Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UMUHIMU WA KUVAA HIJABU NO.3

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UMUHIMU WA KUVAA HIJABU KATIKA JAMII. NO.3

Katika makala zilizopita tulielezea umuhimu wa kuvaa hijabu katika jamii, na tukaashiria baadhi ya masuala ambayo yanahusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu, tunamshukuru Mola kwa kutupa nguvu za kuweza kuyajibu masula hayo, katika makala hii tutaendelea na mada yetu hiyo hiyo, tunategemea mtafaidika na tutakayoyaeleza yanayohusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu.

Miongoni mwa dalili nyengine zinazopelekea wanawake kuvaa hijabu ni kama hizi zifuatazo:-

AMA DALILI YA PILI NI KUHIFADHI HESHIMA NA THAMANI.

 Ikiwa katika jamii uongo utakithiri, na watu wasema kweli wakasema “watu wote hao wenye kusema uongo, usemaji kweli wetu sisi una faida gani?” kisha na wao vile vile wakajiunga na kundi la wasema uongo, na kwa kutokana na kuzidi kwa hiyana katika jamii watu wenye amana nao wakajiunga na kundi la wenye hiyana, na kwa kutokana na watu wengi wasiochunga suala la mavazi, wenye kulithamini suala hilo vile vile wakajiunga na wasiolithamini suala hilo, kama mambo yatakuwa hivyo basi katika jamii mambo yote yenye thamani yatapotea, na kizazi kitakachokuja baadae masuala yenye thamani kubwa katika jamii ambayo tumeyataja hapo nyuma kama vile(amana, ukweli, huruma) yatakuwa ni mageni kwao, na wala hawatoyatambuwa maana yake.

Basi moja kati ya malengo ya kutenda mambo yaliyo sawa hata kama watu watakuwa hawayatilii maanani masuala hayo, ni kuyathamini na kuihifadhi thamani ya mambo hayo, na ikiwa kuna mtu atakuwa anayatekeleza mambo hayo na akawa asirudi nyuma, basi kuna matarajio baadae, mbali ya kule kuihifadhi thamani ya mambo hayo basi atawafanya wengine vile vile, hatua baada ya hatua kujiunga nae, na baadae sifa na tabia njema zitaenea katika jamii.

 Sasa tumefikia kwenye dalili ya tatu ambayo kwa mtizamo wangu ndiyo dalili yenye nguvu zaidi kuliko nyengine:

 KUMTII MOLA NA KUZIHESHIMU SHERIA ZAKE.

Bila ya shaka unaelewa kwamba hukumu na sheria za Mola hata kama kuna watu watakuwa wanazipuuza hukumu na sheria hizo, basi sheria hizo zitabakia pale pale na wala hazitofutika, basi hata kama kuna wengi wasiolithamini suala la hijabu, ambalo ni moja kati ya sheria za Mola, basi bado mpango wa Qur-ani kwa nguvu za Mola utabakia palepale na ni lazima uheshimiwe.

 Nukta nyengine ambayo wewe umeiashiria ni hii ifuatayo:

 Hivi iwapo wanawake wote wakiwa huru wewe huoni kwamba mambo yote yatakwenda sawa kabisa?

 Dada yangu, kutoka kwa wengi mimi nimesikia kwamba, katika jamii yetu iwapo watu watakuwa huru katika kufanya makosa na kutokuwa na mipaka maalum ya kisheria, basi mambo yote yatakwenda kikawaida kabisa, na watu hawatokimbilia na kuwa na hamu ya kufanya makosa, mimi vile vile nawafiki suala la (jamii kuwa na hali ya kawaida) ama kwa mtizamo wangu mimi kuna njia mbili ya mambo kuwa ya kawaida katika jamii:

 Njia ya kwanza ni kwamba ufisadi na utendaji wa makosa uwe ni kawaida kwa watu, na uwe ni jambo la kawaida, na ikifikia hivyo jamii itatafuta daraja ya juu zaidi ya ufisadi, na sio kwamba wataacha ufisadi.

Kijana ambaye sigara kwake ni kitu cha kawaida kabisa, inawezekana kijana huyo sigara kwake ikawa ni kitu cha kawaida kabisa ama ikifikia hivyo basi atapanda daraja ya pili na kuelekea kwenye madawa ya kulevya.

Hali ndio hiyo hiyo katika jamii yetu, lilipokuwa suala la kuziwacha wazi baadhi ya nywele za kichwa limeshazoeleka na hakuna mtu mwenye kulistaajabia, basi kuacha wazi ukosi, kufupisha sketi, kupandisha mikono ya nguo, yote hayo yameanza kupamba moto katika jamii baada ya kuzoeleka hilo la mwanzo, basi kuzoeleka na makosa kuwa ni kitu cha kawaida katika jamii, haisababishi watu kuachana na makosa bali inasababisha kuzidi makosa na kufikia katika hali ya hatari zaidi.

 Njia ya pili, ni kuzoeleka kwa natija ya mambo na makosa  katika jamii, kwa mfano, (mwizi akawa ameshazoea kufungwa na kwake ikawa ni kitu cha kawaida), fikiria kwamba kuna mwanamke aliyekwenda kuonana na rafiki yake, na kwa kustaajabu kabisa akamwambia rafiki yake, “kwa nini kibiriti na mashine ya kusagia nyama, umevificha na umeviweka mbali na macho ya watoto?

 Katika nyumba yetu sisi vitu tumeviweka nje nje, na vitu hivyo watoto wanaviona ni vya kawaida kabisa kwa sababu wameshavizowea, kwani mara ngapi wameviona vitu hivyo na vimeshakuwa ni vya kawaida kwao, ama baada ya dakika chache akaulizwa na rafiki yake, kwa nini watoto wako wadogo hujawaleta nyumbani? Akajibu jana tu mmoja kati ya watoto wangu kidole chake alikitia katika mashine ya kusagia nyama na nikampeleka Hospitali, sasa mtu kama huyu ambae vifaa vya hatari amevifanya viwe ni vya kawaida mbele ya watoto basi muwache aonje mashaka na natija ya kufanya kwake hivyo.

 Dada yangu, ukweli uliopo ni kwamba katika jamii za nchi za Europ jambo ambalo sisi tuna shaka nalo ni kutembea uchi, na kutaka uhuru wa kuwa na mafungamano kati ya mwanamme na mwanamke, ambayo yote hayo hakuna shaka ndio yanayosababisha jamii na watu kuharibikiwa, basi ni vizuri kama utafunguwa magazeti ili kuona nini wameandika kuhusu masuala haya ambayo yameleta athari mbaya katika jamii.

 Mimi nitakuandikia habari mbili tatu zinazohusiana na masuala haya, ambazo zimeandikwa katika magazeti, na wewe utaitafuta habari hii na uisome kwa ukamilifu.

 Kutokana na habari za uchunguzi zilizotolewa na Idara inayuhusika na mambo  ya jamii ya London, katika miezi mitatu ya mwaka uliopita, zaidi ya asilimia 31 ya watoto ambao wanaishi London hawana baba.

 Na katika habari za charnel ya Tv ya c.n.n wameeleza kwamba asilimia 50 za watoto ambao wanaishi America watoto wengi wamezaliwa nje ya ndowa, na masuala ya talaka pia ni mengi zaidi.

 Tv ya c.n.n imeonesha film fupi zenye kuonyesha watoto wa kike na wanawake wakitaka msaada kutoka kwa watu na polisi, na wameelezea kwamba makosa ya jinai katika jamii ya Kimarekani yamefikia upeo wake, kiasi ya kwamba idadi za vifo, kuwabaka wanawake, wizi, na aina nyengine za makosa, zinaongezeka siku hadi siku katika miji ya Kimarekani, na polisi hawawezi kuzuia matokeo hayo, kwa hiyo wanawausia wasichana na wanawake kwa ujumla wachukuwe silaha au dawa za kupotezea fahamu ili waweze kukabiliana na mashambulizi na kujihami kutokana na wakorofi

Mimi kwa ukamilifu kabisa nataka kukujibu barua yako ulipouliza:

Ni kwa nini hata unywele mmoja wa mwanamke hautakiwi kuonekana?

Ili liweze kufahamika suala hili kwanza kuna vipengele viwili ni lazima vifahamike:

1. Sheria zote za Mwenyezi Mungu ambazo zimewekwa  kwa hekima na kwa kutaka kheri na maslahi ya wanaadamu, uchache wake na wingi wake ni lazima zifuatwe, angalia mfano huu (damu ni najisi, ndoo moja ya damu ni najisi, gilasi moja ya damu ni najisi, na hata kiwango cha ncha ya sindano cha damu ni najisi).

Kuiba mali ya watu ni haramu, na hakuna tofauti katika wizi, yaani ukiiba kitu kidogo au kikubwa, vyote hivyo ni haramu.

Suala la hijabu au kivazi ndio hivyo hivyo, kwamba kuonesha nywele mbele ya wanaume ni haramu, sasa iwe ni unywele mmoja au kichwa kizima.

2. Katika utendaji wa makosa ndio hivyo hivyo kwanza Shetani humdanganya mtu kutenda makosa madogo madogo kisha humpeleka kwenye makosa mkubwa makubwa, dada yangu we! Mimi ninakuuliza hivi ni kwa nini unapomuona mwanao mdogo amechukua pakti ya sigara unamkataza? Hivi ni kwa nini unamkataza? Kwani pakti moja ya sigara ina madhara gani? Nikukuuliza hivyo utaniambia hivi: “a suala si kua yeye amekamata pakti ya sigara, bali ni kua ukimuachia leo akamate kesho ataanza kuvuta sigara moja,na baadaye mbili hadi kuendelea.

Kwa ufahamu, kama ukitaka kukabiliana na tabia mbaya ni lazima uanze kukabiliana nazo tokea zinapoanza kujichomoza, la si hivyo baadae itakua ni vigumu kuzing’oa tabia hizo, ni methali nzuri ilioje isemayo (mwizi wa yai leo ni mwizi wa ngamia kesho).

Hivi sasa ninalijibu suala lako la mwisho lililobakisha alama ya suala ndani ya akili yako:

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini