KUZALIWA KWA IMAM MAHDI (A.S)

KUZALIWA KWA IMAM MAHDI (A.S)

KUZALIWA KWAKE

Wakati ukawadia na mnamo tarehe 15 Shaaban mwaka 255 Hijiriya katika Mji wa Samarraa (nchini Iraq) alizaliwa mtoto Mtukufu wakati wa usiku. Imamu Hasan Askari (a.s.) alitoa sadaka ya mikate mingi na nyama nyingi na akachinja mbuzi kadhaa wakati wa sherehe ya "Aqiqah” (kunyolewa kwa nywele za kichwa alizozaliwa nazo).

KUKUA NA MALEZI

Haikuwa kitu kipya kwa ukoo wa Mtume (s.a.w.) kwa watoto wao kutopata elimu ya nje. Ipo mifano mingine kabla ya 'Anayengojewa'. Kwa mfano, babu yake, Imamu Ali Naqi (a.s.) alikuwa na umri wa miaka sita na miezi michache tu alipofariki baba yake Imamu Muhammad Taqi (a.s.) ambaye yeye mwenyewe pia alikuwa na umri wa miaka minane tu alipofariki baba yake Imamu Ali Ridha (a.s.). Ni dhahiri kwamba, muda huo mfupi ukilinganishwa na desturi ya ukuaji wa watoto wa kawaida hautoshi kwa elimu ya nje. Lakini tunapokubali kwamba wamebarikiwa kwa baraka za Mwenyezi Mungu, basi swala la umri halitazingatiwa hata kidogo.

Katika mwezi wa Rabiul-Awwal, (Mfunguo Sita) mwaka 260 Hijiria Imamu Hasan Askari (a.s.) alikufa, na huyu mtoto mdogo wa miaka minne na nusu, alichukua nafasi yake ya Uimamu kwa muda mrefu unaokuja.

MWISHO