NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.1

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.1

Njia walizotumia Mitume katika kukabiliana na waliowakhalifu.

Mitume ya Mwenyeezi Mungu walitumia njia tofauti katika kukabiliana na maadui wao ambao waliwakhalifu. Baadhi ya njia hizo ni kama hizi zifuatazo:-

1. KUJIBAGUA NA MAKAFIRi.

Mwanzoni mwa malinganiajo ya Mitume, kundi la makafiri lilisisitiza na kuwasisitiza watu kubaki katika itikadi za za kikafiri, na hawakukubali kuacha itikadi zao hizo, hata walifanya jitihada sana kuwavuta na kufanya mambo yatakayowavutia Mitume na wafuasi wao katika itikadi zao za kikafiri, katika hali kama hiyo basi, hatua ya mwanzo waliyochukua Mitume ni kutangaza na kuwataka wafuasi wao kukabiliana na kupingana na makafiri, Mitume ilitangaza kujibagua na makafiri, kama tunavyosoma katika Qur-ani kuhusiana na Mtume Muhammad (s.a.w.w):-

قُلْ يَا اَيُّهَا الْكَافِرُون.  لاَ اَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ[1]

Sema: Enyi makafiri! . Siabudu mnacho kiabudu;

2. KUPIGANA VITA NA MAADUI

Maadui wa Kiislamu wakati walipokuwa wakikabiliana na kupingana na yale waliyolingania Mitume, ikiwa kwa kuleta fitna au kuwauwa wafuasi wao, Mitume bila ya kupoteza muda ilikabiliana na maadui hao na kupigana nao vita, ili kuondosha fitna na ufisadi waliokuwa wakiuleta katika jamii, na waliwahukumu kutokana na dini ya Mwenyeezi Mungu ilivyowaamrisha, kama anavyosema Allah (s.w):-

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّي لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ فَإِنِ انتَهَواْ فَلاَ عُدْوَانَ إِلاَّ عَلـٰي الظَّالِمِينَ[2]

Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu.

3. KULETA SULUHU KWA USALAMA

Pindi maadui wa Kiislamu, au wafuasi wa dini nyengine wanapokuwa tayari kukubali kutoleta fitna au kuleta vita, na wakawa thabiti katika ahadi zao walizozitoa, Mitume pia ilikubali suluhu zao kwa uslama, kama anavyosema Allah (s.w):-

وَإِن جَنَحُواْ لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا وَتَوَكَّلْ عَلـٰي اللهِ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ[3]

Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.

[1] Surat Kaafiruna Aya ya 1-2

[2] Suratul-Baqarah Aya ya 193

[3] Surat Al-Anfaal Aya ya 61

MWISHO