Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAFANIKIO YA MITUME NO.2

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MAFANIKIO YA MITUME

*Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu?

MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.2

Katika makala iliyopita tulielezea kwa ufupi kuhusu mafanikio ya Mitume, katika makala hii tutaendelea na mada yetu hiyo hiyo, ama kwa kubainisha kwa kina sababu zilizopelekea Mitume kufanikiwa katika kufikisha ujumbe wao na malinganio yao ya kuwataka wanaadamu wamuabudu Mola mmoja tu. miongoni mwa sababu hizo zilizopelekea mafanikio katika kufikisha ujumbe ujumbe wao ni hizi zifuatazo:-

1. UKWELI NA UAMINIFU

Ukweli na uaminifu ni dalili muhimu zinazowafanya watu waamini na wawe na uhakika ya kile wanachobashiriwa, kama tunavyoona ukweli na uaminifu wa Nabii Yussuf ulimfanya yeye apewe cheo cha kuwa waziri katika kasri nchini Misri, na akawa waziri wa Mfalme wa nchi ya Misri. Mfalme huyo kuhusiana na Nabii Yussuf anasema hivi:-

 وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِى بِهِ اَسْتَخْلِصْهُ لِنَفْسِى فَلَمَّا كَلَّمَهُ قَالَ إِنَّكَ الْيَوْمَ لَدَيْنَا مِكِينٌ اَمِينٌ[1]

Basi mfalme akasema: Mleteni kwangu, awe wangu mwenyewe khasa. Basi alipo msemeza alinena: Hakika wewe leo umekwisha tamakani kwetu na umeaminika.

Mitume walikuwa ni watu maarufu kutokana na ukweli na uaminifu wao, na walipokuwa wakiwalingania watu katika dini ya Mwenyeezi Mungu walizungumzia kuhusu ukweli na uaminifu, hii iliwapelekea watu kuwaamini na kuwatii,  na wao waliwataka watu hao kumtii na kumcha Mwenyeezi Mungu, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani kuhusiana na Nabii Nuhu (a.s):-

إِذْ قَالَ لَهُمْ اَخُوهُمْ نُوحٌ اَلاَ تَتَّقُونَ. إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ اَمِينٌ. فَاتَّقُوا اللهَ وَاَطِيعُونِ[2]

Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu? .Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.

2. UPENDO NA HURUMA
Upendo ni sifa moja wapo inayojenga umoja ndani ya nyoyo za wanaadamu, kama anavyosema Allah (s.w) kuhusu upendo wake kwa Nabii Mussa (a.s):-

اَنِ اقْذِفِيهِ فِى التَّابُوتِ فَاقْذِفِيهِ فِى الْيَمِّ فَلْيُلْقِهِ الْيَمُّ بِالسَّاحِلِ يَاْخُذْهُ عَدُوٌّ لِّى وَعَدُوٌّ لَّهُ وَاَلْقَيْتُ عَلَيْكَ مَحَبَّةً مِّنِّى وَلِتُصْنَعَ عَلـٰي عَيْنِي[3]

Ya kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayo tokana kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu.

Mitume ya Mwenyeezi Mungu ilikuwa na huruma na mapenzi na watu wao, na walikuwa wakisikitika wanapoona watu wao wanapata tabu, kama tunavyosoma kuhusu Mtume Muhammad (s.a.w.w),:-

لَقَدْ جَاءكُمْ رَسُولٌ مِّنْ اَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَؤُوفٌ رَّحِيمٌ[4]

Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.

Maelezo kuhusiana na Aya:

*hapa zinatajwa baadhi ya sifa za Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa yeye kwa umma wake ni kama mzazi,

a) Anataabika akihisi kuwa umma wake unataabika au utataabika;

b)Ana pupa utengenee upesi upesi.

c)Ana rehema na huruma juu yao. Almuradi ni kama mzee na watoto wake .mapenzi na huruma ya Mitume ni kama nuru inayoingia nyoyoni mwa wanaadamu, na wanaadamu hao huwa na imani ya Mitume hiyo na kukubali yale wanayoongozwa na watukufu hao. Katika Qur-ani tunasoma:-

فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللهِ لِنتَ لَهُمْ وَلَوْ كُنتَ فَظّاً غَلِيظَ الْقَلْبِ لاَنفَضُّواْ مِنْ حَوْلِكَ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِى الاَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلـٰي اللهِ إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ[5]

Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.

*Hapa Mwenyeezi Mungu anamtia nguvu Mtume kuendelea na sifa yake ya upole na ustahamilivu juu ya yote yale anayofanyiwa na watu, na anamuonyesha kuwa kupewa upole huo ni rehema kubwa inayotoka kwa Mwenyeezi Mungu.

[1] Surat Yussuf Aya ya 54

[2] Surat shuaraa Aya ya 106-108

[3] Surat Taha Aya ya 39

[4] Surat Tawba Aya ya 128

[5] Surat Al-Imrani Aya ya 159

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini