HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU23%

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU Mwandishi:
: AZIZI NJOZI
Kundi: Wanawake

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU
  • Anza
  • Iliyopita
  • 33 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 47730 / Pakua: 5541
Kiwango Kiwango Kiwango
HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

23

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

HAKI YA MWANAMKE KATIKA NDOA YA WAKE WENGI

Tumeshaelezea sababu za kushindwa kwa ndoa za mke mmoja kuwa na waume wengi na kufanikiwa kwa mitala na tumeelezea sababu mbalimbali zilizosababisha kuibuka kwa mitala. Baadhi ya sababu zilitokana na moyo wa ukandamizaji na ubabe wa mwanaume na nyingine zilitokana na kutofautiana kwa mwanamke na mwanaume kuhusiana na kudumu kwa uwezo wao wa kuzaa na idadi ya watoto ambayo kila mmoja wao anaweza kuzaa. Hizi sababu za pili zinaweza kuchukuliwa kuwa ni sababu thabiti za mitala. Lakini sababu yake kuu katika kipindi chote cha historia imekuwa ni idadi ya wanawake inayozidi ya wanaume wanaofaa kuolewa na kuoa sawia.

Sababu hii husababisha kuzaliwa kwa haki ya mwanamke na jukumu la mwanaume. Ili kuepuka mjadala mrefu, tunaziruka sababu hizi ambazo zinaweza kuchukuliwa kuwa ni uhalalishaji tu wa mitala, na kushughulikia tu sababu yake kubwa, ambayo kama ikiwepo hubadilika kuwa haki ya jinsia dhaifu. Ili kuthibitisha hili, nukta mbili za utangulizi zinapaswa kuwekwa sawa. Kwanza ni kuthibitisha kuwa kwa mujibu wa takwimu za kuaminika, idadi ya wanawake wanaopwaswa kuolewa ni kubwa kuliko idadi ya wanaume wanaofaa kuoa. Nukta ya pili tunayotaka kuithibitisha ni kuwepo kwa mazingira halisi yanayounda wajibu kwa wanaume waliooa na wanawake walioolewa juu ya wanawake walionyimwa haki ya kuwa na ndoa.

Kuhusiana na nukta ya kwanza, kwa bahati nzuri takwimu zote thabiti zipo duniani. Sensa huchukuliwa katika kila nchi katika kila baada ya muda fulani. Katika nchi zilizoendelea, sio tu kwamba idadi wa wanaume na wanawake hukusanywa bali pia idadi ya wanaume na wanawake katika umri mbalimbali huonyeshwa. Takwimu hizi huchapishwa na Umoja wa Mataifa katika ripoti zake za kila mwaka juu ya idadi ya watu.* Inaweza kuonyeshwa kwamba kwa madhumuni yetu, haitoshelezi kujua idadi ya wanaume na wanawake katika kila nchi, tunahitaji pia kujua uwiano wa idadi ya wanaume na wanawake wanaofaa kuoa na kuolewa sawia.

Mara nyingi uwiano huu unatofautiana na uwiano wa jumla wa wanaume na wanawake. Kuna sababu mbili za tofauti hii. Moja ni kuwa wanawake hupevuka mapema zaidi. Hii ndio sababu katika nchi zilizo nyingi umri unaoruhusiwa wasichana kuolewa upo chini kuliko umri wa wavulana wanaoruhusiwa kuoa. Kwa wastani, umri wa mume huwa ni miaka mitano zaidi kuliko mkewe.

Sababu nyingine na muhimu zaidi ni kuwa idadi ya vifo vya wavulana ni kubwa kuliko wasichana, na matokeo yake ni kuwa katika umri wao wa ndoa, wasichana huwa ni wengi kuliko wavulana. Wakati fulani tofauti huwa kubwa. Inaweza kutokea kuwa idadi ya wanaume na wanawake katika nchi inalingana au hata wanaume wakawa wengi kuliko wanawake, lakini bado idadi ya wasichana wanaofaa kuolewa ikawa kubwa kuliko idadi ya wavulana wanaoweza kuoa, tena kwa idadi kubwa.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Uwingi wa watu kwa mwaka 1964, inashuhudia ukweli huu. Kwa mfano, kwa mujibu wa ripoti hii, jumla ya watu katika Jamhuri ya Korea ni 26,277,635. Kati ya hawa wanaume ni 13,145,289 na 13,132,326 ni wanawake. Hivyo idadi ya wanaume ni zaidi ya wanawake kwa 12,943. Uwiano huu unabaki hivi katika umri wa miaka 1-4, 5-9, 12-14 na 15-19.

* Tunayo mbele yetu ripoti ya 1964, iliyochapishwa tena 1965. Takwimu zinaonyesha kuwa katika makundi yote haya ya umri idadi ya wanaume ni kubwa kuliko ya wanawake. Lakini katika kundi la umri la miaka,20-24, uwiano unabadilika. Katika kundi hili la umri idadi ya wanaume ni 1,083,364, na idadi ya wanawake ni 1,110,051. Katika makundi yote ya umri wa juu, ambayo ni makundi ya wanayoweza kuoa na kuolewa idadi ya wanawake ni kubwa zaidi. Hata hivyo, Jamhuri ya Korea ni mfano wa pekee ambapo idadi ya wanaume ni kubwa kuliko idadi ya wanawake. Takribani, katika nchi nyingine zote, sio tu kwamba idadi ya wanawake wanaofaa kuolewa ni kubwa kuliko ya wanaume, bali hata katika idadi ya jumla, wanawake ni wengi kuliiko wanaume.

Kwa mfano idadi ya watu nchini Urusi ni 216,101,000 na wanawake ni 118,261,000, na tofauti hii inaendelea katika makundi yote ya umri, yale ambayo hayajafikia umri wa kuingia katika ndoa na yale yaliyofikia umri huo, hii ni kuanzia 20-24, 25-29, 30-34 na hata 80-84. Hali iko hivi hivi katika nchi nyingine pia kama vile Uingereza, Ufaransa, Ujerumani ya Magharibi, Ujerumani wa Mashariki, Czechoslavakia, Poland, Romania, Hungary, Marekani, Japan n.k. Katika baadhi ya sehemu kama vile Berlin Magharibi na Berlin Mashariki, tofauti ya idadi kati ya wanaume na wanawake ni kubwa mno. Nchini India, katika makundi ya umri ambapo watu wanaweza kuingia katika ndoa, idadi ya wanaume ni kubwa kuliko ya wanawake. Idadi ya wanawake ni kubwa tu kuanzia katika umri wa miaka 50 na kuendelea. Inavyoonekana uchache wa wanawake unatokana na ukweli kwamba watu wengi nchini India hawapendi kutaja majina ya wake zao vijana au binti zao wadogo, wakati wa sensa. Kwa mujibu wa takwimu za sensa iliyopita, Iran ni moja ya nchi ya pekee ambapo, idadi ya wanawake inaizidi ile ya wanaume.

Inashangaza kwamba baadhi ya wakosoaji wanasisitiza kuwa sheria inayoruhusu mitala ipigwe marufuku angalau katika nchi ambazo idadi ya wanaume ni kubwa kuliko ya wanawake. Katika hatua ya kwanza, sheria hii ni ya wote, sio ya nchi maalumu. Pili, haitoshi kujua uwiano wa wanaume na wanawake peke yake. Tumeona kuwa katika Jamhuri ya Korea, idadi ya wanaume ni kubwa kuliko ya wanawake, lakini idadi ya wanawake wanaofaa kuolewa ikawa kubwa kuliko idadi ya wanaume wanofaa kuoa. Aidha, takwimu za sensa, sio za kuaminika sana katika nchi zilizo nyingi.

Kwa mfano, tunajua kuwa ingawa mitala ni mila iliyozoeleka nchini Iran, mijini na vijijini, lakini haijawahi kutokea upungufu wa mabibi harusi watarajiwa. Ukweli huu peke yake unaongea vizuri zaidi kuliko takwimu za sensa. Ashley Montaque, katika kitabu chake, "Woman - The Superior Sex", anakiri kwamba duniani kote, idadi ya wanawake wanaofaa kuolewa ni kubwa kuliko ile ya wanaume wanaofaa kuoa.

Takwimu za mwaka 1950, zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake waliofikia umri wa kuolewa nchini Marekani inaizidi ile ya wanume takriban kwa 1,430,000. Bertrand Russel katika kitabu chake, "Marriage and Morality", anasema kwamba katika Uingereza ya leo, wanawake wanazidi idadi ya wanaume kwa zaidi ya milioni mbili. Kwa mujibu wa mila yao, wanapaswa wabakie bila kupata watoto, jambo ambalo ni dhulma kubwa kwa upande wao.

Miaka kadhaa iliyopita, ilitangazwa kwenye vyombo vya habari kwamba, kufuatia shinikizo kubwa la wanawake wa Kijerumani ambao hawakuweza kupata waume na maisha ya kifamilia, kufuatia vifo vingi vya wanaume katika vita vya Pili vya Dunia, serikali ya Ujerumani imekiomba chuo kikuu cha Al-Azhar kiipatie mwongozo wa mitala. Baadaye ilifahamika kuwa kufuatia upinzani mkali wa kanisa, pendekezo hilo ilibidi liachwe. Kanisa liliona bora wanawake wakae bila kuolewa wala kuzaa wala kuishi maisha ya kifamilia, na ni bora uzinifu na ufuska kuliko kuukubali mfumo wa wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja. Kwa vile tu mfumo huu ni wa Mashariki na wa Kiislamu.

24

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

KWA NINI KUNA WANAWAKE WENGI WA UMRI WA NDOA KULIKO WANAUME?

Ingawa idadi ya wasichana wanaozaliwa sio kubwa kuliko ile ya wavulana, lakini bado kuna idadi kubwa ya wanawake wengi wa umri wa kuolewa kuliko idadi ya wanaume. Sababu iko wazi. Kiasi cha vifo vya wanaume ni kikubwa. Vifo hutokea katika kipindi ambapo mwanamume alipaswa kwa kawaida kuwa mkuu wa familia. Tukizingatia vifo vinavyotokea katika ajali, vita, kufa majini, kuanguka, kugongana kwa magari n.k. tutakuta kwamba wengi wa waathirika ni wanaume. Ni mara chache sana kukutwa kwamba mwanamke ni moja wa waathirika. Iwe ni migongano (ajali) kati ya wanaadamu au kati ya mwanadamu na maumbile, wengi wa waathirika huwa ni wanaume watu wazima.

Ili kujua kwa nini idadi ya wanawake wanaopaswa kuolewa ni kubwa kuliko idadi ya wanaume wanaofaa kuoa, inatosha kufahamu kuwa tokea mwanzo wa historia ya mwanadamu hakuna hata siku moja ambayo imewahi kupita bila kupigana vita na wanaume kupoteza uhai. Vifo vinavyotokea kutokana na vita katika hizi zama za viwanda ni vingi mara mia kuliko vile vilivyokuwa vinatokea katika zama za uwindaji na zama za kilimo. Katika vita vya Pili vya Dunia, idadi ya vifo vilivyotokea inafikia milioni saba. Utakubaliana na sisi ukihesabu vifo vinavyotokea katika vita vya kimkoa huko Mashariki ya Mbali, Mashariki ya Kati na Afrika katika miongo miwili iliyopita.

Will Durant anasema kwamba sababu nyingi zimechangia kudondoka kwa mila hii ya mitala. Maisha thabiti ya kilimo yamepunguza ugumu na hatari za maisha ya wanaume, ambapo matokeo yake ni kuwa idadi za wanawake na wanume zinakaribia kulingana. Anachosema Will Durant kinashangaza sana. Kama ingekuwa kupotea kwa maisha ya watu kunatokana na mapambano ya wanaume dhidi ya muambile tu, kungekuwa kuna tofauti kati ya zama za uwindaji na zama za kilimo.

Lakini kadri muda unavyokwenda, vita vimeendelea kuchukua idadi kubwa zaidi ya uhai wa wanaume na idadi ya vifo vinavyotokana na vita haijapata kupungua katika zama zozote. Pia sababu kubwa kwa nini wanawake hawajakumbwa na ajali nyingi ni kwamba wakati wote wanaume wamekuwa wakiwalinda, na wao wanaume ndio wamekuwa wakifanya kazi za hatari zaidi. Hivyo kama ilivyokuwa katika zama za uwindaji, uwiano usio sawa wa idadi ya wanaume na wanawake umeendelea pia katika zama za kilimo. Will Durant hajasema lolote juu ya zama za viwanda, ingawa hiki ndio kipindi ambacho kimeshuhudia mauaji makubwa zaidi ya wanaume na kipindi ambacho uwiano kati ya idadi ya wanaume na wanawake umepishana mno.

MWANAMKE ANA UWEZO ZAIDI WA KUJIKINGA DHIDI YA MARADHI.

Imegunduliwa hivi karibuni kuwa mwanaume ana uwezo mdogo zaidi wa kujikinga dhidi ya maradhi kuliko wanawake. Hii ni sababu nyingine kwa nini idadi ya vifo vya wanaume ni kubwa zaidi. Miaka kadha iliyopita, Tume ya Takwimu ya Ufaransa iliripoti kuwa nchini Ufaransa, wavulana 105 huzaliwa dhidi ya wasichana 100 lakini cha ajabu idadi ya wanawake ilikuwa ni kubwa kuliko wanaume kwa 1,758,000 (milioni moja na laki saba na elfu hamsini na nane). Inaaminika kwamba tofauti hii inatokana na uwezo mkubwa wa mwanamke wa kujilinda dhidi ya magonjwa.

Si muda mrefu umepita, makala moja ilichapishwa kwenye jaria la UNESCO liitwalo Courier. Kwa mujibu wa makala hii, mwanamke ana uwezo mkubwa zaidi wa akili kuliko mwanamume. Wastani wa kinga yake ni kubwa zaidi. Kwa kawaida, ana afya nzuri zaidi kuliko mwanaume na ana uwezo zaidi wa kustahamili maradhi. Hupona haraka kuliko mwanaume. Katika kila mwanamke mmoja mwenye kigugumizi, kuna wanaume watano wenye kigugumizi. Katika kila mwanamke mmoja asiyeweza kutofautisha rangi, kuna wanaume kumi na sita wasioweza kutofautisha rangi. Na kwa kawaida ni ugonjwa wa wanaume tu. Wanawake wana mfumo bora zaidi wa kinga ya ajali.

Wakati wa vita vya Pili vya Dunia ilithibitika kuwa katika mazingira ya aina moja, mwanamke alikuwa na uwezo zaidi wa kustahamili ugumu wa vizuizi, magereza, na kambi za wafungwa wa vita kuliko wanaume. Takribani katika nchi zote, idadi ya kesi za wanaume kujinyonga ni kubwa mara tatu zaidi kuliko wanawake. Ashley Montague ameitaja nadharia yake ya uwezo mkubwa zaidi wa mwanamke kustahamili maradhi, katika kitabu chake kiitwacho, "Woman, the Superior Sex."

Ikiwa siku moja itatokea mwanaume ataamua kumpeleka mwanamke katika kazi za hatari na za kifo au kama atamsukumia katika uwanja wa vita kukabiliana na bunduki na mabomu, bado idadi ya wanawake itaendelea kuwa kubwa kwa sababu yeye ana uwezo zaidi wa kustahamili maradhi. Haya tuliyoyasema yanahusiana tu na uwingi wa wanawake wanaofaa kuolewa dhidi ya wanaume wanaofaa kuoa. Tunajua kwamba uwingi huu ni ukweli halisi. Pia tunajua sababu zake. Na sababu zake, zile zilizokuwepo tokea mwanzo wa historia ya mwanadamu bado zipo mpaka sasa.

HAKI YA MWANAMKE KATIKA MITALA

Nukta ya pili ni kuwa uwingi wa idadi ya wanawake wanaofaa kuolewa sio tu kwamba hufanya haki kwa ajili yao, bali pia na wajibu kwa ajili ya mwanaume na mwanamke aliyeolewa. Hapana shaka kwamba ndoa ni moja ya haki za asili na ni moja ya haki za msingi za binadamu. Kila mtu awe mwanaume au mwanamke, ana haki ya kuishi maisha ya familia na kupata watoto. Haki hii ni sawa na haki ya kufanya kazi, kuwa na nyumba, kupata elimu na huduma za afya na haki ya kufurahia uhuru na usalama. Ni jukumu la jamii kuhakikisha kwamba hakuna kizuizi kinachowekwa katika upatikanaji wa haki ya asili na ya msingi ya binadamu. Badala yake, jamii inapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha lengo hili.

Ni maoni yetu kuwa moja ya dosari kubwa za Amizio la Haki za Binadamu kwa wote ni kutoipa umuhimu wowote haki hii. Azimio limeitambua haki ya uhuru na usalama, haki ya kupata huduma bora za kimahakama, haki ya kuwa na uraia na kuubadili, haki ya kuoa au kuolewa bila vipingamizi vya rangi au dini, haki ya kumiliki mali, haki ya kukusanyika na haki ya kupumzika na kupumbaa, lakini azimio hili halijaitaja haki ya mtu kuishi maisha ya ndoa halali.

Kwa mwanamke, haki hii ni yenye umuhimu mkubwa sana, kwani anayahitaji maisha ya kifamilia zaidi kuliko mwanaume. Kwa mwanaume kilicho muhimu zaidi, katika ndoa ni ngono na kwa mwanamke kilicho muhimu zaidi ni hisia za moyoni na roho. Kama mwanaume hana familia, angalau anaweza kukidhi sehemu ya mahitaji yake kwa kujiingiza katika ngono holela na ufuska. Lakini kwa mwanamke, familia ina umuhimu mkubwa zaidi. Ufuska hauwezi kukidhi japo sehemu tu ya mahitaji yake ya kimwili na kimhemko (hisia ya moyoni).

Kwa mwanaume, haki ya kuwa na familia ina maana kukidhi tamaa zake za ngono, haki ya kuwa na mwenzi maishani na haki ya kuwa na watoto halali. Lakini kwa mwanamke, ndoa inamaanisha pia kuwa na mlinzi na mwangalizi na ambaye anaweza kumpa msaada wa kimaadili. Baada ya kuzielezea nukta hizi mbili, kwamba kwanza idadi ya wanawake wanaofaa kuolewa ni wengi kuliko idadi ya wanaume wanaofaa kuoa, na pili kwamba ni haki ya asili ya binadamu kuwa na familia, ni rahisi kutoa hitimisho kwamba ikiwa ndoa ya mume kuwa na mke mmoja itafanywa kuwa ndio ndoa pekee iliyo halali, idadi kubwa ya wanawake itakuwa katika hatari ya kunyimwa haki yao ya asili, na hivyo ni ndoa za mitala tu ndio zinaweza kuwarejeshea wanawake hao haki hii iliyo hatarini.

Ni jukumu la wanawake wa Kiislamu, kwamba kama njia ya kutetea haki za wanawake, waitake na kuishinikiza tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kuutambua rasmi mfumo wa ndoa za Kiislamu wa kuwa na wake wengi kama haki ya binadamu, na hii itakuwa ni neema kubwa kwa mwanamke na maadili. Ukweli kwamba kanuni hii imetoka Mashariki na nchi za Magharibi zinapaswa kufuata usionekane kuwa ni dhambi.

NADHARIA YA RUSSEL

Kama ilivyoonyeshwa hapo awali, Bertrand Russel alikuwa anaufahamu ukweli kwamba ndoa za kuoa mke mmoja kufanywa kuwa ndio ndoa pekee zilizo halali kungewanyima wanawake wengi haki ya kuolewa. Amependekeza suluhisho rahisi sana la tatizo hili. Alitaka wanawake waruhusiwe kuwashawishi wanaume na kuzaa watoto wasio na baba. Kama ambavyo baba huwa anasaidia katika matunzo ya watoto, serikali inapaswa kuchukua nafasi ya baba na watoe ruzuku kwa wanawake ambao hawajaolewa.

Russell anasema kwamba hivi sasa nchini Uingereza kuna zaidi ya wanawake milioni mbili waliozidi idadi ya wanaume ambao kamwe hawatarajii kuolewa na kupata watoto kutokana na sheria iliyopo inayotaka mwanaume awe na mke mmoja tu. Hii ni dhulma kubwa. Anasema kwamba mfumo wa mume mmoja mke mmoja umejengwa juu dhana kwamba idadi ya wanaume inalingana na idadi ya wanawake, lakini pindi idadi hizi hazilingani, hawa wanawake waliozidi huwa hatarini kubakia bila kuolewa katika umri wao wote. Aidha, ikitokea haja ya kuongeza, idadi ya watu, aina hii ya ndoa sio tu kwamba haina maslahi na umma, achilia mbali maslahi ya mtu mmoja mmoja. Hili ni suluhisho la tatizo hili la kijamii, kama lilivyopendekezwa na mwanafalsafa mkubwa wa karne ya 20.

Lakini kwa mujibu wa Uislamu, tatizo lote hutatuliwa ikiwa idadi ya kutosha ya wanaume wenye uwezo wa kifedha, wa kimaadili na kimwili watakubali kuoa mke zaidi ya mmoja na kuwatendea uadilifu na kutoonyesha upendeleo baina ya watoto wa wake hawa wawili. Mke wa kwanza anapaswa kumpokea na kumkubali kwa ukunjufu mke wa pili kwa nia na lengo la kutekeleza jukumu la kijamii ambalo ni muhimu sana na ni namna bora ya maadili.

Kinyume na kifra za Uislamu, mwanafalsafa huyu anawashauri wanawake walionyimwa haki ya kuolewa, wawaibe waume wa wanawake wengine na anatoa wito kwa serikali kuwasaidia na kuwatunza watoto hawa waliozaliwa katika mahusiano haramu. Inaonekana kwamba mwanafalsafa huyu wa karne ya 20 anadhani kuwa mwanamke anahitaji ndoa kwa sabau tatu: kukidhi tamaa zake za ngono, kupata watoto na kukidhi mahitaji yake ya kiuchumi. Haja mbili za mwanzo zinaweza kukidhiwa kwa ulaghai na haja ya tatu itekelezwe na serikali. Anasahau kwamba mwanamke ana haja za hisia za moyoni pia. Anataka awe chini ya uangalizi wa mume anayempenda na kwamba mkataba wake na mwanaume huyo usiwe ni wa kingono peke yake. Nukta nyingine ambayo mwanafalsafa huyu hajaipa umuhimu ni hadhi ya watoto walioza liwa katika mahusiano haramu.

Kila mtoto huhitaji wazazi wanaoeleweka vizuri na upendo wao wa dhati. Uzoefu unaonyesha kuwa mara nyingi mwanamke huwa haonyeshi upendo kwa mtoto wake ambaye baba yake hajulikani. Ni vipi ukosefu wa upendo huu unaweza kufidiwa? Je serikali inaweza kufanya chochote katika hili? Bertrand Russell anasikitika kwamba wanawake wengi watabaki bila watoto mpaka pendekezo lake lipewe sura ya kisheria. Lakini anapaswa kujua kuwa wanawake wa kiingereza hawawezi wakasubiri sheria yoyote. Wao wenyewe tayari wameshatatua tatizo hili, wanaiba waume za watu na wanapata watoto wasio na baba.

Katika ripoti ya mwaka ya 1958, iliyoandaliwa na Dr. Z.A. Scott, Mkuu wa Idara ya Utabibu ya Halmashauri ya London, ilionekana kwamba katika watoto kumi waliozaliwa mwaka uliopita, mtoto mmoja ni wa nje ya ndoa. Ripoti hiyo pia ilisema kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa nje ya ndoa inazidi kuongezeka. Idadi ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa ilipaa kutoka watoto 33,838 mwaka 1957 hadi 54,433 katika mwaka uliofuata. Inaonekana kwamba Waingereza wameamua kutatua tatizo lao bila kuwa na haja ya kusubiri kupitishwa kwa pendekezo la Bertrand Russell kuwa sheria.

25

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

MITALA YAKATAZWA, LIWATI YARUHUSIWA

Serikali ya Uingereza, badala ya kuufanyia kazi ushauri wa Russell na kutatua tatizo la wanawake ambao hawajaolewa, imechukua hatua katika mwelekeo kinyume na huu. Imezidi kumnyima zaidi mwanamke haki ya kuwa na mume kwa kuhalalisha liwati. Kwa sasa mitala hairuhusiwi nchini Uingereza lakini liwati (ya wanaume kwa wanaume) inaruhusiwa. Mbele ya macho ya Waingereza sio jambo la ubinadamu kuwa na mke wa pili. Lakini ikitokea kuwa "mke" wa pili ni mwanaume, basi hapo inakuwa 262 sio tatizo.

Wanaiona liwati kuwa ni kitendo kitukufu kinachoafikiana na mahitaji ya karne ya 20. Kwa mujibu wa sheria ya mamlaka ya Uingereza, kuwa na wake wengi hakukatazwi ili mradi tu wake watakaoolewa baada ya mke wa kwanza wawe na ndevu (yaani wanaume). Inasemekana kwamba nchi za kimagharibi zimetatua matatizo ya masuala ya ndoa na familia, na kwamba sisi tunapaswa kuiga mfano wao. Kitendo hiki cha kimagharibi hahishangazi kwani ni matokeo ya mantiki ya jinsi nchi za kimagharibi zinavyokwenda. Kinachoshangaza ni kwamba watu wetu, hasa vijana wasomi, wamepoteza uwezo wao wa kufikiri kwa uhuru na kuchambua mambo. Wamepoteza haiba zao.

Wanawaamini wamagharibi kirahisi mno. Kama wana almasi mikononi mwao na watu kutoka upande mwingine wa dunia wakisema kuwa hiyo sio almasi ni ubao wa fomaika basi huitupa almasi yao. Lakini wakiona ubao wa fomaika mikononi mwa mgeni na wakiambiwa kuwa hiyo ni almasi, wao huamini kirahisi kabisa.

JE MWANAUME ANA ASILI YAKUOA WAKE WENGI?

Utashangaa ukiambiwa kuwa wanasaikolojia na wanafalsafa wa huko Magharibi wanaamini kuwa mwanaume ni mwenye asili ya kuoa wake wengi na kwamba ndoa za mke mmoja ni kinyume cha maumbile yake. Will Durant, akielezea vurugu za kimaadili leo, anasema kuwa sehemu kubwa ya matatizo haya ya kimaadili yanatokana na hamu isiyotibika ya kupenda kuwa na wanawake wa aina mbalimbali. Mwanume kwa asili, hawezi kuridhika na mke mmoja. Anasema kwamba kwa asili mwanaume hupenda kuwa na wake wengi. Ni vikwazo vikali tu vya kimaadili, kiasi cha kutosha cha umasikini na ukaka mavu wa mke wa kwanza ndio vinaweza kumlazimisha kubaki na mke mmoja.

Profesa wa Kijerumani, Schmidt, anasema kuwa katika kipindi chote cha historia, mwanaume amekuwa sio mwaminifu kwa mkewe. Kuna viashirio kuwa hata katika zama za kati, vijana wa kiume walikuwa wakibadili wapenzi wao kila mara, na nusu ya wanaume walioowa hawakuwa waaminifu kwa wake zao. Robert Kinsey katika ripoti yake inayojulikana kama 'Ripoti ya Kinsey', anasema kwamba wanaume na wanawake wa Kimarekani wanawazidi watu wa mataifa mengine yote kwa kutokuwa waaminifu katika ndoa. Katika sehemu nyingine ya ripoti anasema kwamba, tofauti na mwanaume, mwanamke huwa hapendi kubadili wanaume na ndio maana mara nyingi huwa anakataa ofa za wanaume wa nje, lakini mwanamume huona kubadili wanawake kama kujifunza mambo mapya. Kilicho muhimu zaidi kwa mwanaume ni kufurahia ngono kuliko hisia za moyoni na kiroho.

Mwanaume hujifanya kuwa ana hisia za moyoni na za kiroho kabla tu hajapata ngono. Daktari mashuhuri alimwambia Kinsey kuwa ni dhahiri kuwa mwanaume ni mwenye asili ya kuwa na wanawake wengi wakati mwanamke ni mwenye asili ya kuwa na mume mmoja, kwa sababu mamilioni ya manii (mbegu za kiume) hutengenezwa kwa mwanaume wakati kwa mwanamke ni yai moja tu ambalo huzalishwa katika mwezi mzima. Mbali na nadharia ya Kinsey, itakuwa si vibaya kama tutajiuliza sisi wenyewe kama ni vigumu kwa mwanaume kuwa mwaminifu au la. Mwanasosholojia wa Kifaransa akijibu swali hili anasema kuwa mwanaume kuwa mwaminifu katika ndoa sio tu kwamba ni vigumu bali haiwezekani kabisa. Mwanamke mmoja huzaliwa kwa ajili ya mwanaume mmoja, lakini mwanaume mmoja huzaliwa kwa ajili ya wanawake wote. Mwanaume akiwa sio mwaminifu na akimsaliti mke wake, asilaumiwe. Ni kosa la maumbile, ambayo yamemuwekea nguvu zote hizi za kutokuwa mwaminifu ndani yake.

Gazeti moja la Kifaransa lenye kichwa cha habari "Mwenendo wa Mapenzi na Ndoa wa Kifaransa", limeandika kuwa wanandoa wa Kifaransa wameshatatua tatizo hili. Wanajua kanuni za mchezo huo. Ilimradi mwanaume havuki mipaka, mahusiano yake ya mara moja moja na wanawake wengine sio tatizo. Kama kanuni, mwanaume hawezi akaendelea kuwa mwaminifu kwa mke wake baada ya miaka miwili ya ndoa yake. Kwa kiasi fulani hali ni tofauti kwa wanawake na ni bahati kwamba wao pia wanajua tofauti hii.

Nchini Ufaransa, mke huwa haoni kuwa ametendewa ubaya kama mume wake amezini. Hujifariji kwa kusema kwamba anaweza kuwa ameupeleka mwili wake kwa mwanamke mwingine lakini roho na hisia zake za moyoni zinaendelea kuwa zake (huyu mke mwenye mume). Miaka kadhaa iliyopita kulikuwa ubishani juu ya maoni yaliyotolewa na mwanabailojia aitwaye Dr. Russel Lee. Alikuwa na maoni kwamba kitendo cha mwanaume kuridhika na mke mmoja hudhoofisha uzao wake hivyo kitendo hiki huwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Alifikiri kwamba mfumo wa yeye kuwa na wake wengi ulikuwa unawafanya watoto wake kuwa na afya na nguvu.

Tunaamini kwamba maelezo haya yaliyotolewa juu ya maumbile ya mwanadamu sio sahihi hata kidogo. Wasomi hawa wanaonekana kuwa wamehamasishwa na hali ya mazingira ya kimaadili katika sehemu yao ya dunia. Hata hivyo, tunaamini kwamba kibaiolojia na kisaikolojia mwanamke na mwananume wanatofautiana na maumbile yamewafanya hivyo kwa makusudi na kwa malengo maalumu. Hivyo usawa wa haki zao usitumike kama kisingizio cha kuzifanya haki zao kuwa sawiya. Hata kwa maoni ya wale wanaounga mkono ndoa za mke mmoja, wanakiri kuwa tabia ya kisaikolojia ya mwanaume ni tofauti na ya mwanamke. Kwa asili mwanamke anapaswa kuolewa na mume mmoja tu. Yeye kuolewa na waume wengi ni kinyume na asili yake na hakuafikiani na matarajio yake kwa mumewe.

Lakini mwanaume sio mwenye asili ya kuwa na mke mmoja, kwa maana kwamba kwake kuwa na wake wengi sio kinyume na tabia yake pamoja na matarajio yake kwa mkewe. Lakini hatukubaliani na maoni kuwa ndoa za mke mmoja haziafikiani na asili ya mwanaume. Sio sahihi kabisa kusema kwamba tabia ya mwanaume ya kupenda kubadili wanawake haitibiki. Pia hatuamini kuwa mwanaume hawezi kuwa mwaminifu, au kwamba mwanamke mmoja ni wa mwanume mmoja lakini mwanaume mmoja ni wa wanawake wote. Kwa imani yetu, sababu za kutokuwa mwaminifu kwa mwanaume zinahusiana na mazingira ya kijamii na sio maumbile ya mwanaume.

Mambo yaanayosababisha kutokuwa mwaminifu yanatokana na mazingira ambayo yanamhimiza mwanamke atumie aina zote za visahwishi ili kumvuta na kumpotosha mwanaume, kwa upande mmoja na kwa upande wa pili sheria ya kuoa mke mmoja tu huwanyima mamilioni ya wanawake fursa ya kuolewa. Katika ulimwengu wa Kiislamu, kabla ya kuja kwa mila na tabia za kimagharibi, 90% ya wanaume walikuwa wanakaa na mke mmoja tu. Hawakuwa na mke zaidi ya mmoja wala hawakuwa wakijiingiza katika uzinifu na ufuska.

26

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

MITALA KAMA NJIA YA KUOKOA NDOA YA MKE MMOJA

Utashangaa tukisema kuwa mitala ni kipengele muhimu sana kilichohudumia ndoa za mke mmoja katika nchi za Mashariki. Uhalali wake kwa hakika ni kipengele kikubwa mno cha kuokoa, pale ambapo idadi ya wanawake wanaopaswa kuolewa inakuwa kubwa kuliko ya wanaume wanaofaa kuoa, kwa sababu kama haki ya kuolewa ya wanawake waliozidi haitatambuliwa na kama wanaume wenye maadili, uwezo wa fedha na afya njema hawataruhusiwa kuwa na mke zaidi ya moja, ngono holela na vimada lazima itajikitia mizizi, na hivyo kuharibu msingi halisi wa ndoa ya mke mmoja.

Katika ulimwengu wa Kiislamu wa Mashariki, mitala ilikuwa inaruhusiwa kwa upande mmoja na kwa upande wa pili vishawishi vya vitendo visivyo vya maadili mema havikuwepo. Kwa hiyo, ndoa halisi za mke mmoja zilistawi na kushitadi katika familia zilizo nyingi. Tabia ya kuwa na vimada kamwe haikupata nafasi. Katika nchi za Mashariki, kamwe haikupata kudaiwa kuwa mwanaume ana asili ya kuwa na wake wengi na kwamba hawezi kukaa na mke mmoja.

Tunaweza tukauliza, mwanaume afanye nini wakati mitala imezuiwa kisheria na kama wasomi wanavyosema, mwanaume ni mwenye asili ya kuwa na wake wengi. Kwa mujibu wa mawazo ya hawa mabwana jibu liko wazi, kisheria mwanaume awe na mke mmoja lakini kiuhalisia awe na wake wengi. Asiwe na mke zaidi ya mmoja wa halali lakini anaweze akazini na idadi yoyote ya wanawake anaotaka. Vimada ni haki ya asili ya mwanaume. Sio vizuri kumzuia mwanaume kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja.

Tunaamini kuwa muda umefika ambapo wasomaji watakuwa wameelewa tatizo. Swali sio kwamba ndoa ipi ni bora, ya mke mmoja au wake wengi. Hapana shaka kwamba ndoa ya mke mmoja ndio ndoa inayochaguliwa na wengi, kwani ndoa ya mke mmoja ina maana maishi ya wawili tu. Utu haupaswi kuchagua kati ya ndoa ya mke mmoja na ya wake wengi. Tatizo pekee ni kuwa ndoa ya mke mmoja tu, wakati fulani haitekelezeki katika baadhi ya hali za kijamii hasa inapokuwa idadi ya wanawake wanaohitaji kuolewa ni kubwa kuliko idadi ya wanaume wanaoweza kuoa. Ndoa za mke mmoja kutumika kama ndoa pekee ni jambo la kufikirika tu.

Kuna mambo mawili tu ya kuchagua: ama kuitambua rasmi ndoa ya wake wengi au kuhimiza wanaume kuwa na vimada. Katika chaguo la kwanza ni asilimia isiyozidi kumi tu ndio watakaokuwa na mke zaidi ya mmoja na wanawake wote wanaohitaji kuolewa watapata fursa ya kuolewa na kuwa na familia. Katika chaguo la pili, kila mwanamke asiyekuwa na mume wa halali ataweza kufanya ngono na wanaume wengi, na hivyo takribani wanaume wote walioowa kiuhalisia watakuwa na wake wengi. Hii ndio picha sahihi ya mitala. Lakini wafuasi wa mwenendo wa kizungu hawako tayari kuielezea picha halisi ya tatizo hili. Hawataki kueleza ukweli waziwazi. Kiuhalisia wanatetea utaratibu wa kuwa na vimada. Wanamuona mke wa halali kuwa ni mzigo na kizuizi katika njia yao. Kwao hata mke mmoja ni mwingi mno, achilia mbali wawili, watatu au wanne. Wanajifanya kuwa ni watetezi wa ndoa za mke mmoja, lakini kiuhalisia wanataka ndoa zisiwepo kabisa.

HILA ZA MWANAMUME WA KARNE HII

Mwanaume wa karne hii amefanikiwa kumpumbaza mwanamke katika masuala mengi yanayohusiana na haki za kifamilia. Hutumia maneno matamu matamu ya usawa, na uhuru ili kujipunguzia majukumu na kujiogezea fursa za starehe. Lakini kuna masuala machache ambayo ameyafanikisha sana ikiwa ni pamoja na kuingiza imani katika fikra za watu kwamba ndoa za mitala ni mila duni na isiyofaa. Wakati fulani huwa tunakutana na vitabu vinavyotufanya tushangae ikiwa waandishi wake ni wapumbavu au ni wahuni. Mwandishi mmoja, anasema: Kwa sasa, katika nchi zilizoendelea uhusiano kati ya mume na mke umejengwa juu ya msingi wa haki na majukumu yanayofanana, na kwa sababu hiyo ni vigumu kwa mwanamke kukubali ndoa za mitala za muundo wowote kama ilivyo vigumu kwa mwanaume kuwavumilia waume wenza.

Hatufahamu iwapo hivi ndivyo wanavyolielewa tatizo hili au hawaelewi kuwa tatizo hili limetokana na tatizo la kijamii, ambalo huwatwisha mzigo mkubwa wanaume walioowa na wanawake walioolewa, tatizo ambalo halijapatiwa suluhisho jingine lolote zaidi ya mitala. Kulifumbia macho tatizo halisi na kuanzisha kauli mbiu za: 'Idumu ndoa ya mke mmoja' na "Ipotelee mbali ndoa ya wake wengi' hakuwezi kusaidia chochote. Je hawajui kwamba mwanamke kuolewa na wanaume wengi si sehemu ya haki za mwanamke wala za mwanaume? Ndoa ya aina hii haishabihiani kwa namna yoyote na mitala. Ni dhihaka kusema kwamba ni vigumu kwa mwanamke kukubaliana na mitala kama ilivyo vigumu kwa mwanaume kuvumilia waume wenza. Mbali na ukweli kwamba ulinganishaji huu ni wa makosa, inaelekea kwamba mabwana hawa hawajui hali halisi ya ulimwengu wa mwanamke wa leo, kutokana na kumeremeta ambako kumewatia ushamba sana kiasi kwamba mume hutakiwa kuheshimu mapenzi ya nje ya ndoa ya mke wake na pia humtaka astahamili umewenza.

Mfumo wa kimagharibi huondoa uingiliaji wowote wa mume katika masuala ya kimapenzi ya mkewe, yaani hutakiwa kutokuwa na wivu. Tunatamani kwamba vijana wetu wangekuwa na elimu kubwa zaidi juu ya kile kinachoendelea katika nchi za Magharibi. Kwa vile mitala ni matokeo ya tatizo la kijamii na sio silika ya mwanaume, ni wazi kwamba katika jamii ambayo idadi ya wanawake ni sawa na wanume inatarajiwa kuwa mitala haitakuwepo au itakuwa kidogo sana. Lakini haitakuwa sawa hata katika hali hizo kuipiga marufuku mitala. Katazo la kisheria la mitala sio tu kwamba halitoshelezi bali pia sio jambo sahihi. Kuna baadhi ya mambo ambayo lazima yawepo ili lengo hili liweze kufikiwa. Kwanza, uadilifu wa kijamii lazima uwepo na kila mwanaume awe na hakikisho la kupata ajira ili kila mwanaume anayefaa kuoa aweze kuoa. Sharti la pili ni kuwa kila mwanamke anapaswa kuwa huru kuchagua mume wake na asishinikizwe na walezi au wazazi wake.

Ni wazi kuwa mwanamke mwenye fursa ya kuolewa na mwanaume asiyekuwa na mke hataridhia kuolewa na mume mwenye mke. Ni walezi wao ambao huwauza kwa wanaume wenye fedha kwa ajili ya fedha. Sharti la tatu ni kuwa inapaswa pasiwepo na vishawishi vingi ambavyo huwashawishi hata wanawake wenye waume achilia mbali wasio na waume. Kama jamii inataka kuleta mageuzi na kubakiza ndoa ya mke mmoja tu inapaswa kuyafikia masharti yote hayo matatu. Vingenevyo katazo la kisheria la kuzuia mitala litachochea tu kuporomoka kwa maadili.

MATATIZO YANAYOTOKANA NA BAADHI YA WANAWAKE KUKOSA WAUME

Kama wanawake wanaohitaji ndoa ni wengi kuliko wanaume wanaohitaji kuoa, katazo la mitala ni hila dhidi ya wanawake na ubinadamu. Sio suala tu la kukandamiza haki za baadhi ya wanawake. Kama ingekuwa hivyo, lingekuwa lilivumiliwa kwa kisasi fulani. Matatizo ambayo jamii inakabiliana nayo kama matokeo ya ulazimishaji wa kisheria wa ndoa ya mke mmoja, ni tishio la hatari kubwa kuliko tatizo jingine lolote, kwani taasisi ya familia ni taasisi takatifu kuliko taasisi nyingine yoyote. Mwanamke aliyenyimwa haki yake ya asili ni kiumbe mzoefu kwenye hisia zote za viumbe hai kama vile katika hali ya ufukara. ni kiumbe ambaye ana matatizo ya kisaikolojia na hisia. Ni Eva (Hawa) aliye sheheni silaha za kumrubuni mwanaume. Yeye sio ngano au shayiri ambayo inayozidi humwagwa baharini au kuhifadhiwa stoo kwa ajili ya matumizi ya dharura, ya baadaye. Yeye sio nyumba au chumba ambacho kisipopata mpangaji kinaweza kufungwa. Ni mtu anayeishi. Ni mwanadamu. Ni mwanamke. Ana vipaji vya ajabu.

Akipuuzwa anaweza kuiangamiza jamii. Hawezi kuwa mtazamaji tu wakati wengine wanafurahia maisha. Kunyimwa kwake haki ya ndoa kunaweza kuibua athari mbaya na uovu. Uovu na silika vikiungana pamoja, madhara yake yanaweza kuwa mabaya sana. Wanawake walionyimwa haki ya kuwa na maisha ya kifamilia, watafanya kila waliwezalo kuwanasa wanaume na kuutumia vyema udhaifu wa wanaume katika jambo hili. Wake watakaowaona waume zao kutokuwa waaminifu watafikiria kulipiza kisasi hivyo nao watapoteza uaminifu wao. Na matokeo yake hayasemeki. Matokea ya mwisho yamefupishwa katika ripoti mashuhuri ya Kinsey, katika sentensi moja "Wanaume na wanawake wa Kimarekani wamewazidi watu wa mataifa mengine yote kwa kutokuwa waaminifu." Tunaweza tukaona kwamba suala haliishii katika ufisadi na upotofu wa wanaume peke yao. Moto huu hatimaye huwakumba hata wanawake wenye waume na familia.

MATOKEO YA KUWEPO IDADI KUBWA YA WANAWAKE WASIO NA WAUME

Hali ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wanawake wasio na waume imekuwepo katika kipindi chote cha historia ya mwanadamu, lakini matokeo mabaya ya hali hii ambayo huisababishia ugumu jamii, hayajapata kuwa na ukubwa sawa katika jamii mbalimbali. Watu ambao walikuwa wameshikamana zaidi na uchamungu na usafi wa kutozini na ambao walikuwa wanaongozwa na dini tukufu zilizoletwa na mitume walilitatua tatizo hili kwa kutumia mfumo wa ndoa za mitala. Watu wengine ambao hawakuwa wachamungu sana waliitumia hali hii kama fursa ya kujiingiza katika ufuska.

Katika nchi za mashariki, mitala haikuanzishwa na Uislamu na wala kuzuiliwa kwa mitala katika nchi za Magharibi hakukutokana na dini ya Kristo. Kwani hakuna palipoandikwa katika Biblia kuwa hairuhusiwi kuwa na mke zaidi ya mmoja, wala Kristo hakuwahi kutamka kwa kinywa chake kuwa hairuhusiwi kuwa na mke zaidi ya mmoja. Mila hii ilikuwepo katika nchi za Mashariki hata kabla ya Uislamu na ikaja kuruhusiwa na dini za Mashariki. Kwenye Biblia pia kuna mifano tele ya Mitume waliokuwa wakioa mke zaidi ya mmoja. Ndoa za mke mmoja zimepigwa pigo kubwa na mataifa yaliyoamua kuruhusu ufuska kuliko yale yaliyoruhusu ndoa za wake wengi. Dk. Muhammad Husayn Haikal, mwandishi wa kitabu, "Life of Muhammad", baada ya kunukuu Aya kadhaa za Qur'ani juu ya mitala, anasema: Aya hizi zinasaidia na kuimarisha ndoa za mke mmoja.

Zinasema kwamba kama una hofu kwamba hutaweza kufanya uadilifu ukiwa na mke zaidi ya mmoja, basi oa mke mmoja tu. Hata hivyo Aya hizi zinahimiza kuwa kufanya uadilifu kwa ukamilifu haiwezekani. Vyoyote vile kwa mtazamo wa ukweli huu, kuna baadhi ya wakati ambapo mitala huwa haiepukiki. Mtume mwenyewe alioa wake wengi, katika kipindi ambacho idadi kubwa ya wanawake wa Kiislamu ilipoteza waume zao katika vita vya awali vya Uislamu. Je inawezekana kusema kwamba, kufuatia vita, magonjwa ya milipuko na dharura nyinginezo ambazo husababisha vifo vya maelfu na wakati fulani mamilioni ya watu, ni bora kubaki na ndoa ya mke mmoja kuliko mitala kama hali pekee pamoja na sharti la kufanya uadilifu baina ya wake? Je watu wa Magharibi wanaweza wakadai kuwa baada ya vita vya dunia, sheria ya ndoa ya mke mmoja imeongezwa nguvu katika njia ile ile ambayo kwamba kwa sasa imebakia jina tu?

27

HAKI ZA WANAWAKE KATIKA UISLAMU

DOSARI NA KASORO ZA MITALA

Maisha ya ndoa yenye furaha hutegemea, uaminifu, uvumilivu, kujitolea na umoja. Mambo yote haya huhatarishwa na ndoa za wake wengi (mitala). Mbali na mazingira ya wivu kati ya wake na watoto katika ndoa za mitala, majukumu ya mume huwa ni mazito sana na yanayovunja mgongo kiasi kwamba sio burudani kuyabeba. Wanaume walio wengi ambao wana furaha na wameridhika na mitala, ni wale ambao katika hali halisi hukwepa majukumu yao ya kisheria na kimaadili. Humjali mke mmoja tu na huwapuuza wengine, ambao kwa mujibu wa Qur'ani huachwa wamening'inia. Kile ambacho watu wa aina hii wanakiita mitala, kiuhalisia ni ndoa za mke mmoja zilizochanganyika na ubabe, ukatili na dhulma ya jinai.

Kuna methali iliyoenea sana miongoni mwa watu wa kawaida isemayo: "Mungu Mmoja, Mke Mmoja". Kilichosemwa ni imani ya watu walio wengi na tukilipima tatizo kwa kutumia furaha ya mtu mmoja mmoja, ni sahihi. Kanuni ya mke mmoja, hata kama haitekelezwi na wanaume wote lakini ndiyo inayotumiwa na wanaume walio wengi. Kama mtu anafikiri kuwa mitala, pamoja na majukumu yake yote ya kisheria na kiuchumi, ni kitanda cha maua waridi, basi amekosea sana. Kwa upande wa furaha na starehe binafsi, ndoa za mke mmoja ndio zinafaa zaidi.

TATHMINI SAHIHI

Hata hivyo, tathmini sahihi ya mfumo wa mitala, ambao unatokana na mahitaji binafsi na ya kijamii, haiwezi ikafanywa kwa kulinganisha na ndoa za mke mmoja. Namna sahihi ya kutathmini mfumo huu ni kuzinga tia sababu zinazousababisha, ili kuangalia ni madhara gani mabaya yatafuatia, na wakati huo huo tutazame dosari na kasoro za mfumo wa mitala. Ni baada tu ya kupima faida na hasara zote za mfumo huu ndio tutafikia kwenye hitimisho sahihi. Ili kufafanua nukta hii, hebu tuutazame mfano huu. Tukiitazama sheria ya kulazimisha watu kwenda jeshini, ni wazi kwamba kwa upande wa maslahi binafsi, sheria hii sio nzuri. Ingekuwa vizuri zaidi kama sheria hii isingekuwepo, na hakuna mpendwa wa familia ambaye angeondolewa kwenye familia yake (na kupelekwa jeshini) na wakati fulani kupelekwa vitani.

Lakini hii sio tathmini sahihi ya jambo hili pamoja na ubaya wa mtoto kutenganishwa na familia yake, tunapaswa pia kutazama mahitaji ya kiulinzi ya nchi. Tukifanya hivyo tutaona kwamba ni jambo la maana kabisa kuweka idadi ya kutosha ya raia iwekwe tayari kwa ajili ya ulinzi wa nchi na familia zao zinapaswa kustahamili usumbufu na matatizo yanayosababishwa na sheria ya kulazimisha watu kuingia jeshini. Awali tulielezea mahitaji ya mtu mmoja mmoja na ya kijamii ambayo wakati fulani huhalalisha mitala. Sasa kuandaa mazingira ya hukumu ya jumla, hebu tujadili dosari na kasoro za mfumo huu. Tunakubali kwamba mfumo huu una dosari fulani fulani, lakini hatuamini kwamba yote yaliyosemwa dhidi ya mitala ni sahihi. Tunapendekeza kwamba tuzijadili dosari zake katika mitazamo mbalimbali.

KATIKA MTAZAMO WA KISAIKOLOJIA

Mahusiano ya unyumba hayaishii katika ushirikiano wa kimwili na kifedha. Kama ingekuwa hivyo, ingekuwa rahisi kuhalalisha mitala, kwani fedha na matendo ya ndoa yanagawanyika baina ya watu wengi, kila mmoja anapata gawio lake. Msingi wa mahusiano ya unyumba ni wa kimhemko na kisaikolojia. Yamejengwa juu ya vitu kama upendo, mihemko na hisia. Maisha ya ndoa yana maana ya muungano wa mioyo. Kama ilivyo kwa vitu vyote dhahania (visivyoonekana), upendo na hisia havigawanyiki. Haviwezi kugawiwa miongoni, mwa watu wengi wala haiwezekani kila anayehitaji akapewa kijisehemu maalumu cha upendo na hisia hizo. Moyo hauwezi ukagawanywa baina ya watu wawili. Upendo na ibada vinakwenda pamoja. Havikubali mpinzani. Upendo hauwezi ukapimwa wala kugawiwa kama ngano au shayiri. Aidha, hisia haziwezi kudhibitiwa. Moyo humtawala mwanaume, mwanaume hautawali moyo.

Roho ya ndoa, yaani, kipengele chake cha kibinadamu ambacho hutofautisha mahusiano kati ya wanaadamu na wanyama haigawanyiki wala haiwezi kudhibitiwa. Kwa hiyo, mitala haipaswi kuruhusiwa. Kwa imani yetu, maelezo haya yametiwa chumvi. Ni kweli kwamba mihemko na hisia ni roho ya ndoa. Pia ni kweli kwamba hisia hazidhibitiki. Lakini ni mawazo halisi ya kindoto, bali pia ni hoja ya uwongo kusema hisia hazigawanyiki. Sio suala la kugawanya hisia kama vile mali au fedha. Ni suala la uwezo wa kiakili wa mwanaume, ambao ni mdogo kiasi cha kushindwa kumudu mahusiano ya watu wawili. Baba mwenye watoto kumi huwapenda wote na hujitolea mhanga kwa ajili yao. Lakini suala moja liko wazi. Upendo hauwezi kuwa mkubwa sana katika wake wengi kama ndoa ya mke mmoja. Upendo mkubwa, haukubaliani na wingi, lakini pia haukubaliani na hoja za kiakili. Russel katika kitabu chake, "Marriage and Morality" anasema kwamba watu wengi leo hii wanayaona mapenzi kama ubadilishanaji mzuri wa hisia. Hoja hii peke yake, bila kujali hoja nyingine zote, inatosheleza kuzishutumu ndoa za mitala.

Kama ni suala la ubadilishanaji mzuri wa hisia tu, tunashangaa kwa nini ubadilishanaji huu uhodhiwe. Baba mwenye watoto huwapenda wanaye wote nao wote humpenda. Je huu sio ubadilishanaji wa haki wa hisia? Hata baba anapokuwa na watoto wengi, upendo wa baba kwa kila mtoto, mara zote huwa ni mkubwa kuliko upendo wa kila mtoto kwa baba yao. Sehemu inayoshangaza zaidi katika kauli hiyo ni kwamba, imetengenezwa na mtu ambaye anawashauri wanaume kuyaheshimu mapenzi ya nje ya wake zao na kwamba wasiwaingilie. Pia anawapa ushauri kama huo wanawake walioolewa. Je bado anaamini kuwa ubadilishanaji wa hisia kati ya mume na mke utakuwa wa haki?

KUTOKA KATIKA MTAZAMO WA TABIA

Katika ndoa za mitala, mahusiano baina ya wake wenza huwa ni balaa tupu. Kwa kawaida mwanamke humuona mke mwenzake kama adui yake mkubwa kuliko wote. Kuwa na wake wengi mara nyingi husababisha magomvi baina yao na wakati fulani dhidi ya mume wao. Huzusha uovu na huibadili hali ya hewa ya familia, kutoka katika hali ya uaminifu na utulivu iliyotarajiwa na kuwa uwanja halisi wa vita. Uadui na uhasama ambao huwepo baina ya akina mama huhamia mpaka kwa watoto na kambi mbili au zaidi huundwa. Hali ya hewa ya familia, badala ya kuwa shule ya awali ya kuwafundisha watoto maadili, hubadilika na kuwa shule ya magomvi na tabia zisizo za kibinadamu. Hapana shaka kwamba ndoa za mitala zina athari hizi zote mbovu. Lakini nukta moja haipaswi kusahaulika. Tunapaswa kuona kama hizi ni athari za asili za mitala au zinatokana na tabia isiyofaa ya mume na mke wa pili. Tunaamini kwamba athari mbaya zilizo nyingi hazitokani na matokeo ya moja kwa moja ya mitala, bali zinatokana na utekelezaji usiofaa wa mitala.

Jaalia mume na mke wanaishi pamoja na wanaishi maisha ya kawaida. Kisha mume anakuja na mwanamke mwingine ambaye anahamishia upendo wote kwake. Baada ya maelewano ya siri baina ya wawili, mke wa pili huvamia nyumba na huutumia vibaya upendo wa mume, na huyatishia mamlaka ya mke wa kwanza. Tunaweza tukaelewa atakachokifanya mke wa kwanza. Hakuna kitu ambacho huwa kinamuudhi na kumkera mwanamke kama kitendo cha kudharauliwa na mume wake. Kushindwa kuurejesha upendo wa mume wake ni kufeli kukubwa kabisa kwa upande wa mke. Mume anapofanya jeuri na uasherati na mke wa pili ndio hubaki mwenye mamlaka pekee, hapa haitarajiwi mke wa kwanza awe na subira.

Lakini mambo yatakuwa tofauti na migogoro ya ndani itapungua sana ikiwa mke wa kwanza anajua kuwa mume wake ana haki ya kuwa na mke wa pili na kwamba hajamchoka. Mume hapaswi kuonyesha jeuri wala kujishughulisha na ngono na mke wa pili zaidi kuliko kujali hisia za mke wa kwanza. Baada ya kuwa na mke wa pili anafaa kuwa mpole zaidi kwa mke wake wa kwanza na kujali hisia zake. Mke wa pili anapaswa pia kujua kuwa mke wa kwanza pia ana haki zinazopaswa kuheshimiwa. Kwa kifupi pande zote zinazohusika, zinapaswa kukumbuka kuwa zimechukua hatua katika kutatua tatizo la kijamii.

Sheria ya mitala ni suluhisho endelevu la tatizo la kijamii na imezingatia maslahi makubwa na mapana zaidi ya jamii. Wale wanaoitekeleza wanapaswa kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri na wawe wamefundishwa vizuri mwenendo wa Kiislamu. Uzoefu unaonyesha kwamba ikiwa mume sio muasheati na sio mjeuri na mke wake akishawishika kuwa mume wake anahitaji mke wa pili, yeye mwenyewe mke wa kwanza hufanya maadalizi ya ndoa ya mke wa pili. Katika hali hii matatizo huwa hayaibuki, kwani matatizo mengi hutokana na tabia mbaya za wanaume.

3

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA SITA

Sura ya Kumi na Tisa: Surat Maryam. Imeshuka Makka ina Aya 98.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye Kurehemu.

كهيعص ﴿١﴾

1. Kaaf Haa Yaa A’yn Swaad.

ذِكْرُ رَحْمَتِ رَبِّكَ عَبْدَهُ زَكَرِيَّا ﴿٢﴾

2. Huu ni ukumbusho wa rehema ya Mola wako kwa mja wake Zakariya.

إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ نِدَاءً خَفِيًّا ﴿٣﴾

3. Alipomuomba Mola wake kwa siri.

قَالَ رَبِّ إِنِّي وَهَنَ الْعَظْمُ مِنِّي وَاشْتَعَلَ الرَّأْسُ شَيْبًا وَلَمْ أَكُن بِدُعَائِكَ رَبِّ شَقِيًّا ﴿٤﴾

4. Akasema: Mola wangu! Mfupa wangu umedhoofika, na kichwa kiname remeta kwa mvi. Mola wangu! Sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba wewe.

وَإِنِّي خِفْتُ الْمَوَالِيَ مِن وَرَائِي وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا فَهَبْ لِي مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا ﴿٥﴾

5. Na Mimi nahofia jamaa zangu baada yangu na mke wangu ni tasa, Basi nipe mrithi kutoka kwako.

يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ وَاجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا ﴿٦﴾

6. Atakayenirithi mimi na arithi ukoo wa Ya’qub, Ewe Mola wangu mjaaliye mwenye kuridhisha.

ZAKARIYA

Aya 1-6

MAANA

Kaaf Haa Yaa A’yn Swaad.

Umetangulia mfano wake pamoja na tafsiri katika Juz. 1, mwanzo wa Sura Baqara

Huu ni ukumbusho wa rehema ya Mola wako kwa mja wake Zakariya.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anamsimulia Mtume wake mtukufu, katika Aya hizi, jinsi alivyompa rehema Zakariya na akamneemesha kwa mtoto wake Yahya. Zakariya anatokana na kizazi cha Suleiman bin Daud. Alimuoa khalat (mama mdogo) wa Maryam. Naye alikuwa ni mlezi wa Maryam, Yametangulia maelezo ya hayo katika Juz; 3 (3:38), Inasemekana kuwa Zakriya alikuwa seremala.

Alipomuomba Mola wake kwa siri Alimuomba Mola wake akiwa peke yake na akasema: Mola wangu! Mfupa wangu umedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi. Mola wangu! Sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba wewe.

Zakariya alizeeka bila ya kuwa na mtoto, kwa hiyo akamnyenyekea Mola wake, akimshtakia udhaifu wake na uzee wake. Miongoni mwa aliyoyasema ni: “Mola wangu usiniache peke yangu na Wewe ndiye mbora wa wanaorithi” (21:89). Ninakuomba ewe Mola wangu, nikiwa na matarajio ya rehema yako bila ya kukata tamaa. Vipi nikate tamaa na hali hujawahi kuyaangusha matarajio yangu kwako.

Na mimi nahofia jamaa zangu baada yangu na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako atakayenirithi mimi na arithi ukoo wa Ya’qub, Ewe Mola wangu mjaaliye mwenye kuridhisha.

Neno la kiarabu ‘mawalii’ lililofasiriwa jamaa, lina maana ya ndugu wa upande wa baba. Kwa hiyo Zakariya akiwa mzee na mkewe akiwa tasa, alihofia kurithiwa na binamu zake ambao ni wana wa Israil. Inasemekena walikuwa ni waovu.

Na hilo si mbali kwa Waisrail, kuwa wakirithi watawafanyia uovu watu na kuwafanyia ufisadi kwenye dini yao na dunia yao. Pamoja na uzee wake Zakariya na utasa wa mke wake, bado alikuwa na mategemeo makubwa kwa muumba wake, ndio maana akamuomba amtimizie haja yake.

يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا ﴿٧﴾

7. Ewe Zakariya! Hakika sisi tunakubashiria mwana, jina lake ni Yahya, hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.

قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا وَقَدْ بَلَغْتُ مِنَ الْكِبَرِ عِتِيًّا ﴿٨﴾

8. Akasema: Ewe Mola wangu! Vipi nitakuwa na mwana na hali mke wangu ni tasa, na mimi nimekwishafikia ukongwe katika uzee?

قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَقَدْ خَلَقْتُكَ مِن قَبْلُ وَلَمْ تَكُ شَيْئًا ﴿٩﴾

9. Akasema, ndio hivyo hivyo Mola wako amesema, haya kwangu ni mepesi. Na hakika nilikuumba wewe zamani na hukuwa kitu.

قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَ لَيَالٍ سَوِيًّا ﴿١٠﴾

10. Akasema: Mola wangu nijaalie ishara. Akasema, ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa masiku matatu, na hali ni mzima.

فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ مِنَ الْمِحْرَابِ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ أَن سَبِّحُوا بُكْرَةً وَعَشِيًّا ﴿١١﴾

11. Akawatokea watu wake kutoka mihirabuni, akawaashiria kuwa mumsabihi asubuhi na jioni.

BISHARA YA YAHYA

Aya 7 – 11

MAANA

Ewe Zakariya! Hakika sisi tunakubashiria mwana, jina lake ni Yahya, hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.

Mwenyezi Mungu aliitikia dua ya Zakariya na akampa habari njema ya kuzaliwa mtoto wa kiume, na kwamba Mwenyezi Mungu amemuita Yahya akiwa bado yuko kwenye uti wa mgongo wa baba yake. Na hakuna aliyewahi kuitwa jina hilo kabla yake. Inasemekana Yahya ndiye Yohana amabye ni maarufu kwa wakiristo kwa jina la Yohana mbatizaji).

Akasema: “Ewe Mola wangu! Vipi nitakuwa na mwana na hali mke wangu ni tasa, na mimi nimekwishafikia ukongwe katika uzee?

Kusema hivi sio kuona kuwa haiwezekani, bali ni kuadhimisha na kushukuru neema za Mwenyezi Mungu na uweza wake ambao umekiuka desturi na mazoweya. Yeye ni mzee na mkewe ni tasa tena ni mzee, lakini pamoja na yote hayo Mwenyezi Mungu amemneemesha kupata mtoto.

Akasema: ndio hivyo hivyo Mola wako amesema, haya kwangu ni mepesi. Na hakika nilikuumba wewe zamani na hukuwa kitu.

Anayesema kauli zote mbili ni mmoja, naye ni Mwenyezi Mungu. yaani Mwenyezi Mungu anamwambia Zakariya kuwa Mola wako amesema. Desturi hii wanaitumia watungaji wengi wa kiislamu.

Mtu anaweza kusema: “Amesema Muhammad yeye ni Bin Malik” akijikusudia yeye Mwenyewe. Mfano mwingine ni wa Tabariy akijizungumzia yeye mwenyewe: “Amesema Abu Jafar Muhammad bin Jarir At-Tabariy”

Aliposema Mwenyezi Mungu haya kwangu ni mepesi, ni kuwa kwa Mungu hakuna kitu chochote kilicho kigumu. Vitu vyote kwake ni sawa tu; hahitajii isipokuwa neno ‘Kuwa’

Akasema: Mola wangu nijaalie ishara. Akasema, ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa masiku matatu, na hali ni mzima. Akawatokea watu wake kutoka mihirabuni, akawaashiria kuwa mumsabihi asub- uhi na jioni.

Makusudio ya kuwaashiria ni kuwaashiria kwa mkono wake au kwa maandishi, kwa sababu yeye amezuiliwa kuzungumza, Umetangulia ufafanuzi wake katika Juz; 3 (3:41).

يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا ﴿١٢﴾

12. Ewe Yahya! Kishike kitabu kwa nguvu, Na tulimpa hukumu angali mtoto.

وَحَنَانًا مِّن لَّدُنَّا وَزَكَاةً وَكَانَ تَقِيًّا ﴿١٣﴾

13. Na tukampa huruma itokayo kwetu na utakaso na alikuwa ni mwenye takua.

وَبَرًّا بِوَالِدَيْهِ وَلَمْ يَكُن جَبَّارًا عَصِيًّا ﴿١٤﴾

14. Na mwema kwa wazazi wake wala hakuwa jeuri muasi.

وَسَلَامٌ عَلَيْهِ يَوْمَ وُلِدَ وَيَوْمَ يَمُوتُ وَيَوْمَ يُبْعَثُ حَيًّا ﴿١٥﴾

15. Na amani iwe juu yake, siku alipozaliwa na siku atakapokufa na siku atakapofufuliwa.

YAHYA

AYA 12 – 15

MAANA

Ewe Yahya!

Kauli hii inaelezea moja kwa moja kuwa Yahya amekwishazaliwa, amekuwa na akili ya kufahamu na kutia maanani na ana uwezo wa kutumia Tawrat ambayo ndiyo aliyoikusudia Mwenyezi Mungu aliposema:

Kishike kitabu kwa nguvu.

Maana ya kukishika kwa nguvu ni kukitumia kwa bidii na ikhlasi. Kisha akamsifu Yahya kwa sifa zifuatazo:

Na tulimpa hukumu angali mtoto na tukampa huruma itokayo kwetu na utakaso na alikuwa ni mwenye takua na mwema kwa wazazi wake wala hakuwa jeuri muasi.

Makusudio ya kupewa hukumu udogoni ni kujua dini mapema udogoni. Hii ni neema Mwenyezi Mungu aliyomhusisha nayo Yahya; kama alivyomhusisha kwa kuzaliwa na wazazi wazee. Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema yake amtakaye. Baadhi ya riwaya zinasema kuwa siku moja watoto walimwambia Yahya: “Twendeni tukacheze.” Yahya akasema: “Hatukuumbwa kwa ajili ya kucheza, twendeni tukaswali.”

Makusudio ya upole ni upole kwa waja. Utakaso ni utwahara na utakatifu. Takua ni kumtii Mwenyezi Mungu. Kuwatendea wema wazazi wawili ni kinyume cha kuwaudhi.

Kauli yake Mwenyezi Mungu:Wala hakuwa ni jeuri muasi ni kuunganisha kwa kufafanua. Kwa sababu Mwenye utakaso na takua hawezi kuwa jeuri muasi.

Na amani iwe juu yake, siku alipozaliwa na siku atakapokufa na siku atakapofufuliwa

Hili ni fumbo la kuwa Yahya ni Mwenye kuridhiwa mbele ya Mwenyezi Mungu duniani na Akhera. Ilivyo ni kuwa kumridhia kwake Yahya (a.s.) ni matokeo ya sifa alizomsifu nazo Mwenyezi Mungu.

Unaweza kuuliza : Kwanini Mwenyezi Mungu amemuhusisha Yahya na sifa hizi tele akiwa bado angali mdogo?

Jibu : Hakika Mwenyezi Mungu ana mambo yake kwa viumbe vyake. Anaweza akampa fadhila mdogo na akamnyima mkubwa. Na kila kutoa kwake na kuzuia kwake kuna hekima ambayo akili inaweza kujua na isiweze kujua. Lakini akili huwa inajaribu; kama ifuatavyo:

Sio mbali kuwa makusudio ya kusifika Yahya na sifa hizi katika rika hilo ni kutoa hoja kwa Wana wa Israil, watakapohitilafiana naye na wasikilize nasaha zake na mwito wake, Alimuumba Isa bila ya baba, “ili tumfanye kuwa ni ishara kwa watu na rehema itokayo kwetu” Itakuja Aya hii sehemu inayofuatia hii.

Pamoja na hoja hii ya kunyamazisha, lakini bado walimuasi Yahya na wakamfanyia uadui; mwisho wakamuua yeye na baba yake, si kwa lolote isipokuwa ni kwa kuwakataza mabaya. Hili si ajabu kwa yule aliyesema kuwa mikono ya Mwenyezi Mungu imefunga au Mungu ni fukara na sisi ni matajiri. Rudia Juz. 6 (5:64).

Katika kitabu Qasasul-anbiya (Visa vya mitume) imeelezwa kuwa Herod mfalme wa Palestina, wakati huo, alimpenda Herodias, binti wa kaka yake, kutokana na uzuri wake, na akataka kumuoa. Yahya alipopinga hilo

Herodias alichukia na akatoa sharti kwa ami yake kuwa mahari yake yawe kichwa cha Yahya. Kwa hiyo Mfalme akamchinja Yahya na akampelekea mpenzi wake zawadi hiyo ya kichwa.

Kuna riwaya mashuhuri iliyopokewa kutoka kwa Ali bin Husein bin Ali(a.s) kwamba baba yake, alipokuwa akielekea Iraq, alikuwa akimkumbuka sana Yahya na akisema: “Ni katika utwevu wa dunia kwa Mwenyezi Mungu, kwamba kichwa cha Yahya bin Zakariya kitolewe zawadi kwa kahaba miongoni mwa makahaba wa ki bani Israil.”

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا ﴿١٦﴾

16. Na mtaje Maryam katika Kitabu, alipojitenga na watu wake mahali upande wa mashariki.

فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا ﴿١٧﴾

17. Na akaweka pazia kujikinganao, Tukampelekea roho wetu, Akajifananisha kwake sawa na mtu.

قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَـٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا ﴿١٨﴾

18. Akasema: Hakika mimi najilinda kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mwenye takua.

قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا ﴿١٩﴾

19. Akasema: Mimi ni mjumbe wa Mola wako ili nikupe mwana mtakatifu.

قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا ﴿٢٠﴾

20. Akasema: Nitakuwaje na mwana hali hajanigusa mtu yoyote wala mimi si malaya.”

قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا ﴿٢١﴾

21. Akasema; Ndivyo hivyo hivyo, Mola wako amesema, haya kwangu ni mepesi! Na ili tumfanye kuwa ni ishara kwa watu na rehema itokayo kwa kwetu. Nahilo ni jambo lililokwishapitishwa.

MARYAM

Aya 16-21

MAANA

Na mtaje Maryam katika Kitabu, alipojitenga na watu wake mahali upande wa mashariki, Na akaweka pazia kujikinga nao.

Dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa Maryamu alijitenga na watu na akawa peke yake upande wa mashariki na kaweka sitara baina yake na wao, kiasi ambacho hawamuoni wala yeye hawaoni wao.

Kwa nini Maryamu alijitenga? Je, ni kwa kuwa aliona mambo yanayomchukiza au ni kwa kujitenga kwa ajili ya kufanya ibada au ni kwa ajili ya jambo jengine? Je, makusudio ya mahali upande wa mashariki ni kunakotokea jua au ni mashariki ya Baytul-maqdis au ni upande wa mashariki wa nyumba ya watu wake. Pia je, ni aina gani ya pazia aliyoweka, ni ukuta au kibanda?

Hakuna kitu, katika Aya, kinachoashiria majibu ya maswali haya; Kwa sababu hayahusiani na itikadi wala maisha. Sio mbali kuwa Mwenyezi Mungu alimpa ilhamu ya kujitenga huko ili apewe habari na Jibril kuhusu kuzaliwa Isa(a.s) akiwa kando na watu.

Tukampelekea roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu

Makusudio ya roho wetu, ni Jibril. Alijifananisha na mtu kamili. Imeelezwa katika baadhi ya Tafsiri kwamba alikuja na umbo la mtu ili asimwogopeshe. Tafsiri nyingine inasema kuwa aliogopa na akafadhaika, kwa mshtukizo huu.

Mgeni ajitome ndani bila ya hodi na yeye yuko peke yake! Jambo la kushangaza, Kauli hii, ya pili, ina nguvu na usahihi zaidi ya ile nyingine, kwa dalili ya kuwa yeye alifazaika na akasema:

Hakika mimi najilinda kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe, ukiwa ni Mwenye takua.”

Yaani nataka hifadhi kwa Mwenyezi Mungu na shari yako ikiwa wewe unamwamini Yeye na hisabu yake na adhabu yake. Alimuhofisha na Mwenyezi Mungu, kwa sababu hakuwa na nyenzo nyingine yoyote ya kumzuia hapo alipo, isipokuwa hiyo. Vinginevyo yeye ana hifadhi ya Mwenyezi Mungu akiwa anamtegemea Yeye; ni sawa huyo anayemuhofisha ni mwenye takua au muovu.

Akasema: Mimi ni mjumbe wa Mola wako ili nikupe mwana mtakatifu.” Akasema: Nitakuwaje na mwana hali hajanigusa mtu yoyote wala mimi si malaya?

Unanipa habari ya mtoto, vipi na kutoka wapi? Sina mume wala sijafanya uasharati.

Akasema: Ndivyo hivyo hivyo Mola wako amesema, haya kwangu ni mepesi! Na ili tumfanye kuwa ni ishara kwa watu na rehema itokayo kwetu. Na hilo ni jambao lililokwishapitishwa.

Roho mwaminifu alimwambia kuwa sababu za kuzaa, kwa Mungu, sio kuonana na mtu tu. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu anafanya vitu kwa sababu zake zilizozoeleka, vile vile anafanya vitu kwa neno ‘kuwa’ sawa na alivyofanya ulimwengu bila ya kitu chochote na Adamu bila ya baba wala mama.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) alitaka azaliwe mtoto kuonyesha dalili wazi ya ukuu wa muumba na utume wa atakayezaliwa, awe ni rehema kwa ubi- nadamu na hoja ya kunyamazisha wana wa Issrail ambao walijaribu kumuua. Tumeyaeleza hayo kwa ufafanuzi zaidi katika Juz. 3 (3: 45)

فَحَمَلَتْهُ فَانتَبَذَتْ بِهِ مَكَانًا قَصِيًّا ﴿٢٢﴾

22. Basi akachukua mimba yake akaondoka nayo mahali mbali.

فَأَجَاءَهَا الْمَخَاضُ إِلَىٰ جِذْعِ النَّخْلَةِ قَالَتْ يَا لَيْتَنِي مِتُّ قَبْلَ هَـٰذَا وَكُنتُ نَسْيًا مَّنسِيًّا ﴿٢٣﴾

23. Uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya nikawa mwenye kusahaulika kabisa.

فَنَادَاهَا مِن تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا ﴿٢٤﴾

24. Pakanadiwa kutoka chini yake kwamba usihuzunike; hakika Mola wako amejaalia chini yako kijito cha maji.

وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا ﴿٢٥﴾

25. Na litikise kwako shina la mtende utakuangushia tende freshi zilizo mbivu.

فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ الْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِي إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ الْيَوْمَ إِنسِيًّا ﴿٢٦﴾

26. Basi kula na kunywa na uburudishe jicho. Na pindi ukimuona mtu yeyote basi sema hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema ya kufunga. Kwa hiyo leo sitasema na mtu.

MIMBA YA ISA

Aya 22 – 26

MAANA

Basi akachukua mimba yake akaondoka nayo mahali mbali

Inasemekana kuwa Jibril alimpulizia kwenye gauni lake, ikawa ndiyo sababu ya kushika mimba; Rejea ya kauli hii ni dhahiri ya Aya hii:

وَالَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا ﴿٩١﴾

“Na (mwanamke) aliyelinda tupu yake na tukampulizia katika roho yetu” (21:91)

وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا ﴿١٢﴾

“Na Maryam Binti Imrani aliyelinda tupu yake na tukampulizia humo kutoka roho yetu,” (66:12).

Mara kwa mara tumeishiria kuwa Qur’an inajifasiri yenyewe; yaani Aya zinafasiri Aya nyingine. Kwa sababu chimbuko lake ni moja. Tukiangalia msingi huu tutafahamu, kwa ujumla wake wote kuwa makusudio ya kupulizia ni kuumba na kutengenezwa mimba, na makusudio ya Roho ni Isa mwenyewe; kama inavyofahamisha Aya hii: “Masih Isa bin Maryam ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na neno lake tu alilompelekea Maryam, na ni roho iliyotoka kwake.” Juz.6 (4:171)

Maana ya ‘neno lake’ ni neno ‘kuwa,’ambalo anaumbia nalo vitu. Na maana ya ‘alilompelekea Maryam’ ni kuwa Maryam au tumbo lake ndio mahali pa kuumbwa; Kwa ufafanuzi zaidi angalia huko. Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba Maryam alipojihisi ana mimba alijitenga kando na watu wake kwa kuona haya.

Uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya nikawa mwenye kusahaulika kabisa.

Haya ni maneno anayoyasema mtu yeyote anapozongwa na matatizo makubwa, anatamka kupunguza msongo wa moyo na huzuni yake.

Pakanadiwa kutoka chini yake kwamba usihuzunike; hakika Mola wako amejaalia chini yako kijito cha maji.

Yanayokuja akilini mwanzo, kutokana na mfumo wa maneno, ni kuwa aliyenadi ni Isa(a.s) na wala sio Jibril, kama wanavyodai wafasiri wengi. Kunadi huku ni miongoni mwa miujiza ya Isa; sawa na kuzaliwa na kufufua kwake wafu.

Isa aliendelea kumwambia mama yake:

Na litikise kwako shina la mtende utakuangushia tende freshi zilizo mbivu.

Inasemekana huo haukuwa msimu wa tende. Kwa hiyo kupatikana tende ilikuwa ni muujiza. Hili haliko mbali, kwa sababu kila kitu hapa ni muujiza tu na tamko lenyewe pia linafahamisha hivyo.

Basi kula tende na kunywa kutoka kwenye kijito na uburudishe jicho.

Yaani poa moyo kwa kupata mtoto mwenye kubarikiwa.

Na pindi ukimuona mtu yeyote na akakuuliza kuhusu mtoto,basi sema kwa ishara kuwahakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema ya kufunga kwa kunyamaza, Hiyo ndiyo iliyokuwa Swaumu ya waisrail wakati huo.

Kwa hiyo leo sitasema na mtu.

Hapana haja ya ufafanuzi hapa, isipokuwa kufasiri matamshi, kwa sababu akili haina nafasi katika maudhui haya maadamu dhahiri ya maneno haigongani na hukumu ya kiakili katika maudhui haya; Tazama Juz; 3 (3:45–51) kifungu cha ‘Lisilowezekana kiakili na kidesturi.

4

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA KUMI NA SITA

فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا ﴿٢٧﴾

27. Akaenda naye kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu.

يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا ﴿٢٨﴾

28. Ewe dada wa Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu wala mama yako hakuwa kahaba.

فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا ﴿٢٩﴾

29. Ndipo Akashiria kwake, Wakasema: Tutamsemezaje aliye bado mdogo susuni?

قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّـهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا ﴿٣٠﴾

30. Akasema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu amenipa Kitabu na amenifanya nabii.

وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا ﴿٣١﴾

31. Na amenijaalia ni mwenye popote pale niwapo. Na ameniusia Swala na Zaka muda wa kuwa niko hai.

وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا ﴿٣٢﴾

32. Na kumtendea mema mama yangu, Wala hakunifanya niwe jeuri muovu.

وَالسَّلَامُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدتُّ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا ﴿٣٣﴾

33. Na amani iwe juu yangu, siku niliyozaliwa na siku nitakayokufa na siku nitakay- ofufuliwa.

ذَٰلِكَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ قَوْلَ الْحَقِّ الَّذِي فِيهِ يَمْتَرُونَ ﴿٣٤﴾

34. Huyo ndiye Isa Mwana wa Maryam, kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.

مَا كَانَ لِلَّـهِ أَن يَتَّخِذَ مِن وَلَدٍ سُبْحَانَهُ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٣٥﴾

35. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu Kuwa na mwana, Yeye ametakasika! Anapolipitisha jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.

UMELETA KITU CHA AJABU

Aya 27 – 35

MAANA

Akaenda naye kwa jamaa zake amembeba.

Baada ya Maryam kuzaa, alimbeba mwanawe kwenda naye kwa watu wake, akiwa na utulivu bila ya kuwa na wasiwasi; kwani mimba ambayo ilikuwa ni sababu ya kutuhumiwa kwake, sasa ndiyo yenye ushahidi wa kweli wa usafi wake.

Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu kwa kudai kupata mimba bila ya kuguswa na mtu, huo ni uzushi.

Ewe dada wa Harun ! Huyu ni nduguye Musa, na yeye Maryam ni katika kizazi chao. Makusudio ya kumtaja ni kuwa asili yake ni watu wema na kwamba shina likiwa zuri matawi pia yanatakiwa yawe mazuri, sasa imekuwaje kutokewa na yaliyomtokea ambayo hakuna mfano aliyetokewa na hayo?

Baba yako hakuwa mtu muovu wala mama yako hakuwa kahaba.

Unafanana na nani wewe kwa kitendo chako hiki? Hawezi kufanya hivi ila binti wa muovu au wa mama muovu.

Ndipo akaishiria kwake

Yaani kwa mtoto aweze kushuhudia usafi wake naye ni mkweli zaidi ya wanaoshuhudia, kwa sababu anatamka kwa lugha ya Mwenyezi Mungu.

Wakasema kwa mshangao; Tutamsemezaje aliye bado mdogo susuni?

Lakini yule aliye susuni alianza kuwasemesha kabla wao hawajaanza na akasema:

Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu amenipa Kitabu na amenifanya ni nabii.

Yaani atanifanya ni nabii baadaye, kwa sababu kitoto kichanga hakiwezi kuongoza watu na kuwa ni hoja kwao. Ikiwa yeye mwenyewe hana majukumu kwa kauli yake wala vitendo vyake. Atawezaje kuwa na majukumu ya kufikisha risala ya Mwenyezi Mungu kwa waja wa Mwenyezi Mungu?

Huko nyuma tumesema kuwa alitumwa kuwa Mtume akiwa na miaka 30; na kwamba alizungumza utotoni ili kumsafisha mama yake na tuhuma ya zina na uchafu; si kwa kuwa alikuwa ni nabii aliyetumwa, Angalia kifungu ‘Isa na utume wa utoto’ katika Juz.7 (5:109 –111).

Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo.

Kila anayewanufaisha watu kwa namna moja au nyingine basi ni mweye kubarikiwa na kila mwenye kumdhuru mtu mmoja - sikwambii watu wengi- basi huyo ni muovu na mfisadi.

Na ameniusia Swala na Zaka muda wakuwa niko hai na kumtendea mema mama yangu.

Yeye mwenyewe anakiri utumishi na utiifu kwa Mungu na kukana kuwa ni Mungu, mwana wa Mungu au mshirika wake; kama wanavyodai wanaswara (wakristo).

Wala hakunifanya niwe jeuri muovu; kama wanavyodai mayahudi. Bali ni mja mwema na Mtume; kama wanvyoitakidi waislamu.

Na amani iwe juu yangu, siku niliyozaliwa na siku nitakayokufa na siku nitakayofufuliwa.

Umepita punde mfano wake katika Aya 15 ya sura hii.

Huyo ndiye Isa mwana wa Maryam, kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.

Hili ndilo neno la kweli, la kielimu na la kiadilifu, kuhusu Bwana Masih.

Sio mjeuri kama wanavyosema mayahudi; wala si Mungu, mwanawe au mshirika wake; kama wasemavyo wanaswara. Yeye ni Nabii anayefikisha risala ya Mola wake na ni mja miongoni mwa waja wake, anaswali na kutoa Zaka. Vile vile yeye ni mwenye kubarikia anayewanufaisha watu. Pia ni mnyenyekevu anayemfanyia wema mama yake.

Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Yeye ametakasika! Anapolipitisha jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa

Lau Mwenyezi Mungu angelikuwa na watoto wangelijifichia kheri zote na baraka na kuzizuia wengine wasizipate. Pia wangeharibu yale aliyoten- geneza vizuri baba na ulimwengu wangeliujaza shari na upotevu; sawa na wanavyofanya baadhi ya watoto wa viongozi siku hizi. Umepita mfano wake katika Juz. 3 (3:59) na katika Juz.15 (18: 111).

وَإِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٣٦﴾

36. Na Hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Mola Wenu, Basi muabuduni, Hii ndio njia iliyonyooka.

فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن مَّشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٣٧﴾

37. Lakini Makundi yakahitilafiana baina yao, Basi ole wao waliokufuru kuhudhuria siku iliyo kuu.

أَسْمِعْ بِهِمْ وَأَبْصِرْ يَوْمَ يَأْتُونَنَا لَـٰكِنِ الظَّالِمُونَ الْيَوْمَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٣٨﴾

38. Watasikia na wataona vizuri vilioje siku watakayotufikia! Lakini madhalimu leo wako katika upotofu uliodhahiri.

وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na waonye siku ya majuto itakapopitishwa amri nao wamo katika ghafla wala hawaamini.

إِنَّا نَحْنُ نَرِثُ الْأَرْضَ وَمَنْ عَلَيْهَا وَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ ﴿٤٠﴾

40. Hakika sisi tutairithi ardhi na walio juu yake na kwetu sisi wata rejeshwa.

NJIA ILIYONYOOKA

Aya 36 – 40

MAANA

Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Mola wenu, basi muabuduni, Hii ndio njia iliyonyooka.

Aya hii inaungana na kauli ya Isa (hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu...) anawaamuru, kwenye kauli hii, wamwabudu Mungu mmoja wala wasimshirikishe na kitu chochote na kwamaba dini ya tawhid (kumpwekesha Mungu) ndio njia iliyo sawa; mwenye kuifuata ataokoka na mwenye kuiacha atapotea.

Lakini makundi yakahitilafiana baina yao.

Makundi hayo ni kaumu ya Isa. Kuna kundi lililosema kuwa Isa ni Mungu alishuka ardhini kisha akapanda mbinguni, kundi la pili likasema kuwa ni mwana wa Mungu na kundi la tatu likasema ni mja wa Mwenyezi Mungu. Tofauti ilikuwepo hapo zamani, lakini hivi sasa makundi yote yameafikiana kuwa Isa ni Mungu.

Basi ole wao waliokufuru kuhudhuria siku iliyo kuu

Makusudio ya waliokufuru hapa ni kundi la kwanza na la pili. Aya hii ni ibara nyingine ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

ذَٰلِكَ ظَنُّ الَّذِينَ كَفَرُوا فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِنَ النَّارِ ﴿٢٧﴾

“Hiyo ni dhana ya waliokufuru ole wao waliokufuru na moto.”(38:27).

Watasikia na wataona vizuri vilioje siku watakayotufikia!

Makafiri watakapoiona adhabu siku ya Kiyama watasema:

رَبَّنَا أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَارْجِعْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا إِنَّا مُوقِنُونَ ﴿١٢﴾

“Mola wetu! Tumeshaona na tumeshasikia, Turejeshe tukatende mema, kwani hakika sisi tumekwishakuwa na yakini”(32:12).

Walipokuwa wakilinganiwa kwenye haki walikuwa wakisema:

قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا وَقْرٌ ﴿٥﴾

“Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayotuitia na masikio yetu yana uziwi” (41:5)

Lakini madhalimu leo wako katika upotofu ulio dhahiri.

Makusudio ya leo hapa, ni siku ya Kiyama; na upotofu ni adhabu, kwa vile siku hiyo hakutakuwa na njia ya uongofu wala upotofu; bali ni hisabu na malipo, hakuna zaidi ya hivyo.

Na waonye siku ya majuto itakapopitishwa amri nao wamo katika ghafla wala hawaamini

Anaaambiwa Mtume(s.a.w.w) awaonye, Siku ya majuto ni Kiyama. Imeitwa hivyo kwa sababu nafsi yenye hatia siku hiyo itasema:

يَا حَسْرَتَىٰ عَلَىٰ مَا فَرَّطتُ فِي جَنبِ اللَّـهِ وَإِن كُنتُ لَمِنَ السَّاخِرِينَ ﴿٥٦﴾

“Ee majuto yangu kwa yale niliyoyapoteza upande wa Mwenyezi Mungu na hakika nilikuwa miongoni mwa wanofanya maskhara.”(39:56).

Amri itapitishwa siku hiyo ambapo hakutakuwa na kubatilika wala kurejea. Wao hivi sasa wameghafilika, kwani wanaweza kujirudi kufuru yao na upotevu wao, wamuombe Mwenyezi Mungu msamaha, lakini wao hawafanyi, na wameendelea na uasi wao.

Kauli yake Mwenyezi Mungu:wala hawaamini, ni kuwa wao hawaisadiki kauli yetu, kwamba wao watafufuliwa, bali wanapeta vichwa vyao huku wakifanya maskhara.

Hakika sisi tutairithi ardhi na walio juu yake na kwetu sisi watarejeshwa.

Ardhi na vilivyomo ni vya Mwenyezi Mungu, hakuna yeyote mwenye kumiliki kitu. Binadamu ni mpita njia tu. Na kila kilicho mikononi mwa mtu ni cha kuazimwa tu, ana majukumu na kuwajibika nacho ili ahisabiwe kwacho.

Kwa ufupi Aya hii inarudufu neno: “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na Kwake Yeye tutarejea.” Juz. 2 (2:156). Makusudio yake ni kumhadharisha muasi, kumkemea na kupunguza huzuni ya Mtume(s.a.w.w) na uchungu wake kwa kupingwa mwito wake.

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِبْرَاهِيمَ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا ﴿٤١﴾

41. Na mtaje Ibrahi mkatika Kitabu hakika yeye alikuwa mkweli sana, Nabii.

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا ﴿٤٢﴾

42. Alipomwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa nini Unaabudu visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa na chochote.

يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا ﴿٤٣﴾

43. Ewe baba yangu! Hakika imenifikia elimu isyokufikia wewe, Basi nifuate mimi nitakuongoza njia iliyo sawa.

يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ عَصِيًّا ﴿٤٤﴾

44. Ewe baba yangu! Usiabudu Shetani. Hakika shetani ni Mwenye kumuasi Mwingi wa rehema.

يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا ﴿٤٥﴾

45. Ewe baba yangu! Mimi nakuhofia isikupate adhabu ya Mwingi wa rehema ukawa ni walii washetani.

قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنْ آلِهَتِي يَا إِبْرَاهِيمُ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ وَاهْجُرْنِي مَلِيًّا ﴿٤٦﴾

46. Akasema: Unaichukia miungu yangu ewe Ibrahim! Kama hutakoma, Basi lazima nitakupiga mawe na niondokelee mbali kwa muda.

قَالَ سَلَامٌ عَلَيْكَ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّي إِنَّهُ كَانَ بِي حَفِيًّا ﴿٤٧﴾

47. Akasema Ibrahim: Amani iwe juu yako (salamun alayka)! Nitakuombea msamaha kwa Mola wangu Hakika yeye ananihurumia sana.

وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَأَدْعُو رَبِّي عَسَىٰ أَلَّا أَكُونَ بِدُعَاءِ رَبِّي شَقِيًّا ﴿٤٨﴾

48. Nami na ajitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyez Mungu na ninamuomba Mola wangu asaa nisiwe na bahati mbaya.

فَلَمَّا اعْتَزَلَهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَكُلًّا جَعَلْنَا نَبِيًّا ﴿٤٩﴾

49. Alipojitenga nao na yale wanayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tulimpa Is-haq na Ya’qub na kila mmoja tukamfanya nabii.

وَوَهَبْنَا لَهُم مِّن رَّحْمَتِنَا وَجَعَلْنَا لَهُمْ لِسَانَ صِدْقٍ عَلِيًّا ﴿٥٠﴾

50. Na tukawapa katika rehema zetu na tukawajaalia kuwa na sifa za kweli tukufu.

IBRAHIM

Aya 41-50

MAANA

Na mtaje Ibrahim katika Kitabu hakika yeye alikuwa mkweli sana, Nabii.

Makusudio ya Kitabu hapa ni Qur’an. Ukweli ni sifa bora na ya ukamilifu zaidi. Tunalolifahamu kutokana na wasifu wa utume baada ya ukweli, ni kuwa yeye kwa maumbile yake ni mkweli hata kama si mtume.

Katika Juz; 7: (6:74) tumetaja tofauti za maulama katika makusudio ya baba wa Ibrahim, aliyetajwa katika Qur’an, kuwa je, ni baba yake wa hakika au ni baba wa kimajazi au ni ndugu wa baba? Tukasema huko, kuwa hakuna faida ya mzozo huu na kwamba lililo wajib kwa mwislamu ni kuamini utume wa Ibrahim(a.s) . Ama kuitakidi uislamu wa baba yake hilo halihusiani na dini; hasa kwa kuwa dhahiri ya Qur’an inafahamisha ukafiri wake.

Kwa vyovyote iwavyo, ni kuwa Ibrahim alimpa mwito baba yake, awe wa kimajazi au wa kihakika, wa uislamu na akamwambia katika yale aliyomwambia:

Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa na chochote?

Baba yake alikuwa akiabudu masanamu, kwa hiyo akamuhoji kwa manti- ki ya kiakili na kimaumbile. Mawe yaliyonyamaza, hayadhuru wala kunufaisha, unayaabudu na kuyasujudia? Iko wapi akili yako na fahamu yako?

Ewe baba yangu! Hakika imenifikia elimu isiyokufikia wewe, Basi nifuate mimi nitakuongoza njia iliyo sawa.

Kila anayekataa ibada ya masanamu anakuwa na ufahamu na akili zaidi kuliko wanayoyaabudu; sikwambii tena mitume wanaopata elimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa kutojua kunakuwa ni udhuru kwa yule asiyejua, lakini masanamu hayo yenyewe hayawezi kuacha udhuru kwa anayeyaabudu.

Ewe baba yangu! Usiabudu shetani. Hakika shetani ni Mwenye kumuasi Mwingi wa rehema.

Makusudio ya kumwabudu shetani ni kumtii, kwa sababu Mwenye kukitii kitu atakuwa amekiabudu; Kwa hiyo basi kila anayemuasi Mwenyezi Mungu atakuwa amemuabudu shetani.

Ewe baba yangu! Mimi nakuhofia isikupate adhabu ya Mwingi wa rehema ukawa ni walii wa shetani.

Walii wa shetani inaweza kuwa kwa maana ya kutawaliwa na shetani au kwa maana ya kuwa mtawala wa shetani katika kuabudu masanamu; sawa na kusema: watu wanajilinda na shetani na shetani anajilinda na watu. Katika makadirio yote, ni kuwa lengo ni kuhofisha na kuhadharisha kumtii shetani na kumfuata.

Akasema: Unaichukia miungu yangu ewe Ibrahim! kama hutakoma, basi lazima nitakupiga mawe na niondokelee mbali kwa muda.

Tulipokuwa tukisoma huko Najaf, siku moja tukiwa tumemzunguka mwal- imu wetu akifafanua maswala muhimu ya elimu ya misingi ya fiqh (Usuulul-fiqh) baada ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wake wote wamefahamu, alihitimisha darasa, lakini ghafla mmoja wa wanafunzi akamuuliza swali ambalo lilikuwa mbali kabisa na maudhui ya darasa. Basi mwalimu akaachana naye akawaangalia wanafunzi wengine na akasema:

“Hapo zamani palikuwa na mwanafunzi mmoja aliyejifundisha masuala ya Swaumu kwa mwalimu kwa muda wa zaidi ya mwezi. Baada ya kumaliza darasa yake mwalimu akadhania kuwa mwanafunzi wake ameelewa kila kitu kinachohusiana na Swaumu, lakini mwanafunzi akamwambia umeeleza sana na ukafafanua masuala ya Swaumu, lakini hatukufahamu kuwa Swaumu inakuwa usiku au mchana?!”

Haya hasa ndiyo yaliyompata Ibrahim pamoja na baba yake. Baada ya kumpa dalili zote na kumbembeleza kwa kumwambia ‘ewe baba yangu’ mara nne, lakini alimjibu kwa kumwambia kuwa kweli umeazimia kutowaabudu miungu pamoja nami? Ikiwa ni kweli umeazimia hivi, basi mimi sina jengine ila nikurujumu na kukuua au uniondokelee mbali nisikuone machoni mwangu.

Akasema Ibrahim: Amani iwe juu yako (salamun alayka)! Nitakuombea msamaha kwa Mola wangu, Hakika yeye ananihurumia sana”

Yaani Mwenyezi Mungu anamwitikia maombi yake, Umetangulia mfano wake katika Juz:11 (9:114).

Nami najitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu na ninamuomba Mola wangu asaa nisiwe na bahati mbaya.

Ibrahim aliwabughudhi watu wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akawaondokea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akambadilisha familia bora kuliko wao, pale alipompa Is-haq na baada yake Ya’qub bin Is-haq na akawatukuza kwa utume.

Hayo ndio makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Alipojitenga nao na yale wanayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tulimpa Is-haq na baada ya Is-haq ni Ya’qub na kila mmoja tukamfanya Nabii.

Hakuna aliyeacha kitu katika mambo ya dunia kwa kutengeneza dini yake ila humbadilishia bora zaidi yake.

Na tukawapa katika rehema zetu

Mwenyezi Mungu hakubainisha aina ya alichowapa, kwa sababu neno rehema zetu linaashiria hilo. Inatosha kuwa ni zawadi radhi za Mwenyezi Mungu na neema zake.

Na tukawajaalia kuwa na sifa za kweli tukufu.

Makusudio ya sifa za kweli ni sifa wanazozikariri watu kizazi baada ya kizazi kusifia Ibrahim, Is-haq, Ismail na Ya’qub.

Aya hizi zinatia mkazo kwamba mwenye kumfanyia ikhlasi Mungu naye Mungu humsafisha na anakuwa pamoja naye popote alipo; sawa na alivyomfanyia Ibrahim(a.s) .

8

9

10

11

12

13