ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI 20%

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI Mwandishi:
Kundi: Midahalo na majadiliano kielimu

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI
  • Anza
  • Iliyopita
  • 21 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 37847 / Pakua: 4635
Kiwango Kiwango Kiwango
ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

Mwandishi:
Swahili

1

2

3

4

5

6

7

8

13

ILI NIWE PAMOJA NA WAKWELI

MUT'A (AU NDOA YA MUD A)

Kinachokusudiwa ni ndoa ya Mut'a au ndoa ya muda au ndoa ya wakati maalum, na ndoa hii ni sawa na ndoa ya kudumu, kwani haisihi isipokuwa kwa mafungamano yanayokusanya Qabul na I'jab, kwa mfano mwanamke aseme, "Nimekuozesha nafsi yangu kwa mahari kiasi kadhaa," Basi na mwanamume aseme "Nimekubali." Na ndoa hii inazo sharti zake ambazo zimetajwa ndani ya vitabu vya Fiqhi kwa (Madhehebu ya) Imamiya kama vile kubainisha mahari na muda, basi huwa inasihi kwa kila kile ambacho pande mbili hizi zitaridhiana, na (sharti nyingine) ni kama vile uharamu wa kutamatui (kumuona) mwanamke ambaye ni haramu kisheria kumuoa, kama ilivyo katika ndoa ya daima. Na ni juu ya mwanamke aliyeolewa ndoa ya Mut'a kukaa eda baada ya kumalizika muda wa ndoa kwa hedhi mbili na atakaa eda miezi minne na siku kumi kama mumewe atafariki (kabla ya muda kwisha).

Na wawili hawa walioowana ndoa ya Mut'a hawarithiani wala hakuna (sharti ya wajibu wa) chakula (kwa mume kumlisha mke) na mke hamrithi mume wala mume hamrithi mke, na mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa ya Mut'a ni sawa na mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa ya daima kikamilifu kabisa, katika haki za urithi, chakula na haki zote za malezi, maadili ya kimwili na mafunzo, na ni mtoto wa baba huyo. Hii ndiyo ndoa ya Mut'a kwa sharti zake na mipaka yake nayo ni kama uionavyo, siyo miongoni mwa uzinzi kwa hali yoyote ile kama wanavyodai watu.

Na Masunni kama ilivyo kwa ndugu zao Mashia wanaafikiana kuhusu sheria ya ndoa hii kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyopo katika aya ya ishirini na nne ndani ya Suratun-Nisai pale Mwenyezi Mungu aliposema: "Wale mtakaostarehe nao (mtakao waoa Mut'a) miongoni mwao, wapeni mahari yao (ambayo) ni faradhi, wala si vibaya kwenu katika yale muliyoridhiana badala ya yale yaliyotajwa, bila shaka Mwenyezi Mungu ni mjuzi tena mwenye hekima." Ni kama ambavyo pia wameafikiana (Sunni na Shia) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliiruhusu ndoa ya Mut'a na Masahaba walioa (kwa ndoa hiyo) zama zake Mtume.

Isipokuwa wamehitilafiana (Sunni na Shia) kuhusu kufutwa kwa ndoa hiyo au kutokufutwa, kwani Masunni wanasema imefutwa na kwamba iliharamishwa baada ya kuwa ilikuwa ni halali, na kwamba kufutwa huko ilifutwa na Sunna na siyo Qur'an. Shia wao wanasema kuwa ndoa hiyo haikufutwa na kwamba ni halali mpaka siku ya kiyama. Kwa hiyo basi uchambuzi unafungamana tu na kuhusu kufutwa kwa ndoa hiyo au kutokufutwa, na kuzichunguza kauli za pande mbili ili iweze kumbainikia msomaji wazi wazi jambo hili na kwamba wapi ndiko kunakopatikana haki, basi aifuate bila ya chuki na upendeleo.

Ama kwa upande wa Mashia wasemao kwamba haikufutwa na ni halali mpaka siku ya kiyama, hoja yao ni kuwa: Haikuthibiti kwetu sisi kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu aliikataza ndoa hiyo, na Maimamu wetu kutoka katika kizazi kitukufu cha Mtume, wao wanasema kuwa ni halali. Na lau ingekuwa imefutwa na Mtume (s.a.w.), basi Maimamu wa nyumba ya Mtume wangelilijua jambo hilo wakiongozwa na Imam Ali, kwani watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) ndiyo wajuao mno yaliyomo ndani ya nyumba hiyo. Lakini kilichothibiti kwetu sisi ni kwamba Khalifa wa pili Umar bin Al-Khatab ndiye aliyeikataza ndoa hii na akaiharamisha kwa Ij-tihadi yake kama wanavyoshuhudia wanachuoni wa Kisunni wenyewe. Sisi hatuwezi kuacha hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa ajili ya (kufuata) maoni na Ij-tihadi ya Umar bin Al-Khatab.

Basi huu ni muhtasari wa yale wayasemayo Mashia juu ya uhalali wa Mut'a nayo ndiyo kauli ya sawa na ni mtazamo bora. Waislamu wote wanatakiwa wafuate hukmu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wampinge asiyekuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake hata kama anacheo gani pindi Ij-tihadi yake itapokwenda kinyume cha Qur'an na Sunna. Ama Masunni wao wanasema kwamba, Mut'a ilikuwa halali na Qur'an ilishuka kuhusu Mut'a na Mtume aliiruhusu na masahaba wakaifanya, kisha baada ya hapo ilifutwa, na wanatofautiana juu ya kilichoifuta. Wapo miongoni mwao wanasema kwamba, "Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliizuwia kabla ya kufa kwake, na wengine wanasema kwamba Umar bin Al-Khatab, ndiye aliyeiharamisha, na kauli yake (Umar) kwetu sisi (Masunni) ni hoja (yenye nguvu) kufuatia kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema: "Shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za Makhalifa wangu viongozi baada yangu zishikeni kwa nguvu.

Ama wale wasemao kuwa Mut'a ni haramu kwa kuwa Umar bin Al-Khatab aliiharamisha na kwamba kitendo cha Umar ni sunna ya lazima (kufuatwa). Basi watu hawa sisi hatuna maneno nao wala hatuna uchambuzi wowote, kwani (mtazamo wao huo) ni wa kung'ang'ania na kujikusuru. Itakuwaje Mwislamu aache kauli ya Mwenyezi Mungu na kauli ya Mtume na awapinge kisha afuate kauli ya mtu mwenye kujitahidi, anayekosea na kupatia, na hali hii ya kujitahidi kwake juu ya mas-ala fulani (inaweza kuchunguzwa) iwapo ndani ya Qur'an na sunna hakuna tamko (linalohusu ufumbuzi wa mas-ala hayo) ama kama tamko litakuwepo basi, "Haifai kwa Muumini mwanamume na Muumini mwanamke pindi Mwenyezi Mungu na Mtume wake watakapoamua jambo wawe na hiyari katika jambo lao (hilo lililoamriwa) na yeyote atakayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake bila shaka amepotea upotevu ulio wazi". (Qur'an, 33:36)

Na yeyote asiyekubaliana nami juu ya kanuni hii basi ni juu yake kuyarejea maarifa yake na ufahamu wake kuhusu (muongozo) na sheria ya Kiislamu na aisome Qur'an Tukufu na Sunna ya Mtume kwani Qur'an yenyewe binafsi imeeleza katika aya iliyotajwa hapo juu, na aya zingine mfano wa hiyo ni nyingi mno zinafahamisha juu ya kukufuru na kupotea kwa mtu yeyote asiyeshikamana na Qur'an na Sunna ya Mtume (s.a.w.). Ama kwa upande wa dalili ya Sunna tukufu ya Mtume ziko dalili nyingi vile vile, lakini tunatosheka na kauli moja ya Mtume (s.a.w.) isemayo: "Halali iliyo halalishwa na Muhammad ni halali mpaka siku ya Kiyama, na haramu iliyoharamishwa na Muhammad ni haramu mpaka siku ya kiyama. Hivyo basi hana haki mtu yeyote kuhalalisha au kuharamisha katika mas-ala ambayo ndani yake yamethibiti maandiko na ni hukumu kutoka kwa Mwenyezi Mungu au kwa Mtume wake (s.a.w.).

Na kwa yote haya tunawaambia hao wanaotaka kutukinaisha kwamba vitendo vya Makhulafaur-Rashiduna na Ij-Tihadi zao vinatulazimu, sisi tunasema: "Hivi mnajadiliana nasi juu ya jambo la Mwenyezi Mungu ambaye ni Mola wetu na ni Mola wenu, na sisi tuna matendo yetu nanyi mnayo matendo yenu, nasi kwake Mwenyezi Mungu tunajitakasa" (Qur'an, 2:139) Wanaozungumzia dalili hii (bila shaka) wanakubaliana na Mashia kwenye madai ya (kuwa Mtume hakuiharamisha Mut'a) na wanakuwa ni hoja dhidi ya ndugu zao Masunni (wasemao kuwa Mtume aliiharamisha). Hivyo basi uchunguzi wetu tunaufungamanisha tu na kundi lisemalo kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ndiye aliyeiharamisha na akaifuta (aya ya) Qur'an kwa hadithi.

Watu wasemao hivi wanajikanganya wenyewe katika kauli zao na hoja zao zi tupu hazina msingi imara, japokuwa imepokewa kwa Muslim ndani ya sahih yake kuhusu katazo (hilo linalodaiwa), kwani lau kungekuwa na katazo litokalo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), basi katazo hilo lisingefichikana kwa masahaba ambao walioa Mut'a katika zama za Ukhalifa wa Abubakar na sehemu fulani ya Ukhalifa wa Umar kama alivyosimulia jambo hilo Muslim ndani ya sahih yake. Taz: Sahih Muslim Juz. 4 uk. 158. Amesema A'ta', "Jaabir bin Abdillah alikuja hali ya kuwa anafanya Umra nasi tukamfuata nyumbani kwake, watu wakamuuliza mambo mengi, hatimaye wakamuuliza juu ya Mut'a akasema ndio tuliowa zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) na zama za Abubakar na Umar".

Basi lau Mtume wa Mwenyezi Mungu angekuwa ameikataza Mut'a, isingejuzu kwa Masahaba kufanya Mut'a katika zama za Abubakar na Umar kama ulivyosikia. Ukweli uliopo ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) hakukataza Mut'a wala hakuiharamisha, bali katazo lilitokana na Umar bin Khatab kama yalivyokuja maelezo ya jambo hilo ndani ya Sahih Bukhar. Imepokewa toka kwa Musaddad, ametusimulia Yahya kutoka kwa Imran Abu Bakr, ametusimulia Aburajaa kutoka kwa Imran bin Huswain (r.a.) amesema: "Aya ya Mut'a ilishuka ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi tukaitenda wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na haikushuka Qur'an kuiharamisha na wala Mtume hakukataza mpaka alipokufa Mtume, basi mtu fulani kwa maoni yake akasema aliyoyataka, Muhammad akasema, inasemekana mtu huyo ni Umar". Taz: Sahih Bukhar Juz. 5 uk. 158.

Ewe Msomaji unaona ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) hakuikataza Mut'a mpaka kufa kwake kama alivyobainisha Sahaba huyu. Na unamuona anaunasibisha huu uharamishaji kwa Umar wazi wazi bila ya kificho na anaongeza kuwa yeye Umar alisema ayatakayo kwa maoni yake. Huyu hapa Jabir bin Abdillah Al-Ansari anasema wazi wazi kama ifuatavyo:"Tulikuwa tunaoa Mut'a kwa gao la tende na unga kwa siku kadhaa, katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) na (zama za) Abubakar mpaka Umar alipokataza kutokana na suala la A'mri bin Hurayth. Taz: Sahih Muslim Juz. 4 uk. 131. Na miongoni mwa mambo yanayotujulisha kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa na mtazamo kama wa Umar jambo ambalo si geni ni kuwa, imetangulia katika uchambuzi wetu kuhusu msiba wa siku ya Al-Khamis ya kwamba baadhi ya Masahaba walimuunga mkono Umar katika kauli yake aliposema kuwa "Mtume wa Mwenyezi Mungu anaweweseka kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu'!! Kwa hiyo ikiwa walimtia nguvu kwenye jambo la hatari kama hili ambalo alimtuhumu Mtume (s.a.w.) basi ni kwa nini wasikubaliane naye katika baadhi ya Ij-tihadi zake?

Hebu na tuisikilize kauli ya mmoja wao (hao Masahaba wanaomuunga mkono Umar): "Nilikuwa kwa Jabir bin Abdillah, mara alimjia mtu fulani akamwambia: ibn Abbas na ibn Zubair wanahitilafiana kuhusu Mut'a mbili (Mut'a ya ndoa na Mut'a ya Hija) basi Jabir akasema zote mbili tulizifanya zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kisha akatukataza Umar basi hatukurejea tena (kuzifanya). Taz: Sahih Muslim Juz. 4 uk. 131. Kwa ajili hiyo mimi binafsi naamini kabisa kwamba kuna baadhi ya Masahaba walilihusisha kwa Mtume katazo la kuharamishwa kwa Mut'a ili kuutakasa msimamo wa Umar na (kuupitisha) kuwa ni sahihi. Kinyume chake ni kuwa haiwezekani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kuharamisha kilichohalalishwa na Qur'an, kwani sisi hatukuti hata hukmu moja katika hukmu zote za Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu ameihalalisha kisha Mtume akaiharamisha, na hapana yeyote asemaye hivyo isipokuwa ni mpinzani mwenye chuki.

Na lau tutakubali ili kupata jinsi ya kujadili ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliikataza Mut'a, basi Imam Ali bin Abi Talib ambaye ni mtu wa karibu mno kwa Mtume na mjuzi mno kuliko watu wengine asingesema kama ifuatavyo: "Bila shaka Mut'a ni rehma, Mwenyezi Mungu amewahurumia kwayo waja wake, na lau siyo Umar kuikataza, basi asingezini isipokuwa mtu duni". Taz: Ath-Tha'alabi ndani ya tafsirul-Kabir, na Tabari alipoifasiri aya ya Mut'a ndani ya tafsiri yake iitwayo Alk-Kabir. Na hii ni kwa kuwa Umar mwenyewe hakuunasibisha kwa Mtume uharamishaji wa Mut'a bali amesema wazi wazi katika kauli yake ifuatayo: "Mut'a mbili zilikuweko zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu, nami ninazikataza na nitatoa adhabu dhidi ya mwenye kuzitenda, Mut'a ya Hija na Mut'a ya wanawake." Taz: At-Tafsirul-Kabir ya Al-Fakhrur-Razi alipokuwa akifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu "Famastamtaatum Bihi Minhunna." Na hii hapa Musnad ya Imam Ahmad bin Hanbal ambayo ni shahidi mzuri juu ya kwamba Masunni wanahitilafiana mno katika mas-ala haya, wako miongoni mwao wanaihalalisha Mut'a na wako miongoni mwao wanaofuata kauli ya Umar bin Al-Khatab wanaiharamisha.

Imam Ahmad amethibitisha kama ifuatavyo: Imepokewa toka kwa ibn Abbas amesema: "Mtume (s.a.w.) alifanya "Tamattui" (Mut'a) 'Ur-wa ibn Zubair akasema, Abubakar na Umar walikataza Mut'a, basi ibn Abbas akasema: Kinasemaje hiki Kiur-wah akasema: anasema, Abubakr na Umar walikataza Mut'a, ibn Abbas akasema: Nawaona watu hawa wataangamia, nasema kasema Mtume nao wanasema kakataza Abubakr na Umar". Taz: Musnad lmam Ahmad bin Hanbal Juz. 1 uk. 337. Na imekuja ndani ya Sahih Tirmidhi kwamba Abdalla bin Umar aliulizwa kuhusu Mut'a ya Hija akasema:"Ni halali" basi yule muulizaji akamwambia,"Hakika baba yako aliikataza", akasema Ibn Umar:"Waonaje ikiwa baba yangu aliikataza na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliifanya,basije nifuate amri ya baba yangu au amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Yule mtu akasema,"Bali (ufuate) amri ya Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.)."

Taz: Sahih Tirmidhi Juz. 1 uk. 157. Masunni wamemtii Umar juu ya (kuharamisha) Mut'a ya wanawake na wamempinga kuhusu Mut'a ya Hija. Pamoja na kuwa katazo lake (alilitoa) akiwa mahala pamoja kama tulivyotanguliza kueleza. Jambo la maana katika yote haya ni kuwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) na wafuasi wao wamempinga (Umar) na wakasema kuwa Mut'a zote mbili ni halali mpaka siku ya Kiyama. Na kuna wanachuoni wa Kisunni ambao wamewafuata (Mashia) katika jambo hilo na ninamtaja miongoni mwao mwanachuoni Mtukufu wa Tunis ambaye ni kiongozi wa chuo kikuu cha "Az-Zaytuni" Mtukufu Sheikh Ta'hir bin A'shur (Mwenyezi Mungu amrehemu) yeye amesema ndani ya tafsiri yake mashuhuri kuwa Mut'a ni halali pale alipoitaja aya ya "Famastamtaatum Bihi Minhunna Faa'tuhunna-Ujurahunna Faridhah." Taz: At-Tahrir Wat-tan-wir cha Ta-hir A'shur Juz. 3 uk. 5.

Basi namna hii wanachuoni wanatakiwa wawe huru katika itikadi zao wasiathiriwe na upendeleo wala ujamaa na wala wasiogope kulaumiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Baada ya uchambuzi huu mfupi hakuna hoja wala chenye kuwatakasa Masunni kutokana na kebehi na tuhuma yao dhidi ya Shia kuhusu kuhalalisha kwao ndoa ya Mut'a zaidi ya dalili madhubuti na hoja bora walizonazo Shia. Muislamu anawajibika kuiangalia kwa makini kauli ya Imam Ali (a.s.) ya kwamba:"Mut'a ni Rehma, Mwenyezi Mungu amewahurumia kwayo waja wake" Na kwa hali halisi basi, ni ukubwa ulioje wa rehma ambayo inazima moto wa matamanio yenye nguvu yanayomfunika mtu awe mwanamume au mwanamke, (mpaka) akawa kama mnyama mwenye kushambulia. Ni wajibu kwa Waislamu wote na hasa vijana, wafahamu ya kwamba Mwenyezi Mungu amewajibisha kwa mzinifu adhabu ya kuuawa kwa kupigwa mawe kwa wale wenye kuhifadhika wanaume na wanawake basi hawezi Mwenyezi Mungu kuwaacha waja wake bila huruma wakati yeye ndiye muumba wao na ndiye muumba wa maumbile yao na anafahamu kitakachowarekebisha. Iwapo Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu amewahurumia waja wake kwa kuwaruhusu kufanya Mut'a basi hakuna atakayezini baada ya ruhusa hiyo isipokuwa mtu muovu mno. (Mfano wa hili) ni kama mwizi kukatwa mkono kwani kama kutakuwa na Baytul-Mal (Bank) kwa ajili ya kusaidiwa wenye dhiki na shida basi hakuna atakayeiba isipokuwa mtu muovu.

KAULI INAYOHUSU TAHRIFUL-QUR'AN

Kauli hii kwa maana yake halisi ni mbaya sana ambayo Muislamu yeyote aliyeuamini utume wa Muhammad (s.a.w.) hawezi kuivumilia, sawa sawa akiwa ni Shia au Sunni. Hiyo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amebeba jukumu la kuilinda pale aliposema: "Hakika sisi ndiyo tulioiteremsha Qur'an na bila shaka ni sisi ndiyo tutakao ilinda." Hivyo basi haiwezekani kwa yeyote kuipunguza au kuongeza herufi moja, na hii Qur'an ndiyo muujiza wa milele wa Mtume wetu (s.a.w.) ambao hauwezi kujiwa na batili hapo kabla au hapo baadaye. Na ukweli halisi ulivyo kimatendo kwa Waislamu ni kuwa wanapinga Tahrifu ya Qur'an, kwani Masahaba wengi walikuwa wakiihifadhi kwa moyo, na walikuwa wakishindana kuihifadhi na kuihifadhisha kwa watoto wao kwa muda wote mpaka leo, hivyo haiwezekani kwa mtu fulani au kikundi fulani wala dola fulani kuigeuza au kuibadilisha.

Na lau tutaitembelea miji ya Kiislamu Mashariki na Magharibi, Kaskazini na Kusini na kila sehemu ya dunia, basi tutaikuta Qur'an ni ile ile bila ya ziyada wala upungufu, japokuwa Waislamu wametofautiana kwenye Madhehebu na vikundi na mila na mienendo. Basi Qur'an ni msukumo pekee unaowakusanya wala hawatofautiani watu wawili kuhusu Qur'an katika umma (wa Kiislamu), isipokuwa maelezo ya tafsiri, kila kikundi hufurahia yale waliyo nayo. Na yale yanayonasibishwa kwa Mashia kusema kuwa wanaipotosha Qur'an ni wazi kabisa kwamba ni tuhuma na kebehi na wala jambo hilo haliko kabisa katika itikadi za Kishia. Na endapo tutazisoma akida za Kishia ndani ya Qur'an, basi tutakuta kauli yao ya pamoja ni kukitakasa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kutokana na kila aina ya upotoshaji.

Anasema mwenye kitabu kiitwacho "Aqaidul-Imamiyyah Sheikh Muzaffar" "Sisi tunaitakidi kwamba Qur'an ni. ufunuo wa Mwenyezi Mungu, ulioteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ulimi wa Nabii wake Mtukufu, ndani yake (Qur'an) muna ubainisho wa kila kitu, nayo ni muujiza wa kudumu ambao watu wameshindwa kuukurubia katika balagha, ufasaha na katika mambo iliyoyakusanya miongoni mwa ukweli na maarifa ya hali ya juu. Haizukiwi na mabadiliko wala mageuzi wala upotovu, na hii Qur'an tuliyonayo mikononi mwetu tunayoisoma ndiyo ile ile Qur'an iliyoteremshwa kwa Nabii, na yeyote atakayedai kinyume cha hivyo, basi mtu huyo ni mzushi au mpotoshaji au amechanganyikiwa, na wote hao hawako katika uongofu, kwani Qur'an ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo hayajiwi na ubatilifu hapo baadaye wala kabla yake. Na baada ya haya, miji yote ya Kishia inafahamika, na hukmu zao ndani ya fiqhi zinaeleweka kwa watu wote, basi lau wangekuwa na Qur'an nyingine isiyokuwa hii tuliyonayo, watu wangeliitambua.

Mimi ninakumbuka wakati nilipotembelea miji ya Kishia kwa mara ya kwanza, ndani ya mawazo yangu kulikuwa na baadhi ya habari hizi, basi nilikuwa kila nionapo kitabu kikubwa hukichunguza ili huenda nikaigundua hii Qur'an inayodaiwa (kuwa ipo), lakini mawazo haya yaliondolewa kwa haraka sana, na nilifahamu hapo baadaye kuwa hiyo ni moja ya kebehi za uongo zenye lengo la kuwafanya watu wawakimbie Mashia, lakini siku zote kumebakia watu wanaowakebehi Mashia na kutoa hoja dhidi yao kwa kitabu kiitwacho; "Faslul-Khitab Fi Ithbat Tahrifi Kitabi Rabbi'l Ar-Bab" ambacho mtunzi wake ni Muhammad Taqiyyun-Nuri At-Tabrasi aliyefariki mwaka 1320 Hijriyyah naye ni Shia, na hawa wenye kuwashinikiza Mashia wanataka kuwabebesha Mashia jukumu la kitabu hiki, na jambo hili ni kinyume cha uadilifu. Basi kwani vitabu vingapi vimeandikwa ambavyo ukweli havielezi isipokuwa maoni ya mwandishi wake, na ndani yake kuna mambo machafu na mengine yenye hekima, na kuna haki na batili na humo ndani kuna makosa na mengine ya sawa na yote hayo tunayakuta kwa kila vikundi vya Kiislamu, na wala siyo kwa Mashia peke yao na wengine ikawa hakuna hali hiyo. Basi je, inajuzu kwetu sisi kuwabebesha Masunni jukumu la yale yaliyoandikwa na waziri wa utamaduni wa Misri na mkuu wa Elimu ya Kiarabu Doctor Taha Husain kuhusu Qur'an na Mashairi ya zama za Jahiliyah?

Au yale aliyoyasimulia Bukhari, kitabu ambacho ni sahihi kwao Masunni, (yasemayo) kuwa Qur'an ina upungufu na ina ziyada, pia (namna hiyo hiyo) ndani ya Sahih Muslim na vinginevyo.[93] Hebu tutupiliye mbali hayo na tuukabili uovu kwa wema, na bora ya kauli kuhusu maudhui hii ni ile iliyoisemwa na Al-Ustadh Muhammad Al-Madini Mkuu wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Az-har pale alipoandika akasema: Amma (kusema) kwamba Mashia Imamiyyah wanaitakidi kuwa Qur'an imepungua, (sisi) tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu (kutokana na kauli hiyo) bali hizo ni riwaya tu zilizosimuliwa ndani ya vitabu vyao, kama ambavyo kuna riwaya kama hizo zilizosimuliwa ndani ya vitabu vyetu, na wanachuoni wenye kuhakiki kutoka pande hizi mbili (Shia na Sunni) wamezipinga riwaya hizo na wakabainisha upotovu wake, na hapana Shia Imamiyyah au Zaidiyyah anayeitakidi hivyo, kama ambavyo hapana Sunni anayeitakidi hivyo.

Mwenye kutaka anaweza kurejea kwenye kitabu kama "Kitabul-It'qan" cha Suyuti ili apate kuona mfano wa riwaya kama hizi tunazozitupilia mbali. Na kuna Mmisri mmoja katika mwaka wa 1498 alitunga kitabu kiitwacho "Al-Fur-Qan ambacho alikijaza riwaya nyingi kama hizi mbovu zilizoingizwa (tu) na zinapingwa, (lakini) alizinakili kutoka kwenye vitabu na rejea za Kisunni, chuo cha Az-har kiliitaka serikali ya Misri kukipiga marufuku kitabu hiki baada ya kuwa kimebainisha dalili na uchambuzi wa kielimu namna ya upotovu na uovu uliyomo. Serikali ya Misri ilikubali ombi hili na ikakipiga marufuku kitabu hicho, lakini mwandishi wa kitabu hicho alipeleka madai ya kutaka fidia, na kikao cha serikali katika idara ya mahakama kiliyatupilia mbali madai hayo.

(Sasa basi, kutokana na hali kama hii). Je, itasemwa kwamba Masunni wanapinga utakasifu wa Qur'an? Au wanaamini kuwa imepungua kwa sababu tu ya riwaya zilizosimuliwa na fulani? Au kwa sababu tu ya kitabu kilichotungwa na fulani? Basi hali ni hiyo hiyo kwa Mashia Imamiyyah, kuna riwaya ndani ya baadhi ya vitabu vyao kama riwaya zilizomo ndani ya vitabu vyetu. Kuhusu jambo hili Al-Imam Al-Allamah Said Abul-Fadhli bin Al-Hasan At-Tabrasi ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wakubwa wa Kishia katika karne ya sita Hijiriyyah anasema ndani ya kitabu kiitwacho, "Maj-Maul-Bay an Lil-U'lumil-Qur'an""A.m.a kuweko na nyongeza ndani ya Qur'an jambo hili limewafikiwa kuwa ni wazo batili na ama wazo la kuwepo upungufu katika Qur'an limeelezwa na jamaa katika Mashia wenzetu na baadhi ya Masunni kuwa mabadiliko na upungufu upo. Na wazo sahihi kwa mtazamo wa watu wetu ni kinyume na wazo la kuwepo badiliko au upungufu, nalo ndilo alilolinusuru Murtaza Mwenyezi Mungu aitakase roho yake. Usemi wake ulikuwa wa kutosheleza katika majibu ya MASA-ILU-TARABLOSIAT.

Ametaja katika sehemu kadhaa kuwa: Kujuwa kuwa nakala ya Qur'an nakala ni sahihi ni sawa na kujuwa kuwa kuna nchi, matukio makubwa, majanga ya kutisha, vitabu mashuhuri, na mashairi ya Kiarabu,na hiyo ni kwa sababu uangalizi ulikuwa makini, na sababu za kuinakili na kuihifadhi (Qur'an) zilikamilika, zilifikia kiwango cha juu mno yote hayo ni kwa sababu Qur'an ni muujiza wa Mtume na ndiyo chimbuko la elimu za kisheria na hukumu za kidini. Wanachuoni wa Kiislamu pia walifikia kiwango cha juu kabisa katika kuihifadhi na kuilinda, walifikia hata kujuwa kila kitu wametofautiana katika Qur'an kama Irabu yake, usomaji wake, herufi zake, na aya zake. Hivyo basi pamoja na uangalifu wa yakini na udhibiti kama huu yawezekana vipi iwe imebadilishwa au kupunguzwa?

Taz: Maqala ya Al-Ustadh Muhammad Al-Madini Mkuu Kituo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Az-har (iliyoandikwa katika) jarida liitwalo Risalatul-Islam toleo la nne katika mwaka wa kumi na moja uk. 382 na383. Na ili ikubainikie wazi ewe msomaji kwamba tuhuma hii (ya kupunguka kwa Qur'an au kuzidi) kuwa iko karibu mno na Masunni kuliko Mashia, ni kwamba miongoni mwa mambo yaliyonifanya nizirejee(upya) itikadi zangu zote ni kila nilipokuwa nikijaribu kuwakosoa Mashia katika jambo lolote lile na kuwapinga, wao walithibitisha kutohusika nalo na wakiliambatanisha kwangu (kama Sunni kabla kuwa Shia) na ndipo nilipofahamu kwamba wao siku zote wanazungumza kweli na kwa njia ya kufanya uchambuzi namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba nimekinaika.

Na hapa basi nakuletea yatakayothibitisha jambo hilo katika maudhui hii: Wamethibitisha Mabwana Tabrani na Baihaqi ya kwamba, Hakika ndani ya Qur'an muna sura mbili, moja wapo ni: Bismillahir-Rahmanir-Rahim Innaa Nastainuka Wanastaghfiruka Wanuthnii A'laykal-Khaira kullahu Wala nakfuruka Wanakhlau' wanatruku Man Yajjuruka ". Maana Yake: "Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu, Hakika sisi tunakuomba msaada na tunakuomba msamaha na tunakusifu kwa mema yote na wala hatukukatai na tunajiepusha na kumuacha yule anayekufanyia maovu." Na Sura ya pili ni: Bismillahir-Rahmanir-Rahim Allahumma Iyyaka Naabudu Walaka Nusalli Wanasjudu Wailaika Nas-a' Wanahfad, Nar-ju Rahmataka Wanakhsha Adha-Bakal-Jadda Inna Adha-baka Bil-Kafirina Mul-Haq." Maana Yake: Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu, Ewe Mwenyezi Mungu peke yako tu tunakuabudu na tunasali na kusujudu kwa ajili yako na kwako wewe tunatumika, tunataraji rehma zako na tunaiogopa adhabu yako kali, hakika adhabu yako itawapata makafiri".

Sura hizi mbili Ar-Raghibu ndani ya Muhadharat ameziita kuwa ni Sura za Qunut nazo ni miongoni mwa zile ambazo Sayyidina Umar bin Al-Khatab alikuwa akiqunuti kwazo, zinapatikana ndani ya Mus-hafu wa ibn Abbas na Mus-hafu wa Zaid bin Thabit. Taz: Al-It-Qan cha Jalal-ud-Dinis-Suyuti pia ndani ya Ad-Durrul-Manthoor. Imam Ahmad bin Hanbal amethibitisha ndani ya Musnad yake kama ifuatavyo:- "Imepokewa toka kwa Ubayyi bin Kaab amesema:"Ni aya ngapi mzisomazo ndani ya Suratul-Ahzab? akasema:Aya sabini na kidogo hivi, akasema:Hakika mimi niliisoma pamoja na Mtume (s.a.w.) mfano wa sura Al-Baqarah au zaidi kuliko hiyo na hakika ndani yake imo aya ya Rajmi". Taz: Musnad Imam Ahmad bin HanbalJuz. 5 uk. 132. Ewe msomaji mwenye akili hebu ziangalie hizi sura mbili zilizotajwa ndani ya Al-It-Qan na Ad-Durrul-Manthoor ambavyo ni vitabu vya Suyuti, pia zimethibitishwa na Tabran na Baihaqi na zinaitwa kuwa ni sura za Qunut wakati hazimo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Hii ina maana kwamba Qur'an tuliyonayo mikononi mwetu inapungua kwa sura mbili hizi zilizomo ndani ya Msa-hafu wa ibn Abbas na Msa-hafu wa Zaid bin Thabit kama ambavyo pia inajulisha kuwa kuna Misahafu mingine isiyokuwa hii tuliyonayo. Hali hii inanikumbusha ile tuhuma dhidi ya Shia kwamba wanao Msa-hafu wa Fatmah, basi yajuwe haya. Na (inajulisha) kwamba Masunni huzisoma sura hizi katika dua ya Qunut kila asubuhi, nami binafsi nilikuwa nimezihifadhi na kuzisoma katika Qunut ya sala ya alfajiri (nilipokuwa sunni). Ama riwaya ya pili ambayo ameithibitisha Imam Ahmad ndani ya Musnad yake, ni riwaya inayosema kuwa, Suratul-Ahzab imepungua robo tatu nzima, kwani Suratul-Baqarah ina aya 286 wakati ambapo Suratul-Ahzab haizidi aya 73 na tukizingatia hesabu ya Qur'an kwa hizbu, basi bila shaka Suratul-Baqarah ina hizbu tano wakati Suratul-Ahzab ina hizbu moja. Na kauli ya Ubayyi bin Kaa'b aliposema: "Nilikuwa nikiisoma pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu kama ilivyo Suratul-Baqarah au zaidi" wakati ambapo ni miongoni mwa wasomaji mashuhuri waliokuwa wakihifadhi Qur'an katika zama za Mtume (s.a.w.) na huyo ndiye aliyechaguliwa na Umar[94] kuwasalisha watu sala ya Tarawehe, basi kauli yake hii inazusha mashaka na wasi wasi kama inavyoonekana wazi.

Na amethibitisha Imam Ahmad bin Hambal ndani ya Musnad yake[95] mapokezi toka kwa Ubayyi bin Kaab amesema: "Hakika Mjumbe wake alisema, Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniamuru nikusomee Qur'an akasoma: "Lam Yakunil-ladhiina Kafaruu min ahlil-Kitabi", ndani yoke akasoma; "Walau anna ibn Adama Saala Wa-diyan min malin Faa A'taytuhu Lasaala Thaaniyan Falau Saala Thaniyan Faataytuhu Lasaala Thalithan, Wala-Yamlau Jaufa ibn Adama Illat-Turabu Wayatubullahu ala Man Taaba, Wainna dhalikad-Dinul-Qayyimu Indallahil-Hanafiyyah Gharyul-Mushrikah Walal-Yahudiyah Walan-Nasraniyyah Woman Yaf-alu Khayran Falan Yukfarah." Na amethibitisha Al-Hafidh ibn Asakir alipokuwa akitoa Tarjuma ya Ubayyi bin Kaab ya kwamba Abud-Dar-Dai alikwenda Madina akiwa pamoja na jamaa fulani miongoni mwa watu wa Dimishq, akamsomea Omar bin Khatab huko Madina aya hii: "Idh'jaalal-Ladhiina Kafaru Fi Qulubihim Al-Hamiyata Hamiyatal-Jaahiliya Walau Hamaitum kama hamau La Fasadal-Masjidul-Haram."

Umar bin Khatab akasema:"Nani alikusomesheni kisomo hiki"? Wakasema, "Ubayyi bin Kaab" akamwita, na akawaambia "Someni (mlivyosoma)" wakasoma:"Walau hamaltum kama hamau lafasadal-Masjidul-haraam " Ubayyi bin Kaab akamwambia Umar bin Khatab "Ndiyo, ni mimi niliyewasomesha (hivyo)" Umar akamwambia Zaid bin Thabit "Soma ewe Zaid" Zaid akasoma kama wasomavyo watu wote, basi Umar akasema, "Sifahamu kisomo kingine isipokuwa hiki"! Ubayyi bin Kaab akasema: "Ewe Umar namuapa Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika wewe unafahamu kwamba mimi nilikuwa nikihudhuria (mbele ya Mtume) na wao hawahudhurii na nikikurubia (kwa Mtume) wao hujificha, na namuapa Mwenyezi Mungu lau utapenda (nisisome hivi nisomavyo) basi nitabakia nyumbani mwangu wala sitamsomea yeyote mpaka nife" Umar akasema, Samahani, bila shaka wewe unafahamu kwamba, Mwenyezi Mungu amekujaalia elimu, basi wasomeshe watu kile ukijuacho".

Amesema:(Kuna siku) Umar alipita kwa kijana fulani akiwa anasoma ndani ya msahafu kama ifuatavyo: "Annabiyyu aula Bil-Muuminina Mina anfusihim Wa'az-Wajuhu Ummahatuhum Wahuwa Abun-lahum". Umar akasema:"Ewe kijana (imekuwaje) hebu eleza", yule kijana akasema:"Huu ni msahafu wa Ubayyi bin Kaab" Basi Umar akaenda akamuuliza Ubayyi naye akamwambia: "Bila shaka mimi ilikuwa ikinishughulisha Qur'an nawe ulikuwa ukishughulishwa na biashara sokoni." Taz: Tarikh Dimishq ya Al-Hafidh ibn Asakir Juz. 2 uk. 228. Nao ibn Al-Athir ndani ya Jamiul-Usul na Abu Dawud ndani ya Sunan yake na Al-Hakim ndani ya Mustadrak yake wamesimulia mfano wa riwaya kama hii (iliyotangulia).

Mara hii nakuachia ewe ndugu msomaji ufafanue mwenyewe riwaya kama hizi zilizojaa ndani ya vitabu vya Kisunni, hali yakuwa wao hawana habari nazo (kwamba zimo vitabuni mwao) na wanawatuhumu Mashia ambao kwao haipatikani kiasi kama hiki. Lakini huenda baadhi ya watu wakorofi miongoni mwa Masunni wakazikwepa riwaya kama hizi na kuzikataa kama ilivyo kawaida yao. Si hivyo tu bali watampinga Imam Ahmad kwa kuandika uzushi kama huu na Sanad zake kuwa ni dhaifu. Isitoshe wataiona Musnad ya Imam Ahmad bin Hanbal na Sunan ya Abi Dawud kwao Masunni kwamba hazina kiwango cha usahihi kama ule wa Bukhar na Muslim, lakini (inawapasa wafahamu kwamba) riwaya kama hizi zinapatikana pia ndani ya sahih Bukhar na sahih Muslim.

Imam Bukhar amethibitisha ndani ya Sahih yake[96] katika mlango wa Manaqib Ammar na Hudhaifah (r.a.) kutoka kwa Il-Qimah amesema:

"Nilifika Sham nikasali rakaa mbili kisha nikasema,"Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie mwenza mwema, basi nikaenda kwa jamaa fulani nikakaa kwao, mara alikuja mzee mmoja hivi akakaa pembeni yangu, nikasema ni nani huyu"? Wakasema:"Abud-dar-dai" Nikasema:"Hakika nilimuomba Mwenyezi Mungu anisaidie mwenza mwema, amenisaidia wewe". Akasema: "Ni nani wewe"? Nikasema, "Mimi ni miongoni mwa watu wa Kufah" Akasema:"Hivi huko kwenu hayuko mwana wa Ummi Abdi mwenye viatu viwili, mto na birika ya kujitaharishia? Na kwenu yuko mtu ambaye Mwenyezi Mungu amemlinda kutokana na shetani kwa mujibu wa kauli ya Nabii wake (s.a.w.), mtu ambaye hapana mwingine ila yeye, hayuko kwenu mwandani wa Nabii (s.a.w.) ambaye hakuna mwingine ajuaye isipokuwa yeye. Kisha akasema namna gani Abdallah aisomavyo;(Wallayli Idha-Yaghsha)." Basi nikamsomea "Wallayli Idha Yaghsha, Wannahari ldha-Tajalla-Wad-Dhakari Wal-Untha) Akasema:"Wallahi ndivyo alivyonisomea Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kutoka kinywani mwake kuja kinywani mwangu".

Kisha ameongeza kwenye riwaya nyingine amesema, "Watu hawa hawakuniachia mpaka karibu waniondoshe kwenye jambo nililolisikia toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.)". Taz: Sahih Bukhar Juz. 4 uk. 216. Na katika riwaya nyingine amesema: (Wallayli Idha Yaghsha Wannahari,Idha-Tajalla Wad-Dhakari Wal-Untha) Akasema: "Amenisomea Mtume toka kinywani mwake kuja kinywani mwangu basi watu hawa hawakuniacha mpaka karibu wanirudishe." Taz: Sahih BukharJuz. 4 uk. 218 (Babu Manaqib Abdillah, ibn Mas-ud).

Basi riwaya zote hizi zinafidisha kwamba Qur'an tuliyonayo imezidishwa neno lisemalo, "Wamakhalaqa". Na amethibitisha Bukhar ndani ya sahih yake kwa isnadi yake kutoka kwa ibn Abbas ya kwamba Umar ibn Al-Khtab amesema:"Bila shaka Mwenyezi Mungu amemtuma Muhammad (s.a.w.) kwa ukweli na akamteremshia kitabu, miongoni mwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ni aya ya Rajmi, tuliiisoma na tukaifahamu na kuizingatia, na kwa ajili hiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alirujumu (kupiga mawe wazinifu) nasi baada yake tulirujumu, mimi nachelea iwapo zitapita siku nyingi kwa watu atakujasema msemaji, Wallahi hatuioni Ayatur-Rajmi ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu,watapotea kwa kuiacha faradhi aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu, na kurujumiwa kulikomo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu ni stahiki ya aliyezini iwapo amehifadhika miongoni mwa wanaume na wanawake pindi ushahidi ukithibitishwa au ikapatikana mimba na akakiri (kuzini). Kisha tulikuwa tukisoma miongoni mwa yale tuyasomayo ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwamba:"Msiwachukie wazee wenu kwani kuwachukia wazee wenu ni kufru kwenu, au hakika kufru kwenu ni kuwachukia wazee wenu".

Taz: Sahih Bukhar Juz. 8 uk. 26 Babu Rajmil-Hubla Minaz-Zina Idhaa uh-Sinat. Naye Imam Muslim amethibitisha ndani ya Sahih yake mlango wa Lau anna libni Adama Wadiyan Labtagha Thalithan Juz. 3 uk 100, Amesema:"Abu Musa Al-ash-ari alituma ujumbe kwa wasomaji wa Qur'an wa huko Basra wakaingia kwake watu mia tatu ambao wamekwisha soma Qur'an, akasema: Ninyi ndiyo watu wema huko Basra na ni wasomaji wao, basi isomeni (mara kwa mara) isije kukupitieni muda mrefu mioyo yenu itakuwa migumu kama ilivyokuwa migumu mioyo ya waliokuwa kabla yenu, nasi tulikuwa tukisoma sura tukiifananisha kwa urefu na ugumu na sura (isemayo):"Laukana Libni Adama Wadiyaani Min Malin Labtagha Wadiyan Thalithan Wala Yamlau Jaufa bni Adama Illat-Turaab". Tulikuwa tukisoma sura tunayoifananisha na moja ya Musabbihat nimesahaulishwa isipokuwa nimehifadhi sehemu yake (isemayo): "Ya Ayyuahal-Ladhiina A'manu Lima Taquluna Mala Taf-Aluna Fatuktabu Shahadatu Fii Aa'naqikum Fatus-Aluna An-haa yaumal-Qiyamah ". Taz: Sahih Muslim Juz. 3 uk. 100.

Na hizi sura mbili zinazodaiwa ambazo Abu Musa Al-ash-ari amezisahau, moja wapo inafanana na Suratu Baraa yaani aya 129 na ya pili inafanana na mojawapo ya Musabbihat yaani aya ishirini, sura hizi hazipo isipokuwa zimo ndani ya mawazo ya Abu Musa, basi soma na ustaajabu nami nakuachia uamuzi ewe mchunguzi muadiliru. Sasa basi ikiwa vitabu vya Masunni, Musnad zao na Sihahi zao zimejazwa riwaya kama hizi ambazo zinadai kuwa Qur'an imepungua na wakati mwingine imezidi, basi kebehi hizi ni za nini dhidi ya Mashia ambao wameungana kubatilisha upotovu wa madai haya kwa kauli moja? Na kama yule Shia mwenye kitabu kiitwacho; "Fas-Lulkhitab Fi Ith-Bati Tahrif Kitabi Rabbil-Ar-Bab", aliyefariki mwaka 1320 A.H. aliandika kitabu chake karibu miaka mia iliyopita, yeye alitanguliwa na Msunni kutoka Misri yule mwenye kitabu kiitwacho "Al-Fur-Qan" kwa karibu karne nne kama alivyoonesha jambo hilo Shekh Muhammad Al-Madani mkuu wa kitivo cha sheria katika Azhar.

Jambo la muhimu katika yote haya ni kwamba wanachuoni wa Kisunni na wanachuoni wa Kishia miongoni mwa wahakiki wamezibatilisha riwaya kama hizi na wakazizingatia kuwa potovu na wamethibitisha kwa dalili zinazotosheleza kwamba Qur'an iliyoteremshwa kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.) hakuna ziyada ndani yake wala upungufu wala mabadiliko wala mageuzi. Je, ni vipi Masunni wanawakebehi Mashia kwa sababu tu ya riwaya zisizokubalika kwa Mashia na wao Masunni wajitakase wakati ambapo sihahi zao zinathibitisha juu ya usahihi wa riwaya hizo?

Nami huzikumbuka riwaya hizi kwa uchungu mkubwa na huzuni nyingi, kwani hakutusaidii kitu leo hii kuzinyamazia na kuzitupa ndani ya kapu la takataka, lau siyo shinikizo la hujuma iliyoenezwa na baadhi ya watunzi na waandishi miongoni mwa wale wanaodai kuwa wameshikamana na sunna ya Mtume na hali ya kuwa nyuma yao kuna msukumo unaowatikisa na kuwatia nguvu wawatukane Mashia na kuwakufurisha na hasa baada ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Basi watu kama hawa nawaambia: "Muogopeni Mwenyezi Mungu kuhusu ndugu zenu, na mshikamane na dini ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakane, na ikumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyoko juu yenu, pindi mlipokuwa maadui (Mwenyezi Mungu) akaziunganisha nyoyo zenu mkawa kwa neema yake (nyote) ni ndugu.

6

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA TATU

SAURATU AL -IMRAN

Aya 1-6

﴿الم ﴾

1.Alif laam miim

﴿اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﴾

2.Mwenyezi Mungu hakuna mola isipokuwa yeye aliyehai msimamizi wa kila jambo.

﴿نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ﴾

3.Amekuteremshia kitabu kwa haki kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake. Na aliteremsha Tawrat na Injil.

﴿مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ﴾

4.Kabla yake ziwe ni uwongozi kwa watu na ameteremsha upambanuzi. Hakika wale waliokufuru Aya za Mwenyezi Mungu wana adhabu kali, na Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu Mwenye kutia adabu

﴿إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴾

5.Hakika MwenyeziMungu hakifichiki Kwake chochote kilichomo ardhini wala kilichomo mbingu.

﴿هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴾

6. Yeye ndiye anaye kuundeni ndani ya matumbo ya wazazi kwa namna apendayo. Hapana mungu ila Yeye, Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu

MAANA

Yamekwishapita maelezo kuhusu (Alif Laam Miim) katika mwanzo wa Sura Baqara. Vile vile maelezo ya hakuna Mola, yameelezwa mwanzo wa Aya Kursiy (2: 255).

Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake.

Makusudio ya Kitabu ni Qur'an; ambayo inasadikisha vitabu vilivyoteremshiwa Mitume waliotangulia. Kimsingi ni kwamba kusadikishwa yaliyoteremshiwa Mitume waliotangulia, hakulazimishi kusadikisha vitabu vinavyonasibishwa kwao na baadhi ya makundi. Na sisi waislamu tumeamini kauli ya Mtume(s.a.w.w) , lakini pamoja na hivyo hatuamini kila kilicho katika vitabu vya Hadith zilizoelezwa kutokana naye. Ama yule anayeamini vitabu vilivyotangulia, basi ni juu yake kuamini Qur'an, vinginevyo atakuwa anajipinga yeye mwenyewe, Kwa sababu Qur'an inasadikisha vitabu hivyo, Kwa hiyo kuikadhibisha Qur'an ndio kuvikadhibisha vitabu vingine.

Na aliteremsha Tawrat na Injil kabla yake, ziwe ni uwongozi kwa watu.

Kuisifu Tawrat na Injil kuwa ni uongozi, kunalazimisha kuwa vimeteremshwa kwa haki; kama ambavyo kuisifu Qur'an kuwa ni uwongozi kunalazimisha kuwa imeteremshwa kwa haki. Kwa hivyo basi, kila kimoja katika vitabu vitatu hivyo ni cha haki na ni uwongozi. Makusudio ya uwongozi hapa, ni ubainisho wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) wa halali na haramu kupitia katika ulimi wa Mitume Yake.Na ubainifu huu unamaanisha kujua hukumu za Mwenyezi Mungu.

Ama kuzitumia hizo hukumu, kunahitaji aina nyingine ya uwongozi zaidi ya ubainifu.Mimi sikupata tamko jengine la kuelezea aina hiyo isipokuwa neno Tawfiq.Nayo inaashiriwa na neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿ إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ﴾

"Kwa hakika wewe huwezi kumwongoza umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoza amtakaye" (28: 56)

Qur'an inalitumia Neno Tawrat kwa maana ya wahyi ulioteremshiwa nabii Musa(a.s) ; na neno Injil kwa Wahyi ulioteremshiwa nabii Isa(a.s) . Lakini Qur'an imebainisha kuwa Tawrat na Injil inayozikubali sio zile zilizoko kwa mayahudi na wakristo hivi sasa. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

﴿مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ﴾

"Miongoni mwa mayahudi wamo ambao huyabadilisha maneno kuyatoa mahali pake" (4:46)

﴿وَمِنَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ أَخَذْنَا مِيثَاقَهُمْ فَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ﴿١٤﴾ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ ﴾

"Na kwa wale waliosema: Sisi ni wanasara (Wakristo) tulichukua ahadi kwao, lakini wakaacha sehemu ya yale waliyokumbushwa… Enyi watu wa Kitabu! Amekwisha wafikia mtume wetu, anayewabainisha mengi mliyokuwa mkiyaficha katika kitabu…" (5:14-15)

Wahubiri wa kimasihi wanayajua sana haya, lakini pamoja na hayo wanajisifu na kuwavunga watu kuwa Qur'an inakiri Tawrat na Injil iliyochezewa na mikono ya kugeuza.

Ilivyo, ni kuwa Qur'an yote ni moja na jumla moja; kwa hiyo haifai kuamini sehemu fulani na kukanusha sehemu nyingine.

Tawrat ni neno la Kiebrania lenye maana ya sharia; nayo imegawanywa kwenye vitabu vitano:

1. Mwanzo, chenye maelezo ya kuanza kuumbwa ulimwengu na habari za Mitume.

2. Kutoka, ndani yake mna historia ya wana wa Israil na kisa cha Musa.

3. Kumbukumbu la Tawrat, humo mna hukumu za sharia ya Kiyahudi.

4. Walawi, humo mna mambo ya ibada na ndege na wanyama walioharamishwa.

Walawi ni kizazi cha mmojawapo wa watoto wa Yakub anayeitwa Lawi.

5. Hesabu, ndani yake mna mkusanyiko wa koo za Wana wa Israil na majeshi yao. Vitabu hivi vitano ni mkusanyiko wa vitabu vidogo vidogo vipatavyo thelathini na tisa, na wakristo wanaviita Agano la kale. Ama Injil, asili yake ni neno la kiyunani; maana yake ni bishara (khabari njema). Na Injili kwa wakristo ni nne:

1. Mathayo: Historia ya kutungwa kwake ina kiasi cha miaka 60 (A.D) Na iliandikwa katika lugha ya kiarmenia.

2. Marko: iliyotungwa kwenye mwaka wa 63 au 65 (A.D) kwa lugha ya kiyunani.

3. Luka: iliyotungwa pia kwa lugha ya kiyunani kwa tarehe ile ya Marko.

4. Yohana: vile vile kwa lugha ya kiyunani kwenye mwaka 90 (A.D.) Rai ya wakristo ilithibiti mwanzoni wa karne ya 5 A.D kwa kutegemea vitabu ishirini na saba katika vitabu vyao. Wakasema kwamba ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mungu kwa kimaana sio kitamko. Na wakavipa jina la Agano jipya, likiwa ni mkabala wa lile la zamani wanalolitegemea mayahudi. Kwa hiyo Agano la zamani, ni agano la Musa; na lile jipya ni la Isa, umepita ufafanuzi unaombatana na hayo katika Sura ya pili, Aya ya tatu.

Na ameteremsha upambanuzi

Yaani upambanuzi baina ya haki na batili. Wametofautiana sana kuhusu makusudio ya upambanuzi; je, ni akili, Zaburi, Qur'an au ni dalili inayopambanua baina ya haki na batili? Sheikh Muhammad Abduh amechagua akili

Mwenye Majmaul Bayan amechagua Qur'an, Tamko la Aya linachukua maana zote mbili

Hakika wale waliozikufuru Aya za Mwenyezi Mungu wana adhabu kali, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kutia adabu.

Wafasiri wanasema kwamba watu wapatao sitini katika wakristo wa Najran, Yemen, walimfikia Mtume mnamo mwaka wa tisa Hijria; mwaka uliojulikana kama mwaka wa ugeni. Kwani wageni wengi walimfikia Mtume kutoka sehemu mbali mbali za Bara Arabu, wakielezea utii na mapenzi yao kwake, baada ya Mwenyezi Mungu kumpa ushindi kwa maadui. Ugeni wa kinajran ulitoa hoja ya itikadi ya kikiristo ya utatu na uungu wa Isa. Kwa hoja ya kuwa Isa ni mtoto asiyekuwa na baba pamoja na miujiza aliyoifanya ambayo Qur'an imeielezea. Vilevile wafasiri wanasema Sura ya Al-Imran kuanzia mwanzo wake hadi Aya thamanini ilishuka juu ya wakristo wa Najran na majibu yao: Mwenyezi Mungu akaanza kwa kutaja Tawhid (umoja) ili kukanusha utatu; kisha akataja Qur'an, Tawrat na Injil kwamba vitabu vitatu hivi vinamwepusha Mwenyezi Mungu na mtoto na kugawanyika. Vilevile vinakanusha uungu wa Isa. Kisha Mwenyezi Mungu akataja:

Hakika Mwenyezi Mungu hakifichiki kwake chochote kilichomo ardhini wala kilichomo mbinguni

Ikiwa ni majibu ya kauli ya wakristo kwamba Isa alikuwa akijua ghaibu. Tena akaendelea Mwenyezi Mungu (s.w.t) kusema:

Yeye ndiye ambaye huwatia sura matumboni jinsi anavyotaka, hakuna Mola isipokuwa Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hekima.

Mwenyezi Mungu anayataja haya ili abatilishe kauli ya Wakristo kwamba Isa ni Mungu kwa sababu ya kutokuwa na baba; kwa maana ya kuwa Mungu haumbwi na kuwa tumboni mwa mama. Akipenda anaweza kumuumba kupitia baba na kama akipenda anaweza kumuumba bila ya baba, kwa kiasi kile hekima yake takatifu inavyotaka. Kwa ufupi ni kuwa kutolea habari baadhi ya mambo ya ghaibu, kufufua baadhi ya wafu na kuzaliwa bila ya baba, hakumaanishi kuwa Isa (Yesu) ni Mungu. Kwa sababu Mungu ni yule anayejua mambo ya ghaibu, hakifichiki kwake chochote katika ardhi au mbinguni, Mwenye kufufua wafu wote sio baadhi, anayeweza kila kitu hata kuumba bila ya kitu kingine. Kwa dhahiri ni kwamba Isa hakuwa akijua ghaibu zote, wala hakuweza kufufua maiti wote na hakuumba yeyote tumboni mwa mama yake bila ya baba au na baba; bali kinyume chake ndio sahihi, kwani yeye ndiye aliyeumbwa ndani ya tumbo la uzazi

﴿هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴾

7.Yeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu ndani yake zimo Aya zilizo waziwazi ambazo ndizo msingi wa Kitabu na nyingine zenye kufichikana. Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazotatiza kwa kutaka kuharibu na kutaka tafsiri yake. Na hajui tafsir yake isipokuwa Mwenyezi Mungu na waliozama katika elimu. Husema tumeziamini zote zimetoka kwa Mola wetu, Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili.

﴿رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ﴾

8.Mola wetu! Usizipotoshe nyoyo zetu baada ya kutuongoza na utupe rehema kutoka kwako, Wewe ndiwe mpaji mkuu.

﴿رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴾

9.Mola wetu! Wewe ndiwe mwenye kuwakusanya watu katika siku isiyo na shaka ndani yake, Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi.

Aya 7 - 9

Yeye ndiye aliyekuteremshia Kitabu ndani yake zimo Aya zilizo waziwazi nazo ndizo msingi wa kitabu, Na nyingine zenye kufichikana.

Zilizo waziwazi ni Aya ambazo hazihitaji ufafanuzi na makusudio yake yanafahamika kwa njia ya mkato bila ya kuhitaji tafsiri, kuhusisha au kufutwa hukumu (Naskh). Wala haziwapi nafasi wale wenye maradhi ya kupoteza na kufikiri kwa taawili na kugeuza. Mfano: sema Yeye Mwenyezi Mungu ni mmoja Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila jambo Wala hadhulumu (hata amali) sawa na chembe Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi uovu...Na kwamba Kiyama kitakuja hakuna shaka.

Na Aya nyenginezo ambazo anaweza kuzifahamu mwenye elimu na asiyekuwa na elimu. Ama Aya zenye kufichikana ziko aina nyingi: Kuna zinazofahamika kiujumla bila ya upambanuzi, mfano kauli yake Mwenyezi Mungu:

Na tukampulizia katika roho yetu (21:91) Kwa hakika kujua roho yenyewe hasa ni nini, hiyo ni siri ya Mungu haijui yeyote hata wataalamu pia. Na wala sio sharti anayeambiwa kitu kuwa lazima ajue anayoambiwa kwa upambanuzi, bali inatosha tu kufahamu kiujumla.

Nyengine ni zile zinazofahamisha jambo linalokataliwa na akili mfano, kauli yake Mwenyezi Mungu:

﴿الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴾

"Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema amestawi juu ya kiti cha enzi." (20:5)

Hapa akili inakataa kwamba Mwenyezi Mungu akae juu ya kiti, kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni zaidi ya wakati na mahali. Kwa hiyo hapo inabidi kuleta tafsiri kwa maana ya kutawala. Na hapana budi kuwa tafsiri (taawil) iwe ni dalili sahihi itakayotoa maana sahihi ya tamko; na hayo hawayajui isipokuwa watu maalum. Aya nyingine iliyofichikana, ni kukubali tamko baina ya maana mbili na zaidi, mfano:

﴿وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ﴾

Na wanawake walioachwa wangoje mpaka tohara tatu (2: 228)

Hapo kuna 'Quruw' ambalo linakubali maana ya tohara na hedhi. Nyengine ni kuwa tamko ni la kiujumla maana yake ya dhahiri yawaingiza wote ingawaje makusudio ni baadhi tu; mfano:

﴿وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا ﴾

"Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikatwe mikono yao" (5:38)

Hapo wametajwa wezi wote pamoja na kujulikana kuwa kuna wezi wengine hawakatwi; kama ikiwa mwizi ni baba wa aliyeibiwa, au mwaka wa njaa, au kilichoibwa kikiwa hakikuhifadhiwa, au thamani ya kilichoibiwa ikiwa chini ya robo dinari. Nyengine ni kufutwa hukumu na kuwekwa nyengine; kama vile kuswali kuelekea Baitul Maqdis, ambapo ilifahamika kuthibiti Kibla hiki na ikaendelea hukumu mwanzoni mwa uislam, kisha ikaja hukumu ya kufuta hilo na Kibla kikawa Al-kaaba.Sio sharti kutotarajiwa kujulikana Aya za kufichikana kabisa. Kwani aina zote ukiondoa ile ya kwanza, inawezekana kwa wanavyuoni wa Usul - wanaojua njia za taawili, hukmu za kuhusisha na za kiujumla, kufuta na kufutwa na kutilia nguvu baina hukumu mbili zinazopingana - kutoa hukmu za kuhusisha na za kiujumla, kupambanua baina ya kufuta na kufutwa, chenye nguvu na kisicho na nguvu na maana yanayoingilika akilini ambayo yamefanyiwa taawili baada ya kutoingilika akilini.

Ndio! Kwa asiyekuwa na elimu, hizo Aya za kufichikana zinabaki kuwa hivyo hivyo, kwa kuwa haijuzu kufanya taawili au kuchukua dhahiri inayokubali kuhusisha au kufutwa. Kwa ufupi ni kuwa wanavyuoni wanajua maana ya Qur'an ambayo kwao ni fasihi iliyo wazi. Kwa sababu haiwezekani kuwa Mwenyezi Mungu ateremshe maneno yasiyokuwa na maana au yasiyofahamiwa na yeyote. Itakuwaje hivyo ikiwa yeye mwenyewe Mwenyezi Mungu anaamrisha kuizingatia vizuri Qur'an; na mazingatio hayaji ila kwa kinachoingilika akilini; na kisichofahamika hakiwezi kuzingatiwa.

Unaweza kuuliza kuwa Mwenyezi Mungu amekisifu Kitabu Chake kitukufu kwamba Aya zake zote ni Muhkam (zenye maana wazi) pale alipotumia neno Uhkimat (11:1) Tena akasifu kuwa Aya zake zote ni Mutashabihat (zenye kufichikana) kwa kutumia neno Mutashabihat (39: 29). Na katika Aya hii tunayofasiri amekisifu kuwa baadhi yake ni zenye kufichikana na nyengine ziko wazi wazi. Je, Kuna njia gani ya mkusanyiko wa Aya hizi? Jibu: Makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu katika neno Uhkimat ni kuwekwa kwa mpango na kwamba yote ni fasaha iliyo na maana sahihi. Kwa hiyo tafsiri ni:

"(Hiki) ni Kitabu ambacho Aya zake zimepangwa vizuri" Makusudio ya Mutashabihat (kufichikana) ni kibalagha na kimwongozo. Kwa hiyo tafsiri ni: "Kitabu chenye kushabihiana"

Na kuwa nyengine ni Muhkamat na nyengine ni Mutashabihat, ni kama tuliyvotangulia kuelezea kuwa ni baadhi ziko wazi na baadhi zinatatiza zinazohitaji tafsir na tafsir inahitaji maarifa na elimu. Kwa hiyo hakuna mgongano baina ya Aya hizo tatu; ni kama mfano wa mwenye kusema: "Napenda safari, wala sipendi safari" lakini anakusudia kuwa anapenda safari katika nchi kavu lakini hapendi safari ya baharini. Sufi mmoja aliisema kumwambia Mola wake: Ee Mungu nimuonaye, hali yeye hanioni. Ee Mungu anionaye,wala mimi simuoni. Anakusudia kwamba anamuona Mwenyezi Mungu akimfadhilisha lakini Mwenyezi Mungu hamuoni yeye akimtii,na Mwenyezi Mungu anamuona akimuasi wala yeye hamwoni akimwadhibu.

Swali la pili, nini makusudio ya msingi wa Kitabu?

Jibu : Baada ya Mwenyezi Mungu kuelezea kwamba katika kitabu chake kuna Aya zenye kutatiza, ndipo akasema; lakini Aya za misingi ya itikadi - kama vile kumwamini Mwenyezi Mungu na kumwepusha na mshirika vilevile kuuamini utume wa Muhammad(s.a.w.w) na siku ya mwisho - ziko wazi zenye kubainisha makusudio bila ya mikanganyo yoyote; wala hazina nafasi ya kufanyiwa taawili, kuhusishwa au kuwa imefutwa hukumu yake; anaweza kuzifahamu mjuzi na asiyekuwa mjuzi; wakati huo zikiwa ni msingi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa sababu zinaeleza itikadi, na nyenginezo ni matawi.

Kwa hiyo hakuna udhuru wowote kwa ugeni wa Yemen na wengineo kutaka Aya za kutatiza; kama vile Aya inayomsifu Isa kuwa roho wa Mwenyezi Mungu na kuacha Aya zilizo waziwazi zinazokanusha uungu wa Isa. Hakuna lolote kwa mwenye kujitia kutojua Aya waziwazi na kutaka Aya zinazotatiza isipokuwa ni maradhi ya moyo na kukusudia ufisadi tu. Swali la tatu: Kwa nini amesema: Msingi wa kitabu na asiseme Misingi ya kitabu.

Jibu : Amefanya umoja kwa kubainisha kwamba mkusanyiko wa Aya zote nyepesi kufahamika ni msingi wa Kitabu na wala sio Aya moja pekee kuwa ni msingi; mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu.

﴿وَجَعَلْنَا ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ آيَةً﴾

"Na tulimfanya mwana wa Maryam na mama yake ishara" (23:50).

Ishara moja, wala hakusema ni ishara mbili, kwa sababu kila mmoja ni fungu la kutimiza ishara kwa hiyo mama hawezi kuwa ishara bila ya mwana, na mwana hawezi kuwa ishara bila ya mama.

Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazotatiza kwa kutaka kuharibu na kutaka tafsiri yake.

Makusudio ya upotofu hapa ni kuiacha haki, na kutaka kuharibu ni ishara ya kwamba wenye makusudio mabaya wanatafuta yale yenye kutatiza na kuyafasiri kwa tafsiri ya kuharibu nyoyo na kuharibu watu na dini ya haki, kwa mfano wanatoa ushahidi kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na tukampulizia roho yetu" kwamba Masih ni jinsi ya Mwenyezi Mungu kwa sababu kila mmoja ni roho, na wanajitia kutojua Aya zilizo waziwazi mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu:

﴿لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ﴾

"Hakika wamekufuru wale waliosema: Mwenyezi Mungu ni Masih mwana wa Maryam." (5:17)

﴿مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ﴾

"Hakuwa Masih ila ni Mtume, na wamepita Mitume kabla yake, na mama yake ni mkweli." (5:75)

﴿ إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴾

"Hakika mfano wa Isa mbele za Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia kuwa akawa." (3:59)

Zaidi ya hayo kuna Aya inayomuhusu Adam, isemayo:

﴿فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي ﴾

"Nikishamkamilisha na kumpuliza roho yangu" (15:29)

Kwa hiyo basi kutokana na madai yao, Adam pia atakuwa ni Mungu. Katika Majmaul-bayan imeelezwa kuwa mwanzo wa Sura Al-imran mpaka zaidi ya Aya themanini, zimeshuka kwa ugeni wa Najran. Walikuwa watu sitini, wakafika Madina kwa Mtume. Ulipofika wakati wao wa kuswali walipiga kengele na wakaenda kuswali katika msikiti wa Mtume. Masahaba wakasema: "Mbona wanaswali msikitini kwako?" Mtume akasema: "Waacheni" Basi wakaswali wakielekea Mashariki. Walipomaliza kuswali, Mtume alimwambia Seyyid na Aqib ambao walikuwa viongozi wa msafara na majibizano yakawa kama hivi ifuatavyo: Mtume: Silimuni wakristo:

Wakristo: Tumekwisha silimu.

Mtume: Mmesema uongo, si waislamu kwa kudai kwenu kuwa Mwenyezi Mungu ana mtoto, kuabudu msalaba na kwa kula nyama ya nguruwe.

Wakristo: Ikiwa Isa si mtoto wa Mwenyezi Mungu, basi baba yake ni nani?

Mtume: Hamjui kwamba mtoto hufanana na baba yake?: "Hamjui kwamba Mwenyezi Mungu yuko hai, hafi? Na Isa alitoweka?

Wakristo: "Ndio."

Mtume: Hamjui kwamba Mwenyezi Mungu ni msimamizi wa kila kitu?

Wakristo: Ndio

Mtume: Je, Isa anaweza hivyo?

Wakristo: La!

Mtume: Hivi hamjui kuwa Mwenyezi Mungu hali, hanywi wala haendi chooni?

Wakristo: Ndio

Mtume: Hamjui kuwa Isa alichukuliwa mimba na mama yake, kama wanawake wengine, akanyonyeshwa na akalishwa chakula na kwamba Isa anakula ana kunywa na kwenda haja?

Wakristo: Ndio

Mtume: Basi atakuwaje Mungu?

Wakristo: Wakanyamaza wasiwe na la kusema, Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha kuwahusu, mwanzoni mwa Sura Al-imran kiasi cha Aya thamanini.

Na hajui tafsiri yake isipokuwa Mwenyezi Mungu na waliozama katika elimu.

Baadhi ya watu wanasema ni wajibu kuweka kituo kati ya neno Mwenyezi Mungu na waliozama; na kwamba waliozama ni maneno yanayoanza upya; kwa maana ya kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayejua Aya zenye kutatiza, na sio waliozama katika elimu. Kitu cha kuangalia katika kauli hii ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni Mwenye hekima, hawezi kuwaambia watu wasivyovijua na asivyotaka wajue; kama tulivyobainisha. Kwa hiyo sahihi ni kuwa neno 'waliozama katika elimu, linaugana na Mwenyezi Mungu; na kwamba maana yake ni anajua tafsiri yake Mwenyezi Mungu na waliozama katika elimu. Amirul-muminin Ali(a.s) anasema:"Hiyo ni Qur'an iliyonyamaza na mimi ni Qur'an inayosema"

Na Ibn Abbas alikuwa akisema: "Mimi ni miongoni mwa waliozama kaitka elimu; mimi ninajua tafsiri yake" Kwa ujumla ni kwamba mwenye elimu ya haki ni yule anayeepuka kusema bila ya ujuzi. Bali huko kuzama katika elimu ni kuepuka kusema bila ya ujuzi. Iko Hadith isemayo: "Kuepuka yenye kutatiza ni bora kuliko kujingiza katika maangamizi." Unaweza kuuliza kwa nini Mwenyezi Muangu (s.w.t) amefanya baadhi ya Aya za Qur'an ziwe wazi na nyengine zilizofichika? Kwa nini asizijalie kuwa waziwazi zote ? Ili aweze kufahamu mjuzi na asiyekuwa mjuzi?

Swali hilo limejibiwa kwa majibu mengi, lenye nguvu zaidi ni kwamba mwito wa Qur'an unamwelekea mjuzi na asiye na ujuzi, mwerevu na mjinga; na kwamba katika maana yako yaliyo maarufu na yenye kuzoeleka na wote hawahitajii elimu na kujifunza katika kuyajua; yanaweza kueleweka kwa ibara iliyo wazi anayoifahamu kila anayeambiwa. Maana nyengine yako ndani yasiyoweza kufahamiwa ila baada ya darasa na elimu.Wala haiwezekani kufahamika bila ya maandalizi hayo.

Hakika hii anaifahamu kila mtu, Basi hayo ndiyo yaliyofanya kuwa baadhi ya Aya ziwe dhahiri na nyengine za ndani; kuongezea kuwa mara nyengine hekima inataka kuweka maana ya ndani; kama kusema kwake Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mtume wake:

﴿وَإِنَّا أَوْ إِيَّاكُمْ لَعَلَىٰ هُدًى أَوْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴾

Hakika sisi au nyinyi tuko kwenye uongofu au upotevu ulio wazi (34:24)

Husema: "Tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu."

Hii ni jumla iliyoanza upya. Maana yake ni kuwa mjuzi wa haki husema kuwa Aya zilizofichikana na zile nyepesi zote ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na mwenye kuziacha nyepesi na kujishughulisha na za kutatiza tu, kwa kutaka kuharibu basi huyo ni mfisadi mwenye maradhi ya moyo.

Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili

Wale ambao wanajua hekima katika kupatikana za waziwazi na zisizowazi katika Qur'an wala hawazifanyi zile zilizo wazi kuwa ni njia ya kupoteza

"Mola wetu! Usizipotoshe nyoyo zetu baada ya kutuongoza na utupe rehema kutoka kwako. Wewe ndiwe mpaji mkuu"

Hiyo ni dua anayoiomba kila mjuzi mwenye ikhlasi kwa kuhofia asiingie makosani na kufanya uzembe katika kutafuta yaliyo sawa.

﴿إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا وَأُولَـٰئِكَ هُمْ وَقُودُ النَّارِ﴾

10.Hakika wale ambao wamekufuru hazitawafaa kitu mali zao na watoto wao kwa Mwenyezi Mungu; na hao ndio kuni za Moto.

﴿كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ وَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴾

11.Kama desturi ya watu wa firauni na wale waliokuwa kabla yao. Walikadhibisha Aya zetu, Mwenyezi Mungu akawatia adabu kwa sababu ya dhambi zao; na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

﴿قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴾

12.Waambie wale waliokufuru: Mtashindwa na mtakusanywa mtiwe kwenye Jahannam; nako ni makao mabaya.

﴿قَدْ كَانَ لَكُمْ آيَةٌ فِي فِئَتَيْنِ الْتَقَتَا فِئَةٌ تُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَأُخْرَىٰ كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُم مِّثْلَيْهِمْ رَأْيَ الْعَيْنِ وَاللَّـهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِ مَن يَشَاءُ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُولِي الْأَبْصَارِ ﴾

13.Hakika ilikuwa ni ishara kwenu katika yale makundi mawili yalipokutana. Kundi moja likipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na jingine kafiri, likawaona mara mbili zaidi kuliko wao kwa kuona kwa macho hakika katika hayo kuna mazingatio kwa wenye busara.

Hazitawafaa kitu mali zao na watoto wao

HAZITAWAFAA KITU MALI ZAO NA WATOTO WAO

Aya 10 -13

MAANA

Hakika wale ambao wamekufuru hazitawafaa kitu mali zao na watoto wao kwa Mwenyezi Mungu; na hao ndio kuni za moto.

Mwenye kufuatilia Aya za Qur'an, yenye hekima, kuhusu kuwazungumzia matajiri, ataziona kuwa zinawataja kwa sifa mbalimbali mbaya kama ifuatavyo:

-Ujeuri, Mwenyezi Mungu anasema:

﴿ كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾ أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴾

Hakika binadamu hupetuka mipaka kwa kujiona amejitosha (96: 6-7)

–Kuhadaika, Mwenyezi Mungu anasema:

﴿وَدَخَلَ جَنَّتَهُ وَهُوَ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ قَالَ مَا أَظُنُّ أَن تَبِيدَ هَـٰذِهِ أَبَدًا ﴿٣٥﴾ وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً﴾

"Na akaingia katika bustani yake na hali ya kuwa anajidhulumu nafsi yake akasema: "Sidhani kabisa kuwa itaharibika. Wala sidhani kuwa kiyama kitatokea…" (18: 35-36)

-Tamaa Mwenyezi Mungu anasema:

Na nikamjaalia awe na mali nyingi Kisha anatumai nimzidishie.(74:12-15)

-Kuwa na mawazo potofu kwamba mali itawakinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu anasema:

﴿وَقَالُوا نَحْنُ أَكْثَرُ أَمْوَالًا وَأَوْلَادًا وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴾

"Na wakasema: 'sisi tunazo mali nyingi na watoto wengi wala sisi hatutaadhibiwa." (34:35)

Mwenyezi Mungu ameziondoa dhana zote hizi kwa kusema kwamba mali na watoto hazitoshelezi kitu, bali mali zitamfanya aliye nazo kuwa kuni kesho; kama vile miti. Wapotofu wanadhani kwamba mali zao na watoto wao wataweza kuwahami hapa duniani, lakini wanapokabiliana na wenye haki ana kwa ana katika uwanja wa vita hubainika unyonge wao. Kwa sababu Mungu huwapa nguvu wakweli kwa nusura yake na humdhalilisha yule mfisadi aliye mwongo sana.

WENYE MALI

Historia haijajua watu waovu na wadhalimu wakubwa zaidi wakati huu kuliko wenye mali na utajiri waliolundika. Wao ndio wanaoleta fitina, uharibifu na vita; wanapanga kila mbinu kujaribu kuzuia harakati zozote za ukombozi popote pale ulimwenguni. Wanaanzisha vyama vya vibaraka wao, vikosi vya umoja, wapelelezi na majasusi katika pembe zote za dunia ili waugeuze ulimwengu uwe ni kinyang'anyiro cha shirika la mamilionea. Wao hawaamini Mungu wala utu au jambo lolote isipokuwa wanaamini hisa ambazo zitanyonya faida kutoka katika jasho la watu, damu yao na mustakbali wao. Dola zao zinajishughulisha kueneza hofu, wasiswasi na ukandamizaji wa kichumi na kisiasa kwa wanyonge. Wanatumia kila mbinu kuwagawaya watu wasiwe na umoja, ili watu wote wawatumikie wao.

Kwa ajili hiyo, ndipo uislamu ukaharamisha ulanguzi na utajiri usiofuata sharia na kuwakandamiza wanyonge. Na umewatisha wale wanaolimbikiza mali bila ya kuzitoa sabili na kuita wapetukaji mipaka.

Kama desturi ya watu wa firaun na wale waliokuwa kabla yao; walikadhibisha Aya zetu Mwenyezi Mungu akawatia adabu kwa sababu ya dhambi zao na Mwenyezi Mungu ni mkali wa adhabu.

Yaani wingi wa mali na watoto sio sababu ya kufuzu na kuokoka. Mara nyingi mafukara wameshinda matajiri na uchache ukashinda wingi. Historia imejaa ushahidi wa ukweli huu. Firaun na watu wake walikuwa wengi wenye jaha, usultani, mali na vifaa, lakini pamoja na hayo Mwenyezi Mungu aliwafedhehesha na kumpa ushindi Musa asiyekuwa na mali wala wingi wa watu; kama ambavyo alimpa ushindi Nuh kwa watu wa zama zake, Ibrahim kwa Namrud, Hud kwa Ad na Saleh kwa Thamud. Kwa hiyo wingi na utajiri sio hoja, Na wanaomkadhibisha Mtume Muhammad(s.a.w.w) nao mwisho wao utakuwa hivyo hivyo.

Waambie wale waliokufuru: Mtashindwa na mtakusanywa mtiwe katika Jahannam, nako ni makao mabaya.

Imeelezwa katika Majamaul-bayan kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) alipompa ushindi Mtume wake katika vita vya Badr,alipofika Madina Mtume aliwakusanya Mayahudi na kuwaambia: "Tahadharini yasije yakawapata yaliyowapata maquraish katika Badr." Wakamwambia: "Usihadaike, wewe umekutana na watu wasiojua vita; lau ungelikutana na sisi ungelijua kwamba sisi ni watu;" ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii. Mwenyezi Mungu alitimiza miadi yake: Waislamu wakawaua Bani Quraydha wahaini na wakawafagia Bani Nadhir wanafiki, wakaichukua Khaybar na wakawatoza kodi wengine.

Hakika ilikuwa ni ishara kwenu katika yale makundi mawili yalipokutana na kundi moja lilipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na jingine kafiri, likiwaona mara mbili zaidi kuliko wao kwa kuona kwa macho.

Mwenyezi Mungu katika Aya hii anawaonyaMayahudi, manaswara, waislamu na wenye busara wote kwa ujumla kuhusu vita vya Badr wakati kilipokutana kikosi cha Mtume ambacho ni Muhammad na sahaba zake na kikosi cha shetani ambacho kilikuwa zaidi ya watu elfu, wakiwa wamejisheheneza silaha za kutosha. Na kikosi cha Mtume kilikuwa ni theluthi tu ya idadi yao, wakiwa hawana zana zozote zaidi ya farasi wawili, deraya saba na panga nane, lakini pamoja na hayo Mungu aliwaandikia ushindi hao wachache; Mwenyezi Mungu akawaonyesha washirikina kuwa waislamu ni zaidi yao ingawaje ni wachache.

Aya hii iko katika mwelekeo wa Aya inayosema:

﴿وَإِذْ يُرِيكُمُوهُمْ إِذِ الْتَقَيْتُمْ فِي أَعْيُنِكُمْ قَلِيلًا وَيُقَلِّلُكُمْ فِي أَعْيُنِهِمْ لِيَقْضِيَ اللَّـهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴾

"Na mlipokutana, akawaonyesha machoni mwenu kuwa wao ni wachache na akawafanya nyinyi ni wachache machoni mwao, ili Mwenyezi Mungu atimieze jambo lililokuwa liwe, Na mambo yote hurejezwa kwa Mwenyezi Mungu" (8:44)

Kwa mnasaba huu ni vizuri tutaje nasaha ya Imam Ali(a.s) kwa khalifa wa pili alipomtaka ushauri katika vita vya Roma; Imam alisema:

"Yule aliyenusuru Waislamu wakiwa ni wachache bado yuko hai, hafi, wewe ukienda mwenyewe katika vita na ukakimbia basi waislamu hawatakuwa na ngome wala kimbilio. Wewe mpeleke mtu mwenye uzowefu na umwandalie watu wenye uzoefu na wenye ushauri. Ikiwa Mwenyezi Mungu atakudhihirisha ndivyo unavyotaka, vinginevyo utakuwa ni kimbilio la watu.

﴿زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ﴾

14.Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake na watoto na mirundo ya dhahabu na fedha, na farasi wazuri, na mifugo na mashamba. Hivyo ni vitu vya anasa katika maisha ya dunia; na kwa Mwenyezi Mungu ndiko kwenye marejeo mazuri.

KUPENDA MATAMANIO

Aya 14

MAANA

Wametofautiana wafasiri kuwa ni nani anayewafanya watu kupenda matamanio. Baadhi wamesema ni Mwenyezi Mungu na wengine wakasema ni shetani. Lakini ukweli ulivyo, ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amempa mtu tabia ya kupendelea matamanio na shetani naye humtia wasiwasi mtu na kumfanyia nzuri amali mbaya; na ile mbaya anamfanyia aione nzuri. Hata hivyo kupenda wanawake, watoto na mali siko kubaya hasa; na wala Mwenyezi Mungu hakutuharamishia. Vipi isiwe hivyo na hali yeye Mwenyezi Mungu amesema: Waambie nimewahalalishia mema. Na Mtume(s.a.w.w) amesema: "Mimi ninapenda vitu vitatu katika dunia yenu: Manukato, wanawake, na kitulizo cha moyo wangu, Swala"

Makusudio ya matamanio hapa ni vitu anavyovipendelea mtu na kuhisi raha anapovipata. Unaweza kuuliza neno matamanio linakusanya maana ya mapenzi; kama ambavyo mapenzi yanakusanya maana ya matamanio. Kwa hivyo basi maana ya Aya yatakuwa kwamba watu wanapenda mapenzi na wanatamani matamanio, Na maneno ya Mwenyezi Mungu hayawezi kuwa katika hali hii ya kutonyooka.

Jibu : Kupenda kitu kuko namna mbili:

Kwanza : ni mtu kupenda kitu, lakini hapendi akipende, yaani nafsi yake inapenda kama ingewezekana asikipende kitu hicho, Kwa mfano mtu kupenda kuvuta sigara inayomdhuru, Mwenye pendo hili anataka limwondokee kila siku.

Pili : ni mtu kupenda kitu na yeye mwenyewe yuko radhi; kama mtu aliyezoweya kufanya amali za kheri. Mwenyezi Mungu anasema katika kumzungumzia Nabii Suleiman:

Hakika mimi ninapenda pendo la kheri (38:32)

Hili ni pendo la hali ya juu na mwenye pendo hilo hataki limwondokee.

Mrundo ni fumbo la wingi. Hadith inasema: "Lau mtu angekuwa na nyangwa mbili za dhahabu, basi angelitamani wa tatu; na wala hawezi kutosheka isipokuwa kwa mchanga." Kupenda wanawake, watoto na mali, kunapatikana wakati wote bali hayo ni matamanio ya kila nafsi. Ama kupenda farasi, wanyama na mashamba, Mwenyezi Mungu amekuhusisha kukutaja kwa wakati huo kwa sababu ndio vitu vilivyopendelewa zaidi. Wafasiri wengi kama vile Razi na mwenye Al-manar wamerefusha maneno katika kutaja kila moja katika aina hizi sita za ladha na starehe, lakini wametaja mambo ya dhahiri yanayojulikana na kuhisiwa na wote. Kwa hiyo hatukujishughulisha nayo na tunaonelea ni vizuri tutaje raha katika kifungu kinachofuatia.

RAHA

Baadhi ya watungaji wanaona kuwa raha inaweza kukamilika kwa binadamu kama akiwa na nguzo hizi nane: Afya, mke anayeafikiana naye, mali ya kutekeleza haja na jaha itakayohifadhi utukufu. Nafikiri mwenye rai hii ameangalia raha kwa upande wake na haja yake, sio kwa ilivyo hasa. Kama ni hivyo ataziweka wapi hisia za matatizo ya kilimwengu; kama vile hofu, mwisho mbaya na uongo, na matatizo mengineyo yanayousonga moyo. Kwa kweli kabisa raha kamili bado haijapatikana kwa binadamu; na ninafikiri haitapatikana katika maisha haya, ispokuwa maisha mengine. Ama raha ya upande fulani na wakati fulani imeweza kumpitia mtu, ijapokuwa utotoni. Ni vizuri kufafanua raha ya upande fulani kama ifutavyo: Kustarehe kuko kwa aina nyingi, kama kustarehe kwa kuangalia miti wakati wa maleleji na mito na maporomoko ya maji, au kusikiliza mashairi, au kustarehe kwa kusoma vitabu, na mengineyo katika mambo ya starehe za kiroho.

Katika starehe za kimaada ni wanawake, mali na watoto. Ama farasi wanyama na mashamba hiyo ni katika jumla ya mali. Lakini starehe hizi zote hazimpi binadamu raha kamili, kwa sababu dunia haimnyookei yeyote kwa kila upande. Akiwa ana uwezo wa kuyamudu maisha, basi atakuwa na matatizo ya nyumbani au katika uzao wake. Amirul Muumini Ali (a.s.) anasema: "Akipata raha mtu upande mmoja, atapata uchungu upande mwengine, Hawezi kupata mtu starehe ila atapata tabu" Ama raha ya upande fulani tu yaani katika hali fulani hiyo anaipata mtu. Mfano mzuri ni ule niliousoma katika baadhi ya vitabu. Mtungaji anasema: Familia moja ilitoka kwenda kwenye matembezi; akiwemo mama, watoto, ami, mjomba, baba na babu. Walipofika wanapokwenda, mtoto alielekea kwenye nyasi, mwengine akachuma maua, mama naye akatengeneza sandwichi, ami akatafuna tofaha, mjomba akazungusha gramafoni (kinanda), baba akajinyoosha mchangani akiwa anaangalia kondoo na babu naye akawa anajishughulisha na kuvuta buruma.

Basi ikawa kila mmoja anahisi raha kwa upande wake, lakini raha hiyo ni katika hali hiyo tu, sio katika hali zote, Hekima ya Mungu imepitisha kuwa raha kamili haiwezi kupatikana isipokuwa akhera. Kwa sababu hii ndipo akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya kutaja wanawake, watoto na mali kuwa kuna kilicho bora zaidi ya hivyo. Nimeona Riwaya kutoka kwa Imam Jaffar Sadiq(a.s) akizingatiya kuwa tawfiki ya Mungu ni nguzo miongoni mwa nguzo za msingi wa raha. Na, hakika hii nimeijua kwa hisia na majaribio.

﴿قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴾

15.Sema: Je, niwambie yaliyo bora kuliko hayo kwa kwa wamchao Mungu? Kwa mola wao ziko bustani ambazo hupita chini yake mito; watakaa humo milele na wake waliotakaswa na wana radhi ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu anawaona waja.

﴿الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴾

16.Ambao wanasema: "Mola wetu! Hakika sisi tumeamini,basi tughufirie madhambi yetu. Na tuepushe na adhabu ya moto.

﴿الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ ﴾

17.Wanaofanya subira na wanaosema kweli na watiifu na wanaotoa na wanaoomba maghufira kabla ya Alfajiri.

YALIYOBORA

Aya 15-16

MAANA

Sema: Je, Niwaambie yaliyo bora kuliko haya kwa wamchao Mungu?

Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwanza ametaja kupenda wanawake, mali na watoto; kisha vitu vyote hivi akaviita anasa za dunia, na dunia inaondoka; na akabainisha kwamba kwake ndiko kwenye marejeo mazuri, yaani kwamba mtu baada ya kurejea kwa Mola wake atakuta mambo mazuri zaidi kuliko wanawake, mali na watoto na kuliko dunia yote. Baada ya hapo ndipo anafafanua kwa Aya hii.

Kwa Mola wao ziko bustani ambazo huipita chini yake mito; watakaa humo milele na wake waliotakaswa na wana radhi ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anawaona waja.

Haya matatu ni bora kuliko wanawake, mali na watoto, nayo ni marejeo mazuri.

Kwanza : ni, pepo ambayo haitakwisha sio kama shamba, farasi na mifugo.

Pili : ni wanawake waliotakaswa na hedhi, hadathi na uchafu wote. Vilevile wametakaswa na kila kinyaa.

Tatu : ni radhi ya Mwenyezi Mungu ambayo ni kubwa zaidi kuliko dunia na akhera kwa pamoja. Yote hayo Mwenyezi Mungu ameyafanya ni malipo ya mwenye kuogopa kusimama mbele za Mola wake na akaikataza nafsi (yake) na matamanio.

Wanaofanya subira, na wanaosema kweli na watiifu na wanaotoa na wanaoomba maghufira kabla ya Alfajiri.

Mwenye kusubiri ni yule anayekabiliana na mambo kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu; na kuridhia natija ya makabiliano yake. Msema kweli ni yule anayesema ukweli hata kama unamdhuru. Mtiifu ni yule mwenye kufanya ibada akiwa mtiifu. Mtoaji ni yule anayejitolea mali na kuwatolea watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na, wakati wa kabla ya alfajiri; ni wakati bora kuliko wowote kwa ibada na dua; kama ilivyoelezwa katika Hadith. Kwa sababu wakati huo uko mbali kabisa na shub'ha ya ria; Na, ni wakati ambao usingizi ni mtamu sana; kwa hivyo inakuwa tabu kuamka. Na amali bora zaidi ni ile yenye mashaka na tabu, ingawaje kuhudumia mtu ni bora zaidi kuliko Swala na Saumu.

MATUNDA YA IMANI

Sifa zote hizi tano (subira, ukweli, utiifu, kutoa na msamaha) ni matunda ya misingi mitatu ya dini; yaani kumwamini Mwenyezi Mungu mmoja aliye pekee, kuamini utume wa Muhammad(s.a.w.w) na kuamini siku ya mwisho. Misingi hii siyo kuwa ni mambo tu ya dini, bali inayo matunda na hakika zinazokusanywa na umbile tukufu, na amali yenye kunufaisha katika uhai. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ﴾

"Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume atakapowaita katika yale yatakayowapa maisha, (8:24)

Kila asili katika asili ya dini inasimama kwa misingi hii. Vilevile kila tawi katika matawi ya dini, ni misingi inayofungamanisha dini na matendo kwa ajili ya maisha. Mwenyezi Mungu anasema:

﴿فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٩٢﴾ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴾

Basi naapa kwa Mola wako tutawauliza wote. Juu ya yale waliyokuwa wakiyatenda. (15: 92 - 93)

﴿أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ ﴾

Je, mnadhani mtaingia peponi, bila ya Mwenyezi Mungu kuwapambanua wale waliopigana Jihadi miongoni mwenu na kuwapambanua waliofanya subira? (3:142)

Zimekuja Hadith kadhaa Mutawatir kwamba aina bora ya ibada na utiifu ni kufanya amali kwa ajili ya maisha mema na kwamba kubwa ya madhambi makubwa na maasi ni ufisadi na uadui kwa watu. Mtume anasema: "Karibu zaidi anapokuwa mja na Mola wake ni pale anapotia furaha katika moyo wa nduguye." Amirul-Muminiin anasema: "Masurufu mabaya siku ya marejeo ni uadui kwa waja" Mjukuu wake, Imam Baqir, naye anasema: "Mwenyezi Mungu ana watu waliobarikiwa, watu wengine wanaishi katika hifadhi zao; nao ni kama tone. Na kuna watu ni vikwazo, wala watu wengine hawaishi katika hifadhi zao; nao ni kama nzige kila kitu wanakitaka"

﴿شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴾

18.Mwenyezi Mungu na Malaika na wenye elimu wameshuhudia ya kwamba hakuna Mola ila Yeye tu, Ndiye Mwenye kusimamia uadilifu. Hakuna mola isipokuwa Yeye,Mwenye nguvu Mwenye hekima.

﴿إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّـهِ فَإِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴾

19.Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na hawakukhitalifiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia ilimu. Kwa uhasidi uliokuwa baina yao. Na anayezikataa Aya za Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

﴿ فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوا وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴾

20.Na kama wakikuhoji, basi sema: "Nimeusalimisha uso wangu kwa kumwelekea Mwenyezi Mungu, na walionifuata" Na waambie wale waliopewa Kitabu na wale wasiokuwa na kisomo na "Je,mmesilimu? Kama wakisilimu basi wameongoka; na kama wakikengeuka, basi juu yako ni kufikisha tu. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaona waja

MWENYEZI MUNGU, MALAIKA NA WENYE ELIMU

Aya 18 - 20

MAANA

Mwenyezi Mungu na Malaika na wenye elimu wameshuhudia ya kwamba hakuna Mola isipokuwa yeye; Ndiye mwenye kusimamisha uadilifu, Hakuna Mola isipokuwa Yeye, Mwenye nguvu Mwenye hekima.

Kujishuhudia Mwenyezi Mungu yeye mwenyewe kuwa ni mmoja ni kutokana na vitendo Vyake ambavyo haviwezi yeyote isipokuwa Yeye; Mwenyezi Mungu anasema:

﴿سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ﴾

"Tutawaonyesha ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao mpaka iwabainikie kuwa haya ni haki, Je haikutoshi kwamba Mola wako ni shahidi wa kila kitu" ? (41:53)

Ama ushuhuda wa Malaika kwa umoja wa Mungu ni kwamba wao wana maumbile ya imani. Makusudio ya wenye elimu hapa ni Mitume na wanavyuoni wote wanaomjua Mungu ambao wamekuwa makaimu wa Mitume katika kumlingania Mwenyezi Mungu. Na ushahidi wa mwanachuoni unaambatana na hoja ya kumkinaisha anayetafuta uhakika. Makusudio ya uadilifu hapa ni uadilifu katika dini na sharia na katika desturi ya maumbile na nidhamu yake, Mwenyezi Mungu anasema:

﴿وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ﴾

Na hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake kwa mchezo. (21:16)

Unaweza kuuliza nini makusudio ya kukaririka neno: 'Hakuna Mola isipokuwa yeye,' Katika Aya moja?

Jibu : Inajulikana kuwa katika njia ya Qur'an ni kukariri na kutilia mkazo misingi ya itikadi na misingi muhimu, hasa umoja. Hiyo ni kuondoa shaka. Tumefafanua kukaririka katika kifungu mbali, tulipofasiri Aya 48 Sura ya Baqara, Imesemekana kuwa makusudio ya kauli ya kwanza ni kujulisha kuwa yeye pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa. Na, ya pili ni kujulisha kuwa hakuna yeyote mwenye kusimamia uadilifu isipokuwa yeye.

DINI YA MWENYEZI MUNGU NI UISLAMU

Unaweza kuuliza: Dhahiri ya Aya, Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni uislam, inafahamisha kuwa dini zote za mitume - hata dini ya Ibrahim - si chochote isipokuwa dini ya Muhammad (s.a.w.w.) na Qur'an tu? Jibu: Hapana, bali Aya hii inafahamisha kinyume kabisa na hivyo. Kwani dhahiri yake inatamka kwa lugha fasaha kwamba kila dini aliyokuja nayo Mtume miongoni mwa Mitume waliotangulia umbo lake linakuwa na mwito wa kiislamu ambao ameulingania Muhammad bin Abdullah (s.a.w.). Kwa ufafanuzi zaidi angalia hakika hizi zifuatazo:

1. Kabla ya jambo lolote kwanza, uislamu una mambo matatu; Kumwamini Mwenyezi Mungu na umoja wake, kuamini wahyi na Isma yake na kuamini ufufuo na malipo yake. Kila mmoja wetu anaamini kwa imani isiyokuwa na tashwish yoyote kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakupeleka Mtume yeyote isipokuwa kwa misingi mitatu hii. Kwa hali hiyo ndipo Mtume(s.a.w.w) akasema:"Sisi Mitume dini yetu ni moja"Akaendelea kusema: "Mitume ni ndugu katika shughuli (zao) baba yao ni mmoja na mama zao ni mbali mbali"

2. Neno: uislamu linatumiwa kwa maana nyingi; kama kunyeyekea, usafi na kusalimika na ila na uchafu. Hakuna mwenye shaka kwamba kila dini aliyokuja nayo Mtume katika Mitume wa Mwenyezi Mungu ni safi isiyokuwa na uchafu wowote. Kwa hiyo basi inafaa kulitumia neno uislam kwa dini zote za Mitume.

3. Rejea ya Qur'an ni moja, hakuna tofauti kati ya Aya zake, bali hiyo Qur'an inajifasiri yenyewe na kujitolea ushahidi hiyo yenyewe; kama alivyosema Imam Ali(a.s) :"Ikija Aya katika suala fulani au maudhui fulani, basi haifai kuiangalia peke yake, bali ni lazima kufuatilia kila Aya zilizo na uhusiano na suala hilo na maudhui hayo na kuzikusanya katika jumla moja kwa kuunganisha na nyengine, kisha tutoe maana moja katika Aya zinazooana" Tunapoangalia Aya zinazoelezea uislamu katika uhakika huu, tunakuta kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewasifu Mitume wote kwa Uislamu katika Aya nyingi. Kwa hivyo tunajua kuwa neno la Mwenyezi Mungu, Hakika dini mbele za Mwenyezi Mungu ni Uislamu linakusanya dini zote za haki. Siri ya hilo ni hayo tuliyoyaeleza kwamba dini zote za Mitume zinadhamini mwito wa kiislamu katika uhakika wake na dhati yake. Kwa kutilia mkazo imani ya Mwenyezi Mungu, wahyi na ufufuo. Ama tofauti inakuwa kaitka matawi na hukumu, sio katika misingi ya itikadi na imani.

Hebu tuangalie Aya ambazo Mwenyezi Mungu amewasifu Mitume kwa uislamu, tangu zama za Nuh(a.s) mpaka za Muhammad(s.a.w.w) , Amesema Mwenyezi Mungu kuhusu Nuh:

﴿وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ﴿٧١﴾وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴾

Na wasomee habari za Nuh alipowaambia watu wake Enyi watu wangu! ...Nimeamrishwa niwe miongoni mwa waislamu. (10: 71-72)

Kuhusu Ibrahim na Yakub anasema:

﴿وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ﴾

Na Ibrahim akawausia haya wanawe; na Yakub: "Enyi wanangu hakika Mwenyezi Mungu amewachagulia dini hii, basi msife ila mmekuwa waislamu" (2:132)

Kuhusu Yusuf anasema:

﴿أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ﴾

"Wewe ndiwe mlinzi wangu katika dunia na akhera, nifishe hali ya kuwa ni Mwislamu" (12:101)

Kuhusu Musa anasema:

﴿وَقَالَ مُوسَىٰ يَا قَوْمِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّـهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّسْلِمِينَ﴾

"Na Musa akasema: Enyi watu wangu! Ikiwa nyinyi mme mwamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni yeye kama nyinyi ni waislamu" (10:84)

Kwa Umma wa Isa anasema:

﴿وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ﴾

"Na nilipowafunulia wanafunzi (wako) kuwa niaminini mimi na Mtume wangu, wakasema: "Tumeamini na uwe shahidi kuwa sisi ni waislamu" (5:111)

Aya iliyo wazi kuliko zote na inayomuenea wa kwanza na wa mwisho katika Mitume, wafuasi wao na wafuasi wa wafuasi, ni ile isemayo:

﴿وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴾

"Na yeyote mwenye kutaka dini isiyokuwa ya Kiislamu, basi haitakubaliwa kwake, naye akhera atakuwa katika wenye khasara" (3:85)

Ikiwa Mwenyezi Mungu hatakubali isipokuwa Waislamu tu; na huku amekwisha wakubali Mitume kuanzia Adam, Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Mitume wote pamoja na wafuasi wao, basi natija itakuwa kwamba Mitume wote kuanzia Adam mpaka Muhammad(s.a.w.w) na wanaowafuata, ni waislamu. Imam Ali(a.s) anasema:"Uislamu ni kujisalimisha, kujislaimisha ni yakini, yakini ni kusadikisha, kusadikisha ni kukiri, kukiri ni kutekeleza na kutekeleza ni matendo."

Na hawakuhitalifiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia elimu kwa uhasidi uliokuwa baina yao.

Makusudio ya watu wa Kitabu hapa ni mayahudi. Inasemekana ni manasara. Na, inasemekana ni wote, na hiyo ndio sahihi kwa sababu tamko ni la kiujumla na hakuna dalili ya umahsusi. Linalotilia nguvu kuwa tamko ni la kiujumla, ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

﴿وَمِنَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ أَخَذْنَا مِيثَاقَهُمْ فَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ﴾

"Na kwa wale waliosema: Sisi ni Wanaswara tulichukua ahadi yao, lakini wakaacha sehemu ya yale waliyokumbushwa, kwa hivyo tukaweka baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Kiyama." (5:14)

Kuhusu tofauti ya Mayahudi anasema: "Na Mayahudi walisema: 'Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba'

﴿وَأَلْقَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ﴾

"Na tumewatilia uadui na bughudha baina yao mpaka siku ya Kiyama." (5:64).

Katika mambo waliyohitalifiana Mayahudi ni uhai baada ya mauti. Baadhi yao wakasema, hakuna ufufuo kabisa, si katika maisha haya wala mengine na kwamba adhabu ya mwenye makosa na thawabu za mtu mwema zinapatikana katika maisha haya ya duniani. Kikundi kingine kinasema: "Watu wema watafufuliwa mara ya pili hapa duniani ili washiriki katika ufalme wa Masih ambaye atakuja zama za mwisho." Ama itikadi ya Kikristo iligeukageuka,kabla ya kudumu kwenye utatu. Mwanzo ilikuwa inalingania kwenye ibada ya Mungu mmoja, kisha wakagawanyika makundi mawili: Kundi moja lilikuwa katika shirk na jengine likabakia kwenye Tawhid lakini likatofautiana kuwa je, Isa ana tabia mbili ya kiungu na nyengine ya kibinadamu; au ana tabia ya kiungu tu? Na mengine mengi yaliyoandikwa katika vitabu vya historia za dini, Tofauti hizo za kikristo zimeleta umwagikaji damu wa kufehedhesha kusikokuwa na mfano katika historia ya binadamu.

Tofauti ya mayahudi na manaswara (wakristo) hazikutokana na kutojua uhakika. mayahudi walijua kuwa kuna ufufuo; kama ambavyo wakristo walijua kuwa Isa ni mja miongoni mwa waja wa Mungu, lakini walihitalifiana kwa kutaka ukubwa katika dunia kwa uhasidi na ufisadi.

VIKUNDI SABINI NA TATU

Imetangaa kwamba Mtume(s.a.w.w) amesema: "Mayahudi wamegawanyika vikundi sabini na moja, Wakristo vikundi sabini na mbili na umma wangu utagawanyika vikundi sabini na tatu." Maneno yamekua mengi sana kuhusu Hadith hiyo: Kuna mwenye kusema kuwa ni dhaifu, mwengine anasema hiyo ni Hadith iliyopokewa na mtu mmoja ambayo sio hoja katika maudhui. Watatu naye anasema kuwa neno "Vikundi vyote vitaingia motoni" ni katika vitimbi vya walahidi kwa kuwatia doa waislamu. Ama wanne amesema kwa tamko hili: "Vikundi vyote vitakuwa katika pepo isipokuwa wazandiki" Sisi tuna mashaka na Hadith hii, kwa sababu asili ni kuacha kuchukua lolote linalonasibishiwa Mtume(s.a.w.w) mpaka ithibiti kinyume (ukweli). Lakini kama tukihiyarishwa kati ya kukubali kwa "vyote vitakuwa motoni" na vyote vitakuwa peponi." Tutachagua peponi kutokana na sababu mbili:

Kwanza : Hiyo ndiyo iliyo karibu zaidi na rehema ya Mwenyezi Mungu.Pili : Kimsingi ni kwamba vikundi vya kiislamu vinavyotofautiana katika misingi (asili) havifiki sabini na tatu, kutofautiana katika matawi, hakupelekei kuingia motoni. Kwa sababu makosa kwenye matawi yanasamehewa yakiwa yametokea pamoja na kujichunga na baada ya kujitahidi.

Ni umbali ulioje kati ya Hadith hii inayonasibishwa kwa Mtume(s.a.w.w) na kauli ya Ibn Arabi katika kitabu Futuhat: "Haadhibiwi yeyote katika umma wa Muhammad(s.a.w.w) kwa baraka za Ahlu bait"

Na kama wakikuhoji, basi sema: Nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu na walionifuata

Mara nyingi mwanachuoni wa haki hupambana na mbishi mwenye batili. Wala hakuna dawa ya huyu isipokuwa kuachana naye, Na yeyote mwenye kuhasimiana na mshari mwenye vurugu anakuwa mshirika wake katika dhambi.

Imam Ali(a.s) anasema:"Mwenye kubisha sana hupata dhambi. "Kwa ajili hii, Mwenyezi Mungu amemwamrisha Mtume wake Mitukufu kuachana na wabatilifu, walio wapinzani, kwani hakuna ziada ya ubainifu na hoja.

﴿فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ وَعَلَيْنَا الْحِسَابُ ﴾

"Hakika ni juu yako kufikisha tu, na ni juu yetu hisabu." (13:40)

Na waambie wale waliopewa kitabu, yaani mayahudi na manaswara,na wale wasio na kisomo, yaani washirikina katika waarabu.

Mwenyezi Mungu amewanasibisha na neno wasio na kisomo kwa sababu wengi wao hawakujua kusoma na kuandika, Je mmesilimu? Baada ya kuwajia hoja, Kama wakisilimu basi wameongoka kwani hakuna kitu chochote zaidi ya uislamu, isipokuwa kufuru tu na upotevu.

Na kama wakikengeuka basi juu yako ni kufikisha tu.

na kufikisha ndio mwisho wa kazi ya utume, kwani huko ndiko kunakotimiza hoja, Na Mwenyezi Mungu anawaona waja wote anawatendea wanayostahiki.

Faida tunazozipata kutokana na Aya hii ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemchagua Muhammad(s.a.w.w) kuwa Mjumbe Wake na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu amemwekea njia ya kuufikisha ujumbe huo ambao ni kutoa mwito kwa hoja na dalili; pamoja na kuidhibiti nafsi na kujiepusha na uhasama wa ubishani.

Kwa njia hii ya hekima hoja inatimia kwa mhalifu, mpinzani na asibakiwe na udhuru wowote au popote pa kukimbilia. Wafuasi bora zaidi wa Mtume kwenye njia yake, ni watu wa elimu wanaojua dini yake na sharia yake; wenye kulingania kushika mafunzo yake na mwenendo wake.

﴿إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴾

21.Hakika wale ambao wanazikanusha Aya za Mwenyezi Mungu na wakawauwa manabii pasipo haki na wakawaua wanaoamrisha mambo ya haki, wabashirie adhabu iumizayo.

﴿أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴾

22.Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika katika dunia na akhera wala hawana wa kuwanusuru.

WANAOWAUA MITUME

Aya 21 – 22

MAANA

Hakika wale ambao wanazikanusha Aya za Mwenyezi Mungu na wakawauwa manabii pasipo haki na wakawauwa wanaoamrisha mambo ya haki, wabashirie adhabu iumizayo.

Unaweza kuuliza sharia zote za Mwenyezi Mungu na za watu zinaharamisha kuua, bali watu wote wanamuona muuaji ni mkosa, hasa ikiwa aliyeuwawa ni katika watu wema. Kwa hiyo basi kuelezea kuwa muuaji ni mwenye makosa anayestahili adhabu, ni kama kufafanua kilichofafanuka, na hali tunajua kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu yako katika mpangilio mzuri?

Jibu : Makusudio hapa ni mayahudi na wakristo waliokuwako wakati wa Mtume(s.a.w.w) na wakakataa uislamu. Aya imeonyesha kuwa si jambo geni kwao kukataa na kuwa na inadi na uislamu. Kwa sababu mayahudi waliotangulia waliwaua manabii; kama vile Zakariya na manaswara waliotangulia waliwaua wale waliouonyesha wazi umoja wa Mungu na ubashiri wa Masih, kwa vile tu walikuwa wanaamrisha haki na uadilifu na kuutumia. Kwa hivyo Aya imo katika mfumo wa kukemea; kama ilivyo kuwa ni ya kuhofisha.

Swali la pili : Kuua hakukuwa kwa Ahlul-kitab waliokuwa wakati wa Muhammad(s.a.w.w) , sasa vipi wananasibishiwa wao pasipo haki?

Jibu : Tumekwishaeleza mara kadhaa kwamba waliokuja nyuma waliridhia yaliyofanywa na wa kale wao na mwenye kuridhia kitendo anakuwa mshirika, Mara nyingi anayoyafanya baba hutegemezewa mwana.Swali la tatu : Kuwaua manabii hakukuwa haki kwa hali yoyote, sasa kuna faida gani katika msemo huu?

Jibu : Ni kuonyesha kuwa fedheha ya kuwaua mitume si kwa sababu ya vyeo vyao na utukufu wao, bali ni fedheha isiyokuwa na udhuru wowote, na kwamba sio suala la watu au vikundi, bali ni suala zima la haki na ukosefu wa haki. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika katika dunia na akhera Kuharibika duniani ni kwamba wao wanalaaniwa na kila mtu, kutokana na athari zao mbaya walizoziacha. Ama huko akhera wanangojwa na adhabu.

KUAMRISHA MEMA NA KUKATAZA MABAYA

Mafakihi wametaja sharti za kuamrisha mema na kukataza mabaya, kama vile kutohofia mwamrishaji madhara ya nafsi yake, watu wake na mali yake. Lakini baadhi ya mafakihi wamelipinga sharti hili na kuwajibisha kuamrisha mema japo kutapelekea kifo; na wametoa dalili kwa Aya hii. Hoja yao ni kuwa mitume wameamrisha mema na kukataza mabaya, wakauliwa katika njia hii. Kwa ushahidi wa Qur'an tukufu. Tunavyoona sisi ni kwamba mitume katika tabligh walikuwa wana jambo ambalo wanavyuoni hawana. Wao walikuwa wakiongozwa na wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t); kama wakiuwawa katika njia ya tabligh, watakuwa wameuwawa wakiwa wanatekeleza amri ya Mwenyezi Mungu. Ama wanavyuoni, wanategemea yale waliyoyafahamu katika hukumu. Tunavyofahamu sisi kutokana na dalili hizi ni kwamba mtu yeyote inafaa kwake kunyamaza kwenye mambo mabaya ikiwa hakuna faida ya kidini na tena kuna madhara.

Ama ikiwa dhana yake imeelemea kuwa kutapatikana manufaa ya kidini kwa kuamrisha mema na kukataza mabaya, lakini kuna madhara, basi hapo itakuwa ni wajibu kuamrisha. Kwa hiyo lililopo ni kulinganisha kati ya kukinga nafsi na manufaa ya kuamrisha na kukataza. Ikiwa manufaa ya dini ndiyo muhimu; kama vile kuumaliza ukafiri, dhulma na ufisadi. Basi hapa itafaa kuyakubali madhara, na huenda ikawa wajibu. Na, ikiwa kujikinga na madhara ni muhimu zaidi kuliko kukataza mabaya; kama kukataza kula najisi, basi hapo itafaa kujikinga na huenda ikawa ni wajibu, kwa hivyo basi suala litakuwa linatofautiana kwa kutafautiana hali. Na, inatubainikia kwamba kuwalinganisha wasiokuwa Manabii katika suala hili la Manabii ni kuwalinganisha na kitu kilicho tofauti. Tutalirudia suala hili pale litakaponasibika.

﴿ أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُدْعَوْنَ إِلَىٰ كِتَابِ اللَّـهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ وَهُم مُّعْرِضُونَ ﴾

23.Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu, wanaitwa kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kiwahukumu baina yao, kisha baadhi yao wanageuka wanakikataa.

﴿ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ وَغَرَّهُمْ فِي دِينِهِم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴾

24.Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache tu, na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyazua.

﴿ فَكَيْفَ إِذَا جَمَعْنَاهُمْ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴾

25.Basi itakuwaje tutakapowakusanya siku ambayo hapana shaka kuja kwake na itakapolipwa kila nafsi kwa ukamilifu kile ilichokichuma na wao hawataodhulumiwa.

MAYAHUDI TENA

Aya 23 - 25

MAANA

Je huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaitwa kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kiwahukumu baina yao, kisha baadhi yao wanageuka wanakikataa.

Wafasiri wanasema: Makusudio ya wale ambao wamepewa sehemu ya Kitabu ni mayahudi. Hapa Mwenyezi Mungu anasema waliopewa sehemu ya kitabu, na wala hakusema waliopewa Kitabu au watu wa Kitabu; kama ilivyo katika sehemu nyingine, kwa sababu mayahudi waliomhoji Mtume(s.a.w.w) na akawaita kwenye Tawrat iwahukumie, hawakuwa wamehifadhi Tawrat yote, isipokuwa walihifadhi baadhi tu, kama walivyosema wafasiri wengi. Au walihifadhi matamko tu, bila ya kuzingatia maana yake; kama alivyosema Sheikh Muhammad Abduh.

Wengi wao ni wale ambao wanalingania kwenye kuamini vitabu vya Mwenyezi Mungu na msimamo wa kibinadamu, lakini wanasema tu, bila ya kutekeleza kwa vitendo, Na, wakihojiwa, basi hubabaisha. Mifano ya hao ni mingi sana haina idadi. Kama vile watu walioanzisha vita na kuuwa mamilioni, wanadai kwamba wao ni watetezi wa amani. Miongoni mwazo ni zile dola ambazo zinawakandamiza watu huru na zinajigamba kuamini haki na uadilifu. Mfano mwengine ni mayahudi ambao Mtume(s.a.w.w) aliwaita kwenye Kitabu chao Tawrat na kuwaambia nendeni kwenye kitabu hicho, kwani ndani yake mna sifa zangu, lakini walikipa mgongo na kufanya inadi, ndipo ikashuka Aya hii. Kuna kundi la wafasiri waliosema kwamba Aya hii ilishuka kwa ajili ya yahudi mmoja aliyezini na yahudi mwenzake, na mayahudi wakatofautiana katika suala hilo katika makundi mawili. Kundi moja likataka apigwe mawe mpaka afe na kundi jingine likataka ipunguzwe adhabu hiyo. Mzozo ulipozidi wakenda kwa Mtume kuamuliwa; Mtume akahukumu kuwa apigwe mawe, lakini lile kundi la pili likakataa, ndipo Mtume akawakumbusha Tawrat ambayo imeelezea pia habari ya kupiga mawe mzinifu, lakiniwakakataa.

Kwa vyovyote itakavyokuwa sababu ya kushuka Aya hii, kwa hakika ina maana ya jumla na kumgusa yeyote mwenye kutangaza jambo, lakini yeye mwenyewe akajitia hamnazo na kulikataa. Kwa sababu linalozingatiwa ni matendo, sio alama na maneno matupu. Imam Ali(a.s) anasema:"Hatafuzu kwa kheri ila mwenye kuifanya, wala hatalipwa mtu malipo ya shari isipokuwa mwenye kuifanya"

Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache tu, na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyazua.

Mwenyezi Mungu ameeleza aina nyingi za uovu wa mayahudi katika kitabu chake kitukufu; kama vile kuua kwao mitume, kuabudu ndama, kusema kwao kuwa watakaoingia peponi ni mayahudi tu, kusema kuwa wao ni wana wa Mungu na wapenzi Wake na kudai kuwa moto utawagusa siku chache tu. Mwenye Tafsir al-Manar amenakili kutoka kwa mwalimu wake Sheikh Muhammad Abduh kwamba yeye amesema: "Katika vitabu vya mayahudi walivyonavyo hamna kiaga chochote cha akhera."

Imenakiliwa kutoka kwa watu wanaochunguza na kufuatilia mambo kuwa Mayahudi hawaamini akhera, lakini kunukuu kunapingana na kauli ya Qur'an kwa mayahudi: "Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache tu," na kule kusema kwao: "Hataingia peponi isipokuwa Yahud."Si jambo la kushangaza kusema kuwa wahenga wa Kiyahudi walikuwa wakiamini akhera; kisha waliofuatia wakageuza na wakaondoa katika vitabu vyao kila linalofungamana na akhera. Katika Tafsir Al-manar akinukuliwa Sheikh Abduh, anasema: "Watafiti wa kiulaya wamethibtisha kuwa Tawrat imeandikwa baada ya nabii Musa(a.s) kwa miaka nenda miaka rudi. La kushangaza zaidi kuliko yote hayo ni madai ya mayahudi, kwamba Mwenyezi Mungu anawapendelea wao na kwamba Mwenyezi Mungu amewaumba watu wengine kwa ajili ya kuwatumikia wao na kwa masilahi yao, sawa na wanyama. Kwa ajili ya fikra hii ndio wakajiita "Taifa la Mungu lilochaguliwa" Au "Taifa teule la Mungu" Tukiachilia mbali muhali wa madai haya na kutoingilika akilini, pia tunavyoona ni ndoto na ni kumhukumia Mwenyezi Mungu, kwani hakuna jambo lolote la ghaibu linaloweza kujulikana bila ya wahyi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na, wahyi umekwisha walaani, kuwafedhehesha na kutaja adhabu yao.

Fedheha hiyo na adhabu itafichuka siku ambayo hawatakuwa na hila yoyote ya kuikinga, kwa hivyo ndipo Mwenyezi Mungu akasema:

Basi itakuwaje tutakapowakusanya siku ambayo hapana shaka kuja kwake na itakapolipwa kila nafsi kwa ukamilifu kile ilichokichuma na wao hawatadhulimiwa.

Thawabu za mtiifu hazitapunguzwa na huenda zikazidi, lakini adhabu haitazidishwa kabisa bali huenda ikapunguzwa na huenda Mwenyezi Mungu akasamehe kabisa. Mimi nina yakini kabisa kwamba mwenye kumtarajia Mwenyezi Mungu katika dunia yake hii, na wala asimtarajie mwengine amtegemee Yeye tu katika matatizo yote kwa hali yoyote itakayokuwa, akiwa na imani kwamba asiyekuwa Mwenyezi Mungu si chochote isipokuwa ni njia na chombo tu; mwenye kuwa hivi nina yakini kuwa bila shaka atakuta yanayomridhisha kwa Mungu hata kama atakuwa ana maovu.

﴿ قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ بِيَدِكَ الْخَيْرُ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾

26.Sema Ewe Mola uliyemiliki ufalme wote humpa ufalme umtakaye na humwondolea ufalme umtakaye. Na humtukuza umtakaye na humdhalilisha umtakaye. iko mikononi mwako kila kheri. Hakika wewe ni muweza wa kila kitu.

﴿ تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ﴾

27.Huingiza usiku katika mchana na huingiza mchana katika usiku na humtoa aliye hai kutoka aliye maiti na humtoa maiti kutoka aliye hai, Na humruzuku umtakaye bila ya ya hisabu.

HUMPA UFALME AMTAKAYE

Aya 26 - 27

MAANA

Dhahiri ya Aya kwa ukamilifu inalingana na hali ya waislamu katika siku za mwanzo wa Uislamu: ambapo wakati huo hawakuwa na ufalme, nguvu wala usultani. uislamu ulianza katika hali ya ugeni, kama alivyosema Mtume(s.a.w.w) . ufalme ulikuwa wa wafursi na warumi. Lakini baada ya kuja ushindi wa Mwenyezi Mungu, mambo yaligeuka; aliye duni akawa mtukufu na mtukufu akawa duni. wafursi na warumi wakawa wanatawaliwa na waislamu baada ya kuwa wao ndio watawala. Wasilamu wakawa watawala baada ya kuwa wanyonge wakiwaogopa watu, ndipo matakwa ya Mwenyezi Mungu yakathibiti aliyoyabainisha kwa kauli yake:

﴿ وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ ﴾

"Na tukataka kuwaneemesha wale waliofanywa wanyonge katika ardhi na kuwafanya wawe viongozi na kuwafanya warithi." (28:5).

Sema: "Ewe Mola uliyemiliki ufalme wote"

Makusudio ya kumiliki ufalme, ni uweza wake juu ya kila kitu; ni kama kusema Mwenyezi Mungu amemiliki uwezo. Ameleta neno ufalme kwa sababu athari ya kumiliki kitu chochote ni uwezo wa mwenye kumiliki kukitumia wala hapana yeyote anayeweza au kumiliki kitu; isipokuwa kwa kumilikishwa na Mwenyezi Mungu na kupewa uwezo juu yake.

Humpa ufalme umtakaye

Aliwapa waislamu mwanzo pale walipoitikia mwito wa uislamu na kuutumia kwa vitendo.

Na humuondolea ufalme umtakaye

Aliuvua kutoka kwa wafursi, na warumi na washirikina kwa sababu ya kuikufuru haki. Na humtukuza umtakaye, nao ni waislamu. Na humdhalilisha umtakaye nao ni wafursi, warumi na washirikina wa kiarabu.

Iko mikononi mwako kila heri

Makusudio ya kuwa mikononi ni kuwa na uwezo. Heri inakusanya kila lenye manufaa liwe la kimaana au kimaada, Na Mwenyezi Mungu amewapa heri nyingi waislamu kwa baraka za uislamu.

Hakika wewe ni muweza wa kila kitu.

Dalili ya uweza ni kuuvua ufalme kutoka kwa wenye nguvu na kuwapa wanyonge.

Huingiza usiku katika mchana na huuingiza mchana katika usiku.

Ambapo sayari zinakuwa na harakati kwa uweza na msaada Wake; nyingine huzizunguuka nyingine, hapo hupatikana misimu ya mwaka; mara nyingine huchukua usiku katika mchana katika msimu fulani mpaka ukawa na masaa15 na mchana ukawa masaa 9. na mara nyuingine huuchuwa mchana katika usiku katika msimu mwingine mpaka ukawa na masaa 15 na usiku ukawa masaa 9( [7] ).

Na humtoa aliye hai kutoka aliye maiti

Kama vile kumtoa mumin kutoka kwa kafiri na mtukufu kutoka kwa aliye dhalili. Na humtoa maiti kutoka aliye hai. Kama vile kumtoa kafiri kutoka kwa mumin na dhalili kutoka kwa mtukufu.

Na humruzuku amtakaye bila hisabu,

Kama alivyowaruzuku waislamu wa kwanza, ufalme na utukufu kwa baraka za uislamu. Na kama utauliza, kuwa je? ufalme wa mfalme dhalimu na usultani wake hutoka kwa Mungu na ni kwa utashi wake na matakwa yake? Utalikuta jibu la swali lako hili katika tafsiri ya aya 246 Surah Al-Baqrah, Zaidi ya hayo ni kwamba dhahiri ya Aya inatilia nguvu yale yaliyosemwa na kundi la wafasiri kuhusu sababu ya kushuka kwake. Kwa ufupi ni kwamba Mtume(s.a.w.w) alipochukua hatua ya kuchimba handaki kwa ushauri wa Salman Farisi aliwakatia dhiraa arubaini kila sahaba kumi, na Salman alikuwa na nguvu, hivyo Ansar wakamtaka awe nao wakasema: "Salman ni wetu" Mtume akasema kauli yake iliyo mashuhuuri: "Salman ni katika sisi Ahlul-Bait.

Wakati Salman alipokuwa akichimba akakabiliwa na jiwe lililomshinda. Mtume alipoambiwa, alichukua sururu kutoka mikononi mwa Salman na kulivunja jiwe kwa mapigo matatu. Katika mapigo hayo Mtume (s.a.w.w) aliona ikulu ya Fursi, Roma na Yemen; akawaambia sahaba zake: "Umati wangu utatawala ufalme wa Kisra na Kaizari". Basi wanafiki waliposikia waliyachezea shere maelezo haya, ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii:

Sema: "Ewe Mola uliyemiliki ufalme wote! Humpa ufalme umtakaye na humwondolea ufalme umtakaye na humtukuza umtakaye na humdhalilisha umtakaye"

Ikiwa hii ndiyo sababu ya kushuka Aya hii au siyo, lakini dhahiri ya Aya haikatai, na matukio ya historia yanaunga mkono hilo.

﴿لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّـهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ﴾

28.Waumini wasiwafanye Makafiri kuwa ni marafiki badala ya waumini (wenzao). Na mwenye kuyafanya hayo, basi hana kitu kwa Mwenyezi Mungu ila mtakapojilinda nao kwa kujihifadhi na anawatahadharisha Mwenyezi Mungu na Yeye mwenyewe marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.

﴿قُلْ إِن تُخْفُوا مَا فِي صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ وَيَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴾

29.Sema: Mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha Mwenyezi Mungu anayajua na anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

﴿يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُّحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِن سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ أَمَدًا بَعِيدًا وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴾

30.Siku ambayo kila nafsi itakuta kheri iliyoitenda imehudhurishwa Na iliyoyatenda katika uovu, itapenda lau kungekuwa na masafa marefu baina ya uovu huo na yeye. Na anatahadharisha Mwenyezi Mungu na Yeye Mwenyewe, na Mwenyezi Mungu ni mpole kwa waja.

URAFIKI NA KAFIRI

Aya 28-30

LUGHA

Neno: Awliya lina maana ya wasimamizi, Makusudio yake hapa ni marafiki kwa maana ya wasaidizi

MAANA

Waumini wasiwafanye makafiri kuwa ni marafiki badala ya waumini (wenzao).

Mwenyezi Mungu hakutosheka na kukataza tu urafiki na makafiri kwa kusema ni haramu; kama vile uongo na kusengenya, bali amekuzingatia kuwa ni kufuru, kwa dalili ya neno lake:

Na mwenye kuyafanya hayo, basi hana kitu kwa Mwenyezi Mungu.

Kwani dhahiri ya kauli hiyo ni kuwa Mwenyezi Mungu yuko mbali na aliye na urafiki na makafiri; na aliye mbali na Mwenyezi Mungu, basi yeye ni Kafiri. Hili linatiliwa nguvu na Aya hizi:

﴿ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ﴾

"Na atakayefanya urafiki nao miongoni mwenu, basi huyo atakuwa pamoja nao" (5:51)

﴿ لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ﴾

Huwapati watu wanaoamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho kuwa wanawapenda wale wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake; hata wakiwa ni baba zao au watoto wao au ndugu zao au jamaa zao" (58:22)

Dhahiri ya Aya hizi inafahamisha kuwa mwenye kumfanya kafiri kuwa rafiki basi naye ni kafiri. Hata hivyo kuna aina mbali mbali za kumfanya rafiki, nyingine zinawajibisha ukafiri na nyingine haziwajibishi. Ufafanuzi ni kama ufatavyo:

AINA ZA URAFIKI NA KAFIRI

Kila aliyesema: Laillaha Illa Ilah Muhammadun rasulullah. Basi anakuwa na lile walilonalo waislamu wengine, na wao wako na lile alilo nalo, isipokuwa akiwafanya makafiri kuwa ni marafiki katika mojawapo ya hali zinazofuata:

1. Kuwa radhi na ukafiri wao, na hili ni muhali kwa mwislam kwa sababu kuridhia ukafiri ni ukafiri.

2. Kujikurubisha kwa makafari kwa upande wa dini kwa kujaribu kufasiri Aya za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Hadith za Mtume Wake kwa yale yanayoafikiana na mapenzi ya makafiri, maadui wa Mwenyezi Mungu na Mtume, kiasi ambacho tafsiri hiyo itapingana na misingi ya kiislamu na kiitikadi. Ikiwa kwa makusudi na kujua. Huu vile vile ni ukafiri. Unaweza kuuliza: Mtu anayefanya hayo kwa ukaidi ni kafiri bila ya wasiwasi wowote, lakini mwenye kuyafanya kwa kupuuza tu, inafaa awe fasiki tu, sio kafiri; sawa na mwenye kuacha Swala akiwa anaamini kuwa ni wajibu na akanywa pombe akiwa anaamini kabisa kuwa ni haramu? Jibu: Kutofautisha kati ya mkaidi na mpuuzaji kunakuja kwenye Fur'uu (matawi); kama vile Swala, kunywa pombe n.k. Ama kwenye mambo yanayorudia kwenye Usul (Misingi) ya dini na itikadi; kama vile umoja wa Mungu, utume wa Muhammad n.k. Basi kutamka tu kitu kinachokanusha kunawajibisha ukafiri. Ni sawa mtamkaji awe ametamka kwa ukaidi au kwa kupuuza.

3. Kuwa kachero au jasusi wa makafiri dhidi ya waislamu, Huyu ataangaliwa. Ikiwa amefanya hivyo kwa tamaa ya mali au jaha basi atakuwa mwenye makosa aliye fasiki, ama akifanya kwa sababu ya kuwapenda makafiri kwa kuwa wao ni makafiri na kwa kuwachukia waislamu kwa kuwa ni waislamu, basi huyo ni kafiri bila ya shaka yoyote.

4. Kuwapenda makafiri na huku akiwa anajua kabisa kwamba wao wanawapiga vita Waislamu wakiwa wanataka kuwadhalilisha na kuwatumia, basi huyu atakuwa ni mwenye dhambi na mshirika wa dhalimu katika udhalimu wake, hata kama huyo dhalimu ni mwislamu.

5. Kuwataka msaada makafiri wenye amani dhidi ya makafiri wasiokuwa na amani. Msaada huu unafaa kwa maafikiano ya Ijmai (kongamano). Watu wa historia na wafasiri wamenukuu kwamba Mtume(s.a.w.w) aliwekeana mkataba wa kusaidiana na Bani Khuzaa inagawaje walikuwa washirikina. Pia alimtaka msaada Safwan bin Umayya - kabla hajasilimu - kwenye vita ya Hawazan. Vilevile aliwataka msaada Mayahudi wa Bani Qaynuqa na akawagawanyia mali.

Bali yamekuja maelezo kutoka kwa Allama Hili kwamba kundi la mafakihi wamejuzisha kutaka msaada kutoka kwa makafiri katika kuwapiga vita waislamu walio madhalimu. Kwa sababu kuwataka msaada kunaambatana na haki, si kwa ajili ya kuibatilisha batili.

6. Kufanya urafiki kwa sababu za mambo ya kawaida yaliyozoeleka, kama kushirikiana katika kazi au biashara na mengineyo mengi ambao hayahusu dini. Urafiki huu pia unafaa kwa kongamano la maulamaa. Kwa sababu kumpenda kafiri kutakuwa haramu kama kutapelekea kufanyika jambo la haramu, ama kukiwa sio wasila wa kufanya maasi, basi si haramu; bali huenda kukawa kunapendekezwa kama kuna manufaa na heri kwa nchi au watu. Na, Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameamrisha upendano, kuzoweyana na kusaidiana kwa watu wote bila ya kuangalia dini au mila zao. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

﴿ لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴾

"Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakupigana nanyi kwa ajili ya dini wala hawakuwafukuza katika miji yenu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao uadilifu" (60:8)

Sisi hatuna shaka kwamba katika makafiri kuna walio na hulka nzuri na tabia njema - ya ukweli, uaminifu na utekelezaji - kuliko wale tunaowaita na kujiita waislamu. Na kwamba kufanya urafiki nao ni bora zaidi - kibinadamu na kimaslahi ya umma - kuliko wale vibaraka wahaini wanaojionyesha kwa dini ya kiislamu. Maelefu ya rehema na amani yamwendee yule aliyesema: "Aliye karibu ni yule aliye karibu kwa tabia. Huenda aliye karibu akawa mbali zaidi ya aliye mbali na aliye mbali akawa karibu zaidi ya aliye karibu" Hakika hii huitambua mtu kimaumbile tu bila ya hisia zozote.

TAQIYA

Ila mtakapojilinda nao kwa kujihifadhi.

Historia ya Taqiya inaanzia na historia ya uislamu siku ulipokua dhaifu, na shujaa wa kwanza alikuwa Ammar bin Yasir, pale aliposilimu yeye, baba yake na mama yake; wakaadhibiwa na makafiri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakavumilia adhabu na adha bila ya kulalamika. Mtume akawapitia wakiwa wanaadhibiwa: Hakuzidisha chochote Yasir zaidi ya kusema: "Hali ndio hii ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu." Mtume naye akasema: "Vumilieni enyi familia ya Yasir hakika ahadi yenu ni pepo." Akawa Yasir na mkewe Sumaiya ndio mashahidi wa kwanza katika uislam. Washirikina wakamlazimisha Ammar kusema maneno kuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu, akasema kwa ajili ya kujikinga na madhara kwa ajili ya nafsi yake. Hapa baadhi ya Maswahaba wakasema kuwa Ammar amekufuru; Mtume akasema: "Hapana hakika Ammar imani imemtanda kuanzia utosini hadi nyayoni" Ammar akaja kwa Mtume akiwa analia na kujuta. Mtume akampangusa machozi na kuuwaambia: "Usilie, hata kama watarudia, basi wewe rudia uliyoyasema." Hapo ikashuka Aya kumhusu Ammar:

﴿ مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ ﴾

"Mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu baada ya kumwamini (ana adhabu kubwa) isipokuwa yule aliyelazimishwa hali ya kuwa moyo wake umetulia kwenye imani" (16:106)

Hakuna waliohitalifiana kuwa Aya hii, ilishuka kwa mnasaba huo wa Ammar. Kimsingi linalozingatiwa ni kuenea tamko, sio sababu za kushuka Aya, Na tamko hapa linamwenea kila mwenye kulazimishwa hali ya kuwa moyo wake umetulia kwenye imani. Kisha ndipo ikashuka Aya hii tunayoifasiri kutilia mkazo Aya hiyo ya kuhusu Ammar, kama zilivyo Aya nyingine zifuatazo:

﴿ وَقَالَ رَجُلٌ مُّؤْمِنٌ مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَكْتُمُ إِيمَانَهُ ﴾

Na akasema mtu mmoja Mumin katika watu wa firaun afichaye imani yake (40:28)

"Isipokuwa vile mnavyolazimishwa" (6:119)

Ruhusa ya Taqiya haikuja kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu tu, bali katika Hadith vilevile. Ar-Razi katika Tafsir Kabir, na Sayyid Rashid Ridha katika Tafsir Al-Manar, na wengine wanasema: "Musailama Al-Kadhab aliwashika watu wawili katika swahaba wa Mtume, mmoja akamwambia: "Je, washuhudia kuwa mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu?"

Yule mtu akasema: "Ndio," basi akamwacha. Yule wa pili alipomwambia hivyo hivyo, alikataa, basi akamuua. Mtume alipopata habari hizo alisema: "Yule aliyeuawa amekufa na yakini yake na ukweli wake pongezi ni zake. Ama yule mwengine ameruhusiwa, (kufanya hivyo) hana neno" Kuna Hadith katika Tafsir Al-Manar kwamba Bukhari katika Sahih yake akimnukuu Aisha anasema: "Mtu mmoja alibisha hodi kwa Mtume, Mtume akajisemea: "Mtu mbaya huyo", kisha akamruhusu kuingia na akazungumza naye vizuri."

Yule mtu alipoondoka Aisha akamwambia Mtume: "Si umesema uliyoyasema kuhusu mtu huyu, kisha umezungumza naye vizuri? Mtume akasema; "Hakika mwovu zaidi wa watu ni yule anayeachwa na watu kwa kujikinga na shari yake." Na katika Bukhari tena kuna Hadith ya Abu Dardai inayosema: "Sisi tunatabasamu kwenye nyuso za watu na nyoyo zetu zinawalaani" Zaidi ya hayo kuna Hadith nyingine zinafahamisha kujuzu Taqiya (kujikinga) kama vile Hadith: "Hapana dhara wala kudhuriana." Na "Umati wangu umesamehewa yale wanayolazimika nayo." Hadith zote hizi mbili ni Mutawatir kwa upande wa Sunni na Shia. Kwa kutegemea kitabu cha Mwenyezi Mungu na Hadith Mutawatiri za Mtume zilizo sahihi basi Sunni na Shia wamekongamana kwa kauli moja kuwa Taqiya inafaa. Anasema Al- Jasas mmoja wa Maimam wa Kihanafi katika juzuu ya pili ya kitabu Ahkamul Qur'an Uk. 10 chapa ya 1347 A.H. Ninamnukuu: "Ila kwa kujilinda nao" Yaani ni kuhofia kuangamia nafsi au baadhi ya viungo kwa hiyo kujilinda nao kwa kudhihirisha ukafiri bila ya kuutaikidi Na hilo limeafikiwa na watu wa elimu."

Ar-Razi katika tafsiri yake amemnukuu Hassan Al-Basri akisema: "Taqiya inajuzu mpaka siku ya Kiyama". Vilevile amemnukuu Shafi kwamba yeye amejuzisha Taqiya kwa waislamu wote, ikiwa anamhofia mwislam mwenziwe katika tofauti zinazorudia masuala ya dini. Mwenye Tafsir Al-Manar naye anasema kuhusu Aya hii: "Mwenye kutamka neno la kufru akiwa anajikinga na kuangamia kwa kulazimishwa sio kwa kuukubali ukafiri au kwa sababu ya kupenda dunia kuliko akhera, basi si kafiri na unakubaliwa udhuru wake kama alivyokubaliwa Ammar bin Yasir Na amesema Sheikh Mustafa Azurqaa katika Kitabu Fiq-hul-Islam Fi Thawbihil Jadidi mada ya 600, anasema: "Kutishwa mtu kuuliwa kwa kulazimishwa ukafiri, kunamhalalishia kudhihirisha ukafiri ikiwa moyo umetulizana na imani." Zaidi ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Hadith za Mtume na kongamano la Waislamu wa kisunni na kishia, pia akili inakubali Taqiya kwa sababu akili pia inaiona ni nzuri kutokana na desturi isemayo "Dharura inahalalisha yaliyokatazwa" Kwa hiyo basi inatubainikia kuwa Taqiya ni kanuni ya sharia wanayoitegemea Mujtahid wa Kisunni na kishia katika kutoa hukumu. Na kwamba dalili yake ni Qur'an, Hadith, kongamano na akili. Kwa ajili hiyo Taqiya inakuwa ni funzo la kiislamu kwa waislamu wote na kuaminiwa na madhehebu zote; na wala sio ya madhehebu maalum kama wanavyodhania Khawarij.

Hapa kuna swali linalojitokeza; nalo ni ikiwa Taqiya inafaa kwa Qur'an, Hadith, akili na kongamano kutoka kwa Shia na Sunni, kwa nini wanasibishiwe Shia tu, kiasi kwamba Masheikh wengi wa kisunni wameinasibisha kwa Shia na kuwakebehi nayo? Jibu: Kunasibishiwa au kuwa mashahuri zaidi kwa Shia, huenda ikawa ni kwa sababu ya kuwa wao walilazimika kuitumia zaidi ya watu wengine kwa kuangalia vikwazo vingi walivyovipata wakati wa utawala wa Bani Umayya, Bani Abbas na waliowafuatia( [8] ). Kwa sababu ya kulazimika Shia kuwa na Taqiya mara nyingi au zaidi kuliko wengine, ndio maana wakajishughulisha nayo na kuitaja katika vitabu vya fikh tena wakaifafanua kwa kubainisha mipaka yake na wakati wake wa kufaa kuifanya na kutofaa. Muhtasari wa waliyoyasema ni: Inafaa kwa ajili ya kuondoa madhara ya nafsi, na haifai kwa ajili ya kuleta manufaa au kuingiza madhara kwa mwengine. Ama yule anayeihusisha Taqiya na Mashia tu, ama atakuwa ni mjinga au atakuwa mwenye chuki. Hata hivyo hivi sasa Taqiya haitumiki (sana) baada ya kupita wakati wa hofu na vikwanzo.

Na anawatahadharisha Mwenyezi Mungu naye

Yaani na dhati Yake ambayo inajua kila kitu, yenye uweza juu ya kila kitu na kumlipa kila mtu kwa amali yake.

Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.

Ambako italipwa kila nafsi ilichofanya.

Sema: mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kujuzisha Taqiya na kuiruhusu kwa mwenye kulazimika, anasema: linaloangaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni lile lililo moyoni: na yeye anayajua ya moyoni mkifanya siri au kuyadhihirisha.

Siku ambayo kila nafsi itakuta kheri iliyoitenda imehudhurishwa

Lilivyokuwa Mwenyezi Mungu anajua kila kitu, muweza wa kila jambo; mkusanyaji wa watu siku isiyo na shaka. na mwadilifu asiyedhulumu, hayo yote yanamhakikishia mtu kukuta malipo ya amali yake. Baadhi wanasema, mtu atakuta amali yake kesho ikiwa kama umbo zuri la kupendeza kama ni ya kheri; au kama ni mbaya basi itakuwa na umbo la kutisha. Lakini inavyojulikana ni kwamba amali ni mambo ambayo hayabaki wala haiwezekani kuyarudisha na kuyaona. Kwa hiyo makusudio ni kuwa mtu siku ya kiyama ataona malipo ya amali yake sio hiyo amali yenyewe.

Na iliyoyatenda katika uovu, itapenda lau kama kungekuwa na masafa marefu baina ya uovu huo na yeye.

Herufi Wau hapa ni kuanza maneno; yaani mwenye kumwasi Mwenyezi Mungu, hapo kesho atatamani kuweko na masafa kati yake na siku hiyo sawa na umbali wa Mashariki na Magharibi.

Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja.

Hata waasi pia, kwa sababu amewalazimisha wanayoyaweza na amewahadharisha na mwisho mbaya wa maasi. Pia amefungua mlango wa toba kwa yule ambaye nafsi yake imefanya maovu. Kwa hiyo mwasi habaki na udhuru.

12

13

14

15