DALILI ZA KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

DALILI ZA KIAKILI ZA KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU 2

Katika makala zilizopita tulielezea njia na dalili za kumfahamu mwenyeezi mungu, na tukayathibitisha hayo kutokana na akili na Aya za qur-ani,katika makala hii basi tutaendelea kuzielezea dalili hizo, na vile vile tutazithibitisha kutokana na Qur-ani.

Miongoni mwa dalili hizo ni hizi zifuztzzo:-

DALILI ZA MATAMANIO YA KIMOYO (STIMULUS SINCERE)

Mbali ya kuwa mwanaadau ana dalili (matamanio) za kiakili ambazo zinathibitika kwa kutolewa dalili na kutafakari vile vile ana matamanio ya nafsi ambayo yamo ndani ya nafsi ya mwanaadamu, matamanio hayo yanampelekea mwanaadamu kupata majibu kutokana na na matendo ya wengine.

 Na tuzingatie riwaya hii iliyonukuliwa na Imam Baqiri (a.s).

Imam Baqiri (a.s) amesema:-

“Siku moja usiku Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa kwa mke wake bibi Aisha, bibi Aisha akamuuliza suala Hadharati Muhammad ya kuwa kwa nini unafanya jitihada ya kufanya ibada? Hali ya kwamba Mwenyeenzi Mungu Mtukufu amekusamehe madhambi yako ya nyuma na ya masiku ynayokuja? Mtume akamjibu kwa kusema:-

الا اکون عبدا شکورا[1]

“ Hivi hainiwajibikii mimi kuwa ni kiumbe mwenye kumshukuru Mola wake?”

Katika sehemu hii natuzingatie mifano inayotokana na matamanio ya nafsi ambayo inamuongoza mwanaadamu katika njia njema.

KUKUBALIWA DUA
Kukubaliwa dua wakati mwanaadamu anapokuwa kakata tamaa katika mafanikio, na hakuna mtu yoyote anayeweza kumsaidia kutatua matatizo aliyonayo na wakati huu basi mwanaadamu humuomba Mwenyeenzi Mungu na kumtaka msaada ili amsaidie na afanikiwe kwa yale anayoyahitajia,wakati kama huo basi mwaanadamu humkumbuka Mola wake na kuamini ya kuwa hakuna yoyote mwengine anayeweza kumsaidia kutokana na matatizo aliyonayo. Hii inaweza kuwa sababu ya kumuongoza mja huyo na kuwa pamoja na Mola wake.

Qur-ani kariym inaelezea kwa kusema:-

اَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاء الاَرْضِ اَإِلَهٌ مَّعَ اللهِ قَلِيلاً مَّا تَذَكَّرُون[2]َ

Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia.

Maelezo kuhusiana na Aya

Zinatajwa baadhi ya sifa za Mwenyeezi Mungu, basi tumuachie Mwenyewe mwenyeezi Mungu aliyenazo khasa, siyo kuwapa walio mizimuni…kwani hao hawamiliki jambo katika haya.

MAELEZO KWA UFUPI (BRIEFLY).

Kuna dalili tatu ambazo zinamsaidia mwanaadamu kufikia katika njia njema, dalili hizo ni hizi zifuatazo:-

Dalili za kiakili, kinafsi, na dalili za matamanio (upendo).

Masuala.

1- Mwanaadamu mbali ya mapendeleo ya nafsi ambayo ni (nature), (فطری)ana matamanio na dalili gani nyengine zinazoweza kumuongoza katika njia njema?

2- Dalili (matamanio) za kiakili vipi zinaweza kumuongoza mwanaadamu katika njia njema?

3- Elezea vipi mwanaadamu kwa kukubali haki (na ukweli) inamsaidia yeye kuwa na matamanio ya kuelekea kwa Mola wake?

4- Kwa kuzingatia riwaya (hadithi) ya Imam Baqiri (a.s) ambayo tumeieleza hapo nyuma, (riwaya hiyo ni kuhusu hadharati Muhammad (s.a.w.w),elezea dalili ya matamanio ya nafsi.

TAHAKIKI (RESEARCH)

Andika aya tano zinazzoelezea umuhimu wa kutafakari na kufikiri, na baadae andika natija uliyoipata kutikana na aya hizo.

[1] Kafi, juzuu ya 2, mlango wa shukru

[2] Surat-Naml aya ya 62

MWISHO