NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.1

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.1

Kuna nadharia tofauti zilizotolewa na watu mbali mbali kuhusiana na ufafanuzi wa dini, kila kundi au watu limeifafanua dini kutokana na mtazamo wake binafsi au itikadi aliyonayo, katika makala hii tutaelezea nadharia tofauti zilizotolewa na baadhi ya watu kuhusiana na dini, miongoni mwa nadharia hizo ni hizi zifuatazo:-

Baadhi yao wamesema kuwa; “ Dini sio itikadi wala amali au matendo maalumu, na haiwezekani kuiweka imani na suna za dini kuwa kitu kimoja, (mwanaadamu wakati anapokuwa na dini huzingatia mambo yanayohusiana na hatima na malengo ya mwisho, mambo hayo yanaweza kuwa ni siku ya mwisho, Mwenyeezi Mungu, au mambo mengine yoyote yale), na anapozingatia hatima na malengo ya mwisho, humfanya yeye awe na hisia ya kuwa na uhakika wa mambo hayo, kuwa na hisia ya uhakika wa mambo ina maana ya kuwa; mwanaadamu huona thamani ya vitu na mambo mbalimbali, huona nguvu na uwezo wa Mola wake, basi hapo hutafuta taadhima na heshima ya Mola wake. Hii humfanya yeye adiriki ulazima wa kuwa na tabia njema, na hii ni hatua ya mwanzo inayomfanya mwanaadamu afanye jitihada zake zote kwa ajili ya kufikia katika uhakika wa hatima ya mambo.

Kuwa na fungamano la kiroho kuhusiana na hatima ya siku ya mwisho ni jambo la mwanzo – kulinganisha na mambo mengine - linalomfanya mwanaadamu agundue umuhimu wa nafsi yake, na kuwa na fungamano la siku ya mwisho kunamfanya mwanaadamu ajitoe katika ulimwengu wa kimada, basi wakati huo mwanaadamu husema kuiambia siku hiyo “wewe sio kama mimi, basi kila kitu na kitendwe kwa mujibu wa mapendekezo yako”. Hapo huacha moyo wake, nafsi yake, na nguvu zake, na husalimu amri kutokana na mambo yote. Basi ikiwa mwanaadamu ataifahamu dini katika hali kama hiyo,inawezekana kwa wale watu ambao hawana dini kuwa wenye dini, na watu wasio na itikadi ya kuwepo Mwenyeezi Mungu kikawaida wanakuwa na fungamano na hatima ya siku ya mwisho, kwa hiyo ni lazima tuzingatie kuwa inawezekana kwa wale wasiokuwa na imani ya kuwepo Mwenyeezi Mungu kuokoka kutokana na imani waliyonayo, na imani waliyonayo watu kama hao ndio inayojenga uhusiano na Mwenyeezi Mungu, ijapokuwa pengine watu hao hawazingatii hayo”.nadharia hiyo imepingwa na kutafitiwa.

(Utafiti kuhusiana na nadharia hiyo).

Moja: Katika maelezo ya nadharia hiyo, kumepambanuliwa baina ya dini na imani, hali ya kwamba dini ni hiyo hiyo imani. Kwa ufafanuzi zaidi:-Kuwa na itikadi ya Dini moja “yaani dini ya Kiislamu ” ni imani. Hali ya kwamba watu waliotoa nadharia hiyo wana itikadi ya kuwa dini ni imani, na imani sio dini, Ni jambo lisilo shaka kuwa dini sio kitu chengine isipokuwa ni hiyo hiyo imani ya kuwa na dini).

Mbili: Ikiwa dini ni kuwa na imani na fungamano la moyo kuhusiana na hatima ya mwisho, fungamano hilo ni moja, au zaidi ya moja? ikiwa ni fungamano moja, basi ni kitu gani kinacholeta tofauti baina ya imani na dini, na ikiwa ni zaidi ya moja, basi mafungamano hayo yatakuwa hayaingiliani au yanatofautiana. Ikiwa ni tofauti, ni kitu gani kinachosababisha tofauti hiyo, na ikiwa hayaingiliani, basi vipi inawezekana kupatikana ufafanuzi ulio sahihi kuhusiana na imani? hayo yalikuwa ni baadhi ya majibu tu ya nadharia hiyo, katika makala inayofuata tutaelezea na kujibu kwa uwazi kabisa kuhusiana na nadharia hiyo.

MWISHO