa furui za Kidini hazizungumzwi?"

Jawabu Ikiwa lugha hii ndogo hamukuweza kuifahamu, vipi mutaweza kufahamu kitu chenye kuhitaji fani za lugha na usuli na mengineo. Ikiwa mimi niliingia msikitini kwenu Raha Leo nikakuta juu ya ubao wenu munawasomesha vijana na katika darsa hio Mubtadaa mumemwita Fa'il (vipi mutaweza kujadili masuala haya?!!! Mimi nimempongeza Sheikh Bachoo kwa juhudi au moyo wake; na sikumpong eza kwa kulikuza suala ambalo:

1) Ni la furuu'i

2) Lina khilafu. Na hii haina maana kuwa Furu'i zisizungumzwe; suala la Furu'i huwa halishadidiwi; bali unawaacha watu kama walivyo tu. Lakini yeye anapenda kushadidia katika mas-ala kama haya; ndio maana akashadidi hata katika suala la kufunga mikono hata kuwaita watu mipopoo bali na kuwambia kuwa hawana Sala. Kwa hivyo, nieleweni kwamba ninachokipinga ni kushadidia au kuwakoroga watu katika kitu ambacho ni furu'i za dini ilhali yeye kawakuta na msimamo tafauti tangu zamani. Katika mas-ala ya furu'i, wanavyuoni huwa hawashadidi juu ya Mas-ala kama haya. Mimi leo nikisimama nikaanza kufanya kampeni kwamba watu wasiitikie amina wa kisali, nalo ni jambo la furu'i, si nitakuwa natia fitna tu? Jambo kama hili huwachwa wasomi wakalitafiti kaiha kila mmoja akafanya vile ilivyombainikia. Lakini kufanya kampeni maalumu na da'awa kana kwamba waliotangulia wote ni wapotovu, hili ndilo jambo la kulaumiwa.

Ama kauli yenu: "Kwanza anakubali kwamba suala la muandamo wa mwezi lina ikhtilafu katika kufunga kwa kumuelezea Shaykh Naaswir Bachuu kwamba: (Tunampongeza kwa juhudi) Kisha pale pale anageuka kwa kusema: (madamu hili ni suala la khilafu - basi ilikuwa ni kutolizungumza kabisa,) Sasa hebu tumuulize ndio anapongeza nini?" Mwisho wa kunukuu. Na mimi nikuulizeni nyinyi mumenishukuru kwa juhudi yangu kisha mwisho wa kitabu mukaniambia: "Mwisho tunachukua fursa hii kumuonya ndugu Juma kuwa amuogope Mwenyezi Mungu hususan katika mas-ala ya kielimu. Akumbuke kuwa Mwenyezi Mungu Ameonya juu ya mtu kusema jambo au kufanya asilolijua. Aelewe kwamba ataulizwa juu ya hilo. Lingekuwa jambo la busara kama ndugu Juma angalikubali kuuliza na kufanya utafiti zaidi juu ya mas-ala haya kama agizo la Mwenyezi Mungu linavyotutaka". Sasa na nyinyi munanishukuru nini?

Munasema "Sisi tunapenda kumfahamisha kuwa suala hili la kwamba mwezi ukiandama sehemu moja unatosheleza kufuatwa kwa kufunga au kufungua ulimwengu mzima, si suala jipya bali ni jambo la kale. Tunasikitika kwamba hakuangalia vizuri maoni ya Wanavyuoni wakubwa walivyoelezea msimamo huo. Angalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 51-58. Hapa tunanukuu baadhi ya kauli hizo:

Imamun-Nawawy aliyekisherehesha Kitabu cha Sahihi Muslim anasema:

"Na jambo lililo sahihi kwa wenzetu (Mashaffi) ni kuwa muandamo mmoja hauwahusu watu wote bali unawahusu wale walio karibu kwa kiasi ambacho hawaruhusiki kupunguza Sala (Sala ya safari). Pia imesemwa kuwa iwapo matlai ni mamoja watalazimika (watu) kufunga pamoja. Pia imesemwa kuwa ikiwa (wanaishi) katika eneo la Iklimu moja (maili 72 au km 89) (watalazimika kufunga pamoja) vyenginevyo kila mmoja atafunga kwa muandamo wake. Na wakasema wenzetu wengine (Mashaffi) kuwa muandamo katika sehemu moja utawahusu wote wa dunia nzima".

Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar katika kitabu chake "Bayaanullinnas" J. 2 uk 203 - 204 ameandika yafuatayo juu ya kauli hiyo ya Imamun-Nawawy:

"Hapa Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasari kauli zilizomo katika madhehebu ya Kishaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu mengine ya Kiislamu. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika maf ungu matatu makuu: "...Hapo Imamu An-Nawawy ametaja kwa mukhtasar kauli zilizomo katika madhehebu ya Shaffi (juu ya kuandama kwa mwezi) na ambazo pia zimo katika madhehebu nyengine za Kiislam. Kauli hizo tunaweza kuzigawa katika mafungu matatu makuu: Kauli ya kwanza: "Kila nchi iwe na matlai yake, wala muandamo wa nchi moja hautalazimu nchi nyengine ya mbali wala karibu". Kauli ya pili: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi zote za dunia hata kama ziko mbali".

Kauli ya tatu: "Muandamo wa nchi moja unalazimu nchi iliyo karibu nayo au inayowafikiana kimatlai". Kisha, Shaykh Jaadul-Haq akaendelea kusema kwamba:

"Na (kauli) zote hizo ni maoni yatokanayo na Ijtihaadi ambazo hazikusimama juu ya hoja kat-ii, si sanad wala matni. Kwa hivyo ingefaa ichaguliwe kauli ambayo inakubaliana na maslahi ya (Waislam wote wa) dunia nzima kwa jumla"."

Jawabu Sikubaliani na mtazamo wa Sheikh Shaykh Jaadul Haq wa chuo kikuu cha Al-Azhar, kwamba zote hizi ni rai na itihad kwani kanuni ni kuwa "Hakuna ijtihadi mbele ya andiko" Ijtihad mwahala mwake ni musimo andiko. Wakatika katika suala hili, utaona kwamba asemaye kuwa tufunge kwa muandamo mmoja, hoja yake ni Hadithi "Fungeni kwa kuuona"; na anayesema kuwa kila mahala na muandamo wake, anatoa ushahidi wake ni Hadithi ya Ibn Abbaas na Kuraib. Kwa hivyo, ijtihad ni katika kuyafahamu maandiko: si ijtihad kwa maana ya rai tupu pasi na andiko kama alivyosema Sheikh. Kilichobaki ni kuzijadili riwaya mbili hizi zina maana gani?

Munasema Tungependa kumueleza ndugu yetu kwamba hata hapa Afrika ya Mashariki jambo hili hakulianzisha Shaykh Naaswir Bachuu kama alivyodai mwenyewe (Nd. Juma) kwamba: (Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro)) Inasikitisha hakuweza kuangalia katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu uk 161-163 wametajwa walioonyesha kwa vizuri kabisa misimamo hiyo tofauti. Mashaykh wenyewe ni hawa wafuatao: Al-marhuum Shaykh Juma Abdul Waduud (wa Zanzibar), Shaykh Abdillahi Naaswir ( Nairobi Kenya ), na Shaykh Naaswir Khamis Abdul Rahman ( Mombasa Kenya ).

Jawabu Kwani wapi katika kitabu changu nilisema kuwa Sheikh Nassor Bchoo ndiye aliyeanzisha fikra hii hapo Afrika ya Mashariki hata mukaleta dai hili? Mimi nimeeleza kuwa zamani Afrika Mashariki watu wote wakifata muandamo mmoja. Nilisema: Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo. Dr. Ramadhan Al-butti - miongoni mwa wanavyuoni wakubwa wa ulimwengu wa sasa - anaona kwamba harakati hizi hazisifiki kama ni madhehebu: bali ni hatua (phase) katika mapito ya Historia.

Na katika uk. 97, nimesema:

Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya. Kwa hivyo, ni wazi kwamba mimi nazungumzia Afrika Mashariki. Na mfano wa hilo pia kalisema Sheikh Nassor Bachoo, lakini yeye hamukumjibu. Anasema: "Pamoja na kuwa mgogoro wa kuandama kwa mwezi umeanza kuonekana hadharani katika jamii za Waislam wa hapa Afrika ya Mashariki katika miaka ya hivi karibuni". Inasikitisha kwamba hata maneno yangu mumeyakata na kuchukua yale ambayo hayakamilishi maana nilioilenga. Maneno "Karne zimepita" hamukuyataka kwani hayakufikisheni kule mutakako!

Pili narejea tena kusema kwamba hao wanavyuoni aliowataja Sheikh Nassor, hawajathibitisha habari za kuwa watu wafunge au wakifunga kwa muandamo mmoja Africa Masharik, ukimtoa Sheikh Nassir Khamis wa Mombasa ambaye naye pia ni mtu wa sasa. Ama sheikh Juma Abdu-Wadood yeye, kwa mujibu wa nakala hio ya Sheikh Nassor Bachoo, kasema hivi: Kuona huku kwa mwezi kumekusudiwa kuonekana na Waislam, na kuonekana na Waislamu huko, sio lazima kuonekana na Waislamu wote. Bali inatosha shahada ya mtu mmoja muadilifu".

Pia inampasa mtu mmoja pekee kama ameuona mwezi yeye afunge na kila aliyemuamini; hata akiwa haijakubaliwa shahada yake. Haya ndio maneno ya Sheikh Juma Abdu-Wadood kwa mujibu wa alivyomnukuu Sheikh Bachoo. Sasa ikiwa ndugu zetu mumeshindwa kuyafahamu maneno haya ya Sheikh Juma Abdu-Wadood, bado mutaendelea kupoteza watu bila ya elimu?! Sheikh Juma Abdul-Wadood hapa anazungumzia mas-ala ya ushahidi kwamba si lazima - katika suala la kuonekana kwa mwezi - kwamba kila mmoja auone: bali akiona mtu mmoja basi inatosha kwa wengine kufunga. Hii ndio kauli ya Sheikh Juma Abdul-Wadood na hili nimelieleza kwa urefu katika kitabu changu.

Kisha Sheikh Juma Abdul-Wadood akazungumzia suala la kufunga kwa muandamo mmoja akasema: "Rai za Maimamu wengine wameifasiri hadithi isemayo: (Fungeni kwa kuuona Mwezi) kwamba ukionekana popote mashariki au magharibi (watu) wafunge; hapana kutazama masafa fulani au nini. Hii ni rai nayo na wengi wamesema (hivyo) kama Imamu Malik , Ahmad na kundi kubwa la Hanafi. Inakurubia kuwa n dio rai ya Jamhuri - kufata rai hii ni kuhakikisha umoja wa dunia nzima. Wala hatuwezi kusema kwamba rai ya Shaffiy ndio ya Jamhur". Hapa Sheikh Juma anasimulia rai za Maimamu wengine: si rai za Maulamaa wa Afrika Mashariki. Mimi dai langu nililodai ni kuwa jambo hili la kufunga kwa muandamo mmoja, napenda munifahamu: ni jipya kwa Africa Mashariki. Mimi sikusudii jambo la wanazuoni kuzungumzia rai mbali mbali: bali nazungumzia jambo la watu kufata muandamo mmoja kwamba karne zimepita ya sikio la Muafrika Mashariki wa Kawaida halijiapata kusikia. Na nimetumia maneno "Muafrika wa Mashariki wa kawaida" ili kuwatoa wanavyuoni wao hata kama walikuwa hawafati kauli hio, lakini wanaijua. Kwa hali yoyote ile:

1) Sheikh Juma Abdul-Wadoo hajazungumzia kwamba Afrika Mashariki watu walikuwa wakifunga au wafunge kwa muandamo mmoja, bali kazungumzia rai za wanavyuoni wasio wa Afrika Mashariki - Al-Imamu Shafi, Hanbal n.k. Na mimi sijakanusha tafauti hizi.

2) Kauli yake ilikuwa ni kuhusu suala la mashahidi.

Ama Sheikh Abdillahi Nassir, yeye ni mwanachuoni wa sasa. Na mimi sijasema kuwa sasa hakuna rai hizo. Pili ni kuwa nakala alizotupa Sheikh Bachoo za kitabu cha Sheikh Abdillahi utaona kwamba Sheikh Abdillahi hazungumzii kuwa kauli ya kufatwa ni ile ya muandamo mmoja; bali yeye kasema kuwa hili ni suala la khilafu kwa hivyo tusigombane kila mtu afate rai anayoiona kuwa ni sawa. Sheikh Abdillah kayasema haya baada ya kutokea mizozo hii ya sasa. Kwa hivyo tunarudi pale pale kwamba "Karne zimepita bila ya sikio la Muafrika wa Mashariki wa kawaida kusikia sauti ya mgogoro juu ya suala la muandamo wa mwezi. Harakati za elimu zilipobadilika na kuelekea zaidi - kwa kujua au bila kujua - katika mrengu wa Kihanbali na Kiwahabi, pakajitokeza mapinduzi ya ghafla ya fikra na matendo". Kwa hivyo, nukta hii hamukuuijibu: na wala sioni kuwa kuna haja ya kuijibu kwani haina umuhimu katika maudhui yetu. Bali kitabu chenu chote, munachagua mambo yasio na umuhimu "Juma kantutukana; Juma kanfanya hivi" nyinyi ndio munajibu baada ya kuzungumzia dalili za kielimu.

Ama Sheikh Nassor: yeye pia ni mtu wa sasa na ni mfuasi wa skuli hio hio munayoifuata nyinyi, kwa hivyo kusema kwake alivyosema hakujapindua nilioyasema kuwa - kimatendo - hili ni suala jipya kwa kwetu Afrika ya Mashariki. Wala mimi sikusema kuwa Sheikh Nassor Bachoo ndiye muasisi wa fikra hio huko kwetu. Naomba munifahamu ninachokisema kwanza kisha ndio munijibu. Na sijui munapinga nini kitu ambacho watu wote wanakijua. Bila ya kusahau kwamba mimi sikusudii kusema kuwa kitu sahihi ni kilichofanywa zamani au kilichofanywa leo: laa! Bali kitu sahihi ni chenye ushahidi sahihi uliojengeka juu ya misingi sahihi ya kielimu. Na kielimu, suala la kuzingatia muandamo mmoja - hamutoweza kulithibitisha.

MNASEMA

Pia Shaykh Ahmad Al Khalil, Mufti wa Omani amethibitisha kwamba Ikhtilaf hii ya muandamo wa mwezi katika hukmu ya kufunga au kufungua ipo na kwamba ni jambo la kale. Kama alivyosema maneno yake yaliyotafsiriwa na Shaykh Muniir Sulayman 'Aziz kwamba: "Hakuna madhehebu iliyokuwa imesalimika na kuwa na Khitilafu baina ya Wanavyuoni wake juu ya suala la kutafautiana miandamo ya mwezi." Jee ndugu Juma anataka kusema kwamba Shaykh Naaswir Bachuu ndiye mwalimu aliyeanzisha madhehebu zote? Au ndiye aliyeanzisha mtafaruku huu kama alivyouita mwenyewe ndugu Juma?

JAWABU

Suala hilo jiulizeni wenyewe; mujijibu wenyewe; kwani nyinyi ndio mulioliunda: mimi sikusema hivyo kamwe bali nilichokisema ni hiki: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nami sikusudii kusema kwamba upya huo ni katika kuzungunzwa au kusomwa suala hilo katika vitabu; nakusudia kimatendo sula hili lilikuwa halipo Afrika Mashariki. Sasa ili muwe mumenijibu, twambieni nani alikuwa akifata muandamo mmoja hapa Afrika Mashariki. Jamani! Tafuteni hoja mujadili: musijadili kitu kisichokuwa na umuhimu. Kama hamuna hoja nyamzeni musijitie aibu!

MNASEMA

Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani; Ndugu Juma anasema: (Kama tunavyojua kwamba Sheikh Nassor Bachoo, ni mmoja wa wenye kusisitiza ulazima wa kuwa na muandamo mmoja.) Sisi kwa upande wetu tunasema: Katika kitabu cha Shaykh Naaswir Bachuu hakuna pahala alipolazimisha watu wafuate huo aliouita ndugu Juma (msimamo wa Shaykh Naaswir). Bali yeye ameonesha mitizamo ya Wanavyuoni kwa kutumia Aya za Qur-aan, Hadiythi na vitabu vinavyokubalika. Lugha aliyotumia Shaykh Naaswir katika huo unaonekana ni msimamo wake ni maneno yaliyozimuliwa kilugha (polite language) kama vile: (inawezekana) ((inaonyesha) .

JAWABU

Na mimi hapa sijasema kuwa Sheikh Nassir Bachoo kalazimisha watu wafunge kwa muandamo mmoja. Nimesema "Anasisitiza ulazima" yaani yeye analingania msimamo huo kwani kwake ndio msimamo sahihi na ndio wajibu kuufata. Naomba tena tuelewane musiseme kitu kinyume na nilivyosema. Wala musitafute kitu kisicho na maana mukajadili eti ndio jawabu! Pili maneno yenu: "Katika kudhihirisha udhaifu wake wa kumuandama mtu fulani". Sasa je na nyinyi pia munaonesha udhaifu huo huo kwa kumuandama mtu fulani katika kitabu chenu?

MNASEMA

Aliyelazimisha rai ni ndugu Juma mwenyewe kama anavyosema: (Lakini kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali) [uk. 112]

JAWABU

Bali hata Sheikh Bachoo pia kalazimisha kwani ukidai kuwa huu ndio msimamo wa haki au ndio msimamo sahihi au ndio wajibu kufatwa, bila kusema kuwa rai zote zinafaa basi na wewe huwa umelazimisha rai yako. Sasa je Sheikh Bachoo anakubali hivyo kuwa rai zote ni sawa? Mimi kweli sisemi kuwa rai zote ni sawa: nasema kuwa nyinyi mumekosea na sahihi ni kinyume na munavyofanya, na kwa hivyo bado nipo katika msimamo wangu huo huo kwamba: "Kilicho lazima na ambacho tunatakiwa tukubaliane ni kuwa muandamo wa mbali hautendewi kazi mbali".

MUNASEMA

"Kisha katika uk 85 ndugu Juma anataja kwamba msimamo huu wa muandamo mmoja kwa dunia nzima ni ((kitu kipya)) na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu baada ya kutaja baadhi ya nchi zinazofuata miandamo yao - yaani kila nchi na muandamo wake kama Al-yaman , Oman , Misri na Saudia. Kisha hapo hapo akataja: ((isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.)) Inafaa ndugu Juma aulizwe masuala yafuatayo:

i) Kama ni jambo lisilotekelezeka vipi tena Imarat wanalitekeleza?

ii) Je hawa wa Imarat nao ni wanafunzi wa Shaykh Naaswir Bachuu?

iii) Kwani hiyo sio kauli ya Jamhuur ambayo ndio msimamo wa maimamu wakubwa wakiwemo Ahmad bin Hanbal, Malik na Abu Hanifa? (Angalia pia sehemu ya 11 na 13 za kitabu hiki)

JAWABU

Kwanza mumemefanya ghushi: maneno yangu hamukuyanukuu yote. Mimi nimesema: "Kwa kwetu - Afrika Mashariki - kusema kwamba mwezi muandamo wa nchi moja ni muandamo kwa nchi nyengine zote za dunia ni kitu kipya". Nyinyi maneno "Kwa kwetu Afrika Mashariki" mumeyatoa ili ionekane kuwa mimi nasema kuwa hili ni suala jipya kila pahala. Watu kama nyinyi vipi tutakuamini katika dini yenu na uadilifu wenu, ikiwa munaghushi maandiko hivi? Hii ndio kamati ya Msikiti Sunna na hii ndio suna yenyewe?! Halafu mukaendelea na tadlis (ghushi) yenu mukasema: "Na kwamba jambo hilo halitekelezeki na ni kauli iliyobaki vitabuni tu". Mimi sikusema hapa kuwa "Halitekelezeki", bali nimesema:

Lakini ukweli ni kuwa hata katika nchi nyengine zote za dunia taqriban kauli kwamba tufunge kwa muandamo mmoja, ni kauli ilioishia katika vitabu tu, kimatendo (practically) kauli hio haitumiwi isipokuwa na mtu mmoja mmoja. Hadi leo hii: watu Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao, Misr wanafata muandamo wao na nchi zote taqriban ni hivyo, isipokuwa Imarati katika miaka ya mwisho wamekuwa wakifata Saudia.

Haya nionesheni hapa maneno "Halitekelezeki". Mimi nimesema kuwa kimatendo kauli hii, hadi leo haitendewi kazi isipokuwa na baadhi ya watu. Nyinyi mumebadilisha na kuweka ghushi yenu mukasema nimesema halitekelezeki. Kwa hivyo, hilo Sula (a na b) jibuni wenyewe kwani mumesema kinyume na nilivyosema. Suala (d), najibu kuwa sio: hio si kauli ya jumhur bali jumhur kauli yao ni kinyume na hivyo na hili nimelithibitisha katika uk. 189-193 wa chapa ya pili ya kitabu changu au uk. 171 wa kitabu hicho chapa ya kwanza. Na Al-Imamu Malik riwaya zake zimegongana na riwaya kwamba kila watu na muandamo wao ndio ilio bora kwani ni riwaya ya Madina aliko kuweko Al-Imamu Malik, wakati riwaya nyengine ni ya watu wa Irak kulikokuwa na viwanda vya kutunga riwaya!

MNASEMA

Na sisi tunamuongezea habari moja ambayo ni vyema kuielewa, kwamba nchi ya Uganda iliyo katika Afrika ya Mashariki pia inafuata rasmi muandamo mmoja wa duniani. Pia aelewe kwamba huo msimamo wa kila nchi na mwezi wake huku Afrika ya Mashariki haukuwepo tokea zamani. Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja. Yeye anaendelea kushika msimamo wake: (Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka.

JAWABU

1) Kitu rasmi Uganda hakizingatiwi kwani Uganda kimsingi sin chi ya Kiislamu wala ya Waislamu: Waislamu ni wachache ukilinganisha na Wasio Waislamu. Kwa hivyo, hakuna kitu rasmi. Na jambo hilo ni jambo la sasa. Na mimi sijapinga kwamba sasa fikra hio ipo Afrika Mashariki.

2) Ama kauli yenu: "Mashaykh wote wa huku wanakubaliana mwezi ukionekana popote katika nchi hizi tatu ( Kenya , Uganda na Tanzania ) wanafunga pamoja". Ndio maana nikatumia lafdhi "Kwa kwetu Afrika Mashariki" nikijua kuwa wanavyuoni wote wa kwetu Afrika Mashariki wana msimamo huo. Ama kauli yenu: "Yeye anaendelea kushika msimamo wake: ((Al-yaman wanafata muandamo wao, Oman wanafata muandamo wao, Saudia wanafata muandamo wao,)). Lile analoliona yeye halitekelezeki, basi ndio linatekelezeka". Mwisho wa kunukuu. Inaonesha kuwa kitabu changu mumekijibu bila ya kukifahamu. Nilichosema ni kuwa, ijtihadi ifanywe katika kubainisha wapi hadi wapi watu wafunge pamoja. Kwa vile, hakuna andiko lililobainisha hivyo. Ama muandamo mmoja kwa dunia nzima hili ni kinyume na andiko. Kwa hivyo, wakiwa wanavyuoni wa zamani wamefanya ijtihad hio, sisi tunafata ijtihad yao kwa vile hapa ni mahala pa ijtihad na haikugongana na andiko. Ama madai yenu nyinyi ni kinyume na andiko lilivyoonesha.

MNASEMA

"Kuna suala moja la nyongeza tunapenda tumuulize ndugu yetu Juma: Hata kama hizo nchi alizozitaja ( Al-Yaman , Oman , Misri na Saudia) hazijakubaliana kufuata muandamo mmoja, je hakuna uwezekano (japo wa sadfa) unaoweza kutokea kufunga siku moja ijapokuwa kila mmoja ameona mwezi katika nchi yake? Sasa tuseme kila nchi katika hizo imeona mwezi usiku wa Alkhamisi kuamkia Ijumaa - Wote si watafunga siku moja ya Ijumaa? Basi huo ndio utekelezaji aliosema hautekelezeki. Ni wazi kuwa unatekelezeka.

JAWABU

Munaendelea kuuliza masula haya kwa sababu masuala yenu mumeyajenga katika kitu nisichokisema kamwe. Wapi nimesema kuwa "Hilo halitekezeki" hata mukauliza masuala haya?

4

5

6

7

8

9

10

11

12

13