DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.6

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI NO.6

Katika makala iliyopita tulielezea madai yaliyotolewa na baadhi ya wafuasi wa dini tofauti, miongoni mwa hao ni wafuasi wa dini ya kiyahudi na Manasara, watu hao wanadai kuwa dini zote ni haki na Mola (s.w) atawalipa waja wake wote ujira mwema na kuwaongoza katika njia ya saada. tuliyajibu madai ya watu hao kwa kutoa dalili za Qur-ani takatifu kuwa dini ya haki ni dini ya Kiislamu tu, katika makala hii tutaendelea kuyajibu madai hayo kwa dalili mbali mbali inshaallah. tuliyajibu madai hayo na tukafikia kifungu cha tatu, na sasa hivi tutkielezea kifungu cha nne kwa kusema:-

Nne: Katika Qur-ani takatifu kuna Aya nyingi zinazoelezea kwa uwazi kabisa kuhusiana na akida za Mayahudi na Manasara, na Mwenyeezi Mungu amezichukia na kubainisha kuwa akida hizo sio sahihi, pale aliposema:-

وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَنُ وَلَداً . لَقَدْ جِئْتُمْ شَيْئاً إِدّاً . تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الاَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدّاً. اَن دَعَوْا لِلرَّحْمَنِ وَلَداً[1]

Na wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana! Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno! Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana.

Na katika Aya nyengine anasema:-

وَقَالُواْ لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلاَّ مَن كَانَ هُوداً اَوْ نَصَارَي تِلْكَ اَمَانِيُّهُمْ قُلْ هَاتُواْ بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ[2]

Na walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Yahudi au Mkristo. Hayo ni matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli.

Na katika Aya nyengine anasema hivi:-

وَلَن تَرْضَي عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَي حَتَّي تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَي اللهِ هُوَ الْهُدَي وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ اَهْوَاءهُم بَعْدَ الَّذِى جَاءكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللهِ مِن وَلِيٍّ وَلاَ نَصِيرٍ[3]

Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.

Na katika Surat Almaidah anasema hivi:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَي اَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ اَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِى الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ[4]

Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.

Maelezo kuhusiana na Aya

Aya nyingi sana zimetukataza kuwafanya wasiri wetu, na baadhi yake tumekwisha kuzitaja. Tumehimizwa kuwafanyia:-

a) Uadilifu katika haki zao.

b)Kuwafanyia mema kwa chetu na yetu, ama hapana ruhusa kuwafanya wasiri wetu, kwa kila namna hawana usafi wa roho na sisi, wana misiba ya nyoyo juu yetu na uadui wa milele.

[1] Surat Maryam Aya ya 88-91

[2] Surat Albaqarah Aya ya 111.

[3] Surat Albaqarah Aya ya 120

[4] Surat Almaidah Aya ya 51

MWISHO