ARDHI ILIYOSAHAULIKA

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

ARDHI ILIYOSAHAULIKA
UTANGULIZI
Ardhi hii iliyosahaulika ilikuwa na migongano mingi sana baina ya staarabu tofauti, baina ya Uislamu na Ukafiri, baina ya haki na batili na baina ya at-Tawheed na shirki. Migongano hii ilikuwa ya kutumia silaha au baridi kwa kuelezea, kujadiliana na kulingania. Mgomgano wa mwisho ni ule ulioletwa na maandishi ya Mkataba wa Sykes - Picot ulioandikwa 1916 baina ya Uingereza na Ufaransa.Ardhi hii inatajwa ana lakini haipo kwenye ramani na imesahaulika sana na hususan sisi Waislamu. Allah, Mtume Wake na historia imetupatia sifa tofauti ya ardhi hii. Sifa hizi zimefanya kila taifa kuigombea.

ITIKADI YA MUISLAMU JUU YA ARDHI HII
1. Ardhi Tukufu:
Allah (s.w.t.) amesema: Enyi watu wangu! Ingieni katika hiyo ardhi iliyotakaswa ambayo Allah amekuandikieni. Wala msirudi nyuma, msije mkaw wnye kukhasirika.(5:21)

Je, hii aya imewapatia Mayahudi urithi wa moja kwa moja kwenye ardhi ya Palestina? Je, huu ni urithi wa majukumu au wa dam? Allah amesema yafuatayo kuhusu Nabii Ibrahim (a.s.): Na pindi Mola wako alipomfanyia Nabii Ibrahim mtihani kwa amri nyingi; naye akazitimiza. Akamwambia: "Hakika Mimi nitakufanya kiongozi wa watu". Ibrahim akasema: "Je, na katika kizazi changu pia?" Akasema: "Ndio lakini ahadi yangu haitawafikia madhalim (waovu).(2:124) Kuna dhulma gani kuliko a Ma-Israeli kuwafanyia ndugu zetu Palestina. Hususan angazia yaliyotokea kuanzia tarehe 29 Machi 2002 mpaka wakati wetu huu wa sasa. 2. Ardhi Iliyobarikiwa:

Ardhi hii imebarikiwa kiroho na kirutba. Ni jambo hili ndilo lililowafanya watu na staarabu tofauti kuigombania. Agano la Kale inatuhadithia ya kuwa ardhi hii ilibubujika asali na maziwa.(Hesabu, 13:27) Na katika kitabu cha Hesabu Sura ya 13 inatueleza kuwa majasusi wa Nabii Musa (a.s.) walipata humo matunda ya makudhumani, tini na zaituni ambayo yalikuwa makubwa na kila tunda kubebwa na watu wawili. Allah (s.w.t.) anasema: …mpaka Msikiti wa mbali (wa Aqsa) ambao tumeubariki na tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake…(17:1). Lakini ardhi yote ya Palestina imebarikiwa. Allah amesema: Na tulimuokoa yeye na Lut tukawapeleka katika ardhi tuliyoibarikia kwa ajili ya walimwengu.(21:71) 3. Ardhi ya Mitume:

Katika ardhi hii Mitume tofauti ima walihamia au walizaliwa na kuishi utotoni mwao au walifanya Da'wah na kuzikwa katika sehemu hii au walizuru japokuwa kwa muda mfupi. Miongoni mwao ni Manabii kama Ibrahim, Isma'eel, Ishaaq, Ya'qub, Lut, Daud, Sulayman, Zakariya, Yahya, 'Isa na Muhammad. 4. Ardhi ya Wahyi:

Wahyi ndio uliokuwa na mpaka sasa unajenga ustaarabu na utamaduni za watu tofauti. Miongoni mwa Vitabu vilivyoteremshwa kutoka kwa Allah katika ardhi hii ni Suhuf za Nabii Ibrahim, Zaburi ya Nabii Daud, Injil ya Nabii 'Isa na pia baadhoi ya aya katika Suratuz Zukhruf katika Qur'an. 5. Ardhi ya Isra Wal Meeraj:

Hii ni safari ya usiku aliyopelekwa Mtume Muhammad (s.a.w.). Isra ni safari ya kutoka Msikiti Mtukufu wa Makkah mpaka Baytil Muqaddas. Meeraj ni ngazi ya kutoka Baytil Muqaddas mpaka wingu wa saba. Natija mzuri kabisa ya safari hii ni kufaridhiwa Ummah huu salah TANO, mchana na usiku. Salah ya kwanza ya jamaa ilifanyika katika Msikiti Mtukufu wa Aqsa ambapo Mtume (s.a.w.) aliwasalisha Mitume wote (a.s.). hii inatukumbusha kila tunaposali mahusiano yetu ya karibu sana na ardhi hii. 6. Ardhi ya Msikiti wa Aqsa:

Msikiti huu ulikuwa kibla cha kwanza kwa Waislamu. Kwa miezi 16 au 18 baada ya Mtume (s.a.w.) na Masahaba zake kuhamia Madinah waloikuwa wakielekeza nyuso zao kwa upande wa Baytil Maqdis mpaka Allah (s.w.t.) alipokibadilisha kwa kuteremsha aya ya 144 na 150 ya Suratil Baqarah. Msikiti huu ni watatu kwa utukufu baada ya Msikiti Mtukufu wa Makkah na msikiti wa Mtume Madinah. Salah moja katika Msikiti huu ina dhawabu mara 500 kuliko Misikiti mengine ila Msikiti wa Makkah na Madinah.(at-Tabarani)

Kwa hivyo kila Muislamu ulimwenguni ana hamu sana ya kwenda kuuzuru na kusali ndani yake. Lakini je, tunaujua Msikiti huu ni upi? Wengi wetu tunaujua ule Msikiti ambao unachapishwa katika magazeti na majarida, kuonyeshwa katika televisheni, kuwepo kwenye makalenda, picha zinazotundikwa majumbani, n.k. Huu Msikiti ninaouzungumzia una sifa ya kipekee na unajulikana kwa kuwa na Qubba rangi ya njano au ya dhahabu. Lakini ndugu zangu wapendwa, Masjidul Aqsa ni eneo lote ambalo lipo katika kuta nne ikiwemo Masjid Qubbatis Sakhraa (Msikiti wa Qubba ya Jabali au Dome of the Rock), Masjid Aqsa (huu ulijengwa baada ya ule wa Qubbatus Sakhraa), Masjid Marwani, miti ambayo imo ndani, shule na kuta zenyewe. Sehemu hii yote ni tukufu na ndio Msikiti wa Aqsa bila ya tofauti yeyote baina ya wanavyuoni wote wa Kiislamu. 7. Ardhi ya Masahaba:

Masahaba watukufu waliipigania ardhi hii na kuweza baada ya taufiki ya Allah (s.w.t.) kuitawala. Masahaba 200 walioshiriki katika Vita vya Badr walikuwa katika msitari wa mbele wakuuteka mji wa al-Quds. Takribani makaburi 18,000 ya Masahaba yanapatikana katika ardhi hii.

8. Ardhi ya Jihadi, Ribati na Vita vya Mwisho:
Vita vitagavyopiganwa baina ya waislamu upande mmoja na Mayahudi upande mwengine. Mtume (s.a.w.) anatueleza: "Kiyama hakitafika mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi. Mayahudi watakuwa wanauliwa na kuwafanya wajifiche nyuma ya miti na mawe ambayo itasema: 'Ewe Muislamu! Ewe mja wa Allah! Njoo nyuma yangu yupo Yahudi umuue…."(al-Bukhari na Muslim)

HITIMISHO
Ndugu zetu wanauliwa kila saa na dakika. Je, tufanyeje ili kuwasaidia ndugu zetu katika ardhi hii yetu? 1. Tumjuwe ALLAH vilivyo na tuongeze IMANI yetu kwa kufuata mafundisho ya UISLAMU na kuacha makatazo yake. Tujipinde na IBADAH.
2. Tuanze kususia bidhaa za Israeli na Marekani ambaye ni rafiki yake wa chanda na pete na wa hali na mali. Kwa mfano tusinunue soda za kampuni ya coca-cola na pepsi cola, rangi ya kiwi na bidhaa nyenginezo. Kampuni za coca-cola na pepsi zinamsaidia vilivyo Israeli.

3. Tusiwasahau ndugu zetu katika Du'aa hata baada ya kujiombea nafsi zetu hususan tunapokuwa katika sijdah, tunaposafiri, tunapofunga, tunapoinuka usiku kwa Salah ya Tahajjud, n.k.
KUMBUKENI NI JIHADI PEKEE INAYOWEZA KUIKOMBOA ARDHI HII.
MWISHO