KAULI YA MWENYEEZI MUNGU JUU YA MAKAFIRI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KAULI YA MWENYEEZI MUNGU JUU YA MAKAFIRI 1

MAKAFIRI WANAMKADHIBISHA NA KUMTUKANA MTUME (S.A.W.W)

Makafiri wakimwambia Mtume (s.a.w.w) :-

“Wewe si Mtume”, kama tulivyoona na tutavyoona katika Aya nyingi, basi anaambiwa Mtume asijali kukataliwa na wao maadam Mwenyeezi Mungu Mwenyewe Anamkiri kuwa ni Mtume Wake. Kwa kusema:-

قُلْ اَيُّ شَيْءٍ اَكْبَرُ شَهَادةً قُلِ اللهِ شَهِيدٌ بِيْنِى وَبَيْنَكُمْ وَاُوحِيَ إِلَيَّ هَذَا الْقُرْآنُ لاُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ اَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ اَنَّ مَعَ اللهِ آلِهَةً اُخْرَي قُل لاَّ اَشْهَدُ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِى بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ[1]

Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnao washirikisha.

Makafiri ijapokuwa wanaujua ukweli wa dini ya kiislamu – lakini wanaipinga tu na kuwazuilia watu kuifuata – wanajiangamiza wenyewe.

Wanajitia nguvu wenyewe katika kufanya mabaya – na wanawatia nguvu wengine – kwa kuwaambia:-

“Hakuna kufufuliwa wala kulipwa, natufanye tunayoyataka  tunavyopenda.”Mwenyeezi Mungu anawaambia watu hao:-

وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْاَوْنَ عَنْهُ وَإِن يُهْلِكُونَ إِلاَّ اَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ[2]

Nao huwazuia watu, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi ila nafsi zaotu, wala wao hawatambui. Na katika Aya nyengine anasema:-                           

وَلَوْ تَرَي إِذْ وُقِفُواْ عَلـٰي رَبِّهِمْ قَالَ اَلَيْسَ هَذَا بِالْحَقِّ قَالُواْ بَلَي وَرَبِّنَا قَالَ فَذُوقُواْ العَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُون قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُواْ بِلِقَاء اللهِ حَتَّي إِذَا جَاءتْهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُواْ يَا حَسْرَتَنَا عَلـٰي مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ يَحْمِلُونَ اَوْزَارَهُمْ عَلـٰي ظُهُورِهِمْ اَلاَ سَاء مَا يَزِرُونَ[3]

Na lau ungeli ona watavyo simamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, akawaambia: Je, si kweli haya? Na wao watasema: Kwani? Tunaapa kwa Mola Mlezi wetu ni kweli. Yeye atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyo kuwa mnakataa.

Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipo wajia Saa kwa ghafla, wakasema: Ole wetu kwa tuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Ni maovu hayo wanayo yabeba.

Maelezo kuhusiana na aya ya 30-31

Hapa yanatajwa baadhi ya yatakayowafika makafiri na waovu.

Mtume alikuwa ni binaadamu anayehisi upesi mema na mabaya, kwa hivi akihuzunika sana kuona watu hawafuati yale mazuri anayowaambia wala hawakubali kuwacha yale mabaya anayowakataza. Na akihuzunika kwa kule kukadhibishwa, na hali ya kuwa wanamjua kuwa si muongo. Basi Mwenyeezi Mungu ndiyo Anawaambia:-

“Hawa makafiri wanakujua kuwa wewe si muongo lakini hawayataki tu haya uliyokuja nayo ambayo yatawaondoshea mabaya yao waliyoyazowea”.“Mzoea ya kunyonga ya kuchinja hayawezi”.

Na anabainishiwa katika Aya ya 34 kuwa hayo yanayomfika yeye ndiyo yaliyowafika Mitume wengine.

وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ فَصَبَرُواْ عَلـٰي مَا كُذِّبُواْ وَاُوذُواْ حَتَّي اَتَاهُمْ نَصْرُنَا وَلاَ مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِ اللهِ وَلَقدْ جَاءكَ مِن نَّبَإِ الْمُرْسَلِينَ[4]

Na hakika walikanushwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa, mpaka ilipo wafikia nusura yetu. Na hapana wa kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu. Na bila ya shaka zimekujia baadhi ya khabari za Mitume hao.

[1] Surat Al-an-aam Aya ya 19

[2] Surat al-an-aam aya ya 26

[3] Surat al-an-aam Aya ya 30-31

[4] Surat Al-anaam Aya ya 34

MWISHO