MSUKUMO WA HEWA WENYE KUIHIFADHI ARDHI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

 B. MSUKUMO WA HEWA WENYE KUIHIFADHI ARDHI B

Katika makala iliyopita tulionesha mifano inayoashiria elimu, katika makala hii tunaendelea kuelezea mifano mengine, nayo ni hii ifuatayo:

Allah (s.w) katika suratul-Anbiyaa Aya ya 32 anasema:-

وَجَعَلْنَا السَّمَاء سَقْفاً مَّحْفُوظاً وَهُمْ عَنْ آيَاتِهَا مُعْرِضُونَ[1]

Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyohifadhiwa, lakini wanazikengeuka ishara Zake (Mwenyeezi Mungu).

Ardhi imezungukwa na kufunikwa na hewa ambayo unene wake unafikia kilomiter 350, kiwango cha hewa ya gesi ya nitrogen ni asilimia 78/03, na kiwango cha oxygen ni asilimia 20/99, na kiwango cha carbon die oxide ni asilimia 0/04, na mvuke wa maji (water vapour) na gesi nyengine ni asilimia 0/94, kutokana na wingi wa uhifadhiwaji huo wa hewa, na kiwango hicho kikubwa cha gesi huifanya ardhi isiweze kuathiriwa kutokana na mawe mengi yanayoanguka kutoka mbinguni, na kufika sehemu mbali mbali za ulimwengu, kwa hiyo kama kusingelikuwepo na hifadhi hiyo ya ardhi ingelikuwa ni hatari kwa wanaadamu, kwani ni jambo la muhali kuishi katika hali kama hiyo.

Mbali ya hayo kuwepo ukanda wa Ozon katika ardhi kuna umuhimu mkubwa katika maisha ya wanaadamu, (ukanda wa ozon ni ukanda ambao huhifadhi miale ya jua isiwafikie wanaadamu), ukanda huo hutokea kutokana na radi na mimwesa, na huihifadhi ardhi kutokana na mabalaa mbali mbali, na kama pasingelikuwepo ukanda huo ingelikuwa ni jambo lisilowezekana wanaadamu kuishi, Qur-ani kariym imeashiria muujiza huo wa kielimu miaka elfu moja mia nne iliyopita, aya iliyokuja katika Qur-ani inayoashiria muujiza huo wa kielimu ni hii ifuatayo:-

 (سقفا محفوظا).

Tukiendelea na kuelezea vipengele vya miujiza, katika sehemu hii tanakielezea kipengele cha tatu cha miujiza ya Qur-ani.

[1] suratul-Anbiyaa Aya ya 32

MWISHO