Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

HEKIMA YA ALLAH (S.W) KWA NABII IBRAHIMU (A.S)

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

HEKIMA YA ALLAH (S.W) KWA NABII IBRAHIMU (A.S).

Kisa cha Nabii Ibrahim (a.s) kinaonyesha Utukufu katika Miujiza ya Mwenyeezi Mungu, na Miujiza ni moja wapo miongoni mwa utukufu na hekima za Mwenyeezi Mungu katika nidhamu za kimaumbile, kwa sababu, kama tunavyojua kuwa vitu vyote ni vya Mwenyeezi Mungu basi athari ya vitu vyote hivyo pia ni ya Mwenyeezi Mungu, lakini baadhi ya wakati Mwenyeezi Mungu huleta muujiza ili kuthibitisha uhakika wa vitu hivyo, na baadhi ya wakati huleta athari za kimaumbile katika kuthibitisha hayo.

Mfano: Pale alipouamrisha moto uwe baridi kwa ajili ya Nabii Ibrahim (a.s), au kubadilika fimbo ya Nabii Mussa (a.s) na kuwa nyoka, na miujiza mengine mingi aliyoileta ili kuthibitisha utukufu wake.

قُلْنَا يَا نَارُ كُونِى بَرْداً وَسَلاَماً عَلـٰي إِبْرَاهِيمَ[1]

Sisi tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahim!

قَالَ اَلْقِهَا يَا مُوسَي .  فَاَلْقَاهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٌ تَسْعَي [2]

 Akasema: Itupe, ewe Musa! . Akaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio.

 HEKIMA ZA MWENYEEZI MUNGU KATIKA NIDHAMU ISIYO YA KIMAUMBILE.

Milki na amri zake Mwenyeezi Mungu katika dunia nzima, ni dalili iliyo wazi kabisa inayoonesha hekima ya Mwenyeezi Mungu katika nidhamu isiyo ya kimaumbile. Kama tunavyosoma katika Qur-ani:-

 مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِ إِلاَّ اَسْمَاء سَمَّيْتُمُوهَا اَنتُمْ وَآبَآؤُكُم مَّا اَنزَلَ اللّهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ إِنِ الْحُكْمُ إِلاَّ لِلّهِ اَمَرَ اَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ ذٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـكِنَّ اَكْثَرَ النَّاسِ لاَ يَعْلَمُونَ[3]

Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote.

Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu.

 Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui.

*Anawabainishia baadhi ya Tawhiyd ya Mwenyeezi Mungu, mtu huchukua fursa ya kufundisha popote anapopatia wasaa. Usiitupe fursa ukiipata. Usije ukajuta.

Kwa hiyo mmiliki wa haki wa vitu vyote duniani vya siri na vya dhahiri. Na Yeye ndiye anayejua mwanaadaamu anahitajia nini, basi Yeye ndiye m-bora katika kuweka kanuni zake na kuhukumu kutokana na hukumu hizo. Mwenyeezi Mungu anasema:-

اَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ اَحْسَنُ مِنَ اللهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ[4]

Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?

* Hapa wanahadidiwa wanaokataa hukumu alizotoa Mwenyeezi Mungu, wakakhitari mila ya kienyeji (customary laws and decrees), na wako watu namna hii, basi wamo katika hatari kubwa kabisa.

Ni juu ya kila muislamu kuridhia aliyoyasema Mwenyeezi Mungu katika Qur-ani yake na aliyoyasema Mtume katika hadithi zake, akiyakataa haya basi kisha kusimama katika ukingo wa moto wa jahannam tayari kutumbukia.

Na kwa sababu hiyo basi Mwenyeezi Mungu Mtukufu anawataabiria wale watu ambao wanahukumu kile ambacho Mwenyeezi Mungu hajakiteremsha, kwa kusema:-

إِنَّا اَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ اَسْلَمُواْ لِلَّذِينَ هَادُواْ وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالاَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُواْ مِن كِتَابِ اللهِ وَكَانُواْ عَلَيْهِ شُهَدَاء فَلاَ تَخْشَوُاْ النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلاَ تَشْتَرُواْ بِآيَاتِى ثَمَناً قَلِيلاً وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا اَنزَلَ اللّهُ فَاُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَافِرُون[5]َ

Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.

*Hapa inasifiwa Taurati kitabu cha Nabii Mussa kuwa kitabu hicho ijapokuwa aliteremshiwa Nabii Mussa lakini Mitume wengi kabisa wa Kiyahudi waliokuja baada ya Nabii Mussa waliambiwa wakifuate hiki hiki, basi kikatumiwa na chungu ya Mitume na chungu ya wanavyuoni na chungu ua wacha Mungu.

Na juu ya hivi chungu ya Mayahudi walikipinga, na mwisho wakageuza geuza watakavyo.
Na katika aya nyengine watu hao wametajwa kwa jina la dhalimu na fasiqi, pale Allah (s.w) aliposema:-

وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا اَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالاَنفَ بِالاَنفِ وَالاُذُنَ بِالاُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا انزَلَ اللّهُ فَاُوْلَـئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ[6]

Na humo tuliwaandikia ya kwamba roho kwa roho, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, na jino kwa jino, na kwa majaraha kisasi. Lakini atakaye samehe basi itakuwa ni kafara kwake.

Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.

وَلْيَحْكُمْ اَهْلُ الإِنجِيلِ بِمَا اَنزَلَ اللّهُ فِيهِ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا اَنزَلَ اللّهُ فَاُوْلَـئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ[7]

Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.

*Hapa zinatajwa baadhi ya hukumu zilizokuwamo humo, na inatajwa Injili, kitabu alichoteremshiwa Nabii Issa juu ya kuambiwa afuate na Taurati pia. Hii Injili ilikuwa ina mawaidha zaidi kuliko hukumu.

Na Taurati ina hukumu nyingi zaidi kuliko mawaidha, ilivyokuwa mwishowe Mayahudi wameharibika sana ndiyo hiyo Injili ikajazwa mawaidha hivyo ili zilainike kidogo nyoyo za Mayahudi lakini wapi.

Na huyu Nabii Issa alipelekwa kwa Mayahudi vile vile kama Nabii Mussa, si kwa Wazungu ila wengi kabisa walikataa kumfuata, akafuatwa na Wazungu kwa kulinganiwa na hao Mayahudi waliomfuata.

Hawa Wazungu wamefuata nyuma, baada ya kuondoka ulimwenguni nabii Issa (a.s) kwani dini ya Mweenyeezi Mungu haina wenyewe makhsusi.

Basi natija tunayoipata katika maelezo hayo ni kwamba Mwenyeezi Mungu ndiye mmiliki wa kila kitu duniani, na kwa wale watu ambao wanadai kuwa wao wamiliki Mwenyeezi Mungu anawambia:-

يُولِجُ اللَّيْلَ فِى النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِى اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِى لِاَجَلٍ مُّسَمًّى ذٰلِكُمُ اللهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ[8]

Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia. Kila kimoja wapo kinakwenda kwa muda maalumu.

Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi.

Ufalme ni wake. Na hao mnao waomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende.

 

[1] Surat Al-Anbiyaa aya ya 69

[2] Surat Taha Aya ya 19-20

[3] Surat Yussuf Aya ya 40

[4] Surat Maidah Aya ya 50

[5] Surat Al-Maidah Aya ya 44

[6] Surat al-Maidah Aya ya 45

[7] Surat al-Maidah Aya ya 47

[8] Surat faatir Aya ya 13

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini