TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE Juzuu 8

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE33%

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE Mwandishi:
: HASANI MWALUPA
Kundi: tafsiri ya Qurani

Juzuu 1 Juzuu 2 Juzuu 3 Juzuu 4 Juzuu 5 Juzuu 6 Juzuu 7 Juzuu 8 Juzuu 12 Juzuu 13 Juzuu 14 Juzuu 15 Juzuu 16 Juzuu 17 Juzuu 18 Juzuu 19 Juzuu 20 Juzuu 21 Juzuu 22 Juzuu 23 Juzuu 24
  • Anza
  • Iliyopita
  • 17 /
  • Inayofuata
  • Mwisho
  •  
  • Pakua HTML
  • Pakua Word
  • Pakua PDF
  • Matembeleo: 13111 / Pakua: 3679
Kiwango Kiwango Kiwango
TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASIF JUZUU YA NANE Juzuu 8

Mwandishi:
Swahili

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA NANE

IMEANDIKWA NA: SHEIKH MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYA

IMETAFSIRIWA NA: SHEIKH HASAN MWALUPA

IMEHARIRIWA NA: USTADH ABDALLAH MOHAMED

IMEPANGWA KATIKA KOMPYUTA NA: UKHT PILI RAJABU

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingi sana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahau Marhum Abu Muhammad wa London.

Kama lilivyo jina la Tafsiri yenyewe ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayo mwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katika fani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo. Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katika vitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyo kujipatia wasomaji wengi sana.

Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, ni mtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undani sana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribu sana kwenda na wakati.

Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusisha sana na kung'ang'ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wadhifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo ina madhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo, hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yake kulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilimsaidia sana hata kuweza kutoa kitabu kitwacho 'Al-Fiqh a'laa madhaahabil-khamsah' (Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali na Shia (ambacho twataraji kitatoka hivi karibuni Inshaallah).

Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.

Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi, visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msomaji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishi amewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasyansi kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), na wengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.

Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabaka mbalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.

Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.

Mwisho : Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitolea usiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyo na kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabu kimemfikia msomaji.

MAKOSA YA CHAPA

Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, cha zamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa, Nafikiri sitasoma kitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungo zangu, lakini sikufanikiwa.

Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi ya msahafu mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfano neno yabswutu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa ya Tafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146). Imeandikwa La Ya'alamuun, (hawajui) badala ya Ya'alamuun (wanajua), Mfano wa makosa haya hausameheki.

Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa "Fawqahum ila yawmil qiyama” badala ya “Fawqahum yawamal qiyama",Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.

Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu jabal amail 'Makosa ya chapa.'

Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: " Hatta idha balagha arbai' na sanah badala ya: Hattaidha balagha ashuddahu arbai ' na sanah"

Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakayoyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kama litatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefungua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuri wa maana.

Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia: "Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa, kama kwamba hakuna kitu chochote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote hao ninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa ya kifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin(a.s) :"Watu wote ni wapungufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu."

Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubali- ayale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazi chake, ziwashukie rehema na amani (Amin).

MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH

1

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA NANE

Muendelezo Wa Sura Ya Sita: Al-An'am

وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ ﴿١١١﴾

111.Na lau kama tungewateremshia Malaika, na wafu wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu ana kwa ana, wasingeliamini ila atake Mwenyezi Mungu, Lakini wengi wao wamo ujingani.

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١١٢﴾

112.Na kama hivyo tukamfanyia kila Nabii adui, mashetani watu na majini. Baadhi yao wanawapa wenzao maneno ya kupambapamba kuwahadaa. Na kama Mola wako angelitaka wasingeliyafanya. Basi waache na wanayoyatunga.

وَلِتَصْغَىٰ إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ ﴿١١٣﴾

113.Na ili zielekee hayo nyoyo za wale wasioamini akhera, nao wayaridhie na ili wayachume wanayoyachuma.

AINA YA WATU AYA

Aya 111 – 113

MAANA

Na lau kama tungewateremshia Malaika, na wafu wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu ana kwa ana, wasingeliamini ila atake Mwenyezi Mungu.

Tumesema katika Tafsir ya Aya iliyotangulia kuwa jamaa katika washirikina walimtaka Mtume(s.a.w.w) awaletee muujiza maalum; na kwamba waumini walitamani lau Mwenyezi Mungu angeliitikia maombi yao; na Mwenyezi Mungu akawajibu waumini kwa kauli yake: “Na ni kitu gani kitakachowatambulisha ya kuwa zitakapowafikia hawataamini?”

Baada ya kuishiria yote hayo, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemfafanulia Mtume wake mtukufu, kwamba hawa washirikina ambao wamekutaka waliyoyataka katika miujiza, hawatakuamini kwa hali yoyote; hata kama tutawateremshia Malaika kutoka mbinguni, na tukawafufulia wafu wakashuhudia kwa lugha fasaha ya Kiarabu kuwa wewe ni Mtume, bali hata kama utakushuhudia ulimwengu ardhi yake na mbingu yake, wasingelikusadiki wala kukufuata ‘ila atake Mwenyezi Mungu;’ yaani Mwenyezi Mungu awalazimishe wakuamini wewe kwa nguvu.

Unaweza kuuliza : Je, kukadiria huku ni sawa?. Na je aina hii ya watu inaweza kupatikana, katika hali ya kawaida?. Itakuwaje kikundi kidogo kiukadhibishe ulimwengu na vilivyomo? Je, inawezekana mtu asiamini masikio yake na macho yake, kwa kuwaona wafu wanafufuka kutoka katika makaburi yaliyochakaa maelefu ya miaka na waseme. ‘Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu (na) Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu;’ wasikie wanyama na ndege na samaki na miti na nyota zote, zikinadi shahada mbili; inawezekana kweli aweko mtu atakayekadhibisha miujiza yote hii? Si ajabu hiyo?

Jibu : Kukadiria hivi si sawa, bali ni muhali kwa wale wanaoathirika na haki na dalili yake, na wanaokwenda pamoja na wahyi wa mantiki ya kiak- ili na umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Kwa sababu miu- jiza hii ni dalili mkato isiyokuwa na shaka yoyote.

Ama kukadiria huku kwa watu ambao hisia zao zote zinatawaliwa na masilahi mahususi na kuyaona kuwa ndio akili, ndio umbile na ndiyo haki na uadilifu, basi ni sahihi. Kwa sababu aina hii ya watu ipo, nao ni wakoloni na walanguzi na wengineo mfano wao, ambao wanaishi kwa unyang’anyi na ufisadi.

Wale wanaoona ajabu kukadiria huku hawaitambui hali halisi ya kundi hili, na wamechanganya baina ya mantiki ya kiakili na ya yule mwenye kuongozwa na manufaa.

Akili kwa maana ya akili ni ile tu iliyo mwongozi, anayeamrisha na kukataza; wala haimsikilizi isipokua anayetafuta haki kwa njia ya haki. Ama chenye kuongoza na kuelekeza kwenye manufaa basi hicho ni manufaa ya kibinafsi.

Hicho peke yake ndicho kinachowaongoza katika mambo yao na silika zao. Ndiyo dini yao, ndiyo akili yao, bali ndiyo utu wao na uhai wao. Kwa sababu hiyo, hakuna mantiki yoyote yanayowafaa isipokuwa nguvu aliyoiashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t) kwa kauli yake: ‘Ila atake Mwenyezi Mungu.’

Lakini wengi wao wamo ujingani

Hawajui kuwa wao ni kikundi kiovu ambacho hakifaliwi na mantiki ya kiakili na maumbile wala na mantiki ya dini na utu; wala kitu chochote ila nguvu na kushindwa. Ni makosa na ni kupoteza wakati kuzungumza na watu hawa kwa lugha ya elimu na ubinadamu.

Na kama hivyo tukamfanyia kila Nabii adui, mashetani watu na majini.

Shetani mtu ni maarufu, ni kila anayehadaa watu kwa kuwaingiza kwenye batili na kuwavisha nguo ya haki. Ama jinni yeye ni katika mambo ya ghaibu ya Mwenyezi Mungu. Nasi tunaamini kijumla na kimsingi; wala hautuhusu ufafanuzi; kwani hatutaulizwa kuhusu yeye; sawa na ilivyo katika Malaika. Wala si ajabu kwa Manabii kuwa na maadui. Kwa sababu, ni kawaida kuwe na uadui kati ya kheri na shari, na baina ya haki na batili.

Unaweza kuuliza : Ikiwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye aliyewajaalia Manabii wawe na maadui, kama inavyoonyesha katika Aya, kwa nini basi awaadhibu kwa kuwafanyia uadui Mitume? Vilevile vipi ameamrisha kuwafuata Mitume kisha akawafanyia maadui watakaowapinga na kuwahadaa watu kuwapinga na kuupinga Utume wao?

Jibu : Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t) amewatuma Mitume na akafanya kazi yao ni kulingania Tawhid na uadilifu na kuondoa dhuluma na ushirikina.

Kazi hii, kwa tabia yake, huleta mgongano na vita baina ya Manabii na wale waabudu masanamu na wanyonyaji. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu (s.w.t) ni sababu ya kutumwa Manabii, na Manabii ni sababu ya uadui. Kwa kuzingatia haya umenasibishwa uadui kwake kimajazi, Anasema Mwenyezi Mungu akimsimulia Nuh(a.s) :

﴿قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا ﴿٥﴾ فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَائِي إِلَّا فِرَارًا﴾

“Ewe Mola wangu! Kwa hakika nimewalingania watu wangu usiku na mchana, lakini mwito wangu haukuwazidishia ila kukimbia” (71: 5 – 6)

Kwa hiyo kukimbia kumenasibishiwa mwito wa Nuh(a.s) , na mwito wa Nuh(a.s) ni amri ya Mwenyezi Mungu. Kwa ufasaha zaidi tupige mfano huu: Mtu amemwachia mwanawe utajiri, na ule utajiri ukamsababishia uadui na husda. Basi kimajazi: “Mzazi wake ndiye aliyempa husda ile mwanawe!”

Baadhi yao wanawapa wenzao maneno ya kupambapamba kuwahadaa.

Maneno ya kupambapamba ni maneno yaliyochanganywa na uwongo. Dhahiri yake ni rehema na ndani yake ni adhabu. Maana ni kuwa waovu wanawatia wasiwasi wenzao kwa mambo ya batili yaliyochanganywa haki, kwa makusudio ya kuhadaa na kuipinga haki na watu wake.

Na kama Mola wako angelitaka wasingeliyafanya.

Dhamir ya wasingeliyafanya inarudia kwenye amali zao mbaya; yaani uadui kwa Mitume na kuambiana wao kwa wao maneno ya kupamba. Maana ni kuwa lau Mola wako angelitaka kuwazuia kwa nguvu kufanya ubaya wasingelikuwa na uadui huo wala kuambiana. Lakini hekima yake imepitisha kuwaacha kama walivyo, wawe na hiyari bila ya kuendeshwa, wapate kuhisabiwa waliyoyafanya na kuadhibiwa wanayostahiki.

Basi waache na wanayoyatunga katika uwongo.

Wajibu wako ni kufikisha na ni juu yetu kuhisabu na malipo.

Na ili zielekee hayo nyoyo za wale wasioamini akhera.

Yaani waovu wanaambiana kauli za kupambapamba ili wazisikilize makafiri na waridhie baada ya kuzisikiliza na wazitumie bila ya kufanya utafiti. Na ili wayachume wanayoyachuma katika maasi na madhambi; na apambanuke mumin na kafir na mwenye ikhlasi na mnafiki.

Kwa ufupi ni kuwa maiblis waovu wanapambapamba kauli ili wawahadae wenye nafsi dhaifu na wapondokee kwao na wachume dhambi.

Amesema Abu Hayani Al-andalusi: “Maneno haya yako katika upeo wa fasihi, kwani mwanzo inakuwa ni hadaa, inayofuatiwa na kupondokea, kisha kuridhia na kuchuma (dhambi); kama kwamba kila moja linasababishwa na lililo kabla yake.

فَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١١٤﴾

114.Je, nimtafute hakimu asiyekuwa Mwenyezi Mungu na hali yeye ndiye aliyewateremshia Kitab kinachofafanua. Na wale tuliowapa Kitab wanajua kwamba imeteremshwa na Mola wako kwa haki, Basi usiwe miongoni mwa wanaotia shaka.

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١١٥﴾

115.Na limetimia neno la Mola wako kwa ukweli na uadilifu. Hakuna wa kubadilisha neno lake. Na Yeye ni msikizi, mjuzi.

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿١١٦﴾

116.Na kama ukiwatii wengi katika waliomo ardhini watakupoteza na njia ya Mwenyezi Mungu. Hawafuati ila dhana na hawakuwa ila wenye kuzua tu.

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿١١٧﴾

117.Hakika Mola wako anawajua vyema wanaopotea njia yake na anawajua sana wanaoongoka.

NIMTAFUTE HAKIMU ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU

Aya 114 – 117

MAANA

Je, nimtafute hakimu asiyekuwa Mwenyezi Mungu na hali yeye ndiye aliyewateremshia Kitab kinachofafanua?

Aya hii inaambatana na ile Aya ya ugomvi na uadui baina ya Mtume na washirikina ambao walimtaka awaonyeshe muujiza. Maana ni kuwa Mtume(s.a.w.w) aliwaambia washirikina kwamba nyinyi mnatoa hukumu katika kutaka miujiza na mnanipangia mambo, na mimi siwezi kuikiuka hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Qur’an imekwisha washukia, inatosha na kutekeleza mnayoyahitajia kujua haki, halali na haramu. Haina mfano wake katika misingi yake na mafunzo yake. Ni yenye kuthibitisha ukweli wake kwa kutumia ufasaha wake ushindao, ina sharia zenye kudumu milele na kutoa habari nyingi za ghaibu. Kwa hiyo, huku kutaka kwenu mambo mengi si lolote ispokuwa ni inadi tu.

Na wale tuliowapa Kitab wanajua kwamba imeteremshwa na Mola wako kwa haki.

Yaani wale wenye insafu katika maulama wa kiyahudi na kinaswara, wana- jua kwa yakini ukweli wa Qur’an na Utume wa Muhammad(s.a.w.w) . Tazama Aya yenye maneno kama haya katika Juz. 2 (2:146).

Basi usiwe miongoni mwa wanaotia shaka.

Wafasiri wengi wamesema kuwa msemo huu (usitie shaka) anaambiwa Mtume na makusudio ni asiyekuwa yeye kwa njia ya fumbo.

Ama sisi tunaona kuwa msemo unaelekezwa kwa Mtume, na yeye ndiye makusudio, pamoja na kujua kuwa Mtume hatii shaka Qur’an, bali ni muhali kwake kutia shaka. Imesihi kuelekezwa msemo kwake pamoja na isma yake, kwa vile unatoka kwa aliye juu (Mwenyezi Mungu) kwenda kwa aliye chini, Hayo tumeyaeleza mara nyingi.

Na limetimia neno la Mola wako kwa ukweli na uadilifu.

Makusudio ya neno la Mola wako hapa ni Qur’an au Uislam ambao umeshinda juu ya dini zote wajapochukia washirikina. Haya ndiyo makusudio kwa ukamilifu. Ama maana ya kwa ukweli na uadilifu ni kuwa Qur’an ni kweli katika kila inayoyasema, na ni uadilifu katika kila inay- ohukumu na kuwekea sharia.

Hakuna wa kubadilisha neno lake.

Kwa sababu ni ukweli na uadilifu na kila ambalo ni ukweli na uadilifu basi ni hali halisi, wala haiwezi kusemwa jambo ni ukweli na uadilifu ikiwa halina msingi halisi. Na msingi huu haubadiliki wala haugeuki; yaani hauepukani na athari na natija iliyopangiwa.

Na yeye msikizi wa wanayoyasemamjuzi wa wanayoyafanya na wanayoyadhamiria.

Na kama ukiwatii wengi katika waliomo ardhini watakupoteza na njia ya Mwenyezi Mungu. Hawafuati ila dhana na hawakuwa ila wenye kuzua tu.

Kila mwenye kushikamana na dini basi huamini kwa imani ya moja kwa moja, na hushikamana nayo kwa upofu, na kila rai anayoiona huona ni kweli, na kwamba mengineyo ni njozi na dhana tu. Kwa hiyo tukizikusanya rai zote na itikadi zote na tukazipima kwa vipimo vya Mwenyezi Mungu, natija ni kuwa watu wengi hufuata dhana za makosa na za uongo.

Kwa ajili hiyo ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake asiwasikilize watu na kutowaheshimu na ada zao na itikadi zao; na kwamba ni juu yake kufuata yale aliyopewa Wahyi na Mwenyezi Mungu kwa sababu ndiyo njia ya haki na uwongofu.

Ikiwa watu wengi wako kwenye makosa katika rai na dini, basi hakuna kipimo cha kauli zao na hukumu zao kwa uwongofu wa hili na upotofu wa lile. Isipokuwa hukumu katika hilo ni ya Mwenyezi Mungu peke yake; yaani yale aliyoyabainisha katika misingi na uthabiti uliomo katika Kitabu chake chenye hekima.

Haya ndiyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Hakika Mola wako anawajua vyema wanaopotea njia yake na anawajua sana wanaoongoka.

Katika msingi hiyo ya Mwenyezi Mungu inayowapambanua wenye haki na wenye batili ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

﴿ وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴾

“Na ni nani mbora wa kusema kuliko alinganiaye kwa Mwenyezi Mungu, na akafanya amali njema na akasema: Mimi ni miongoni mwa waislamu.” (41:33).

2

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA NANE

فَكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِآيَاتِهِ مُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾

118.Basi kuleni katika wale waliosomewa jina la Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi mnaziamini ishara zake.

وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ ﴿١١٩﴾

119.Mna nini hamli katika wale waliosomewa jina la Mwenyezi Mungu? Na amewafafanulia aliyowaharamishia isipokuwa vile mnavyolazimika, Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya ilimu, Hakika Mola wako anawajua vyema wanaoru- ka mipaka.

وَذَرُوا ظَاهِرَ الْإِثْمِ وَبَاطِنَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَكْسِبُونَ الْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا يَقْتَرِفُونَ ﴿١٢٠﴾

120.Na acheni dhambi zilizo dhahiri na zilizofichikana. Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ ﴿١٢١﴾

121.Wala msile wale wasiosomewa jina la Mwenyezi Mungu kwani huko ni ufasiki, Na hakika mashetani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na kama mkiwatii, hakika mtakuwa washirikina.

BISMILLAH KWA KINACHOCHINJWA

Aya 118 – 121

MAANA

Basi kuleni katika wale waliosomewa jina la Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi mnaziamini ishara zake.

Waarabu wakati wa ujahiliya walikuwa wakila mfu, na wakitaja majina ya masanamu wanayoyaabudu wakati wa kuchinja. Mwenyezi Mungu akaharamisha hilo kwa Wailsamu; akahalalishia kula wanaochinjwa kwa sharti ya kutaja jina Lake na sio jina la mwengine.

Unaweza kuuliza : kuwa kujuzu kula aliyechinjwa, aliyesomewa jina la Mwenyezi Mungu, hakuambatani na kumwamini Mwenyezi Mungu na ishara zake. Ambapo inajuzu kwa kafiri kumla huyo; kama ambavyo kumwamini Mwenyezi Mungu hakuambatani na kula aliyesomewa Jina la Mwenyezi Mungu. Ambapo Mumin anakuwa Mumin hata kama hakumla. Lakini dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa kuamini ni sharti la uhalali wa kula chinjo hilo. Kwa sababu maana yake ni, kuleni ikiwa nyinyi ni waumini.

Jibu : Kauli yake Mwenyezi Mungu, ‘Ikiwa nyinyi mnaziamini ishara zake,’ sio sharti la uhalali wa kula chinjo lililosomewa jina la Mwenyezi Mungu, isipokuwa hii ni kuonyesha kuwa anayemtaja asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwa chinjo, basi amemfanyia Mwenyezi Mungu mshirika.

Kwa sababu, ameelekeza tendo lake hili kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kama walivyokuwa wakifanya washirikina wa Kiarabu; na kwamba mwenye kutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa chinjo basi atakuwa amemwamini Mwenyezi Mungu na amemkanushia mshirika, Kwa vile atakuwa amemwelekea yeye tu peke yake.

Mna nini hamli katika wale waliosomewa jina la Mwenyezi Mungu?

Inaonyesha, kutokana na Aya hii, kwamba baadhi ya Waislamu walijizuilia kula chinjo ambalo limesomewa jina la Mwenyezi Mungu kwa kujitatiza; kwamba inakuwaje mtu achinje mnyama kwa mkono wake na ataje jina la Mwenyezi Mungu kisha ale na isijuzu kula mnyama aliyeuliwa na Mwenyezi Mungu ambaye amekufa mwenyewe!

Ndipo Mwenyezi Mungu akalipingia hilo kwa kusema: Mna nini hamli katika wale waliosomewa jina la Mwenyezi Mungu

Na amewafafanulia aliyowaharamishia isipokuwa vile mnavyolazimika.

Kuhusu aliyowafafanulia anakusudia wale aliowaishiria katika Aya 145, katika Sura hii, ambayo itakuja tafsir yake Inshaalah. Pia anaashiria wale waliotajwa katika Juz.2 (2:173).

Tumezungumzia kwa ufafanuzi kuhusu walioharamishwa na hukumu ya aliyelazimika katika Juz.2 (2:173).

Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya ilimu.

Yaani wanahalalisha na kuharamisha kulingana na matamanio yao bila ya dalili. Miongoni mwa hayo ni kuwa washirikina wa Kiarabu walihalalisha kula nyamafu na kuharamisha kula bahira, saiba, wasila na hami. Umetangulia ufafanuzi wa hayo katika Juz.6 (5:3).

Hakika Mola wako anawajua vyema wanaoruka mipaka.

Ambao wanahalalisha na kuharamisha kwa hawaa zao na matamanio yao, Na kwamba atawaadhibu inavyostahiki.

Na acheni dhambi zilizo dhahiri na zilizofichikana.

Makusudio ya dhambi ni kitendo cha haramu kinacholeta dhambi; na dhahiri yake ni kufanya maasi dhahiri; na kufichikana ni kuyafanya kisiri. Mwenyezi Mungu amekataza kufanya maasi yote ya dhahiri na ya batini.

Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa yale waliyokuwa wakiyachuma, katika kufuata matamanio bila ya elimu; wala hawataachwa bure bure bila ya hisabu na adhabu.

Wala msile wale wasiosemowa jina la Mwenyezi Mungu kwani huko ni ufasiki.

Dhamiri ya huko inarudia kula, Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuhalalishia waliochinjwa kwa jina lake, anaharamisha ambao hawakutajiwa.

Kwa kutegemea hilo, ndipo mafakihi wote, isipokuwa Shafii, wamekonga- mana kuwa mchinjaji akiacha kutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa makusudi, basi ni haramu; sawa na nyamafu. Inatosha jina la Mwenyezi Mungu tu, mfano: Allah, Allahu Akbar, Al-Hamdulillah, Bismillah, Lailaha illa Ilah na mfano wake.

Wametofautiana kuacha kusoma jina la Mwenyezi Mungu kwa kusahau. Hanafi, Jaafariya (Shia) na Hanbal wamesema si haramu nyama hiyo. Malik akasema ni haramu na Shafii amesema kuwa akiwacha kusoma jina la Mwenyezi Mungu kwa makusudi pia si haramu, sikwambii tena kusahau.

Na hakika mashetani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi.

Makusudio ya mashetani hapa ni maiblis–watu ambao wanauviringa ukweli na kutunga maneno wanayowahadalia wale wenye akili za juu juu. Kwa mafano, baadhi ya washirikana na maiblis wao walikuwa wakiwaambia wafuasi wao.

Waulizeni Masahaba wa Muhammad, vipi mnakula mnyama mliyemuua nyinyi wenyewe, kumchinja kwa mikono yenu; na wala hamli mnyama aliyeuawa na Mwenyezi Mungu, aliyekufa mwenyewe ambapo aliyeuawa na Mwenyezi Mungu ni bora kuliko mliyemuua nyinyi?

Huo ndio mjadala wao ambao mashetani waliwashauri marafiki zao kwa makusudio ya kuingiza shaka katika nyoyo dhaifu za baadhi ya Waislamu na kuwafitini na dini yao.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) akasema kuwaambia hawa wadhaifu:

Na kama mkiwatii, hakika mtakuwa washirikina.

Yaani mwenye kuwasikiliza washirikina na akahalalisha kula nyamafu, kama walivyohalalisha, basi yeye ni mshirikina kama wao, na hukumu hii haihusiki na kula nyamafu peke yake, bali kila anayepinga hukumu ya sharia akijua kuwa imethibiti, basi huyo ni kafiri.

أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَافِرِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٢﴾

122.Je, aliyekuwa maiti kisha tukamhuisha na tukamjaalia nuru, hutembea mbele za watu kwayo, mfano wake ni kama yule aliyegizani asiyeweza kutoka humo? Namna hiyo wamepambiwa makafiri waliyokuwa wakiyafanya.

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَابِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا فِيهَا ۖ وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿١٢٣﴾

123.Na kama hivyo tumejaalia katika kila mji wakubwa wa wakosefu wake ili wafanye vitimbi humo; wala hawafanyii vitimbi isipokuwa wanajifanyia wenyewe, lakini hawatambui.

وَإِذَا جَاءَتْهُمْ آيَةٌ قَالُوا لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَا أُوتِيَ رُسُلُ اللَّـهِ ۘ اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ۗ سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِندَ اللَّـهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ ﴿١٢٤﴾

124.Na zinapowafikia ishara husema: Hatutaaamini mpaka tupewe sawa na yale waliyopewa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi wa kujua mahali anapoweka ujumbe wake. Itawafika wale waliokosea dhila inayotoka kwa Mwenyezi Mungu na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya.

KUMHUISHA MAITI

Aya 122 – 124

MAANA

Je, aliyekuwa maiti kisha tukamhuisha na tukamjaalia nuru, hutem- bea mbele za watu kwayo, mfano wake ni kama yule gizani asiyeweza kutoka humo?

Huu ni mfano alioupiga Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kulinganisha baina ya mumin na kafiri. Ufafanuzi wake ni kuwa, kuwalinganisha wawili hao ni sawa na kulinganisha mauti na uhai. Na mwanga na giza. Kafiri ni maiti akiamini hufufuliwa upya na kurudiwa na uhai na imani yake ni nuru anayokwenda nayo katika uhai wake.

Anayebakia kwenye ukafiri na shirki ni kama anajikokota gizani, anakwenda bila ya uongozi na haimfikii kheri yoyote katika maisha yake yote.

MWENYE KUULIZWA NA MUULIZAJI MKUU

Mtu anaweza kusema kuwa : Aya imefananisha imani na uhai; na ukafiri na mauti; ingawaje makafiri na walahidi, katika zama hizi, wanaishi maisha ya anasa na wenye utajiri zaidi kuliko waumini na wenye kuabudu?

Jibu : Makusudio ya uhai katika Aya hii sio kuishi mtu katika neema na anasa, akawa anakula vizuri, kuvaa nguo za thamani na kunywa vinywaji vitamu. Hakika anasa hazihusiani na ukafiri wala imani. Kama ni hivyo waumini wa Mashariki na Magharibi wangelikuwa sawa katika maendeleo na uchumi mzuri, vilevile walahidi na makafiri.

Hali nzuri ya maisha ina sababu na mambo yanayoambatana nayo ambayo hayafungamani na chochote katika imani au ukafiri. Isipokuwa makusudio ya uhai, katika Aya hii, ni imani na hisia za kidini zinazompa mtu msukumo wa kutekeleza wajibu, akiwa ni mtu atakayeulizwa kuhusu mwenendo wake, atahisabiwa na kulipwa thawabu kwa wema wake, na adhabu kwa uovu wake.

Lau mtu angelikuwa si mwenye kuulizwa chochote, ingelikuwa sharia na kanuni ni maneno tu, yasiyokuwa na maana yoyote. Na tukipitisha kuwa mtu ataulizwa wala hataachwa bure bure, basi itatulazimu tupitishe kwam- ba yeye ataulizwa mbele ya yule ambaye

﴿ لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ﴾

“Haulizwi anayoyafanya, na wao ndio wanaoulizwa” (21:23)

Lau muulizaji huyu anaulizwa, basi ingelipaswa kupatikana atakayemuuliza, na kuendelea hivyo hivyo bila mwisho.

Mwenye kukanusha kuweko muulizaji mkuu kabisa ambaye huuliza na haulizwi, basi atakuwa amekanusha maulizo; Kwa sababu hakuna maulizo bila ya muulizaji, Na mwenye kukanusha maulizo amekanusha maisha ya kijamii.

Unaweza kusema : Ndio mtu ataulizwa, lakini si lazima muulizaji awe Mwenyezi Mungu; watu wanaweza kuchagua kundi (kamati) ambalo litauliza watu.

Nasi tutauliza je kundi hilo likikosea, liulizwe na lihukumiwe na nani? Ikijibwa ni dhamir.

Tutasema :Kwanza , dhamir ni jambo la kimaana si la kidhati.

Pili , dhamiri anayo kila mtu, kwanini huyu aache dhamiri yake afuate ya mwingine?

Kwa hiyo, basi hakuna muulizaji asiyeulizwa ila Mwenyezi Mungu peke yake. Mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu akailazimisha nafsi yake kufuata sharia za Mwenyezi Mungu na hukumu zake, basi atakuwa na busara ya mambo yake, itikadi yake na tabia zake. Vinginevyo atakuwa kama aliye gizani asiyeweza kutoka.

Namna hiyo wamepambiwa makafiri waliyokuwa wakiyafanya.

Yaani kama waliyvopambiwa waumini amali zao, vilevile washirikina wamepambiwa amali zao. Tofauti ni kuwa wao wamepambiwa kinyume na hali halisi, wamepambiwa, kimawazo na kinjozi tu.

Na kama hivyo tumeajaalia katika kila mji wakubwa wa wakosefu wake.

Makusudio ya mji ni kila jamii (mkusanyiko) wa watu, wachache au wengi. Maana ni kuwa: Ewe Muhammad kama ambavyo wanapatikana katika jamii yako viongozi wa waovu wanaofanya vitimbi na kuifanyia uadui dini ya Mwenyezi Mungu, vilevile katika jamii zilizotangulia walikuwapo; na hivi sasa pia wako viongozi wanaowafanyia vitimbi watu wao na kuwa katika msimamo wa kuifanyia uadui haki na wenye haki.

Unaweza kuuliza : Dhahiri ya Aya hii inafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye aliyewafanya wakubwa kuwa waovu kwa watu wa haki, na tunajua kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hukataza vitimbi na uovu; je, kuna taawili gani hapa?

Jibu : Makusudio ya kunasibishwa kwake huku Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuashiria kwamba matakwa ya Mwenyezi Mungu yamepitisha kuwa desturi ya jamii iwe kwenye misingi ya kupingana baina ya wenye haki na wenye batili, baina ya viongozi wenye kufanya uadui na wenye kufanyiwa uadui.

Hakuna kimbilio la kuepuka mgongano huu ila kumalizwa waovu; na hapana budi kutimia hilo na kutukuka neno la haki mikononi mwa wanaolingania uadilifu na utengenevu; hata kama batili itakuwa kubwa kiasi gani. Hilo amelisajili Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Kitabu chake, aliposema:

﴿اسْتِكْبَارًا فِي الْأَرْضِ وَمَكْرَ السَّيِّئِ وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا سُنَّتَ الْأَوَّلِينَ فَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا وَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَحْوِيلًا﴾

“Na vitimbi vibaya havimpati ila yule aliyevifanya, Basi hawangoji ila desturi iliyokuwa kwa watu wa zamani, wala hutakuta mabadiiko katika desturi ya Mwenyezi Mungu, wala hutakuta mageuko katika desturi ya Mwenyezi Mungu.” (35:43)

Kukaririka huku ni kutilia mkazo kwamba mwisho ni wa wanaomcha Mwenyezi Mungu; kadiri zitakavyorefuka zama. Hivi ndivyo tunapata tafsir ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

Ili wafanye vitimbi humo; wala hawafanyii vitimbi isipokuwa wanajifanyia wenyewe, lakini hawatambui.

Na zinapowafikia ishara husema: Hatutaaamini mpaka tupewe sawa na yale waliyopewa Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Wametofautiana wafasiri katika maana ya Aya hii kwa kauli mbili: Kwanza, kwamba wakubwa waovu katika Waarabu walimtaka Muhammad(s.a.w.w) awaletee muujiza kama aliopewa Musa, wa kupasua bahari; na wa Isa, wa kufufua wafu.

Kauli ya pili, ni kuwa wao walimwambia hatutakuamini mpaka utushushie wahyi kama ulivyowashukia Mitume. Razi akasema: “Hii ndio kauli mashuhuri baina ya wafasiri.”

Nasi tunaipa uzito kuliko ya kwanza; Kwa sababu mfumo wa Aya unafahamisha hivyo, ambapo Mwenyezi Mungu anawajibu wakubwa waovu kwa kauli yake:

Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi wa kujua mahali anapoweka ujumbe wake.

Kuongezea kuwa kutaka kwao Mwenyezi Mungu awateremshie Wahyi kunaafikiana na hasadi yao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amesema:

﴿ أَمْ يَحْسُدُونَ النَّاسَ عَلَىٰ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ﴾

“Au wanawahusudu watu kwa alichowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake?.” Juz.5 (4:54)

Katika Majmaul-bayan na kwengine, imeelezwa kuwa Walid bin Mughira alimwambia Mtume(s.a.w.w) :“Lau Utume ungelikuwa ni kweli mimi ningelistahiki zaidi kuliko wewe, kwa sababu mimi ni mkubwa kuliko wewe, na nina mali nyingi kushinda wewe.”

Maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi wa kujua mahali anapoweka ujumbe wake’, ni kuwa yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu anauchagulia ujumbe wake mtu atakayefaa katika viumbe vyake, na Muhammad ni Mtukufu zaidi wa viumbe vya Mwenyezi Mungu na aheshimiwaye zaidi kwao.

Itawafika wale waliokosea dhila inayotoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa sababu walijifanya wakubwa wakajiadhimisha, Ndipo wakastahiki malipo ya udhalilifu na fedheha. Kuna Hadith isemayo kuwa wenye kutakabari watafufuliwa katika Sura ya chembe (kama sisimizi) watakanyagwa na watu kwa nyayo zao, ikiwa ni malipo ya kujifanya kwao wakubwa katika dunia.

Na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya.

Udhalili ni malipo ya kiburi, na adhabu ni malipo ya vitimbi na hadaa. Kwa maneno mengine ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t) anawafanyia wale wenye nia mbaya na malengo ya ufisadi kinyume cha wanavyokusudia na wanavyolenga.

3

TAFSIRI YA QURANI AL-KAASHIF JUZUU YA ISHIRINI

Sura Ya Ishirini Na Nane: Surat Al-Qasas. Tabrasi amesema imeshuka Makka. Ina Aya 88.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

طسم ﴿١﴾

1. Twaa Siin Miim.

تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾

2. Hiyo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

نَتْلُو عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِالْحَقِّ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣﴾

3. Tunakuosomea habari za Musa na Firauni kwa haki kwa ajili ya watu wanaoamini.

إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٤﴾

4. Hakika Firauni alitakabari katika nchi akagawa watu wake makundi. Akidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiwaacha watoto wao wa kike. Hakika yeye alikuwa katika wafisadi.

وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ ﴿٥﴾

5. Na tunataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi na kuwafanya wawe ni viongozi na kuwafanya ni warithi.

وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَنُرِيَ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُم مَّا كَانُوا يَحْذَرُونَ ﴿٦﴾

6. Na kuwamakinisha katika ardhi. Na kumuonyesha Firauni na Hamana na majeshi yao yale waliyokuwa wakiyahadhari kwao.

AYA ZA KITABU

Aya 1 – 6

TWAA SIIN MIIM.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1)

Hiyo ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

Hiyo ni ishara ya Sura hii, Kitabu ni Qur’an na kubainisha ni kupambanua baina ya upotevu na uongofu.

Tunakuosomea habari za Musa na Firauni kwa ajili ya watu wanaoamini.

Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemsomea Mtume wake mtukufu habari mara kwa mara. Katika Juz. 16 kifungu cha ‘Kukaririka Kisa’ (20:9) tumeeleza lengo la kukaririka kisa cha Musa.

Hakika Firauni alitakabari katika nchi akagawa watu wake makundi.

Alipetuka mipaka na akajifanya jabari, akawagawa wananchi wake kwenye makundi wakigombana, ili udumu utawala wake.

Akidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiwaacha watoto wao wa kike. Hakika yeye alikuwa katika wafisadi.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:49) na Juz. 9 (7:127).

KWA NINI FIRAUNI ALIWAKANDAMIZA WANA WA ISRAIL?

Mmoja katika wafasiri wa kisasa anasema: “Firauni aliwakandamiza wana wa Israil kwa sababu walikuwa na itikadi isiyoafikiana na itikadi yake. Wao walikuwa wakifuata dini ya babu yao Ibrahim na Ya’qub. Ingawa itikadi yao ilikuwa na upotofu, lakini walibakia na itikadi ya Mungu mmoja.”

Sisi tunamuuliza mfasiri huyu mpya: Umejua vipi kuwa mayahudi waliokuwa wakati wa Firauni walikuwa kwenye dini ya Ibrahim(a.s) na kwamba walibaki na itikadi ya Mungu mmoja? Je, umepata kujua kutokana na kuli yao: “Ewe Musa! Hebu nasi tufanyie waungu kama hawa walivyo na waungu.” Au kauli yao: “Hatutakuamini mpakae tumwone Mungu wazi wazi.”

Au ni kutokana na kuabudu kwao ndama au kwa kuwaua kwao mitume? Ikiwa Firauni aliwakandamiza kwa sababu ya itikadi yao, kwa nini Mtume wao na mwenye ikhlasi zaidi, Musa aliwapa wasifa huu ufuatao? Ufuska, Juz. 6 (5:25), wapumbavu, Juz. 9 (7:155), wabatilifu Juz. 9 (7:153) na ujinga Juz. 9 (7:138). Kama amabavyo Mwenyezi Mungu (s.w.t) katika Aya kadhaa amewasifu kwa ufisadi, uovu na kwa kila aina ya hatia?

Qur’an imetaja kwamba Firauni aliwakandamiza wana wa isaril na kwam- ba yeye alipituka mpaka katika dhulma yake, lakini haikuashiria sababu.

Kwa hiyo maulama wametofautiana katika kuielezea. Kuna waliosema kuwa kuhani alimwambia Firauni kuwa atazaliwa mtoto katika wana waisrail, atakayekuja mvua ufalme wake, wengine wakasema kuwa mitume waliokuwa kabla yake walitoa bishara ya kuja kwake.Firauni alipojua hivyo akahofia na kuanza kuwachinja watoto wa kiume wa wana wa israil. Na sikuona yoyote aliyesema kuwa Firauni aliwakandamiza kwa sababu ya kuwa kwenye dini ya Ibrahim.

Tukiangalia sera ya wana wa israil kwa Mtume wao Musa(a.s) na mitume wengine waliokuja baada ya Musa; ambapo walikuwa wakikadhibisha wengine na wengine wakiwaua. Pia tukiangalia sera yao katika miji wanayoiteka jinsi wanavyoleta fitna, kupanga njama, kujaribu kutawala nyenzo na propaganda zote.

Tukiangalia yote haya basi tunakubaliana na Sheikh Maraghi aliyesema: “Firauni aliwakandamiza wana wa israil kwa vile aliwahofia wanaume ambao walikuwa na ufundi na mikononi mwao mlikuwa na hatamu za uchumi; kuwa muda ukiendelea watakuwa juu kiuchumi waje wawashinde wamisri. Na uchumi ndio wenye nguvu kiutawala.”

Ni kweli kuwa Firauni alipetuka mpaka katika dhulma kwa kuwachinja watoto wa kiume na kuwafanya watumwa watoto wa kike wa wana wa israil, lakini sababu ya yote haya ni wayahudi.

Kwa hiyo lawama ni la wote wawili. Mayahudi kwa sababu ya chuki yao, tabia yao na malengo yao mabaya na pia kwa Firauni kwa sababu aliwatesa wasiokuwa na hatia kwa sababu ya wenye hatia.

LINI MWENYEZI MUNGU ATAWAFADHILI WALIODHOOFISHWA?

Na tunataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi.

Waliodhoofishwa katika ardhi ni wale waliokandamizwa na wenye nguvu, waliotawala nyenzo zao na nguvu zao kimabavu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) atawafadhili uhuru na kujikomboa kwenye ukandamizaji ikiwa watafanya juhudi na kujitolea kwa ajili ya maisha yao na heshima yao; sawa na mgonjwa atapona ikiwa atafanya matibabu mazuri na mkulima atapata mavuno akilima vizuri.

Mwenyezi Mungu ana desturi katika maumbile yake, na wala hutapata mabadiliko katika desturi ya Mwenyezi Mungu kabisa. Kila mwenye kufuata njia atafika, awe mumin au kafiri. Ama malipo ya kafiri na mumin ni siku ya Kiyama, si katika maisha haya.

Basi atakayemnyenyekea dhalimu, Mwenyezi Mungu humdhalilisha na humwachia atakayemdhulumu, hata kama ataswali, kufunga na kuhiji. Kwa sababu ameidhalilisha haki na akisaidia batili na akhera hana kitu.

Na mwenye kujikomboa kutoka kwa dhalimu na watu wake, na akajitolea mhanga kwa ajili ya heshima yake, Mungu humpa nusra kuwashinda mad- halimu na wababe; kwa sababu atakuwa amekutana na utashi wa Mwenyezi Mungu na amri yake, kwa jihadi na uimara.

Hatuna haja ya kurudia historia ya mbali kutafuta ushahidi wa hakika hii. Kwani ukakamavu wa wananchi wa Vietnam mbele ya taifa hilo na nguvu kubwa ya shari na ufisadi, ni dalili kuwa Mwenyezi Mungu yuko pamoja na mwenye kudhulumiwa anayepigana jihadi aliye mvumilivu, kwa namna yoyote ile atakayokuwa.

Kwa ufupi ni kuwa Mwenyezi Mungu hapigani kwa ajili ya waliodhoofishwa, lakini anakuwa nao na kuwapa msaada wake, ikiwa watapigana na kupinga kwa lengo la haki, uadilifu na kujikomboa kutoka kwenye makucha ya ukoloni na dhulma. Mwenyezi Mungu yuko pamoja na hawa, kwa sababu, yuko pamoja na kila mwenye kufanya juhudi na akatenda kwa ajili ya maisha.

Haya tumeyafafanua zaidi katika Juz. 13 (13:11).

Unaweza kuuliza : Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwangamiza Firauni na watu wake, akawaokoa wana wa israil na adhabu yao na ukandamizwaji wao. Hii inamaanisha kuwa Mwenyezi Mungu anapigana kwa ajili ya wanyonge; bali kuna Aya isemayo:

إِنَّ اللَّـهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا ﴿٣٨﴾

“Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walioamini.” Juz. 17 (22:38)?

Jibu : Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwangamiza Firauni na watu wake kwa sababu ya shirki yao na kuwakadhibisha kwao mitume na sio kuwasaidia wana wa israili; sawa na alivyoangamiza kaumu ya Nuh na washirikina wengineo.

Kwa hiyo wana wa israil na wengineo wakapona na dhulma na ukandamizwaji. Ama makusudio ya walioamini, wanaokingwa na Mwenyezi Mungu ni wale wanopigana jihadi. Na wavivu wako kwenye dini ya wale waliomwambia Musa:

فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ ﴿٢٤﴾

“Nenda wewe na Mola wako mkapigane, hakika sisi ni wenye kukaa hapa.” Juz. 6 (5:24)

Na kuwafanya wawe ni viongozi.

Yaani tuwafanye mitume miongoni mwao.

Na kuwafanya ni warithi na kuwamakinisha katika ardhi.

Mwenyezi Mungu anawafanya huru kwa muda mrefu baada ya kuwa utumwani.

Na kumuonyesha Firauni na Hamana na majeshi yao yale waliyokuwa wakiyahadhari kwao.

Kwao ni kwa hao wana wa israil. Maana ni kuwa Firauni na watu wake walihofia utawala wao usiingie mikononi mwa wana wa israil, ndio wakachukua hadhari, lakini Mwenyezi Mungu (s.w.t) akawaingiza kwenye yale waliyoyahofia.

وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧﴾

7. Na tulimpa wahyi mama wa Musa kuwa mnyonyeshe. Na utakapomhofia basi mtie mtoni. Na usihofu wala usihuzunike. Hakika sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa mitume.

فَالْتَقَطَهُ آلُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُوًّا وَحَزَنًا إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا خَاطِئِينَ ﴿٨﴾

8. Basi wakamwokota watu wa Firauni aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa.

وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّي وَلَكَ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾

9. Akasema mke wa Firaun: Ni kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa au tumfanye kuwa mtoto wetu. Wala wao hawakutambua

وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَارِغًا إِن كَادَتْ لَتُبْدِي بِهِ لَوْلَا أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠﴾

10. Moyo wa mamake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kudhihirisha, lau tusingeliuimarisha moyo wake ili awe miongoni mwa waumini.

وَقَالَتْ لِأُخْتِهِ قُصِّيهِ فَبَصُرَتْ بِهِ عَن جُنُبٍ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١١﴾

11. Akamwambia dadake (Musa) mfuatie. Basi akawa anamwangalia kiupande upande na wao hawatambui.

وَحَرَّمْنَا عَلَيْهِ الْمَرَاضِعَ مِن قَبْلُ فَقَالَتْ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ أَهْلِ بَيْتٍ يَكْفُلُونَهُ لَكُمْ وَهُمْ لَهُ نَاصِحُونَ ﴿١٢﴾

12. Na tukamharamishia wanyonyeshaji tangu mwanzo. Akasema (dadake): Je, niwaonyeshe watu wa nyumba watakaowalelea na watakuwa wema kwake?

فَرَدَدْنَاهُ إِلَىٰ أُمِّهِ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ وَلِتَعْلَمَ أَنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾

13. Basi tukamrudisha kwa mama yake ili yaburudike macho yake na ajue kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Lakini watu wengi hawajui.

MAMA WA MUSA

Aya 7 – 13

MAANA

Na tulimpa wahyi mama wa Musa kuwa mnyonyeshe.

Makusudio ya wahyi hapa ni ilhamu; ni mfano kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na Mola wako akampa wahyi nyuki.” Juz. 14 (16:68). Katika Juz. 9 (7: 103 -112).

Tumenukuu kutoka kitabu Qisasul-qur’an, kwamba jina la mama yake Musa ni Yukabid (Jochebed). Kisha tukasoma katika Tawrat kuwa hilo ndilo jina lake na kwamba aliolewa na Amram, mtoto wa kaka yake. Musa ndiye mdogo katika watoto wa baba yake, akiwa ni watatu, baada ya Maryam na Harun.

Na utakapomhofia basi mtie mtoni.

Makusudio ya mto hapa ni mto Nile. Maana ni akimhofia kuchinjwa amtie mtoni kwa mkono wake! Itakuwaje, mwenye akili aweze kujitupa motoni?

Lakini akaambiwa: Na usihofu wala usihuzunike. Hakika sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa mitume.

Usimhofie, hakika Mwenyezi Mungu ndiye mhifadhi na mlinzi. Yule ambaye ameujaalia moto kuwa baridi na salama kwa Ibrahim, ataijalia bahari kuwa amani kwa Musa. Alimpa habari ya usalama wa mtoto wake na kwamba yeye atamlea na pia akampa habari njema kuwa amemchagua kwa risala yake na kumhusu kwa rehema yake. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:38).

Basi wakamwokota watu wa Firauni aje kuwa adui kwao na huzuni.

Walimwokota na kumlea kwa kumfanya mtoto wao, lakini akaja akawa ni adui wa itikadi yao na desturi yao. Akaingiza huzuni nyoyoni mwao na mwisho wa ufalme wao ukawa mikononi mwake.

Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa, wapotevu katika vitendo vyao vyote; hasa kuua maelefu ya vijana ili kujiepusha na Musa, lakini ikawa wao wanamwepusha Musa na mauti ili aje awamalize. Katika kamusi ya Kitabu kitakatifu[4] , imeelezwa kuwa maisha ya Musa katika nyumba ya Firauni hayakujulikana kwa ufafanuzi na kwamba wanahistoria wametofautiana kuhusu wakati wake alioishi. Wengine wakasema ni wakati wa Firauni Amenophis (Amenhotep II) (1411 – 1436 Bc), wengine wakasema ni Ramesses II (1223 – 1290 Bc). Pia kuna waliosema ni wakati wa Mernptsh ( 1211 – 1223 Bc).

Akasema mke wa Firaun: Ni kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuue! Huenda akatufaa au tumfanye kuwa mtoto wetu. Wala wao hawakutambua.

Kuburudika macho ni furaha. Mke wa Firauni ni Asiya bint Muzahim. Mwenyezi Mungu (s.w.t) amemsifu pale aliposema:

وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١١﴾

“Na Mwenyezi Mungu amewapiga mfano walioamini – mke wa Firauni, aliposema: “Mola wangu! Nijengee kwako nyumba Peponi na uniokoe na Firauni na vitendo vyake na uniokoe na watu madhalimu.” (66:11).

Na katika Hadith imesemwa kuwa wanawake bora ni wane: Maryam binti Imran, Asiya binti Muzahim, Khadija bint Khuwaylid na Fatima bint Muhammad. Firauni alipomwangalia mtoto alishtuka na kusema, imekuaje huyu mtoto wa ki Hebrew amepona kuchinjwa? Majasusi hawakumuona au wamenificha?

Mkewe akamtuliza na akamfanya ampende mtoto ili awe kiburudisho cha macho yao, lakini akawa ni kero ya macho yao na huzuni ya nyoyo zao.

Moyo wa mamake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kudhihirisha, lau tusingeliuimarisha moyo wake ili awe miongoni mwa waumini.

Alimtupa mtoto wake baharini akiwa na matumaini ya kuukotwa na ambaye atamwepusha na Firauni. Mara kadari ikamtoa baharini hadi nyumbani kwa Firauni!

Alipopata habari kuwa ameanguka mikononi mwa mchinjaji, alijua mtoto wake amekwisha.

Akafazaika sana na akajisahau na ahadi aliyoahidiwa na Mungu kuwa atamrudisha kwake; akawa karibu adhihirishe fazaa yake kwa kutamka jina la kipenzi chake, lakini Mwenyezi Mungu akampa utuvu, akaufanya thabiti moyo wake ili awe miongoni mwa wanaoamini ahadi yake. Kwa hiyo akawa na subira na akatulia.

Akamwambia dadake (Musa), mfuatie na uchunguze habari yake.

Akaenda na akamkuta kwa Firauni.

Basi akawa anamwangalia kiupande upande na wao hawatambui.

Wengine wamefasiri alimwangalia kwa mbali.

Maana ni kuwa alimwangalia kama vile hataki wala hamkusudii yeye, huku watu wa Firauni hawajui lengo lake au kuwa yeye ni dada wa mtoto waliyemuokota ufukweni.

Na tukamharamishia wanyonyeshaji tangu mwanzo.

Firauni alimsikiliza mkewe, akamwacha mtoto baada ya Mwenyezi Mungu kutia mahaba moyoni mwake na akaamrisha atafutwe mnyonyeshaji atakayemlea na kumtunza.

Wakaletwa wanyonyeshaji kutoka huku na huko, kila mmoja anapendelea akubali matiti yake ili apate hadhi mbele ya Firauni. Lakini mtoto aliwakataa wote.

Akasema (dadake): Je, niwaonyeshe watu wa nyumba watakaowalelea na watakuwa wema kwake.

Dadake Musa alipoona kuduwaa kwa watu wa Firauni kuhusu mtoto alijitokeza kuwaelekeza atakayekubali matiti yake na kumshughulikia bila ya kuzembea. Umetangulia mfano wake katika Juz. 16 (20:40).

Basi tukamrudisha kwa mama yake ili yaburudike macho yake.

Vile vile umetangulia mfano wake katika Juzuu hiyo hiyo.

Na ajue kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli.

Yaani mamake Musa ajue kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kurudishiwa mwanawe na kuwa miongoni mwa mitume, ni kweli.

Lakini watu wengi hawajui, mipangilio yake Mwenyezi Mungu Mtukufu na undani wa hekima yake.

4

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٤﴾

14. Na alipofikilia kukomaa kwake na akastawi, tulimpa hukmu na elimu. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.

وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ قَالَ هَـٰذَا مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ عَدُوٌّ مُّضِلٌّ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

15. Na akaingia mjini wakati wenyeji wake wako kwenye mghafala. Akakuta humo watu wawili wanapigana – huyu ni katika kundi lake na huyu ni katika adui zake. Yule aliye katika kundi lake alimtaka msaada dhidi ya yule aliye katika adui zake. Musa akampiga, akammaliza. Akasema: Hiki ni kitendo cha shetani; hakika yeye ni adui mpotezaji dhahiri.

قَالَ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي فَغَفَرَ لَهُ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿١٦﴾

16. Akasema: Mola wangu! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu, basi nisamehe. Akamsamehe; hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

قَالَ رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِّلْمُجْرِمِينَ ﴿١٧﴾

17. Akasema: Mola wangu! Kwa ulivyonineemesha, sitakuwa msaidizi wa wakosefu.

فَأَصْبَحَ فِي الْمَدِينَةِ خَائِفًا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا الَّذِي اسْتَنصَرَهُ بِالْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُ قَالَ لَهُ مُوسَىٰ إِنَّكَ لَغَوِيٌّ مُّبِينٌ ﴿١٨﴾

18. Akapambaukia mjini akiwa na hofu na hadhari, mara yule aliyemtaka msaada jana anampigia kelele. Musa akamwambia: Hakika wewe ni mpotevu dhahiri.

فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَن يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَّهُمَا قَالَ يَا مُوسَىٰ أَتُرِيدُ أَن تَقْتُلَنِي كَمَا قَتَلْتَ نَفْسًا بِالْأَمْسِ إِن تُرِيدُ إِلَّا أَن تَكُونَ جَبَّارًا فِي الْأَرْضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ مِنَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٩﴾

19. Basi Musa alipotaka kumkamata kwa nguvu, yule aliye adui yao akasema: Ewe Musa! Unataka kuniua, kama ulivyomuua mtu jana? Hutaki ila kuwa jabari katika ardhi, wala hutaki kuwa miongoni mwa wema.

ALIPOFIKIA KUKOMAA

Aya 14 – 19

MAANA

Na alipofikilia kukomaa kwake na akastawi, tulimpa hukmu na elimu. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa watendao mema.

Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 12 (12:22). Kule imekuja kwa wasifu wa Yusuf na hapa ni wa Musa.

Na akaingia mjini wakati wenyeji wake wako kwenye mghafala. Akakuta humo watu wawili wanapigana – huyu ni katika kundi lake na huyu ni katika adui zake. Yule aliye katika kundi lake alimtaka msaada dhidi ya yule aliye katika adui zake. Musa akampiga, akam- maliza.

Makusudio ya mji hapa ni mji wa Misri.

Siku moja Musa aliingia mitaani bila ya kujulikana na yeyote. Akawaona watu wawili wanagombana na kupigana – mmoja ni Mkibti katika wafuasi wa Firauni na mwingine ni Mwisrail katika jamaa za Musa. Kwa ujumla Wakibti walikuwa wakiwakandamiza waisrail na wakiwahisabu ni watumishi na watumwa wao.

Basi yule Mwisrail akamtaka msaada Musa. Musa naye akampiga ngumi au fimbo kwa kukusudia kumtia adabu na kukinga dhulma, si kwa kukusudia kuua na yule akaanguka ni maiti. Huku kunaitwa kuua kimakosa.

Akasema: Hiki ni kitendo cha shetani; hakika yeye ni adui mpotezaji dhahiri.

Anakusudia kile kitendo cha kugombana wale wawili sio pigo alilopiga Musa. Maana ni kuwa mapigano baina ya wawili, chanzo chake ni wasi-wasi wa shetani na hadaa yake ya kuingiza kwenye uasi na madhambi.

Akasema: Mola wangu! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu, basi nisamehe. Akamsamehe; hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye kurehemu.

Mitume na mawili wanajiona mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wapungufu. Hiyo ni katika aina ya kunyenyekea na dua. Hilo halifahamishi kuweko dhambi wala upungufu.

Kwa sababu anayemjua Mwenyezi Mungu kisawasawa huwa anaituhumu nafsi yake kuwa na upungufu wa kumtii Mwenyezi Mungu na kumwabudu.

Ndio maana humwomba msamaha wa dhambi. Wa kale walisema: “Uovu wa watu wema ni wema wa waovu.” Tazama tuliyoyaeleza kwa anuani ya ‘Toba na maumbile’ katika Juz. 4 (4:17-18).

Akasema: Mola wangu! Kwa ulivyonineemesha, sitakuwa msaidizi wa wakosefu.

Musa alimuomba msamaha Mola wake na akamwahidi kuwa atawapiga vita mataghuti na wakosefu; kama vile Firauni na jeshi lake na kumsaidia kila mumin.

Akapambaukia mjini akiwa na hofu na hadhari.

Musa alihofia kuuawa kwa sababu ya Mkibti na kutarajia shari kutoka kwa Firauni na watu wake.

Wakati akiwa katika hali hiyo, mara yule aliyemtaka msaada jana anampigia kelele. Anampigia kelele za kumtaka msaaada. Musa akamwambia: Hakika wewe ni mpotevu dhahiri.

Wewe kazi yako ni kugombana na Wakibti na kutusababishia matatizo. Hebu chunga upotevu wako!

Basi Musa alipotaka kumkamata kwa nguvu yule aliye adui yao,

Musa alitaka kumkamata Mkibti, kwa sababu wakibti ndio waliokuwa wakiwachokoza waisrail na kuwachukulia kuwa ni watumwa wao, kama tulivyoashiria mwanzo. Mkibti alidhani kuwa Musa anataka kumuua, kwa hiyo akasema:

Ewe Musa! Unataka kuniua, kama ulivyomuua mtu jana? Hutaki ila kuwa jabari katika ardhi, wala hutaki kuwa miongoni mwa wema.

Jana ulimuua mtu na leo unataka kuniua mimi, je wewe ni mbabe au mtu mwema? Hii inaashiria kwamba Musa alikuwa ni katika watu wema mwenye tabia nzuri na kwamba kuua hakuendani na tabia yake.

وَجَاءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢٠﴾

20. Na akaja mtu kutoka mwisho wa mji akaipiga mbio, akasema: Ewe Musa! Wakubwa wanapanga kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha.

فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢١﴾

21. Basi akatoka mjini akiwa na hofu na hadhari. Akasema: Mola wangu! Niokoe na watu madhalimu.

وَلَمَّا تَوَجَّهَ تِلْقَاءَ مَدْيَنَ قَالَ عَسَىٰ رَبِّي أَن يَهْدِيَنِي سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿٢٢﴾

22. Alipoelekea upande wa Madyana alisema: Asaa Mola wangu akaniongoza njia iliyo sawa.

وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ النَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ ﴿٢٣﴾

23. Alipoyafikia maji ya Madyana alikuta umati wa watu wakinywesha (wanyama wao), na akakuta nyuma yao wanawake wawili wanazuia (wanyama wao). Akasema: Mna nini? Wakasema: Hatunyweshi mpaka wamalize hao wachunga na baba yetu ni mzee sana.

فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ ﴿٢٤﴾

24. Basi akawanyweshea kisha akarudi kivulini na akasema: Mola wangu! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayoniteremshia.

فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥﴾

25. Basi mmoja wa wale wanawake wawili akamjia naye anatembea akiona haya. Akasema: Baba yangu anakuita akulipe ujira wa kutunyweshea.Basi alipomjia na kumsimulia visa vyake, alisema: Usiogope; umekwishaokoka na watu madhalimu.

قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ ﴿٢٦﴾

26. Akasema mmoja katika wale wanawake: Ewe baba! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumwajiri ni mwenye nguvu na mwaminifu.

قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾

27. Akasema: Mimi ninataka kukuoza mmoja wa mabinti zangu hawa wawili kwa kunifanyia ajira ya miaka minane na kama ukitimiza kumi hiyari yako. Mimi sitaki kukutaabisha. Inshaallah utanikuta miongoni mwa watu wema.

قَالَ ذَٰلِكَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ أَيَّمَا الْأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلَا عُدْوَانَ عَلَيَّ وَاللَّـهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ ﴿٢٨﴾

28. Akasema: Hayo yamekwishakuwa baina yangu na yako. Muda wowote kati ya miwili nitakoumaliza nisifanyiwe ubaya na Mwenyezi Mungu ni wakili juu ya haya tunayoyasema.

NJAMA

Aya 20 – 28

MAANA

Na akaja mtu kutoka mwisho wa mji akaipiga mbio, akasema: Ewe Musa! Wakubwa wanapanga kukuua. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanaokupa nasaha.

Firauni na wapambe wake walijua yaliyotokea baina ya Musa na Mkibti wa kwanza aliyemuua kimakosa na wa pili aliyemwambia unataka kuniua. Kwa hiyo wakashauriana kuhusu mambo ya Musa na kuazimia kumuua. Mmoja wa waumini alipojua hilo alikimbia kwa Musa kumpa habari na akamshauri awakimbie madhalimu.

Wafasiri wengi wamesema kuwa mumin huyu ni yule aliyeashiriwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu:

“Na akasema mumin aliyekuwa mmoja katika watu wa Firauni aliyeficha imani yake: Mtamuua mtu kwa kusema Mola wangu ni Mwenyezi Mungu naye amewajia na hoja zilizo wazi?” (40:28).

Basi akatoka mjini akiwa na hofu na hadhari. Akasema: Mola wangu! Niokoe na watu madhalimu.

Musa alitoka mjini bila ya maandalizi yoyote; hana chakula wala maji, au yeyote wa kuongozana naye. Alitoka kwa hadhari akihofia asionekane na chinjachinja wa Firauni. Zaidi ya hayo alikuwa hajui anakwenda wapi? Basi akamkimbilia Mola wake, akamwachia Yeye mambo yake na akamwomba kuongoka na kuokoka na Firauni na watu wake.

Alipoelekea upande wa Madyana alisema: Asaa Mola wangu akaniongoza njia iliyo sawa.

Musa alitembea bila ya kujua anakwenda wapi, lakini ana yakini kuwa Mola wake atamwongoza njia iliyo sawa ambayo itampelekea kuokoka na kufaulu. Mwenyezi Mungu (s.w.t) akamshika mkono na kumwelekeza Madyana, mji wa Shua’yb, ambao baina yake na Misri pana masafa ya mwendo wa siku nane katika jangwa pana sana.

Basi Musa akakata mbuga kwa tawfiki ya Mwenyezi Mungu. Alikuwa akila mimea ya ardhini. Jana alikuwa ikulu ya Firauni akistarehe. Mimea ya ardhi na hofu ni bora mara elfu kwa wenye ikhlasi kuliko starehe pamoja na dhulma; kama alivyosema Imam Husein(a.s) : “Wallahi! Sioni mauti ila ni wema; na sioni kuishi pamoja na madhalimu ila ni uovu.”

Alipoyafikia maji ya Madayana alikuta umati wa watu wakinywesha (wanyama wao) na akakuta nyuma yao wanawake wawili wanazuia (wanyama wao). Akasema: Mna nini? Wakasema: Hatunyweshi mpaka wamalize hao wachunga na baba yetu ni mzee sana.

Mwendo wa Musa uliishia kwenye kisima. Akakuta kundi la watu waki-wanywesha maji wanyama wao na akawaona wanawake wawili pembeni wakiwa na kondoo wao wanataka kunywa maji, lakini wao wanawazuia.

Musa akashtuliwa na hali hii, akawauliza, kwa nini mnawazuia nao wana kiu? Wakasema sisi ni wanawake dhaifu, hatuwezi kusukumana na wanaume. Tunangoja mpaka wamalize ndio nasi tupate nafasi, na baba yetu ni mzee sana, hawezi kuja kuchota maji. Nafsi ya Musa ikataharaki kidini na kiubinadamu, akawasaidia.

Hakuna ajabu kwa Musa kuwasaidia wanawake dhaifu; wala si ajabu kwa Shua’yb na mabinti zake kuishi kwa jasho lao.

Hii ndiyo sera ya mitume na makhalifa wao wenye takua, tangu zamani na baadaye. Bali ajabu ni kuwa roho hii ya Qur’an haina athari yoyote katika nafsi zetu sisi tunaodai kumjua Mwenyezi Mungu, Kitabu chake, na sera ya mitume wake. Ajabu ya maajabu ni kwamba tunashindana katika kuitafuta dunia na mapambo yake.

Basi akawanyweshea, kisha akarudi kivulini na akasema: Mola wangu! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayoniteremshia.

Musa aliwapatia maji wanyama wa wasichana wawili, kisha akaenda chini ya mti kupata kivuli, akiwa na uchovu na njaa. Akamwomba Mwenyezi Mungu fadhila na ukarimu wake. Wala hakung’angania sana au kuomba zaidi, kwa sababu alichokitaka ni kuziba tumbo tu.

Kama angelikuwa anaomba akhera angeling’ang’ania. Katika Nahjul balagha imeelezwa: “Wallahi hakumuomba isipokuwa mkate wa kula tu. Rangi ya kijani ya majani ilikuwa ikionekana kwenye ngozi ya tumbo lake kwa wembamba wake na kutengana na nyama yake.”

Basi mmoja wa wale wanawake wawili akamjia naye anatembea akiona haya. Akasema: Baba yangu anakuita akulipe ujira wa kutunyweshea.

Wale wasichana wawili walirudi kwa baba yao na wakamwelezea yaliyotokea. Basi akamwambia mmoja wao: Nenda kamwite tuje tumlipe hisani yake. Basi akaenda msichana akiwa amegubikwa na haya, ustahi na heshima na kumweleza alivyosema baba yake.

Basi alipomjia na kumsimulia visa vyake, alisema: Usiogope; umekwishaokoka na watu madhalimu.

Musa alikubali mwito, na mzee akamkaribisha na kumshukuru kwa kitendo chake. Musa alipotulia na kumwamini yule mzee, alimsimulia yaliyompitia kwa Firauni na watu wake. Yule mzee akamwambia usihofu, umefika. Hapa kwetu ni ngome ya amani, haifikiwi na Firauni wala mfano wake katika madhalimu.

Wafasiri wametofautiana kuhusu mzee huyu ni nani? Wengi wao wamesema ni Shuaib na wengine wakasema siye. Hakuna ya kutegemewa kwa hawa wala wale. Nasi hatuna haja na tofauti hizi madam hazina uhusiano wowote na imani wala maisha.

Sisi tumechagua jina la Shua’yb kiasi cha kumwelezea huyo mzee tu, sio kuwa tumekubaliana na jina hilo na pia kwa kuwa ni jina liloenea kwa wengi; kama lilivoenea baina ya wanafunzi na ulamaa wa Najaf.

Akasema mmoja katika wale wanawake ambaye alimwita kwa baba yake: Ewe baba! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumwajiri ni mwenye nguvu na mwaminifu.

Tunasema aliyesema ni yule aliyemwita kutokana na kauli yake ‘mwenye nguvu’ pale alipowasaidia kuchota maji na ‘mwaminifu’ pale alipokuwa na staha wakati wakielekea kwa baba yake.

Akasema: Mimi ninataka kukuoza mmoja wa mabinti zangu hawa wawili kwa kunifanyia ajira ya miaka minane na kama ukitimiza kumi hiyari yako. Mimi sitaki kukutaabisha. Inshaallah utanikuta miongoni mwa watu wema.

Musa mkimbizi, fukara asiyekuwa na chochote, ambaye kwa siku kadhaa, ameishi kwa kula mimea ya ardhi; mpaka akamuomba Mola wake tonge ya kumwezesha kuishi, leo anahiyarishwa kuchagua mke amtakaye. Bila shaka hapa kuna siri ya utu wa Musa na utukufu wake uliomgusa mzee na mabinti zake. Vile vile katika masimulizi yake na sera yake kwa Firauni na watu wake.

Mzee alitambua, kutokana na akili yake safi, kwamba mtu huyu atakuwa na athari ya mbali. Kwa sababu matendo ya mtu aghlabu yanatoka kwenye chimbuko moja. Kwa hiyo mzee, hapa alifuzu kutokana na ukwe huu. Kuna faida gani kubwa zaidi ya kuwa mkwe wa Mtume na mwenye takua.

SHARIA YA KIISLAMU IMEFUTA SHARIA ZOTE

Mafaqihi wamezungumza mengi kuhusiana na Aya hii, wakaitolea dalili kuwa walii wa mwanamke ndiye atakayetamka tamko la ndoa. Lakini ilivyo ni kuwa inafaa kwa mwanamume au mwanamke mwenyewe kutam- ka. Hilo linafahamika kimsingi bila ya kuhitaji nukuu. Shafii na Imamiya wamesema kuwa ndoa haifungiki isipokuwa kwa tamko la ziwaj na nikah. Hii ni baada ya kuiunganisha Aya hii, yenye tamko la nikah, na ile yenye tamko la ziwaj.

فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا ﴿٣٧﴾

“Basi Zaid alipokwisha haja naye tulikuoza wewe” (33:37).

Malik na Hambal wakasema pia ndoa inafungika kwa neno hiba, kutokana na Aya yenye neno hiba:

وَامْرَأَةً مُّؤْمِنَةً إِن وَهَبَتْ نَفْسَهَا لِلنَّبِيِّ ﴿٥٠﴾

“Na mwanamke mumin akijitoa mwenyewe kwa Nabii.” (33:50).

Hanafi naye akasema kuwa ndoa inafungika kwa neno lolote linalofahamisha kutaka kuoana.

Mafaqihi wengi wamesema kuwa muda wa kuchunga wanyama miaka minane au kumi haukuwa mahari au sehemu yake. Bali mahari yalikuwa mbali; na kwamba kauli ya mzee: “kunifanyia ajira” maana yake ni kuwa ukichunga wanyama kwangu kwa ajira, nitakuoza mmoja wa mabinti zangu kwa mahari; sawa na kusema: ‘Ukifanya hivi nami nitafanya hivyo.’

Haya ndio maana sahihi ya Aya. Kwa vyovyote iwavyo, hakuna hoja yoyote, katika Aya hii kwa, waliyoyasema mafaqihi. Kwa sababu hizo ni simulizi za sharia zilizotangulia. Nasi tuna uhakika kwamba sharia ya Kiisalmu imefuta sharia zote zilizotangulia, wala haifai kutumia hukumu yoyote miongoni mwa hukumu hizo zilizotangulia, isipokuwa kwa dalili maalum au ya kiujmla kutoka katika Kitab au Sunna. Na hapo itakuwa ni kukitumia Kitab au Sunna, sio kuitumia sharia hiyo.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ﴿٣٨﴾

“Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote.” Juz. 7 (6:38).

Na kauli yake:

وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ ﴿٨٩﴾

Na tumekuteremshia Kitabu hiki kubainisha kila kitu.” Juz.14: (16:89),

Yaani kila kitu katika misingi ya kiislamu na sharia yake.

Mtume(s.a.w.w) naye anasema: “Hakuna kitu kitakachowakurubisha nyinyi Peponi isipokuwa nimewaamrisha, na hakuna kitu kitakachowaweka mbali na moto isipokuwa nimewakataza.”

Akasema: Hayo yamekwishakuwa baina yangu na yako. Muda wowote kati ya miwili nitakoumaliza nisifanyiwe ubaya na Mwenyezi Mungu ni wakili juu ya haya tunayoyasema.

Haya ni maneno ya Musa. Muda wa kwanza ni Hijja nane na wa pili ni Hijja kumi. Maana ni kuwa Musa alimwambia mzee, nimekubali na kuridhia kuoa na kuchunga wanyama.

Mimi nitakuwa na hiyari ya kumaliza nane au kumi. Muda wowote nitakaoumaliza basi usiwe na hoja kwangu na Mwenyezi Mungu ndiye shahidi juu ya haya uliyojiwajibishia na niliyojiwajibishia.

Kuna Hadith isemayo kuwa Musa alichagua muda wa kumi. Wafasiri wengi wanasema kuwa yeye alimchagua mdogo naye ndiye aliyesema, baba yangu anakuita. Na pia kumwambia baba yake, hakika yeye ana nguvu na ni mwaminifu.

5

6

7

8

9