MAYAHUDI NDANI YA QUR_ANI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MAYAHUDI NDANI YA QURANI

Mwenyeezi Mungu Mtukufu ndani ya Kitabu chake kitakatifu (Qur-ani) Suratul-Baqarah Aya ya 85 anasema hivi:-

ثُمَّ اَنتُمْ هَـؤُلاء تَقْتُلُونَ اَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقاً مِّنكُم مِّن دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِم بِالإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِن يَاتُوكُمْ  اُسَارَي تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ اَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ فَمَا جَزَاء مَن يَفْعَلُ ذٰلِكَ

مِنكُمْ إِلاَّ خِزْيٌ فِى الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَي اَشَدِّ الْعَذَابِ وَمَا اللّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ

Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnawatoa baadhi yenu majumbani kwao, mkisaidiana kwa dhambi na uadui. Na wakikujieni mateka mnawakomboa, na hali kuwatoa mmekatazwa. Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda.

Maelezo kuhusiana na Aya:

Madina kulikuwa na makabila mawili: Aws na khazraj. Watu wa makabila haya kabla ya kusilimu walikuwa mara kwa mara wakipigana, Mayahudi wa madina waligawanyika makundi mawili,wengine wakaunga mkono upande wa Aws, na wengine upande wa Khazraj. Kwa hivyo wakati yanapopigana makabila mawili haya, Mayahudi wa upande mmoja walikuwa wakiua Mayahudi wenzao wa upande mwengine,, na iwapo baadhi ya jamaa zao wamekuwa mateka walikuwa wakiwakomboa, hapa wanaambiwa:-

“Iwapo mnawakomboa mateka wa kiyahudi kwa sababu ya kufuata Taurati, kwa nini mnapigana nyinyi kwa nyinyi? Na hilo pia limekatazwa katika Taurati?. Mnaamini baadhi ya Taurati na kuikanusha baadhi nyengine?.

Na kama alivyosema Mwenyeezi Mungu, walipata fedheha ya kuuliwa, kutolewa katika miji na kufanywa mateka, na siku ya Kiyama watapata adhabu iliyotajwa mwisho wa Aya.

Ama kuhusu madai ya kuwa dini ya Mayahudi na Manasara pia ni dini za Mwenyeezi Mungu na zimeteremshwa kupitia Mitume yake Allah (s.w). tunasema hivi:

* Ni sahihi kuwa dini hizo ni dini za Mwenyeezi Mungu na zilikuja kuwalingania watu kwa mujibu wa maamrisho yake Allah (s.w). lakini dini hizo hazikuwa kamili katika zama zake kabla ya kuja dini ya Kiislamu, hivyo dini ya Kiislamu imekuja kuzikamilisha dini hizo.

* Kabla ya kudhuhuru dini ya Kiislamu katika vitabu vya Mayahudi na Manasara kulielezewa kwa uwazi kabisa kuhusiana na dini hiyo.

* Baada ya kupita muda dini hizo za Mayahudi na Manasara zilipotoshwa na kuharifiwa.

* Dini za Mayahudi na Manasara zilikuja kwa ajili ya kuiunga mkono dini Tukufu ya Kiislamu.

Kwa hiyo, natija inayopatikana katika majibu hayo yaliyoelezewa ni kuwa ; neno dini lina maana maluumu, na dini ya haki ni dini ya Kiislamu peke yake, hivyo ni wadhifa wa kila mwanaadamu kufanya uhakiki kuhusiana na dini ili apate taaluma ya kutosha inayohusiana na maudhui hayo, baada ya kufanya utafiti atapata ufumbuzi, hapo anaweza kuifafanua dini, na kuchagua haki iko wapi.

[1] Surat Albaqarah Aya ya 85

MWISHO