NJIA ZA UFUMBUZI WA DINI NO.2

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

NJIA ZA UFUMBUZI WA DINI NO 2

Katika makala iliyopita tulielezea njia mbili zinazoweza kumuongoza mwanaadamu katika uhakiki wake wa dini, katika makala hii tutajibu ile kauli isemayo kuwa; dini imeteremshwa kulingana na tamaduni za watu, hivi kweli kauli hiyo ni sahihi? kwa hakika kauli hiyo sio sahihi kwa mujibu wa maelezo haya yafuatayo.

Dini imekuja kurekebisha na kusawazisha tamaduni potofu na kuwaongoza watu katika maadili yaliyo mema.

katika sehemu hii natuangalie baadhi ya mambo mabaya yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya watu, vikundi au makabila, mambo ambayo yamesawazishwa na kutengenezwa kupitia dini takatifu ya Allah (s.w).

Miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo:-

- kukataza kuabudu masanamu, na kuabudu Mola mmoja mtakatifu

- kusahihisha ibada ya tawafu, baadhi ya watu walikuwa wakitufu hali ya kuwa wako uchi bila ya nguo, dini imesawazisha na kuwataka watufu kwa mujibu wa misingi maalumu.

- Mauaji ya kabila na kabila:

Baadhi ya wakati makabila yalikuwa yakikhitilafiana, au kabila moja kuuwa mtu wa kabila jengine, kabila la mtu aliyeuliwa lilikuwa likitoka na kwenda kulipiza kisasi kwa watu wote wa kabila hilo, na si kuuwa mtu mmoja tu ambaye amemuuwa mtu fulani,dini imesawazisha na kuwaambia :-

وَلَكُمْ فِى الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَاْ اُولِيْ الاَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ[1]

Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike.

Maelezo kuhusiana na aya:

*Watakuwa na uhai mzuri kwa sababu, kila mtu atakaa kwa adabu yake, kwani anajua kuwa akiua atauawa, na akidhuru na yeye atafikishiwa madhara. Katika kujikimbizia madhara nafsi yake yanakimbizika hayo madhara ya watu wengine *“Alqisas hayat” yaani ndani ya kisasi pia mna maisha, hivyo katika kisasi watu wanaweza wakafanya suluhu au kusameheana.

[1] Suratul Baqarah aya ya 179

MWISHO