FUNGAMANO KATIIKA QUR_ANI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI 

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

VIPENGELE VYA MIUJIZA YA QUR-ANI -1- (C)

D. FUNGAMANO KATIKA QUR-ANI  (MNASABA ULIOPO KATIKA AYA ZA QUR-ANI)

Tukiendelea na mada yetu kuhusiana na vipengele vya miujiza ya Qur-ani, katika makala zilizopita tulizungumzia baadhi nyanja za miujiza ya Qur-ani, katika makala hii tunazungumzia nyanja ya nne miongoni mwa vipengele vya miujiza ya Qur-ani.

Aya za Qur-ani ziko katika hali ya mparaganyiko, na zimeteremshwa kutokana na minasaba tofauti, lakini kutokana na uzingatiwaji uliozingatiwa na – wanaelimu – katika zama hizi – kuhusiana na yale yaliyomo katika kila sura, wamefikia natija ya kuwa kila sura ina hadafu (dhumuni) maalumu – miongoni mwa Aya za kila sura – na masuala ya muujiza wa Qur-ani ni katika nukta hii hii, katika zama hizi tulizonazo umoja huo wa maudhui yaliyo dhahiri katika kila sura unajulikana kwa jina la (umoja katika maudhui).

Ni lazima tukumbushie: Kwamba kuna baadhi ya watu, mbali nakutowa nadharia za kuwa kuna mnasaba baina ya Aya, vile vile wametowa nadaharia nyengine na kusema kuwa kuna mnasaba baina ya sura, na wamesema:-

“Katika utaratibu wa sura pia kuna mnasaba maalumu”. Hata baadhi yao wamekiuka mpaka na kusema kuwa muujiza wa Qur-ani pia uko katika utaratibu wa sura,[1]

Hivyo ni lazima tukumbushane na kuzingatia kuwa hakuna mnasaba wowote uliomo ndani ya sura, na utaratibu wa sura uliopo sasa ndani ya Qur-ani sio utaratibu uliopangwa kwa amri ya Mwenyeezi Mungu wala Mtume wake, bali utaratibu huo umepangwa na Masahaba baada ya kufariki Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwa kuzingatia baadhi ya minasaba, kwa mfano sura ndogo na sura kubwa, n.k .

Ndani ya Qur-ani kumetumika aina mbali mbali za Istiara (Istiara ni uwazimaji wa maneno na kuyatumia sehemu isiyokuwa yake), kinaya, majaz, tashbih, aina zote hizo zimezingatiwa na zile aina zilizozoeleka katika jamii ya watu Kiarabu, ama utumiwaji huo uliotumiwa katika Qur-ani ni wa makini sana, hata imesababisha kuwavutia wanaelimu wakubwa walio mahiri katika lugha ya kiarabu, wazungumzaji wengi walio mahiri katika lugha ya kiarabu wamekubali na kusema kuwa utumiwaji huo uliotumika katika Qur-ani ndiyo utumiwaji bora.

Ibni Athiyr ambaye ni mahiri mkubwa katika lugha ya kiarabu, akielezea kuhusu mifano iliyotolewa ndani ya Qur-ani, katika Suratul-Nabaa Aya ya 10 anasema:-

وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاساً[2]

Na tukaufanya usiku kama guo (mnalofunikwa).

Mfano huo uliotolewa ndani ya Qur-ani kwa kuushabihisha au kuufananiza usiku na nguo, ni kwa sababu ya giza hilo liliopo wakati wa usiku, kiasi ya kwamba watu hawawezi kuonana, na iwapo kunapotokea adui mtu anaweza kujificha katika giza hilo na kujihami na adui huyo, mfano huo uliotolewa wa kufananiza giza na nguo ni katika nukta ambayo inaonekana ndani ya Qur-ani tu na hakuna maneno sehemu nyengine iliyoonekana imetumia maneno kama hayo hata katika lugha ya kiarabu pia ni muhali kuonekana.

[1] rejea Tafsiri Nuwiyni, ukurasa wa 19-20

[2] Suratul-Nabaa Aya ya 10

MWISHO