Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

SABABU YA KUCHUKIWA UISLAMU NI UJAHILI

0 Voti 00.0 / 5

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

SABABU YA KUCHUKIWA UISLAMU NI UJAHILI

Rita De Milo, mhadhiri wa masuala ya utafiti wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Rome, mji mkuu wa Italia amesema kuwa ujahili wa wasiokuwa Waislamu na raia wengi wa nchi za Magharibi kuhusiana na Uislamu ni sababu kuu ya kuenea chuki yao dhidi ya Uislamu na hivyo kuwapelekea kuiogopa dini hii.

Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharqul Ausat, Rida De Milo amesema kuwa Uislamu umebainisha vyema na kwa kina masuala mbalimbali yanayomuhusu mwanadamu, likiwemo suala la haki za binadamu na hasa haki za mwanamke.

Amesisitiza kuwa hakuna taasisi wala dini nyingine ilivyobainisha vyema na kutetea haki za mwanamke kama ulivyofanya Uislamu. Amesema sheria za Kiislamu ni nguzo muhimu inayopasa kupewa umuhimu mkubwa katika sheria za kimataifa kwa kutilia maananni kwamba zinabainisha vyema umuhimu wa kulindwa haki za binadamu bila ya kujali dini, rangi, ukabila wala utaifa wao.

De Milo ameendelea kusema kuwa kuenea kwa dini tukufu ya Kiislamu katika nchi za Magharibi ni dalili ya wazi kuwa mafundisho ya dini hii yanawahusu wanadamu wote. Amesema kuwa hata kama kuna hujuma ya makusudi inayoenezwa na makundi fulani dhidi ya dini hii lakini ni wazi kuwa hujuma hiyo haitadumu kwa muda mrefu kwa sababu Waislamu nao wameanzisha mbinu za kujitetea na kulinda thamani za dini yao dhidi ya hujuma hiyo.

Mhadhiri huyo mtaalamu wa masuala ya Kiislamu amesema kuwa baada ya kutalii Uislamu kwa muda mrefu amefikia uamuzi huu kwamba Uislamu ni dini muhimu na kubwa sana ambayo inadhulumiwa pamoja na wafuasia wake katika nchi za Magharibi.

Mtafiti huyo wa masuala ya Kiislamu wa Italia amesisitiza kwamba ameandika vitabu ambavyo vinabainisha vyema mafundisho ya dini ya Kiislamu ambayo yanashajiisha wafuasi wake kuwa na maadili bora pamoja na kuishi na wenzao wa dini tofauti kwa amani na ushirikiano.

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini