• Anza
  • Iliyopita
  • 12 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 25803 / Pakua: 2888
Kiwango Kiwango Kiwango
DALILI ZA KIAMA

DALILI ZA KIAMA

Mwandishi:
Swahili

DALILI ZA KIAMA

KIMEANDIKWA NA: HARUN YAHYA

KIMEFASIRIWA NA: SHUAYBU HUSEIN KIFEA

Dalili za Kiyama Katika kipindi chote cha historia ya ulimwengu Wanaadamu wameuelewa ukubwa wa milima na upana wake, na ukubwa wa mbingu kutokana na njia zao mbali mbali za uchunguzi ijapokuwa wamekuwa na fikra potofu kuwa maumbile haya yatadumu milele. Imani hii ndio iliyozaa falsafa za kishirikina na za kilahidi za Ugiriki na dini za Sumeria za Misri ya kale. Qur'an inatuambia kuwa wale wanaoamini hivi wapo katika hatia kubwa. Miongoni mwa vitu ambavyo Mwenyezi Mungu amevibainisha katika Qur'an ni kuwa Ulimwengu umeumbwa na kwamba utakuwa na mwisho wake. Ulimwengu, kama walivyo binadamu na viumbe vingine hai, utatoweka.

Dunia hii iliyopangiliwa vizuri ambayo imefanya kazi bila kasoro kwa mabilioni ya miaka, ni kazi yake Mola ambaye ameumba kila kitu, siku moja kwa amri yake itakoma kufanya kazi. Wakati huo tayari Mwenyezi Mungu amekwisha upanga. Wakati huo ambapo ulimwengu na kila kiumbe tokea vile visivyoonekana kwa macho hadi binadamu pamoja na Nyota na Magalaksi yatasita kufanya kazi, unaitwa "Saa" katika Qur'an. "Saa" hii haina maana kuwa muda wowote bali ni neno mahususi lililotumika katika Qur'an kuelezea wakati ambao dunia itakuwa imefika mwisho wake.

Pamoja na maelezo ya mwisho wa dunia, Qur'an ina maelezo ya kina ya namna tukio zima litakavyotokea; "Mbingu zitakapopasuka," "Bahari zitakapowashwa moto," "Milima itakapoendeshwa (angani kama vumbi)" "Jua litakapo kunjwa kunjwa". Kihoro na khofu ambayo watu watakuwa nayo katika tukio hili la kutisha imeelezwa kwa kina katika Qur'an. Aya zinasisitiza kuwa hakutakuwa na pa kukimbilia wala pa kujificha. Tunachoweza kukisema hapa ni kuwa Ulimwengu utakuwa katika janga kubwa ambalo halijawahi kutokea hapo kabla.

Aya nyingi za Qur'an zinabainisha kuwa suala la mwisho wa dunia limegusa hisia za watu wengi katika kila kipindi cha historia. Katika aya kadhaa inaelezwa kuwa watu walimuuliza Mtume (s.a.w) juu ya lini utakuwa mwisho wa dunia;

Wanakuuliza juu ya Saa hiyo (yaani Kiama) kutokea kwake kutakuwa lini? (7:187) ,

Wanakuuliza Kiama kutokea kwake kutakuwa lini? (79:42)

Mwenyezi Mungu akamuamrisha Mtume kulijibu swali hilo hivi; Ilimu yake iko kwa Mola wangu tu. Hakuna wa kuhidhirisha wakati wake ila yeye tu (7:187).

Hii maana yake ni kuwa Allah pekee ndiye aijuaye tarehe ya siku hiyo. Kutokana na aya hii tunaelewa kuwa elimu juu ya lini utafika wakati huo imefichwa kwa wanadamu. Lazima kuna sababu maalumu kwanini Mwenyezi Mungu ameifanya siku hii kuwa siri. La muhimu ni watu kujihadhari nayo; Ambao wanamuogopa Mola wao hata wanapokuwa Faraghani, na pia hukiogopa kiama (21:49). Kwahiyo watu wachunge mamlaka ya Mwenyezi Mungu na wautafakari ukubwa wake. Kabla ya siku hiyo ya machungu na majonzi haijawatokea kwa ghafla, watu waelewe kuwa mbali na Mwenyezi Mungu hakuna mahala pa kukimbilia. Kama siku ya mwisho ingejulikana watu walioishi huko nyuma pengine wasingelazimika kuufikiria kwa makini mwisho wa dunia, wasingejali matukio ya mwisho yaliyotajwa katika Qur'an.

Ispokuwa lazima ieleweke kuwa kuna aya nyingi zinazoelezea Saa hiyo na pale tunapozisoma tunakutana na ukweli madhubuti. Qur'an haitaji muda maalumu wa tukio hilo, bali inaelezea matukio ambayo yatatokea kabla yake. Aya hii inaelezea dalili kadhaa za saa hiyo;

Kwani wanangoja jingine ila Kiama kiwajie kwa ghafla? Basi alama zake (hicho Kiama) zimekwisha kuja. Kutawafaa nini kukumbuka wakati kitakapowajia? (47:18)

Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa Qur'an inaelezea dalili zinazoonesha kufika kwa siku ya mwisho. Ili kuzielewa dalili hizi lazima tuzitafakari aya hizi. Vinginevyo kama aya inavyosema tafakuri yetu haitakuwa na maana pale Kiama kitakapotekea kwa ghafla. Baadhi ya hadithi za Mtume (s.a.w.w) ambazo zimetufikia zinazungumzia dalili za Kiama. Katika hadithi hizi za Mtume (s.a.w.w) , kuna dalili za Kiama na maelezo ya kina kuhusu kipindi kinachokaribia kuhusu muda wa kukaribia Kiama, kipindi hiki ambacho dalili za Kiama zitatokea kinaitwa "Siku za Mwisho"

Suala la siku za mwisho na dalili za kiama, limevuta hisia za wengi katika kipindi chote cha historia ya Uislamu. Ndio maudhui makuu ya vitabu vingi vya wanazuoni na watafiti wa Kiislamu. Tunapoyakusanya pamoja maelezo yote haya, ndipo tutakapofikia hitimisho muhimu. Aya za Qur'an na hadithi za Mtume (s.a.w.w) zinaoneshakuwa kipindi cha siku za mwisho kimegawanyika katika awamu mbili:

Awamu ya kwanza: ni pale ambapo mitihani ya kiroho na mali itausibu Ulimwengu.

Awamu ya pili: inaitwa zama bora, ni wakati ambapo mafundisho ya kimaadili ya Qur'an yatatawala na kuleta ustawi bora wa mwanadamu. Zama hizi zitakapofika mwisho wake na dunia itakapoingia katika kipindi ambacho jamii zitaporomoka, Kiama kitakuwa kimefika.

Shabaha ya mfululizo huu wa mafundisho ya Qur'n ni kuzitazama dalili za Kiama kupitia aya za Qur'an na hadithi za Mtume (s.a.w.w) na kubainisha kuwa dalili hizi zimekwishaanza kujitokeza katika wakati huu tulionao.

Ule ukweli kwamba kujitokeza kwa dalili hizi kulikwisha elezwa karne 14 zilizopita umzidishie Muumini Imani kwa Allah na unyenyekevu kwake. Kitabu hiki kimetayarishwa kwa kuzingatia ahadi ya Mola wetu;

Sema sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, karibuni hivi atakuonesheni ishara zake na mtazifahamu (27:93)

Nukta yenye umuhimu makhsusi ambayo kwayo tunataka kumkumbusha msomaji ni kuwa Allah ndiye ajuaye ukweli juu ya kila kitu. Kama ilivyo katika mambo mengine yote, tuna chokijua sisi kuhusu mwisho wa dunia ni kile tu ambacho Allah amekibainisha kwetu.

1

DALILI ZA KIAMA

SAA INAKARIBIA

Watu wengi angalau hujuwa jambo fulani kuhusu siku ya mwisho na karibu kila mmoja amesikia jambo hili au lile kuhusu kishindo cha saa hiyo. Hata hivyo wengi wanaonekana kuwa na mwenendo ule ule juu ya suaala hili kama walivyo katika masuala mengine yenye uzito mkubwa. Kwamba hawataki kulizungumzia au hata kulifikira jambo hili.

Wanajitahidi kwa kila hali kujighafilisha na khofu watakayo ipata siku ya mwisho. Hawajali ukumbusho wa siku ya mwisho uliomo katika kitabu juu ya msiba wa kuhuzunisha. Wanaepuka kuutafakari ukweli kuwa siku hiyo hapana shaka itafika. Hawataki kuwasikiliza watu wanaoizungumzia siku hii nzito au kusoma maandiko juu siku hiyo.

Hizi ni baadhi ya hila ambazo watu wamezidumisha ili kuepuka kuifikiria hatari ya siku ya mwisho. Wengi hawaamini kwa dhati kuwa saa hiyo inakuja. Tumepewa mfano wa watu hawa katika aya moja ya suratil-al-Kahf inayomzungumzia tajiri aliyemiliki bustani; ambaye alikitilia shaka Kiama;

Wala sidhani kuwa Kiama kitatokea. Na kama (kitatokea hicho Kiama) nikarudishwa kwa Mola wangu, bila shaka nitakuta kikao chema kuliko hiki (alichonipa Ulimwenguni) (18:36)

Aya hiyo inabainisha taasubi ya mtu anayemuamini Allah lakini anayekwepa kufikiria hakika ya siku ya mwisho na anatoa madai yanayopingana na aya za Qur'an. Aya nyingine inaelezea wasi wasi na mashaka yaliyowajaa makafiri kuhusiana na siku ya mwisho;

Na wale waliokufuru wataambiwa je! Hazikuwa aya zangu zikisomwa kwenu, nanyi mkajivuna na mkawa watu waovu? Na inaposemwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Kiama hakina shaka mlikuwa mkisema; hatujuwi Kiama ndio nini; hatudhani ila dhana tu wala hatuna yakini. (45:31-32).

Watu wengine ndio kabisa wanakana kuwa Kiama kipo. Wale wenye dhana hii wanatajwa hivi katika Qur'an:

Bali wanakadhibisha Kiama na tumewaandalia wanaokadhibisha Kiama Moto mkali kabisa. (Moto huo utakapowaona tokea mbali kabisa watasikia hasira yake na ngurumo yake). (25:11).

Chanzo kinachoweza kutuongoza katika njia sahihi na kutubainishia ukweli ni Qur'an. Tunapoangalia yale inayoyaelezea, tunabaini ukweli ulio dhahiri. Wale wanaojidanya kuhusu siku ya mwisho wanafanya dhambi kubwa sana, kwani Allah anabainisha katika Qur'an kuwa hakuna shaka yoyote siku ya mwisho ikaribu:

Na kwamba Kiama kitakuja, hapana shaka ndani yake;

Na kwa hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini (22:7) Na hatukuziumba Mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake ispokuwa kwa haki. Na bila shaka Kiama kitafika (15:85)

Kwa yakini Kiama kitakuja, nacho hakina shaka lakini watu wengi hawaamini (40:59).

Yawezekana kuna watu wanaodhani ujumbe wa Quraan kuhusiana na siku ya mwisho ulifunuliwa zaidi ya miaka 1400 iliyopita na kwamba hiki ni kipindi kirefu kulinganisha na muda wa maisha ya binadamu. Lakini hapa ni suala la mwisho wa dunia, jua, nyota na kwa kifupi ulimwengu mzima. Tunapo chukulia kuwa ulimwengu una umri wa mabilioni ya miaka, karne kumi na nne ni kipindi kifupi sana cha wakati. Mwanazuoni mkubwa wa kiislamu wa zama hizi, Bediuzzaman Said Nursi alilijibu swali hilo namna hii :

Saa (ya kufika kiyama) imekaribia (54 :1) kwamba siku ya mwisho iko karibu. Hata kama ni baada ya miaka elfu moja au miaka mingi zaidi ya hii bado hili halivurugi ukaribu wake. Kwa sababu siku ya mwisho ni saa iliyopangwa kwa ajili ya ulimwengu, na katika uwiano wa maisha ya ulimwengu, miaka elfu moja au elfu mbili ni sawa na dakika moja au mbili katika mwaka. Kwa hiyo siku ya mwisho sio tu ni saa iliyopanga kwa ajili ya binadamu kwamba ionekane iko mbali sana.

Kuhubiriwa kwa mafundisho ya Qur'an ulimwenguni Katika Quran, tunakuta maneno yanayorudiwarudiwa; suna ya Allah yaani kawaida au dasturi [Sunnat Lllahi]: huu ni msemo wenye maana ya njia au sheria ya MwenyeziMungu. Kwa mujibu wa Quraan,sheria hizi hazibadiliki daima. Aya inasema: Hii ni kawaida ya mwenyezimungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani; walahutapata mabadiliko katika kawaida ya mwenyezimungu. (33:62)

Kanuni mojawapo ya mwenyezimungu isio badilika nikuwa, kabla ya mangamizi,kwanza jamii hupelekewa muonyaji[mjumbe].ukweli huu unabainishwa kwa maneno haya: Walahatukuangamiza mji wowote ila ulikuwa na waonyaji wa kuwakumbusha wala hatukuwa madhalim,tukawawngamiza pasina kuwapelekea waonyaji] (26:208-209). Katika historia yote, Mwenyezi Mungu ametuma muonyaji au mkumbushaji kakika kila jamii iliyokengeuka, akiwalingania kufuata njia sahihi. Sasa wale walio endelea nauovu wao ndio walio angamizwa baada ya kutimiza ule muda waliopangiwa na wakawa fundisho kwa vizazi vilivyo fuata. Tunapo iangalia kanuni hii ya mwenyezi Mungu siri nyingi muhimu zina bainika kwetu Siku ya mwisho ni msiba wa mwisho utakao ukumba ulimwengu. Quraan ni kitabu cha mwisho cha mwenyezi Mungu kilichoshushwa kuwanasihi walimwengu. Muongozo wa Qur'an utabakia hadi mwisho wa dunia. Moja ya aya zake inasema-

Hayakuwa haya ila nimawaidha kwa watu wote (6:90). Wale wanaodhani kuwa Qur'an inazungumzia wakati au mahali fulani wanakosea sana kwasababu Qur'an ni wito wa jumla kwa walimwengu wote. Tokea wakati wa Mtume (s.a.w.w) ujumbe wa Qur'an ulikwishaenea duniani kote. Kutokana na maendeleo ya makubwa ya Teknolojia ya zama zetu,Qur'an yaweza kusambazwa kwa wanadamu wote. Hivi leo, sayansi, elimu, mawasiliano na usafilishaji vinafikia hatua ya mwisho ya maendeleo yao hasa hasa tekinolojia ya kompiuta na mtandao wa Internent, watu katika sehemu mbalimbali wanaweza kubadilishana taarifa papo kwa hapo.

Mapinduzi ya sayansi na tekinolojia yameunganisha mataifa yote ya dunia nzima maneno kama utandawazi (Globolization) yameongezwa katika msamiati. Kwa kifupi vikwazo vyote vinavyo kwaza umoja wa walimwengu vinaondoshwa kirahisi tu. Kwakuzingatia ukweli huu ni rahisi kusema kuwa katika zama zetu hizi za mawasiliano ya papo kwa hapo, Mwenyezi Mungu ameweka aina zote za maendeleo ya tekinolojia kwa manufaa yetu ni jukumu la Waislamu kutumia vema tekinolojia hizi kwa ajili ya dawa katika maisha yote ili watu wayapate mafundisho ya Qur'an.

2

DALILI ZA KIAMA

MITUME

Tumezungumzia kanuni zisizobadilika ambazo zimewekwa na Allah tokea kuumbwa kwa ulimwengu.kanuni ya Allah nikuwa yeye hatoiadhibu jamii ambayo hajaipelekea mjumbe.ahadi hii imetolewa katika aya zifuatazo:

Na Mola wako haangamizi miji mpaka ampeleke mtume katika mji wao mkuu,awasomee Aya zetu [wakatae ndio wangamizwe]walahatuiangamizi miji mpaka watu wake wamekuwa madhalimu. (28:59)

Na sisi si wenye kuwadhibisha[viumbe]mpaka tuwapelekee mtume.(17;15).

Wala hatukuangamiza mji wowote ilaulikuwa na waonyajikuakumbusha wala hatukuwa madhalimu.(26;208-209).

Aya hizi zinabainisha kuwa Mwenyezi Mungu kuwatuma Mitume kwenye miji mikuu kuwaonya watu. Mitume hawa huyahubiri maamrisho ya Mwenyzi Mungu lakini makafiri katika kila zama wamewadhihaki Mitume hawa nakuwaita waongo,wandawazimu na kuwasingizia kila jambo. Kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu huziangamiza jamii zinazoendelea kuishi katika maovu. Huwapelekea mangamizi katika wakati wasiotarajia kabisa. Kuangamia kwa watu wa Nuhu , Lutwi, Aadi, Thamuud na wengine waliotajwa katika Qur'an ni mifano ya aina ya maangamizi haya.

Katika Qur'an , Mwenyezi Mungu anabainisha sababu ya kutuma mitume;nayo ni kutoa habari njema katika jamii, kuwapa watu fursa muhimu ya kuachana na imani zao potofu na kuishi kwa kufuata dini ya Allah na kuwaonya watu ili wasipate kisingizio siku ya mwisho. Aya hii ya Qur'an inasema:

Hao ni mitume waliotoa habari nzuri kwa watu , wakawaonya ili wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletwa mitume. NaMwenyezi Mungu ni mwenye nguvu na mwenye Hekima.(4:165)

Kama inavyosema aya ya 40 ya suratil Ahzab , Mtume Muhammad ni mtume wa mwisho, 'Muhammad ni mtume wa Mungu na mwisho wa mitume.'

Kwa maneno mengine, baada ya Mtume Muhammad, Wahy kutoka kwa Allah umekamilika. Hata hivyo jukumu la kuwafikishia watu ujumbe na kuwakumbusha watu limebakia kwa kila Muislamu hadi siku ya mwisho. Miongoni mwa maudhui ya Qur'an ni yale yanayohusu watu ambao Mwenyezi Mungu amewangamiza kwasababu ya uovu na uasi wao. Na mafundisho yanayopatikana kutokana na maangamizi yaliyowafika watu hao. Kuna mlingano mkubwa kati ya jamii hizo zilizopita na jamii yetu ya leo.

Hivi leo kuna watu ambao tabia na mwenendo wao wa maisha ni mbaya zaidi kuliko hata ule mwenendo mchafu wa watu wa Lut, au ule wa dhulma wa watu wa Madian au ule wa kibri na dharau wa watu wa Nuhu au ule wa uasi na uovu wa watu wa Thamud au ule wa kukosa shukrani wa watu wa Iram pamoja na jamii nyingine zilizoangamizwa. Sababu ya wazi ya upotevu wa kimaadili wa watu hao ni kuwa walimsahau Mwenyezi Mungu na lengo la kuumbwa kwao.

Mauaji, dhulma katika jamii, ufisadi, udanganyifu na mmomonyoko wa maadili katika zama hizi vimewafikisha watu mahala pa kukata tamaa. Lakini, isisahaulike kuwa Qur'an inatutaka tusikate tamaa na rehma za Mwenyezi Mungu. Kukata tamaa na kupoteza matumaini ni mambo yasiokubalika kwa waumini. Mwenyezi Mungu ameahidi kuwa wale wanaomuabudia kwa ikhlasi bila kumshirikisha na viumbe vyake kama miungu badala yake na wanaofanya vitendo vizuri, watapata rehma yake na kunyanyuliwa katika nafasi ya juu:

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri kuwa atawafanya Makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya Makhalifa wale waliokuwepo kabla yao na kwa yakini atawasimamishia dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikishi na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo; basi hao ndio wavunjao amri zetu (24:55).

Katika aya nyingi, Qur'an inasema kuwa:

Ni kanuni ya Mwenyezi Mungu kwamba wale waja walioamini na kushikamana na dini sahihi katika nyoyo zao watafanywa warithi wa dunia hii: Na hakika tumeandika katika Zaburi baada ya (kuandika katika) Allawhul Mahfudh ya kwamba ardhi (hii) watairidhi waja wangu walio wema (21:105).

Na tutakukalisheni (nyinyi) katika nchi baada yao. Watapata haya wale waliogopa kusimamishwa mbele yangu na wakaogopa maonyo yangu. (14:14).

Na kwa yakini tumekwishaziangamiza umma nyingi kabla yenu, zilipofanya mabaya: Na waliwajia Mitume wao kwa hoja wazi wazi; lakini hawakuwa wenye kuamini. Namna hii tunawalipa watu wanaofanya uovu. Kisha tukakufanyeni nyinyi ndio wenye kushika mahala pao baada ya (kuangamizwa) hao katika ardhi ili tuone jinsi mtakavyotenda. (10:13-14). Musa akawaambia kaumu yake:

Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu na subirini. Ardhi ni ya Mwenyezi Mungu, atamrithisha amtakaye katika waja wake; na mwisho mwema ni wawamchao. Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia na (pia sasa) baada ya wewe kutujia. (Musa) akasema: Asaa Mola wenu atamwangamiza adui yenu na kukufanyeni watala katika nchi ili aone jinsi mtakavyofanya (7:128-129).

Sanjari na habari njema zilizotolewa katika aya hizo, Mwenyezi Mungu pia ametoa ahadi muhimu sana kwa waumini. Amebainisha katika Qur'an kuwa dini ya Uislamu imeshushwa kwa wanadamu ili izipiku dini zote (iwe juu ya dini zote):

Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu amekataa hivyo ataitimiza tu Nuru yake, ijapokuwa Makafiri wanachukia. Yeye ndiye aliyemleta Mtume wake kwa uwongofu na dini ya haki ili aijaalie kushinda dini zotep; ijapokuwa watachukia hao Makafiri (9:32-33).

Wanataka kuzima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao na Mwenyezi Mungu atakamilisha Nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia. Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu na kwa dini ya haki ili kuifanya ishinde dini zote, ijapokuwa makafiri watachukia(61:8-9).

Hapana shaka kuwa Mwenyezi Mungu atatimiza ahadi zake. Muongozo ambao utazishinda Falsafa zote potofu, itikadi potofu na mafundisho ya dini potofu ni muongozo wa Uislamu. Aya zilizonukuliwa hapo juu zinasisitiza kuwa makafiri hawawezi kuzuia jambo hili lisitimie. Wakati ambao muongozo wa Uislamu utakaposimama utakuwa wakati wa upendo, ukarimu, heshima, haki, Amani na ustawi wa kila mtu. Kipindi hiki kimeitwa kipindi kitukufu kwasababu ya kushabihiana kwake na mazingira ya pepo lakini hadi sasa zama hizo bado hazijawa. Zama hizo za kheri zitakuja kabla ya siku ya mwisho; hivi sasa zinasubiri wakati wake ambao Mwenyezi Mungu ameshapanga kuwa utafika tu.

3

DALILI ZA KIAMA

KURUDI KWA NABII ISA DUNIANI.

Isa au Yesu (a.s) ni Mtume aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu. Ni mmoja kati ya Mitume wanaozungumziwa sana katika historia ya dunia. Al-hamdulillahi kipo chanzo ambacho kwacho twaweza kupembua kipi sahihi na kipi si sahihi katika yale yaliyozungumzwa juu yake. Chanzo hicho ni Qur'an, kitabu pekee cha ufunuo ambacho hakija badilishwa wala kuhujumiwa.

Katika Qur'an tunasoma ukweli huu kuhusu Nabii Issa:

Masihi Issa bin Maryam ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni tamko lake (4:171)

Kumbukeni waliposema Malaika: Ewe Maryam! Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za neno litokalo kwake (la kukwambia 'zaa' utazaa). Jina lake ni masihi, Issa, mwana wa Maryam, mwenye heshima katika dunia na akhera, na ni miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyezi Mungu. (3:45)

Na (mtaje yule mwanamke) aliyejilinda, (aliyejihifadhi) nafsi yake, na tukampulizia Roho yetu na tukamfanya yeye na mwanaye kuwa miujiza kwa walimwengu (21:91).

Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utu uzima wake na atakuwa katika watu wema (kabisa) (3:46).

Issa (Yesu) alifanya miujiza kadhaa. Muujiza mwingine atakaofanya ni kuwa atarudi tena duniani katika siku za mwisho na atazungumza na watu.

Kisha tukawafuatisha nyuma Mitume wetu na tukamfuatisha Issa bin Maryam na tukampa Injili (57:27).

Bila shaka wamekufuru wale waliosema, Mwenyezi Mungu ni Masihi (Issa) bin Maryam (5:72).

Na makafiri (Mayahudi) walifanya (hila dhidi yake ili kumuua) na Mwenyezi Mungu akazipindua hila zao na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa kupindua hila (3:54).

Mwenyezi Mungu hakuacha Makafiri wamuue Issa/Yesu (a.s.), bali alimtowesha na akatoa habari njema kwa walimwengu kuwa siku moja atarudi tena duniani. Qur'an inatoa maelezo ya kurejea kwa Issa kwa ishara zifuatazo:

Na kwa ajili ya kusema kwao: Sisi tumemuua Masihi Issa Mwana wa Maryam Mtume wa Mungu hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine). Na kwa hakika wale waliohitilafiana katika suala hilo wamo katika shaka. Hawana yakini kabisa juu ya jambo hili ispokuwa wanafuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumuua (4:157)

Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake na Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu na mwenye hekma (4:158).

Katika aya ya 55 ya suratil Al- Imran, tunasoma kuwa Mwenyezi Mungu atawaweka juu ya makafiri wale watu wanaomfuata Issa hadi siku ya kufufuliwa. Ni ukweli wa kihistoria kuwa, miaka 2000 iliyopita wafuasi wa Issa hawakuwa na nguvu za kisiasa. Wakristo ambao wameishi enzi hizo na ambao wanaishi zama hizi wameamini itikadi nyingi potofu. Kubwa kuliko zote ni Itikadi ya Utatu.

Hivyo ni wazi kuwa hawataweza kuitwa wafuasi wa Issa kwani kama inavyoelezwa katika Qur'an, wale wanaoamini Utatu wametumbukia katika upotofu. Kwa hali hiyo katika kipindi hicho cha kuelekea kiama, wafuasi halisi wa Issa watawashinda wapotevu na wao ndio watakaotimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyotolewa katika Suratil-Al Imran. Bila shaka kundi hili tukufu litajulikana pale Issa atakaporudi tena duniani. Isitoshe Qur'an inasema kuwa watu wa kitabu wote watamuamini Issa kabla hajafa:

Na hakuna yeyote katika watu waliopewa kitabu ila humuamini Issa kabla ya kifo chake. Naye siku ya kiama atakuwa shahidi juu yao (4:159). Tunasoma wazi wazi katika aya hizi bado kuna ahadi tatu zinazomuhusu Issa ambazo bado hazijatimia. Kwanza kama walivyo binadamu wengine, Issa (a.s) atakufa. Pili Watu wote wa kitabu watamuona katika umbile lake la mwili na watamtii wakati akiwa hai. Hapana shaka kuwa biashara hizi mbili zitatimizwa pale Issa atakaporudi tena kabla ya siku ya mwisho. Bishara ya tatu juu ya Issa (a.s) kuwa shahidi juu ya watu wa kitabu, hiyo itatimizwa siku ya mwisho.

Aya nyingine katika Suratil Maryamu inaelezea kifo cha Issa (a.s) :

Na amani ipo juu yangu siku niliyozaliwa na siku nitakayokufa na siku nitakayofufuliwa (19:33).

Tunapoilinganisha aya hii na aya ya 55 ya suratil Al-Imran tunaweza kubaini ukweli muhimu sana. Aya ya suratil Al-Imran inazungumzia kunyanyuliwa kwa Issa. Katika aya hii hakuna taarifa inayotolewa kuwa Issa alikufa au la. Lakini katika aya ya 33 ya Suratil-Maryam, kifo cha Issa kinazungumziwa. Kifo hiki kitatokea pale Issa atakaporudi tena duniani na kuishi kwa muda fulani na kisha kufa (Allah ndiye ajuaye).

Aya nyingine inayoelezea kurejea kwa Nabii Issa (a.s) Duniani inasema:

Na (Mwenyezi Mungu) atamfunza (Isa) kitabu na kujua elimu na kujua Taurati na Injili. (3:48).

Ili kuelewa maana ya kitabu ambayo imetajwa katika lugha ya Kiarabu katika Aya hii, lazima tuziangalie aya nyingine za Qur'an ambazo zinahusiana na suala hili. Iwapo kitabu kinatajwa pamoja na Taurati na Injili katika aya moja, basi hiyo lazima iwe na maana kuwa kitabu hicho ni Qur'an. Aya ya tatu ya Suratil Al-Imrani yaweza kuwa mfano wa jambo hilo:

Mwenyezi Mungu, hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye - Mwenye uhai wa milele, na mwendeshaji wa mambo yote. Amekuteremshia kitabu kwa haki, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili zamani - ziwe uongozi kwa watu. Na akateremsha vitabu vingine vya kupambanua baina ya haki na Batil. (3:2-4).

Kwa hali hiyo kitabu kilichozungumziwa katika aya ya 48 ambacho Nabii Issa (a.s) anatakiwa kujifunza ni Qur'an tu. Tunajuwa kuwa Nabii Issa aliijuwa Taurati na Injili katika kipindi alichokuwa duniani ambacho ni takribani miaka 2000 iliyopita. Ni dhahiri kabisa kuwa ni Qur'an atakayoisoma pale atakaporudi tena duniani. Maelezo yanayotolewa na aya ya 59 ya Suratil Al-Imrani yanaonesha usawa baina ya Issa na Adam (a.s) :

Bila shaka hali ya Issa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam, alimuumba kwa udongo kisha akamwambia kuwa basi akawa. Katika aya hii twaweza kuona kuwa lazima viwepo vigezo vingi vya usawa baina Manabii hawa wawili. Kama tujuavyo, Adam na Issa (a.s.) wote wawili hawakuwa na Baba. Pia twaweza kupata usawa mwingine zaidi kutokana na aya ya hapo juu ambao ni kushuka kwa Nabii Adam ardhini akitokea peponi na kushuka kwa Nabii Issa kutoka alikohifadhiwa na Mwenyezi Mungu katika zama za mwisho. Qur'an inasema hivi kuhusu Issa:

Na kwa kweli (Issa) ni alama ya kiama, msikifanyie shaka na nifuateni. Hii ndio njia iliyonyooka. (43:61).

Tunajuwa kuwa Nabii Issa aliishi karne sita kabla ya Qur'an kushushwa. Kwa hiyo aya hii haizungumzii kipindi cha kwanza cha maisha yake bali inazungumzia kuja kwake tena duniani katika zama za mwisho mwisho. Ulimwengu wa Kiislamu na wa Kikristo kwa pamoja unamsubiri kwa hamu Nabii Issa. Ujio mtukufu wa mgeni huyu utakuwa ishara muhimu ya siku ya mwisho.

Aidha ushahidi mwingine zaidi wa kurudi kwa Nabii Issa unabainishwa na neno la kiarabu, Wakahlan katika aya ya 110 ya Suratil Maida na aya 46 ya Suratil Al-Imran. Katika aya hizi tunabainishiwa haya:

Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Issa Mwana wa Maryam! Kumbuka Neema yangu juu yako na juu ya Mama yako, nilipokusaidia kwa roho takatifu (Jibril), ukazungumza na watu katika Utoto wako na katika utu uzima wako (Wakahlan) (5:110).

Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utu uzima wake na (atakuwa) katika watu wema (kabisa) (3:46).

Neno hili (Wakahlan) linajitokeza katika aya hizi mbili tu na linamzungumzia Issa peke yake. Neno hili limetumika kuelezea umri mkubwa zaidi wa Issa. Neno hili linazungumzia makamo baina ya miaka 30 na 50 ambacho ni kipindi cha mwisho cha ujana na mwanzo wa utu uzima. Wanazuoni wa Kiislamu wameafikiana juu ya tafsiri ya neno hili ambayo ni kipindi kinachovuka umri wa miaka 35.

Wanazuoni hawa wanaegemea hadithi iliyosimuliwa na Ibni Abasi inayosema kuwa Issa (a.s) alinyanyuliwa kwa Allah wakati alipokuwa kijana yaani mwanzoni mwa miaka ya 30 na atakaporudi tena duniani atakuwa na miaka mingine 40 ya kuishi. Issa (a.s) ataendelea kuishi hadi uzeeni baada ya kurudi duniani, hivyo basi aya hii yaweza kuchukuliwa kama ushahidi wa kurejea tena kwa Issa (a.s) duniani.

Kama ilivyokwishaelezwa, tunapoiangalia Qur'an kwa makini, tunaona kuwa neno hili Wakahlan limetumika kumuelezea Issa tu. Manabii wote wamezungumza na watu na kuwalingania kufuata dini moja sahihi. Wote kati yao walileta ujumbe wakiwa na umri mkubwa. Lakini Qur'an haisemi chochote kuhusiana na jambo hilo juu ya Mtume mwingine yeyote. Neno hili limetumika kwa Issa (a.s) tu na huu ni muujiza.

Misemo hii miwili, "katika utoto wake" na katika "utu uzima" inagusia miujiza miwili mikubwa. Muujiza wa kwanza ni kuwa Issa alizungumza wakati akiwa mtoto mchanga. Hili ni jambo ambalo halikuwahi kutokea hapo kabla na Qur'an inalielezea tukio hili la kimiujiza mara kadha wa kadha. Mara baada ya maneno haya kuzungumza na watu utotoni yanafuata maneno kuzungumza na watu katika utu uzima. Maneno haya pia yanaelezea muujiza. Kama maneno katika utu uzima yangezungumzia maisha yake ya awali kabla hajatoweshwa na Allah, kusema kwa Issa kusingelikuwa muujiza.

Na kwa vile usingekuwa muujiza basi usemi huu usingelitumika baada ya ule usemi wa kuzungumza katika utoto au kwa namna ya kuelezea muujiza. Kwa hali hiyo ule usemi wa "katika utoto" hadi katika "utu uzima" ungetumika na ungeelezea umri wa Issa tokea pale alipoanza kusema utotoni hadi pale aliponyanyuliwa kwa Mwenyezi Mungu.

Lakini aya inatutaka tuzingatie matukio mawili makubwa ya kimiujiza. La kwanza ni lile la kuzungumza katika utoto na lingine ni lile la Issa kuzungumza katika umri wa utu uziama. Hivyo basi usemi huu wa utu uzima una maana kuwa wakati ambao utakuwa ni muujiza. Nao ni ule wakati ambapo Issa atazungumza na watu katika umri wa utu uzima baada ya kuwa amerudi tena duniani. (Allahu A'alam).

Katika hadithi za Mtume (s.a.w.w) kuna habari ya kurudi tena kwa Issa (a.s) Katika hadithi chache habari hii inazungumzwa na habari juu ya kile ambacho Issa (a.s) atakifanya pale atakapokuwa duniani. Yafaa kumkumbusha msomaji juu ya jambo moja muhimu sana. Kwamba Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa Walimwengu wote akiwa kama Mtume wa mwisho. Mwenyezi Mungu alimfunulia Qur'an Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuwataka watu wote wafuate mafundisho ya Qur'an hadi siku ya hukumu.

Issa (a.s) atarudi tena kimiujiza duniani katika zama za mwisho lakini, kama alivyosema Mtume (s.a.w.w) , hatoleta mafundisho mapya. Dini sahihi ambayo Mitume wote wamefundisha ni Uislamu ambayo Isa atapaswa kuifuata pale atakaporudi duniani. Katika Qur'an na katika Hadithi hakuna utata kuwa Issa (a.s) atarudi tena duniani katika zama za mwisho. Baada ya Waislamu kusema kuwa yumkini Isa (a.s) atarudi tena Duniani, na Mumammad (s.a.w.w) ni mtume wa mwisho, hakuna mpingano kati ya mambo haya mawili; Muhammad kuwa Mtume wa mwisho na Issa kurudi tena Duniyani.

Pale Issa atakaporejea kwa mara ya pili, hatoleta Dini mpya, bali atafuata yaleyale aliyofundisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) , Qur'an na Sunnah. Al-A'llama Imam Rabbani anasema ; "Issa (a.s) atashuka toka mbinguni , lakini atafuata njia ya Muhammad". [Imam Rabbani, Vol.11, Letter 67].

Imam Nawawi kasema Isa (a.s) atarejea na kufuata njia ya Muhammad (s.a.w.w). [Al-Qawl al-mukhtasar fi a'llamat al-Mahd al-Muntanzar]. Qadi Lyad nae kasema; Isa atatawala kwa sheria aizopewa Muhammad na atahuisha mambo ambayo watu wake waliyatelekeza. [Ibin Majah].

Mwanazuoni mkubwa wa karne iliyopita Bediuzzaman Said Nursi ametoa ufafanuzi muhimu juu ya suala hili katika kitabu chake Risalel Nnuur Collection. Kwa mujibu wa ufafanuzi wake, Isa (a.s) atarudi tena Duniani katika zama za mwisho, na atazihamisha itikadi zinazopingana na Uislamu. Chini ya uongozi wake, Wakristo watasilimu, Nguvu kubwa ya wapinzani wa Dini ya Haki itaondoshwa kabisa, imani za kipuuzi zitaondoshwa, na ulimwengu utafuata Qur'an. Labda swali muhimu linalotarajiwa kuulizwa ni je, Isa atatambuliwa namna gani? Au ni sifa gani zitakazowawezesha watu kumtambua Issa?

Jibu ni kuwa, atakuwa na dalili zote za Utume zilizotajwa katika Qur'an. Mbali na hivyo, atakuja na ishara zinazomthibitisha kuwa yeye ndiye Masihi Isa Bin Maryamu. Wakati atakapokuja hapatakuwa na hata mtu mmoja ambaye alipata kumuona hapo kabla. Ndio kusema hakutakuwa na mtu hata mmoja atakayemtambua. Hakuna atakayeweza kumtambua kwa haiba wala sauti yake. Hakuna atakayeweza kusema kuwa yeye alimjua hapo kabla kwa kiwiliwili chake au alimwona mahali fulani na hakutakuwa na hata mmoja aliyeiona familia au nduguze ili kuweza kumfananisha.

Wale wote waliomjua walikwishakufa miaka 2000 iliyopita. Maryamu (a.s) , Zakariya (as) , Wanafunzi(wafuasi) wake walioishi naye kwa miaka miwili ya ujumbe wake pamoja na wale wote waliokuwepo wakati wake walikwishakufa. Kama tulivyofafanua katika kurasa za mbele, kwa amri ya kun fayakun ya Mwenyezi Mungu, Isa aliweza kuja duniani bila baba. Mwenyezi Mungu anamfananisha Isa na Adamu katika aya hii:

Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adamu; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia "kuwa", basi akawa(3:59).

Ayah hii inabainisha kuwa Mwenyezi Mungu alisema "kuwa" Adamu akawa na Isa pia akawa kwa nyakati tofauti. Adamu hakuwa na mama wala baba wakati ambapo Isa hakuwa na baba lakini alikuwa na mama. Lakini akirudi tena duniani mama yake hatokuwa hai. Hivyo basi, ule ubabaishaji utakaokuwa umefanywa na Masihi wa uongo zama hata zama hautakuwa na hautaleta utatanishi. Hakutakuwa na shaka Isa kama ni yeye au la. Hakuna atakayepata kisingizo kusema huyo sio Isa (a.s). Kwa kumalizia hapa ni kwamba maelezo yote yaliyotolewa yatupelekee kutanabahi kuwa muda au miadi kuhusu kurudi tena kwa Yesu duniani na mambo atakayoyafanya, hauko mbali. Ahadi ya kurejea kwa Isa iwe changamoto kwetu ya kujiandaa kukutana naye.

4

DALILI ZA KIAMA

UTAFITI WA ANAGA NA UVUMBUZI

Sura ya 54 ya Qur'an inaitwa "Surat al- Qamar." Kwa kiswahili qamar tafsiri yake ni mwezi. Katika aya kadhaa sura hii inatutajia maangamizi yaliyowafika watu wa Nuhu, Ad, Thamud, Lut na Firaun kwasababu walikadhibisha mawaidha ya mitume. Wakati huo huo katika aya ya kwanza ya sura hii kuna ujumbe muhimu sana unaohusiana na siku ya mwisho:

Saa (ya kufika kiama) imekaribia; na Mwezi umepasuka (54:1).

"Neno kupasuka" lililotumika katika aya hii ni tafsiri ya neno Shaqqa, ambalo katika kiarabu lina maana mbali mbali. Miongoni mwa maana hizo ni kukatua, kulima au kuchimbua ardhi. Kutoa mfano wa hili tunaweza kurejea aya ya 26 ya suratil Al-Abasa:

Hakika tumemimina maji kwa nguvu (kutoka mawinguni). Kisha tukaipasua pasua ardhi. Kisha tukaotesha humo (vyakula vilivyo) chembe chembe. Na mizabibu na mboga. Na Mizaituni na Mitende. (80:25-29).

Kwahiyo maana ya neno "Shaqqa" hapa ni kukatua, kuchimbua ardhi ili kuotesha mimea mbali mbali. Kama tutarejesha kumbukumbu zetu mwaka 1969, tutaona moja ya maajabu makubwa ya Qur'an. Majaribio yaliyofanywa mwezini mnamo Julai 20,1969 yaweza kuwa kielezeo cha kutimia kwa maneno yaliyosemwa miaka 1400 iliyopita katika Suratil Qamar.

Katika tarehe hiyo, wanaanga wa Marekani walikanyaga mwezini. Wakachimba udongo wa mwezini na kufanya uchunguzi wa Kisayansi walichukuwa sampuli ya mawe na udongo. Kwa kweli hili ni jambo lenye mvuto mkubwa kwani kitendo hiki kinawafikiana kabisa na maelezo yaliyotolewa katika aya hiyo ya 26. Kusisitiza hili ni kwamba wakati wa Mtume hakuna mtu aliyejua kama mwezini kuna udongo mithili ya ardhi. Kwahiyo kutumika kwa neno shaqqa lenye maana ya kuchimba, kuchimbua au kukatua kama lilivyotumika katika aya hiyo ya 26 kunathibitishwa na huo uchunguzi wa mwaka 1969 ambapo wanaanga waliokwenda mwezini walichimba udongo wa mwezini ndio kusema wameitimiza kwa vitendo aya hiyo ya Qur'an. Ndio maana tunasema hii ni moja ya maajabu ya Qur'an.

Wakati wanaanga hawa walipochimba udongo wa mwezini, walikusanya kilo 15.4 za sampuli ya mawe na udongo. Sampuli hizi zikaja kuvuta hisia za wengi. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la anga la Marekani, NASA hamasa iliyoonyeshwa na watu juu ya sampuli hizi ilivunja rekodi ya hamasa zote zilizooneshwa katika safari zao zote za angani za karne ya 20. Safari ya mwezini inaelezewa kwa kauli mbiu hii "hatua moja ndogo ya mtu mmoja ni mwendo mkubwa wa kuruka kwa wanadamu wote". Huu ulikuwa ni wakati wa kihistoria wa utafiti wa anga. Ni tukio lililochukuliwa na Kamera, na kila mtu kutoka wakati huo hadi leo amelishuhudia.

Kama ilivyoelezwa katika aya ya kwanza ya Suratil al- Qamar, tukio hili kubwa lenyewe pia laweza kuwa ishara ya siku ya mwisho. Yaweza kuwa ishara kuwa ulimwengu upo katika siku za mwisho kabla ya hukumu. (Allahu A'alam). Mwisho hatuna budi kuzingatia kuwa kuna onyo kubwa kufuatana na aya hizi. Kuna ukumbusho kuwa ishara hizi zinatoa fursa muhimu kwa watu kuacha mwendo mbaya na kwamba wale wasiozingatia onyo hili basi watapata fadhaa kubwa pale watakapofufuliwa siku ya hukumu ambayo katika Qur'an inaelezewa kama siku yenye huzuni isiyoelezeka:

Saa (ya kufika Kiama) imekaribia na Mwezi umepasuka. Na wakiona muujiza hugeukia upande mwingine na kusema uchawi tu unazidi kuendelea! Ndio wamekadhibisha hivi na wamefuata matamanio ya nafsi zao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti. Na kwa yakini zimewajia habari zenye makatazo makubwa. Zenye hikma kamili lakini maonyo kwao hayafai kitu. Basi jiepushe nao. Na wakumbushe siku atakapoita mwiitaji huyo kuliendea jambo zito (la kiama). Macho yao yatainama chini, wanatoka katika makaburi kama kwamba ni Nzige waliotawanyika, wanamkimbilia muhitaji huyo na huku wanasema hao makafiri: Hii ni siku ngumu kabisa. (54:1-8).

Miaka 1400 iliyopita Mtume Muhammad (s.a.w.w) alitoa bishara nyingi kuhusiana na siku za mwisho na akaelezea maono yake juu ya wakati huo kwa maswahaba wake. Maneno haya muhimu yamerithishwa kwa vizazi na vizazi hadi kufikia leo hii. Yamo katika vitabu vya hadithi na katika maandiko ya wanazuoni wa Kiislamu.

Hadithi ambazo tutazinukuu katika kitabu hiki zina bishara hizo zilizotolewa na Mtume (s.a.w.w) Labda yaweza kuzuka shaka kwa msomaji kuhusiana na ukweli na usahihi wa hadithi hizi zinazozungumzia mwisho wa dunia. Ni ukweli unaofahamika kuwa, huko nyuma kulikuwa na hadithi nyingi za kughushi ambazo zilidaiwa kuwa za Mtume (s.a.w.w) lakini hadithi zinazoelezea mada yetu hii zitatambuliwa kirahisi kuwa zilitoka kwa Mtume (s.a.w.w) .

Kuna utaratibu wa kutofautisha hadithi sahihi na hadithi zisizo sahihi. Kama tujuavyo hadithi zinazozungumzia zama za mwisho zinahusiana na matukio yatakayotokea baadaye. Kwasababu hii pale hadithi inapothibiti kulingana na wakati, shaka zote juu ya chanzo chake huondoka.

Wanazuoni kadhaa wa Kiislamu waliofanya utafiti juu ya mada ya zama za mwisho na juu ya dalili za kiama wametumia kigezo hiki. Mwana taaluma wa fani hii, Ulamaa Bediuzzaman Said Nursi amesema kuwa ule ukweli kwamba hadithi zinazohusu zama za mwisho zimeshabihiana na matukio na mambo yaonekanayo katika zama zetu unabainisha ukweli wa hadithi hizo. Baadhi ya dalili zilizotajwa katika hadithi ziliweza kuonekana katika baadhi ya maeneo ya dunia katika wakati wowote ule wa historia ya miaka 1400 ya Uislamu.

Lakini hilo pekee lisingeliweza kuthibitisha kuwa kipindi hicho kilikuwa zama za mwisho. Ili kipindi kiitwe cha zama za mwisho basi zile dalili zote za siku ya mwisho lazima zionekane na zitokee katika kipindi hicho hicho. Hii inaelezwa katika hadithi: Dalili zinafuatana moja baada ya nyingine kama vile shanga za mkufu zinavyoanguka moja baada ya nyingine pale kamba yake inapokatika (Tirmidhi).

Tunapoziangalia zama za mwisho kwa kuzingatia maelezo yaliyotolewa hapo juu, tunaibuka na hitimisho la kuajabisha. Dalili ambazo Mtume (s.a.w.w) alizielezea kwa kina zinatokea, hivi leo moja baada ya nyingine katika kila pembe ya dunia kama vile vile zilivyoelezwa. Kwahiyo hadithi moja kwa moja zinatoa picha kamili ya wakati wetu. Huu kwa hakika ni muujiza unaohitaji mazingatio makubwa sana. Kila dalili inayotokea inawakumbusha watu kuwa zama za mwisho zimekaribia, ile siku ambayo watu watatoa wenyewe hesabu ya amali zao mbele ya Mwenyezi Mungu. Hivyo basi watu wanapaswa kurejea upesi upesi katika maadili ya Qur'an.

5

DALILI ZA KIAMA

VITA NA MACHAFUKO

Katika Hadithi moja Mtume (s.a.w.w) alizielezea zama za mwisho hivi: Mtume wa Allaha alisema:

Harji (itazidi kuongezeka), Watu wakauliza harji ndio nini? Akajibu, ni mauaji, ni mauaji. (Bukhari). Maana ya harji iliyotajwa katika hadithi ya hapo juu ya Mtume (s.a.w.w) ni "machafuko makubwa" na "vurugu" ambavyo havitaishia mahala pamoja bali vitaenea duniani kote.

Pia kuhusiana na swala hili maneno mengine ya Mtume yanasema:

Ile saa itafika wakati vurugu, umwagaji damu na machafuko yatakapokuwa mambo ya kawaida. (Al-Muttaqi Al-Hindi, Muntakhab Kanzul Ummaal) Ulimwengu hautakoma mpaka zije enzi ambapo kutakuwa na mauaji makubwa na umwagaji mkubwa wa damu (Muslim).

Tukizitafakari Hadithi hizo, tunafikishwa katika hitimisho muhimu. Mtume (s.a.w.w) alielezea mitafaruku, fujo, mauaji na vita vitavyoikumba dunia nzima na kuenea kwa hali ya khofu na akabainisha kuwa matukio haya ni ishara ya Kiama.

Tukiangalia katika karne 14 zilizopita, twaona kuwa vita vilikuwa vya Kinchi kabla ya karne 20. Hata hivyo vita ambavyo vimemuathiri kila mtu duniani, vilivyoathiri mifumo ya siasa, na mifumo ya uchumi na jamii, vimerindima zaidi katika nyakati za karibuni hususan katika vita kuu mbili za dunia.

Katika vita kuu ya kwanza ya dunia zaidi ya watu Milioni 20 walikufa, na katika vita kuu ya pili ya dunia, zaidi ya watu Milioni 50 waliuawa. Vita kuu ya pili ya dunia ndiyo inayotambuliwa kuwa ni vita iliyomwaga damu nyingi mno, iliyokuwa kubwa mno na iliyoleta maangamizi makubwa katika historia.

Teknolojia ya sasa ya Kijeshi ikiwa ni pamoja na Silaha za Kibaolojia, Kikemia na Nyuklia ndio iliyozidisha madhara ya vita katika kiwango ambacho hakijapata kutokea katika historia. Kutokana na silaha za maangamizi ambazo zimezidi kuboreshwa, inakubaliwa na wengi kuwa Ulimwengu hautaingia katika vita ya tatu ya dunia.

Migogoro ambayo imetokea baada ya vita kuu ya pili ya dunia, vita baridi, vita vya Korea, vita ya Vietnam, mgogoro wa Warabu na Waisrael vita vya Ghuba na Iraq ni miongoni mwa matukio mabaya sana ya wakati wetu. Hali kadhalika vita vya kieneo, migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisha maangamizi makubwa katika sehemu nyingi za dunia. Katika nchi kama Bosnia, Palestina, Chechnya, Iraq, Afghanistan, Kashmiri na sehemu nyingine nyingi, matatizo haya bado yanaendelea kumkumba mwanadamu.

Mfano mwingine wa machafuko yanayomuathiri mwanadamu mithili ya vita ni Ugaidi unaoratibiwa kimataifa kama wanavyokubali viongozi wengi kuwa vitendo hivi vya Ugaidi vimeongezeka mno katika nusu ya pili ya karne ya 20. Kwa kweli yawezekana kusema kuwa Ugaidi ni jambo makhususi la karne ya 20.

Jamii zilizobobea katika ubaguzi, Ukomunist na Itikadi nyingine kama hizo au zenye malengo ya Utaifa zimeshiriki katika vitendo vya kinyama kwa msaada wa teknolojia ya leo. Katika historia ya karibuni tu, vitendo vya Ugaidi mara kwa mara vimeleta maangamizi. Damu nyingi imemwagika na watu wasio na hatia ama wamejeruhiwa au wameuawa lakini bado wanadamu hawajapata fundisho kutokana na matukio haya ya balaa. Katika nchi nyingi za dunia Ugaidi unaendelea kuwa msingi wa tawala na sera.

Kuna aya nyingi katika Qur'an zinazohusiana na jambo hili. Katika Surati Arum inaelezwa kuwa machafuko yameikumba dunia kwasababu ya yale ambayo watu wameyafanya kwa mikono yao:

Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwasababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu ili awaonjeshe adhabu ya baadhi ya mambo waliyoyafanya, huenda wakarudi (wakatubia kwa Mwenyezi Mungu) (30:41). Hatuna budi kusema kuwa aya hii inatukumbusha ukweli muhimu sana. Machungu na Masahibu yanayotokana na makosa ya wanadamu yanatupa fursa ya kutanabahi na kuepuka kuyarudia.