MATAKWA YA MOLA KWA MITUME NO.2

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MATAKWA YA MOLA KWA MITUME NO.2

Allah (s.w) amewapa Mitume yake nyadhifa mbali mbali, miongoni mwa nyadhifa hizo ni kufikisha ujumbe wake kwa waja wake, ujumbe huo waliopewa Mitume na Mola wao kuufikisha kwa walimwengu ni kwa ajili ya kumuongoza mwanaadamu na kumpatia saada ya duniani na Akhera.

kwa sababu hiyo basi Mitume walitumia njia zote tatu katika kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa watu. katika makala iliyopita tulielezea baadhi ya njia hizo, na katika makala hii tutaelezea njia nyengine.

c) MWENENDO WA MITUME.

Mitume ya Mwenyeezi Mungu, kwa matendo yao na mwenendo wao waliweza kuufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu katika jamii, kiasi ya kwamba watu kwa kuona amali, mwenendo na matendo yao, vipi wanaishi na watu kitabia, na wanatekeleza na kuyafanyia amali yale ambayo Mola wao amewaamrisha, na kutokana na amali na matendo yao walikuwa ni kama taa yenye nuru inayomurika na kuwaonyesha wanaadamu njia njema na yenye saada, basi natuzingatie Aya hii tukufu inayohusiana na Mtume Muhammad (s.a.w.w):-

وَدَاعِياً إِلَي اللهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجاً مُّنِيراً[1]

Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa yenye kutoa nuru.

 Maelezo kwa ufupi kuhusiana na makala zilizopita

* Neno tabligh ndani ya Qur-ani limekuja likiwa na maana ya kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa watu.

* Madhumuni na hadafu ya Mitume katika kufanya tablighi ni kuwakinaisha watu na kuwatia shauku ya kufanya matendo mema.

* Miongoni mwa njia muhimu walizotumia Mitume katika kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu ni kuwabashiria watu mabashirio mema, kuwaonya na kuwatia hofu ya adhabu ya siku ya Kiama.

* Hekima, mawaidha, na majadiliano mazuri ni njia tatu nyengine walizotumia Mitume katika kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu.

* Mbali ya njia za kielimu walizotumia Mitume, kuyafanyia amali yale wanayowaamrisha watu katika maisha yao ni njia nyengine walizotumia Mitume katika kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu.

Masuala.

1. Mitume ya Allah (s.w) ilikuwa na hadafu gani katika kuufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa watu?.

2. Neno kuonya lina maana gani? Na Mitume iliitumia vipi njia hii kuwalingania watu katika njia ya Allah (s.w)?

3. Mitume iliwahofisha watu kwa kupitia vitu gani walipokuwa wakiwalingania watu katika njia ya Allah (s.w)?

4.Mitume iliwabashiria watu mabashirio mema kutokana na vitu gani?.

5. Neno hekima lina maana gani?.

6. Elezea maana ya neno mawaidha.

7. majadiliano mazuri yanajadiliwa vipi?

8. Mwenendo wa Mitume ulileta athari gani katika kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu?.

[1] Surat Al-Ahzaab Aya ya 46

MWISHO