MAPENDEKEZO 12 KWA AJILI YA UMOJA

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

MAPENDEKEZO 12 KWA AJILI YA UMOJA

Pamoja na kuwepo uhasama wa maadui kuhusiana na msimamo huu na hasa sehemu inayohusiana na umoja wa Waislamu, ambao mteteaji wake mkuu alikuwa ni marehemu Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu), lakini pamoja na hayo fikra hii imeendelea kuwa imara, ya kimantiki, inayoweza kutekelezwa na muhimu katika kulinda umoja wa Kiislamu.

Kuhusiana na suala hilo tunapasa kufanya kila liwezekanalo ili kuepuka mitazamo inayopindukia mipaka na kukabiliana vilivyo na wale wanaoeneza fikra kama hizo potofu, wawe wako miongoni mwetu au katika upande wa pili. Watu ambao huwa hawajali maisha ya Mashia wala Masuni na kutosita katika kulipua mabomu yanayoleta hasara na maafa makubwa au kujilipua katika kufikia malengo yao haramu wanapaswa kung'olewa kutoka katika jamii ya Waislamu ili kuiepusha na madhara yao.

Kwa kutumia uzoefu wa kihistoria na uchunguzi wa kisiasa, tumejaaliwa kutaja hapa baadhi ya misingi ambayo iwapo itazingatiwa na kutekelezwa ipaswavyo inaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuleta umoja na mfungamano katika jamii ya Kiislamu. Hata kama huenda misingi hii si mipya lakini huenda njia iliyotumika katika uwasilishaji wake ikatofautiana sana na njia zilizotumika huko nyuma na hivyo kumfanya msomaji kuizingatia.

1- Mwanzo, Serikali za Kiislamu zinapaswa kulazimishwa kukubali kwamba umoja wa Kiislamu ni msingi muhimu usioweza kupuuzwa, ambao sera na siasa zote za serikali zinapaswa kubuniwa juu yake ili kuweza kufikia malengo na maenedeleo yanayotarajiwa. Mojawapo ya matokeo muhimu ya ukweli huu ni kwamba sera zote zinapaswa kubuniwa ili kuleta umoja miongoni mwa Waislamu.. Mojawapo ya sera zinazopaswa kupewa umuhimu hapa ni ile inayoweza kusaidia katika kung'oa mizizi ya ushabiki usio na muelekeo na ukabila, jambo ambalo linaweza kusaidia sana katika umoja wa kisiasa na mfungamano katika ulimwengu wa Kiislamu. Tunatahadharisha hapa kwamba kuihusisha sana serikali katika jambo hilo kuliko kiwango cha kawaida huenda kukazusha matatizo na kukabiliwa na radiamali mbaya kutoka kwa watu na viongozi wa jadi wasiopendelea mageuzi.
Tunapaswa kutafuta njia inayofaa kuhusiana na suala hili. Hii ni kwa sababu hatuna chaguo jingine isipokuwa kuendelea na njia ya umoja kwa lengo la kudhamini maslahi ya baadaye ya ulimwengu wa Kiislamu. Jambo ambalo tumekuwa tukilishuhudia hadi sasa katika nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi ni kuwa zimekuwa zikitoa nara tupu tu za kuwepo umoja wa Kiislamu bila ya kuchukua hatua yoyote ya kivitendo kwa madhumuni ya kufikia lengo hilo. Kwa hakika nara hizo zimekuwa zikienda kinyume kabisa na siasa zao za kuleta katika eneo watu ambao wamekuwa wakieneza uadui na chuki dhidi ya Waislamu. Bila shaka njia pekee ya kukabiliana na hali hiyo ni kwa jumuiya za Kiislamu kupasisha sheria ambazo zitazuia vitendo na siasa hizo hatari na pia kuweka wazi njia za kusailiwa na hata kuadhibiwa serikali za nchi kama hizo ziazohatarisha maslahi ya ulimwengu wa Kiislamu. Kuhusiashwa kwa serikali za Kiislamu katika jambo hili muhimu kunaweza kuvunja njama za maadui walio na nia mbaya ya kutaka kukuza na kueneza chuki na miongoni mwa Waislamu ili kuwatenganisha katika misingi ya kimadhehebuna kikabila na hatimaye kuweza kufikia malengo yao haramu katika nchi za Kiislamu.
2- Hatua muhimu: Kuwasilisha utafiti na uchunguzi wa kielimu kwa misingi ya ukweli wa kihistoria tu na mbali kabisa na ushawishi pamoja na mielekeo ya kimadhehebu na kikabila. Kwa kutilia maananni kwamba imani za kishabiki zinazozunguka ukweli wa mambo zinaweza kupunguza athari za ukweli huo, ni wazi kwamba utafiti na uchunguzi uliosimamam katika misingi ya uhakika mbali na mielekeo ya kishabiki unaweza kuwa na nafasi muhimu katika kubainisha ukweli wa mambo mengi.
Ni wazi kwamba watu wasio na lmielekeo ya kishabiki ndio tu wanapaswa kuruhusiwa kuandika vitabu na majarida kuhusiana na masuala yanayohusu ulimwengu wa Kiilsmau. Watu kama hao wanahitajika kuwa wakweli na waaminifu katika uandishi wao wa vitabu na kufanya juhudi maradufu ili kutoudhi wala kudhuru imani za Waislamu wa upande wa pili. Bila shaka utafiti kama huo wa kielimu ambao hauna aina yoyote ya uchochezi unaweza kuwa na nafasi muhimu katika kubadilisha mawazo ya wasomi ambao nao kwa upande wao wanaweza kuwa na athari kubwa katika kubadili mitazamo ya Waislamu.
Katika miaka ya hivi karibuni, wasomi na wanafikra wa Kiislamu wameandika makala, vitabu na majarida mengi kuhusiana na suala hili, ambayo hata kama baadhi yao yamekuwa na athari mbaya lakini mengi yamekuwa na athari nzuri katika kubadilisha mitazamo ya kizazi kipya. Ni matarajio yetu kwamba kwa kupita wakati, athari ya vitabu na majarida hayo itahisika kwa mapana zaidi katika nchi za Kiislamu. 3- Inapaswa kuzingati wa kwamba ushabiki wa kimadhehebu na ghasia hazitekelezwi na waliowengi bali na waliowachache wanaoishi miongoni mwa wengi ambao mara nyingine huwalazimisha kutekeleza vitendo hivyo vya aibuvya umwagaji damu ya watu wasio na hatia.
Sababu ya jambo hilo inatokana na ukweli kwamba kila wakati kundi la waliowachache linapohisi kuwa linakabiliwa na hatari kutoka upande wowote ule, hupata moyo wa kushikilia na hata kung'ang'ania zaidi misimamo na imani yake. Kwa hivyo, iwapo matatizo yanayohusiana na makundi ya waliowachache hayatatatuliwa, matatizo ambayo huyafanya makundi hayo yaendelee kung'ang'ania imani zao ili kulinda utambulisho na maslahi yao, ni wazi kwamba mamtizo hayp yaliyopo kati yao na makundi mengine hayawezi kutatuliwa kirahisi. Makundi ya wachache yanapaswa kuwekwa katika hali ambayo hatahisi kuwa hayana tofauti na makundi mengine na kwamba hayakabiliwa na hatari kutoka upande wowote ule, na bila saka lengo hilo linaweza kufikiwa kwa kupewa nmakundi8 hayo haki zao zaote.
4- Kiongozi wa kila kundi la kimadhehebu wanapaswa kufanya juhudi maradufu ili kuhakikisha kwamba umoja wa Kiislamu unapatikana. Lengo hilo linaweza kufikiwa katika hatua mbili: Kwanzi, ni kuwaandaa watu kifikra ni hilo ni jukumu la wasomi katika jamii. Pili, kutumia ushauri wa kielimu, jambo ambalo tabaka la tatu la wasomi au hata la pili huwa halina uwezo wa kulitekeleza. Ili mpango huu uweze kuzaa matunda ya kuridhisha unapaswa kutangazwa na kiongozi wa juu zaidi wa kidini ambaye anaheshimika na kutegemewa na watu wa kawaida na pia wanazuoni wengine. Utolewaji wa maoni na mitazamo na wengine katika uwanja huo huenda ukasaidia hali ya mambo lakini kwa kawaida kuna uwezekano mkubwa wa hali hiyo kuzusha shaka miongoni mwa baadhi ya watu. Tunawajibika kila mara kuwashauri na kuwaweka mbele viongozi wa madhehbu muhimu katika kuongoza juhudi za kuleta umoja na mfungamano katka jamii za Kiislamu.
Ni muhimu kutaja nukta hii hapa kwamba juhudi za kuleta umoja miongoni mwa Waislamu hazipaswi kuachiwa wanazuoni na wasomi peke yao. Hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi yao huwa hawana ushawishi mkubwa miongoni mwa umma kutokana na kuwa huenda baadhi yao wakawa wanatuhumiwa kuwa wana mielekeo ya Kimagharibi au hata wanapinga suala la kutawala dini katika masuala ya kijamii na kisiasa ya mwanadamu. Tabaka la jamii linalopaswa kuongoza juhudi za kuleta umoja na mfungamano miongoni mwa Wailsmu ni lile linalowaongoza kidini. Kwa kawaida watu hutegemea na kumwamini zaidi imam wao anayewaongoza katika swala kuliko wanavyomwamini muhadhiri wa chuo kikuu. Hata kama hali ya mambo imebadilika kidogo kuhusiana na jambo hilo lakini ni wazi kwamba ukweli utaendelea kuwa kwamba watu huamini na kuwategemea viongozi wao wakuu wa dini ambao hubainisha mambo wazi na bila ya kusita kuliko kupoteza wakati wao katika kuwategemea watu wanaotumia istilahi zisizofahamika vyema kuhusiana na mambo ya kielimu na kifalsafa.
5- Hatua nyingine muhimu katika kuleta umoja kati ya Waislamu ni kubuni nara za umoja ambazo zinapasa kuigwa na kuenezwa na vyombo vya habari na usambazaji. Vitua na taasisi zote za sanaa zinapaswa kutayarishwa vyema ili kufikia lengo hilo. Tunatoa mfano mmoja hapa ili kubainisha zaidi suala hili: Miaka hamsini iliyopita kulikuwepo na jarida moja lililokuwa likijulikana kwa jina la Muslimim, ambalo lilikuwa likichapishwa mjini Tehran. Arida hilo lilikuwa likijadili na kuchambua kwa usawa na bila ya ubaguzi wa kimadhehebu wala kikabila, masuala yaliyokuwa yakihusiana na nchi zote za ulimwengu wa Kiislamu. Lilichambua masuala ya Waislamu katika nchi zote zilizo na jamii za Kiislamu zikiwemo za India, Indonesia na Afrika. Jambo la kuvutia ni kuwa kwenye jalada lake, kulichapishwa picha ndogondogo za misikiti mikuu ya nchi za Kiislamu. Picha hizo daima zilikuwa zikichapishwa kwenye jalada hilo na kuwavutia watu wengi katika nchi za Kiislamu. Ni wazi kwamba kuchambuliwa kwa mambo yanayohusiana na ustaarabu wa Kiislamu na kusisitiza umuhimu wa kurudishwa utukufu na adhama ya Uislamu ambayo ililetwa na umoja wa Waislamu katika karne za nne na tano Hijiria, ni jambo linaloweza kuyaandaa vyema mataifa ya Kiislamu na kuyafanya yapiganie izza, hadhi na utukufu wao wa zamani.
6- Mojawapo ya hatua zinazoweza kuchukuliwa katika kuandaa umma kifikra ni kwa watafiti, waandishi na vyombo vya habari na mawasiliano kuwatahadharisha wananchi kuhusiana na hatari na uharibifu uliofanywa na chuki pamoja na utengano wa kimadhehebu katika historia. Wanapasa kusisitiza mara kwa mara kwamba mbali na kuharibu sehemu nzuri ya nishati na uwezo wa umma wa Kiislamu chuki hizo za kimadhehebu hazina matunda wala matokeo mengine. Wanapasa kufanya utafiti, kuandika na kutangaza ripoti na habari nyingi kuhusiana na suala hilo muhimu kadiri ya uwezo wao.
Kwa ibara nyingine ni kuwa kukaririwakaririwa kwa matukio machungu yaliyopita katika historian a yaliyotokana na chuki za kimadhehebu na kikabila kunaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kuwafanya watu wasirejee makosa hayo yaliyofanywa na wenzao waliotangulia katika historia. Hata hivyo ni muhimu kuashiria nukta hii hapa kwamba kuna baadhi ya makundi ambayo yamekiuwa yakiitumia nukta hiyo nyeti katika kueneza fitina na mgawanyika katika umma wa Kiislamu. Kila mara huashiria mambo yaliyopita na kuyalaumu makundi mengine ya Kiislamu na hivyo kuandaa njia ya uchochezi dhidi ya makundi ya upande wa pili.
7- Pengo la kielimu kati ya makundi mawili ya Kiislamu hufanya kuwa ngumu juhudi za kuyakutanisha na kwa kawaida huwa hayaheshimiani. Kila kundi hujaribu kuliondoa jingine ili lipate kutawala na kuleta umoja kwa njia hiyo. Njia ya Qur'ani ya kutatua tatizo hili imesimama katika msingi wa tafauti za mataifa kuyafanya yajuane. Msingi huo ndio unapaswa kuchukuliwa kuwa kigezo cha mataifa kufahamiana na kujuana. Kwa ibara nyingine ni kuwa jitihada zinapaswa kufanyika ili kuyafanya makundi na mataifa yanayotofautiana kijamii na kikabila kuweza kufahamiana zaidi. Nukta chanya za kila upande zinapaswa kuzingatiwa na kudhihirishwa zaidi ili kupunguza mvutano wa pande hizo na kujaribu kuondoa katika vichwa vya fikra hii potofu kwamba kila upande unaopinga fikra za upande wa pili ni kafiri usiopaswa kupewa umuhimu. Jitihada hizo zinaweza kuimarishwa kwa kutumia njia za sanaa kama vile filamu za sinema, televisheni au usanii mwingine wowote.
8- Historia ya ustaarabu wa Kiislamu inathibitisha wazi kwamba umoja wa Kiislamu hufikiwa mara moja kwa kusisitizwa masuala ya kiirfani na kimaanawi. Wakati ulimwengu wa Kiislamu uliopoonyesha mvuto maalumu kuhusiana na masuala hayo, ulifanikiwa kuleta vizazi na mataifa mbalimbali ya Kiislamu chini ya kivuli cha umoja wa Kiislamu na kuweza kufanikiwa kuyafanya kuwa umma mmoja ambapo yote yalifahamiana na kushirikiana kwa njai za kuvutia kabisa. Irfani, zikiondolewa nukta hasi ambazo mara nyingi huzushwa katika elimu hiyo na baadhi ya watu, iliweza na ingali inaweza kuleta umoja unaotamaniwa na Waislamu kote ulimwenguni. Mafanikio hayo yanatokana na uwezo mkubwa wa elimu hoyo katika kusisimua nukta za kimaanawi alizoumbwa nazo mwanadamu. Nukta hizo zinafanana katika wanadamu wote.
Iwapo marekebisho yatafanyika katika elimu hiyo na kuondolewa nukta zote hasi huku nukta chanya za umoja miongoni mwa Waislamu zikisisitizwa na kutiliwa mkazo kama dini inavyofundihsa, bila shaka tunaweza kuwa na matumaini makubwa ya kugfikiwa umoja na mfungamano miongoni mwa Waislamu wote duiniani. Huenda hiyo ikawa ni nukta ya kuzingatiwa katika kukubali Waislamu wa Misri miito ya kuwepo Umoja miongoni mwa umma wa Kiislamu na kukataliwa kwa jambo hilo na Wasialmu wa Saudi Arabia ambapo Mawahabi wan chi hiyo wanapinga vikali elimu ya falsafa na irfani.
9- Katika dunia ya leo, suala la utandawazi ni jambo muhimu lililoenea katika kila pembe ya dunia. Jambo linalokusudiwa hpa nu kuufanya ulimwengu mzima kuishi na kuwa na tabia ya aina moja katika usambazaji wa thamani za kijamii na kiutu. Ni wazi kuwa tukio hili litatupata na sisi. Katika kukabiliana nalo tunatakiwa kubuni mapendekezo ya Kiislamu yatakayotuwezesha kupambana na utandawazi huo hatari unaotokomeza maadili ya kiutu na Kiislamu. Kwa ibaranyingine ni kuwa kutokana na ukweli kwamba hivi sasa ulimwengiu mzima unazungumzia utandawazi, tunapasa kupasa kutumia fursa iliyopoa kwa lengo la kuufanya utandawazi huo ukubaliane na misingi ya mafundisho ya Kiislamu au kwa maneno mengine tuweze kuwaunganisha Wasialmu. Bila shaka ili kufikia lengo hilo tunatalkiwa tueneze thamani muhimu za Kiislamu zinazokubaliwa na madhehebu yote katika kila pembe ya ulimwengu wa Kiislamu na ikiwezekana kuyafanya madhehebu yote yazikubali thamani hizo. Baada ya hapo tunahitajika kuhubiri na kutangaza utandawazi wa Kiislamu katika nchi za Kiislamu. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumefanikiwa kuepuka madhara ya utandawazi hatari wa nchi za Magharibi kwa uapnde mmoja na kuweza kuleta muungano na umoja wa Kiislamu miongoni mwamataifa ya Kiislamu kwa upande wa pili.
10- Kufichua na kuzuia kutekelezwa kwa vitendo hatari vmakundi yenye misimamo ya kupindukia pamoja na kulaani vitendo hivyo visivyo vya kibinadamu yanapasa kuwa majukumuyetu muhimu. Katika hatua ya kwanza vitendo hivyo vya kihayawani ambavyo hutekelezwa na makundi hayo dhidi ya wasio wasio na hatia kwa kisingizio cha kutetea na kulinda makundi ya kidini vinastahili kulaaniwa kwa maneno. Hatuapasi kutoa mwanya wa makundi haya kutekeleza vitendo hivyo vya kishetani na kigaidi dhidi ya watu wasio na hatia. Kwa kusema hivi tuna maana ya kwamba, watu wanaowajibika na wasiowajibika wote hawapasi kutoa matamshi ambayo huenda yakachukuliwa na magaidi na wafuasi wao kuwa ni idhini isiyo ya moja kwa moja ya kuhalalisha vitendo kama hivyo vya kinyama dhidi ya wenzao. Serikali zinawajibika kuchukua hatua za haraka na za kisheria katika kukabiliana na vitendo vya makundi kama hayo yanayoharibu jina zuri la Uislamu, la sivyo, huenda magaidi hao wakachukulia kimya cha serikali kuwa na maana ya kuridhia na kuunga mkono vitendo vyao hivyo viovu.
Aina hiyo ya uzembe wa serikali unaweza kuzusha tatizo jingine hatari, nalo ni kuwa, kundi lililokosewa na kufanyiwa uhalifu na serikali kutochukua hatua yoyote ya kukabiliana na kitendo hicho, huenda likajichukulia sheria mikononi na kuamua kulipiza kisasi dhidi ya kundi halifu. Hapo ndipo mambo hutoka katika udhibiti wa serikali na vitendo vya ghasia kuenea katika kila upande, na hivyo kufanya suala la kutafuta nani aliyekuwa mwanzilishi wa ghasia hizo kuwa humu. Inafaa kuashiria hapa kwamba vitendo vya kinyama na kikatili wanavyofanyiwa Mashia wa Iraq na makundi ya kigaidi kwa visingizo mbalimbali vya kimadhehebu na kisiasa au ugaidi unaofanywa dhidi ya Mashia nchini Pakistan ni sehemu ndogo tu ya jinai kubwa zinazopaswa kusimamishwa kwa kila njia na serikali za Kiislamu.
Hii ni kwa sababu iwapo vitendo kama hivyo vitaruhusiwa kuendelea huenda vikasababisha jinai kubwa katika siku zijazo. Wakati huohuo iwapo vitendo hivyo vitaruhusiwa kuendelea vinaweza pia kuchochea na kuwafanya watu wengine wenye misimamo ya kupindukia katika madhehebu ya Shia kulipiza kisasi na kutokuwa tayari hata kidogo kusikiliza nasaha za kuleta umoja miongoni mwa Waislamu. Watu kama hao wanaweza kuanza kushuku na kuwahoji walio na misimamo ya wastani ni kwa nini wanaeneza nara za umoja katika hali ya kutekelezwa jinai kama hizo za kinyama dhidi yao? Ni wazi kwamba makundi kama hayo ya upinzani yanapatikana katika kila sehemu na jamii na kila kitendo cha ugaidi kinachofanywa na kundi moja hukabiliwa na kitendo kingine kama hicho kutoka upande wa pili. Ni wazi kwamba iwapo vitendo vya kigaidi vitaruhusiwa kuendelea na kukabiliwa na kimya cha serikali husika, vinaweza kuenea na kuzikumba jamii na nchi nyinginezo jirani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kama mazingira ya jamii fulani hayatruhusu ulipizaji kisasi dhidi ya ugaidi, watu walio na nia ya kulipiza kisasi watahamia kwingineko na kutekelezea huko vitendo vyao vya kisasi.
11- Nukta nyingine ni kwamba wanazuoni na wasomi wanaofanya juhudi kubwa kwa lengo la kuleta umoja na utengemano miongoni mwa Waislamu wanawajibika kufanya kila wawezalo ili kujiepusha na matamshi yanayoweza kuzusha fitina na uchochezi miongoni mwa wafuasi wao. Wapasa kutambua kwamba wanatembea katika njia nyembamba na iliyo na ncha kali. Wanawajibika kuzingatia na kuyapa umuhimu masuala yanayozusha utata miongoni mwa madhehebu tofauti. Iwapo wataamaua kueneza fikra ambazo zinagongana na thamani pamoja na misingi inayokubaliwa na Waislamu wote kwa kisingizio cha kufanya marekebisho na upatanishi, ni wazi kuwa juhudi hizo haziwe3zi kuchukuliwa kuwa ni za kuleta umoja katika jamii ya Waislamu.
Kuna baadhi ya mambo ambayo hata kama ni muhimu katika dhati yao lakini hayapaswi kusemwa au kutendwa na watu wanaofuatilia juhudi za kuleta umoja na mfungamano miongoni mwa Waislamu. Wasomi wapendeleao marekebisho ndio wanaotakiwa kubeba mzigo huo mzito wa kuleta umoja miongoni mwa Waislamu na kuchukua jukumu lolote linalotokana na suala hilo. Wakati huohuo watetezi wa umoja wa Kiislamu wa Waislamu wanapasa kuchukua tahadhari maradufu wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ili wasije wakatamka maneneo ambayo yanaweza kuwatenganisha Waislamu na kuwafanya wafuasi wao waanze kushuku nia zao halisi.
12- Katika juhudi za kuleta umoja miongoni mwa Waislamu matukio ya kihistoria yanayokubalika na pande mbili hasimu yanapaswa kutajwa na kutolewa dalili ili kujaribu kuleta umoja kati yao. Kwa mfano, maisha ya Mtume Muhammad (SAW) yanapaswa kuchunguzwa na kuchambuliwa kwa uangalifu mkubwa katika jamii za Kiislamu zikiwemo za Kishia. Kwa kufanya hivyo, kuna mambo ya pamoja ambayo yanaweza kujadiliwa na pande zote na hivyo kuepuka mambo yenye utata ambayo huzusha ghasia na hata umwagaji damu miongoni mwa Waislamu. Ni wazi kuwa iwapo tunaweza kuleta umoja wa Kiislamu kwa kuzingatia na kusisitiza urithi wa pamoja wa Kiislamu, hilo litakuwa ni jambo la kuvutia litakalowaridhisha Waislamu wote. Hii ni kwa sababu kwa kufany hivyo tutakuwa tumefanikiwa kulinda dini yetu na wakati huohuo kuepuka sharui ya maadui na athari mbaya inayoletwa na utengano wa kimadhehebu.

MWISHO