Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.2

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

NADHARIA KUHUSIANA NA DINI NO.2

Katika makala iliyopita, (makala namba moja) tulielezea nadharia iliyotolewa kuhusu ufafanuzi wa dini, tukajibu nadharia hiyo katika vipengele viwili, katika makala hii tutaendelea kuijibu nadharia hiyo.

Tatu: Watu waliotoa nadharia hiyo wana dalili gani inayothibitisha kuwa, kuzingatia na kuwa na fungamano na hatima ya malengo muhimu ya mwisho ni imani? Hivi kweli tukirudia katika historia ya mwanaadamu anaweza kupatikana mtu ambaye hata kwa dakika moja hakuwa na mazingatio? Sasa vipi tunaweza kusema kuwa mazingatio hayo ni imani? Hali ya kwamba watu wote hata wale wasio na itikadi na Mwenyeezi Mungu, au washirikina wote walikuwa na sifa hiyo ya kuwa na mazingatio ya mambo tofauti, natushuhudie Aya hii ifuatayo, Allah (s.w) anasema:-

وَلَئِن سَاَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللهُ قُلْ اَفَرَاَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللهِ إِنْ اَرَادَنِيَ اللهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ اَوْ اَرَادَنِى بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ قُلْ حَسْبِيَ اللهُ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ[1]

Na ukiwauliza “Ni nani aliyeziumba mbingu na ardhi?” bila ya shaka watasema: “Ni Mwenyeezi Mungu.” Sema: “Je, mnawaonaje wale mnaowaomba kinyume cha Mwenyeezi Mungu?, kama Mwenyeezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake?” Sema:-

“Mwenyeezi Mungu ananitosha, kwake wategemee wanaotegemea.”

Hivi kuna tofauti gani baina ya watu walio na dini na wale wasio na dini? Hali ya kwamba watu wa aina mbili hizo wote wanashirikiana katika sifa hiyo yaani vikundi hivyo viwili vina sifa hiyo ya kuwa na mazingatio ya mambo fulani, au kwa lugha nyengine mazingatio kuhusiana na hatima ya malengo ya mwisho. Kwa upande mwengine watu waliotoa nadharia hiyo wamesema na kuthibitisha kuwa, mazingatio ndio yanayomfanya mtu awe na hisia za uhakika, na hisia hizo ndizo zinazomfanya arudi nyuma (aporomoke na kusujudu) kwa ajili ya kumtukuza na kutafuta taadhima na heshima ya Mola wake, basi hivi kweli wale wasiokuwa na dini, au hawana itikadi na dini, wao hawakuwa na hisia za uhakika, au hawakuwa na taadhima wala heshima yoyote kwa ajili ya Mola wao?. Nne:Watu waliotoa nadharia hiyo wana itikadi ya kuwa, kuamini Mwenyeezi Mungu sio dini, dini ni kuamini hatima na malengo ya siku ya mwisho, mbali ya Mwenyeezi Mungu, (yaani malengo sio Mwenyeezi Mungu), kwa sababu kuwa na mazingatio na hisia za uhakika, na kuamini hatima ya mwisho kunamfanya mwanaadamu ajenge uhusiano na Mwenyeezi Mungu, kutokana na kauli  ya watu hao kumejitokeza masuala mingi, miongoni mwa hayo ni kama ifuatavyo:-

A: Kuna uwiano gani baina ya kuamini hatima ya mwisho, na kuamini Mwenyeezi Mungu?, Hivi kweli kuna malazimiano yoyote baina ya vitu hivyo viwili? kwa lugha nyengine; vitu viwili hivyo vinategemeana? ikiwa vinategemeana basi ni lazima tuseme hivi:-kuwa wale wasioamini Mwenyeezi Mungu, wana imani na Mwenyeezi Mungu, (yaani tunakusudia kusema kuwa; kwa upande mmoja wana imani na Mwenyeezi Mungu, na kwa upande wa pili hawana imani na Mwenyeezi Mungu), basi vipi itakubalika hali kama hiyo, wakati huo huo mtu kuwa na imani, na wakati huo huo kutokuwa na imani? hali ya kwamba kitu kama hicho hakiingiliki akilini, kwa sababu watu ambao hawana imani na Mwenyeezi Mungu hawamuamini Mwenyeezi Mungu, basi kusema hivyo sio sahihi. Na kama vitu hivyo vitakuwa havitegemeani, na havilazimiani katika kitu chochote, basi kuna dalili gani zinazopelekea watu kutokana na hisia za uhakika au kuwa na imani na hatima ya mwisho kunawafanya watu wajenge uhusiano na Mwenyeezi

Mungu?.
B: Dini ambayo haitokuwa na udhati katika kumuamini Mwenyeezi Mungu kwa hakika hiyo sio dini, - sio dini sahihi – na hicho sio kitu chengine isipokuwa ni kubagua uhakika wa dini na dhati ya dini.

[1] Surat Azumar Aya ya 38

[1] Surat Azumar Aya ya 38

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini