Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

SAUTI TUKUFU YA QUR_ANI

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

SAUTI TUKUFU YA QUR_ANI

SAUTI TUKUFU YA QUR_ANI INAYOMVUTIA MWANAADAMU NA KUMUWEKA KATIKA UTULIVU

Abu Jahli, Abu Sufiyani, na Akhnas bin Shariq walikuwa ni washirikina maarufu, vichwa ngumu na ni maadui wa Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, na - hadharati Muhammad (s.a.w.w) - watu hao walichukiwa sana walipoona kwamba sauti ya Qur-ani inawavutia watu kwa kuingia katika dini ya kiislamu, na walifanya jitihada sana ili kuuzima na kuuondowa uislamu, lakini kwa uweza wake Mola hawakufikia wala kufanikiwa katika natija (malengo) yao.

Siku moja watu watatu hao kila mmoja peke yake na bila ya kufahamu malengo ya mwenziwe waliamua kwenda nyumbani kwake Mtume (s.a.w.w) usiku, watu hao walijificha sehemu iliyokuwa na giza katika ukuta wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) wakisikiliza sauti ya Qur-ani iliyokuwa ikisikilika nyumbani kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Watu watatu hao walivutiwa na aya za Mwenyeezi Mungu katika usiku huo, kiasi ya kwamba hawakujua muda umemalizika vipi, na walikuja kujitambua walipoona jua linachomoza na mbingu zinan’gaa, hapo walighumiwa wakiwa na hofu ya watu kuwaona, haraka walirejea majumbani mwao, wote watatu walionana njiani wakijilaumu kwa jambo walilolifanya la kwenda kusikiliza Qur-ani nyumbani kwa Mtume, walihofu waislamu wasije wakafahamu hivyo walikaa na kushauriana wafanye nini, mwisho walikubaliana wafunge ahadi ya kwamba wasikariri tena kulirejea jambo hilo kwa mara ya pili, na wala wasiende au kuonekana nyumbani kwake hadharati Muhammad (s.a.w.w).

Lakini usiku wa siku ya pili vile vile walivutiwa na sauti tukufu ya Qur-ani waliamka vitandani mwao wakaelekea nyumbani kwa mtume wa Mwenyeezi Mungu ili kusikiliza Qur-ani, kama usiku wa mwanzo kila mtu alikwenda kujificha pembe yake na kuisikiliza Qur-ani, walikuja kujitanabahi karibu ya jua kuchomoza, kwa mara ya pili wakakutana tena njiani na wakalaumiana kwa jambo walilolifanya wakaahadiana tena kutokwenda nyumbani kwa Mtume na kusikiliza Qur-ani.

Usiku wa siku ya tatu vile vile walikariri kwenda kwa Mtume na kusikiliza Qur-ani.

Asubuhi kulipokucha “Akhnas” alielekea nyumbani kwa “Abusufiyani” walikaa na kujadiliana kuhusu Qur-ani, na baadae wakaelekea nyumbani kwa Abu jahli baada ya mazungumzo marefu yaliyohusiana na Qur-ani (na waliingiwa na yakini ya kwamba Qur-ani inasema haki na kweli, lakini kutokana na kiburi, ulajuji, na matamanio ya dunia walikataa kuamini yale yaliyomo ndani ya Qur-ani, na hii iliwapelekea kupotoka katika njia ya Mwenyeezi mungu), mwishoni mwa majadiliano yao Abujahli alisema:-

“Naapa ya kwamba hatutoamini yale aliyokuja nayo Muhammad (s.a.w.w), na hapana shaka kwamba Akhnas vile vile alitaka kuwaambia Abusufiyani na Abujahli wasiamini yale waliyoyasikia katika Qur-ani na wala wasiamini aliyokuja nayo Muhammad (s.a.w.w).

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini