ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI 0%

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI Mwandishi:
Kundi: Midahalo na majadiliano kielimu
Kurasa: 16

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

Mwandishi: TIJANI SAMAWI
Kundi:

Kurasa: 16
Matembeleo: 7537
Pakua: 394

Maelezo zaidi:

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI
 • UTANGULIZI

 • DIBAJI

 • QUR'AN KWA UPANDE WA SHIA NA SUNNI

 • MTUME KWA MASUNNI NA MASHIAIMAMIYYAH

 • AQIDA ZA KISHIA NA KISUNNI

 • ITIKADI YA MUNGU KISHIA NA KISUNNI

 • ITIKADI YA UTUME KISHIA NA KISUNNI

 • UIMAMU KISHIA NA KISUNNI

 • MJADALA WA UKHALIFA

 • UFAFANUZI

 • AYA YA KUKAMILISHA DINI

 • MJADALA JUU YA AYA YA KUKAMILISHA DINI

 • UCHAMBUZI WA MADA

 • Kwanza

 • Pili

 • Tatu

 • HUZUNI NA MAJUTO

 • USHAHIDI MWINGINE KUHUSU UONGOZI WA ALI (A.S.)

 • Ushuhuda wa Kwanza:

 • Ushahidi wa Pili:

 • UFAFANUZI JUU YA MASHAURIANO (SHURAA)

 • KHITILAFU INAYOHUSU VIZTIO VIWILI

 • Mtazamo wa Kwanza:

 • Mtazamo wa Pili:

 • Mtazamo wa Tatu:

 • Mtazamo wa Nne:

 • Mtazamo wa Tano:

 • Mtazamo wa Sita:

 • Mtazamo wa Saba:

 • Khitilafu kati ya bibi Aisha na ibn Umar.

 • QADHAA NA QADAR (KWA MASUNNI)

 • ITIKADI YA MASHIA KUHUSU QADHAA NA QADAR

 • UFAFANUZI JUU YA UKHALIFA

 • KHUMS (1/5)

 • TAQ-LIID

 • Mar-hala ya Kwanza:

 • Mar-hala ya Pili:

 • ITIKADIAMBAZO MASUNNI HUWAKEBEHI MASHIA

 • ISMAH

 • IDADI YA MAIMAMU (NI KUMI NA WAWILI)

 • ELIMU YA MAIMAMU

 • AL-BADA'U

 • TAQIYYAH

 • MUT'A (AU NDOA YA MUD A)

 • KAULI INAYOHUSU TAHRIFUL-QUR'AN

 • KUKUSANYA BAINA YA SALA MBILI

 • KUSUJUDU JUU YA UDONGO

 • AR-RAJ-A' (KUREJEA KWENYE UHAI)

 • KUVUKA MIPAKA KATIKA KUWAPENDA MAIMAMU

 • MAHDI ANAYENGOJEWA

 • REJEA ZILIZOTUMIKA

Tafuta ndani ya kitabu
 • Anza
 • Iliyopita
 • 16 /
 • Inayofuata
 • Mwisho
 •  
 • Matembeleo: 7537 / Pakua: 394
Kiwango Kiwango Kiwango
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

Mwandishi:
Swahili
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI
KIMEANDIKWA NA: TIJANI SAMAWI KIMETARJUMIWA NA: MUSABAHA SHABAN UTANGULIZI Na: Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
Kwa Jina la Mwenyezi Muijgu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho Liakuuna Ma'as-Sadiqin kilichoandikwa na Shaikh Muhammad Tijani Samawi wa Tunisia. Ndani ya Kitabu hiki ameelezea mkusanyiko wa itikadi za Kiislamu kwa namna zilivyo ndani ya Qur'an na Sunna Tukufu ya Mtume (s.a.w.w.).

Kitabu hiki ni kama kile cha mwanzo, nacho kimepata umaarufu hasa kutokana na jinsi mwandishi alivyozichambua itikadi hizo kwa mujibu wa mtazamo wa Sunni na Shia, kisha akayabainisha maeneo wanayohitilafiana. Kwa mara nyingine tena mimi binafsi sikusita kumuomba Shaikh Musabah Shaban Mapinda kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake ya lugha ya Kiarabu.

Sababu iliyoifanya Mission yetu isimamie kazi hii ni kama ile ya kwanza, ambayo inatokana na maombi ya Maulamaa wengi katika Afrika Mashariki kututaka tukifasiri kitabu hiki kiingie kwenye lugha ya Kiswahili.

Namshukuru Shaikh Musabah kwa kukubali ombi langu na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja. Nimeiangalia pamoja naye tafsiri hii kwa makini kuhakikisha kuwa maudhui yake ya asili hayakupotoshwa katika lugha ya Kiswahili.

Shaikh Tijani Samawi ameandika vitabu zaidi ya hivi, na. Sheikh wetu Musabah Shaban Mapinda ametafsiri kitabu kingine cha mwandishi huyu kiitwacho Fa'salu Ahlad-Dhikri (Waulizeni wanaofahamu) ambacho tayari kimeshapangwa katika kompyuta. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tena kwani kitabu chetu cha "Hatimaye Nimeongoka" kimependwa mno na wasomaji na hivyo kutupa ari ya kuchapisha hiki ulichonacho mkononi na kitakachofuatia Insha-Allah.

Ushahidi wa kupendwa kwa kitabu hicho ni shukurani na pongezi tunazozipokea toka kwa wasomaji kwa namna mbalimbali ikiwemo kutuandikia barua n.k. Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa mfasiri na kwa wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine katika uchapishaji wa kitabu hiki.

Wa Ma Tawfeeq Ilia Billah
Sayyid Saeed Akhtar Rizvi
Dar -es- Salaam
17th Rabbi-Ul-Awwal, 1422 l(fh June, 2001

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu ENYI MLIOAMINI! MCHENI MWENYEZI MUNGU NA MUWE PAMOJA NA WAKWELI (TAUBAH: 119) Shukurani zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, Mola ambaye ametuboresha kwa kutupa uongofu, usimamizi na akatupa uwezo. Na ndiye Mola mwenye kuwaneemesha waja kwa kila ya kheri na mafanikio ili wapate kuwa waja wema. Yeyote mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu, atamtosheleza na kumlinda kutokana na vitimbi vya mashetani, na yeyote mwenye kuiacha njia yake, basi huyo atakuwa miongoni mwa wenye kufedheheka. Kisha Sala na Salamu zimshukie Mtume aliyetumwa kuwa ni Rehma kwa walimwengu, yeye ndiye mkombozi wa wanyonge na wenye kudhulumiwa, na ni kipenzi cha masikini ambao wamemuamini Mwenyezi Mungu kwa kutamania kuyapata yale aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waja wake wenye utakaso wa moyo.

Kadhalika Sala na Salamu ziwashukie watu wa kizazi chake (Mtume), kizazi chema kilichotakasika (nao ni wale) ambao Mwenyezi Mungu ameinyanyua daraja yao juu ya viumbe wengine ili wapate kuwa kiigizo cha wenye kutambua, na wawe ni nuru ya uongofu na Safina ya uokovu, usia (kuipanda) atakuwa miongoni mwa wenye kuangamia. Kisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie Masahaba wa Mtume waliobarikiwa, ambao walimpa kiapo cha utii wakamsaidia na hawakuwa miongoni mwa waliotengua kiapo (hicho) na waliimarika juu ya usia wake baada yake na hawakubadilisha wala kugeuka na wakawa miongoni mwa wenye kushukuru... (Kadhalika radhi za Mwenyezi Mungu) ziwashukie wale waliowafuata hao kwa wema na wakaenda juu ya mwendo wa uongofu wao, (ziwashukie radhi hizo) wale wafuasi wa mwanzoni na waliokuja mwishoni mpaka siku ya hukumu.

Ewe Mola wangu! nikunjulie kifua changu na uniwepesishie mambo yangu na uufungue mfundo katika ulimi wangu ili maneno yangu yapate kufahamika. Ewe Mola wangu nakuomba uufungue moyo wa kila atakayesoma kitabu changu auone ukweli, na kwa kupitia ukweli huo wewe unawaongoa waja wako wenye utakaso wa moyo.

Amma baad, kwa hakika kitabu changu kiitwacho, "Thummah-Tadaitu" kimepata mapokezi mazuri mbele ya wasomaji watukufu ambao wametoa baadhi ya maoni muhimu kuhusu maudhui mbali mbali zilizomo ndani ya kitabu hicho, na wameomba waongezewe ufafanuzi zaidi kuhusu mambo ambayo Waislamu wengi Masunni na Mashia wametofautiana katika kuyafahamu. Ili kuondoa utatanishi wa jambo hilo kwa yule atakaye uthibitisho na kupata msimamo uliowazi, basi nimetunga kitabu hiki kwa mfumo ule ule nilioutumia katika kitabu kile, ili iwe rahisi kwa mtafiti aliye muadilifu kuufikia ukweli kwa njia zake zilizo bora.

Kwa kuwa mimi niliweza kuufikia ukweli kwa njia ya utafiti na kulinganisha (baina ya hoja za upande huu na upande mwingine), kitabu hiki nimekipa jina la "Maa'Sa'diqin" hali ya kuwa nataraji baraka za Mwenyezi Mungu. Nimefanya hivyo ili kufaidika na kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Enyi mlioamini, mcheni Mwenyezi Mungu na muwe pamoja na wakweli." Je! ni Muislamu gani anayepinga au kutokuwa na haja ya kuwa pamoja na hao wakweli?

Mimi binafsi nimekinaika na ndilo jambo ambalo najaribu kulibainisha kwa wengine kwa kiasi nitakachoweza bila ya kulazimisha maoni yangu tu, bali ni pamoja na kuheshimu kwangu maoni ya wengine. Basi Mweyezi Mungu peke yake ndiye mwenye kuongoa naye ndiye mwenye kuwasimamia watu wema. Kwa hakika wako baadhi ya watu wameipinga anuani ya jina la kitabu (changu) kilichotangulia, "Thummah-Tadaitu" (Hatimaye nimeongoka) kutokana na utata unaoweza kupelekea kufikiri na kujiuliza kwamba, Je, (Waislamu) wengine wako katika upotovu na ni kipi hicho kitakachojulisha juu ya upotovu huo ikiwa hii ndiyo maana iliyokusudiwa?

Na kwa msingi wa upinzani huu, ninajibu kwa ufafanuzi: Kwanza: Ndani ya Qur'an tamko "Dhalalah" (yaani upotovu) limekuja kwa maana ya kusahau. Mwenyezi Mungu Anasema: (Qa'la Il-muha inda Rabbi fikitabin la Yadhillu Rabbi wala yansa). Maana yake: "Akasema elimu yake iko kwa Mola wangu ndani ya kitabu, Mola wangu hasahau wala haghafiliki". (Qur'an, 20:52)
Na amesema tena Mwenyezi Mungu: (Antadhilla ihdaahuma fatudhakkira Ihdaahumal-Ukhra), "Mmoja wao akisahau mwingine amkumbushe". (Qur'an 2:282)
Kama ambavyo pia limekuja ndani ya Qur'an Tukufu tamko la "Dhalalah" likielezea maana ya kutaka uhakika, kuchunguza na kutafiti. Mwenyezi Mungu amesema alipokuwa akimsemesha Mtume wake Mtukufu (s.a.w.) (Wawajadaka dhallan fahada) Qur'an, 93:7. Yaani, Alikukuta ukitafuta ukweli naye akakuongoa kwenye ukweli huo. Ni jambo maarufu katika sera yake Mtume (s.a.w.) kwamba, kabla ya kumshukia wahyi alikuwa akiwahama jamaa zake hapo Makkah ili apate kukaa faragha ndani ya pango la Hiraa kwa siku kadhaa akitafiti juu ya ukweli.

Na miongoni mwa maana kama hii kuna kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo: (Al-Hikmatu dhallatul-Muumin Ayna Mawajadaha akhadhaha): "Hekima ni kitu akitafutacho muumini, basi popote aikutapo na aichukue". Kwa hiyo ile anuani ya jina la kitabu changu cha mwanzo ni katika maana hii.

Pili: Kwa kukadiria (tuseme) kwamba anuani hiyo inayo maana ya upotevu ambao ni kinyume cha uongofu. Uongofu tunaoukusudia ni kwa kiwango cha kifikra kuweza kuipata njia ya Uislamu sahihi unaotuweka kwenye njia iliyonyooka, kama walivyofasiri hivyo baadhi ya wasomaji. Basi na iwe hivyo, nao ni ukweli ambao baadhi ya watu wanaogopa kuukabili kwa moyo thabiti wa kutenda unaokwenda sambamba katika akili na kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema: "Nimeacha miongoni mwenu vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu, vitu ambavyo mkishikamana navyo hamutapotea kamwe baada yangu".

Basi hadithi iko wazi mno katika kuonyesha upotofu wa yeyote asiyeshikamana na viwili hivyo kwa pamoja (yaani kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume). Na kwa hali yoyote ile mimi nimekinaika kuwa nimeongoka kwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani nimeshikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume (s.a.w.). Basi namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuongoa kwenye ukweli huu na kuwa tusingeongoka lau Mwenyezi Mungu asingetuongoa. Bila shaka wamekwisha kutufikia Mitume wa Mola wetu wakiwa na ukweli (tunaowajibika kuufuata).

Hivyo basi kitabu changu cha kwanza na cha pili vimebeba anuani zitokanazo ndani ya Qur'an, nayo Qur'an ndiyo maneno ya kweli mno na ni mazuri mno, na yote niliyoyakusanya ndani ya vitabu hivyo viwili - kama siyo haki tupu basi yako karibu mno nayo - kwani ni katika yale ambayo wameafikiana Waislamu wote Masunni na Mashia na ni katika yale yaliyothibiti kwa pande zote mbili kuwa ni sahihi, basi matokeo ya hayo yamekuwa ni kupatikana kwa vitabu hivi viwili "Thummah-Tadaytu na Liakuna Maas-Sadiqin " yote haya ni kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu.

Namuomba Mwenyezi Mungu auongoe umma wote wa Muhammad (s.a.w.) ili uwe ni umma bora na uongoze ulimwengu wote kwenye nuru na uongofu chini ya bendera ya Imam Mahdi anayengojewa, ambaye babu yake alituahidi - ili aje aujaze ulimwengu uadilifu na usawa baada ya kuwa umejazwa dhulma na ujeuri, na ili nuru ya Mwenyezi Mungu ipate kutimia japokuwa makafiri watachukia.1
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

DIBAJI Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu, Sala na Salamu zimshukie mbora wa mitume bwana wetu na mpenzi wetu Muhammad na pia (Sala na Salamu) ziwashukie watu wa kizazi chake walio wema tena waliotakasika. Amma Baad:

Bila shaka kimsingi dini inategemea itikadi ambazo huwa ni mkusanyiko wa misingi na mategemeo ambayo huyaamini waliyoikubali Dini hii au ile, na misingi hiyo ndiyo ambayo hapana budi imani yao isimame kwayo juu ya dalili madhubuti na hoja iliyo wazi ambayo inakubaliana na akili wanayoiamini watu wote ili itoe fursa ya kuwatosheleza kwa yale inayowaitia.

Japo kuwa hali ni hiyo lakini ziko fikra ambazo ni ngumu kwa ulimwengu kuzifasiri kama ilivyo ugumu kwa akili kuzisadiki kwa mara ya kwanza.

Miongoni mwa hizo kwa mfano, moto kuwa baridi na salama wakati elimu na akili zinakubaliana kwamba moto una joto kali linaloangamiza, au ndege kukatwa katwa na kuwa vipande vipande vilivyotawanyika juu ya mlima kisha vikaitwa na kuja haraka wakati ambapo elimu na akili vinapinga hilo, au kuponywa kipofu na mwenye mbaranga au bubu kwa kiasi cha Nabii Isa kumgusa, bali zaidi ya hapo kama kufufua wafu, wakati ambapo elimu na akili havipati tafsiri ya jambo hili... nayo ni a ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka kwenye mikono ya Mitume wake amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao, na miujiza hiyo inapatikana kwa Waislamu na Mayahudi na Wakristo.


Bila shaka Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiweka miujiza hiyo na mambo yaliyo kinyume na maumbile kwa Manabii wake na Mitume wake (a.s.) ili waja wapate kufahamu kwamba akili zao ni fupi kuweza kufahamu na kudhibiti kila kitu, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwapa elimu isipokuwa kidogo tu, na huenda hilo ni kwa ajili ya manufaa yao na ukamilifu wao unaowahusu.

Kwa hakika watu wengi walikufuru kutokana na neema za Mwenyezi Mungu na wengi wakapinga kuwepo kwake Mwenyezi Mungu, wengi miongoni mwao wakajivuna kwa elimu na akili mpaka wakaviabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu. Hali hii ilitokea pamoja na huo uchache wa elimu na akili fupi, hivyo basi hali ingekuwaje lau Mwenyezi Mungu angewapa elimu ya kila kitu?!

Na kwa sababu ya umuhimu wa aqida na ubora wake katika imani ya Muislamu, bila shaka kitabu changu hiki kimeleta mkusanyiko wa itikadi za Kiislamu ambazo zimekuja ndani ya Qur'an Tukufu na Sunna Tukufu ya Mtume na ni itikadi ambazo zimekuwa ndiyo mahala pa tofauti za madhehebu ya Kiislamu. Basi mimi nimetenga mlango maalum unaohusu itikadi za Kisunni na Kishia ndani ya Qur'an na Sunna ya Mtume, kisha nimefuatisha baada ya hapo mas-ala mengine ambayo wametofautiana ndani yake na baadhi yao kuwafedhehesha baadhi nyingine bila ya sababu ya halali.


Nimefanya hivyo nikilenga kubainisha kile ambacho mimi nimekiona kuwa ndiyo haki hali ya kuwa natamani kumsaidia yeyote anayetaka kuutafuta ukweli, pia nikiwa nataraji kutoa mchango kwa hilo katika kusimamisha umoja wa Kiislamu juu ya msingi imara kifikra. Namuomba Mwenyezi Mungu atuwafikishe sote kwa yale ayapendayo na kuyaridhia na aiunganishe kalima ya Waislamu juu ya ukweli bila shaka yeye ndiye mwenye nguvu mwenye uwezo.

QUR'AN KWA UPANDE WA SHIA NA SUNNI QUR'AN (INAVYOTAMBULIKANA) KWA MASUNNI NA MASHIA IMAMIYYAH Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyoteremshwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), nayo hiyo Qur'an haiwezi kutanguliwa (na sheria yeyote) hapo kabla na baadaye nayo ndiyo rejea kuu kwa Waislamu katika hukmu zao na ibada zao na itikadi zao, yeyote mwenye kuitilia shaka au akaitweza basi huyo huwa kajitoa nje ya dhamana ya Uislamu. Kwa hiyo Waislamu wote wamekubaliana waitukuze na kuiheshimu na kufanya ibada (zao) kwa mujibu wa (mafunzo) yaliyokuja ndani yake.

Lakini Waislamu wametofautiana katika kuifasiri na kuifafanua. Rejea ya Mashia katika tafsiri na taawili za Qur'an hurudi kwa Mtume (s.a.w.) na ufafanuzi uliotolewa na Maimamu watokanao na nyumba ya Mtume (s.a.w.). Ama rejea ya Masunni,wao hurudi kwenye hadithi za Mtume (s.a.w.) pia, lakini Masunni huwategemea Masahaba bila ya kuchambua au Maimamu wanne wenye Madhehebu mashuhuri, (wao huwategemea hao) katika kunakili hadithi, ufafanuzi wake na tafsiri yake.

Na kutokana na hali hiyo ndipo ilipoanzia tofauti katika mas-ala mengi ya Kiislamu hasa yale ya Kifiq-hi, na ilipokuwa kuna tofauti iliyowazi baina ya Madhehebu manne ya Kisunni, hivyo siyo ajabu tofauti hiyo kuwa kubwa zaidi baina ya Masunni na madhehebu yanayofuata mafunzo yatokanayo na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.).

Kama nilivyoeleza mwanzoni mwa kitabu, bila shaka mimi sitaeleza baadhi ya mifano kwa nia ya kufupisha maelezo, na ni wajibu wa yeyote yule atakaye kutafiti na kupata ziada apige mbizi chini ya bahari (atafiti kwa undani zaidi) ili aweze kutoa kile akiwezacho miongoni mwa ukweli uliomo ndani ya johari zilizojificha!!

Masunni na Mashia wote wameafikiana juu ya kauli isemayo kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliwabainishia Waislamu hukmu zote za Qur'an na alizitafsiri aya zake zote, lakini wametofautiana juu ya nani ambaye inapasa kumrejea baada ya kufariki Mtume (s.a.w.) ili kufahamu ubainisho huo aliobainisha Mtume na tafsiri aliyotafsiri.

Masunni wao wamekwenda upande wa kuwategemea Masahaba bila kuchambua (ni Sahaba gani afaaye na yupi hafai kwao wote ni sawa tu) na baada ya Masahaba Masunni wanawategemea Maimamu wanne na wanachuoni wa umma wa Kiislamu. Ama Mashia, wao wamesema kwamba: "Maimamu watokanao na nyumba ya Mtume (s.a.w.) ndiyo wanaostahiki kurejewa na pia Masahaba wateule, kwani Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) ndiyo wale wenye kumbukumbu ambazo Mwenyezi Mungu ametuamuru tuwarejee pale aliposema:

"Waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui" (Qur'an, 16:43)
Na ndiyo wale ambao Mwenyezi Mungu amewateua na akawarithisha elimu ya kitabu (yaani Qur'an) pale aliposema:
"Kisha tumewarithisha kitabu wale ambao tumewateua miongoni mwa waja wetu". (Qur'an, 35:32)
Na kwa ajili ya yote hayo Mtume (s.a.w.) amewafanya wao kuwa mfano wa Qur'an na ni kizito cha pili ambacho amewaamuru Waislamu kushikamana nacho pale aliposema: "Nimeacha kwenu vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu watu wa nyumba yangu, vitu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu." Taz: Sahih Tirmidhi Juz. 2 uk. 329, pia Annasai na Imam Ahmad.


Na katika tamko la Sahihi Muslim amesema: "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu wa nyumba yangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu" alisema hivyo mara tatu.
Taz: Sahih Muslim Juz. 2 uk. 362. Mlango wa Fadhail za Ali Bin Abi Talib Na ni jambo linalofahamika mno kwamba watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) wao walikuwa ni wajuzi na wachamungu na ni wabora mno kuliko watu wengine.

Amesema Farazdaq kuhusu watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.): "Ikiwa watahesabiwa wachamungu, basi wao watakuwa ndiyo viongozi wa wachamungu hao, au pakisemwa ni kinanani walio bora kuliko watu wa ardhini? Patasemwa ni wao". Hapa ninaleta mfano mmoja ili kukumbusha mtiririko wa maungamano yaliyopo baina ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) na Qur'an Tukufu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Basi ninaapa kwa maanguko ya nyota, na hakika hicho bila shaka ni kiapo kikubwa, laiti mngelijua, hakika hii (mnayosomewa) ni Qur'an Tukufu (yenye heshima kubwa) imetolewa ndani ya kitabu kilichohifadhiwa kweli kweli hawawezi kukifahamu (vilivyo maana yake) ila wale waliotakaswa" (Qur. 56:75-79)

Aya hizi zinaashiria bila ya kificho ya kwamba, watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) wakiongozwa na yeye mwenyewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) wao ndiyo wale ambao wanaozifahamu maana za Qur'an zilizo ngumu kufahamika (kwa wengine), kwani lau sisi tutaangalia kwa makini kuhusu kiapo alichokiapia Mwenyezi Mungu Mtukufu, tutayakuta mambo yafuatayo:

Ikiwa Mwenyezi Mungu huapia Alasiri na Kalamu na Mti wa Tini na Mzeituni, basi utukufu wa kuapia maanguko ya nyota uko wazi kutokana na yale yanayoshikamana juu yake miongoni mwa siri na athari zipatikanazo juu ya ulimwengu kwa amri yake Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na tunaona" utukufu wa kiapo ndani ya mfumo wa Nafyi na Ithba't na baada ya kiapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweka mkazo ya kwamba hii ni Qur'an Tukufu iliyotolewa ndani ya kitabu kilichohifadhiwa kweli kweli, kisha Mwenyezi Mungu anasema, "Hawawezi kuifahamu vilivyo maana yake isipokuwa wale waliotakaswa." Na hii "La" iliyopo hapa (La-Yamassuhu) ni yakukanusha, na hii (Yamassuhu) inamaanisha kuifahamu Qur'an, na makusudio yake siyo kugusa kwa mkono kwani kuna tofauti baina ya tamko la "Al-Lamsu"na "Al-Massu".

Mwenyezi Mungu Amesema:
"Hakika wale wanaomuogopa Mwenyezi Mungu shetani anapowatia wasi wasi, hukumbuka na mara huiona haki (na kuifuata)". (Qur'an, 7:201)
Na amesema tena Mwenyezi Mungu:
"Wale wanaokula riba hawasimami ila ni kama asimamavyo yule ambaye shetani amemvuruga kwa kumzuga". (Qur'an, 2:275) Basi tamko "Al-massu" linalopatikana hapa linafungamana na akili na kufahamu na siyo kushika kwa mkono, itakuwaje basi Mwenyezi Mungu Mtukufu aape kwamba Qur'an haiguswi kwa mkono isipokuwa na yule aliyejitwahirisha, na hali ya kuwa historia inatusimulia kwamba baadhi ya mijitu mijeuri iliichezea na kuichana na pia tumeshuhudia Waisraeli wakiikanyaga kwa miguu yao (Mwenyezi Mungu atulinde na shari zao). Pia tumewaona wanaichoma moto pale walipoivamia Beirut katika vurugu zao mbaya walizozifanya, na Televisheni ziliinasa hali hiyo mbaya ya kutisha.

Kwa hiyo maana ya kauli hiyo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuwa: "Hawezi kufahamu maana za ndani za Qur'an ila wale wateule miongoni mwa waja wake ambao amewateua na akawatakasa sana." Na hilo tamko la "Mutahharu'n" liliomo ndani ya aya hii ni jina la kilichotendewa yaani kule kutahirika kumetuka juu yao. Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu amekuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na kukutakaseni sana sana". (Qur'an, 33:33)

Basi kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema, "La Yamassuhu Illal-Mutahharun " maana yake ni kuwa, "Hawezi kufahamu uhakika wa Qur'an isipokuwa Mtume (s.a.w.) na watu wa nyumba yake (a.s.) na kwa ajili hiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema kuwahusu Ahlul-Bait kama ifuatavyo. "Nyota ni amani kwa watu wa ardhini (zinawaongoza) wasiangamie (baharini), na watu wa nyumba yangu ni amani kwa umma wangu (wanawaongoza) wasihitilafiane, basi ikiwa kabila fulani miongoni mwa Waarabu litakwenda kinyume (na kizazi changu), basi watahitilafiana na watakuwa kundi la ibilisi".

Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 149, imepokewa toka kwa Ibn Abbas na amesema kuwa Isnad ya Hadithi hii ni Sahih. Kwa hiyo mwendo waufuatao Mashia kuhusu tafsiri na taawili ya Qur'an unategemea Qur'an Tukufu na hadithi za Mtume (s.a.w.) ambazo zimepokelewa pia kwa Masunni kama tulivyokuta.

MTUME KWA MASUNNI NA MASHIAIMAMIYYAH MTUME (INAVYOTAMBULIKANA) KWA MASUNNI NA MASHIAIMAMIYYAH
Sunna ni kila kile alichokisema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), au alichokitenda au kukithibitisha. Nayo Sunna ndiyo rejea ya pili baada ya Qur'an Tukufu kwa Masunni na Mashia katika hukmu zao na ibada zao na itikadi zao. Masunni huongeza kwenye Sunna ya Mtume, Sunna za Makhalifa wanne ambao ni Abubakr, Umar, Uthman na Ali, na hilo wanalifanya kutokana na hadithi wanayoisimulia isemayo kuwa:

"Shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za Makhalifa viongozi walioongoka baada yangu zing'ang'anie kwa magego". Na hilo ni dalili ya wazi kutokana na kufuata kwao Sunna ya Ummar Bin Khattab inayohusu sala ya tarawehe ambayo Mtume (s.a.w.) aliikataza (isisaliwe jamaa). Na baadhi ya Masunni huongeza kwenye Sunna ya Mtume, Sunna ya Masahaba wote (yaani Sahaba yeyote yule awaye) na hulifanya hilo kutokana na hadithi yao isemayo:
"Masahaba zangu ni kama nyota, yeyote mutakayemfuata mtaongoka". Vilevile kuna hadithi nyingine isemayo: "Masahaba wangu ni amani ya umma wangu".

Taz: Sahih Muslim Kitabu Fadhailus-Sahabah na Musnad Ahmad bin HanbalJuz. 4 uk. 398.
Amma ile hadithi ya sahaba zangu ni kama nyota, bila shaka haikubaliani na akili, mantiq na ukweli wa kielimu, kwani Waarabu walikuwa hawaongoki katika safari zao za jangwani kwa kiasi cha kufuata nyota yoyote ile miongoni mwa nyota bali walikuwa wakiongoka kwa kufuata nyota maalum zinazotambulikana majina yake kuhusu safari zao.

Kadhalika hadithi hii haiungwi mkono na matukio halisi ambayo yalidhihirika kutoka kwa baadhi ya Masahaba baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), kwani wako miongoni mwa Masahaba walioritadi, kama ambavyo Masahaba walihitilafiana katika mambo mengi yaliyosababisha kushutumiana wao kwa wao na kulaaniana wao kwa wao na kuuwana wao kwa wao. Kadhalika kuna baadhi ya Masahaba waliadhibiwa kwa makosa ya kunywa pombe, kuzini, wizi na mengineyo. Basi ni vipi mtu mwenye akili ataikubali hadithi ambayo inaamuru kuwafuata watu kama hawa? Na ni vipi mtu ataongoka kwa kumfuata Muawiyah aliyetoka dhidi ya Imam wa zama zake pale alipoamua kumpiga Imam Ali (a.s.) na hali mtu huyo anatambua kwamba Mtume (s.a.w.) alimuita Muawiyah kuwa ni kiongozi wa kundi lenye kuasi.

Na ni vipi mtu atakuwa ameongoka kwa kumfuata Amr bin Al-A's, Mughira bin Shuubah na Bisr bin Ar-Taah. Watu hawa waliwaua raia bila makosa ili tu wauimarishe ufalme wa Banu Umayyah. Nawe Ewe msomaji mwenye utambuzi utapoisoma hadithi isemayo, "Masahaba wangu ni kama nyota" itakubainikia kwamba hadithi hiyo ni ya kuzushwa kwani inaelekezwa kwa Masahaba wenyewe, basi ni vipi Mtume (s.a.w.) atasema kuwaambia hao hao Masahaba "Enyi Sahaba zangu wafuateni Masahaba zangu"? Ama hadithi ya kusema, "Enyi Sahaba zangu shikamaneni na Maimamu watokanao na watu wa nyumba yangu, wao watakuongozeni baada yangu" hadithi hii iko karibu mno na ukweli kwani inao ushahidi mwingi unaoungwa mkono na Sunna ya Mtume (s.a.w.).

Nao Mashia Ithna-Asheriyah wanasema kwamba makusudio ya hadithi isemayo kuwa: "Shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za Makhalifa viongozi waliongoka baada yangu" Makhalifa hao ni Maimamu kumi na wawili miongoni mwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.), wao ndiyo wale ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ameuwajibishia umma wake kushikamana nao na kuwafuata kama wanavyoshikamana na kukifuata kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Taz: 1. Sahih TirmidhiJuz. 5 uk. 328
2. Sahih Muslim Juz. 2 uk. 362.
3. Khasaisun-Nasai
4. Kanzul-Ummal Juz. 1 uk. 44.
5. Musnad Imam Ahmad bin Hanbal Juz. 5 uk 289.
6. Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 148.
7. As-Sawaiqul-Muhriqah ya ibn Hajar uk. 48.
8. At-Tabaqatul-Kubra ya ibn Saad Juz. 2 uk. 194.
9. At-Tabrani Juz. 1 uk. 131.

Na kwa kuwa nilikuwa nimeapa kwamba sitatoa dalili isipokuwa zile ambazo Mashia huzitolea ushahidi kutoka ndani ya vitabu vya Masunni, basi bila shaka nitatosheka kwa hoja hiyo, lakini vinginevyo ndani ya vitabu vya Kishia kuna hoja zaidi ya hizo tena kwa maelezo yaliyo bayana zaidi. Natoa mfano mmoja tu wa hoja hizo; As-Saduq amethibitisha ndani ya Ikmal kwa sanad inayoishia kwa Imam As-Sadiq naye amepokea toka kwa baba yake ambaye naye kapokea toka kwa babu yake amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema, Maimamu baada yangu ni kumi na mbili, wa kwanza wao ni Ali na wa mwisho wao ni "Al-Qaim" (Al-Mahdi) wao ndiyo makhalifa wangu na ndiyo mawasii wangu". Ni lazima ifahamike kwamba, Mashia hawasemi kuwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) wanayo haki ya kuweka sheria kwa maana ya kwamba sunna yao iwe ni ijtihadi itokanayo na wao, bali wanasema kwamba hukmu zao zote zinatokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu alimfundisha Ali, na Ali naye akawafundisha wanawe, na hiyo ni elimu ambayo wanarithiana.Mashia wanazo dalili nyingi walizozinakili kutoka kwa Ahlul Sunna wal jamaah ndani ya Sihah, Masnad na vitabu vya historia juu ya jambo hili.

Swali ambalo siku zote linabakia, Je, ni kwa nini Masunni hawakuyatumia yaliyomo ndani ya hadithi hizi ambazo na kwao pia ni Sahihi? Kisha baada ya hayo, Mashia na Masunni wanahitilafiana kuhusu tafsiri ya hadithi zilizothibiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kama ulivyotangulia ufafanuzi wake katika maelezo juu ya kuhitilafiana kwao katika tafsiri ya Qur'an. Wanahitilafiana kuhusu maana ya Khulafaur Rashidun ambayo imekuja ndani ya hadithi yake Mtume (s.a.w.) na pande zote mbili zinakubaliana juu ya usahihi wa hadithi hiyo, lakini Masunni huifasiri kwamba hao ni Makhalifa wanne ambao walikikalia cheo cha Ukhalifa baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, nao Mashia wanaifasiri maana ya Khulafaur-Rashidun kuwa ni Makhalifa kumi na wawili nao ni Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.).

Kwa hali hii basi tunaiona tofauti na hitilafu imeenea katika kitu ambacho kinafungamana na watu ambao Qur'an imewatakasa na Mtume naye ameamuru kuwafuata. Mfano wa jambo hilo ni ile kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema:
"Wanachuoni wa umma wangu ni bora kuliko Manabii wa Bani Israil" au "Wanachuoni ni warithi wa Manabii".
Taz: Sahih Bukhar Juz. 1 Kitabul-Ilmi, na Sahihi Tirmidhi, Kitabul-Ilmi pia. Masunni wao huieneza hadithi hii kwa wanachuoni wote wa umma, wakati ambapo Mashia Ithna-asheriyyah wao huihusisha kwa Maimamu kumi na wawili tu. Kwa ajili hiyo ndiyo maana wao huwaboresha Maimamu hao juu ya Manabii isipokuwa wale Ulul-Azm miongoni mwa Mitume.

Na ukweli ulivyo ni kwamba akili inaelekea kukubaliana na uhusishaji huu. Kwanza: Qur'an imewarithisha elimu ya kitabu wale ambao Mwenyezi Mungu amewateua miongoni mwa waja wake, hivyo huko ni kuhusisha (kitu kwa watu maalum) kama ambavyo Mtume wa Mwenyezi Mungu amewahusisha watu wa nyumba yake kwa mambo mengi ambayo hakuwashirikisha ndani ya mambo hayo mtu yeyote mpaka akawaita wao kuwa ni Merikebu ya uokovu na akawaita kuwa ni Maimamu waongofu, ni taa za kuondosha kiza na ni kizoto cha pili ambacho kinawalinda (Waislamu) wasipotee.

Hivyo basi, inadhihiri kutokana na hali hii kwamba kauli ya Masunni inapingana na kuhusisha ambako Qur'an imekuthibitisha na pia sunna ya Mtume, nayo akili haikubaliani na kauli hiyo kutokana na utata uliomo na kutokufahamika kwa wanachuoni hao ambao Mwenyezi Mungu amewaondoshea uchafu na kuwatakasa, pia Masunni kutokuwapambanua wanachuoni ambao watawala wa Kibanu Umayya na Banu Abbas walilazimisha wafuatwe. Kuna tofauti kubwa mno baina ya hao wanachuoni (waliowekwa na watawala) na baina ya Maimamu kutoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.), Maimamu ambao historia haielezi habari za mwalimu yeyote ambaye wamesoma kwake isipokuwa wao mtoto hupata kwa baba yake. Pamoja na hayo wanachuoni wa Kisunni katika elimu zao wamepokea riwaya nyingi za ajabu na hasa kwa Imam Al-Baqir na Imam As-Sadiq na Imam Arridha ambaye kwa elimu yake aliwanyamazisha Maqadhi arobaini waliokusanywa kwake na Maamun, hali ya kuwa Imam Ridha akiwa bado mtoto mdogo. Taz:Al-Iqdul-Farid cha ibn Abd Rabih-Al-Fusul-Muhimmah cha ibns-Sabbagh Al-Maliki Juz. uk. 42.

Na miongoni mwa mambo yanayotia nguvu kuwapambanua watu wa nyumba ya Mtume na watu wengine ni ile hali ya kutofautiana Maimam wa Madhehebu manne ya Kisunni katika Mas-ala mengi ya Kifiqhi wakati ambapo Maimamu kumi na wawili katika Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) hawatofautiani hata katika suala moja. Pili: Lau tutaichukua kauli ya Masunni katika kuenea kwa aya hizi na hadithi hizi kwa wanachuoni wote wa umma huu, basi ingewajibika kuwepo maoni na madhehebu mengi kila zama zinavyopita na kungekuwa na maelfu ya madhehebu. Na huenda wanachuoni wa Kisunni walizindukana mapema kutokana na ubovu wa rai hii na kutenguka kwa umoja wakiitikadi, basi haraka wakafunga mlango wa ijtihad tangu hapo zamani za kale.

Amma kauli ya Mashia, inaita kwenye umoja na mshikamano juu ya Maimamu wanaotambulikana, ambao Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamewahusisha kwa maarifa yote ambayo Waislamu wanayahitajia katika nyakati zote.Hivyo basi haiwezekani kwa mzushi yeyote kuzua uongo dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mturne na wala hawezi kuzua madhehebu yatakayowalazimisha watu kuyafuata.

Hivyo basi tofauti yao (Masunni na Mashia) kuhusu mas-ala haya ni kama ilivyo tofauti baina yao juu ya Mahdi ambaye pande zote mbili zinamuamini, lakini Mahdi kwa Mashia anafahamika na kutambulikana (wazazi wake) baba yake na babu yake, na kwa Masunni mpaka sasa hajulikani na (wanasema) atazaliwa zama za mwishoni, na ndiyo maana utaona wengi miongoni mwao hudai kuwa wao ndiye yule Mahdi (aliyeahidiwa) . Nami binafsi(nilipokutana na) Sheikh Ismail ambaye ni kiongozi wa Tariqa ya Madaniyyah aliniambia kwamba yeye ndiye yule Mahdi anayengojewa, na aliyasema madai hayo mbele ya rafiki yangu ambaye alikuwa miongoni mwa wafuasi wake lakini(rafiki yangu huyo) baadaye alizindukana.

Ama kwa Mashia wao wanasema, haiwezekani kabisa kwa mtoto atakayezaliwa kwao wao kudai jambo hilo hata kama kuna mtu atamuita mwanawe jina la Mahdi, kwani kufanya hivyo itakuwa ni kwa ajili ya kutabaruku tu kwa jina hilo la Imam wa zama hizi, na ni kama ambavyo mmoja wetu awezavyo kumwita mwanawe jina la Muhammad au Ali kwani kwa Mashia kudhihiri kwa Mahdi ni jambo ambalo kwa dhati yake ni muujiza kwa kuwa Mahdi alizaliwa tangu karne kumi na mbili zilizopita na akawa katika ghaibah. Kisha baada ya yote haya huenda Masunni wakatofautiana juu ya maana ya hadithi sahihi iliyothibiti katika pande zote mbili hata kama hadithi hiyo haifungamani na watu, na kuhusu hilo ni mfano wa hadithi isemayo: "Ikhtilafu katika Umma wangu ni Rehma" hadithi ambayo Masunni wanaifasiri kwamba ikhtilafu za hukmu za kifiqhi katika jambo moja ni rehma kwa Muislamu ambaye anaweza kuchagua ni hukmu ipi inayomnasibu na kukubaliana na ufumbuzi anaouridhia, basi kufanya hivyo ni rehma kwake. Kwa mfano Imam Malik atakuwa ni mgumu katika mas-ala fulani, basi Muislamu anaweza kumfuata Abu Hanifah ambaye amerahisisha hukmu katika jambo hilo.


Ama kwa Mashia, wao wanaifasiri hadithi hiyo kwa maana isiyokuwa hiyo na wanasimulia kwamba, Imam Jaafar As-Sadiq (a.s.) alipoulizwa juu ya hadithi hii isemayo "Ikhtilafu katika umma wangu ni Rehma" yeye alisema, "Amenena kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu", basi muulizaji akasema, "Ikiwa ikhtilafu yao ni Rehma basi mshikamano wao ni balaa"!! Imam As-Sadiq akasema, "Sivyo ulivyofahamu wewe na wanavyofahamu wengine, bali Mtume alikusudia ikhtilifu ya baadhi yao kwa baadhi nyingine yaani baadhi yao kusafiri kwenda kwa baadhi nyingine na kwenda kwa mwanachuoni yule na kumkusudia kwa ajili ya kusoma, na hapo Imam akatolea ushahidi kwa kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Litoke kundi katika kila taifa miongoni mwao ili wakajifunze dini na kisha waje kuwaonya wenzao watakaporudi ili wapate kujihadharisha" (Qur'an, 9:122).

Kisha aliongeza akasema: "Ikiwa watahitilafiana katika, dini basi watakuwa ni kundi la ibilisi". Na hii tafsiri kama tuionavyo ni tafsiri inayokinaisha na kuita kwenye umoja wa itikadi na siyo kuhitilafiana ndani yake. Nayo ni kama tunavyoona tafsiri inayokinaisha ni kwa sababu inaita kwenye umoja wa kiitikadi na siyo mfarakano.[1] Kisha hadithi hii kwa maf-humu ya Kisunni haikubaliki, kwani inapelekea kuleta mgawanyiko na kuhitilafiana, maoni kuwa mengi, madhehebu nayo kuwa mengi na yote haya yanapingana na Qur'an Tukufu ambayo inatuita kwenye umoja na mshikamano juu ya kitu kimoja.

Mwenyezi Mimgu Mtukufu anasema:
"Na kwa yakini huu umma wenu ni umma mmoja na mimi ni Mola wenu, basi niogopeni". (Qur'an, 23:52)
Na anasema tena: "Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala musitengane" (Qur'an, 3:103)
Na anasema tena: "Na wala musizozane mutashindwa na nguvu zenu zitapotea". (Qur'an, 8:46)
Basi ni kuzozana kupi na kutengana kwa aina gani kukubwa kuliko umma mmoja kugawanyika kwenye madhehebu na vikundi vinavyotofautiana baadhi hii na baadhi nyingine na upande huu kuudharau upande ule bali zaidi ya hivyo ni kukufurishana kwa baadhi hii kuikufiirisha baadhi ile kiasi cha upande fulani kuhalalisha damu ya upande mwingine? Na haya yanatokea kwa vitendo siku zote na historia ndiyo shahidi mkubwa wa hayo, mambo ambayo Mwenyezi Mungu alikwisha kutuonya kutokana na matokeo yake mabaya ambayo umma wetu utayafikia iwapo utafarakana akasema:
"Musiwe kama wale waliofarakana na kuhitilafiana baada ya kuwafikia hoja zilizowazi". (Qur'an, 3:105)
"Hakika wale waliofarikisha dini yao na wakawa makundi makundi, huna uhusiano nao wowote ule". (Qur'an, 6:159)
"Na wala musiwe miongoni mwa washirikina, katika wale ambao waliitenga dini yao na wakawa makundi makundi kila kikundi kinafurahia kilicho nacho". (30:31-32)


Na hapa inapendeza kuashiria kwamba maana ya neno, "Shiyaan" halina uhusiano na "As-shiah" (au Shia) kama ambavyo baadhi ya watu wa kawaida wanavyo dhania hasa pale aliponijia mtu fulani akinipa nasaha juu ya madai yake akasema: "Ndugu yangu nakuapia Mwenyezi Mungu wachana na Ushia kwani Mwenyezi Mungu anaukemea na Mtume wake naye ametutahadharisha tusiwe miongoni mwao." Mimi nikasema, "Ameukemea na kututahadharisha namna gani"? Akasema: "Hakika wale walioifarikisha dini yao na wakawa makundi makundi (Shiyaan) huna nao uhusiano wowote". Mimi nilijaribu kumkinaisha kwamba "Shiyaan" maana yake ni makundi na wala hakuna uhusiano na "Shia", lakini Bwana yule inasikitisha kwamba hakukinaika kwani kiongozi wake ambaye ni Imam wa msikiti ndivyo alivyomfundisha na akamtahadharisha dhidi ya Mashia, basi hawezi kukubali isipokuwa fikra hiyo.

Narejea kwenye maudhui na ninasema kwamba mimi nilikuwa nikichanganyikiwa kabla sijafahamu kila nisomapo hadithi ya "Ikhtilafu katika umma wangu ni Rehma" na nilikuwa nailinganisha na hadithi isemayo:
"Watafarikiana umma wangu makundi sabini na mbili na yote yataingia motoni isipokuwa kundi moja." Basi nilikuwa najiuliza itakuwaje ikhtilafu ya umma kuwa rehma wakati huo huo ni jambo linalowajibisha kuingia motoni? Na baada ya kuwa nimeisoma tafsiri ya Imam Jafaar As-Sadiq (a.s.) inayohusu hadithi hii, basi mushkeli wangu uliondoka na wao ndiyo hasa Maimamu wa uongofu na ndiyo taa zinazoondosha kiza , wao ndiyo wenye haki ya kuifasiri Qur'ani na sunna ya Mtume, na ni sawa kabisa kwa Mtume (s.a.w.) aseme kuhusu haki yao Maimamu hao wa nyumba yake kama ifuatavyo:- "Mfano wa watu wa nyumba yangu kwenu ninyi ni kama Safina ya Nuhu, yeyote mwenye kupanda Safina hiyo ataokoka na atakayeikhalifu (akakosa kupanda)atazama, musiwatangulie mutaangamia na wala musiwakhalifu mutaangamia na wala musiwafundishe kwani wao ni wajuzi mno kuliko ninyi".

Taz: 1). As-Sawaiqul-Muhriqah ya ibn Hajar uk. 136
na uk. 227.
2). Al-Jamius-Saghir ya Suyut Juz. 2 uk. 132. 3). Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 3 uk. 17 na Juz. 4 uk.
4). Hil-Yatul-Auliyaa Juz. 4 uk. 306. 5). Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 151. 6). Al-Muujamus-Saghir ya TabraniJuz.2 uk. 22. Na ilistahiki kabisa kwa Imam Ali (a.s.) aseme kama ifuatavyo:"Waangalieni watu wa nyumba ya Mtume wenu, shikamaneni na kizazi chao na mufuate nyayo zao, hawatakutoeni kwenye uongofu na hawatakurudisheni kwenye maangamivu, basi wakitua nanyi tuweni, wakinyanyuka nanyi nyanyukeni. Na wala musiwatangulie mutaangamia na musiwaache mutaangamia." Taz: Nahjul-Balagha ya Imam Ali Juz. 2 uk. 190.

Na amesema tena Imam Ali (a.s.) katika khutba yake nyingine akitambulisha daraja ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.): "Wao ndiyo uhai wa elimu na wao ndiyo kifo cha ujinga, upole wao utakuelezeni kiwango cha elimu yao, na dhahiri yao itakuelezeni undani wao, na ukimya wao utakuelezeni hekima ya mantiq yao, hawaendi kinyume na haki na wala hawatofautiani ndani yake, wao ndiyo nguzo za Uislamu na ndiyo tegemeo la umoja. Kwao wao haki ilirejea mahala pake na batili ikaondoka mahala ilipokuwa imesimama na ulimi wake ukakatika pale ulipootea, wameizingatia haki kwa mazingatio ya kuhifadhi na siyo mazingatio ya kusikia na kueleza kwani waelezaji wa elimu ni wengi na wanaohifadhi ni wachache." Taz: Nahjul-Balagha ya Imam Ali Juz. 3 uk. 439.

Naam, bila shaka Imam Ali amesema kweli kwa hayo aliyoyabainisha kwani yeye ndiye mlango wa mji wa elimu, kwa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya yule aliyeifahamu dini kwa akili ya mazmgatio na kuihifadhi na yule aliyeifahamu dini kwa akili ya kusikia na kueleza tu. Na wasikiao na kueleza wako wengi, kwani ilikuwaje idadi ya Masahaba wengi waliokuwa wakikaa na Mtume (s.a.w.) na kusikiliza hadithi nyingi na wakizinakili bila kufahamu wala kujua? Hivyo basi maana ya hadithi hubadilika na huenda ikapelekea kinyume cha makusudio ya Mtume (s.a.w.), na huenda baadhi ya nyakati ikapelekea kwenye kufru kutokana na ugumu wa Masahaba kuelewa maana halisi ya hadithi hizo.


Mfano wa jambo hili ni ile riwaya aliyoieleza Abuhurairah kwamba: "Mwenyezi Mungu amemuumba Adam kwa Sura yake". Lakini Imam Jaafar As-Sadiq (a.s.) alifafanua jambo hilo akasema, "Hakika Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.) aliwasikia watu wawili wakitukanana, basi mmoja wao akamwambia mwenziwe, Mwenyezi Mungu na auharibu uso wako na uso wa yeyote afananaye na wewe, hapo ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu amemuumba Adam kwa sura yake", yaani wewe kwa tusi lako kumtukana afananaye na huyu hakika umemtukana Adam kwani yeye anafanana naye".

Amma wale wanaoizingatia elimu na kuihifadhi ni wachache mno, na huenda mtu akamaliza umri wake katika kuitafuta elimu na asipate isipokuwa kidogo, na huenda akajihusisha na mlango fulani miongoni mwa milango ya elimu au fani fulani miongoni mwa fani mbali mbali za elimu na asiweze kuidhibiti milango yote.

Lakini jambo linalofahamika ni kwamba Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) walikuwa ni wajuzi wa elimu nyingi za aina mbali mbali, na hili limethibitishwa na Imam Ali kama wanavyolishuhudia wanahistoria. Kadhalika Imam Muhammad Al-Baqir na Jaafar As-Sadiq ambaye maelfu ya masheikh wamesoma kwake elimu mbali mbali na maarifa mengi katika falsafa, utibabu, kemia na elimu za maumbile na nyinginezo nyingi.2
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

AQIDA ZA KISHIA NA KISUNNI Miongoni mwa mambo yaliyonizidishia yakini kwamba Mashia Imamiyyah ndiyo lile kundi lenye kuokoka, ni itikadi zao bora ambazo ni nyepesi kukubalika kwa kila mwenye akili yenye hekima na hisia iliyo salama. Kwa Mashia tunakuta kila mas-ala miongoni mwa mas-ala na kila itikadi miongoni mwa itikadi inayo tafsiri inayotosheleza toka kwa mmoja wa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.), kitu ambacho huenda tusikipatie ufumbuzi kwa Masunni na kwa vikundi vingine (vya Kiislamu). Nitazifuatilia katika mlango huu baadhi ya itikadi zilizo muhimu kwa pande zote mbili (Shia na Sunni), na nitajaribu kuonesha yale ambayo mimi nimeyakinai, na nitamuachia msomaji uhuru wa kufikiri na kuchagua na kukosoa.

Ninakumbusha tu kwamba, itikadi ya msingi kwa Waislamu wote ni itikadi moja ambayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, Malaika wake, vitabu vyake na Mitume wake. Waislamu hawamtengi yeyote miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu kama ambavyo wanaafikiana kwamba moto ni kweli (kuwa upo) na pepo ni kweli (ipo) na kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini na kuwakusanya siku ya hesabu.

Kama ambavyo wanaafikiana juu ya Qur'an na wanaamini kwamba Mtume wao Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kibla chao ni kimoja, lakini hitilafu ilitokea katika maf-humu ya itikadi hizi na hapo ndipo pakawa mahala pa malumbano na wakawa wana maoni mbali mbali na madhehebu mengi.


ITIKADI YA MUNGU KISHIA NA KISUNNI ITIKADI KUMUHUSU MWENYEZI MUNGU MTUKUFU KWA PANDE MBILI (SHIA-SUNNI) Cha muhimu kitakachoelezwa katika maudhui hii ni suala la kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu. Masunni wamethibitisha jambo hilo la kumuona Mwenyezi Mungu huko akhera ya kuwa waumini wote watamuona Mwenyezi Mungu.

Na tunapozisoma sihahi za kisunni kama vile Bukhari na Muslim, tunakuta zimo riwaya nyingi zinazosisitiza kumuona Mwenyezi Mungu hasa na siyo kwa majazi,[2] bali tunakuta ndani yake kuna kumfananisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na eti kwamba anacheka[3] na anakuja na kutembea, anashuka kwenye mbingu ya dunia[4] bali atafunua muundi wake ambao unayo alama atakayotambulikana kwayo[5] na ataweka unyayo wake ndani ya Jahannam nayo itajaa iseme basi basi (inatosha) na mengineyo miongoni mwa mambo na sifa ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu ametakasika nazo na mfano wa hayo.[6] Katika ukurasa wa 202 anathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ana mkono na vidole.


Nakumbuka kwamba wakati fulani nilipata kupita katika mji wa Lamu huko Kenya Afrika ya Mashariki, nilimkuta Imam wa Kiwahabi akiwahutubia watu msikitini anawaambia kwamba: "Mwenyezi Mungu ana mikono miwili na miguu miwili na uso". Nilipompinga juu ya hilo alisimama na kutoa ushahidi kutoka katika Qur'an akasema: "Na Mayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba, (sivyo bali) mikono yao ndiyo iliyofumba na wamelaaniwa kwa sababu ya yale waliyoyasema, lakini mikono ya Mwenyezi Mungu i wazi". (Qur'an, 5:64)

Na akasema tena:
"Na tengeneza Jahazi mbele ya macho yetu". (Qur'an, 11:37) Na alisema tena:
"Kila kilicho juu yake kitaondoka na utabaki uso wake (dhati yake)". (Qur'an, 55:26-27) Mimi nilisema: Ewe ndugu yangu aya zote hizi ulizozileta na nyinginezo zote ni majazi siyo hakika (kama zinavyoonesha)!! Alijibu akasema:
"Qur'an yote ni hakika wala hapana ndani yake majazi". Mimi nikasema: Kama ni hivyo basi ipo tafsiri ya aya isemayo kuwa, "Na aliyekipofu katika hii (dunia) basi atakuwa kipofu katika akhera". (Qur'an, 17:72)
Basi Je, ninyi mnaichukulia aya hii kwa maana ya hakika (kama inavyoonekana)? Kwani (inajulisha kuwa) kila aliye kipofu duniani atakuwa kipofu huko akhera"? Sheikh huyo alijibu: "Sisi tunazungumzia juu ya mkono wa Mwenyezi Mungu na jicho la Mwenyezi Mungu na uso na Mwenyezi Mungu wala kabisa hatuna habari na vipofu!!" Nikasema: Hebu na tuachane na habari ya vipofu, basi je, ni ipi tafsiri yenu kuhusu aya uliyoitaja isemayo, "Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake". (Qur'an, 28:88)

Aliwageukia waliohudhuria mskitini akawaambia," hivi yuko miongoni mwenu ambaye hakuifahamu aya hii? hapana shaka kwamba ikowazi mno mfano wa ile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo: "Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake". Mimi nikasema kumwambia: "Hakika wewe umezidisha maji ndani ya unga (umezidi kuharibu), Ewe ndugu yangu, bila shaka tumehitilafiana kuhusu Qur'an, wewe umedai kwamba ndani ya Qur'an hakuna majazi bali Qur'an yote ni hakika (yaani isomekavyo ndivyo itakavyotafsiriwa) nami nimedai kwamba ndani ya Qur'an mna majazi na hasa kuhusu aya ambazo ndani yake kunaonesha kumfanyia kiwiliwili Mwenyezi Mungu au kumfananisha. Iwapo utaing'ang'ania rai yako hiyo basi itakulazimu useme kwamba kila kitu kitaangamia isipokuwa uso wake, hii ikiwa na maana kwamba mikono yake na miguu yake na mwili wake wote utatoweka na kuangamia na hakitabakia ila uso wake, na Mwenyezi Mungu ni mtakatifu mno hana sifa kama hiyo. Kisha niliwageukia waliohudhuria hapo nikawaambia, "Hivi kweli mnakubaliana na tafsiri hii (ya Sheikh huyu?)" Wote walinyamaza na Sheikh wao aliyekuwa akihadhiri naye hakusema kitu, basi nikawaaga nikatoka hali ya kuwa nawaombea uongofu na mafanikio.


yao kuhusu Mwenyezi Mungu kama ilivyo ndani ya vitabu vyao na katika mihadhara yao.Naweza tu kusema kwamba, wako baadhi ya wanachuoni wetu wa Kisunni wanaipinga itikadi hiyo lakini wengi wao wanaamini kuwa watamuona Mwenyezi Mungu huko akhera na watamuona kama wanavyouona mwezi mpevu ambao haukufunikwa na mawingu. Na kuhusu jambo hili wao hutolea ushahidi wa aya isemayo kuwa: "Siku hiyo nyuso zitang'ara zikingoja rehma ya Mola wao" (Wujuhun Yaumaidhin Nadhirah Ila Rabbiha Nadhirah)[7]. (Qur'an, 75:22)

Na kwa hakika ni kiasi tu cha wewe kuifahamu itikadi ya Mashia Imamiyyah kuhusu jambo hili, nafsi yako italiwazika na akili yako itakubaliana na taawili za aya za Qur'an zinazoonesha kuwa kuna namna fulani ya kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa ana mwili, au kumfananisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kitu fulani, bali kuzichukulia aya hizo kuwa ni majazi na istiarah na siyo kama zinavyoonekana, wala dhahiri ya matamko yake kama wanavyodhani baadhi ya watu. Imam Ali (a.s.) anasema kuhusu jambo hili: "Azma ya hali ya juu haifikii kumtambua Mwenyezi Mungu, wala fahamu yenye uerevu wa hali ya juu kabisa haitomuelewa Mwenyezi Mungu jinsi alivyo. Mwenyezi Mungu ambaye sifa zake hazina mipaka ijulikanayo, hapana jinsi ya kumsifu, wala hana wakati ulio na upeo wala muda."[8]

Naye Imam Muhammad Al-Baqir katika kuwapinga wanaomshabihisha Mwenyezi Mungu anasema, "Bali kila katika undani wa maana zake, basi hicho ni kiumbe kilichotengenezwa kama sisi na kitarudishwa kwetu". Taz: Aqaidul-Imamiyyah. Na kuhusu jambo hili linatutosha jawabu la Mwenyezi Mungu ndani ya Qur'an aliposema: "Hakuna chochote chenye mfano wake". Na kauli yake nyingine "Macho hayamdiriki Mwenyezi Mungu". Pia kauli ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake Musa (a.s.) pale alipotaka amuone Mwenyezi Mungu akasema, "Ewe Mola wangu nioneshe nikuone akasema kamwe huwezi kuniona." Herufi hii ya "Lan" iliyoko kwenye aya hii inamaanisha "Kamwe, Abadan" kama wasemavyo wanazuoni wa fani ya nahau.

Yote hayo ni dalili pasina shaka yoyote juu ya kusihi kwa kauli za Mashia ambao wanategemea kauli za Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) kuhusu jambo hilo, Maimamu hao ambao ndiyo wenye undani wa elimu na nyumba yao ambayo ndiyo mahala pa utume na wao ndiyo wale ambao Mwenyezi Mungu amewarithisha elimu ya kitabu (Qur'an). Basi yeyote yule atakaye ziyada kuhusu uchunguzi huu, anawajibika kuvirejea vitabu vilivyofafanua maudhui hii kama vile kitabu kiitwacho "Kalimatun Haular-Ruuyah " cha Sayyid Shara'fud-Din mwandishi wa Al-Murajaat"[9]


ITIKADI YA UTUME KISHIA NA KISUNNI Tofauti iliyopo baina ya Shia na Sunni katika mlango huu ni maudhui inayohusu "Ismah " (kuhifadhika kutokana na makosa). Mashia wanakubali Ismah kwa Manabii (a.s.) kabla ya kutumwa kwao na baada ya kutumwa. Masunni wanasema kwamba, Manabii ni Maasum (wamehifadhika) tu katika yale wanayoyafikisha miongoni mwa maneno ya Mwenyezi Mungu, ama yasiyokuwa hayo wao ni kama watu wengine wanakosea na kupatia, na wamenakili riwaya nyingi kuhusu jambo hilo ndani ya vitabu vyao zinazothibitisha kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikosea katika minasaba mingi. Kulikuweko baadhi ya Masahaba wakimsahihisha kama vile kwenye qadhiya ya mateka wa Badri ,qadhiya ambayo Mtume alikosea na Umar akapatia, na lau siyo yeye Umar basi Mtume wa Mwenyezi Mungu angeliangamia.


Taz: Albidayatu Wan-Nihaya cha Ibn Kathir, naye amenakili kwa Imam Ahmad na Muslim na Abu Dawud na Tirmidhi. Na miongoni mwa riwaya hizo ni ile isemayo kuwa, Mtume alipofika Madina aliwakuta watu wa hapo wakiipandisha mitende akawaambia, "Msipandishie baadaye zitakuwa tende". Yakatokea mavuno hafifu (walipokuwa wameacha kuipandishia), watu wa Madina wakaja wakamlalamikia juu ya hilo. naye Mtume akawaambia, "Ninyi ni wajuzi wa mambo ya dunia yenu kuliko mimi". Katika riwaya nyingine aliwaambia, "Bila shaka mimi ni mtu tu, basi nitapokuamuruni jambo fulani katika dini yenu ichukueni, na nitapokuamuruni jambo fulani kwa maoni yangu basi mimi ni mtu tu (chunguzeni)". Taz: Sahihi Muslim Kitabul-Fadhail Juz. 7 uk. 95, Musnad ya Imam Ahmad Juz. 1 uk. 162 na Juz. 3 uk. 152.

Na kuna wakati Masunni wanasimulia kuwa Mtume (s.a.w.) alifanyiwa uchawi na akabakia katika hali hiyo ya kufanyiwa uchawi kwa siku kadhaa akiwa hajuwi alitendalo mpaka akawa hudhania kwamba yeye huenda kwa wakeze kumbe hawaendei.[10] Au hudhani amefanya kitu fulani kumbe hakukifanya.[11] Na kuna wakati wanasimulia kuwa, alisahau ndani ya sala yake hakufahamu ni rakaa ngapi ameswali[12] na kwamba yeye Mtume alilala akapitiwa na usingizi mpaka kukasikika kukoroma kwake kisha akaamka na akasali bila ya udhu.[13] Na wanasimulia kwamba Mtume hukasirika na kumtukana na kumlaani asiyestahiki hilo kisha husema: "Ewe Mwenyezi Mungu bila shaka mimi ni mtu tu, basi Muislamu yeyote niliyemlaani au kumtukana, mfanyie hiyo kwake iwe ni zaka na rehma.[14]


Na wanasimulia kwamba Mtume alikuwa amelala nyumbani kwa bibi Aisha mapaja yakiwa wazi, Abubakr akaingia Mtume akazungumza naye akiwa katika hali ile ile, kisha aliingia Umar na akazungumza naye na Mtume akiwa katika hali ile ile, na alipobisha hodi Uthman Mtume akarekebisha nguo zake, bibi Aisha alipomuuliza Mtume juu ya kufanya kwake hivyo, Mtume akamwambia bibi Aisha:
"Basi ni kwa nini nisimstahi mtu ambaye Malaika walimstahi."[15] Pia wanasimulia kwamba, Mtume alikuwa akiamka na janaba katika mwezi wa Ramadhan[16] na sala ya asubuhi humpita.Basi na mambo mengineyo mengi miongoni mwa hadithi ambazo akili haiwezi kuzikubali wala dini na hata muruwa wa mtu hauwezi kukubaliana."[17]

Ama Mashia kwa kuwategemea Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) wao wanawatakasa Mitume kutokana na uzushi huu na mwingine aliozushiwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.) na Mashia wanasema ya kwamba, "Mtume ametakasika kutokana na makosa, madhambi na maasi madogo au makubwa, naye ni maasum (amehifadhiwa) kutokana na kukosea, kusahau na kughafilika na amehifadhiwa dhidi ya uchawi na kila kitu kinachovuruga akili, bali yeye ametakasika mno na hata yale yote yasiyokubaliana na muruwa na tabia njema kama vile kula njiani, au kucheka kwa sauti ya juu au mzaha usiyostahiki au kitendo chochote kinachochukiza kukitenda kwa mujibu wa jamii inavyofahamu, bali wachilia mbali kuweka shavu lake juu ya shavu la mkewe mbele za watu na kuangalia yeye na mkewe mchezo wa Masoudani.[18] Wakati mwingine wanasema eti Mtume humtoa nje mkewe kwa kusudi la kushindana naye, basi kuna wakati Mtume humshinda mkewe na mara nyingine mke aibuke mshindi dhidi ya Mtume, kisha Mtume amwambie mkewe: "Ushindi huu ni mahali pa ule"![19]

Mashia wanaziona riwaya kama hizi zinazopingana na Ismah ya Manabii kuwa riwaya za uzushi zilizozushwa na Banu Umayyah na wasaidizi wao. Kwanza, kwa lengo la kuiporomosha heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) na pili, ili tu wapate sababu ya kuhalalisha matendo yao machafu na makosa yao ambayo historia imeyasajili, kwani ikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu anakosea na anapondokea kwenye matamanio kama walivyosimulia katika kisa cha Mtume kumtamani bibi Zainab binti Jahshi pindi alipomuona akichana nywele zake hali ya kuwa ni mke wa Zaidi bin Harithi eti Mtume alisema: "Umetukuka ewe Mwenyezi Mungu mwenye kugeuza nyoyo."[20] Au kile kisa cha Mtume kumpenda mno bibi Aisha na kukosa uadilifu kwa wakeze wengine mpaka kuna wakati fulani wakamtuma bibi Fatmah (a.s) na wakati mwingine bibi Zainab binti Jahshi ili kumtaka afanye uadilifu.[21] Basi ikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ndiyo yuko katika hali kama hii, Muawiyah bin Abi Sufiyan, Mar-wan bin Al-Hakam na Amr bin Al-A's na Yazid bin Muawiyah na Makhalifa wote ambao walitenda maovu na kuvunja heshima za vitu vitakatifu na wakawauwa watu bila makosa watakuwa hawana lawama (kutokana na movu hayo waliyoyafanya).


Maimamu watokanao katika nyumba ya Mtume (s.a.w.) ambao ndiyo Maimamu wa Mashia wao wanasema kuwa, Mtume (s.a.w.) ni Maasum na huzipa tafsiri aya za Qur'an ambazo dhahiri yake hufahamisha kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimkemea Mtume wake kama vile aya ya "Abasa Watawalla" au zile ambazo baadhi yake huonesha kuthibitisha kuwa Mtume anayo madhambi kama asemavyo Mwenyezi Mungu "Ili Mwenyezi Mungu akusamehe madhambi yako yaliyotangulia (hapo kabla) na yale yajayo" Au kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
"Bila shaka Mwenyezi Mungu amemsamehe Mtume" (Laqad Taaba LLahu Ala Nnabi) na ile isemayo, "Mwenyezi Mungu amekusamehe kwa wewe kuwaruhusu.


Na aya zote hizi haziangushi "Ismah" ya Mtume (s.a.w.), kwani baadhi ya aya hizo Mtume siye aliyekusudiwa kwenye aya hizo na nyingine huchukuliwa kuwa ni majazi na siyo kama dhahiri ya matamko ilivyo, na jambo hilo (la kuweko majazi) latumika mno katika lugha ya Kiarabu na Mwenyezi Mungu amelitumia katika Qur'an Tukufu. Na yeyote atakaye ufafanuzi na kupata uhakika wa mambo hayo, basi anawajibika kuvirejea vitabu vya Tafsiri vya Mashia kama vile "Almizan Fi Tafsiril-Qur'an ya Allamah Attabatabai na Tafsirul-Kashif ya Muhammad Jawad Mughniya, na Al-Ihtijaj ya Tabrasi na wengineo, 136 Babu Fadhail Aisha.

kwani mimi nimeleta kwa ufupi na kuonesha itikadi za pande hizi mbili kwa ujumla, na lengo la kitabu hiki siyo jingine isipokuwa ni kubainisha kukinaika kwangu binafsi ambako nimekinaika, na ni uchaguzi wangu binafsi wa Madhehebu yale yasemayo kuwa Mitume ni "Maasum" na Mawasii wao baada ya Mitume ni "Maasum ". Na itikadi hii inaifanya akili yangu iwe na raha na kuniondoshea mashaka na utatanishi. Na kusema eti Mtume anakuwa Maasum tu katika kufikisha maneno ya Mwenyezi Mungu hii ni kauli mbaya isiyokuwa na hoja ndani yake, kwani hakuna dalili inayoonesha kwamba sehemu hii katika maneno ya Mtume ndiyo iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu na sehemu ile ni maneno yatokayo kwake mwenyewe. Basi vipi iwe katika yale ya mwanzo ni Maasum na katika yale ya pili asiwe Maasum hivyo uwepo uwezekano wa kuwa na makosa ndani yake.


Mimi najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kauli hii inayojichanganya, kauli ambayo inasababisha kuleta shaka na tuhuma kuhusu utakatifu wa dini. Na jambo hili linanikumbusha majadiliano yaliyopita kati yangu na jamaa fulani miongoni mwa marafiki zangu baada ya mimi kuuona ukweli, na nilikuwa nikijaribu kuwakinaisha kwamba Mtume (s.a.w.) ni Maasum, nao walikuwa wakijaribu kunikinaisha kwamba Mtume ni Maasum tu katika kufikisha Qur'an, na miongoni mwao alikuwemo mtaalam kutoka "Tuzad" "Sehemu ya Al-Jarid" nao jamaa wa kutoka sehemu hiyo wanafahamika sana kwa akili pevu na elimu na utambuzi wa ajabu. mtaalam huyo alifikiri kidogo kisha akasema: "Enyi jamaa, mimi ninayo maoni fulani kuhusu mas-ala haya".

Basi sote tukasema: "Tafadhali leta maoni uliyonayo". Akasema: "Hakika haya ayasemayo ndugu yetu Tijani kwa niaba ya Mashia ni kweli na ndiyo sahihi, na sisi tunawajibika kuitakidi kuwa Mtume ni maasum moja kwa moja vinginevyo tutaingiza mashaka ndani ya Qur'an yenyewe!! Wale jamaa wengine wakasema: "Kwa vipi itakuwa hivyo"?
Yeye alijibu kwa haraka aksema: "Hivi mmepata kuikuta sura yeyote miongoni mwa sura za Qur'an kwamba mwishoni mwake kuna uthibitisho wa Mwenyezi Mungu Mtukufu"?
Na anakusudia uthibitisho kuwa ni:"Muhuri ambao huhitimishiwa mapatano na barua Hi kuonesha uhakika wa muhusika na kwamba barua hiyo inatoka kwake". Basi jamaa hao wote walicheka tu kutokana na utambuzi huu wa ajabu lakini wenye maana kubwa sana. Lakini mtu yeyote asiyekuwa na chuki atazingatia kwa akili yake na ukweli utamgonga tu, na ukweli huo ni kuwa: "Kuitakidi kwamba Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu ni kuitakidi Ismah ya yule anayeifikisha moja kwa moja bila ya kugawa (Ismah yake kuwa ni ya nyakati fulani tu na nyakati zingine inatoweka) kwani haiwezekani kwa yeyote kudai kwamba alimsikia Mwenyezi Mungu akizungumza, na wala hawezi yeyote akadai kuwa alimuona Jibril wakati akiteremka na wahyi.


Kwa kifupi kauli ya Mashia kuhusu Ismah ni kauli ya sawa na kwayo hiyo hutuliza na kuondosha wasi wasi wa nafsi na ushawishi wa shetani na inakata kabisa njia ya wachochezi wenye fitna hasa maadui wa dini miongoni mwa Wayahudi na Wakristo na Walahidi ambao hutafuta vipenyo vya kupitia ili kuvuruga itikadi zetu na dini yetu na kumshambulia Mtume wetu. Basi mara nyingi utawaona wanatoa hoja dhidi yetu kwa kutumia yale yaliyomo ndani ya Sahih Bukhari na Muslim miongoni mwa matendo na maneno ambayo hunasibishwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa Mtume yu mbali mno nayo (hakusema hayo wala hakutenda).[22]

Basi tutafanyaje ili tuwakinaishe kwamba kitabu cha Bukhari na Muslim ndani yake kuna mambo ya uzushi, na jambo hili bila shaka ni gumu kwani Masunni hawalikubali kwa kuwa Bukhari kwao wao ni kitabu sahihi mno baada ya kitabu cha Mwenyezi Mungu!223
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

UIMAMU KISHIA NA KISUNNI ITIKADI INAYOHUSU UIMAMU KWA PANDE MBILI Makusudio ya Uimamu katika mlango huu ni ule Uimamu mkuu kwa ajili ya Waislamu, yaani nakusudia Ukhalifa, utawala, kuongoza na kusimamia.

Na kwa kuwa kitabu changu katika uchambuzi wake kimetegemea kulinganisha baina ya madhehebu ya Kisunni na yale ya Shia Imamiyyah, basi hapana budi kwanza nitoe misingi ya Uimamu kwa pande zote mbili ili imbainikie msomaji na mwenye kuchunguza ni ipi misingi na mafunzo ambayo kila upande unayategemea, na pia afahamu kukinaika kwangu ambako kulinilazimisha kukubali kugeuka na kuacha vile nilivyokuwa hapo kabla. Uimamu kwa Mashia ni msingi miongoni mwa misingi ya dini kutokana na umuhimu mkubwa ulionao na ni daraja tukufu ya kuuongoza umma bora uliotolewa kwa watu. Pia uongozi huo unazo sifa kadhaa na mambo maalumu ya kipekee yanayouhusu nami ninataja baadhi yake tu.


Miongoni mwa sifa hizo ni: Elimu, Ushujaa, Upole, Utakatifu, Kutosheka, Uchamungu, kuipa nyongo dunia na Mashia wanaitakidi kwamba Uimamu ni cheo akitoacho Mwenyezi Mungu kumpa aliyemteua miongoni mwa waja wake wema ili aweze mtu huyo kusimamia suala nyeti ambalo ni kuongoza ulimwengu baada ya Mtume (s.a.w.), na kwa msingi huu Imam Ali bin Abi Talib alikuwa ndiye kiongozi wa Waislamu kwa kuchaguliwa na Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu alimpelekea wahyi Mtume wake ili amtawalishe (Ali) kuwa kiongozi wa watu. Bila shaka Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtawalisha na akaujulisha umma baada ya hija ya kuaga katika bonde la Khum, Waislamu nao walikula kiapo cha utii. Hivi ndiyo wasemavyo Mashia.


Ama Masunni wao pia wanasema kuwa ni lazima kuwepo Uimamu ili kuuongoza umma, lakini wao wanaupa umma haki ya kumchagua kiongozi wake, na ndiyo maana Abubakar bin Abi Quhafah alipokuwa Imam wa Waislamu kwa kuchaguliwa na Waislamu wenyewe baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ambaye (kama wasemavyo) alilinyamazia jambo la ukhalifa na wala hakuubainishia umma kitu chochote kuhusiana na suala hilo na akaliacha liwe ni mashauriano baina ya watu. Ukweli uko wapi?

Mtu anayechunguza, akizingatia kauli za pande mbili na akafikiri kwa makini juu ya hoja za makundi haya mawili bila ya chuki basi huenda akaukaribia ukweli bila shaka yoyote. Nami hapa nitakuonesheni ukweli ambao mimi niliufikia kwa njia ifuatayo:
1. Uimamu ndani ya Qur'an Tukufu:
Mwenyezi Mungu Anasema:
"Na kumbukeni Ibrahim alipofanyiwa mtihani na Mola wake kwa amri nyingi naye akazitimiza, (Mwenyezi Mungu) akamwambia hakika mimi nitakufanya uwe kiongozi wa watu wote. Ibrahim akasema; na miongoni mwa kizazi changu (wafanye wawe viongozi) akasema, ahadi yangu haiwafikii madhalimu". (Qur'an, 2:124) Ndani ya aya hii Tukufu, Mwenyezi Mungu anabainisha kwamba Uimamu ni cheo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu, na humpa cheo hicho yule amtakaye miongoni mwa waja wake pale aliposema: "Nitakufanya kiongozi (Imam) wa watu." Kama aya ilivyobainisha kwamba Uimamu ni ahadi toka kwa Mwenyezi Mungu hawaipati isipokuwa waja wema ambao Mwenyezi Mungu amewateua kwa ajili ya lengo hili, na hii hutokana na kuwakanusha kwake madhalimu ambao hawastahiki ahadi hiyo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mwenyezi Mungu amesema:


"Na tumewafanya kuwa Maimamu wanaoongoza kwa amri yetu na tukawapelekea wahyi wa kufanya mambo ya kheri na kusimamisha sala na kutoa zaka na wakawa ni wenye kutunyenyekea". Qur'an, 21:73)
Pia amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na tukawafanya miongoni mwao kuwa Maimamu wanaoongoza kwa amri yetu, (hii ni kwa kuwa) walisubiri na walikuwa wakiziamini aya zetu". (Qur'an, 32:24)
Vile vile amesema:
"Na tunataka kuwafanyia ihsani wale waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya kuwa Maimamu na kuwafanya kuwa warithi". (Qur'an, 28:5)
Huenda baadhi ya watu wakafikiri kwamba aya hizi zilizotajwa zinajulisha kwamba Uimamu uliokusudiwa hapa ni Utume na Unabii, (kufikiri) hivyo ni kosa katika maana ya ujumla ya Uimamu, kwani kila Mtume ni Nabii na ni Imam, na siyo kila Imam ni Mtume au Nabii!!

Na kwa lengo hili basi Mwenyezi Mungu ameweka wazi ndani ya kitabu chake kitukufu kwamba, waja wake wema inawezekana kwao kumuomba yeye Mwenyezi Mungu cheo hiki kitukufu ili wasimamie jukumu la kuwaongoza watu, ili wapate malipo makubwa. Mwenyezi Mungu amesema:
"Na wale ambao hawashuhudii ushuhuda wa uongo na wanapopita penye upuuzi hupita kwa heshima, na wale ambao wanapokumbushwa aya za Mola wao hawaziangukii kwa uziwi na upofu, na wale wanaosema, Mola wetu tupe miongoni mwa wake zetu na watoto wetu yaburudishayo macho yetu na utujaalie kuwa Maimam wa wachamungu". (Qur'an, 25:72-74)
Kama ambavyo Qur'an vile vile imelitumia tamko la Imamah ili kujulisha viongozi na watawala madhalimu ambao wanawapoteza wafuasi na raia wao na kuwaelekeza kwenye maovu na mateso duniani na akhera.


Imekuja ndani ya Qur'an simulizi juu ya Firauni na majeshi yake pale Mwenyezi Mungu aliposema: "Basi tukamtesa yeye na majeshi yake na tukawatumbukiza baharini basi angalia ulikuwaje mwisho wao, na tuliwafanya kuwa Maimamu waitao kwenye moto na siku ya Qiyama hawatasalimishwa, na tukawafuatishia laana katika dunia hii na siku ya Qiyama watakuwa miongoni mwa wenye hali mbaya mno." (Qur. 28:40-42)

Na kwa msingi huu, kauli ya Mashia iko karibu na kile ambacho Qur'an imekithibitisha, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka wazi kwa maelezo ambayo hayatoi nafasi yoyote ya mashaka, kwani Uimamu ni cheo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu na hukiweka pale atakapo. Na cheo hicho ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ambayo amekataa wasiipate madhalimu, na kwa kuwa mtu asiyekuwa Ali miongoni mwa masahaba wa Mtume bila shaka yoyote kuna kipindi kabla ya Uislamu alifanya ushirikina, Hapana shaka kwa ajili hiyo wanakuwa miongoni mwa madhalimu, hivyo hawastahiki ahadi ya Mwenyezi Mungu ya Uimamu na Ukhalifa, na hapo inabakia kauli ya Mashia ya kwamba Imam Ali bin Abi Talib peke yake ndiyo alistahiki ahadi ya Mwenyezi Mungu ya Uimamu kuliko Masahaba wengine, kwani yeye Ali (a.s.) hakuabudia sanamu, bali Mwenyezi Mungu ameutukuza uso wake kinyume cha Masahaba, kwani Ali hakupata kusujudia sanamu.


Na iwapo patasemwa kuwa Uislamu unafuta yaliyotendeka hapo kabla, sisi tutasema ndiyo lakini bado inabakia tofauti kubwa kati ya yule aliyekuwa mshirikina kisha akatubu na yule aliyekuwa mtakatifu na hakumtambua Mola mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu.
2. Uimamu katika Sunna ya Mtume:
Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema kauli nyingi kuhusu Uimamu, kauli ambazo zimenakiliwa na Mashia na Masunni ndani ya vitabu vyao na Musnad zao, kuna wakati alizungumza juu ya Uimamu kwa tamko la "Al-Imamah" na wakati mwingine kwa tamko la "Al-Khilafah" na kuna wakati alitumia tamko la "Al-Wilayah" au Al-Imarah." Kuhusu tamko la Al-Imamah imekuja kauli ya Mtume kama ifuatavyo:
"Maimamu wenu bora ni wale munaowapenda nao wanakupendeni, na mnaowaombea nao wanakuombeeni, na Maimamu wenu waovu ni wale munao wachukia nao wanakuchukieni na munawalaani nao wanakulaanini". Wakasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je, tuwapige upanga?


Mtume akasema, "Hapana madam wanasali sala miongoni mwenu". Taz: Sahih Muslim Juz. 6 uk. 24 Babu Khiyaril-Aimati wa Shirarihim. Na amesema Mtume (s.a.w.):
"Baada yangu watakuwepo Maimamu ambao hawatafuata muongozo wangu na wala hawatafuata suna yangu, na watakuja simama miongoni mwao watu ambao nyoyo zao ni nyoyo za shetani zikiwa ndani ya miili ya watu". Taz: Sahih Muslim Juz. 6 uk. 20 Babul-Amri Biluzumil-Jamaah Inda Dhuhuril-Fitan. Na kuhusu tamko la "Al-Khilafah" imekuja kauli yake Mtume kama ifuatavyo:
"Dini haitaacha kuwa imara mpaka kiama kitakaposimama hadi wakufikieni Makhalifa kumi na mbili na wote watatokana na Makuraishi".


Na imepokewa toka kwa Jabir bin Samurah amesema, "Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: Uislamu hautaacha kuwa na nguvu kupitia kwa Maimamu kumi na wawili, kisha alisema neno ambalo sikulifahamu, nikamwambia baba yangu,Mtume amesemaje? Akasema wote ni kutokana na Makuraishi". Na imekuja kauli ya Mtume kuhusu tamko la "Al-Imarah" kama ifuatavyo:
"Itakuwepo aina fulani ya Maamiri ambao mtawatambua na mtawapinga, mwenye kuwatambua amejitakasa na mwenye kuwapinga amesalimika, lakini yeyote atakayewaridhia na kuwafuata... Wakasema Je, tuwapige, akasema, hapana maadamu wanasali".

Taz: Sahih Muslim Juz. 6. uk. 23 Babu Wujubil-Inkari Alal-Umarai. Na amesema tena Mtume kuhusu tamko la "Al-Imarah ": "Watakuwepo Maamiri kumi na wawili wote ni Makuraishi" Taz: Sahih Bukhar Juz. 8 uk. 127. Na imekuja toka kwa Mtume (s.a.w.) akiwatahadharisha Sahaba wake: "Mtaupupia Uamiri na kutakuwa na majuto siku ya Qiyama, mwenye kunyonya ameneemeka, na aliyeacha kunyonya ameathirika." Taz: Sahih BukhariJuz, 8 uk. 106. Kama ambavyo Mtume amezungumza tena kwa tamko la "Wilayah" "Mambo ya watu hayataacha kuwa na mafanikio maadamu watakuwa wanatawaliwa na watu kumi na wawili wote ni Maquraishi". Taz: Sahih Muslim Juz. 6 uk. 3.


Na baada ya maelezo haya mafupi juu ya maf-humu ya Al-Imamah na Al-Khilafah ambayo nimeitoa ndani ya Qur'an na Sunna sahihi ya Mtume bila ya tafsiri wala taawili, bali nimetegemea vitabu vya Kisunni bila ya (kutegemea)vitabu visivyokuwa vyao miongoni mwa (vitabu vya) Mashia, kwani jambo hili (yaani la Ukhalifa wa Makhalifa kumi na wawili na wote ni Makuraishi) kwa Masunni ni katika mambo yanayokubalika na wala hakuna utata juu yake, wala hawatofautiani wawili kuhusiana nalo na hiyo ni pamoja na kufahamu kwamba baadhi ya wanachuoni wa Kisunni wanabainisha kwamba Mtume (s.a.w.) amesema: "Kutakuwepo na Makhalifa kumi na wawili wote ni katika bani Hashim." Taz: Yanabiul-Mawaddah Juz. 3uk. 104.

Na imepokewa toka kwa Shaabi, naye toka kwa Mas-Rooq, amesema: "Wakati fulani sisi tulikuwa kwa ibn Mas-ud tunaaridhi Misahafu yetu kwake basi kijana fulani akamwambia, hivi Mtume wenu alikuusieni kuwa watakuwepo Makhalifa wangapi baada yake, akasema hakika wewe ni mdogo kwa umri na jambo hili hajaniuliza mtu kabla yako, ni kweli alituusia Mtume wetu (s.a.w.) kwamba baada yake watakuwepo Makhalifa kumi na wawili kwa idadi ya Mabwana wa kizazi cha Israeli... Taz: Yanabiul-Mawaddah Juz. 3 uk. 105.

Na baada ya haya, hebu basi na tuangalie juu ya kusihi kwa madai ya kila upande kwa kuyapitia maandiko yaliyowazi kama ambavyo tutajadili taawili ya kila moja ya pande mbili hizi kuhusu suala hili muhimu ambalo limewagawa Waislamu tangu siku aliyofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) mpaka leo hii, na kutokana na kutengana huko kukawa kumetokea Madh-hebu mengi na makundi mengi na mafundisho mengi ya kifikra na maneno, wakati hapo zamani Waislamu walikuwa ni umma mmoja. Basi kila tofauti iliyotolewa baina ya Waislamu sawa sawa iwe ni ya Fiqhi au tafsiri ya Qur'an au katika kuifahamu Sunna tukufu ya Mtume, basi asili yake na sababu yake ni Ukhalifa.

Ni kitu gani basi kitakujulisha huo Ukhalifa ni jambo gani? Ukhalifa ambao baada tu ya Saqifah limekuwa ni jambo ambalo kwa sababu yake hadithi sahihi na aya zilizo wazi zimekuwa zikipingwa na (badala yake) kutengenezwa hadithi nyingine zisizokuwa na msingi ndani ya sunna ya Mtume ili tu kuuthibitisha na kuupa usahihi Ukhalifa ulio patikana ndani ya Saqifa? Jambo hili linanikumbusha namna ilivyo Israel na hali halisi iliyopo, nayo ni kuwa, Wafalme na Maraisi wa (Mataifa ya) Waarabu walikutana na wakaafikiana kuwa wasiitambue nao wala amani, kwa maana kwamba kilicho chukuliwa kwa nguvu kisirudishwe ila kwa nguvu. Baada ya miaka michache (Waarabu) wakakutana upya, mara hii kwa ajili ya kuvunja uhusiano wao na Misri ambayo imetambua kuwepo kwa Wazayoni, na baada ya miaka michache wakarejesha uhusiano wao na Misri na hawakuilaani kuhusu uhusiano wake na Israel pamoja na kuwa Israel haikubaliani na haki za Taifa la Wapalestina na haikubadilisha chochote kutoka kwenye msimamo wake, bali ilizidisha kero zake na ikaongeza kuwakandamiza wananchi wa Palestina. Basi historia inajirudia yenyewe kwani Waarabu wamezoea kukubaliana na matokeo yalivyo.


MJADALA WA UKHALIFA MAONI YA MASUNNI KUHUSU UKHALIFA NA MJADALA JUU YA HILO Maoni yao juu ya Ukhalifa yanaeleweka, nayo ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alificha na hakumbainisha yeyote kushika Ukhalifa, lakini watu wenye hekima miongoni mwa Masahaba walikusanyika ndani ya Klabu ya bani Saidah na wakamtawalisha Abubakr ashike mahala pa Mtume (s.a.w.), na hiyo ni kwa sababu Mtume (s.a.w.) alimuachia kusalisha wakati wa maradhi yake, basi wakasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alimridhia Abubakar kwa ajili ya jambo la dini yetu basi ni kwa nini sisi tusimridhie kwa mambo ya dunia yetu?
Hivyo basi kauli ya Masunni kwa ufupi imefungamana na vifungu vifuatavyo:
1). Mtume (s.a.w.) hakumbainisha yeyote.
2). Ukhalifa hauwezi kusihi isipokuwa kwa njia ya mashauriano.
3). Kumtawalisha Abubakr ni jambo lililotendeka kupitia Masahaba wakubwa.


Bila shaka haya ndiyo yalikuwa maoni yangu wakati nilipokuwa nikifuata Madhehebu ya Malik, na nikiyatetea kwa nguvu zote nilizopewa na nikiyatolea dalili ya aya zinazohusu kushauriana, na nilikuwa nikijaribu kwa uwezo wangu kueleza kuwa dini ya Kiislamu ni dini yenye demokrasi katika maamuzi na kwamba yenyewe ndiyo iliyoanza kuweka msingi huu wa kibinaadamu, msingi ambao mataifa yaliyoendelea yanajivunia.

Zaidi ya hapo nilikuwa nikisema, "Ikiwa mataifa ya Magharibi hayakupata kuutambua utaratibu huu wa jamhuri mpaka katika karne ya kumi na tisa, basi bila shaka Uislamu umeyatangulia mataifa hayo na kuufahamu utaratibu huo tangu karne ya sita. Lakini baada ya kukutana kwangu na wanachuoni wa Kishia na kusoma vitabu vyao na kuzichunguza hoja zao zenye kukinaisha, hoja ambazo zimo ndani ya vitabu vyetu nilibadili maoni yangu ya mwanzo pale nilipopambanukiwa na hoja zilizo wazi, kwani haiwezekani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuuacha umma bila ya Imam (kiongozi) kwani yeye Mwenyezi Mungu ndiye asemaye: "Bila shaka wewe ni muonyaji, na kila kaumu inaye muongozaji".

Kama ambavyo haistahiki kabisa kwa mujibu wa huruma yake Mtume kuuacha umma wake bila mchungaji na hasa tutakapofahamu ya kwamba Mtume alikuwa akichelea utengano[23] wa umma wake na kurudi kinyume nyume[24] na kushindania dunia[25] kisa cha kuuana wao kwa wao[26] na kufuata nyendo za Mayahudi na Wakristo[27] Na Iwapo Ummul-Muuminina Aisha binti Abubakr alimtumia ujumbe Umar bin Al-Khattab wakati alipopigwa dharuba ya upanga (iliyopelekea kifo chake) akamwambia:

"Mtawalishe mtu juu ya umma wa Muhammad (kabla hujafa) na usiwaache watu hivi hivi tu, hakika mimi nachelea fitina juu yao." Taz: Al-Imamah wa Siyasah. Na iwapo Abdallah bin Umar naye anaingia ndani kwa baba yake alipokuwa kapigwa dhoruba hiyo ya upanga na kumwambia: "Hakika watu wanadai kwamba wewe humtawalishi mtu (baada yako) basi waonaje lau ungekuwa na mchungaji wa ngamia au mchungaji wa mbuzi kisha akaja kwako na akaiacha mifugo hiyo bila shaka itapotea, basi usimamizi wa watu ni jambo muhimu zaidi." Taz: Sahih Muslim Juz. 6 uk. 5, Baabul-Istikhlafi wa Tarkih.

Na kama Abubakr mwenyewe naye ndiye yule Waislamu walimtawalisha kwa mashauriano yeye ndiye anayebomoa msingi huo na haraka anamtawalisha Umar baada yake ili kwa tendo hilo akate mizizi ya utengano wa hitilafu na fitna. jambo hili la Abubakr kumtawalisha Umar baada yake, Imam Ali (a.s.) alilitambua mapema wakati ule Umar alipomlazimisha Imam Ali ampe Baia Abubakar, basi Imam Ali alisema kumwambia Umar: "Niandae nafasi ili wewe uwe na hisa, na leo hii nimuimarishe ili kesho akurudishiye"! Taz: Al-Imamah Was-Siyasah cha ibn Qutaibah Juz.l uk.18.
Basi mimi nasema, "Ikiwa Abubakr hayaamini mashauriano, ni vipi sisi tutaamini kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliliacha jambo hili bila kumuweka mtu, na je tuseme Mtume alikuwa hakijui kile walichokuwa wakikijua kina Abubakr, bibi Aisha na Abdallah bin Umar? Na ni kitu ambacho watu wote


wanakitambua moja kwa moja nacho ni kutokea hitilafu ya maoni na kila mmoja kutamani namna yake iwapo suala la kuamua lingeachwa mikononi mwao na hasa pale jambo lenyewe litakapohusu uongozi na kukalia madaraka ya Ukhalifa". Na hali hiyo ndiyo iliyotokea kwa vitendo hata kwenye uchaguzi wa Abubakr siku hiyo ya Saqifah, kwani tumeona kupinga kwa Bwana mkubwa wa Kiansar Saad bin Ubbadah na mwanawe Qais bin Saad, Ali bin Abi Talib, Zubair bin Al-Awwam,[28] Abbas bin Abdil-Mutalib, Bani Hashim wengine na baadhi ya Masahaba ambao walikuwa wakiona kuwa Ukhalifa ni haki ya Ali (a.s.) na walipinga baia hiyo na wakabakia nyumbani kwa Ali mpaka wakatishiwa kuchomwa moto.[29]


Kwa kulinganisha hayo tunaona Mashia wanathibitisha kinyume cha usemi wa Masunni na wanasisitiza ya kwamba Mtume (s.a.w.) alimbainisha Ali kuwa ni Khalifa na akatamka hili katika matukio mengi na lililo mashuhuri ni lile la Ghadir Khum. Na iwapo uadilifu unakulazimisha kumsikiliza mgomvi wako ili naye alete maoni yake na hoja zake kuhusu jambo fulani mlilohitilafiana wewe na yeye, basi hali itakuwaje iwapo mgomvi wako atatoa hoja kupitia kitu ambacho wewe mwenyewe unashuhudia kuwa kilitokea?


Na dalili za Mashia siyo dalili za kipuuzi au dhaifu mpaka uwepo uwezekano wa kuzipuuza na kujisahaulisha kirahisi, bali mambo wanayotolea ushahidi yanafungamana na aya za Qur'an Tukufu zilizoshuka kuhusu jambo hili (la Ukhalifa), naye Mtume (s.a.w.) alizipa umuhimu na udhibiti muda wote wa uhai wake, na zikanakiliwa na pande zote mbili mpaka zikavijaza tele vitabu vya historia na vile vya hadithi, nao wapokezi wakazisajili zama baada ya zama.
1. Uongozi wa Ali (a.s.) ndani ya Qur'an:
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
"Mtawala wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husali sala na hutoaza kahali ya kuwa wamerukuu, na yeyote atakayemtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wale walioamini, bila shaka kundi laMwenyezi Mungu ndilo litakaloshinda" (Qur'an, 5:55-56)

Ameandika Abu Is-haq At-Thalabi ndani ya tafsiri yake iitwayo At-Tafsir-rul Kabir kwa Isnad ya Abu Dharri Al-Ghifari amesema: "Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa (masikio) haya mawili vinginevyo yazibe, na nilimuona kwa (macho) haya mawili vinginevyo na yapofuke akisema:"Ali ni kiongozi wa watu wema, na muangamizaji wa kufru, basi atasaidiwa atakayemsaidia, na atadhalilishwa atakayemdhalilisha.Kwa yakini mimi siku moja nilisali pamoja na Mtume, basi akaomba muombaji ndani ya Msikiti, hakuna mtu yeyote aliyempa kitu, na Ali alikuwa amerukuu basi akamnyooshea yule muombaji kidole chake kilichokuwa na pete, yule muombaji akaja akaichukua ile pete kidoleni mwa Ali, hapo Mtume (s.a.w.) akamnyenyekea Mwenyezi Mungu Mtukufu akamuomba akasema:

Ewe Mwenyezi Mungu, hakika ndugu yangu Musa alikuomba akasema: Mola wangu kifungue kifua changu na uniwepesishie jambo langu na ukifungue kifundo cha ulimi wangu ili kauli yangu ifahamike, na uniwekee waziri kutoka miongoni mwa jamaa zangu ndugu yangu Harun, ziimarishe kwake nguvu zangu ili tupate kukutakasa sana na tukutaje kwa wingi bila shaka wewe kwetu sisi ni mwenye kutuona,kisha ukampa habari (Musa) kuwa, Umepewa maombi yako Ewe Musa. Ewe Mwenyezi Mungu nami mja wako na Mtume wako nikunjulie kifua changu na uniwepesishie jambo langu na uniwekee waziri kutoka miongoni mwa jamaa zangu Ali ziimarishe kwake nguvu zangu".


Abu Dharri amesema:"Wallahi Mtume hakukamilisha maneno yake ila aliteremka Jibril na aya hii "Mtawala wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husali sala na hutoa zaka hali ya kuwa wamerukuu, na yeyote mwenye kumtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini basi bila shaka kundi la Mwenyezi Mungu ndilo litakaloshinda". Taz: Al-Jams-u Baina Sihahis-Sittah, Sahihun-Nasai, Musnad Ahmad bin Hanbal ibn Hajar ndani ya Sawaiq yake pia ameisimulia ibn Abil-Hadid ndani ya Shar-h ya Nahjul-Balagha.

Hapana ikhtilafu yoyote kwa Mashia kwamba aya hii ilishuka kwa ajili ya Ali bin Abi Talib kwa mapokezi yatokayo kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) nayo ni miongoni mwa khabari zinazokubalika kwao kwani imesimuliwa aya hii ndani ya vitabu vingi vya Kishia vinavyotegemewa kama vile:
1). Biharul-Anwar cha Majlisi 2). Ithbatul-Hudat cha Al-Hurru Al Amili 3). Tafsirul-Mizan cha Allamah Tabatabai 4). Tafsirul-Kashif cha Muhammad Jawad Mughiniyah 5). Al-Ghadir cha Al-Allamah Al-Amini na wengine wengi. Kama ambavyo imesimuliwa juu ya kushuka kwa aya hii kumuhusu Imam Ali bin Abi Talib toka kwa wanachuoni wengi wa Kisunni nitataja miongoni mwa hao wale wa Tafsiri tu:

1). Tafsirul-Kash-Shaf ya Zamakhari Juz.l uk. 649
2). Tafsirut-Tabari Juz. 6. uk. 288.
3). Zadul-Masirifill-Mit-Tafsir cha ibn Jauzii Juz.2uk. 383.
4). Tafsirul-Qur-Tibii Juz. 6 uk. 219
5). Tafsirul-Fakhrir-Razi Juz. 12 uk. 25,
6). Tafsirubni Kathir Juz. 2 uk. 71.
7). Tafsirun-Nasfii Juz. 1 uk. 289. X
8). Shawahidut-Tanzil . ya Al-Haskani Al-Hanafi Juz.l uk!61.
9). Ad-Durul-Manthur Fi Tafsir bil-Maathur ya Suyuti Juz. 2
uk.293.
10). Asbabun-nuzul cha Al-Imamul-Wahidi uk. 148. 11). Ahkamul-Qur'an cha Aljas-Sas Juz. 4 uk. 102. 12). At-Tas-hilu Liulumit-Tanzil cha Alkalbii Juz.l uk. 181.


Na vitabu vya Kisunni ambavyo sikuvitaja ni vingi zaidi kuliko vile nilivyovitaja. 2. Ayatul-Balagh pia yahusika na utawala wa Ali:
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
"Ewe mtume fikisha uliyoteremshiwa toka kwa Mola wako, na kama hukufanya basi hukufikisha ujumbe wake, na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu". (Qur'an, 5:67) Baadhi ya wafasiri wa Kisunni wanasema kwamba aya hii ilishuka mwanzoni mwa wito wa Uislamu pale Mtume (s.a.w.) alipokuwa akiweka walinzi wa kumlinda kwa kuchelea kuuawa, na iliposhuka kauli hii isemeyo, "Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu" Mtume akasema: "Nendeni zenu bila shaka Mwenyezi Mungu amekwisha kunilinda". Ibn Jarir na ibn Mardawaih wamethibitisha toka kwa Abdallah bin Shaqiq kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema: "Hakika kulikuwa na watu miongoni mwa Masahaba wake wakikaa nyuma yake (kumlinda) basi iliposhuka aya isemayo "Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu Mtume alitoka akasema:

"Enyi watu nendeni zenu, bila shaka Mwenyezi Mungu amekwisha nilinda kutokana na watu" Taz: Ad-Durul-Manthur Fit-Tafsir Bil-Maathur Juz. 3 uk. 119.
Naye ibn Hibban na ibn Mar-dawaih wamethibitisha toka kwa Abu Hurairah amesema: "Tulikuwa tukisafiri pamoja na Mtume safarini tunamuachia sehemu kubwa ya kivuli naye huketi chini yake, basi siku moja akaketi chini ya mti na akauning'iniza upanga wake kwenye mti, kuna mtu fulani alikuja akachukua upanga ule kisha kasema, Ewe Muhammad ni nani atakulinda kutokana nami? Mtume akasema, Mwenyezi Mungu ndiye atakayenilinda kutokana nawe uweke upanga huo, yule mtu akauweka na ndipo iliposhuka aya hii ya "Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu" Taz: Rejea iliyotangulia.


Ni kama ambavyo Tirmidhi na Al-Hakim na Abu Nuaim wao wametoa mapokezi toka kwa bibi Aisha amesema: "Mtume (s.a.w.) alikuwa akilindwa mpaka iliposhuka aya isemayo "Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu", akatoa kichwa chake kwenye Qubbah akasema "Enyi watu nendeni zenu hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kunilinda". Naye Tabrani na Abu Nuaim ndani ya Ad-Dalail na ibn Mar-Dawaih na ibn Asakir wamethibitisha kutoka kwa Ibn Abbas amesema: "Mtume (s.a.w.) alikuwa akilindwa na ammi yake bwana Abu Talib ambaye alikuwa akimtumia kila siku mtu miongoni mwa Bani Hashim ili kumlinda, basi Mtume akasema ewe ammi yangu hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kunilinda sina haja na hao unaowatuma".


Nasi tunapofanya mazingatio kuhusu hadithi hizi na taawili hizi, tunazikuta hazikubaliani na mafuhumu ya aya tukufu wala mtiririko wake, kwani riwaya zote hizi zinafidisha kwamba aya hii ilishuka mwanzoni mwa daawa hata baadhi yake zinaonyesha wazi kwamba ilikuwa ni kipindi cha uhai wa Abu Talib yaani kabla ya Hijra kwa miaka mingi, na hasa riwaya ya Abu Hurairah ambayo ndani yake anasema kuwa: "Tulikuwa tukifuatana na Mtume wa Mwenyezi Mungu safarini tunamuachia kivuli kikubwa..." Riwaya ni dhahiri kabisa kwamba ni ya kuzua, kwani Abu Hurairah hakuujua Uislamu wala kumjua Mtume (s.a.w.) isipokuwa katika mwaka wa saba wa Hijra ya Mtume kama anavyoshuhudia yeye mwenyewe[30] jambo hilo, basi ni vipi riwaya hiyo itakubalika na hali ya kuwa wafasiri wote wa Kisunni na Kishia wamekubaliana kwamba Suratul-Maidah imeshuka Madina nayo ndiyo ya mwisho kushuka katika Qur'an?

Hapana shaka Ahmad amethibitisha, naye Abu Ubaid ndani ya Fadail yake, An-Nasai, Ibnul-Mundhir, Al-Hakim, Ibnu Mar-Dawaih na Baihaqi ndani ya Sunan yake, kutoka kwa Jubair Bin Nufair amesema: "Nilihiji na kisha nikaingia kwa Aisha akasema: Ewe Jubair unaisoma Suratul-Maidah? Nikasema ndiyo, akasema bila shaka hiyo ni sura ya mwisho kushuka basi mtakacho kikuta ndani yake kuwa ni halali kihalalisheni, na mtakachokikuta ndani yake kuwa ni haramu basi kiharamisheni.[31]

Kama ambavyo wamethibitisha Ahmad, Tirmidhi, Al-Hakim, ibn Mar Dawaih na Baihaqi ndani ya Sunani yake kutoka kwa Abdallah bin Amri amesema: "Sura ya mwisho kushuka ni "Al-Maidah". Taz: Ad-Durrul-Manthur Juz. 3 uk. 3. Na amethibitisha Abu Ubaid toka kwa Muhammad bin Kaab Alqurtubi amesema: "Suratul-Maidah iliteremka kwa Mtume katika Hijja ya kuaga (akiwa) kati ya Maka na Madina hali yakuwa Mtume yuko juu ya ngamia wake, bega la ngamia yule likavunjika na Mtume (s.a.w.) akashuka."

Taz: Ad-Durrul-Manthur Juz. 1 Tafsir Bil-Maathur Juz. 3 uk. 4. Naye ibn Jarir amethibitisha toka kwa Rabii bin Anas amesema: Suratul-Maidah ilishuka kwa Mtume (s.a.w.) njiani wakati wa Hija ya kuaga Il-Hali Mtume yuko juu ya kipando chake, basi kipando hicho kikapiga magoti kutokana na uzito wa sura hiyo". Taz: Ad-Durrul-Manthur Fitafsir Bil-Maathur Juz. 3 uk. 4.

Pia amethibitisha Abu Ubaid toka kwa Damrah bin Habib na A'tiyyah bin Qais wamesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema: Sura ya Maidah ndiyo ya mwisho kushuka katika Qur'an, basi ihalalisheni halali yake na muiharamishe haramu yake". Taz: Rejea iliyotangulia.

Basi ni vipi iwe kwa mtu mwenye akili, tena muadilifu atakubaliana baada ya yote haya na madai ya yule asemaye kwamba sura hiyo ilishuka mwanzoni mwa Utume? Na sababu ya kufanya hivyo ni kutaka kuigeuza toka kwenye maana yake halisi. Zaidi ya hivyo Maisha hawahitilafiani kuwa kama Suratul-Maidah ndiyo sura ya mwisho kushuka katika Qur'an na kwamba aya hii isemayo: "Ewe Mtume fikisha yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako...." ndiyo aya iitwayo kuwa ni aya ya 'Kufikisha' (Ayatul-Balagh) iliteremka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) siku ya kumi na nane ya mfunguo tatu baada ya Hijja ya kuaga huko kwenye bonde la Khum kwa mnasaba wa Mtume kumsimika Imam Ali bin Abi Talib mbele za watu ili awe ni Khalifa wake baada yake na hiyo ilikuwa ni siku ya Al-Khamis, Jibril alishuka na sura hiyo baada ya kupita saa tano za mchana akasema: "Ewe Muhammad Mwenyezi Mungu anakutakia amani na anakuambia: Ewe Mtume fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako na ikiwa hukufanya, basi hujafikisha ujumbe wake na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu .


Kwa kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu inasema: "Ikiwa hukufanya basi hujafikisha ujumbe wake" Hii inajulisha dalili iliyo wazi kwamba ujumbe (aliotumwa) umefikia mwisho au ukingoni, na kilichobakia ni jambo muhimu ambalo dini haikamiliki isipokuwa kwa jambo hilo. Kama ambavyo aya hii inavyoonesha kwamba Mtume anachelea kufanywa muongo na watu pindi atapowalingania jambo hili muhimu, lakini Mwenyezi Mungu anamtaka aitumie fursa hiyo kwani wakati umeshafika na hiyo ndiyo fursa nzuri mno na mahala pake ni mahala panapostahiki mno, kwa sababu watu. waliokusanyika pamoja na Mtume walikuwa zaidi ya laki moja ambao walifuatana naye katika Hijja ya kuaga. Isitoshe nyoyo zao zilikuwa bado zimeshikamana na mambo matukufu ya Mwenyezi Mungu na ziko tayari kupokea agizo lolote la Mtume wa Mungu naye akatangaza katika fursa hiyo habari za kwisha umri wake.


Kauli ya Mtume alipowaambia kwamba, "Huenda mimi nisikutane nanyi baada ya mwaka huu, kwani karibu atanijia mjumbe wa Mola wangu nami nitaitwa na nitaitika", watu hawa watatawanyika baada ya mkusanyiko huu unaotisha na warejee majumbani kwao na huenda wasipate fursa ya kukutana kwa mara nyingine kwa idadi hii kubwa. Na hapo Ghadir Khum ndiyo njia panda, hivyo haiwezekani kwa Muhammad (s.a.w) kuikosa fursa hii kwa namna yoyote ile.

Basi iweje imkose hali ya kuwa Wahyi umekwishamfikia kwa njia inayofanana kama onyo ya kwamba, ujumbe wote umefungwa kwenye kufikisha hili (litakiwalo hapo) naye Mwenyezi Mungu amemdhamini ulinzi kutokana na watu, hapana cha kumfanya achelee kupingwa na watu hao kwani ni Mitume wangapi kabla yake waliopingwa na hilo halikuwarudisha nyuma katika kufikisha yale waliyoamrishwa kwa kuwa ni juu ya Mtume kufikisha tu, japokuwa Mwenyezi Mungu yuwafahamu kwamba wengi wa watu hao wanaichukia haki[32] na japokuwa anafahamu kuwa wengi wao ni wapinzani,[33] hiyo haiwi sababu kwa Mwenyezi Mungu kuwaacha bila kusimamisha hoja juu yao ili watu wasije pata hoja dhidi ya Mwenyezi Mungu baada ya kufika Mitume na Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu tena mwenye hekima.[34]


Na kwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anacho kiigizo chema kwa ndugu zake miongoni mwa Mitume waliomtangulia ambao walipingwa na watu wao. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Na kama wakikupinga, bila shaka walipinga kabla yao watu wa Nuhu na watu wa Adi na watu wa Thamud na watu wa Lut na watu wa Madyan, na Musa pia alikadhibishwa nikawapa muda makafiri kisha nikawatia mikononi, basi ilikuwaje adhabu yangu". (Qur'an, 22:42-44)

Nasi tutakapoacha chuki mbaya na kuacha kutetea madhehebu, bila shaka tutakuta ufafanuzi huu unakubaliana na akili na unakwenda sambamba na mtiririko wa aya na matukio yaliyoitangulia na kuifuatia. Na kwa hakika wengi wa wanachuoni wetu (wa Kisunni) wamethibitisha kwamba sura hiyo ilishuka huko kwenye bonde la Khum kuhusiana na kusimikwa kwa Imam Ali (a.s.) kuwa Khalifa, na riwaya hizo zinazohusu sura hiyo wamezithibitisha kuwa ni sahihi ndugu zao miongoni mwa wanachuoni wa Kishia na wameafikiana nao juu ya hilo nami nitataja kuonesha mfano wa wanachuoni wa(kisuni) waliolithibitisha hilo kama ifuatavyo:
1). Al-Hafidh AbuNuaim ndani ya Kitabu chake kiitwacho:
"Nuzulul-Qur 'an.
2). Al-Imamul-Wahidi ndani ya kitabu chake kiitwacho; Asbabun Nuzul uk. 150.
3). Al-Imam Abu Is-haq Ath-Thalabi ndani ya Tafsirul-Kabir.
4). Al-Hakim Al-Haskani ndani ya kitabu chake kiitwacho As-Shawahidut-TanzilLiqawaidit TafdhilJuz. 1 uk. 187.
5). Jalalud-Din As-Suyuti ndani ya kitabu chake kiitwacho Ad Durrul-Manthur Fitafsir Bil-Maathur Juz. 3 uk. 117.
6). Al-Fakhrur-Razi ndani ya Tafsirul-Kabir Juz. 12 uk. 50.
7). Muhammad Rashid Rida ndani ya Tafsir Al-Manar Juz. 2 uk. 86 Juz. 6uk. 463.
8). Tarikh Dimishq cha Abu Asakir Ash-Shafi Juz. 2 uk. 86.
9). Fat-Hul-Qadir cha Shaukani Juz. 2 uk. 60.
10). Matalibus-Suul cha Ibn Tal-hah Ashqfi Juz. 1 uk. 44
11). Al-Fusulul-Muhimmah cha IbnAs-Sabbagh Al-Maliki uk. 25
. 12). Yanabiul-Mawaddah cha Al-Qanduzi Al-Hanafi uk. 120.
13).Al-Milal Wan-Nihal cha As-Shahir Stani Juz.luk. 163.
14). Ibn Jarir A'tabari ndaniya Kitabul-Wilayah. 15). Ibn SaidAs-Sajistani ndaniya Kitabu chake Al-Wilayah.
16). Umdatul-Qarii Fit Shark Al-Bukhari cha Badrud-Din Al-Hanafi Juz. 8 uk.584.
17). Tafsirul-Qur'an cha Abdul-Wahhab Al-Bukhari.
18). Ruhul-Maani cha Al-Alusi Juz.2 uk.384.
19). Faraidus-Simtain cha Al-Hum-wayni Juz. 1 uk.185.
20). Fat-Hul-Bayan Fi Maqasidil-Qur'an cha Al-Allamah As-Sayyid Siddiq Hasan Khan Juz.3 uk.63.


Hii ni sehemu ndogo miongoni mwa vitabu vyao nilivyonavyo, lakini wako zaidi ya hawa miongoni mwa wanachuoni wa Kisunni ambao Al-Allamah Al-Amin amewataja ndani ya Kitabu cha Al-Ghadir. Basi ni jambo gani Ewe bwana alilolifanya Mtume wa Mwenyezi Mimgu (s.a.w.) pindi Mwenyezi Mungu alipomuamrisha kufikisha yale aliyoteremshiwa?

Mashia wanasema kwamba: "Mtume aliwakusanya watu kwenye uwanja huo mahala hapo paitwapo Ghadir Khum, na akawahutubia hotuba ndefu yenye kina kisha akawashuhudisha nafsi zao na wakashuhudia kwamba yeye Mtume (s.a.w.) ni bora kwao kuliko nafsi zao, na hapo ndipo alipounyanyua mkono wa Imam Ali bin Abi Talib akasema "Yeyote ambaye mimi ni mtawala wake basi huyu Ali ni mtawala wake, Ewe Mwenyezi Mungu mtawalishe atakayemtawalisha Ali na umpinge atakayempinga Ali, na umsaidie atakayemsadia na umdhalilishe atakayemdhalilisha na uipeleke haki iwe pamoja na (Ali) popote atakapokuwa." Hii ndiyo ile hadithi iitwayo Hadithul-Ghadir na wameithibitisha wanazuoni wa Kishia na wale wa Kisunni kwa maelezo ya namna moja.

Kisha Mtume alimvalisha Ali kilemba chake na akamtengenezea mahali kisha akawaamuru Masahaba wampongeze kwa kuwa kwake Amiri wa Waumini, nao wakafanya kama walivyoamriwa na Mtume (s.a.w.). Watu wa mwanzo kumpongeza walikuwa ni Abubakar na Umar na wakamwambia "Hongera Ewe mwana wa Abu Talib umekuwa mtawala wa kila Muumini mwanamume na mwanamke". Taz: Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 4 uk. 281. At-Tabari katika Tafsiri yake, Ar-Razi ndani ya Tafsiri yake Juz. 3 uk. 636, Ibn Hajar ndani ya As-Sawaiq, Daraqutni, Al-Bayhaqi na Al-Khatibul-Baghdadi n.k.

Walipokwisha kumpongeza, Mwenyezi Mungu akamteremshia Mtume kauli yake isemayo "Leo nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema yangu na nimekuridhieni Uislamu kuwa ndiyo dini yenu". Hivi ndivyo wasemavyo Mashia, na kauli hii kwao ni katika mambo ambayo wote wanaafikiana. Basi Je, tukio hili kwa Masunni limeelezwa ili tusibakie tunaegemea kwao na tunafurahishwa na kauli yao? Bila shaka Mwenyezi Mungu ametutahadhirisha kwa kusema:

"Na miongoni mwa watu kuna ambaye kauli yake inakufurahisha hapa duniani, naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu yale yaliyomo moyoni mwake na hali ya kuwa yeye ni mgomvi mkubwa kabisa" (Qur'an, 2:204) Basi ni wajibu tufanye tahadhari na tuichunguze maudhui hii kwa hadhari na kuzitazama dalili za pande zote mbili kwa uadilifu hali ya kuwa tukitaka radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Jawabu ni ndiyo, (tukio hili limetajwa kwa Masunni) na kwa hakika wengi miongoni mwa wanachuoni wa Kisunni wanalitaja tukio hili kwa namna lilivyo na ufuatao ni ushahidi kutoka katika vitabu vyao:
1) Imam Ahmad bin Hanbal amethibitisha kutoka kwenye hadithi ya Zaidi bin Ar-Qam amesema: " Tulishuka pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kwenye bonde liitwalo Khum, basi Mtume akaamuru paswaliwe, Mtume akaswali mchana wa joto kali,kisha akatuhutubia, na alitengenezewa kivuli kwa kutumia nguo kwenye mti kutokana na jua kisha Mtume akasema: Je, hivi hamjuwi, au je, hivi hamshuhudii kwamba mimi ni bora mno kwa kila muumini kuliko nafsi yake? Watu wakasema, kwa nini (tusishuhudie hilo) Mtume akasema, basi yeyote ambaye mimi ni mtawala wake Ali ni mtawala wake, Ewe Mwenyezi Mungu msaidie atakayemsaidia (Ali) na umfanye adui atakaye mfanya Ali kuwa niadui..."


Taz: Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 4 uk. 3 72. 2) Imam An-Nasai amethibitisha katika Kitabul-Khasais kutoka kwa Zaid bin Ar-Qam amesema, "Pindi Mtume (s.a.w.) aliporudi kutoka kwenye Hijja ya kuaga na akafika Ghadir Khum, aliamuru kutengenezwe vivuli na mara vikaaandaliwa kisha akasema: "Kama kwamba mimi nimeitwa na nimeitika na kwa hakika ninaacha kwenu vizito viwili, kimojawapo ni kikubwa kuliko kingine nacho kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa yumba yangu, kwa hiyo angalieni ni vipi mtanifuata ndani ya viwili hivyo, kwani havitatengana mpaka vinifikie kwenye birika, kisha akasema, bila shaka Mwenyezi Mungu ndiye mtawalia mambo yangu nami mtawalia mambo ya kila muumini, halafu akaushika mkono wa Ali akasema: "Yeyote ambaye mimi ni mtawalia mambo yake huyu (Ali) ni mtawalia mambo yake, Ewe Mwenyezi Mungu msaidie atakayemsaidia (Ali) na mfanye adui atakayemfanya adui". Abu Tufail amesema, "Nikamwambia Yazid, Je uliyasikia haya kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu" akasema, "Ndiyo, hapana aliyekuwako katika vivuli hivyo ila alimuona kwa macho yake na alimsikia kwa masikio yake". Taz: An-Nasai katika Kitabul-Khasais, uk. 21.


3) Al-Hakim An-Nishaburi amethibitisha toka kwa Zaidi Bin Ar-Qaam kwa njia mbili zilizo sahihi tena kwa sharti za Bukhari na Muslim amesema: "Wakati Mtume aliporejea toka Hijja ya kuaga alifika kwenye bonde laKhum akaamuru atengenezewe vivuli,akaandaliwa kisha akasema: "Kama kwamba mimi nimeitwa na nimeitika, na kwa hakika nimeacha kwenu vizito viwili, kimojawapo ni kikubwa kuliko kingine navyo ni kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, basi angalieni namna gani mutanifuata katika viwili hivyo, kwani havitaachana mpaka vinifikie kwenye Haudh. Kisha akasema, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mtawalia mambo yangu nami ni mtawalia mambo ya kila muumini, halafu akaushika mkono wa Ali akasema,Yeyote ambaye mimi ni mtawalia mambo yake basi huyu hapa (Ali) ni mtawalia mambo yake, Ewe Mwenyezi Mungu msaidie atakayemsaidia na umfanye adui atakayemfanyia uadui". Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 109.

4) Kama ambavyo ameithibitisha hadithi hii Muslim ndani ya Sahih yake na kuitegemezea kwa Zaid bin Ar-Qam, lakini Muslim ameifupisha akasema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) siku moja alisimamaakatuhutubia tulipokuwa katika bonde liitwalo Khum lililokobaina ya Maka na Madina akamtukuza Mwenyezi Mungu na kumsifu, akatoa mawaidha na akakumbusha kisha akasema, Ammabaad, fahamuni enyi watubila shaka mimi ni kiumbe, karibu atanijia mjumbe wa Mola wangu na nitaitika, naminakuachieni vizito viwili, cha kwanza ni kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani yake kuna uongofu na kuna nuru, kishikeni kitabucha Mwenyezi Mungu namshikamane nacho, akahimiza juu ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na akasisitizia kisha akasema, Na watu wa nyumba yangu nakukumbusheni MwenyeziMungu juu ya watu wanyumba yangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa yumba yangu,nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa yumba yangu ...." Taz: Sahih Muslim Juz. 7 uk. 122 Babu Fadhail Ali ibn Abi Talib, pia hadithi hii wameitaja Imam Ahmad, Tirmidhi, ibn Asakir na wengineo.4
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

UFAFANUZI Pamoja na kwamba Imam Muslim amelifupisha tukio hili na hakulisimulia kikamilifu, lakini Al-Hamdulillah inatosheleza na labda ufupisho huu ulitoka kwa Zaid bin Ar-Qam mwenyewe pale hali halisi ya kisiasa ilipomlazimisha kuificha hadithi ya Ghadir na hili tunalifahamu kutokana na mfumo wa hadithi ulivyokuja kwani msimuliaji anasema:

"Mimi, Husain bin Sabrah o na Umar bin Muslim tulikwenda kwa Zaid bin Ar-Qam, tulipokaa Husain akamwambia Zaid, Bila shaka ewe Zaid umepata kheri nyingi, umemuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) umesikia hadithi zake na umepigana vita pamoja naye na umesali nyuma yake, kwa hakika umepata kheri nyingi mno, hebu tusimulie ewe Zaidi yale uliyoyasikia kwa Mtume (s.a.w.)". Zaid akasema, "Ewe mtoto wa ndugu yangu nimekwisha kuwa mzee sasa na umekuwa mrefu muda wangu, nimesahau baadhi ya mambo ambayo nilikuwa nikiyahifadhi toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) basi yale nitakayokusimulieni yakubalini na yale nisiyokusimulieni msinilazimishe, kisha akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu siku moja alisimama kwenye maji yaitwayo Khum akahutubia..."


Kutokana na mtiririko wa hadithi inadhihiri kwamba, Husain alimuuliza Zaid bin Ar-Qam tukio la Ghadir naye Zayd akalitoa jibu la suali hili mbele ya wote waliohudhuria, hivyo basi hapana shaka Zaid alikuwa akitambua kwamba kutoa jawabu la wazi wazi juu ya suali hilo ingemsababishia matatizo mbele ya serikali ambayo ilikuwa ikiwalazimisha watu kumlaani Ali bin Abi Talib, na kwa ajili hii tunamkuta anajitetea kwa muulizaji ya kuwa sasa amekuwa mtu mzima na muda mrefu umempitia na ameyasahau baadhi ya mambo aliyokuwa akiyahifadhi, kisha anaongeza kwa kuwataka waliohudhuria wakubali yale anayowasimulia na wala wasimlazimishe kuyasimulia yale anayotaka kuyanyamazia.

Pamoja na woga wake na kulifupisha kwake tukio hili bila shaka Zaidi bin Ar-Qam (Mwenyezi Mungu amlipe Kheri) ameubainisha ukweli mwingi na akaichenga hadithi ya Ghadir hakuitaja ile kauli yake isemayo "Mtume (s.a.w.) alisimama akatuhutubia kwenye bonde la Khum liliko kati ya Maka na Madina," kisha baada ya hapo akataja ubora wa Ali (a.s.) na kwamba yeye ni mshirika wa Qur'ani katika hadithi ya vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na watu wa nyumba yangu", na hakulitaja jina la Ali (a.s.) akawaachia waliohudhuria hapo hapo watumie akili zao kwani Waislamu wote wanafahamu kwamba Ali(a.s.) ndiyo kiongozi wa watu wa nyumba ya Mtume.


Na ndiyo maana tunamuona hata Imam Muslim mwenyewe alifahamu kutokana na hadithi hiyo kile ambacho sisi tumekifahamu, kwani ameiandika hadithi hii katika mlango wa Fadhail za Ali bin Abi Talib(a.s.) ingawaje hadithi haikutaja jina la Ali bin Abi Talib!! Taz: Sahih Muslim Juz. 7 uk. 122 Babu Fadhail Ali. 5) At-Tabrani amethibitisha ndani ya Muujamul-Kabir kwa sanad iliyo sahihi toka kwa Zaid bin Ar-Qam na Hudhaifah bin Usayd Al-Ghifari amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu alihutubia huko Ghadir Khum chini ya miti akasema:

"Enyi watu yakaribia nitaitwa na nitaitika, nami nitaulizwa nanyi mtaulizwa, ni nini mtakachokisema?" Wakasema, "Tunashuhudia ya kwamba wewe umefikisha na umepigania (dini) na umetoa nasaha Mwenyezi Mungu akulipe mema". Mtume akasema, "Je, hivi hamushuhudii ya kwamba hapana Mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wake, na kwamba pepo yake ni kitu cha kweli na moto wake ni kitu cha kweli, na kuwa mauti ni kitu cha kweli na kwamba kufufuliwa baada ya kufa ni kitu cha kweli. Na kwamba kiyama kitakuja bila ya shaka yoyote na kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini?

Wakasema, tunashuhudia yote hayo," Mtume akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu shuhudia" kisha akasema, "Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ni mtawalia mambo yangu na ni mtawalia mambo ya waumini nami ni bora mno kuliko nafsi zao, basi yeyote ambaye mimi ni mtawalia mambo yake huyu hapa ni mtawala wake (yaani Ali.) ewe Mwenyezi Mungu msaidiye atakayemsaidia na umfanye adui atakayemfanya adui kisha akasema, "Enyi watu hakika mimi nakutangulieni nanyi mutanifikia kwenye haudh, haudh ambalo upana wake ni kati ya Basra na San-aa, kwa hakika nitakuulizeni mtaponifikia kuhusu vizito viwili ni vipi mtanifuata katika vizito hivyo, kizito kikubwa ni kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu sehemu ya ncha yake iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na nyingine iko mikononi mwenu, shikamaneni nayo msipotee wala msibadilishe, na (kizito cha pili) ni kizazi changu watu wa nyumba yangu, hapana shaka Mwenyezi Mungu mjuzi amenijulisha mimi ya kwamba viwili hivi havitatengana mpaka vinifikie kwenye Haudh."


Taz: Ibn Hajar ndani ya Sawaiq uk. 25 amenakili kwa Tabrani, Al-Hakim na Tir-midhi. 6) Kama ambavyo amethibitisha Imam Ahmad kwa njia ya Al-Barraa bin Azib kwa njia mbili amesema: "Tulikuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu tukafika Ghadir-Khum, ikanadiwa sala ya jamaa Mtume akaandaliwa mahali chini ya miti miwili akaswali sala ya adhuhuri na akaushika mkono wa Ali kisha akasema: "Je, hamjui kwamba mimi ni bora mno kwa waumini kuliko nafsi zao" Wakasema kwa nini (twalijua hilo), akaushika mkono wa Ali(a.s.) kisha akasema, yeyote ambaye mimi ni mtawala wa mambo yake basi Ali ni mtawala wa mambo yake, Ewe Mwenyezi Mungu msaidie atakaye msaidia na mfanye adui atakayemfanyia uadui." Baada ya tukio hilo Umar akamkuta Ali akamwambia, "Hongera Ewe mwana wa Abu Talib umekuwa mtawalia mambo ya kila muumini mwanaume na mwanamke". Taz: Musnad Ahmad bin Hanbal Juz. 4 uk. 281 Kanzul-Ummal Juz. 15uk. 117. Fadhailul-Khamsah Minas-Sihahis-Sittah. Juz. 1 uk. 350.


Na kwa kifupi hadithi ya Ghadir (wameisimulia) wanachuoni wengi wa Kisunni zaidi kuliko tuliowataja, k.m Tirmidhi, Ibn Asakir, Abunuaim, Ibnul-Athir, Al-Khawar-Zami na Suyuti. Wengine ni Ibn Al-Haithami, Ibnus-Sabbagh Al-Maliki, Al-Al-Hanafi, Ibnul-Maghazili, Al-Humuwaini, Al-Haskani, Al-Ghazali na Bukhari ndani ya tarikh yake. Al-Allamah Al-Amin mwenye kitabu cha Al-Ghadir amewataja wanachuoni wa Kisunni walioisimulia hadithi hii ya Ghadir na wakaithibitisha ndani ya vitabu vyao, pamoja na tofauti zao za kimadhehebu tangu karne ya kwanza Hijiriyyah mpaka karne ya kumi na nne. Idadi yao ilikuwa inazidi wanachuoni mia tatu na sitini, na yeyote mwenye kutaka ushahidi basi ni juu yake kukirejea kitabu cha Al-Ghadir.[35]

Basi Je baada ya yote haya inawezekana akasema mwenye kusema kwamba hadithi ya Ghadir ni miongoni mwa uzushi wa Kishia?
Kinachoshangaza ni kuwa, wengi wa Waislamu wakati unapowatajia hadithi ya Ghadir hawaifahamu au unaweza kusema kuwa hawajaisikia.La kushangaza zaidi kuliko hili ni kwamba, ni vipi basi wanachuoni wa Kisunni baada ya kuwepo kwa hadithi hii ambayo imekubaliwa usahihi wake wanadai kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakuacha Khalifa (aliyembainisha) bali aliacha jambo hili liwe la mashauriano miongoni mwa Waislamu?


Basi je, kuna hadithi iliyotoa maana ya wazi kuhusu Ukhalifa na ikabainisha kuliko hii enyi waja wa Mungu? Kwa hakika mimi nayakumbuka majadiliano yangu na mmoja wa wanachuoni kutoka Az-Zaitunah nchini kwetu pale nilipomtajia hadithi ya Ghadir nikiitolea ushahidi juu ya Ukhalifa wa Ali (a.s.), basi alikiri kuwa hadithi hiyo ni sahihi bali aliiongezea nguvu akanionyesha tafsiri ya Qur'an aliyoiandika yeye mwenyewe, tafsiri ambayo ndani yake ameitaja hadithi ya Ghadir na kuwa ni sahihi na baada ya hapo akasema ndani ya tafsiri yake:

"Mashia wanadai kwamba hadithi hii ni tamko linalohusu Ukhalifa wa Ali Karrama Llahu Waj-hahu na madai hayo ni batili kwa Masunni kwani yanapingana na ukhalifa wa bwana wetu Abubakar As-Siddiq na bwana wetu Umar Al-Faruq na bwana wetu Uthman Dhin-Nurain, basi hapana budi kulipa tafsiri nyingine tamko la Al-Maula (mtawalia mambo) lililokuja ndani ya hadithi hii liwe na maana ya mpenzi na msaidizi kama ilivyokuja ndani ya Qur'an na hivi ndivyo walivyolifahamu Makhalifa waongozi na Masahaba watukufu Mwenyezi Mungu awawie radhi wote, na hivi ndivyo walivyochukua toka kwao waliofuatia na wanachuoni wa Kiislamu. Basi hapana mazingatio yoyote kwa tafsiri ya Marafidhi (Mashia) kuhusu hadithi hii kwani wao hawakubali ukhalifa wa makhalifa (Abubakar, Umar, Uthman) na wanawatukana Masahaba wa Mtume na hili peke yake linatosha kuupinga uzushi wao na kuyabatilisha madai yao" Mwisho wa maneno yake yaliyomo ndani ya kitabu chake.


Basi mimi nilimuuliza: "Je, tukio hili lilitokea huko Ghadir Khum?"
Akajibu "Lau lingekuwa halikutokea wanachuoni na wataalam wa hadithi wasingelisimulia"!! Nikasema:
"Hivi kweli inakubalika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kuwakusanya Masahaba wake katika jua kali linalounguza na kuwahutubia hotuba ndefu ili tu awaambie kuwa Ali ni mpenzi wenu na mtetezi wenu? Hivi kweli munaridhia tafsiri hii?" Akajibu:
"Bila shaka wako baadhi ya Masahaba walio mlalamikia Ali na walikuwepo wenye kumchukia na kumbughudhi hivyo basi Mtume (s.a.w.) alitaka aizidishe chuki yao ndipo alipowaambia kwamba Ali ni mpenzi wenu na ni mtetezi wenu ili tu wampende na wasimkere." Mimi nikasema:
"Basi kama jambo lenyewe ni hilo, halihitaji kuwasimamisha wote na kuwasalisha kishaa kuanza kuwahutubia kwa kuwaambia: "Je, mimi siye bora kwenu kuliko nafsi zenu." Ili Mtume aifafanue maana ya Maula, na kama mambo yatakuwa kama unavyosema basi ilikuwa inawezekana kwake Mtume kuwaambia wale waliomlalamikia Ali (kumshitakia kwa Mtume) kwamba: "Ali ni kipenzi chenu na ni mtetezi wenu" na mambo yakaisha bila ya yeye Mtume kulizuwia katika jua kali kundi hilo kubwa ambalo lilikuwa na watu zaidi ya laki moja wakiwemo wazee na wanawake. Mtu mwenye akili hawezi kabisa kukubaliana na hivyo (usemavyo).


Akasema: "Je, mtu mwenye akili ataamini kwamba Masahaba laki moja hawakuifahamu maana uliyoifahamu wewe na Mashia?" Nikasema: "Kwanza wengi wao walikuwa hawakai Madina, pili hakika wao moja kwa moja walifahamu kama nilivyofahamu mimi na Mashia na ndiyo maana wanachuoni wamesimulia kwamba, Abubakr na Umar walikuwa miogoni mwa waliompongeza Ali waliposema: "Hongera Ewe mwana wa Abu Talib umekuwa mtawalia mambo ya kila muumini". Akasema: "Basi ni kwa nini hawakumpa baia baada ya Mtume kufariki? Unawaona kwamba wao waliasi na kwenda kinyume cha amri ya Mtume (Astaghfirullah) Mwenyezi Mungu anisamehe kutokana na kauli hii". Mimi nikasema:"Ikiwa wanachuoni wa Kisunni wanashuhudia ndani ya vitabu vyao kwamba baadhi yao yaani Masahaba walikuwa wakienda kinyume cha maamrisho ya Mtume zama za uhai wake tena mbele yake[36] basi siyo ajabu kuyaacha maamrisho yake baada ya kufariki kwake, na ikiwa wengi wao walimtuhumu Mtume kwa kumpa uamirijeshi Usamah bin Zaid kutokana na umri wake kuwa mdogo pamoja na kuwa jeshi hilo la Usama lilikuwa ni kwa muda mfupi basi ni vipi wao watakubali Ali awe amiri juu yao tena mwenye umri mdogo kisha kwa muda wa uhai wao (au wake) na Ukhalifa wake ni kwa kila kitu, nawe umeshuhudia mwenyewe kwamba baadhi yao walikuwa wakimchukia Ali na kumkera?

Alinijibu huku akiwa amekasirika: "Lau kama Imam Ali Karrama Llahu Waj-hahu angekuwa anafahamu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amemtawalisha Ukhalifa, basi asingenyamazia haki yake naye alikuwa mtu shujaa isitoshe Masahaba wote walikuwa wakimuogopa" Mimi nikasema: "Bwana wangu hii ni maudhui nyingine nami sitaki kuiingia kwani wewe hukutosheka na hadithi za Mtume zilizosahihi na unajaribu kuziawili na kuzibadilisha maana yake ili tu ulinde utukufu wa viongozi waliopita, basi mimi nitakukinaisha- namna gani suala la kunyamazia kwa Imam Ali au kutoa hoja kwake dhidi yao kuhusu haki yake ya Ukhalifa?


Yule bwana alitabasamu huku akisema: "Wallahi mimi ni miongoni mwa watu wanaomtukuza Bwana wetu Ali Karrama llahu Waj-hahu juu zaidi kuliko wengine, na lau ningekuwa na uwezo nisingemtanguliza juu yake Sahaba yeyote, kwani yeye (Ali) ndiye mlango wa mji wa elimu na ndiye simba wa Mwenyezi Mungu aliyemshindi, lakini matakwa ya Mwenyezi Mungu yanamtanguliza amtakaye na kumbakisha nyuma amtakaye, haulizwi (Mwenyezi Mungu) kile akifanyacho nao viumbe wataulizwa".


Nami nilitabasamu na nikasema: "Na hii pia ni maudhui nyengine inatutaka tuzungumzie Qadhaa na Qadar na hapo kabla tumetangulia kuizungumzia na kila mmoja wetu akawa amebakia kwenye mtazamo wake, kwa hakika ninashangaa ewe bwana wangu ni kwa nini kila ninapozungumza na mwanachuoni wa Kisunni na ninapomshinikiza kwa hoja haraka sana huikimbia maudhui tuliyonayo na kushika maudhui nyingine ambayo haina uhusiano na utafiti tunao ulenga".

Akasema: "Nami nabakia kwenye mtazamo wangu siwezi kuubadilisha." Basi nilimuaga nikaondoka, na nikabaki ninafikiri saa zote, ni kwa nini simpati mwanachuoni miongoni mwa wanachuoni wetu atakayekamilisha pamoja nami mazungumzo haya na ausimamishe mlango mguuni kwake kama isemavyo methali mashuhuri huku kwetu. Baadhi yao huanza mazungumzo na pale anapojikuta hawezi kusimamisha hoja juu ya maneno yake huepa kwa kusema, "Hao ni umati uliokwisha pita, wanayo yao waliyoyachuma nanyi munayo yenu mliyoyachuma", na baadhi yao husema: "Tunahaja gani ya kuzusha fitna na chuki, la muhimu ni kuwa Masunni na Mashia wanaamini Mungu mmoja na Mtume mmoja basi hii inatosha" Na wengine husema kwa kifupi tu, "Ewe ndugu yangu muogope Mwenyezi Mungu juu ya Masahaba". Basi je, kuna nafasi yoyote inayobakia kwa watu hawa kutafiti, kuchunguza kielimu, kuing'arisha njia na kurejea kwenye haki ambayo hapana baada yake isipokuwa upotofu? vipi) mbinu za Qur'an ambazo zinawataka watu kusimamisha dalili "Waambie leteni hoja zenu ikiwa ninyi mnasema kweli." Pamoja na kufahamu kwamba lau wao wataacha kuwashutumu na kuwahujumu Mashia basi tusingelazimika kujadiliana nao hata kwa yale yaliyo mema.


AYA YA KUKAMILISHA DINI AYA YA KUKAMILISHA DINI PIA INAHUSIANA NA SUALA LA UKHALIFA Kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni Neema yangu na nimeuridhia kwenu Uislamu kuwa ndiyo dini" (Qur'an, 5:3) Mashia wanakubaliana kuwa ilishuka hapo Ghadir Khum baada ya Mtume (s.a.w.) kumsimika Imam Ali kuwa ni Khalifa wa Waislamu, na hiyo ni riwaya iliyopokelewa toka kwa Maimamu wa kizazi kitakatifu, na ndiyo maana utawaona (Mashia) wanauhesabu Uimamu kuwa ni miongoni mwa "Misingi ya Dini" (Usulud-Din). Pamoja na kwamba wengi wa wanachuoni wetu wa Kisunni wanaisimulia aya hii kuwa ilishuka hapo Ghadir Khum baada ya kusimikwa Imam Ali nami ninataja miongoni mwao kama mfano:

1). Tarikh Dimishq ya ibn Asakir Juz. 2 uk. 75.
2). Manaqib Ali bin Abi Talib cha Ibn Maghazili As-Shafiiuk.19.
3). Tarikh Baghaad cha Al-Khatib Al-Baghdadi Juz.8 uk. 290.
4). Al-It-Qan cha SuyutiJuz. 1 uk. 31.
5). Tadhikiratul-Khawas cha ibn Al-Jauzi uk. 30.
6). Al-Manaqib cha Al-Khawar-Zami Al-Hanafi uk. 80.
7). Tafsir ibn KathirJuz. 2 uk. 14.
8). Ruhul-Maani ya Al-Alusi Juz. 6uk. 55.
9). Al-Bidayatu Wan-Nihayah ya Ibn Kathir Juz.5 uk. 213.
10). Ad-Durrul-Manthur ya Suyuti Juz. 3 uk. 213.
11). Yanabiul-Mawaddah cha Al-Qanduzi Al-Hanafi uk. 115.
12). Shawahidut-Tanzil cha Al-Haskani Juz. 1 uk. 157.


Mimi nasema, pamoja na yote hayo wanachuoni wa Kisunni wamelazimika kuibadilisha aya hii na kuiweka kwenye munasaba mwingine, na kufanya hivyo ni kwa ajili ya kulinda heshima ya viongozi waliopita miongoni mwa Masahaba, vinginevyo kama wangekubali kwamba aya hiyo imeshuka hapo Ghadir Khum na wangekiri kwamba kutawazwa kwa Imam Ali ndiyo jambo ambalo kwalo Mwenyezi Mungu aliikamilisha dini na akawatimizia Waislamu kwa jambo hilo neema yake, na pia ungelitoweka Ukhalifa wa Makhalifa watatu ambao walimtangulia Imam Ali na ungeporomoka uadilifu wa Masahaba na hadithi nyingi zingeyeyuka kama chumvi inavyoyeyuka ndani ya maji. Lakini jambo hili haliwezekani na ni jambo zito kwani lahusika na itikadi ya umma mkubwa wenye historia yake na wanachuoni wake na watukufu wake, hivyo basi imeshindikana kwetu sisi kumpinga Bukhari na Muslim ambao wanasimulia ya kwamba aya hiyo ilishuka Ijumaa jioni ya siku ya Arafa.


Na kwa riwaya hizo za kina Bukhari zile riwaya za mwanzo zinaonekana kuwa ni uzushi wa Kishia na hazina msingi wowote wa usahihi, na kuwashutumu Mashia inakuwa ni bora mno kuliko kuwashutumu Masahaba, kwani Masahaba hawa wamehifadhika kutokana na makosa[37] na wala hapana uwezekano wa mtu yeyote kuyakosoa matendo yao na maneno yao. Amma hao Mashia wao ni majusi, makafiri, wazandiki, na ni walahidi na muasisi wa madhehebu yao ni Abdallah bin Saba[38] ambaye ni Myahudi aliyesilimu zama za Uthmani bin Affan ili kuwavuruga Waislamu na Uislamu. Kufanya hivyo ni jambo jepesi mno ili kuupotosha umma ambao umeleleka juu ya msingi wa kuwatukuza na kuwaheshimu Masahaba (yaani Sahaba yeyote yule japokuwa alimuona Mtume mara moja) basi itawezekana vipi kwetu sisi kuwakinaisha watu kwamba riwaya hizo siyo uzushi wa Kishia bali ni hadithi za Maimamu kumi na wawili ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu alitamka kuhusu Uimamu wao, Maimamu ambao serikali za Kiislamu katika karne ya kwanza zilifanikiwa kupandikiza mapenzi na kuwaheshimu Masahaba dhidi ya Ali na wanawe juu ya Mimbar na kuwafuatilia Mashia wao kwa kuwauwa na kuwafukuza, na hapo ndipo ilipoanzia chuki na karaha dhidi ya kila Shia kutokana na mambo yaliyosambazwa na vyombo vya habari katika zama za Muawiyah ikiwa ni pamoja na itikadi mbaya dhidi ya Shia, na leo hii Mashia wanaitwa kuwa ni kundi la upinzani ili tu kuwatenga na kuwamaliza.


Na kwa ajili hiyo tunawakuta hata waandishi na wanahistoria katika zama hizo wakiwaita Mashia kuwa ni Ar-Rawafidhi" (yaani wapinzani) na huwakufurisha na kuwauwa ili tu kujipendekeza kwa watawala. Ulipoanguka utawala wa Banu Umayyah na ukafuatiwa na dola ya Banu Abbas baadhi ya wanahistoria walibadili muelekeo wao, baadhi yao wakaitambua haki ya watu wa nyumba ya Mtume hiyo ni kwa sababu ya Maimamu wa nyumba ya Mtume nafsi zao zilishikamana na Akhlaq yao njema na elimu zao ambazo zilijaa ulimwenguni, na uchamungu wao na utukufu aliowapa Mwenyezi Mungu.

Kutokana na mazingira haya wanahistoria hao wakajaribu kufanya uadilifu na ndipo walipomuunganisha Ali kwenye Makhalifa waliomtangulia, lakini pamoja na hayo hawakuthubutu kuiweka wazi haki yake, na ndiyo maana utawaona hawakuandika ndani ya vitabu vyao isipokuwa sehemu ndogo tu ya ubora wa Ali na tena wanatoa zile sifa ambazo hazipingani na Ukhalifa wa waliomtangulia. Baadhi yao wameweka hadithi nyingi zinazohusu ubora wa Abubakar, Umar na Uthman kwa kupitia ulimi wa Ali mwenyewe ili wapate kukata njia ya Mashia wanaosema kuwa Ali ni bora zaidi.


Kwa kupitia uchunguzi wangu nimegundua kwamba umashuhuri wa watu na utukufu wao ulikuwa ukipimwa kwa kiwango cha kumchukia Ali bin Abi Talib, kwani Banu Umayya na Banu Abbas walikuwa wakimkurubisha na kumtukuza kila yule ambaye alikuwa akimpiga vita Imam Ali au akisimama dhidi yake kwa upanga au ulimi, ndiyo maana utawaona wanawatukuza baadhi ya Masahaba na kuwatweza wengine. Si hivyo tu bali (Banu Umayya na Banu Abbas) wakiwasheheneza kwa mali nyingi baadhi ya washairi na kuwauwa wengine, na huenda mama Aisha Ummul-Muuminina asingekuwa na hadhi kwa kiwango hicho kwa Masunni lau siyo kumchukia[39] kwake Ali na kumpiga vita.


wanaonekana wamefikia kiwango cha upuuzi na ujinga wa akili na maoni potofu kwa vile wanaitakidi juu ya Uimamu wa Mahdi anayengojewa ambaye ataujaza ulimwengu uadilifu na usawa kama ambavyo umejazwa dhulma na ujeuri. Na sasa tunarudi kuzijadili kauli za pande mbili kwa Sasa hebu turudi na tuzijadili kauli za pande mbili kwa utulivu bila ya chuki ili tufahamu ni munasaba upi na ni sababu ipi ya kushuka kwa aya ya kukamilisha dini ili itupambanukie haki na tuifuate. Hapo sasa hatuwajibiki kukubaliana na ridhaa ya hawa au chuki ya wale maadam kabla ya chochote tunaikusudia radhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujiokoa kutokana na adhabu yake siku ambayo haitamfaa mtu mali yake wala watoto ila yule atakayemjia Mwenyezi Mungu na moyo uliosalimika. Siku ambayo nyuso zitang'ara na nyuso zingine zitakuwa nyeusi, ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi, je, mlikufuru baada ya kuamini? Basi ionjeni adhabu kwa yale muliyokuwa mukikufuru. Na ama wale ambao nyuso zao zitang'ara basi hao watakuwa katika Rehma za Mwenyezi Mungu wao wataingia humo. (Qur'an, 3:106)5
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

MJADALA JUU YA AYA YA KUKAMILISHA DINI MJADALA JUU YA KAULI ISEMAYO: AYA YA KUKAMILISHA DINI ILISHUKA SIKU YA ARAFA'
Bukhari ameeleza ndani ya sahihi yake amesema: "Ametusimulia Muhammad bin Yusuf, ametusimulia Sufian kutoka kwa Qais bin Muslim naye toka kwa Tariq bin Shihab kuwa watu fulani miongoni mwa Mayahudi walisema, Lau aya hii ingeshuka kwetu basi siku hiyo tungeifanya kuwa sikukuu, Umar akasema, aya gani? Wakasema, "Leo nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema yangu." Basi Umar akasema, "Mimi najua mno mahala gani ilishuka, ilishuka wakati Mtume akiwa amesimama Arafa". Taz: Sahih Bukhar Juz. 5 uk. 125.

Na amethibitisha Ibn Jarir kutoka kwa Isa bin Harithah Al-Ansari amesema: "Tulikuwa tumekaa ndani ya Ofisi, basi Mkristo mmoja akatuambia, Enyi Waislamu! hakika mmeshushiwa aya ambayo lau ingeteremshwa kwetu basi siku hiyo na saa hiyo (ilioteremshwa) tungeifanya kuwa ni sikukuu muda wote japo watabakia miongoni mwetu watu wawili, nayo ni ile aya isemayo: "Leo nimekukamilishieni dini yenu" Basi hapana yeyote miongoni mwetu aliyemjibu, nikakutana na Muhammad bin Kaab Al-Qurtubi nikamuuliza kuhusu jambo hilo akasema: "Hivi hamkumjibu"? Umar bin Al-Khatab alisema: "Ilishuka kwa Mtume hali ya kuwa amesimama juu ya mlima siku ya Arafah, basi haijaacha siku hiyo kuwa ni sikukuu kwa Waislamu muda wote ataobakia mmoja miongoni mwao". Taz: Ad-Durrul-Manthur Juz. 3 uk. 18.


Kwanza: Tunaona kwa kupitia riwaya hizi kwamba, Waislamu walikuwa hawajuwi tarehe ya siku hiyo kuu na wala Waislamu walikuwa hawasherehekei jambo ambalo liliwafanya Mayahudi kwa mara ile ya kwanza na Wakristo kwa mara nyingine tena wawaambie Waislamu: "Lau aya hii ingeshuka kwetu, basi siku hiyo iliyoshuka tungeifanya kuwa sikukuu." Hali hii ilimlazimisha Umar bin Al-Khatab aulize ni aya gani hiyo? Na waliposema: "Leo nimekukamilishieni dini yenu" Umar akasema hakika mimi najua mno mahala gani iliteremshwa, iliteremshwa hali ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) akiwa amesimama Arafah.

Kwa hakika sisi tunahisi kwamba kuna namna fulani ya utata na kuficha ukweli katika riwaya hii, na kwamba watu walioizua hadithi hii kupitia ulimi wa Umar bin Al-Khatab katika zama hizo za Bukhari walitaka kuafikiana na Mayahudi na Wakristo juu ya kwamba siku hiyo ni siku tukufu ni wajibu iwe sikukuu, na kwa kuwa wao Waislamu hawaisherehekei siku hiyo wala kuikumbuka japo mara moja mpaka wameisahau na wakati kinachotakiwa ni kuwa iwe miongoni mwa siku kubwa kwa Waislamu kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwakamilishia Dini yao ndani ya siku hiyo na akawatimizia neema yake na kuwaridhia Uislamu kuwa dini yao. Na kwa ajili hiyo utaona katika riwaya ya pili kauli ya msimuliaji pale alipoambiwa na yule Mkristo "Enyi Waislamu kwa hakika mmeteremshiwa aya ambayo lau ingeteremshwa juu yetu basi siku hiyo tungeifanya kuwa ni sikukuu japo watabakia watu wawili miongoni mwetu".


Msimuliaji amesema: "Hakuna yeyote aliyemjibu miongoni mwetu" Na hiyo ni kwa sababu ya kutokujua kwao tarehe na heshima ya siku hiyo na Utukufu wake. Inaonesha kwamba msimuliaji mwenyewe alishangaa ni kwa vipi Waislamu wanapuuza kusherehekea siku kama hiyo ndiyo maana tunamuona anapokutana na Muhammad bin Kaaba Al-Qurtuni na kumuuliza juu ya jambo hilo huyu naye anamjibu kuwa, "Umar bin Al-Khatab alisimulia kwamba aya hiyo ilishuka kwa Mtume (s.a.w.) akiwa amesimama kwenye mlima siku ya Arafah."

Kwa hiyo basi lau siku hiyo ingekuwa inajulikana kwa Waislamu kwamba ni sikukuu basi wapokezi hawa wasingekosa kuijua sawa sawa wakiwa ni miongoni mwa Masahaba au waliowafuatia Masahaba, kwani kilichothibiti na kinachojulikana kwao ni kwamba Waislamu wanasikukuu mbili tu nazo ni sikukuu ya mfunguo Mosi na sikukuu ya mfunguo Tatu mpaka hata wanachuoni na wanahadithi kama vile Bukhari na Muslim na wasiokuwa hao unawaona wanathibitisha ndani ya vitabu vyao, "Kitabul-Idain " (Yaani Mlango unaohusu sikukuu mbili) - (au) Sala ya Idi mbili na Khutba za Idi mbili na mambo mengineyo yanayokubalika kwao na kwa wengine lakini hakuna sikukuu ya tatu.


Dhana kubwa iliyopo ni kwamba wale wasemao juu ya misingi ya mashauriano kuhusu Ukhalifa na waasisi wa nadharia hii, wao ndiyo ambao waliogeuza kushuka kwa aya hiyo kutoka kwenye ukweli wake halisi, ambao ni siku ya Ghadir Khum baada ya kutawazwa Imam Ali, ikawa ni rahisi kwao kuigeuzia kuwa siku ya Arafah. Siku ya Ghadir ilikusanya jumla ya watu laki moja au zaidi na hakuna tukio munasaba katika Hijja ya kuaga linalofanana na Ghadir katika kulinganisha kuliko siku ya Arafa, kwani Mahujaji hawakukusanyika mahala pamoja isipokuwa sehemu mbili hizo, na kinachofahamika ni kuwa watu huwa wametawanyika kwa makundi mbali mbali katika siku zote za Hijja na wala hawakusanyiki mahala pamoja isipokuwa Arafa.


Kwa hiyo basi tunaona kwamba wale wasemao kuwa ilishuka siku ya Arafa wanasema kuwa iliteremka mara tu baada ya hotuba mashuhuri ya Mtume (s.a.w.) hotuba ambayo wameithibitisha wana hadithi ndani ya vitabu vyao. Basi iwapo tamko la Ukhalifa wa Ali bin Abi Talib wameliondosha kwenye ukweli wake na wakashitukiza watu miongoni mwao akiwa Ali mwenyewe na wale waliokuwa pamoja naye wakishughulika kuandaa mazishi ya Mtume kwa kumpa baia Abubakar huko kwenye Saqifah bani Saidah (Klabu ya Bani Saidah) bila kutegemea, na kisha wakayatupilia mbali yale maagizo ya Ghadir na kuyasahau kabisa, je,itawezekana kwa mtu yeyote baada ya hayo yaliyotokea kutoa hoja kuwa aya hiyo ilishuka siku ya Ghadir? Aya haiko wazi zaidi katika kufahamika maana yake kuliko hadithi ielezayo khabari ya Wilaya,(utawala) bali maana iliyo katika aya hiyo ni kukamilika kwa dini na kutimia kwa neema na kuridhika kwa Mola. Na hii si kwa kitu kingine ila ni ishara ya aya juu ya kupatikana kwa tukio katika siku hiyo nalo ndiyo sababu ya ukamilikaji wa dini.


Kinachotuongezea yakini juu ya kusihi kwa itikadi hii, ni ile khabari aliyoisimulia ibn Jarir kutoka kwa Qabaisah bin Abi Dhubaib amesema: "Kaabu alisema Lau wasiokuwa umma huu ndiyo ambao wangeshukiwa na aya hii basi wangeithamini siku iliyoshushwa ndani yake na wangeifanya kuwa ni sikukuu wanayokusanyika ndani yake", Umar akasema aya gani hiyo ewe Kaab" akasema: "Leo nimekukamilishieni dini yenu" Umar akasema, Hakika mimi nafahamu siku iliyoshuka na mahala ambapo ilishukia, ilishuka siku ya Ijumaa na ilikuwa siku ya Arafah na zote hizo Al-Hamdulillah kwetu sisi ni siku kuu".

Pili: Kauli isemayo kuwa aya ya "Leo nimekukamilishieni Dini yenu" kuwa ilishuka siku ya Arafah inapingana na aya ya "Tabligh" isemayo kuwa "Ewe Mtume fikisha yale uliyoteremshiwa" aya ambayo inamuamuru Mtume (s.a.w.) kufikisha jambo muhimu ambalo Utume hautimii ila kwa jambo hilo, na ni aya ambayo hapo kabla tumetangulia kuifanyia uchambuzi na ikabainika kuwa ilishuka baina ya Maka na Madina baada ya Hijja ya kuaga, khabari ambayo wameisimulia zaidi ya Masahaba mia moja ishirini na pia wameisimulia zaidi ya wanachuoni mia tatu na sitini wa Kisunni, basi ni vipi Mwenyezi Mungu ataikamilisha dini na kuitimiza neema yake siku ya Arafa kisha baada ya wiki moja amuamuru Mtume wake (s.a'.w.) wakati akirudi awafikishie watu jambo muhimu ambalo Utume wake hautakamilika isipokuwa kwa jambo hilo?
Vipi basi itasihi hali hiyo enyi wenye kutumia akili?


Tatu: Mwenye kuchunguza kwa undani atakapoifanyia mazingatio hotuba ya Mtume (s.a.w.) katika siku ya Arafah hawezi kukuta ndani ya hotuba hiyo jambo jipya ambalo Waislamu walikuwa hawalijuwi, kiasi ambacho iwezekane kuzingatiwa kuwa ni jambo muhimu ambalo kwalo Mwenyezi Mungu ameikamilisha dini na kuitimiza. Ndani ya hotuba hiyo hapakuwa isipokuwa ni mkusanyiko wa mausio ambayo Qur'an imekwisha kuyataja au mwenyewe Mtume alikwisha kuyaeleza ndani ya minasaba mingi tu na siku hiyo ya Arafah akawa anayasisitiza.
Hebu yaangalie mambo yaliyomo katika hotuba hiyo kama walivyoisajili wapokezi wote: Mwenyezi Mungu amezipa heshima damu zetu na mali zetu kama alivyoupa heshima mwezi wenu huu na siku yenu hii (kwa kuharamisha umwagaji damu katika mwezi huu). Mcheni Mwenyezi Mungu wala musiwapunje watu vitu vyao na wala musieneze ufisadi katika nchi, mwenye kuwa na amana na aitekeleze.

Watu wote ndani ya Uislamu wako sawa Mwarabu hana ubora juu ya asiyekuwa Mwarabu isipokuwa kwa kumcha Mungu. Kila damu iliyokuwa zama za jahiliya iko chini ya unyayo wangu (kuuawa mtu kwa kulipiza kisasi kwa mtindo wa zama za ujinga sasa hapana tena). Kila riba iliyokuwa katika zama za Jahiliyah iko chini ya unyayo wangu (yaani sasa hapana tena riba katika mfumo wa Jahiliyah, kabla ya kuja Uislam). Bila shaka idadi ya miezi mbele ya Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na miwili, kati ya hiyo iko minne ni mitukufu. Nakuusiyeni juu ya wanawake watendeeni wema, bila shaka ninyi mumewachukuwa chini ya amana ya Mwenyezi Mungu na mumezihalalisha tupu zao kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu.


Nakuusieni wale ambao imewamiliki mikono yenu ya kuume, walisheni kile mnachokula na muwavalishe kile munachovaa. Hakika Muslimu nduguye ni Muislamu, asimdanganye wala asimfanyie khiyana, wala usimsengenye wala damu yake si halali kwake wala chochote katika mali yake. Bila shaka shetani amekwisha kata tamaa ya kuabudiwa baada ya leo, lakini atatiiwa katika lisilokuwa hilo miongoni mwa matendo yenu mnayoyadharau. Adui mkubwa kwa Mwenyezi Mungu ni yule amuuwaye mtu ambaye Mwenyezi Mungu hataki kumuuwa na yule ampigaye asiyempiga, na mwenye kukufuru neema ya walii wake basi atakuwa amekufuru yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa Muhammad, mwenye kujinasibisha kwa asiyekuwa baba yake basi laana ya Mwenyezi Mungu na Malaika wake na watu wote imshukie.


Hakika nimeamuriwa nipigane na watu mpaka waseme "Hapana mwenye haki ya kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu na kwamba mimi ni Mtume wake", na wataposema hivyo, basi damu yao na mali zao zimehifadhika tokana nami isipokuwa kwa haki na hesabu yao iko kwa Mwenyezi Mungu. Msirudi ukafirini baada yangu mkawa wenye kupotea na kuuwana ninyi kwa ninyi. Haya yote ndiyo yaliyosemwa katika khutba ya Arafa kwenye Hija ya kuaga, nami nimekusanya milango yake kutoka kwenye rejea zote zinazotegemewa ili pasije bakia chochote miongoni mwa usia wa Mtume (s.a.w.) walioutaja wanachuoni wa hadithi isipokuwa niwe nimeutoa.
Basi je, ndani ya usia huo kuna jambo jipya kwa upande wa Masahaba?
Hapana kabisa, yote yaliyokuja ndani yake yametajwa ndani ya Qur'an na hukmu yake imebainishwa ndani ya Sunna ya Mtume, kwani Mtume (s.a.w.) alitumia uhai wake wote akiwabainishia watu yale waliyoteremshiwa na akiwafundisha yote madogo na makubwa, basi hakuna uhusiano wowote kwa kushuka aya ya kukamilisha dini na kutimiza neema na radhi ya Mwenyezi Mungu. Baada ya usia huu ambao Waislamu wanaufahamu, Mtume aliukariri kwao ili kutia mkazo kwani hiyo ilikuwa ni mara yao ya kwanza kukusanyika mbele ya Mtume kwa idadi hiyo kubwa, na pia kabla ya kutoka kwenda Hijja Mtume aliwaambia kuwa hiyo ni Hijja yake ya kuaga, kwa hiyo basi ilikuwa ni wajibu kwake kuwasikilizisha usia huo.


Ama kama tutaichukua ile kauli ya pili, nayo ni ile ya kushuka kwa aya hiyo siku ya Ghadir Khum baada ya kusimikwa Imam Ali kuwa ni khalifa wa Mtume (s.a.w.) na ni amiri wa Waumini, hapana shaka ile maana inalingana na kuafiki, kwani Ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.) ni miongoni mwa mambo muhimu na wala Mwenyezi Mungu hawezi kuwaacha waja wake hivi hivi tu, wala haipasi kwa Mtume kuondoka tu bila ya kuweka kiongozi na kuuacha umma wake bila mchungaji, na hali ya kuwa yeye Mtume alikuwa haondoki Madina ila atamwacha mtu miongoni mwa Masahaba kuwa Khalifa wake hapo mjini, basi ni vipi tutaamini kuwa alifariki na hakufikiria juu ya suala la Ukhalifa?


Iwapo wasiokuwa na dini katika zama zetu hizi wanauamini msingi huu (wa kuacha mtu maalum baada ya mtawala kuondoka) na hufanya kila njia kumbainisha mrithi wa Rais hata kabla ya Rais huyo kufariki ili tu waweze kuwaongoza watu wasiwaache hata siku moja bila ya kuwa na Rais!! Basi haiwezekani kabisa kuwa dini ya Kiislamu ambayo ni dini iliyokamilika kuliko zote na imetimia, na ni dini ambayo Mwenyezi Mungu alihitimisha kwayo sheria zote, haiwezekani kamwe kulipuuza jambo muhimu kama hili. Na hapo kabla tumefahamu kwamba bibi Aisha na ibn Umar na kabla yao Abubakr na Umar kila mmoja wao alitambua kwamba hapana budi Khalifa abainishwe vinginevyo basi itatokea fitna, kama ambavyo jambo hilo walilitambua pia wale waliokuja baada yao miongoni mwa Makhalifa ndipo kila mmoja wao alimbainisha atakayekuja baada yake, basi ni vipi hekima hii inapotea kwa Mwenyezi Mngu na Mtume wake?


Basi kauli isemayo kuwa Mwenyezi Mungu alimpelekea Wahyi Mtume wake katika ile aya ya mwanzo "Aya ya Tabligh, kufikisha" wakati akirejea toka kwenye Hijja ya kuaga kwamba amsimike Ali kuwa Khalifa wake pale Mwenyezi Mungu aliposema: "Ewe Mtume fikisha yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako na kama hukufanya, basi hujafikisha ujumbe wake na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu". Hii ikiwa na maana kwamba: Ewe Muhammad iwapo hautafikisha nililokuamuru ya kwamba Ali ndiye msimamizi wa waumini baada yako basi ni kama kwamba hukukamilisha umuhimu wa jambo ambalo kwalo umetumwa, kwani kukamilika dini kwa Uimamu ni jambo la lazima kwa kila wenye akili.


Na inaonesha kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa akichelea upinzani wao kwake na kumkadhibisha, kwani imekuja ndani ya baadhi ya riwaya kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo: "Kwa hakika Jibril ameniamuru kutoka kwa Mola wangu kwamba nisimame mahala hapa na nimjulishe kila aliye mweupe na mweusi yakuwa Ali bin Abi Talib ni ndugu yangu na ni wasii wangu na ni Khalifa wangu na ni Imam baada yangu, nikamuomba Jibril anitakie msamaha kwa Mola wangu (juu ya jambo hili) kutokana na kutambua kwangu uchache wa wamchao Mungu (miongoni mwa sahaba zangu) na kuwepo wengi wanao nibughudhi kwa ajili ya mimi kushikamana mno na Ali na kumuelekea mno yeye Ali mpaka wakaniita kuwa (Udhunu) mtu asikilizaye kila aambiwalo kwa kauli moja. Na kwa hilo Mwenyezi Mungu akasema: "Na miongoni mwao wako ambao wanambughudhi Mtume na wanamuambia kuwa yeye huamini kila aambiwalo" lau ningetaka kuwataja na kuwatambulisha ningefanya hivyo lakini nimewaheshimu kwa kuwasitiri, basi Mwenyezi Mungu hakuridhia isipokuwa kufikisha (aliyoniamuru) kuhusu Ali, fahamuni enyi watu ya kwamba Mwenyezi Mungu amekuchagulieni Ali awe ni mtawala na kiongozi na amefaradhisha kwa kila mtu amtii...[40]


Mwenyezi Mungu alipomteremshia Mtume (s.a.w.) kauli yake isemayo: "Na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu." Pale pale bila kuchelewa Mtume alitekeleza amri ya Mola wake akamtawalisha Ali kuwa ni Khalifa baada yake na akawaamuru Masahaba wake kumpongeza kwa uamiri wake kwa waumini na wakampongeza, na baada ya hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipowateremshia kauli yake isemayo: -
"Leo nimekukamilishieni Dini yenu na nimeitimiza neema yangu kwenu na nimewaridhia Uislamu kuwa ndiyo dini yenu". Zaidi ya yote hayo ni kwamba sisi tunawakuta baadhi ya wanachuoni wa Kisunni wanakiri wazi wazi kuwa aya ya Tablighi ilishuka kuhusu Uimamu wa Ali, wamepokea kutoka kwa Ibn Mar-Dawaih naye toka kwa ibn Mas-ud amesema: "Katika zama za Mtume tulikuwa tukisoma, Ewe Mtume fikisha uliyoteremshiwa toka kwa Mola wako- kwamba Ali ni mtawala wa kila muumini - na ikiwa hutafanya, basi hujafikisha ujumbe wake na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu". Na baada ya uchunguzi huu tukiongezea riwaya za Kishia zitokazo kwa Maimamu watakatifu inatubainikia kwamba Mwenyezi Mungu aliikamilisha dini yake kwa Uimamu, na kwa ajili hiyo basi Uimamu kwa Mashia umekuwa ni msingi miongoni mwa misingi ya dini.


Na kwa Uimamu wa Ali bin Abi Talib Mwenyezi Mungu alitimiza neema yake kwa Waislamu ili wasije baki hivi hivi tu wakivutwa na matamanio na fitna ikiwatenganisha na watawanyike kama kondoo wasio na mchungaji. Mwenyezi Mungu aliwaridhia Uislamu kuwa ndiyo dini yao kwani yeye Mwenyezi Mungu aliwachagulia Maimamu aliowaondolea uchafu na kuwatakasa kisha akawapa hekima na kuwarithisha Elimu ya Kitabu ili wawe ni mawasii wa Muhammad (s.a.w.) hivyo basi ni wajibu juu ya Waislamu wayaridhie maamuzi ya Mwenyezi Mungu na wakubaliane na uchaguzi wake kikamilifu, kwani Maf-humu ya Uislamu kwa ujumla ni kusalimu amri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amesema:
"Na Mola wako ndiye anayeumba akitakacho na ndiye anayechagua (akitakacho) wao hawana uchaguzi (hiyari) ametakasika Mwenyezi Mungu na ametukuka kutokana na vile wanavyomshirikisha, na Mola wako anajua yanayofichwa na nyoyo zao na yale wanayoyadhihirisha naye Mwenyezi Mungu (ni yeye tu peke yake) hapana Mola ila yeye, ni zake sifa zote njema mwanzoni na mwishoni na hukmu pia ni yake na kwake ndiko mtarejeshwa" (Qur'an, 28:68-70)


Na kwa kupitia yote hayo inafahamika kwamba siku ya Ghadir Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliifanya kuwa ni siku ya Sikukuu kwani baada ya kumtawalisha Imam Ali na baada ya kumshukia kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Leo nimekukamilishieni Dini yenu..." Mtume alisema: Ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa kuikamilisha dini na kuitimiza neema na Mola ameuridhia Utume wangu na utawala wa Ali bin Abi Talib baada yangu[41] kisha akamtengenezea jukwaa ili Waislamu wampongeze, na Mtume alikaa ndani ya hema na akamkalisha Ali pembeni yake kisha akawaamuru Waislamu wakiwemo wakeze Mtume waingie kwa makundi makundi wampongeze Ali kwa cheo hicho na wamsalimie kwa maamkizi ya kuwa kwake Amirul-Muuminina.watu wakafanya walichoamuriwa, na miongoni mwa waliompongeza Amirul-Muuminina Ali bin Abi Talib katika tukio hili ni Abubakar na Umar.


Walimjia wawili hawa (Abubakar na Umar) wakamwambia hongera hongera ewe Mwana wa Abu Talib umepambazukiwa na kumekuchwea hali ya kuwa ni mtawala wetu na ni mtawala wa kila muumini mwanamume na mwanamke.[42] Na pindi Has-san bin Thabit aliyekuwa mshairi wa Mtume (s.a.w.) alipotambua furaha ya Mtume kuhusiana na siku hiyo alisema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unaniruhusu niseme beti za shairi utazozisikiliza kuhusiana na mahala hapa." Mtume akasema, "Kwa baraka za Mwenyezi Mungu sema, (ewe) Has-san hukuacha kuwa ni mwenye kuungwa mkono na roho tukufu muda wote unapotunusuru kwa ulimi wako". Basi akasoma ushairi ufuatao: "Siku ya Ghadir Mtume wao anawaita hapo Khum, Hebu sikiliza Mtume anatangaza..." Mpaka mwisho wa beti ambazo wamezitaja wanahistoria.[43]


Lakini pamoja na yote hayo. hakika Maquraishi walijichagulia wenyewe (Kiongozi wao) na wakapinga Utume na Ukhalifa kuwa kwa bani Hashim wasije jifakharisha mno kwa watu wao, hayo ni kama alivyobainisha Umar bin Al-Khattab kwa Abdallah bin Abbas katika mazungumzo yaliyofanyika baina yao:[44] Taz: Tarikhut-Tabari Juz. 5 uk. 31, Tarikhu Ibnul-Athir Juz. 3 uk. 31 na Shark Nahjul-Balagha ya Ibn Abil-Hadi Juz. 2 uk. 18. Basi hapakuwa na yeyote aliyesherehekea sikukuu hiyo baada ya kutajwa kwake kwa mara ile ya kwanza ambayo Mtume alisherehekea. Na iwapo kama walijisahaulisha tamko la Ukhalifa (alilolitamka Mtume) na wakalififisha akilini mwao na haukupita muda isipokuwa miezi miwili (tangu kutamkwa) pamoja na muda huo (mchache) hapana yeyote aliyezungumzia, ni vipi kumbukumbu ya Ghadir itakumbukwa baada ya kupita mwaka kamili?


Na ilipita miaka mingi mpaka pale haki iliporejea kwa mwenye nayo baada ya robo karne, hapo ndipo Imam Ali akaifufua upya siku hiyo baada ya kuwa ilikuwa karibu kuzikwa, hapa ilikuwa katika ukumbi wa Msikiti wa Al-Kuufah Iraq, wakati Imam Ali alipowataka Masahaba wa Muhammad (s.a.w.) wakiwemo wale waliohudhuria sikukuu ya Ghadir wasimame na washuhudie mbele ya watu baia ya Ukhalifa (iliyofanyika siku hiyo) wakasimama Masahaba thelathini, kumi na sita miongoni mwao walikuwa ni mashujaa wa Badri (wote) wakashuhudia.[45] Ama yule aliyeficha ushahidi huo na kudai kuwa amesahau kama alivyofanya Anas bin Malik ambaye ilimsibu dua ya mja mwema kwani hakuwahi kusimama toka mahala alipokuwa ila alipatwa na maradhi ya mbaranga, basi akawa siku zote hulia na kusema, yamenisibu maombi ya mja mwema kwani nilificha ushahidi wake.[46] Kwa tendo hilo (la ushahidi) Abul-Hasan aliisimamisha hoja juu ya umma huu, na tangu zama hizo mpaka leo hii na mpaka Qiyama Mashia wanasherehekea kumbukumbu ya siku ya Ghadir na kwao ni sikukuu kubwa. Ni kwanini isiwe hivyo hali ya kuwa ndiyo siku ambayo Mwenyezi Mungu alitukamilishia dini na akatutimizia neema yake na kuturidhia Uislamu kuwa ndiyo dini yetu, nayo ni siku yenye utukufu mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini.


Baadhi ya wanachuoni wa Kisunni wameeleza toka kwa Abu Huraira kwamba amesema: "Pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alipoushika mkono wa Ali na akasema, yeyote ambaye mimi nilikuwa mtawalia mambo yake basi Ali ni mtawalia mambo yake... mpaka mwisho wa khutba Mwenyezi Mungu aliiteremsha "Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimeitimiza neema yangu kwenu na nimewaridhia Uislamu kuwa ndiyo dini yenu". Abu Huraira amesema: "Ilikuwa ni siku ya Ghadir Khum, basi yeyote mwenye kufunga siku ya kumi na nane mfunguo tatu huandikiwa thawabu za miezi sitini". Taz: Al-Bidaya Wan-Nihayah, Juz. 5 uk. 214.


Ama riwaya za Mashia kutoka kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) zinazohusu ubora wa siku hiyo ni nyingi mno, basi kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu aliyetujaalia kuwa miongoni mwa wanaoshikamana na utawala wa Amirul-Muuminina Ali (a.s.) na wenye kusherehekea sikukuu ya Ghadir. Kwa kufupisha uchambuzi huu ni kwamba hadithi ya Ghadir isemayo; "Yeyote ambaye mimi nilikuwa natawalia mambo yake basi huyu Ali ni mtawalia mambo yake, ewe Mwenyezi Mungu muunge atakayemuunga, na umpinge atakayempinga, na umsaidie atakayemsaidia na umdhalilishe atakayemdhalilisha na izungushe haki anako zungukia". Hadithi hii au bora ni zaidi kusema, "Ni tukio kubwa la kihistoria ambalo umma wa Kiislamu umeafikia na katika kulinakili, na hapo kabla tumetajiwa wanachuoni mia tatu na sitini wa Kisunni na wengine wa Kishia zaidi ya hao wa Kisunni".


Na yeyote atakaye kutafiti na kupata ziyada, basi ni juu yake kuangalia Kitabul-Ghadir cha Al-Allamah Al-Amin. Baada ya haya tuliyoyaeleza basi siyo ajabu umma wa Kiislamu kugawanyika Masunni na Mashia.Kundi la kwanza limeshika maana na misingi ya Shuraa,yaani mashauriano yaliyofanyika katika klabu ya Bani Saidah, na kuyabadilisha matamko ya wazi (aloyatoa Mtume) na hivyo kwenda kinyume na kile ambacho wapokezi wa hadithi ya Ghadi wameafikiana pia maelekezo mengine (ya Mwenyezi na Mtume). Kundi la pili halikubali badali na limewapa baia Maimamu kumi na wawili kutoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.) na halikutaka kinyume chao. Ukweli halisi ulivyo ni kwamba, mimi kila ninapoyachunguza Madhehebu ya Kisunni hasa juu ya hili suala la Ukhalifa ninakuta limejengeka kwenye msingi wa dhana na Ij-Tihadi, kwani kanuni ya uchaguzi haina dalili madhubuti ndani yake na hiyo ni kwa kuwa yule mtu tunayemchagua leo hii (tunamuona) ni bora kuliko mwingine na hali sisi hatujui khiyana ya macho na yaliyofichwa nyoyoni, na kwa kuwa sisi wanaadamu ukweli ulivyo tumeumbwa na sifa ya upendeleo chuki na ubinafsi uliomo ndani ya nafsi zetu na umbile hili linaweza kuitumia nafasi yake ikiwa suala la kumchagua mtu litawakilishwa kwetu.


Na mas'ala niliyoyatoa siyo jambo la kubuni au la kutia chumvi, kwani yeyote atakayeifuatilia fikra hii, yaani fikra ya (watu) kumchagua Khalifa atakuta kwamba msingi huo unaopigiwa ngoma haukufanikiwa na kamwe hauwezi kufanikiwa. Huyu hapa Abubakr ambaye ndiye kiongozi wa hiyo Shuraa, pamoja na kuwa yeye aliupata Ukhalifa kwa uchaguzi wa kushauriana, tunamuona yeye wakati alipokaribia kufariki haraka sana alimteuwa Umar bin Al-Khatab awe Khalifa wake bila ya kutuma njia ya mashauriano.

Na Umar bin Al-Khatab ambaye alishiriki kuujenga Ukhalifa wa Abubakr tunamuona baada ya kufariki Abubakr anawatangazia waislamu kwamba, "Baia ya Abubakar ilikuwa ni jambo lililopatikana ghafla Mwenyezi Mungu aliwakinga Waislamu kutokana na shari yake".[47]
Kisha baada ya hayo tunamuona Umar wakati aliposhambuliwa na akayakinisha kwamba ajali yake imekaribia alichagua watu sita ili wamchague mmoja miongoni mwao awe Khalifa na hali ya kuwa anafahamu fika kwamba kikundi hiki pamoja na uchache wao watahitilafiana licha ya kuwa wao ni masahaba wa mwanzo kuingia katika Uislamu na ni wachamungu, bila shaka upendeleo wa kibinaadamu utajitokeza, hataepukana nao isipokuwa yule aliye Maasum, na kwa ajili hiyo tunamuona eti kwa kuzuwia hitilafu anaupa uzito upande wa Abdur-Rahman bin Auf akasema: "Iwapo mtahitilafiana basi kuweni upande ule alioko Abdur-Rahman". na baada ya hapo wakamchagua Imam Ali ili awe Khalifa lakini wakamuwekea sharti kuwa awahukumu kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake na Sunna ya Masheikh wawili yaani Abubakar na Umar.


Imam Ali alikubali kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wa Mungu na alikataa kuhukumu kwa mujibu wa Sunna ya Masheikh wawili.[48] Ama Uthman yeye alilikubali sharti hili nao wakampa baia ya Ukhalifa na ndipo Imam Ali aliposema: "Oh! haulingani ukhalifa wa Mwenyezi Mungu na Shuraa! ni lini imeingia shaka kati yangu na Khalifa wa kwanza miongoni mwao, mpaka imefikia nilinganishwe na watu kama hawa lakini mimi nilikwenda nao kama walivyokwenda, bali kuna mtu miongoni mwao ameelemea kwenye chuki zake, na mwingine kuelemea kwenye ujamaa wake".[49]
Ikiwa hawa ndiyo wateule miongoni mwa Waislam, na ni watu makh-susi kati ya watu wanaotegemewa,ni vipi upendeleo unawachezea na wanakuwa na chuki na ubinafsi kati yao?


Hali hii iko wazi kwani Abdur-Rahman bin Aufi hatimaye alijutia uchaguzi alioufanya, akamkasirikia Uthman na akamtuhumu kwa kwenda kinyume cha ahadi yalipotokea yaliyotokea, na Masahaba wakubwa wakamjia wakamwambia: "Ewe Abdur-Rahman hii ndiyo kazi iliyofanywa na mikono yako". Akawaambia: "Nilikuwa simdhanii kwa haya (ayatendayo) lakini namuapa Mwenyezi Mungu kwamba kamwe sitamsemesha". Kisha Abdur-Rahman bin Auf alifariki hali ya kuwa amemkasirikia Uthrnan, mpaka wamesimulia kwamba Uthman alikwenda kumzuru Abdur-Rahman alipokuwa mgonjwa basi Abdur-Rahman aligeuzia uso wake ukutani na hakumsemesha.[50]


Hatimaye yakawa yaliyokuwa, mapinduzi yakasimama na mwishoni mwake Uthman akauawa umma ukarejea tena baada ya hapo kwenye uchaguzi na safari hii wakamchagua Ali. Lakini waja wa Mwenyezi Mungu wana kila hali ya kusikitikiwa, kwani Dola ya Kiislamu ilikwisha vurugika ikawa ni uwanja wa wapinzani na wenye tamaa ya kukalia cheo cha Ukhalifa kwa thamani yeyote ile na kwa njia yeyote ile japokuwa kwa kuuwa watu wasio na makosa, hukmu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake zikawa zimebadilishwa kwa muda huo wa miaka ishirini na mitano, hapo Imam Ali (a.s.) alijikuta yuko katikati ya bahari yenye mawimbi yanayopigana yenyewe kwa yenyewe tena kwenye kiza nene na upepo mkali.


Hivyo basi alimaliza Ukhalifa wake katika vita zilizomwaga damu, vita ambavyo vililazimishwa na wapinzani na waliotoka katika dini, na hakutoka kwenye vita isipokuwa kwa kuuawa kishahidi hali ya kuwa akiusikitikia umma wa Muhammad. Mwana wa muachwa huru Muawiyah bin Abisufiyan aliingiwa na tamaa ya Ukhalifa na walio kama yeye kama kina Amri bin-Al-as na Mughirah bin Shuubah na Mar-wan bin Al-Hakam na wengineo wengi, na hakuna kilichowafanya watu hawa wathubutu kufanya hayo waliyoyafanya isipokuwa ni ile fikra ya Shuraa na uchaguzi.

Umma wa Muhammad ukawa umezama ndani ya bahari ya damu na watu wapumbavu na watwevu ndio wakawa wanauamulia umma huu hatima yake na baadaye Shuraa ikageuka na kuwa Ufalme mfano wa utawala wa Kaisari na Kisra. Basi kipindi hicho kikapita, kipindi ambacho wamekipa jina la Ukhalifa uliyoongoka na kwa jina la Ukhalifa huo wakaitwa Makhalifa wanne kuwa ndiyo waongofu, lakini ukweli ulivyo ni kuwa hata hawa wanne hawakuwa Makhalifa kwa kuchaguliwa na kwa mashauriano isipokuwa Abubakar na Ali, na tukimtoa Abubakar kwani baia yake ilikuwa ya kushitukiza bila kutegemea kwa mujibu wa usemi wa Umar ambapo izingatiwe kuwa halikuhudhuria kwenye baia hiyo "Kundi la upinzani" kama isemwavyo leo hii nalo ni la Ali na Bani Hashim na wale wenye mtazamo kama wa Bani Hashim, hakuna anayebakia ambaye baia yake ilifungamana na njia ya mashauriano na uchaguzi isipokuwa Ali bin Abi Talib ambaye Waislamu walimbai atake asitake pamoja na hayo baadhi ya masahaba waligoma lakini Imam Ali hakuwalazimisha wala kuwatishia.


Mwenyezi Mungu alitaka Ali bin Abi Talib awe khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa tamko litokalo kwa Mwenyezi Mungu na kwa uchaguzi wa Waislamu, na umma wa Kiislamu wote Masunni na Mashia wamekubaliana juu ya ukhalifa wa Ali na wamehitilafiana juu ya ukhalifa wa wengine kama ambavyo jambo hili liko wazi. Mimi nasema; "Wanafaa kusikitikiwa waja (wa Mwenyezi Mungu) lau wao wangekubali alichowachagulia Mwenyezi Mungu basi wangeneemeka kila upande na Mwenyezi Mungu angewateremshia baraka nyingi kutoka mbinguni na leo hii Waislamu wangekuwa ndiyo mabwana wa ulimwengu na ni viongozi wake kama alivyowatakia Mwenyezi Mungu lau wangelimfuata" "Nanyi ni watukufu ikiwa ni wenye kuamini."


Lakini ibilisi aliyelaaniwa, adui yetu aliyedhahiri alisema kumwambia Mwenyezi Mungu: "Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawakalia (waja wako) katika njia yako iliyonyooka (Ili niwapoteze) kisha nitawaijia kwa mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao na wengi katika wao hutawakuta wenye kukushukuru" (Qur'an, 7:16-17). Basi mwenye akili na aiangalie hali ya Waislamu katika ulimwengu, wao ni madhalili hawawezi chochote wanakimbia nyuma ya madola mengine na wanaitambua Israel wakati yenyewe inakataa kuwatambua na hata kidogo haiwaruhusu kuingia katika Qudsi ambayo sasa imekuwa ndiyo mji wake mkuu, na unapowaangalia Waislamu utawaona wako chini ya huruma ya Amerika na Urusi, na kwa kweli umasikini umeyatafuna mataifa yao na wanauawa kwa njaa na maradhi wakati mbwa wa Ulaya wanakula aina mbali mbali za nyama na samaki, "Lahaula wala Quwwata IllaBillah".

Bibi Fatma (a.s.) mbora wa wanawake alieleza wakati alipomgombeza Abubakr kisha akatowa hotuba kwa wanawake wa Muhajirina na Answari na mwisho wa hotuba hiyo alieleza habari ya hatima ya umma huu akasema, "Ama naapa hatua ya mwanzo imefanywa tungoje huenda ikaleta matunda wamefanya mambo yaliyoleta maangamizi, hapo watakuwa hasarani watenda batili na watajua watakaofuatia maovu yaliyowapata wa mwanzo, kisha furahieni dunia yenu na kuweni na yakini kuwa fitna ihangaishayo nyoyo itakuja, na tazamieni upanga mkali, na ukali wa muamizi dhalimu na vurugu itakayoenea kila mahali na ubinafsi wa wadhalimu utaacha hali yenu ya ulinzi dhalili na kuangamiza umoja wenu, hasara iliyoje kwenu!Mmekuwa hamtambui je tukulazimisheni kuyatambua hayo hali yakuwa hampendi?[51]

Alisema kweli mbora wa wanawake kwa aliyo yaeleza naye ni bintiye Mtume, Mtume ambaye ni chimbuko la ujumbe usemi wake bi Fatma umejaa maelezo kuhusu hali ya baadaye ya maisha ya umma huu toka pale umma ulipogeuka nyuma. Basi nani ajuaye huenda yanayotazamiwa kutokea ni mabaya mno kuliko yaliyopita, hayo ni kwa kuwa waliyachukia aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu wakaharibu mtendo yao.6
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

UCHAMBUZI WA MADA Madda muhimu katika uchambuzi: Imebakia madda moja muhimu ndani ya uchambuzi wote huu, madda ambayo inataka kuangaliwa kwa makini na kusomwa, na huenda hiyo pekee ndiyo kikwazo ambacho huwachemua wapinzani pale wanaposhinikizwa kwa hoja nzito. Utawaona wanashangaa na kutokuamini ya kuwa Masahaba wapatao laki moja walihudhuria kutawazwa kwa Imam Ali (kuwa Khalifa wa Mtume) na hatimaye hao hao Masahaba wakaafikiana wote kumkhalifu Imam Ali na kumpuuza na miongoni mwao wamo Masahaba wakubwa.

Hali hii (ya kushangazwa kwa wapinzani) imepata kunitokea mimi mwenyewe wakati nilipoingia kikamilifu ndani ya utafiti, sikuamini na haiwezekani kwa mtu yeyote kuamini pindi tukio hili linapoaridhiwa kama lilivyo, lakini wakati tunapolisoma tukio hili kwa pande zote basi kule kushangaa kunaondoka kwani hali halisi haiko kama tunavyoitazamia sisi au kama wanavyoiaridhi Masunni (ya kuwa) haiwezekani Masahaba laki moja wakaenda kinyume na amri ya Mtume, hivyo basi ilikuwaje mambo yakatokea kama yalivyotokea?

Kwanza Siyo kila aliyehuduria Baia ya Ghadir alikuwa akiishi Madina, bali ilikuwa kama ambavyo hali halisi ilivyokuwa kwamba kwa kiasi kikubwa itakuwa ni watu elfu tatu au Nne tu miongoni mwa Masahaba hao ndiyo waliokuwa wakiishi Madina.Na tutakapofahamu ya kwamba wengi wa hawa walikuwa ni watumwa na walioachwa huru na wanyonge ambao walimfikia Mtume (s.a.w.) kutoka sehemu mbali mbali na hapo Madina hawakuwa na uwenyeji wala jamaa (kwa mfano watu wa As-Safah) basi haitabakia isipokuwa nusu yao yaani watu elfu mbili tu, na hata hawa nao ni watiifu kwa viongozi wa makabila na muongozo wa kidugu ambao ndiyo wanaohusika nao na Mtume aliwakubalia (kuwa watiifu kwa viongozi wao) kwani ulipokuwa ukimfikia ujumbe wa kabila fulani, Mtume (s.a.w.) humtawalisha juu yao kiongozi wao, na kwa ajili hiyo ndiyo tumekuta katika Uislamu Istilahi ya kuitwa kwao kuwa ni Ahlul-Hilli wal-Iqdi, watu wanaotumainiwa kutowa maamuzi katika jamii au nchi.


Kadhalika tunapoutazama mkutano wa Saqifah ambao ulikutana mara tu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.), tunawakuta waliohudhuria ambao waliuthibitisha uchaguzi wa Abubakar kuwa ni khalifa, idadi yao haizidi watu mia moja kwa makadirio ya juu, kwani katika Ansari ambao ndiyo wenyeji wa Madina hawakuhudhuria isipokuwa viongozi wao kama ambavyo Muhajirina ambao ni wenyeji wa Maka waliohama pamoja na Mtume (s.a.w.) hawakuhudhuria isipokuwa watu watatu au wanne wakiwakilisha Maquraishi. Hali hii itoshe basi kuwa ni dalili ya kupima ukubwa wa hiyo Saqifah ikoje, Saqifah ambayo ilikuwa haina nafasi ya kutosha, kwani haikuwa inakosa kuwa karibu katika kila nyurnba.

Kwa hiyo haikuwa uwanja wa maadhimisho wala siyo jumba la mikutano, na tunaposema kuwa watu mia moja walihudhuria hapo Saqifah bani Saida basi idadi hiyo sisi ndiyo tunaoizidisha ili tu, mwenye kutafiti aweze kufahamu kwamba wale Masahaba laki moja hawakuwepo wala hata hawakusikia mazungumzo yalivyofanyika ndani ya Saqifah isipokuwa baada ya muda mrefu kupita, .kwani hapo zamani hapakuwa na mawasiliano ya anga wala simu au Satellite.

Na baada ya mabwana wakubwa hawa kuafikiana juu ya Abubakar pamoja na upinzani wa bwana wa Kiansari Saad bin Ubbadah ambaye ni kiongozi wa kabila la Khazraj na mwanawe Qais, lakini wengi mno miongoni mwao (kama isemwavyo hii leo) walipitisha makubaliano hayo na kumpa Abubakar mkono wa Baia, wakati ambapo Waislamu wengi hawakuwepo hapo Saqifah, na baadhi yao walikuwa wameshughulika kumuandaa Mtume (s.a.w.) kwa mazishi au walihamanika kutokana na khabari za kifo chake, ambapo Umar bin Al-Khatab naye alikuwa amewatisha na kuwatia khofu iwapo watasema kuwa Mtume amefariki. Taz: Sahih BukhariJuz. 4 -195.

Zaidi ya hayo wengi wa Masahaba wa Mtume walikuwa amewateua wawemo ndani ya Jeshi la Usamaha na wengi wao walikuwa wameweka kambi mahala paitwapo Jorfi wakiwa tayari kwenda vitani na jeshi la Usamah hawakuwepo Mtume alipofariki wala hawakuhudhuria mkutano wa Saqifah. Basi je, inaingia akilini baada ya haya yaliyotokea kwamba mtu fulani katika kabila au ukoo kumpinga kiongozi wake kwa lile alilolipitisha na hasa inapokuwa hilo alilolipitisha lina ubora na utukufu mkubwa ambao kila kabila linaukimbilia? Ni nani ajuwaye ya kwamba huenda siku moja naye atawatawalia Waislamu wote, maadamu mwenye haki hiyo kisheria amekwisha tupwa mbali na mambo sasa yanakwenda kwa kushauriana wanabadilishana kwa kuachiana, basi ni kwa nini wasilifurahie hilo, na ni kwa nini wasiliunge mkono?


Pili Ikiwa wenye uwezo wa kuamua ni wakaazi wa Madina na wamepitisha jambo fulani, basi watu walio mbali katika sehemu mbali mbali za bara Arabu hawawezi kupinga na hali ya kuwa hawajui yanayopita wakati hawapo kwani vifaa vya mawasiliano kwa zama hizo vilikuwa ni vile vya kizamani kisha wao walikuwa wakifahamu kwamba wakazi wa Madina ndiyo waliokuwa wakiishi na Mtume wa Mwenyezi Mungu hivyo basi hao ndiyo wajuao mno mambo mapya miongoni mwa hukmu, kwani huenda ukashuka Wahyi wakati wowote au siku yoyote. Kisha kama kuna kiongozi wa kabila lolote lililo mbali na makao makuu basi jambo la Ukhalifa kwake si muhimu sana sana iwapo Abubakr atakuwa Khalifa au Ali au mtu mwingine yeyote, kwani watu wa Maka ndiyo wajuao zaidi utaifa wao, na cha muhimu kwao ni kubakia kwenye uongozi wa ukoo wake ambapo hakuna anayemkera katika uongozi huo.


Basi ni nani ajuwaye kwamba huenda baadhi ya watu waliulizia juu ya jambo hilo (la Ukhalifa) na walitaka kufahamu mambo yalivyokwenda lakini vyombo vya mtawala viliwanyamazisha sawa iwe kwa njia ya kuwapa tamaa ya mali au vyeo au vitisho, na huenda kisa cha Malik bin Nuwairah ambaye alikataa kutoa zaka kwa Abubakr ni utokea jambo hilo. Na yeyote mwenye kufuatilia matukio hayo yaliyotokea katika vita ya wanaokataa kutoa zaka katika zama za Abubakr atakuta kuna kupingana (kwa maelezo), wala hawezi kutosheka kwa maelezo yaliyoelezwa na baadhi .ya wanahistoria kwa lengo la kulinda heshima ya Masahaba na hasa wale watawala.


Tatu Kiini cha tatizo hili ni kule kushitukizwa ghafla kupatikana kwa Khalifa, hili ni jambo lililochangia mno kukubalika kwa kile ambacho leo kinaitwa kuwa "Hali halisi iliyopo". Kwani mkutano wa Saqifah ulifanyika ghafla kwa kuwashitukiza baadhi ya Mashaba ambao walikuwa wakimshughulikia Mtume (s.a.w.), na miongoni mwao alikuwa Imam Ali na Abbas na wengine miongoni mwa Bani Hashim, Miq-dad, Salman, Abu Dharri, Ammar, Zubair na wengineo wengi. Ama wale waliokuwa Saqifah walipotoka huko hali ya kuwa wakimshangilia Abubakr walielekea msikitini huku wakitoa mwito kwa watu wafanye baia ya jumla na watu wakaipokea baia hiyo kwa wingi watake wasitake kipindi hicho Imam Ali na wafuasi wake walikuwa hawajamaliza wajibu wao Mtukufu ambao tabia zao (mwenendo wao) mwema uliwalazimisha (wautimize) basi haikuwezekana kwao kumuacha Mtume (s.a.w.) bila ya kumkosha, kumvisha sanda, kumtayarisha na kumzika eti badala yake wakimbilie Saqifah kugombea Ukhalifa.


Walipomaliza wajibu wao huo, mambo yalikuwa yamekwisha kamilika kwa Abubakr na yeyote mwenye kwenda kinyume na baia hiyo akawa anahesabiwa kuwa ni miongoni mwa watu wenye fitna ambaye anabomoa umoja wa Waislamu, hivyo ni wajibu kwa Waislamu kumpinga au hata kumuuwa ikiwa itabidi, na ndiyo maana tunamuona Umar alimuonya Saad bin Ubbadah kuwa atauawa pale alipokataa kumbai Abubakr, Umar akasema, "Muuweni hakika yeye ni mtu wa fitna"[52] na baada ya hapo Umar aliwatishia wote waliobaki ndani ya nyumba ya Ali ya kuwa atachoma moto nyumba hiyo na wote waliomo humo. Tukishakufahamu vyema maoni ya Umar bin Al-Khatab kuhusu baia tutatambua mengi baada ya hapo miongoni mwa mambo yanayotatanisha.


Kwa hakika Umar anaona kuwa baia inatosha kusihi pale mmoja miongoni mwa Waislamu anapowahi, basi hapo inakuwa ni lazima kwa wengine kumfuata na yeyote atakayeasi miongoni mwao huyo atakuwa ametoka nje ya mshikamano ya Waislamu na ni wajibu kumuuwa. Basi hebu na tumsikilize yeye mwenyewe hasa kuhusu baia, kama alivyoeleza Bukhar ndani ya Sahih yake juzuu ya nane ukurasa wa ishirini na nane, Babu Rajmi Al-Hubla Minaz-Zinaa Idha-Ah-Sanat amesema: akisimulia yale yaliyotokea ndani ya Saqifah. "Basi fujo ikazidi na sauti zikapaa mpaka nikatishika kuwa kutatokea kuhitilafiana, nikasema, Ewe Abubakr kunjua mkono wako, Abubakar akakunjua mkono wake nikambai nao muhajirina wakambai[53] Ansari (nao wakambai) na tukamruka Saad bin Ubbadah, akasema msemaji miongoni mwao, "Mmemuuwa Saad bin Ubbadah" Mimi nikasema:

"Mwenyezi Mungu amuuwe Saad bin Ubbadah" Umar akasema: "Wallahi sisi hatujakutana na jambo gumu katika yote tuliyohudhuria kuliko kumbai Abubakar, tulichelea kuwa hawa jamaa tukiwaacha bila kupitisha baia, basi watambai mtu miongoni mwao baada yetu, hivyo imma tuwape madaraka, jambo ambalo hatulikubali, au tuwapinge itokee uharibifu, (naonya) yeyote atakayetoa baia bila ya kushauriana na Waislamu asifuatwe yeye wala yule aliyembai ili asiuawe. Basi jambo lililovyo kwa Umar siyo uchaguzi wala hiyari wala mashauriano, bali inatosha pale Mwislamu mmoja anapoiwahi baia hiyo iwe ni hoja kwa wengine na ndiyo maana alimwambia Abubakr, "Kunjua mkono wako Ewe Abubakar," na Abubakr naye akakunjua mkono wake akambai bila ya mashauriano tena haraka haraka kwa kuchelea kutanguliwa na mwingine na kwa hakika Umar amekwisha ieleza rai hii pale aliposema:

"Tulichelea lau tutawaacha watu hawa bila ya kuipitisha baia, watambai mtu miongoni mwao baia yetu (Umar aliwachelea Maansar wasimtangulie wakambai mtu miongoni mwao), na kinachomuongezea ufafanuzi zaidi ni pale anaposema: "Basi imma tuwape Baia jambo ambalo hatulikubali na au tuwapinge patokee uharibifu."[54]


Na ili tuwe waadilifu katika maamuzi na wenye kuchunguza kwa undani, inatupasa tukiri kwamba Umar bin Al-Khatab alibadilisha mtazamo wake kuhusu baia mwishoni mwa uhai wake na hilo ni pale mtu mmoja alipomjia Umar mbele ya Abdur-Rahman bin 'Auf katika Hijja yake ya mwisho aliyohiji, yule mtu akamwambia: "Ewe Amirul-Muuminina unayo habari kuwa fulani anasema, bila shaka Umar akifa hakika nitambai fulani kwani wallahi baia ya Abubakar haikuwa isipokuwa kwa kushitukiza tu na ilitimia". Umar alikasirika na kwa ajili hii alisimama akawahutubia watu alipokuwa akirudi Madina, miongoni mwa aliyoyasema katika khutba yake ni haya yafuatayo:
"Kwa hakika nimepata habari kwamba kuna asemaye miongoni mwenu kuwa, Wallahi lau Umar atakufa nitambai fulani, basi na asijidanganye mmoja wenu kusema kuwa baia ya Abubakar ilikuwa hivyo lakini Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake.."[55] Kisha Anasema: "Yeyote mwenye kumbai mtu bila mashauriano kutoka kwa Waislamu, basi huyo asipewe baia yeye wala huyo aliyembai kuhofia asije uwawa.[56]


Basi laiti Umar angekuwa na mtazamo huu siku ya Saqifah na asiwalazimishe Waislamu kumbai Abubakr ambako kulikuwa kwa kushitukiza, na Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake kama alivyoshuhudia yeye mwenyewe, lakini imekuwaje Umari awe na rai hii mpya katika mtazamo huu mpya, hakika atakuwa amejihukumia kifo yeye mwenyewe na rafiki yake (Abubakr) kwa kuwa kwenye mtazamo wake mpya anasema: "Yeyote mwenye kumbai mtu bila ya mashauriano toka kwa Waislamu basi asipewe Baia yeye wala huyo aliyembai ili asije uwawa."

Imebakia juu yetu kufahamu ni kwa nini Umar alibadilisha maoni yake mwishoni mwa uhai wake pamoja na kwamba yeye anafahamu mno kuliko mwingine ya kuwa mtazamo wake mpya unatengua baia ya Abubakar iliyotimia bila ya mashauriano toka kwa Waislamu na ilikuwa ni baia ya kushitukiza? Pia mtazamo wake huu mpya unatengua baia yake yeye aliyopewa, kwani aliupata ukhalifa kwa tamko la Abubakar wakati wa kufa bila ya makubaliano kutoka kwa Waislamu, kiasi baadhi ya masahaba walikwenda kwa Abubakar wakamkemea kwa kuwatawalishia mtu msusuavu tena mgumu wa tabia.[57] Na Umar alipotoka ili awasomee watu maandiko ya Abubakr kuna mtu alimuuliza: "Ewe Baba Hafs kuna nini ndani ya waraka huo?" Umar akasema, Sijuwi, lakini mimi nitakuwa wa kwanza kusikiliza na kutii." yule mtu akasema: "Lakini Wallahi mimi najua kilichomo, wewe ulimtawalisha (Abubakar) kipindi cha mwanzo naye amekutawalisha kipindi hiki".


Taz: Al-Imam Was-Siyasah cha Ibnu Qutaibah Juz. 1 uk. 25Mlango unaohusu maradhi ya Abubakri na kumtawalisha kwake Umar. Kauli hii inafanana na kauli ya Imam Ali kumwambia Umar pale alipomuona anawalazimisha watu kwa nguvu wambai Abubakr akasema "Nifanye jambo ambalo wewe utakuwa na hisa (wanitaka) leo nilikazanie jambo lake ili kesho akurudishie"? Taz: Al-Imamah Was-Siyasah cha ibnu Qutaiba Juz. 1 uk. 18. Cha muhimu ni kufahamu ni kwa nini Umar alibadilisha mtazamo wake kuhusu Baia?

Mimi ninakurubia kuamini kwamba, wakati alipowasikia baadhi ya Masahaba wanataka kumbai Ali bin Abi Talib baada ya kufa Umar jambo ambalo yeye Umar kamwe hakubaliani nalo, kwa kuwa yeye ndiye aliyezipinga maagizo ya Mtume yaliyobayana, na akapinga Mtume (s.a.w.) asiwaandikie yale maandiko[58] kwa kuwa yeye alilifahamu lengo lake kiasi kwamba akamtuhumu Mtume kuwa anaweweseka na akawatisha watu wasiseme kuwa Mtume amekufa[59] yote hayo ni kwa sababu wasije wakawahi kumbai Ali. Umar alitilia mkazo baia ya Abubakr na akawalazimisha watu kwa nguvu waikubali baia hiyo na kisha kumuonya kila atayepinga kuwa atamuua[60] ili tu kumtenga mbali Ali na ukhalifa.


Hivi itawezekana Umar aridhie aseme msemaji kwamba fulani atapewa baia lau Umar atakufa? Hasa pale msemaji huyu ambaye jina lake limebakia kuwa halijulikani na hapana shaka kuwa alikuwa miongoni mwa Masahaba wakubwa? Msemaji huyu alitumia hoja ya kitendo alichokitenda Umar mwenyewe alipombai Abubakar pale anaposema: "Wallahi Baia ya Abubakr haikuwa isipokuwa ya kushitukiza na ikatimia", yaani pamoja na kuwa ilitokea kwa kuwashitukiza Waislamu na bila kupata ushauri wao lakini ilitimia na likawa jambo lililothibitika, kwa hiyo ilifaa kwa Umar kulifanya kwa Abubakr kwa nini isifae kwake kulifanya yeye mwenyewe kwa njia ile ile kwa mwingine? Na hapa tunaona kwamba ibn Abbas na Abdur-Rahman bin Auf na Umar bin Khatab wanakwepa kulitaja jina la huyu msemaji kama ambavyo wanakwepa kulitaja jina la mtu anayetaka kupewa baia msemaji huyu. Na ilipokuwa wawili hawa wanao umuhimu mkubwa kwa Waislamu, tunamuona Umar alikasirika kwa usemi huu na haraka katika Ijumaa ya kwanza aliwahutubia watu na akaieleza maudhui ya Ukhalifa itakavyokuwa baada yake na akawaonesha maoni yake mapya kuhusiana na Ukhalifa, ili azuwie njia ya huyu anayetaka kurudisha ile ghafla iliyokwisha tokea kwani njia hiyo itamnufaisha mgomvi wake, kwani kwa kupitia uchunguzi tumefahamu kuwa usemi huo haukuwa ni maoni ya fulani tu peke yake, bali ulikuwa ndiyo mtazamo wa Masahaba wengi, na ndiyo maana Bukhari anasema: "Umar alichukia na kisha akasema bila shaka apendapo Mwenyezi Mungu mimi nitasimama usiku huu miongoni mwa watu niwaonye hawa ambao wanataka kuwapora mambo yao..." [61]


Basi kubadilisha kwa Umar mtazamo wake kuhusu Baia ilikuwa ni kuwapinga hawa ambao wanataka kuwapokonya watu mambo yao na wambai Ali, na hili ni jambo ambalo Umar hakubaliani nalo kwani yeye anaitakidi kuwa Ukhalifa ni miongoni mwa mambo ya watu na siyo haki ya Ali bin abi Talib, na itikadi hii itapokuwa ni sahihi, basi ni kwa nini yeye Umar aliruhusu kuwapokonya watu mambo yao baada ya kufariki Mtume (s.a.w.) na haraka haraka akambai Abubakar bila ya makubaliano na Waislamu. Na msimamo wa Abu Hafs (Umar) dhidi ya Abul-Hasan (Ali) unaeleweka na ni mashuhuri mno, nao ni kumtenga Ali kwenye utawala kwa kutumia njia yoyote inayowezekana.

Na matokeo haya hatukuyafahamu kutokana na hotuba yake (Umar) iliyotangulia hapo kabla peke yake, lakini yeyote mwenye kufuatilia historia atafahamu kuwa Umar bin Al-Khatab alikuwa ndiye mtawala mtendaji hata katika Ukhalifa wa Abubakr na ndiyo maana tunamuona Abubakr anamuomba Usamah bin Zaid amuachie Umar bin Al-Khatab ili amsaidie kuhusu suala la Ukhalifa kama alivyoeleza hilo Ibn Saad ndani ya Tabaqat yake na pia wanahistoria wengi walioelezea jeshi la Usamah - pamoja na hayo tunamuona Ali bin Abi Talib anabakia mbali na majukumu, hawakumpa cheo chochote wala utawala wowote wala kumpa uamiri wa jeshi lolote lile na wala hawakumuamini kuwa mweka hazina na yote haya ni kwa kipindi cha Ukhalifa wa Abubakr, Umar na Uthman, nasi sote twamjua Ali bin Abi Talib ni nani.


Cha kushangaza kuliko yote haya ni kuwa, sisi tunasoma ndani ya vitabu vya historia kwamba kifo kilipomfikia Umar alisikitika kwamba lau Abu Ubaidah bin Al-Jarrah au Salim Huru wa Abu Hudhaifah wangekuwa hai angewatawalisha baada yake. Lakini hapana shaka Umar alikumbuka kuwa hapo kabla alikwisha badilisha mtazamo wake juu ya baia kama hii na akaiona kuwa ni ya kushitukiza na ni kupokonya mambo ya Waislamu, basi hapana budi kwake aweke njia mpya kuhusu baia ili kati kwa kati asije yeyote akafaulu kumbai amuonaye kuwa anafaa na kuwalazimisha watu kumfuata kama alivyofanya yeye kwa Abubakr na kama alivyofanya Abubakar kwake Umar au kama atakavyofanya fulani ambaye anangoja kufa kwa Umar ili ambai jamaa yake.Basi hili haliwezekani baada ya Umar kuwa ameuhukumia Ukhalifa kuwa ni jambo lililofanyika ghafla na kuwa linataka kuwa ni jambo la kupora, na haiwezekani pia kwake kuliacha jambo hili liwe la makubaliano baina ya Waislamu. Na ule mkutano wa Saqifah uliofuatia kufariki kwa Mtume (s.a.w.) yeye Umar alihudhuria na akajionea mwenyewe hitilafu iliyotokea ambayo karibu zitoke roho za watu na damu imwagike.


Basi baadaye alitoa fikra ya watu wa mashauriano au (tuseme) watu sita ambao peke yao ndiyo wenye haki ya kumchagua Khalifa na Muislamu mwingine yeyote hana haki ya kushirikiana nao katika jambo hilo, na Umar alikuwa akitambua kwamba tofauti baina ya watu hawa sita haiwezi kuepukwa, ndiyo maana aliusia ikiwa watatofautiana basi wawe kwenye upande alioko Abdur-Rahman bin Auf hata kama itapelekea kuwauwa watu watatu ambao watamkhalifu Abdur-Rahman bin Auf wakati watakapogawika watu hawa sita makundi mawili, na hilo ni muhali kwani Umar anafahamu kwamba Saad bin Abi Waqas ambaye ni ibn Ammi ya Abdur-Rahman bin Auf na wawili hawa ni ukoo wa Bani Zuhrah, na alifahamu pia kwamba Saad hampendi Ali na moyoni mwake kulikuwa na chuki kwani Ali ndiye aliyewauwa wajomba zake wa ukoo wa Abdis-Shams, kama ambavyo Umar alikuwa akifahamu kwamba Abdur-Rahman bin Auf ni shemeji wa Uthman kwani mkewe aliyekuwa akiitwa Ummu Kul-thum ni dada wa Uthman. Si hivyo tu kadhalika alifahamu kuwa Tal-hah akimpenda Uthman kutokana na mahusiano yaliyokuwepo baina yao kufuatana na maelezo ya baadhi ya wapokezi wa khabari, na hakika ilitosha kwa Tal-hah kumpenda Uthman kutokana na kumpinga kwake Ali kwani yeye Tal-hah ni katika ukoo wa Bani Taym, na kulikuwa na chuki fulani baina ya Bani Hashim na Bani Taym kutokana na Ukhalifa wa Abubakar.


Taz: Shark Najul-Balaghah ya Muhammad Abdoh, Juz. 1 uk. 88.
Umar alikuwa akiyajuwa yote hayo na kwa ajili hii ndiyo maana akawachagua hawa peke yao. Umar aliwachagua hawa watu sita na wote wakiwa ni Maquraish na wote ni kutoka katika Muhajirina na hakuna yeyote kati yao ambaye ni kutoka miongoni mwa Ansar na wote hawa kila mmoja wao akiwakilisha na kuongoza kabila lenye umuhimu wake na athari yake.

1. Ali bin Abi Talib, kiongozi wa Bani Hashim.
2. Uthman bin Affan kiongozi wa Bani Umayyah
3. Abdur-Rahman bin Auf, kiongozi wa Bani Zuhrah
4. Saad bin Abi Waqqas, yeye ni kutoka katika Bani Zuhrah na wajomba zake ni Bani Umayyah.
5. Tal-ha bin Ubaidullah, Bwana wa Bani Taym.
6. Zubair bin Al-Awwan, yeye ni mtoto wa Safiyyah ambaye ni shangazi yake Mtume na ni mume wa As-maa binti Abubakr.
Basi hawa ndiyo wenye kutoa maamuzi, na hukmu yao ikubaliwe na Waislam wote, sawa sawa wakiwa ni wakaazi wa Madina (Makao Makuu ya Ukhalifa) au wengineo katika ulimwengu wote wa Kiislamu na ni wajibu wa Waislamu yeyote atakayetoka miongoni mwao akawa kinyume cha maamuzi yao basi damu yake imwagwe (auawe). Na hili ndilo jambo pekee tulilokuwa tunataka kulisogeza katika akili ya msomaji kuhusiana na kunyamaziwa kwa tamko la Ghadir katika maelezo yaliyotangulia.


Na ikiwa Umar anaufahamu undani, mapenzi na mtazamo wa watu hawa sita, basi bila shaka yeye alikuwa kisha mpendekeza Uthman bin Affan kuwa Khalifah au alikuwa anajua kuwa wengi miongoni mwa hawa sita hawamkubali Ali, vinginevyo ni kwa nini na ni kwa haki gani Umar anatilia nguvu upande wa Abdur-Rahman bin Auf dhidi ya Ali bin Abi Talib wakati ambapo Waislamu tangu hapo zamani na mpaka leo wamekuwa wakishindana juu ya ubora wa Ali na Abubakar na hatujamsikia yeyote akimlinganisha Ali na Abdur-Rahman bin Auf.

Na hapa hapana budi nisimame kidogo ili niwaulize Masunni ambao wanatetea msingi wa mashauriano na pia (niwaulize) watu wenye fikra iliyohuru wote kwa ujumla, nawauliza wote hawa, ni vipi mnaafiki baina ya mashauriano kwa maana yake ya Kiislamu na baina ya fikra hii ambayo kama itajulisha kitu fulani basi haitajulisha isipokuwa ni maoni ya ki-dikteta, kwani yeye Umar ndiye aliyewachagua watu hawa sita na siyo Waislamu, na iwapo kuufikia kwake Ukhalifa lilikuwa ni jambo la ghafla, basi ni kwa haki ipi anawalazimisha Waislamu wakubali mmoja wa hawa sita?


Kinachojitokeza kwetu ni kwamba Umar anauona Ukhalifa kuwa ni haki ya Muhajirina peke yao na mwingine yeyote hana haki ya kuwakorofisha kwenye jambo hili, bali zaidi ya hivi ni kuwa Umar anaitakidi kama anavyoitakidi Abubakar kwamba Ukhalifa ni milki ya Maquraish, bali wamo pia wasiokuwa Waarabu, hivyo basi haistahiki kwa Sal-man Al-Farisi wala Ammar bin Yasir wala Bilal wa Uhabeshi wala Suhayb Mrumi, wala Abu Dharri Al-Ghifari wala maelfu ya Masahaba ambao siyo Maquraish (haistahiki kwao) kujitokeza kwa ajili ya Ukhalifa. Na haya siyo madai ya hivi hivi tu sivyo kabisa, bali hiyo ndiyo itikadi yao ambayo historia na wataalamu wa hadithi wameisajili kutoka vinywani mwao (kina Abubakar na Umar) na hebu tuirudie khutba yenyewe ambayo Bukhari na Muslim wameieleza ndani ya Sahih zao:
Umar bin Al-Khatab anasema:
"Nilitaka kusema, na nilikuwa nimetunga vizuri usemi ambao ulinifurahisha nikitaka niutamke mbele ya Abubakr na nilikuwa nikimzunguka karibu. Basi nilipotaka kusema Abubakr akasema, tulia (ewe Umar), na sikupenda kumkasirisha. Abubakar akazungumza, na alikuwa mpole mno kuliko mimi na mtulivu mno, Wallahi hakuacha neno lolote katika maneno nilioyaandaa isipokuwa aliyasema vizuri zaidi mpaka aliponyamaza kisha akasema, nilichokieleza kwenu katika wema ninyi ndiyo mnaostahiki (akiwaambia Maansari) na wala jambo hili halitatambulika isipokuwa kwa upande huu wa Maquraish. Taz: Sahih Bukhar Babul-Wasiyyah.


Kwa hiyo inatubainikia wazi- kwamba Abubakr na Umar hawaamini mashauriano na hiyari, na baadhi ya wanahistoria wanasema kwamba Abubakar alitoa hoja dhidi ya Maansar kwa hadithi ya Mtume (s.a.w.) isemayo kuwa "Ukhalifa uko kwa Maquraish" Na hadithi hiyo hapana shaka ni sahihi (kama walivyoitaja Bukhar na Muslim na Sahih zote kwa Masunni na Mashia) Mtume (s.a.w.) amesema: "Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili na wote ni kutoka kwa Maquraishi" na hadithi iliyo wazi zaidi kuliko hii ni ile kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema:
"Jambo hili (la Ukhalifa) halitakoma kwa Maquraish muda wote hata wakibakia watu wawili"[62] pia kauli yake isemayo "Watu ni wafuasi wa Maquraishi katika kheri na shari[63].
Basi ikiwa Waislamu wote wanaziamini hadithi hizi, ni vipi mtu aseme kuwa Mtume aliliwacha suala la Ukhalifa liwe la mashauriano baina ya Waislamu wamchague wamtakaye? Na haiwezekani kwetu sisi kukwepa kupingana huku, isipokuwa tutakapoyachukua maneno ya Maimamu wa nyumba ya Mtume na wafuasi wao na baadhi ya wanachuoni wa Kisunni ambao wanasisitiza kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwataja Makhalifa na akawabainisha kwa idadi yao na majina yao, na hapo ndipo utakapoweza pia kuufahamu msimamo wa Umar na kuuthibiti Ukhalifa kwa Maquraish na huyu Umar ni mtu aliyefahamika kwa Ijtihadi yake dhidi ya maagizo ya Mtume hata katika uhai wake mwenyewe Mtume (s.a.w.), kwani matukio ya Sul-hu ya Hudaybiyah[64] kuwasalia wanafiki,[65] msiba wa siku ya Al-Khamis,[66] na kuzuwiya kwake kubashiria watu pepo[67] ni ushahidi mkubwa wa haya tuyasemayo.


Basi haishangazi kwa Umar kufanya Ij-tihad baada ya kufariki Mtume dhidi ya hadithi inayohusu Ukhalifa, haoni ulazima wa kukubali agizo linalomuhusu Ali bin Abi Talib ambaye ni Quraish, mdogo kwa umri. Ni yeye aliyeidhibiti haki ya kumchagua Khalifa kwa Maquraish peke yao, na ni yeye ambaye alilazimisha peke yake kuchagua watu sita miongoni mwa watukufu wa Kiquraishi kabla hajafa ili ikubaliane kati ya hadithi ya Mtume (s.a.w.) na vile aonavyo yeye juu ya haki ya Maquraishi peke yao kuhusika na Ukhalifa. Huenda kumuingiza Ali katika kundi hilo hali yakuwa akifahamu kwamba wao hawatamchagua, ni udhibiti wake kwa Umma ili amlazimishe Ali kuingia pamoja nao ndani ya mchezo wa Kisiasa kama wanavyouita leo hii na ili pasibakie kwa Ali na wafuasi wake na wapenzi wake ambao walikuwa wakidai kuwa yeye ndiye wa mwanzo (pasibakie kwao) hoja yeyote. Lakini Imam Ali aliyazungumza yote hayo katika hotuba yake mbele ya watu wote akasema kuhusu jambo hilo:

"Nilivumilia muda wote wa taabu na majaribu mpaka alivyoondoka akauweka (Ukhalifa) chini ya maamuzi ya kikundi cha watu sita akidhania kuwa mimi nafanana nao oh! hayawi sawa ya Mungu na mashauriano! Toka lini nikatiliwa mashaka na wa kwanza miongoni mwao mpaka imebidi nilinganishwe na watu kama hawa! lakini nilitua walipotua na niliruka waliporuka (yaani, niliishi nao kwa hekima).


Nne: Hakika Imam Ali (a.s.) alitoa hoja dhidi yao kwa kila namna lakini bila mafanikio, na je, Imam Ali aombe baia ya watu ambao walimgeuzia nyuso zao na nyoyo zao zikawaelekea wengine imma kwa husuda dhidi yake kutokana na yale aliyompa Mwenyezi Mungu miongoni mwa fadhila zake, na imma kwa chuki dhidi yake kwani yeye ndiye aliyewaua mabwana zao, akawabomoa mashujaa wao, akawakatisha tamaa, akawadhalilisha na kuvunja ujeuri wao kwa upanga wake na ushujaa wake mpaka wakasilimu na kujisalimisha hali ya kuwa Imam Ali akiwa ni Mtukufu akimtetea mwana wa ammi yake (Mtume s.a.w.) na alipokuwa akifanya hayo haikumzuwia kuyatenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lawama ya mwenye kulaumu na wala hakurudi nyuma kwenye azma yake kutokana na tamaa ya dunia. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) naye alikuwa akiyajua vema hayo na kila tukio alikuwa akitilia mkazo fadhaila za nduguye na mwana wa ammi yake ili kuwafanya wampende. Mtume alikuwa akisema "Kumpenda Ali ni (dalili ya) imani na kumchukia (ni dalili ya) unafiki"[68] Na pia husema "Ali anatokana nami, nami natokana na Ali."[69] Na alikuwa akisema: "Ali ni mtawala wa kila muumini baada yangu"[70] na husema kuwa, "Ali ni mlango wa mji wa elimu yangu na ni baba wa wanangu."[71] Pia Mtume alikuwa akisema, "Ali ni Bwana wa Waislamu na ni Imamu wa wachamungu na ni kiongozi wa waumini wenye kutowa mwanga na nuru."[72]


Lakini inasikitisha kwamba yote hayo hayakuwazidishia isipokuwa chuki na husuda na kwa ajili hiyo Mtume alimuita Ali kabla ya kufariki akamkumbatia kisha akalia na akamwambia: "Ewe Ali bila shaka mimi nafahamu kwamba ndani ya nyoyo za jamaa hawa kuna shinikizo la chuki dhidi yako, na hapo baadaye watakudhihirishia baada yangu mimi, iwapo watakupa baia kubali vinginevyo basi subiri mpaka hapo utapokutana nami hali ya kuwa mwenye kudhulumiwa". Taz: Ar-Riyadun-Naz-Rah Fi Manaqibil-Asharah cha Tabari Babu Fadail Ali ibn Abi Talib. Basi ikiwa Abul-Hasan (a.s.) ilimlazimu kuvumilia baada ya baia ya Abubakr, hilo ni kutokana na usia wa Mtume kwake yeye na ndani ya hilo muna hekima ambayo iko wazi.

Tano: Zaidi ya yote hayo yaliyotangulia ni kwamba, Muislamu ataposoma Qur'an Tukufu na kuzizingatia aya zake, atafahamu kwa kupitia masimulizi yake kuhusu mambo ambayo yaliwafika watu na mataifa yaliyopita kwamba, kwao yalitokea mengi kuliko yale yaliyotokea kwetu sisi. Basi mwangalie huyu Qabil anamuuwa nduguye Habil kwa dhulma na uadui tu, na huyu hapa Nuh ambaye ni babu wa Manabii, baada ya miaka elfu moja ya jihadi hakuna aliyemfuata katika watu wake isipokuwa wachache tu, isitoshe mkewe na mwanawe walikuwa miongoni mwa makafiri.

Mtazame Nabii Lut haikupatikana katika kitongoji chake isipokuwa nyumba moja tu ya Waumini. Nao Mafirauni ambao walikuwa wenye kiburi katika nchi wakawafanya watu kuwa watumwa, hapakuwepo miongoni mwao isipokuwa Muumini mmoja anayeficha imani yake. Hawa hapa nduguze Yusuf watoto wa Yaaqub nao ni kikundi, wanakula njama kumuuwa ndugu yao mdogo asiye na kosa lolote lakini (wanafanya hivyo) kwa kumhusudu kwa kuwa yeye ni kipenzi kwa baba yao. Watazame wana wa Israel ambao Mwenyezi Mungu aliwaokoa kupitia kwa Musa na akawapasulia bahari na kumuangamiza adui yao Firauni na askari wake bila ya kuwakalifisha taabu yoyote ya vita, basi mara walipotoka baharini na nyayo zao hata hazijakauka, wakawafikia watu wanaoabudia sanamu (wana wa Israel) wakasema:

"Ewe Musa tutengenezee Mungu kama wao walivyo na Miungu, Musa akawaambia hakika ninyi ni watu msiojua." Na alipokwenda kwenye ahadi ya Mola wake na kumuacha nduguye Harun, walifanya njama dhidi yake karibu wamuuwe, wakamkufuru Mwenyezi Mungu, na wakamuabudia ndama kisha baadaye waliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema: "Kila walipokufikieni Mitume kwa yale ambayo nafsi zenu haziyapendi mlijivuna, kundi moja mlilipinga na kundi jingine mkaliua".(Qur'an, 2:87)


Huyu hapa naye Bwana wetu Yahya bin Zakariya naye ni Nabii na Mtawa miongoni mwa watu wema anauwawa na kichwa chake anazawadiwa mtu muovu miongoni mwa waovu wa Kibani Israel. Mayahudi na Wakristo nao walikula njama kumuua na kumsulubu bwana wetu Isa. Nao ummati wa Muhammad wanaandaa jeshi la kiasi ya watu elfu thelathini ili kumuuwa kipenzi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu na Bwana wa vijana wa peponi ambaye hawakuwa pamoja naye isipokuwa watu Sabini miongoni mwa wafuasi wake, wakawauwa wote ikiwa ni pamoja na mwanawe mchanga. La ajabu ni lipi baada ya yote haya? Lipi litashangaza baada ya kauli ya Mtume kuwaambia Masahaba wake yakuwa: "Mutafuata nyendo za wale waliokuwa kabla yenu shubiri baada ya shubiri na dhiraa baada ya dhiraa mpaka hata wakiingia kwenye shimo la kenge nanyi mutaingia". wakasema, "Wadhani kuwa hao ni Mayahudi na Wakristo"? Mtume akasema, "Ni kina nani basi (kama si hao)"?

Taz: Sahih BukharJuz. 4 uk. 144 na Juz. 8 uk. 151. Ni kipi cha ajabu basi, nasi twasoma ndani ya Bukhar na Muslim kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo: "Siku ya Kiyama Masahaba wangu watapelekwa upande wa kushoto nami nitasema wanapelekwa wapi? Patasemwa Wallahi Motoni, nitasema, Ewe Mola wangu Masahaba wangu hao, patasemwa, Hakika wewe hujuwi waliyoyazusha baada yako, nitasema atengwe mbali aliyebadilisha baada yangu, na sitamuona anaokoka miongoni mwao isipokuwa kikundi kidogo kama cha ngamia waliotelekezwa".

Tax: Sahih Bukhar Juz. 7 uk. 209 na Sahih Muslim Babul-Haudh. Basi lipi la ajabu baada ya kauli yake Mtume (s.a.w.) aliposema: "Umati wangu utagawanyika makundi sabini na tatu na yote yataingia motoni isipokuwa kundi moja". Taz: Sunan Ibn Majah Kitabul-Fitan Juz. 2 hadith Na. 3993, Ahmad Juz. 3 uk. 120, Sunan Tirmidhi Kitabul-Iman. Amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola mwenye nguvu na Utukufu, mjuzi wa undani wa nyoyo pale aliposema: "Na watu wengi hawataamini japo utapupia" (Qur'an, 12:103)
"Bali amewajia na ukweli na wengi wao wanaichukia kweli" (Qur'an,23:70)
"Bila shaka tumekujieni na ukweli lakini wengi wenu hawaupendi ukweli" (Qur'an 43:78)
"Fahamuni ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli lakini wengi wao hawafahamu" (Qur'an, 10:55)
"Wanakuridhisheni kwa vinywa vyao na nyoyo zao zinakataa, na wengi wao ni mafasiki (Qur'an, 9:8)
"Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru" (Qur'an, 10:60)
"Wanaitambua Neema ya Mwenyezi Mungu kisha wanaipinga na wengi wanakataa ila kukufuru tu" (Qur'an, 25:50)
"Na wengi wao hawawezi kumuamini Mwenyezi Mungu ila hali ya kuwa wanamshirikisha" (Qur'an, 12:106)
"Bali wengi wao hawaijuwi haki basi wao wanapinga" (Qur'an, 21:24)
"Hivi mwashangazwa na mazungumzo haya na mnacheka wala hamlii hali ya kuwa ninyi mmeghafilika (mmejisahau)" (Qur'an, 53:617
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

HUZUNI NA MAJUTO Kwa nini nisijute; bali ni kwa nini kila Muislamu asijute wakati asomapo ukweli huu unaohusu hasara waliyoipata Waislamu kutokana na kutengwa kwa Imam Ali kwenye Ukhalifa ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtawalisha, na hivyo kuunyima umma (wa Kiislamu) uongozi wake na hekima, na elimu yake nyingi. Na pindi Muislamu atakapochunguza bila ya chuki wala upendeleo, atamkuta Imam Ali ndiyo mjuzi mno kuliko watu wote baada ya Mtume, kwani historia inashuhudia kwamba wanachuoni wa Kisahaba walikuwa wakimuuliza Ali kwa kila lililowatatiza, na kauli ya Umar bin Al-Khatab aliyoisema zaidi ya mara sabini ya kwamba "Lau kama si Ali basi Umar angeliangamia' wakati ambapo Imam Ali (a.s.) hakupata kamwe kumuuliza Sahaba yeyote miongoni mwao.

Taz: Manaqibul-Khawar Zami uk. 48, Al-Istiabu Juz.3 uk. 39. Tadhkiratus-Sibt uk. 87, Matalibus-Suuli uk. 13, Tafsir Nishapur katika Surat Ahqaf, Faidhul-QadirJuz.4uk.357. Kama ambavyo historia inakiri kuwa Ali bin Abi Talib ni shujaa mno na mwenye nguvu kuliko Masahaba wote, na kuna mashujaa wengi miongoni mwa Masahaba walipata kukimbia vita katika sehemu nyingi tu, wakati ambapo Ali (a.s.) alisimama imara mahala pote palipopiganwa vita, na inatosha kuwa ni dalili ile nishani aliyopewa na Mwenyezi Mungu pale Mtume (s.a.w.) aliposema: "Kesho nitampa bendera yangu mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, naye anapendwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, mkali katika mapambano si mwenye kukimbia, Mwenyezi Mungu amekwisha utahini moyo wake kwa imani". Masahaba wakaitamania (kuipata) bendera hiyo, Mtume akampa Ali bin Abi Talib.


Kwa kifupi, bila ya shaka maudhui ya elimu , nguvu na ushujaa, mambo ambayo Imam Ali amepwekeka kwayo, ni maudhui inayofahamika kwa wote (Sunni na Shia) na ukiachilia mbali maandiko yanayojulisha kwa uwazi wa kuashiria juu ya Uimamu wa Ali, hapana shaka kwamba Qur'an haikubali uongozi na Uimamu isipokuwa kwa mtu mwenye elimu, shujaa tena mwenye nguvu. Mwenyezi Mungu anasema kuhusu wajibu wa kuwafuata wanachuoni (wenye elimu): "Basi aongozaye katika haki ndiye anayestahiki zaidi kufuatwa au (anastahiki) yule asiyeongoka isipokuwa aongozwe, basi mna nini, ni vipi mnahukumu?" (Qur'an, 10:35)


Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu wajibu wa kumfuata mwenye elimu, shujaa tena mwenye nguvu: "Wakasema, ni vipi atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tunastahiki zaidi kupata ufalme kuliko yeye, naye hakupewa wasaa wa mali? Akasema, Mwenyezi Mungu amemchagua juu yenu na amemzidishia wasaa wa elimu na kiwiliwili na Mwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye, naye Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa mwenye kujua". (Qur'an, 2:247) Hapana shaka Mwenyezi Mungu Mtukufu amemzidishia Imam Ali wasaa wa elimu kuliko Masahaba wote, akastahiki kuwa ni "Mlango wa elimu," akawa ndiye rejea pekee kwa Masahaba baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) nao Masahaba walikuwa kila wanaposhindwa kutatua mambo husema "Mas-ala haya magumu hakuna ayawezaye isipokuwa Abul-Hasan." Taz: Manaqibul-Khawar-Zami uk. 58, Tadhkiratus-Sibt uk. 87 Ibnul-Maghazili Tarjumah ya Ali uk. 79.


Na alimzidishia wasaa wa kiwiliwili, kwa kweli alistahiki kuwa simba wa Mwenyezi Mungu aliye mshindi, na nguvu zake na ushujaa wake ni wenye kupigiwa mfano katika kila zama kiasi kwamba wanahistoria wamesimulia visa vingi kuhusu ushujaa na nguvu zake visa ambavyo vinakurubia kuwa ni miujiza, kama vile kuung'oa mlango wa Khaybar, wakati ambapo Masahaba ishirini walishindwa hata kuutikisa[73] Na pia kuling'oa Sanamu kubwa la Hubal[74] kutoka juu ya paa la Al-Kaabah na kulisogeza jiwe kubwa ambalo jeshi lote lilishindwa hata kulitikisa[75] na mengineyo miongoni mwa riwaya mashuhuri. Na Mtume (s.a.w.) alimsifu na kumtaja kwa ubora mwana wa ammi yake Ali, na akazibainisha fadhila zake mahala mbali mbali na aliyatambulisha mambo yake maalum yanayomuhusu na daraja yake.

Kuna wakati Mtume akisema:
"Hakika huyu ni ndugu yangu na ni wasii wangu na ni Khalifa wangu baada yangu, basi msikilizeni na mumtii" Taz: 1) Tarikhut-Tabari Juz. 2 uk. 319. 2) Tarikhu ibn Athir Juz. 2 uk. 62. Na kuna wakati Mtume humwambia Ali (a.s.): "Wewe kwangu mimi unayo daraja ya Harun kwa Musa isipokuwa hapana Nabii baada yangu". Taz: 1) Sahih Muslim Juz. 7 uk. 120. 2) Sahih Bukhar katika Fadhail za Ali Na kuna wakati mwingine Mtume akisema:
"Yeyote mwenye kutaka kuishi nilivyoishi mimi na kufa mauti (kama) yangu na akae katika bustani ya milele aliyoniahidi Mola wangu, basi na amtawalishe Ali bin Abi Talib, kwani yeye hatakutoeni kwenye uongofu na kamwe hatakuingizeni katika upotofu". Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk.' 128 na At-Tabrani ndani ya Al-Kabir.


Na yeyote atakayefuatilia sera ya Mtume Mtukufu (s.a.w.) atamkuta Mtume hakutosheka kwa kusema maneno tu na hadithi zinazomuhusu Ali, bali maneno yake yakionekana kwa matendo yake, kwani katika uhai wake Mtume katika uhai wake hakupata kumuwekea Ali amiri yeyote juu yake miongoni mwa Masahaba pamoja na kwamba alikuwa akiwawekea maamiri Masahaba wengine wao kwa wao. Hapana shaka kwamba Mtume aliwawekea Abubakar na Umar amiri (wa kuwaongoza) katika vita ya "Dhatus-Salasil" amiri huyo alikuwa Amr bin Al-As.

Taz: Siratul-Halabiyah, Ghaz-Watu Dhatis-Salasil, na Tabaqat ya ibn Saad. Kama ambavyo Mtume (s.a.w.) aliwawekea Masahaba amiri ambaye alikuwa kijana mdogo Usamah bin Zaid na hilo alilifanya katika jeshi la Usamah kabla ya kufariki kwake yeye Mtume (s.w.a.). Amma Ali bin Abi Talib hakuwa katika ujumbe wowote ila yeye ndiye amiri, hata kuna wakati fulani Mtume (s.a.w.) alituma ujumbe wa namna mbili, akampa uamiri Ali kwenye moja ya ujumbe huo na Khalid bin Walid akampa uamiri kwenye ule wa pili kisha akawaambia:
"Mutakapoachana kila mmoja awe amiri wa jeshi lake na mkikutana basi Ali ndiye amiri wa jeshi lote. Kutokana na maelezo yote yaliyotangulia tunakuta kwamba Ali ndiye mtawalia mambo ya waumini baada ya Mtume (s.a.w.) na haifai kwa yeyote yule kumtangulia.


Lakini kwa masikitiko makubwa, Waislamu wamepata hasara kubwa, na ndiyo maana wanapata taabu hadi leo na wanachuma matunda ya kile walichokipanda, na bila shaka waliokuja baadaye wamekwisha yatambua yale yaliyoasisiwa na hao waliotangulia. Hivi kweli inawezekana kwa mtu yeyote kufikiria kuna Ukhalifa ulioongoka zaidi ya ule Ukhalifa wa Ali bin Abi Talib? Lau umma huu ungelifuata kile alichokichagua Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa kuwa Ali alikuwa ndiye mwenye uwezo wa kuuongoza umma (huu) kwa muda wote wa miaka thelathini juu ya mfumo mmoja kama vile alivyouongoza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) bila ya mabadiliko yoyote. Tunasema hayo kwa kuwa Abu Bakar na Umar walibadilisha na wakafanya ijtihadi zao dhidi ya maagizo na matendo yao yakawa ndiyo sunna inayofuatwa. Uthman naye alipokuja kwenye Ukhalifa akabadilisha mengi mno mpaka ikasemwa kuwa alikikhalifu kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake pia Sunna ya Abubakar na Umar, hapo ndipo Masahaba walipompinga na yakafanyika dhidi yake mapinduzi makubwa yaliyoangamiza Maisha yake na kusababisha fitna kubwa katika umma (fitna ambayo) jeraha lake halijapona hadi leo.


Amma Ali bin Abi Talib, yeye alikuwa akifungamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake, hakwenda kinyume japo kwa nchi moja, na ushahidi mkubwa wa hilo ni kwamba yeye Imam Ali alikataa kuchukua Ukhalifa pale walipomuwekea sharti ya kuhukumu kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume wake na sunna ya Makhalifa wawili waliomtangulia.

Huenda akauliza muulizaji: Basi ni kwa nini Ali anashikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume wake wakati ambapo Abubakar na Umar na Uthman walilazimika kufanya ijtihadi na mabadiliko?
Jawabu ni kuwa, yeye Ali anayo elimu ambayo wao hao hawakuwa nayo, isitoshe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alimuhusisha kwa milango elfu moja ya elimu na katika kila mlango anaweza kufungua milango elfu moja. Taz: Kanzul-ummal Juz. 6 uk.392 hadithi Na.6009 Yanabiul-Mawaddah uk. 73,77 Tarekh Dimishq Juz. 2 uk. 483.
Pia alimwambia: "Wewe Ewe Ali utaubainishia umma wangu yale watakayotofautiana ndani yake baada yangu." Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 122, Tarekh Dimishq Juz. 2 uk. 488.

Amma hao Makhalifa walikuwa hawajuwi mambo mengi katika hukmu za Qur'an za dhahiri licha ya taawili ya Qur'an, hali hii wamethibitisha Bukhar na Muslim ndani ya sahih zao katika mlango wa kutayamamu ya kwamba, kuna mtu fulani alimuuliza Ummar bin Al-Khatab katika zama za Ukhalifa wake akasema yule mtu: "Ewe Amirul-Muuminina hakika mimi nimepatwa na janaba na sikupata maji, basi nifanyeje"? Umar akasema: "Usiswali"!! Kadhalika Umar hakuifahamu hukmu ya watoto wa ndugu wa kiume wa baba (ibnu Ammi) mpaka amekufa na hali ya kuwa anasema, "Natamani lau ningemuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu juu ya watoto wa Ammi".Wakati ambapo hukmu yake imetajwa ndani ya Qur'ani Tukufu, kwa hiyo Umar ambaye Masunni wanasema kuwa alikuwa miongoni mwa wenye kupewa Il-hamu (na Mwenyezi Mungu) hali ya elimu yake ilikuwa katika kiwango hiki, (basi kama Umar ni hivi) hao wengine wala usijisumbue kuuliza, hao ndiyo ambao waliingiza Bid'a (uzushi) ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu bila ya kuwa na elimu wala uongofu wala kitabu cha kuwaongoza isipokuwa jitihada zao binafsi.


Na huenda msemaji akasema: "Ikiwa mambo ndiyo yako namna hii, basi ni kwa nini Imam Ali (a.s.) hakuubainishia umma yale ambayo walitofautiana ndani yake baada ya Mtume (s.a.w.)" Jawabu ni kuwa: Imam Ali (a.s.) hakuacha kufanya juhudi katika kubainisha yale yaliyoutatiza umma, na yeye alikuwa ndiye marejeo ya Masahaba kwa kila lililowatatiza alikuwa akija na kufafanua na kutoa nasaha. Hivyo basi walikuwa wakiyachukua yale wayapendayo na yasiyopingana na siasa zao na kuyaacha yasiyokuwa hayo, na historia ndiye shahidi mkubwa kwa haya tuyasemayo.


Kwa kweli lau siyo Ali bin Abi Talib na Maimamu miongoni mwa wanawe, basi watu wasingeyafahamu mafunzo ya dini yao, lakini watu (walivyo) ni kama ilivyotufunza Qur'an yakuwa hawaipendi haki, basi walifuata matamanio yao na kuzusha madhehebu dhidi ya Maimamu wa nyumba ya Mtume ambao serikali zilizokuwa katika wakati wao zilikuwa zikifuatilia kila wasemalo, wala hazikuwapa uhuru wa kushughulika na kufanya mahusiano ya moja kwa moja na watu. Basi Imam Ali (a.s.) alikuwa akipanda juu ya mimbari na kuwaambia watu, "Niulizeni kabla hamjanikosa" Na yatosha kuwa Imam Ali ameacha Nahjul-Balagha, nao Maimam kutoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.) wameacha elimu ambayo imeenea ulimwenguni na hilo wamelishuhudia viongozi wa Kiislamu Masunni na Mashia.


Ninarejea kwenye maudhui na ninasema: "Kwa msingi huu, lau Ali angewezeshwa kuuongoza umma kwa miaka thelathini kwa mujibu wa sera ya Mtume (s.a.w.) basi Uislamu ungeenea na kuimarisha itikadi katika nyoyo za watu zaidi na kwa undani wala pasingekuwa na fitna ndogo au kubwa wala (mauaji ya) Karbala yasingekuwepo wala msiba wa Ashuraa. Lau tutaukadiria uongozi wa Maimamu kumi na moja baada ya Ali, Maimamu ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwataja, na uhai wao uliendelea kwa kipindi cha karne tatu, basi pasingebaki hapa duniani miji isiyokuwa ya Kiislamu, na ulimwengu usingekuwa katika hali tunayoishuhudia leo hii na maisha yetu yangekuwa ya kibinaadamu kwa maana yake ya hakika lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Alif Lam Mim, Je, watu wanadhani kwamba wataachwa kwa kuwa wanasema: "Tumeamini" wasijaribiwe (wakapata Mitihani)? (Qur'an, 29:2) Umma wa Kiislamu umefeli katika mtihani huu kama vile zilivyofeli umma zilizotangulia, kama ambavyo Mtume wa Mwenyezi Mungu[76] alivyotamka katika minasaba mbali mbali na kama ambavyo Qur'an ilivyosisitiza mara nyingi ndani ya aya nyingi.[77]

USHAHIDI MWINGINE KUHUSU UONGOZI WA ALI (A.S.) Kama kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka Wilayah ya Ali iwe ni mtihani kwa Waislamu, basi kila ikhtilafu iliyotokea imekuwa ni kwa sababu ya Wilayah hiyo, naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mpole kwa waja wake, hawezi kuwaadhibu waliokuja baadaye kwa makosa yaliyofanywa na wale wa mwanzo. Kwa ajili hiyo imetukuka hekima yake, tukio hili la ukhalifa likazungukwa na mfululizo wa matukio mengine makubwa yafananayo na miujiza, ili iwe ni kichocheo kwa umma. Waliinakili hali hii waliokuwepo ili wapate mazingatio wajao baadaye huenda wakaongoka na kuelekea kwenye haki kwa njia ya kufanya utafiti.

Ushuhuda wa Kwanza: Unafungamana na adhabu kwa wale waliokadhibisha Wilayah ya Ali, hilo lilitokea baada ya kuenea kwa habari za Ghadir Khum na kusimikwa kwa Imam Ali kuwa ni Khalifa wa Waislamu kutokana na kauli ya Mtume alipowaambia "Aliyeshuhudia tukio hilo amfikishie habari asiyehudhuria ".

Habari hizo za tukio la Ghadir zilimfikia Harith bin Nuuman Al-Fihri na hakufurahishwa na habari hizo- Hapa kuna dalili kwamba walikuwepo Mabedui waliokuwa wakiishi nje ya Madina ambao walikuwa wakimchukia Ali na pia Mtume (s.a.w.). Basi huyu bwana alimsimamisha mnyama wake mbele ya mlango wa msikiti akaingia kwa Mtume (s.a.w.) akasema: "Ewe Muhammad bila shaka wewe umetuamuru tushuhudie kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, tumekukubalia hilo, na umetuamuru tusali mara tano kwa siku, tufunge Ramadhan, Tuhiji na tutoe zaka mali zetu tukakukubalia, kisha hukuridhika kwa haya mpaka umeinyanyua mikono ya mwana wa ammi yako na umemboresha juu ya watu ukasema: "Yeyote ambaye mimi ni mtawalia mambo yake basi Ali ni mtawalia mambo yake". Jambo hili latoka kwako au latoka kwa Mwenyezi Mungu"?

Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema hali ya kuwa macho yake yamekuwa mekundu: "Namuapa Mwenyezi Mungu ambaye hapana Mola isipokuwa yeye, jambo hilo latoka kwa Mwenyezi Mungu na halitoki kwangu" Akasema maneno hayo mara tatu.!! Harith alisimama huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa ayasemayo Muhammad ni ya kweli, basi tuletee mawe toka mbinguni au utuletee adhabu kali". Msimulizi wa kisa hiki anasema: "Wallahi hakumfikia ngamia wake bali Mwenyezi Mungu alimpiga kwa jiwe toka mbinguni likaangukia kichwani na kutokea kwenye makalio akafa. Pale pale Mwenyezi Mungu akateremsha aya isemayo: "Muombaji aliomba adhabu itakayotokea (adhabu ambayo) haina wa kuizuia kwa makafiri." (Qur'an 70:1-2) Tukio hili wameliandika wanachuoni wengi wa Kisunni[78] wasiokuwa wale tuliokwisha kuwataja, basi mwenye kutaka ziyada kutoka katika rejea ni juu yake kutazama kitabu kiitwacho Al-Ghadir cha Al-Allamah Al-Amin.Ushahidi wa Pili: Unahusu adhabu ya yule aliyeficha ushahidi wa tukio la Ghadir na dua ya Imam Ali ikampata. Hilo lilitokea wakati Imam Ali aliposimama katika zama za Ukhalifa wake kwenye siku iliyoshuhudiwa pindi Imam Ali alipowakusanya watu katika msikiti wa Kufah akatangaza akiwa juu ya mimbar akasema: "Namsihi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Muislamu ambaye alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema siku ya Ghadir Khum kwamba, yeyote ambaye mimi ni mtawalia mambo yake basi Ali ni mtawalia mambo yake namnasihi asimame na kushuhudia aliyoyasikia, na asisimame isipokuwa yule aliyemuona kwa macho yake nakumsikia kwa masikio yake." Walisimama Masahaba thelathini, kumi na sita miongoni mwao ni mashujaa wa Badri, wakashuhudia kwamba Mtume (s.a.w.) aliushika mkono wake (Ali) na akawaambia watu kuwa: "Je, mnafahamu kuwa mimi ni bora mbele ya waumini kuliko nafsi zao? Wakasema ndiyo, Mtume (s.a.w.) akasema, Yeyote ambaye mimi namtawalia mambo yake basi huyu hapa Ali ni mtawalia mambo yake, ewe Mwenyezi Mungu mtawalishe atakayemtawalisha na umpinge anayempinga ..."


Lakini baadhi ya Masahaba waliohudhuria tukio la Ghadir, chuki na husuda dhidi ya Imam Ali ziliwakalisha chini hawakusimama kushuhudia, na miongoni mwa hawa ni Anas bin Malik. Imam Ali aliposhuka kutoka kwenye Mimbar alimwambia "Ewe Anas una nini mbona hukusimama pamoja na Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ili ushuhudie yale uliyoyasikia toka kwake siku hizo kama walivyoshuhudia wengine?" Anas akasema, "Ewe Amirul-Muumina umri wangu umekuwa mkubwa (nimekuwa mzee) na nimesahau". Imam Ali (a.s.) akasema: "Ikiwa wewe ni muongo, basi Mwenyezi Mungu akubabue kwa weupe ambao kilemba chako hakitaufunika." Anas hakusimama isipokuwa uso wake ulikwisha kuwa mweupe kwa mbaranga, na baada ya hapo akawa hulia na kusema, "Imenipata dua ya mja mwema kwa sababu nilificha ushahidi wake". Kisa hiki ni mashuhuri, Ibnu Qutaibah amekitaja ndani ya kitabu kiitwacho Al-Maarif uk. 251, pale alipomuweka Anas miongoni mwa waliodhurika (kutokana na dua ya Imam Ali) katika mlango unaozungumzia mbaranga, pia Imam Ahmad bin Hambal ndani ya Musnad yake Juz. 1 uk.119 (amekitaja kisa hiki) aliposema: "Wakasimama isipokuwa watu watatu hawakusimama basi iliwapata dua yake."


Na hapa inafaa tuashirie kwa kuwataja watu hawa watatu ambao Imam Ahmad amewataja kwa riwaya ya Al-Balaadhuri[79] amesema baada ya kuleta nasaha ya Imam Ali kuhusu ushahidi, na chini ya mimbar alikuweko Anas Bin Malik, Al-Bar-raa bin Azib na Jarir bin Abdallah Al-Balli, Imam Ali alirudia nasaha ile lakini hakuna yeyote aliyemjibu miongoni mwao, basi Ali akasema, "Ewe Mwenyezi Mungu, yeyote mwenye kuficha ushahidi huu na hali ya kuwa anaufahamu basi usimtoe katika dunia hii mpaka umuwekee alama atakayotambulika kwayo." Amesema msimuliaji, "Anas bin Malik akapatwa na mbaranga, Al-barraa bin Azib akawa kipofu na Jarir akarudi kuwa bedui baada ya Hijra yake na akaenda Sharaat akafia ndani ya nyumba ya mama yake".[80] Kisa hiki ni mashuhuri wamekinakili wanahistoria wengi. Basi zingatieni enyi wenye akili:

Yeyote mwenye kufuatilia atafahamu kwa kupitia tukio hili[81] pale alipowanasihi Masahaba washuhudie hadithi ya Ghadir, tukio ambalo Imam Ali alilihuisha baada ya kupita na robo karne, na karibu lilikuwa lisahauliwe. Hivyo basi atakayefuatilia atafahamu ni ipi daraja ya Imam Ali na utukufu wake pia kiwango cha azma yake na usafi wa nafsi yake, wakati ambapo subira aliipa nafasi zaidi kuliko haki yake, na aliwapa nasaha kina Abubakr na Umar na Uthman kitu ambacho alifahamu kuwa katika kuwanasihi hao kuna mas-lahi kwa Uislamu na Waislamu. Pamoja na hayo alikuwa amelihifadhi moyoni mwake tukio la Ghadir kwa maana zake zote na lilikuwemo katika dhamira yake muda wote wa uhai wake, hivyo alipata fursa nzuri ya kulitoa na kulihuisha upya mpaka akawataka wengine walishuhudie mbele ya masikio na macho ya watu.


Tazama ni namna gani ilivyokuwa njia ya kuuhuisha ukumbusho huu wenye baraka, na yale yaliyomo miongoni mwa hekima kubwa kwa ajili ya kuisimamisha hoja juu ya Waislamu wale waliohudhuria kwenye tukio lenyewe na wale ambao hawakuwepo, basi lau Imam Ali angesema: "Enyi watu kwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu aliusia siku ya Ghadir Khum kuhusu Ukhalifa wangu", basi jambo hilo lisingekuwa na umuhimu katika nafsi za watu waliokuwepo hapo na wangehoji juu ya kunyamaza kwake kwa muda wote huo. Lakini yeye Imam Ali aliposema:"Namsihi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kila Muislamu ambaye alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema aliyoyasema siku ya Ghadir Khum (namsihi) asimame na ashuhudie", basi ikawa tukio hilo limenakiliwa kwa hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kupitia ndimi za Masahaba thelathini, kumi na sita miongoni mwao ni mashujaa wa Badri, kwa ajili hiyo Imam Ali akawa ameziba njia dhidi ya wapinzani na wenye mashaka na wale wenye kuhoji juu ya kunyamaza kwake kwa muda wote huo, kwani kunyamaza kwa watu hawa thelathini pamoja naye hali ya kuwa wao ni miongoni mwa Masahaba wakubwa mno dalili kubwa juu ya msimamo huu, na kwamba kunyamaza huko ndani yake mna maslahi kwa Uislamu jambo ambalo liko wazi.


UFAFANUZI JUU YA MASHAURIANO (SHURAA) Katika maelezo yaliyotangulia tumeona kwamba Ukhalifa kwa mujibu wa kauli ya Mashia ni uchaguzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na ubainisho wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) baada ya ufunuo unaofunuliwa kwake. Kauli hii inakubaliana kabisa na hekima ya Uislamu katika hukmu zake zote na sheria zake, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye yeye ambaye "Anaumba akitakacho na kuchagua, wao (viumbe) hawana hiyari" (Qur'an. 28:68) Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka ummati wa Muhammad (s.a.w.) uwe ni umma bora uliotolewa kwa watu, basi hapana budi uwe na uongozi wenye hekima, uongofu, elimu, nguvu, ushujaa, ucha Mungu na kutosheka katika nyanja za Imani. Jambo hili hawezi kulipata isipokuwa yule ambaye kateuliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akamtengeza kwa sifa maalum zinazomstahiki kwa ajili ya utawala.


Mwenyezi Mungu anasema:"Mwenyezi Mungu anachagua wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu, bila shaka Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kuona." (Qur'an, 22:75) Na kama ilivyo ya kwamba Mwenyezi Mungu amewachagua Manabii, ndivyo hivyo hivyo (amewachagua) Mawasii, na bila shaka Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema:"Kila Nabii anaye wasii, nami wasii wangu ni Ali bin Abi Talib". Taz: Ibn Asakir As-Shafii Juz. 3 uk. 5, Manaqib Al-Khawarzami uk. 42, Yanabiul-Mawdddah uk. 79. Na katika hadithi nyingine Mtume (s.a.w.) amesema:"Mimi ndiyo mwisho wa Manabii na Ali ndiye mwisho wa Mawasii". Taz:Yanabiul-Mawaddah Juz. 2 uk. 3 akinakili toka kwa Ad-Dailami-Manaqib Al-Khawarzami Dhakhairul-'Uqba. Na kwa msingi huu basi, Mashia wameyasalimisha mambo yao kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na hapakubakia yeyote miongoni mwao anayeudai Ukhalifa kwa nafsi yake au kuutamania, siyo kwa njia ya "Nassi" wala kwa kuchaguliwa, kwanza kwa kuwa "Nassi" inapinga uchaguzi na shuraa na pili ni kwamba "Nassi" imekwishapatikana kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kuwahusu watu walioandaliwa na kubainishwa kwa idadi na majina yao,[82] hakuna mtu miongoni mwao anayeunyooshea shingo na ikiwa yuko atayefanya basi huyo ni muovu na ametoka katika dini.


Ama Ukhalifa kwa Masunni ni jambo la uchaguzi na makubaliano, na kwa ajili hiyo wamefungua mlango ambao haiwezekani kumfungia yeyote miongoni mwa watu wa umma huu, na akautamania Ukhalifa (baada ya kuufungua mlango huu) kila mtu aliye mbali na aliye karibu, kila mnyonge na mwenye nguvu na hatimaye ukageuka kutoka kwa Maquraishi mpaka kwa watumwa na waliopewa uhuru,Wafursi na wafalme hadi kwa Waturuki na Wamongolia.

Na zile sharti walizoziweka kuhusu Ukhalifa zikatoweka, kwani mtu asiye Maasum amejaa(sifa ya) upendeleo, wema na ubaya, hivyo basi kiasi tu cha yeye kuupata utawala hawezi kusalimika na kisha kugeuka na kuwa mbaya zaidi kuliko alivyokuwa, na historia ya Kiislamu ndiye shahidi bora wa haya tuyasemayo. Nachelea baadhi ya wasomaji watadhani kwamba mimi natia chumvi, basi haiwalazimu ila kuisoma ( na kuichambua) historia ya kizazi cha bani-Umayyah na bani- Abbas na wengineo ili wafahamu kwamba kuna (miongoni mwa hao) yuko aliyejiita kuwa ni Amirul-Muuminina. huyu alikuwa akinywa pombe wazi wazi, akichezea tumbili na kuwavisha dhahabu. Yuko mwingine naye alimvalisha mjakazi wake mavazi yake ya kiume ili awasalishe Waislamu, na kuna mwingine aliyejiita Amirul-Muuminina, mjakazi wake aliyempenda mno alipofariki, akili zake zilimruka, na kuna Amirul-Muuminina mwingine yeye alikuwa akifurahishwa na mashairi kisha anabusu uume wake.


Basi ni kwa nini tuzame zaidi juu ya habari za watu hawa ambao waliwatawala Waislamu, kwani wao hawawakilishi isipokuwa ufalme wenye matatizo na wala hawawakilishi Ukhalifa, na hilo ni kutokana na hadithi ambayo wanaisimulia (wao Masunni) ambayo ni kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo: "Ukhalifa baada yangu ni miaka thalathini kisha utakuwa Ufalme" Na hii siyo maudhui ya uchambuzi wetu (tunaoufanya) basi mwenye kutaka kufahamu zaidi juu ya hilo na arejee Tarikhut-Tabari, Tarikhu Ibn Athir, Abul-Fidaa na ibn Qutaybah na wengineo.

Nami hapa nilitaka tu kubainisha ubaya wa kuchagua na ubaya wa nadharia hii katika misingi yake, kwani tumchaguaye leo huende kesho tukamkosoa na ikatubainikia kwamba tumekosea na hatukuchagua vizuri-kama yalivyomtokea hayo Abdur-Rahman bin Auf wakati alipomchagua Uthman bin Affan kwa ajili ya Ukhalifa na baadaye akajuta, lakini majuto yake hayakuusaidia chochote umma baada ya kuangamia, basi kama sahaba Mtukufu miongoni mwa kundi la kwanza ambaye ni Uthman anashindwa kutekeleza ahadi aliyompa Abdur-Rahman bin Auf, na pia itakapokuwa Sahaba Mtukufu miongoni mwa kundi la mwanzo ambaye ni Abdur-Rahman bin Auf anashindwa kuchagua vizuri, basi haiwezekani kwa mwenye akili baada ya hayo kukubaliana na nadharia hii butu, nadharia ambayo hapakuzalikana kutokana nayo isipokuwa vurugu na kukosekana utulivu na (hatimaye) kumwagika damu.


Hivyo basi ikiwa baia ya Abubakr ilitimia ghafla kama alivyoieleza Umar bin Khatab na kwamba Mwenyezi Mungu aliikinga shari yake kwa Waislamu na waliikhalifu na kuipinga Masahaba wengi, na iwapo pia Baia ya Ali bin Abi Talib baada ya hayo iliyofanyika mbele ya macho ya watu wengi, lakini baadhi ya Masahaba walitengua baia hiyo na ikasababisha jambo hilo kuleta vita vya Jamal, vita vya Siffin na vita vya Nah-rawan, ambapo roho nyingi zisizo na makosa zikateketea, basi ni vipi atairidhia mwenye akili baada ya yote haya hii kanuni ambayo ilijaribiwa na ikashindwa vibaya tena haraka tu mwanzoni mwake na ikawa na matokeo mabaya kwa Waislamu? Na hasa pale tutakapofahamu kwamba hawa wasemao juu ya Shuraa, wanamchagua Khalifa kisha baada ya hapo wanashindwa kumbadilisha au kumuuzulu, na bila shaka Waislamu walijaribu kwa juhudi zao kumuuzulu Uthuman lakini alikataa akasema: "Siwezi kuvua kanzu aliyonivalisha Mwenyezi Mungu".


Na miongoni mwa mambo yanayotufanya tuzidi kuichukia nadharia hii, ni mambo tuyaonayo leo katika madola ya Magharibi yaliyoendelea, yanayodai kuwa na demokrasi katika kumchagua rais wa nchi, utaona vyama vingi vinagombea na kulumbana na kushindana ili kupata kiti cha utawala kwa gharama yoyote ile, na hutumika katika kazi hiyo mabilioni ya mail ambayo huhusishwa kwa ajili ya kampeni kwa kila njia, na hupoteza nguvu kubwa ya wanyonge miongoni mwa raia masikini ambao huenda wakawa na haja kubwa ya mail hizo, na mara mmoja wao anapofikia kwenye cheo cha urais basi upendeleo huwa unamchukua akawatawalisha wasaidizi wake na wajumbe wa chama chake na marafiki zake na nduguze, huwapa vyeo vya uwaziri na majukumu makubwa na sehemu nyeti katika idara, na wengine waliobaki huanza kumpinga katika kipindi cha urais wake ambacho waliafikiana (kumpa) na hapo huwa wanazusha uchochezi na hujaribu kwa juhudi zao kumuumbua na kumuangamiza, na katika yote hayo ni hasara tupu kwa raia wanaotawaliwa.


Basi ni mara ngapi watu wema wameangushwa na ni mara ngapi mashetani waovu wamenyanyuliwa kwa kutumia uhuru wa demokrasia chini ya vielelezo vizuri hatima yake liwat ikawa ni kanuni ya kisheria na zinaa badala ya kuoa ikawa ni maendeleo, na mambo kama haya yasemwe na hapana ubaya. Basi utukufu ulioje wa Aqida ya Shia pale wasemapo kuwa Ukhalifa ni msingi katika misingi ya dini, na ukoje Utukufu wa kauli yao kwamba cheo cha Ukhalifa ni uchaguzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hii ni kauli ya sawa kabisa na rai iliyoongoka inakubaliwa na akili na dhamira (na nafsi) hupoa. Kauli hiyo inaungwa mkono na maandiko yatokayo ndani ya Qur'an na sunna, pia inawakatisha tamaa wengine wenye mabavu, wafalme na masultani na inaeneza utulivu na amani katika jamii.8
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

KHITILAFU INAYOHUSU VIZTIO VIWILI Hapo kabla kwa kupitia uchambuzi uliotangulia tumefahamu mtazamo wa Mashia na Masunni kuhusu Ukhalifa na namna Mtume alivyoufanyia umma kwa mujibu wa kauli za makundi hayo mawili. Basi je, Mtume wa Mwenyezi Mungu aliuachia ummati wake kitu ambacho utakitegemea na kukirejea endapo itatokea hitilafu ambayo ni lazima itokee nayo ni ile aliyoisajili Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu chake aliposema: "Enyi mulioamini mtiini Mwenyezi Mungu na mumtii Mtume na wenye mamlaka miongoni mwenu, basi na kama mtahitilafiana kuhusu jambo fulani, lirejesheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume ikiwa ninyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kufanya hivyo ni bora na matokeo yaliyo mema." (Qur'an, 4:59)


Naam, hapana budi kwa Mtume (s.a.w.) auachie ummah kanuni utakayoitegemea, kwani yeye Mtume ametumwa kuwa ni Rehma kwa viumbe, naye ni mwenye hima juu ya ummati wake uwe ni umma bora kuliko nyumati zingine na usije ukahitilafiana baada yake na kwa ajili hii basi wamepokea Mashaba wake na wana hadithi kutoka kwake kwamba yeye amesema: "Nimekuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo kamwe hamtapotea baada yangu (navyo ni) Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu, na havitaachana viwili hivi mpaka vinifikie kwenye haudh, basi angalieni ni vipi mtakavyonifuata ndani ya viwili hivyo."

Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 148.
Na hadithi hii ni Sahih imethibiti na wameithibitisha wana hadithi kutoka pande zote mbili za Masunni na Shia, na wameisimulia ndani ya Musnad zao na katika sihahi zao kwa njia zaidi ya Masahaba thelathini. Na kwa kuwa mimi kama kawaida yangu sitoi hoja kupitia vitabu vya Mashia wala kauli za wanachuoni wao, basi imenilazimu niwataje wanachuoni wa Kisunni tu ambao wameithibitisha hadithi ya vizito viwili tena hali ya kuwa wanakiri juu ya usahihi wake ili uchambuzi huu siku zote uwe ni maudhui inayosifika kwa uadilifu (pamoja na kwamba uadilifu unapelekea pia kutaja kauli za Shia). Na hii ni orodha fupi ya wapokezi wa hadithi hii miongoni mwa wanachuoni wa Kisunni:


1) Sahih Muslim, Kitabu Fadhail Ali bin Abi Talib Juz. 7 uk.122.
2) Sahih Tirmidhi Juz. 5 uk. 328.
3) Al-Imamun-Nasai ndani ya Khasais yoke uk.21.
4) Imam Ahmad bin Hanbal Juz. 3 uk. 17.
5) Mustadrak Al-Hakim Juz. 3uk.l09.
6) Kanzul-Ummal Juz. 1 uk. 154.
7) At-Tabaqaatil-kubra cha ibn Saad Juz. 2 uk.194.
8) Jamiul-Usul cha Ibn Al-Athir Juz. 1 uk. 187.
9) Al-Jamius-Saghir cha Suyuti Juz.l uk.353.
10) Maj-Mauz-Zawaid cha Al-Haithami Juz.9 uk.163.
11) Al-Fat-Hul-Kabir cha Nabahani Juz. 1 uk.451.
12) Usudul-Ghabah Fi Maarifatis-Sahabah cha ibn Athir juz,. 2 uk. 12.
13) Tarikh ibn AsakirJuz. 5 uk.436.
14) Tafsiri ibn KathirJuz. 4 uk.113.
15) At-Tajul-Jami'u Lil-Usul, Juz.3 uk.308.


Zaidi ya hawa yuko ibn Hajar ambaye ameitaja ndani ya Kitabu chake kiitwacho As-Sawaiqul-Muhriqah (ameitaja) hali yakuwa anakiri kusihi kwake na A-Dhahabi ameitaja ndani ya Tal-Khis yake hali ya kuwa amekiri kusihi kwake kwa sharti ya masheikh wawili (Bukhar na Muslim). Na Al-Khawar Zami Al-Hanafi, ibn Maghazili As-Shafii na Tabrani ndani ya Muujam yake, vile vile mwenye Siratun-Nabawiyyah katika Hamish ya Siratul-Halabiyyah na mwenye Yanabiul-Mawaddah na wengineo... Basi Je, hivi inafaa baada ya haya mtu yeyote akadai kwamba hadithi hii ya vizito viwili (Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume) Masunni hawaifahamu na eti kuwa ni katika uzushi wa Kishia? Mwenyezi Mungu aiangamize chuki, mtindo wa fikra na upinzani wa kijinga. Kwa hiyo basi, hadithi ya vizito viwili ambayo ndani yake Mtume (s.a.w.) ameusia kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi chake kitukufu, ni hadithi mutawatir, na ni sanad itokayo kwa Maimamu watukufu (wa nyumba ya Mtume s.a.w.).


Basi ni kwa nini baadhi ya watu wanaitilia mashaka hadithi hii na wanajaribu kwa juhudi zao kuibadilisha iwe ni "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna zangu" pamoja na kuwa huyo mwenye kitabu cha "Miftahu Kunuzis-Sunnah" ameithibitisha katika ukurasa wa 478 kwa anuani isemayo, "Usia wake Mtume juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake," akiwa amenakili kwa Bukhari, Muslim, Tirmidhi na ibn Majah, lakini iwapo utafanya utafiti katika vitabu hivi vinne vilivyotajwa huenda usipate ishara ya karibu au ya mbali inayoashiria hadithi hii. Naam huenda ukapata ndani ya Bukhari anuani isemayo; "Mlango wa kushikamana na kitabu (cha Mwenyezi Mungu) na Sunnah" lakini hutaikuta hadithi hii. Sana sana kinachopatikana ndani ya Sahih Bukhar na katika vitabu vilivyotajwa ni hadithi isemayo:"Ametusimulia Tal-Hah bin Musarrif amesema:Nilimuuliza Abdallah bin Abi Afii r.a. (nikasema) hivi Mtume (s.a.w.) alikuwa ameusia? akasema, hapana nikasema, Vipi kumefaradhishwa kuusia kwa watu au wameamrishwa kuusia? akasema: Aliusia (kushikamana na) kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Taz: Sahihi Bukhari Juz. 3 uk. 186 oSahihi Tirmidhi Kitabul-Wasaya Sahihi Muslim Kitabul-Wasaya Sahihi ibn Majah Kitabul-Wasaya. Na wala hakuna hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ambayo ndani ya hadithi hiyo Mtume anasema:"Nimekuachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna yangu." Hata kwa makadirio ya kuwepo kwa hadithi hii ndani ya baadhi ya vitabu ni jambo lisilo na maana yeyote ile kwani Ijmai (makubaliano yaliyopo) yako kinyume cha hadithi hiyo kama ilivyotangulia hapa kabla. Kisha lau tutafanya uchambuzi kuhusu hii hadithi ya "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna yangu" tutaikuta haikubaliani na ukweli ulivyo siyo kwa maandiko wala kiakili nasi katika kuipinga hadithi hiyo tunayo baadhi ya mitazamo.

Mtazamo wa Kwanza: Wanahistoria na wanahadithi wameafikiana kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alizuia kuandika hadithi zake, na hapana yeyote aliyedai kwamba yeye alikuwa akiandika sunna ya Mtume katika zama zake, kwa hiyo kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo kuwa nimekuachieni "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna yangu " haikubaliki. Ama kuhusu Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kiliandikwa na kuhifadhiwa katika vifua (nyoyo) vya watu na iliwezekana kwa sahaba yeyote kurejea kwenye msahafu hata kama hakuwa miongoni mwa waliohifadhi.


Na ama kuhusu sunna ya Mtume hakuna kilichokuwa kimeandikwa au kukusanywa katika zama zake Mtume (s.a.w.), kwani sunna ya Mtume kama inavyoeleweka na kukubalika ni kila alichokisema Mtume au kukitenda au kukiri, na inavyofahamika pia ni kwamba Mtume alikuwa hawakusanyi Masahaba wake ili kuwafundisha sunna yake, bali alikuwa akizungumza katika kila tukio fulani na huenda wakahudhuria baadhi yao na huenda asiwe na mtu miongoni mwa Masahaba wake isipokuwa mmoja, basi itawezekana vipi kwa Mtume katika hali kama hii aseme kuwa nimekuachieni sunna yangu?

Mtazamo wa Pili: Pindi Mtume alipozidiwa na maumivu hali ambayo ilitokea siku tatu kabla ya kufariki kwake, aliwataka Masahaba wamletee karatasi na wino ili awaandikie maandiko ambayo kamwe hawatapotea baada yake, Umar bin Al-Khatab akasema, "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu anaweweseka, kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu." Taz: Sahih Bukhar, Babu Maradhin-Nabii Wawafatih Juz. 5 uk 138. Bila shaka lau Mtume wa Mwenyezi Mungu hapo kabla angekuwa amewaambia kwamba nimekuachieni "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna zangu," ni kwa nini Umar alisema kuwa, Kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu? Na kwa kufanya hivyo yeye na Masahaba waliokubali usemi wake huo watakuwa wanampinga Mtume wa Mwenyezi Mungu? Nami sidhani kama Masunni wanaliridhia jambo hili.!!


Kwa hiyo basi tumefahamu yakuwa hadithi hii ilizushwa na baadhi ya watu waliokuja baadaye ambao wanawachukia watu wa nyumba ya Mtume na hasa baada ya kuwaweka mbali na Ukhalifa, na inakuwa kama kwamba huyu aliyeizusha hadithi hii ya "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna yangu" alishangazwa kuwaona watu wameshikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na wamekiacha kizazi cha Mtume na kuwafuata watu wengine, basi akadhania kuwa kwa kuzusha hadithi hii atausahihisha mwenendo wao na kuepusha kukosolewa Masahaba ambao walikwenda kinyurne na usia wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.).

Mtazamo wa Tatu: Ni jambo maarufu kwamba tukio la kwanza lililomkabili Abubakar mwanzoni mwa Ukhalifa wake ni kule kuthibitisha kwake kuwapiga vita wanaozuwia kutoa zaka, licha ya upinzani wa Umar bin Al-Khatab dhidi yake na kutoa kwake ushahidi wa hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliposema: "Yeyote atakayesema Lailaha Illa llahu Muhammadun Rasulullah basi mali yake na damu yake vimehifadhika tokana nami isipokuwa kwa haki yake na hesabu yake iko kwa Mwenyezi Mungu". Basi lau kama sunna ya Mtume (s.a.w.) ingekuwa inajulikana, Abubakr asingekosa kuifahamu wakati yeye anastahiki mno kuijua sunna ya Mtume.


Pamoja na hayo hatimaye Umar bin Al-Khatab alikinaishwa na tendo la Abubakr kuibadilisha hadithi aliyoisimulia Umar na (pia akakinaishwa na) kauli ya Abubakr kwamba zaka ni haki iliyomo katika mali, lakini wao hao waliisahau au walijisahaulisha Sunna ya Mtume ya vitendo ambayo haikubali kubadilishwa, nayo ni ile inayohusu kisa cha Thalabah ambaye alikataa kutoa zaka kwa Mtume (s.a.w.), na Qur'an ikashuka kumuhusu huyo Thalabah. Pamoja na yote hayo Mtume wa Mwenyezi Mungu hakumuuwa Thalabah (kwa kukataa kwake kutoa zaka) wala hakumlazimisha kuitoa. Basi ni vipi hali ya Abubakr na Umar (je, hawakifahamu) kisa cha Usamah bin Zaid ambaye Mtume (s.a.w.) alimtuma kwenye jeshi fulani, na alipowavamia watu hao na kuwashambulia, alimkuta mtu fulani, alipomkamata yule mtu akasema, Lailah Illaha illa llah!! Lakini Usamah akamuuwa mtu yule, na khabari hizo zilipomfikia Mtume (s.a.w.) akasema, "Ewe Usamah umemuuwa baada ya kuwa amesema Lailaha Illa llah"? Usamah akasema:"Huyo alikuwa anajikinga tu" Basi Mtume (s.a.w.) hakuacha kukariri jambo hilo mpaka nikatamani lau nisingekuwa nimesilimu kabla ya siku hiyo. Taz: 1) Sahih Bukhar Juz. 8 uk. 36.


2) Sahih Muslim Juz. 1 uk. 67. Kwa hiyo basi, hatuwezi kuisadiki hadithi isemayo, "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna yangu" Kwani wao Masahaba ndiyo wa mwanzo kutoijua sunna ya Mtume, basi itakuwaje kwa wale waliokuja baada yao na itakuwaje kwa mtu ambaye maskani yake yako mbali na Madina? (Hatoifahamu kabisa Sunna ya Mtume).

Mtazamo wa Nne: Ni jambo maarufu pia kwamba mengi katika matendo ya Masahaba baada ya Mtume (s.a.w.) yalikuwa kinyume cha Sunna yake,kwa hiyo imma Masahaba hawa walikuwa wanaifahamu Sunna ya Mtume (s.a.w.) na waliikhalifu kwa makusudi kutokana na ijtihadi zao dhidi ya Nassi (matamko, matendo na iqrari) za Mtume (s.a.w.), na kwa ajili hiyo Masahaba hawa inawakumba kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pale aliposema:"Haiwi kwa Muumini wa kiume wala Muumini wa kike Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapoamua jambo wao wawe na hiyari katika jambo lao, na yeyote mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotevu ulio wazi." (Qur'an, 33:36) Na labda (tuseme) walikuwa hawaijui Sunna ya Mtume (s.a.w.), kwani haistahiki kabisa kwa Mtume (s.a.w.) katika hali kama hii kuwaambia Masahaba wake nimekuachieni Sunna yangu hali yakuwa yeye Mtume anajua kwamba Masahaba wake ambao ni watu wa karibu mno kwake hawaifahamu Sunna yake, basi hali itakuwaje kwa watakaokuja baada yao wakati hata Mtume hawakumfahamu na wala hawakumuona?


Mtazamo wa Tano: Inafahamika pia kwamba Sunna ya Mtume haikuandikwa isipokuwa katika zama za dola ya Bani Abbas, na kwamba kitabu cha mwanzo kilichoandikwa kuhusu hadithi ni "Muwataa" cha Imam Malik, na hiyo ni baada ya fitna kubwa (kupita) baada ya tukio la Karbala na kushambuliwa mji wa Madina, kisha kuuawa kwa Masahaba hapo mjini Madina. Basi ni vipi baada ya matukio hayo mtu atakosa kuwatilia mashaka wasimulizi wa hadithi (za Mtume) ambao walijipendekeza kwa watawala ili waipate dunia? Kwa ajili hiyo hadithi za (Mtume) zimevurugika na kupingana zenyewe kwa zenyewe, nao umma wa Kiislamu umegawanyika kwenye Madhehebu mengi (kiasi kwamba) jambo ambalo limethibiti kwenye madhehebu haya, kwenye madhehebu mengine halikuthibiti, na kitu ambacho kwa hawa wanakiona ni sahihi, wale wanakipinga. Ni vipi tutaamini kamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema kuwa "Nimekuachieni kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna yangu, na hali ya kuwa yeye anafahamu kwamba wanafiki na wapinzani watakuja mzulia? Hapana shaka Mtume (s.a.w.) alipata kusema,"Wako wengi wenye kunizulia, basi yeyote mwenye kunizulia na ajiandalie makazi yake motoni". Hivyo basi iwapo wazushi walikuwa wengi katika zama za uhai wake, ni vipi Mtume aulazimishe umma wake kufuata Sunna yake na hali hawaifahamu Sunna iliyo sahihi kutokana na ile isiyo sahihi na dhaifu kutokana na ile yenye nguvu?


Mtazamo wa Sita: Masunni wanasimulia ndani ya vitabu vyao sahihi kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ameacha vizito viwili au Makhalifa wawili au vitu viwili, na wakati mwingine wanasimulia kuwa (Mtume ameacha) kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume wake na wakati mwingine wanasimulia kuwa (Mtume amesema) shikamaneni na sunna zangu na sunna za Makhalifa waongofu baada yangu. Jambo la muhimu (inataka lifahamike) ni kuwa, hadithi hii ya mwisho inaongeza kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake (inaongeza) sunna za Makhalifa, hivyo misingi ya sheria inakuwa ni mitatu badala ya miwili. Na yote hii inapingana na hadithi ya vizito viwili ambayo ni sahihi kwa kuwa wameafikiana kwenye hadithi hiyo Masunni na Mashia nayo ni ile isemayo; "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu", hadithi ambayo tumekwisha taja zaidi ya rejea ishirini (inamopatikana) miongoni mwa rejea za Kisunni zinazotegemewa ukiachilia mbali rejea za Kishia ambazo hatukuzitaja.


Mtazamo wa Saba: Ikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu anafahamu vilivyo kwamba Masahaba wake ambao Qur'an ilishuka kwa lugha yao na Lahaja (Matamshi) yao (kama wasemavyo)-hawakuyafahamu mambo mengi miongoni mwa tafsiri ya (Qur'an) wala taawili yake, basi vipi itakuwa kwa watu watakaokuja baada yao, na ni vipi itakuwa kwa walioukubali Uislamu miongoni mwa Warumi na Wafursi na Wahabeshi na wote wasiokuwa Waarabu ambao hawakukifahamu Kiarabu wala kukizungumza? Na imethibiti katika athari ya kwamba Abubakr aliulizwa kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo: "Wafakihatan-Waabba" yaani, "Na matunda na malisho," basi Abubakr akasema:Ni mbingu gani itakayonifunika na ardhi gani itaniacha niketi humo endapo nitasema kuhusu kitabu cha Mwenyezi Mungu nisilolijua"? Taz: Al-Qastalani ndani ya Ir-shaad As-Sari Juz. 10 uk. 298 na ibn Hajar ndani ya Fat-h Al-Bari Juz. 13 uk. 230. Kama ambavyo Umar bin Al-Khatab pia hakuifahamu maana hii.

Imepokewa toka kwa Anas bin Malik amesema, "Hakika Umar bin Al-Khatab alisoma akiwa juu ya Minbar (Faanbat-naa Fiha Habban Wainaban Waqadh-ban Wazaitunan Wanakhlan Wahadaiqa Ghul-ban Wafakihatan Waabba) Yaani, "Kisha tukaotesha humo (vyakula vilivyo) chembe chembe, na mizabibu na mboga, na mizeituni na mitende, na mabustani yenye miti iliyosongamana na matunda na malisho". ( Qur 'an 80: 27- 31) Umar akasema: "Yote haya tunayajua, sasa hii Abban ni kitu gani? Kisha akasema: "Namuapa Mwenyezi Mungu hii ni takilifu (taabu) hulazimiki kufahamu nini Abban, fuateni yaliyobainishwa kwenu ndani ya kitabu, basi na muyatumie na yale msiyoyajua yategemezeeni kwa Mola wake". Taz: Tafsiri ibn Jarir Juz. 3 uk. 38 na Kanzul-Ummal Juz. 1 uk. 287, Al-hakim ndani ya Mustadrak Juz. 2 uk: 14 na Ad-Dhabi ndani ya Tal-Khis yake na Al-Khatib ndani ya Tarikh yake Juz. 11 uk. 468.


Na yasemwayo hapo kuhusu tafsiri ya kitabu cha Mwenyezi Mungu ndiyo yasemwayo kuhusu sunna tukufu ya Mtume, kwani ni hadithi ngapi za Mtume zimebakia kuwa ni mahali pa ikhitilafu baina ya Masahaba na baina ya Madhehebu na kati ya Masunni na Mashia, sawa sawa ikhtilafu hiyo iwe imekuja kutokana na usahihi wa hadithi au udhaifu wake, au tafsiri yake na kuifahamu hadithi hiyo, na kwa ufafanuzi ninamletea msomaji Mtukufu baadhi ya mifano kuhusu jambo hilo. 1. Khitilafu baina ya Masahaba juu ya kusihi kwa Hadithi au kuipinga Hadithi hiyo. Jambo hili lilimtokea Abubakr mwanzoni mwa siku zake za Ukhalifa pale bibi Fatmah binti ya Mtume (s.a.w.) alipomjia (Abubakr) akimtaka ampe shamba la Fadak ambalo Abubakr alilichukua kutoka kwa bibi Fatmah baada ya Mtume (s.a.w.) kufariki. Abubakr aliyakanusha madai ya bibi Fatmah yasemayo kwamba, baba yake bibi Fatmah ambaye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu alimzawadia shamba hilo zama za uhai wake, pia bibi Fatmah alimtaka Abubakr ampe mirathi ya baba yake. Basi Abubakr akawambia bibi Fatmah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema:"Sisi Mitume haturithiwi, chochote tulichokiacha ni sadaka."


Bibi Fatmah naye alimpinga Abubakr kuhusu hadithi hiyo (inayodaiwa) kuwa ni ya baba yake na alimpinga kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, na hapo ugomvi na khitilafu ukapamba moto kiasi kwamba bibi Fatmah alifariki akiwa kamkasirikia Abubakr wala hakumsemesha tena. Haya ni kama yalivyo ndani ya sahihi mbili, yaani Bukhar na Muslim. Kadhalika kuna khitilafu baina ya Aisha Ummul-muuminina na Abu Hurairah kuhusu Mtume, ambaye eti huamka asubuhi akiwa na janaba ndani ya mwezi wa Ramadhani. Kwa upande wa bibi Aisha anaona jambo hilo kuwa ni sahihi, wakati ambapo Abu Hurairah anaona kwamba mwenye kuamka asubuhi hali yakuwa ana janaba hana saumu.

Basi hebu kiangalie kisa hiki kwa ufafanuzi:
Imam Malik amethibitisha ndani ya Muwat-Taa, naye Bukhar ndani ya Sahihi yoke, imepokewa toka kwa bibi Aisha na Ummu Salamah wakeze Mtume (s.a.w.) kwamba wao wamesema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikuwa akiamka asubuhi akiwa na janaba inayotokana na jimai na siyo kujiotea katika mwezi wa Ramadhani kisha hufunga saumu" Na imepokewa toka kwa Abubakr bin Abdur-Rahman amesema:"Tulikuwa mimi na baba yangu tuko kwa Mar-wan bin Al-Hakam ambaye alikuwa ndiyo Amir wa Madina, akaelezwa kwamba Abu Hurairah anasema kuwa, mwenye kuamka asubuhi na janaba (katika mwezi wa Ramadhani) saumu ya siku hiyo ni batili." basi Mar-wan akasema:"Nakuapia ewe Abdur-Rahmah huna budi kwenda kwa mama wa waumini Aisha na Ummu Salamah ili uwaulize juu ya hilo" Abdur-Rahman alikwenda nami nikaenda naye mpaka tukaingia kwa Aisha akamsalimia kisha akasema, "Ewe Ummul-Muuminina, sisi tulikuwa kwa Mar-wan bin Al-Hakam akaambiwa kuwa Abu Hurairah anasema, mwenye kuamka asubuhi hali ya kuwa ana janaba, basi siku hiyo hana saumu, Aisha akasema, Sivyo alivyosema Abu Hurairah ewe Abdu Rahman je, hupendi kufanya vile alivyokuwa akifanya Mtume wa Mwenyezi Mungu"?


Abdur-Rahman akasema, "Hapana Wallahi", Aisha akasema, "Namshuhudia Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba yeye alikuwa akiamka hali yakuwa anayo janaba iliyotokana na jimai na siyo ya kujiotea kisha hufunga siku hiyo." Amesema, Kisha tulitoka mpaka kukaingia kwa Ummu Salamah na akamuuliza juu ya hilo, naye akasema kama alivyosema Aisha, amesema, "Nakuapia ewe Abdur-Rahman hakika utapanda mnyama wangu yuko hapo mlangoni, na uende kwa Abu Hurairah kwani yeye yuko kwake huko basi umueleze jambo hilo. Kisha Abdur-Rahman akapanda nami nikapanda pamoja naye mpaka tukafika kwa Abu Hurairah. Abdur-Rahman akazungumza naye kiasi cha muda kisha akamueleza jambo hilo, basi Abu-Hurairah akasema: "Mimi sina ujuzi wa jambo hilo kwani kuna mtu fulani tu alinieleza." Taz: Sahihi Bukhar Juz. 2 uk. 232.

Babus-Saim Yasbahu Junuban, Muwat-Taa ya Malik. Tan-Wirul-Hawalik Juz. 1 uk. 272. Muangalie ewe ndugu msomaji sahaba kama Abu-Hurairah ambaye kwa Masunni ni msimulizi (mashuhuri wa hadithi) katika Uislamu ni vipi anatoa fat-wa kwenye hukmu za dini yake kwa njia ya kudhani na kuinasibisha fat-wa hiyo kwa Mtume (s.a.w.) na hali yakuwa hamjui hata aliyemueleza hadithi hiyo! Kisa kingine cha Abu Hurairah ambacho ndani yake anajipinga mwenyewe. Amepokea Abdallah bin Muhammad, ametusimulia Hisham bin Yusuf, ametueleza Maamar naye kutoka kwa Az-Zuhri ambaye kapokea toka kwa Abu Maslamah naye toka kwa Abu Hurairah (r.a.) amesema "Amesema Mtume (s.a.w.), hapana kuambukiza wala ugonjwa wa manjano wala mkosi."

Bedui mmoja akasema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu itakuwaje kwa ngamia ambaye huwa mchangani kama paa kisha akachanganyika na ngamia mwenye upele akamuambukiza, Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, basi ni nani aliyemuambukiza yule wa kwanza"? Na imepokewa toka kwa Abu Salamah kwamba amemsikia Abu Hurairah akisema, "Mtume (s.a.w.) amesema, Mgonjwa asimkurubie asiyeumwa,"Kwa hiyo Abu Huraira akawa ameikanusha ile hadithi yake ya mwanzo sisi tukasema, "Siyo wewe uliyesimulia kwamba; hakuna kuambukiza? Basi akazungumza kihabeshi.(hatukumuelewa) Abu Salamah akasema basi sikumuona tena kusahau hadithi isipokuwa hiyo..."

Taz: Sahih Bukhar Juz. 7 uk. 31. Sahih Muslim Juz. 7 uk. 32. (Babu La 'Ad-wa- Walatirah). Ewe msomaji mwenye utambuzi hii ndiyo sunna ya Mtume, au ukipenda sema, "Haya ndiyo yanayonasibishwa kwa Mtume, mara Abu Hurairah aseme kwamba hana ujuzi wa hadithi yake ya mwanzo na kuwa eti kuna mtu fulani alimwambia, na mara nyingine wanapomkabili kutokana na kupingana (kwa hadithi zake) anashindwa kujibu lolote, bali anazungumza Kihabeshi ili asijefahamu yeyote yule."

Khitilafu kati ya bibi Aisha na ibn Umar. Ibn Juraij amesimulia akasema, "Nilimsikia'Ataa' akieleza akasema, Ur-wa bin Zubair amenieleza akasema, Nilikuwa mimi na Umar tumeegemea kwenye chumba cha Aisha na hali yakuwa tunamsikia anavyopiga mswaki , mimi nikasema, Ewe baba Abdur-Rahman Mtume alifanya Umrah katika mwezi wa Rajab, akasema, ndiyo, basi mimi nikamwambia Aisha, Ewe mama yangu unasikia ayasemayo baba Abdur-Rahman, akasema kwani anasemaje? Nikasema anasema kuwa Mtume alifanya Umra katika mwezi wa Rajab, basi bibi Aisha akasema "Mwenyezi Mungu amsamehe baba Abdur-Rahman naapa Mtume hakufanya Umrah katika Mwezi wa Rajab na hakuna Umrah aliyoifanya isipokuwa mimi nilikuwa pamoja naye. Amesema mpokezi, yote hayo Ibn Umar anayasikia na hakusema hapana wala ndiyo alinyamaza". Taz: Sahih Muslim Juz. 3 uk. 61. Sahih Bukhar Juz. 5 uk. 86.


2. Khitilafu za Madhehebu kuhusu Sunna ya Mtume. Ikiwa Umar na Abubakr wanahitilafiana kuhusu sunna ya Mtume (s.a.w.)[83] na iwapo Abubakr anatofautiana na bibi Fatmah juu ya sunna ya Mtume,[84] na kama wakeze Mtume (s.a.w.) wanahitilafiana kuhusu sunna ya Mtume (s.a.w.)[85] pia Abu Hurayrah anajipinga na kuhitilafiana na mwana Aisha juu ya sunna ya Mtume.[86] Si hivyo tu, bali ibn Umar anahitilafiana na bibi Aisha katika sunna ya Mtume[87] naye Abdallah ibn Abbas na ibn Zubair nao wanahitilafiana juu ya sunna ya Mtume.[88] Kama ambavyo Ali bin Abi Talib na Uthman wanahitilafiana kuhusu sunna ya Mtume[89] kadhalika Masahaba wanahitilafiana baina yao kuhusu sunna ya Mtume kiasi cha kuwafanya waliofuata baada yao kuwa na madhehebu zaidi ya sabini, basi ibn Masoud akawa na madhehebu yake, pia ibn Umar, ibn Abbas, ibn Zubair, ibn Uyaynah, ibn Juraij na Al-Hasan Al-Basri na Sufiyan Athauri, Malik, Abu Hanifah, Shafii, Ahmad bin Hanbal na wengineo wengi, lakini mabadiliko ya kisiasa yaliyauwa madhehebu mengine yote na hapakubakia isipokuwa madhehebu manne maarufu kwa Masunni.

Pamoja na kupungua idadi ya madhehebu lakini wanatofautiana katika mas-ala mengi ya Kifiqhi, na hiyo imekuja kutokana na kutofautiana kwao katika sunna ya Mtume, kwani mmoja wao huenda akajengea hukmu yake katika mas-ala fulani kufuatana na hadithi aliyoiona kuwa ni sahihi miongoni mwa hadithi za Mtume (s.a.w.) wakati ambapo mwingine atajitahidi kwa maoni yake atafanya makisio (Qiyas) katika mas-ala mengine kutokana na kukosekana "Nassi" - Qur'an au hadithi.
3. Ikhtilafu ya Sunni na Shia kuhusu Sunna ya Mtume. Amma ikhtilafu ya Sunni na Shia katika mas-ala haya huenda ni kwa ajili ya sababu mbili za msingi. Mojawapo ni kule kukosa kusihi kwa hadithi upande wa Shia, itakapokuwa mmoja wa wapokezi ni mwenye kutuhumiwa katika uadilifu wake japokuwa ni sahaba, kwani Mashia hawasemi kuwa Masahaba wote ni waadilifu kama hali ilivyo kwa Masunni. Zaidi ya hapo Mashia wanaipinga hadithi inayopingana na riwaya (mapokezi) ya Maimamu wa nyumba ya Mtume, ina maana kwamba wao hutanguliza riwaya ya Maimamu hawa kuliko riwaya ya wengine hata kama wana daraja gani. Na kwa kufanya hivyo wanazo dalili kutoka ndani ya Qur'an na Sunna iliyothibiti (kwao wao) hata kwa makhasimu wao, na hapo kabla baadhi yake zimeashiriwa.


Ama sababu ya pili kuhusu hitilafu iliyoko baina yao ni ile inayotokana na kufahamika kwa hadithi yenyewe, kwani huenda Masunni wakaifasiri vile ambavyo wasivyoifasiri Mashia, kama ile hadithi ambayo tumeionesha hapo kabla nayo ile kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema: "Ikhitilafu katika umma wangu ni rehma". Masunni huifasiri kwamba inahusu ikhtilafu ndani ya madhehebu manne katika mambo ya Kifiqhi kuwa hiyo ni rehma kwa Waislamu. Wakati ambapo Mashia huifasiri kuwa ni safari ya baadhi yao kwenda kwa wengine na kutilia mkazo suala la elimu (katika safari hizo) na mengineyo miongoni mwa mambo yenye faida. Au huenda tofauti baina ya Shia na Masunni ikawa siyo katika maf-humu ya hadithi ya Mtume, bali ikahusu mtu au watu waliokusudiwa na hadithi hiyo, na hilo ni kama ilivyo kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema: "Shikamaneni na sunna yangu na sunna ya Makhalifa waongofu baada yangu". Masunni huwa wanamaanisha kuwa waliokusudiwa hapo ni Makhalifa wanne, ama Mashia wao humaanisha kuwa ni Maimamu kumi na wawili kwa kuanza na Ali bin Abi Talib na kumalizia kwa Mahdi Muhammad bin Al-Hasan Al-Askari (a.s.).


Au kama vile kauli yake Mtume (s.a.w.) aliposema: "Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili na wote ni Maquraish". Mashia humaanisha kuwa ni Maimamu kumi na wawili kutoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.) wakati ambapo Masunni hawapati tafsiri ya kutosheleza kwenye hadithi hii, na kwa hakika wamehitilafiana (Mashia na Masunni) hata katika matukio ya kihistoria ambayo yanahusiana na Mtume (s.a.w.) kama ilivyo kuhusu siku aliyozaliwa Mtume, kwani Masunni husherehekea kuzaliwa kwa Mtume tarehe kumi na mbili mfunguo sita wakati Mashia husherehekea tarehe kumi na saba mwezi huo huo. Basi naapa, hakika hitilafu hii kuhusu sunna ya Mtume ni jambo la kawaida halikwepeki kama kutakuwa hakuna rejea watayoirejea wote na hukumu yake ipite na rai yake ikubalike kwa wote kama alivyokuwa Mtume (s.a.w.), kwani alikuwa akikata chanzo (chochote) cha hitilafu na akivunja ugomvi (vurugu) na kuhukumu kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu amemuonyesha hivyo (wafuasi wake) husalim amri japokuwa ndani ya nyoyo zao kuna dhiki (uzito), kwa hiyo kupatikana kwa mtu kama huyu ni jambo la lazima katika maisha ya umma (wa Kiislamu) kwa muda wote!!


Hivi ndivyo inavyohukumu akili na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) hawezi kughafilika kwa hilo na hali ya kuwa anafahamu kwamba umati wake utayabadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu baada yake, basi ikawa ni lazima kwake kuuwekea umma wake mwalimu mwenye uwezo wa kuuongoza kwenye njia ya sawa pindi utakapotaka kupinda kutoka kwenye njia iliyonyooka. Na bila shaka Mtume aliuandalia kwa vitendo umma wake kiongozi Mtukufu ambaye yeye Mtume alitoa kila juhudi zake kumlea na kumfunza (kiongozi huyo) tangu alipozaliwa mpaka akafikia ukamilifu na kwa Mtume akawa na daraja ya Harun kwa Musa kisha akamkabidhi jukumu hili tukufu kwa kusema:
"Mimi nitapigana nao katika kushuka Qur'an nawe utapigana nao katika kuiawili" Taz: Al-Khawar-Zami ndani ya Manaqib uk. 44, Yan-Abiul-Mawaddah uk. 233. Al-Isabah cha ibn Hajar Al-Asqalani Juz.l uk. 25, Kifayatut-Talib uk. 334, Muntakhab Kanzil-Uinmal Juz. 5 uk. 36. Ih-Qaqul-Haqqi Juz. 6 uk. 36.

Na kauli yake Mtume isemayo: "Wewe ewe Ali utaubainishia umma wangu yale watayotofautiana ndani yake baada yangu". Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 122, Tarikh Dimishq ya ibn Asakir Juz. 2uk. 488, Al-Manaqib cha Al-Khawarzami uk. 236, Kanzul-Haqaiq cha Al-Manawi uk. 203, Muntakhab Kanzil-Ummal Juz. 5 uk.33, Yanabiul-Mawaddah uk. 128. Basi ikiwa kama Qur'an ambayo ni kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu inahitajia mtu atakayeipigania katika njia ya kuifasiri na kuiweka bayana, kwa kuwa chenyewe ni kitabu ambacho hakisemi na kimebeba namna nyingi mbalimbali, na ndani yake kuna mambo ya dhahiri na yaliyojificha (yahitaji ufafanuzi) basi itakuwaje kuhusu hadithi za Mtume? Na kama mambo yako namna hii kuhusu kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna, basi haiwezekani kwa Mtume (s.a.w.) kuuachia umma wake vizito viwili vilivyo kimya visivyozungumza, kwani wenye nyoyo potovu hawataacha kuvibadilisha kwa lengo lao na wafuate zenye kushabihiana kwa kutaka fitna na kutaka dunia na itakuwa ni sababu ya kupotea wale wataokuja baada yao, kwani wao wamewadhania dhana nzuri na wakaitakidi juu ya uadilifu wao, na siku ya kiyama watajuta ndipo itakapothibitika kwao kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:


"Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa (kuunguzwa) motoni watasema, laiti tungemtii Mwenyezi Mungu na tungemtii Mtume, na watasema, Mola wetu hakika tuliwatii mabwana wetu na wakubwa wetu basi wametupoteza njia, Mola wetu wape hawa adhabu maradufu na uwalaani laana kubwa" (Qur'an, 33:66-68) "Kila utakapoingia umma utawalaani wenzao mpaka watakapokusanyika wote humo wa nyuma yao watasema kwa wale wa mwanzo wao, Mola wetu hawa ndiyo waliotupoteza basi wape adhabu ya moto maradufu, atasema itakuwa kwenu nyote (adhabu) maradufu lakini ninyi hamjui" .(Qur'an, 7:38)

Bila shaka upotevu haukuwa isipokuwa kwa mambo kama hayo, kwani hakuna umma ambao Mwenyezi Mungu aliutumia Mtume akawabainishia njia na kuwamulikia mahala pa kupita lakini wao (hao wenye kubainishiwa) baada ya Mtume wao walikuwa wakigeuza na kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu, basi je, mwenye akili anadhani kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu Isa (a.s.) aliwaambia Wakristo kwamba yeye ni Mungu? Kamwe hakuwaambia hivyo; "Sikuwaambia isipokuwa yale uliyoniamuru" Lakini matamanio na matakwa (yao) na kuipenda dunia ndiyo yaliyowavuta Wakristo kufanya hilo, je hakuwabashiria Nabii Isa kuja kwa Muhammad? Na kabla yake Musa aliwabashiria pia, lakini wakabadilisha jina la Muhammad na Ahmad kuwa "Mwokozi" nao mpaka leo bado wanamngojea!


Na je, Umati wa Mtume Muhammad ulikuwa umegawanyika kwenye madhehebu na vikundi vingi kufikia sabini na tatu na vyote vitaingia motoni isipokuwa kundi moja (hayakutokea haya) isipokuwa kwa sababu ya kubadilisha (ukweli ulivyo), na leo hii sisi tunaishi katikati ya vikundi hivi, je, kipo kikundi ambacho chenyewe kinajisema kuwa kimepotea, au kwa maelezo mengine? Je, kipo kikundi kimoja ambacho kinadai kwamba kimekwenda kinyume na kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume wake? Kinyume chake ni kwamba kila kikundi kinasema kuwa chenyewe ndicho kilichoshikamana na Kitabu (Qur'an) na Sunna, basi ufumbuzi uko wapi?

(Tuseme) ufumbuzi wa hili ulikuwa umefichika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) au zaidi ya hapo (tuseme ufumbuzi wake ulifichika) hata kwa Mwenyezi Mungu? Namuomba Mwenyezi Mungu anisamehe, bila shaka yeye ni mpole kwa waja wake na anawapendelea mema, basi hapana budi awawekee ufumbuzi ili aangamie mwenye kuangamia hali yakuwa panaubainifu. (Nijuu yake kuchagua uongofu au upotofu). Siyo katika utaratibu wa Mwenyezi Mungu kuwapuuza viumbe wake na kuwaacha bila ya uongofu, vinginevyo basi labda kama tutaitakidi kwamba yeye ndiye aliyewatakia khitilafu hizo na vikundi hivyo na upotevu ili tu awatupe ndani ya moto wake, na hiyo ni itikadi batili na mbaya.

Namuomba Mwenyezi Mungu anisamehe na ninatubia kwake kutokana na kauli hii ambayo hailingani kabisa na utukufu wa Mwenyezi Mungu na hekima yake na uadilifu wake. Basi ile kauli ya Mtume (s.a.w.) kwamba yeye ameacha kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume wake siyo ufumbuzi unaoingia akilini kuhusu qadhiya yetu, bali inatuongezea utata na taawili ambayo haikati mzizi wa wenye fitna na wenye kupotoka, kwani huwaoni pale walipotoka dhidi 'ya Imam wao walinyanyua kitambulisho kisemacho: "Hapana hukmu yako ewe Ali bali hukmu ni ya Mwenyezi Mungu!! Hakika kwa nje ni kitambulisho kizuri, kinaichukua akili ya msikilizaji akadhani kuwa msemaji anahamu ya kutekeleza hukmu za Mwenyezi Mungu, na anapinga hukmu isiyokuwa hiyo miongoni mwa hukmu za watu, lakini ukweli halisi hauko hivyo. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Na wako miongoni mwa watu ambao kauli zao hapa duniani zinakufurahisha na humshuhudisha Mwenyezi Mungu yaliyomo nyoyoni mwao na hali wao ni wagomvi wakubwa kabisa". (Qur'an, 2:204) Naam ni mara ngapi tunahadaika kwa vitambulisho ambavyo dhahiri ni vizuri na wala hatujui ni kitu gani kilichojificha nyuma yake, lakini Imam Ali analifahamu hilo kwani yeye ni mlango wa mji wa elimu yeye aliwajibu "Hakika hayo ni maneno ya kweli yamekusudiwa (kutekeleza) uovu ".


Naam, ni maneno yaliyo ya kweli lakini yanakusudiwa (kutekeleza) maovu ilikuwaje hali hiyo? Ni wakati Makhawarij wanamwambia Imam kuwa, "Hukmu ni ya Mwenyezi Mungu na siyo yako ewe Ali". Je, hivi Mwenyezi Mungu atajidhihirisha hapa ardhini na awapambanulie yale waliyohitilafiana? Au wao wanafahamu kuwa hukmu ya Mwenyezi Mungu imo ndani ya Qur'an, lakini Ali ameibadilisha kwa maoni yake? Ikoje, basi hoja yao na ya yule asemaye kuwa wao ndiyo waliyoibadilisha hukmu ya Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa Ali ndiye mjuzi mno kuliko wao na ndiye aliyetangulia kusilimu?

Kwa hiyo hicho ni kitambulisho kizuri ili kuwadanganya watu wenye mawazo ya kawaida wapate kuwaunga mkono na kuwasaidia kumpiga vita Imam Ali na ili wapate maslahi yao kwa vita hivyo, kama inavyotokea leo hii kwani nyakati ni nyakati, na watu ni watu tu, vituko na vitimbi haviishi bali vinazidi kukua kwani wenye vitimbi wa zama hizi wanafaulu kutokana na uzoefu wa wale wa mwanzo, ni mara ngapi maneno ya kweli yanakusudiwa uovu katika siku zetu hizi? Ni anuani nzuri kama ile ambayo wanaitangaza Mawahabi mbele ya Waislamu nayo ni "Tauhidi, kutofanya shirki", basi ni nani miongoni mwa Waislamu atakayekosa kukubali?

Na kama vile kundi fulani la Waislamu kujiita wenyewe kuwa ndiyo "Ahlis-Sunnah wal-Jamaa" Basi ni nani miongoni mwa Waislamu ambaye hatakubali kuwa pamoja na jamaa ambayo inafuata sunna za Mtume? Na kama kitambulisho cha Mabaathi (chama cha siasa Iraq na Syria) ambacho kina anuani isemayo, "Ummah mmoja wa Kiarabu wenye ujumbe wa kudumu" basi nani miongoni mwa Waislamu ambaye hatahadaika na kitambulisho hiki? Kabla hajafahamu undani wa chama cha Baath ambacho muasisi wake ni Mkristo aitwaye Mit-chel Aflaq? Ewe Ali bin Abi Talib, hapana shaka hekima yako imebakia na itaendelea kubakia, ni yenye kuvuma katika masikio ya zama zote, kwani ni maneno mangapi ya kweli lakini yamekusudiwa batili?


Kuna mwanachuoni fulani alipanda kwenye kiriri cha kutolea khutba na akatangaza kwa sauti kubwa akasema:"Yeyote mwenye kusema kwamba mimi ni Shia sisi tunasema wewe ni kafiri, na yeyote atakayesema mimi ni Sunni tunamwambia wewe ni kafiri, sisi hatutaki Shia wala Sunni bali tunataka Uislamu tu." Hakika ni maneno ya kweli lakini yamekusudiwa uovu, kwani ni Uislamu gani autakao mwanachuoni huyu? Na katika ulimwengu wetu leo kuna Uislamu wa aina nyingi, bali hata katika karne ya mwanzo Uislamu ulikuwa wa aina nyingi. Kuna Uislamu wa Ali na Uislamu wa Muawiyah na kila mmoja wao anao wafuasi wanaomuunga mkono mpaka mambo yakafikia kupigana. Pia upo Uislamu wa Husein na Uislamu wa Yazid aliyewaua watu wa nyumba ya Mtume eti kwa niaba ya kutetea Uislamu, na Husein (alionekana) katoka nje na Uislamu kwa ajili ya kumpinga Yazid. Upo pia Uislamu wa Maimamu wa nyumba ya Mtume na wafuasi wao, na kuna Uislamu wa watawala na raia zao na kila siku zinavyopita tunakuta tofauti baina ya Waislamu. Si hivyo tu, bali upo Uislamu wa kuwaachia watu watende wapendavyo (ilimradi wao ni Waislamu) kama wanavyouita watu wa Magharibi kwani wafuasi wa Uislamu huu wanawapendelea Mayahudi na Wakristo na wanawanyenyekea wenye nguvu kubwa (Marekani na Urusi wakati huo). Kadhalika upo Uislamu wa siasa kali kama unavyoitwa na watu wa magharibi kuwa ni Uislamu usiopenda mageuzi au hata kuwaita wendawazimu?


Na baada ya yote haya hakuna nafasi inayobakia ya kuisadiki hadithi ya "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna yangu" Kutokana na sababu zilizotajwa. Ukweli unabakia kuwa wazi katika ile hadithi ya pili ambayo Waislamu wameafikiana kwayo, nayo ni ile isemayo "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu," kwani hadithi hii inatatua matatizo yote na hakuna ikhtilafu inayobakia katika kuiawili aya yoyote ndani ya Qur'an, na au kuisahihisha na kuifasiri hadithi yoyote ile ya Mtume pindi tutakapowarejea watu wa nyumba ya Mtume ambao tumeamriwa kuwarejea hasa pale tutakapofahamu kwamba hawa ndiyo ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwabainisha kuwa ndiyo wanaostahiki kwa hilo. Hakuna Mwislamu yeyote mwenye mashaka juu ya elimu yao nyingi, uchamungu wao na kuipa kwao nyongo dunia, na bila shaka Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu, akawatakasa na kuwarithisha elimu ya kitabu (Qur'an), basi hawakhitilafiani kuhusu kitabu hicho wala hawatatengana nacho mpaka siku ya Qiyama. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema:

"Hakika ninaacha kwenu makhalifa wawili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooshwa kutoka mbinguni hadi ardhini, na kizazi changu watu wa nyumba yangu, bila shaka viwili hivyo havitatengana mpaka vinifikie kwenye Haudhi". Taz: 1) Musnad Ahmad bin Hanbal, Juz. 5 uk. 122.


2) Ad-Durrul-Manthoor Juz. 2 uk. 60.
3) Kanzul-UmmalJuz. 1 uk. 154.
4) Maj-Mauz-Zawaid Juz. 9 uk. 162.
5) Yanabiul-Mawaddah uk. 38 na 183.
6) Abaqatul-An-war Juz. 1 uk. 16.
7) Mustdrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 148.

"Na ili niwe pamoja na wakweli Assadiqina, inanipasa kusema haki na isinizuwie kufanya hivyo lawama ya yeyote mwenye kulaumu, na lengo langu ni kupata radhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuiridhisha dhamiri yangu kabla ya watu kuniridhia". Na ukweli uliyomo ndani ya uchunguzi huu uko upande wa Mashia ambao wamefuata wasia wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusu kizazi chake na wamewatanguliza juu ya nafsi zao, na wakawafanya kuwa ni Maimamu wao ambao kwao hujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwapenda na kuwafuata. Hakika wanastahiki pongezi kwa kufuzu hapa duniani na huko akhera pale atakapofufuliwa mtu pamoja na yule aliyempenda, basi ana hali gani siku hiyo aliyewapenda (watu wa nyumba ya Mtume) na akafuata uongofu wao?


AmesemaAz-Zamakhshari kuhusu makusudio haya: "Yamekuwa mengi mashaka na ikhtilafu, na kila mmoja anadai kuwa yeye ndiyo njia ya sawa. Mimi nimeshikamana na Lailaha Illa llah, na mapenzi yangu yako kwa Ahmad na Ali. Hakika mbwa alifaulu kwa kuwapenda watu wa pangoni (As-habul-Kahfi), basi vipi mimi niwe muovu kwa kukipenda kizazi cha Mtume? Ewe Mwenyezi Mungu tujaalie tuwe miongoni mwa wanaoshikamana na kamba ya kuwatawalisha wao (kizazi cha Mtume), na utujaalie miongoni mwa wapitao njia zao na wale wapandao ndani ya Merikebu yao na wale wanaoueleza Uimamu wao na wenye kufufuliwa katika kundi lao, bila shaka wewe unamuongoa umtakaye kwenye njia iliyonyooka.9
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

QADHAA NA QADAR (KWA MASUNNI) Katika maisha yangu yaliyopita Qadhaa na Qadar lilikuwa ni fumbo gumu, kwani sikulipatia tafsiri inayotosheleza ambayo itaipumzisha fikra yangu na kuukinaisha moyo wangu, hivyo nilibakia mwenye kuchanganyikiwa baina ya mafunzo niliyoyasoma katika madarasa ya Masunni ya kwamba mtu ni mwenye kuendeshwa (hana hiyari) katika matendo yake yote kwa yale yanayowafiki, "Kila mtu amefanyiwa wepesi kutenda aliloumbiwa" Ni kwamba (inasemwa) Mwenyezi Mungu Mtukufu huwatuma Malaika wawili miongoni mwa Malaika kwenda kwa mtoto aliye tumboni mwa mama yake na humo huandika muda wake na rizki yake na kazi yake, na kama atakuwa muovu au mwema,[90] (nilibaki ndani ya itikadi hii hali ya kuwa nimechanganyikiwa hivyo) na baina ya kile ambacho kinashinikizwa na akili yangu na nafsi yangu katika uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutokuwa kwake dhalimu kwa viumbe wake. Itakuwaje awashinikize kwenye matendo fulani kisha awaadhibu kwa ajili ya makosa aliyowaandikia na akawashinikiza wayafanye?


Hapana shaka nilikuwa kama wengine miongoni mwa vijana wa Kiislamu nikiishi katika fikra hizo zinazogongana katika mtazamo wangu kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye yeye mwenye nguvu mwenye uwezo ambaye haulizwi yale ayatendayo nao viumbe wataulizwa (Qur'an 21:23). Naye ni mwenye kufanya alitakalo (Qur'an 85:16). Amewaumba viumbe akawagawa, sehemu fulani miongoni mwao itakuwa peponi na sehemu nyingine motoni, kisha yeye ni mwingi wa rehma mpole mwenye kurehemu waja wake, hadhulumu kiasi hata cha chembe ndogo (Qur'an, 4:40). "Na Mola wako si mwenye kuwadhulumu waja" (Qur'an Fus-silat, 46). "Bila shaka Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu chochote lakini watu wanajidhulumu nafsi zao (Qur'an. 10:44).

Kisha yeye Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma mno kuliko mwanamke alivyo na huruma kwa mwanawe kama ilivyokuja ndani ya hadithi tukufu. BukhariJuz. 7 uk. 75. Na ni mara nyingi kulikuwa kukijitokeza kupingana ndani ya akili yangu kuhusu aya za Qur'an Tukufu, kwani wakati mwingine nilikuwa nikifahamu kwamba mtu anafahamu ndani ya nafsi yake naye peke yake ndiye mwenye jukumu la matendo yake. "Basi yeyote atakayetenda wema wenye uzito wa chembe (ndogo) atauona (wema huo) na yeyote mwenye kutenda uovu wenye uzito wa chembe (ndogo) atauona (uovu huo)." (Qur'an, 99:7-8)

Na wakati mwingine nilikuwa nikifahamu kwamba, mtu ni mwenye kuendeshwa na hana ujanja wala nguvu, hana mamlaka ya nafsi yake kujinufaisha, na au kukinga madhara wala namna ya kutafuta rizki. "Wala hamtataka (kitu) isipokuwa atake Mwenyezi Mungu" (Qur'an, 76:30). "Mwenyezi Mungu humpotoa amtakaye na humuongoa amtakaye" (Qur'an 35:8). Na siyo mimi peke yangu bali Waislamu wengi wanaishi katika hali hii ya kupingana kifikra na ndiyo maana utawakuta Masheikh wengi na wanachuoni pindi unapowauliza juu ya maudhui ya Qadhaa na Qadar huwa hawapati jawabu la kukinaisha nafsi zao wenyewe kabla ya kuwakinaisha wengine bali wao husema, "Maudhui hii si lazima kuingia kwa undani". Kuna baadhi yao huharamisha kuichimbua kwa undani na husema: "Inapasa kwa Muislamu kuamini Qadhaa na Qadar za kheri na shari, na kwamba zote zinatoka kwa Mwenyezi Mungu."


Na pindi mpinzani anapowauliza: "Ni vipi Mwenyezi Mungu atamshinikiza mja wake kutenda maovu kisha amtupe motoni"? Basi Masheikh hao humtuhumu kukufuru na uzandiki na kuwa eti ametoka katika dini, na tuhuma nyinginezo mbaya zisizokuwa hizo. Na kwa sababu hiyo akili (za watu) zimepooza na kutindia, imani (zao) zinaamini kwamba kuoa (hakupatikani ila) kama umeandikiwa, na talaka ( nayo haituki ila) kama imeandikwa, na hata kuzini (nalo ni suala la) kuandikiwa kwani wanasema, "Kila utupu umeandikiwa jina la yule utakayemuoa. Si hivyo tu,bali hata kunywa pombe, kuua nafsi na hata kula na kunywa huwezi kula wala kunywa isipokuwa kile alichokuandikia Mwenyezi Mungu!

Niliwaambia baadhi ya wanachuoni wetu (wa Kisunni) baada ya kuyaaridhi mas-ala haya kwamba, "Qur'an inapinga madai haya na wala haiwezekani kwa hadithi kuipinga Qur'an!! Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu jambo la kuoa "Waoweni muwapendao katika wanawake" (Qur'an, 4:3) Aya hii inajulisha juu ya kuwa na hiyari, na amesema Mwenyezi Mungu kuhusu talaka, "Talaka ni mara mbili, kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa wema" (Qur'an, 2:229). Hii nayo pia ni hiyari. Na kuhusu zinaa amesema, "Musiikurubie zinaa hakika ni jambo chafu na ni njia mbaya (Qur'an, 12:32).


Hii nayo ni dalili ya kuwa na hiyari. Kuhusu pombe amesema, "Hakika shetani anataka kukutilieni uadui na bughdha baina yenu kwa ajili ya pombe, na kamari, na anataka kukuzuwieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali basi komeni (kunywa pombe) (Qur'an5:91). Nayo pia inakataza kwa maana ya kuwa na hiyari. Amma kuua nafsi Mwenyezi Mungu amesema kuhusiana na jambo hilo,"Na msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha (kuiua) isipokuwa kama kuna haki (ya kuuawa)" (Qur'an, 6:151) Na amesema tena Mwenyezi Mungu: "Na yeyote atakayemuua Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni motoni, ataishi humo milele, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia,amemlaani na amemuandalia adhabu kali" (Qur'an, 4:93) Aya hii pia inaonyesha hiari kuhusu kuua. Na hata mambo yanayohusu kula na kunywa, Mwenyezi Mungu ametuwekea mipaka akasema: "Na kuleni na mnywe lakini msivuke mipaka hakika yeye Mwenyezi Mungu hawapendi wanaovuka mipaka" (Qur'an 7:31). Kadhalika hii inaonyesha hiyari.

Basi ni vipi ewe Bwana wangu baada ya dalili zote hizi za Qur'an ninyi (bado) mwasema kwamba kila kitu kinatokana kwa Mwenyezi Mungu na mja yeye ni mwenye kuendeshwa katika matendo yake yote? Alinijibu akasema kwamba, "Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye peke yake ndiye ambaye anauendesha ulimwengu na akatolea ushahidi kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Sema: Ewe Mola uliyemiliki ufalme wote, humpa ufalme umtakaye, humuondolea ufalme umtakaye, humtukuza umtakaye, na humdhalilisha umtakaye, kheri imo mkononi mwako bila shaka wewe ni mwenye uwezo juu ya kilakitu".(Qur'an,3:26) Mimi nikasema: "Hapana hitilafu yoyote baina yetu juu ya kutaka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na pindi anapotaka kufanya jambo, mtu au jini wala viumbe wengineo hawana uwezo wa kupinga kutaka kwake, bali hitilafu iliyopo ni kuhusu matendo ya waja, je, matendo hayo yanatokana na waja au yanatokana kwa Mwenyezi Mungu"?


Akanijibu: "Ninyi muna dini yenu nami nina dini yangu" Hapo akaufunga mlango wa majadiliano kutokana na usemi huo. Basi hizi mara nyingi ndizo hoja za wanachuoni wetu, na ninakumbuka kwamba nilirejea baada ya siku mbili nikamwambia "Ikiwa itikadi yako ni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye atendaye kila kitu na waja hawana hiyari ya kufanya chochote, basi ni kwa nini husemi kuhusu Ukhalifa kama hivi usemavyo, ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye ndiye mwenye kuumba na kuchagua na wao (waja) hawana hiyari"? Akasema: "Ndiyo hivyo ndivyo nisemavyo, kwani Mwenyezi Mungu ndiye aliyemchagua Abubakar na Umar na Uthman kisha Ali, lau Mwenyezi Mungu angelimtaka Ali awe ndiye Khalifa wa kwanza, basi watu na majini wasingeweza kulizuwia jambo hilo." Mimi nikasema:"Sasa umenasa." Akasema, "Kwa vipi nimenasa?" Nikasema: "Basi imma useme kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliye wachagua hao Makhalifa wanne kisha baada ya hapo akawaachia watu uamuzi wa yule wamtakaye, na imma useme kwamba Mwenyezi Mungu hakuwaachia watu uamuzi wa kumchagua wamtakaye bali yeye ndiye humchagua kila Khalifa tangu kufariki Mtume mpaka siku ya Qiyama"


Akajibu: "Nasema tena mara ya pili, "Sema, Ewe Mola uliyemiliki ufalme wote, unampa ufalme (mtu) umtakaye na unamuondolea ufalme umtakaye " Nikamwambia, "Kwa hiyo kila upotofu na kila maovu yaliyotokea katika Uislamu kutokana na wafalme na watawala yote yanatokana kwa Mwenyezi Mungu, kwani yeye ndiye aliyewatawalisha watu hawa juu ya shingo za Waislamu? Akajibu: "Ndivyo ilivyo na miongoni mwa wema wako waliosoma hivi, "Na tukitaka kuangamiza kijiji tunawapa amri watu wa kijiji wanaishi kwa raha yaani tunawafanya maamiri" Nikasema hali ya kushangazwa:"Kwa hiyo kuuawa kwa Ali kwa mkono wa Ibn Mul-Jam na kuuawa Husein bin Ali ni kutaka kwake Mwenyezi Mungu"?

Akasema katika hali ya kujitetea: "Naam, moja kwa moja, je, hukupata kuisikia kauli ya Mtume kumwambia Ali, "Mtu muovu mno katika watu wa hapo baadaye ni yule atakayekupiga juu ya hiki mpaka zilowane hizi, na akaashiria kichwa chake (Ali) na ndevu zake, na hivyo hivyo Imam Husein, Mtume (s.a.w.) aliyafahamu mauaji yake huko Karbala na alimsimulia mama Ummu Salama juu ya mauaji hayo, kama ambavyo Mtume alifahamu kwamba Sayyidna Hassan Mwenyezi Mungu ataleta upatanishi kupitia kwake kati ya makundi mawili makubwa miongoni mwa Waislamu. Basi kila kitu kimeandaliwa na kuandikwa tangu hapo zamani na mtu hana njia ya kukwepa, na kwa hali hii wewe ndiyo umenasa na siyo mimi."


Nilinyamaza kidogo na kumuangalia hali ya kuwa anatamba kwa maneno haya, akidhani kwamba ameninyamazisha kwa dalili madhubuti, (nikitafakari) ni vipi nitamkinaisha ya kwamba kujua kwa Mwenyezi Mungu juu ya kitu fulani haimaanishi moja kwa moja kwamba yeye ndiye aliyekadiria na kuwashinikiza watu juu ya kitu hicho, nami natambua tangu hapo mwanzo kwamba fikra yake haiwezi kuzingatia nadharia kama hii. Nilimuuliza tena mara nyingine: "Kwa hiyo marais na wafalme waliopita na waliopo sasa ambao wanaupiga vita Uislamu na Waislamu, Mwenyezi Mungu ndiye aliyewatawalisha? Akasema, "Bila shaka". Nikamwambia, "Hata wakoloni wa Kifaransa walioitawala Tunisia, Al-geria na Morocco nao ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu". Akasema: Ndiyo, kwani pindi ulipofika wakati maalum Wafaransa waliondoka kwenye nchi hizo". Mimi nikasema: Sub-hanallah!! Basi ni vipi ulikuwa ukiitetea nadharia ya Masunni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikufa na kuliwacha jambo la Ukhalifa liwe la mashauriano baina ya Waislamu ili wamchague wamtakaye"? Akasema:"Mpaka sasa bado niko kwenye msimamo huo na nitabakia hivyo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu".


Nikasema: "Basi ni vipi unakubaliana na kauli mbili, uchaguzi wa Mwenyezi Mungu na uchaguzi wa watu kwa mashauriano"? Akasema:"Hiyo ni kwa kuwa Waislamu walimchagua Abubakar basi bila shaka Mwenyezi Mungu kishamchagua"! Nikasema: "Aliwateremshia Wahyi (ufunuo) hapo Saqifah kuwajulisha juu ya kumchagua Khalifa"? Akasema:Astaghfirullah!!(Mwenyezi Mungu anisamehe) hapana Wahyi baada ya Muhammad kama wanavyoamini Mashia. (Mashia kama inavyofahamika hawaitakidi jambo hili bali hizo ni tuhuma zilizoambatanishwa kwao na maadui zao). Mimi nikasema: "Hebu tuachane na Mashia na uzushi wao, na ututosheleze kwa maelezo uliyonayo, ni vipi wewe umefahamu kwamba Mwenyezi Mungu alimchagua Abubakar"?


Akasema "Lau Mwenyezi Mungu angetaka kinyume cha hivyo basi, Waislamu na walimwengu wote wasingeweza kwenda kinyume cha vile atakavyo Mwenyezi Mungu". Basi hapo nilikumbuka kisa kingine nilipokuwa nikitembea katika shamba fulani pamoja na rafiki yangu, shamba ambalo lilikuwa na Mitende mingi nami nilikuwa nikimsimulia juu ya Qadhaa na Qadar, basi ghafla ilidondoka tende mbivu juu ya kichwa changu, nami nikaichukua toka kwenye majani ili niile na nikaiweka kinywani mwangu. Rafiki yangu alishangaa hali ya kuwa anasema: "Huwezi kula ila kile alichokuandikia Mwenyezi Mungu tende hii imedondoka kwa ajili yako". Mimi nikasema:"Maadamu wewe unaamini kwamba tende hiyo nimeandikiwa basi mimi sitaila" nikaitema. Akasema,"Subhanallah!! Ikiwa kitu hakikuandikwa kwa ajili yako, Mwenyezi Mungu atakitoa hata kama kimo tumboni mwako." Nikasema:"Kama ni hivyo basi nitaila" nikaiokota tena na kuimeza.

Hapo akasema:"Wallahi tende hiyo imeandikwa kwa ajili yako (akiwa na maana Mwenyezi Mungu amekuandikia) akawa amenishinda kwa njia hiyo kwani siwezi tena kuitoa tende hiyo tumboni mwangu. Naam, basi hiyo ndiyo itikadi ya Masunni kuhusu Qadhaa na Qadar au (ukipenda) sema hii ndiyo iliyokuwa itikadi yangu nilipokuwa sunni. Na kwa mujibu wa hali halisi ni kwamba (hali hii) inatufanya tuishi kutokana na itikadi hii tukiwa ni wenye kuchanganyikiwa kifikra baina ya mambo yanayopingana, na moja kwa moja tutabakia hivyo hivyo tunasubiri Mwenyezi Mungu atubadilishie mambo yetu, badala ya sisi wenyewe kubadili ili Mwenyezi Mungu atubadilishie, na tunakwepa majukumu ambayo tumeyabeba na tunamtupia majukumu hayo yeye Mwenyezi Mungu. Iwapo utamshutumu mzinifu au mwizi au hata muovu ambaye kamteka msichana asiyejiweza na akamuua baada ya kumaliza matamanio yake basi atakujibu kwa kusema "Mwenyezi Mungu ndiye mwenye nguvu, Mola wangu amenikadiria.


Nashangazwa, Mola huyu huyu anamuamuru mtu amzike binti yake akiwa hai kisha atamuuliza ni kwa kosa gani binti. huyu aliuawa? Umetakasika Ewe Mwenyezi Mungu, bila shako, huu ni uzushi mkubwa (uliozushwa). Ni jambo la kawaida wataalamu wa kimagharibi wanavyotudharau na kutucheka kutokana na akili yetu mbovu, bali wanatupachika majina na kutuita; "Waarabu walioandikiwa " na huifanya kuwa ndiyo sababu ya msingi ya ujinga wetu na kutokuendelea kwetu. Pa ni kawaida watu wenye kuchunguza wafahamu kwamba itikadi hii ilianza toka kwenye dola ya Banu Umayyah ambao walikuwa wakieneza uzushi kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyewapa ufalme na akawatawalisha juu ya watu, basi ni wajibu kwa watu kuwatii na kutokuwapinga, kwani yeyote mwenye kuwatii kamtii Mwenyezi Mungu, na mwenye kuwapinga basi kampinga Mwenyezi Mungu na ni lazima auawe.


Na kuhusu jambo hili tunao ushahidi mwingi kutoka katika historia ya Kiislamu: Huyu hapa Uthman bin Affan alipotakiwa ajiuzulu anapinga na kusema, "Siwezi kuivua kanzu aliyonivalisha Mwenyezi Mungu " Taz: Tarikh Tabari Hisar Uthman, pia Tarikh Ibn Athir. Basi kwa mtazamo wake (Uthman) Ukhalifa ni vazi la Mwenyezi Mungu kamvalisha, haipasi kwa yeyote miongoni mwa watu kumvua isipokuwa Mwenyezi Mungu, yaani kwa labda afe. Huyu hapa naye Muawiyyah pia anasema: "Kwa hakika mimi sikuwapigeni ili mfunge na mtoe zaka, bali nimewapigeni ili niwatawaleni, na bila shaka Mwenyezi Mungu amenipa hilo hali ya kuwa hamtaki". Taz: Maqatilut-Talibin uk. 70, Ibn Kathir Juz. 8 uk. 131 Ibn Abil-Hadid Juz. 3 uk. 16.


Na hata kumchagua mwanawe Yazid na kumtawalisha juu ya watu bila ridhaa yao, Muawiya alidai kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyempa Ukhalifa mwanawe Yazid juu ya watu, na hilo wamelisimulia wanahistoria pale Muawiyah alipoandika baia yake na kuisambaza sehemu mbali mbali, na Gavana wake huko Madina alikuwa Mar-wan bin Al-Hakam, akamuandikia kile ambacho Mwenyezi Mungu (kwa mujibu wa madai yake) amekipitisha kupitia ulimi wake kuhusu baia ya Yazid. Taz: Al-Imamah Was-Siyasah Juz. 1 uk. 151 Baiatu Muawiya Liyazid Bis-Sham. Hivyo hivyo ndivyo alifanya yule muovu ibn Ziyad, pale walipomuingiza Imam Ali Zainul-Abidin kwa huyo ibn Ziyad hali yakuwa (Imam Zainul Abidin) kafungwa kwa minyororo basi aliuliza akasema:"Ni nani huyu" wakasema, "Ni Ali bin Husain" Akasema, Je, Mwenyezi Mungu hajamuua Ali bin Husayn"? Bibi Zainab shangazi yake Imam Zainul-Abidin akamjibu, "Sivyo bali waliomuua ni maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake".

Ibn Ziyad akamwambia bibi Zainab: "Waonaje ni jinsi gani Mwenyezi Mungu alivyowafanya watu wa nyumba yako". Bibi Zaynab akasema:"Sikuona isipokuwa wema tu, hawa ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewafaradhishia kuuawa, walitoka hadi kwenye malazi yao, na Mwenyezi Mungu atakukutanisheni wewe na wao kisha muhojiane na kusutana, basi zingatia ni nani atakayeshindwa siku hiyo, mama yako akuhuzunikie ewe mwana wa Mar-Janah". Taz: Maqatilut-Talibin, Maq-Talul-Husayn. Basi hivi ndivyo ilivyoenea itikadi hii itokayo kwa Bani Ummayyah na wasaidizi wao na wakaisambaza ndani ya umma wa Kiislamu isipokuwa Mashia (Wafuasi) wa watu wa Nyumba ya Mtume (s.a.w.).

ITIKADI YA MASHIA KUHUSU QADHAA NA QADAR Tangu nilipowafahamu wanachuoni wa Kishia- k.m. Shahid Muhmmad Baaqir As-sadri aliyenitosheleza mambo mengi kuhusu maudhui hii (Mwenyezi Mungu amrehemu) pia Sayid Al-khui na Al-allaamah Muhammad Ali Tabatabai na Sayid Hakiim na wengineo na kusoma vitabu vyao niligundua elimu mpya inayohusu Qadhaa na Qadar. Na bila shaka Imam Ali alikwisha kuifafanua kwa ubainifu mkubwa mno unaoenea pale alipomwambia mtu aliyemuuliza juu ya Qadhaa na Qadar. "Ole wako huenda wewe umedhania Qadhaa ya lazima na Qadar iliyokwishapitishwa, basi lau ingekuwa hivyo, thawabu na adhabu vingebatilika na ahadi na maonyo vingeporomoka. Bila shaka Mwenyezi Mungu amewaamuru waja wake kwa kuwahiyarisha na akawakataza kwa kuwatahadharisha, na akakalifisha mambo mepesi wala hakukalifisha mambo mazito, na hakuasiwa eti kwa kuwa ameshindwa na wala hakutiiwa hali ya kukarahisha, na hakuwatuma Manabii kwa ajili ya mchezo na wala hakuwateremshia waja vitabu kwa ajili ya upuuzi, na wala hakuumba mbingu na ardhi bure bure, hiyo ni dhanna ya wale waliokufuru, basi ole wao wale waliokufuru (wataadhibiwa adhabu ya) moto".


Taz: Sharh Nahjul-Balaghah ya Sheikh Mohammad Abdooh Juz. 4 uk. 673. Basi ubainifu ulioje, sijapata kusoma maneno yenye ufafanuzi wa kina na hoja inayojulisha ukweli kuliko maneno hayo (ya Ali), basi Muislamu hutosheka (na akafahamu) kwamba matendo yake yanatokana na kutaka kwake halisi na uamuzi wake, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamuru lakini akatuachia uhuru wa kuamua nayo ndiyo ile kauli ya Imam Ali aliposema, "Bila shaka Mwenyezi Mungu amewaamrisha waja wake kwa kuwahiyarisha ". Kama ambavyo Mwenyezi Mungu ametukataza na akatutahadharisha kutokana na adhabu iwapo tutamkhalifu, basi maneno yake yakajulisha ya kwamba mtu anao uhuru wa kutenda na anao uwezo wa kwenda kinyume na amri za Mwenyezi Mungu, na katika hali hii inamuwajibikia adhabu na hiyo ndiyo ile kauli ya Imam Ali (a.s.) aliposema, "Na akawakataza kwa kuwatahadharisha ". Zaidi ya hapo Imam Ali (a.s.) aliongeza kuyafafanua mas-ala haya akasema kwamba, "Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuasiwa eti kwa kuwa amezidiwa". Na maana ya hayo ni kwamba lau Mwenyezi Mungu angetaka kuwashinikiza waja wake na kuwalazimisha kufanya kitu, basi wote wasingekuwa na uwezo wa kumshinda kuhusu amri yake. Hapo (Imam Ali) amejulisha ya kuwa Mwenyezi Mungu amewaachia (waja wake) uhuru wa kuamua kutii au kuasi, na (kauli hii) inathibitisha kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema, "Wambie huu ni ukweli utokao kwa Mola wenu, atakaye na aamini na atakaye akufuru." (Qur'an, 18:29)


Kisha baada ya hayo Imam Ali (a.s.) anaielekeza dhamira ya mtu ili iweze kufikia undani wa hali yake halisi, analeta dalili madhubuti na isemayo,"Lau mtu angekuwa ni mwenye kulazimishwa juu ya matendo yake kama wanavyoitakidi baadhi ya watu, basi kutumwa kwa Mitume na kuteremshwa vitabu ni aina ya mchezo na upuuzi, jambo ambalo Mwenyezi Mungu ametakasika nalo, kwani nafasi ya Manabii wote na kuteremshwa vitabu vyote ni kwa ajili ya kuwarekebisha watu na kuwatoa kwenye kiza, kuwapeleka kwenye nuru na kuwapa tiba yenye manufaa juu ya maradhi yao ya kinafsi na kuwabainishia njia bora ya maisha mazuri, Mwenyezi Mungu anasema, "Bila shaka hii Qur'an inaongoza katika njia iliyonyooka mno." (Qur'an, 17:9).

Imam Ali (a.s.) anakamilisha kwa kubainisha kwamba, itikadi ya watu kuwa ni wenye kulazimishwa katika matendo yao ni itikadi inayomaanisha kuwa, "Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo bure bure tu." Hii ni kufru na Mwenyezi Mungu amewaonya wasemao hivyo kwa adhabu ya moto. Na tunapoichambua kauli ya Mashia kuhusu Qadhaa na Qadar tunaikuta kuwa ni kauli ya sawa na ni rai muafaka. (Ni vema ifahamike kwamba), wakati kikundi fulani kilipochupa mpaka na kikaitakidi itikadi ya "Jabri" (kutenzwa nguvu) kmgine nacho kikachupa mpaka kikaamini kuwa kuna "Taf-widh"(uhuru usiyo na mipaka). Hapo watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) wakaja kusahihisha Maf-hum (ufahamu) wa itikadi na kuwakosoa jamaa hawa na wale wao wakasema: "Hapana Jabri (kutenzwa nguvu) wala Taf-widh (uhuru usiyo na mipaka) lakini liko jambo baina ya mawili hayo". Taz: Itikadi za Mashia Juu ya Qadhaa na Qadar.


Naye Imam Jaafar As-Sadiq amepiga mfano ulio wazi juu ya jambo hilo, mfano ambao watu wote wanaweza kuufahamu kwa kadiri ya akili zao, nao ni pale alipomwambia muulizaji aliyeuliza: "Ni nini maana ya kauli yako kwamba hapana Jabr wala Taf-widh lakini liko jambo baina ya mawili hayo"? Imam Jaafar alimjibu muulizaji huyo (akasema) "Kutembea kwako juu ya ardhi siyo sawa na kuanguka kwako juu ya ardhi hiyo". Na maana ya maneno hayo ni kuwa, sisi tunatembea juu ya ardhi kwa hiyari yetu, lakin pindi tunapoanguka ardhini hilo siyo kwa hiyari yetu, kwani ni nani basi miongoni mwetu apendaye kuanguka jambo ambalo huenda likasababisha kuvunjika kwa baadhi ya viungo katika miili yetu na hatimaye kuwa vilema?


Hapo ndipo Qadha na Qadar inapokuwa ni jambo moja baina ya mambo mawili, yaani sehemu fulani inatokana nasi na kwa utashi wetu nasi ndiyo tuitendayo kwa kutaka kwetu kikamilifu, na sehemu ya pili iko nje ya matakwa yetu nasi ni wenye kuikubali tu (kuitii) na wala hatuwezi kuizuwia, basi tutaulizwa kwa ile sehemu ya kwanza na hatutaulizwa kwa hii sehemu ya pili. Hivyo basi katika hali hii na ile mja ni mwenye kuhiyarishwa na ni mwenye kuendeshwa kwa wakati huo huo. A. Ni mwenye kuhiyarishwa katika matendo yake ambayo yanatokana naye baada ya kufikiri na kutambua, kwani hapo huwa anapita katika nyanja za hiyari na upinzani baina ya kutenda au kujizuwia kutenda, na mwishoni mwake mambo huwa ni imma atende au asitende, na hiki ndicho alichokiashiria Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema: "Na (ninaapa) kwa roho na aliyeitengeneza, kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake, bila shaka amefaulu aliyeitakasa nafsi yake". (Qur'an, 91:7-9).


Kuitakasa nafsi na kuichafua ni matokeo ya hiyari ya dhamira ipatikanayo kwa kila mtu, kama yalivyo mafanikio na kutofanikiwa vitu ambavyo moja kwa moja ni matokeo yanayokwenda sambamba na utashi. B. Mtu ni mwenye kuendeshwa katika kila yale ambayo yamzungukayo miongoni mwa siri za ulimwengu na nyendo zake zote ambazo zinatii atakavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila sehemu zake (hizo siri za ulimwengu) na maumbile yake, sayari zake na nguvu zake. Basi hapo mtu hana hiyari kuchagua jinsi yake kuwa mwanamume au mwanamke wala (hawezi) kuchagua rangi yake ukiachilia mbali kuchagua wazazi wawili ili tu awe katika malezi ya wazazi wawili matajiri badala ya kuwa na wazazi masikini, wala hawezi kuchagua hata urefu wa kimo chake na umbo la mwili wake.


Hivyo mtu ni mwenye kuyatii mambo mengi yenye kutenza nguvu (kama vile maradhi ya kurithi) na kanuni za kimaumbile zinazofanya kazi kwa faida yake bila ya yeye kulazimika, kwani yeye anapochoka hulala na huamka baada ya kupumzika, anakula anapohisi njaa, anakunywa anapohisi kiu, na hucheka na kuchangamka pale anapofurahi, hulia na kunyongea pale anapohuzunika hali ya kuwa ndani yake (mwanadamu) muna vitendea kazi na viwanda vya kutengeneza Hormone, chembechembe za uhai na maji yenye uwezo wa kubadilika. Vyote hivi kwa wakati huo huo huwa vinauweka mwili wake kwenye uwiano wa kufanya kazi kwa njia ya ajabu kabisa, hali ya kuwa yanapotendeka yote haya hana habari wala hafahamu kwamba uangalizi wa kiungu umemzunguka wakati wote katika nyakati za uhai wake bali hata baada ya kufa kwake.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kuhusu maana hii (iliyoelezwa hapo kabla): "Je, hivi mtu anadhani kuwa ataachwa hivi hivi tu, je, hivi yeye hakuwa ni tone la manii lililotonwa? Kisha akawa pande la damu, hatimaye (Mwenyezi Mungu) akamuumba na akamsawazisha (akawa mwanadamu kamili) kisha akamfanya namna mbili (akawepo) mwanaume na mwanamke, basi je, (aliyefanya hayo) hakuwa ni muweza wa kuhuisha na kufisha?" (Qur'an, 75:36-40) Hapana shaka Mwenyezi Mungu ni muweza, umetakasika na umetukuka Ewe Mola wetu wewe ndiwe uliyeumba na kusawazisha, nawe ndiwe ambaye umekadiria (kila kitu) na umekiongoza, nawe ndiwe ambaye umefisha kisha ukahuisha, utakatifu ni wako na utukufu ni wako, hakika ameangamia na amepotea yeyote mwenye kukupinga na kujitenga nawe na hakukutukuza vilivyo. Basi hebu tukamilishe uchambuzi huu kwa maneno aliyoyasema Imam Ali bin Musa Ar-Ridhaa ambaye ni Imam wa nane miongoni mwa Maimam wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) naye kwa hakika alikuwa mashuhuri kwa elimu katika zama za Maamuni (Khalifa wa Banu Abbas) na kabla hata hajafikia umri wa miaka kumi na minne alikuwa kesha kuwa ndiye mtu mjuzi mno wa watu wa zama zake.


Taz: Al-iqdul-Farid cha ibn Abdi Rabih Juz. 3, uk. 42. Kuna mtu alimuuliza Imam Ridhaa kuhusu maana ya maneno ya babu yake Al-Imam Jaafar As-Sadiq aliposema kuwa: "Hapana Jabr wala Taf-widh, bali kuna jambo baina ya mambo mawili" Basi Imam Ar-Ridhaa alimjibu mtu huyo (akasema): "Yeyote mwenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu anatenda matendo yetu kisha hutuadhibu juu ya matendo hayo, basi huyo atakuwa anazungumzia juu ya Jabr, na yeyote adhaniye kwamba Mwenyezi Mungu ameachia mambo ya viumbe na riziki kwa Maimamu wake, basi bila shaka huyo atakuwa amezungumzia Taf-widh, na asemaye kuhusu Jabr ni kafiri na asemaye kuhusu Taf-widh ni mshirikina."

Amma maana ya jambo baina ya mambo mawili ni kule kuwepo njia ya kuyatenda aliyoyaamuru Mwenyezi Mungu, na kuacha aliyoyakataza, yaani Mwenyezi Mungu amempa(mwanaadamu) uwezo wa kutenda maovu na kuyaacha kama ambavyo amempa uwezo wa kufanya mema na kuyaacha na akamuamuru kufanya hili la wema na kuacha la uovu." Naapa kuwa huu ndiyo ubainifu uliowazi unaotosheleza, ambao uko kwenye kiwango cha akili na unaofahamika kwa watu wote wenye taaluma na wasio na taaluma. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema kweli pale alipozungumza juu ya haki inayowastahiki Maimamu wa nyumba yake (Amani ya Mwenyezi Mungu iwashukie) akasema: "Musiwatangulie mtaangamia na wala musiwapuuze pia mtaangamia, wala musiwafundishe kwani bila shaka wao ni wajuzi mno kuliko ninyi." Taz: 1) Ibn Hajar katika Sawaiq Al-Muhriqah uk. 148
2) Maj-mauz-zawaid Juz. 9 uk. 163.
3) Yanabiul-Mawaddah uk. 41.
4) Ad-Durrul-Manthoor cha Suyuti Juz. 2 uk. 60.
5) Kanzul-UmmalJuz. 1 uk. 168.
6) Usudul-Ghabah Juz. 3 uk. 137.
7) Abaqatul-An-war Juz. 1 uk. 184.
10
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

UFAFANUZI JUU YA UKHALIFA UFAFANUZI JUU YA UKHALIFA NDANI YA QADHA'A NA QADAR Cha ajabu katika maudhui hii ni kwamba, Masunni pamoja na itikadi yao juu ya Qadhaa na Qadar na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye ndiye anayewaendesha waja wake katika matendo yao na kwamba wao hawana hiyari kwa lolote lile, lakini Masunni haohao kuhusu jambo la Ukhalifa wanasema kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikufa na akaliwacha jambo hilo kuwa ni la mashauriano baina ya watu ili wao wenyewe wafanye uchaguzi. Nao' Mashia wako kinyume kabisa (na Masunni), kwani pamoja na itikadi yao kwamba watu ni wenye kuhiyarishwa katika matendo yao na kwamba waja wa Mwenyezi Mungu wanafanya wayatakayo (kulingana na kauli isemayo kuwa hapana kutenza nguvu wala uhuru usio mpaka, lakini kuna jambo moja baina ya mawili hayo) isipokuwa wao (Mashia) kuhusu Ukhalifa wanasema kwamba (wanaadamu) hawana haki ya kumchagua Khalifa! Na hapa inadhihiri kama kwamba kuna kupingana katika pande mbili hizo za Kisunni na Kishia toka hapo mwanzo, lakini ukweli hauko namna hiyo.


Masunni wanaposema kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye ambaye anayewaendesha waja wake katika matendo yao wanapingana na ukweli halisi, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu (kwao wao) ndiye mwenye utashi wa utendaji, lakini yeye Mwenyezi Mungu anawaachia waja utashi wa kufikiria tu, kwani aliyemchagua Abubakr siku ile ya Saqifah ni Umar, kisha baadhi ya Masahaba lakini wao hao ni wenye kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu ambaye amewafanya wao wawe ni njia tu si vinginevyo, haya ni kwa mujibu wa madai yao.

Amma Mashia pindi wanaposema kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa hiari (utashi) waja wake katika matendo yao, siyo kwamba wanapingana na kauli yao, kwani suala la Ukhalifa liko katika utashi wa Mwenyezi Mungu peke yake,- Na Mola wako anaumba akitakacho na ndiye mwenye kuchagua, wao hawana hiyari (katika hilo), - hii ni kwa kuwa Ukhalifa ni kama Utume siyo katika matendo ya waja na wala halikuwakilishwa kwao. Basi kama ambavyo Mwenyezi Mungu anavyomchagua Mtume wake kutoka miongoni mwa watu na kumtuma kwao, basi ndivyo hivyo hivyo kumuhusu Khalifa wa Mtume, na watu wanaweza kutii amri ya Mwenyezi Mungu na wanaweza wakaiasi kama hali halisi ilivyotokea zama za uhai wa Mitume katika zama zote. Hapo waja wanakuwa huru kukubali utashi wa Mwenyezi Mungu, muumini mwema atakubali alichokichagua Mwenyezi Mungu, na mwenye kukufuru neema ya Mola wake atakipinga kilichochaguliwa na Mwenyezi Mungu na atakifanyia ufidhuli.

Mwenyezi Mungu amesema:
"Basi yeyote atakayefuata muongozo wangu hatapotea wala hataaibika, na atakayepuuza mawaidha yangu, basi bila shaka atakuwa na maisha ya dhiki na siku ya Kiyama tutamfufua hali yakuwa ni kipofu, aseme ewe Mola wangu mbona umenifufua kipofu na hali nilikuwa nikiona? Mwenyezi Mungu atasema hivyo ndivyo, zilikujia aya zetu ukazipuuza kadhalika leo unapuuzwa. (Qur'an 20:123-126). Kisha hebu itazame nadharia ya Masunni juu ya jambo hili huenda usimtwishe lawama mtu yeyote kwani kila kilichotokea na kinachotokea kwa sababu ya Ukhalifa na damu zote zilizomwagika na kuvunjwa heshima (za vitu vitakatifu) yote hayo yanatokana na Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba baadhi ya Masunni wanaodai kuwa na elimu waliambatisha (matukio hayo) na kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

"Lau Mola wako angetaka basi wasingeyafanya." (Qur'an, 6:112). Ama nadharia ya Mashia yenyewe inambebesha jukumu kila aliyesababisha upotofu na kila aliyeasi amri ya Mwenyezi Mungu, na kila mmoja kwa kadiri ya kosa lake na kosa la waliofuata uzushi wake mpaka siku ya kiyama: "Kila mmoja wenu ni mchunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu uchunga wake".

Mwenyezi Mungu amesema: "Wasimamisheni, bila shaka wao ni wenye kuulizwa" (Qur'an, 37:24).

KHUMS (1/5) Khums vile vile ni miongoni mwa maudhui ambazo Mashia na Masuni wamehitilafiana ndani yake. Na kabla ya kuhukumu dhidi yao au kuwapasisha, hapana budi tufanye uchambuzi kwa kifupi juu ya maudhui ya Khums. Basi na tuanze na Qur'an tukufu: Mwenyezi Mungu anasema: "Na jueni ya kwamba chochote mnachokipata, basi sehemu yake ya tano (Khums) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume na Qaraba wa Mtume na Mayatima na Masikini na Wasafiri". (Qur'an, 8:41)


Naye Mtume (s.a.w.) amesema: "Nakuamuruni mambo manne:"Kumuamini Mwenyezi Mungu, na kusali Sala, na kutoa zaka na kufunga Ramadhan na mtoe (Khums) sehemu ya tano ya kile mnachokipata kwa ajili ya Mwenyezi Mungu". Taz: Sahih Bukhar Juz. 4 uk. 44. Basi Mashia kwa kufaata amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) huwa wanatoa sehemu ya tano (Khums) ya kile walichokipata kwa muda wa mwaka, na wanafasiri maana ya "Ghanimah" kuwa ni kila anachokipata mtu katika faida kwa ujumla. Ama Masunni wao wameafikiana kuhusisha Khums kwenye ngawira za vita peke yake na wakaifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Na jueni kwamba chochote mlichokiteka (mlichokipata) wakakusudia kuwa "Mlicho kipata katika vita ". Huu ni ufupi tu wa kauli za pande mbili- kuhusu Khums, na bila shaka wanachuoni wa pande mbili hizi wameandika makala nyingi tu kuhusu mas-ala haya.

Nami binafsi sijuwi ni vipi nitaikinaisha nafsi yangu na au mtu mwingine juu ya maoni ya Masunni ambayo nadhani yametegemea kauli za watawala wa kibanu Umayyah wakiongozwa na Muawiyah bin Abi Sufiyan ambaye alijinyakulia kila aina ya mali za Waislamu na kuzifanya kuwa ni zake yeye na jamaa zake. Basi kwa Masunni siyo ajabu kubadilisha aya ya Khums na kuifanya ihusike na uwanja wa vita tu, kwani mfumo wa aya tukufu umekuja ndani ya aya zinazohusu vita na-mapigano, na Masunni wanazo aya nyingi walizozibadilisha kwa kutegemea aya zilizokuja kabla yake au baada yake. Wao wanabadilisha, kwa mfano aya ya kuondolewa uchafu na kutakaswa mno watu wa nyumba ya Mtume, kwamba aya hiyo inahusika kwa wakeze Mtume kwa kuwa kilicho kabla yake na kilicho baada yake kinazungumzia wakeze Mtume (s.a.w.). Kama ambavyo wanaibadilisha kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Na ambao wanalimbikiza dhahahbu na fedha na hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu wabashirie adhabu kali) kwamba aya hii ni makhsusi kwa Ahl-kitabi (watu wa Kitabu, Wayahudi na Wakristo).


Na kisa cha Abu Dhar Al-Ghifa'ri (r.a.) yeye pamoja na Muawiyah na Uthman bin A'ffan na (jinsi Uthman) alivyomfukuza Abu Dhar toka Madina na kumpeleka Rub-Dhah kwa ajili ya jambo hilo (la kulimbikza dhahabu na fedha), ni kisa mashuhuri, kwani Abu dhar aliwakosoa kulimbikiza kwao dhahabu na fedha na alikuwa akitolea hoja kwa aya hii, lakini Uthman alimtaka ushauri Kaab Al-Ahbar kuhusu aya hiyo, naye akamwambia kuwa aya hiyo ilishuka maalum kwa Ahlul-Kitab. Abu-Dharr alimshutumu na kumwambia huyo Kaab "Umeangamia ewe mwana wa Kiyahudi, Je, wewe unatufundisha dini yetu?" Kwa ajili hiyo Uthman alikasirika kisha alimfukuza Abu-Dhar toka Madina akampeleka Rub-Dhah baada ya makemeo makubwa ya Abu-Dhar dhidi ya Uthman, Abu-Dharr alikufa huko akiwa peke yake na binti yake, hakupata hata mtu wa kumkosha na kumkafini. Masunni wanayo fani maarufu ya kubadili aya za Qur'an na hadithi za Mtume na wanayo elimu mashuhuri (kuhusu hilo) nayo ni kule kufuata (kwao) yale waliyoyabadilisha Makhalifa wa mwanzo na Masahaba Mashuhiri kuhusu maandiko yaliyowazi katika Kitabu na Sunna.[91]


Na lau tungetaka kulieleza hilo kwa undani basi ingebidi kuandika kitabu maalum, inatosha kwa mchunguzi arejee kitabu kiitwacho An-Nasu Wal-Ij-Tihad ili apate kufahamu ni vipi wabadilishaji walivyozichezea hukmu za Mwenyezi Mungu Mtukufu.. Nami kama mtafiti siwezi kuzibadili aya za Qur'an na hadithi za Mtume vile nipendavyo au kama yanavyonikalifisha Madhehebu yangu ninayoyafuata. Lakini sina njia iwapo Masunni wenyewe ndiyo ambao wamethibitisha ndani ya vitabu vyao sahihi kuwa Khums ni faradhi (kutolewa) mahala pasipo na vita, kwa ajili hiyo wakaitengua taawili yao na madhehebu yao (wakayatengua). Imekuja ndani ya Sahihi Bukhari katika mlango wa (Rikazut-Khums), Na amesema Malik na ibn Idris kwamba "Rikaz ni mali iliyo katika zama za Jahiliya, ikiwa kidogo au nyingi itolewe Khums na madini siyo Rikaz, na Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema, Ndani ya madini hapana kitu na katika rikaz itolewe Khums.


Taz: Sahihi Bukhari Juz. 2 uk. 237 mlango wa Rikaz na Khums: Na imekuja ndani ya mlango wa vinavyotolewa baharini: Ibn Abbas (r.a.) amesema:"Nyangumi siyo katika rikaz, 'ni kitu ambacho bahari imekitoa", na amesema Hasan kuhusu Nyangumi na lulu, kuwa (hutolewa) Khums, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ameweka khums katika rikaz na si katika kitu ambacho hupatikana ndani ya maji. Taz: Sahihi Bukhari Juz: 2 uk. 136, "Babu Maa-yustakhraju minal-bahr. Na mchunguzi yeyote atafahamu kwa kupitia hadithi hizi kwamba machumo ya Ghanimah ambayo Mwenyezi Mungu amewajibisha khumsi ndani yake hayahusiki na mali ya uwanja wa vita pekee yake kwani rikaz ambayo ni hazina inayochimbuliwa ardhini ni miliki ya aliyeichimbua, lakini ni wajibu kutoa khums katika hazina hiyo kwa kuwa ni kipato.


Kama ambavyo mwenye kumvua nyangumi na lulu kutoka baharini inawajibikia kutoa khums kwani ni kipato. Na kutokana na hadithi alizozithibitisha Bukhar ndani ya sahihi inatubainikia kwamba khums haihusu kipato cha vita peke yake. Basi maoni ya Mashia siku zote yanabakia kuwa ni uthibitisho wa ukweli ambao haupingani ndani yake wala hauhitilafiani, na hiyo ni kwa kuwa wao katika hukmu zao na itikadi zao huwarejea Maimamu waongofu ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na amewatakasa mno, nao ndiyo wenza wa Qur'an, hapotei mwenye kushikamana nao na hupata amani mwenye kuwategemea. Hiyo ni kwa sababu hatuwezi kutegemea vita ili kuisimamisha dola ya Kiislamu na jambo hilo linakwenda kinyume na moyo safi wa Uislamu na wito wake wa amani, kwani Uislamu siyo dola ya kikoloni inayosimama (kuimarika) kwa kuyakalia mataifa na kuyapora uchumi wake jambo ambalo tawala za kimagharibi zinajaribu kutuhusisha nalo pale wanapomzungumzia Mtume wa Uislamu kwa kila aina ya dharau na wanasema kwamba, yeye Mtume alieneza Uislamu kwa nguvu na shinikizo la upanga ili kuyakalia mataifa mengine.


Na ilivyokuwa mali ni nguzo ya maisha na hasa ikiwa nadharia ya uchumi wa Kiislamu iriasisitiza juu ya kuanzisha kile ambacho leo hii kinaitwa kuwa ni Bima ya kijamii ili kuwadhamini maisha yao wale wenye dhiki na wasiojiweza kwa heshima, basi haiwezekani kwa dola ya Kiislamu kutegemea kile wanachokitoa Masunni katika zaka, kiasi ambacho katika hali nzuri kinalingana na asilimia mbili na nusu na hicho ni kiwango kidogo mno hakiwezi kusimamia mahitaji ya dola katika kuandaa nguvu na kujenga mashule, hospitali na kurahisisha mawasiliano, licha ya kumdhamini mtu mmoja mmoja kwa kipato cha kutosheleza mahitaji yake na kuyadhamini maisha yake, kama ambavyo haiwezekani kwa dola ya Kiislamu kutegemea vita zinazomwaga damu na muaji ya watu ili tu idhamini kuwepo kwake na kuendeleza taasisi zake kwa hesabu za waliouawa ambao hawakuutaka Uislamu.


Kwa hiyo Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) wao walikuwa ni watambuzi mno wa makusudio ya Qur'an, basi ni kwa nini isiwe hivyo wakati wao ndiyo wafafanuzi wa hiyo Qur'an, na walikuwa wakiiwekea mipango dola ya Kiislamu kuhusu mafundisho ya uchumi na jamii lau kama wangekuwa wanakubalika. Lakini kwa masikitiko makubwa ni kuwa utawala na uongozi ulikuwa mikononi mwa watu wengine, watu ambao waliupora Ukhalifa kwa nguvu na shinikizo, kwa kuwauwa watu wema miongoni mwa Masahaba na kuwateka kama alivyofanya Muawiyah, na walizibadilisha hukmu za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa na kidunia, basi wao wenyewe wakapotea na kuwapoteza wengine na kuuacha umma huu ukiwa chini ya unyonge ambao haukuweza kujikwamua mpaka leo hii. Hivyo basi mafunzo ya Maimamu wa Ahlul-Bayt yamebakia kuwa ni fikra na nadharia inayoaminiwa na Mashia, nao hawakupata hata hiyo nafasi ya kuziambatanisha kimatendo, kwani Mashia hao walikuwa wakifukuzwa mashariki na magharibi ya ulimwengu (kutokana na kuadhibiwa), si hivyo tu bali watawala hao wa Kibanu Umayah na Bani Abbas waliwafuatilia Mashia katika zama zote.


Wakati dola mbili hizo zilipovunjika na Mashia wakaanzisha jamii (yao), hapo ndipo walipoutenda utekelezaji wa Khums ambayo walikuwa wakiitoa kwa Maimam (a.s.) kwa siri, na leo hii wanaitoa (hiyo Khums) kwa Mar-jaa wanayemqalid (kufuata Fat-wa zake) kwa niyaba ya Imam Mahdi (a.s.). Hawa Mar-jaa huisimamia hiyo khums kwa kuigawa katika sehemu zinazohusika kisheria, miongoni mwake ikiwa ni taasisi na vyuo vya elimu na sehemu zingine na kheri na maktaba za Jumuiya, na majumba ya mayatima na mahala pengine katika sehemu za mambo matukufu kama vile kulipa posho ya mwezi kwa wanafunzi wa elimu ya dini na maarifa mengine na pia mambo mengine (ya kheri) yasiyokuwa hayo.

Na inatutosha kutokana na maelezo haya kupata natija kuwa wanachuoni wa Kishia hawaitegemei serikali, kwani khums inatosheleza mahitaji yao na wao husimamia kumpa haki kila mwenye haki yake. Ama wanachuoni wa Kisunni wao wanategemea watawala na maofisa wa serikali katika nchi, na hapo ndipo mtawala anapopata nafasi ya kumkurubisha amtakaye miongoni mwao na au kumtenga (amtakaye) kufuatana na ushirikiano wao hao wanachuoni wa Kisunni na ofisa huyo ikiwemo kutoa kwa Fat-wa kwa maslahi yake. Kutokana na hali hiyo mwanachuoni (wa Kisunni) anakuwa yu karibu mno na mtawala kiasi cha kuwa mwanachuoni tu (haangalii maslahi ya dini) na hizo ndizo baadhi ya athari zenye madhara ambayo yameifanya faradhi ya khums isitumike kwa ile maana yake ambayo watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) walivyo ifahamu.


TAQ-LIID Mashia wanasema: "Ama Furuud-Din ambazo ni hukmu za kisheria zinazohusika na matendo ya kiibada, kama vile Sala, Saumu, Zaka na Hijja, ni wajibu katika hukmu za mambo hayo lipatikane moja kati ya mambo matatu:
1) Mtu ajitahidi na achunguze dalili za hukmu kama anao ustahiki wa kufanya hivyo (uwezo wa elimu).
2) Au awe ni mwenye Ih-Tiyat katika matendo yake ikiwa anaweza kufanya Ih-Tiyat.
3) Au amfuate, Muj-Tahid ambaye amezimiliki sharti (za Ij-Tihad) na awe hai huyo anayemfuata, mwenye akili, muadilifu, mwenye elimu, mwenye kuihifadhi nafsi yake, mwenye kuheshimu dini yake, mwenye kuyapinga matamanio yake na mwenye kutii amriza Mola wake.
Na hii Ij-Tihad katika hukmu za furui ni wajibu wa kutosheleza (Wajibul-Kifayah) kwa Wasialmu wote, basi atapojitokeza mtu ambaye zimetimia kwake sharti, wajibu huo huondoka kwao Waislamu wengine, na hufaa kwao kumfuata huyo na kumrejea katika Furui za dini yao, kwani daraja ya Ij-tihad siyo katika mambo mepesi wala haipatikani kwa kila mtu bali inahitaji muda mwingi na elimu kubwa, maarifa na uchunguzi, na haya hayatengeneki isipokuwa kwa mtu mwenye bidii na juhudi na akautumia umri wake katika utafiti na kujifunza na hawapati Ij-tihad isipokuwa wale wenye hadhi tukufu.


Mtume (s.a.w.) amesema: "Yeyote ambaye Mwenyezi Mungu amemtakia kheri, humtaalamisha katika dini". Na kauli hii ya Mashia haitofautiani na kauli ya Masunni., isipokuwa katika sharti la kuwa hai yule Muj-Tahid. Tofauti iliyo bayana baina ya Mashia na Masunni ni katika kuitenda hiyo Taqlid, wakati ambapo Mashia wanaitakidi kuwa Muj-Tahid ambaye ametimiza sharti zilizotajwa ni naibu wa Imam (a.s.) katika hali ya kuwa kwake katika ghaibah (haonekani), basi Muj-Tahid ndiye mtawala na kiongozi kwa kila kitu, anayo haki aliyo nayo Imam katika kuamua mambo na kuhukumu baina ya watu. Hivyo basi Muj-Tahid aliyetimiza sharti kwa Mashia siyo mwenye kurejewa tu katika Fat-wa, bali anao utawala wote juu ya wafuasi wake, watamrejea katika hukmu na maamuzi baina yao katika yale waliyotofautiana miongoni mwa maamuzi, na watampa zaka na khums ya mali zao, azitumie kama inavyomuwajibishia sheria kwa niyaba ya Imam wa zama (a.s.) Ama kwa Masunni, Muj-Tahid hana daraja hii, lakini wao humrejea katika mas-ala ya Kifiqh mmoja wa Maimamu wa Madhehebu manne, ambao ni Abu Hanifa , Malik, Shafii na Ah-mad bin Hanbal, na hawa Masunni wa leo huenda wakakosa kulazimika kumfuata Imam mmoja maalum miongoni mwa hawa, kwani hupata wakachukua baadhi ya mas-ala toka kwa mmoja wao, na mas-ala mengine wakachukua kwa mwingine kufuatana na yanavyopelekea mahitaji yao, kama alivyofanya Sayyid Sabiq ambaye ametunga Fiqh iliyochukukuliwa toka kwa Maimamu hao wanne.


Hiyo ni kwa kuwa Masunni wanaitakidi kwamba kuna rehma ndani ya kuhitilafiana (wao kwa wao), kwa mfaho anayefuata Madhehebu ya Malik anaweza kufuata maoni ya Abu Hanifa pindi atakapokuta ufumbuzi wa tatizo lake ambalo huenda asiukute ufumbuzi wake kwa Malik. Nitapiga mfano juu ya jambo hilo ili imbainikie msomaji apate kufahamu makusudio hayo: Katika kikao cha Mahakama moja huko kwetu Tunisia kulikuwa na msichana aliyempenda mtu fulani na akataka aolewe na mtu huyo, lakini baba ya msichana huyo alikataa kumuoza binti huyo kwa kijana huyo kwa sababu ambazo Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye, basi yule binti akatoroka nyumbani kwa baba yake na akaolewa na kijana yule bila idhini ya baba yake, hapo ndipo baba yake alipopeleka mashitaka mahakamani dhidi ya ndoa hii.

Binti yule na mumewe walipofika mbele ya Qadhi na hakimu akamuuliza yule binti sababu ya kutoroka nyumbani na kuolewa bila idhini ya walii wake alisema: "Ewe Bwana wangu, umri wangu ni miaka ishirini na tano na nilipenda kuolewa na mume huyu kwa mujibu wa muongozo wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kwa kuwa baba yangu anataka kunioza mtu nisiyemtaka, basi nimejiozesha kwa mujibu wa maoni ya Abu Hanifah ambayo yananipa haki ya kuolewa na mtu nimtakaye kwani mimi tayari nimekwisha vunja ungo.


Basi yule Qadhi (Mwenyezi Mungu amrehemu ambaye yeye binafsi alinisimulia kisa hiki) anasema: "Basi tukayafuatilia mas-ala haya na tukamkuta yule msichana anayo haki, nami ninaamini kuwa kuna mwanachuoni fulani ambaye ni mtafiti ndiye aliyemuelekeza ni jambo gani atalolisema msichana huyo". Qadhi huyo anasema:"Nikayatupilia mbali madai ya yule baba na nikaipitisha ndoa ile, na yule baba alitoka hali ya kuwa amekasirika akipiga viganja vya mikono yake huku anasema: "Hanafatil-Kalbah" Yaani binti yake ameacha Madhehebu ya Malik na kumfuata Abu Hanifah, na hili neno "Al-Kalbah" ni la kumtweza binti yake ambaye hatimaye baba huyu alitamka kuwa amejitenga na binti yake (hayuko pamoja naye). Mas-ala yaliyopo hapa ni tofauti ya Ij-tihadi ya Madhehebu, wakati ambapo Malik anaona kuwa binti aliyebikra hafai kuolewa isipokuwa kwa idhini ya walii na hata kama atakuwa mkubwa, basi walii wake atakuwa mshiriki katika ndoa yake kumuozesha, hawezi kujiozesha na ni lazima huyo walii amkubalie. Abu Hanifah yeye anaona kwamba, Mwanamke bikra aliyevunja ungo, au akawa ni mkubwa anao uhuru wa kuchagua mume na kujiozesha mwenyewe.


Basi mas-ala haya ya kifiqh yaliwatenganisha baba na binti yake mpaka baba akamsusa binti, na ni mara nyingi wazazi wamekuwa wakiwasusa mabinti zao kwa sababu mbali mbali, miongoni mwake ikiwa ni kutoroka nyumbani na mwanaume fulani anayempenda amuowe, na kususa huku kuna matokeo mabaya, kwani ni mara nyingi (kwa kumsusa binti) humpelekea kumzulia binti kupata mirathi yake, na hatimaye binti anabakia kuwa ni adui wa nduguze ambao nao humsusa dada yao ambaye amewaaibisha. Kwa hiyo mambo hayako kama wasemavyo Masunni kuwa, ndani ya kutofautiana kwao kuna rehma au kwa uchache ni kuwa hakuna rehema katika kila Mas-ala yenye Ikhtilafu. Baada ya maelezo haya inabakia tofauti nyingine baina ya Masunni na Mashia, ambayo ni suala la kumfuata (katika Fat-wa) mtu aliyekwisha kufa.


Masunni wao wanawafuata Maimamu waliokwisha kufa tangu karne nyingi zilizopita, na kuwa mlango wa Ij-tihad umefungwa kwa hao tu tangu zama hizo, na wote waliokuja baada yao miongoni mwa wanachuoni wamefungika katika kufanya sherehe na tunzi za mashairi ya Fiqhi ndani ya Madhehebu manne. Na kwa hakika ziko sauti na makelele ya baadhi ya wanachuoni wa zama hizi kutaka mlango huo ufunguliwe na kuirejea Ij-tihad, kutokana na maslahi ya zama yanavyolazimisha na kutokana na upya wa mambo ambayo yalikuwa hayajulikani zama za Maimamu hao wanne.

Ama Mashia hawaruhusu kumfuata mtu aliyekwisha kufa, na wao humrejea katika kila hukmu zao Muj-Tahid aliyehai ambaye ametimiza masharti tuliyoyataja hapo kabla, na hali hii ni tangu baada ya Ghaibah ya Imam aliye Maasum ambaye aliwalazimisha kuwarejea wanachuoni waadilifu katika zama za kuwa kwake katika Ghaibah mpaka atakapodhihiri. Sunni wa madhehebu ya Malik kwa mfano anaweza kusema jambo hili ni halali na hili ni haramu kwa mujibu wa Imam Maliki, hali ya kuwa Malik amekwisha kufa zaidi ya karne kumi na mbili zilizopita, hivyo hivyo msunni wa Hanafi na Shafii na Hambal, kwani wote hawa waliishi katika kipindi kimoja na baadhi yao wakasoma kwa wenzao. Kama ambavyo Masunni hawaamini juu ya Ismah ya Maimamu hawa ambao wao binafsi hawakudai kuwa na Ismah (kuhifadhika na dhambi) bali walikubali kukosea na wakati mwingine kutokosa, na wanasema kwamba wao wanalipwa katika kila Ij-tihad zao ajira mbili iwapo watapatia, na watalipwa ujira mmoja iwapo watakosea. Na Shia Imamiyyah kwa mfano, wanazo Mar-hala mbili katika Taqlid.

Mar-hala ya Kwanza: Ni zile zama za Maimamu kumi na wawili, na zama hizo ziliendelea kwa muda wa kiasi cha karne tatu na nusu, na ndani ya zama hizo Shia alikuwa akimfuata Imam aliye Maasum (aliyehifadhiwa kutokana na makosa) ambaye hasemi jambo kwa maoni yake na jitihada yake, bali kwa elimu na riwaya alizozirithi toka kwa Babu yake ambaye ndiye mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.). Imam huyo husema kuhusu mas-ala (aliyoulizwa)." Baba yangu kapokea toka kwa Babu yangu ( na Babu yangu kapokea) toka kwa Jibril (na Jibril kapokea) toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu."

Mar-hala ya Pili: Ni zama za Ghaibah (ya Imam a.s.) zama ambazo zimeendelea mpaka leo, basi Shia husema kwa mfano: hili ni halali na hili ni haramu kwa maoni ya Sayyid Al-Khui au Sayyid Khumain na kila mmoja wao akiwa hai (sasa hivi wote wamefariki) na maoni yao Maimamu hawa hayavuki Ij-tihad katika kutoa hukmu ndani ya Qur'an na Sunna kwa mujibu wa riwaya za Maimamu wa nyumba ya Mtume kwanza, kisha Masahaba waadilifu. Nao wakati wanapozitafiti riwaya za Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) huziweka kwenye daraja la mwanzo, kwani Maimamu hawa wanapinga kutumia maoni binafsi ndani ya sheria na wanasema: "Hapana jambo lolote isipokuwa Mwenyezi Mungu anayohukmu yake, na iwapo hatukuiona hukmu fulani hiyo haimaanishi kwamba Mwenyezi Mungu amelipuuza hukmu hiyo, lakini kutokujuwa kwetu na kushindwa kwetu ndiyo mambo ambayo hayakutufikisha kwenye kuifahamu hukmu hiyo. Hivyo kutokukifahamu kitu siyo dalili ya kutokuwepo kwake Na dalili ya hilo ni kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Na hapana chochote tulichokiacha Kitabuni humu" (Qur'an, 6:38)


ITIKADIAMBAZO MASUNNI HUWAKEBEHI MASHIA Miongoni mwa itikadi ambazo Masunni huwakebehi Mashia, jambo ambalo ni wazi kabisa kuwa hivyo ni vitimbi na matatizo yaliyoanzishwa na Banu Umayyah na Banu Abbas mwanzoni mwa Uislamu kutokana na chuki yao dhidi ya Imam Ali (a.s.) ambaye walimkera mpaka wakawa wanamlaani juu ya mimbari kwa miaka arobaini. Kwa ajili hiyo siyo ajabu kwao kumshutumu kila aliyemfuata Ali (a.s.) na kumtupia kila aina ya fedheha na aibu mpaka mambo yakafikia kwa Banu Umayyah na Banu Abbas aambiwe mmoja wao kuwa: "Uyahudi ni bora mno kwake kuliko kuambiwa kuwa yeye ni Shia ".


Na wafuasi wao waliliendeleza hilo kila wakati na kila mahala, na Shia akawa ni mwenye kutukanwa kwa Masunni kwa kuwa anawapinga katika itikadi zao na ametoka katika jamii yao, basi wao Masunni humuaibisha wapendavyo na kumtupia kila aina ya tuhuma na kumpachika majina mbali mbali, na kumkhalifu katika kila kauli zake na matendo yake. Je, huoni kwamba baadhi ya wanachuoni mashuhuri wa Kisunni wanasema kwamba, "Kuvaa pete mkono wa kulia ni sunna ya Mtume lakini ni wajibu kuiacha sunna hiyo kwa kuwa Mashia wamelifanya jambo hilo kuwa ni alama yao". Taz: Musanniful-Hidayyah. Kama alivyothibitisha Az-Zamakh-Shari ndani ya kitabu chake Rabiul-Abrar ya kwamba: "Mtu wa kwanza aliyevaa pete mkono wa kushoto kinyume cha Sunna ya Mtume ni Muawiyah bin Abi Sufiyan. Naye Hujjatul-Islam Abu Hamid Al-Ghazali anasema: "Bila shaka kusawazisha makaburi ndivyo ilivyosheria katika dini, lakini Marafidh (Mashia) walipolifanya jambo hilo kuwa ni kitambulisho chao tumewacha kusawazisha makaburi na tukawa tunayainulia mgongo."


Na huyu Ibn Taimiyyah anayesifiwa kuwa ni mwenye kuleta usuluhishi na wengine wanasema kuwa yeye muhuyishaji na muimarishaji (wa Sunna) anasema:"Na kutokana na hayo wameamua miongoni mwa wanazuoni kuacha baadhi ya sunna zitakapoonekana kuwa ni kitambulisho chao (Mashia), japokuwa kuacha siyo jambo la wajibu, lakini kulidhihirisha tendo hilo (la sunna) ni kujifananisha nao, na hapo anakuwa hatambulikani Sunni kutokana na Shia, na faida ya kujibagua kutokana nao kwa ajili ya kuwatenga na kwenda kinyume nao ni kubwa kuliko faida ya Sunna hii". Taz: Min-Hajus-Sunnah Juz. 2 uk. 143.


Na Al-Hafidh Al-Ira'qi alipokuwa akijadili juu ya kuteremsha kiremba amesema:"Sikuona kinachojulisha juu ya kuhusisha upande wa kulia isipokuwa ndani ya hadithi dhaifu kutoka kwa Tabrani na hata kwa kukadiria kuhusisha kwake huenda alikuwa akikiteremshia upande wa kulia na kisha hukirejesha upande wa kushoto kama wafanyavyo baadhi yao, isipokuwa jambo hilo limekuwa ni kitambulisho cha Mashia basi inapasa kuliepuka ili kuacha kujifananisha nao. Taz: Shar-Hul-Mawahibi cha Az-Zir-Qani Juz. 5 uk. 13. Sub-hanallah Walahaula wala Quwwata Ilia Billah!! Angalia Ewe ndugu yangu msomaji chuki hii yenye upotofu, ni vipi wanachuoni hawa wanaruhusu kwenda kinyume na Sunna ya Mtume (s.a.w.) kwa sababu tu Mashia wameshikamana na Sunna hizo mbili mpaka zikawa ni kitambulisho chao, kisha wanachuoni hao hawaoni vibaya kukiri wazi wazi juu ya jambo hilo, nami nasema: "Namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ameidhihirisha haki kwa wenye macho, na kwa kila mwenye utakaso wa moyo anayetafuta ukweli.


Shukrani zinamstahikia Mwenyezi Mungu ambaye ametuonyesha kuwa Mashia ndiyo ambao wanaofuata sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) na hilo ni kwa ushuhuda wenu ninyi Masunni kama ambavyo mumeshuhudia wenyewe kwamba ninyi mumeiwacha sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kwa makusudi ili tu muwapinge Maimamu wa nyumba ya Mtume na wafuasi wao wenye utakaso wa moyo, na mumefuata sunna ya Muawiyah bin Abi Sufiyan kama alivyoshuhudia hilo Imam Zamakhshari pale alipothibitisha kwamba, mtu wa kwanza kuvaa pete mkono wa kushoto kinyume cha sunna ya Mtume ni Muawiya bin Abi Sufiyan. Taz: Kitabu Rabii ul-Abrar cha Zamakh-shari.


Pia mmefuata sunna ya Umar katika bid'a yake ya tarawehe kinyume na sunna ya Mtume ambayo Waislamu wameamriwa waswali sunna majumbani mwao mmoja mmoja na siyo jamaa, kama alivyothibitisha jambo hilo Bukhar. Taz: Sahih yake Juz. 7 uk. 99 (Babu Maa-yajuzu Minal-Ghasbi Wash-Shiddat Liamri llah). Na kama ambavyo Umar mwenyewe amekiri kwamba Tarawehe ni Bid'a aliyoizusha pamoja na kuwa yeye hakuiswali kwani hakuiamini. Taz: Sahih Bukhar Juz. 2 uk. 252. Kitab Sala'tit-Tarawih. Imekuja riwaya ndani ya Sahih Bukhar iliyopokewa toka kwa Abdur-Rahman bin Abdil-Qari kwamba yeye amesema:"Nilitoka mimi na Umar bin Al-Khatab (r.a.) katika usiku mmoja wa mwezi wa Ramadhan kwenda msikitini tukawakuta watu wametawanyika, kuna anayesali peke yake na mwingine anasali na kigurupu, Umar akasema, hakika mimi naona lau nitawakusanya hawa (wakaswali) nyuma ya msomaji mmoja litakuwa ni jambo jema, kisha aliazimia akawakusanya nyuma ya Ubayi bin Kaa'b, halafu nilitoka pamoja naye usiku mwingine (tukawakuta) watu wanasali kufuata sala ya msomaji wao, Umar akasema "Bid'a nzuri ni hii". Taz: Sahih Bukhar Juz. 2 uk. 252 Kitabut-Tarawih.


Jambo la kushangaza ni kuwa yeye Umar aliiona kuwa ni Bid'a nzuri baada ya Mtume kuikataza? Na aliikataza pale Masahaba walipopiga makelele na kuugonga mlango wake (Mtume) ili aje awasalishe sunna ya mwezi wa Ramadhan, Mtume akawatokea hali ya kuwa amekasirika akawaambia: "Mmeng'ang'ania tendo lenu (hili) mpaka nikadhania kwamba mtafaradhishiwa, basi salini (sunna) majumbani mwenu kwani sala iliyo bora kwa mtu ni ile asaliyo nyumbani kwake isipokuwa sala ya faradhi". Taz: Sahih Bukhar Juz. 5 uk. 99, (Babu Ma'Yajuzu Minal-Ghadhab Wash-Shiddat Liamrillah). Kama ambavyo ninyi (Masunni) mlivyoifuata sunna ya 'Uthman bin 'Affan ambayo ni kutimiza sala ya safari kinyume na sunna ya Mtume (s.a.w.) ambapo alisali kwa kupunguza.

Taz: Sahih Bukhari Juz. 2 uk. 35. Pia bibi Aisha alibadilisha na akasali rakaa nne. Taz: uk. 36 Sahih Bukhari Juz. 2 Na lau ningetaka kuyakusanya yote mambo ambayo ndani yake mmeikhalifu sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) basi jambo hilo lingelazimu kuandika kitabu maalum, lakini ushahidi wenu unatosha katika yale mliyoyakiri ninyi wenyewe na ushahidi wenu pia unatosha kwa kukiri kwenu kuwa Mashia ndiyo ambao wameifanya sunna ya Mtume kuwa ni kitambulisho chao. Hivi baada ya haya inabakia dalili yoyote kuhusu kauli ya watu wajinga ambao wanadai kuwa Mashia wamemfuata Ali bin Abi Talib na Masunni wao ndiyo wamemfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu? Je, watu hawa wanataka kuthibitisha kwamba Ali alikwenda kinyume cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) .... na akazusha dini mpya? Hakika ni maneno machafu kabisa yatokayo vinywani mwao, kwani Ali mwenyewe ndiyo sunna halisi ya Mtume naye ndiye mfasiri wa sunna hiyo na ndiye mwenye kuisimamia na Mtume alikwishasema kumuhusu Ali: "Ali kwangu mimi anayo daraja niliyonayo mimi kwa Mola wangu".


Taz: As-Sawaiqul-Muhriqah. As-Sawaiqul-Muhriqah cha ibn Hajar uk. 106, Dhakhairul-Uqba uk. 64, Riyadhun-Nadhrah Juz. 2 uk. 215, Ihqaqul-Haq Juz. 7uh217. Maana ya hadithi hiyo ni kwamba: Kama ambavyo Mtume Muhammad ndiye pekee anayefikisha ujumbe toka kwa Mola wake, basi Ali ndiye pekee atayefikisha ujumbe toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.). Lakini dhambi ya Ali ni kule kutokuukubali Ukhalifa wa aliyekuwa kabla yake, na dhambi ya Mashia wake ni kwamba wao wamemfuata katika hilo wakapinga kuwa chini ya Ukhalifa wa Abubakar, Umar na Uthman na kwa ajili hiyo wakaitwa kuwa ni "Marafidh " yaani wapinzani.


Kwa hiyo basi, pindi Masunni wanapopinga itikadi za Kishia na kauli zao hilo ni kwa sababu mbili tu: Ya Kwanza:Ni uadui ambao moto wake uliwashwa na watawala wa Kibanu Umayyah kwa kutumia uongo na madai (ya uzushi) na kutengeneza riwaya za uongo. Ya Pili:Ni kwamba itikadi za Mashia zinapingana na mwenendo wa Masunni wa kuwaunga mkono Makhalifa (ambao hawakustahiki Ukhalifa) na pia kuyaona makosa yao na Ij-Tihadi zao dhidi ya maandiko (Qur'an na Sunna) kuwa ni sawa na ni sahihi, khususan watawala wa Kibanu Umayyah wakiongozwa na Muawiyah bin Abi Sufiyan. Na mpaka hapa mwenye kutafiti na kufuatilia atakuta kwamba tofauti baina ya Shia na Sunni ilianza siku ya Saqifah na ikaendelea ikawa kubwa na kila tofauti iliyokuja baada yake imezaliwa na kutokana ana hapo, Dalili kubwa ya hilo ni kwamba itikadi zile ambazo Masunni huwakebehi ndugu zao Mashia, zinao uhusiano thabiti na maudhui ya Ukhalifa na zinatokana na maudhui hiyo; kama vile tofauti ya idadi ya Maimamu, Tamko la Uimamu, Ismah, Elimu ya Maimamu, Badau, Taqiyyah, Mahdi anayengojewa na mengineyo.


Nasi tunapochunguza ndani ya kauli za pande mbili hizi (Shia na Sunni) hali ya kuwa ni wenye kujiepusha na upendeleo basi huenda tusikute tofauti kubwa baina ya itikadi zao, na wala hatutakuta uhalali wa kuikuza (tofauti iliyopo) na kebehi hii, kwani wewe wakati unasoma vitabu vya Sunni anayewashutumu Mashia, utadhania kabisa kwamba Mashia wamebomoa Uislamu na kwenda kinyume cha misingi yake na sheria zake na wamezusha dini nyingine. Wakati ambapo mtafiti muadilifu atakuta katika kila itikadi ya Kishia iko asili iliyothibiti ndani ya Qur'an na Sunna hata katika vitabu vya hao wanaowapinga Mashia na kuwatukana kutokana na msimamo wao ndani ya itikadi hizo. Vile vile hakuna ndani ya itikadi hizo jambo linalopingana na akili nukuu au mwenendo mwema. Na ili ukubainikie usahihi wa haya ninayoyadai ewe msomaji mwenye utambuzi, nitakuonesha itikadi hizo.11
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

ISMAH Mashia wanasema:"Tunaitakidi kwamba Imam ni kama Nabii, ni wajibu awe Maasum (mwenye kuhifadhika) kutokana na machafu yote na maovu yenye kudhihiri na yenye kufichikana tangu miaka ya utotoni mpaka kufa (asiyafanye hayo) kwa kukusudia au kusahau. Kama ambavyo ni wajibu Imam awe amehifadhiwa kutokana na kusahau, kukosea na kughafilika, kwa sababu Maimamu ndiyo walinzi wa sheria na ndiyo wenye kuisimamia, hivyo hali yao katika jambo hilo ndiyo hali ya Mtume. Dalili ambayo imetupelekea tuitakidi Ismah ya Manabii ndiyo hiyo hiyo iliyotupelekea tuitakidi Ismah ya Mamimau bila tofauti yoyote. Taz: Aqaidul-Imamiyah uk. 67. Naam hivi ndivyo tunavyoona, haya ni maoni ya Mashia kuhusu maudhui ya Ismah basi je, ndani ya itikadi hii kuna kitu kinachopinga Qur'an na Sunna? Au kuna ambacho akili inakipinga? Au kuna ambacho kinauharibu Uislamu na kuuvuruga, au kipo kinachoshusha heshima ya Mtume au Imam?


Hapana, kamwe hatukukuta ndani ya kauli hii isipokuwa ni kukiunga mkono kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume wake, na mambo ambayo yanakubaliana na akili iliyo salimika na wala hakuna kinachoipinga, na yamo mambo ambayo yananyanyua heshima ya Mtume na Imam na kumtukuza. Basi hebu na tuanze utafiti wetu kwa kuisoma Qur'an Tukufo. Mwenyezi Mungu amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu na kukutakaseni sana enyi watu wa nyumba (ya Mtume)". Qur'an, 33:33 Iwapo kuondoshewa uchafu ambako kunakusanya mambo mabaya, na kutakaswa kutokana na kila dhambi hakufidishi Ismah, basi ni nini maana yake? Mwenyezi Mungu anasema: "Hakika wale wanaomuogopa (Mwenyezi Mungu) zinapowagusa pepeso za shetani hukumbuka, basi mara huwa wamekwishaiona njia". (Qur'an, 7:201) Ikiwa Muumini mcha Mungu, Mwenyezi Mungu humuhifadhi kutokana na vitimbi vya Shetani pindi anapojaribu kumwita na kumpotosha, Muumini hukumbuka na kuiona haki kisha huifuata, hivyo basi unafikirije kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemteua na akamuondoshea uchafu na kumtakasa sana sana?

Na anasema Mwenyezi Mungu: "Kisha tumewarithisha (tumewapa) kitabu wale tuliowachagua miongoni mwa waja wetu". (Qur'an, 35:32) Na yeyote achaguliwaye na Mwenyezi Mungu Mtukufu bila shaka anakuwa ni Maasum (aliyehifadhiwa) kutokana na makosa. Aya hii ndiyo aliyoitolea hoja Imam Ridhaa ambaye yeye ni miongoni mwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) dhidi ya wanachuoni aliowakusanya Khalifa wa Kibani Abbas aitwaye Maamum bin Harun Rashid. Imam aliwathibitishia kwamba wao Maimamu wa nyumba ya Mtume ndiyo waliokusudiwa kwenye aya hii, na kwamba Mwenyezi Mungu amewachagua na kuwarithisha wao elimu au Kitabu (Qur'an), na hao wanachuoni walimkubalia juu ya jambo hilo. Taz: Al-I'Qdul-Farid cha ibn Abdirabbih Juz. 3 uk. 42.

Hii ni baadhi ya mifano iliyokuja ndani ya Qur'an Tukufu, na ziko aya nyingine zinazofidisha juu ya Ismah ya Maimamu, kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo: "Maimamu wanaoongoza kwa amri yetu." Na nyinginezo, lakini tunatosheka kwa kiasi hiki kwa nia ya kufupisha maelezo. Na baada ya Qur'an Tukufu hebu angalia maelezo yaliyokuja ndani ya sunna ya Mtume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema: "Enyi watu hakika mimi ninaacha kwenu vitu ambavyo mkivichukua hamtapotea, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu": Taz: 1). Sahih Tirmidhi Juz. 5 uk. 328. 2). Al-Hakim ndani ya Mustadrak Juz. 3 uk. 148. 3). Al-Imam Ahmad bin Hambal ndani ya Musnad yake Juz. 5 uk. 189. Kama unavyoona bayana kwamba Maimamu kutoka nyumba ya Mtume (s.a.w.) wamehifadhiwa. Kwanza: Ni kwa kuwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kimehifadhiwa, hakifikwi na upotofu kabla au baadaye ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na mwenye kukitilia shaka basi amekufuru. Pili: Ni kwamba mwenye kushikamana navyo "Kitabu na kizazi cha Mtume" atasalimika kutokana na upotofu. Hivyo basi hadithi hii imejulisha kwamba kitabu na kizazi cha Mtume haiwezekani kuwa vinamakosa. Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.): "Bila shaka mfano wa watu wa nyumba yangu ni kama Safina ya Nuhu, atakayeipanda ataokoka na mwenye kuiacha ataangamia".


Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 2 uk. 343, Kanzul-Ummal Juz. 5 uk. 95, As-sawaiqul-Muhriqah cha ibn Hajar uk. 184. Kama uonavyo ubainifu kuwahusu Maimamu kutoka nyumba ya Mtume (s.a.w.) kwamba wao ni Maasum (wamehifadhiwa) kutokana na makosa, na kwa ajili hiyo husalimika kila apandaye Safina yao na kila atayeacha kupanda Safina hiyo ataangamia katika upotofu. Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.): "Yeyote atakayependa kuishi maisha niliyoishi mimi na afe kifo nilichokufa mimi na aingie ndani ya pepo ambayo Mola wangu ameniahidi nayo ni pepo ya milele, basi na amtawalishe Ali na watoto wake baada yake, bila shaka wao hawatakutoweni nje ya mlango wa uongofu na hawatakuingizeni ndani ya mlango wa upotofu". Taz:

1) Kanzul-Ummal Juz. 6 uk. 155.
2). Maj-Mauz-Zawaid cha Al-Haithami Juz. 9 uk. 108.
3). Al-isabah cha Ibn Hajar Ai-As-Qalani.
4). At-Tabrani ndani ya Al-Jamiul-Kabir.
5). Tarikh Ibn AsakirJuz. 2 uk. 99.
6). Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 128
7). Hilyatul-Auliyai Juz. 4 uk. 349. 8). Ihqaqul-Haqi Juz. 5 uk. 108.
Kama uonavyo ya kwamba Maimamu kutoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.) ambao ni Ali na wanawe,
wamehifadhiwa kutokana na makosa kwani wao kamwe hawatawaingiza watu waliowafuata katika mlango wa upotofu. Na hapana upinzani kwamba mtu anayekosea haiwezekani kwake kuwaongoa watu.
Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.):
"Mimi ni muonyaji na Ali ni muongozaji, na kwako ewe Ali wataongoka wenye kuongoka baada yangu:
Taz: 1). Tafsir At-Tabari Juz. 13 uk. 108.
2). Tafsir Ar-Razi Juz. 5 uk. 271.
3). Tafsir ibn Kathir Juz. 2 uk. 502.
4). Tafsir Ash-Shaukani Juz. 3 uk. 70.
5) Ad-Durrul-Manthoor cha Suyuti Juz. 4 uk. 45.
6). Nurul-Ab-Sar uk. 71.
7). Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 129.
8). Tafsir ibn JauziJuz. 4 uk. 307.
9). Shawahidut-TanzilJuz. 1 uk. 293.
10). A 1-Fusulul-Muhimmah Na yanabiul-Mawaddah.

Hii ni hadithi nyingine iliyo bayana kabisa kuhusu Ismah ya Imam kama ambavyo haifichikani kwenye akili. Imam Ali kwa nafsi yake mwenyewe ameithibitisha Ismah kwake mwenyewe na kwa Maimamu miongoni mwa wanawe pale aliposema: "Mnakwenda wapi na ni vipi mnadanganywa hali ya kuwa muongozo upo na aya ziko wazi na minara imesimikwa, basi vipi mnapotoshwa bali ni jinsi gani mnapotea hali yakuwa miongoni mwenu kimo kizazi cha Nabii wenu ambao ni walinzi wa haki, na ndiyo muongozo wa dini na ndimi za ukweli, basi waheshimuni kwa heshima nzuri ya Qur'an na muwafuate kama ngamia mwenye kiu kali afuatavyo (maji). Enyi watu kichukuweni kutoka kwa Mtume wa mwisho (s.a.w.), hakika hufariki mwenye kufariki miongoni mwetu (sisi watu wa nyumba ya Mtume) lakini anakuwa hajafariki, na huchakaa mwenye kuchakaa miongoni mwetu lakini siyo kwamba amechakaa, basi msiseme msiyoyajua, kwani haki imo ndani ya vile mnavyovikanusha. Na toshekeni kwa mtu ambaye ninyi hamna hoja yoyote dhidi yake, nami ndiye huyo mtu, basi je, sikukitumia ndani yenu kizito kikubwa na ninakuachieni kizito kidogo nami nimesimika kwenu bendera ya Imani..."[92]


Taz: Nahjul-Balaghah ya Imam Ali Juz. 1 uk. 155. Na baada ya ubainifu huu kutoka ndani ya Qur'an Tukufu na sunna tukufu ya Mtume na kauli za Imam Ali ambazo zote zinajulisha juu ya Ismah yao (a.s.) basi hivi kweli akili itapinga Ismah ya wale aliowachagua Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya uongofu? Jawabu ni kwamba, kamwe haiwezi kupinga, kinyume chake ni kwamba akili inasema kuwa, kuna ulazima wa kuwepo hiyo Ismah kwani yeyote ambaye amewakilishwa wajibu muhimu wa uongozi na kuongoa watu haiwezekani awe ni mtu wa kawaida anayezukiwa na makosa, kusahau na kisha kushehenezwa madhambi na makosa halafu aaibishwe na akosolewe na watu. Bali akili inaona ni lazima awe mjuzi mno kuliko wengine katika zama zake na muadilifu, mchamungu, na shujaa kuliko wote, sifa ambazo zinapandisha cheo cha kiongozi na kumtukuza mbele za watu na kumletea heshima kwa wote na utukufu na hatimaye wakamtii bila ya woga.


Ikiwa hali ya mambo iko namna hiyo, basi yanini kebehi yote hii na vitisho dhidi ya wanao itakidi hivyo? Bila shaka imasikia na kusoma Masunni wanavyoikosoa maudhui ya Ismah kwa kusema kwamba, Mashia ndiyo wanaomvisha nishani ya Ismah yule wampendaye, au yeyote azungumzaye kuhusu kuthibiti kwa Ismah (kwao wao) huwa amesema jambo bay a na la kufru, basi si hili wala lile, bali Ismah kwa Mashia ni kuwa huyo Maasum awe amezungukwa na uangalizi na uhifadhi wa Mola ili shetani asiweze kumpoteza, na wala nafsi inayoamrisha maovu isiweze kuishinda akili yake ikampeleka kwenye maasi. Jambo hili Mwenyezi Mungu hakuliharamisha kwa waja wake wamchao kama ilivyotangulia katika ay a isemayo: "Wale ambao wamchao Mwenyezi Mungu unapowapata upepeso wa Shetani hukumbuka, basi mara huiona haki". Na hii Ismah iliyokadiriwa kwa waja wa Mwenyezi Mungu huenda ikaondoka kwa kukosekana sababu zake ambazo ni ucha Mungu kwa hiyo mja atakapokuwa mbali na ucha Mungu Mwenyezi Mungu hawezi kumuhifadhi. Ama Imamu ambaye Mwenyezi Mungu amemchagua, huyo hapotoki wala kulegalega kwenye ucha Mungu na kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu.


- Bila shaka imekuja ndani ya Qur'an simulizi juu ya Bwana wetu Yusuf (a.s.): "Kwa'hakika mwanamke huyo alimkusudia (Yusuf) na (Yusuf) naye angemkusudia mwanamke yule, lau kama asingeona dalili toka kwa Mola wake, tumefanya hivyo ili tumwepushie kila jambo la ubaya na la uovu. Hakika yeye (Yusuf) ni miongoni mwa waja wetu waliotakaswa". (Qur'an, 12:24) Na kwa sababu Bwana wetu Yusuf hakukusudia kufanya zinaa kama walivyofasiri baadhi ya wafasiri, kwani haiwezekani kabisa kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu kufanya tendo hili baya.

IDADI YA MAIMAMU (NI KUMI NA WAWILI) Mashia wanasema kwamba idadi ya Maimamu Ma'asum baada ya Mtume (s.a.w.) hi kumi na wawili, hawazidi wala kupungua, na Mtume wa Mwenyezi Mungu amewataja kwa majina yao na idadi yao. Taz: Yanabiul-Mawaddah cha Al-Qanduzi Al-Hanafi uk. 99 Juz. 3. Nao ni hawa wafuatao:

1) Imam Ali bin Abi Talib
2) Imam Hasan bin Ali
3) Imam Husein bin Ali
4) Imam Ali bin Husein (Zainul-Abidin)
5) Imam Muhammad bin Ali (Al-Baqir)
6) Imam Ja'afar bin Muhammad (As-Sadiq)
7) Imam Musa bin Ja'afar (Al-Kadhim)
8) Imam Ali bin Musa (Ar-Ridha)
9) Imam Muhammad bin Ali (Al-Jawad)
10) Imam Ali bin Muhammad (Al-Hadi)
11) Imam Al-Hasan bin Ali (Al-Askari)
12) Imam Muhammad bin Al-Hasan (Al-Mahdi)

Basi hawa ndiyo Maimamu kumi na wawili ambao Mashia wanazungumza kuhusu Ismah yao ili baadhi ya Waislamu wasijegubikwa na vitimbi. Hivyo basi Mashia hawaitambui hapo zamani wala sasa hivi Ismah nyingine isiyokuwa ya Maimamu hawa ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwataja kabla hata hawajazaliwa, na baadhi ya wanachuoni wa Kisunni wameyathibitisha majina yao (hao Maimamu) kama ilivyotangulia (kuelezwa). Nao Bukhar na Muslim wamethibitisha ndani ya Sahih zao hadithi inayohusu Maimamu kwa idadi yao ambayo ni kumi na wawili na wote ni kutokana na Qur'aish. Taz: 1). Sahih Bukhar Juz. 8 uk. 127. 2). Sahih Muslim Juz. 6 uk. 3. Na hadithi hizi hazisimami wala hazisihi isipokuwa tutakapozifasiri kuwahusu Maimamu wa nyumba ya Mtume ambao Mashia Imamiyah ndiyo wanaowazungumzia, na Masunni wao ndio wanaotakiwa kutatua utata huu, kwani idadi ya Maimamu kumi na wawili ambayo wameithibitisha ndani ya vitabu vyao mpaka sasa kwao imebakia kuwa ni fumbo ambalo hawalipatii jawabu!

ELIMU YA MAIMAMU Na miongoni mwa mambo ambayo Masunni huwakebehi Mashia ni kauli ya Mashia isemayo kwamba: "Maimamu kutoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.), Mwenyezi Mungu amewahusisha na elimu ambayo hakuwashirikisha pamoja na yeyote miongoni mwa watu, na kwa kuwa Imamu ni mjuzi mno kuliko watu wote wa zama zake, basi haiwezekani kwa yeyote kumuuliza Imam kisha akashindwa kutoa jawabu!! Basi je, madai haya yanayo dalili? Na tuanze na Qur'an kama ilivyo kawaida yetu katika kila uchambuzi tunaoufanya.. Mwenyezi Mungu anasema: "Kisha tumewarithisha (tumewapa elimu ya) kitabu wale ambao tumewateua miongoni mwa waja wetu". (Qur'an, 35:32) Aya hii inajulisha dalili iliyo wazi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameteua waja miongoni mwa watu na akawarithisha elimu ya Kitabu.


Basi je, tunaweza kuwafahamu waja hawa walioteuliwa? Hapo kabla tumeeleza kuwa Imamu wa nane miongoni mwa wale Maimamu wanaotoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.) ambaye ni Ali bin Musa Ar-Ridhaa alitoa ushahidi ya kuwa aya hii ilishuka kuwahusu wao, na hali hii (aliisema) pindi Maamuni (Khalifa wa Banu Abbas) alipomkusanyia Imam (huyu) Maqadhi arobaini miongoni mwa Maqadhi mashuhuri, na kila mmoja wa Maqadhi hawa aliandaa mas-ala arobaini ili kumuuliza Imam Ali Ar-Ridhaa. Basi Imam (a.s.) aliwanyamazisha (alipowajibu wote bila kubabaika) na wao wakakiri kuwa yeye Imam ni mjuzi mno. ; Taz: Al-Iqdul-Farid cha ibn Abd Rabbih Juz. 3 uk. 42. Hivyo basi, ikiwa Imam huyu wa nane ambaye alikuwa hata hajafikia umri wa miaka kumi na minne wakati wa majadiliano kati yake na wanachuoni hao ambao walikiri juu ya elimu yake, basi vipi ishangaze (na kuwa ngeni) kauli ya Mashia isemayo kuwa Maimamu ni wajuzi mno, maadamu wanachuoni wa Kisunni wanakiri kuhusu hali hiyo kwa Maimamu. Ama tukitaka kufasiri Qur'an kwa Qur'an, basi tutapata aya nyingi zinazoelekeza maana moja, na zinabainisha kwamba Mwenyezi Mungu kwa hekima yake amewahusisha Maimamu kutoka ndani ya nyumba ya Mtume (s.a.w.) kwa elimu itokayo kwake, amewapa ili wawe ni Maimamu wa uongofu na taa za kuondosha kiza.


Mwenyezi Mungu anasema: "Humpa hekima amtakaye, na yeyote aliyepewa hekima, basi bila shaka amepewa kheri nyingi, na hawakumbuki ila wenye akili". (Qur'an, 2:269) Na amesema vile vile: "Basi ninaapa kwa maangukio ya nyota, na bila shaka hicho ni kiapo kikubwa lau kama mngejuwa, hakika hii ni Qur'an Tukufu, iliyowekwa ndani ya Kitabu kilichohifadhiwa (madhubuti) hapana atayekigusa (kukifahamu vyema) isipokuwa wale waliotakaswa". (Qur'an, 56:75-79) Mwenyezi Mungu ameapa katika aya hii kwa kiapo kikubwa ya kwamba Qur'an Tukufu inazo siri na maana za ndani zilizodhibitiwa, hawawezi kutambua maana zake na uhakika wake isipokuwa wale waliotakaswa, na hao waliotakaswa ni wale ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na amewatakasa sana sana.

Pia aya imejulisha kwamba, Qur'an ina undani ambao Mwenyezi Mungu amewahusisha kwa undani huo Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) na wala haiwezekani kwa asiyekuwa wao kuufahamu undani huo isipokuwa kupitia kwao. Hivyo basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ameelekeza juu ya ukweli huu akasema: "Msiwatangulie (Maimamu) mutaangamia, na wala msiwapuuze mtaangamia, na wala msiwafunze kwani wao ni wajuzi mno kuliko ninyi". Taz:
1). As-sawa'iqul-Muhriqah cha ibn HajarAsh-Shqfti uk. 148.
2). Ad-Durrul-Manthoor cha Suyuti Juz. 2 uk. 60.
3). Kanzul-UmmalJuz. 1 uk. 168.
4). Usudul-Ghabah Fii Maa'rifatis Sahabah Juz. 3 uk. 137.
Na kama alivyosema Imam Ali mwenyewe:
"Wako wapi wale waliodai kuwa wao wamebobea katika elimu kuliko sisi, huo ni uongo na ni dhulma dhidi yetu, Mwenyezi Mungu ametunyanyua sisi na wao akawatweza, na ametupa sisi wao akawanyima, na ametuingiza sisi wao akawatoa, kwetu sisi ndiko kunakoombwa uongofu na upotofu huondoka... Hakika Maimamu wanatokana na Quraish wamepandikizwa ndani ya tumbo hili toka kwa Hashim, haukubaliki Uimamu kwa asiyekuwa wao wala utawala haukubaliki toka kwa asiyekuwa wao." Taz: Nahjul-Balaghah Juz. 2 uk. 143, Muhammad Abdoh, Khutba namba 143. Na amesema Mwenyezi Mungu: "Waulizeni wenye kumbukumbu iwapo ninyi hamujui" (Qur'an, 16:43 na 21:7). Aya hii vile vile imeshuka kuwahusu Ahlul-Bait (a.s.).


Taz: 1). Tafsirut-Tabari Juz. 14 uk. 134. 2). Tafsir ibn Kathir Juz. 2 uk. 570. 3). Tafsirul-Qur-tubi Juz. 11 uk: 272. ;,. 4). Shawahidut-Tanzil cha Al-Haskani Juz.luk. 334. 5). Yanabiul-Mawaddah. 6). Ih-Qa-Qul-Haqq cha At-Tustari Juz. 3 uk. 482. Na inafidisha kwamba umma (wa Kiislamu) baada ya kuondoka kwa Mtume wake hauna budi kuwarejea Maimamu wanaotoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.) ili kuufahamu ukweli, na bila shaka Masahaba (r.a.) walimrejea Imam Ali bin Abi Talib ili awabainishie yaliyokuwa yakiwatatiza, kama ambavyo watu walivyowarejea Maimamu wa nyumba ya Mtume kwa miaka mingi ili wapate kufahamu halali na haramu na wapate (kunywa) elimu yao na mwenendo wao. Na iwapo Abu Hanifah anasema: "Lau si miaka miwili, basi Nuu'man angeangamia" akikusudia miaka miwili aliyoitumia kusoma kwa Imam Jaa'far Sadiq (a.s.) Na Imam Malik naye anasema: "Jicho halijaona wala sikio halijasikia, wala halijapita wazo katika moyo wa mtu yeyote (kuwa kuna) mbora kuliko Jaafar As-Sadiq kwa utukufu, elimu, ibada, na ucha Mungu" Taz: Kitabu Manaqib Ali bin Abi Talib kuhusu mazingira ya Imam Jaafar As-Sadiq. Kama mambo yako namna hii, Maimamu wa Kisunni wanakiri, basi ni za nini kebehi zote hizi na upinzani huu ni wa nini baada ya kuwepo dalili zote hizi na (hasa) baada ya historia ya Waislamu wote (kukubali) kwamba Maimamu toka katika nyumba ya Mtume (s.a.w.) walikuwa ni wajuzi mno kuliko watu wote wa zama zao? Basi ajabu iko wapi kwa Mwenyezi Mungu kuwahusisha mawalii wake aliowachagua (akawahusisha) kwa hekima na elimu, akawafanya kuwa ni kigezo cha waumini na kuwa viongozi wa Waislamu?

Lau Waislamu wangelifuatilia dalili za wao kwa wao, bila shaka wangetosheka na kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wangekuwa umma mmoja unaopeana nguvu na pasingekuwa na tofauti wala madhehebu mengi. Lakini hapana budi yatokee yote hayo ili Mwenyezi Mungu apate kupitisha jambo ambalo lilikuwa lazima litendeke:"Kusudi aangamiae, aangamie kwa dalili iliyo wazi na anayezindukana azindukane kwa dalili iliyo wazi na Mwenyezi Mungu ni msikivu mjuzi" (Qur'an 8:42)

AL-BADA'U Al-Bada'u: Ni kumdhihirikia kitu katika jambo fulani alilotaka kulifanya kisha rai yake kubadilika kuhusu jambo hilo na akafanya kitu ambacho hakuwa ameazimia kukifanya hapo kabla. Ama kauli ya Mashia kuhusu Al-Bada'u na kuinasibisha kwa Mwenyezi Mungu, na kebehi dhidi yao kwamba (Al-Bada'u) inawajibisha kutokujuwa na upungufu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kama watakavyo Masunni kuichukulia kwa maana hii, basi tafsiri hii ni potofu na wala Mashia hawasemi hivyo kamwe, na yeyote mwenye kuwanasibishia hilo bila shaka amewazulia. Zifuatazo ndizo kauli zao zinazowashuhudia tangu hapo zamani mpaka sasa. Amesema Sheikh Muhammad Ridha Al-Mudhaffar ndani ya kitabu chake kiitwacho "Aqaidul-Ima 'miyyah': "Al-Bada'u kwa maana hii ni muhali kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwani (itakuwa) ni kutokujua na ni upungufu, na hili haliwezekani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu (kutokujuwa na kuwa mpungufu wa sifa) na wala Mashia hawasemi hivyo". Imam Jaa'far As-Sadiq amesema: "Mwenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu amedhihirikiwa na kitu mdhihiriko wa majuto, basi mtu huyo kwetu sisi (atakuwa) amemkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu" Na amesema pia kwamba: "Mwenye kudai kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amedhihirikiwa na kitu ambacho jana alikuwa hakukifahamu basi mimi niko mbali naye".


Kwa hiyo basi "Al-bada'u" waisemayo Mashia haivuki mipaka ya Qur'an kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema: "Mwenyezi Mungu hufuta ayatakayo na huyathibitisha (ayatakayo) na kwake ndiko kwenye msingi wa Kitabu" (Qur'an, 13:39). Na kauli hii Masunni wanaisema kama waisemavyo Mashia, basi ni kwa nini wanaumbuliwa Mashia na wala Masunni hawaumbuliwi ambapo wao (Masunni) wanasema Mwenyezi Mungu anabadilisha hukumu na kugeuza muda na riziki? Ibn Mar-Dawaih na ibn Asakir wamethibitisha (mapokezi) toka kwa Ali (a.s.) kwamba yeye alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kuhusu aya hii isemayo: "Mwenyezi Mungu hufuta ayatakayo na huyathibitisha (ayatakayo) na kwake ndiko kwenye msingi wa kitabu." Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia: "Nitakutuliza kwa tafsiri ya aya hii, na nitawatuliza umma wangu baada yangu kwa tafsiri yake, (Mtume akasema) Kutoa sadaka kwa namna inayostahiki na kuwatendea wema wazazi wawili, na kutenda mema (ni mambo) yanayobadilisha maovu kuwa mema, na yanaongeza umri (wa kuishi) na yanakinga misukosuko ya maovu"

Naye ibn Al-Mindhir na ibn Abi1 Hatim na Al-Baihaqi ndani ya Ash-Shuabi toka kwa Qais bin Ubba'd (r.a.) amesema: "Kuna jambo Mwenyezi Mungu hulitenda katika kila usiku wa kumi wa miezi mitukufu, ama katika usiku wa kumi wa mwezi wa Rajab, ndani yake Mwenyezi Mungu huyafuta ayatakayo na huyathibitisha ayatakayo. Na amethibitisha Abd bin Hamid, ibn Jarir na ibn Mundhir toka kwa Umar bin Al-Khatab (r.a.) kwamba yeye Umar alisema hali yakuwa anatufu Al-Qaaba: "Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa umeniandikia uovu au dhambi basi ifute, hakika wewe unafuta ukitakacho na unakithibitisha ukitakacho, na kwako ndiko kwenye msingi wa kitabu hivyo basi fanya iwe ni wema na ni msamaha".


Taz: Ad-Durrul-Manthoor Juz. 4 uk. 661. Naye Bukhar ndani ya sahihi yake juzuu ya nne ukurasa sabini na nane (Kitabu Bad'il-Khalqi Babu Dhikri L-Malaikah) amethibitisha kisa cha ajabu kinachosimulia miiraji ya Mtume (s.a.w.) na kukutana na Mola wake; miongoni mwa aliyoyasema Mtume (s.a.w.) ni kama ifuatavyo: "Kisha nikafaradhishiwa sala khamsini, nikaondoka mpaka nikafika kwa Musa akasema: Je, kuna nini ulichofanya? Nikasema nimefaradhishiwa sala khamsini, akasema: Mimi nawajua mno watu kuliko wewe nimeshughulika na wana wa Israel sana, hakika ummati wako hautaweza, basi rudi kwa Mola wako umuombe (akupunguzie), nikarudi nikamuomba na akazifanya kuwa arobaini. Nikarudi tena kwa Musa akaniambia kama alivyoniambia kwanza nikarudi kwa Mola naye akanipunguzia zikawa thelathini, Ishirini, Kumi, kisha tano, nikaja kwa Musa akasema umefanya nini? Nikasema amezifanya kuwa sala tano, akasema kama kwanza. Nikamwambia, Nimesalimu amri. Pakanadiwa Hakika mimi nimepitisha faradhi zangu na nimewapunguzia waja wangu na nitakuwa nalipa kwa kila tendo jema moja thawabu kumi." Na ndani ya riwaya nyingine vile vile Bukhari ameinakili riwaya hiyo ameandika, Na baada ya Muhammad (s.a.w.) kurudi kwa Mola wake mara nyingi baada ya kufaradhishiwa sala tano, Musa (a.s.) alimtaka Muhammad (s.a.w.) arudi kwa Mola wake ili ampunguzie, kwani ummati wake hawawezi (kutekeleza) japo sala tano, lakini Muhammad (s.a.w.) alimjibu Musa; "Namuonea haya Mola wangu".


Taz: Sahih BukharJuz. 4 uk. 250 Babul-Miiraj, Sahih Muslim Juz. 1 uk. 101 mlango wa Israi ya Mtume na kufaradhishwa swala. Naam (msomaji) soma na uone maajabu ya itikadi hizi zisemwazo na wasimuliaji wa Kisunni, lakini pamoja na hayo Masunni wanawatukana Mashia ambao ni wafuasi wa Maimamu kutoka katika nyumba ya Mtume kuhusu kauli ya Al-Bada'u. Na hawa Masunni ndani ya kisa hiki wanaitakidi kwamba Mwenyezi Mungu alimfaradhishia Muhammad (s.a.w.) sala khamsini kisha baada ya Muhammad kumrudia Mwenyezi Mungu (mara nyingi) ikamdhihirikia azifanye kuwa arobaini kisha ikamdhihirikia baada ya Muhammad kumrejea mara ya pili akazifanya kuwa thelathini, kisha ikamdhihirikia baada ya kurejea mara ya tatu akazifanya zikawa ishirini kisha baada ya kumrejea mara ya nne akazifanya kuwa kumi, kisha ikamdhihirikia baada ya kumrejea mara ya tano Mwenyezi Mungu akazifanya zikawa sala tano.


Na tukifumbia macho suala la kukubali riwaya hii au kutoikubali, ni kweli kabisa kwamba kauli ya "Al-Bada'u" ni Aqida madhubuti inayokubaliana na mafunzo ya dini ya Kiislamu na msingi wa Qur'an. "Bila shaka Mwenyezi Mungu habadilishi mambo ya watu mpaka wabadilishe yaliyoko katika nafsi zao". Na lau siyo itikadi yetu - Masunni na Mashia - kwamba Mwenyezi Mungu anabadilisha na kugeuza, basi sala zetu na dua zetu zisingekuwa na faida wala sababu wala maana, kama ambavyo sote tunaamini kwamba Mwenyezi Mungu hubadilisha hukmu na kufuta sheria kutoka kwa Nabii mmoja hadi mwingine, na hata katika sheria ya Mtume wetu (s.a.w.) kuna nasikh na mansukh (aya inayofuta na inayofutwa), hivyo basi kauli kuhusu "Al-Bada'u" siyo kufuru wala siyo kutoka katika dini na haiwafalii Masunni kuwaumbuwa Mashia kwa ajili ya itikadi hii, kama ambavyo haiwafalii Mashia vile vile kuwaumbuwa Masunni. Na ukweli ulivyo mimi naiona hii riwaya ya miraji kuwa inawajibisha kumnasibishia ujinga Mwenyezi Mungu Mtukufu na inaitia dosari heshima ya mtu Mtukufu aliyetambulikana katika historia ya wanaadamu naye ni Mtume wetu Muhammad (s.a.w.), pale inaposema kwamba Musa alimwambia Muhammad "Mimi nawajua mno watu kuliko wewe", na pia riwaya hii inamfanya Musa kuwa ni mbora ambapo lau si yeye, basi Mwenyezi Mungu asingeupunguzia ummati Muhammad.


Nami nashindwa kufahamu ni vipi Musa alifahamu kwamba ummati Muhammad hawawezi hata sala tano wakati ambapo Mwenyezi Mungu hakulijua hilo na anawakalifisha waja wake jambo wasiloliweza akawafaradhishia sala khamsini? Na hebu Ewe ndugu msomaji, wewe na mimi kwa pamoja tupime ni vipi zitafaradhishwa sala khamsini kwa siku moja, basi hapatakuwa na shughuli yoyote wala kazi yoyote wala hakuna kusoma hata kutafuta riziki wala harakati yoyote au jukumu lolote, (na kama ni hivyo) basi mtu atakuwa kama Malaika aliyekalifishwa kwa sala na ibada tu. Na hebu fanya mahesabu mepesi ili none uongo wa riwaya hii. Ukizidisha dakika kumi ambazo ni muda unaokubalika kiakili kutekeleza faradhi moja ya sala ya jamaa (uzidishe) mara khamsini utakuja muda uliofaradhishwa (kwa ajili ya sala) ni masaa kumi, hivyo basi ni juu yako uvumilie au uikatae dini hii inayowakalifisha wafuasi wake mambo zaidi ya uwezo wanaoweza kuumudu na kuwafaradhishia wasiyoyaweza.


Basi ikiwa Masunni wanawakebehi Mashia kwa kusema kwao juu "Al-Bada'u", na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hubadilisha na kugeuza vile apendavyo, hivyo ni kwa nini wao wenyewe hawajikosoi kuhusu kauli yao kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amegeuza na kubadilisha hukumu mara tano katika faradhi moja ndani ya usiku mmoja ambao ni usiku wa miraji? Mwenyezi Mungu ailaani chuki ya upofu na upinzani mbaya ambao unafunika ukweli na kuugeuza chini juu. Basi mtu mwenye chuki anamshinikiza anayemkhalifu katika maoni na kumpinga kwa mambo yaliyo wazi, kumkebehi, kueneza uzushi dhidi yake na vitisho kutokana na mambo ya kawaida ambayo yeye anayo makubwa kuliko hayo. Hali hii inanikumbusha yale aliyoyasema Bwana wetu Isa (a.s.) kuwaambia Wayahudi aliposema: "Ninyi mnatazama kapi kwenye macho ya watu, na wala hamtazami boriti lililoko machoni kwenu". Au kwa mfano wa msemaji aliposema: "Alinitupia maradhi yake na akatokomea"


Na huenda mtu fulani anaweza akapinga (akasema) kwamba tamko la "Al-Bada'u" halikutoka kwa Masunni, na kwamba kisa hiki (baina ya Mtume Muhammad na Mtume Musa) pamoja na kuwa maana yake kinajulisha juu ya kuweko mabadiliko katika hukmu, lakini haiwezekani kukata shauri kuwa lilimdhihirikia Mwenyezi Mungu. Nami ninasema hivi, kwa kuwa ni mara nyingi nilikuwa nikikieleza kisa cha Miiraji ili kutolea ushahidi wa kauli ya "Al-Bada'u" kwa Masunni, basi baadhi yao walinipinga juu ya rai hii, lakini baadaye waliikubali na niliwasimamisha kwenye riwaya nyingine kutoka ndani ya Sahih Bukhari inayoitaja "Al-Bada'u" kwa tamko lililo wazi bila ya utatanishi. Bukhari ameeleza maelezo yaliyotoka kwa Abu Hurairah kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema: "Hakika kulikuwa na watu watatu miongoni mwa Bani Israeli mwenye mbaranga, kipofu na mwenye upara, Mwenyezi Mungu akaona awape mtihani, akawatumia Malaika, Malaika akamuendea mwenye mbaranga akamwambia, ni kitu gani ukipendacho mno, akasema, (napenda) rangi nzuri na ngozi nzuri (ya mwili) watu wamenichukia (kwa ubaya wa ngozi yangu) basi Malaika akampangusa na ugonjwa ule ukamuondokea, akampa rangi nzuri na ngozi nzuri, kisha akamwambia ni mali ipi uipendayo, akasema, ngamia, basi akapewa ngamia mwenye mimba. Kisha Malaika yule akamwendea mwenye kipara akamwambia, ni kitu gani ukipendacho mno, akasema, nywele nzuri na hiki kipara kiniondokee, watu wamenichukia (kwa ajili hii) basi Malaika akampangusa na kipara kikaondoka na akapewa nywele nzuri, kisha Malaika akamwambia, ni mali gani uipendayo, akasema ngombe, basi akampa ngombe mwenye mimba. Halafu Malaika akamwendea kipofu akamwambia, ni kitu gani ukipendacho mno, akasema, Mwenyezi Mungu ayarudishe macho yangu, basi akampangusa na Mwenyezi Mungu akamrudishia macho yake akamwambia ni mali gani uipendayo, akasema, mbuzi, basi akampa mbuzi mwenye kuzaa...


Ulipita muda fulani, yule Malaika alirudi baada ya ngamia, ng'ombe na mbuzi walipokuwa wengi kwa watu hawa kiasi kila mmoja wao akawa anamiliki kikundi (cha wanyama hao) basi akawaendea mwenye mbaranga na mwenye kipara na yule kipofu na kila mmoja wao akiwa katika hali yake, na akamtaka kila mmoja wao ampe alicho nacho, basi yule mwenye kipara na mwenye mbaranga wakamkatalia, na Mwenyezi Mungu akawarudisha katika hali yao waliyokuwa nayo hapo zamani, (ama) yule kipofu yeye akampa (Malaika alichokitaka) Mwenyezi Mungu akamzidishia na akambakishia macho yake. Taz: Sahih Bukhar Juz. 2uk. 259.

Na kwa sababu hii basi mimi nawaambia ndugu zangu (Masunni) ile kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Enyi mlioamini (watu fulani) wanaume wasiwakebehi wanaume (wengine) huenda wakawa bora kuliko wao, wala wanawake fulani wasiwakebehi wanawake (wengine) huenda wakawa bora kuliko wao, wala msijiaibishe wenyewe na wala msiitane majina mabaya, jina baya la ufasiki ni lile (aitwalo mtu) baada ya imani, na wasiotubu hao ndio madhalimu." (Qur'an, 49:11) Ni kama ambavyo natamani kwa moyo wangu wote kwamba Waislamu wangerejea kwenye muongozo wao, na waipuuze chuki (iliyojengeka baina yao) na waache ushabiki ili akili ipate kutulia mahala pake katika kila uchambuzi (unaofanywa) hata kama (uchambuzi huo) utafanywa na mpinzani wao, na wajifunze kutoka ndani ya Qur'ani Tukufu taratibu za uchambuzi na majadiliano kwa njia iliyo bora zaidi.


Bila shaka Mwenyezi Mungu alimpelekea ufunuo Mtume wake (s.a.w.) awaambie wapinzani, "Bila shaka ni sisi au ninyi, (kuna ambaye) yuko juu ya uongofu au katika upotofu uliodhahiri" (Qur'an, 34:24). Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anaipandisha daraja ya washirikina hawa, naye anajiteremsha na kuwapa sehemu fulani itakayowafanya walete dalili zao na hoja zao ikiwa wanasema kweli. "Basi sisi tuko wapi kutokana na hii tabia tukufu (ya Mtume (s.a.w.)?12
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

TAQIYYAH Kama tulivyotangulia kusema kuhusu kauli ya "Al-Bada'u, basi Taqiyyah nayo vile vile ni miongoni mwa mambo yanayopingwa kwa Masunni, na wao huwakejeli ndugu zao Mashia kwa hilo na kuwaona kuwa ni wanafiki, kwani hukidhihirisha ambacho sicho walichokificha...!! Na ni mara nyingi nimezungumza na baadhi yao na nikajaribu kuwakinaisha kwamba Taqiyyah siyo unafiki, lakini hawakukinaika, bali wakati mwingine utamkuta anayesikiliza jambo hili anachukia na wakati mwingine anashangaa, na hali yakuwa anadhani kuwa itikadi hii imezushwa katika Uislamu na kama kwamba ni miongoni mwa yaliyofanywa na Shia na uzushi wao. Lakini pindi mwenye kufuatilia atapofanya uchambuzi na akawa muadilifu, atakuta kwamba itikadi hii yote ni katika uti wa mgongo wa Uislamu na imetokana na Qur'an Tukufu na Sunna Tukufu ya Mtume (s.a.w.), bali mafunzo ya dini tukufu ya Kiislamu na hii sheria madhubuti havisimami ila kwa Taqiyyah.


Na jambo la kushangaza kwa Masunni ni kwamba, wao wanazipinga itikadi ambazo wanazitaja (ndani ya vitabu vyao) na vitabu vyao na sihahi zao na Musnad zao zimejaa mambo hayo na zinashuhudia dhidi yao. Hebu tuyasome kwa pamoja yale wayasemayo Masunni kuhusu Taqiyyah: Ibn Jarir na ibn Abi Hatim wamethibitisha kwa njia ya Al-Au'fi kutoka kwa ibn Abbas katika kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Isipokuwa kwa ajili ya kujilinda kutokana na shari zao" (Qur'an, 3:28) Amesema ibn Abbas "Taqiyyah (kujilinda) ni kwa ulimi, yeyote atakayelazimishwa jambo fulani aliseme hali ya kuwa jambo hilo ni la kumuasi Mwenyezi Mungu, naye akalisema kwa kuwachelea watu, na moyo wake umetulizana kwa imani, basi hali hiyo haitamdhuru kwani Taqiyyah ni kwa ulimi"

Taz: Ad-Durrul-Manthoor Fi Tafsir Bil- Maathur cha Jalalud-Din Suyuti. Na Al-hakim ameandika hadithi na kuisahihisha, na Al-Baihaqi ndani ya Sunan yake kwa njia ya A'taa1 kutoka kwa ibn Abbas amesema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:"Isipokuwa kwa ajili ya kujilinda kutokana na shari zao" Kwamba: "At-Tuqah" yaani Taqiyyah ni kusema kwa ulimi na hali yakuwa moyo umetulizana (umethibiti) kwa imani: Taz: Sunanul-Baihaqi na Mustad-Rak Al-Hakim. Na amethibitisha Abdu bin Hamid kutoka kwa Al-Hasan amesema:"Taqiyyah inajuzu hadi siku ya Kiyama." Taz: Ad-Durrul-Manthoor cha Jalalud-Dinis-Suyuti Juz. 2 uk. 176.

Naye Abdur-Razzaq, ibn Saad, ibn Jabir, ibn Abi-hatim na ibn Mar-dawaih wamethibitisha na Al-Hakim amesahihisha ndani ya Mustadrak yake na Al-Baihaqi ndani ya Ad-Dalail amesema: "Washirikina walimuadhibu Ammar bin Yaasir hawakumwachia mpaka alipomtukana Mtume (s.a.w.) na akawataja Miungu yao kwa wema ndipo walipomuachia, alipofika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) Mtume akasema, kuna nini huko? Ammar akasema shari tupu, kwani sikuachiwa mpaka nilipokutukana na nikawataja miungu wao kwa wema, Mtume akasema, wauonaje moyo wako, Ammar akasema, umetulizana (umethibiti) kwa imani, Mtume akasema, basi wakirudia tena nawe rudia tena, basi hapo ikashuka (aya isemayo) "Isipokuwa yule aliyelazimishwa na hali moyo wake umetulizana kwa imani" (Qur'an, 16:106) Na amethibitisha ibn Saa'd kutoka kwa Muhammad bin Siriin kwamba Mtume (s.a.w.) alimkuta Ammar hali yakuwa analia, basi Mtume akawa anampangusa macho yake huku akisema "Wamekuadhibu makafiri wakakuzamisha ndani ya maji nawe ukasema kadha wakadha, basi iwapo watarudia tena waambie hivyo hivyo (ulivyowaambia kwanza). Taz: Atabaqatul-Kubra cha ibn Saad.


Na wamethibitisha ibn Jarir, ibn Mundhir, ibn Abi-Hatim na Al-Baihaqi ndani ya sunan yake kwa njia ya Ali kutoka kwa ibn Abbas kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu ..." Amesema: "Mwenyezi Mungu ameeleza kwamba, yeyote mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu baada ya kuwa amemuamini, basi mtu huyo ghadhabu toka kwa Mwenyezi Mungu zimshukie na atapata adhabu kali, ama yule mwenye kushurutishwa akasema kwa ulimi wake na moyo wake uko kinyume (cha hivyo) kwa kuwa na imani, (lakini akakufuru) kwa kujiokoa tokana na maadui zake, basi huyo hana makosa, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu huwaadhibu waja kwa yale waliyoamini mioyoni mwao". Taz: Sunan Al-Bayhaqi.


Na wamethibitisha mabwana ibn Abi Shaibah, ibn Jabir, Ibn Mundhir na ibn Abi Hatim kutoka kwa Mujahid amesema: "Aya hii ilishuka kwa watu wa Maka walioamini, basi baadhi ya Masahaba kutoka Madina wakawaandikia (wakasema), Hameni, hakika sisi hatuoni kwamba ninyi ni miongoni mwetu mpaka muhame mje kwetu, basi wakatoka kuelekea Madina, ghafla Maqurayshi wakawakamata njiani wakawatesa, wakakufuru hali ya kulazimishwa kufanya hivyo, basi kwa ajili yao ilishuka aya hii, "Isipokuwa yule aliyelazimishwa na hali moyo wake umethibiti kwa imani", Taz: Ad-Durrul-Manthoor cha Jalakud-Dinis-Suyuti Juz. 2uk 178. Naye Bukhar amethibitisha ndani ya sahih yake katika Babul-Mudaarati Maan-Nas, na ameeleza kutoka kwa Abud-Dar-dai amesema: "Hakika sisi tunaonyesha meno mbele ya nyuso za watu na hali yakuwa nyoyo zetu zinawalaani". Taz: Sahih Bukhar Juz. 7 uk. 102.


Naye Al-Halabi amethibitisha ndani ya Sira yake amesema: "Pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu alipoushinda mji wa Khaybar, Hajjaj bin Ala-t alimwambia Mtume, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi ninazo mali huko Maka na ninao jamaa huko, nami nataka kuwatembelea, basi je, ninayo ruhusa ikiwa nitakutukana na nikasema jambo fulani? Mtume wa Mwenyezi Mungu alimruhusu aseme alitakalo". Taz: As-Si'ratul-Halabiyyah Juz. 3 uk. 61. Na imekuja ndani ya Kitabu kiitwacho Ihyau-Ulum cha Imam Ghazali amesema: "Hakika kuhifadhika damu ya Muislamu ni jambo la wajibu basi wakati wowote itakapokuwa makusudio ya kumwaga damu ya Muislamu yamefichikana ndani ya dhalimu, kumwambia uongo ni wajibu." Taz: Ihyau Ulumid-Din cha Hujjatul-Islam Abu Hamid Al-Ghazali.


Na amethibitisha Jalalud-Din As-Suyuti ndani ya kitabu kiitwacho Al-Ash-Ba'hu Wan-Nadhair amesema: "Inaruhusiwa kula mzoga wakati wa njaa (hakuna chakula kingine) na kunywa funda la pombe na kutamka neno la kufru (wakati wa matatizo) na lau haramu itaenea katika sehemu fulani kiasi kwamba haipatikani halali katika sehemu isipokuwa kwa nadra, basi inaruhusiwa kutumia (haramu) kwa kiasi cha Haja". Na amethibitisha Abubakr Ar-Razi ndani ya kitabu chake Ahkamul-Qur-an katika kufasiri kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Illa Antat-Taqu Minhum Tuqatan" Yaani (isipokuwa kwa ajili ya kujilinda kutokana na shari zao) amesema ina maana kuwa mtakapochelea kuzidhuru nafsi au baadhi ya viungo basi mtajilinda kutokana nao kwa kudhihirisha kuwafuata bila ya kuyaamini hayo yao, na hii ndiyo bayana inayokubaliana na tamko hilo na ndiyo msimamo wa kongamano la wanachuoni, kama ilivyokuja kutoka kwa Qatada juu ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
"Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wandani wao (watawala) kinyume cha Mwenyezi Mungu". Amesema (Qatadah) haifai kwa Muumini kumfanya kafiri kuwa mtawala katika dini yake, na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo, "Isipokuwa kwa kujilinda na shari zao inapelekea ruhusa ya kudhihirisha kufru wakati wa Taqiyyah Taz: Ahkamul-Qur'an cha Ar-Razi Juz. 2 uk. 10,


Naye Bukhari amethibitisha ndani ya sahih yake kutoka kwa Qutaibah bin Said, kutoka kwa Sufiyan, kutoka kwa Al-Mukandar, amemsimulia toka Ur-Wah bin Zubair kwamba bibi Aisha alimueleza yakuwa, "Kuna mtu alibisha hodi nyumbani kwa Mtume (s.a.w.), Mtume akasema mkaribisheni, Oh! Mwana wa Al-Ashira ni muovu, au alisema ni muovu ndugu wa Al-Ashira. Alipoingia Mtume alizungumza naye kwa maneno laini, basi mimi nikasema (Yaani Aisha) Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu umesema uliyoyasema kisha umemfanyia upole katika mazungumzo? Mtume (s.a.w.) akasema: Ewe Aisha hakika watu wenye daraja ya shari kwa Mwenyezi Mungu ni mtu yule waliyemuacha watu au kumtelekeza ili kujilinda na uovu wake." Taz: Sahih Bukhari Juz. 7uk.81.

Na hii inatutosha kuwa ni dalili baada ya kuwa tumeonesha ndani ya maelezo yaliyotangulia ya kwamba masunni wanaamini kuwepo ruhusa ya Taqiyah mpaka kwenye mipaka yake ya mbali kwamba Taqiyah inaruhusiwa hadi siku ya qiyama kama maelezo yaliyopita hapo kabla, na kuwa ni wajibu kusema uongo kama alivyosema Ghazali, na kudhihirisha kufru nayo ni mwenendo na makubaliano ya wanachuoni, kama alivyolikubali jambo hilo Arrazi, na pia kujuzisha Tabasamu kwa dhahiri na kulaani kwa ndani, kama alivyokiri Bukhar. Na ruhusa ya mtu kusema atakavyo na kumtia dosari Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kuchelea mali yake kama alivyobainisha jambo hilo mwenye Sira tul-Halabiyyah, na mtu kusema mambo ambayo ndani yake ni maasi kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwachelea watu kama alivyokiri jambo hili Suyuti.


Basi hapana litalo halalisha kebehi ya Masunni na upinzani wao dhidi ya Mashia kwa ajili ya itikadi ambayo wao wenyewe wanaisema na kuisimulia ndani ya Sihahi zao na Musnad zao. (Vitabu vyao) ya kwamba itikadi hiyo (ya Taqiyyah) inaruhusiwa bali ni wajibu. Na Mashia hakuna chochote walichoongeza juu ya vile wasemavyo Masunni isipokuwa wao (Mashia) wametambulikana mno kuliko wengine katika matumizi ya Taqiyyah, kutokana na mateso, dhulma, na maudhi waliyoyapata toka kwa watawala wa Kibanu Ummayyah na Banu Abbas, kwani katika zama hizo ilikuwa inatosha kabisa kwa mtu kusema kwamba: "Huyu ni mfuasi wa Ahlul-Bayt" ili apambane na kifo chake na kuuliwa kwa mauaji mabaya akiwa mikononi mwa maadui wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.). Hivyo basi ilikuwa hapana budi kwa Mashia kuitumia Taqiyyah kwa kufuata maelekezo ya Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.). Imepokewa kutoka kwa Imam Jaafar As-Sadiq (a.s.) amesema:"Taqiyyah ni dini yangu na ni dini ya wazazi wangu" na amesema: "Asiyekuwa na Taqiyyah basi huyo hana dini".


Na bila shaka Taqiyyah ilikuwa ni kielelezo cha Maimamu wa Nyumba ya Mtume kwa kujikinga na madhara wao wenyewe na wafuasi wao na wawapendao pia kuhifadhi damu yao na kusuluhisha hali ya Waislamu waliofitiniwa katika dini yao kama alivyofitiniwa Ammar bin Yasir (r.a.) na wengine. Ama Masunni, wao walikuwa mbali na balaa hilo, kwani wao kwa kipindi kirefo walikuwa wakikubaliana na watawala, hivyo basi hawakusumbuliwa si kwa kuuawa wala kuporwa mali (zao) na dhulma (yoyote dhidi yao haikuwepo) basi moja kwa moja hali hiyo ikawafanya wawe wapinzani mno wa Taqiyyah na kuwakejeli wanaoitumia. Kwa hakika watawala wa Kibanu Umayyah na Kibanu Abbas walitoa mchango mkubwa kuwafanya Mashia watambulikane mno kuitumia Taqiyyah.


Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameteremsha Qur'an (ikazungumzia) Taqiyyah, (Qur'an ambayo) inasomwa na hukmu zinatekelezwa, na kwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) yeye mwenyewe aliitumia Taqiyah kama ilivyokudhihirikia ndani ya Sahih Bukhar. Kadhalika Mtume alimruhusu Ammar bin Yasir amtukane na akufuru iwapo makafiri watarudia tena kumuadhibu. Si hivyo tu bali wanachuoni wa Kiislamu wameruhusu jambo hilo kwa kufuata kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake, sasa basi ni kejeli gani na ni upinzani gani baada ya yote haya utakaokubalika kuelekezwa kwa Mashia? Bila shaka Masahaba watukufu walitumia Taqiyyah katika zama za watawala waovu mfano wa Muawiyah ambaye alikuwa akimuuwa kila aliyekataa kumlaani Ali bin Abi Talib, na kisa cha Hujri bin Adiyyi Al-Kindi na jamaa zake ni mashuhuri. Na mfano (watawala waovu) ni kama vile kina Yazid, ibn Ziyad na Abdul-Malik bin Marwan na wengine kama hao. Na lau ningetaka kukusanya ushahidi wa matendo ya Masahaba kuhusu Taqiyah, basi ingelazimu kitabu kamili, lakini ushahidi niliouleta miongoni mwa dalili za Masunni unatosha, shukrani zote ni zake Mwenyezi Mungu. Na sitaiacha fursa hii ipite ila niwasimulie kisa kizuri kilichonitokea mimi binafsi (nikiwa) pamoja na mwanachuoni mmoja miongoni mwa wanachuoni wa Kisunni ambaye tulikutana naye ndani ya ndege. Tulikuwa tumealikwa kuhudhuria mkutano wa Kiislamu huko Uingereza, na tukawa tunazungumza juu ya Ushia na Usunni kwa kipindi cha masaa mawili. Huyu mwanachuoni alikuwa miongoni mwa watu wanaolingania umoja (miongoni mwa Waislamu) na nilipendezwa naye, isipokuwa sikupendezwa na kauli yake aliposema kwamba: "Inabidi Mashia waziache baadhi ya itikadi ambazo zinasababisha Waislamu wahitilafiane na kukebehiana wao kwa wao."


Mimi nilimuuliza: "Kama itikadi gani"? Kwa haraka sana akajibu: "Kama vile Mut'a na Taqiyyah." Mimi nilijaribu kumkinaisha kwa uwezo wangu ya kwamba Mut'a ni ndoa ya kisheria na Taqiyyah ni ruhusa toka kwa Mwenyezi Mungu, lakini aliendelea na mtazamo wake na haikumkinaisha kauli yangu wala hoja zangu, akidai kwamba yote niliyoyaleta ni sahihi lakini inabidi kuyaacha kwa ajili ya Maslahi muhimu ambayo ni umoja wa Waislamu. Nilishangazwa sana na hekima hii inayoamuru kuacha hukumu za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya umoja wa Waislamu na nikamwambia kwa kumfurahisha tu ya kwamba: "Lau umoja wa Waislamu utasimama juu ya jambo hili basi nitakuwa wa mwanzo kuitikia".

Tulishuka uwanja wa ndege wa London, nami nilikuwa nikitembea nyuma yake, na pindi tulipowafikia askari wa uwanja wa ndege yeye aliulizwa sababu za yeye kuja Uingereza na akawajibu kwamba amekuja kwa ajili ya matibabu, nami nilidai kwamba nimekuja kuwatembelea jamaa zangu fulani. Basi tukapita kwa salama bila ya kucheleweshwa mpaka tukafika mahala pa kukaguliwa mizigo na hapo ndipo nilipomnong'oneza nikamwambia, "Waonaje, Taqiyyah ni jambo linalofaa katika nyakati zote"? Akasema, "Kwa vipi"? Nikamwambia "Hapana shaka sisi tumewadanganya askari hawa, mimi kwa mujibu wa kauli yangu nimesema kuwa nimekuja kuwatembelea jamaa zangu, nawe kwa mujibu wa kauli yako umesema kuwa umekuja kwa ajili ya matibabu, wakati ambapo sisi tumekuja kwa ajili ya mkutano".


Basi alitabasamu na akagundua kwamba amesema uongo mbele yangu hali ya kuwa ninamsikia, hivyo akasema: "Kwani katika mkutano wa Kiislamu si kuna matibabu ya nafsi zetu"? Mimi nilicheka huku nikisema: "Je, ndani ya mkutano huo si kuna kuwatembelea ndugu zetu"? Sasa ninarejea kwenye maudhui na ninasema kwamba, "Taqiyyah ilivyo, siyo kama wanavyodai Masunni kwamba eti ni namna fulani ya unafiki, bali kinyume chake ndiyo sahihi. Kwani unafiki ni kudhihirisha imani na kuficha ukafiri, wakati ambapo Taqiyyah ni kudhihirisha kufru na kuficha imani, na misimamo hii miwili iko mbali mbali kabisa. Msimamo huu yaani wa unafiki ni ule ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu ameusema (kama ifuatavyo):
"Na wanapokutana na wale walioamini husema tumeamini, na wanapokuwa faragha kwa mashetani wao husema sisi tuko pamoja nanyi, hakika sisi tunawacheza shere." Basi hii ndiyo imani kwa nje na ni kufru kwa ndani "Unafiki." Ama namna ya pili ya Taqiyyah ambayo Mwenyezi Mungu ameieleza (kama ifuatavyo): "Na akasema mtu mmoja muumini kutoka katika watu wa Firaun anayeficha imani yake." Hii ina maana ya kufru kwa nje na ni imani kwa ndani "Taqiyyah." Basi bila shaka muumini wa watu wa Firaun alikuwa akificha imani yake kwa ndani na hakuna aliyejua isipokuwa Mwenyezi Mungu na alikuwa akijidhihirisha kwa Firauni na watu wote kwamba yeye yuko kwenye msimamo wa dini ya Firaun. (Mwenyezi Mungu amemtaja ndani ya Kitabu choke kwa kuitukuza heshima yake). Ewe msomaji Mtukufu hebu twende pamoja ili upate kufahamu kauli ya Mashia juu ya Taqiyyah usije ukadanganyika na maneno ya uzushi na uongo yasemwayo juu ya Mashia.


Amesema Sheikh Muhammad Ridhaa Al-Mudhaffar ndani ya kitabu chake kiitwacho, "Aqaidul-Imamiyyah ". Ufuatao ndio usemi wake: "Taqiyyah inazo hukumu zake katika hali ya kuwa ni wajibu na kutokuwa wajibu kufuatana na tofauti ya mahala penye khofu ya madhara, (hukumu hizo) zimetajwa katika milango yake ndani ya vitabu vya wanachuoni wa Fiqh. Na Taqiyyah siyo wajibu katika kila hali, bali huenda ikajuzu au ikawajibika kinyume chake katika baadhi ya nyakati, kama vile itakapokuwa wakati wa kuidhihirisha haki na kuionesha kwa ajili ya kutetea dini na kuutumikia Uislamu na kuupigania katika njia yake, basi wakati huo mali hupuuzwa haipewi kima na wala nafsi hazipewi heshima (yaani haitoruhusiwa Taqiyyah ili kuokoa mali au kuokoa nafsi na dini iangamie). Na huenda Taqiyyah ikawa haramu katika matendo ambayo yanalazimisha kuua nafsi zinazo heshimika au (watu) kuzama katika batili au uovu ndani ya dini au madhara makubwa kwa Waislamu kwa kuwapotosha na kueneza dhulma na ujeuri miongoni mwao. Kwa vyovyote vile maana ya Taqiyyah kwa Shia siyo kuifanya Taqiyyah miongoni mwao kuwa ni Jumuiya ya siri kwa lengo la kuvunja na kuharibu - kama wanavyoidhania baadhi ya maadui zao wasio na upeo wa kufahamu mambo kwa mwelekeo wake na wala hawajilazimishi nafsi zao kufahamu mtazamo uliosahihi.


Kama ambavyo maana ya Taqiyyah siyo kuifanya dini na hukmu zake viwe ni mambo ya siri miongoni mwa siri ambazo haifai kuzitangaza kwa asiyefuata dini hiyo. Sasa basi inakuwaje (kudhaniwa vibaya) wakati Mashia wameandika ndani ya tunzi zao mambo yanayohusu Fiqhi, hukumu na uchambuzi wa maneno na itikadi zimejaa mashariki na magharibi na zimevuka mipaka inayotarajiwa na umma wowote unaofuata dini yake. Nawe msomaji bila shaka unaona ya kwamba, hakuna unafiki wala udanganyifu au uongo wala hadaa kama wanavyodai maadui wa Mashia.13
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

MUT'A (AU NDOA YA MUD A) Kinachokusudiwa ni ndoa ya Mut'a au ndoa ya muda au ndoa ya wakati maalum, na ndoa hii ni sawa na ndoa ya kudumu, kwani haisihi isipokuwa kwa mafungamano yanayokusanya Qabul na I'jab, kwa mfano mwanamke aseme, "Nimekuozesha nafsi yangu kwa mahari kiasi kadhaa," Basi na mwanamume aseme "Nimekubali." Na ndoa hii inazo sharti zake ambazo zimetajwa ndani ya vitabu vya Fiqhi kwa (Madhehebu ya) Imamiya kama vile kubainisha mahari na muda, basi huwa inasihi kwa kila kile ambacho pande mbili hizi zitaridhiana, na (sharti nyingine) ni kama vile uharamu wa kutamatui (kumuona) mwanamke ambaye ni haramu kisheria kumuoa, kama ilivyo katika ndoa ya daima. Na ni juu ya mwanamke aliyeolewa ndoa ya Mut'a kukaa eda baada ya kumalizika muda wa ndoa kwa hedhi mbili na atakaa eda miezi minne na siku kumi kama mumewe atafariki (kabla ya muda kwisha).


Na wawili hawa walioowana ndoa ya Mut'a hawarithiani wala hakuna (sharti ya wajibu wa) chakula (kwa mume kumlisha mke) na mke hamrithi mume wala mume hamrithi mke, na mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa ya Mut'a ni sawa na mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa ya daima kikamilifu kabisa, katika haki za urithi, chakula na haki zote za malezi, maadili ya kimwili na mafunzo, na ni mtoto wa baba huyo. Hii ndiyo ndoa ya Mut'a kwa sharti zake na mipaka yake nayo ni kama uionavyo, siyo miongoni mwa uzinzi kwa hali yoyote ile kama wanavyodai watu.

Na Masunni kama ilivyo kwa ndugu zao Mashia wanaafikiana kuhusu sheria ya ndoa hii kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyopo katika aya ya ishirini na nne ndani ya Suratun-Nisai pale Mwenyezi Mungu aliposema: "Wale mtakaostarehe nao (mtakao waoa Mut'a) miongoni mwao, wapeni mahari yao (ambayo) ni faradhi, wala si vibaya kwenu katika yale muliyoridhiana badala ya yale yaliyotajwa, bila shaka Mwenyezi Mungu ni mjuzi tena mwenye hekima." Ni kama ambavyo pia wameafikiana (Sunni na Shia) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliiruhusu ndoa ya Mut'a na Masahaba walioa (kwa ndoa hiyo) zama zake Mtume.


Isipokuwa wamehitilafiana (Sunni na Shia) kuhusu kufutwa kwa ndoa hiyo au kutokufutwa, kwani Masunni wanasema imefutwa na kwamba iliharamishwa baada ya kuwa ilikuwa ni halali, na kwamba kufutwa huko ilifutwa na Sunna na siyo Qur'an. Shia wao wanasema kuwa ndoa hiyo haikufutwa na kwamba ni halali mpaka siku ya kiyama. Kwa hiyo basi uchambuzi unafungamana tu na kuhusu kufutwa kwa ndoa hiyo au kutokufutwa, na kuzichunguza kauli za pande mbili ili iweze kumbainikia msomaji wazi wazi jambo hili na kwamba wapi ndiko kunakopatikana haki, basi aifuate bila ya chuki na upendeleo.

Ama kwa upande wa Mashia wasemao kwamba haikufutwa na ni halali mpaka siku ya kiyama, hoja yao ni kuwa: Haikuthibiti kwetu sisi kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu aliikataza ndoa hiyo, na Maimamu wetu kutoka katika kizazi kitukufu cha Mtume, wao wanasema kuwa ni halali. Na lau ingekuwa imefutwa na Mtume (s.a.w.), basi Maimamu wa nyumba ya Mtume wangelilijua jambo hilo wakiongozwa na Imam Ali, kwani watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) ndiyo wajuao mno yaliyomo ndani ya nyumba hiyo. Lakini kilichothibiti kwetu sisi ni kwamba Khalifa wa pili Umar bin Al-Khatab ndiye aliyeikataza ndoa hii na akaiharamisha kwa Ij-tihadi yake kama wanavyoshuhudia wanachuoni wa Kisunni wenyewe. Sisi hatuwezi kuacha hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa ajili ya (kufuata) maoni na Ij-tihadi ya Umar bin Al-Khatab.

Basi huu ni muhtasari wa yale wayasemayo Mashia juu ya uhalali wa Mut'a nayo ndiyo kauli ya sawa na ni mtazamo bora. Waislamu wote wanatakiwa wafuate hukmu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wampinge asiyekuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake hata kama anacheo gani pindi Ij-tihadi yake itapokwenda kinyume cha Qur'an na Sunna. Ama Masunni wao wanasema kwamba, Mut'a ilikuwa halali na Qur'an ilishuka kuhusu Mut'a na Mtume aliiruhusu na masahaba wakaifanya, kisha baada ya hapo ilifutwa, na wanatofautiana juu ya kilichoifuta. Wapo miongoni mwao wanasema kwamba, "Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliizuwia kabla ya kufa kwake, na wengine wanasema kwamba Umar bin Al-Khatab, ndiye aliyeiharamisha, na kauli yake (Umar) kwetu sisi (Masunni) ni hoja (yenye nguvu) kufuatia kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema: "Shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za Makhalifa wangu viongozi baada yangu zishikeni kwa nguvu.


Ama wale wasemao kuwa Mut'a ni haramu kwa kuwa Umar bin Al-Khatab aliiharamisha na kwamba kitendo cha Umar ni sunna ya lazima (kufuatwa). Basi watu hawa sisi hatuna maneno nao wala hatuna uchambuzi wowote, kwani (mtazamo wao huo) ni wa kung'ang'ania na kujikusuru. Itakuwaje Mwislamu aache kauli ya Mwenyezi Mungu na kauli ya Mtume na awapinge kisha afuate kauli ya mtu mwenye kujitahidi, anayekosea na kupatia, na hali hii ya kujitahidi kwake juu ya mas-ala fulani (inaweza kuchunguzwa) iwapo ndani ya Qur'an na sunna hakuna tamko (linalohusu ufumbuzi wa mas-ala hayo) ama kama tamko litakuwepo basi, "Haifai kwa Muumini mwanamume na Muumini mwanamke pindi Mwenyezi Mungu na Mtume wake watakapoamua jambo wawe na hiyari katika jambo lao (hilo lililoamriwa) na yeyote atakayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake bila shaka amepotea upotevu ulio wazi". (Qur'an, 33:36)

Na yeyote asiyekubaliana nami juu ya kanuni hii basi ni juu yake kuyarejea maarifa yake na ufahamu wake kuhusu (muongozo) na sheria ya Kiislamu na aisome Qur'an Tukufu na Sunna ya Mtume kwani Qur'an yenyewe binafsi imeeleza katika aya iliyotajwa hapo juu, na aya zingine mfano wa hiyo ni nyingi mno zinafahamisha juu ya kukufuru na kupotea kwa mtu yeyote asiyeshikamana na Qur'an na Sunna ya Mtume (s.a.w.). Ama kwa upande wa dalili ya Sunna tukufu ya Mtume ziko dalili nyingi vile vile, lakini tunatosheka na kauli moja ya Mtume (s.a.w.) isemayo: "Halali iliyo halalishwa na Muhammad ni halali mpaka siku ya Kiyama, na haramu iliyoharamishwa na Muhammad ni haramu mpaka siku ya kiyama. Hivyo basi hana haki mtu yeyote kuhalalisha au kuharamisha katika mas-ala ambayo ndani yake yamethibiti maandiko na ni hukumu kutoka kwa Mwenyezi Mungu au kwa Mtume wake (s.a.w.).


Na kwa yote haya tunawaambia hao wanaotaka kutukinaisha kwamba vitendo vya Makhulafaur-Rashiduna na Ij-Tihadi zao vinatulazimu, sisi tunasema: "Hivi mnajadiliana nasi juu ya jambo la Mwenyezi Mungu ambaye ni Mola wetu na ni Mola wenu, na sisi tuna matendo yetu nanyi mnayo matendo yenu, nasi kwake Mwenyezi Mungu tunajitakasa" (Qur'an, 2:139) Wanaozungumzia dalili hii (bila shaka) wanakubaliana na Mashia kwenye madai ya (kuwa Mtume hakuiharamisha Mut'a) na wanakuwa ni hoja dhidi ya ndugu zao Masunni (wasemao kuwa Mtume aliiharamisha). Hivyo basi uchunguzi wetu tunaufungamanisha tu na kundi lisemalo kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ndiye aliyeiharamisha na akaifuta (aya ya) Qur'an kwa hadithi.

Watu wasemao hivi wanajikanganya wenyewe katika kauli zao na hoja zao zi tupu hazina msingi imara, japokuwa imepokewa kwa Muslim ndani ya sahih yake kuhusu katazo (hilo linalodaiwa), kwani lau kungekuwa na katazo litokalo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), basi katazo hilo lisingefichikana kwa masahaba ambao walioa Mut'a katika zama za Ukhalifa wa Abubakar na sehemu fulani ya Ukhalifa wa Umar kama alivyosimulia jambo hilo Muslim ndani ya sahih yake. Taz: Sahih Muslim Juz. 4 uk. 158. Amesema A'ta', "Jaabir bin Abdillah alikuja hali ya kuwa anafanya Umra nasi tukamfuata nyumbani kwake, watu wakamuuliza mambo mengi, hatimaye wakamuuliza juu ya Mut'a akasema ndio tuliowa zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) na zama za Abubakar na Umar".

Basi lau Mtume wa Mwenyezi Mungu angekuwa ameikataza Mut'a, isingejuzu kwa Masahaba kufanya Mut'a katika zama za Abubakar na Umar kama ulivyosikia. Ukweli uliopo ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) hakukataza Mut'a wala hakuiharamisha, bali katazo lilitokana na Umar bin Khatab kama yalivyokuja maelezo ya jambo hilo ndani ya Sahih Bukhar. Imepokewa toka kwa Musaddad, ametusimulia Yahya kutoka kwa Imran Abu Bakr, ametusimulia Aburajaa kutoka kwa Imran bin Huswain (r.a.) amesema: "Aya ya Mut'a ilishuka ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi tukaitenda wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na haikushuka Qur'an kuiharamisha na wala Mtume hakukataza mpaka alipokufa Mtume, basi mtu fulani kwa maoni yake akasema aliyoyataka, Muhammad akasema, inasemekana mtu huyo ni Umar". Taz: Sahih Bukhar Juz. 5 uk. 158.


Ewe Msomaji unaona ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) hakuikataza Mut'a mpaka kufa kwake kama alivyobainisha Sahaba huyu. Na unamuona anaunasibisha huu uharamishaji kwa Umar wazi wazi bila ya kificho na anaongeza kuwa yeye Umar alisema ayatakayo kwa maoni yake. Huyu hapa Jabir bin Abdillah Al-Ansari anasema wazi wazi kama ifuatavyo:"Tulikuwa tunaoa Mut'a kwa gao la tende na unga kwa siku kadhaa, katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) na (zama za) Abubakar mpaka Umar alipokataza kutokana na suala la A'mri bin Hurayth. Taz: Sahih Muslim Juz. 4 uk. 131. Na miongoni mwa mambo yanayotujulisha kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa na mtazamo kama wa Umar jambo ambalo si geni ni kuwa, imetangulia katika uchambuzi wetu kuhusu msiba wa siku ya Al-Khamis ya kwamba baadhi ya Masahaba walimuunga mkono Umar katika kauli yake aliposema kuwa "Mtume wa Mwenyezi Mungu anaweweseka kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu'!! Kwa hiyo ikiwa walimtia nguvu kwenye jambo la hatari kama hili ambalo alimtuhumu Mtume (s.a.w.) basi ni kwa nini wasikubaliane naye katika baadhi ya Ij-tihadi zake?

Hebu na tuisikilize kauli ya mmoja wao (hao Masahaba wanaomuunga mkono Umar): "Nilikuwa kwa Jabir bin Abdillah, mara alimjia mtu fulani akamwambia: ibn Abbas na ibn Zubair wanahitilafiana kuhusu Mut'a mbili (Mut'a ya ndoa na Mut'a ya Hija) basi Jabir akasema zote mbili tulizifanya zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kisha akatukataza Umar basi hatukurejea tena (kuzifanya). Taz: Sahih Muslim Juz. 4 uk. 131. Kwa ajili hiyo mimi binafsi naamini kabisa kwamba kuna baadhi ya Masahaba walilihusisha kwa Mtume katazo la kuharamishwa kwa Mut'a ili kuutakasa msimamo wa Umar na (kuupitisha) kuwa ni sahihi. Kinyume chake ni kuwa haiwezekani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kuharamisha kilichohalalishwa na Qur'an, kwani sisi hatukuti hata hukmu moja katika hukmu zote za Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu ameihalalisha kisha Mtume akaiharamisha, na hapana yeyote asemaye hivyo isipokuwa ni mpinzani mwenye chuki.


Na lau tutakubali ili kupata jinsi ya kujadili ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliikataza Mut'a, basi Imam Ali bin Abi Talib ambaye ni mtu wa karibu mno kwa Mtume na mjuzi mno kuliko watu wengine asingesema kama ifuatavyo: "Bila shaka Mut'a ni rehma, Mwenyezi Mungu amewahurumia kwayo waja wake, na lau siyo Umar kuikataza, basi asingezini isipokuwa mtu duni". Taz: Ath-Tha'alabi ndani ya tafsirul-Kabir, na Tabari alipoifasiri aya ya Mut'a ndani ya tafsiri yake iitwayo Alk-Kabir. Na hii ni kwa kuwa Umar mwenyewe hakuunasibisha kwa Mtume uharamishaji wa Mut'a bali amesema wazi wazi katika kauli yake ifuatayo: "Mut'a mbili zilikuweko zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu, nami ninazikataza na nitatoa adhabu dhidi ya mwenye kuzitenda, Mut'a ya Hija na Mut'a ya wanawake." Taz: At-Tafsirul-Kabir ya Al-Fakhrur-Razi alipokuwa akifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu "Famastamtaatum Bihi Minhunna." Na hii hapa Musnad ya Imam Ahmad bin Hanbal ambayo ni shahidi mzuri juu ya kwamba Masunni wanahitilafiana mno katika mas-ala haya, wako miongoni mwao wanaihalalisha Mut'a na wako miongoni mwao wanaofuata kauli ya Umar bin Al-Khatab wanaiharamisha.


Imam Ahmad amethibitisha kama ifuatavyo: Imepokewa toka kwa ibn Abbas amesema: "Mtume (s.a.w.) alifanya "Tamattui" (Mut'a) 'Ur-wa ibn Zubair akasema, Abubakar na Umar walikataza Mut'a, basi ibn Abbas akasema: Kinasemaje hiki Kiur-wah akasema: anasema, Abubakr na Umar walikataza Mut'a, ibn Abbas akasema: Nawaona watu hawa wataangamia, nasema kasema Mtume nao wanasema kakataza Abubakr na Umar". Taz: Musnad lmam Ahmad bin Hanbal Juz. 1 uk. 337. Na imekuja ndani ya Sahih Tirmidhi kwamba Abdalla bin Umar aliulizwa kuhusu Mut'a ya Hija akasema:"Ni halali" basi yule muulizaji akamwambia,"Hakika baba yako aliikataza", akasema Ibn Umar:"Waonaje ikiwa baba yangu aliikataza na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliifanya,basije nifuate amri ya baba yangu au amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Yule mtu akasema,"Bali (ufuate) amri ya Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.)."

Taz: Sahih Tirmidhi Juz. 1 uk. 157. Masunni wamemtii Umar juu ya (kuharamisha) Mut'a ya wanawake na wamempinga kuhusu Mut'a ya Hija. Pamoja na kuwa katazo lake (alilitoa) akiwa mahala pamoja kama tulivyotanguliza kueleza. Jambo la maana katika yote haya ni kuwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) na wafuasi wao wamempinga (Umar) na wakasema kuwa Mut'a zote mbili ni halali mpaka siku ya Kiyama. Na kuna wanachuoni wa Kisunni ambao wamewafuata (Mashia) katika jambo hilo na ninamtaja miongoni mwao mwanachuoni Mtukufu wa Tunis ambaye ni kiongozi wa chuo kikuu cha "Az-Zaytuni" Mtukufu Sheikh Ta'hir bin A'shur (Mwenyezi Mungu amrehemu) yeye amesema ndani ya tafsiri yake mashuhuri kuwa Mut'a ni halali pale alipoitaja aya ya "Famastamtaatum Bihi Minhunna Faa'tuhunna-Ujurahunna Faridhah." Taz: At-Tahrir Wat-tan-wir cha Ta-hir A'shur Juz. 3 uk. 5.

Basi namna hii wanachuoni wanatakiwa wawe huru katika itikadi zao wasiathiriwe na upendeleo wala ujamaa na wala wasiogope kulaumiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Baada ya uchambuzi huu mfupi hakuna hoja wala chenye kuwatakasa Masunni kutokana na kebehi na tuhuma yao dhidi ya Shia kuhusu kuhalalisha kwao ndoa ya Mut'a zaidi ya dalili madhubuti na hoja bora walizonazo Shia. Muislamu anawajibika kuiangalia kwa makini kauli ya Imam Ali (a.s.) ya kwamba:"Mut'a ni Rehma, Mwenyezi Mungu amewahurumia kwayo waja wake" Na kwa hali halisi basi, ni ukubwa ulioje wa rehma ambayo inazima moto wa matamanio yenye nguvu yanayomfunika mtu awe mwanamume au mwanamke, (mpaka) akawa kama mnyama mwenye kushambulia. Ni wajibu kwa Waislamu wote na hasa vijana, wafahamu ya kwamba Mwenyezi Mungu amewajibisha kwa mzinifu adhabu ya kuuawa kwa kupigwa mawe kwa wale wenye kuhifadhika wanaume na wanawake basi hawezi Mwenyezi Mungu kuwaacha waja wake bila huruma wakati yeye ndiye muumba wao na ndiye muumba wa maumbile yao na anafahamu kitakachowarekebisha. Iwapo Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu amewahurumia waja wake kwa kuwaruhusu kufanya Mut'a basi hakuna atakayezini baada ya ruhusa hiyo isipokuwa mtu muovu mno. (Mfano wa hili) ni kama mwizi kukatwa mkono kwani kama kutakuwa na Baytul-Mal (Bank) kwa ajili ya kusaidiwa wenye dhiki na shida basi hakuna atakayeiba isipokuwa mtu muovu.


KAULI INAYOHUSU TAHRIFUL-QUR'AN Kauli hii kwa maana yake halisi ni mbaya sana ambayo Muislamu yeyote aliyeuamini utume wa Muhammad (s.a.w.) hawezi kuivumilia, sawa sawa akiwa ni Shia au Sunni. Hiyo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amebeba jukumu la kuilinda pale aliposema: "Hakika sisi ndiyo tulioiteremsha Qur'an na bila shaka ni sisi ndiyo tutakao ilinda." Hivyo basi haiwezekani kwa yeyote kuipunguza au kuongeza herufi moja, na hii Qur'an ndiyo muujiza wa milele wa Mtume wetu (s.a.w.) ambao hauwezi kujiwa na batili hapo kabla au hapo baadaye. Na ukweli halisi ulivyo kimatendo kwa Waislamu ni kuwa wanapinga Tahrifu ya Qur'an, kwani Masahaba wengi walikuwa wakiihifadhi kwa moyo, na walikuwa wakishindana kuihifadhi na kuihifadhisha kwa watoto wao kwa muda wote mpaka leo, hivyo haiwezekani kwa mtu fulani au kikundi fulani wala dola fulani kuigeuza au kuibadilisha.


Na lau tutaitembelea miji ya Kiislamu Mashariki na Magharibi, Kaskazini na Kusini na kila sehemu ya dunia, basi tutaikuta Qur'an ni ile ile bila ya ziyada wala upungufu, japokuwa Waislamu wametofautiana kwenye Madhehebu na vikundi na mila na mienendo. Basi Qur'an ni msukumo pekee unaowakusanya wala hawatofautiani watu wawili kuhusu Qur'an katika umma (wa Kiislamu), isipokuwa maelezo ya tafsiri, kila kikundi hufurahia yale waliyo nayo. Na yale yanayonasibishwa kwa Mashia kusema kuwa wanaipotosha Qur'an ni wazi kabisa kwamba ni tuhuma na kebehi na wala jambo hilo haliko kabisa katika itikadi za Kishia. Na endapo tutazisoma akida za Kishia ndani ya Qur'an, basi tutakuta kauli yao ya pamoja ni kukitakasa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kutokana na kila aina ya upotoshaji.


Anasema mwenye kitabu kiitwacho "Aqaidul-Imamiyyah Sheikh Muzaffar" "Sisi tunaitakidi kwamba Qur'an ni. ufunuo wa Mwenyezi Mungu, ulioteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ulimi wa Nabii wake Mtukufu, ndani yake (Qur'an) muna ubainisho wa kila kitu, nayo ni muujiza wa kudumu ambao watu wameshindwa kuukurubia katika balagha, ufasaha na katika mambo iliyoyakusanya miongoni mwa ukweli na maarifa ya hali ya juu. Haizukiwi na mabadiliko wala mageuzi wala upotovu, na hii Qur'an tuliyonayo mikononi mwetu tunayoisoma ndiyo ile ile Qur'an iliyoteremshwa kwa Nabii, na yeyote atakayedai kinyume cha hivyo, basi mtu huyo ni mzushi au mpotoshaji au amechanganyikiwa, na wote hao hawako katika uongofu, kwani Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo hayajiwi na ubatilifu hapo baadaye wala kabla yake. Na baada ya haya, miji yote ya Kishia inafahamika, na hukmu zao ndani ya fiqhi zinaeleweka kwa watu wote, basi lau wangekuwa na Qur'an nyingine isiyokuwa hii tuliyonayo, watu wangeliitambua.


Mimi ninakumbuka wakati nilipotembelea miji ya Kishia kwa mara ya kwanza, ndani ya mawazo yangu kulikuwa na baadhi ya habari hizi, basi nilikuwa kila nionapo kitabu kikubwa hukichunguza ili huenda nikaigundua hii Qur'an inayodaiwa (kuwa ipo), lakini mawazo haya yaliondolewa kwa haraka sana, na nilifahamu hapo baadaye kuwa hiyo ni moja ya kebehi za uongo zenye lengo la kuwafanya watu wawakimbie Mashia, lakini siku zote kumebakia watu wanaowakebehi Mashia na kutoa hoja dhidi yao kwa kitabu kiitwacho; "Faslul-Khitab Fi Ithbat Tahrifi Kitabi Rabbi'l Ar-Bab" ambacho mtunzi wake ni Muhammad Taqiyyun-Nuri At-Tabrasi aliyefariki mwaka 1320 Hijriyyah naye ni Shia, na hawa wenye kuwashinikiza Mashia wanataka kuwabebesha Mashia jukumu la kitabu hiki, na jambo hili ni kinyume cha uadilifu. Basi kwani vitabu vingapi vimeandikwa ambavyo ukweli havielezi isipokuwa maoni ya mwandishi wake, na ndani yake kuna mambo machafu na mengine yenye hekima, na kuna haki na batili na humo ndani kuna makosa na mengine ya sawa na yote hayo tunayakuta kwa kila vikundi vya Kiislamu, na wala siyo kwa Mashia peke yao na wengine ikawa hakuna hali hiyo. Basi je, inajuzu kwetu sisi kuwabebesha Masunni jukumu la yale yaliyoandikwa na waziri wa utamaduni wa Misri na mkuu wa Elimu ya Kiarabu Doctor Taha Husain kuhusu Qur'an na Mashairi ya zama za Jahiliyah?


Au yale aliyoyasimulia Bukhari, kitabu ambacho ni sahihi kwao Masunni, (yasemayo) kuwa Qur'an ina upungufu na ina ziyada, pia (namna hiyo hiyo) ndani ya Sahih Muslim na vinginevyo.[93] Hebu tutupiliye mbali hayo na tuukabili uovu kwa wema, na bora ya kauli kuhusu maudhui hii ni ile iliyoisemwa na Al-Ustadh Muhammad Al-Madini Mkuu wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Az-har pale alipoandika akasema: Amma (kusema) kwamba Mashia Imamiyyah wanaitakidi kuwa Qur'an imepungua, (sisi) tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu (kutokana na kauli hiyo) bali hizo ni riwaya tu zilizosimuliwa ndani ya vitabu vyao, kama ambavyo kuna riwaya kama hizo zilizosimuliwa ndani ya vitabu vyetu, na wanachuoni wenye kuhakiki kutoka pande hizi mbili (Shia na Sunni) wamezipinga riwaya hizo na wakabainisha upotovu wake, na hapana Shia Imamiyyah au Zaidiyyah anayeitakidi hivyo, kama ambavyo hapana Sunni anayeitakidi hivyo.


Mwenye kutaka anaweza kurejea kwenye kitabu kama "Kitabul-It'qan" cha Suyuti ili apate kuona mfano wa riwaya kama hizi tunazozitupilia mbali. Na kuna Mmisri mmoja katika mwaka wa 1498 alitunga kitabu kiitwacho "Al-Fur-Qan ambacho alikijaza riwaya nyingi kama hizi mbovu zilizoingizwa (tu) na zinapingwa, (lakini) alizinakili kutoka kwenye vitabu na rejea za Kisunni, chuo cha Az-har kiliitaka serikali ya Misri kukipiga marufuku kitabu hiki baada ya kuwa kimebainisha dalili na uchambuzi wa kielimu namna ya upotovu na uovu uliyomo. Serikali ya Misri ilikubali ombi hili na ikakipiga marufuku kitabu hicho, lakini mwandishi wa kitabu hicho alipeleka madai ya kutaka fidia, na kikao cha serikali katika idara ya mahakama kiliyatupilia mbali madai hayo.

(Sasa basi, kutokana na hali kama hii). Je, itasemwa kwamba Masunni wanapinga utakasifu wa Qur'an? Au wanaamini kuwa imepungua kwa sababu tu ya riwaya zilizosimuliwa na fulani? Au kwa sababu tu ya kitabu kilichotungwa na fulani? Basi hali ni hiyo hiyo kwa Mashia Imamiyyah, kuna riwaya ndani ya baadhi ya vitabu vyao kama riwaya zilizomo ndani ya vitabu vyetu. Kuhusu jambo hili Al-Imam Al-Allamah Said Abul-Fadhli bin Al-Hasan At-Tabrasi ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wakubwa wa Kishia katika karne ya sita Hijiriyyah anasema ndani ya kitabu kiitwacho, "Maj-Maul-Bay an Lil-U'lumil-Qur'an""A.m.a kuweko na nyongeza ndani ya Qur'an jambo hili limewafikiwa kuwa ni wazo batili na ama wazo la kuwepo upungufu katika Qur'an limeelezwa na jamaa katika Mashia wenzetu na baadhi ya Masunni kuwa mabadiliko na upungufu upo. Na wazo sahihi kwa mtazamo wa watu wetu ni kinyume na wazo la kuwepo badiliko au upungufu, nalo ndilo alilolinusuru Murtaza Mwenyezi Mungu aitakase roho yake. Usemi wake ulikuwa wa kutosheleza katika majibu ya MASA-ILU-TARABLOSIAT.

Ametaja katika sehemu kadhaa kuwa: Kujuwa kuwa nakala ya Qur'an nakala ni sahihi ni sawa na kujuwa kuwa kuna nchi, matukio makubwa, majanga ya kutisha, vitabu mashuhuri, na mashairi ya Kiarabu,na hiyo ni kwa sababu uangalizi ulikuwa makini, na sababu za kuinakili na kuihifadhi (Qur'an) zilikamilika, zilifikia kiwango cha juu mno yote hayo ni kwa sababu Qur'an ni muujiza wa Mtume na ndiyo chimbuko la elimu za kisheria na hukumu za kidini. Wanachuoni wa Kiislamu pia walifikia kiwango cha juu kabisa katika kuihifadhi na kuilinda, walifikia hata kujuwa kila kitu wametofautiana katika Qur'an kama Irabu yake, usomaji wake, herufi zake, na aya zake. Hivyo basi pamoja na uangalifu wa yakini na udhibiti kama huu yawezekana vipi iwe imebadilishwa au kupunguzwa?

Taz: Maqala ya Al-Ustadh Muhammad Al-Madini Mkuu Kituo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Az-har (iliyoandikwa katika) jarida liitwalo Risalatul-Islam toleo la nne katika mwaka wa kumi na moja uk. 382 na383. Na ili ikubainikie wazi ewe msomaji kwamba tuhuma hii (ya kupunguka kwa Qur'an au kuzidi) kuwa iko karibu mno na Masunni kuliko Mashia, ni kwamba miongoni mwa mambo yaliyonifanya nizirejee(upya) itikadi zangu zote ni kila nilipokuwa nikijaribu kuwakosoa Mashia katika jambo lolote lile na kuwapinga, wao walithibitisha kutohusika nalo na wakiliambatanisha kwangu (kama Sunni kabla kuwa Shia) na ndipo nilipofahamu kwamba wao siku zote wanazungumza kweli na kwa njia ya kufanya uchambuzi namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba nimekinaika.


Na hapa basi nakuletea yatakayothibitisha jambo hilo katika maudhui hii: Wamethibitisha Mabwana Tabrani na Baihaqi ya kwamba, Hakika ndani ya Qur'an muna sura mbili, moja wapo ni: Bismillahir-Rahmanir-Rahim Innaa Nastainuka Wanastaghfiruka Wanuthnii A'laykal-Khaira kullahu Wala nakfuruka Wanakhlau' wanatruku Man Yajjuruka ". Maana Yake: "Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu, Hakika sisi tunakuomba msaada na tunakuomba msamaha na tunakusifu kwa mema yote na wala hatukukatai na tunajiepusha na kumuacha yule anayekufanyia maovu." Na Sura ya pili ni: Bismillahir-Rahmanir-Rahim Allahumma Iyyaka Naabudu Walaka Nusalli Wanasjudu Wailaika Nas-a' Wanahfad, Nar-ju Rahmataka Wanakhsha Adha-Bakal-Jadda Inna Adha-baka Bil-Kafirina Mul-Haq." Maana Yake: Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu, Ewe Mwenyezi Mungu peke yako tu tunakuabudu na tunasali na kusujudu kwa ajili yako na kwako wewe tunatumika, tunataraji rehma zako na tunaiogopa adhabu yako kali, hakika adhabu yako itawapata makafiri".

Sura hizi mbili Ar-Raghibu ndani ya Muhadharat ameziita kuwa ni Sura za Qunut nazo ni miongoni mwa zile ambazo Sayyidina Umar bin Al-Khatab alikuwa akiqunuti kwazo, zinapatikana ndani ya Mus-hafu wa ibn Abbas na Mus-hafu wa Zaid bin Thabit. Taz: Al-It-Qan cha Jalal-ud-Dinis-Suyuti pia ndani ya Ad-Durrul-Manthoor. Imam Ahmad bin Hanbal amethibitisha ndani ya Musnad yake kama ifuatavyo:- "Imepokewa toka kwa Ubayyi bin Kaab amesema:"Ni aya ngapi mzisomazo ndani ya Suratul-Ahzab? akasema:Aya sabini na kidogo hivi, akasema:Hakika mimi niliisoma pamoja na Mtume (s.a.w.) mfano wa sura Al-Baqarah au zaidi kuliko hiyo na hakika ndani yake imo aya ya Rajmi". Taz: Musnad Imam Ahmad bin HanbalJuz. 5 uk. 132. Ewe msomaji mwenye akili hebu ziangalie hizi sura mbili zilizotajwa ndani ya Al-It-Qan na Ad-Durrul-Manthoor ambavyo ni vitabu vya Suyuti, pia zimethibitishwa na Tabran na Baihaqi na zinaitwa kuwa ni sura za Qunut wakati hazimo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.


Hii ina maana kwamba Qur'an tuliyonayo mikononi mwetu inapungua kwa sura mbili hizi zilizomo ndani ya Msa-hafu wa ibn Abbas na Msa-hafu wa Zaid bin Thabit kama ambavyo pia inajulisha kuwa kuna Misahafu mingine isiyokuwa hii tuliyonayo. Hali hii inanikumbusha ile tuhuma dhidi ya Shia kwamba wanao Msa-hafu wa Fatmah, basi yajuwe haya. Na (inajulisha) kwamba Masunni huzisoma sura hizi katika dua ya Qunut kila asubuhi, nami binafsi nilikuwa nimezihifadhi na kuzisoma katika Qunut ya sala ya alfajiri (nilipokuwa sunni). Ama riwaya ya pili ambayo ameithibitisha Imam Ahmad ndani ya Musnad yake, ni riwaya inayosema kuwa, Suratul-Ahzab imepungua robo tatu nzima, kwani Suratul-Baqarah ina aya 286 wakati ambapo Suratul-Ahzab haizidi aya 73 na tukizingatia hesabu ya Qur'an kwa hizbu, basi bila shaka Suratul-Baqarah ina hizbu tano wakati Suratul-Ahzab ina hizbu moja. Na kauli ya Ubayyi bin Kaa'b aliposema: "Nilikuwa nikiisoma pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu kama ilivyo Suratul-Baqarah au zaidi" wakati ambapo ni miongoni mwa wasomaji mashuhuri waliokuwa wakihifadhi Qur'an katika zama za Mtume (s.a.w.) na huyo ndiye aliyechaguliwa na Umar[94] kuwasalisha watu sala ya Tarawehe, basi kauli yake hii inazusha mashaka na wasi wasi kama inavyoonekana wazi.

Na amethibitisha Imam Ahmad bin Hambal ndani ya Musnad yake[95] mapokezi toka kwa Ubayyi bin Kaab amesema: "Hakika Mjumbe wake alisema, Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniamuru nikusomee Qur'an akasoma: "Lam Yakunil-ladhiina Kafaruu min ahlil-Kitabi", ndani yoke akasoma; "Walau anna ibn Adama Saala Wa-diyan min malin Faa A'taytuhu Lasaala Thaaniyan Falau Saala Thaniyan Faataytuhu Lasaala Thalithan, Wala-Yamlau Jaufa ibn Adama Illat-Turabu Wayatubullahu ala Man Taaba, Wainna dhalikad-Dinul-Qayyimu Indallahil-Hanafiyyah Gharyul-Mushrikah Walal-Yahudiyah Walan-Nasraniyyah Woman Yaf-alu Khayran Falan Yukfarah." Na amethibitisha Al-Hafidh ibn Asakir alipokuwa akitoa Tarjuma ya Ubayyi bin Kaab ya kwamba Abud-Dar-Dai alikwenda Madina akiwa pamoja na jamaa fulani miongoni mwa watu wa Dimishq, akamsomea Omar bin Khatab huko Madina aya hii: "Idh'jaalal-Ladhiina Kafaru Fi Qulubihim Al-Hamiyata Hamiyatal-Jaahiliya Walau Hamaitum kama hamau La Fasadal-Masjidul-Haram."


Umar bin Khatab akasema:"Nani alikusomesheni kisomo hiki"? Wakasema, "Ubayyi bin Kaab" akamwita, na akawaambia "Someni (mlivyosoma)" wakasoma:"Walau hamaltum kama hamau lafasadal-Masjidul-haraam " Ubayyi bin Kaab akamwambia Umar bin Khatab "Ndiyo, ni mimi niliyewasomesha (hivyo)" Umar akamwambia Zaid bin Thabit "Soma ewe Zaid" Zaid akasoma kama wasomavyo watu wote, basi Umar akasema, "Sifahamu kisomo kingine isipokuwa hiki"! Ubayyi bin Kaab akasema: "Ewe Umar namuapa Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika wewe unafahamu kwamba mimi nilikuwa nikihudhuria (mbele ya Mtume) na wao hawahudhurii na nikikurubia (kwa Mtume) wao hujificha, na namuapa Mwenyezi Mungu lau utapenda (nisisome hivi nisomavyo) basi nitabakia nyumbani mwangu wala sitamsomea yeyote mpaka nife" Umar akasema, Samahani, bila shaka wewe unafahamu kwamba, Mwenyezi Mungu amekujaalia elimu, basi wasomeshe watu kile ukijuacho".


Amesema:(Kuna siku) Umar alipita kwa kijana fulani akiwa anasoma ndani ya msahafu kama ifuatavyo: "Annabiyyu aula Bil-Muuminina Mina anfusihim Wa'az-Wajuhu Ummahatuhum Wahuwa Abun-lahum". Umar akasema:"Ewe kijana (imekuwaje) hebu eleza", yule kijana akasema:"Huu ni msahafu wa Ubayyi bin Kaab" Basi Umar akaenda akamuuliza Ubayyi naye akamwambia: "Bila shaka mimi ilikuwa ikinishughulisha Qur'an nawe ulikuwa ukishughulishwa na biashara sokoni." Taz: Tarikh Dimishq ya Al-Hafidh ibn Asakir Juz. 2 uk. 228. Nao ibn Al-Athir ndani ya Jamiul-Usul na Abu Dawud ndani ya Sunan yake na Al-Hakim ndani ya Mustadrak yake wamesimulia mfano wa riwaya kama hii (iliyotangulia).

Mara hii nakuachia ewe ndugu msomaji ufafanue mwenyewe riwaya kama hizi zilizojaa ndani ya vitabu vya Kisunni, hali yakuwa wao hawana habari nazo (kwamba zimo vitabuni mwao) na wanawatuhumu Mashia ambao kwao haipatikani kiasi kama hiki. Lakini huenda baadhi ya watu wakorofi miongoni mwa Masunni wakazikwepa riwaya kama hizi na kuzikataa kama ilivyo kawaida yao. Si hivyo tu bali watampinga Imam Ahmad kwa kuandika uzushi kama huu na Sanad zake kuwa ni dhaifu. Isitoshe wataiona Musnad ya Imam Ahmad bin Hanbal na Sunan ya Abi Dawud kwao Masunni kwamba hazina kiwango cha usahihi kama ule wa Bukhar na Muslim, lakini (inawapasa wafahamu kwamba) riwaya kama hizi zinapatikana pia ndani ya sahih Bukhar na sahih Muslim.
Imam Bukhar amethibitisha ndani ya Sahih yake[96] katika mlango wa Manaqib Ammar na Hudhaifah (r.a.) kutoka kwa Il-Qimah amesema:
"Nilifika Sham nikasali rakaa mbili kisha nikasema,"Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie mwenza mwema, basi nikaenda kwa jamaa fulani nikakaa kwao, mara alikuja mzee mmoja hivi akakaa pembeni yangu, nikasema ni nani huyu"? Wakasema:"Abud-dar-dai" Nikasema:"Hakika nilimuomba Mwenyezi Mungu anisaidie mwenza mwema, amenisaidia wewe". Akasema: "Ni nani wewe"? Nikasema, "Mimi ni miongoni mwa watu wa Kufah" Akasema:"Hivi huko kwenu hayuko mwana wa Ummi Abdi mwenye viatu viwili, mto na birika ya kujitaharishia? Na kwenu yuko mtu ambaye Mwenyezi Mungu amemlinda kutokana na shetani kwa mujibu wa kauli ya Nabii wake (s.a.w.), mtu ambaye hapana mwingine ila yeye, hayuko kwenu mwandani wa Nabii (s.a.w.) ambaye hakuna mwingine ajuaye isipokuwa yeye. Kisha akasema namna gani Abdallah aisomavyo;(Wallayli Idha-Yaghsha)." Basi nikamsomea "Wallayli Idha Yaghsha, Wannahari ldha-Tajalla-Wad-Dhakari Wal-Untha) Akasema:"Wallahi ndivyo alivyonisomea Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kutoka kinywani mwake kuja kinywani mwangu".


Kisha ameongeza kwenye riwaya nyingine amesema, "Watu hawa hawakuniachia mpaka karibu waniondoshe kwenye jambo nililolisikia toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.)". Taz: Sahih Bukhar Juz. 4 uk. 216. Na katika riwaya nyingine amesema: (Wallayli Idha Yaghsha Wannahari,Idha-Tajalla Wad-Dhakari Wal-Untha) Akasema: "Amenisomea Mtume toka kinywani mwake kuja kinywani mwangu basi watu hawa hawakuniacha mpaka karibu wanirudishe." Taz: Sahih BukharJuz. 4 uk. 218 (Babu Manaqib Abdillah, ibn Mas-ud).

Basi riwaya zote hizi zinafidisha kwamba Qur'an tuliyonayo imezidishwa neno lisemalo, "Wamakhalaqa". Na amethibitisha Bukhar ndani ya sahih yake kwa isnadi yake kutoka kwa ibn Abbas ya kwamba Umar ibn Al-Khtab amesema:"Bila shaka Mwenyezi Mungu amemtuma Muhammad (s.a.w.) kwa ukweli na akamteremshia kitabu, miongoni mwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ni aya ya Rajmi, tuliiisoma na tukaifahamu na kuizingatia, na kwa ajili hiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alirujumu (kupiga mawe wazinifu) nasi baada yake tulirujumu, mimi nachelea iwapo zitapita siku nyingi kwa watu atakujasema msemaji, Wallahi hatuioni Ayatur-Rajmi ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu,watapotea kwa kuiacha faradhi aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu, na kurujumiwa kulikomo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu ni stahiki ya aliyezini iwapo amehifadhika miongoni mwa wanaume na wanawake pindi ushahidi ukithibitishwa au ikapatikana mimba na akakiri (kuzini). Kisha tulikuwa tukisoma miongoni mwa yale tuyasomayo ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwamba:"Msiwachukie wazee wenu kwani kuwachukia wazee wenu ni kufru kwenu, au hakika kufru kwenu ni kuwachukia wazee wenu".


Taz: Sahih Bukhar Juz. 8 uk. 26 Babu Rajmil-Hubla Minaz-Zina Idhaa uh-Sinat. Naye Imam Muslim amethibitisha ndani ya Sahih yake mlango wa Lau anna libni Adama Wadiyan Labtagha Thalithan Juz. 3 uk 100, Amesema:"Abu Musa Al-ash-ari alituma ujumbe kwa wasomaji wa Qur'an wa huko Basra wakaingia kwake watu mia tatu ambao wamekwisha soma Qur'an, akasema: Ninyi ndiyo watu wema huko Basra na ni wasomaji wao, basi isomeni (mara kwa mara) isije kukupitieni muda mrefu mioyo yenu itakuwa migumu kama ilivyokuwa migumu mioyo ya waliokuwa kabla yenu, nasi tulikuwa tukisoma sura tukiifananisha kwa urefu na ugumu na sura (isemayo):"Laukana Libni Adama Wadiyaani Min Malin Labtagha Wadiyan Thalithan Wala Yamlau Jaufa bni Adama Illat-Turaab". Tulikuwa tukisoma sura tunayoifananisha na moja ya Musabbihat nimesahaulishwa isipokuwa nimehifadhi sehemu yake (isemayo): "Ya Ayyuahal-Ladhiina A'manu Lima Taquluna Mala Taf-Aluna Fatuktabu Shahadatu Fii Aa'naqikum Fatus-Aluna An-haa yaumal-Qiyamah ". Taz: Sahih Muslim Juz. 3 uk. 100.

Na hizi sura mbili zinazodaiwa ambazo Abu Musa Al-ash-ari amezisahau, moja wapo inafanana na Suratu Baraa yaani aya 129 na ya pili inafanana na mojawapo ya Musabbihat yaani aya ishirini, sura hizi hazipo isipokuwa zimo ndani ya mawazo ya Abu Musa, basi soma na ustaajabu nami nakuachia uamuzi ewe mchunguzi muadiliru. Sasa basi ikiwa vitabu vya Masunni, Musnad zao na Sihahi zao zimejazwa riwaya kama hizi ambazo zinadai kuwa Qur'an imepungua na wakati mwingine imezidi, basi kebehi hizi ni za nini dhidi ya Mashia ambao wameungana kubatilisha upotovu wa madai haya kwa kauli moja? Na kama yule Shia mwenye kitabu kiitwacho; "Fas-Lulkhitab Fi Ith-Bati Tahrif Kitabi Rabbil-Ar-Bab", aliyefariki mwaka 1320 A.H. aliandika kitabu chake karibu miaka mia iliyopita, yeye alitanguliwa na Msunni kutoka Misri yule mwenye kitabu kiitwacho "Al-Fur-Qan" kwa karibu karne nne kama alivyoonesha jambo hilo Shekh Muhammad Al-Madani mkuu wa kitivo cha sheria katika Azhar.

Jambo la muhimu katika yote haya ni kwamba wanachuoni wa Kisunni na wanachuoni wa Kishia miongoni mwa wahakiki wamezibatilisha riwaya kama hizi na wakazizingatia kuwa potovu na wamethibitisha kwa dalili zinazotosheleza kwamba Qur'an iliyoteremshwa kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.) hakuna ziyada ndani yake wala upungufu wala mabadiliko wala mageuzi. Je, ni vipi Masunni wanawakebehi Mashia kwa sababu tu ya riwaya zisizokubalika kwa Mashia na wao Masunni wajitakase wakati ambapo sihahi zao zinathibitisha juu ya usahihi wa riwaya hizo?


Nami huzikumbuka riwaya hizi kwa uchungu mkubwa na huzuni nyingi, kwani hakutusaidii kitu leo hii kuzinyamazia na kuzitupa ndani ya kapu la takataka, lau siyo shinikizo la hujuma iliyoenezwa na baadhi ya watunzi na waandishi miongoni mwa wale wanaodai kuwa wameshikamana na sunna ya Mtume na hali ya kuwa nyuma yao kuna msukumo unaowatikisa na kuwatia nguvu wawatukane Mashia na kuwakufurisha na hasa baada ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Basi watu kama hawa nawaambia: "Muogopeni Mwenyezi Mungu kuhusu ndugu zenu, na mshikamane na dini ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakane, na ikumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyoko juu yenu, pindi mlipokuwa maadui (Mwenyezi Mungu) akaziunganisha nyoyo zenu mkawa kwa neema yake (nyote) ni ndugu.14
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

KUKUSANYA BAINA YA SALA MBILI Miongoni mwa mambo ambayo Mashia wanaumbuliwa, ni kuchanganya Sala ya Adhuhuri na Alasiri na baina ya Sala ya Magharibi na I'sha. Masunni wakati wanapowaumbuwa Mashia, wenyewe huwa wanasisitiza kwamba wao ndiyo wanaoilinda Sala kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: "Bila shaka Sala kwa Waumini imekuwa ni faradhi yenye wakati maalum". Na kabla ya kuwaunga mkono au kuwa dhidi yao tunawajibika kufanya uchambuzi juu ya maudhui hii kwa kila upande na tuzione kauli za pande mbili (Shia na Sunni).

Ama Masunni wanaafikiana kuwa inafaa kukusanya baina ya (Sala ya) Adhuhuri na Alasiri na inaitwa "Jam'u1 Taqdi'm" Na kuchanganya huko Muz-Dalifah wakati wa I'sha baina ya hiyo sala ya I'sha na faradhi ya Magharibi na inaitwa: "Jam'u't-Taakhir". Na hili wanalikubali Waislamu wote Mashia na Masunni, bali vikundi vyote vya Kiislamu bila kubagua. Na tofauti iliyopo baina ya Mashia na Masunni ni ruhusa ya kukusanya baina ya faradhi mbili yaani Adhuhuri na Alasiri na Magharibi na I'sha katika siku zote tena bila ya udhuru wa safari. Ama Madhehebu ya Hanafi wao wanasema kuwa hairuhusiwi hata katika safari. Pamoja na kuwa kuna maandiko yaliyo wazi yanayoruhusu, na hasa katika safari, na kwa kusema kwao hivyo wamekwenda kinyume na makubaliano ya umma wa Kisunni na Kishia.


Ama Maliki na Shafii na Hanbal wao wanasema kuwa inaruhusiwa kukusanya baina ya faradhi hizo mbili wakati wa safari na wanahitilafiana baina yao juu ya ruhusa hiyo kwa udhuru wa khofu, maradhi, mvua, na tope. Ama Shia wao wanakubaliana bila kipingamizi juu ya ruhusa ya kukusanya wakati ambao siyo wa safari wala maradhi wala khofu yoyote. Na hiyo ni kwa kufuata maelezo waliyoyapokea kutoka kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) katika kizazi kitukufu. Na hapa tunalazimika tusimame msimamo wa tuhuma na mashaka dhidi yao, kwani kila mara Masunni wanapotoa hoja dhidi ya Mashia, wao hujibu kwamba Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) ndiyo waliowafundisha na wakawabainishia kila lenye kuwatatiza na hujifakharisha kwamba wao wanawafuata Maimamu Maasum ambao wanaifahamu vyema Qur'an na Sunna. Nami binafsi naikumbuka sala yangu ya mwanzo niliyokusanya ilikuwa baina ya adhuhuri na alasiri, na iliongozwa na shahidi Muhammad Baqir As-Sadr (r.a.) wakati nilipokuwa Najaf, na hapo kabla nikitenganisha baina ya sala ya adhuhuri na Alasiri,* mpaka ilipofika siku hiyo njema ambayo nilitoka pamoja na Sayyid Muhammad Baqir As-Sadr nyumbani kwake kwenda kwenye Msikiti ambao alikuwa akiwaongoza wafuasi wake.Watu hao waliniheshimu na wakaniachia nafasi nyuma yake.


Sala ya Adhuhuri ilipomalizika iliqimiwa sala ya alasiri, nafsi yangu ilinishauri nijitoe kwenye safu lakini nilibaki kwa sababu mbili: Ya kwanza, heshima ya Sayyid As-Sadr na unyenyekevu wake katika sala kiasi kwamba nilitamani sala iendelee, na ya pili ni kuwepo kwangu katika nafasi ile nami nikiwa karibu mno kwake miongoni mwa wenye kusali na nilihisi nguvu yenye shinikizo inanifunga kwake.

Tulipomaliza kuswali faradhi ya alasiri watu wakasongamana kwake wakimuuliza, basi nilibakia nyuma yake nikisikiliza maswali na majibu yake isipokuwa yale ambayo sikuyasikia vizuri (pindi yaulizwapo au pindi yajibiwapo). Hatimaye Sayyid alinichukua twende pamoja naye nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha mchana, na huko nilijikuta kuwa ni mgeni mheshimiwa, na hapo ndipo nilipoitumia fursa ya kikao hicho kumuuliza juu ya kukusanya baina ya Sala mbili nikasema: "Ewe Bwana wangu hivi inawezekana kwa Muislamu kukusanya baina ya faradhi mbili kama anayo dharura"? Akasema: "Inawezekana kukusanya baina ya faradhi mbili katika hali zote na bila ya dharura yoyote." Nikasema: "Ni ipi hoja yenu"? Akasema: "Ni kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikusanya baina ya faradhi mbili akiwa Madina na siyo katika safari wala khofu wala mvua wala dharura yoyote. Na hiyo ni kwa sababu tu ya kutuondoshea uzito, na jambo hili Al-Hamdulillah limethibiti kwetu sisi kupitia kwa Maimamu watakatifu na vile vile kwenu umethibiti".


Nilishangaa sana, ni vipi kwetu sisi limethibiti na sijalisikia kabla ya leo na wala sijamuona yeyote miongoni mwa Masunni akilitumia bali kinyume chake Masunni wanasema kuwa sala hubatilika ikiwa itasaliwa japo dakika moja kabla ya adhana, basi itakuwaje kwa anayeisali kabla ya masaa chungu nzima tena akaifuatisha baada ya Adhuhuri, au akasali sala ya I'sha wakai wa Magharibi, basi kwetu sisi inaonekana ni jambo baya na batili.

Sayyid Muhammad Baqir As-Sadr alifahamu wasi wasi wangu na kushangazwa kwangu, na hapo akamnong'oneza mmoja wa waliokuwepo hapo, yule akasimama haraka na akarudi na vitabu viwili, nikavifahamu kuwa ni Sahih Bukhar na Sahih Muslim. Sayyid As-Sadr akamkalifisha mwanafunzi yule anioneshe hadithi zinazohusu kukusanya baina ya faradhi mbili: Nikasoma mwenyewe ndani ya Sahih Bukhari namna Mtume alivyokusanya baina ya faradhi ya adhuhuri na alasiri, na vile vile faradhi ya magharibi na i'sha, kama ambavyo ndani ya Sahihi Muslim nilisoma mlango mzima unaohusu kukusanya baina ya sala mbili nyumbani bila ya khofu wala mvua wala safari.

Sikuficha kustaajabu na kushangaa kwangu japokuwa mashaka yaliniingia kwamba Bukhari na Muslim walizonazo wao huenda zikawa zimepotoshwa na nikanyamazia moyoni tu kwamba nitavirejea (kuvisoma) vitabu hivi (nyumbani) Tunisia. Sayyid Muhammad Baqir aliniuliza maoni yangu baada ya dalili hii. Nikasema: "Ninyi mko kwenye ukweli nanyi wakweli katika hayo myasemayo na napenda kukuulizeni swali jingine" Akasema: "Tafadhali (uliza)". Nikasema: "Je, inafaa kukusanya baina ya sala nne kama wafanyavyo watu wengi huko kwetu pindi warudipo usiku wanasali Qadhaa adhuhuri, alasiri na magharibi na i'sha"? Akasema: "Haifai".


Nikasema:"Uliniambia hapo kabla kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alitenganisha (Sala) na alikusanya na kwa ajili- hiyo tumefahamu nyakati za sala ambazo Mwenyezi Mungu ameziridhia." Akasema: "Hakika faradhi ya adhuhuri na alasiri zina wakati unaoshirikiana na unaanzia tangu kupinduka jua mpaka kuzama, na faradhi ya magharibi na i'sha pia zina wakati unaoshirikiana na unaanzia tangu kuzama jua hadi nusu ya usiku, na faradhi ya asubuhi ina wakati mmoja, unaanzia tangu kuchomoza al-fajiri hadi kuchomoza jua, basi yeyote atayekwenda kinyume cha nyakati hizi atakuwa amekwenda kinyume cha aya tukufu isemayo: "Bila shaka sala kwa waumini imekuwa ni faradhi yenye wakati maalum". Haiwezekani kwetu sisi kwa mfano kusali sala ya asubuhi kabla ya al-fajiri wala baada ya kuchomoza jua, kama ambavyo haiwezekani kwetu sisi kuswali faradhi mbili za adhuhuri na alasiri kabla ya kupinduka jua au baada ya kuzama jua kama ambavyo haifai kwetu sisi kuswali faradhi ya magharibi na i'sha kabla ya kuzama jua na baada ya nusu ya usiku.

Nilimshukuru Sayyid Muhammad Baqir As-Sadr, japokuwa nilikuwa nimekinaika kwa kauli zake zote lakini sikukusanya baina ya faradhi mbili baada ya kuachana naye isipokuwa niliporudi Tunisia na nikazama katika uchunguzi na nikauona ukweli. Hiki ndicho kisa changu na Shahid As-Sadr Mwenyezi Mungu amrehemu kuhusu kukusanya baina ya faradhi mbili, nakisimulia ili iwabainikie ndugu zangu miongoni mwa Masunni: Kwanza:Waone ni namna gani zinavyokuwa tabia za wanachuoni ambao ni wanyenyekevu mpaka kwa kweli wamekuwa ni warithi wa Mitume katika elimu na tabia. Pili:Ni namna gani hatuyajuwi mambo yaliyomo ndani ya sihah zetu na tunawaumbuwa wengine kwa mambo ambayo sisi wenyewe tunayaamini kusihi kwake na yamo ndani ya sihah zetu.


Imam Ahmad bin Hanbal amethibitisha ndani ya Musnad yake[97] kutoka kwa ibn Abbas amesema:"Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alisali (rakaa) saba na (rakaa) nane akiwa mjini Madina na hakuwa safarini". Na amethibitisha Imam Malik ndani ya kitabu kiitwacho Muwatta[98] kutoka kwa ibn Abbas amesema "Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alisali adhuhuri na alasiri zote (kwa pamoja) na magharibi na i'sha zote kwa pamoja pasi na khofu wala safari". Naye Imam Muslim amethibitisha ndani ya Sahih yake katika mlango wa kukusanya baina ya-sala mbili nyumbani (bila kuwa safarini) amesema:
"Imepokewa toka kwa ibn Abbas amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alisali adhuhuri na alasiri zote kwa pamoja, na magharibi na i'sha zote kwa pamoja bila khofu wala safari".[99] Kama ambavyo amethibitisha kutoka kwa ibn Abbas tena amesema:"Mtume wa Mwenyezi Mungu alikusanya baina ya sala ya adhuhuri na alasiri na magharibi na i'sha akiwa Madina bila ya khofu wala mvua amesema nikamwambia ibn Abbas: "Kwa nini alifanya hivyo"? Akasema: "Ili asiwape uzito ummati wake."[100]

Na miongoni mwa mambo yatakayokujulisha ewe ndugu msomaji kwamba sunna hii ilikuwa mashuhuri kwa Masahaba na wakiitumia, ni yale aliyoyaeleza Muslim, ndani ya sahihi yake katika mlango huu huu amesema: "Ibn Abbas alituhutubia siku moja baada ya sala ya alasiri mpaka jua likazama na nyota zikadhihiri, watu wakaanza kusema, "Sala sala", amesema:Akamjia ibn Abbas mtu mmoja miongoni mwa Bani Tamim hapunguzi wala hakomi(kusema) sala sala. Basi ibn Abbas akasema, Je, unanifundisha sunna, ole wako, kisha akasema:Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amekusanya baina ya sala ya adhuhuri na alasiri na magharibi na i'sha, na katika mapokezi mengine, ibn Abbas alimwambia mtu yule "Ole wake unatufundisha sala nasi tulikuwa tukikusanya baina ya sala mbili zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.). Taz: Sahih Muslim Juz. 2 uk. 153 (Babul-jam'i bainas-salatain fil-hadhr).


Naye Imam Bukhar amethibitisha ndani ya sahih yake katika mlango wa wakati wa Magharib amesema, "Ametusimulia Adam, amesema. Ametusimulia Shuubah, ametusimulia Amr bin Dinar, amesema nilimsikia Jabir bin Zaid, kutoka kwa ibn Abbas amesema: Mtume (s.a.w.) aliswali (rakaa) saba zote kwa pamoja na (rakaa) nane zote kwa pamoja. Taz: Sahih Bukhar Juz. 1 uk.140 (Babu waqtil-maghrib). Kama ambavyo Bukhar amethibitisha ndani ya Sahih yake katika mlango wa wakati wa alasiri amesema: "Nilimsikia Abu Amamah akisema, tulisali na Umar bin Abdil-A'ziz sala ya adhuhuri kisha tukatoka mpaka tukaingia kwa Anas bin Malik tukamkuta anasali sala ya alasiri mimi nikasema: ewe Ammi ni sala gani hii uliyosali? Akasema:"Alasiri, na hii ni sala ya Mtume wa Mwenyezi Mungu tulikuwa tukiisali pamoja naye". Taz: Sahih BukharJuz. 1 uk. 138. (Babu waqtil-asr).


Pamoja na uwazi wa hadithi hizi, utakuta bado kuna watu wanaowakebehi Mashia kwa jambo hilo, na kuna wakati fulani hali hiyo ilitokea huko Tunis, pale Imam mmoja aliposimama mbele yetu katika mji wa Qafsah ili atutukane na kutuadhiri mbele ya wanaosali akasema: "Je, mumeiona hii dini waliokuja nayo, hakika wao baada ya sala ya adhuhuri husimama wakasali alasiri, bila shaka hii ni dini mpya siyo dini ya Muhammad ambaye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, watu hawa wanakwenda kinyume cha Qur'an ambayo inasema: "Bila shaka sala kwa waumini imekuwa faradhi yenye wakati maalum." Na hakuacha kitu illa alishutumu wote waliouona ukweli.

Kuna mmoja wao alikwisha kuuona ukweli huu alinijia na alikuwa ni kijana mwenye kiwango kikubwa cha maarifa, akanisimulia kwa uchungu yale aliyoyasema Imam yule, basi mimi nilimpa Sahih Bukhar na Sahih Muslim, na nikamtaka amuoneshe juu ya kusihi kwa suala la kukusanya na ni sunna ya Mtume (s.a.w.) (nilifanya hivyo) kwa kuwa mimi sitaki kujadiliana naye kwani hapo kabla nilijadiliana naye kwa njia nzuri yeye akanikabili kwa shutuma na matusi na tuhuma mbaya. Hivyo la muhimu ni kwamba rafiki yangu (huyu) hakuacha kusali nyuma yake na baada ya kuisha sala yule Imam alikaa kama kawaida yake kwa ajili ya kusomesha, basi yule rafiki yangu alimuuliza juu ya kukusanya baina ya faradhi mbili. Yule Imam akasema:"Huo ni uzushi wa Mashia". Rafiki yangu akamwambia, "Lakini jambo hilo limethibiti ndani ya Sahih Bukhar na Sahih Muslim". Akampa, akausoma mlango wa kukusanya baina ya sala mbili. Basi ukweli ulipomgonga tena mbele ya watu wanaosali humo na kusikiliza darasa zake, alikifunga na akanirejeshea huku akisema: "Jambo hili lilikuwa ni maalum kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu nawe mpaka utapokuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu basi unaweza kusali (hivyo).

Rafiki yangu huyu anasema: "(Baada ya jibu hili) nikafahamu kwamba Imam yule ni mjinga tena mwenye chuki, nami nikaapa kuwa kuanzia siku ile sintasali nyuma yake"[101] Baada ya hayo nilimtaka rafiki yangu amrudie yule Imam amuonyeshe kwamba ibn Abbas alikuwa akiswali sala hiyo, na vile vile Anas bin Malik na Masahaba wengi. Basi ni kwanini yeye anataka kuihusisha kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Je, haikuwa kwetu sisi Mtume ni kiigizo chema? Lakini rafiki yangu alitoa udhuru akasema: "Hapana haja ya jambo hili huyo hawezi kukubali hata kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) atakuja.

Kwa hakika Mwenyezi Mungu anastahiki shukrani, kwani baada ya vijana wengi kufahamu ukweli huu ambao ni kuchanganya baina ya sala mbili Tangu hapo wengi wao wameirudia sala baada ya kuwa waliiacha kwa sababu walikuwa wakipata taabu ya kupitwa na sala kwa nyakati zake na huzikusanya nyakati nne usiku na nyoyo zao zinachoka. Si hivyo tu, bali wameifahamu hekima ya kukusanya sala katika nyakati zake hali ya kuwa wametulizana, na wamefahamu hekima ya kauli ya Mtume (s.a.w.) isemayo: "Nisije kuwapa taabu umma wangu".


KUSUJUDU JUU YA UDONGO Wanachuoni wa Kishia wamekubaliana juu ya kauli inayohusu ubora wa kusujudu juu ya ardhi kutokana na mapokezi wanayoyapokea kutoka kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.), mapokezi hayo ni kauli ya babu yao ambaye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliposema: "Bora ya Sijda ni (kusujudu) juu ya ardhi". Na katika mapokezi mengine (amesema), "Sijida haijuzu isipokuwa juu ya ardhi au kile kilichooteshwa ardhini kisicholiwa wala kuvaliwa".

Na mwenye Kitabu kiitwacho Wasailus-Shia' amesimulia toka kwa Muhammad bin Ali bin Husain kwa isnadi yake, toka kwa Hisham bin Al-Hakam toka kwa Abu Abdillah (a.s.) amesema: "Kusujudu juu ya ardhi ni bora kwani kunazidisha unyenyekevu, na unyenyekevu (ufanywe) kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu". Na ndani ya mapokezi mengine kutoka kwa Muhammad bin Al-Hasan kwa isnad yake toka kwa Is'haq bin Al-Faali kwamba yeye alimuuliza Abu Abdillah (a.s.) kuhusu kusujudu juu ya mkeka na jamvi lililofumwa kwa matete, akasema, "Hapana ubaya, na kusujudu juu ya ardhi kwangu mimi ni bora zaidi, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikuwa akipenda hivyo (yaani) kuweka bapa lake la uso ardhini, basi nami nakupendelea wewe kile alichokuwa akikipenda Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.)" Ama wanachuoni wa Kisunni wao hawaoni vibaya kusujudu juu ya mabusati na mazulia japokuwa ilivyo bora kwao ni kusujudu juu ya jamvi.


Na kuna baadhi ya riwaya ambazo amezithibitisha Bukhar na Muslim ndani ya sahihi zao (riwaya) ambazo zinasisitiza kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikuwa na mswala uliotengenezwa kwa makuti akisujudu juu yake. Muslim amethibitisha ndani ya sahihi yake katika Kitabul-Haidh kutoka kwa Yahya bin Yahya na Abubakr bin Abi Shaibah, kutoka kwa Abu Muawiyah kutoka kwa Al-Aa'mash, naye toka kwa Thabiti bin Ubaid kutoka kwa Qasim bin Muhammad, naye toka kwa Aisha amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliniambia, nimchukulie jamvi langu humo msikitini, Aisha akasema, nikamwambia mimi ninahedhi, Mtume akasema:Bila shaka hedhi yako haiko mkononi mwako". Taz: Sahihi Muslim Juz. 1 uk. 168. Babu-Jawaz Ghaslil-Haidh Ra'asa Zaujiha), Sunan Abi Dawud Juz. 1 uk. 68 (Babul-Haidh Tanawul Minal-Masjid).


Sasa Muslim anasema, Al-Khumrah ni kifaa kidogo cha kusujudia kwa kiasi cha kutosha kusujudu juu yake. Na miongoni mwa mambo ambayo yanatujulisha kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikuwa akipenda kusujudu juu ya ardhi ni mapokezi aliyoyathibitisha Bukhar ndani ya sahih yake kutoka kwa Abu-Said Al-Khudri (r.a.) kwamba, "Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikuwa akikaa itikafu katika kumi la kati ndani ya mwezi wa Ramadhani. Basi kuna mwaka fulani alikaa itikafu mpaka ilipofika usiku wa tarehe ishirini na moja nao ni usiku ambao asubuhi yake anatoka katika itikafu yake, akasema, yeyote aliyekuwa akikaa itikafu pamoja nami, basi na akae itikafu kumi la mwisho kwa hakika usiku huu nilioteshwa kisha nikasahaulishwa na uliniona vile nikisujudu katika maji na tope,basi utafuteni katika kumi la mwisho na muutafute katika (tarehe za witri). Mvua ilinyesha usiku huo na msikiti ulikuwa wa hema basi msikiti ukavuja, na macho yangu yalimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) juu ya uso wake kuna alama ya maji na tope asubuhi ya tarehe ishirini na moja". Taz: Sahih Bukhar Juz. 2 uk. 256 (Babul-itikaf -Fil-A 'shril-Awa'khiri).

Pia miongoni mwa mambo yanayotujulisha ni kwamba, Masahaba walikuwa wakiboresha kusujudu juu ya ardhi, na wakifanya hivyo mbele ya Mtume (s.a.w.) kama alivyothibitisha Imam An-Nasai ndani ya sunan yake katika mlango wa "Tabridul-haswa Lis-Sujud Alaiha"akasema: "Ametueleza Qataybah amesema, ametusimulia Ubba'd kutoka kwa Muhammad bin Amr kutoka kwa Said bin Al-Harith naye toka kwa Jabir bin Abdillah amesema:"Tulikuwa tukisali pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) sala ya adhuhuri, basi nikachukua gao la changarawe katika kiganja changu kulipoza kisha huligeuzia kwenye kiganja kingine ninaposujudu huliweka gao hilo kwa ajili ya paji langu la uso".


Taz: Sunan Al-Imam An-Nasai Juz. 2 uk. 204 (Babu Tabridul-Haswa Lis-Sujud A 'laih. Zaidi ya yote hayo, ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema: "Ardhi imefanywa kwa ajili yangu kuwa ni mahala pa kusujudia na tahara". Taz: Sahih Bukhar Juz. 1 uk. 86 (Kitabut- Tayammum). Na vile vile amesema:
"Ardhi yote tumefanyiwa kuwa ni mahala pa kusujudia na udongo wake ni tahara." Taz: Sahih Muslim Juz, 2 uk. 64, (Kitabul-Masajid Wamawa-dhiu's-Salah). Basi ni vipi Masuni wanakuwa na chuki dhidi ya Mashia kwa kuwa tu wanasujudu juu ya ardhi badala ya kusujudu kwenye mabusati. Na ni vipi mambo yanafikia kiasi cha kuwakufurisha na kuwakejeli na kuwazulia kwamba wao (Mashia) ni waabudu sanamu? Na vipi wanawapiga (Mashia) huko Saudi Arabia kwa kuwa tu kumepatikana Turba (Udongo) ndani ya mifuko yao au mabegi yao? Je, huu ndiyo Uislamu unaotuamuru kuheshimiana sisi kwa sisi na kutokumdharau Muislamu anayempwekesha Mwenyezi Mungu, (Muislamu) ambaye anashuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, anasali, anatoa zaka na kufunga Ramadhan na kuhiji Maka.


Je, inaingia akilini kwamba Mashia wanavumilia taabu hizo na kupata hasara na kuja kuhiji kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu na kuzuru kaburi la Mtume (s.a.w.) na hali ya kuwa wanaabudu jiwe kama wanavyopenda baadhi ya watu kufikiria hivyo? Basi je, Masunni hawatosheki na kauli ya Shahidi Muhammad Baqir As-Sadr ambayo nimeinakili ndani ya kitabu changu cha mwanzo kiitwacho, "Thummah-Tadaytu" wakati nilipomuuliza juu ya Turbah akasema: Na kama isingalikuwa juu yenu fadhila ya Mwenyezi Mungu na Rehma yake katika dunia na akhera, bila shaka ingalikupateni adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyoyashughulikia. Pindi mnapotangaza kwa ndimi zenu na mnasema kwa vinywa vyenu msilolijua na mnadhani ni jambo jepesi kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni jambo kubwa kabisa (Qur'an, 24:14)15
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

AR-RAJ-A' (KUREJEA KWENYE UHAI) Kauli inayohusu mas-ala haya, wanayo Mashia peke yao, nami nimetafiti ndani ya vitabu vya Masunni sikukuta athari yoyote inayotajwa juu ya mas-ala haya. Mashia katika kuithibitisha "Ar-Raja'h" wametegemea khabari na riwaya walizozipokea kutoka kwa Maimamu watakatifu (a.s.) ya kwamba, "Mwenyezi Mungu Mtukufu atawafufua baadhi ya waumini na baadhi ya watu waovu ili waumini wawaadhibu maadui zao ambao pia ni maadui wa Mwenyezi Mungu hapa duniani kabla ya akhera. Riwaya hizi zikisihi na ni sahihi tena kwa daraja ya mutawatiri kwa upande wa Shia, basi haziwalazimu Masunni iwapo hawataamini kusihi kwake na kwa ajili hiyo wao hawalazimiki kuziitakidi, kwani Maimau wa nyumba ya Mtume wamezisimulia toka kwa Babu yao Mtume Muhammad (s.a.w.) hivyo basi siyo sawa kabisa (kuwalazimisha waziitakidi) kwani sisi tumejilazimisha wenyewe kuwa waadilifu na kutokuwa na chuki katika utafiti (tuufanyao) hivyo hatutawakalifisha kitu isipokuwa kile walichojilazimisha wenyewe na wakakithibitisha ndani ya vitabu vyao.


Na kwa kuwa riwaya za "Ar'Raja'h" kwao hazikuja, basi wao wako hum kutozitumia riwaya hizo na wako huru kuzipinga, na hali hii itakuwepo kama kuna Shia fulani anataka kuwalazimisha kuzikubali riwaya hizo. Ama Mashia wenyewe hawakumlazimisha yeyote akubaliane na itikadi ya Ar-Raja'h wala hawamkufurishi anayeipinga. Hivyo basi hapana sababu yoyote inayopelekea kukebehi na vitisho dhidi ya Shia hasa ikiwa wao wanazifasiri baadhi ya aya kwa namna inayokubaliana na itikadi hiyo, kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Na siku tutakapowafufua katika kila umma makundi ya wale wanaopinga aya zetu nao watawekwa mafungu mafungu". (Qur'an, 27:83) Imekuja ndani ya Tafsiri Al-Qummi kutoka kwa ibn Abi Umair kutoka kwa Hammad naye toka kwa Abu Abdillah Jaa'far As-Sadiq (a.s) amesema:
"Watu wanasema nini kuhusu aya isemayo, Na siku tutakapowafufua katika kila umma makundi? Nikasema, wanasema hiyo ni katika siku ya Kiyama, akasema: Sivyo kama wasemavyo hakika hiyo ni katika Ar-Raja'h, basi je, Mwenyezi Mungu atafufua siku ya Qiyama kundi katika kila umma na kuwaacha wengine? Bila shaka aya ya Kiyama ni ile isemayo: "Na siku hiyo tutawafufua (viumbe wote) wala hatutamuacha hata mmoja miongoni mwao". (Qur'an, 18:47)

Kama ilivyokuja ndani ya kitabu kiitwacho, A'qaidul-Imamiyyah cha Sheikh Muhammad Ridha Al-Muzaffar aliposema: "Hakika kile ambacho Mashia Imamiyyah wanakubaliana nacho kwa mujibu wa mapokezi yaliyokuja toka kwa watu wa kizazi cha Mtume (s.a.w.) ni kwamba; Mwenyezi Mungu Mtukufu atawarejesha duniani watu fulani miongoni mwa watu waliokufa kwa sura zao zile zile walizokuwa nazo. Kisha atawapa nguvu kikundi cha watu fulani na kuwadhalilisha kikundi kingine na atawalipizia kisasi wenye kutenda haki dhidi ya wale waliokuwa wakitenda batili na wenye kudhulumiwa dhidi ya madhalimu, na hilo litakuwa zama zile atakaposimama Mahdi wa kizazi cha Muhammad (s.a.w.).

Na hatarudi isipokuwa yule ambaye daraja yake katika imani ilikuwa ni ya juu au yule aliyefikia' upeo wa juu katika maovu kisha baada ya hapo watarudishwa kwenye mauti, na baada ya hapo ndiyo itakuwa Kiyama na kulipwa wanayostahiki miongoni mwa thawabu au adhabu, kama alivyoeleza Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'an yake juu ya kutamani kwa watu hawa wenye kurejea ambao hawakujirekebisha kwa kurejea (bali) wakapata adhabu ya Mwenyezi Mungu (watatamani) kurudi mara ya tatu huenda wakajirekebisha: "Wakasema Ewe Mola wetu, umetufisha mara mbili na umetuhuisha mara mbili nasi tukakiri makosa yetu. Basi je, iko njia ya kutoka (tukarejezwa duniani)? (Qur'an, 40:11) Taz: Aqaidul-Imamiyyah uk. 80, (Aqidah No. 32).


Mimi nasema ikiwa Masunni hawaamini Raja'h wanayo haki kikamilifu, lakini hawana haki yoyote ya kuwakebehi wanaoamini Raja'h kutokana na kwamba kwa wale wanaoamini yamethibiti maandiko. Hivyo basi asiyejua hana hoja dhidi ya ajuwaye na wala mjinga hana hoja dhidi ya mwanachuoni na siyo kwamba kukosa kukiamini kitu ni dalili ya kuwa kitu hicho ni batili, kwa sababu kuna hoja chungu nzima zenye nguvu walizonazo Waislamu lakini Ah-lul-Kitab miongoni mwa Wayahudi na Wakristo hawaziamini. Na kuna itikadi nyingi tu na riwaya nyingi hasa kuhusu Mawalii na watu wema ambazo ni muhali na mbaya lakini watu wa Tariqa za kisufi wanaziamini, lakini zote hizo hazilazimu ikebehiwe na iumbuliwe itikadi ya Kisunni. Na ikiwa Raja'h inayo Sanad ndani ya Qur'an na Sunna ya Mtume na ni kitu ambacho siyo muhali kwa Mwenyezi Mungu ambaye ametupigia mifano kuhusiana nacho ndani ya Qur'an kama pale aliposema: "Au kama yule aliyepita kwenye mji uliokuwa umekufa, akasema ni lini Mwenyezi Mungu ataufanya hai mji huu baada ya kufa kwake, basi Mwenyezi Mungu akamfisha kwa miaka mia kisha akamfufua". (Qur'an, 2:259)


Au kama ile kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Je, huzingatii habari ya wale waliotoka majumbani mwao nao wakiwa maelfu wakiogopa mauti, Mwenyezi Mungu akawaambia kufeni kisha akawafufua" (Qur'an, 2:243) Na wako watu fulani miongoni mwa Wana wa Israel, Mwenye Mungu aliwafisha kisha akawapa uhai tena, amesema Mwenyezi Mungu:
"Na kumbukeni pale mliposema, Ewe Musa hatutakuamini mpaka tumuone Mwenyezi Mungu wazi wazi, yakakunyakueni mauti ya ghafla (ya moto wa radi) na hali mnaona, kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru" (Qur'an, 2:55-56) 'Na amesema Mwenyezi Mungu kuhusu As-Habul-Kahf ambao walikaa katika pango lao hali ya kuwa wamekufa kwa zaidi ya miaka mitatu:
"Kisha tukawafufua ili tujuwe ni lipi katika makundi mawili liwezalo kukadiria vyema muda waliokaa (humo pangoni)". (Qur'an, 18:12)


Basi hiki ni kitabu cha Mwenyezi Mungu kunasimulia kwamba Raja'h ilikwisha tokea katika nyumati zilizotangulia hivyo siyo muhali kutokea katika umma wa Muhammad (s.a.w.) na hasa hasa jambo hilo litakapokuwa limesimuliwa na Maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.) kwani wao ni wakweli na ni wajuzi. Ama kauli ya baadhi ya watu wenye mawazo ya kitoto kwamba Raja'h ni kauli ya "Tanasukh" (kuwa Roho huingia ndani ya kiwiliwili kingine) kauli ambayo inaaminiwa na baadhi ya makafiri, basi hiyo ni wazi kabisa kuwa ni ufisadi na ni batili, na lengo la kauli hiyo ni kuwakejeli na kuwatukana Mashia. Izingatiwe pia kuwa wanaoamini "Tanasukh" wao hawasemi kwamba mtu atarudi duniani akiwa na mwili wake na roho yake na sura yake kama jinsi alivyokuwa.

Bali wao wanasema kuwa roho huhama toka kwa mtu aliyekufa kwenda kwa mtu mwingine ambaye huzaliwa upya au hata kwenda kwa wanyama. Na kauli hii kama tunavyofahamu iko mbali mno na akida ya Waislamu wanaosema kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini kwa miili yao na roho zao. Hivyo basi "Raja'h" siyo miongoni mwa "Tanasukh" kwa namna yoyote ile, na hiyo Tanasukh ni miongoni mwa kauli za watu wajinga ambao hakuna wakijuacho au ni makundi ya watu wasio na utambuzi.


KUVUKA MIPAKA KATIKA KUWAPENDA MAIMAMU Kuvuka mpaka kwa hapa hatukusudii kuwa ni kutoka katika haki na kufuata matamanio kiasi cha kuwa huyo mwenye kupendwa huwa ni Mungu mwenye kuabudiwa. Kwani kufanya hivyo ni kufru na ni shirki, hapana Muislamu yeyote anayeitakidi ujumbe wa Kiislamu na Unabii wa Muhammad (s.a.w.) anayesema hivyo. Na kwa hakika Mtume (s.a.w.) ameweka mipaka ya pendo hili pale aliposema kumwambia Imam Ali (a.s.). "Wameangamia kwa sababu yako wewe watu wawili, mwenye kukupenda kupita kiasi na mwenye kukuchukia." Na kauli yake tena Mtume (s.a.w.) "Ewe Ali bila shaka unao mfano wa Isa mwana wa Maryam, Mayahudi walimchukia mpaka wakamsingizia mama yake machafu na walimpenda Wakristo mpaka wakampa daraja ambayo haistahiki" Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 123, Tarikh Dimishq cha Ibn 'Asakir Juz. 2 uk. 234, Tarikhul-Kabir cha Bukhar Juz. 2 uk. 281, Tarikhul-Khulafai cha Suyuti uk. 173, Khasaisun-Nasai uk. 27, Dhakhairul-Uqba uk. 92, As-Sawaiqul-Muhriqah cha ibn Hajar uk. 74.


Na hiyo ndiyo maana ya kuvuka mpaka inayopingwa, na kuvuka mpaka katika kupenda mpaka huyo mwenye kupendwa afanywe Mungu na apewe daraja asiyokuwa nayo au kuvuka mpaka katika kumchukia kiasi ikafikia daraja ya kuzua uongo na tuhuma batili. Mashia katika kumpenda Ali na Maimamu miongoni mwa wanawe hawakuvuka mpaka, isipokuwa wamewaweka kwenye daraja inayokubalika kiakili. Daraja ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu amewatawalisha nayo ni kwamba wao ni mawasii wa Mtume na ni Makhalifa wake, na hapana yeyote aliyesema kwamba wao ni Manabii sembuse Uungu. Hebu zitupilie mbali kauli za wazushi ambao wanadai kwamba Mashia wamemfanya Ali kuwa ni Mungu, na kama itasihi habari hii kwamba (kuna wanaodai hivyo) basi hilo halikuwa kundi fulani wala Madhehebu wala Mashia wala Khawarij. Sasa basi,ni lipi kosa la Mashia ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Waambie sikutakeni malipo yoyote isipokuwa kuwapenda Qaraba zangu."


Ni jambo linalofahamika ya kwamba "Mawaddah" yana daraja ya juu kuliko kupenda. Na ikiwa Mtume (s.a.w.) amesema: "Hawezi kuwa Muumini mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake kile anachokipendelea nafsi yake." Kwani upendo (Mawaddah) unakulazimisha wewe kuinyima nafsi yako kitu fulani ili umpendelee kwacho mwenzako". Na liko wapi kosa la Mashia iwapo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anasema: "Ewe Ali, wewe ni Bwana (Mtukufu) duniani na ni Bwana (Mtukufu) akhera, basi yeyote mwenye kukupenda, bila shaka amenipenda mimi, na yeyote mwenye kukuchukia bila shaka amenichukia mimi, na mpenzi wako ni mpenzi wa Mwenyezi Mungu, na mgomvi wako ni mgomvi wa Mwenyezi Mungu, na ole wake mwenye kukuchukia." Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 128, amesema hadithi hii ni sahihi kwa sharti zinazokubalika kwa Bukhar na Muslim, pia Taz: Nurul-Absar cha Ash-Shablanji uk. 73, Yanabiul-Mawaddah uk. 205, Ariyadhun-Nadhrah Juz. 2 uk. 165. Pia Mtume anasema:
"Kumpenda Ali ni imani na kumchukia ni unafiki."


Taz: Sahih Muslim Juz. 1 uk. 48, As-Sawaiqul-Muhriqah uk. 73, Kanzul-Ummal Juz. 15 uk. 105. Na anasema Mtume (s.a.w.): "Yeyote atakayekufa hali yakuwa anakipenda kizazi cha Muhammad, atakufa hali ya kuwa ni shahidi, .fahamuni yakuwa yeyote atakayekufa hali yakuwa anakipenda kizazi cha Muhammad atakufa hali ya kuwa amesamehewa, fahamuni kwamba, yeyote atakayekufa hali ya kuwa anakipenda kizazi cha Muhammad atakufa hali ya kuwa ametubia, fahamuni ya kwamba, yeyote atakayekufa hali ya kuwa anakipenda kizazi cha Muhammad atakufa hali yakuwa ni muumini mwenye imani iliyokamilika, fahamuni ya kuwa yeyote atakayekufa hali yakuwa anakipenda kizazi cha Muhammad, Malaika wa mauti atambashiria pepo..." Taz:
1) Tafsiri Atha'alabi iitwayo Al-Kabir katika Ayatul-Mawaddah.
2) Tafsiruz-Zamakhshari iitwayo Al-Kash-Shaf.
3) Tafsiru Fakhrir-Razi Juz. 7 uk. 405.
4) Ihqaqul-Haq cha At-Tustari Juz. 9 uk. 486.
Ni lipi kosa la Mashia ikiwa wao wanampenda mtu ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema kumuhusu mtu huyo kwamba: "Kesho nitampa bendera yangu mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu na Mtume wake (nao) wanampenda mtu huyo". Taz: Sahih Bukhar Juz. 4 uk. 20 na Juz. 5 uk. 76, Sahih Muslim Juz. 7 uk. 12. (Babu Fadhail All bin Abi Talib). Basi mpenzi wa Ali ni mpenzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na mtu huyo ni muumini, na mgomvi wa Ali ni mgomvi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na mtu huyo ni mnafiki. Naye Imam Shafii amesema kuhusu kuwapenda kizazi cha Mtume: "Enyi watu wa nyumba ya Mtume, kukupendeni ninyi ni faradhi itokayo kwa Mwenyezi Mungu ameteremsha ndani ya Qur'an." Yakutosheni kuwa na ubora mkubwa kwamba yeyote asiyekusalieni ninyi hana sala. Naye Far-Zadaq amesema kuhusu kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume: "Katika kuwapenda wao hiyo ndiyo dini na kuwachukia ni kufuru, kuwa karibu nao ni jambo linalookoa na kuhifadhi.


Wakihesabiwa wachamungu wao watakuwa ndio Maimamu au isemwe nani aliye mbora hapa ardhini jibu litakuwa, Ni wao!" Basi Mashia wamempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na pendo lao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndilo lililo faradhisha pendo la watu wa nyumba ya Mtume ambao ni Fatmah, Ali, Hasan na Husein. Hadithi zinazohusu maana hii ni nyingi hazina idadi, na wamezithibitisha wanachuoni wa Kisunni ndani ya vitabu vyao na baadhi yake tumevitaja kwa ajili ya kufanya mukhtasari. Hivyo basi ikiwa kumpenda Ali na Ahlul-Bayt kwa ujumla ni kumpenda Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) basi tunawajibika kufahamu ukomo wa pendo hili linalotakiwa kutoka kwa Waislamu ili tufahamu kama kuna kuvuka mpaka kama wanavyodai.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema: "Hawezi kuwa muumini mmoja wenu mpaka mimi niwe mpendwa mno kwake kuliko mwanawe na mzazi wake na watu wote." Taz: Sahih Bukhar Juz. 1 uk. 9 (Babu Hubbir-Rasul Minal-iman), .Sahih Muslim Juz. 1 uk. 49, (mlango unaowajibisha kumpenda sana Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuliko jamaa, mtoto, mzazi na watu wote). Na kwa msingi huu basi Muislamu hanabudi kumpenda Ali na wanawe ambao ni Maimamu watakatifu (awapende) zaidi kuliko watu wote wakiwemo mke na watoto, na wala haitimii imani isipokuwa kwa kufanya hivyo, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema, "Hawi muumini mmoja wenu mpaka mimi niwe ni mpendwa mno kwake ..."


Hivyo basi Mashia hawavuki mpaka bali wanampa haki kila mwenye haki yake, na Mtume wa Mwenyezi Mungu amewaamuru wampe Ali daraja kama ile ya kichwa kwenye kiwiliwili, na daraja ya macho katika kichwa, basi je, kuna mtu anayepuuza macho yake au kichwa chake? Lakini kinyume chake ni kwamba kuna wanaovuka mpaka katika Masunni kwa kuwapenda Masahaba na kuwatakasa zaidi kuliko wanavyostahiki. Bali ukweli unaodhihiri ni kuwa tendo hilo' la Masunni kuvuka mpaka katika kuwapenda Masahaba ni kisasi dhidi ya Mashia ambao hawaitakidi juu ya uadilifu wa Masahaba wote, hali hii ni kwa kuwa Banu Umayyah walikuwa wanazipandisha daraja za Masahaba na kuporomosha heshima ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.), wakafikia kuwa kila wanapomsalia Muhammad na kizazi chake huwaongezea juu yao Masahaba wote, kwani ndani ya sala hiyo ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) kuna ubora ambao hakutangulia kuupata yeyote na hatoupata yeyote basi wakataka kuwanyanyua Masahaba wafikie daraja hiyo ya juu na wakasahau kwamba Mwenyezi Mungu amewaamuru Waislamu wakiwemo hao Masahaba wote wamsalie Muhammad, Ali, Fatmah, Hasan na Husein, na yeyote asiyewasalia sala yake haikubaliwi, Mwenyezi Mungu hataikubali ikiwa atamsalia Muhammad peke yake kama ilivyothibiti ndani ya Sahih Bukhar na Muslim.


Na tutaposema kwamba kufanya hivyo ni kuvuka mpaka, hiyo ni kwa sababu Masunni wanavuka mipaka ya kiakili pale wanaposema kwamba Masahaba wote ni waadilifu wakati Mwenyezi Mungu na Mtume wake wameshuhudia kwamba miongoni mwao Masahaba wamo Mafasiqq na wenye kutoka katika dini na wengine wamepotoka na ni wanafiki. Kuvuka kwao mpaka (Masunni) kuko wazi wakati wanaposema kwamba, "Mtume wa Mwenyezi Mungu anakosea na kusahihishwa na Sahaba, au kwamba shetani anacheza na kurukaruka mbele ya Mtume, lakini shetani huyohuyo anamkimbia Umar. Pia wanavuka mpaka pale wanaposema kwamba, "Lau Mwenyezi Mungu angewashushia msiba Waislamu akiwemo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, basi asingeokoka isipokuwa Ibn Al- Khatab." Na huko kuvuka mpaka kuko wazi mno kutokana na kupuuza kwao sunna ya Mtume (s.a.w.) na kufuata sunna ya Masahaba na hasa Khulafaur-Rashidina. Na bila shaka tumekubainishia baadhi ya hayo na kama utataka ziyada, basi huna budi kutafiti na kuzingatia ili ufahamu zaidi kuhusu mifarakano hii.


MAHDI ANAYENGOJEWA Jambo hili pia ni miongoni mwa maudhui ambazo Masunni wanafanya kebehi dhidi ya Mashia. Wako baadhi ya Masunni ambao wamefikia mpaka kudharau na kukejeli, kwani wao wanapinga au unaweza kusema wanaitakidi kuwa haiwezekani mtu kubakia muda wa karne kumi na mbili akiwa hai amejificha haonekani machoni mwa watu. Imefikia hadi, baadhi ya waandishi wa zama hizi wakasema kwamba "Mashia wamezusha fikra ya Imam aliyeghaib (aliyejificha) ambaye atawaokoa, na hiyo ni kutokana na dhulma nyingi na ujeuri waliopambana nao toka kwa watawala kwa muda mrefu, basi wakajifariji nafsi zao kwa tarajio la kuja Imam Mahdi anayengojewa ambaye ataijaza ardhi uadilifu na usawa na kulipiza kisasi kwa maadui zao".

Katika miaka ya hivi karibuni na baada ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kumekuwa na mazungumzo mengi kuhusu Mahdi anayengojewa, Waislamu na hasa vijana wasomi kila mahali wamekuwa wakiulizana juu ya ukweli wa Mahdi, kuwa je, jambo hilo linao ukweli na linapatikana katika itikadiza Kiislamu au ni miongoni mwa uzushi wa Mashia? Pamoja na kuwepo yaliyoandikwa na wanachuoni wa Kishia wa hapo zamani na wa sasa hivi-Kama vile Shahid Muhmmad Baqir As-sadr ndani ya kitabu chake kiitwacho Bah-thun haulal-Mahdi-kuhusu suala la Mahdi, pia bila kujali mawasiliano (ya Masunni) na ndugu zao Mashia ambayo ni ya miaka mingi katika mikutano mingi na mazungumzo baina yao yanayohusu maudhui mbali mbali za kiitikadi, maudhui hii ya Mahdi wao hawajazowea kusikia riwaya kama hizi. Basi ukoje ukweli kuhusu Mahdi ndani ya itikadi za Kiislamu?


Utafiti juu ya maudhui hii unagawanyika sehemu mbili: Sehemu ya kwanza itahusika na utafiti kuhusu Mahdi ndani ya Qur'an na Sunna. Na sehemu ya pili, itahusu utafiti juu ya maisha yake na ghaiba yake kutoonekana na kudhihiri kwake. Ama katika utafiti wa mwanzo, Mashia na Masunni wameafikiana kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alimbashiri Mahdi na akawajulisha Masahaba ya kwamba Mwenyezi Mungu atamdhihirisha katika zama za mwisho. Na hadithi zinazomuhusu Mahdi (a.s.) wote Mashia na Masunni wamezithibitisha ndani ya vitabu vyao na Musnad zao, nami kwa upande wangu kama ilivyo kawaida kwa namna nilivyo jilazimisha katika kila utafiti, sitoi dalili isipokuwa ile iliyothibiti na ni sahihi kwa Masunni.

Hivyo basi, imekuja ndani ya Sunan Abi Dawud: Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Lau kama haitabaki katika dunia isipokuwa siku moja Mwenyezi Mungu atairefusha siku hiyo mpaka amtoe mtu kutoka katika watu wa nyumba yangu jina lake linalingana na jina langu, na jina la baba yake ni jina la baba yangu, ataijaza ardhi usawa na uadilifu kama ilivyojazwa dhulma na ujeuri." Taz: Sunan Abi Dawud Juz. 2 uk. 422. Na imekuja ndani ya Sunan ibn Majah Juz. 2. hadithi na. 4082 na 4087, Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Sisi Ahlul-Bait Mwenyezi Mungu ametuchagulia akhera dhidi ya dunia, hapana shaka watu wa nyumba yangu baada yangu watakumbana na balaa kubwa na kufukuzwa mpaka waje watu fulani toka upande wa mashariki wakiwa na bendera nyeusi, wataomba amani hawatapewa, basi watapigana na watashinda, hivyo watapewa walichokiomba lakini hawatakikubali mpaka wakitoe kwa mtu miongoni mwa watu wa nyumba yangu, basi yeye atakijaza usawa kama kilivyojazwa ujeuri".


Na amesema ibn Ma'jah ndani ya Sunan yake: "Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Mahdi ni kutokana nasi Ahlul-Bait, Mahdi ni miongoni mwa watoto wa Fatmah" Na amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) "Katika Umma wangu atakuwepo Mahdi (atabaki) kama ni miaka midogo basi ni saba kama sivyo ni tisa Umma wangu utaneemeka humo neema ambayo haukupata kuneemeka mfano wake, utajiwa na chakula chake wala hawatokuwa wanahodhi kitu, mali zitakuwa tele siku hizo, mtu atamwambia Mahdi, Ewe Mahdi! nipe, atamwambia chukuwa."


Taz: Sunan ibn Majah Juz. 2 hadithi No. 4086. Na imekuja ndani ya Sahih Tirmidhi: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema: "Atatawala mtu toka katika watu wa nyumba yangu, jina lake linalingana na jina langu, na lau haitabaki katika dunia isipokuwa siku moja, basi Mwenyezi Mungu atairefusha siku hiyo mpaka atawale". Taz: Al-Ja'mius-Sahih Juz. 9 uk. 74-75. Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.): "Duniya haitaondoka mpaka awamiliki Waarabu mtu kutoka katika watu wa nyumba yangu, jina lake linalingana na jina langu". Taz: Sahih Bukhar Juz. 4 uk. 143, (Babu Nuzuli I'sa ibn Maryam).

Na ameandika Imam Bukhar ndani ya sahih yake amesema: "Ametusimulia bin Bakir, ametusimulia Al-Laith kutoka kwa Yunus naye toka kwa ibn Shihab naye kutoka kwa Nafii1 huru wa Abi Qatadah Al-Ansari ya kwamba, Abu Hurairah (r.a.) amesema, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema, mtakuwa na hali gani ninyi pindi mwana wa Maryam atakapokushukieni na Imamu wenu atatoka miongoni mwenu."? Na amesema mwenye Gha-yatul-Maa'mul: "Imekuwa (ni jambo) mashuhuri miongoni mwa wanachuoni wa hapo mwanzo na waliokuja baadaye kwamba hapo zama za mwisho ni lazima adhihiri mtu kutoka katika watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) aitwaye Mahdi."


Hadithi za Mahdi wamezisimulia jamaa miongoni mwa Masahaba wema na wakazithibitisha wanahadithi wakubwa kama vile Abu Dawud, Tirmidhi, ibn Majah, Tabrani, Abu Yaa'la, Imam Ahmad bin Hanbal na Al-Hakim, Mwenyezi Mungu awawiye radhi wote, na kwa hakika amekosea aliye zikosoa hadithi zote za Mahdi. Amesema Al-Hafidh ndani ya Fat-Hul-Bari: "Zimeenea kwa njia ya Mutawatir Khabari zisemazo kwamba Mahdi atatokana na umma huu, na kwamba I'sa mwana wa Maryam atashuka na ataswali nyuma yake." Taz: Fat-Hul-Bari Juz. 5 uk. 362. Na amesema ibn Hajar Al-Haithami ndani ya As-Sawa'iqul-Muhriqah: "Na hadithi ambazo zimekuja na ndani yake muna utajo wa kudhihiri Mahdi ni nyingi tena mutawatir."


Taz: As-Sawai'qul-Muhriqah ya ibn Hajar Juz. 2 uk. 211. Naye Shaukani ndani ya Risalatul-Musammat, akibainisha juu ya (hadithi) mutawatir zilizokuja kuhusu (Mahdi) anayengojewa na Dajjal na Masih na baada ya kuziorodhesha hadithi za Mahdi akasema: "Na hadithi zote tulizoleta zimefikia kiwango cha mutawatir kama isivyofichikana kwa mwenye ubora wa kuchunguza". Na amesema Sheikh Abdul-Haq ndani ya Lum-a'-t: "Kwa hakika hadithi ni nyingi mno zilizofikia kiwango cha mutawatir kuhusu Mahdi kwamba yeye ni kutoka katika watu wa nyumba ya Mtume miongoni mwa watoto wa Fatmah". Taz: Hashiyatu Sahih At-Tirmidhi, Juz. 2 uk. 42.


Naye As-Sabban amesema ndani ya kitabu chake kiitwacho Is-'afur-Raghibina: '"Kwa hakika khabari mutawatir (zimekuja) kutoka kwa Mtume (s.a.w.) kuhusu kutokea kwake (Mahdi) na kwamba atatokana na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) na kwamba ataijaza ardhi uadilifu". Taz: Is-A'fur-Raghibina Juz. 2 uk. 140. Na As-Suwaidi amesema ndani ya kitabu chake kiitwacho, Saba-Ikud-Dhahab uk. 78. "Kauli waliyoafikiana wanachuoni ni kwamba Mahdi ndiye atakayesimama zama za mwisho, na kwamba ataijaza ardhi uadilifu, na hadithi zinazohusu kudhihiri kwake ni nyingi". Naye ibn Khaldun ndani ya Muqaddimah yake amesema: "Fahamu ya kwamba (kauli) iliyo mashuhuri baina ya Waislamu kwa zama zote ni kuwa katika zama za mwisho, hapana budi adhihiri mtu kutoka katika watu wa nyumba ya Mtume atakayeitia nguvu dini na atadhihirisha uadilifu na anaitwa Mahdi". Taz: Muqaddimatu Ibn Khaldun uk. 367.


Kama ambavyo amezithibitisha hadithi za Mahdi mwanachuoni wa zama hizi mufti wa Ikhwanul-Muslimina Sayyid Sa-biq ndani ya kitabu chake kiitwacho, "Al-A 'qaaidul-Islamiyyah " na amesisitiza kwamba fikra ya Mahdi ni miongoni mwa itikadi za Kiislamu ambazo ni wajibu kuziamini. Na vitabu vya Kishia pia vimethibitisha hadithi zinazomuhusu Mahdi kwa wingi mpaka ikasemwa kwamba, hapakupokelewa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu hadithi nyingi kuliko zilizopokelewa toka kwake kuhusu Mahdi. Na ametoa mtafiti aitwaye Lutfullahis-Safi ndani ya Mausuat yake iitwayo, "Muntakhabul-Athar" rejea zaidi ya sitini toka vitabu vya Kisunni hadithi zinazomuhusu Mahdi (a.s.) ndani yake zimo sihah sita, na zaidi ya rejea tisini toka vitabu vya Kishia ndani yake vimo vitabu vinne.

Ama kuhusu utafiti wa sehemu ya pili ambao unahusu kuzaliwa kwa Mahdi, maisha yake, ghaibah yake na kwamba hajafa, sehemu hii pia baadhi ya wanachuoni wa Kisunni wanaoheshimika hawakuipinga, na ndiyo ambao wanaitakidi kwamba Mahdi ni Muhammad bin Al-Hasan Al-A'skari, ambaye ni Imamu wa kumi na mbili miongoni mwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) amekwisha zaliwa na yungali hai na atadhihiri zama za mwisho na kuujaza ulimwengu uadilifu na usawa na Mwenyezi Mungu atainusuru dini yake kupitia kwake (Mahdi), hivyo basi wanachuoni hao wa Kisunni wanaafikiana na kauli za Mashia Imamiyyah.

Miongoni mwa wanachuoni hao ni hawa wafuatao: 1. Muhyid-din bin Al-Arabi-ndani ya Futuha'til-Makiyyah.
2. Sib-ti bin Al-Jauzi ndani ya kitabu chake kiitwacho,
3. Tadh-Kiratul-Khaw-was.
3. A'bdul-Wahab Ash-Shaa'rani ndani ya kitabu chake kiitwacho Aqaidul-Akabir.
4. Ibnul-Khash-Shab ndani ya kitabu chake kiitwacho,"Tawarikh Mawalid Al-Aimmah Wawafiyya-tihim."
5. Muhammad Al-Bukhari Al-Hanafi ndani ya Kitabu chake Faslul-Khitab.
6. Ahmad bin Ibrahim Al-bala-dhuri, ndani ya kitabu chake kiitwacho, Al-Hadithul-Mutasal-sal
1. Ibnus-Sabbagh al-Maliki, ndani ya kitabu chake kiitwacho, Al-Fusulul-Muhimmah.
8. Al-A'rif A'bdur-Rahman ndani ya kitabu chake Mir- atul-as-rar.
9. Kama-lud-din bin Tal-hah ndani ya kitabu chake kiitwacho Matalibus-suul Fi Manaqib Alir-Rasul. l0. Al-Qanduzi Al-Hanafi ndani ya kitabu chake kiitwacho, Yanabiu'l-Mawaddah.
Na lau mwenye kutafiti atafuatilia atawakuta wanachuoni wa Kisunni zaidi ya hawa tuliowataja ambao wanazungumzia kuzaliwa kwa Mahdi na kubakia kwake hai mpaka Mwenyezi Mungu amdhihirishe. Na baada ya haya hakuna wanaobakia miongoni mwa Masunni isipokuwa wale wanaopinga kuzaliwa na kubakia kwake hai baada ya kukiri kwao kusihi kwa hadithi, na hawa siyo hoja dhidi ya wengine wanaokubaliana na suala hili. Nayo Qur'an Tukufu haikanushi wazo hili, na ni mara nyingi Mwenyezi Mungu ametoa mifano juu ya jambo hilo kwa watu wenye akili ngumu ili wajikwamue na kuzipa uhuru fikra zao na akili zao ili ziyakinishe na kukubali kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni muweza juu ya kila kitu.


Kwa hiyo basi Muislamu ambaye moyo wake umejaa imani haoni ajabu kuwa Mwenyezi Mungu kumfisha Uzair kwa muda wa miaka mia moja kisha akamfufua ili akiangalie chakula chake na kinywaji chake ambavyo havijaharibika, na punda wake namna gani Mwenyezi Mungu anavyoinyanyua mifupa yake na kuivisha nyama na kuirudisha kama ilivyokuwa baada ya kuwa mifupa yake hiyo imechakaa, basi pindi ilipombainikia akasema: "Nimefahamu kwamba Mwenyezi Mungu ni muweza juu ya kila kitu". Sub-hanallah!! alibadilika kwa haraka mtu huyu, wakati hapo kabla ya tukio hili alipopita kwenye kijiji kilichokufa alishangaa na kupinga akasema: "Ni vipi Mwenyezi Mungu atakifufua kijiji hiki baada ya kufa kwake"?

Na Muislamu anayeisadiki Qur'an Tukufu hashangai kuwa Bwana wetu Ibrahim kumkatakata ndege na kuvitawanya viungo vyake na manyoya yao juu ya jiwe kisha akaviita vikamjia mara moja. Pia Muislamu hashangai moto kupoa usimuunguze wala kumuudhi Bwana wetu Ibrahim wakati alipotupwa ndani ya moto huo na Mwenyezi Mungu akauambia, "Ewe moto kuwa baridi na salama ". Si hivyo tu Muslamu hashangai kwamba Bwana wetu I'sa amezaliwa bila mbegu ya kiume yaani bila baba na kwamba yu hai hakufa na atarudi ulimwenguni. Kadhalika Muislamu hashangai ya kwamba Bwana wetu I'sa alikuwa akiwafufua watu na kuwaponya vipofu na wenye mbaranga, na pia Muislamu hashangai juu ya kufunguka bahari kwa ajili ya Bwana wetu Musa na wana wa Israeli wakapita bila kulowana na fimbo ya Musa kugeuka nyoka na maji ya mto Nile kugeuka na kuwa damu.


Vile vile Muislamu hatoshangaa ya kwamba Bwana wetu Sulaiman alikuwa akizungumza na ndege na majini na kuchukuliwa kiti chake kubebwa kwenye busati la upepo, na kukisimamisha (mbele yake) kiti cha Bal-Qis kwa muda mfupi. Wala Muislamu hashangazwi juu ya Mwenyezi Mungu kwamba aliwafisha As-Habul-Kahfi kwa karne tatu na wakazidisha tisa kisha akawafufua basi kipindi hicho mjukuu wa mjukuu alikuwa ni mkubwa kwa umri kuliko Babu wa Babu. Wala hatoshangaa Muislamu ya kwamba Sayydina Al-Khidhr (a.s.) yu hai hakufa na alikutana na Bwana wetu Musa (a.s.). Na pia Muislamu hatoshangaa ya kwamba Ibilisi aliyelaaniwa na Mwenyezi Mungu yu hai hajafa naye ni kiumbe aliyeumbwa kabla ya Adam (a.s.) mpaka sasa angali anafuatilia nyendo za mtu tangu mwanzo wa kuumbwa kwake mpaka kufa kwake. Pamoja na hayo Ibilisi amejificha licha ya matendo yake machafu na kazi zake mbaya, na yeye anawaona watu wote. Kwa hakika Muislamu anaamini yote haya wala hashangai kutokea kwake. Basi je, hivi Muislamu atashangazwa na kuwepo kwa Mahdi ambaye amefichikana kwa kipindi fulani kutokana na hekima aitakayo Mwenyezi MunguMtukufu?

; Basi yote yaliyotajwa na Qur'an ambayo ni mengi mno kuliko tuliyoyataja sisi katika ufupisho huu ni miongoni mwa mambo yaliyo nje ya mazowea yanayofahamika, wala si katika mambo waliyoyazowea watu, wala hawawezi kuyafanya hata kama watashirikiana. Bali ni miongoni mwa uumbaji wa Mwenyezi Mungu ambaye hapana kinachomshinda duniani wala mbinguni, na Waislamu wanaamini hilo kwani wao wameamini yote yaliyokuja ndani ya Qur'an tukufu bila kuchagua wala kupinga. Na kwa kuwa Mashia wao ndiyo wanayafahamu zaidi mambo ya Mahdi (a.s.) kwa kuwa ni Imam wao na wameishi naye yeye na wazazi wake. (Kuna mithali husemwa): "Watu wa Makkah ndiyo wanaovifahamu mno vichochoro vyake". Mashia wanawaheshimu Maimamu wao na kuwatukuza na wameyatengeneza na kuyajengea makaburi ya Maimamu wa nyumba ya Mtume na wamejilazimisha kuyatembelea (kuyazuru) na kutabaruku kwayo. Basi lau Imam wa kumi na mbili ambaye ni Mahdi (a.s.) angekuwa amekufa basi kaburi lake lingekuwa linatambulikana, na wangeweza kusema kuwa inajuzu kufufuka baada ya kufa maadamu jambo hili linawezekana, kama ilivyoeleza Qur'an na hasa kwa kuwa wanaitakidi Raja'h. Lakini utawaona Mashia wanakazia kusema kwamba Mahdi (a.s.) yu hai na anaruzukiwa na amejificha kwa hekima aliyotaka Mwenyezi Mungu Mtukufu hekima ambayo wanaweza wakaifahamu wale waliobobea katika elimu na Mawalii wake.


Kadhalika Mashia huomba ndani ya Sala zao Mwenyezi Mungu aiharakishe Faraja yake tukufu kwani katika kudhihiri kwake ni heshima kwa waislamu na ni mafanikio yao na ushindi wao na kwa kupitia kwake Mwenyezi Mungu ataitimiza nuru yake japokuwa makafiri watachukia. Kwa hiyo tofauti iliyopo baina ya Sunni na Shia' juu ya suala la Mahdi (a.s.) siyo tofauti ya msingi maadam wote wanaitakidi juu ya kudhihiri kwake hapo zama za mwisho na kwamba I'sa (a.s.) ataswali nyuma yake. Pia Mahdi ataijaza dunia usawa na uadilifu kama ilivyojazwa dhulma na ujeuri, na Waislamu wataimiliki dunia yote katika zama zake na neema zitaenea asibakie hata masikini mmoja.

Tofauti pekee inayobakia ni kuhusu kauli ya Mashia juu ya kuzaliwa kwake na kauli ya Masunni kwamba atazaliwa hapo baadaye na kauli za makundi haya zinakutana kwenye kudhihiri kwake katika zama za mwisho. Hivyo basi Waislamu na washikamane kwenye neno la kweli na kuimarisha umoja wa umma ambao umesambaratika na wote wamuombe Mwenyezi Mungu kwa ukweli kabisa katika maombi yao na katika kila sala zao ili Mwenyezi Mungu amdhihirishe kwa haraka, kwani kudhihiri kwake ni faraja na ni ushindi kwa umma wa Mtume Muhammad (s.a.w.). Na maombi yetu ya mwisho ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, na sala na salamu zimshukie Mtukufu wa Mitume na Manabii Bwana wetu na msimamizi wetu Muhammad na pia kizazi chake (watu) walio wema tena watakatifu. Muhammad Tijani As-Samawi

REJEA ZILIZOTUMIKA Vitabu vya Tafsir: 1. Qur'an Tukufu
2. Tafsir At-Tabari
3. Tafsir ibn Kathir
4. Tafsir Qur-Tubi
5. Tafsir Jalalain
6. At-Tafsirul-Kabir ya Fakhrur-Razi.
7. Tafsirul-Manar ya Muhammad Abd.
8. Tafsirun-Nasfi
9. Tafsirul-Kha-zin
10. Tafsirul-Kash-Sha'f ya Zamakh-shari
11. Tafsirul-Hakim Al-Haskani
12. Tafsirun-Naisa-Buri
13. Ad-Durrul-Manthoor Fit-Tafsir Bil-Maathur ya Suyuti
14. Za-Dul-Masir Fi Ilmit-Tafsir ya ibn Al-Jauzi
15. Shawahidut-Tanzil ya Al-Hakim Al-Haskani
16. Tafsiru Fat-Hil-Qadir ya Al-Haskani
17. At-Tas-Hil Lil-Ulumit-Tanzil ya Al-Kal-bi
18. As-Babun-Nuzul cha Al-Wahidi
19. Ahkamul-Qur'an cha Al-Jas-Sas
20. Tafsirul-Kabir cha At-Thaalabi
21. Nuzulul-Qur'an cha Al-Hafidh Abu Nuaim
22. Maa, Nazala Minal-Qur'an Fii Ali, Abu Nuaim Al-Is-Bahani
23. Muqaddimatu Usulit-Tafsiri cha ibn Taimiyyah
24. Tafsirul-Mizan cha Al-Allama Tabatabai.

Vitabu vya hadithi: 1. Sahih Bukhar
2. Sahih Muslim
3. Sahih Tirmidhi
4. Sahih ibn Ma-jah
5. Sunan Abi Dawood
6. Sunanun-Nasai
7. Musnad Imam Ahmad
8. Muwatt'a ya Imam Malik.
9. Mustadrak Alhakim.
10. Kanzul-Ummal.
11. Sunan Ad-darami
12. Sunan Albaihaqi
13. Aljam'u bainas-sihahis-sittah.
14. Sunan Ad-darami.
15. Jam'ul-jawami'i
16. Min-hajus-sunnah cha ibn Taimiyyah.
17. Maj-ma'uz-zawaid cha Al-haithami.
18. Kunuzul-haqaiq cha Al-manawi.
19. Jami'ul-usul cha ibn Al-athir.
20. Fat-hulbari Fi-Sharhil-Bukhari

Vitabu vya Tarikh: 1. Tarikhul-umami Wal-muluk ya At-tabari.
2. Tarikhul-khulafai cha Suyut.
3. Tarikhul-kamil ya ibn Al-athir.
4. Tarikh Dimishqi ya ibn Asakir.
5. Tarikhul-Mas'udi (Murujudhahabi)
6. Tarikhul-Yaqubi
7. Tarikh Baghdad cha Khatib Baghdad
8. Tarikh Abul Fidaa
9. Tarikh ibn Shahnah
10. Tarikh ibn Kathir
11. Tarikhul-Kabir ya Muhammad Bukhari
12. Al-Imamah wa As-siyasah
13. Al-Iqdul-Farid ya ibn Abdu Rabih
14. Atabaqatul-Kubra ya ibn Saad
15. Tarikh ibn Khaldun
16. Sharh Nahjul-Balagha ya ibn Abil-Hadid

1. Siratu ibn Hisham
2. Al-isabah fi Tamyiz Sahabah
3. Siratul-Halabiyah
4. Usudil-Ghabah fi maarifat Sahabah
5. Siratu Dahlaniyah
6. Ar-riyadhu An-nadharah ya Tabari
7. Al-Istiabu
8. Hayatu Muhammad ya Muhammad Husain Haikal
9. Al-Maarif ya ibn Qutaibah
10. Ansabul-Ashraaf yaBalaadhuri
11. Hilyatul-Auliyai ya Abu-Nuaim
12. Al-Fitnatul Kubra ya Twaha Husain

Aina mbalimbali ya vitabu: 1. As-sawaiqul-Muhriqah cha ibn Hajar
2. Al-futuhatul-Makiyah cha ibn Arabi
3. As-silatu Baina Tasawufi wa-Tashayui cha Shaid
4. Akaidul-Akabir cha Sha'awani
5. Khasaisu Amiril-muuminina cha Nasai
6. Tawarikhu Mawalidil-Aimah cha ibn Khishab
7. Al-milalu Wan-nihal cha Shahirstani
8. Fas-lul-Khitabi cha Bukhari
9. Dalailul-Imamah cha Tabari
10. Al-hadithul-Mutasal-salu cha Al-Balaadhuli
11. Balaghatun-Nisai cha ibn Taighur
12. Mir-atul-Asraril-arif cha Abdurahman
13. A'alamun-Nisai cha Umar Ridha Kuhalah
14. Ihqaqul-Haqi cha Tustari
15. Kifayatut-Talib cha Al-Kanji Ashafii
16. Sharhul-Mawahib cha Zirqani
17. Al-Izdihar fi maaqadahus-Shuarau Minal-Ash-ari cha Suyuti
18. Siratu A'alamin-Nubalai cha Dhahabi
19. Al-wilayatu cha ibn Jariri Tabari
20. Sirul-Alamina cha Abu-Hamid Al-ghazali
21. Tadhkiratul-Khawasi cha ibn Jawzi
22. Ihyau Ulumid-diin cha Ghazal
23. Tadhkiratus-Sibti ibn Jawzi
24. Matalibus-Suuli cha ibn Talha Ashafii
25. Irshadus-Sari cha Qastalani
26. Yanabiul-Mawadah cha Al-Qanduzi Al-Hanafi
27. Nurul-Absari cha As-shablanji

________________________________________
[1]-Mfano: Bismillah katika sala ni makruhu kuisoma kwa mujibu wa Malik, na ni wajibu kwa Shafii, ni Sunna kwa Hanafi, na Hanbal wamesema isidhihirishwe katika sala zajahara
[2]-Sahih Bukhari Juz. 2 uk. 47, Juz. 5 uk. 179 na Juz. 6 uk. 33.
[3]-Sahih Bukhari Juz. 4 uk. 226, Juz.5 uk.47-48, Sahih Muslim Juz. 1 uk. 114 -122.
[4]-Sahih Bukhari Juz. 8. uk. 197
[5]-Sahih Bukhari Juz. 8. uk. 182.
[6]-Sahih Bukhari Juz. 8. uk. 187. Na katika uk. 202 anathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ana mkono na vidole.
[7]-Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) wameifasiri aya hii kwamba, nyuso siku hiyo zitapendeza na kung'ara zikingojea rehma za Mola wao (neno"Nadhirah" kwa maana ya kupendeza na kung'ara).
[8]- Nahjul-Balagha Sharh ya Muhammad Abdoh Juz. 1 Khotba na. I
[9]-9 Kitabu cha "Al-Murajat ni miongoni mwa vitabu ambavyo ni wajibu akisome kila mtu anayetaka kufahamu itikadi za Shia Imamiyyah na fikra zao.
[10]-Sahih Bukhari Juz. 7 uk. .29.
[11]- Sahih Bukhari Juz. 4 uk. 68,
[12]- Sahih Bukhari Juz. 1 uk. 123
[13]- Sahih Bukhari Juz. 1 uk. 37, na uk. 44 na 171.
[14]- Sahih .Muslim mlango wa Fadail Uthman Juz. 7 uk. 117
[15]-Sahih BukhariJuz. 2 uk, 232 na uk. 234.
[16]- Sahih Bukhari Juz. 3 uk. 114 na Juz. 7 uk. 96.
[17]- Sahihi Bukhari Juz. 3 uk. 228 na Juz. 2 uk. 3 Kitabul-Idain.
[18]- Sahihi Bukhari Juz. 3 uk. 228 na Juz. 2 uk. 3 Kitabul-Idain
[19]-Musnad Imam Ahmad bin Hambal Juz. 6 uk. 75.
[20]- Tafsir Al-Jalalain katika tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo."Unaficha yaliyomo nafsini mwako ambayo Mwenyezi Mungu anayadhihirisha.
[21] - Sahih Muslim Juz. 7uk.
[22]- Bukhari ameandika ndani ya kitabu chake Juz. 3 uk. 152 mlango wa shahada ya kipofu kutoka Kitabus-Shahadat amesema ametusmulia Ubeid bin Maimun, ametueleza Isa kutoka kwa bibi Aisha amesema: "Mtume (s.a.w.) alimsikia mtu akisoma msikitini basi akasema Mwenyezi Mungu amrehemu kwa hakika amenikumbusha aya fulani niliyoisahau kutoka katika sura fulani.
[23]-Tirmidhi na Abu Dawud na Ibn Majah na Musnad ya Ahmad Bin Hanbal Juz. 2uk.332.
[24]- Sahihi Bukhar Juz. 7 uk. 209 Babul-Haud na Juz. 5 uk. 192.
[25]Sahihi Bukhari Juz. 4 uk. 63.
[26]-Sahih Bukhar Juz. 7 uk. 112.
[27]-Sahih Bukhar Juz. 4 uk. 144 na Juz. 8 uk. 151
[28]-Sahih Bukhar Juz. 8 uk. 26 Babu Rajmil-Hubla Minaz-zina.
[29]--Tarikhul-Khulafai cha Ibn Qutaibah Juz. 1 uk. 18 na zinazofuata.
[30]-Fat-hul-Bari Juz. 6 uk. 31, Al-Bidayatu Wan-Nihayah Juz. 8 uk. 102 Sair Aa'la-Min-Nubalai cha Dhahabi Juz. 2 uk. 436, Al-Isabah cha Ibn Hajar Juz. 3 uk. 287.
[31]-Ad-Durrul-Manthur cha Suyuti Juz. 3 uk. 3.
[32] - Qur'an, 43:78
[33]- " 69:49
[34] -" 4:165
[35] - Kitabu cha alghadir kilichoandikwa na Al-allaama Al-amin kinajuzuu kumi na moja na ni kitabu madhubuti, mwandishi amekusanya kila kinachohusu hadithi ya Ghadir kutoka ndani ya vitabu vya Kisuni.
[36]- Maimu Bukhari na Muslim wameandika upinzani wa aina nyingi uliofanywa na masahaba k.m,katika sulhu ya Hudaibiya,katika msiba wa siku ya Alkhamisi na mengineyo
[37]- Kwa sababu wao wanaamini kwamba Masahaba ni kama nyota, yeyote mtakayemfuata mtaongoka.
[38] - Soma Kitabu kiitwacho Abdallah bin Sabai cha Allamah Al-Askari ili ufahamu kwamba huyu Abdallah bin Sabai hakupata kuwepo duniani bali ni katika watu walioumbwa (kuzushwa) na Seifbin Umar At-Tamimi ambaye ni mashuhuri kwa kuzusha na kuweka (yasiyokuweko) na pia soma Kitabu kiitwacho Al-Fitnatul-Kubra' cha Taha Husain na ukitaka soma Kitabu 'Kiitwacho As-Silatu Baynat-Tasawwuf Wat-Tashayui' cha Doctor Mustafa Kamil As-Shaybi ili ufahamu kwamba Abdallah bin Sabai huyu asemwaye si mwingine bali ni Sayyidna Ammar Bin Yasir (r.a.)
[39]- Mama Aisha alikuwa hawezi kumtaja Ali Jina lake, Taz: Bukhar Juz.l uk 161, Juz.l uk.18, Juz.5 uk. 140. Na wanahistoria wanasema mama Aish zilipomfikia khabari za kuuawa kwa Ali (a.s.) alisujudu kumshukuru Mwenyezi Mungu na alisoma mashairi kuhusu tukio hilo.
[40]- Ameiandika kwa ukamilifu khutba hii Al-Hafidh Ibn Jarir At-Tabari Ndani ya Kitabul-Wilayah, kama ambavyo ameiandika Jalalud-Din Suyuti ndani ya Ad-Durrul-Mathur Juz. 2 uk. 298.
[41]- Taz: Al-Hakim Al-Haskani kutoka kwa Abuu Said Al-Khudur katika tafsiri yake kuhusu aya hii na Al-Hafidh Abu Nuaim Al-Is-Bahani ndani ya Kitabu chake "Ma Nazala Minal-Qur'an Fi Ali".
[42]- Wamekisimulia kisa hiki Imam Abu Hamid Al-Ghazali katika kitabu chake Sirul-Alamina uk. 6, Imam Ahmad bin Hambal ndani ya Musnad yake Juz. 4 uk. 281, Tabari ndani ya tafsiri yake Juz. 3 uk. 428, Baihaqi, Daraqutni, Fakhrur-razi na ibn Kathir na wengineo.
[43]- Al-Hafidh Abu-Nuaim Al-isbahani ndani ya kitabu chake Maanazala Minal-Qur'an fi Ali, Al-Khawarzami ndani ya kitabu Manaqib uk. 80, Al-Kanji Ashafii ndani ya Kifayatut-talib na Jalalud-din Suyuti ndani ya kitabu chake Al-Izdiharfi maa-Aqadahu Ashuarau minal-Ash-ari.
[44]- Tabari ndani ya Tarikh yake Juz. 5 uk. 31, Tarikh ibn Athir Juz.3 uk.31. Shark Nahjul-Balaghah ya ibn Abil-Hadid Juz. 2 uk. 18.
[45]- Musnad Imam Ahmad bin Hambal Juz. 4 uk. 370, na Juz. 1 uk. 119, An-nasai ndani ya Khasais uk. 19 Kanzul Umal Juz. 6 uk. 397, ibun Kathir ndani ya tarikh yake Juz. 5 uk. 211, ibn Athir ndani ya Usudid-ghabah Juz.4 uk. 28 na ibn Hajar Al-Asqalani ndani ya Isaabah Juz. 2 uk. 408, na Suyuti ndani ya Jam 'ul-Jawami 'i.
[46]- Maj-mauzawaid kitabu cha Al-haithami Juz. 9 uk.106, Ibn Kathir katika tarekh yake Juz. 5 uk. 21, Ibn Al-Athir ndani ya Usudul-ghabah Juz. 3 uk. 321,
Hiliyatul-Auliyai Juz.5 uk. 26, Ahmad bin HambalJuz. 1 uk. 119.
[47]- Sahih Bukhari Juz. 8 uk. 26, Babu Rajmil-Hubla Minaz-Zina.
[48]- Tarikh Tabari na ibn Athir baadaya kifo cha Umar bin Hatab na Ukhalifa wa Uthman
[49]- Shark Nahjul-Balaghah ya Muhammad Abdoh Juz. 1 uk. 88.
[50]- Tarikh Tabari na Ibnul-Athir katika Matukio ya mwaka wa 36 Hijiriyyah, Muhammad Abdoh Shark Nahjul-Balaghah Juz.luk. 88.
[51]- Tabari ndani ya Dalailul-Imamah Balaghatun-Nisai A 'lamun-Nisai utunzi wa Umar Ridha Kuhalah Juz. 4 uk. 123 na ibn Abil-Hadid ndani ya Shark Nahjul-Balaghah
[52]- Sahih_ Bukhari Juz. 8 uk. 26, Tarikh Tabari na Tarikh Alkhulafau ya ibn Qutaibah
[53]- Wanahistoria wote wameeleza kwamba hawakuhudhuria Saqifah isipokuwa
Muhajirina wanne, kwa hiyo aliposema, mimi nikampa baia na Muhajirina wakampa baiainapingana na kauli yake aliposema: Walitupinga sisi Ali na Zubair na waliokuwapamoja nao. Amesema hayo ndani ya hotuba He He, angalia Sahihi Bukhari Juz. 8 uk. 26.
[54]- ' Sahih Bukhari.Juz.8 uk 26
[55]- Sahih Bukhari Juz,8 uk 26
[56]- Sahih Bukhari Juz,8 uk 26.
[57]- Tarikh Tabari-Istikhlaf Umar bin Hatab, Shark Nahjul-Balaghah ya ibn Abil- Hadid Juz. 1
[58]- Sahihi Muslim Juz. 5 uk. 75 (Kitabul-Wasiyah), Sahihi Bukhari Juz. 7 uk. 9.
[59]- Sahihi Bukhari Juz. 4 uk. 195
[60]- Sahihi Bukhari Juz. 8 uk. 28, Tarikh Al-Khulafaa Juz. 1 uk. 19.
[61]- Sahihi Bukhari Juz. 8 uk. 25.
[62]- Sahihi Muslim Juz. 6 uk. 2-3, Sahih Bukhari Juz. 8 uk. 27.
[63]- Sahihi Muslim Juz. 6 uk. 2-3, Sahih Bukhari Juz. 8 uk. 27.
[64]- Sahih BukharJuz. 2 uk. 81, Sahih Muslim Babu Sul-Hul Hudaybiyyah
[65]- Sahihi BukharJuz. 2 uk. 76
[66]- Sahih BukharJuz. 1 uk. 37.
[67]- Sahih Bukhar Juz. 1, Babu Man Laqiya llah Bil-Iman Wahuwa Ghairu Sha-Kinfih Dakhalal Jannah uk. 45.
[68]- Sahih Muslim Juz. 1 uk. 61.
[69]- Sahih BukhariJuz. 3 uk. 168.
[70]- Musnad Ahmad Juz. 5 uk. 25 na Mustadrak Al-Hakim Juz 3 uk. 124
[71]- Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 126
[72]- Muntakhab Kanzul-Ummal Juz. 5 uk. 34.
[73]- Sharh Nahjul-Balaghah cha ibn Abil Hadid ndani ya utangulizi.
[74]- Sharh Nahjul-Balaghah cha ibn Abil Hadid ndani ya utangulizi.
[75]- Sharh Nahjul-Balaghah cha ibn Abil Hadid ndani ya utangulizi.
[76]- K.m, Hadithi ya kuwafuata Wayahudi na Wakristo shubiri baada ya shubiri na dhiraa baada ya dhiraa
[77]- K.m. Kauli ya Mwenyezi Mungu, Akifa au akiuawa mtageuka kwa visigino vyenu (muwe makafiri kama zamani)? Qur. 3:144.
[78]- Shawahidut-Tanzil cha Al-Haskani Juz. 2 uk. 286, Tafsirut-Thaalabi katika sura ya Saala Sailunbiadhabin Waqii, Tafsir Al-Qur-Tubi Juz. 18 uk. 278, Tafsir Al-Manar ya Rashid Ridha juz. 6 uk. 464, Yanabiul-Mawaddah ya Al-Qanduzi Al-Hanafi uk. 328, Al-Hakim ndani ya Mustadrak yake juz. 2 uk. 502, As-Siratul-Halabiyyah juz. 3 uk. 275, Tadhkiratul-Khawas cha Ibn Al-Jauzi uk. 37
[79]- Ansabul-Ashraf cha Al-Balaadhuri Juz. I nay a pill uk. 152.
[80]- Tarikh ibn Asakir inayoitwa Tarikh Dimishqi Juz. 2 uk. 7 na Juz .3uk .150,Sharh Nahjul-Balaghah ya ibn Abil Hadid uhakiki wa Muhammad Abul- Fadhli Juz. 19 uk. 217, Abaqatul-Anuwari Juz. 2 uk. 309, Manaqib Ali ibn Abi Talib cha ibn Maghazili Ashafii uk. 23 na Siratul-Halabiyah Juz. 3 uk. 337.
[81]- Ni katika siku ile ya Ruhbah ambapo Imam Ali (a.s.) aliwataka Masahaba washuhudie hadithi ya Ghadir na wamelisimulia tukio hili wanahadithi wengi na wanahistoria wengi kama tulivyotangulia kueleza, kama vile Ahmad bin
Hambal, ibn Asakir, ibn Abil-Hadid na wengineyo.
[82]- Bukhari na Muslim wamesimulia idadi yao, na katika Yanabiul-Mawadah amesimulia idadi na majina Juz. 3 uk. 99.
[83]-Inaashiria kutofautiana kwao katika kumpiga vita mwenye kuzuia zaka. Na hilo tumekwisha lionesha kwenye rejea, basi nawe rejea huko.
[84]- Inaashira kisa cha Fadak na hadithi isemayo: Sisi Mitume haturithiwi. Na hilo tumeliashiria kwenye rejea.
[85]- Inaashiria kisa cha kumnyonyesha mtu mzima alichokisimulia mama Aisha na wakampinga wake wengine wa Mtume (s.a.w.).
[86]- Inaashiria riwaya isemayo Mtume alikuwa akiamka na janaba. Riwaya ambayo mama Aisha ameipinga.
[87]- Inaashiria riwaya isemayo Mtume alifanya Umra mara nne (4) mojawapo katika mwezi wa Rajab, na ameipinga riwaya hii mama Aisha.
[88]- Inaashiria kutofautiana kwao katika uhalali wa Mut'a na uharamu wake."Angalia Bukhari Juz. 6 uk. 129."
[89]- Inaashiria kutofautiana kwao kuhusu Mut'a ya Hija. "Angalia Bukhari juz. 2 uk. 153."Ni kuhusu Bismillah katika udhu na katika sala ya msafiri, na katika masa-ala mengi ya kifiqhi ambayo haiwezekani kuyadhibiti yote.
[90]- Sahih Muslim Juz. 8 uk. 44.
[91]- Imam Sharafud-din amekusanya ndani ya kitabu choke kiitwacho An-nas wal-Ijtihaad,mambo zaidi ya mia moja ambayo wameyabadilisha wakati yanazo hukmu za kitabu na Sunna zilizo wazi.
[92]- Nahjul-Balaghah ya Imam Ali Juz. 1 uk. 155. Amefafanua Sheikh Muhammad Abdoh katika Shark ya hotuba hii akasema: "Hakika anakufa mwenye kufa miongoni mwa Maimamu wa nyumba ya Mtume hali ya kuwa ukweli hajafa kutokana na kubakia roho yake yenye nuru inayoangaza katika ulimwengu."
[93]- Kitabu kiitwacho Fas-lul-khitab si miongoni mwa vitabu vya kutegemewa kwa Mashia, wakati ambapo riwaya zakupungua Qur'ani na kuzidi zimeandikwa ndani ya vitabu vya Kisunni kama vile Bukhar, Muslim na Musnad cha Imam Ahmad.
[94]- Bukhari Juz.2uk.252.
[95]- Musnad Imam Ahmad bin Hambal Juz. 5uk.l31
[96]- Sahih Bukhar Juz. 4 uk.215
[97]- Musnad Imam Ahmad ibn Hanbal. Juz. I. uk. 221.
[98]- Muwatta Imam Malik (Sharhul-hawalik) Juz. 1 uk.161.
[99]- Sahih Muslim Juz. 2 uk. 151. (Babul-jam'i Bainas-salatain fil-hadhr)
[100]- Sahih Muslim Juz. 2 uk. 152.
[101]- Inasimuliwa kwamba kuna jamaa wawili walikwenda kuwinda kwa mbali wakaona weusi mmoja akasema bila shaka yule ni kunguru,huyu wapili akmpinga mwenzake akasema huyo ni paa wakapingana na kila mmoja akang'ang'ania msimamo wake. Walipoukaribia ule weusi kumbe ni kweli alikuwa kunguru akaruka. Yule wa mwanzo akasema: Je, sikukuambia kwamba yule ni kunguru? Sasa umeamini? Lakini rafiki yake aliendelea kung'ang'ania msimamo wake na akasema "Sub'hanallah paa huyo anaruka!!16