QUR_ANI NA WATOTO

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
QUR_ANI NA WATOTO
 UTANGULIZI

Baada ya kupita miaka mingi na kuonekana uzoefu na tajruba (experience) ya kutoa mafunzo ya Qur-ani katika maudhui tofauti yanayowafunza watoto kuielewa Qur-ani, mafunzo hayo yanafundishwa kwa njia ya ishara ili kuwasaidia watoto kuihifadhi Qur-ani kwa urahisi zaidi. Na watu wengi wameyapokea mafunzo hayo na kuridhika nayo, na kwa sababu hiyo basi imetulazimika kutayarisha kitabu hiki ambacho kimekusanya maudhui tofauti , aya za qur-ani, tarjuma (translate), na michoro ambayo inamaanisha na kuonesha ufahamu wa aya hizo za qur-ani, nah ii inasaidia watoto kutamka herufi  za Qur-ani kwa urahisi zaidi.

NJIA ZA KUTUMIA KITABU HIKI

1- Baada ya kuthibitika kwamba mtoto amefahamu ishara ya aya, inamlazimika achore picha inayoonesha maana ya aya hiyo.

2- Wazazi inawapasa wawatake watoto wao wachore picha zinazooana na aya hizo.

3- Watake watoto wenu wachore picha inayoonesha maudhui ya aya katika mabuku yao wanayochorea picha.

4- Wazazi wanatakiwa kuwafahamisha watoto wao kwa upole na upendo pindi wanapochora picha zao zinazohusiana na aya za Qur-ani wazingatie utukufu na wachore michoro yao kwa heshima.

Dua ya kuongeza kiwango cha elimu

Aya:

وَقُل رَّبِّ زِدْنِى عِلْما[1]

Tarjuma:

Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.

Kutoa katika vile mnavyovipenda

Aya:

لَن تَنَالُواْ الْبِرَّ حَتَّي تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَ[2]  

Tarjuma:

Kabisa hamtafikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda.
[1] Surat Taha Aya ya 114

[2] Surat Al_imrani Aya ya 92
MWISHO