MAARIFA YA QUR'AN KWA QUR'AN.

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

MAARIFA YA QUR'AN KWA QUR'AN.

SOMO LA KWANZA.

IMANI JUU YA ULAZIMA WA KUIFAHAMU QUR'AN TUKUFU.

Kwa hakika kufanya tadabbur na kuizingatia Qur'an Tukufu hutegemea kuifahafu Qur'an,kwa ibara nyingine ni kwamba:Huwezi kufanya kuizingatia Qur'an Tukufu ikiwa huifahamu.Kwa sababu utafutaji wa kila kitu hutegemea au huegemea katika kukifikiria kwanza kitu kile na kufikiria faida zake pamoja na kuwa na imani na kitu hicho.Hivyo kabla ya kuitadabbur Qur'an hii na kuizingatia ni lazima kwanza kuifahamu au ni lazima kwanza uhakiak wa Qur'an.

Na itakuwa wazi kwa kila mtu kwamba kitakachogundulika baada ya kufanya tadabbur na mazingatio katika Qur'an Tukufu ni ujinga (yaani kushindwa) wa kutofahamu uhakika wake,ispokuwa nikwamba ujinga una aina zake,kuna wakati ujinga unakuwa ni ule wa kupandana! Yaani ujinga juu ya ujinga. Mfano:Mtu hajui kama hajui! Na aina hii ya ujinga ni mbaya zaidi ukilinganisha na aina zingine za ujinga.Na aina nyingine ya pili ya ujinga ni ile inayoambatana na (uangalifu) wa mtu (yaani yuko attention) kuwa hajui.Huyu ni mjinga lakini anajua kuwa ni mjinga.Katika sura hii itakuwa ni rahisi sana kujaribu kutafuta jinsi ya kutatua tatizo la ujinga huu kwa kurejea kwa A'alimu na Mjuzi wa Qur'an Tukufu.

MAARIFA YA QUR'AN KWA QUR'AN.

Marhala ya kwanza ya kuifahamu Qur'an Tukufu ni kufahamu uhakika wake kupitia Aya zake,na marhala ya pili ni kuifahamu Qur'an kupitia kurejea kwa Ahlul-bayt (a.s).Hivyo mada yetu itakuwa katika ile marhala ya kwanza,kwamba ni lazima tuifahamu Qur'an Tukufu kwa kupitia Qur'an au kwa ibara nyingine tunaweza kusema kwamba:Ni lazima tuifahamu Qur'an kupitia Qur'an kasha tutazame,je Qur'an hii inatujulisha chochote kunako Ahlul-bayt (a.s) au la?

Imepokewa katika riwaya mbali mbali kama ilivyopokelewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) amesema:
*من لم يعرف الحق من القران لم يتنكب الفتن*
Kwa maana kwamba yeyote yule ambaye hataifahamu haki kutoka katika Qur'an basi maarifa yake yake hayatamfaa chochote pindi itakapotokea fitina.

MAANA YA LAFDHI:AL-QUR'AN AL-KARIMU.

Kwa hakika maana ya neon (Al-qur'an) ni maneno na herufi zilizohifadhiwa kati ya jalada au magamba mawili, na huitwa kitabu cha Mwenyeezi Mungu na maneno ya Mwenyeezi Mungu (s.w).Na tofauti iliyopo baina ya majina haya mawili ni kwamba:Anuani ya (maneno) huthibitika kwa kutazama yanakotokea maneno haya(yaani kutokea kwa mzungumzaji),ndio maana tunasema aya hizi ni maneno ya Mwenyeezi Mungu (s.w),kwa maana kwamba yametoka kwake (s.w).Na ile anuani ya pili,yaani (Kitabu cha Mwenyeezi Mungu) Qur'an huitwa kwa jina hili yaani (Kitabu) kwa kutazama sehemu ambayo imeathiriwa na Qur'an hii(kwa maana kitendo cha kutulia katika sehemu hii).Hivyo neno ni neno kwa itibari lilipotokea,na kitabu ni kitabu kwa itibari ya ile sehemu kilipo. Hivyo anuani hizi mbili kidhati ni kitu kimoja lakini zinatofautina katika mitazamo na itibari,ni kama vile tunavyosema (Kukifanya kitu kuwepo) na (Kuwepo) yaani (Al-iyjaad) na (Wujuud),ni maneno mawili ambayo kidhati ni kitu kimoja lakini kimtazamo na kwa itibari,yanatofautiana. Hivyo kila neno ni kitabu na kila kitabu ni neon.

KUTHIBITI KWA MARHALA NYINGINE YA QUR'AN TUKUFU.

Je,maneno haya yaliyohidhiwa baina ya majarida au magamba mawili ni jambo lingine? Kwa maana kwamba:Je,nyuma ya dhahiri hii kuna uhakika (katika batini) kwa kina zaidi,ili tuweze kufanya juhudi nyuma yake kwa ajili ya kutafuta uhaka huo au la? Zimekuja riwaya mbali mbali kutoka kwa Zainul-A'bidina Ali bin Husein (a.s) kama hii ifuatayo kwamba amesema (a.s):
کتاب الله عزوجلِّ على أربعة أشياء:على العبادة والإشارة واللطائف والحقائق.فالعبادة للعوام-والإشارة للخواص- واللطائف للأولياء والحقائق للأمبياء.

"Kitabu cha Mwenyeezi Mungu kipo katika vitu vinne: katika ibara,na ishara,na upole (huruma) na uhakika,na ibara ni kwa ajili ya watu wote,na ishara ni kwajili ya watu khaasi,na upole ni kwa ajili ya Mawalii (wa Mwenyeezi Mungu) na uhakika ni kwa ajili ya Mitume"

Ibara huitwa neno kwa itibari kwamba kupitia neno maana huweza kujulikana'ma ishara huitwa neno kwa itibari kwamba ishara hujulisha kile ambacho kinaambatana na maana, na upole huitwa neno kwa itibari kwamba ni wenye kumfanya mtu kujua na kutambua maana.Na hakika huitwa neno kwa itibari kwamba hujulisha maana ambayo ni (ya batini) na hii ndio maana ya kauli ya Mtume (s.a.w) aliposema:
*ما أنز الله عز وجلَّ آية إلا ولها ظاهر وباطن وکل حرف حد وکل حد مطلع*

"Hakuteremsha Mwenyeezi Mungu (s.w) aya ispokuwa ina dhahiri na batini, na kila herufi ina maana (yake) na kila maana niyenye kujulikana" Hivyo riwaya hizi mbili na nyinginezo zinajulisha kwamba Qur'an Tukufu ina marhala.Hivyo sio kwamba Quir'an ni maneno tu yaliyohifadhiwa baina ya magamba mawili,bali maneno haya ni marhala miongoni mwa marhala za Qur'an tukufu,bali pia ni kwamba Qur'an ina marhala ambazo hawafiki katika marhala hizo ispokuwa wale watu wa kipekee wenye sifa za kipekee miongoni mwa watu, nao si wengine bali wale aliowataja (s.w) aliposema:

*إنه لقرآن کريم*في کتاب مکنون*لا ?مسُّه إلا المطهرور*

"Hakika ni Qur'an Tukufu (yenye heshima)*Iliyotolewa katika hicho kitabu kilichohofadhiwa kweli kweli(katika lawhul-Mahfudh) *Hawaifahamu ispokuwa (wale tu ) waliotwaharishwa" Tazama:suuratul-waaqia:aya ya (77-79). Nasi tunataka kuashiria katika uhakika huu wa Qur'an tukufu ambao ndio daraja ya juu kabisa katika Ulimwengu na daraja ya juu kabisa katika Mbingu na ni bora zaidi iliyotoka kwa Mola wa viumbe wote.Allah (s.w) anataja (Neema) katika Suuratur-rahmaan kasha baada ya kutaja kila neema anasema:

*فبأي آلاء ربِّکم ما تکذبان*

"Basi nyinyi viumbe namna mbili (yaani Binadamu na Majini) ipi katika neema za Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)?" Kisha hakuacha kutaja katika sura hii moto wa jahaanam kwa nao ni lutfu (upole kwa mja) kwani humzuia mja kufanya maasi,anasema:
*يرسل عليکما شواظ من نار ٍونحاسٌ فلا تنتصران*فبأي آلاء ربِّکما تکذبان*

"Mtaletewa muwako wa moto na shaba (iliyoyeyushwa); wala nyinyi hamtaweza kujilinda navyo." Lakini kitu cha kwanza kabisa ilichoanza nacho sura hii tukufu ni ni kauli ya Allah (s.w):

*الرَّحمان*علم القرآنَ*خلق الإنسان* علمه البيان*

"Mwenyeezi Mungu) Mwingi wa rehema*Amefundisha Qur'an*Amemuumba Binadamu*Akamfundisha kunena…." Hivyo neema ya kwanza kabisa aliyoneemesha Mwenyeezi Mungu (s.w) ni Qur'an Tukufu,na kutanguliza kitu si tu hivi hivi pasina malengo bali ni dalili tosha inayoonesha kutilia umuhimu kitu hicho,hivyo kutangulia kwa Neema ya Qur'an ni dalili tosha juu ya umuhimu mkubwa wa Qur'an tukufu.Kwani neema hii ya Qur'an tukufu imekuwepo hata kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu nah ii ni kulingana na utaratibu wa aya hizi zilivyo,kwani (s.w) amesema:

*علَّم القرآن*خلق الإنسان*

"Amefundisha Qur'an*Amemuumba binadamu*…" Hivyo ni kwa jinsi Qur'an tukufu inakuwa neema (hata) kwa yule aliyekuwepo kabla ya Nabii wetu Muhammad (s.a.w)? Tukifahamu uhakika wa Qur'an tutakuwa tumefahamu ni kwajinsi gani Qur'an inakuwa neema kwa wanadamu wote (na si kwa wanadamu tu) bali pia hata kwa viumbe wote.

MWISHO