Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.3

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

SIFA TUKUFU ZA MITUME (A.S) NO 3.

Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu sifa tukufu za Mitume (s.a), na tukaelezea miongoni mwa sifa hizo kuwa ni elimu, katika makala hii tutaendelea kuelezea sifa nyengine ambazo wanatakiwa Mitume (a.s) kuwa nazo. Sifa ya tatu ni kuweza kuleta miujiza.

3. Muujiza.

Muujiza yaani ni kufanya matendo ambayo wengine hawana uwezo wa kuyafanya, na tukifikiria kiakili tutagundua kuwa kuna umuhimu wa kuwepo muujiza, kwa sababu kuwepo muujiza kunaleta mafanikio kwa watu wote duniani. Miujiza ya Mitume ni dalili tosha iliyowazi inayothibitisha madai yao, kuwa Mitume hiyo imeteremshwa kwa idhini ya Mola wao, kama anavyosema Nabii Mussa (a.s) kumwambia Firauna:-

قَالَ اَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَيْءٍ مُّبِينٍ. قَالَ فَاْتِ بِهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ. فَاَلْقَي عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ . وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاء لِلنَّاظِرِينَ[1]  

Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?

Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli.Basi akaitupa fimbo yake,mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri.Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao.

Kuwa na uwezo wa kufanya miujiza ni miongoni mwa sifa za Mitume ya Mwenyeezi Mungu, na Mitume huifanya Miujiza hiyo kwa idhini ya Mola wao, na hakuna mtu yoyote anayeweza kuipinga miujiza hiyo isipokuwa wale ambao ni madhalimu. Kama anavyosema Allah (s.w) kuwaambia kaumi ya Thamudi:-

وَمَا مَنَعَنَا اَن نُّرْسِلَ بِالآيَاتِ إِلاَّ اَن كَذَّبَ بِهَا الاَوَّلُونَ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُواْ بِهَا وَمَا نُرْسِلُ بِالآيَاتِ إِلاَّ تَخْوِيفاً[2]

Na hapana kinacho tuzuia kupeleka miujiza ila ni kuwa watu wa zamani waliikanusha. Na tuliwapa Wathamudi ngamia jike kuwa ni Ishara iliyo dhaahiri, lakini walidhulumu kwaye. Nasi hatupeleki Ishara ila kwa ajili ya kuhadharisha.

Miujiza ya Mitume inafanywa kutokana na mnasaba wa zama jinsi watu walivyokuwa wakiishi, kwa mfano katika zama za Nabii Mussa uchawi ulikuwa ni maarufu, hivyo Nabii Mussa alikuwa ni mahiri katika uchawi, na akakabiliana na wachawi wa zama hizo, kama anavyosema Allah (s.w):-

فَاَلْقَي مُوسَي عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَاْفِكُونَ[3]

Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua.

Na Nabii Issa (a.s) alikuja katika zama ambazo watu walikuwa ni mahiri katika masuala ya matibabu na udaktari, aliwapa shafaa wagonjwa, na akawafufua wafu (waliokufa), kama anavyosema Allah (s.w):-

وَرَسُولاً إِلَي بَنِى إِسْرَائِيلَ اَنِّى قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ اَنِّى اَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَاَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْراً بِإِذْنِ اللهِ وَاُبْرِئُ الاكْمَهَ والاَبْرَصَ وَاُحْيِـي الْمَوْتَي بِإِذْنِ اللهِ وَاُنَبِّئُكُم بِمَا تَاْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِى بُيُوتِكُمْ إِنَّ فِى ذٰلِكَ لآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِين4

Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini.

*Hapa inatajwa baadhi ya miujiza aliyokuja nayo Nabii Issa (a.s).

Na Mtume Muhammad (s.a.ww.) akaja katika zama ambazo wanamashairi walikuwa maarufu katika kuandika visa, basi Mtume akawa ni mtu bora kabisa katika mashairi na kuandika au kusoma visa. Kama anavyosema Allah (s.w):-

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ اَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا اَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ[5]

 Sisi tunasimulia simulizi nzuri kwa kukufunulia Qur'ani hii. Na ijapo kuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa wasio jua.

[1] Surat shuaraa Aya ya 30-33

[2] Surat Asraa Aya ya 59

[3] Surat Shuaraa Aya ya 45

[4] Surat Al-Imrani Aya ya 49

[5] Surat Yussuf Aya ya 3

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini