• Anza
  • Iliyopita
  • 12 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 10686 / Pakua: 4474
Kiwango Kiwango Kiwango
UKWELI WA USHIA

UKWELI WA USHIA

Mwandishi:
Swahili

5 UKWELI WA USHIA

KUYAJENGEA MAKABURI

FUADI : Ewe Jaafar, je unaniruhusu nikuulize kuhusiana na maudhui ya Shia na Sunni?[13]

JAAFAR : Uliza kwani nina penda sana kila mtu awe ni mwenye kufahamu mambo, mwenye elimu na anae fahamu mambo kutokana na utafiti na kwa kupata yakinina hawi ni mwenye msimamo legelege na mwenye kufuata kila akisikiacho na kipepeacho angani, au kila sauti ijitokezayo na kutangaa anganibila ya kufahamu usahihi wake na ubatilifu wake au ufisadi wake.

FUADI : Je maneno yangu utayaamini ikithibitika kuwa sisi (Ahli sunna) ndio wenye haki?

JAAFAR : Kwa hakika mimi niko msitari wa mbele kati ya wale wenye kuamini mambo ya kweli haraka pale wanapo yafahamu, na mimi sikushikamana na ushia isipokuwa ni baada ya kuuona kuwa ni haki na wewe unafahamu ya kuwa baba yangu na mama yangu na ndugu zangu na watu wa kabila langu wote ni masunni na kati yao hakuna Shia hata mmoja, na mimi sikufuata Ushia isipokuwa ni kwa ajili ya ukweli nilio uona na kuukuta ndani ya madhehebu hayo.. na lau nitafahamu usahihi wa maneno yako mimi ni wa mwanzo kuyaamini.

FUAD : Nyie Mashia mnayajengea makaburi ya Manabii, Maimamu, Maulamaa na watu wemamajengo makubwa, mnasali kwenye makaburi, wakati jambo hilo ni shirki, kama washirikina wanavyo abudu masanamu nanyi Mashia mnaaabudu majengo ya makaburi ya mawalii.

JAAFAR : Ni wajibu sisi tuwe wakweli na tunao kwenda sambamba na uhakika wa mambo, tusiwe ni watu wachukuao maganda na kuacha kiini, tusiangalie yasemwayo na fulani au fulani, bali tuangalie ukweli ulio wazi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake(s.a.w.w) , na mwenendo wa watu wema walio tangulia.

FUAD : Ndio, nami ni hivyo hivyo, ninapenda kufahamu ukweli wa mambo kupitia njia za kielimu na ufahamu sahihi, si kufuata mambo ufuataji wa kipofu.

JAAFAR : Kwanza kabisa: Sio sisi Mashia pekee tuhusikao na suala la kuyajengea makaburi, kwani waislaam wote wanayajengea makaburi ya Manabii na Maimam na wanazuoni wakubwa au viongozi wao, na ifuatayo ni mifano juu ya hayo: Kaburi la Mtume(s.a.w.w) na makaburi ya makhalifa wawili bado hadi hivi sasa yamejengewa kwa jengo kubwa na yenye kuba kubwa na ya hali ya juu kabisa.

Makaburi ya Mitume kadhaa, kama vile kaburi la Nabii Ibrahim(a.s) lililoko Jodan katika mji wa (Al-khaliil) makaburi hayo yana dharihi (yamejengewa) na juu yake kuna kuba na majengo makubwa. Kaburi la Nabi Mussa(a.s) lililoko Jodan kati ya mji wa (Qudsi) na (Omman) lina jengo kubwa. Kaburi la Abi Hanifa lililoko Baghdad hadi leo bado limejengewa kwa jengo kubwa, na juu yake kuna kuba. Kaburi la Abi Hurairah katika (Misri) hufanyiwa ziara na limejengewa na juu yake kuna kuba. Kaburi la Abdul-qaadir lililoko (Baghdaad) kaburi hilo lina uwanja mkubwa na dharihi na juu yake kuna kuba.

Na makaburi mengine ya Mitume, na makaburi ya Maimamu na wanazuoni wakubwa wa madhehebu, yote hayo yana majengo na juu yake kuna kuba, na yana waqfu maalum ambapo waqfu hizo faida zake hutumika kuyaimarisha na kuyakarabati makaburi hayo na kuyalinda yasiharibike.

Na Miji ya kiislaam imejawa na majengo kama hayo.. na Waislaam wote pamoja na tofauti za madhehebu yao tangu siku ya kwanza hadi leo huyapenda mambo hayo, na huwaamrisha watu kuyatekeleza hayo, na hawakukataza kufanya hivyo hata siku moja, kwa hivyo si sisi Mashia pekee tuhusikao na hukumu hii, bali wanakubaliana nasi na kuwafikiana nasi Waislaam wengine wote, na wao pia huyajengea makaburi ya maimamu wao na wakati wote huyatembelea.

Pili: Sisi- Mashia- au waislaam wengine wakati tunapo Sali pembezoni mwa makaburi ya mawali, hatusali kwa ajili ya mawalii hao bali tunasali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee. Na liwezalo kukujulisha hilo ni kuwa sisi tunapokuwa katika sala huelekea kibla na wala hatuyaelekei makaburi hayo, na lau kama tunge kuwa tukiyasalia makaburi yale, na kuelekea kwenye ibada zatu kwenye dharihi zile (majengo yale ya makaburi), ingewajibika kuyaelekea, na tusinge elekea kwenye kibla.

FUAD : Kwa nini mnasali nyuma ya makaburi hayo, mpaka mkayafanya kuwa ni kibla chenu?

JAAFAR : Hakika sisi wakati tunapo Sali nyuma ya makaburi, tunaelekea kibla na wala hatuyaelekei makaburi, bali makaburi yale-imetokea tu- yakawa mbele yetu, bila ya sisi kukusudia kuyaelekea.

Na hili halitokei isipokuwa kwa mtu anae Sali akiwa ameelekea kibla katika sehemu fulani na ikatokea kwa mfano kukawa na jengo kubwa mbele yake, je kusali katika sehemu hiyo kunamaanisha kuwa mwenye kusali anaabudu jengo hilo?! Na zaidi ya hayo Maulamaa wote wa Waislaam wanasema kuwa: Inajuzu kusalia katika majumba ya ibada za washirikina hali ya kuwa umeelekea kibla hata kama mbele ya mwenye kusali kutakuwa na sanamu lenye kuabudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu, Kwani mwenye kusali humuelekea Mwenyezi Mungu na wala halielekei sanamu. Je hii inamaana kuwa mwenye kusali analiabudu sanamu lile?

FUAD : Ikiwa kuyajengea makaburi si shirki- kama unavyo sema- na waislam wote wanasema ya kuwa inajuzu kufanya hivyo, ilikuwaje wakavunja madharihi (majengo ya makaburi) na makuba yaliyo jengwa juu ya makaburi ya maimamu na wengineo, kwa hoja ya kuwa kufanya hivyo ni shirki na ni kumuabudu asie kuwa Mwenyezi Mungu, na maulamaa wa Hijazi wakatoa fat'wa ya kufanya hivyo?

JAAFAR : Kwa hakika ni baadhi tu walio toa fat'wa kama hiyo kati ya maulamaa wa Hijazi katika zama zile, kwani kuna baadhi ya Mashekhe waishio katika mji wa Madina walio nihadithia na kunisimulia kwa kusema: Kwa hakika wakati huo walipo toa amri ya kubomoa makuba na majengo ya makaburi, maulamaa wenyewe wa Hijazi walipinga amri hiyo, wakitoa hoja kuwa hilo si shirki bali vitu kama hivyo ni sunna katika sheria ya kiislaam, kutokana na kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:jambo lililo pelekea kufukuzwa kwa maulamaa wale, na kuwauz ulu wengine katika nyadhifa zao na kuwatenga. Kwa hivyo basi: Fat'wa hiyo haikutolewa isipokuwa na baadhi tu ya maulamaa wa Hijaz.

FUAD: Kwa hakika mimi nilikuwa nikifikiria na kujiuliza ya kuwa: Ikiwa kujenga madharihi na makuba ni haram na shirki, kwa nini maulamaa wa Waislaam hawakuzinduka na kuliona hilo tangu zama za Mtume(s.a.w.w) hadi leo, na kwanini hawakuzuwia kufanya hivyo? Na ilikuwaje Waislaam wasilifahamu hilo kwa muda wa karne kumi na tatu?

JAAFAR: Nitakuongezea elimu na maarifa: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alikiri na kukubali kujengea makaburi, madharihi na makuba na hakukataza kufanya hivyo. Kwa mfano hili ni jengo la hijri Ismail mahala alipo zikwa Nabi (Ismail) na sehemu alipo zikiwa mama yake Haajar. Na haya hapa makaburi ya Manabii wengine-kama Ibrahim Musa na wengineo- walio zikiwa pembezoni mwa baytul-maqdas, yalikuwa ni yenye majengo makubwa katika zama za Mtume(s.a.w.w) na hadi zama zetu hizi, na wala hakuzuwia yeyote si Mtume Mwenyewe (s.a.w) wala mmoja wapo kati ya makhalifa wake.

Na lau kama tendo hilo linge kuwa haram au linge kuwa ni shirki basi Mtume ange amuru kuvunjwa na kubomolewa kwa majengo na makuba hayo, na ange kataza kufanya hivyo. Na kutokana na ukweli kuwa hakufanya hivyo tunafahamu na kuwa na yakini ya kuwa mfano wa vitu kama hivyo au kufanya hivyo ni kitu kinacho juzu na kinafaa.

Hivyo hivyo baada ya kufariki Mtume(s.a.w.w) , kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo chukuliwa roho yake alizikwa katika chumba chake, na mlango wa chumba kufungwa, na kaburi lake likawa katikati ya chumba kilicho jengewa kuta na dari, na lau kama sahaba yeyote ange sikia kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) kuwa tendo kama hilo ni haram basi wasinge thubutu kumzika Mtume katika chumba hicho kilicho jengewa, na lau kama ingelazimika kumzika chumbani mwake basi ingekuwa wajibu kubomoa chumba hicho ili kaburi hilo lisiwe na jengo au lisiwe ni lenye kujengewa.

Na kutokana na kutofanya kwao hivyo, tukafahamu ya kuwa kujenga juu ya makaburi si haram, sasa vipi itakuwa ni shirki?.

FUAD: Ninakushukuru kwa wema wako kwani umeniongoza kwenye ukweli (haki), na kunijulisha ya kuwa kujenga juu ya makaburi si haram wala shirki, na kwamba wale ambao wanaharamisha jambo hilo hawana dalili yoyote katika sheria wawezayo kuitegemeza kwayo kauli yao.Na kwa hakika mimi nitakushukuru daima juu ya hili.

JAAFAR: Nami ninakushukuru kwa kukubali kwako ukweli na haki baada ya kuifahamu, na kuufuata kwako uongofu pale ulipo uona, kwani wewe ni mwenye kufuata muongozo wa akili na mantiki sahihi, kwa hivyo basi ninapenda kukuzidishia maarifa zaidi kuhusiana na haki na ukweli, na kukupatia maarifa mbali mbali katika dini, je unawakati zaidi ili niweze kuzungumza na wewe?

FUAD: Kwa hakika mimi ninapenda sana maneno ya kweli, zungumza ulitakalo, hakika mimi niko tayari kukusikiliza na kuyajaza masikio yangu kwa maarifa.

JAAFAR: Kutokana na mazungumzo yetu yaliyo pita imethibiti kuwa kujenga juu ya makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu ni jambo linalo faa na inajuzu kufanya hivyo, na jambo hilo si haram.

FUAD: Ndio.. nami niko pamoja nawe katika hilo.

JAAFAR : Hivi sasa nataka kusema hivi: Hakika kujenga juu ya makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuweka madharihi juu yake na kujenga makuba.. yote hayo ni sunna, hupewa thawabu mwenye kuyafanya hayo yote, si tu kwamba inajuzu.

FUAD : Vipi inakuwa sunna?

JAAFAR : Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:( Na anayeziheshimu alama za Mwenyeezi Mungu basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo). Kwa hivyo kila kitu ambacho huzing atiwa na kuhesabiwa kuwa ni katika shiari za Mwenyezi Mungu kukitukuza ni sunna katika Uislaam.

FUAD: Ndio..lakini vipi itakuwa kujenga juu ya makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu ni katika shiari za Mwenyezi Mungu?

JAAFAR: Shiari ni vitu ambavyo huitukuza dini katika mtizamo wa ulimwengu bila kuwepo dalili juu ya uharamu wake.

FUAD: Je dini hutukuzwa kwa majengo na makuba hayo?

JAAFAR : Ndio.

FUAD: Ki vipi?

JAFAAR: Kujengea makaburi ya maulamaa na viongozi watukufu wa kiislaam, na kujenga makuba juu yake, na kuyahifadhi yasiharibike na yasibomoke, ni kuwatukuza watukufu hao bila shaka yoyote. Kwa mfano: Akijitokeza mtu fulani na kupanda uwa waridi kwenye kaburi la mtu alie kufa, je mtu huyu haonekani kuwa amemtukuza maiti yule, na kuwa amemuenzi?

FUAD : Ni sahihi.

JAAFAR : Vipi ikiwa atajenga juu ya kaburi lake jengo kubwa na kuweka kuba juu yake, hakika kufanya hivyo ni kumtukuza na kumuenzi maiti huyo bila shaka yoyote. Na kuwatukuza viongozi na maulamaa wa kiislaam pia maimamu na mawalii.. ni kuutukuza Uislaam, na kuitukuza na kuienzi dini ambayo watu hawa walikuwa wakiilingania, na wakiwaelekeza watu kwenye dini hiyo. Je mtu fulani anapo mtukuza Raisi wa chama fulani, au walinganiaji wa itikadi za chama hichohuzingatiwa kuwa ni mwenye kukitukuza chama kile na itikadi ile au laa?

FUAD: Ndio ni kama usemavyo.

JAAFAR: Kwa hivyo basi kuyajengea makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu ni kuwatukuza wao na kumtukuza Mwenyezi Mungu, na ni kuuinua na kuutukuza Uislamm, na kila kitu ambacho kukifanya kutakuwa ni kumtukuza Mwenyezi Mungu na ndani yake kuna kuuinua Uislaam, kitu hicho ni katika shiari za Mwenyezi Mungu ambazo anahimiza kuzifanya, kwani anasema:Suratul- haji aya 32.

FUAD: Kwa hivyo..kuvunja na kubomoa maka buri ya mawalii na Mitume na maimam, inakuwa ni kuidhalilisha dini, na kuutia dosari utukufu wa kiislaam.. kwani kuyabomoa ni kuwadharau viongozi wetu, na ni kuwahini wao.. na kuwahini wao ni kuihini dini, na kuutia dosari utukufu wao ni kuutia dosari utukufu wa Uisalaam.

JAAFAR: Na mimi pia nimekuwa Shia, na nimefuata madhehebu ya Ahlil-bayti (a.s) na nimebadilisha jina kutoka jina la Waliid na kuwa Jaafarkwa sababu hii hii? Kwa hakika mimi wakati nilipo kuwa nikifuata rai za watu wengine sikuwa nikidha nia ya kuwa hakuna alie kwenye haki kinyume changu mimi, lakini nimeitafuta haki na kuifuata hadi kuifikia. Na mtu wakati wote anapo acha nyuma na kuzitupilia mbali asabia za madhehebu, na kukifungua kifua chake kwa ajili ya kuikubali haki, na kuitafuta haki.. hapana budi ataifikia haki hiyo na kuipata.

FUAD: Mimi, na baada ya msimamo na mawkifu haya, nitakuwa makini katika mambo mbali mbali, na nitakuwa ni mwenye kuitafuta haki, mpaka niweze kuifuata haki kokote nitako ikuta. Na kwa hakika nitakushukuru kwa muda wote.. Basi niruhusu nende zangu kwani nina ahadi na mtu fulani.

JAAFAR: Nenda, Mwenyezi Mungu akulinde.

FUAD : Fii amani llahi.

JAAFAR : Uwe katika amani ya Mwenyezi Mungu.

Abu haatam Ar-raziy katika kitabu chake (Az-ziinah) anasema: Kwa hakika jina la kwanza lililo dhihiri katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu ni Shia, na jina hili ndilo lililo kuwa jina mashuhuri (Laqab) la masahaba wane nao ni: Abu Dharri Salman Miqdaad na Ammar.

Na Shekh Mohammad Husein Kaashiful-Ghitaa katika kitabu chake kiitwacho (Aslush-shia wa Usuuliha) anasema: Hakika mbegu ya mwanzo ya Ushia iliwekwa na kupandikizwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) tangu zama za mwanzo kuanza kueneza Uislaam bila ya kutofautisha kati ya vitu viwili hivyo na vikiwa sawa.

Na ushahidi ni hadithi zake tukufu si kupitia njia za Mashia na upokezi wa wapokezi wa Kishia Imamiyyah pekee bali ni hadithi za maulamaa wa kisunni na wanazuoni wao na kupitia njia zao wanazo ziamini ambazo hazidhaniwi kuwa zina chembe ya uongo, na katika hadithi hizo ni hadithi iliyo pokelewa na Suyuut katika kitabu chake (Ad-durrul-manthuur fii tafsiri kitabillahi bil-ma'athur) katika kuitafsiri kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu:(Hao ndio viumbe bora) (suratul bayyinah aya 7). Ame sema: Ametoa hadithi Ibn Asakir kutoka kwa Jaabir bin Abdillahi amesema: Tulikuwa kwa Mtume(s.a.w.w) mara akatokea Ali na kuingia na Mtume(s.a.w.w) akasema: Nina apa kwa haki ya yule ambae nafsi yangu iko mikononi mwake hakika huyu na wafuasi (Mashia) wake ndio walio faulu na kufuzu siku ya kiama. Na hapo ikatelemka aya isemayo:(Hakika wale ambao waliamini na kufanya matendo mema hao ndio viumbe bora). (Suratul-bayyinah aya 7). Ibnu Hisham katika Siir atun-nabawiyyah anasema:Hakika umma wa kiarabu uligawanyika katika makundi mawili Masunni na Mashia tangu siku ya Sakifa.

Muhammad Abu Zuhra anasema katika kitabu chake kiitwacho Taarikhul-madhaahibil-islaamiyyah:(Ushia ni madhehebu ya kiislaam ya kisiasa ya tangu muda mrefu na Mashia walidhihiri na madhehbu yao hayo tangu mwishoni mwa zama za Uthuman na kukua na kupata nguvu katika zama za ukhalifa wa Ali, kwani kila alipo pata nafasi ya kuchanganyika na watu walizidi kupendezewa na kuvutiwa kutokana na kipawa chake na kutokana na nguvu ya Imani yake ya dini na elimu yake).

Ibnu Abil-hadiid anasema katika kitabu chake Sharhu Nahjul-balagha:(Hakika Mashia katika zama za dola na utawala wa Muawia walikuwa wakifadhilisha kuitwa Al-kitabiy na wasiitwe Shia. Kwani Ushia anwani yake na shiari yake ni kushikamana na Ahlul-bayti na kufuata elimu yao na kujiepusha na watu wa Bidaa (Uzushi) na kushikamana na kizazi kitwaharifu na kilicho pambika na tabia njema na bora kabisa) (Rejea kitabu Taarikhul-firaqil-islaamiyyah cha Shekh Muhammad Khaliil Az-zayni ukurasa wa 108-109).

Neno Sunnah: Lenye shadda, asili ya neno hilo ni njia, na neno hilo limepanuka maana yake katika makundi tofauti, na linapo tumika huwa lina maana ya aliyo yafanya Mtume (s.a.w) kama kauli vitendo au aliyo yakataza na kuyakemea, na hutumika katika maana hizo kupitia ndimi za wanazuoni na hadithi za Mtume(s.a.w.w) . Na katika zama za hivi karibuni neno Sunnah limekuwa likitumika katika mukabala wa neno Shia, na Husemwa: As-sunnatu wal-jamaah katika mukabala wa watu maalum, na katika ufahamu wa Shekh wa madhehebu ya Hanbali Ibnu Taimiyyah: Neno Sunnah: lina maana ya kumpenda Ali Uthmani na kumtanguliza Abubakar na Omar kwa wawili hao walio tangulia.

Na madhehebu yalipokithiri na makundi kuwa mengi, baadhi wakashikamana na rai isemayo kuwa tamko Sunni lilikuwa likitumika kwa mtu ambae anafuata dini kwa kuwapenda na kuwatawalisha mashekhe wawili, (Abubakar na Omar), na ilikuwa ikisemwa Sunaatul-umariyyh) Rejea kitabu Tariikhul-firaqil-islaamiyyah ukurasa 44-45).

6 UKWELI WA USHIA

KUPAMBWA KWA MAKABURI YA MAIMAM

KHALID : Salaamun alaykum.

BAAQIR : Wa alaykumus-salaam warahmatullahi wabarakatuhu.KHALID : Umefanya vizuri umekuja lini?

BAAQIR : Nimekuja kumtembelea mtoto wa ami yangu anaishi hapa.KHALID : Nakuomba leo hii ukaribie nyumbani kwetu.

BAAQIR : Kwa hakika ninakazi nyingi nilizo ziacha kwa ajili ya kuwatembelea ndugu (kuunga udugu) na kuomba unisamehe sana kwa wito huo.

KHALID : Haiwezekani..marafiki wawili baada ya kutengana kwa muda wa miaka kumi wanakutana kisha wasibakie na kufuatana walau kwa muda wa saa moja. Hakika mimi -pia nina haki ya udugu wa kiislaam. Kisha kulitokea mazungumzo kati yangu na ndugu yangu mmoja muumini kuhusiana na maudhui ya Shia na Sunna na kutokana na kuwa mimi ninamatumaini na imani na wewe ninataka na ninakusudia kufanya mazungumzo na wewe kuhusu maudhui hayo ili niweze kuelewa ukweli na uhaki katika maudhui hayo.

BAAQIR : Hakuna shaka. Walifuatana pamoja hadi nyumbani kwa Khalid, na kufika nyumbani kwake, na kila mmoja akaketi pembezoni mwa mwenziwe. Na baada ya kuzungumza kuhusiana na mambo yanayo wahusu na yaliyo maalum kwa ajili yao wawili, Baaqir akamuwahi mwenzie kwa kumuuliza swali na kusema: Ni mazungumzo gani yaliyo fanyika kati yenu?

KHALID : Mazungumzo yalikuwa yakihusiana na kuyapamba makaburi ya Manabii, maimam, maulamaa, waumini na watu wema na mfano wa hao, kwa Dhahabu na Fedha na mapambo mengineyo.

BAAQIR : Ni tatizo gani lililopo kuhusiana na jambo hilo?

KHALID : Je kufanya hivyo si haram?

BAAQIR : Kwanini iwe haram?

KHALID : Je maiti anafaidika na mapambo hayo?

BAAQIR : Hapana, hafaidiki nayo.

KHALID : Kwa hivyo, hayo yote ni Israfu na matumizi mabaya, na Mwenyezi Mungu anasemaWala usitawanye (mali yako) kwa ubadhirifu. Hakika watumiao kwa ubadhirifu ni ndugu za mashetani. suratul- israai aya 26-27.

BAAQIR : Unasemaje kuhusiana na nguo ifunikwayo juu ya Kaaba na mapambo yake, na Dhahabu Fedha na vitu ambavyo vipo juu ya Kaaba na ndani ya Kaabah?

KHALID: Sijui.

BAAQIR : Ndio, Kaaba ina nguo ambayo hufunikwa juu yake, na kuna Dhahabu nyingi, ambayo watu huitoa zawadi kwa ajili ya Kaaba kutoka sehemu tofauti za Dunia tangu zama za ujahilia hadi katika zama zetu hizi. Ibnu Khaladuni[14] anasema katika utangulizi wa kitabu chake:

[15] Kwa hakika tangu zama za Ujahilia kaumu mbali mbali walikuwa wakiitukuza Kaaba, na wafalme walikuwa wakituma mali na vitu vya thamani kwenye nyumba hiyo kama vile Kisraa na wengineo, Na kisa cha mapanga na nguo zilizo fumwa kwa dhahabu, vitu ambavyo Abdulmutwalib alivikuta chini alipo chimba kisima cha Zamzam ni maarufu sana).

Na Mtume(s.a.w.w) alipo ikomboa Makka alikuta katika kisima kirefu kukiwa na Awqiyah sabini elfu za Dhahabu vitu ambavyo wafalme walikuwa wakizitoa zawadi kwa ajili ya nyumba ya Allah. Na kulikuwa na dinari milioni moja, yaani zenye uzito wa Kintwari milioni mbili. Na Ali(a.s) alisema kumwambia Mtume: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unaonaje ukitumia mali hii ikakusaidia katika vita vyako? Mtume hakufanya hivyo. Kisha akamwambia Abubakar nae hakuzitoa. (hadi akasema)

(Amesema Abu waail): Niliketi kwa Shaibah bin Othuman nae akasema Aliketi kwa Omar bin Khattab, akasema: Niliazimia nisibakishe katika nyumba hiyo chembe yoyote ya Dhahabu wala Fedha isipokuwa nitaigawa kati ya Waislaam. Nikasema Hutafanya hivyo?

Akasema: Kwanini nisifanye hivyo?

Nikasema: Sahiba wako hakufanya hivyo.

Akasema: Hao wawili ndio ambao hufuatwa nyendo zao.[16]

Je Kaabah ilikuwa ikifaidika na Dhahabu na Fedha hizo ewe Khalid?

Au -Mwenyezi Mungu -ametakasika na hili- alikuwa akifaidika na vitu hivyo viwili?

KHALID : Hapana.

BAAQIR : Pamoja na hayo Mtume(s.a.w.w) hakuunyoosha mkono wake kwenye mali hiyo iliyo kuwa imelimbikizana, wala hakutumia hata chembe moja ya mali hiyo, pamoja na kuwa wakati ule Uislaam ulikuwa ukihitajia sana mali na pesa nyingi wakati ambapo hazina ilikuwa imejaa, kwa ajili ya kuimarisha nguzo zake katika miji na nchi mbali mbali. Kwa nini hakufanya hivyo? Ni kwa sababu mali hiyo nyingi ilikuwa ni mali ya Kaabah na huiongezea Kaabah utukufu na heba yake machoni mwa watu, japokuwa utukufu na daraja yake ya kweli iko kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, utukufu ambao haupungui wala kuongezeka, sawa iwe na mali zote za dunia, au isiwe na chochote.

Na maneno ni hayo hayo kuhusiana na makuba ya Dhahabu, na milango ya Dhahabu na Fedha, na nguo ifunikwayo juu yake na mapambo yatolewayo zawadi na kupambwa nayo makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu mtukufu kama vile: Amirul-muuminiin, Imam hasan na Imam Husein, Imam Ridhaa na wengineo juu yao rehma na amani. Watu hawa cheo na daraja yao ya kweli waliyo pewa na Mwenyezi Mungu haipungui wala kuzidi kwa kuwepo madini hayo ya thamani kwenye makaburi yao, na wala haipungui ikiwa hayakuwepo, kwa mfano Imam Hasan bin Ali(a.s) ni bora kuliko nduguye Husein(a.s) japokuwa kaburi la Imam Hasan(a.s) hupigwa na jua katika jangwa la Bakii'i likiwa halikujengewa juu yake au juu yake kukiwa hakuna jengo lolote, na likiwa halikupambwa na pambo la aina yoyote, na kaburi la Imam Husein(a.s) lilikuwa na majengo makubwa makubwa ya dhahabu halisi iangazayo angani na kuyaondoa mawingu.

Lakini tumeyafanya hayo kwa ajili yao, na kutoa zawadi ya mapambo ya Dhahabu kwenye makaburi yao, na makuba ya makaburi yao kuyatia dhahabu na mengineyo, yote hayo kwa ajili ya kuwaenzi na kuwatukuza wao.

KHALID : Je vitu hivi vinawapatia hawa utukufu katika macho ya watu?BAAQIR : Ndio. Na hivi sasa nitakufanya ukiri jambo hilo. Kwa mfano ukienda kwa Mayahudi na kuyaona makaburi ya maulamaa wao yakiwa yameharibika, yakipigwa na jua, hakuna kizuizi chochote juu yake au chumba ambacho mwenye kuyatembelea anaweza kujikinga jua kwenye kivuli chake. Kisha ukenda kwa Wakiristo, na ukakuta makaburi ya maulamaa wao yakiwa yamejengewa vizuri na kuhifadhika, yakiwa yamejengewa makuba na yakiwa yamepambwa kwa dhahabu na fedha, na mapambo mengine ya madini mbali mbali. Je ni maulamaa gani utakao waona kuwa ni wenye utukufu, ni maulamaa wa Mayahudi au Wakiristo, pamoja na kuwa unafahamu ya kuwa wewe ni Muislaam na unafahamu ya kuwa wote wawili wako kwenye batili?

KHALID : Bila shaka kutokana na mandhari ya makaburi ya pande mbili niliyo yaona nitachukua picha fulani ya utukufu wa maulamaa wa Wakiristo, na picha ya udhalili wa maulamaa wa Mayahudi.

BAAQIR : Kwa hivyo basi wayafanyayo Mashia na Masunni kwa kujenga madharihi juu ya makaburi, na kujenga haram na makuba na mengineyo juu ya makaburi ya maimamu na Mitume.. ni kwa ajili ya kuwatukuza wao na kuwaenzi, kwa sababu hiyo huyapamba kwa Dhahabu Fedha na mapambo mengine ya madini mbali mbali.

KHALID : Yote hayo ni sahihi lakini je jambo hilo linakitoa kitendo hicho kwenye sifa ya israfu na matumizi mabaya na yasiyo ya lazima?.BAAQIR : Ndio, na zaidi ya hapo. Ikiwa itathibiti kuwa matendo haya ni kuwatukuza mawalii wa Mwenyezi Mungu, wakati huohuo ni kuutukuza Uislaam, kwani kuwatukuza viongozi na watukufu wa Uislaam ni kuutukuza Uislaam, na kila kitu ambacho ndani yake kuna kuutukuza Uislaam basi kitu hicho ni katika shiari za Mwenyezi Mungu ambazo Mwenyezi Mungu amesema kuhusiana nazo:Kwa hivyo basi kuyapamba makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu ni katika shiari za Mwenyezi Mungu ambazo ni sunna kuzifanya na kufanya kazi kwa ajili yake, na mtu mwenye kufanya hivyo hupewa thawabu kwa matendo yake hayo. KHALID : Nakuomba samah ani, kwa kuchukua kiasi hiki cha wakati wako lakini mbele ya Mwenyezi Mungu ni mwenye malipo, kwani umenitoa kwenye kiza cha ujinga na kuniweka kwenye nuru ya elimu na ufahamu, ni kwa kiasi gani nilikuwa nikifikiria kuhusiana na upambaji huu wa makaburi na nisielewe siri yake na faida yake na usahihi wake, kwa hakika hivi leo-wewe- umenitia nuru kwa elimu yako hii, na umenifikisha niliko kuwa nikipakusudia.

BAAQIR : Sasa shaka yote uliyo kuwa nayo kuhusiana na kupamba makaburi imetoweka?

KHALID : Ndio.. hakuna shaka yoyote niliyo bakia nayo kwani kufanya hivyo ni sunna na jambo lililo himizwa na Qur'ani tukufu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu:

BAAQIR : Alaa ayyi hal (Kwa hali yoyote ele):Hakika mimi niko tayari kufahamiana nawe katika maudhui kama haya ili niweze kufaidika, au wewe pia ufaidike, na wote kwa pamoja tuwe ni wenye kuyafahamu mambo kwa ufahamu mzuri na wenye mazingatio.

KHALID : Ninakushukuru sana sana, na ninamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akuwafikishe kwa yale ayaridhiayo.

7 UKWELI WA USHIA

KUBUSU MADHARIHI (MAKABURI)

MAALIK: Ewe Swaadiq ni sababu gani iwafanyayo kubusu Dharihi ya kaburi la Mtume na maimam na kutoacha kitendo hicho?

SWAADIQ: Je kuna tatizo (ishkali) lolote kufanya hivyo?

MAALIK: Inasemekana kuwa kufanya hivyo ni miongoni mwa matendo ya shirki.

SWADIQ: Nani asemae kuwa kufanya hivyo ni shirki?

MAALIK: Waislaam ndio wasemao hivyo.

SWADIQ: Ajabu! Basi ni watu gani ambao wanabusu madharihi?MAALIK: Inasemekana kuwa ni kikundi kidogo cha Mashia.

SWADIQ: Je umewahi kwenda hija?

MAALIK: Ninamshukuru Mwenyezi Mungu.. ndio nimefanikiwa kwenda hija.

SWADIQ: Je umelitembelea kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) katika mji wa Madinah?

MAALIK: Ninamshukuru Mwenyezi Mungu nimefanikiwa kulitembelea.SWAADIQ: Je hukuwaona maelfu ya waislaam wa madhehebu ya sunni wakikusudia na kutaka kulibusu dharihi la kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu na huku wakipigwa na walinzi wa kikundi cha (Hay'atu amri bil-maarufi)?!!

MAALIK: Ndio..

SWAADIQ: Kwa maana hiyo si sisi Mashia pekee tunao busu madharihi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, bali waislaam wote huyabusu.

MAALIK: Sasa kwanini baadhi wanasema kuwa kufanya hivyo ni haram, na kwamba kufanya hivyo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu mtukufu?

SWAADIQ: Hawa ni watu wachache wa kikundi fulani kati ya makundi ya waislaam, wajionao kuwa wao ndio wenye haki, na kwamba wao ndio waislam wa kweli na wanawaona waislaam wengine kuwa ni makafiri na washirikina wanamuabudu asie kuwa Mwenyezi Mungu, na hawawaoni watu wengine kuwa ni waislaam walio kosea, kwa hivyo ndio maana huwaona wakiyakufurisha madhehebu (makundi) mengine yote ya kiislaam. Je hukuona ile kamati ya (Al-amri bil-maarufi)!! katika nchi ya Hijazi wakimpiga anaekusudia na kutaka kubusu dharihi la kaburi la Mtume(s.a.w.w) na kumwambia:Ewe kafiri! Ewe mshirikina! Ewe zindiki! Ewe nguruwe! Ewe mbwa! Na mengineyo kati ya aina mbali mbali za matusi na tuhuma zilizo mbaya kabisa.

Na matusi hayo humuelekea kila mtu: Sawa awe Shia, Hanafiy, Maalikiy, Shafiiy, Hanbaliy, Zaydiah, na waislaam wengine..[17]

MAALIK: Ndio.. yote hayo nimeyaona, na yaliyo mabaya zaidi kuliko hayo: Kwa hakika mimi niliwaona wakimpiga kichwani mtu mmoja alie ng'ang'ania kufanya hivyo kwa fimbo kiasi kwamba huenda pigo hilo lilipelekea kumpasua na kutoka damu, na wakati mwingine huwapiga kwa mikono yao-kwa nguvu- na wakiwapiga vifuani waislaam walio kuja kufanya ziara mapigo ambayo huwaumiza na kuwadhuru vifua vyao na kuwasababishia maumuvu na maradhi miili yao! Na ni kwa kiwango gani niliumia kwa kuyao mambo hayo na vitendo hivyo!!.

Hija ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni kongamano la waislaam wote ulimwenguni ili waweze kuzungumza katika kongamano hilo kuhusu mambo yao mbali mbali, hivi leo imekuwa ni mahala pa kutia tofauti kati ya waislaam kutokana na matendo ya kikundi hicho kidogo kinacho jiita kuwa ni (hay'atul-amri bil-maaruf wannahyi anil-munkar)!!!.SWAADIQ: Ala ayyi hal, ewe Maalik.. je wewe unambusu mwanao?MAALIK: Ndio!

SWADIQ: Je unamshirikisha Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kumbusu mwanao?

MAALIK: Hapana, hapana.. kamwe simshirikishi Mwenyezi Mungu.SWADIQ: Vipi usimshirikishe Mwenyezi Mungu kwa kumbusu mwanao?MAALIK: Kwa hakika mimi ninambusu mwanangu kwa ajili ya mapenzi yangu kwake, na hilo si shirki.

SWADIQ: Je wewe unaibusu Qur'ani?

MAALIK: Ndio.

SWADIQ: Je kwa kufanya kwako hivyo humshirikishi Mwenyezi Mungu?

MAALIK: Hapana.

SWADIQ: Je jalada la Qur'ani unalo libusu si ngozi ya mnyama?MAALIK: Ndio.

SWADIQ: Kwa hivyo wewe unamshirikisha Mwenyezi Mungu, na unaifanya ngozi ya mnyama kuwa ni mshirika wa Mwenyezi Mungu.. ametakasika Mwenyezi Mungu na hilo.

MAALIK: Si hivyo. Kwa hakika mimi ninaibusu Qur'ani kwa sababu imekusanya maneno ya Mwenyezi Mungu, kutokana na mapenzi ya maneno ya Mwenyezi Mungu ndio maana ninalibusu jalada lililo ifunika Qur'ani hiyo, na hii ni kutokana na mapenzi mengi, na wingi wa shauku yangu kwa Qur'ani, ni tofauti iliyoje kati ya kitendo hiki na kumshirikisha Mwenyezi Mungu?

Kisha ninapo ibusu Qur'ani ninapata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya hivyo, kwa sababu kuibusu Qur'ani ni kuitukuza na kuienzi na kuiinua daraja yake, na kuitukuza Qur'ani kuna thawabu na malipo mbele ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo ni tofauti iliyoje iliyopo kati ya tendo hili na kumshirikisha Mwenyezi Mungu?

SWADIQ: Kwa nini maneno kama hayo usiyasema katika kubusu dharihi la Mtume(s.a.w.w) na madharihi ya maimam(a.s) [18] au unadai ya kuwa wale ambao wanabusu madharihi huvifanya vyuma hivyo kuwa ni washiriki wa Mwenyezi Mungu mtukufu?! Ikiwa ni hivyo kwanini hawabusu vyuma mbali mbali vilivyoko huku na kule katika ardhi? Lakini..kutokana na ukweli kuwa dharihi hilo limefunika kaburi la Mtume(s.a.w.w) au kaburi la mmoja wapo kati ya maimamu(a.s) , kutokana na mapenzi ya Mtume(s.a.w.w) na maimamu na kutokana na shauku yao kwao ndio maana wanalibusu dharihi la kaburi lake kwa sababu wao hawawezi kumfikia Mtume na imamu mwenyewe(a.s).

Pamoja na kufanya kwao hivyo hakika wao hupata malipo kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, na hupawa thawabu kwa kufanya hivyo, kwani kulibusu dharihi la mtu fulani ni kumtukuza mtu yule. Na kumtukuza Mtume(s.a.w.w) au mmoja wapo kati ya maimamu(a.s) , ni kuutukuza Uislaam ambao huyu alikuwa ni Mtume wake(s.a.w.w) au alikuwa ni imamu wake alie kuwa akilingania watu kwenye Uislaam huo.

Na jambo lolote litakapo kuwa na sura ya kuutukuza Uislaam basi jambo hilo ni katika shiari za Mwenyezi Mungu ambazo amezizungumzia kwa kusema:suratul-haji aya 32.

MAALIK: Ikiwa ukweli ni huo basi kwanini baadhi ya watu wanasema kuwa nyinyi ni wenye kumshirikisha Mwenye zi Mungu?

SWAADIQ: Imepokelewa katika Hadithi tukufu kama ifuatavyo:(Kwa hakika matendo hufanyika kutokana na Nia) [19] ikiwa mtu yeyote anabusu dharihi na katika kubusu kwake huko anakusudia kumshirikisha Mwenyezi Mungu bila shaka mtu huyo ni mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu (mshirikina). Na ikiwa kubusu huku kunatokana na mapenzi mengi, na kwa ajili ya kupata thawabu kwa ajili ya kuadhimisha na kutukuza shiari za Mwenyezi Mungu kwa kufanya hivyo, basi hupewa thawabu yule mwenye kuyatekeleza matendo hayo. Na wewe waulize wote wale ambao wanayabusu madharihi kati ya Mashia na Masunni kama ifuatavyo: Kwa nini mnabusu madharihi?

Hata kujibu yeyote kati yao isipokuwa kwa kusema tunafanya hivyo kutokana na mapenzi makubwa na shauku kubwa tuliyo nayo na kwa ajili ya kupata thawabu, na huwezi kumsikia yeyote kamwe-bila shaka yoyote- akisema ya kuwa anabusu dharihi kwa ajili ya jambo lingine tofauti na hili tulilo litaja.

MAALIK: Ni kweli, maneno yako ni sahihi.

SWADIQ: Na ikiwa kubusu peke yake bila kukusudia kumshirikisha Mwenyezi Mungu kunamfanya mtu kuwa mshirikina, bila shaka huwezi kumpata mwanadamu yeyote asie mshirikina, kwani waislaam imma wanabusu madharihi, au wanabusu Qur'ani.. kwa msingi wa hali mbili hizi wao-wote-ni washirikina. Sasa ikiwa hali ni kama hiyo Muislaam ni nani?

MAALIK: Ninakushukuru sana, na kwa hakika mimi nitafanya mazungumzo na majadiliano na baba yangu alie kuwa akinilisha na kunifundisha mambo kama haya ya asabia yasiyo na maana yoyote, na sinto sikiliza maneno ya mtu yeyote wa madhehebu mengine, kwa hakika nimefahamu ya kuwa haki na ukweli uko pamoja nanyi-nyinyi Mashia- na wewe unahaki juu yangu milele, kwa sababu umenionyesha njia, si katika jambo hili tu bali katika mambo yote, ili nisifuate kila kinifikiacho masikioni mwangu, bila ya kufikiria kuhusu usahihi wake na ubatilifu wake.

5

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI NA MOJA

Sura Ya Thelathini na Nne: Surat Saba. Imeshuka Makka. Ina Aya 54.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي الْآخِرَةِ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١﴾

1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na sifa ni zake katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari.

يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ الرَّحِيمُ الْغَفُورُ ﴿٢﴾

2. Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni na yanayopanda huko na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwingi wa maghufira.

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَأْتِينَا السَّاعَةُ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأْتِيَنَّكُمْ عَالِمِ الْغَيْبِ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٣﴾

3. Na walisema wale ambao wamekufuru: Haitatufikia Saa. Sema: Ndio! Naapa kwa Mola wangu, itawafikia. Mjuzi wa ghaibu. Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo katika hivyo wala kikubwa zaidi; ila vimo katika Kitabu chenye kubainisha.

لِّيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٤﴾

4. Ili awalipe wale ambao wameamini na wakatenda mema. Hao watapata maghufira na riziki yenye heshima.

وَالَّذِينَ سَعَوْا فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن رِّجْزٍ أَلِيمٌ ﴿٥﴾

5. Na wale ambao wamehangaika kuzipinga ishara zetu wakiona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu.

وَيَرَى الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ الَّذِي أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ هُوَ الْحَقَّ وَيَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿٦﴾

6. Na wale ambao wamepewa ilimu wanaona kuwa uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako ni haki na huongoza kwenye njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.

SIFA NJEMA ZOTE NI ZA MWENYEZI MUNGU

Aya 1 – 6

MAANA

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na sifa ni zake katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye kustahiki kusifiwa kwa sifa njema katika nyumba mbili. Ni mmliki wa ulimwengu na mpangiliaji wake kwa vyote vilivyomo ndani yake, kulingana na elimu yake na hekima yake.

Kwenye Nahjul-Balagha, imesemwa: “Tunamsifu kwa ukubwa wa hisani yake na wema wa dalili yake na ziada ya fahila zake na neema zake. Sifa ambazo ni haki yake (sisi) kuzitekeleza na kulipa shukrani zake na kujikurubisha kwenye thawabu zake na kutaka ziada ya wema wake.”

Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo na yanayoteremka kutoka mbinguni na yanayopanda huko na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwingi wa maghufira.

Maana ya Aya hii yamekaririka katika Aya kadhaa; ikiwemo Juz. 7 (6:59) na Juz. Juz. 11 (10:61). Ufupisho wake ni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

Na walisema wale ambao wamekufuru: Haitatufikia saa ya Kiyama. Sema: Ndio! Naapa kwa Mola wangu, itawafikia.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 11(10:53).

Mjuzi wa ghaibu. Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo katika hivyo wala kikubwa zaidi; ila vimo katika Kitabu chenye kubainisha.

Kitabu chenye kubainisha ni kinaya cha kuhifadhi. Maana ni kuwa hakuna anayejua wakati wa Kiyama isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. Tazama Juz. 9 (7:187).

Ili awalipe wale ambao wameamini na wakatenda mema. Hao watapata maghufira na riziki yenye heshima. Na wale ambao wamehangaika kuzipinga ishara zetu wakiona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu.

Huu ni ubainifu wa hekima ya ufufuo, ambayo ni kulipwa mema waliofanya wema na wale waliofanya uovu walipwe kwa uovu wao. Tazama Juz. 11 (10:3-4). Kifungu cha “Hisabu na malipo ni lazima.”

Na wale ambao wamepewa ilimu wanaona kuwa uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako ni haki na huongoza kwenye njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.

Makusudio ya wale waliopewa ilimu ni kila mwenye ilimu aliye na insafu, wakati wowote na mahali potepote. Na makusudio ya uliyoteremshiwa ni Qur’an. Maana ni kuwa yeyote mwenye ilimu atakayeisoma Qur’an kiusahihi, lazima ataishia kuwa ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu; kwa sababu iko sawasawa kwenye itikadi yake, sharia yake na mafunzo yake yote.

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا هَلْ نَدُلُّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ يُنَبِّئُكُمْ إِذَا مُزِّقْتُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّكُمْ لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ ﴿٧﴾

7. Na wale ambao wamekufuru walisema: Je, tuwajulishe mtu anayewaambia mtakapocham- buliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya?

أَفْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَم بِهِ جِنَّةٌ بَلِ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ فِي الْعَذَابِ وَالضَّلَالِ الْبَعِيدِ ﴿٨﴾

8. Amemzulia Mwenyezi Mungu au ana wazimu? Bali wale ambao hawaamini akhera wamo adhabuni na upotofu wa mbali.

أَفَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِن نَّشَأْ نَخْسِفْ بِهِمُ الْأَرْضَ أَوْ نُسْقِطْ عَلَيْهِمْ كِسَفًا مِّنَ السَّمَاءِ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ ﴿٩﴾

9. Je, hawaoni yaliyo mbele yao na nyuma yao ya mbingu na ardhi. Tungelipenda tungeliwadidimiza ardhini, au tungeliwateremshia vipande vya mbingu. Hakika katika hayo kuna ishara kwa kila mja aliyetubia.

WANAOPINGA SIKU YA MWISHO

Aya 7 – 9

MAANA

Na wale ambao wamekufuru walisema: Je, tuwajulishe mtu anayewaambia mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya? Amemzulia Mwenyezi Mungu au ana wazimu?

Hivi ndivyo washirikina walivyomwambia Muhammad, ni muongo au mwendawazimu – Mungu apishie mbali. Kwa nini walisema neno la ukafiri kama hilo? Ni Kwa sababu Mtume aliwaambia kuwa mtu atafu- fuliwa baada ya mauti. Hawana dalili yoyote ya kupinga kwao huku isipokuwa kushangaa tu; kama walivyosema:

أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ ﴿٥﴾

“Amewafanya miungu wote kuwa ni mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.” (38: 5).

Hali yao hii, kama inavyonekana, inategemea vile wanavyofikiria. Maana yake ni kupinga hali halisi kwa fikra na mawazo; pamoja na kuwa fikra haiwi ya kweli ila ikiwa inaakisi hali halisi na kwamba yeyote anayeikum- batia nadharia yoyote hana budi kutafuta dalili ya ukweli wake kwa kuweko uhalisi unaoitafsiri, na haifai kukana uhalisi kwa fikra isiyokuwa na msingi wowote.

Katika hili Imam Ali(a.s) anaashiria kwa kusema:“Watu wanajulikana kwa haki, wala haki haijulikani kwa watu.”

Bali wale ambao hawaamini akhera wamo adhabuni na upotofu wa mbali.

Hao ni wajinga na wapotevu, kwa sababu wameipima haki na uhalisi kwa fikra zao na mawazo yao; na walitakiwa wapime fikra zao kwa haki na uhalisi.

Je, hawaoni yaliyo mbele yao na nyuma yao ya mbingu na ardhi.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawaambia wakadhibishaji: Kuna ajabu gani ya kufufuliwa kwenu baada ya mauti:

أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ﴿٨١﴾

“Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao?” (36:81).

Je, umbile hili halifahamishi umoja wake na ukamilifu wa uweza wake; ukiwemo kuwarudisha watu baada ya mauti?

Tumelizungumzia hilo mara nyingi. Tazama Juz. 1 (2:28 -29), Juz. 5 (4:85 – 87) na Juz. 11 (10:3–4).

Tungelipenda tungeliwadidimiza ardhini, au tungeliwateremshia vipande vya mbingu. Hakika katika hayo kuna ishara kwa kila mja aliyetubia.

Hayo ni ishara ya kuumba mbingu na ardhi. Kwa sabubu hilo, kwa mwenye akili, linafahamisha ukuu wa Mwenyezi Mungu na uweza wake wa kuipa uhai mifupa iliyochakafuka. Ama kauli yake Mwenyezi Mungu:

‘Tungelipenda tungeliwadidimiza ardhini,’ ni karipio na makemeo kwa yule anayepinga siku ya mwisho, kwamba anaweza kumezwa na ardhi au kupigwa na kimondo kutoka mbinguni, kimuunguze.

وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ مِنَّا فَضْلًا يَا جِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُ وَالطَّيْرَ وَأَلَنَّا لَهُ الْحَدِيدَ ﴿١٠﴾

10. Na kwa hakika tulimpa Daud fadhila kutoka kwetu. Enyi milima sabihini pamoja naye na ndege. Na tukamlainishia chuma.

أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١﴾

11. Kwamba utengeneze nguo za chuma pana na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika ninayaona mnayotenda.

وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهْرٌ وَرَوَاحُهَا شَهْرٌ وَأَسَلْنَا لَهُ عَيْنَ الْقِطْرِ وَمِنَ الْجِنِّ مَن يَعْمَلُ بَيْنَ يَدَيْهِ بِإِذْنِ رَبِّهِ وَمَن يَزِغْ مِنْهُمْ عَنْ أَمْرِنَا نُذِقْهُ مِنْ عَذَابِ السَّعِيرِ ﴿١٢﴾

12. Na kwa Suleiman upepo. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamtiririshia chemchem ya shaba. Na katika majini kuna waliofanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake. Na anayejitenga na amri katika wao tunamwonjesha adhabu ya moto unaowaka.

يَعْمَلُونَ لَهُ مَا يَشَاءُ مِن مَّحَارِيبَ وَتَمَاثِيلَ وَجِفَانٍ كَالْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَّاسِيَاتٍ اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ ﴿١٣﴾

13. Wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu na masanamu na sinia kubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiyoondoka mahali pake. Fanyeni amali enyi watu wa Daud kwa kushukuru. Ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.

فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ الْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَىٰ مَوْتِهِ إِلَّا دَابَّةُ الْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنسَأَتَهُ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ الْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ الْغَيْبَ مَا لَبِثُوا فِي الْعَذَابِ الْمُهِينِ ﴿١٤﴾

14. Tulipomkidhia mauti, hapana aliyewajulisha mauti yake ila mnyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Alipoanguka majini walitambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu ya kufedhehesha.

DAUD NA SULEIMAN

Aya 10 – 14

MAANA

Na kwa hakika tulimpa Daud fadhila kutoka kwetu. Enyi milima sabihini pamoja naye na ndege. Na tukamlainishia chuma.

Katika Juz. 6 (4:163) Mwenyezi Mungu anasema: “Na Daud tukamapa Zaburi,” kwenye Juz. 19 (27:15) anasema: “Na hakika tulimpa Daud na Suleiman elimu” na kwenye Aya hii tuliyo nayo anaseama kuwa amempa neema ya sauti nzuri ambayo ilikuwa inakurubia kwenda sambamba na sauti ya milima na ndege.

Katika Juz. 17 (21:79) tulisema kuwa inawezekana kuwa tasbihi ya milima na ndege ni tasbihi halisi hasa pamoja na Daud, Kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. Kuna msemaji aliyesema kuwa makusudio ya kusabihi milima na ndege pamoja na Suleimani ni kuwa ilikuwa ikimfanya asabihi; alipokuwa akiiona husema: “Subhana man khalaqa wa swawwara...” (Kutakasika ni kwa aliyeumba na akatia sura...).

Pia Mwenyezi Mungu alimneeemesha Daud kwa kukifanya chuma vile anavyotaka yeye bila ya kukitia motoni au kukigonga na nyundo. Inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu alimfahamisha sababu na nyenzo za kukilainisha chuma.

Kwamba utengeneze nguo za chuma pana na kadiria sawa katika kuunganisha.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Daud atengeneze deraya kutokana na chuma na atengeneze vizuri kuzuia panga mishale na mikuki na ziwe pana kwa namna ambayo mvaaji haitamzuia na harakati zozote.

Na tendeni mema. Hakika ninayaona mnayotenda.

Maneno yanaelekezwa kwa Daud na kizazi chake. Mwenyezi Mungu anawaamrisha wafanye mema na kuwa ameayaandalia malipo na thawabu. Umetangulia mfano wa Aya mbili hizi katika Juz. 17 (21:79 – 80).

Na kwa Suleiman upepo. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja.

Dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa upepo ulikuwa ukimchukua Suleiman, anakotaka, kwa amri ya Mungu na kwamba masafa ya mwezi mzima kwa ngamia au kutembea kwa miguu alikuwa akienda kwa asubuhi moja na vile vile jioni.

Na tukamtiririshia chemchemi ya shaba.

Makusudio ya kumtiririshia hapa ni kumyeyushia. Yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu alimyeyushia chuma Suleimani kama alivyomyeyushia baba yake Daud. Inawezekana kuwa Mwenyezi Mungu alimuongoza kwenye sababu za kuyeyusha.

Na katika majini kuna waliofanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake. Na anayejitenga na amri katika wao tunamwonjesha adhabu ya moto unaowaka. Wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu na masanamu na sinia kubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiyoondoka mahali pake.

Imetangulia pamoja na tafsiri yake katika Juz. 17 (21:82).

Fanyeni amali enyi watu wa Daud kwa kushukuru. Ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.

Ibn Al-arabi ameitaja Aya hii katika Futuhat Juz. 4, akasema: Shukrani ni kuiona neema kuwa imetoka kwa Mungu si kwa mwingine. Mwenyezi Mungu (s.w.t) alimpa wahyi Musa akamwambia: Nishukuru kwa haki ya kushukuru. Akasema Musa: “Ni nani anayeweza hilo ewe Mola?” Akamwambia: “Ikiwa unaona neema imetokana na mimi basi umenishukuru.”

Tulipomkidhia mauti, hapana aliyewajulisha mauti yake ila mnyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Alipoanguka majini walitambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu ya kufedhehesha.

Aliyekidhiwa na mauti ni Suleiman. Mnyama wa ardhi ni mchwa anayekula miti. Maana ni kuwa Suleimani alifikiwa na mauti akiwa ameegemea fimbo yake; akabakia hivyo mpaka muda aliotaka Mwenyezi Mungu, majini na watu wakimwangalia na kumdhania kuwa yuko hai, mpaka pale mchwa walipokula fimbo yake kwa ndani, ikavunjika na Suleiman akaanguka; hapo wote wakajua kuwa amekufa; ikadhihirika kwa watu kuwa majini hawajui ghaibu. Kwa sababu lau wangelijua basi wasingelikuwa katika utumishi wa Suleiman akiwa ni maiti.

Ikiwa baadhi ya yaliyo katika Aya hii yanaonekana, kwa kawaida, ni vigumu kutokea, lakini kiakili inakubalika kutokea. Ndio maana tunayasadiki na kuyakubali; tukiwa tunaamini msingi wa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Mtume(s.a.w. w ) wake mtukufu.

Tazama Juz. 3 (3:45 – 51) kifungu cha “Lisilowezekana kiakili na kidesturi.”

KUPINGA FIKRA YA KIDINI

Kutoka na kutajwa majini na mambo yasiyo ya kawaida katika Aya hii, ni vizuri tutaje yaliyoelezwa kwenye kitabu kilichotoka hivi karibuni, kina- choitwa Naqdu lfikri ddiniy. (Kupinga fikra ya kidini).

Hivi sasa tuko katika mwezi wa Novemba 1969. Yamezungumzwa mengi kuhusu kitabu hicho na mtungaji wake. Mwenye kusoma kitabu hicho mara moja atamhukumu mtungaji wake kuwa ana shaka na wasiwasi na dini zote. Hilo amelisema waziwazi kwenye Uk. 29, 77 na nyinginezo.

Lakini mwenye kukifuatilia kitabu na kuchukua dhahiri yake, ataona kuwa yaliyopelekea shaka na wasiwasi huu ni mambo yafutayo:

Kwanza : Kujaribu baadhi ya waumini kulazimisha kuoanisha nukuu za Qur’an na ugunduzi wa kisayansi, na kuzama sana kuleta taawili iliyo mbali na matamshi. Mtunzi wa kitabu hicho amelitolea ushahidi mwingi hilo, yakiwemo yale aliyoyanukuu katika Uk. 37, kwamba ugunduzi wa chembe za mwanga unafahamisha kuweko malaika na majini.

Mtungaji akielezea kauli hii alisema: “Sijui kuna uhusiano gani baina ya nadharia ya mwanga na kuweko majini.”

Pili : Mazoweya na nembo za kidini zilizoganda haziendani na maendeleo ya karne ya ishirini; kama anavyodai mwandishi.

Tatu: Baadhi ya wakuu wa dini kuunga mkono ukabaila na ukoloni kwa kutumia jina na Uislamu au Ukristo. Kitabu kimejaa ushahidi wa hilo; kama vile kwenye uk. 23: “Dini huko ulaya ilikuwa rafiki mkubwa wa serikali za kikabaila, hali ambayo inaendelea hadi sasa katika miji mbalimbali, hasa ndani ya miji ya kiarabu na nje, na vile dini inavyoungana moja kwa moja na ukoloni mambo leo unaongozwa na Marekani.”

Mtungaji aliongeza katika kupinga kitabu “Almasihiyya wal Islamu fi Lubnan” (Ukiristo na Uislmu Lebanon) ambacho ni mkusanyiko wa mihadhara ya Lebanon ya mwaka 1965, iliyotolewa na wakuu wa kidini wane: mmoja wa kisunni, mwengine wa kishia na wawili wa kikiristo.

Na wengine wane wa wasiokuwa na dini yoyote, lakini walizungungumza kwa niaba ya dini. Wote wakamwahidi Mwenyezi Mungu kuwa watafanya bidii ya kudumu kuondoa pingamizi zinazowekwa baina ya Uislamu na ukiristo.

Miongoni mwa aliyoyasema mtungaji huyu, katika kuwarudi wale waliotoa ahadi, ni yale yaliyo katika ukurasa wa 64, wa Kitabu chake hicho: “Lengo la kwanza la mihadhara na ahadi hizo ni wakristo kuunga mkono serkali ya Lebanon, kwa vile inawanufaisha wao zaidi kuliko waislamu walio na ufukara sana.

Baadhi ya waislamu nao wanaikubali serikali na kuungana na wakiristo, na kuaiachia serikali usimamizi wote wa kisiasa, kijamii na kiuchumi, si kwa lolote ila ni kwa kuwa wanapata manufaa fulani na faida kutoka serikalini. Kiasi ambacho maovu ya serikali yamesahaulika na kuelekea kwenye nembo ya mshikamano wa wakiristo na waislamu.”

Dalili mkataa kuwa malengo ni masilahi sio mshikamano wa kidini, mwandishi anaiweka wazi kwenye Uk. 60, katika kitabu chake, akisema: “Hakika Uislamu hauikubali Biblia, utatu, mhanga, kusulubiwa Bwana Masih, kuzikwa kwake na kutoka kwake kaburini n.k. Kama ambavyo wakiristo nao hawaikubali Qur’an wala utume wa Muhammad(s.a.w. w ) n.k. Sasa hawa wahadhiri na ahadi zao wataondoa vipi pingamizi hizi? Usawa hasa ni kufahamiana na kuelewena Walebanoni kwa uzalendo wao tu na misingi ya ushirikiano kwa masilahi yao, lakini dini aachiwe hiyari kila mtu kulingana na alivyokinai na mazoweya yake.”

Kutokana na kauli ya mwandishi huyu na wengineo wengi, katika kupinga fikra ya dini, inatubainikia kuwa siri ya upinzani wao, kama tulivyodokeza mwanzoni, imetokana na wakuu wa dini kuukumbatia ukoloni, udhalimu na ukandamizaji na kuupamba kwa jina la dini.

Lau wakuu wote wa dini wangeifanyia ikhlasi, wakaifahamisha kwa ufahamu sahihi na wakaibanisha kama alivyoiteremsha Isa na Muhammad na wasiiuze kwa thamani ndogo, basi wapinzani au washambulizi wa kulipwa wasingelipata mwanya wa kuituhumu au kuwa na shaka na dini ya kiislamu wala ya kikiristo.

Lakini jambo la kuvunja moyo ni kuwa watu wamelitumia jina la dini kwa uzushi na wengine wakasimama kuiharibu na kuingiza shaka baada ya kulipwa na maadui wa Mwenyezi Mungu; ndio ikawa radiamali hii kuto- ka kwa mwandishi huyu wa kitabu ‘Kupinga fikra ya dini’ na wengineo. Inasemekana pia mwandishi huyu ni katika wanaolipwa.

Hata hivyo, kwani dini itakuwa imekosea nini ikituhumiwa na wazushi na wenye upendeleo? Ilitakikana mwandishi aangalie ushahidi mwingi ulio katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na suna za Mtume wake na pia katika historia ya Uislamu kuwa dini ni nguvu inayomwelekeza mtu kwenye maisha bora na kwamaba iko mbali na kila jambo lisiloingilika akilini na kugongana na hakika ya maisha.

Hakika hii wanakubaliana nayo wataalamu wengi wa mashariki na wa magharibi wasiokuwa waislamu. Tazama Juz. 1 (2:1-5) kifungu cha ‘Qur’an na Sayansi,’ Juz. 9 (8:24) kifungu cha ‘Dini na maisha,’ na Juz. 15 (17:9-12) kifungu cha ‘Uislamu ni dini ya maumbile.

6

لَقَدْ كَانَ لِسَبَإٍ فِي مَسْكَنِهِمْ آيَةٌ جَنَّتَانِ عَن يَمِينٍ وَشِمَالٍ كُلُوا مِن رِّزْقِ رَبِّكُمْ وَاشْكُرُوا لَهُ بَلْدَةٌ طَيِّبَةٌ وَرَبٌّ غَفُورٌ ﴿١٥﴾

15. Hakika ilikuwa ishara kwa wasabaa katika maskani yaobustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mola wenu na mumshukuru. Mji mzuri na Mola mwenye maghufira.

فَأَعْرَضُوا فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ سَيْلَ الْعَرِمِ وَبَدَّلْنَاهُم بِجَنَّتَيْهِمْ جَنَّتَيْنِ ذَوَاتَيْ أُكُلٍ خَمْطٍ وَأَثْلٍ وَشَيْءٍ مِّن سِدْرٍ قَلِيلٍ ﴿١٦﴾

16. Lakini wakaacha, basi tukawapelekea mafuriko makubwa na tukawabadilishia bustani zao kwa bustani nyingine mbili zenye matunda makali na mivinje na miti michache ya kunazi.

ذَٰلِكَ جَزَيْنَاهُم بِمَا كَفَرُوا وَهَلْ نُجَازِي إِلَّا الْكَفُورَ ﴿١٧﴾

17. Hayo tuliwalipa kwa vile walikufuru, nasi kwani tunamwadhibu isipokuwa anayekufuru?

وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ الْقُرَى الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا قُرًى ظَاهِرَةً وَقَدَّرْنَا فِيهَا السَّيْرَ سِيرُوا فِيهَا لَيَالِيَ وَأَيَّامًا آمِنِينَ ﴿١٨﴾

18. Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki, tuliweka miji iliyo dhahiri na tukaweka humo vituo vya safari: Nendeni humo usiku na mchana kwa amani.

فَقَالُوا رَبَّنَا بَاعِدْ بَيْنَ أَسْفَارِنَا وَظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ فَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ وَمَزَّقْنَاهُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ ﴿١٩﴾

19. Wakasema: Mola wetu, weka mwendo mrefu baina ya safari zetu. Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi na tukawatawanyatawanya. Hakika katika hayo, bila shaka kuna ishara kwa kila aliye na subira sana mwenye kushukuru.

وَلَقَدْ صَدَّقَ عَلَيْهِمْ إِبْلِيسُ ظَنَّهُ فَاتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٠﴾

20. Na hakika Ibilisi alisadikisha dhana yake juu yao. Na walimfuata isipokuwa kundi la waumini.

وَمَا كَانَ لَهُ عَلَيْهِم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يُؤْمِنُ بِالْآخِرَةِ مِمَّنْ هُوَ مِنْهَا فِي شَكٍّ وَرَبُّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ ﴿٢١﴾

21. Naye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, ila ni kwa sababu tujue ni nani mwenye kuamini Akhera na nani anayetilia shaka. Na Mola wako ni mwenye kuhifadhi kila kitu.

SABAA

Aya 15 – 21

LUGHA

Sabaa ni jina la kabila la waarabu, lililotokana na jina la baba ambaye kizazi chao kinatokana naye.

KISA KWA UFUPI

Katika Tarikh almas’ud imeelezwa kuwa mfalme wa kwanza wa Yemen alikuwa ni Sabaa bin Yashjab bin Ya’arab bin Qahtan. Jina lake hasa lilikuwa ni Abdu Shams. Aliitwa Sabaa kutokana na kuchukua kwake mateka[2] . Ardhi ya Sabaa ilikuwa ndio ardhi yenye rutuba na utajiri zaidi katika Yemen.

Kabla yake, ardhi hiyo, ilikuwa ikikumbwa na mafuriko yaliyoangamiza mimea na majengo. Basi akawakusanya wataalamu wa zama hizo kutafuta suluhisho la tatizo hilo. Wakaafikiana kujengwe ukuta baina ya milima miwili na kuweka mlango wa kuyafungulia maji kwa kiasi wanachokitaka.

Ukuta huu ulijulikana kwa jina la mji wa Maaribu uliokuwa karibu na ukuta. Kadiri siku zilivyoendelea kupita ndivyo maji nayo yalivyoongezeka, ukuta ukaharibika na maji yakavunja majumba na mashamba. Watu wakagura na wakatawanyika sehemu kadhaa za nchi. Hapa ndipo ilipochukuliwa mithali: ‘Mikono ya sabaa imetawanyika.’

Katika Tafsir At-Tabari na Majmaul-Bayan imeelezwa kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w. w ) kuhusu Sabaa, akasema: ‘Kulikuwa na mtu mmoja mwarabu aliyekuwa na watoto kumi, sita katika wao walikwenda upande wa Yemen na wane wakaenda upande wa Sham.

Waliokwenda upande wa Yemen ni: Kinda, Himyar, Azd, Ash’ar, Madh-hij na Anmar, miongoni mwao ni Khath’am na Bujayla. Ama wale waliokwenda upande wa Sham ni: Amila, Judham, Lakhmu na Ghassan.

Katika Tafsir Al-Ma raghi imeelezwa kuwa watafiti walikuwa wakitilia shaka jambo hili la ukuta, mpaka mgunduzi wa kifaransa Arno alipoweza kufika Maarib mnamo mwaka 1843 na akaona athari yake na kuweza kuchora picha iliyosambazwa kwenye magazeti ya ufaransa mwaka 1874. Baadaye Halevi na Glazr, wakatembelea sehemu hiyo, wakaafikiana na aliyoyasema.

MAANA

Hakika ilikuwa ishara kwa wasabaa katika maskani yaobustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mola wenu na mumshukuru. Mji mzuri na Mola mwenye maghufira.

Ishara ni dalili na alama ya neema za Mwenyezi Mungu zilizo nyingi katika mji huo. Bustani mbili kulia na kushoto, ni kinaya cha rutuba na mazao mengi yaliyopatikana kila pembe ya mji huo. Kila aliyepita ardhi ya Sabaa aliweza kuona mazao mengi kulia na kushoto.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwaamrisha watu wa Sabaa, kupitia kwa manabii na Mitume wake, kuwa waneemeke na kheri zake na wamshukuru na wampwekeshe.

Lakini wakaacha, basi tukawapelekea mafuriko makubwa na tukawabadilishia bustani zao kwa bustani nyingine mbili zenye matunda makali na mivinje na miti michache ya mikunazi.

Neema ya Mwenyezi Mungu waliitumia kwa kumuuasi. Akawahadharisha kupitia Mitume wake, lakini halikuwafaa onyo wala kuzingatia mawaidha. Basi Mwenyezi Mungu akawapelekea mafuriko yaliyobomoa ukuta na kuharibu mimea. Mwenyezi Mungu akabadilisha bustani za matunda na konde za mazao kwa miti isiyoshibisha; kama vile: mikwaju, mikunazi na mingineyo inayomea jangwani ambayo wanakula wanyama wenye njaa au mtu aliyeishiwa kabisa.

Hayo tuliwalipa kwa vile walikufuru, nasi kwani tunamwadhibu isipokuwa anayekufuru?

Aliwalipa ufukara, ambao ni malipo ya kufedhehesha zaidi. Kuna Hadith isemayo: “Ufukara unakurubia kuwa ni ukafiri.” Nyingine inasema: “Ufukara unasawijisha uso duniani na akhera.” Imam Ali(a.s) alimwambia mwanawe Muhammad Al-Hanafiya: “Hakika ufukara unapunguza dini –yaani unampeleka mtu kumwasi Mwenyezi Mungu – unazubaisha akili na unaita mateso.”

Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki, tuliweka miji iliyo dhahiri na tukaweka humo vituo vya safari: Nendeni humo usiku na mchana kwa amani.

Baina yao ni watu wa Sabaa. Makusudio ya miji ni Sham – kama walivyosema wafasiri-ambao Mwenyezi Mungu aliubariki kwa maji, miti, rutuba na matunda. Iliyodhahiri maana yake ni kuwa karibu ikijitokeza na kuonana.

Kuweka vituo vya safari baina ya mji mmoja na mwengine; kiasi ambacho msafiri anakuwa kwenye mji mmoja asubuhi na jioni anakuwa kwenye mji mwingine. Aya inausifia mji wa Sabaa kabla ya kuharibika. Maana yake ni kuwa miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu na fadhila zake ni kuwa anayetaka kusafiri anakuwa kwenye amani ya nafsi yake na mali yake na hakuwa na haja ya kuchukua masurufu ya safari au kuhofia kiu wala njaa.

Lakini wakachoka na neema wakasema: Mola wetu weka mwendo mrefu baina ya safari zetu.

Yaani weka mbuga na nyika ili tutafute usafiri na tuchukue masurufu ya safari; sawa na walivyofanya wana wa israil walipochoka na Manna na Salwa na kumwambia Musa: “Basi tuombee

Mola wako atutolee vile vinavyooteshwa na ardhi miongoni mwa mboga zake, na matango yake na ngano yake na adesi zake na vitunguu vyake. Akasema: ‘Mnabadili vitu duni kwa vile vilivyo bora?” Juz.1(2:61).

Na wakazidhulumu nafsi zao kwa kupituka mipaka na kukufuru neema. Basi tukawafanya ni masimulizi na tukawatawanyatawanya. Hakika katika hayo, bila shaka kuna ishara kwa kila aliye na subira sana mwenye kushukuru.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliwatawanya ardhini mpaka wakawa ni historia kwa vizazi na mazingatio kwa mwenye kuvumilia shida na akushukuru wakati wa raha.

Na hakika Ibilisi alisadikisha dhana yake juu yao. Na walimfuata isipokuwa kundi la waumini. Naye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao.

Shetani aliwahadaa wamuasi Mwenyezi Mungu; wakamsikiliza na kumtii wale waliopetuka mipaka na kukufuru na wakamwasi wale walioamini na kuwa na takua. Aya hii inaashiria kauli ya Ibilisi aliposema:

وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٣٩﴾ إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ ﴿٤٠﴾ قَالَ هَـٰذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ ﴿٤١﴾ إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ ﴿٤٢﴾

“Na nitawapoteza wote; isipokuwa waja wako waliosafishwa. Akasema (Mwenyezi Mungu): Hii ni njia juu yangu mimi iliyonyooka. Hakika waja wangu hutakuwa na mamlaka nao, isipokuwa wale wapotofu waliokufua- ta.” Juz. 14 (15:39 – 42).

Ila ni kwa sababu tujue ni nani mwenye kuamini Akhera na nani anayetilia shaka.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawajua zaidi waja wake kuliko wao wenyewe, lakini anawajaribu kwa raha na dhiki na kwa matamanio na hawaa, ili awadhihirishe ulimwenguni na yaonekane makusudio yao na vitendo vyao ambavyo vinastahiki thawabu na adhabu.

Maana ya Aya hii yamekaririka mara nyingi, ikiwemo Juz. 4 (3: 140).

Na Mola wako ni mwenye kuhifadhi kila kitu.

Hakimpotei chochote kilichomo mbinguni wala ardhini. Kuna Hadith isemayo: “Mche Mwenyezi Mungu kama kwamba wewe unamuona; ukiwa humuoni basi Yeye anakuona.”

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ ﴿٢٢﴾

22. Sema: Waombeni hao mnaodai kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu. Hawamiliki hata chembe katika mbingu wala ardhini. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala hawana msaidizi miongoni mwao.

وَلَا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ عِندَهُ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُ حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٢٣﴾

23. Wala hautafaa uombezi mbele yake ila kwa yule aliyempa idhini. Hata itakapoondolewa fazaa kwenye nyoyo zao, watasema: Kasema nini Mola wenu? Watasema: Haki, naye ndiye aliye juu, Mkubwa.

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ وَإِنَّا أَوْ إِيَّاكُمْ لَعَلَىٰ هُدًى أَوْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢٤﴾

24. Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini? Sema, ni Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila shaka tuko kwenye uongofu au upotofu ulio wazi.

قُل لَّا تُسْأَلُونَ عَمَّا أَجْرَمْنَا وَلَا نُسْأَلُ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٢٥﴾

25. Sema: Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda.

قُلْ يَجْمَعُ بَيْنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفْتَحُ بَيْنَنَا بِالْحَقِّ وَهُوَ الْفَتَّاحُ الْعَلِيمُ ﴿٢٦﴾

26. Sema: Mola wetu atatukusanya kisha atatuhukumu kwa haki, naye ndiye Hakimu, Mjuzi.

قُلْ أَرُونِيَ الَّذِينَ أَلْحَقْتُم بِهِ شُرَكَاءَ كَلَّا بَلْ هُوَ اللَّـهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٧﴾

27. Sema: Nionyesheni wale mliowaunganisha naye kuwa washirika. Hapana! Bali Yeye ni Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾

28. Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mtoaji bishara na muonyaji, lakini watu wengi hawajui.

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٩﴾

29. Na wanasema: Ni lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?

قُل لَّكُم مِّيعَادُ يَوْمٍ لَّا تَسْتَأْخِرُونَ عَنْهُ سَاعَةً وَلَا تَسْتَقْدِمُونَ ﴿٣٠﴾

30. Sema: Mna miadi ya siku ambayo hamtaakhirisha saa wala hamtaitangulia.

SEMA WAITENI MNAODAI KUWA NI WAUNGU

Aya 22 – 30

MAANA

Sema: Waombeni hao mnaodai kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu.

Washirikina waliabudu Malaika na masanamu, Mtume(s.a.w. w ) akawakataza lakini hawakusikia, akawaambia kwa amri ya Mwenyezi Mungu: iko wapi dalili ya mnaowafanya kuwa ni miungu? Waombeni manufaa au kukinga madhara, muone kuwa wanasikia na kuwajibu?

Lengo la matakwa haya ni kusimamisha hoja isiyoshindwa. Ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾

“Sema:“Waombeni hao mnaodai badala Yake hawawezi kuwaondolea madhara wala kuyabadilisha.” Juz. 25 (17:56).

Hawamiliki hata chembe katika mbingu wala ardhini. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala hawana msaidizi miongoni mwao.

Maneno yanaelekezwa kwa washirikina. Hata chembe ni kinaya cha kuwa hawamiliki hata kitu kilicho kidogo na duni. Maana ni kuwa hana mshirika wala msaidizi.

Wala hautafaa uombezi mbele yake ila kwa yule aliyempa idhini.

Hii ni kuwarudi washirikina na kauli yao:

مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ ...﴿٣﴾

“Hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu.” (39:3).

Kwa maelezo zaidi Tazama Juz. 1 (47 – 48) kifungu cha ‘Shufaa.’

Hata itakapoondolewa fazaa kwenye nyoyo zao, watasema: Kasema nini Mola wenu? Watasema: Haki, naye ndiye aliye juu, Mkubwa.

Wafasiri wametofautiana kuhusu watakaoondolewa fazaa, watakaouliza na wataoulizwa.

Kauli yenye nguvu zaidi ni watakaoondolewa fazaa ni wote walioko mbinguni na ardhini; kwamba fazaa itawaenea wote isipokuwa atakaowataka Mwenyezi Mungu; kama ilivyoelezwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu:

وَيَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَاخِرِينَ ﴿٨٧﴾

“Na siku itakapopuziwa parapanda, watafazaika waliomo mbinguni na waliomo ardhini, ila amtakaye Mwenyezi Mungu. Na wote watamfikia hali ya kuwa ni wanyonge.” Juz. 20 (27:87).

Mara kwa mara tumesema kuwa Qur’an inajifasiri yenyewe. Kwa hiyo maana yanakuwa kwamba wakati wa Kiyama, wa mbinguni na wa ardhini watagawanyika mafungu mawili: Kuna kundi litakalokuwa na fazaa kubwa na kundi jingine litakuwa na amani. Hawa ndio walioashiriwa na kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ila amtakaye Mwenyezi Mungu.” Kundi la kwanza ikitulia fazaa yake, watauliza kundil la pili: Mola wenu amesema nini na mwisho wetu ni upi? Watakoulizwa watajibu kuwa Mwenyezi Mungu amesema haki naye ndiye aliye juu, Mkubwa.

Jibu hili kwa ujumla linaashiria kuwa Mwenyezi Mungu hana mshirika wala msaidizi. Pia hakuna atakayeombea kwake isipokuwa aliyempa idhini.

Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini?

Maneno yanaelekezwa kwa Mtume(s.a.w. w ) awaambie washirikina. Riziki ya kutoka mbinguni ni mvua na mwangaza na riziki ya ardhini ni mazao ya porini na yanayopandwa.

Sema : ni Mwenyezi Mungu, siyo masanamu au Malaika, wala sio Isa au Uzayr. Kwa vile hili ndio jibu pekee, ndio maana Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake mtukufu awajibie walioulizwa.

Na hakika sisi au nyinyi bila shaka tuko kwenye uongofu au upotofu ulio wazi.

Nabii ana uhakika kwamba yeye yuko kwenye uongofu na kwamba washirikina wako kwenye upotevu, lakini walipoukataa uwongofu na haki ndio akatumia mfumo huu wa hekima na kuwaambia kuwa mja wetu atakuwa kwenye haki na mwingine kwenye upotevu, basi zirudieni akili zenu muone ni nani aliye kwenye usawa?

Huu ndio mfumo wa Mtume wa uwongofu na rehema, kuongezea kuwa mwenye haki anajiamini hata wakimhalifu watu wote wa ardhini.

Sema: Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda.

Huu ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t):

وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ أَنتُم بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٤١﴾

“Na kama wakikukadhibisha, basi sema: Mimi nina amali yangu na nyinyi mna amali yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa ninayoyatenda, na mimi sina jukumu kwa mnayoyatenda.” Juz. 11 (10:41).

Sema: Mola wetu atatukusanya kisha atatuhukumu kwa haki, naye ndiye Hakimu, Mjuzi.

Siku ya mwisho ina majina mengi; miongoni mwayo ni siku ya mkusanyiko. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

يَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ﴿٩﴾

“Siku atakayowakusanya kwa ajili ya Siku ya mkusanyiko” (64:9).

Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) atatukusanya sisi na na nyinyi ili tuangalie hisabu, malipo na matendo. Hapo pazia litafunuka na mtajua kundi gani ndio lililoelekea njia ya kunyooka.

Sema: Nionyesheni wale mliowaunganisha naye kuwa washirika.

Hapa kuna manaeno ya kukadiria kuwa nionyesheni dalili ya kuwa masanamu ni washirika wa Mwenyezi Mungu au watawajongeza kwa Mwenyezi Mungu.Hapana! Yeye hana mshirika wala msaidizi wala wa kuombea mbele yake isipokuwa aliyempa idhini.

Bali Yeye ni Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Hakuna enzi wala nguvu isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Ama dalili za hekima yake na utukufu wake zinajitokeza katika kuumba ulimwengu na maajabu yake.

Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mtoaji bishara na muonyaji, lakini watu wengi hawajui.

Tazama Juz. 7 (6:92) na Juzuu hii tuliyo nayo (33:40) Kifungu cha ‘Kwanini utume umeishilia kwa Muhammad(s.a.w. w ) ?’

Na wanasema: Ni lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?”

Imetangulia neno kwa neno katika Juz. 11 (10:48).

Sema: Mna miadi ya siku ambayo hamtaakhirisha saa wala hamtaitangulia.

Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameahidi ufufuo, hisabu na malipo, naye bila shaka, ni mwenye kutekelza miadi yake, lakini kwa wakati alioupanga yeye ambaye hekima yake imetukuka, hatanguliwi wala hacheleweshwi. Basi yasiwahade mliyo nayo enyi washirikina, kwa sababu yatakwisha tu, muda mfupi au mrefu, kisha marejeo yenu nyote ni kwa Mwenyezi Mungu awajulishe yale mliyokuwa mkiyafanya.

4