MAANA YA UIMAMU KILUGHA NA KIISTILAHI

BISMILLAH AR-RAHMANI AR-RAHIIM.

KWA JINS LS MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEM.

MAANA YA UIMAMU KILUGHA NA KIISTILAHI

Neno Uimam, linatumika katika maana mbili: Maana ya kwanza: Ni maana ya Kilugha.
UIMAMU KIISTILAHI
Maana ya pili:Ni maana khaasi na ambayo ni Istilahi ya Kisheria, au kwa ibara nyingine tunaweza kusema kwamba Imam kiistilah ni yule aliyeteuliwa na Mwenyeezi Mungu (s.w) kuwa Imam na Imam Kilugha ni yule yeyote ambaye kuteuliwa kwake hakunasibishwi kwa Mwenyeezi Mungu (s.w). Hivyo mtu yeyote na kitu chochote ambacho ni kiongozi au ambacho kinafuatwa,kilugha huitwa Imam,sawa sawa awe Mtu,au Kitabu au kitu chochote kile.

Katika Qur'an Tukufu maana hii ya Imam kilugha pia imetumika.Kwa mantiki hiyo,Watu na hata Kitabu,vitaitwa au vitatumia (yaani vitu hivi viwili) jina la Imam.Na watu,ni neno linalo jumuisha watu wazuri na watu wabaya,katika kundi la watu wazuri ambao kuteuliwa kwao kunanasibishwa katika upande wa Mwenyeezi Mungu (s.w) au ukitaka sema:(walioteuliwa na Mwenyeezi Mungu s.w),kwa mtazamo wa kilugha watu hao wataitwa (Maimam) au watatumia jina la Imam.Na vile vile kundi la upande wa pili,yaani watu wabaya (au hata kama si wabaya) ili mradi tu ikithibitika kuwa wamefanikiwa kujipatia uongozi,lakini kuchaguliwa kwao au uteuzi wa watu hao si kutoka kwa Mwenyeezi Mungu (s.w) bali kutoka kwa asiyekuwa yeye (s.w),kwa mtazamo wa kilugha pia watu hao wataitwa Maimam au watatumia jina la Imam.

Kwa hiyo,hapa ndugu msomaji bila shaka unaweza kutofautisha kati ya Imam kwa maana ya Kiistilah na Imam kwa maana ya kilugha.Ambapo si kila mtu huitwa au ana haki ya kuitwa Imam kwa mtazamo wa Kiistilah na Kisheria,bali yule tu ambaye kuteuliwa kwake ni kutoka kwa Mwenyeezi Mungu (s.w) na si asiyekuwa yeye (s.w) basi huyo ndiye Imam kwa maana ya Kiistilah na ndiye Imam kisheria.

Ama jina la Imam kwa mtazamo wa kilugha,ataitwa mtu yeyote yule (au kitu chochote kila kama vile kitabu) mwenye majukumu ya uongozi kwa kuchaguliwa na jamii au mwenyewe tu kaamua kujipa majuku ya uongozi (kwa kujipachika mwenyewe katika uongozi),sawa sawa awe muovu kupindukia ataitwa Imam,awe mzuri kupindukia ataitwa Imam,awe amechaguliwa na kuteuliwa na Mwenyeezi Mungu (s.w),ataitwa Imam,awe hakuteuliwa na wala kuchaguliwa na Mwenyeezi Mungu (s.w) vile vile ataitwa Imam,kiwe kitabu kinachoongoza katika haki ,kitaitwa Imam,kiwe kitabu kinachoongoza katika batili kitaitwa Imam,n.k.

Na hapa tunagundua kuwa Imam kwa mtazamo wa kilugha ni neno ambalo ni pana zaidi kiasi kwamba linaweza kutumika kwa watu wazuri na wabaya na hata kwa kituchochote kile ambacho si katika jamii ya watu.Ama neno Imam kwa mtazamo wa kisheria na kiistilah,ni neno lenye mipaka katika matumizi,neno lenye masharti au sifa,na endapo mtu itaonekana katimiza masharti hayo au sifa hizo,basi atakuwa na haki ya kuitwa Imam kwa mtazamo wa kiistilah na kisheria.

Ili kuelewa zaidi nikinenacho hapa,lazima turudi katika Qura'an Tukufu ili tuone ni jinsi gani Mtu anaweza kuwa kiongozi kwa kuteuliwa na Mwenyeezi Mungu (s.w). Mwenyeezi Mungu (s.w) amesema katika suuratul-Ambiyaa aya ya 73 kwamba:

(وجعلناهم أئمة ?هدون بأمرنا وأوح?نا إل?هم فعل الخ?رات....)

"Na tukawafanya kuwa Maimam wanaoongoza kwa amri yetu,na tukawapelekea wahyi kuzifanya kheri…." Aya hii inaweka wazi kabisa kwamba aliyewafanya (yaani hao wanaozungumziwa kwenye Aya Tukufu) kuwa Maimam si asiyekuwa Mwenyeezi Mungu (s.w) bali ni Mwenyeezi Mungu (s.w).Hii inaonyesha kwamba kuna Maimam ambao huteuliwa moja kwa moja na Allah (s.w) na kuna maimam wasio teuliwa na Allah (s.w).

Tunaposema mfano: Imam Ali (a.s) tunamaanisha kuwa nikiongozi aliyeteuliwa na kuchaguliwa na Mwenyeezi Mungu (s.w) kupitia Mjumbe wake Muhammad (s.a.w),kwa hiyo tunakuwa tumelitumia neno Imam kwa maana ya kiistilah,ama tunaposema Imam Shafi au Imam Maalik bin Hambari au Imam Khomaini ,hatumaanishi kuwa ni Maimam kwa mtazamo wa kiistilah bali ni Maimam kwa mtazamo wa kilugha.
MWISHO
Katika sehemu ijayo tutaendelea na ufafanuzi kuhusu Imam,ambapo tutazungumzia kunako mashartina sifa anazotakiwa kuwa nazo Imam katika maana zote mbili kilugha na kihistilah. Ndugu msomaji!Jitahidi kufuatili sehemu ya pili ijayo Inshaallah ili upate kujua ni masharti yapi na ni sifa zipi yatakiwa kuwa nazo kiongozi wa watu.