NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.2

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
NJIA ZA KUKABILIANA NA WAKHALIFU NO.2
Njia walizotumia Mitume katika kukabiliana na waliowakhalifu.
Katika makala iliyopita tulielezea njia tatu walizotumia Mitume katika kukabiliana na wale waliowakhalifu. katika makala hii tutmalizia mada yetu hiyo kwa kuelezea njia nyengine waliotumia watukufu hao katika kukabiliana na wale waliowapinga na kuwakhalifu.
Mitume ya Mwenyeezi Mungu walitumia njia tofauti katika kukabiliana na maadui wao ambao waliwakhalifu. Baadhi ya njia hizo ni kama hizi zifuatazo:-
4. KUWAONDOLEA MASHAKA NA KUWALETEA AMANI
Kabla ya kuja Mitume, watu wengi walikuwa wakiishi maisha ya madhila na mateso, na hii ni kwa sababu ya serikali ya watu madhalimu ambao walikuwa wakitawala katika zama hizo, na baada ya kuja Mitume pia hawakuwa katika amani, na mateso hayo yaliendelea siku hadi siku kwa sababu tofauti, ikiwa ni kwa sababu ya kudai uhuru wao, au kwa sababu ya kuamini dini ya Mwenyeezi Mungu na kuwatii Mitume yake, kama walivyosema watu wa Bani Israeyl kumwambia Nabii Mussa (a.s):-

قَالُواْ اُوذِينَا مِن قَبْلِ اَن تَاْتِينَا وَمِن بَعْدِ مَا جِئْتَنَا قَالَ عَسَي رَبُّكُمْ اَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِى الاَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ[1]
Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamhiliki adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtavyo kuja tenda nyinyi.

Ama tofauti inayoonekana katika mateso hayo ni kwamba, kabla ya kuja Mitume watu walikuwa katika tabu na mashaka kwa muda mrefu maishani mwao, lakini baada ya kuja Mitume walikuwa wakipata tabu katika muda maalumu, kwani Mitume hawakukaa kimya kuona mateso hayo bali walikabiliana na maadui na kuwaangamiza na kuwahilikisha, na watu walineemeka kwa kupata uhuru ambao chanzo chake ni kuja kwa Mitume hiyo, kama anavyosema Nabii Mussa (a.s) kuwaambia watu wa Kaumu yake:-

قَالُواْ اُوذِينَا مِن قَبْلِ اَن تَاْتِينَا وَمِن بَعْدِ مَا جِئْتَنَا قَالَ عَسَي رَبُّكُمْ اَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِى الاَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ[2]
Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamhiliki adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtavyo kuja tenda nyinyi.
Kwa hiyo wafuasi wa kweli wa Mitume ni lazima waelewe kuwa, haiwezekani kupata mafanikio bila ya kupata mateso na tabu, na mtu hawezi kupata daraja ya pepo bila ya kupigana jihadi,kustahamili au kuuhama mji wake na kuwacha kila anachokipenda katika mji wake kwa ajili ya kupigania dini ya Mwenyeezi Mungu tu, na kutii amri za Mola wake na Mitume yake.
Maelezo kwa ufupi kuhusiana na makala zilizopita.
* kuja kwa Mitume kulisababisha watu waishi katika maisha yenye furaha na mategemeo katika jamii, na Mitume iliwaondoa watu katika madhila na mateso.
* Kuja kwa Mitume kuliwafanya watu wajenge umoja katika kuihifadhi dini yao.
* Mitume ya Mwenyeezi Mungu ilitumia njia tofauti katika kukabiliana na Makafiri, miongoni mwa njia hizo ni, kujibagua na makafiri, kupigana nao vita na kufanya nao suluhu kwa usalama na amani.
* Mategemeo na utulivu ambayo Mitume iliwaletea wafuasi wake, ilisababisha watu waweze kustahamili mashaka na mateso waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa maadui wa Kiislamu kwa urahisi kabisa, na lengo lao lilikuwa ni kuihifadhi dini ya Mwenyeezi Mungu.
Masuala.
1. Ni watu wa aina gani waliopata mategemeo katika maisha yao baada ya kuja kwa Mitume,?.
2. Ni alama gani iliyoonekana katika maisha ya wanaadamu baada ya kuja Mitume katika jamii?.
3. Ni sababu gani zinazopelekea hitilafu katika jamii?.
4. Mitume ya Mwenyeezi Mungu ilikabiliana vipi na watu ambao waliwahalifu?.
5. watu walifaidika na nini baada ya kuja kwa Mitume?.

[1] Surat Al-Aaraf Aya ya 129

[2]  Surat Al-Aaraf Aya ya 129

MWISHO