• Anza
  • Iliyopita
  • 12 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 9941 / Pakua: 2565
Kiwango Kiwango Kiwango
UKWELI WA USHIA

UKWELI WA USHIA

Mwandishi:
Swahili

8 UKWELI WA USHIA

KUTAWASSALI KUPITIA KWA MAWALII WA MWENYEZI MUGNU

KHALID: Salaamun alaykum.

WALIID: Oh..ni akina nani hawa makafiri na mazindikiwanao jiita kuwa ni waislaam. Jihadharini.. kutokana na watu hawa.

MUHAMMAD: Unawakusudia watu gani?

WALIID: Hawa Mashia.

MUHAMMAD: Usiwatukane, na wala usiwanasibishe katika ushirikina, kwani wao ni Waislaam.

WALIID: Watu hawa ni bora zaidi kuuwawa kuliko hata makafiri.MUHAMAAD: Ni ghadhabu gani hii isiyo kuwa na hisia za ubinadamu uliyo nayo, kwa nini wao wawe washirikina?

WALIID: Hakika wao wanamshirikisha Mwenyezi Mungu na kumuwekea waungu wengine, na wanamuabudu Mungu mwingine asie kuwa Allah asie wadhuru wala kuwanufaisha.

MUHAMMAD: Wanamshirikisha vipi Mwenyezi Mungu?

WALIID: Wao wanafanya tawassuli kupitia kwa Mitume, maimam na mawalii wa Mwenyezi Mungu ili awakidhie haja zao na wanasema: Ewe Muhammad ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ewe Ali, ewe Husein, ewe Swahibuz-zaman)[20] na mengineyo wakidai ya kuwa mawalii hawa wanauwezo wa kukidhi haja zao. Na hili si jambo lingine bali ni ushirikina wa wazi kabisa na ukafiri, na ni kumuabudu asie kuwa Mwenyezi Mungu.?

MUHAMMAD: Nina mazungumzo kiasi ni ruhusu tuweze kuzungumza.WALIID: Sema unacho taka kukisema.

MUHAMMAD: Mimi nilikuwa ni miongoni mwa watu walio kuwa wakiwabebesha na kuwatwisha Mashia aina tofauti za matusi na shutuma, na nilikuwa sikai chini wala kusimami isipokuwa nitawatukana na kuwatuhumu, na yote nikiyafanya nikiwa mbali nao, mpaka safari ya hija ilipo nikutanisha na mmoja wa Mashia, na nilipo zungumza nae nilikuwa mkali na nikizungumza kwa ukali na nilito aina zote za matusi na maneno mabaya yaliyo kuwa yakinikera kifuani mwangu kutokana na ghadhabu niliyo kuwa nayo kwa miaka mingi, na Shia yule hakuna alicho kifanya isipokuwa alikuwa na subira kwa yale niliyo kuwa nikiyasema, na kuyanyamazia, na huku akinicheka, na bashasha au furaha ndiyo iliyo kuwa ikionekana na kudhihiri usoni mwake, na mimi kila nilivyo kuwa nikizidisha matusi kwake ndivyo alivyo zidisha ukunjufu usoni mwake na akinipoza kwa lile harara nililo kuwa nalo kwa tabasamu ambazo zilikuwa hazikatiki midomoni mwake, tabia ile njema ilizima moto na harara nililo kuwa nalo la kuwafanyia uadui na kuwatukana.

Na mimi nilipo nyamaza, akanielekea kwa maneno akisema: Ewe ndugu yangu katika dini..Muhammad je unaniruhusu nizungumze nawe maneno kadhaa? Kisha akasema, nami nikasema, akasema..nami nikasema, akasema..nami nikasema..hadi ikanibainikia na kunidhihirikia ya kuwa wana haki katika maudhui mengi sana ambayo tuliyazungumzia. Na miongoni mwa maudhui niliyo yaona kuwa wanahaki katika maudhui hayo ni maudhui ya kutawasuli kupitia kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu.

WALIID: Je uliathirika na uongo wao, hadaa zao na ushirikina wao..ni kwa kiasi gani umekosa muongozo katika dini, na ni kwa kiasi gani umekosa maarifa ya kiislaam!

MUHAMMAD: Kwa hakika mimi kwa hivi sasa niko tayari kujadiliana na wewe kuhusu maudhui ya kutawasali kupitia kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu, kwa mujibu wa Qur'ani yenye hekima, na Sunna tukufu na Mwenendo wa Watu wema kati ya waislaam.

WALIID: Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu ni mpole sana kwa waja wake kuliko viumbe wengine, na hakuna kizuizi chochote kati yake na waja wake, kwa hivyo basi ni juu ya kila mja kufanya mawasiliano na Mwenyezi Mungu mtukufu- moja kwa moja bila ya kuwa na wasila wa aina yoyote kwa muda wowote ule, na katika sehemu zote, yaani afanye mawasiliano na Mwenyezi Mungu moja kwa moja na atawasali kwake yeye mwenyewe, kwani haijuzu kutawasali kupitia kwa yeyote asie kuwa Mwenyezi Mungu vyovyote cheo chake kitakavyo kuwa kikubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, hata kama atakuwa ni Mtume au Imam au mfalme au mja mwema na wengineo.

MUHAMMAD: Kwanini haijuzu kufanya hivyo?

WALIID: Kwa sababu mwanadamu anapo fariki anakuwa ametoweka na kumalizika, na alie kwisha toweka na kumalizika haiwezekani kufaidika nae, sasa vipi utatawasali na mtu alie toweka na kumalizika?

MUHAMMAD: Utasemaje kuwa mauti ni kumalizika, nani anae itakidi na kusema hivyo?

WALIID: Imam Muhammad bin Abdul wahhab amesema: Kutawasali kupitia watu wema walio fariki ni sawa na kukizungumzia kitu kilicho toweka na kumalizika na kisicho kuwepo, na tendo hilo ni tendo baya kiakili. Na imenukuliwa kutoka kwa mmoja wa wafuasi wake au ilimfikia habari na kuiridhia ya kuwa (Fimbo yangu hii ni bora kuliko Muhammad, kwa sababu hufaidika nayo kuulia nyoka na nge na mfano wa hivyo na Muhammad amekufa na hana manufaa tena)[21] - Kwa hivyo haya na mengineyo yanatujulisha juu ya ubaya wa kutawasali kupitia kwa maiti hata kama atakuwa ni Nabii au Mtume wa Mwenyezi Mungu.

MUHAMMAD: Ukweli ni kinyume na unavyo sema, kwani mwanadamu anapo kufa hufunukiwa na kuona ulimwengu zingine ambazo hazikuwa ni zenye kumfunukia kabla ya kufariki kwake. Mwenyezi Mungu mtukufu anasema:Tumekuondolea pazia lako na kuona kwako leo kuwa kukali. suratul-qaf aya 22. Pia amesema Mwenyezi Mungu mtukufu (Wala msiseme kwamba wale walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wa hai lakini nyinyi hamtambui). Suratul-baqarah aya ya 154. Na pia anasema (Wala usidhani wale walio uliwa katika njia ya Mwenyeezi Mungu kuwa ni wafu, bali ni hai wanaruzukiwa kwa Mola wao) suratu Al-imraan aya 169.

Na katika Bukhari[22] imepokelewa kuwa Mtume(s.a.w.w) alifika kwenye shimo Walilo zikiwa washirikina walio uwawa katika vita vya Badri na kuwazungumzia washirikina kwa maneno yafuatayo: (Hakika sisi tumepata tuliyo ahidiwa na Mwenyezi Mungu na tumekuta kuwa aliyo tuahidi ni kweli, je ninyi mmeyakuta aliyo waahidi mola wenu ni ya kweli) akaulizwa je unawauliza watu walio kufa? Mtume(s.a.w.w) akasema: (Hakika nyinyi si wenye kusikia zaidi kuliko wao)[23] . Hakika mwanadamu sawa awe muumini au kafiri anapo kufa hawi kama kitu kisicho na hisia kisicho ona wala kusikia. Na Ghazaliy[24] nae akiwa ni mmoja kati ya maimamu wa madhehebu ya Shafiiy amesema: (Baadhi wakidhania kuwa kifo ni kutoweka kabisana hii ndio rai ya walahidi (wasio muamini Mungu..). [25] .

WALIID: Imam Ghazaliy anaona kuwa kauli ya kutoweka kabisa kwa mwanadamu kupitia kifo ni Ilhadi (kufru)? Hayo ameyasema wapi?MUHAMMAD: Ameyataja katika kitabu chake kiitwacho ( Ihyaaul-uluum)[26] rejea kitabu hicho, utaipata nassi ya haya tuliyo yasema na kuyataja.[27] .WALIID : Maneno haya ni ya ajabu kutoka kwa mtu kama Ghazaliy!

MUHAMMAD: Hilo si jambo la ajabu kutoka kwa Ghazaliy bali la ajabu ni hili litokalo kwako ya kuwa huyafahamu hayo. Je hukusikia Mtume(s.a.w.w) alivyo wazungumzia washirikina katika kisima cha badri, na lau kama wangekuwa wametoweka kabisa kwa kufa kwao, hawasikii wala kufahamu, Mtume(s.a.w.w) asinge wazungumzisha, pamoja na kuwa Mtume(s.a.w.w) alisema: (Nyinyi si wenye kusikia zaidi kuliko wao).[28] Hiyo ina maana kuwa wao wanasikia kama msikiavyo, na wanafahamu kama mnavyo fahamu. Je umekinaika na haya?

WALIID: Ndio nimekinaika. Lakini mimi ninatahayari ni vipi mimi katika muda wa miaka yote hiyo sikuwa ni mwenye kudadisi na kuiangalia kwa makini aya hii ili niweze kuyafikia maana haya?! Ni vipi sikuisikia hadithi hii ya Mtume(s.a.w.w) , na kauli hii ya Imam (Ghazaliy)?

MUHAMMAD: Je hadi hivi sasa umeamini nusu ya kauli za Mashia ya kuwa: Mtu hatoweki kabisa kwa kufariki? Au bado unashaka?

WALIID: Hapana..hakuna shaka yoyote niliyo bakia nayo katika hilo, lakini mimi ninautata katika jambo lingine!

MUHAMMAD: Ni utata gani huo?

WALIID: Utata wenyewe ni kuwa, inakuwaje ibnu Abdul-wahhab anaitakidi ya kuwa mtu anatoweka kabisa kwa kufariki, pamoja na kuwa Ghazaliy anasema ya kuwa hayo ni maneno ya walahidi? Pamoja na kuwa Mtume(s.a.w.w) anasema wazi ya kuwa mtu alie fariki (mfu) anasikia kama asikiavyo mtu alie hai na hakuna tofauti kati yao? Kisha nivipi ibnu Abdul-wahhab na wengineo wanasimama kwa ushupavu bila woga na kusema: (Fimbo yangu hii ni bora kuliko Muhammad, kwani fimbo hii inamnufaisha mtu, na Muhammad hamnufaishi mtu kwa chochote) ?![29] Haya ndio yaliyo nifanya nitahayari.

MUHAMMAD: Usitahayari. Kwa hakika sisi inatulazimu kuwafahamu watu kutokana na kufuata kwao misingi ya dini, kwa maana kila mtu ambae kauli zake na matendo yake yanawafikiana na Qur'ani na Sunna na sira ya waja wema walio tangulia (As-salaf-s-swalih) huyo ndio muumini, si kuifahamu dini kupitia watu fulani, kwani sisi tutakapo mfahamu fulani mtoto wa fulani kwa mfano ya kuwa ni muumini mwenye ikhlasi haijuzu kuzihesabu kauli zake na matendo yake kuwa ni sehemu ya Uislaam, hata kama tutayaona na kufahamu waziwazi ya kuwa yanapingana na kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake(s.a.w.w) na sira ya waja wema walio pita, na kwamba hiyo ni kufru na ilhadi, bali lililo wajibu kwetu, wakati tunapo ona upotovu kwa mtu yeyote vyovyote atakavyo kuwa cheo chake ni wajibu kwetu kujitenga nae na kuwa mbali nae, na kuifuata haki iliyo tudhihirikia na kuiona.

WALIID: Maneno yako ni sahihi..na mimi ni miongoni mwa waumini walio kuwa na imani kubwa kwa mtu huyu, na hivi sasa umenionyesha na kunifahamisha makosa makubwa ya mtu huyu, ambayo huzingatiwa kuwa ni ilhadi na kufru katika dini, kwa hakika imani yangu kwake imetoweka, na sinta mzingatia kuwa ni mwanazuwoni ambae anafaa kuchukua kutoka kwake hukumu za kiislaam.

MUHAMMAD: Achana na kumzungumzia Ibnu fulani, ili tuweze kuzungumzia mambo mengine.

WALIID: Ndio..ni kweli kuwa maiti hatoweki na wala hamaliziki kabisa kwa kufariki kwake, lakini inajuzu vipi kutawasali kupitia kwake ikiwa ni Mtume au Imam au ni katika watu wema? Pamoja na kuwa tunafahamu ya kuwa kuna watu waizingatiao tawassuli kupitia kiumbe ni shirki na ni kutoka katika dini?.

MUHAMMAD: Je inajuzu kutawasuli kupitia kwa mtu alie hai, na kumuomba haja fulani, au kumuomba dua na mengineyo, kwa mfano kusema: Ewe Baaqir, au Ewe Jaafar, au Ewe Ridhaa au Ewe fulani..nipatie Dinari, au niombee kwa Mwenyezi Mungu anisamehe, au nishike mkono hadi msikitini na mengineyo yasiyo kuwa haya?

WALIID: Ndio inajuzu kufanya hivyo.

MUHAMMAD: Kwa hivyo baada ya kuthibiti ya kuwa maiti anasikia kama asikiavyo mtu alie hai, ni kizuizi gani kizuiacho kutawasali kupitia kwa maiti baada ya kufariki kwake, na kumuomba haja fulani? Waliid aliinamisha kichwa chake na kufikiria ..kisha akainua kichwa chake na kusema: Ndio ni kama usemavyo ewe Muhammad, maneno yako ni sahihi.

MUHAMMAD:Na tunayo dalili nyingine inayo ruhusu na kujuzisha kufanya tawassuli kupitia kwa Mtume (s.a.w.w)na waja wema.

WALIID: Ni dalili ipi hiyo?

MUHAMMAD: Hakika maswahaba [30] katika zama za Mtume (s.a.w.w)na baada ya kufariki kwake walikuwa wakitawassali kupitia kwa Mtume, na si Mtume mwenyewe wala sahaba yeyote kati ya masahaba walio bakia alie kuwa akiwazuwia kufanya hivyo, na lau kama kutawassali kupitia mtu mwingine asie kuwa Mwenyezi Mungu ni shirki wange zuwia vitendo hivyo.

WALIID: Ni nani alie tawassali kupitia kwa Mtume(s.a.w.w) baada ya kufariki kwake?

MUHAMMAD: Ifuatayo ni baadhi ya mifano hai ya watu walio fanya hivyo: Amepokea Baihaqiy[31] , na Ibnu Abi Shaibah kwa sanadi sahihi. Kama ilivyo pokelewa kutoka kwa Ahmad bin Zainiy Dahlan ya kuwa: Watu walipatwa na ukame katika zama za utawala wa Omar, Bilal bin Haarith akaja kwenye kaburi la Mtume(s.a.w.w) na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu waombee umma wako wanyeshewe na mvua kwa hakika wameangamia[32] Lau kama kumuomba Mtume na kutawasuli kupitia kwake ni shirki, Bilal asinge fanya hivyo- Bilal ambae alifuatana na Mtume kwa muda mrefu- na kuchukua hukumu mbali mbali kutoka kwenye kinywa cha Mtume(s.a.w.w) na masahaba wengine wange mzuwia. Na hii ni dalili yenye nguvu sana juu ya kujuzu kutawassuli kupitia kwa Mtume(s.a.w.w) .

Na Baihaqiy amepokea[33] kutoka kwa Omar ni Khattab, amesema: Amesema Mtume(s.a.w.w) : Adam alipo tenda makosa alisema:Ewe Mola ninakuomba unisamehe kwa haki ya Muhammadhadi mwisho wa hadithi. Lau kama kutawassuli kupiti kwa Mtume kunge kuwa ni haram na shirki basi Nabii Adam (a.s) asinge fanya hivyo. Na imepokelewa ya kuwa [34] Mansour Dawaniqiy ali po hiji, na kuzuru kaburi la Mtume (s.a.w) alimuuliza Imam Maalik[35] (Imam wa madhehbu ya Maalikihhay) na kumwambia: Ewe Aba Abidillahi, Nielekee kibla na kuomba, au nimuelekee Mtume wa Mwenyezi Mungu? Imam Maalik akasema: (Kwa nini huuelekezi uso wako kwake wakati ambapo yeye ni wasila wako na wasila wa baba yako Adam kumuelekea Mwenyezi Mungu, bali muelekee yeye, na Muombe shafaa atakuombea Shafaa, Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:(Na lau wangelikujia walipojidhulumu nafsi zao wakaomba msamaha kwa Mwenyeezi Mungu, na Mtume akawaombea msamaha, bila shaka wangemkuta Mwenyeezi Mungu, Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu) . [36] . Na katika kauli ya Maalik: Yeye ni wasila wako na wasila wa baba yako Adam kwa Mwenyezi Mungu.[37] , kuna dalili ya wazi juu ya kujuzu kufanya tawassuli au kutawasali, bali kuna dalili ya kuwa ni sunna pia kufanya hivyo.

Na bwana Daarimiy pia amepokea[38] katika sahihi yake[39] kutoka kwa Abil-jawzaai, amesema: Watu wa madina walipatwa na ukame mkali, wakamshitakia Aisha, Aisha akasema: Liangalieni kaburi la Mtume na lifanyeni kuwa ni wasila wenu kuelekea mbinguni ili kusiwe na kizuizi kati ya kaburi hilo na mbingu. Wakafanya vile, na mvua ikanyesha hadi nyasi zikaota.

Na kuna mamia ya ushahidi juu ya hilo, utaupata kwenye vitabu vilivyo yaelezea kwa upana mambo haya, sasa ikiwa kutawasali kupitia kwa Mtume(s.a.w.w) inajuzu na si haram, wala shirki, kutawassuli kupitia kwa Maimam, Malaika na watu wema miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu pia ina juzu. Kwani kutawassuli ikiwa ni shirki ni wajibu iwe haram hata kama kutawassuli huko kutakuwa ni kupitia kwa Mtume(s.a.w.w). Na kama inajuzu basi si kutawassuli kupitia kwa Mtume pekee bali hata kupitia kwa watu wote wema kati ya waja wa Mwenyezi Mungu.

WALIID: Hadithi hizi ulizo zinukuu ni za ajabu sana kwangu, kwa hakika sija iona hata hadithi moja kati ya hadithi hizo!

MUHAMMAD: Kama unge rejea kwenye vitabu vya hadithi bila shaka unge ona mamia ya ushahidi uthibitishao kutawassuli kupitia kwa Mtume (s.a.w), na mawaliii wa Mwenyezi Mungu walio wema, na unge ona ya kuwa hadithi hizi nilizo kunukulia si chochote bali ni kama tone katika bahari,[40] na inaonekana ya kuwa si mwingi wa kusoma vitabu vya hadithi na sira ya watu wema walio tangulia?

WALIID: Wingi wa shughuli zangu na kazi nilizo nazo ndizo zinizuiazo kupitia vitabu vya hadithi na sira, pamoja na kuwa nina shauku kubwa sana ya kufanya hivyo.

MUHAMMAD: Sasa ikiwa ni mwenye maarifa machache ya hadithi vipi unathubutu kuwatukana Mashia- bali inakuwaje unathubutu kuwatukana waislaam wote- na kuwanasibisha kwenye shirki kwa sababu tu ya kauli ya Muhammad bin Abdil-wahhab wakati hufahamu chochote katika hadithi? Kwa hivyo si sahihi wala si sawa, na ninakuomba uniruhusu nikueleze kiuwazi na kwa upana zaidi.

WALIID: Kwa tabasamu lako na ukunjufu wa uso wako, sema kila ulicho nacho moyoni mwako ewe Muhammad, hakika sisi ni marafiki, kwa hakika nimeanza mazungumzo haya ili nipate nuru ya elimu yako, na niweze kufaidika kutoka kwako.

MUHAMMAD: Kwa hakika mfano wako ni sawa na mfano wa makafiri wa kikuraishi bila tofauti yoyote, makafiri walio kuwa wakiyaabudu na kuyasujudia masanmu yao, kwa hoja ya kuwa:(Kwa hakika tuliwakuta baba zetu juu ya desturi na hakika sisi tunafuata nyao zao) .[41] Kwanini Mwenyezi Mungu anawakemea? Kwa sababu wao pindi walipo kuwa wakiona haki walikuwa hawaisikilizi haki hiyo, ili waweze kufahamu ni sahihi au laa? Na wakabakia wakiyasujudia na kuyaabudu masanamu yao.

Na wewe ndugu yangu Waliid usiwafuate baba zako ufuataji wa kipofu, bali kuwa ni mwenye kufuata nuru na mwenye kufanya utafiti kuhusu ukweli ili uweze kuipata au kuifikia na kuyajenga maisha yako juu ya haki hiyo, lau kama ungepekua na kufungua vitabu vya hadithi ungekuta kwamba wayasemayo watu fulani ya kuwa haijuzu kutawassali kupitia kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake, na kwamba kufanya hivyo ni shirki ..ni maneno waliyo kubaliana madhehbu zote za waislam na makundi yao yote kinyume na hivyo, je unge amini hivyo?

WALIID: Ndio..kwa sababu inadhihiri ya kuwa Mashia wako na haki na waislaam wengine wako kwenye haki pia katika hilo, lakini nifanye nini kuhusiana na suala la kuwatukana kwangu Mashia?

MUHAMMAD: Muombe msamaha na maghafira Mwenyezi Mungu, na wakati wote utafute ukweli, huenda Mwenyezi Mungu akakusamehe, na wakati wote unapo sikia itikadi yoyote ya Shia ifanyie utafiti, hadi uufikie ukweli, na achana na asabia, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) amesema: Mwenye kuwa na asabia au akafanyiwa asabia kwa hakika amevuliwa na kutolewa imani shingoni mwake (yaani amevuliwa imani).[42]

WALIID: Nitayafanya yote hayo na ninakushukuru sana

9

UKWELI WA USHIA

KUZURU MAKABURI

JAMIIL : Ni zogo gani hili mnalo jisababishi nyinyi Mashia bila ya sababu yoyote?

JAWAD: Ni zogo lipi hilo?

JAMIIL: Kulizuru kwenu kaburi la Mtume(s.a.w.w) na makaburi ya maimam na watu wema.

JAWAD: Je kunatatizo lolote kufanya hivyo?

JAMIIL: Hakika tendo hilo ni haram na kufanya hivyo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu.

JAWAD: Je wewe Jamiil ni punguwani.. mpiga kelele na kila apigae kelele, na mwenye kufuata upepo kama bendela? Kwa hakika mimi sikuwa nikitarajia jambo kama hili kwa mtu kama wewe-mtu mwenye elimu na mwenye kuelewa mambo- unafuata mambo kutokana na asabia bila ya kuwa na dalili wala uthibitisho, nilikuwa nikikuona mtu wa maana sana-hadi hivi sasa- kutokana na hamasa ya kufanya utafiti uliyo nayo na kuufuatilia ukweli na kwenda sambamba na haki kokote uikutako.

JAMIIL: Je maneno yangu haya yanatokana na msukumo wa asabaia za madhehebu yangu?

JAWAD: Ndio..si kinyume na hivyo.

JAMIIL: Unasema ziara ya wapi?

JAWAD: Hebu tuyazungumzie maudhui haya hivi sasa-kuzuru makaburi- na tuyaweke kwenye meza ya mazungumzo ili tuweze kuona nani yuko kwenye haki, na nani yuko katika upotovu?

JAMIIL: Kwa hakika mimi niko tayari, kwa sababu mimi ninafahamu ya kuwa kuzuru makaburi ni shirki.

JAWAD: Utasemaje ya kuwa kuzuru makaburi ni shirki?

JAMIIL: Kwa sababu kitendo hicho kinafanana na namna washirikina walivyo kuwa wakiyatembelea Masanam wakati wote na kuto acha kuyazuru masanamu yao.

JAWAAD: Kwa sababu hiyo imekuwa shirki?

JAMIIL: Ndio..kwani kuyazuru makaburi ni sawa na kuyatembelea makaburi wakati wote, kama vile washirikina wanavyo yatembelea masanamu yao na kuto acha kufanya hivyo.

JAWAD: Je kuwa wakati wote kwenye makaburi ndiko kuliko ifanya ziara kuwa ni shirki?

JAMIIL: Ndio.

JAWAD: Kwa maana hiyo, waislaam wote- bila kubagua- ni washikina, na hakuna mtu yoyote katika dunia asie kuwa mshirikina, na wewe pia ni katika washirikina!

JAMIIL: Kivipi ?

JAWAD: Je umefanikiwa kwenda hija?

JAMIIL: Ndio, ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo.

JAWAD: Je ulifanikiwa kusali ndani ya masjidul-haram (msikiti mtukufu wa makka)?

JAMIIL: Ndio. Ninamshukuru Allah.

JAWAD: Je uliwaonaje waislaam-wakati wa sala-wakiizunguuka na kukaa pembezoni mwa kaaba kwa ajili ya sala, kwa mfano alie simama upande wa magharibi huupa mgongo upande wa magharibi na kuielekea kaabah, na alie simama upande wa kusini huupa mgongo upande wa kusini na kuielekea kaabah, na alie simama upande wa kaskazini mgongo wake huuelekeza upande wa kaskazini na kuielekea kaabah, na kila mmoja upande wowote atakapo kuwa huuelekeza mgongo wake upande ule na kuielekea kaabah kwa ajili ya sala rukuu na sijda, na mengineyo, je hayo uliyaona?

JAMIIL: Ndio yote hayo niliyaona na kuyashuhudia, na mimi nilikuwa nikifanya hivyo hivyo wakati wa sala, upande wowote wa msikiti niliko kuwa nilikuwa nikiuelekeza mgongo wangu huko na kuelekea kibla, kwa sababu sala bila kuelekea kibla ni batili.

JAWAD: Kwa hivyo waislaam wote ni washirikina, na pia wewe ni mshirikina.

JAMIIL: Kwa nini?

JAWAD: Kwani kuelekea kwako kwenye kaaba ukiwa katika ibada kunafanana na waabudu masanamu wayaelekeavyo masanamu wakati wakiyaabudu masanamu yao hayo, kwani tunakuta kwamba waabudu masanamu huyaelekea masanamu waliyo yatengeneza kwa mikono yao-wakati wakiabudu, na wewe unaelekea kwenye nyumba yenye kuta ndefu na iliyo jengwa kwa mawe wakati unapo Sali.

JAMIIL: Lakini kunatofauti kubwa kati ya kuielekea kaaba, na kati ya waabudu masanamu wayaelekeavyo masanamu yao.

JAWAD: Ni tofauti ipi hiyo?

JAMIIL: Kwa hakika mimi wakati ninapo elekea kwenye kaaba-katika sala-siizingatii kaaba kuwa ni Mungu ninae muabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu-ninajikinga na Mwenyezi Mungu-hivyo hivyo waislaam wengine, hawaielekei kaaba katika sala zao kama Mungu, bali tunaelekea kibla kwa sababu Mwenyezi Mungu ametuamuru hivyo, na waabudu masanamu huyaelekea masanamu yao- katika ibada zao-wakiyafanya masanamu hayo kuwa ni miungu yenye kuabudiwa kinyume cha Mwenyezi Mungu alie takasika, kwani wao huyaelekea masanamu yao wakati wa ibada kwa nyoyo zao, na sisi wakati wa sala huelekeza nyoyo zetu kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, na tendo lao hilo ni shirki ya wazi kabisa!

Lakini nitofauti iliyoje kati ya matendo hayo, na kuelekea kwetu kwenye kaaba wakati wa sala? Kati ya mambo mawili hayo kunatofauti kubwa kama tofauti iliyopo kati ya mbingu na ardhi!!

JAWAAD: Kwa hivyo basi kufanana kwake sio sababu ya shirki, laa sivyo matendo yako nayo yange kuwa ni shirki kwa kufanana kwake na matendo ya wenye kuabudu masanamu, na kitu ambacho kimeyafanya matendo ya wenye kuabudu masanamu kuwa ni shirki ni nia yao ya kuyakusudia kwao masanamu, si yale matendo pekee. Na jambo ambalo liliitoa hali yako ya kuelekea kwenye kaaba kusiwe shirki ni kuto kusudia kwako kuiabudu kaaba kwa kuielekea kwako.

JAMIIL: Ndio.

JAWAD: Na sisi Mashia, pia waislaam wengine, katika ziara tuzifanyazo hatukusudii kamwe kumuabudu Mtume Imam au kumuabudu maiti yule alie mwema.. na kufanana kwa ziara hiyo na matendo ya washirikina ikiwa hilo ni sahihi, kwa hakika kufanana huko hakuifanyi ziara hiyo iwe ni jambo la haram na shirki ikiwa mwenye kufanya ziara hakukusudia kuabudu kwa ziara yake hiyo.

Kwa mfano imepokelewa katika hadithi tukufu:[43] Kwani yawezekana amali na tendo moja likawa ni shirki ikiwa atamkusudia kumuabudu asie kuwa Mwenyezi Mungu kwa tendo hilo, na lina weza kuwa tendo hilo linajuzu kulifanya ikiwa hakukusudia kumuabudu asie kuwa Mwenyezi Mungu. Kwa mfano: Ikiwa utasimama sehemu kwa ajili ya sala na mbele yako kuna sanamu limewekwa, ikiwa katika sala yako utakusudia kuliabudu sanamu hilo utakuwa ni mshirikina kwa sala yako hiyo, na ikiwa utakusudia kwa sala yako hiyo kumuabudu Mwenyezi Mungu mtukufu bila ya kukusudia kulielekea sanamu kwa moyo wako sala yako itakuwa ni sahihi na tendo hilo litakuwa ni tendo linalo juzu au linalo faa na kwa kufanya kwako hivyo huwi ni mshirikina.

JAMIIL: Baada ya kufikiria sana.. yote hayo ni sahihi. Nina muomba Mwenyezi Mungu mtukufu akuhifandhi ukiwa ni nguzo yetu tuitegemeayo, kwani umenifahamisha mambo muhimu sana, mambo ambayo asabia ilinizuia kuweza kuyaelewa. Lakini nataka kufaidika zaidi kwa kuuliza swali moja.

JAWAD: Uliza hakuna taabu yeyote.

JAMIIL: Nimefahamu ya kuwa kuzuru makaburi si jambo la haram bali ni jambo linalo faa (linalo juzu), lakini ni siri gani iliyoko katika kuendelea kwenu na kuyatilia umuhimu mkubwa makaburi hayo, na ni sababu gani iwafanyayo kufanya hivyo?

JAWAD: Kwa sababu ni sunna muakkadah (iliyo tiliwa mkazo).JAMIIL: Ni sunna kufanya hivyo?

JAWAD: Ndio..na sunna hiyo imetiliwa mkazo sana.

JAMIIL: Je kuna hadithi inayo julisha kuwa kuzuru kaburi la Mtume na makaburi ya waumini wema(s.a.w.w) ni sunna?

JAWAD : Ndio..kuna hadithi nyingi sana, ukiongezea matendo ya Mtume (s.a.w) mwenyewe, na sira (mwenendo) wa waislaam tangu mwanzoni mwa kuja Uislaam hadi hivi leo.

JAMIIL: Tafadhali nitajie baadhi ya mifano hai juu ya hilo.

JAWAD: 1-Imepokelewa katika hadithi sahihi[44] ya kuwa Mtume (s.a.w) aliwazuru mashahidi walio kufa katika vita vya Uhudi.

2-Imepkelewa pia ya kuwa Mtume(s.a.w.w) alikwenda kuyazuru makaburi ya Baqii'i.

3-Imepokelewa katika (Sunanun-nasaiy) na (Sunanu ibnu Majah) na (Ihyaaul-uluum) cha Ghazaliy kutoka kwa Abi Hurairah

amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu:

[45] Yatembeleeni (yazuruni) makaburi kwani yana kukumbusheni Akhera).

4- Imepokelewa katika kitabu hicho hicho kutoka kwa Abi Hurairah amesema: Mtume (s.a.w) alizuru na kulitembelea kaburi la mama yake na kulia na kuwaliza walio kuwa pembezoni mwake, na akasema:Basi yatembeleeni (yazuruni) makaburi kwa ni makaburi ni yenye kuku kumbusheni Akhera. [46]

5-Na mlango wa hadithi zilizo pokelewa kuhusiana na jinsi na namna ya kuwazuru walio fariki umejawa na hadithi nyingi katika vitabu vyote vya hadithi, kama vile vitabu vya Sahihi na Sunanu. Na kati ya hadithi hizo ni kuwa: Mwenye kuyazuru makaburi anapotoka na kwenda kwenye Baqii'i inabidi aseme:

(Salam iwe juu yanu enyi watu mlioko makaburini kati ya waumini na waislaam).[47] Hizi ni zile hadithi zihusianazo na sunna ya kuzuru makaburi ya waja wema na waumini, na namna inavyo sisitizwa na kuhimizwa kufanya hivyo.Ama zihusianazo na kulizuru kaburi la Mtume(s.a.w.w) ni nyingi sana, na tutataja baadhi ya hadithi hizo:

1-Imepokelewa na Daru Qutniy[48] na Ghazaliy[49] na Baihaqiy[50] na wengineo ya kuwa Mtume(s.a.w.w) alisema:(Atakae nizuru na kulitembea kaburi langu basi itakuwa ni wajibu kupata shafaa yangu).

2-Na imepokelewa ya kuwa Mtume(s.a.w.w) alisema:(Mwenye kunizuru katika mji wa Madina akitaraji thawabu za Mwenyezi Mungu basi nitakuwa ni muombezi wake na mwenye kumshuhudia siku ya kiama) [51] .

3- Imepokelewa kutoka kwa Naafiu, kutoka kwa Ibnu Omar, kutoka kwa Mtume (s.aw) amesema:

(Mwenye kwenda hija na asinizuru hakika atakuwa maenitelekeza na kuniacha nikiwa mpweke) . [52]

4-Imepokelewa kutoka kwa Abi Hurairah, kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) amesema:([53] ) (Mwenye kunizuru baada ya kufariki kwangu ni kana kwamba amenizuru nikiwa hai) .

5-Imepokelewa kutoka kwa Ibnu Abbas, kutoka kwa Mtume(s.a.w.w) amesema:(Mwenye kufanya hija na akanikusudia kwa kunifanyia ziara katika msikiti wangu atakuwa na hija yenye kukubaliwa) .[54] Na kuna hadithi zingine nyingi zisizo kuwa hizi zinazo julisha na kusisitiza juu ya kuwa sunna kwa tendo hili na kwamba ni sunna iliyo tiliwa mkazo kulizuru kaburi la Mtume(s.a.w.w) na kuyazuru makaburi ya waja wema kati ya waumi.

Je kauli ya Mtume(s.a.w.w) isemayo: (hakika amenitelekeza)[55] haitujulishi ya kuwa ni sunna iliyo sisitizwa kumzuru? Je kauli yake (s.a.w) isemayo: Mwenye kunizuru atawajibikiwa na shafaa yangu) haijulishi ya kuwa kuna sunna kubwa katika tendo hilo.[56] Je kauli yake(s.a.w.w) isemayo: Yatembeleeni (yazuruni) makaburi kwani yanawakumbusheni akhera)[57] haitujulishi ya kuwa imeamuriwa kuyafanyia ziara, na amri hapa ikiwa haikutujulisha kuwa tendo hilo ni wajibu je kuna shaka yoyote ya kuwa amri hiyo katika hadithi hiyo ni ya sunna?

JAMIIL: Hadithi hizi zimetajwa wapi na katika kitabu gani?

JAWAAD: Vitabu vya hadithi vimejawa na hadithi kama hizi na mfano wa hizi, wewe rejea kwenye vitabu hivyo na usome utaona hadithi nyingi sana.

JAMIIL : Kwa hakika mimi hadi sasa sijaona , wala sijasikia hadithi hata moja kati ya hadithi hizi.

JAWAD: Je umesoma sahihi Bukhariy?[58]

JAMIIL: Kwa bahati mbaya hatuna kitabu hicho?

JAWAD: Je umesoma sahihi Muslim?[59]

JAMIIL: Babu yangu alikuwa nacho lakini alipo fariki baba yangu mdogo akakichukua.

JAWAD : Je umefanikiwa kusoma Sunanu Nasaiy?[60]

JAMIIL : Ni ipi hiyo?

JAWAD : Ni kitabu cha hadithi.

JAMIIL : Hapana ..sijawahi kukiona kitabu hicho.

JAWAD : Sasa ni hadith zipi ulizo zisoma?

JAMIIL : Samahani kwa hakika mimi ni mwanafunzi katika chuo cha udaktari, na bado ninafanya juhudi na kuhudhuria shuleni kwangu ili niweze kufaulu katika masomo yangu, na sina muda wala fursa ya kusoma hadithi pamoja na kuwa ninapenda sana kuzisoma.

JAWAD : Ikiwa hujawahi kusoma hadithi yoyote, na huja angalia kitabu chochote cha hadithi inakuwaje unakuwa na ushupavu na ujasiri wa kupinga kumzuru Mtume(s.a.w.w) na maimam(a.s) , bila kuwa na maarifa yoyote ya hadithi? Je maarifa yako ya kwamba kuzuru makaburi ni shirki hayakuwa ni yenye kujitegemeza kwenye dalili yoyote?

JAMIIL : Kila nililo lisikia kwa baba yangu, babu yangu na marafiki zangu..kuhusiana na zira halikuwa ni jambo jingine, bali ilikuwa ni kupinga na kukemea jambo hilo, na hakuna hata siku moja niliyo sikia hadithi hizi ulizo zitaja na kuzinukuu hapa.

JAWAD : Ni wajibu kwa kila mtu kufanya uchunguzi kuhusu ukweli ili aweze kuufikia ukweli huo na asibakie akishikamana na kauli azisikiazo kwenye mazingira na jamii anayo ishi, huenda wao walikuwa kwenye makosa kwenye itikadi hizo, basi ni wajibu ayafanyie uchunguzi yeye mwenyewe, na yeye mwenyewe afuatilie kwa karibu zaidi ukweli huo na asome vitabu mbali mbali, mpaka afike kwenye hatua ya kuishi kiitikadi na katika matendo yake na kauli zake kama atakavyo Mwenyezi Mungu mtukufu.

JAMIIL : Hivi sasa nimeamini ya kuwa kulitembelea kaburi la Mtume (s.a.w) ni sunna iliyo tiliwa mkazo na iliyo sisitizwa, vile vile kuzuru makaburi ya maimam na makaburi ya waumini na watu wema kati ya waja wa Mwenyezi Mungu.

JAWAD : Nina ombi moja kwako.

JAMIIL : hakuna tatizo sema tu.

JAWAD : Kwa hakika mimi ninasisitiza ombi langu kwako ya kuwa usiwe mtu mjinga mwenye kufuata kila sauti uisikiayo na kila muitaji aitae, na wala usifuate itikadi zilizoko kwenye jamii unayo ishi isipokuwa baada ya kuzifahamu kupitia njia za kielimu na kuzifanyia utafiti, kwani ikiwa utafanya hivyo utakuwa umefaulu.

JAMIIL : Na hili ndilo nilikusudialo kulifanya siku za mbeleni, kwani baada ya kuwa nilikuwa nikiitakidi ya kuwa kuzuru makaburi ni shirki nimefahamu kupitia njia ya Uislaam ya kuwa ni sunna iliyo sisitizwa, na nimefahamu ya kuwa ninacho takiwa kukifanya ni kufanya uchunguzi katika maudhui tofauti. Na kuhusu jambo hili kwanza kabisa nitakwenda kufanya mazungumzo na baba yangu , -kabla ya jambo lolote lile-baba ambae ndie aliekuwa ni sababu pekee ya mimi kuitakidi maudhui haya, huenda nikajaaliwa kumuongoza.

JAWAD : Ninakushukuru.

JAMIIL: Nami ninakushukuru kwa kuniongoa.