MAUMBILE YA DINI

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UHAKIKI WA DINI

UHAKIKI WA DINI KUPITIA MSINGI WA IJTIHADI

MAUMBILE YA DINI NO.1

Dini imegawika katika maumbile mawili yafuatayo:

- Umbile la dhahiri (umbile la nje):

Umbile hilo linamsaidia mwanaadamu katika kuifahamu na kunufaika na misingi ya dini kijumla jamala.

- Umbile la batini (umbile la ndani).

Umbile hilo linamsaidia mwanaadamu katika kufahamu na kunufaika na mambo mbali mbali yaliyomo ndani ya dini, zikiwemo hukumu za mbalimbali katika mambo ya jamii, siasa, uchumi,n.k. Hukumu hizo humletea mwanaadamu athari nyingi nzuri katika maisha yake, kwa hiyo mwanaadamu anapaswa kuwa na elimu ya dini ya kutosha na mwenye kufanya jitihada ili kutambua umuhimu wa falsafa ya dini.

8. Sheria ya dini inatupa amri ya kuitambua dini, kama anavyosema Allah (s.w).

"وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةً فَلَوْلاَ نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَآئِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِى الدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُواْ إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ[1]"

Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadharisha?  na ikiwa amri ya kutafuta taaluma za dini katika maisha ya wanaadamu ni wadhifa wa kila mmoja wetu.

Maelezo kuhusiana na Aya:

Masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa hima kubwa yao ya kutaka kujua dini, na kutaka kutwa kucha wawe pamoja na Mtume Muhammad (s.a.w.w), walikuwa wanaacha miji yao wakisilimu wanakuja wote kukaa Madina, wakakatazwa hayo isije ikafa hiyo miji, na Madina isije ikawachukua wote, hauwezi mji mmoja kuchukua watu wa chungu ya miji, basi ikaambiwa kuwa wawe wakija baadhi ya watu tu katika kila mji. Na Mtume Muhammad (s.a.w.w) ana kauli maarufu inayothibitisha umuhimu wa elimu, yeye anasema:-

طلب العلم فریضة علی کل مسلم و مسلمة[2]" "
Yaani: Kutafuta elimu ni jambo la lazima kwa kila Muislamu mwanamme na mwanamke. Kwa hiyo, falsafa ya dini itatambulika kutokana na elimu ya dini, na sheria za dini, kutokana na maelezo hayo, tunapata natija ya kuwa, kuitambua falsafa ya dini ni jambo la lazima katika maisha ya mwanaadamu .

[1] Surat Tawba Aya ya 122

[2] Usuli kaafi, juzuu ya kwanza, ukurasa wa 30 .

MWISHO