MNADO NDANI YA QUR_ANI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

TAHADIY(MNADO) NDANI YA QUR_ANI

Moja katika dalili muhimu nyengine za miujiza ya Qur-ani ni Aya zinzozungumzia na kutoa mnado.

Madhumuni ya aya za tahadiy (mnado)ni aya ambazo zinazungumzia juu ya maadui wanaoupinga uislamu na Qur-ani, aya hizo zinawataka maadui na makafiri kama wanasema kweli walete aya kumi,na kama hawatoweza kuleta aya hizo basi nawalete angalau aya moja mfano wa Qur-ani, miongoni mwa aya hizo ni:-

 فَلْيَاْتُوا بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِ إِن كَانُوا صَادِقِينَ[1]  

Basi nawalete Hadithi kama hizi; ikiwa wanasema kweli (kuwa hii Qur-ani akaitunga Nabii Muhammad).

 قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الإِنسُ وَالْجِنُّ عَلـٰي اَن يَاْتُواْ بِمِثْلِ هَـذَا الْقُرْآنِ لاَ يَاْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيراً

Sema “ hata wakijikusanya watu (wote) na majinni ili kuleta mfano wa hii Qur-ani basi hawangaliweza kuleta mfano wake; hata kama watasaidiana (vipi) wao kwa wao.

  اَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ فَاْتُواْ بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُواْ مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ

Ndiyo kweli wanasema kuwa: “Amekitunga mwenyewe (Muhammad kitabu hiki)?” Sema: “Basi leteni sura kumi za uwongo zilizotungwa mfano wa hii, na witeni muwawezao (kuweta) badala ya Mwenyeezi Mungu (waje wakusaidieni kutunga hivyo) ikiwa mnasema kweli.

MAUDHUI YA QUR_ANI

Qur-ani nzima inaelezea maudhui ya aina nne:-

1: Itikadi: Maudhui ya itikadi yanahusiana na kumuamini Mwenyeezi Mungu, Mitume yake, vitabu vya mitume wake, malaika wake, siku ya kiama, pepo na moto, njia iliyonyooka (haki), njia isiyonyooka (batili), n.k.

2: Sheria na kanuni: sheria na kanuni zimegawika katika sehemu mbili, nazo ni ibada na muamala.

3:Maudhui yanayohusiana na ikhlaki.

4: Visa vilivyo na mafunzo ndani yake.

ISTIKHARA (KUMTAKA MUNGU USHAURI).

Hekima za kutumia istikhara ni pale ambapo mwanaadamu anapokuwa anataka kufanya jambo lakini yuko katika hali ya shaka na anataka kufanikiwa katika kulifanya jambo hilo, na hii ni kwa sababu mtu mwenye kufanya jambo akiwa na shaka hawezi kufanikiwa, na kwa sababu hiyo basi humuomba Mwenyeezi Mungu na kumtaka ushauri ili amsaidie.

Jambo la kutaka ushauri kupitia kwa watu wengine kumetiliwa umuhimu mkubwa katika dini ya kiislamu, na katika Qur-ani kuna aya nyingi zinazoelezea kuhusu kutaka ushauri kwa watu wengine. Katika kufanya Istikhara au (kutaka ushauri kwa watu wengine), ni vizuri mwanaadamu baada ya kupata ushauri kupitia kwa wengine kubakia na hiyari katika uamuzi wake.

[1] Surat-Tuuri aya ya 34

MWISHO