Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAFANIKIO YA MITUME NO 1

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MAFANIKIO YA MITUME

*Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu?

MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.1

Mwenyeezi Mungu Mtukufu katika Qur-ani anasema hivi kuhusu Mitume:-

اُوْلَـئِكَ الَّذِينَ هَدَي اللّهُ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ قُل لاَّ اَسْاَلُكُمْ عَلَيْهِ اَجْراً إِنْ هُوَ إِلاَّ ذِكْرَي لِلْعَالَمِينَ[1]

Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya yao. Sema: Mimi sikuombeni ujira. Haya hayakuwa ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.

Kwa hiyo kama tukifuata njia waliotuonesha Mitume, hapana shaka tutaongoka, basi ili kufuata njia hizo, ni lazima tuelewe siri ya mafanikio ya Mitume hiyo. Ama ni lazima tuzingatie kuwa tunaposema mafanikio ya Mitume haina maana kuwa watu wote wameongoka na kufuata njia ya Mitume, kwa sababu Mwenyeezi Mungu anasema:-

لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ[2]

Wewe si mwenye kuwatawalia.

Kwa hiyo tunaposema Mitume imefanikiwa katika kufikisha ujumbe wao, yaani Mitume imeweza kufikisha sauti ya Tawhiyd kwa wanaadamu wote ulimwenguni, na kuwataka watu wamuabudu Mola mmoja, Mola wa mbingu na ardhi. Kwa hiyo njia ya uongofu iko wazi kabisa kwa wale wacha Mungu, na kwa upande mwengine wameleta uadilifu, na kuwataka wanaadamu wawe waadilifu, na watake uadilifu, na kwa sababu hiyo basi nyoyo za wanaadamu ziliridhika na ujumbe wa Mitume hiyo, kiasi ya kwamba waliweza kuhifadhi imani yao kwa kustahamili tabu,mashaka, na adhabu walizokuwa wakizipata, watu hao walithibitisha ukweli wao, na walikuwa waaminifu katika kupigania haki ya kile walichokithibitisha na kilichowathibitikia, wakapambanua baina ya haki na batili, na Mwenyeezi Mungu akawajaalia watu hao kuwa ni hoja kwa viumbe wake wengine, kama anavyosema ndani ya Qur-ani:-

رُّسُلاً مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلاَّ يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلـٰي اللهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ وَكَانَ اللّهُ عَزِيزاً حَكِيماً[3]

Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Kwa hiyo, pindi wanaadamu wakifahamu sababu zilizowapelekea Mitume kufanikiwa katika kufikisha ujumbe wao, inaweza kutusaidia sisi katika kufuata njia zao. Basi katika makala ijayo tutatupilia macho sababu muhimu za mafanikio ya Mitume.

[1] Surat Al _an-aam Aya ya 90

[2] Surat Al-ghashiyah Aya ya 22

[3] Suratun-Nisaa Aya ya 165

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini