KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU 2

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU.2

Mafakihi, na Maulamaa wamehitalifiana katika kutafsiri maana ya uadilifu.

- Kuna miongoni katika wao mwenye kusema, ya kwamba ni dhahiri ya uislam bila ya kudhihirisha  ufasiki.

- Mwingine akasema, ni tabia iliyomo ndani ya nafsi inayopelekea kufanya wajibu na kuacha yale  yaliyoharamishwa.

- Wengine wakasema, ni sitara na kujistahi.

- Na wengine wakasema ni kuacha kutenda madhambi makubwa na kutoendelea na kumuasi  Mwenyeezi Mungu kwa kufanya madhambi madogo.

Katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:-

"Msifuate hawaa (yaani kufanya maasi kwa kufuata yale ambayo nyoyo zinapendelea kuyafanya) ili  mfanye uadilifu."

 Na ili kuthibitisha kuwa uadilifu ni kuhalifu hawaa. Amirul-muminin Ali (a.s.) alimsifu ndugu yake, kwa Mwenyezi Mungu, katika aliyomsifu kuwa; "Alikuwa akijiwa ghafla na mambo mawili huangalia lipi lililo karibu zaidi na hawaa kisha akalikhalifu." Na akasema: "Mwanzo wa uadilifu wake ulikuwa ni kukanusha hawaa ya nafsi yake."

Amesema Mjukuu wake, Imam Jafar as-Sadiq: "Ama katika mafaqih atakayekuwa anaichunga nafsi yake, mwenye kuihifadhi dini yake, mwenye kukhalifu hawaa yake, mwenye kutii amri ya Mola wake basi ni juu ya watu kumfuata."  Na mkiupotoa au mkaachana nao basi Mwenyezi Mungu ana habari ya myatendayo.

 Yaani msicheleweshe au kuacha kutoa ushahidi. Kisha akatoa tisho na kusema kwamba mwenye  kuyafanya hayo Mwenyezi Mungu anamjua na atamwadhibu.

 Alla (s.w) anasema:-

والَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا اُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا اُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ"[1]    "

Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo.

Enyi mlioamini! Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu ambacho amemteremshia Mtume wake na Kitabu alichokiteremsha kabla.

*Tamko la “na yaliyoteremshwa kabla yako” ni la kuonyesha kuwa muislamu hana ruhusa kuamini kuwa Mwenyeezi Mungu atamteremshia Utume mtu mwengine BAADA ya Nabii Muhammad (s.a.w.w), basi mtu huyo atakuwa kafiri tu.

Mtu anaweza kuamini Muumbaji na kukanusha utume na vitabu vya Mwenyezi Mungu. Na anaweza akakubali utume wa baadhi na baadhi ya vitabu; au kukanusha kuwapo Malaika au Siku ya Mwisho. Kama pale Allah (s.w) aliposema:-

"آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا اُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ اَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُواْ سَمِعْنَا وَاَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِير"ُ[2]

Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.

 * Katika sehemu hii na tuangalie maelezo machache yanayohusiana na Aya hiyo.

*Ayah ii ni yenye fadhila kubwa kama ile Ayatu Kursiyyu,  na inahimizwa kusomwa mwahala mle mlimosuniwa kusomwa ile Ayatu kursiyyu.

* Na inaonyesha baadhi ya sifa za waislamu na mambo yao wanayoyaamini, na moja katika hayo ni kuwa wanakubali Mitume wote wa Mwenyeezi Mungu waliokuwa kabla ya Nabii Muhammad(s.a.w.w), na qur-ani yote inasema min qablika , yaani waliokuwa kabla yako.

Kama alivyobainisha hivi Mwenyeezi Mungu katika Qur-ani yote- kuwa Mitume yote walipewa Utume kabla ya Nabii Muhammad, yeye Nabii Muhammad ndiye Mtume wa mwisho- Khaataman Nabiyyin.

Asiyesadiki hivi akamsadiki anayejisingizia kuwa kapewa kapewa utume baada ya Nabii Muhammad basi mtu huyo ni kafiri pamoja na huyo mtume wake, Waislamu hawamkatai hata mmoja katika Watume (Mitume) waliokuwa kabla ya Nabii Muhammad, na wanaitakidi kuwa sharia zao za mambo ya kufanya sasa hazifuatwi, hizi ni zama za kufuata sharia aliyokuja nayo Nabii Muhammad katika mambo ya kufanya, ama katika mambo ya itikadi Mitume wote wamekuja na sharia namna moja, katika alivyosema Mwenyeezi Mungu katika Aya ya 13 ya surat Shuura, na katika sura nyenginezo.

شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّي بِهِ نُوحاً وَالَّذِى اَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَي وَعِيسَي اَنْ اَقِيمُوا الدِّينَ وَلاَ تَتَفَرَّقُوا فِيهِ كَبُرَ عَلـٰي الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ اللهُ يَجْتَبِى إِلَيْهِ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِى إِلَيْهِ مَن يُنِيبُ[3]

Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.

*Ayah ii vile vile inafundisha baadhi ua adabu za Uislamu na Dua za kuomba, na ni za kutaja fadhila za Mwenyeezi Mungu zilizoko juu ya waja wake. Kuwa hawakalifishi wasiyoyaweza, bali hata magumu sana tu hawakalifishi, anawakalifisha yaliyo mepesi kwao, wala hawatesi wanapofanya jambo kwa kusahau au kwa dharura kubwa, na kuonyesha vile vile kuwa mzee hatateswa kwa kosa la mtoto, wala mtoto hatateswa kwa kosa la mzee wala.. kwa kosa la … Kila mtu ana lawama za amali zake mwenyewe- si za mtu mwengine. Lakini juu yake kuamrisha mema na kukataza mabaya- si juu yake wakitofuata.

Aya hii imebainisha nguzo za imani ambazo ni wajibu kuzikubali kila mwenye kuacha shirki na ulahidi na kuziamini zote sio baadhi ya sehemu zake. Nguzo zenyewe ni kumwamini Mwenyezi Mungu na Mitume yake yote, vitabu vyake na Malaika wake na pia Siku ya Mwisho.

 Kwa hiyo makusudio ya neno 'wale walioamini,' ni wale walioacha ushirikina na ulahidi. 'Na wale walioamini' la pili ni imani ya uhakika, sio kudumu imani na kuthibiti kwenye imani kama walivyosema wafasiri, Makusudio ya Mtume wake, ni Muhammad (s.a.w.w). Na Kitabu ambacho amemteremshia Mtume wake ni Qur'an na Kitabu alichokiteremshia kabla, ni kila Kitabu cha Mwenyezi Mungu alichokiteremsha kabla ya utume wa Muhammad (s.a.w.w) Na mwenye kumkataa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Siku ya Mwisho, basi amepotea upotevu ulio mbali.

Aya hii ni dalili wazi kwamba kuamini ghaibu ni nguzo katika nguzo za Kiislamu na kwamba asiyeamini si Mwislamu. Umetangulia mfano wa Aya hii pamoja na tafsiri yake katika sura

(إِنَّ الَّذِينَ آمَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ آمَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ ازْدَادُواْ كُفْرًا لَّمْ يَكُنِ اللّهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلاَ لِيَهْدِيَهُمْ سَبِيلاً)[4]

 Hakika wale walioamini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakakufuru, tena wakazidi ukafiri, Mwenyeezi Mungu hatawasamehe wala hatawaongoza njia ya(kheri). Na anasema:-

 [5](بَشِّرِ الْمُنَافِقِينَ بِأَنَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا)

 Wape bishara wanafiki kuwa wana adhabu iumizayo.

 (الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاء مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ العِزَّةَ لِلّهِ جَمِيعًا)[6]

Ambao huwafanya makafiri ndio marafiki badala ya waumini. Je wanataka kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.

Katika aya hiyo unakaririwa ubaya wa wanafiki.

[1] Albaqara, 4

[2] Albaqara 285

[3] Surat Shuura ,Aya ya 13.

[4] Anisaa 137

[5] Nisaa, 138

[6] Nisaa 139

MWISHO